Simuelewi Mzazi mwenzangu, tumeachana lakini bado anasumbua

Simuelewi Mzazi mwenzangu, tumeachana lakini bado anasumbua

Bi dentamol

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2014
Posts
1,018
Reaction score
2,130
Huyu mzazi mwenzangu sielewi anatatizo gani.

Ni miaka 8 tangu tumeachana tena sio kuachana aliniaacha kisa kapata mchumba mwalimu mi kwa wakati huo nilikua jobless na mimba ya miez 6 nikarudi home. Baada ya miaka 3 nikaolewa sasa alivyogundua nimeolewa akaanza usumbufu mara nataka mtoto wangu, mara anapigaa usiku.

Nikaona isiwe tabu nikamwambia mtoto wako akimaliza la saba atakua kajitambua nitakupa nikamblock. Tumekaa miaka 3 bila mawasiliano yoyote kuhusu mtoto juzi kati kanitafuta namba mpya anaitaarifu babu yake mtoto kafariki nikampa pole.

Anadai naomba niwe naongea na mtoto kwenye cm yan nimruhusu apray part kama baba nikasema Sawa ila uwe na heshima mimi ni mke wa mtu.

Sasa ana choniuz akikusalimia kidogo mara mr wako ajambo. Mara nikiweza profile ya mr anaichukua yan maongez sio ya mtoto tena ni mimi na mr wangu. Anashida gani huyu mbuzi? Simpendi namchukia sababu kwanza aliniaacha kwa madharau.

Mbona mimi simfatilii japo aliniambia bado hajaoa? Yaani nikiweza picha profile anauliza hapo ni kwako?
 
Huyu mzazi mwenzangu sielewi anatatizo gani.
Ni miaka 8 tangu tumeachana tena sio kuachana aliniaacha kisa kapata mchumba mwalimu mi kwa wakati huo nilikua jobless namimba ya miez 6..nikarud home
Wewe umekuja kutuchora tu bado mnapendana mtu akioa singo maza, usijipe imani ya 100% kwamba unamka wako na uko peke yako
 
Haya wale mlio sema singo maza haoleki oneni shuhuda alietulia na kakaza msimamo wake hamna cha kiporo kupashika wala nini.

Saaasa game tunaligeuza kwenu wanaume

Mkikataa kulea mkaikimbia mimba,mkome kuwasumbua

NB: huyo mbuzi 😄anaumia anajua alipokuacha ungetetereka zaidi ya alivokuacha, so anatafta option ya kuku weka chini zaidi ya ulikokuwa.
 
Sasa anachoniuz akikusalimia kidogo mara mr wako ajambo
Mara nikiweza profile ya mr anaichukua yan maongez sio ya mtoto tena ni mimi na mr wangu
Anashida gani huyu mbuzi???
Mbona rahisi
Hatua ya kwanza ya kufanya kwa huyo mbuzi ni kumwambia mazungumzo yenu yawe ni kuhusu mtoto tu

Kama hatakuwa muelewa hatua ya pili ni kukata mawasiliano nae

Ama wewe unaona ugumu kwenye jambo lako ni upi?
 
Huyo jamaa ni fala....na usimuendekeze hata kidogo atakuvunjia ndoa. Mfanye ajute maisha yake yote kwa kumpiga block kila kona...au jifunze matusi ya nguoni akikugusa aambulie matusi mapya mapya afe kwa stress
 
haya wale mlio sema singo maza haoleki oneni shuhuda alietulia na kakaza msimamo wake hamna cha kiporo kupashika wala nini.

saaasa game tunaligeuza kwenu wanaume

mkikataa kulea mkaikimbia mimba,mkome kuwasumbua

NB: huyo mbuzi 😄anaumia anajua alipokuacha ungetetereka zaidi ya alivokuacha, so anatafta option ya kuku weka chini zaidi ya ulikokuwa.
Jambo aliloleta ni dogo sana kwa mtu mwenye msimamo....sidhani kama kuna msimamo hapo

Ipo dalili ya kiporo kupashwa
 
Namba yake usiisave kwenye contacts kisha set watsup who view ur profile kuwa contacts na watakaaona status yako ni contacts wako tu. Pia punguza kupokea simu zake,mara moja moja akipiga weka karibu na mumeo apokee ili kukomesha tabia yake
 
Jambo aliloleta ni dogo sana kwa mtu mwenye msimamo....sidhani kama kuna msimamo hapo

Ipo dalili ya kiporo kupashwa
Katika kosa ambalo nikilifanya Mungu aniadhibu ni hili,, kaka anilifukuza kwa dharau sana nilipauka nyumban pia baba akanifukuza nikaenda kuuza baa ninamimba ya miez 7, huyu baba kanioa wala hakuna anaejuaa kama sio mtoto wake pamoja na mitihan ya ndoa lkn kwa mtoto anamtreate kama wake ...siwezi kumlipa hilo kwakweli
 
haya wale mlio sema singo maza haoleki oneni shuhuda alietulia na kakaza msimamo wake hamna cha kiporo kupashika wala nini.

saaasa game tunaligeuza kwenu wanaume

mkikataa kulea mkaikimbia mimba,mkome kuwasumbua

NB: huyo mbuzi [emoji1]anaumia anajua alipokuacha ungetetereka zaidi ya alivokuacha, so anatafta option ya kuku weka chini zaidi ya ulikokuwa.
Ni suala la mda hicho kipora kitapashwa tu hamna mkate mgumu kwenye chai.....
 
Katika kosa ambalo nikilifanya Mungu aniadhibu ni hili,, kaka anilifukuza kwa dharau sana nilipauka nyumban pia baba akanifukuza nikaenda kuuza baa ninamimba ya miez 7, huyu baba kanioa wala hakuna anaejuaa kama sio mtoto wake pamoja na mitihan ya ndoa lkn kwa mtoto anamtreate kama wake ...siwezi kumlipa hilo kwakweli
Pole sana
 
Back
Top Bottom