Simulizi; Bahari ya Hindi

Simulizi; Bahari ya Hindi

Dam55

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2015
Posts
5,641
Reaction score
11,958
Simulizi : Bahari Ya Hindi
Sehemu Ya Kwanza (1)

Ilionekana gari moja aina ya Mark II (old model) ya kizamani,ikipaki nje ya geti la kuingilia bandarini….wakashuka watu wawili,,Mwanaume mmoja na mwanamke mmoja,,watu hao walikuwa wanafanya kazi sehemu moja,katika kituo cha Habari,,,yule mwanaume alifahamika kwa jina la TOBI na yule mwanamke anaitwa RODA….ghafla!!! ukasikika mlio mkali wa honi ya meli,,honi hiyo ikiashiria kuwa muda umekwisha,,meli inataka kung’oa nanga…wakakimbia haraka kuingia ndani ya geti…lakini Tobi alizuiliwa kuingia ndani ya meli…kwa sababu alikuwa amesahau tiketi nyumbani kwake,,hakuwa na ujanja akalazimika kubaki ili afanye mpango wa kukata tiketi katika meli nyingine…

Roda alisikitika sana,,lakini hakuwa na namna…akaingia ndani ya meli,,huku akimuacha Tobi hapo bandarini…baada ya dakika mbili kupita Meli ikang’oa nanga,, na safari ikaanza,,,wakati huo ilikuwa ni majira ya saa mbili za asubuhi,,Meli hiyo ilikuwa anatokea Mombasa kuelekea Zanzibar…Safari hiyo ya Roda na Tobi walikuwa waende Zanzibar kukusanya na kuandika habari kuhusu watawala wa kale(wakoloni)

Lakini Roda akalazimika kusafiri peke yake!!! Bila Tobi.
Meli ilizidi kuchana mawimbi na baada ya mwendo wa masaa matatu kupita..meli hiyo ikapata hitirafu,,injini zote mbili zikashindwa kuendelea kufanya kazi,,hivyo meli hiyo ikazimika na kubaki ikielea juu ya maji yenye kina kirefu sana…chenye urefu wa mita sabini kwenda chini!! Nahodha wa meli hiyo..akatangaza kwa kutumia kipaza sauti(MIC) sauti ya nahodha huyo ikasikika kwenye spika zilizokuwa zimewekwa kila kona,,, ndani ya meli hiyo!

Nahodha alisema hivi,,”Tunawaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza hivi punde!!!..hivyo muwe wavumilivu,,wakati mabaharia na mafundi wakiwa wanatengeneza meli hii….

Wakati huohuo,,wakaonekana mabaharia watano(mafundi wa meli) wakiingia kwenye milango inayotokezea kwenye chemba ya kwenda upande wa injini za meli hiyo….wakaanza kutafuta chanzo cha injini hizo kushindwa kufanya kazi!!!

Walitumia masaa mawili mfululizo kutafuta chanzo ni nini!!...punde si punde…mmoja kati ya mabaharia hao,,akagundua kuwa kuna kifaa kimepasuka inatakiwa kichomwe na kuunganishwa kwa moto wa gesi…bila kuchelewa mabaharia wengine wakaleta mtungi wa gesi haraka na kazi ikaanza..wakachoma kifaa hicho kwa kuunganisha na kile kipande kilichopasuka….waliifanya kazi hiyo kwa lisaa limoja wakawa wamemaliza……pamoja na yale masaa mawili yakawa masaa matatu yametimia.

Baharia mmoja akatoka kwenye chemba hiyo na kwenda kutoa taarifa kwa Nahodha kuwa tayari kazi imekwisha,,hivyo awashe mitambo safari iendelee…lakini yule Nahodha kila akijaribu kuwasha mitambo…haikuwaka,,, bado ilionekana kuwa kunatatizo katika upande wa injini..

Yule baharia akashuka kule chini ilipokuwepo injini kwa kupitia ule mlango wa chemba..kwenda kuwajulisha wenzake kuwa bado kunatatizo

Upande wa juu ya meli..alionekana Roda akiwa amesinzia kwenye kile kiti alichokuwa ameketi!! Akastuka kutoka usingizini…akaangaza angaza macho yake huku na kule..akaona abiria wenzake wakiwa wamesinzia!! Huku wengine wakiwa macho wazi…ukimya ulitawala ndani ya meli hiyo!!!.haikusikika hata sauti ya mtu akiongea na jirani yake!

Roda akainua mkono wake na kutazama saa aliyokuwa kaivaa mkononi mwake….akastahajabu!!! ilikuwa yapata saa kumi kasoro za jioni..akastuka akajisemea moyoni,,inamaana tangu muda ule mpaka sasa meli haijaondoka!!!? Roda akaanza kuingiwa na wasi wasi…
Kule nje,,,Upepo ulivuma kwa kasi..

Upepo huo ulisababisha maji ya bahari kutengeneza mawimbi makubwa sana..yakawa yanapiga kwenye ubavu wa meli hiyo..ikawa inayumbayumba huku ikielea.

Abiria wote waliokuwemo ndani ya Meli hiyo wakaanza kuingiwa na hofu……ukimya ukazidi kutawala
/
Roda akanyanyuka na kuzipiga hatua kuelekea chooni kujisaidia…

Akiwa anatembea,,kabla hajaufikia mlango wa choo,,kuna wimbi kubwa lililokuja kwa kasi na kupiga ubavuni mwa meli hiyo ikayumba kupita kiasi!!,, nusu Roda adondoke akawahi kushikilia kingo za korido ya meli hiyo..mkononi mwake alikuwa kashikilia kifaa kidodo chenye ukubwa sawa na simu ya kawaida!!(TAPE RECORDER) kifaa hicho kilimponyoka kutoka mkononi na kutumbukia kwenye ile chemba ya kuelekea kule chini,,zilipo inji za meli hiyo….kikadondoka chini zaidi…

Upande mwingine kule kwenye chumba cha Nahodha wa meli hiyo,Nahodha huyo alionekana kuingiwa na wasiwasi!!! Akajiuliza,,”mbona mpaka sasa hivi sijapokea taarifa yoyote kutoka kwa mabaharia(mafundi wa meli) kuna tatizo gani???

Nahodha huyo alijiuliza maswali bila kupata jibu…akaendelea kuwa mvumilivu,,kusubiri taarifa kutoka kwa mabaharia waliokuwa wakitengeneza injini za meli hiyo……

Upande mwingine alionekana Roda akijilaumu sana..akajisemea moyoni,,”siwezi kukiacha kifaa hicho(TAPE RECORDER)..ndicho kinatunza kumbukumbu ya kazi zangu za uandishi wa habari…isitoshe..kunahabari imo ndani yake na habari hiyo ni muhimu sana…
Roda akaamua kusukuma mlango wa chemba hiyo..akashuka upande wa chini kwa kutumia ngazi iliyokuwemo ndani ya chemba hiyo…alipofika upande wa chini akafanikiwa kukiona kifaa chake(TAPE RECORDER)….kabla hajakiokota akasikia vishindo vya mtu akikimbia kuja upande wake!!!

Akashtuka…..ghafla akasikia sauti ya mtu akilia kwa sauti kali,,ghafla sauti hiyo ikanyamaza….Roda akaamua kuchungulia aone nini kimetokea…..akashtuka!! macho yakamtoka baada ya kuona wale mabaharia watano wakiwa wameuwawa kikatiri huku damu nyingi zikitoka mwilini mwao!!! Roda akaingiwa na hofu kubwa..akatimua mbio kuifuata chemba ili atoke na kurudi kule upande wa juu..ghafla akahisi kaona kitu kimepita mbele yake kama upepo!!.lakini hakukitambua kuwa ni kitu gani!! Wakati anatahamaki,,,,,,ghafla akaguswa begani………

Alipogeuka hakuona mtu,,hofu ikazidi kuongezeka,,akajikuta anatamani apige kelele,,lakini akawa anaogopa,,endapo kelele hizo zitasikika,,wahusika wa meli hiyo wakija na kukuta wale mabaharia wameuwawa…basi yeye atakuwa hatiani…akaingia kwenye chemba,,ili apande ngazi atokezee uoande wa juu….akaanza kupanda gazi harakaharaka..alipokanyaga ngazi ya mwisho ili atokezee upande wa juu ghafla mlango ukajifunga!! Akashtuka akaachia mikono yake akadondoka chini na kupoteza fahamu!

