Simuelewi hata kidogo

Simuelewi hata kidogo

nameless girl

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2012
Posts
4,195
Reaction score
2,678
2008 kipindi nipo kidato cha tano, nilitokea kuwa na rafiki wa kiume ambaye tuliheshimiana kama dada na kaka. Wakati nikiwa rafiki wa kijana huyo, pia nilikuwa na shoga yangu ambapo wote watatu tulikuwa darasa moja, jambo lililopelekea wote watatu kuwa marafiki sana.Baada ya kumaliza kidato cha sita, urafiki wangu na kijana huyo ulikuwa wa karibu zaidi kuliko nilivyokuwa na shoga yangu. Baada ya siku kadhaa, kijana huyu alinieleza ukweli kuwa yeye na shoga yangu walikuwa wapenzi toka kidato cha tano. Kiasi taarifa hizo zilinishtua kidogo kutokana na kunificha ingawa wote watatu tulikua na ukaribu wa kuambiana lolote. Baada ya kuniambia hayo, kijana huyu aliniomba twende nje kidogo ya mji tukae angalau kwa siku mbili. Sikuona ubaya wowote kwani ni mara nyingi tulizoea kwenda sehemu mbalimbali. Tatizo lililoibuka ni kuwa huyu kijana alitaka tukae chumba kimoja kwa siku mbili na nisimwambie mpenzi wake (shoga yangu). Kiukweli sikuweza kwenda kwani sikujisikia amani yoyote kufanya hivyo. Sehemu zote tulizotoka, ilikuwa ni siku moja na hata mpenzi wake nilikuwa nikimjulisha kuwa tupo sehemu fulani (kipindi hiko sikuwa najua kama ni wapenzi mpaka kijana huyo aliponijulisha mwenyewe) nilijaribu kumwelewesha athari za kufanya hivyo lakini alikimbilia kunieleza kwamba hakuwa ananitamani au kunipenda kama nilivyofikiria ingawa sikuwa nimefika huko kinachonishangaza ni kijana huyu kunikwepa mara tu nilipoonyesha kumkatalia alilolitaka, hapokei simu yangu yoyote na wala hanijulii hali kama ilivyokuwa mwanzo. Mimi binafsi nampenda kama rafiki yangu wa kawaida na sipendi mimi kuwa chanzo cha ugomvi wao katika mapenzi yao. Sijamweleza shoga yangu haya yote na mpaka leo ni rafiki yangu wa karibu. Simwelewi kabisa huyu mtu. s
 
Hakuna kitu kama urafiki wa dada na kaka. Hakipo na hakitakuwapo, ulichokiexperience kwa huyo kaka kabla hajakuomba mtoke kwa siku mbili ni uoga tu, hata wewe ukijichunguza vizuri utakuta hayo mapenzi uliyonayo kwake unayoyaita ni mapenzi ya ukaka na udada sio kweli, na wewe unamtaka pia.
 
nameless girl,

Katika maelezo uliyotoa hapa ni kama kuna mambo baadhi hujayaweka wazi sana ambayo nafikiri ungeyaweka wazi ingesaidia kukupa ushauri unaofaa....Anayway,

Kwa mtazamo wangu nahisi kwamba the bond you created between wewe na huyo kijana was going deep than you thought (huenda kwakuwa wakati huo hukuwa unajua kama walikuwa na mahusiano zaidi ya yale uliyokuwa unayajua na rafiki yako) Yes hamkuwa mmefikia hatua ya yeye kukwambia hayo aliyokwambia lakini perhaps mlikuwa mnaongea kwa vitendo bila wenyewe kujua.

Nimepata taabu kidogo kupata majibu ya maswali haya "Kwanini mpaka sasa hujamwambia rafiki yako? au at least kumuuliza kuhusu mahusiano yake na huyu kijana?" Napata tabu kidogo kuunganisha stori yako kwasababu inaonekana kama mwanzo unasema ulikubali kwenda ila tabu ikawa kulala chumba kimoja then unasema hukwenda..........Napata tabu kidogo kukupa ushauri productive. Hebu weka stori vizuri ili nijue wapi pa kuanzia
 
Last edited by a moderator:
Hakuna urafiki kati ya msichana na mvulana huyo jamaa ana kupenda.
 
mmmh? Sasa hapa huelewe nini?

