Simulizi: Akwelina

SEHEMU YA 20 YA 50



Mvua hiyo ilinyesha kwa muda mrefu sana, Yalipofika majira ya asubuhi kakinga alikuwa anatetemeka kutokana baridi kakinga alipomkagua akwelina alimuona anapumua kwa tabu hali iliyompatia Kakinga wasiwasi mkubwa sana kakinga alihisi huenda akwelina anasikia baridi akaenda katika mgahawa akanunua chai ya moto akaweka ndani ya mfuko akamuwekea katika nguo za akwelina ili apate joto, Hali ilizidi kuwa mbaya kwa akwelina ikampelekea akwelina akawa anatetemeka sana , kakinga alipoona hali imezidi kuwa mbaya aliondoka hadi hospital alipofika daktari ampima akagundua mtoto amepata ugonjwa unaotokana na baridi kali :



β€œβ€β€ kijana mtoto wako amepatwa na baridi Kali ambayo linaweza kumsababishia kifo kwahiyo inatakiwa ukalipie shilingi laki moja ( Tsh 100000 ) kwa ajili ya matibabu ya mtoto wako sawa kwa sasa nampatia huduma ya kwanza na dawa hizo zitadumu ndani ya siku tatu baada ya hapo anaweza kupoteza maisha hakikisha umelipia.



Daktari alipomaliza kumueleza Kakinga alimchukua akwelina akaenda kumpatia huduma ya kwanza .



?? Mungu wangu naitoa wapi hiyo pesa Mimi daah mungu nisaidie nipate kazi yeyote ili niokoe maisha ya akwelina ??



Yalikuwa ni maneno ya kakinga akijiuliza wapi anaweza kupata pesa kwa ajili ya kumtibu akwelina. Kakinga akaingia mtaani kutafuta kazi, kakinga alitafuta kazi ndani ya siku mbili akapata pesa kidogo akanunua mayai akayachemsha akaanza kuuza ili apate pesa kwa haraka. Safari ya Kakinga ilikuwa ngumu kutembeza mayai bila kupumzika wakati kakinga anavuka barabara lilitokea gari likamgonga kidogo kakinga akadondosha mayai yake yote ambayo alikuwa anayategemea kwa kusaidia maisha ya akwelina , Kakinga kwa hasira alisimama akafuata lile gari akafungua mlango akamkuta mwanamke akamshika mkono yule mwanamke alipomtazama kakinga , Kakinga hakuamini macho yake kwamba aliye mbele yake ni monna ..





Monna kakinga aliuachia mkono was Monna kama mtu aliyepigwa na shoti ya umeme kakinga akarudi nyuma hatua chache cha ajabu Monna alipiga magoti mbele ya kakinga Monna alikuwa anashindwa kumtazama kakinga usoni kwa matendo aliyomtendea, Monna akiwa chini amepiga magoti alishindwa kuyamiliki macho yake akayaruhusu machozi yamtawale, Mvua ya machozi ilinyesha kwa muda mrefu sana katika macho ya Monna , kakinga hata hakujali hilo alisogelea mayai yake akayaokota yote akarudi alipokuwa monna kakinga akamrushia Monna yale mayai alafu akamwambia :-



KAKINGA ?? Samahani dada umesababisha niharibu biashara yangu hii naomba pesa yangu ni shilingi elfu kumi na mbili tu ( 12000/= ) naomba hiyo pesa nina mambo mengi ya kufanya .



MONNA ?? Kakinga mume wangu leo hii unaniita mimi dada kweli daaah nimejisikia vibaya sana niangalie vizuri ni Mimi Monna mke wako au umenisahau jamani ?



KAKINGA ?? Dada eee samahani buana naomba pesa yangu unanipotezea muda hapa nani Monna mbele yangu naomba pesa yangu kabla sijakuitia watu kwamba unataka kuniibia mayai yangu .



Monna alitamani kufa akasimama akaingia kwenye gari akachukua pesa nyingi sana akamrushia kakinga, baada ya kuzirusha Monna alisema kwa sauti ya juu akiwa analia kwa uchungu mno :-



?? Chukua kakinga chukua pesa zote hizo kama unapenda pesa chukua hizo na ukitaka zaidi nitakupatia chukuaaaaaaa .



Pesa zile zilikuwa nyingi mno lakini kakinga alichukua elfu ishirini ( 20000/= ) kwakua zilikuwa ni noti za elfu kumi kumi kakinga akachukua chenchi akamrudishia Monna alafu akasema :-



β€œβ€ Chenchi yako hii hapa Dada na kingine nakushauri pesa zinahitajika kutunzwa sio kutupwa ovyo kama hivi kwa sababu pesa huwa inakimbia na siku ikikukimbia hutaipata tena jaribu kutunza pesa zako sawa kwaheri .



Kakinga alipomaliza kuzungumza maneno hayo aliondoka , Monna hakuchoka alimfuata kakinga nyuma nyuma na gari lake popote alipokwenda siku hiyo kakinga aliunguka sana katika mji huo yalipofika majira ya jioni kakinga alirudi hospital kwa daktari alipofika daktari alimwambia imebaki siku moja kwahiyo kesho anatakiwa akachukue maiti ya mtoto wake kama hatopata hizo pesa , Monna alisubiri kwa muda mrefu alipoona kakinga hatoki nje Monna alishuka kwenye gari akaingia ndani ya hospital hiyo kwa mbali akamuona kakinga anazungumza na daktari mmoja, Kakinga aliposikia maneno hayo alijaribu kumuomba sana daktari huyo lakini haikusaidia kitu .
 
Jitahid iyo story ifike kilelen
Story zinazotolewa na BURE SERIES ZOTE ZINAISHA .

Pitia Msimu wa kwanza wa Story zilizorushwa wakati ukisubiri muendelezo.

Simulizi Zinazorushwa na BURE SERIES Msimu wa kwanza

1. Simulizi: Kurudi Kwa Moza

Bonyeza hapa chini kusoma
Simulizi: Kurudi Kwa Moza

2. Riwaya: Kasri ya Mwinyi Fuad
Bonyeza hapa chini kusoma
Riwaya: Kasri ya Mwinyi Fuad

3.Simulizi: Nini maana ya mapenzi
Bonyeza hapa chini kusoma
Simulizi: Nini maana ya mapenzi

4. Simulizi : Nguvu Ya Mapenzi
Bonyeza hapa chini kusoma
Simulizi : Nguvu Ya Mapenzi

5. Mkuki Kwa Nguruwe (Kisa Cha Kweli)
Bonyeza hapa chini kusoma
Mkuki Kwa Nguruwe (Kisa Cha Kweli)

6. RIWAYA: Sauti Yake Masikioni Mwangu
Bonyeza hapa chini kusoma
RIWAYA: Sauti Yake Masikioni Mwangu

7. NDOA ILIVYOTETERESHA IMANI YANGU (Kisa Cha Kweli)
Bonyeza hapa chini kusoma
NDOA ILIVYOTETERESHA IMANI YANGU (Kisa Cha Kweli)

8. RIWAYA: Mume Gaidi
Bonyeza hapa chini kusoma
RIWAYA: Mume Gaidi

9. STORY: Sitaki Tena

Bonyeza hapa chini kusoma
STORY: Sitaki Tena

10. Nilivunja Ndoa Zangu 3 Kulipiza Kisasi (Kisa Cha Kweli)

Bonyeza hapa chini kusoma
Nilivunja Ndoa Zangu 3 Kulipiza Kisasi (Kisa Cha Kweli)
 