Kule juu ya meli katika chumba cha Nahodha, alionekana Nahodha akizioiga hatua kuifuata chemba ya kushuka chini kule kwenye injini za meli hiyo,,,aliamua kwenda huko baada ya kuona ni masaa mawili mfululizo hajapata taarifa yoyote,,kutoka kwa mabaharia,,alipoufikia mlango wa chemba hiyo,,akastaajabu kukuta mlago huo umefungwa kwa ndani!!!,,,

Kutokana na uzoefu wa kuendesha meli hiyo miaka mingi,,alikuwa anazijua chemba zote za meli hiyo…..akaamua kuelekea kwenye chemba nyingine inayotikezea kule chini ya meli kwenye injini.

Wakati huo abiria wote waliokuwa wamepanda meli hiyo,,walionekana kuwa na hofo na wasiwasi juu ya safari yao,,walijiuliza mpaka mda huu bado wapo katikati ya bahari,,alafu hawajapata taarifa yoyote kutoka kwa wahusika wa meli hiyo,,kuhusu maendeleo ya matengenezo ya meli hiyo!

Nje ya meli,,Mawimbi makubwa ya maji yaliendelea kupiga kwenye ubacu wa meli hiyo..na kusabavisha mtikisiko mkubwa na meli hiyo kuyumbayumba kila wakati!! Masaa yalizidi kusonga na giza likaanda kutanda kuizunguka bahari…

