Dam55
JF-Expert Member
- Oct 8, 2015
- 5,641
- 11,958
Simulizi : Bahari Ya Hindi
Sehemu Ya Kwanza (1)
Ilionekana gari moja aina ya Mark II (old model) ya kizamani,ikipaki nje ya geti la kuingilia bandarini….wakashuka watu wawili,,Mwanaume mmoja na mwanamke mmoja,,watu hao walikuwa wanafanya kazi sehemu moja,katika kituo cha Habari,,,yule mwanaume alifahamika kwa jina la TOBI na yule mwanamke anaitwa RODA….ghafla!!! ukasikika mlio mkali wa honi ya meli,,honi hiyo ikiashiria kuwa muda umekwisha,,meli inataka kung’oa nanga…wakakimbia haraka kuingia ndani ya geti…lakini Tobi alizuiliwa kuingia ndani ya meli…kwa sababu alikuwa amesahau tiketi nyumbani kwake,,hakuwa na ujanja akalazimika kubaki ili afanye mpango wa kukata tiketi katika meli nyingine…
Roda alisikitika sana,,lakini hakuwa na namna…akaingia ndani ya meli,,huku akimuacha Tobi hapo bandarini…baada ya dakika mbili kupita Meli ikang’oa nanga,, na safari ikaanza,,,wakati huo ilikuwa ni majira ya saa mbili za asubuhi,,Meli hiyo ilikuwa anatokea Mombasa kuelekea Zanzibar…Safari hiyo ya Roda na Tobi walikuwa waende Zanzibar kukusanya na kuandika habari kuhusu watawala wa kale(wakoloni)
Lakini Roda akalazimika kusafiri peke yake!!! Bila Tobi.
Meli ilizidi kuchana mawimbi na baada ya mwendo wa masaa matatu kupita..meli hiyo ikapata hitirafu,,injini zote mbili zikashindwa kuendelea kufanya kazi,,hivyo meli hiyo ikazimika na kubaki ikielea juu ya maji yenye kina kirefu sana…chenye urefu wa mita sabini kwenda chini!! Nahodha wa meli hiyo..akatangaza kwa kutumia kipaza sauti(MIC) sauti ya nahodha huyo ikasikika kwenye spika zilizokuwa zimewekwa kila kona,,, ndani ya meli hiyo!
Nahodha alisema hivi,,”Tunawaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza hivi punde!!!..hivyo muwe wavumilivu,,wakati mabaharia na mafundi wakiwa wanatengeneza meli hii….
Wakati huohuo,,wakaonekana mabaharia watano(mafundi wa meli) wakiingia kwenye milango inayotokezea kwenye chemba ya kwenda upande wa injini za meli hiyo….wakaanza kutafuta chanzo cha injini hizo kushindwa kufanya kazi!!!
Walitumia masaa mawili mfululizo kutafuta chanzo ni nini!!...punde si punde…mmoja kati ya mabaharia hao,,akagundua kuwa kuna kifaa kimepasuka inatakiwa kichomwe na kuunganishwa kwa moto wa gesi…bila kuchelewa mabaharia wengine wakaleta mtungi wa gesi haraka na kazi ikaanza..wakachoma kifaa hicho kwa kuunganisha na kile kipande kilichopasuka….waliifanya kazi hiyo kwa lisaa limoja wakawa wamemaliza……pamoja na yale masaa mawili yakawa masaa matatu yametimia.
Baharia mmoja akatoka kwenye chemba hiyo na kwenda kutoa taarifa kwa Nahodha kuwa tayari kazi imekwisha,,hivyo awashe mitambo safari iendelee…lakini yule Nahodha kila akijaribu kuwasha mitambo…haikuwaka,,, bado ilionekana kuwa kunatatizo katika upande wa injini..
Yule baharia akashuka kule chini ilipokuwepo injini kwa kupitia ule mlango wa chemba..kwenda kuwajulisha wenzake kuwa bado kunatatizo
Upande wa juu ya meli..alionekana Roda akiwa amesinzia kwenye kile kiti alichokuwa ameketi!! Akastuka kutoka usingizini…akaangaza angaza macho yake huku na kule..akaona abiria wenzake wakiwa wamesinzia!! Huku wengine wakiwa macho wazi…ukimya ulitawala ndani ya meli hiyo!!!.haikusikika hata sauti ya mtu akiongea na jirani yake!
Roda akainua mkono wake na kutazama saa aliyokuwa kaivaa mkononi mwake….akastahajabu!!! ilikuwa yapata saa kumi kasoro za jioni..akastuka akajisemea moyoni,,inamaana tangu muda ule mpaka sasa meli haijaondoka!!!? Roda akaanza kuingiwa na wasi wasi…
Kule nje,,,Upepo ulivuma kwa kasi..
Upepo huo ulisababisha maji ya bahari kutengeneza mawimbi makubwa sana..yakawa yanapiga kwenye ubavu wa meli hiyo..ikawa inayumbayumba huku ikielea.