SEHEMU YA 21 YA 50



Kakinga akatoka nje ya hospital hiyo akiwa amechanganyikiwa sana , baada ya kakinga kutoka Monna alimfuata yule daktari akazungumza nae yule daktari alimueleza Monna mambo yote yanayomsumbua kakinga , Monna akalipa gharama zote za matibabu ya akwelina alafu akamuomba daktari huyo ampeleke sehemu ambayo akwelina yupo. Yule daktari alimpeleka chumba alichokuwepo akwelina Monna alishikwa na huruma sana alipomuona akwelina anaishi kwa kutumia gesi Monna alilia kupita kiasi akamsogelea akwelina akambusu sana akasema :-



β€œβ€β€ Nisamehe mwanangu nakupenda sana leo upo katika hali hii daah nisamehe sana binti yangu β€œβ€



Muda ulizidi kwenda Monna alikuwa bado yupo hospital anamsubiri kakinga arudi, Monna alisubiri sana lakini kakinga hakurudi yalipofika majira ya saa mbili usiku Monna aliamua kurudi nyumbani. Safari ilikuwa ndefu sana hatimae Monna alifika nyumbani alipofungua malango alimkuta Patrick kasimama mlangoni Monna alipotaka kumkumbatia Patrick , Patrick alimpiga kibao Monna ……





Safari ilikuwa ndefu sana hatimae Monna alifika nyumbani alipofungua mlango alimkuta Patrick kasimama mlangoni Monna alipotaka kumkumbatia Patrick , Patrick alimpiga kibao Monna alafu Akamshika nywele akazikunja kisha akamuuliza : Ulikuwa wapi mbuzi wewe ?



Patrick akampiga Monna kibao kingine alafu akamsukuma mbali, Kibao alichopigwa Monna kilimpatia maumivu makali sana, Monna hakuamini kama Patrick angeweza kumpiga kibao na kumfanyia unyama huo wakati Monna akiwa katika mshangao mkali damu zilimtoka katika pua yake, Monna akagusa puani akahisi kuna vitu kama maji yanatoka akayatazama vizuri maji hayo akagundua zilikuwa ni damu zinamtoka puani na sio maji .



Patrick hakutosheka akamvuta Monna akamsukuma hadi kwenye kiti akamfuata akampiga sana , Monna alipigwa sana usiku huo kipigo kilivyozidi Monna alipoteza fahamu, Patrick hakujali hilo alimuacha Monna kwenye kiti akaingia chumbani kwake bila kujali wala kumpatia msaada wowote .



Muda ulikwenda, Masaa yakasonga mbele yalizidi Monna bado hali ya Monna ilizidi kuwa mbaya, Patrick alitoka ndani akamkuta Monna bado amelala Patrick akachukua kinywaji chenye kilevi kikali ndani yake ( Pombe ) akanywa chupa tatu akili ilianza kutoka taratibu Patrick akazidisha chupa nyingine , Kinywaji hicho kiliibadirisha akili ya Patrick akaanza kusema hovyo hovyo Patrick akasogea kwenye kiti alipokuwa amelala Monna akamwangalia sana kuanzia kichwa hadi miguu, akarudia tena kumtazama Monna alipofika kwenye mapaja aliona yapo wazi kutokana na kumpiga sana Monna nguo zilipanda juu mapaja yakabaki wazi kutokana na uzuri wa Monna , Patrick alimtamani sana Akaweka chupa la kinywaji pembeni akamvua nguo zote, Patrick akamuingilia Monna bila kujali Monna kapoteza fahamu, Patrick alifanya mapenzi na Monna kwa muda mrefu hadi alipojirishisha akanyanyuka akarudi chumbani kwake akalala .



Yalipofika majira ya saa kumi na moja asubuhi kulikuwa na upepo mkali wenye baridi ndani yake kwakua mlango ulikuwa upo wazi baridi iliingia ndani kwa wingi , baridi ile ilisaidia kurudisha fahamu za Monna , Monna alipopata fahamu alikaa kwenye kiti alihisi kizunguzungu , kichwa kilikuwa kinamuuma sana , Monna alitulia kwa muda kiasi kichwa kilipotulia Monna alistuka baada ya kujiona hanavaa nguo yeyeote ( Utupu ) hali hiyo ilimpatia mashaka sana .



Monna alijisikia tofauti katika sehemu zake za siri alipojichunguza aligundua ameingiliwa kimwili, Monna alilia sana akasimama akaenda ndani akamkuta Patrick amelala akiwa uchi Monna akajua Patrick ndio aliyemfanyia kitendo kile Monna alishikwa na hasira mno akaenda jikoni akachukua kisu akarudi chumbani akamchoma Patrick kisu cha shingo alafu akavaa nguo zake akatoka nje akakimbia.



Yalipofika majira ya asubuhi na mapema Kakinga alienda hospital akiwa amechoka sana alipofika hospital Kakinga alienda katika chumba cha Daktari akamkuta Daktari anajaza karatasi , Daktari alipomuona Kakinga alimkaribisha ndani Kakinga akapiga magoti mbele ya daktari kisha akamwambia :



KAKINGA : Tafadhali Daktari naomba saidia maisha ya mtoto wangu nampenda sana nipo tayari kukutumikia maisha yangu yote nimekosa pesa nisaidie kaka yangu nimetafuta sana pesa lakini nimekosa msaidie mtoto wangu nipo tayari kufanya kazi kwako kwa muda utakao hitaji lakini mwanangu apone nisaidie ndugu yangu tafadhali .
 
SEHEMU YA 22 YA 50



Daktari alifurahi sana akasema : Oooh daah kweli unampenda sana mtoto wako simama acha kupiga magoti na mwanaume wa kweli huwa hatoe machozi mshukuru mungu kwa sababu kuna Dada amekuja hapa amekulipia gharama zote za matibabu simtambui ni nani huenda Mungu kasikia kilio chako kijana wangu kwahiyo kuwa na amani mtoto wako yupo salama kabisa twende ukamchukue pia unaruhusiwa kuondoka nae kwa sababu hali yake kwa sasa ni nzuri .



Kakinga hakuamini alinyanyua mikono juu kisha akasema : Ahsante sana Mungu wangu kwa kusikia kilio changu ?? ewe Mungu mjalie mema huyo Dada aliyempatia mtoto wangu msaada mjalie kila jema liwe kwake.



Baada ya Dua hiyo Kakinga aliondoka na Daktari akiwa na furaha sana wakaingia ndani ya chumba alichokuwepo Akwelina akamkuta anacheza juu ya kitanda Kakinga alimnyanyua Akwelina akambusu kwa furaha zote , Daktari aliingiza mkono mfukoni akachomoa pesa kidogo akampatia Kakinga na kumwambia : Tumia pesa hiyo kupata nauli na mahitaji madogo madogo Mungu atakujalia huko uendako utakuwa salama .



Kakinga alipokea pesa hizo akamshukuru sana Daktari, Kakinga akamchukua Akwelina akaondoka akiwa anacheza nae alipofika nje ya Hospital Kakinga akakutana uso kwa uso na Monna ...........



Kakinga alimchukua akwelina akaondoka akiwa anacheza nae alipofika nje alikutana uso kwa uso na monna kakinga alistuka sana kidogo amdondoshe mtoto chini, Monna alikuwa na wasiwasi sana hali iliyomshangaza kakinga sana walisimama muda kiasi hapo mlangoni pasipo kuzungumza chochote kakinga akaamua kuondoka cha ajabu kakinga alipokuwa anakwenda monna alimfuata kama kimvuli kinachofuata mwili , kakinga alizidi kupata mashaka ikabidi akimbie akiwa na akwelina katika mikono yake, Monna nae hakuchoka alimfukuza kakinga , Monna na kakinga walipokuwa wanakimbizana walizungukwa na askari wa jiji hilo wale askari walimvuka kakinga wakamfuata monna mmoja wa wale askari alitoa kitambulisho akasema :-



ASKARI __ Dada sisi ni askari kutoka kituo cha kati kuanzia sasa upo chini ya ulinzi tunaomba twende kituoni huna haki ya kupinga wito huu lakini unahaki ya kutafuta mwanasheria utakapokuwa kituoni .