itaendelea
 
BAHARI YA HINDI
SEHEMU YA 2
ILIPOISHIA….Nje ya meli,,Mawimbi makubwa ya maji yaliendelea kupiga kwenye ubacu wa meli hiyo..na kusabavisha mtikisiko mkubwa na meli hiyo kuyumbayumba kila wakati!! Masaa yalizidi kusonga na giza likaanda kutanda kuizunguka bahari…
Uoande mwingine alionekana nahodha wa meli hiyo akizioiga hatua,,hatimae kaifikia chemba nyingine,itakayoitumia kuelekea kule kwenye injini za meli hiyo,,,akafungua mlango,,akawasha swichi za taa zinazomulika huko chini ya meli..akaanza kuzipiga hatua kuzifuata injini zilipo.. ghafla akasikia sauti ya mlango ukijifunga,akashtuka!!!
Akaangaza angaza macho yake lakini hakuona mtu aliyefunga mlango huo…hakujali,,akahisi huenda kwa sababu meli inayumbishwa na mawimbi,,ndio sababu mlangu umjifunga,,akaendelea kuzipiga hatua,,alipokaribia kwenye sehemu zilipokuwepo injini za meli hiyo..akashtuka! macho yakamtoka!! Baada ya kuona mabaharia wote wameuwawa huku wakionekana kitapakaa damu mwili mzima!! Akatoa bastora iliyokuwa kwenye pochi ndogo iliyofungwa kwa mkanda kiunoni mwake…akaiweka tayari kupambana na chochote kitakachojitokeza mbele yake. Ghafla taa zikaanza kuzima na kuwaka,bila kuonekana mtu anayefanya hivyo!!!
Kule upande wa juu ya mwili,,bado walionekana abiria wa meli hiyo,, kuwa katika hali ya wasiwasi,,na hofu kubwa kuliko,,,ukimya ulitawala,,zilisikika tu kelele za mawimbi yakigpiga kwenye ubavu wa meli na kusambaa…ghafla taa zikazimika,baada ya sekunde kadhaa zikawaka,,abiria wakaanza kupiga mayowe na kelele,,wakiomba wapate taarifa kuhusu maendeleo ya meli hiyo,,kutoka kwa wahusika!!!
Ghafla taa zikazimika!!! Hazikuwaka tena,,giza lilitawala,,na kila abiria alibaki kimya akiMuomba mungu , kwa imani yake..
Nje ya meli upepo uliendelea kuvuma kwa kasi,,huku mawimbi makubwa yakiendelea,,kuizonga bahari!! Vingu kubwa likatanda,,,,hatimae mvua kubwa ikaanza kunyesha….
Kule chini ya meli, zilipo injini za meli hiyo,,alionekana Nahodha wa meli hiyo,,,akiwa ameshikilia bastola huku macho yake yakitazama kwa tahadhali!
Wakati huohuo alionekana Roda akiwa bado kalala pale chini baada ya kudondoka kutoka juu ya ngazi..
Roda akaanza kupata fahamu,,akafumbua macho,,
Akashtuka kuona giza nene limetanda!!! Akanyanyuka haraka,,akaanza kubahatisha nzia kwa kupiga hatua huku katanguliza mikono yake yote miwili mbele huku akipapasa papasa aendako,,,ghafla akagusa makalio ya Nahodha!!
Nahodha akashtuka akajikura anafyatua risasi ovyo ovyo bila kumuona mtu anayemshambulia..
Roda alipiga kelele huku kachuchumaa,,,akaziba masikio yake kwa kutumia viganja vyake vya mikono…
Nahodha huyo aitwae YUVE,,akapaza sauti na kusema,,”WEWE NI NANI?? JITAMBULISHE HARAKA KABLA SIJATENGANISHA ROHO NA KIWILIWILI CHAKO!
Yuve aliuliza swali hilo huku akiwa na uwoga wa hali ya juu…
Ikasikika sauti ya Roda ikisema,,usiniuwe kaka yangu!! Naomba msaada wako unitoe huku niweze kurudi kule juu ya meli,, kwenye kiti changu.
Yuve akasema kwa sauti ya msisitizo,,”nataka uniambie wewe ni nani? Na umeingiaje huku kwenye chumba cha injini!!! Na ulikuwa na lengo gani??
Roda alishindwa kujibu chochote,,ghafka ikasikika sauti ya kitu kikijigonga kwenye nguzo moja iliyopo eneo hilo….
Yuve akazidi kuchanganyikiwa….jwa sababu alikuwa haoni mtu yeyote,,bali alisikia sauti tu,,kutikana na giza totoro lililokuwa limetanda humo baada ya taa kuzimwa na mtu asiyejulikana…..
Wakati Yuve bado yupo katika hali ya mshangao!!!
Ghafla zikasikika sauti za abiria kule juu ya meli wakipiga mayowe ya kuomba msaada!!
Roda akasema,,”kaka upo wapi naomba unisaidie kunitoa huku,,,Roda aliongea maneno hayo huku mapigo yake ya moyo yakipiga kwa kasi,,na hofu kubwa kutanda juu yake,,kwa sababu alikuwa hamuoni mtu anayeingea nae, kutikana na giza nene ndani ya chumba hicho maalumu kwa injini za meli hiyo..
Yuve alizidi kuchanganyikiwa akajikuta anatetemeka mwili mzima kutokana na uwoga wa hali ya juu! Akazipiga hatua kwa kutumia hisia na uzoefu kuufuata mlango wa kutokezea kwenye chemba ya kufika uoande wa juu ya meli..ghafla taa zikawaka,,na mwanga ukamulika kila kona ya chemba hiyo….Yuve akaangaza angaza macho yake huku na kule akamuona Roda,,akastaajabu sana akamuuliza,,huku ulikuja kutafuta nini???
Yuve aliuliza huku bado akiwa na mashaka na Roda.
Roda akajibu,,”nimekuja kufata kifaa changu kilidondija huku chini wakati nataka kuingia chooni(TOILET)! Yuve akashtuka akauliza kwa mshangao!! Kifaa chako?? Kifaa kipi hicho??
Kabla Roda hajajibu taa zikazimika,,na giza likatanda!! Baada ya sekunde kadhaa taa zikajiwasha bila kuonekana mtu anayewasha taa hizo….walipotahamaki..wakamuona mtoto mdogo wa kiume kasimama katikati yao huku akiwa amevalia mavazi meupe yanayo ng’aa,,mtoto huyo alionekana kuwa na umri kati ya miaka minne(4) au mitano(5) akaachama mdomo wake,,machi yake yakabadilika na kuwa kama ya mnyama paka! Meno mawili ya juu na chini uakawa marefu kama ya mbwa..kucha zake za mikononi zikaanza kurefuka akazipiga hatua kumfuata Roda…
Roda akapiga mayowe kwa uoga wa hali ya juu..hofu kubwa ilitanda juu yake,,Yubv akafyatua pqrisasi mbili kumlenga yule mtoto kichwani. Risasi zikaingia ndani ya kichwa cha mtotoq huyo…akageuza shingo yake kumtazama Yuve..mtoto huyo akapindisha shingo yake kushoto kulia,,huku akiendelea kumtazama Yuve.punde si punde Yuve akahisi kukabwa shingoni na kitu kisichoonekana….akaanza kushindwa kuvuta pumzi wala kutoa pumzi..akaachilia bastola baada ya dakikamoja kupita akadondoka chini na kupoteza maisha…Roda akatimua mbio akajificha chini ya injini moja ya meli hiyo!
Akawa anachungulia ili aone mtoto huyo atafanya nini baada ya hapo!! Yule mtoto akageuza shingo yake na kutazama ule upande ilipokuwepo injini ya meli hiyo..
Roda akashtuka,,akiamini kuwa yeye ndiye anayefuata kuuwawa!! Akajiziba mdomo kwa kutumia kiganja cha mkino wake mmoja…ili asipige kelele ikasikika kwa mtoto huyo….
Roda aliendelea kuchungulia akimtazama mtoto huyo..ghafla mtoto huyo akatoweka kimiujiza,,na kutokomea kusikojulikana…
Kule juu ya meli Abiria waliendelea kupiga mayowe ya kuomba msaada,,baada ya kuona abiria mmoja mmoja anauwawa na mtu asiyeonekana kwa macho….huku taa zikizimika na kujiwasha pasipo mtu yeyote kuonekana akifanya kitendo hicho!!! Ghafla taa zikawaka na mwanga ukaangaza kila kona ndani ya meli hiyo.
Abiria wote wakanyamaza,,na ukimya ukatawala…
Wakati huo meli ilikuwa inayumba yumba, kutokana na mawimbi makubwa yaliyokuwa yanapiga ubavuni mwa meli hiyo..
Upande mwingine,, chini ya bahari,kilionekana kiumbe kisichokuwa na mfano kikija upande wa juu ya bahari,,kiumbe hicho kilionekana kutisha sana,,ghafla kikatoweka,,kikajitokeza ndani ya meli hiyo!!! Kule juu sehemu ya abiria.
Abiria wote wakaingiwa na hofu baada ya kumuona kiumbe huyo,,wakaanza kupiga mayowe,,ghafla taa zikazimika!!! Giza likatawala kupita kiasi,,baada ya sekunde kadhaa,,ukasikika mngurumo wa injini za meli,,na meli ikawaka,,,taa zote zikawaka,, na kuangaza kila kona ndani ya meli hiyo,,meli ikaanza kuondoka,,
Roda akashtuka kutoka usingizini…akaangaza angaza macho yake huku na kule akaona abiria wote wameketi huku wengine wamesinzia…akajisemea moyoni..MUNGU WANGU..hii ndoto ina maana gani? Sijawahi kuota mdoto ya kutisha kiasi hiki!!! Akajipapasa mifukobi mwake kuangalia kifaa chake kinachomrahisishia kazi…katika shughuri zake za uandishi wa habari..
Akakiona kimo ndani ya mfuko wa koti alilokuwa amelivaa…akatazama upande wa nje kwa kupitia moja ya dirisha la meli hiyo..akaona meli inaendelea na safari..
Kumbe mambo yale yote yaliyotokea ilikuwa ni mdoto aliyoiota baada ya kuketi na kupitiwa usingizi ndani ya meli hiyo…
Akahisi kiu,,akanyanyuka na kuufuata mgahawa uliokuwemo ndani ya meli hiyo maalumu kwa abiria…akanunua maji pia akaagiza chakula akaanza kula huku akichezea simu yake..
Alipo angaza macho yake,,kwa mbali akamuona mtoto mdogo wa kiume…mtoto huyo alifanana kila kitu,mpaka mavazi na yule mtoto aliyemuona kwenye ndoto….Roda akashtuka akajisemea moyoni,,”mmh! Mbona nimeanza kuingiwa na wasiwasi!!! Akanyanyuka haraka,,akazioiga hatua kumfuata mtoto huyo…akamuona anaelekea kwenye kiti kilichokuwa wazi,,na kando yake kulikuwa na Bibi kizee mmoja,, akamuona mtoto huyo akiongea na huyo Bibi huku wakicheka na kufurahi,,mkononi alionekana kushikilia sahani iliyokuwa na chipsi kuku pamoja na chupa ya maji ikiwa nusu.
Roda akajisemea moyoni,”bila shaka huyo ni Bibi yake…au itakuwa nilimuona huyu mtoto kavla sijasinzia na ndio maana nimeota na kumfananisha!!
Roda hakujali,akaamua kurudi kule ndani ya mgahawa ili aendelee kula chakula chake,,,alipoikaribia meza aliyokuwepo mwanzo akastaajabu..kutokuiona sahani iliyokuwa na chakula chake alichoagiza,,pia ile chupa ya maji aliyoiacha ikiwa na maji nusu haikuwepo!!!...akajisemea moyoni,,”jamani niliacha hapa juu ya meza hii sahani ikiwa na chipsi kuku. Nani atakuwa kachukua chakula changu????
Wazo likamjia akajisemea moyon,,”huenda wahudumu wa mgahawa huu wamekiifadhi baada ya kuona nimeondoka,,wacha mikawaulize.
Akazipiga hatua kumfuata muhudumu mmojawapo kati ya wahudumu wa mgahawa huo akauliza,,”chakula changi nilikiacha kwenye meza ilepale!! Nani kakitoa wakati mimi bado sijamaliza kula!!! Yule muhudumu akaonekana kumshangaa Roda!!! Kisha akasema,,”kwa kweli mimi sifahamu chochote kuhusu chakula chako…
Kaba hajamaliza kuongea sentensi hiyo..ghafla meli ikazimika…na baada ya sekunde kadhaa Nahodha akatangaza kwa kutumia kilaza sauti,,akisema,,”abiria wote tunaomba muwe wavumilivu,,mele imepata hitirafu..na muda si mrefu mafundi(mabaharia) wataitengeneza haraka iwezekanavyo….
Roda akashtuka!! Akazipiga hatua kutoka ndani ya mgahawa huo…alipoangaza macho yake kwenye kile kiti alichokuwa ameketi yule Bibi kizee pamoja na yule mtoto hakuwaona tena….
Roda akaingiwa na wasiwasi….akazipiga hatua za haraka haraka akapanda ngazi kuelekea kwenye chumba maalumu cha Nahodha anayeiongoza meli hiyo…alipofika akafungua mlango wa chumba hicho bila ruhusa,,akaingia kwa pupa mlaka upande wa ndani!! Nahodha akashtuka akauliza kwa mshangao kulikoni? Hiki ni chumba maalumu kwa ajili ya mtu anayeingoza meli ikiwa safarini,,haruhusiwi mtu yeyote kuingia bila ruhusa au kibali…kwani ,ulikuwa na shida gani?
Roda akauliza,,”Jina lako unaitwa nani?
Nahodha akamtazama Roda kwa macho ya mshangao,,akasita kwa sekunde kadhaa kisha akajibu,,”Mimi naitwa Sam.
Roda akauliza kwa mshangao Yuve ni nani?
Nahodha akasema,,”hakuna muhusika wa meli hii anayeitwa Yuve!!! Labla jina lingine…
Punde si punde akaingia mmoja kati ya mabaharia ambaye ni fundi wa Meli hiyo…akamwambia Sam,,”kuna paipu moja imepasuka kule kwenye injini ya upande wa kushoto…
Sam akasema,,”fanyeni uwezekano wa kuiziba ili tuendelee na safari.
Yule baharia akafungua mlango na kutoka nje,,akaelekea kwenye chemba za kushuka kule chini zilipokuwepo injini za meli hiyo..
Roda akagisi kuchanganyikiwa akamtazama Sam ambaye ni nahodha wa Meli hiyo,,akataka kusema neno lakini akasita akafungua mlango na kutoka ndani ya chumba hicho. Akazipiga hatua za haraka haraka kuelekea sehemu ya abiria… kwa mbali akamuona yule mtoto wa kiume akiishilizia kwenye korido ya kuelekea kwenye vyoo vya Meli hiyo..Roda akaamua kumfuata mtoto huyo angalau amchunguze,,
Lakini Roda alipoifikia korido hiyo akaona mguu mmoja wa mtoto huyo ukiishilizia kuelekea katika chumba cha choo.
Roda akazipiga hatua za kunyatia kumfuata aone mtoto huyo anafanya nini!!!! Alipokikaribia kwenye choo hicho…..akashtuka!! akahisi kuna mtu anamfatilia kwa nyuma….Roda akageuza shingo yake haraka ili atazame ni nani aliopo nyuma yake!! Akamuona yule bibi kizee akiishilizia kwenye kina ya korido kuelekea kule sehemu ya abiria…..Rose akajiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu,,”kwa nini kila nikiangaza macho yangu namuona yule mtoto akiwa anaishilizia kukatisha kona…hata huyu bibi yake pia,,mmh!! Bila shaka kuna jambo ambalo si la kawaida!!! Roda akaamua kuchungulia kwenye kile choo alichoingia yule mtoto… alipotazama kwa makini hakuona mtu ndani ya choo hicho!!
Akashtuka akajisemea moyoni,,”au sio chumba hiki!!? Lakini mbona niliona anaingia humu?
INAENDELEA
 
