Abdallahking
JF-Expert Member
- Mar 19, 2018
- 3,985
- 10,840
- Thread starter
- #21
SEHEMU YA 20 YA 50
Mvua hiyo ilinyesha kwa muda mrefu sana, Yalipofika majira ya asubuhi kakinga alikuwa anatetemeka kutokana baridi kakinga alipomkagua akwelina alimuona anapumua kwa tabu hali iliyompatia Kakinga wasiwasi mkubwa sana kakinga alihisi huenda akwelina anasikia baridi akaenda katika mgahawa akanunua chai ya moto akaweka ndani ya mfuko akamuwekea katika nguo za akwelina ili apate joto, Hali ilizidi kuwa mbaya kwa akwelina ikampelekea akwelina akawa anatetemeka sana , kakinga alipoona hali imezidi kuwa mbaya aliondoka hadi hospital alipofika daktari ampima akagundua mtoto amepata ugonjwa unaotokana na baridi kali :
“”” kijana mtoto wako amepatwa na baridi Kali ambayo linaweza kumsababishia kifo kwahiyo inatakiwa ukalipie shilingi laki moja ( Tsh 100000 ) kwa ajili ya matibabu ya mtoto wako sawa kwa sasa nampatia huduma ya kwanza na dawa hizo zitadumu ndani ya siku tatu baada ya hapo anaweza kupoteza maisha hakikisha umelipia.
Daktari alipomaliza kumueleza Kakinga alimchukua akwelina akaenda kumpatia huduma ya kwanza .
?? Mungu wangu naitoa wapi hiyo pesa Mimi daah mungu nisaidie nipate kazi yeyote ili niokoe maisha ya akwelina ??
Yalikuwa ni maneno ya kakinga akijiuliza wapi anaweza kupata pesa kwa ajili ya kumtibu akwelina. Kakinga akaingia mtaani kutafuta kazi, kakinga alitafuta kazi ndani ya siku mbili akapata pesa kidogo akanunua mayai akayachemsha akaanza kuuza ili apate pesa kwa haraka. Safari ya Kakinga ilikuwa ngumu kutembeza mayai bila kupumzika wakati kakinga anavuka barabara lilitokea gari likamgonga kidogo kakinga akadondosha mayai yake yote ambayo alikuwa anayategemea kwa kusaidia maisha ya akwelina , Kakinga kwa hasira alisimama akafuata lile gari akafungua mlango akamkuta mwanamke akamshika mkono yule mwanamke alipomtazama kakinga , Kakinga hakuamini macho yake kwamba aliye mbele yake ni monna ..
Monna kakinga aliuachia mkono was Monna kama mtu aliyepigwa na shoti ya umeme kakinga akarudi nyuma hatua chache cha ajabu Monna alipiga magoti mbele ya kakinga Monna alikuwa anashindwa kumtazama kakinga usoni kwa matendo aliyomtendea, Monna akiwa chini amepiga magoti alishindwa kuyamiliki macho yake akayaruhusu machozi yamtawale, Mvua ya machozi ilinyesha kwa muda mrefu sana katika macho ya Monna , kakinga hata hakujali hilo alisogelea mayai yake akayaokota yote akarudi alipokuwa monna kakinga akamrushia Monna yale mayai alafu akamwambia :-
KAKINGA ?? Samahani dada umesababisha niharibu biashara yangu hii naomba pesa yangu ni shilingi elfu kumi na mbili tu ( 12000/= ) naomba hiyo pesa nina mambo mengi ya kufanya .
MONNA ?? Kakinga mume wangu leo hii unaniita mimi dada kweli daaah nimejisikia vibaya sana niangalie vizuri ni Mimi Monna mke wako au umenisahau jamani ?
KAKINGA ?? Dada eee samahani buana naomba pesa yangu unanipotezea muda hapa nani Monna mbele yangu naomba pesa yangu kabla sijakuitia watu kwamba unataka kuniibia mayai yangu .
Monna alitamani kufa akasimama akaingia kwenye gari akachukua pesa nyingi sana akamrushia kakinga, baada ya kuzirusha Monna alisema kwa sauti ya juu akiwa analia kwa uchungu mno :-
?? Chukua kakinga chukua pesa zote hizo kama unapenda pesa chukua hizo na ukitaka zaidi nitakupatia chukuaaaaaaa .
Pesa zile zilikuwa nyingi mno lakini kakinga alichukua elfu ishirini ( 20000/= ) kwakua zilikuwa ni noti za elfu kumi kumi kakinga akachukua chenchi akamrudishia Monna alafu akasema :-
“” Chenchi yako hii hapa Dada na kingine nakushauri pesa zinahitajika kutunzwa sio kutupwa ovyo kama hivi kwa sababu pesa huwa inakimbia na siku ikikukimbia hutaipata tena jaribu kutunza pesa zako sawa kwaheri .
Kakinga alipomaliza kuzungumza maneno hayo aliondoka , Monna hakuchoka alimfuata kakinga nyuma nyuma na gari lake popote alipokwenda siku hiyo kakinga aliunguka sana katika mji huo yalipofika majira ya jioni kakinga alirudi hospital kwa daktari alipofika daktari alimwambia imebaki siku moja kwahiyo kesho anatakiwa akachukue maiti ya mtoto wake kama hatopata hizo pesa , Monna alisubiri kwa muda mrefu alipoona kakinga hatoki nje Monna alishuka kwenye gari akaingia ndani ya hospital hiyo kwa mbali akamuona kakinga anazungumza na daktari mmoja, Kakinga aliposikia maneno hayo alijaribu kumuomba sana daktari huyo lakini haikusaidia kitu .