Simulizi: Asante kwa Kunifuta Machozi (Hisia Zangu)

Simulizi: Asante kwa Kunifuta Machozi (Hisia Zangu)

SEHEMU YA 19 KATI YA 50

?Mimi na wewe.?

?Sawa.?

Wakakata simu zao.

Tayari alikuwa ameshafika chumbani kwake. Akaweka vitabu vyake kabatini kisha akajitupa kitandani. Mawazo yakaanza kufukuzana.

Alikuwa akimuwaza Pam.

***

Edo aliyatoa macho yake kwa mshtuko. Bado hakuamini kama kweli email ile mpya ilitoka tena kwa Lilian. Ni dhahiri Lilian alichanganyikiwa kabisa!

?Naanza kupata wasiwasi sasa,? akajisemea Edo.

Lilian alikuwa amemwandikia ujumbe wenye maneno makali sana. Ilikuwa vigumu kuamini kama ni kweli ujumbe ule ulitoka kwake.

Ujumbe wenyewe ulisomeka: Nashukuru kwa uamuzi wako. Usinitishe, mimi ni mwanamke niliyekamilika. Wewe ukiniona sifai, wapo wenzako wengi wanafukuzana kunitafuta ili waninase.

Huna jipya wewe. Kwanza nilikuvumilia tu kwa kipindi chote nilichokuwa na wewe. Sijawahi kufurahia chochote na sina cha kujivunia kutoka kwako.

Maisha mema.

Ndimi, msichana mrembo ninayejiamini,

Lilian.



Edo alirudia kusoma ile email zaidi ya mara tano, maneno yaliendelea kuwa yaleyale. Sasa aliamua kuchana na Lilian moja kwa moja. Hakuwa na wazo la kuwa naye tena katika maisha yake.

?Nimenawa mikono yangu sasa, siwezi kuwa na mwanamke wa aina hii. Atakuja kunisumbua tu huko mbeleni, lazima,? akajisemea kwa sauti Edo.

Alidhamiria kuhamishia akili yake yote kwenye masomo tu. Sasa aliamua kuachana kabisa na wazo kuwa ana msichana anayeitwa Lilian Tanzania.

***

Si Edo wala Lilian waliogundua kuwa kuna mchezo uliokuwa ukiendelea katika mawasiliano yao. Ilikuwa kazi ndogo sana kwa mtu ambaye alidhamiria jambo lake lifanikiwe.

Lucy ndiye aliyekuwa akijua mchezo ulivyokuwa. Edo hakuwa akiwasiliana na Lilian kwenye email. Aliyekuwa akiandika email zote alikuwa ni Lucy.

Kwa kushirikiana na mtaalamu wa kompyuta, Lucy alifanikiwa kuyateka mawasiliano ya email ya Lilian. Muda aliowaacha wakijisomea na wenzake, siku ambayo jioni yake walitoka na kwenda Maisha Club, ndiyo mchezo ulipofanyika.

Lucy alimwita mtaalamu ambaye alimmilikisha akaunti ya Lilian. Ujumbe wowote wa Lilian ulioingia uliingia kwa Lucy na alikuwa anaweza kumwandikia mtu yeyote kwa anwani ya Lilian.

Hilo halikujulikana!

Hii inamaana kuwa, ni Lucy ndiye aliyekuwa akimwandikia ujumbe wa hovyo Edo akiwa na lengo la kumkasirisha ili aachane na Lilian, sababu ikiwa ni kuwakutanisha kwa urahisi zaidi na pedeshee Pam.

Hiyo ilikuwa siri nzito.

Siri iliyojulikana na watu watatu tu; Lucy, Pam na mtaalamu aliyefanya kazi hiyo Rwegeshora. Hapakuwa na mtu wa nne.

***

Kazi ya kujikwatua ilikamilika ndani ya dakika ishirini. Akiwa amevalia gauni refu la rangi nyeusi na mtandio wa rangi ya buluu, Lilian alisimama mbele ya kioo kilichokuwa kwenye meza ya kujipambia.

Alimwangalia msichana aliyekuwa akionekana ndani ya kioo kile, kisha akatabasamu! Hakuwa na shaka kuwa, msichana yule alikuwa mrembo sawasawa.

Aligeuza shingo, akamwangalia. Akageuza upande mwingine tena, akaachama midomo yake. Akageuka upande, akachanganywa na hips za kuvutia kama bastola zilizochomoza pembeni mwa mapaja ya msichana yule.
 
SEHEMU YA 20 KATI YA 50

Sasa akageuka nyuma!

?Mh! Msichana mzuri sana. Mrembo mwenye sifa zote. Anavutia hakika,? akasema akitabasamu.

Lilian alikuwa akimsifia msichana aliyekuwa ndani ya kioo mbele yake. Alikuwa akiangalia taswira yake mwenyewe kwenye kioo. Hakuwa na shaka kuwa, eneo lote la Mlimani City, jioni hiyo kusingekuwa na mwanamke mzuri aliyependeza kama yeye!

Mara simu ikaita!

Ni Pam alikuwa anampigia!

Akapokea...

?Nimeshafika mama, upo tayari?? Pam akamwuliza.

?Bila shaka, dakika mbili tu nitakuwa hapo barabarani,? akasema Lilian kisha akakata simu.

Mara moja akatumbukiza miguu yake kwenye viatu virefu kiasi. Akachukua mkoba na kuubamiza mlango!

Akatembea kama Twiga!





Ni saa 10:00 alasiri, muda ambao kipindi kilikuwa kimemalizika. Kama walioambiana, Lucy na Latifa walitoka kwa pamoja darasani. Wakashuka ngazi taratibu wakianza kutembea kuelekea hosteli.

Tangu wanatoka darasani mpaka wanafika barabara kubwa ya lami, hakuna cha maana walichozungumza zaidi ya stori za hapa na pale.

Lakini baadaye, Latifa akaamua kuvunja ukimya. Akaanza kumzungumzia Lilian...

?Vipi mwenzangu, ulimuona Lilian alivyotoka darasani?? akauliza akionekana kuwa na shauku ya kusikia jibu kutoka upande wa pili.