Simulizi : Bahari Ya Hindi
Sehemu Ya 3
/
Wakati Roda anajiuliza maswali hayo..ghafla ikasikika sauti ya mtoto wa kiume ikiongea kwa lugha ya kiarabu,, sauri hiyo ilijirudia rudia(mwangwi) Roda akastaajabu..akachungua tena….lakini hakumuona mtu anayetoa sauti hiyo!!!
Akaingiwa na hofu akageuza shingo yake kutazama mbele ili atimue mbio kurudi kule sehemu ya abiria,, akashtuka kumuona yule mtoto akizipiga hatua kutokea kule sehemu ya abiria akija upande ambao Roda kasimama!!!Roda akaingiwa na hofu kwa sababu alimuona mtoto huyo kaingia chooni alafu sasa hivi anamuona anatokea kwenye sehemu ya abiria…
Yule mtoto akazidi kuzipiga hatua kumsogelea Roda…wakat huo Macho yalikuwa yamemtoka Roda akataka kupiga kelele kutokana na mauzauza aliyoyaona….ghafla akaonekana abiria mmoja wa kiume akija upande huo huo kwa lengo la kwenda chooni kwa ajili ya kujisaidia haja ndogo,,,
Wasiwasi ukaanza kupungua kwa Roda….akamtazama yule mtoto kwa macho ya uwoga.
Yule mtoto akafungua mlango na kuingia chooni huku akimtazama Roda kwa macho ya msisitizo,,,,Roda akaamua kuzipiga hatua kutoka kwenye korido hiyo,,na kuelekea kule kwenye sehemu ya abiria…
Yule abiria wa kiume akafungua mlango na kuingia chooni….
Kabla Roda hajafika mnali akasikia sauti ya mtu akipiga kelele huku akigonga gonga mlango ufunguliwe atoke nje..ghafla sauti hiyo haikusikika tena…
Roda akatimua mbio na kuelekea kwenye kiti chake..akaketi,,huku akipumua kwa mfululizo,,aliogopa hata kugeuza shingo yake kutazama kushoto wala kulia…ghafla wingu likatanda nda mvua ikaanza kunyesha.
Wakati huo huo upande mwingine walionekana mabaharia kadhaa wakiingia kwenye moja ya chemba inayoelekea kule kwenye injini za Meli…bila kuchelewa ukaletwa mtungi wa gesi maalumu kwa kuchoma(kuunganisha) chuma chepesi..na kazi ikaanza mara moja.
Wakaiziba paipu hiyo kisha baharia mmoja akatoka na kupandisha kule juu kumpa taarifa Sam kuwa tayari wameshamaliza kufanya matengenezo,,hivyo awashe mitambo Meli iwake na safari iendelee…..
Upande wa nje mvua kubwa iliendelea kunyesha mfululizo,,Ghafla!!! Likaonekana wimbi kubwa kupita kiasi likiifuata meli hiyo…likaizonga na kuifunika Meli ikatoweka kimiujiza..
Hakuna abiria yeyote aliyefahamu nini kimetokea!
Kwa sababu kilikuwa ni kitendo cha sekunde moja tu…Meli hiyo ikajitokeza kwenye sehemu tofauti kabisa…hata Sam(Nahodha) alishangaza sana kila akiangalia muelekeo ulionesha tofauti katika kifaa maalumu (DIRA) (COMPASS) cha kuangalia muelekeo wa meli inapokwenda..kilionesha meli hiyo inaelekea magharibi mwa bahari ya hindi..akashtuka akatazama nje ya meli hiyo kwa kupitia kioo cha Meli hiyo,,kilichokuwa maalumu kwa Nahodha kutazama ulande wa nje.
Sam akashuka kuona bahari nyingine tofauti ma muonekano wa bahari aliyoizoea siku zote akiwa anakiendesha chombo hicho majini..
Akaamua kufungua mlango akatoka na kuelekea kwenye chumba cha abiria..akastaajabu kuwaona abiria hawana wasiwasi kabisa…wametulia tuli..
Sam akaamua kuelekea kwenye chemba inayotokezea ke chini kwenye injini za meli hiyo.
Alipofika akastaajabu kuwaona mafundi wa meli hiyo(mabaharia) wakiwa wanapiga stori bila wasiwasi! Sam akauliza,,”jamani mbona kama mimi naona meli inaelekea magharibi na bahari inaonekana tofauti kabisa inatisha kupita kiasi..wale mabaharia wakashtuka wakaamua kuingia kwenyechemba inayotokezea nje kabisa ya meli hiyo(upande wa juu)
/
Upande mwingine alionekana Roda akiwa bado kaketi kwenye kiti chake..lakini alionekana kuwa na wasiwasi na hofu kubwa…akanyanyuka na kuzipiga hatua kuelekea kwenye korido inayotokezea nje ya meli….kwa mbali akamuona yule Bibi kizee akiishirizia kwenye kona…Roda akashtuka akageuka ili arudi kwenye kiti chake..ghafla akakutana uso kwa uso na yule mtoto akiwa amesimama mbe yake..Roda akaingiwa na hofu,,macho yakamtoka huku mapigo yake ya moyo yakipiga kwa kasi ya ajabu..
Punde si punde taa zikazimika na kujiwasha zenyewe,, Roda akatazama ile sehemu aliyokuwa kasimama yule mtoto,,hakumuona tena…hapo Roda akagundua kuwa ile ndoto aliyoiota sio ya kawaida..na hicho anachokiona sasa hivi sio ndoto tena bali ni kweli,anashuhudia kwa macho yake…akatimua mbio kurudi kule sehemu ya abiria. Ghafla taa zikazimika tena…
Abiria wengine hawakuwa na wasiwasi,,walijua huenda radi zilizokuwa zinapiga nje..zinasababisha,,mgusano wa nyaya (shot) ndio sababu taa zinazimika na kujiwasha zenyewe..
Roda akashindwa kuvumilia akapaza sauti na kusema,,”JAMANI TUSIKILIZANE. Humu ndani ya Meli kunamauza uza na nimeyashuhudia kwa macho yangu…
Kabla Roda hajaongea neno lingine ukasikika mngurumo wa kutisha sana..kisha taa zikazimika.
Sasa hivi taa hazikuwaka tena,,giza likatawala…ghafla ulengurumo ukatoweka..na ukimya ukatawala..
Taa zikawaka abiria wote wakaanza kupiga mayowe ya uwoga baada ya kuona baadhi ya abiria wakiwa wameuwawa na mtu asiye fahamika !! ni kitendo cha sekunde ikawa ni mtafutano ndani ya Meli hiyo..kila abiria alikimbia kutafuta sehemu ya kujificha lakini ikashindikana…kelele za vilio zilitawala ndani ya Meli hiyo..punde si punde..taa zikazimika tena!!!!
Abiria wote wakabaki kimya bila kujua hatma yao ni ipi?
Ikasikika sauti ya milango ya chuma ikijifunga…ghafla taa zikawaka….abiria walipojaribu kufungua milango haikufunguka ilikuwa imefungwa..hakuna aliyeweza kutoka nje ya Meli hiyo…
Upande mwingine,,walionekana mafundi wa meli hiyo(mabaharia)kule kwenye chemba ya kutokezea nje ya Meli hiyo wakiwa wanazipiga hatua mdani ya chemba….ghafla mlango ukajifunga…wakatimua mbio kuufuata mlamgo wa kutokezea nje kabisa,,walipoukaribia pia ukajifunga…kisha taa zikazimika…giza likatawala..lilikuwa ni giza totoro ambalo huwezi kuona kitu kilichopo mbele yako.. ghafla ikasikika sauti ya Baharia mmoja akipiga mayowe ya kuomba msaada…wale mabaharia wengine wakaingiwa na hofu!! Punde si punde ikasikika sauti ya baharia mwingine akivurutwa na mtu asiyeonekana akapiga kelele ghafla sauti ikanyamaza na maji yakawarukia wale mabaharia wawili waliobaki ndani ya chemba hiyo..
Baharia mmoja akashtuka kumwagikiwa na maji usoni mwake..akajifuta maji yale akanusa…akashtuka kusikia harufu ya damu mbichi na sio maji!!! Akamwambia mwenzake kuna hatari! Hatupo sehemu salama..wakaanza kupiga kelele za kuomba msaada..
ITAENDELEA
 