Monna alianza kulia akiwa anamtazama kakinga wale askari walipoona monna anamtazama sana kakinga wakamuuliza :-



ASKARI ?? Na huyo mwanaume ni nani yako ?



MONNA ?? Ni mume wangu .



ASKARI ?? Kama ni mume wako inatakiwa tumchukue na yeye ili akatoe maelekezo , kaka tunaomba tuondoke na wewe kwa sababu wewe ni mume wa huyu dada .



KAKINGA ?? Nani weee hebu tuheshimiane huyo sio mke wangu sina mke Mimi kweli mwanzo nilikuwa ninamke lakini kwa sasa sina mke mimi ninyi mpelekeni tu .



MONNA ?? Haaaaaah !!! ?? Kakinga leo hii unanikana kweli daah siwezi amini kakinga mume wangu wewe kweli wa kunikana Mimi kakinga ??



Kakinga aliondoka eneo hilo wale askari walimpamdisha monna kwenye gari wakaenda nae kituoni.



Monna alipofika kituoni alisomewa shitaka la kufanya mauaji kwa kijana anayeitwa PATRICK alfajiri ya siku hiyo , Monna alijaribu kukataa shitaka hilo askari walimpatia adhabu kali sana monna baada ya adhabu hiyo monna akawekwa jela. Baada ya wiki moja Maisha ya kakinga akiwa na akwelina mtaani yalikuwa magumu sana hali iliyomfanya kakinga awe ombaomba katika vituo vya mabasi kakinga alikuwa anaomba pesa kwa watu akiwa amembeba akwelina mgongoni, kakinga alitembea alikuwa anatembea kuanzia asubuhi hadi majira ya usiku pesa alizokuwa anazipata alizitumia kununua chakula na nguo za akwelina.



Siku zilizidi kwenda monna alikuwa bado hataki kukubali shitaka lile , askari walijaribu kumpiga na kumpatia adhabu kali monna lakini bado monna hakukubali shitaka lile. Baada ya miezi sita kupita Monna akiwa jela , siku moja asubuhi monna alichukuliwa na askari hadi katika chumba cha mahojiano , Wale askari wakaondoka wakamuacha monna peke yake monna alikaa ndani ya chumba hicho peke yake zaidi ya masaa matatu hali iliyompatia monna wasiwasi kipindi monna akiwa anajiuliza kuna kipi alisikia mlango unafunguliwa akaingia mtu aliyevaa mavazi ya kijeshi monna alipomtazama alimuona ni yule kiongozi wa wanajeshi Monna alistuka sana aka..
 
SEHEMU YA 23 YA 50





Monna alistuka sana akasimama alipokuwa amekaa akarudi nyuma akiwa anaogopa sana, kiongozi wa wanajeshi alicheka sana baada ya kumuona monna anamuogopa:



__Sogea hapa wewe binti acha kuogopa unafikiri unaweza ukanikimbia eneo hili hahaha huwezi usipoteze muda leo nimekuja kwa wema rudi kwenye kiti tuzungumze.



Monna alikaa kwenye kiti akiwa anahofu kubwa moyoni mwake, Yule kiongozi alisema :-



β€œβ€ Binti najua hunifahamu Mimi ni nani na huenda hutambui kwanini nipo hapa leo nahitaji unifahamu Mimi ni nani. Jina langu naitwa JULIUS Mimi ni mkuu msaidizi wa jeshi la nchi hii Mimi nilikuwa na mke wangu na nimebahatika kuzaa nae mtoto mmoja ambaye mtoto huyo yupo katika mikono yenu anaitwa AKWELINA pia jina lake hilo ameandikwa nyuma ya mgongo, Sasa nataka nikusaidie lakini na wewe nahitaji unisaidie nimpate mtoto wangu, kingine jarada lako lipo mikononi mwangu naweza kufuta kesi yako kama utakubali kunisaidia nimpate mtoto wangu vinginevyo utanyongwa .



Maneno aliyosema julius yalimfanya monna atafakari sana , monna alifikiria mateso aliyokuwa anayapata ndani ya jela hiyo ikabidi akubali kushirikiana na julius, monna alipokubali kile Julius alichokuwa anataka. Julius alimchukua monna akaenda nae nyumbani kwake. Yalipofika majira ya usiku baada ya chakula monna alitoka nje alipofika nje monna alitazama sana nyota angani akiwa anatazama nyota alikumbuka, Siku moja majira ya usiku Kakinga alikuwa anatazama angani monna alipomuuliza mume wake anatazama nini angani Kakinga alimjibu kwa kusema :



?? Mke wangu wewe ndio mtu pekee ninaekutegemea katika maisha yangu Mimi ni yatima sina baba wala mama na sikubahatika kuwafahamu ndugu zangu wengine zaidi ya baba na mama yangu tu kwa sasa wewe ndio ndugu yangu wa pekee tafadhali nakukabidhi maisha yangu naomba yatunze nakuamini sana mke wangu , Tazama nyota zile alafu zungumza kwamba hautakuja kuniacha kwa hali yeyote hadi kifo kitakapo tufikia.



Kumbukumbu hizo zilimtoa machozi monna hakika monna alijutia sana kwa aliyomfanyia mume wake kipenzi , monna alijiona hana thamani tena katika hii dunia alitamani kujiua ili maumivu anayoyapata moyoni mwake yaondoke. Julius alipokuwa chumbani kwake alimuona monna nje akiwa anatazama juu, Julius alimfuata Monna akamkuta yupo analia Julius akasema :-



JULIUS ?? Kulia kwako haitokusaidia kitu cha msingi nahitaji kutambua akwelina yupo wapi ?



MONNA ?? Akwelina yupo na mume wangu mtaani ndani ya mji huu lakini kwa sasa yule sio mume wangu tena naomba ahadi yako nikifanikiwa kumkamata utanipatia nini ?



JULIUS ?? Ukifanikiwa kumpata ukaniletea mtoto nitakupatia Mali nyingi sana .



MONNA ?? Kesho tutaanza kumtafuta rasmi ndani ya mji wote huu lazima tutampata hawezi kwenda mbali na mji huu naomba niamini kwa hili .



Julius alifurahi mno baada ya kusikia maneno hayo toka kwa monna Julius akampatia monna bastola ili imsaidie katika kazi anayoenda kufanya . Asubuhi na mapema palipokucha monna alichukua bastola aliyopewa na Julius akaingia mtaani kumtafuta Kakinga , ilikuwa ngum sana monna kumpata Kakinga kwa sababu jiji hilo lilikuwa kubwa , monna alizunguka mwezi mzima akimtafuta Kakinga usiku na mchana lakini hakufanikiwa. Julius alipoona monna bado hajampata Kakinga, Julius aliungana na monna pamoja na watu wake wakaingia mtaani kumtafuta monna siku hiyo kakinga akiwa na akwelina mgongoni alikuwa anatembea kwenye magari mbalimbali akiomba pesa kama kawaida yake ghafla akakutana na Julius kakinga akakimbia Julius akampiga simu monna kwa sababu walijigawa , Kakinga akiwa anakimbia alikutana na monna mbele yake Kakinga akasimama , Monna hakupoteza muda akanyanyua bastola kisha ……