?Nilimuona sana.?

?Unadhani ana nini??

?Anajua mwenyewe lakini kwa vyovyote vile, mapenzi ya Pam yatakuwa yameshaanza kumkolea. Unafanya mchezo na pesa??

?Lakini kweli...?

?Si unamuona Leila, si alijifanya mjanja na mwenye msimamo, yuko wapi sasa? Si aling?ang?ania kuondoka na Big jana. Kuna mjanja kwenye pesa?? akasema.

Wote wakacheka!

Ilikuwa dili!

Kwao ilikuwa furaha, maana fedha ilikuwa inaingia kama kawaida.

?Lakini Pam amenitumia ujumbe nikiwa darasani,? Lucy akasema.

?Amesemaje??

?Mambo mazuri, leo ana mtoko na Lilian. Watajuana wenyewe. Unajua ninachompendea Pam, hana papara na anajua anachokifanya.?

?Kweli kabisa.?

?We subiri, siku mbili hizi usikie kama utamsikia Lilian akizungumza habari za Edo tena. Kila kitu kitafunikwa na fedha za Pam, niamini mimi.?

?Kwa nini nisiamini wakati dalili zinaonekana wazi??

?Umeanza kuwa mjanja sasa, unaona maneno hayo??

?Wewe! Kwani tangu lini nikawa mshamba??

?Haya bwana, ratiba ya leo vipi??

?Kiukweli sitaki hata kujichosha sana. Tukapumzike, usiku twende tu hapo Udasa tukale mbuzi choma na ndizi, kisha tushushie na wine, nadhani itakuwa poa!?

?Sawa.?

Wazo likapita!

Fedha kwa wasichana hao ilikuwa jambo dogo sana. Walikuwa na uhakika wa kufanya chochote bila kutegemea fedha zinazoingizwa kwenye akaunti zao na serikali kwa ajili ya matumuzi ya kawaida.

Walitumia usichana wao kujipatia fedha na kufanya kila aina ya anasa za mjini. Ni jambo moja tu walijua, pamoja na yote hayo, vichwani mwao walikuwa na madini ya ajabu.

Walikuwa wakifanya vizuri sana kiasi kwamba, wengine waliamini walikuwa wakitoa rushwa ya ngono kwa wahadhiri ili wawafaulishe. Haikuwa hivyo.

Ukweli ni kwamba, walijua vizuri kujisomea na kujadiliana katika kundi lao. Cha kushangaza ni kwamba,
 
Simulizi Zinazorushwa na BURE SERIES Msimu wa kwanza

1. Simulizi: Kurudi Kwa Moza

Bonyeza hapa chini kusoma
Simulizi: Kurudi Kwa Moza

2. Riwaya: Kasri ya Mwinyi Fuad
Bonyeza hapa chini kusoma
Riwaya: Kasri ya Mwinyi Fuad

3.Simulizi: Nini maana ya mapenzi
Bonyeza hapa chini kusoma
Simulizi: Nini maana ya mapenzi

4. Simulizi : Nguvu Ya Mapenzi
Bonyeza hapa chini kusoma
Simulizi : Nguvu Ya Mapenzi

5. Mkuki Kwa Nguruwe (Kisa Cha Kweli)
Bonyeza hapa chini kusoma
Mkuki Kwa Nguruwe (Kisa Cha Kweli)

6. RIWAYA: Sauti Yake Masikioni Mwangu
Bonyeza hapa chini kusoma
RIWAYA: Sauti Yake Masikioni Mwangu

7. NDOA ILIVYOTETERESHA IMANI YANGU (Kisa Cha Kweli)
Bonyeza hapa chini kusoma
NDOA ILIVYOTETERESHA IMANI YANGU (Kisa Cha Kweli)

8. RIWAYA: Mume Gaidi
Bonyeza hapa chini kusoma
RIWAYA: Mume Gaidi

9. STORY: Sitaki Tena

Bonyeza hapa chini kusoma
STORY: Sitaki Tena

10. Nilivunja Ndoa Zangu 3 Kulipiza Kisasi (Kisa Cha Kweli)

Bonyeza hapa chini kusoma
Nilivunja Ndoa Zangu 3 Kulipiza Kisasi (Kisa Cha Kweli)
 
SEHEMU YA 21 KATI YA 50

hawakutaka mtu yoyote aungane nao kwenye kundi zaidi ya wao wanne tu; Leila, Lucy, Latifa na Lilian.

Ndivyo msimamo wao ulivyokuwa!

***

Hakutaka lakini alijishangaa akitaka kuingia kwenye anwani pepe yake. Hiyo ni baada ya kuamua kujisomea kwa nguvu na kuachana kabisa na mawazo ya Lilian.

Edo alishaamua kuachana na mambo ya mapenzi. Kichwani mwake aliamini kuwa, Lilian hakuwa mwanamke sahihi kwake, hivyo alijipa muda kutafakari na pengine kutafuta mwingine ambaye angekuwa na penzi la dhati.

Lakini sasa uamuzi huo aliupinga ghafla. Kuna kitu alihisi kikizunguka kichwani mwake. Alitakiwa kujiridhisha tena kupitia maandiko yale kwenye email yake.

?Lilian anaweza kunitusi mimi? Anaweza kunikejeli? Napata shaka na jambo hili. Kuna kitu kipo nyuma kinafanyika. Kipo, naamini kipo,? akawaza.

Muda huo huo akafungua email yake, kisha akaenda kwenye ujumbe wa mwisho kutoka kwa Lilian. Kwa uchungu moyoni, akarudia tena kuusoma. Sasa aliamua kusoma kwa sauti kabisa.

Hakuna kilichobadilika. Maneno yalikuwa ni yaleyale. Alihisi kupasuka kichwa kwa mawazo. Akapata wazo lingine la haraka. Alitakiwa kuzungumza na Lilian muda uleule ili amwulize vizuri kuhusu email alizokuwa akimtumia.