BAHARI YA HINDI
SEHEMU YA 4
ILIPOISHIA….Baharia mmoja akashtuka kumwagikiwa na maji usoni mwake..akajifuta maji yale akanusa…akashtuka kusikia harufu ya damu mbichi na sio maji!!! Akamwambia mwenzake kuna hatari! Hatupo sehemu salama..wakaanza kupiga kelele za kuomba msaada..
Libaki baharia mmoja alikuwa ni mtumiaji wa kilevi aina ya bangi!
Alishindwa kuongozana na wenzake akabaki hapo kumalizia kuvita kipisi cha bangi..ghafla akasikia sauti za mabaharia wenzake wakiomba msaada..
Akaamua kuufuata mlango ili awafungulie wenzake..
Alipoufungua kikarushwa kiwiliwili cha mmoja kati ya mabaharia walioingia kwenye chemba hiyo..kikiwa nusu,,kuanzia kiunoni kushuka chini..
Kiwiliwili hicho kikadondoka mbele yake..akashtuka akajisemea moyoni,,”bila shaka hizi ni bangi zimenilevya, Binadamu gani anakuwa nusu!! Akachuchumaa na kugusa damu,alipozinusa akagundua kuwa ni damu..akili ikamkaa sawa,,akanyanyuka haraka huku akiwa na hofu kubwa kupita kiasi..akaifuata chemba inayotokezea kule kwenye ulande wa abiria..gjafla akamuona ye Bibi kizee akiwa anazipiga hatua kuja upande wake..lakini alipomtazama kwa makini akaona Bibi kizee huyo miguu yake haikanyagi chini..anatembea hewani..
Alipogeuza shingo yake ili atimue mbio kutafuta chemba nyingine akakutana uso kwa uso na yule mtoto..wakatazamana machoni!! Ghafla damu zikaanza kutoka machoni mwa Baharia huyo huku akihisi kukabwa shingoni..akakosa pumzi akashindwa kupumua akadondoka chini ma kupoteza maisha..**********************
Kule juu sehemu ya abiria,,alionekana Roda akiwa anatafuta sehemu ya kujificha..kwa mbali akaona kuna chumba kipo wazi hakijafungwa mlango akatimuabio kukifuata chumba hicho akajifiche..akaingia haraka ndani ya chumba hicho akaufunga mlango haraka…..akasimama kando..ghafla akasikia mlango huo unafujinga wenyewe kwa ufunguo. Punde si punde taa iliyokuwa inamulika ndani ya chumba hicho ikazimika na giza likatawala….Roda akaingiwa na hofu kubwa kupita kiasi baada ya kusikia vishindo vya mtu akitembea ndani ya chumba hicho..
Hofu ikazidi kuongezeka! Akapiga kelele ghafla taa ikawaka.na mlango ukafunguka wenyewe.Roda akaogopa hata kutoka nje ya chumba hicho,akabaki kasimama,,
Kelele za abiria wakipiga mayowe ya kuomba msaada zilitawala ndani ya meli hiyo..
Roda akazipiga hatua za taratibu kutoka ndani ya chumba hicho huku macho yake yakitazama kwa umakini wa hali ya juu…alipotoka ndani ya chumba hicho..akatimua mbio..kutafuta uwezekano wa kujificha…
Upande mwingine alionekana Sam akiwa amejifungia katika kile chumba maalumu cha kuiongoza meli…Sam alikuwa na wasiwasi kupita kiasi..akatazama upande wa nje,kwa kupitia kile kioo cha nahodha kutazama upande baharini.
Sam akashtuka kuona Giza limetanda ndani ya sekunde moja…Sam akaogopa akafungua mlango na kutimua mbio kuelekea sehemu ya abiria,,akashtuka kuina abiria wote wanatafuta jinsi ya kutoka nje ya meli hiyo,,huku abiria wengine wakiwa chini wameuwawa…damu zilionekana kutapakaa kila kona ndani ya meli hiyo!! Utadhani ni uwanja wa vita.
Upande mwingine alionekana Roda akiendelea kutafuta sehemu ya kujificha…….alipoangaza macho yake kwa mbali akaona chemba moja ikiwa wazi..akaamua kuifuata chemba hiyo akaingia haraka akajifiche…akapita ndani ya chemba hiyo akajikuta anatokezea kule chini kwenye injini za meli hiyo.akatereza nakudondoka akaangukia juu ya maiti ya mmoja kati ya mabaharia waliouwawa…Roda akapiga kelele kwa sauti kalinmfululizo..akanyanyuka haraka akatimua mbio pasipo kujua ni wapi anaelekea…akaingia kwenye chemba nyingine..akapita humo akajikuta anatokezea nje ya meli(upande wa juu) akastaajabu kumkuta ye bibi kizee akiwa amesimama peke yake.bila kuonekana mtu mwingine yeyote…Roda akajificha akaendelea kuchungulia ili aone Bibi kizee huyo anafanya nini..
Akamuona ananyanyua mikono yake juu ghafla Bibi kizee huyo akageuza shingo yake haraka akatazama ule upande aliokuwepo Roda..
Sura ya Bibi huyo ikabadilika na kuinekana kutisha sana kisha bibi huyo akamfuata Roda huku anazioiga hatua hewani hewani..Roda akajikuta anapiga kelele akatimua mbio kuridi ndani ya chemba ghafla Roda akamuona ye bibi kizee ndani ya chemba hiyo akiishirizia mguu wa mwisho kutoka ndani ya chemba hiyo..
Roda akahisi kuchanganyikiwa akaitimua mbio kurudi upande wa nje ya meli..akaufunga mlango wa chemba hiyo kwa komeo la nje..
Akaangaza angaza macho yake pande zote..kwa mvali akaona taa inawaka baharini..akagundua kuwa ni boti ndogo inakuja upande huo..akaanza kupata matumaini…
Upande wa ndani ya meli hali ilizidi kutisha zaidi..yule bibi kizee alijitokeza mbele ya Sam akakutanisha macho na Sam…ghafla Sam akabadilika akuingiwa na roho ya kikatiri kupita kiasi…bibi kizee huyo akatoweka kimiujiza..
Sam akaingia ndani ya meli akabadilisha muelekeo wa meli ikawa inaelekea mashariki mwa bahari ya hindi…aliiongoza meli hiyo pasipo yeye kujitambua mpaka ukingoni mwa bahari..kwenye sehemu iliyoonekana kuwa na mapango na miamba mikubwa kupita kiasi…Kwa mbali akaonekana mwanamke amelala nchi kavu akiwa.nusu binadamu nusu samaki…mwanamke huyo akajivuruta akaingia ndani ya bahari na kutokomea kusikojulikana..
Roda alishuhudia tukio hilo kwa sababu alikuwa kule nje juu ya meli hiyo.pia taa kubwa ya meli hiyo ilimulika vyema ulande wa nje…hofu ikazidi kuongezeka akakosa pa kukimbilia..aliogopa kurudi ndani ya meli kwa sababu alishuhudia mauzauza na mauwaji ya kutisha..ghafla meli hiyo ikaanza kuzama taratibu kuelekea chini ya bahari…Roda akaingiwa na wasiwasi!! Macho yakamtoka akatafakari nini cha kufanya lakini alishindwa akaamua kuruka kutoka juu ya meli na kujitosa baharini…akastahajabu maji hayamgusi..huku akizidi kuelekea chini zaidi..akaanza kupiga kelele..lakini kelele hizo hazikumpa msaada..akazidi kuelekea chini..akiwa ndani ya maji hakuweza kuona kitu chochote kwa sababu ya giza kuwa totoro…lakini alizidi kustaajabu akajiuliza,,”mbona maji hayagusi mwili wangu? Yani kama nipo angani..wakati anajiuliza maswali hayo yasiyokuwa na majibu..ghafla akaanza kuona mwanga chini ya bahari..mwanga huo ulimulika pakawa kama mchana…akaanza kuona majengo na magari ya kifahari huku watu wakiendelea na shughuri zao kama wapo nchi kavu….alipoangaza angaza macho yake akashtuka kumuona yule bibi kizee….
Macho yakamtoka Roda ghafla akaangukia juu ya paa la nyumba..akashtuka akaingiwa na hofu kubwa kupita kiasi… punde si pundeikasikika sauti ikisema..ebu katazame nini kimedondika juu ya bati… Roda akajaribu kupiga mbizi akadondika kutoka juu ya paa la nyumba hiyo..akaanguka chini..wakati anatahamaki…yule mtoto akajitokeza mbele yake akagusa mwili wa Roda….yule mtoto akaanza kubadilika…ngozi yake ikaanza kujivua yenyewe mwilini..kumbe ni mwiko kugusa mwili wa binadamu wa kawaida..kitendo hicho kikamshtua Roda macho yakamtoka..ghafla akasikia sauti ya kitu kikidondoka kutoka juu..aliponyanyua shingo yake alishtuka kuiona meli ikiangukia hiyo sehemu aliyosimama..ni ile meli iliyozama muda mchache uliopita yeye akajitosa baharini..
Roda akatimua mbio ghafla akavutwa na mtu asiyeonekana……
ITAENDELEA
 