Abiria wote waliokuwemo ndani ya Meli hiyo wakaanza kuingiwa na hofu……ukimya ukazidi kutawala
/
Roda akanyanyuka na kuzipiga hatua kuelekea chooni kujisaidia…
Akiwa anatembea,,kabla hajaufikia mlango wa choo,,kuna wimbi kubwa lililokuja kwa kasi na kupiga ubavuni mwa meli hiyo ikayumba kupita kiasi!!,, nusu Roda adondoke akawahi kushikilia kingo za korido ya meli hiyo..mkononi mwake alikuwa kashikilia kifaa kidodo chenye ukubwa sawa na simu ya kawaida!!(TAPE RECORDER) kifaa hicho kilimponyoka kutoka mkononi na kutumbukia kwenye ile chemba ya kuelekea kule chini,,zilipo inji za meli hiyo….kikadondoka chini zaidi…
Upande mwingine kule kwenye chumba cha Nahodha wa meli hiyo,Nahodha huyo alionekana kuingiwa na wasiwasi!!! Akajiuliza,,”mbona mpaka sasa hivi sijapokea taarifa yoyote kutoka kwa mabaharia(mafundi wa meli) kuna tatizo gani???
Nahodha huyo alijiuliza maswali bila kupata jibu…akaendelea kuwa mvumilivu,,kusubiri taarifa kutoka kwa mabaharia waliokuwa wakitengeneza injini za meli hiyo……
Upande mwingine alionekana Roda akijilaumu sana..akajisemea moyoni,,”siwezi kukiacha kifaa hicho(TAPE RECORDER)..ndicho kinatunza kumbukumbu ya kazi zangu za uandishi wa habari…isitoshe..kunahabari imo ndani yake na habari hiyo ni muhimu sana…
Roda akaamua kusukuma mlango wa chemba hiyo..akashuka upande wa chini kwa kutumia ngazi iliyokuwemo ndani ya chemba hiyo…alipofika upande wa chini akafanikiwa kukiona kifaa chake(TAPE RECORDER)….kabla hajakiokota akasikia vishindo vya mtu akikimbia kuja upande wake!!!
Akashtuka…..ghafla akasikia sauti ya mtu akilia kwa sauti kali,,ghafla sauti hiyo ikanyamaza….Roda akaamua kuchungulia aone nini kimetokea…..akashtuka!! macho yakamtoka baada ya kuona wale mabaharia watano wakiwa wameuwawa kikatiri huku damu nyingi zikitoka mwilini mwao!!! Roda akaingiwa na hofu kubwa..akatimua mbio kuifuata chemba ili atoke na kurudi kule upande wa juu..ghafla akahisi kaona kitu kimepita mbele yake kama upepo!!.lakini hakukitambua kuwa ni kitu gani!! Wakati anatahamaki,,,,,,ghafla akaguswa begani………
Alipogeuka hakuona mtu,,hofu ikazidi kuongezeka,,akajikuta anatamani apige kelele,,lakini akawa anaogopa,,endapo kelele hizo zitasikika,,wahusika wa meli hiyo wakija na kukuta wale mabaharia wameuwawa…basi yeye atakuwa hatiani…akaingia kwenye chemba,,ili apande ngazi atokezee uoande wa juu….akaanza kupanda gazi harakaharaka..alipokanyaga ngazi ya mwisho ili atokezee upande wa juu ghafla mlango ukajifunga!! Akashtuka akaachia mikono yake akadondoka chini na kupoteza fahamu!
Kule juu ya meli katika chumba cha Nahodha, alionekana Nahodha akizioiga hatua kuifuata chemba ya kushuka chini kule kwenye injini za meli hiyo,,,aliamua kwenda huko baada ya kuona ni masaa mawili mfululizo hajapata taarifa yoyote,,kutoka kwa mabaharia,,alipoufikia mlango wa chemba hiyo,,akastaajabu kukuta mlago huo umefungwa kwa ndani!!!,,,
Kutokana na uzoefu wa kuendesha meli hiyo miaka mingi,,alikuwa anazijua chemba zote za meli hiyo…..akaamua kuelekea kwenye chemba nyingine inayotikezea kule chini ya meli kwenye injini.
Wakati huo abiria wote waliokuwa wamepanda meli hiyo,,walionekana kuwa na hofo na wasiwasi juu ya safari yao,,walijiuliza mpaka mda huu bado wapo katikati ya bahari,,alafu hawajapata taarifa yoyote kutoka kwa wahusika wa meli hiyo,,kuhusu maendeleo ya matengenezo ya meli hiyo!
Nje ya meli,,Mawimbi makubwa ya maji yaliendelea kupiga kwenye ubacu wa meli hiyo..na kusabavisha mtikisiko mkubwa na meli hiyo kuyumbayumba kila wakati!! Masaa yalizidi kusonga na giza likaanda kutanda kuizunguka bahari…
itaendelea