Ni Lilian pekee ndiye angemaliza utata uliokuwa umemzunguka kichwani mwake. Akachukua simu yake mezani kisha akampigia. Simu ikaita kwa muda mrefu sana, lakini haikupokelewa!

Akarudia kupiga kwa mara nyingine, bado haikupokelewa!

?Shiiiiit!? akasema kwa sauti na kuishusha simu hiyo kwa hasira.

Hakuweza tena kuendelea kusoma, alibadilisha nguo, akavaa suti za michezo, akatoka na kwenda uwanjani kwa ajili ya mazoezi ya viungo.

***

Alifungua mlango na kuingia ndani ya gari. Alikutana na tabasamu pana lililodhihirisha fedha kutoka kwa Pam. Lilian akakaa, huku akijishangaa namna woga ulivyoanza kumuondoka kwa kasi.

?Karibu mrembo!? Pam akasema.

?Ahsante. Pole na kazi.?

?Nashukuru, nawe pole kwa masomo.?
 
SEHEMU YA 22 KATI YA 50

?Ahsante sana. Siku yangu haijawa nzuri sana leo, kichwa kimekuwa kizito sana.?

?Usijali, amini kwamba utaimaliza siku vizuri sana.?

?Nashukuru Pam.?

Gari likaungurumishwa!

Walikuwa wanaelekea Mlimani City. Hapakuwa mbali, dakika tatu tu Pam alikuwa anaegesha gari kwenye maegesho eneo hilo. Akashuka, kisha akazunguka upande wa pili haraka na kumfungulia mlango Lilian.

Akashuka!

Wakaongozana hadi Samaki Samaki. Wakapata chakula cha jioni kisha vinywaji vikafuata. Kwa mara ya pili Lilian alikunywa mvinyo. Kidogo alianza kuuzoeazoea!

Hawakukaa sana, saa nne usiku, Pam alimrudisha Lilian chuoni. Akiwa ameegesha gari nje ya jengo la hosteli anayoishi, Pam alitoa bahasha na kuchomoa maburungutu matatu ya fedha na kumkabidhi.

Zilikuwa milioni tatu!

Lilian akasita kupokea.

?Chukua tu!?

?Hapana Pam. Kwa nini unanifanyia yote haya? Hebu niambie ukweli, unataka nini kwangu?? Lilian akamwuliza.

?Unataka kujua ukweli?? Pam akamwuliza akiwa amemkazia macho.

?Ndiyo niambie ukweli Pam, kuwa wazi...? akasema Lilian akionekana kukolea kwa kilevi kidogo.





Pam alidhamiria kuwa mkweli. Hakutaka kuendelea kubaki na mzigo moyoni mwake. Ukweli ndiyo jambo pekee ambalo lingeweza kuwa msaada kwake.



Alimwangalia Lilian kwa macho yaliyojaa ubembe wa mahaba. Ndani ya moyo wake alimpenda sana. Ni kweli alikuwa na mke. Hilo asingeweza kulikataa, lakini pamoja na hilo, alikuwa amenasa katika himaya ya Lilian.



Alihisi moyo wake umezimia. Aliendelea kumwangalia Lilian kwa macho tulivu, huku naye akionekana dhahiri kuwa na hisia ya jambo fulani kutoka kwa Pam.



“Hawezi kunipa fedha zote zile bila sababu, hawezi kunifanyia mambo yote yale hivihivi tu, lazima kuna kitu. Natakiwa nijue ili baadaye isiwe tabu!” akawaza Lilian.



Bado Pam hakuwa tayari kufunua kinywa chake kusema chochote. Alimwangalia tu Lilian ambaye naye alikuwa akimtazama!
 
SEHEMU YA 23 KATI YA 50

Walikuwa wakitazamana! Kila mmoja na lake kichwani! “Pam...” Lilian hatimaye akaita. “Nakusikia.” “Nahitaji kusikia kitu kutoka kwako.”



“Chukua kwanza huu mzigo wako.”



“Kumbuka huu mzigo ndiyo sababu ya mimi kutaka kujua lengo lako kwangu!” akasema Lilian.



“Kwani wewe una lengo gani na Pam?” “Sijakuelewa.” “Nauliza, kwa upande wako una nia gani na mimi?” Pam akauliza kwa kujiamini sana. Lilian akatulia! Lilikuwa swali mahususi! Tena lililotaka majibu ya moja kwa moja. Kwani wewe una lengo gani na Pam? Swali hilo likajirudia tena kichwani mwake akiendelea kumwangalia mwanaume huyo, kipande cha mwanaume!



Walikutana wote wenye misemo na maneno mengi. Kila mmoja alikuwa akipima uwezo wa mwenzake wa kujieleza na kutoa majibu yenye maana. “Pam,” Lilian akaita. “Ndiyo.” “Nataka kujua kwako kwanza.” “Ok! Ni rahisi sana. Unatakiwa kujua kuwa nakuhitaji uwe rafiki yangu – nashuhukuru kuwa tayari jambo hilo limeshafanyika. Sisi ni marafiki. Sina la zaidi,” akasema Pam akionyesha kujiamini kupita kiasi. “Hivyo tu?” “Unafikiri kuna mengine?” “Kweli Pam, hilo linatosha kuwa sababu ya wewe kunipatia fedha kila wakati tena nyingi?”



“Sina hakika kama kuna lingine, lakini kama lipo, wakati utazungumza. Wazungu wanasema; time will tell – let us wait. Tujipe muda zaidi Lilian, tunahitaji muda zaidi...” sauti ya Pam ilikuwa tulivu iliyoonekana dhahiri kuhitaji huruma.



“Mh! Haya...” akasema Lilian, akinyoosha mkono wake wa kuume, akapokea zile fedha.



Pam haraka sana akajiosogeza karibu yake, alijifanya kama anataka kumnong’oneza kitu sikioni... Akambusu! Lilian akasisimka! Akamwangalia Pam usoni. Pam naye akamwangalia. Sasa wakawa wanaangaliana. Bila shaka yoyote, waliweza kuzungumza vyema bila kutoa sauti. Macho yao yalitosha kabisa kupeana mawasiliano ya kueleweka.
 