Monna hakupoteza muda akanyanyua bastola kisha akamuweka Kakinga chini ya ulinzi , Monna akamwambia Kakinga apige magoti alafu amuweke akwelina chini kakinga hakufanya kile monna alichohitaji , monna kwa hasira alimsogelea kakinga akampiga kibao muda huo huo Julius akiwa na watu wake walifika eneo hilo wakamkuta monna anamshushia mvua ya makofi Kakinga Julius alifurahi sana akasema :-



β€œβ€β€ Upo vizuri sana mwanzo nilikuwa sikuamini lakini kwa sasa nakuamini hahaha usimpige sana usije
 
SEHEMU YA 24 YA 50

ukamuumiza mtoto wangu daah mtoto wangu amekuwa mkubwa sana jamni vijana nileteeni huyo mtoto Mara moja β€œβ€β€



Julius alizungumza maneno hayo akiwa na furaha sana , Vijana waliopewa kazi hiyo walimsogelea Kakinga ili wamchukue mtoto kabla vijana hao hawajamfikia kakinga , Kakinga alimtoa akwelina mgongoni akamleta kifuani alafu akafunga vizuri nguo aliyokuwa amembebea akwelina , Walipofika wale vijana walijaribu kumchukua akwelina lakini ilikuwa ngumu sana kakinga alimbana akwelina kwa uwezo wake wote ili watu hao wasimchukue. Muda ulizidi kusonga mbele bila mafanikio wale vijana wakachukia wakaanza kumpiga kakinga, pamoja na kipigo hicho kakinga hakukubali kumuachia akwelina hali iliyompatia hasira sana Julius akamfuata kakinga alipofika akachomoa bastola yake akaweka katika Kichwa cha Kakinga akamuuliza :-



JULIUS ?? Unanipatia mtoto au nimchukue baada ya kuchukua maisha yako ?



KAKINGA ?? Ili umpate huyu mtoto lazima uniue Mimi kwanza vinginevyo huwezi kumpata kabisa.



Majibu ya kakinga yalizidi kumpatia hasira Julius akamwita monna , Monna alipofika Julius akamwambia monna ampige risasi Kakinga, Monna aliweka bastola katika kichwa cha kakinga , Kakinga akafumba macho kujiandaa kupokea kifo, cha ajabu monna alitoa ile bastola katika kichwa cha Kakinga akaweka katika kichwa cha Julius , Julius hakuamini kitendo alichofanya monna. Kakinga akiwa akiwa amefumba macho alisikia monna anamwambia :-



β€œβ€* Ondoka Kakinga wewe bado ni mume wangu nakupenda nenda kamlinde akwelina , Najuta sana kukusaliti mwanzo najua sina thamani mbele yako kwa nilichofanyiwa na sioni umuhimu wa kuishi katika dunia hii nimeshaharibu maisha yangu naomba ondoka nenda mbali lakini kumbuka nakupenda sana mume wangu ??



Monna alisema maneno hayo machozi yakiwa yanamteremka kwa wingi sana Kakinga japo alikuwa anamchukia monna lakini alimuonea huruma sana , Kakinga akaondoka na akwelina wake. Julius alikaa chini ya ulinzi kwa muda mrefu sana monna alipozubaa kidogo Julius alimnyanganya ile bastola vijana wa Julius wakamkamata monna wakaondoka moja kwa moja hadi nyumbani kwake walipofika , Julius alimfunga monna kwenye kiti akampiga sana , Julius alimpiga monna kama mwizi, kipigo kilipozidi monna alipoteza fahamu. Julius alichukua maji ya baridi akamwagia monna , Monna aliporudisha fahamu kipigo kikaendelea kama mwizi.



Baada ya wiki mmoja kupita Kakinga aliishi bila furaha kabisa mawazo yote yalikuwa kwa monna japo alimkosea sana lakini roho ya huruma ilikuwa bado inamsumbua sana kakinga , Mawazo yalipomzidi kakinga alisahau kama alikuwa na mtoto na kwakua akwelina alikuwa ameanza kutambaa alimuona ndege aina ya njiwa upande wa pili wa barabara akwelina alimtamani sana yule njiwa akwelina akamfuata muda wote huo Kakinga alikuwa yupo ndani ya dimbwi zito la mawazo , akwelina alizidi kuifuata ile njiwa alipofika katikati ya barabara lilikuja gari moja likiwa kasi sana ……







Kakinga akiwa yupo ndani ya mawazo Akwelina alikuwa anacheza pembeni ya Kakinga ghafla Akwelina akamuona ndege mzuri ( Njiwa ) upande wa pili mwa barabara, Akwelina alimtamani na kumpenda sana yule njiwa Akwelina akatambaa taratibu na kumfuata Njiwa huyo muda huo Kakinga alikuwa yupo ndani ya dimbwi zito la mawazo , Akwelina alizidi kumfuata njiwa alipofika katikati ya barabara lilikuja gari moja likiwa kasi sana Dereva wa gari hilo alimuona mtoto mbele yake akajaribu kupiga breki ili gari lisimame lakini haikuwa rahisi kutokana na kasi ya gari hilo, ghafla ukasikika mlio mkali wa gari lililosimama kwa kasi, Mlio huo uliwastua watu wote waliokuwa katika eneo hilo .



Baada ya mstuko huo Kakinga aligeuka akatazama sehemu aliyomuweka Akwelina cha ajabu hakumuona, Kakinga alichanganyikiwa akasimama na kuanza kumtafuta Akwelina, Macho ya Kakinga yalizunguka huku na huko kumtafuta Akwelina .



" Mungu wangu yule mtoto kidogo apoteze maisha mtoto mdogo kama yule kafikaje katikati ya Barabara .



Yalikuwa maneno ya Mwanamke mmoja aliyekuwa karibu na Kakinga, maneno hayo yalimstua sana Kakinga akatazama upande wa Barabara akamuona Akwelina yupo katikati ya Barabara Kakinga alikurupuka na kuingia ndani ya Barabara ili akamchukua Akwelina, Kitendo cha Kakinga kumnyanyua Akwelina na kurudi nae nyuma hatua chache Gari lingine lililokuwa linatoka chini lilimgonga Kakinga na kumrusha mbali, Wananchi wa eneo hilo walipiga simu kituo cha polisi kuomba msaada baada ya muda
 
SEHEMU YA 25 YA 50

mfupi kupita askari walifika wakawakuta wananchi wanashambulia gari kwa kupiga mawe , Askari walituliza gasia hiyo kwa kupiga mabomu ya machozi.



Wananchi walipokimbia Askari walimkuta Kakinga amelala kifudifudi walipomgeuza walimkuta mtoto katika mikono ya Kakinga , Askari walimkagua Akwelina wakagundua alikuwa mzima na hana jeraha lolote lakini Kakinga alikuwa amepoteza fahamu, Askari hao walimchukua Kakinga pamoja na mtoto wakawapeleka hospital kwa matibabu na vipimo zaidi, askari waliobaki walimshusha mtu aliyefanya ajali hiyo akashuka msichana mzuri sana mwenye sifa zote askari wakamchukua msichana huyo wakampakiza kwenye gari lao kisha wakaondoka nae .



Safari haikuwa ndefu sana muda mchache walifika hospital madaktari walifanya vipimo kwa haraka zaidi baada ya vipimo daktari alitoka nje akawakuta Askari wakiwa na Msichana aliyefanya ajali Daktari akasema : Jambo la kumshukuru mungu mtoto ni mzima na hana tatizo lolote lakini kwa upande wa kijana mliomleta atarudisha fahamu kwa muda mchache lakini vipimo vinaonesha kuna baadhi ya viungo vyake havitafanya kazi kwa sababu uti wa mgongo wake umepata matatizo kwahiyo kuanzia kwenye miguu hadi katika kiuno hata hisi chochote, Mtoto mnaweza kumchukua hana tatizo lolote.