BAHARI YA HINDI
SEHEMU YA 5
ILIPOISHIA…..Roda akatimua mbio ghafla akavutwa na mtu asiyeonekana……
Akajikuta yumo ndani ya jumba la kifahari.akashtka sana hakujua amefikaje fikaje ndani ya nyumba hiyo..akaangaza angaza macho yake. Hakuina mtu hata mmoja kuinekana ndani ya jumba hilo la kifahari…akazipiga hatua za haraka haraka akaufuata mlango alipojaribu kuufungua mlango haukufunguka ulikuwa umefungwa kwa nje.,,,akaamua kuchungulia dirisha..akastaajabu kuona ile meli imegota chini..huku bahari imebadirika rangi na kuonekana ni damu tupu..damu hiyo ilizunguka kwenye eneo la meli hiyo pekee..Roda akaingiwa na hofu,,akajiuliza,,”hivi mimi naota! Au naona kweli mambo haya yanatendeka!!!?
Roda akanyanyua mkono wake akajipiga kofi..akahisi maumivu..akagundua kuwa hayupo katika ndoto bali anayaona mambi hayo yanatendeka kweli!!! Macho yalimtoka..ghafla akamuona Mwanamke mrembo kupita kiasi..mwanamke huyo alikuwa anatokea upande wa ndani ya meli..huku mdomo wake ukiwa umezungukwa na damu…
Roda akastaajabu kuona zile damu mdomoni mwa mwanamke huyo hazisambai wakati maji ya bahari yamemzunguka mwanamke huyo!!!.lakini mwanamke huyo alikuwa anazipiga hatua kama anatembea nchi kavu…Roda akatazama miguu ya mwanamke huyo haikuonekana ilikuwa imefunikwa na gauni refu lililokuwa linaburuza chini. Ghafla mwanamke huyi akatoweka kimiujiza haikujulikana ni wapi kaelekea..
/
Roda akazidi kuchanganyikiwa..akajikuta anaangua kilio bila kujua hatma yake ni nini…
Kwa mbali akamuona yule bibi kizee akizipiga hatua kuifuata nyumna hiyo..Roda akaingiwa na wasiwasi,,hofu ikazidi kuongezeka..akatimua mbio akaingia kwenye chumba kilichokuwa karibu na sebule…akajifungia humo..akaangaza angaza macho yake akastaajabu kuona vitu vingingi vya thamani..vitu hivyo vilitengenezwa kwa madini ua dhababu tupu…ghafla kumbukumbu ikamjia! Akakumbuka marehemu babu yake aliwahi kumsimulia kuhusu majini…pia akakumbuka kuwa makazi yao ni baharini sehemu yenye kina kirefu sana..ghafla akahisi kunusa marashi..marashi hayo yalinukia vyema kupita kiasi…
Akashtuka akajisemea moyoni,,”bila shaka nipo kwenye himaya ya majini.Eee Mungu ninusuru nitoke salama..
Punde si punde akabmuona yule Bibi kizee kaingia ndani ya chumba hicho pasipo mlango kufunguliwa…bibi kizee huyo alioenda kwenye ukuta kama upepo na kujitokeza upande wa ndani.
Roda akapiga kelele..lakini kelele hizo hata yeye mwenyewe hakuzisikia!!! Ingawa alikuwa anapaza sauti kali lakini sauti haikutoka..
Yule bibi kizee akaketi kwenye kiti kilichokuwa ndani ya chumba hicho,, akaanza kumuongelesha Roda kwa lugha iliyofanana na maneno ya lugha ya kiarabu..Roda akabaki mdomo wazi huku amekodoa macho kumtazama bibi huyo…
Ghafla Roda akanza kusikia na kuielewa lugha hiyo!! Akajisemea moyoni,,”mbona sijawahi kujifunza lugha hii!!! Iweje nasikia na kuelewa kile anachokiongea huyu bibi kizee!!?
Wakati Roda anawaza hayo yote..
Bibi kizee huyo akaonge tena kwa ligha hiyo..
Roda akaelewa kilicho ongelewa bibi huyo alimaanisha kuwa,,”umefanya kosa kubwa ambalo ni vigumu kuepuka adhabu ambayo unastahiri kuipata..kulingana na kosa ulilolifanya.
Roda akashtuka kusikia hivyo..hofu ikazidi kuongezeka,,mapigo yake ya moyo yakaanza kupiga kwa kasi zaidi huku jasho likimtoka kwa uwoga wa hali ya juu.
Ghafla bibi kizee huyo akatoweka kimiujiza!
Ikasikika sauti ya milango ikijifungua yenyewe..kila baada ya sekunde..
Roda akatimua mbio kutoka ndani ya chumba hicho akaelekea sebuleni akashtuka kumuona Tobi ameketi kwenye sofa,,Roda akastaajabu sana akauliza kwa mshangao,,”na wewe wamekuleta huku??
Roda aliuliza swali hilo huku akimtazama Tobi..lakini Tobi alionekana kutokuwa na wasiwasi kuwepo sehemu hiyo..
Furaha ya Roda ikaanza kurejea taratibu,,kwa sababu kamuona mtu wake wa karibu anaye fanya nae kazi katika kituo cha habari.
(uandishi wa habari),,,Roda akazipiga hatua za haraka haraka mpaka kwenye sofa alilokuwa amelikalia Tobi..akamuuliza,”kulikoni mbona upo hapa!? Hivi unaweza kuitambua sehemu hii?
Tobi akatabasamu tu,bila kujibu kitu chochote.
Akabaki kimya kwa sekunde kadhaa kisha akanyanyuka kutoka pale alipokuwa ameketi.akazipiga hatua kadhaa,,akasimama akageuza shingo yake na kumtazama Roda..
Roda akaanza kuingiwa na hofu..alishangazwa na kitendo cha Tobi kutokuwa na wasiwasi kabisa..yani Tobi alionekana kama hapo ni nyumbani kwake..au sehemu anayoijua..
Tobi akasema,,”Roda…mbina unaonekana kuwa na wasiwasi? Kuwa huru jisikie upo nyumbani.
Machi yakamtoka Roda baada ya kusikia kauli hiyo kutoka kinywani mwa Tobi!!
Roda akaingiwa na hofu akauliza kwa sauti ya msisitizo,,”nijisikie nipo nyumbani??
Tobi acha utani hii ni sehemu ya majini!! Wewe huogopi??
Tobi akacheka kwa sekunde nyingi. Kisha akasema,,”bila shaka haujakosea..hapa ni nyumbani kwetu nilipozaliwa..na yule bibi kizee uliyekuwa unaongea nae ni mama yangu mzazi..na yule mtoto uliyekuwa unamuona mara kwa mara ndani ya meli ni mimi..
Rose akaanza kumuogopa Tobi!! Akajisemea moyoni,,”inamaana Tobi kayajuaje haya yote wakati nilimuacha Mombasa pale bandarini baada ya yeye kusahau tiketi yake nyumbani!!!
Kumbe Tobi alikuwa anajua kila kitu anachokiwaza Roda akilini mwake..
Tibi akasema,,”ni kweli uliniacha lakini tulisafari safari moja pasipo wewe kujua…lakini kini ulifanya kosa kubwa ambalo limemfanya mama yangu ambaye ni Malkia wa bahari kukasirika sana.
Roda akadakia,,akauliza kwa mshangao,,”KOSA!!! KOSA GANI HILO?
Tobi akajibu,,”kunakitu ulibeba ndani ya begi lako..
Pia kuna kitu umekivaa mwilini mwako..vitu hivyo ni adui wa Malkia wa Bahari.ambaye ni mama yangu.
Roda akauliza kwa mshangao,,”mbona sikuelewi Tobi!! Inamaana wewe ni jini??? Na mbona haukuniambia miaka yote hiyo tuliyofanya kazi pamoja,,na wewe ni rafiki yangu wa karibu!!
Pia kwa nini usinge niambia tangu jana kabla sijaianza safari?
Tobi akasema sio jani..ni miaka kumi imepita..sisi kwetu huku ujinini.siku moja ni miaka kumi kwetu. Roda akashtuka sana hofu ikazidi kuongezeka akamtazama Tobi kwa macho ya uwoga…
Tobi akasimama akasema humu ndani,,hivi vitu vyote uvionavyo sio vipya kama uonavyo kwa macho yako,, wala hii siyo nyumba ya kifahari..Tobi alipomaliza kuongea maneno hayo ghafla muinekano wa ndani ya nyumba hiyo ukawa wa kutisha kupita kiasi..Punde si punde Tobi akabadilika na kuwa na muonekano kama mzee wa miaka tisini(90)
ITAENDELEA
 