SEHEMU YA 24 KATI YA 50



Ni Lilian ndiye aliyeanza. Alijisogeza jirani na Pam, kisha akajitupa kifuani mwake. Midomo yao ikakutana... mara wakaanza kufyonzana!



Dakika tano za moto wa mahaba zilipita, wote wakiwa hoi kabisa. Pam alikuwa kwenye wakati mgumu sana. Ndoto zake zilitimia kirahisi sana.



Akamsogeza Lilian pembeni. Akamtulizia macho usoni mwake. Midomo yake ikaanza kutingishika akionekana kuwa na jambo zito alilotaka kuzungumza.



“Tunaweza kuondoka?” Pam akamwuliza. “Kwenda wapi?” “Hotelini.” “Kufanya nini?” “Lilian tafadhali naomba unielewe mama.”



“No! Siyo rahisi kiivyo,” akasema Lilian kwa kujiamini. “Unasema?” “Siyo rahisi kama hivi Pam, kama ni pesa zako chukua.”



“Usifanye hivyo, ok! Nafikiri sasa umeshaelewa na hata wewe umeshindwa kushindana na hisia zako. Nafurahi maana tayari tumeshafungua ukurasa mpya wa maisha yetu. Nimefurahi sana.



“Hata kama ukiondoka hapa, utaniacha nikiwa na amani sana moyoni mwangu. Nakuhakikishia nimefurahi sana. Makovu yote moyoni mwangu sasa yamekauka. Ahsante sana mpenzi,” akasema Pam. “Pam unanipenda?” “Kuliko neno lenyewe. Nakupenda sana Lilian.” “Unaniahidi nini?” “Nakuahidi furaha siku zote, hilo litakuwa jukumu langu.”



“Ahsante sana mpenzi. Naomba uniruhusu niende.” “Bila shaka mpenzi wangu.” Lilian akatoka. Akabamiza mlango. Akavuka barabara, Pam akiwa bado ameegesha gari lake. Akamsindikiza kwa macho mpaka alipopotea katika upeo wa macho yake.



Akaondoa gari!



ILIKUWA ni usiku wa saa sita, Lucy na Latifa wakiwa wamelala katika kitanda chao cha juu, Leila alikuwa amelala chini, wakati Lilian akiwa amekaa kwenye meza ya kusomea akiendelea kusoma.



Akiwa amezama kwenye somo alilokuwa akipitia, simu yake ya mkononi ikaita. Alipoangalia kwa makini namba, akagundua zilikuwa za nje ya nchi.



Alipotulia kwa muda zaidi akazitambua. Ni namba za Edo. Aliangalia kwa muda, akifikiria kitu, akageuza shingo kuwaangalia wenzake, wote walikuwa wamepitiwa na usingizi. Akapokea! “Halooo,” akatamka Lilian baada ya kupokea.
 
SEHEMU YA 25 KATI YA 50



“Habari yako Lilian?” akauliza Edo katika upande wa pili wa simu.



Edo alizungumza kwa sauti ndogo, iliyoonyesha haina ukali tena, bali yenye kusihi. “Salama, leo umenikumbuka?” “Ndiyo. Nataka kujua jambo moja Lilian.” “Nini?”



?Ni wewe kweli ndiye unayenitumia meseji mbaya kwenye email yangu?? Edo akauliza kwa utulivu.



Lilian akashtuka!

?Meseji mbaya??

?Ndiyo meseji mbaya. Hebu nijibu na uwe mkweli, ni wewe??

Lilian akazidi kuchanganyikiwa!

Hakukumbuka kumwandikia ujumbe wowote mbaya zaidi ya kumtumia mara moja tu, akitaka kujua kuhusu ukimya wake!

Hiyo ilikuwa ni ukimya baada ya kuingia nchini Malaysia mara walipoachana Uwanja wa Ndege jijini Dar es Salaam.

Taa nyekundu iliwaka kichwani mwake.

Ulikuwa mchezo!

Hata hivyo, hakuna aliyeujua. Si yeye wala Edo.





LILIAN alitulia kwa muda akiiacha simu hewani bila kuzungumza kitu. Alitakiwa kutulia kwa muda ili aweze kutafakari japo kwa muda mfupi kuhusu mambo yaliyokuwa yakitokea wakati huo.

Yalikuwa mambo mageni kabisa. Edo hakuwa yule aliyemzoea. Japokuwa moyoni alikiri wazi kuwa alishachafua penzi lao kwa kumwingiza Pam lakini kwa kiasi kikubwa, Edo alichangia.

Swali la Edo likaendelea kugonga kichwani mwake. Kwa nini anamwambia asimfiche. Ni wazi kuwa isingekuwa rahisi kwa Edo kugundua kuwa alikuwa na mpenzi mwingine na tayari mapenzi yalishaanza kuchanua.

Ilikuwa vigumu sana!

Angejuaje?

Malaysia na Tanzania wapi na wapi? Kuala Lumpur na Dar es Salam, wapi na wapi? Ni nchi mbili tofauti. Majiji mawili tofauti, tena yaliyotenganishwa na nchi nyingi katikati.

?Hawezi kujua kuhusu Pam,? akajipa moyo.

?Ndiyo....hawezi jua. Atajuaje sasa? Nani wa kumwambia? Siamini kama anaelewa kuhusiana na Pam. Lakini bado nachanganywa na jambo moja. Kwa nini anasema nimemtumia email yenye maneno machafu?

?Ni lini mimi nimemtumia email? Kuna kitu kinaendelea hapa. Lazima kuna mchezo mchafu unafanyika.
 
SEHEMU YA 26 KATI YA 50

Napaswa kuwa makini sana, lakini ngoja kwanza nimsikilize. Nitaujua ukweli tu,? akazidi kuwaza Lilian.

Ni kweli Lilian alikuwa katika mawazo sahihi kabisa. Kila kitu ni kama kilikuwa kimejificha ndani. Hakuwa na uwezo wa kuona lakini alijiahidi kuupata ukweli.

?Lilian...? Edo akaita baada ya kimya cha muda mrefu.

?Nakusikia Edo.?