Askari walimchukua Akwelina pamoja na yule msichana wakaenda kituo cha polisi walimkabidhi askari wa kike mtoto alafu msichana aliyefanya ajali walimueka jela kwa uchunguzi zaidi . Uchunguzi ulichukua wiki mbili askari waligundua yule msichana alikuwa hana kosa lolote , walimuachia yule msichana lakini kabla hajaondoka Msichana huyo alimfuata askari aliyekuwa ameshika kesi yake alipofika askari alisema :



ASKARI : Oooh Warda karibu na pole sana kwa kuwa hapa wiki mbili lakini ndio sheria inasema hivyo kwa sasa upo huru pia kingine naomba nikuulize kama hautojali unaishi wapi na umeolewa ?



Warda alitabasamu kidogo kisha akajibu : Hahah naishi Canada japo nimezaliwa hapa Tanzania na sijaolewa bado Kaka yangu .



ASKARI : Wooooh naomba nikuoe kama hutajali hata Mimi sina mke .



Warda alizidi kufurahi na kusema : Hahaha hapana sijaja hapa kwa ajili ya hayo mambo lakini ninaombi kwako kama itawezekana ?



ASKARI : Omba chochote usijali .



WARDA: Naomba nipatie yule mtoto nahitaji nikamlee hadi baba yake atakapokuwa sawa pia naomba ruhusa ya kumchukua yule kaka hospital nahitaji kwenda nae nje ya nchi kwa matibabu zaidi .



Yule askari japo alikuwa amechukia alimpatia yote WARDA aliyokuwa anahitaji, Warda akaondoka na askari huyo wakamfuata Askari wa kike aliyepewa Akwelina ili akamtunze , yule askari alimpatia WARDA mtoto baada ya kupatiwa mtoto Akwelina akaondoka hadi hospital akamchukua Kakinga akaenda nae hotelini alipokuwa anaishi. Baada ya mwezi mmoja maisha ya Monna yalizidi kuwa magumu sana , Monna alikuwa mtu wa kulia usiku na mchana hali iliyompelekea Monna kupoteza tumaini la kuishi tena , Julius alimtesa sana Monna bila huruma, Usiku wa siku ya pili Julius akiwa ndani kwake alipigiwa simu akapokea kisha akasema : Ndio kiongozi wangu, ndio , ndio , ndio hapana hajasema hadi sasa ....... Aaah bado yupo kwenye kamba .



Mpigaji akamwambia Julius : MALIZA MAISHA YA HUYO MSICHANA HARAKA .



Julius alifikiria kidogo kisha akajibu : Sawa kiongozi wangu kazi imeisha .







MONNA : Jamani hongera sana kwa kustiri mwili wako pia ni wazo zuri la kuhitaji kuolewa kwa sababu kama mali unazo, nani huyo mwenye bahati ya kupendwa na Msichana mzuri na tajiri kama wewe ?



WARDA : Ndugu yangu nahitaji Kakinga anioe nafsi yangu imemkubali anaonekana ni mwema sana, Ukweli nimetokea kumpenda sana Kakinga nahitaji awe mume wangu kwa gharama yeyote .



Monna alistuka sana akasema : ??Hapana yaani haiwezekani kwanini lakini Kwanini tafadhali Dada yangu usinifanyie hivyo nampenda bado, Ukweli nampenda sana Kakinga wangu nimetoka nae mbali sana leo hii unataka kuninyanganya Kakinga wangu kweli daah hapana nakuomba usinifanyie hivyo Dada yangu ??



Monna alijikuta anazungumza maneno mengi mbele ya Warda , Warda alishindwa kuelewa Monna alichokuwa anazungumza Warda akamshika bega Monna kisha akamwambia : Tulia kwanza Dada
 
SEHEMU YA 26 YA 50

usizungumze maneno kama hayo unajua sikuelewi alafu mimi ni mdogo kwako usiniite Dada najisikia vibaya sana nitaonekana kama nakunyanyasa , Zungumza taratibu ili nikuelewe sawa ?



Monna bado alikuwa amechanganyikiwa akaendelea kusema : Kakinga ni Mume wangu mimi, alinioa miaka mingi iliyopita sasa inakuaje unataka kumchukua Kakinga wangu jamani .



Ilikuwa ngumu sana Warda kuyaelewa maneno ya Monna, Warda alimtuliza Monna kisha akasema : Taratibu Dada kuna shida gani mbona sikuelewi kabisa na kwanini unasema unampenda Kakinga, kwani Kakinga unamfahamu ?



Monna alijibu kwa upole : Ndio Kakinga ni mume wangu mimi .



Warda alistajabu sana akasema : Nini ! sasa kwanini hujaniambia kama ni mume wako mbona kama siamini unachonieleza ?



Warda alikasirika sana kwa sababu moyo wake ulikuwa umeshampenda sana Kakinga, Warda aliamua kuondoka akamuacha Monna Sebuleni, Monna alipomuona Warda kaondoka akiwa amekasirika alifurahi sana kisha akasema : Warda mdogo wangu laiti ungejua jinsi ninavyompenda Kakinga hakika siwezi kukubali umchukue .



Yalipofika majira ya usiku Warda akiwa chumbani kwake siku hiyo alikosa usingizi kabisa maneno aliyoambiwa na Monna yalimtesa sana ikampelekea Warda kutoka chumbani kwake akaelekea chumbani kwa Kakinga kwa bahati nzuri alimkuta Kakinga bado hajalala , Warda alifika akapanda juu ya kitanda kisha akamuuliza : Kakinga hujalala kumbe ?



Kakinga akijibu : Ndio sijalala nipo macho Dada yangu lakini inaonekana wewe ni msichana mdogo una miaka mingapi ?



WARDA : Nina miaka kumi na tisa .



Jibu la Warda lilikuwa tofauti sana, Kakinga aligundua Warda hayupo sawa akamuuliza : Kuna tatizo ?



Warda aligeuza kichwa chake akamtazama Kakinga kwa muda mrefu kisha akamwambia : Kakinga leo naomba nikueleze ukweli kuhusu moyo wangu sijui utanitafsiri vipi lakini siwezi kuficha hisia zangu kwako, Kakinga moyo wangu umevutiwa sana na wewe, Ukweli NAKUPENDA sana Kakinga Moyo wangu unakuhitaji sana japo najua una mke wako nahisi unampenda zaidi, lakini hata mimi nakupenda nahitaji kuwa mke wako haijalishi kama ni Mke wa pili nitakubali tu.



Moyo wa Kakinga ulipata mstuko wa ajabu sana baada ya kusikia maneno hayo toka kwa binti mrembo na mwenye fedha kama Warda, Kakinga hakuhitaji kupoteza bahati hiyo alimkumbatia Warda kwa furaha, Machozi ya furaha yalimtoka Kakinga kwa wingi, Kakinga akasema : ?? Daaah nilijua kuwa sitopendwa tena katika hii Dunia kutokana na ulemavu wangu huu ahsante sana Mungu kwa kumleta Warda katika mikono yangu, Nisikilize Warda hata mimi nakupenda, na umeniambia kwamba mimi nina mke hapana Sina mke kwa sasa japo mwanzo niliwahi kuwa na mke lakini kwa sasa sina najua Monna atakuwa kakueleza mengi mno nami acha nikueleze ukweli ni kweli miaka mingi iliyopita Monna alikuwa mke wangu lakini alinisaliti na akaomba taraka yake nami nikampatia taraka yake huo ndio ulikuwa mwisho wa Ndoa yetu .