Simulizi : Bahari Ya Hindi
Sehemu Ya Tatu 6
Piaa madhari ya nyumba hiyo ikabadilika na kuonekana ni ndani ya nyumba ambayo imechakaa kupita kiasi..yani kama nyumba ambayo imetelekezwa miaka mingi bila kuishi mtu ndani yake….Roda akaingiwa na hofu akatamani kupiga kelele lakini alishindwa!!
Tobi akasema..mimi ninamiaka zaidi ya mia moja(100)tangu nizaliwe..lakini ninaishi katika umbile la binadamu wa kawaida tangu miaka arobaini iliyopita…
Roda alishtuka kusikia maneno hayo aliyoyaongea Tobi.
Roda akauliza kwa mshangao!!! ,,”inamaana miaka hiyo yote tuliyokuwa tunafanya kazi pamoja ulikuwa ni jini katika umbile la binadamu?
Roda aliongea maneno hayo huku akimtazama Tobi kwa macho ya uwoga! Mapigo yake ya moyo yalipiga kwa kasi zaidi.
Tobi akajibu,,”ndiyo ni kweli kabisa hayo usemayo.
Roda akageuza shingo yake kutazama huku na kule ili atimue mbio..lakini alishindwa hakuweza kuona sehemu ya kukimbilia…kwa sababu kila kona palionekana kutisha sana. Punde si punde Tobi akanyoosha mkono wake,,ghafla muonekano wa nyumba hiyo ukabadilika..pakaonekana ni ndani ya jumba la kifahari..pia Tobi akajibafilisha na kuonekana muonekano wake wa kawaida!
Macho yakamtoka Roda! Nisu atimue mbio..
Tobi akasema..usiogope,,wala usikimbie kwa sababu hakuna sehemu ambayo utakimbilia.
Naomba unisikilize kwa makini, kuna jambo ambalo nataka nikueleze ujue..
Tobi akaanza kusimulia..
Ilikuwa hivi….Siku moja majira ya saa kumi jioni, ulikuwa na marafiki zako Coco beach..ukaingia bafuni kwenda kubadilisha mavazi…wakati unatika bafuni,,uliokota mkufu, ukauvaa mkufu huo wa dhahabu shingoni mwako,,ukaingia baharini kuogelea…mkufu huo ulikuwa ni mtego ambao Mama yangu Malkia wa Bahari aliutegesha..ili mimi niweze kurudi duniani na kuishi kama wanavyoishi binadamu wengine,,hii ni baada ya mimi kuuwawa na Binadamu aliyekuwa ni Mchungaji..
Wakati nipo kwenye mawindo yangu ya kutafuta chakula(Damu) mchungaji huyo aliniona akaniangamiza kwa maombi..nikafa na kurudi ujinini nikawa sina uwezo tena wa kurudi kuishi maisha ya Duniani..Mama yangu akatumia mkufu huo wa Dhahabu kuutegesha,,ili mtu yeyote atakayeuokota mkufu huo na kuuvaa shingoni mwake,,, mimi nitaweza kutoka ujinini na kuishi maisha ya Duniani…
Lakini wewe ulipouokota mkufu huo na kuuvaa,,nikatokea kukupenda sana,, nikalazimika kukufatilia kila sehemu unakokwenda,, nikapajua kazini kwako..nikaja kuomba kazi ili tufanye kazi pamoja na kutengeneza ukaribu zaidi…
Nimekuwa nikishirikiana nawe kimwili kila nilipokuhitaji..pasipo wewe kujua…mara nyingi nilikuwa nakutokea usiku ukiwa usingizini,,lakini wewe ulikuwa ukiamini ni ndoto…La! Hasha haikuwa ndoto, bali mambo hayo yalitendeka kweli….na nilikufunga kimiujiza ili usipendwe na mwanaume yeyote wala usimfikirie mwanaume mwingine zaidi ya mimi kuwa karibu yako kikazi.
Macho yalimtoka Roda akadakia,,”kwa nini ulinifanyia hayo yote?
Tobi akasema,,”ni kwa sababu nakupenda sana.
Roda akauliza kwa mshangao,,”UNANIPENDA!!!?
Nitawezaje kuwa na mpenzi jini?
Tobi akacheka kwa sekunde kadhaa kisha akajibu,”inawezekana na ndio maana nimekuwa na mahusiano na wewe kwa miaka mingi pasipo wewe kujua,, nilitamani ujue lakini ungeniogopa na ndio maana nikafanya iwe siri yangu.
Roda akasema,,”naomba kurudi nyumbani kwangu tafadhali..kama kweli unanipenda naomba ufanye jambo hilo..
Tobi akasema,,”hilo tu ondoa shaka lakini inabidi utimize masharti yafuatayo..
Kabla Tobi hajaanza kueleza masharti hayo..ghafla akaonekana yule Bibi kizee akiingia ndani ya jumba hilo la kifahari..
Roda akaingiwa na hofu akasema,,”tafadhali nawaomba msinidhuru..nitafanya chochote mtakachokitaka..
Bibi kizee huyo(Malkia wa Bahari) ambaye ni mama mzazi wa Tobi akaongea maneno yaliyofanan na lugha ya kiarabu akimaanisha,”hakuna atakaye kudhuru,,lakini kuna kosa kubwa ambalo umelifanya,,na siku ya leo ndiyo imgekuwa mwisho wa uhai wako..umenusurika kwa sababu wewe ni chaguo la mwanangu wa pekee..amekuchagua ili akuoe..
Roda akashtuka sana kusikia maneno hayo..pia alistaajabu ameweza kuelewa maneno aliyoyaongea bibi kizee huyo bila kujifunza lugha hiyo.
Bibi huyo akazipiga hatua na kupita kwenye mlango bila mlango huo kufunguliwa!!
ITAENDELEA
 