?Hutaki kuniambia ukweli??

?Unataka ukweli gani mwingine? Mimi nimekuambia nimekuandikia email mara moja tu. Tena nilikuuliza kama umefika salama na kwa nini hukunijulisha. Hivyo tu, hakuna email nyingine niliyokutumia mpenzi.?

?Una hakika??

?Ndiyo.?

?Naanza kupata picha sasa.?

?Picha gani??

?Hapo ulipo si unayo laptop??

?Ndiyo.?

?Sawa...naomba uingie kwenye akaunti yako mara moja, halafu unijulishe.?

?Mh! Haya bwana. Kwani kuna nini??

?Fanya hivyo.?

?Sawa.?

Wakakata simu.

Mara moja Lilian akaivuta laptop yake, akaingia kwenye mtandao wa google.com kisha akaenda moja kwa moja kwenye anwani pepe ya gmail. Akaandika jina la akaunti yake ambayo ilisomeka; lilygirldsm, kisha akaenda mahali pa kuandika neno siri, akaandika.

Haikuwa ngumu, ilikuwa ni muunganiko wa majina yake na Edo. Aliandika lilianed, kisha akaingia. Alitumia muda kidogo kuperuzi, akaangalia email zilizoingia na kutoka.

Akagundua ni ileile ya mwisho aliyomtumia Edo. Hapakuwa na nyingine. Lilikuwa jambo lililomshangaza sana. Muda huo huo akampigia Edo.

Edo hakupokea, alimkatia na baadaye akampigia yeye...

?Tayari?? Edo akamwuliza haraka baada ya Lilian kupokea simu.

?Ndiyo mpenzi.?

?Sasa fanya hivi, nenda kwenye sehemu ya kuandika ujumbe, andika neno lolote hata kama ni fupi tu, kisha nitumie. Ukishafanya hivyo naomba unijulishe kwa simu,? akasema Edo.

?Sawa baba.?

Lilian akafanya hivyo. Kwake yalikuwa majaribio ya kushangaza sana. Hakuelewa ni kwa nini alikuwa akimwambia afanye hivyo. Hata hivyo hakuwa na la kufanya zaidi ya kutekeleza maagizo yale.

Akaenda kwenye sehemu ya kuandika ujumbe, akamwandia maneno manne tu kwa herufi kubwa; I LOVE U EDO! Mara moja akamtumia. Alipokamilisha zoezi hilo, akamtumia sms kupitia simu yake, kumjulisha kuwa tayari alishamtumia.
 
SEHEMU YA 27 KATI YA 50

Ilipita dakika moja bila Edo kujibu kitu, kisha simu yake ikaita. Alipotupa macho yake kwenye kioo cha simu yake, akakutana na namba za Edo. Mara moja akapokea.

?Una hakika umenitumia??

?Ndiyo mpenzi.?

?Kwenye email yangu ileile??

?Ndiyo baby.?

?Unaweza kunitajia??

?Kabisa, ni eddyhb@yahoo.co.uk.?

?Sasa nimeanza kupata picha.?

?Ni nini mpenzi??

?Hakuna email iliyofika huku.?

?Kivipi sasa wakati nimekutumia??

?Ndiyo maana nimekuambia nimeshaanza kupata picha. Kifupi kuna mtu ameyateka mawasiliano yako. Bila shaka ni mtu wako wa karibu na anayekujua sana. Lengo lake kubwa ni kuharibu uhusiano wetu.

?Sasa nimeshajua cha kufanya. Najua unao marafiki zako wa karibu. Kuna mmoja wao anajaribu kufanya huu ujinga. Sasa mimi sijali wala wewe usijali na usijaribu kumshirikisha mtu yeyote kuhusu hili jambo.

?Unachotakiwa kufanya kwa sasa ni kufungua akaunti nyingine ya email. Hiyo ya zamani achana nayo na usiitumie tena. Lakini usiwaambie rafiki zako kuwa umeamua kubadilisha akaunti,? akasema Edo.

?Lakini baby...? akasema Lilian lakini kabla hajamalizia, Edo alikuwa ameshadakia.

?Hakuna cha lakini hapo, fuata maelekezo yangu.?

?Sawa baba, nimekuelewa.?

Wakakata simu.

Lilian alizima kila kitu pale mezani. Alizima mpaka simu, kisha akajitupa kitandani kulala. Kichwa kilikuwa kizito kuliko kawaida. Mawazo mengi yalimtawala.

Bado alikuwa hajaelewa, ni nani aliyeteka mawasiliano yake na kwa nini aliamua kumgombanisha na mwanaume wa maisha yake. Jambo hilo lilisababisha usiku huo uwe mgumu, mzito na mrefu kuliko kawaida!

Alikesha akiwaza!

Usingizi angeupata wapi?

?Hakuna marefu yasiyo na ncha,? akajisemea.

Angalau maneno hayo yalimtia faraja, kidogo akajihisi mwepesi na macho yake sasa yakaanza kumlemea kwa uzito. Bila uamuzi wake, aliyafumba,mara usingizi mzito ukamchukua!







ALIAMKA mapema sana. Saa 11 alfajiri Lilian alikuwa macho. Ilikuwa vigumu sana kuufaidi usingizi wa
 
SEHEMU YA 28 KATI YA 50

asubuhi. Hakuwa na kipindi cha asubuhi, zaidi alitakiwa kuingia darasani saa nane mchana, hivyo alikuwa na uhuru wa kuendelea kulala.

Kichwa chake kiliendelea kuwaza juu ya mtu aliyeteka mawasiliano yake. Ni nani mtu huyo na kwa nini afanye hivyo? Alijiuliza bila kupata majibu yakinifu.

Aliamini kwa vyovyote vile, aliyehusika kumfanyia kitendo kile alikuwa kati ya rafiki zake anaolala nao bweni moja. Ndivyo ukweli wenyewe ulivyokuwa.

Aliwafikiria rafiki zake wote na tabia zao, hakujua ni nani angekuwa amefanya tukio hilo. Mawazo yake yalimpeleka kwa Lucy lakini baadaye akayaondoa.

