Simulia "Sitosahau" ya maisha yako

Simulia "Sitosahau" ya maisha yako

Siku tulipozingirwa na kafanikiwa kuchomoka na kupotelea Msituni kwa masiku ...njaa na kiu ikazidi kukamata mwili na roho.

Katika kuzunguka huku mashaka yakiwa jirani na Mimi nikakutana na mmoja ya mwenzetu akiwa kachakaa na kachoka Kama mimi.

Tuliendelea kutafuta pakutokea bila matumaini.
Kuna sehemu tulifika tuliona maji yanashuka toka maeneo ya juu tuliyafuata kwa minyato mikali.
Tulikunywa Kama Mbwa.

Ajabu yalikuwa na chumvi nyingi kumbe haikuwa chumvi ya asili.
Tulikuja kukuta miili mingi mno ya wenzetu waliokufa imemwagwa na kuozea kwenye maji ambayo ndiyo yalikuwa yakitirirka kuja maeneo ya chini huku.

COMRADES WHO NEVER RETURN.
pole sana mkuu! Mwaka gani huo na ilikuwa katika harakati gani?
 
Nilijifanya sterling nakujikuta komando kipensi!, vibaka walivamia usiku wa manane watu wamelazwa wanatolewa mali mimi nikawa mbogo sitaki kutoa vya watu!.
Ile wamenikaribia si nikanyanyuka haraka!, kibaka aliekuwa karibu yangu alikuwa anarungu akavugumisha nikakwepa!, alivyoona nimekwepa hapohapo akaruka teke la ubavu nikadaka mguu!, ule mguu mmoja uliokuwa umebaki nikaupiga mtama hivyo lile likibaka likaanguka!.

wenzake kuona ile purukushani walikuja kama mafisi!, ghafla panga la ubapa likatua mgongoni sijakaa sawa banzi la uso ile nataka kukurupuka nikapigwa kabali!, nilikula ngumi za tumbo kama tano hivi almanusra nitapike ugali mchicha niliokuwa nimekula!, walivyoona nimekwisha habari wakaniacha, wakanishachi wakakuta nina elfu moja miatano wakabeba kwa hasira kwasababu nilikuwa mtekwaji pekee ambae niliwaletea tafrani wakanisaula nguo zote wakaniacha uchi hivyo malighafi zangu zilionekana na kila mtu pale!, na nilivivyokuwa nimeachia lile rumba hapo chini kwa mjomba aisee! niliaibika mbele ya watu tofauti tofauti pisi na zisizo pisi, wazee na wasio wazee pamoja na watoto wasiokuwa watoto!.

Hapo ndo nilijua ukitekwa unatakiwa uwe zwazwa pro max utajiepusha na vingi!.
 
Binafsi siwezi kusahau siku nilipojiwa na wazo la kwenda kuwinda swala kwenye mbuga moja hivi ya wanyama huko Mkoani Iringa! Ile naingia tu mbugani na gobore langu, nikajikuta nimeshikwa na bumbuwazi baada ya kuwakuta wanyama wa porini wa kila aina!

Yaani kuanzia swala, simba, ngiri, chui, nyati, fisi, nyani, tembo, nk!! Kuangalia mfukoni, vibali vya kuwindia ninavyo! Basi nilichofanya ni kumlenga swala mmoja aliyenona, nikampiga risasi moja tu na kumpeleka sehemu! Nikamchuna ngozi, nikambanika kwenye moto, na kumtafuna. Na kwa kweli nyama yake ilikuwa laini na tamu sana. Yaani ile siku siwezi kuisahau kamwe.
 
😁😁😁mbuga gani hiyo ulienda mkuu?
 
Back
Top Bottom