Simuelewi mama yangu!

Simuelewi mama yangu!

HorsePower

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2008
Posts
3,612
Reaction score
2,567
Mimi ni kijana niliyehitimu kidato cha sita na kuchaguliwa kuingia chuo fulani kikuu huko Dom mwaka jana. Nimelelewa kwa mapenzi makubwa ya baba na mama ambyo yamenifanya niwe na mafanikio sana ya kishule na maisha kwa ujumla. Baba yangu amkuwa na rafiki wangu wa karibu sana na mara kwa mara huwa tunashauriana mambo mengi .

Wiki iliyopita mama alikuja kunitembelea na akaomba jmosi twende Dar. Nilipomuuliza kulikoni kwenda dar akasema eti anataka kunionyesha baba yangu, huyu aliyenilea na kunitunza kwa mapenzi makubwa mpaka leo si baba yangu mzazi! Nimepigwa na butwaa mpaka muda huu.

Naomba ushauri nifanyaje ndugu zangu? Akili inanizunguka.

***** Hii ni email niliyopokea toka maeneo ya Dodoma Kijana akiomba ushauri wa haraka juu ya hayo aliyoeleza*****
 
Duh, mpe pole. Kitu chana kwanza ningemshauri awakutanishe wote watatu ili mambo yote yawe wazi kwanza. Then uamuzi wake binafsi utakuja tuu baada ya hili.
 
huyo baba yake halisi alikuwa wapi wakati wote mtoto/kijana anakua mpaka anafikia umri huo
haya mambo ndo huwa nakataa maana nimelelewa na baba na mama ambao najua fika ni wazazi wangu
At the end umekuwa mtu mzima mama anakuambia huyu sio baba yako sijui baba yako ni fulani
Sijawahi kumuona wala kumsikia wala hajawahi kuja kunitembelea wala kujua hali yangu.

Nilipokuwa naugua baba niliyekuwa naye ndo alikuwa karibu yangu
Kwenye shida na raha baba alikuwa nami
Siku ya siku eti huyo sio baba yako baba yako sijui ni fulani.

Aende zake huko alikokuwa miaka yote bana. Kijana aangalie ustaraabu na la muhimu aangalie maisha yake na huyo baba aliyemlea ambaye kwa moyo wake na imani yake anamjua na ndie aliyekuwa nae karibu miaka yote.

Mengine hayo ni mbwembwe tuu za kuharibiana maisha
 
Kweli mtoto ni wa mama!
Kwanza baba aliyekulea kwa mapenzi makubwa anaijua hii scenario? Mwambie mama mkae ninyi watatu mliongelee hili suala ili baba msingiziwa ajue kinachoendelea na yeye aseme maoni yake, lakini kikubwa mwenye uamuzi ni wewe kuamini kuwa baba aliyekulea ndio baba yako au huyo mpya wa dar

Hii ilishatokea kwa watu wangu wa karibu sana, mtoto aligoma kabisa kumtambua baba mzazi (mpya) aliendelea kuamini kuwa baba aliyemlea na kumsomesha ndio baba yake mzazi, wapo hadi leo na maisha yanaendelea kama kawaida
 
wamama wengine nuksi kweli wanaharibu amani/upendo wa watoto wao, atabaki kuwa biological father, aliyemtunza toka utoto mpka kufika hapo ndio baba yake
 
Hizi lebo nyingine hizi, sasa akimjua huyo baba mwingine ndio ili iweje?
Nashangaaaaaaaaa! yani ningekua mie ndio hata kusikiliza staki ningemwambia mama nakuheshimu na huyo jamaa
hata sura yake staki kumuona. yani wanawake wengine jamani..........
 
Dah pole kaka..we nenda tu ukamwone baba mzazi
 
Hizi lebo nyingine hizi, sasa akimjua huyo baba mwingine ndio ili iweje?