Pamoja na yote alikuwa na amani kidogo moyoni mwake kuona kuwa, sasa mpenzi wake alielewa kuwa hakuwa amemfanyia kitu chochote kibaya.

Changamoto ilikuwa moja tu; uhusiano mpya aliouanzisha na Pam. Jambo hilo pekee ndilo lililousumbua ubongo wake.

***

Pam alipanda ngazi kama anakimbizwa! Zilikuwa ngazi fupi katika Hoteli ya Tarahan iliyokuwa Mikocheni katika eneo lililotulia mno.

Alifika moja kwa moja Mapokezi ambapo alipokelewa na tabasamu mwanana la msichana mrembo sana.

“Mambo vipi?” Pam akamsalimia.

“Poa, shikamoo.”

“Acha hizo mtoto mzuri, shikamoo siyo muhimu sana...sema mambo poa.”

Yule msichana akacheka, kisha akamjibu: “Haya poa.”

“Hayo ndiyo mambo!” akasema Pam.

“Mh! We’ baba una mambo! Niambie...naomba nikusikilize.”

“Nahitaji makazi ya muda hapa kwako. Nataka chumba kizuri, chenye hadhi ya juu kuliko vyote. Kifupi nataka chumba cha gharama kuliko vyote!

“Nina mgeni muhimu ambaye ana tukio lake leo, nataka lifanyike ndani ya chumba. Naamini inawewezekana maana wewe unajua vyumba vyote ndani ya hoteli hii,” akasema Pam akitabasamu.

Tabasamu lake lilisababisha hata yule msichana naye ashindwe kujizuia na kuachanua midomo yake akitabasamu.

“Umepata.”

“Bei gani?”

“Laki mbili ndiyo kizuri zaidi, kinachofanana na wewe kwa kila kitu.”

“Sawa. Unaweza kunipeleka?”

“Bila shaka.”
 
SEHEMU YA 29 KATI YA 50

Yule msichana, akamwita mhudumu ambaye alipanda na Pam hadi ghorofa ya nne kilipokuwa chumba alichohitaji. Aliingia ndani na kukikagua.

Kilikuwa kizuri sana, chenye hadhi na ubora zaidi ya ule ambao alikuwa akiufikiria. Pam alimwangalia yule msichana aliyeongozana naye, akatabasamu...

“Panafaa kabisa,” akasema wakitoka nje ya chumba kile na kukifunga.

Aliposhuka chini alilipa kisha akamwambia: “Nasisitiza, kuna tukio muhimu sana. Kama kuna uwezekano, mnaweza kuongeza manjonjo zaidi kwenye kile chumba.”

“Hakuna shida kaka, nadhani ukirudi utafurahi zaidi. Tutajitahidi kuongeza nakshi.”

“Nitafurahi sana.”

“Unatarajia kuja saa ngapi kwa ajili ya hiyo shughuli?”

Pam akacheka kidogo, kisha akajibu: “Jioni. Sina hakika sana na muda lakini itakuwa zaidi ya saa moja usiku.”

“Karibu sana.”

“Nashukuru.”

Pam akaondoka zake.

***

Ilikuwa saa nane kasoro mchana. Lilian, Leila, Latifa na Lucy walikuwa wakitembea taratibu kuelekea kwenye kipindi. Wakiwa njiani, Lilian akaanzisha mjadala. Hakuona sababu ya kuendelea kuishi na mawazo kichwani wakati kulikuwa na uwezekano wa kudodosa ili kupata ukweli.

“Hivi ni nini kinaendelea kati yetu?” alianza kuuliza Lilian.

Wote walipigwa na butwaa.

“Unamaanisha nini?” Lucy alikuwa wa kwanza kuuliza.

“Hujui ninachomaanisha? Huu ni urafiki gani sasa jamani? Kwa nini tunatibuliana mambo?” akasema tena Lilian.

Ilikuwa vigumu sana yeyote kati yao kuelewa alichokuwa akimaanisha. Wote walionekana kama wanasikia habari mpya kabisa kutoka kwa Lilian.

“Kwani kuna nini? Si useme ukweli? Hebu kuwa wazi tuelewe unachomaanisha,” akasema Leila.

“Anayejua alichofanya anajijua na anatakiwa kufahamu tu kuwa nimeshagundua mchezo wake ila mambo hayaendi hivyo kwa sisi marafiki, hayo ni mambo ya kinafiki!” akasema Lilian akionekana kukasirika sana.

Muda huohuo simu yake ikaita, alipotazama kwenye kioo, akakutana na jina la Pam. Akasimama na kuwaacha wenzake waendelee mbele kidogo ili apate kumsikiliza.
 
SEHEMU YA 30 KATI YA 50

Walipofika mbali kidogo, akabonyeza kitufe cha kupokea, kisha akaanza kuzungumza: “Haloo.”

“Niambie mrembo wangu.”

“Poa.”

“Nahitaji kutoka na wewe leo jioni, ni muhimu sana mpenzi wangu.”

“Utanifuata?” akauliza Lilian kwa haraka.

“Haina shida, saa moja kamili usiku nitakuwa hapo chuoni au kama vipi uchukue taksi nikueleze pa kunikuta?”

“Hapana bwana...wewe njoo unichukue tu!”

“Hilo limepita.”

“Poa Pam, ngoja mimi niingie kwenye kipindi.”

“Masomo mema mama.”

“Ahsante.”

***

Pam alifungua mlango wa gari, Lilian naye akafanya hivyo. Wakashuka na kuibamiza kwa nguvu. Wakatembea wakiwa wameshikana mikono hadi Mapokezi ambapo Pam alichukua funguo.

Waliamua kutumia ngazi kupanda hadi ghorofa ya nne kilipokuwa chumba alichochukua Pam. Pam akafungua mlango. Lilian alishangazwa sana na namna chumba kile kilivyokuwa kimepambwa vizuri na kuvutia.

Zaidi alishangaa kuona kadi zikiwa zimezagaa kitandani. Pam akasimama nyuma yake kisha akamshika kiuno, akasema: “Happy Birthday Lilian, Happy Birthday to you!”