Warda alifurahi mno akarudi chumbani kwake akiwa na furaha sana . Asubuhi palipokucha Warda alichukua gari lake akamchukua Kakinga alafu akamwita Monna akampatia pesa za kutosha alafu akamwambia : Naenda mbali sana na Kakinga kwa ajili ya matibabu naomba tunza vitu vyangu sawa .



Warda alitoka nje akaingia ndani ya Gari Kakinga akauliza : Warda tunakwenda wapi ?



WARDA : Tunakwenda Canada kidogo Mume wangu mtarajiwa.



Kakinga alistuka kisha akasema : Naomba mchukue Akwelina tafadhali usimuache na Monna .



Warda alirudi ndani akamchukua Akwelina wakaenda uwanja wa ndege kisha wakaondoka kwenda Canada . Walipofika Warda alitafuta madaktari bingwa wakampatia Kakinga matibabu ya uhakika , baada ya mwezi mmoja kupita Kakinga alipona akarudi katika hali yake ya awali, Warda hakupoteza muda akiwa huko huko Canada akafunga ndoa na Kakinga baada ya ndoa hiyo wakarudi Tanzania .



Asubuhi ya Siku ikiyofuata Monna akiwa Hotelini aliona mlango unasukumwa akaingia Warda akiwa na Kakinga wakati huo Kakinga alikuwa amembeba Akwelina, Monna alishangaa kumuona Kakinga akiwa mzima kama zamani Monna alipatwa na furaha ya ajabu alipotaka kumkumbatia Kakinga , Warda alimshika mkono Monna kisha akamwambia : Samahani Dada Unapotaka kumsogelea au kumgusa
 
SEHEMU YA 27 YA 50

Mume wangu omba ruhusa kwanza.



Kauli ya Warda ilimshangaza sana Monna, Monna akasema : Mume wakoo! ?? .WARDA: Ndio mume wangu kuna kitu hujaelewa hapo Dada yangu ? Monna alihisi kuchanganyikiwa akaweka mikono kichwa mwake kisha akasema : Bado sijakuelewa Mdogo wangu unamanisha nini kusema Kakinga ni Mume wako ilimhali unajua kila kitu, acha utani kama huo buana utaniua kwa presha.







WARDA : Sawa fanya haraka nina kiu kikali sana .



Monna alichukua pesa akatoka nje akaenda kununua sumu, Maji pamoja na Bomba la Sindano akafyonza sumu kisha akatoboa chupa la maji kwa kutumia sindano kisha akafinyia sumu hiyo ndani ya chupa la maji aliyoinunua alafu akarudi nyumbani akampelekea maji yenye Sumu Warda, Warda alichukua maji hayo bila wasiwasi wowote kutokana na kiu kikali alichokuwa nacho, Warda alihitaji kunywa maji yale kwa haraka lakini kabla glasi ya Maji haijafika katika mdomo wa Warda, Kakinga alichukua glasi hiyo kisha akamwambia Mke wake : Hivi mke wangu unawezaje kunywa maji kabla ya kumchumu mume wako eee ?? sasa hunywi haya maji hadi unibusu Mumeo .



Kiu kilizidi kumsumbua Warda akamwambia Kakinga : Mume wangu jamani nina kiu kikali nitakufa kwa kiu Mume wangu tafadhali nipe maji.



Kwakua Kakinga alikuwa anapenda sana kumtania mke wake hakujali maneno ya Mke wake, Kiu kilizidi kumshika Warda, Warda akasimama na kumfukuza Mume wake katika purukushani hiyo glasi ya Maji ilidondoka chini ikavunjika. Baada ya Glasi ya maji kuvunjika Monna alichukia sana baada ya kuona glasi yenye maji ambao yanasumu ndani yake imevunjika Monna aliamua kuondoka akaenda jikoni na kusema : Una bahati sana leo umepona Warda lakini kumbuka bado Upo katika mikono yangu nitakupata tu wewe Subiri utaona .



Glasi ya maji ilipovunjika Warda alikasirika sana Kakinga alipoona mke wake amekasirika alichukua pesa haraka haraka akaenda Dukani akanunua maji muda mchache akarudi akampatia maji mke wake , Wakati Warda anakunywa maji walimuona Akwelina anawafuata Kakinga akasema : Dede Dede simama mama yangu enhee njoo, Njoo aaah umeanguka haha Simama tena Mtoto wangu simama basi enhee njoo njoo eyaa mwaaah, Umeanza kutembea lakini umechelewa sana mtoto wangu kwa sababu nimekupata muda mrefu mno ndio waanza kutembea leo .



Warda alijibu : Hiyo huwa inatokea kutokana matunzo lakini sio mbaya kwakua ameanza kutembea basi ni jambo la kumshukuru Mungu inatakiwa akue haraka haraka ili ampokee mdogo wake wa kike .



KAKINGA : Weee unasemaje lazima Mtoto wangu awe wa kiume kama Mtoto wa kike huyu hapa tunae .



Warda alitabasamu kisha akasema : Na ndio hupati Mtoto wa Kiume hapa tutazaa wakike hadi ukome haha ??



Siku baada ya siku ujauzito wa Warda ulizidi kukua taratibu taratibu , Kakinga alijitahidi sana kumpatia furaha na chochote alichokuwa anahitaji Warda, Warda alideka mno hali iliyozidi kumpatia maumivu makali Monna .



Maisha yalizidi kusogea mbele baada ya miezi kadhaa Ujauzito wa Warda ulikuwa mkubwa zaidi hali ikabadirika Ujauzito ulianza kumsumbua Warda kutokana na kula vyakula vyenye mafuta mengi hali ya Warda ilibadirika na kuwa mbaya Kakinga alimchukue Warda akampeleka hospital walipofika Hospital Madaktari walimfanyia Vipimo Warda kisha Daktari mmoja akamfuata Kakinga akamwambia : Kijana kutokana na hali ya mke wako ilivyo inabidi apewe kitanda ili apate matibabu zaidi kwahiyo chukua bili hii nenda Dirishani kalipie sawa ?



KAKINGA: Sawa Daktari .



Kakinga alisogea dirishani haraka akampatia karatasi ya malipo mtoa huduma kisha akaingiza mkono mfukoni ili alipe bili akajikuta pesa hana Kakinga alichanganyikiwa akamwambia mtoa huduma : Samahani Dada yangu nimesahau pesa nyumbani naomba nikuachie simu yangu inauzwa bei kubwa sana naomba nipatie dawa hizo ili nisaidie maisha ya mke wangu alafu naomba nipe dakika kumi nakuletea pesa yako yote nisaidie tafadhali ?? .



Mtoa huduma akajibu: Sio rahisi Kaka yangu kufanya hivyo utakavyo cha kufanya wewe fuata pesa kwanza kabla ya huduma nikifanya hivyo naweza kupoteza kazi yangu Kaka naomba radhi kwa hili .
 
SEHEMU YA 28 YA 50



Kakinga hakuchoka alimfuata Daktari aliyempatia karatasi ya malipo kamueleza matatizo yake Daktari akamwambia : Nesi yupo sahihi kwa sababu siku hizi huduma hazitolewi pasipo kulipa kwanza alafu ni bora ungefanya haraka kwani hali ya mke wako ni mbaya sana, Usipoteze muda hapa fuata pesa kijana .



KAKINGA: Sawa Daktari naomba linda uhai wa mke wangu narudi sasa hivi Kaka yangu .



DAKTARI: Sawa jitahidi kuwahi .