Ndo hapo sasa
Kuharibiana maisha tuu na kupotezeana malengo ya maisha maana mtu ameshafikia mbali kiasi hicho kimaisha ndo anakuja kuambiwa eti huyu sio baba yako baba yako ni mwingine
Inaumiza sana
 
Eti uende Dar? Tamana nae, wala usihangaike kwenda kumfahamu. Endelea na huyo aliekulea. Mpuuzie Maza na usimwonyeshe kuwa umempuuza.
 
Inauma sana kuambiwa "huyo sio baba yako" mtu ambaye amekulea, kusomesha na kukutunza vizuri, kama mwanae, binafsi sintakubali kwenda labda aje yeye na tutaishia kujuana tu siku ya utambulisho thn kila mtu kivyake..
 
haya mambo ya kuja kuambiwa mzazi wako ukubwani yanawachanganya watu sana
Kuna mzee mmoja mitaa ya nyumbani alikuja kutambulishwa baba yake akiwa mzee kabisa ana wajukuuu eti anakuja kuambiwa baba yako sio yule unayemjua ila ni huyu
Sasa hapo inanisaidia nini
Nimekaa na baba ambaye amenilea kwa shida na kunisomesha bila kunibagua kanitunza na alikuwa baba bora katika maisha yangu
hajawahi kuacha kunionyesha upendo wa baba kwa mmwanawe wala kunibagua kwa jambo lolote
At the end mama anakuja na story zake kuwa huyu sio baba yako baba yako ni fulani

kama mama alikuwa ni mwelewa angefanya hayo wakati nikiwa mdogo kabisa na huyo ambaye kwa sasa naenda kuonyeshwa ni baba yangu atake responsibility ya kunilea na kunisomesha na kunipa upendo wa baba
Sio asubiri nimelelewa na baba mwingine na nimekuw amtu mzima aje ajitokeze kusema ni baba yangu
Hii ni kuharibiana maisha
 
Huyo anayeitwa baba yako na mama yako alikuwa wapi siku zote,

Yaelekea alikukana, sasa kuna kitu kinamkwaza,

kama alikukana mkane na yeye pia, aliyekulea ndio bb yako
 
The art of fatherhood lies in the combination of bringing up, winning daily bread for, educating, encouraging, comforting, picking up when one falls down, loving, opening one's eyes about the world, protecting and always be there. Young man-whoever gave u all that is your true father!
 
Lazima ajue msimamo maana atakusumbua usimpuuzie mwambie ukweli, ili akamweleze huyo anayejita baba
 
The art of fatherhood lies in the combination of bringing up, winning daily bread for, educating, encouraging, comforting, picking up when one falls down, loving, opening one's eyes about the world, protecting and always be there. Young man-whoever gave u all that is your true father!

Umesema mkuu
Yaani hapa umemaliza kila kitu na huyo kijana azingatie hili
Sio mtu amekaa anauza sura huko hajui hata uliishije, ulivaa nini, nani alikupa pesa ya dawa ukiwa mgonjwa au kukuhudumia hata ulipokuwa na shida, nani alikupa tumaini ukiwa na majonzi, nani alikuonyesha dunia wakati unahitaji kuiona dunia, then from no where anakuja kukuambia eehh mimi ni baba yako
To hell na fatherhood ya kuchonga
 
Nadhani c vibaya akimjua mtu aliyemleta duniani ila huyo c baba yake...

Alivyoniambia yeye hana upendo na hamu ya kumjua baba yake mzazi. Anamuona kama kamfanyia ukatili sana, na kitendo cha kumjuwa huyo mzazi kwa sasa kinaweza kumfanya asimpende huyu baba yake mlezi kitu ambacho hakitamani kimtokee. Anaumizwa na kusutwa na matunzo mazuri ya baba mlezi.
 
Nenda kamuone huyo mzee wako.kisha mkutanishane wote watatu mfikie mwafaka.
Baba mzazi atajulikana kupitia DNA Kama kutakuwa na mgongano wowote kwa hizo njemba mbili.

Kama itafahamika usemi wa mama yake ni kweli, Mpe RESPECT Aliyekulea.
 
Back
Top Bottom