Wanamme wengine wako 'nipe mzigo vingivyo hakuna urafiki'

sasa ndo ujue huyo kaka hataki urafiki wa 'wapendwa'
 
unataka kumuelewa nini sasa?
Si alitaka kipochi manyoya tu?
Shida yake ilikuwa agonge asepe.....
 
mmmh? Sasa hapa huelewe nini?

Wanamme wengine wako 'nipe mzigo vingivyo hakuna urafiki'

sasa ndo ujue huyo kaka hataki urafiki wa 'wapendwa'

Umenena la ukweli. mi kuna mtu mmoja alikuwa ananifundisha lugha moja ya kigeni,so tukawa marafiki kama mwaka na miezi kadhaa,he siku ya siku ananiambia ananipenda anataka niwe mpenzi wake nikamwambia haiwezekani. akaniambia "x nimekuwa nikikupenda siku zote sasa kwakua umenikataa umekua adui yangu,nakuchukia sanaa" toka wakati huo ni mwaka sasa hatuna mawasiliano. nikaamini kwa wanaume wengine hakuna just a friend.
 
..mwanaume km simba,anakuwa rafiki yako lkn siku njaa ikimkaba atakutafuna, dada yangu mwanaume akiwa mwema kwako au anatengeneza urafiki na wewe, ukafarijika kwamba ni rafiki yako, mwanaume anakuwa na lengo moja tu, ipo siku atakupata. hakuna u kaka na dada, hizo ni mbinu za kukutia mtegoni. kwa feelings unazozielezea hata wewe ulikuwa unasubiri tu uambiwe NAKUPENDA.
 
binafsi kama umesoma vizuri, nilikuwa namwambia shoga yangu kama leo nimetoka nae na nipo sehemu fulani kwa kusudi la kutaka nae atujoin ingawa hakuwai kufanya ivo hata siku moja, siku ambayo huyo kijana aliniambia tutoke nje ya mji sikupata mashaka kwakuwa ni kawaida yetu lakini kulala chumba kimoja ndipo hapo nilipokataa condition hiyo, sikutaka kumwambia shoga yangu kwakuwa sikupenda kuwa chanzo cha ugomvi kwao ni hayo M'JR
 
hata kumtamani cjamtamani, kilichonifanya niwe nae mara nyingi ni kutumia muda mwingi kuongelea mambo ya kimaendeleo mpk pale yaliponikuta
 
hata kumtamani cjamtamani, kilichonifanya niwe nae mara nyingi ni kutumia muda mwingi kuongelea mambo ya kimaendeleo mpk pale yaliponikuta

men have got only two emotion hungry and horny. If a man is not hungry is horny.
 
pole mpotezee,kaa nawe kimya hapo annafanya makusudi kukuchunia ili ulegeze kamba uvue chupi,usikubali he is not worth it.....
 
Hakuna kitu kama urafiki wa dada na kaka. Hakipo na hakitakuwapo, ulichokiexperience kwa huyo kaka kabla hajakuomba mtoke kwa siku mbili ni uoga tu, hata wewe ukijichunguza vizuri utakuta hayo mapenzi uliyonayo kwake unayoyaita ni mapenzi ya ukaka na udada sio kweli, na wewe unamtaka pia.

ni kweli, huyu dada pia anaonekana ana hisia zilizofichika kwa huyu msela sema anaogopa urafiki wake na shoga ake utakapoishia. otherwise muda si muda moto wa mapenzi utawaka......
 
Nameless girl ushauri wangu kwako ni kuwa urafika kati ya dada na kaka huishia mlipofika, kama kweli huna malengo ya mahusiano ya mapenzi acha naye. Halafu ningekushauri uendeleze msimamo uliouonyesha, wakati mwingine unapokuwa na urafiki na mkaka weka mipaka na ieleweke kwako itakusaidia. pia usihau kuwa wewe ni kwaajili ya mumeo acha mchezo wa kuanza mapenzi kabla ya ndoa sawa eeeh!
 
Si alitaka kipochi manyoya tu? Nimeipenda.
Urafiki wa ukaka na dada sio kwa wabongo labda wadhungu.
 
sasa kwanini unaumia mana kuumia kwako kunaleta mashaka kua upendo wako kwake ni zaidi ya kaka na dada,rafiki na rafiki yani umezidi hapo kidooogo na unakoelekea na kubaya hata kama ukikataa ila unaelekea huko so ikimbie iyo zambi mapemaa
 
inavyoonekana unampenda na acngekwambia kuwa anauhusiano na shoga yako ungekubali kulala nae chumba kimoja.
 
Back
Top Bottom