Kakinga alipanda kwenye gari lake moja kwa moja hadi nyumbani akamkuta Monna anampatia Akwelina chakula Kakinga alipitiliza hadi chumbani kwake, Monna alisimama akafunga mlango mkubwa alafu ufunguo akauchomoa akauficha ndani ya sidilia yake , Kakinga alichukua pesa za kutosha haraka haraka akatoka nje ili kuwahisha fedha Hospital, Kakinga alipoufikia mlango cha ajabu mlango ulikuwa umefungwa Kakinga alijaribu kufungua mlango kwa pupa lakini mlango haukufunguka Monna akamsogelea Kakinga akamwambia: Kakinga leo huondoki ufunguo ninao Mimi nina maongezi na wewe Kakinga na nahitaji majibu mazuri laaa sivyo sikupi ufunguo .



Kakinga aligeuka kwa hasira kisha akasema: ?? Unasemaje wewe naomba nipatie ufunguo haraka , huu sio muda wa matani Monna hali ya Warda sio nzuri na ninahitajika nipeleke pesa kwa matibabu yake nipatie ufunguo haraka Monna .



MONNA : Mimi sijali hilo Kakinga na bora afe tu ili nikupate kijana ninaekupenda kuliko unavyofikiria, siwezi kukubali Kukupoteza kwa hali yeyote Kakinga wangu nakupenda .



Kakinga alizidi kushikwa na hasira akasema kwa sauti ya juu : Nipatie ufunguo monnaaaaaaa sina muda wa kupoteza mjinga wewe ??



Monna hakujali akajibu : Sikupi Ufunguo na fanya utakavyo lakini sikupi ufunguo hadi ufanye nitakacho usinitishe ufunguo hauta upata na nikuambie ukweli ufunguo upo katika nguo zangu nimeuficha lakini ndio huwezi kuupata Kakinga wangu .



Kakinga alishikwa na hasira zaidi akamfuata Monna akampiga kibao alafu akamkagua katika nguo zake ili achukue ufunguo, Monna nae hakukubali kukaguliwa, Vurugu iliendelea kwa muda mrefu sana , wakati vurugu zinaendelea Akwelina hakuwa mbali nao , Kakinga alishindwa kuvumilia akamsukuma Monna kwa nguvu Monna akampamia Akwelina kwa bahati mbaya Akwelina akajigonga kwenye ukuta akapoteza fahamu papo hapo.



Monna hakuamini kama ujinga wake ungeweza kuleta madhara kama hayo, Kakinga akambeba Akwelina Monna akafungua mlango haraka wakapanda kwenye gari wakaondoka hadi hospital. Kakinga akiwa amembeba Akwelina alikwenda katika chumba alichomuacha Warda kwa ajili ya kumfuata Daktari aliyempatia karatasi ya malipo, Walipofika katika chumba hicho Kakinga alisukuma mlango kwa haraka walipofika ndani Kakinga alimuona Warda anazungumza na Daktari, Daktari huyo aliposikia mlango umefunguliwa kwa kasi alistuka na kugeuka, Kakinga na Monna hawakuamini kumuona Daktari huyo ni PATRICK ?? Monna ali ..........





Monna na Kakinga hawakuamini kama daktari yule ni PATRICK ?? Monna aliogopa mithiri ya kudondoka chini , moyo wake ulipata mstuko wa ajabu sana kwa kumuona Patrick akiwa hai , kakinga alishikwa na hasira sana kwa kumuona Patrick mbele yake :



"__Mmeambiana mkutane ndani ya hospital hii sio ?

Kakinga alimuuliza monna akiwa na hasira mno , hasira zilichanganya kichwa chake hadi akasahau kama akwelina anahitaji tiba japo alikuwa katika mikono yake



"__Hapana hapana huyu sio mtu Kakinga, Patrick alishakufa muda mrefu huyu sio yeye " Monna alimjibu Kakinga akiwa anatetemeka sana na kujificha nyuma ya mgongo wa Kakinga. Kakinga alishindwa kuelewa alichokuwa anasema monna .



""__Usiogope monna Mimi bado nipo hai sijafa japo unajua nilikufa na labda nikueleze kitu monna serikali ipo mikononi mwangu. Unajua kwanini nilikuhitaji kipindi kile? Nilikuhitaji kwa sababu nilihitaji kupata ladha ya mapenzi yako tu na kutokana na tamaa zako nilifanikiwa hilo. Siku uliyotoroka ndio ingekuwa siku ya mwisho kwako kuishi katika hii dunia, unahabati sana kutoroka siku ile. Kakinga huyu warda ni mdogo wangu na ajali ile Mimi ndio niliyoitengeneza nikiwa na mdogo wangu warda tulipanga suala hilo *



Yalikuwa maneno ya Patrick akimueleza monna , ilikuwa ngumu upande wa Kakinga kuamini kama warda mke wake ni mdogo wa adui yake aliyemnyanganya mke wa zamani ( monna ) patrick hakuishia
 
SEHEMU YA 29 YA 50

hapo aliendelea kusema :-



**" Haha najua huwezi kuamini Kakinga lakini ukweli ndio huo kipindi ukiwa na mawazo nilikuwa upande wa pili wa barabara nikamtuma njiwa wa bandia kwa kutumia remote control nilifanikiwa kumvuta mtoto katikati ya barabara hatimae ajali ikatimia, Nilimtumia mdogo wangu kwa kutumia mapenzi ili iwe rahisi kukupata na kingine umechelewa sana Kakinga mimba uliyompatia mdogo wangu tumeshaitoa kwa sababu kazi yake imeshaisha. Ooooh kakinga najua inakuuma sana pole hahaha, pia unajua lengo la kufanya yote hayo ni nini .. Lengo ni mtoto huyo kwa bahati nzuri umemleta mwenyewe kwa maana tulitaka tumfuate huko hotelini .



Bado akili ya kakinga ilikuwa inapinga ukweli huo , Ghafla akatokea Julius ( kiongozi wa wanajeshi ) akiwa na wanajeshi wengi akamchukua mtoto katika mikono ya kakinga alafu akamfunga pingu , Warda alisimama akamfuata Kakinga baada ya kuona amefungwa pingu akamwambia :-



"" Najua huwezi kuamini Kakinga mume wangu hiki kilichotokea mbele yako amini huu ndio ukweli pamoja na yote nakupenda sana kakinga wangu japo hii ilikuwa ni kazi ""



Warda alipomaliza kumwambia kakinga maneno hayo alishika mikono ya kakinga akampatia ufunguo wa pingu alafu akaondoka.

Julius alitoa amri kwa wanajeshi wake wakamchukua Kakinga na monna wakatoka nje moja kwa moja hadi kwenye gari safari ikaanza japo kakinga na monna hawakutambua wapi wanaelekea wakiwa ndani ya gari Patrick alimpatia tiba akwelina baada ya muda mfupi akwelina alirudisha fahamu akaanza kumlilia Kakinga , Patrick ikabidi ampatie mtoto Kakinga , Akwelina alipofika katika mikono ya kakinga alitulia.

Safari ilizidi kusonga mbele Kakinga akiwa na akwelina alishusha mikono chini akafungua zile pingu alizofungwa alafu akatulia . Gari zilikuwa zinaondoka kwa mwendo wa kasi sana zikafika katika daraja kubwa ambalo chini ya daraja hilo lilikuwa na mto , zile gari zilipunguza mwendo ili kuvuka daraja hilo. Gari zilipofika katikati ya daraja Kakinga alifungua mlango wa gari akatoka nje ya gari akajirusha akiwa na akwelina katika mikono yake



a ndani ya gari baada ya kumuona kakinga amejirusha hawakuamini kama kakinga angekuwa jasili kiasi hicho, monna alilia sana alipohitaji kujirusha kujirusha ili amfuate kakinga Patrick alimzuwia akamrudisha ndani ya gari wakaendelea na safari Julius alikuwa na hasira sana akiwa ndani ya gari.