BAHARI YA HINDI
SEHEMU YA 7
ILIPOISHIA…
Roda akashtuka sana kusikia maneno hayo..pia alistaajabu ameweza kuelewa maneno aliyoyaongea bibi kizee huyo bila kujifunza lugha hiyo.
Bibi huyo akazipiga hatua na kupita kwenye mlango bila mlango huo kufunguliwa!!
Roda akauliza kwa mshangao! ,,” unamaanisha kunioa niwe mke wako?? Na itawezekana vipi wakati wewe si binadamu bali ni jini!
Tobi akajibu,,”inawezekana hakuna tatizo kabisa.
Roda akatumia ujanja akakubali ili Tobi asimdhuru
Lakini akilini mwake alikuwa makini sana,,huku macho yake yakimtazama Tobi muda wote..
Upande mwimgine kule nje ya bahari(nchi kavu) palionekana ni mchana wa saa saba hivi.
Lakini kule chini ya bahari (ujinini) palionekana ni usiku wa manane,,masaa ya huko ni tofauti na masaa ya duniani…hivyo wakati binadamu wamelala usiku..Majini hutumia muda huo kufanya shughuri zao za kutafuta chakula(damu)
Kwa sababa kwa masaa ya ujinini inakuwa ni nyakati za mchana..
Tobi akasema,,”nifuate,,aliongea hivyo huku akizipiga hatua kukifuata chumba kimojawapo kati ya vyumba vilivyokuwemo ndani ya jumba hilo la kifahari.
Roda akamfuata Tobi kwa nyuma hukua akionekana kuwa na wasiwasi mkubwa,,wakaingia ndani ya chumba hicho kilikuwa kinanukia marashi,,
Tobi akasema,,”Penzi la kweli halifi,,likifa haliozi,,na kama likioza harufu yake hupendeza
Roda akauliza ,,”unamaanisha nini?
Tobi akamsogelea Roda akambeba na kumlaza kitandani…
Roda alikuwa makini sana kutazama Tobi anataka kufanya nini?
Roda akauliza swali la kimitego ili ajue namna ya kutoka huko ujinini kurudi duniani.
Tobi akajibu..inawezekana lakink ni lazima kuzingatia masharti..
Roda akauliza kwa kudadisi zaidi,,”masharti gani hayo? Sasa hivi Roda aliuliza huku akitabasamu kumtega Tobi atoboe siri.
Kama ilivyo kawaida mapenzi yana nguvu kuliko kitu chochote..Tobi akajikuta anaelezea siri ambayo haitakiwi binadamu yoyote wa kawaida ajue.
Tobi akasema,,”ni lazima uvae pete maalumu..kisha akanyanyuka na kufungua droo akatoa pete iliyokuwa na jiwe la RUBI NYEKUNDU
Akasema,,”pete hii itamfanya binadamu wa kawaida atoke ujinini na kurudi Duniani ndani ya sekunde moja…naomba usiniogope sasa hivi sipo katika hali ya ujini mpaka nitakapokunywa damu ya mtoto mchanga..mimi ni yule Tobi uliyemzoea siku zote. Kwa hiyo usiku wa leo tutalala wote kama binadamu wa kawaida kabisa..tafadhali usiniogope..
Roda akamuita Tobi kitandani huku akitabasamu,,Tobi alikuja haraka,.akamkumbatia ..kisha akasema,,”tafadhali Tobi naomba tusifanye chochote usiku huu…na ninaomba uniahidi kuwa autanifanya chochote!
Tobi akakubali kwa sababu alikuwa anampenda sana Roda..wakalala usingizi bila kugusana..
Roda hakuweza kulata usingizi..akili yake yote ilikuwa inawaza juu ya pete ile aliyo onyeshwa na Tobi..
Baada ya lisaa limoja kupita…wazo likamjia Roda akamtazama Tobi akamuona kalala usingizi mzito! Roda akanyanyuka kitandani taratibu,,akazipiga hatua za kunyatia akafungua droo na kuichukua ile pete ili aivae,aweze kutoroka na kurudi Duniani. Ghafla yule bibi kizee (malkia wa bahari) akajitokeza..
Roda akaivaa pete hiyo harakaharaka..punde si punde akatoweka!! Ni kitendo cha sekunde moja akajikuta yupo ufukweni mwa bahari..akastaajabu kuona miamba mikubwa na miti mingi midago midogo!! Akapanda juu ya miamba na kuanza kutafuta njia…lakini kila akitazama huku na kule..aliona kazungukwa na miti..Roda akaanza kuingiwa na wasiwasi akajisemea moyoni,,”hapa ni wapi? Mbona hapaoneshi dalili ya mtu yeyote kuwahi kufika eneo hili!!
Sehemu hiyo palionekana kutisha sana,,zilisikika sauti za ndege warukao…na ngurumo za upepo uvumao kwa kasi..
Roda akaingiwa na hofu kubwa…
ITAENDELEA
 
BAHARI YA HINDI
SEHEMU YA 8
ILIPOISHIA…….kazungukwa na miti..Roda akaanza kuingiwa na wasiwasi akajisemea moyoni,,”hapa ni wapi? Mbona hapaoneshi dalili ya mtu yeyote kuwahi kufika eneo hili!!
Sehemu hiyo palionekana kutisha sana,,zilisikika sauti za ndege warukao…na ngurumo za upepo uvumao kwa kasi..
Roda akaingiwa na hofu kubwa…
Upande mwingine kule chini ya bahari,,alionekana Tobi akiandaa mikakati ya kwenda kumnasa Roda amrudishe kwenye himaya yake..
Yule bibi kizee (Malkia wa bahari) ambaye ni mama mzazi na Tobi..akaamua kumuamuru jini mmoja aende duniani..akalete damu ya mtoto mchanga aliyezaliwa dakika hiyohiyo ili Tobi anywe aweze kurudi katika hali ya ujini…arudi duniani kwenda kumtafuta Roda.
Upande mwingine kule Duniani lilionekana gari la wagonjwa(ambulance) likiingia ndani ya geti la Hospitali ya Muhimbili..gari hilo lilikuwa limebeba mama mjamzito..ambaye alikuwa ametimiza siku ziku ya kujifungua(kuzaa) manesi walimpokea mama hiyo harakaharaka na kumkimbiza kwenye chumba cha uzalishaji. Mama huyo alijaribu kusukuma mtoto lakini ikashindikana….alitumia nguvu nyingi sana..akaishiwa nguvu akapoteza fahamu….
Madaktari wakaamua kumpeleka haraka kwenye chumba cha upasuaji ili wamfanyie upasuaji wanusuru maisha ya mtoto… ni kitendo cha sekunde kadhaa upasuaji ukaanza.
Apunde si punde akajitokeza mwanamke mmoja aliyevalia mavazi ya kidaktari huku kafunika pua na mdomo wake kwa kifaa maalumu wanachokivaa madaktari na manesi kwa ajili ya kutokuvuta hewa chafu wakati wa ulasuaji.
Mwanamke huyo akazipiga hatua hatua kadhaa akafungua mlango wa chumba cha uoasuaji akaingia upande wa ndani…wale madaktari waliokuwemo ndani ya chumba hicho wakashtuka..wakashangaa ni nani kaingia humo wakati upasuaji unaendelea!!
Yule mwanamke hakuongea neno lolote akakifuata kitanda maalumu kwa ajili ya upasuaji..akaanza kushirikiana na madaktari hao…mwanamke huyo kumbe ni yule jini aliyetumwa akalete damu ya mtoto mchanga aliyezaliwa dakika hiyohiyo..
Mwanamke huyo akazibadilisha akili za madaktari..wakajikuta wanamkata mtoto kwenye shingo pasipo wao kujitambua..
Damu nyingi zikaanza kutoka shingoni mwa mtoto huyo mchanga hatimae akafa…yule mwanamke jini..akaitazama damu hiyo ghafla damu hiyo ikatoweka….
Punde si punde mwanamke huyo naye akatoweka kimiujiza na kurudi ujinini..
Ghafla akili za madaktari zikarudi katika hali ya kawaida…wakastaajabu kuona mtoto huyo kakatwa shingoni na ameshapoteza uhai..wakamtoa haraka tumboni na kuanza kuishona ile sehemu iliyopasuliwa ya mama wa mtoto huyo…
Madaktari walisikitika sana…tangu waanze kufanya upasuaji hawajawahi kufanya upasuaji wakamkata mtoto!!
Baada ya lisaa limoja kupita..mama huyo alipata fahamu akawa na shauku ya kutaka kumuona mwanae…akauliza,,”mtoti wangu yuko wapi??
Nesi akasema,,”pole sana dada nasikitika kukwambia kuwa mtoto kafariki wakati unafanyiwa upasuaji.
Yule mama akapata mshtuko wa moyo.. akapoteza fahamu…madaktari walijitahidi kumfanyia huduma ya kwanza lakini ilishindikana..tayari alikuwa amepoteza maisha dakika chache zilizopita..
Upande mwingine,,kule chini ya bahari ,alionekana
Tobi akinywa damu..
Damu hiyo ni ya yule mtoto mchanga aliye uwawa kule hospitali, dakika chache zilizopita.
Tobi alipomaliza kunywa damu hiyo akapata uwezo wa kurudi Duniani..akafumba macho yake akagundua ni wapi Roda alipo!!!,,akatabasamu..ghafla akatoweka kimiujiza
Wakati huo huo alionekana Roda akiendelea kutimua mbio,,alikimbia bila kujua ni wapi aendako…
Baada ya lisaa limoja kupita akatokezea kwenye barabara,,,akaanza kupata amani…akazipifa hatua za harakaharaka huku macho yake yakitazama huku na kule..
Kwa mbali akaona gari limeegeshwa!! Akaamua kulifuata gari hilo,,alipolikaribia akamuona mwanaume mmoja kafungua boneti analitengeneza gari hilo….Roda akamuongelesha mwanaume huyo…,,”habari yako kaka!!
Mwanaume huyo hakujibu kitu chochote aliendelea kulitengeneza gari lake!
Roda hakuweza kuona sura ya mwanaume huyo kwa sababu alikuwa ameinamisha uso wake…
Roda akasema,,”kaka nakusalimia…
Mwanaume huyo akageuza shingo yake,, na kumtazama Roda..
ITAENDELEA
 
Haya wadau mzigo huo tukutane kesho
 
Back
Top Bottom