Lilian akashtuka sana!

“Siamini Pam mpenzi wangu, leo ni birthday yangu?”

“Ndiyo mpenzi wangu. Hongera sana!” akasema tena Pam.

“Ahsante kwa kunijali. Yaani nilikuwa nimeshasahau kabisa,” akasema Lilian huku akimwaga machozi.

Yalikuwa machozi ya furaha.





MARA zote huwa hakumbuki siku yake ya kuzaliwa. Aliyekuwa akimkumbusha kuhusu siku yake ya kuzaliwa alikuwa ni mpenzi wake Edo na wakati mwingine rafiki zake akina L (Latifa, Lucy na Leila) ambao humnunulia kadi na kumwimbia nyimbo za Birthday.

Siku hiyo Edo hakumkumbuka, wala hakumwambia kuwa ni siku yake ya kuzaliwa. Kitendo cha Pam kuonyesha kuikariri haraka ingawa penzi lao lilikuwa bado changa kulimchanganya sana Lilian na kuzidisha mapenzi kwa mwanaume huyo.

Lilian alimwangalia sana Pam kisha akamsogelea na kumbusu tena. Mashavu yake yalikuwa yamejaa machozi. Hakuamini macho yake.

?Inanipasa nifanye hivi kwako, maana nakupenda kwa moyo wangu wote. Kwa nini unashangaa baby, mimi ndiye mwanaume wako,? akasema Pam.
?Unaniahidi Pam??

?Ndiyo.?

?Nimefurahi sana kusikia hivyo.?

Kilikuwa chumba nadhifu sana, kisafi chenye nakshi za kila aina ndani. Macho yao kwa pamoja yalifurahishwa na kila kilichokuwa ndani ya chumba kile.

Ingawa walikuwa wawili tu, Pam alikuwa ametayarisha shampeni. Alichukua chupa kisha akaifungua kwa ustadi, iliporuka ilikwenda kumlowanisha Lilian alipokuwa amesimama.
 
SEHEMU YA 31 KATI YA 50



Wakamimiana kisha wakaanza kunywa kwa furaha. Baada ya kunywa glasi moja moja, kwa kuwa haikuwa yenye kilevi, Pam alifungua mvinyo mwekundu ambao ulikuwa na kilevi kisha akajaza glasi mbili.

Akampatia Lilian moja na moja akaishika yeye. Wote kwa pamoja wakagonganisha glasi zao na kuanza kunywa kwa furaha. Walikunywa taratibu, hadi walipoanza kuchangamka!

?Baby sasa inabidi tupate chakula, utapenda kula nini?? Pam akamwuliza Lilian.

?Utakachokula wewe, nami nitakula hichohicho.?

?Sawa, natamani sana tule samaki, wewe unaonaje??

?Samaki ni sawa, samaki gani lakini??

?Unapenda wa ziwani au baharini??

?Ziwani ni wa watamu zaidi, itakuwa vyema kama watakuwa sato na chipsi...? akasema Lilian akitabasamu.

?Sawa mpenzi, ni chaguo langu pia.?

Pam akasogea kwenye meza ndogo iliyokuwa na simu, akanyanyua mkonga wa simu kisha akabonyeza namba za mapokezi na kuunganishwa na jikoni, akatoa oda yake.

Waliendelea kuzungumza mengi mle chumbani, Lilian akijihisi kuzidi kumpenda Pam kuliko awali.

?Najisikia kukupenda sana Pam,? akasema Lilian.

?Unamaanisha kuwa mwanzoni hukuwa ukinipenda??

?Siwezi kusema hivyo ila ukweli ni kwamba, kwa sasa nahisi kukupenda zaidi ya mwanzo. Nakupenda sana.?

?Ahsante sana Lilian, mimi nilikupenda kwa dhati tangu mwanzo.?

?Sasa nakukaribisha rasmi kwenye moyo wangu, uwe mwanaume wangu wa kweli,? akasema tena Lilian.

?Nimefurahi kusikia hivyo, nakuhakikishia nitakuwa mwanaume mwema kwako. Nitahakikisha unakuwa mwenye furaha siku zote. Narudia kukuambia tena, nilikupenda tangu mwanzo, tangu naonana na wewe mara ya kwanza nilikupenda na ninauamini moyo wangu,? akasema Pam akiachia tabasamu.

?Ahsante my love,? akasema Lilian.

Mlango uligongwa, Pam akasimama na kwenda kufungua. Alikuwa ni mhudumu amefika na vyakula walivyoagiza. Pam akapokea na kuingia navyo ndani.

Waliketi mezani kisha wakaanza kula kwa furaha. Kama walivyotarajia ndivyo ilivyokuwa, chakula kilikuwa kitamu sana na wote walikifurahia sana.

Baada ya chakula wakaendelea na vinywaji. Lilian hakujua kitakachotokea baadaye, kilevi kilivyomkolea alijikuta akijiachia kihasarahasara, michezo ya kimapenzi ya hapa na pale ikaanza.

Hapo ukawa mwanzo wa kuelekea kwenye dimbwi la mahaba. Kwa ushawishi wa Pam, Lilian akajikuta akiharibiwa usichana wake. Kwa mara ya kwanza alikutana na mwanaume.

Alipata maumivu makali sana. Lilian alivunja ahadi aliyokuwa amewekeana na mpenzi wake Edo. Maumivu makali aliyopata, ukichanganya na ulevi aliokuwa nao, alijihisi mchovu sana.

Pam na Lilian walilala hadi asubuhi hotelini hapo.

***

Lilian aliamka asubuhi na mapema. Alipojigeuza na kufumbua macho, akamuona Pam amelala pembeni yake, hapo akagundua kuwa kweli alilala na Pam.

Akili za pombe zilimtoka, sasa akagundua thamani ya usichana wake. Alimkumbuka Edo na ahadi walizowekeana. Alimtingisha Pam aliyekuwa bado amelala pembeni yake.

Akashtuka!

?Vipi mpenzi wangu?? Pam akauliza mara baada ya kushtuka usingizi.

