Mpatanishi
JF-Expert Member
- Jul 1, 2011
- 1,811
- 623
mimi ni kijana niliyehitimu kidato cha sita na kuchaguliwa kuingia chuo fulani kikuu huko dom mwaka jana. Nimelelewa kwa mapenzi makubwa ya baba na mama ambyo yamenifanya niwe na mafanikio sana ya kishule na maisha kwa ujumla. Baba yangu amkuwa na rafiki wangu wa karibu sana na mara kwa mara huwa tunashauriana mambo mengi .
Wiki iliyopita mama alikuja kunitembelea na akaomba jmosi twende dar. Nilipomuuliza kulikoni kwenda dar akasema eti anataka kunionyesha baba yangu, huyu aliyenilea na kunitunza kwa mapenzi makubwa mpaka leo si baba yangu mzazi! Nimepigwa na butwaa mpaka muda huu.
Naomba ushauri nifanyaje ndugu zangu? Akili inanizunguka.
***** hii ni email niliyopokea toka maeneo ya dodoma kijana akiomba ushauri wa haraka juu ya hayo aliyoeleza*****
Laana huwa haziwashiki watu wasio na atia,mimi ningemzaba vibao huyo mama kwani huo ni udharirishaji,mwambie amsaidie na kumheshimu huyo anayemjua kuwa ni baba yake.
Imeshakupitia akilini mwako kuwa huenda baba yako mzazi hata yeye pia hajui kama wewe ni mtoto wake??For sure ningemtimua huyo mama, kama amepokea rushwa kwa huyo the so called baba mzazi itakuwa imekula kwake. hivi na uzee huo unahitaji kumwona biological father wa kazi gani? hata kama ungekuwa bado mdogo, una baba ambaye anakupenda sana na anakufanyia kila kitu, huyo mwingine wa nini? kuongezeana tu ma-extended family, maana huyo baba mzazi anakuja na ukoo wake, ukimkubali yeye basi na ukoo wote unaukubali, so unakuwa na koo 3, + 2 za mtarajiwa mke wako..........................
Huyo baba anayeenda kuonyeshwa si baba yake bali ni MPACHIKAJI MIMBA" alikuwa wapi mda wote wakat watu wanalea hadi mtoto anakuwa mkubwa? Kuna baadhi ya wanaume wanapenda sana KITONGA(MTEREMKO)
Noana wachangiai wengi wametoa maoni ya jumla jumla ambayo yanaashiria vitu vifuatavyo. Moja, kuwa baba mzazi alikuwa anafahamu uwepo wa mtoto wake na hakufanya chochote kuhusu mwanaye; mbili, Kuwa baba mlezi alifahamu fika kuwa huyo mtoto si wake lakini bado alimlea kwa mapenzi bila kumbagua na tatu kuwa mama mtu kwa makusudi bila sababu yeyote ya msingi aliamua kuficha ukweli kwa kushirikiana na mzazi mwenzie. Lakini hebu tujaribu kufikiri kwa mapana zaidi. Je haiwezekani kuwa baba mzazi hajui wala hakuwahi kujua kuwa huyo mtoto ni wake? na kama hivyo ndivyo, huyu baba mzazi ni kweli ana makosa kama ambavyo wengi wetu tungependa kujiaminisha hapa. Kingine ni kuwa Je kama huyu baba mlezi angejua kuwa huyu si mwanaye (wa kibaiolojia), angemlea kwa mapenzi yote kama alivyofanya?
My take:
Aongee na mama yake amueleze kinaga ubaga imekuwaje hadi yeye akalelewa na baba ambaye aliaminishwa kuwa ni mzazi wake kumbe sio. Pia je kwa kipindi chote hiki huyo baba yake mzazi alikuwa anajua uwepo wake na kama sio ni kwanini sasa mama ameona umuhimu wa yeye kujua? Kingine ni muhimu huyo baba mlezi akahusishwa katika hili suala kuliko kutaka kulifanya kinyemela kama anavyotaka kufanya huyu mama. Mwisho mimi ninaamini msalaba mkubwa anaubeba huyu mama (Maana yeye ndiye chanzo cha yote).
Hivi ukienda kupanda mbegu zako kwenye shamba jirani yako bila ya taarifa wala ruksa yake na mwenye shamba akapalilia akaweka dawa na kulitunza mpaka likawa tayari kwa kuvuna unaweza kwenda kudai mavuno kwa sababu wewe ndie uliyepanda mbegu bila taarifa wala ruksa ya mwenye shamba?
Ningekuwa mimi ningemwambia huyo mama kuwa nashukuru kwa taarifa ila anipe muda wa kutafakari taarifa hizo na nikienda likizo nyumbani nitampa majibu ya ombi lake wakiwa pamoja na baba msingiziwa. Ila nitampa kazi ya kwenda kumweleza baba msingiziwa kuwa nitakuwa na mazungumzo na wote wawili yaani mama yangu na huyo baba yangu msingiziwa kuhusu suala hili.
mitihani ya maisha.