Kakinga akiwa na mtoto mikononi mwake alisukumwa na maji ya mto ule akiwa anajipigiza katika mawe mbalimbali yaliyokuwepo ndani ya mto huo , Maji yalizidi kumsukuma Kakinga hali iliyompatia wakati mgumu sana kupambana na maji hayo ili kusaidia maisha ya akwelina. Pamoja na kupambana na maji hayo lakini maji yalikuwa na nguvu sana walimzidi nguvu Kakinga akapoteza fahamu akiwa ndani ya mto huo baada ya kakinga kupoteza fahamu maji yalimsukuma hadi nje ya mto katika msitu mkubwa. Baada ya muda mrefu kupita alikuja Mzee mmoja ambaye alikuwa mvuvi alipofika sehemu aliyokuwa anaitumia kuvua samaki alishangaa sana kumuona kijana mmoja akiwa amemshikilia mtoto kifuani kwake, Yule mvuvi alimsogelea Kakinga akamvuta ili kumtoa ndani ya maji yale ya mto , Mvuvi alifanikiwa kumtoa nje Kakinga kwakua yule mvuvi alikuwa anayatambua maji vizuri alimsaidia Kakinga kumtoa maji yalikuwa ndani ya kifua chake kwa uwezo mkubwa aliokuwa nao mvivu huyo alifanikiwa kurudisha fahamu kwa Kakinga .



Kakinga alipopata fahamu yule mvuvi alimchukua akaondoka nae hadi nyumbani kwake, Hali ya akwelina ilikuwa mbaya japo yule mvuvi alijitahidi sana kumpatia tiba mtoto lakini bado haikusaidia kitu, Siku zilizidi kusonga mbele bado hali ya akwelina ilizidi kuwa mbaya. Usiku mmoja Kakinga akiwa nje ya nyumba ya mvuvi yule alikuwa amembeba akwelina machozi yakimteremka , Yule mvuvi aliporudi nyumbani alimkuta Kakinga analia .



"" Kwanini unalia kijana wangu ? Mvuvi alimuuliza Kakinga baada ya kumuona analia sana .



"" Daah nafsi inaniuma sana babu binti huyu ndio tumaini langu la mwisho kwanini anataka kuniacha peke yangu kama akifa bora na Mimi nife sioni sababu ya kuishi tena sina familia nyingine zaidi yake huyu mtoto ndio familia yangu.
 
SEHEMU YA 30 YA 50



Yalikuwa maneno ya kakinga akimjibu mvuvi huyo. Baada ya wiki mbili akwelina alionesha dalili ya kupoteza maisha Kakinga alilia sana alitambua akwelina amepoteza maisha yule mvuvi alichimba kaburi kwa ajili ya maziko ya akwelina, Kakinga alibeba mwili wa akwelina akaenda nao hadi katika kaburi lile alipotaka kumzika akwelina cha ajabu akwelina alipiga chafya alafu akaanza kulia Kakinga hakuamini kama akwelina hakupoteza maisha. Maisha ya monna yalikuwa magumu sana ndani ya utawala wa Julius , Monna akiwa ndani ya mateso hayo alimuona warda anakuja mbele yake akiwa na msichana mmoja amefungwa kitambaa usoni alipofika karibu yake warda alifungua kitambaa kile monna alistuka sana kumuona mama aliyempatia AKWELINA siku ya kwanza ndani ya msitu , Warda akasema :-



WARDA ?? Unamkumbuka huyu mama ? Najua unamkumbuka huyu ndio mama yake na akwelina aliyekupatia mtoto wake wewe . Unafikiri alikufa hapana bado yupo hai na kama ulikuwa hufahamu huyu ni mke wa Julius , Unajiuliza nimejuaje yote haya usijali kwakua upo hapa utafahamu kila kitu.



Monna alishikwa na butwaa kwa maneno aliyosikia toka kwa warda. Baada ya miaka sita kupita akwelina alianza kukua akiwa na afya njema siku zote akwelina alikuwa anapenda kuwa karibu na Kakinga kutokana na upendo wa juu sana aliokuwa nao akwelina kwa kakinga. Japokuwa hali ilikuwa mbaya na maisha ya chini waliyokuwa wanaishi lakini furaha zilitawala mioyo , Siku moja majira ya asubuhi akwelina alimfuata kakinga ( baba mlezi ) akamuuliza :



"" Baba hivi Mimi nina mama kweli ?



.......



Kakinga alitulia kimya kwa muda mrefu sana bila kujibu chochote , Akwelina akamuuliza Kakinga kwa mara nyingine : Baba mbona hunijibu nataka kumuona Mama yangu .



Kakinga alimgeukia Akwelina kisha akamwambia : Binti yangu siku natamani sana kukueleza kitu muhimu lakini kwa sasa muda haujafika kuwa na amani sawa ?



Akwelina alipoteza furaha akasema : Marafiki zangu wote wana Mama na Baba kila siku wanacheza na Mama zao kwanini Mimi sina Mama ?



KAKINGA : Mtoto wangu usijisikie vibaya inatakiwa uishi na kukubaliana na hali iliyopo kwa sababu leo nipo na wewe vipi kama kesho na mimi nikiwa sipo wewe utafanyaje ?



Maneno hayo yalimfanya Akwelina aogope akajikuta anasema : Baba unataka kunikimbia na wewe ?



Kakinga alimbeba Akwelina na kumwambia : Binti yangu sote niwapitaji katika hii Dunia, kila kitu kitaondoka na hakuna ataebaki mzima sote tutakufa Mtoto wangu .



Akwelina alimkumbatia Kakinga akaanza kulia Kakinga akamuuliza : Unalia nini binti yangu ?



Akwelina alijibu : Sihitaji uondoke Baba tafadhali usiniache peke yangu Nakupenda sana Baba yangu kipenzi



Kakinga alimtuliza Akwelina moyoni mwake akasema : Akwelina upo sahihi binti yangu una haki ya kupata mapenzi toka kwa Mama yako ili nawe uwe na furaha kama watoto wengine lakini simjui Mama yako Binti yangu na sijui nifanyaje ili nawe umuone Mama yako daah ?? Lakini usijali mtoto wangu nitakulea hadi mwisho wa maisha yangu Mimi ndio Mama na ndio Baba yako pia .



Siku hiyo iliisha Akwelina akiwa hana furaha na alikuwa mnyonge sana, Usiku ulipotanda Akwelina alimfuata Babu ( mvuvi ) alimkuta Babu yupo anaimba wimbo nzuri wa kilugha, Wimbo aliyokuwa anaimba Babu ulimvutia sana Akwelina japo alikuwa hana furaha wimbo ule ulimpatia faraja moyoni mwake, Akwelina alipofika karibu ya Babu alikaa karibu yake kisha akamuuliza Babu : Babu unaimba wimbo mzuri sana huo wimbo una maana gani ?



Babu alicheka mno kisha akajibu : Haha Akwelina mjukuu wangu wimbo huu ni wa asili ya kwetu nakumbuka nilikuwa namwimbia marehemu mke wangu ambaye ni Bibi yako , kwahiyo siku nikimkumbuka basi huwa naimba wimbo huu kama ulivyosikia .



Akwelina akauliza tena : Hivi Babu Mama yangu yupo wapi ?



Babu alishanga mno kisha akajibu : Mmnh swali hilo gumu sana mjukuu wangu nenda kamuulize baba yako, lakini usijali siku moja Mama atarudi na utamuona sawa mjukuu wangu kwahiyo ondoa wasiwasi .
 










Nakuaminia mkuu
 










Nakuaminia mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…