?Pam, kwa nini umenifanyia hivi?? akauliza Lilian kwa hasira.

?Tuliza hasira basi, kwani kuna nini kibaya mpenzi wangu??

?Huoni kama ni vibaya siyo? Huoni ubaya? Ona sasa umeharibu usichana wangu!? akasema Lilian.

?Wasiwasi wako ni nini wakati wewe ni mpenzi wangu? Nipo kwa ajili yako mpenzi. Mimi ni wako na wala si kwamba nimekuwa na wewe kwa siku moja tu, umeshakuwa wangu na utandelea kuwa wangu milele.?

?Hayo ni maneno ya wanaume, siku zote wamekuwa na maneno ya kudanganya tu baada ya kupata wanachotaka, wanaondoka!?

?Mimi nikuache wewe? Nani kasema? Sibahatishi, naujua moyo wangu. Najiamini kuwa nakupenda kwa dhati,? akasema Pam.

?Kweli??
 
SEHEMU YA 32 KATI YA 50

?Nakuhakikishia,? akasema Pam.

Lilian akajivuta kwa Pam, akalala kifuani mwake. Penzi jipya lilifumuka kwa wawili hao.

Waliamka kwa pamoja na kuelekea bafuni kuoga kisha wakavaa na kuondoka. Pam alimrudisha Lilian mpaka chuoni.

Lilian alikuwa na jambo moja tu kichwani mwake; angemwambia nini Edo kuhusu usichana wake? Hakuwa na jibu!

Huo ndiyo mtihani mgumu uliokuwa mbele yake.





ULIKUWA zaidi ya mtihani. Siku zote alimwambia alikuwa na usichana wake, jambalo lilikuwa la kweli tupu. Ahadi yao ilikuwa ni kukutana faragha mara baada ya kufunga ndoa.

Ni msimamo ambao yeye ndiye aliyeushikilia zaidi. Kilichomuuma ni kuja kuutoa usichana wake kirahisi kiasi kile. Alijua wazi kuwa, hakuwa na mapenzi hata kidogo na Pam, ni fedha ndizo zilizomchanganya.

Moyoni alikuwa na majuto makubwa, tamaa ya fedha ndiyo mwanzo wa matatizo yote hayo. Hata hivyo moyoni alikiri kuwa, hakuwa na njia nyingine zaidi ya hiyo.

Isingekuwa rahisi awe na Pam, ampe fedha zake bila chochote kuendelea. Hilo lingekuwa jambo la ajabu sana.

?Sina namna, tayari nimeshaingia kwenye mambo ya kikubwa, siamini kama imekuwa rahisi kiasi hiki,? alijisemea wakati akitembea taratibu kuelekea hosteli.

Akiwa anatembea, simu yake ikaita, alipotupa macho yake kwenye kioo cha simu, akakutana na namba za mpenzi wake, Edo. Mara moja akapokea.

?Haloo!?

?Haloo mpenzi wangu, habari za huko??

?Salama. Wewe je??

?Mimi ni mzima, nashukuru naendelea vyema na masomo. Nimekupigia simu hii kwa ajili ya mambo mawili muhimu.?

?Mambo gani??

?Kwanza kukuomba msamaha.?

?Msamaha??

?Ndiyo mpenzi, kukuomba wewe msamaha.?

?Kwa kosa gani tena mpenzi?? akauliza Lilian akionekana kuwa na mashaka kidogo.

Alijaribu kuwaza kuhusu msamaha aliosema, akashindwa kuelewa kabisa. Kwa namna ilivyokuwa, yeye ndiye aliyetakiwa kuomba msamaha kutokana na kuvunja ahadi yao.

Kichwa kikamuuma, akawaza kuwa huenda Edo alikuwa akizungumza mambo kinyume. Kwamba huenda alikuwa akimaanisha yeye.

?Hata kama alikuwa akimaanisha mimi, itawezekanaje basi hata ajue? Yeye yupo Malaysia, mimi Tanzania, wapi na wapi? Hili ni jambo gumu kutokea bwana,? akazidi kuwaza.

?Lilian,? Edo akaita.

?Nakusikia Edo.?

?Nisamehe mpenzi.?

?Baby niambie bwana.?

?Jana ilikuwa siku yako ya kuzaliwa!?

?Najua Edo.?

?Kosa langu ni kutokupongeza mapema tangu jana, lakini nina sababu za msingi ingawa sipendi kukueleza, ila naomba ufahamu kuwa ninajua umuhimu wa siku yako hiyo na thamani yangu kwako kama mwanaume wako. Happy birthday Lilian,? akasema Edo kwa msisitizo sana.

?Thanks. Usijali, najua huko utakuwa na majukumu mengi, kwa hiyo kawaida tu, isikupe shida sana mpenzi wangu,? akasema Lilian.

?Nashukuru.?

?Ila kuna jambo kubwa sana nitakufanyia siku chache zijazo,? akasema Edo.

?Mh! Bwana unanitisha sasa. Ni jambo gani hilo??

?Surprise, siwezi kusema chochote kwa sasa, muda ukifika utajua tu. Vuta subira mpenzi wangu,? akasema Edo.

?Poa mpenzi.?

Wakakata simu zao.

Lilian wakati akizungumza na simu alikuwa amesimama, hivyo alivyokata tu simu akaanza kutembea tena. Chumbani kwao aliwakuta Lucy, Latifa na Leila wakiwa bado wamejilaza. Hata hivyo hawakuwa kwenye usingizi.

?Mama lao nakuona!? akasema Lucy kwa sauti iliyoonyesha alikuwa akijua kilichoendelea.

?Mambo zenu,? akasalimia.

?Poa, pole mwaya!? akadakia Latifa.

?Pole ya nini tena?? Lilian akauliza akiwa ameukunja uso kidogo.

?Naona mwenzetu hujarudi kabisa jana!? akasema Latifa.

?Sasa ndiyo unipe pole??

Wote wakacheka.

?Ungepewa nini sasa, maana wenzako wote kweli tuna mambo hayo, lakini hadi asubuhi??
 
Back
Top Bottom