Elton Tonny
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 396
- 2,976
- Thread starter
-
- #241
DRAXTON
A Story by Elton Tonny
Familia, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Siri, Tamaa, Hila, Unyanyasaji, Usaliti, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa
(R-rated 18+)
Enjoy!
★★★★★★★★★★★★★★
SEHEMU YA KUMI
★★★★★★★★★★★★★★
Mark na Darla wakamsaidia Draxton kunyanyuka, naye akasimama kabisa na kujitahidi kujipa utulivu zaidi. Alihisi nguvu fulani mpya mwilini, iliyozidi kuongezeka tu, na maumivu yoyote yaliyokuwa yamebaki yakawa yametoweka kabisa.
"You good? Do you need anything? Water? (Uko vizuri? Unahitaji chochote? Maji?)" Darla akamuuliza kwa kujali.
"I'm fine. Thanks (Niko sawa. Asante)," Draxton akasema.
"You've done this in less than an hour. You really are strong (Umefanikiwa kufanya jambo hili chini ya saa. Wewe kweli una nguvu sana)," Mark akamwambia Draxton.
"Was it supposed to take longer? (Ilitakiwa ichukue muda mrefu zaidi?)" Draxton akauliza.
"Yeah, and with a lot of trouble. Father used to say that for those who don't.... (Ndiyo, na kungekuwa na usumbufu mwingi. Baba alikuwa akisema kwamba kwa wale ambao hawawezi....)"
Maneno hayo ya Mark yakakatishwa baada ya wote kusikia sauti ya kengele mlangoni kutokea kule juu, na wote wakaangaliana.
"You expecting someone? (Kuna mgeni unayetegemea aje?)" Darla akamuuliza Mark.
"Not really... no (Siyo kabisa... hakuna)," Mark akajibu.
"Well it shouldn't be Ed or Gia cause they are far dead in their sleep (Haiwezi kuwa Ed ama Gia maana wamesinzia kama vile wamekufa)," Darla akasema.
"It could be a neighbor. Let me check (Inaweza ikawa jirani. Wacha nikaangalie)," Mark akasema.
Akawaacha wawili hao ndani hapo na kwenda kuangalia mgeni aliyefika alikuwa nani.
Darla akamsogelea Draxton zaidi na kusema, "I can't imagine the ordeals you've had to experience in your life. You must feel heavily burdened... and tired (Siwezi kupigia picha ni mitihani ipi imekupasa uipitie maishani mwako. Ni lazima uhisi kulemewa na mzigo mzito... na kuchoka pia)."
Draxton akatazama chini na kusema, "You are right. When you live as long as I have, you get... (Uko sahihi. Ukiishi kwa muda mrefu kama mimi nilivyoishi, unapatwa na...)"
Akaishia hapo kuzungumza baada ya kuingiwa na jambo fulani kwenye hisi zake za kusikia. Aliweza kutambua sasa mgeni aliyefika huko nje ambaye Mark alienda kuangalia ni nani, na hakuwa mwingine ila Aysel. Alimsikia Mark akimuuliza kwa nini amekuja hapo, Aysel akimjibu kwamba aliwa-miss, Mark akijaribu kumwambia kwamba aondoke kabla hajaonwa na mtu asiyetakiwa kumwona, na ikaonekana kwamba mwanamke huyo aliingia ndani kwa lazima baada ya kusema hana mahala pengine pa kwenda kwa sababu hana sehemu ya kukaa, na kilichomleta haikuwa kumwona yeye Mark ila Draxton.
Darla aliona umakini wa Draxton umehama kutoka kwenye mazungumzo yao, naye alipofungua hisi zake vizuri zaidi akatambua kwamba Aysel alikuwa ameingia ndani. Akahisi hasira na kuonyesha kutaka kumpita Draxton ili aende kushughulika na mwanamke yule yeye mwenyewe, lakini Draxton akaushika mkono wake kumzuia.
Darla akamwangalia usoni na kusema, "Let go, we got an intruder (Niachie, tumevamiwa)."
"Calm down, Darla... (Tuliza hisia, Darla...)"
"She's not supposed to be here! At least not now. What if Gianna wakes up and catches her scent in here? (Hatakiwi kuwa hapa! Angalau si kwa sasa. Vipi Gianna akiamka na kuikamata harufu yake ndani humu?)"
"Why? What will happen? What did she do to you? (Kwa nini? Nini kitatokea? Kwani aliwafanyaje?)" Draxton akauliza.
Darla akashusha pumzi na kutikisa kichwa, naye akasema, "I'll tell you everything at the right moment. Just... please come up and help me get rid of her (Nitakwambia kila kitu kwa wakati sahihi. Ila... tafadhali njoo nami unisaidie kumwondoa)."
Kisha mwanamke huyo akajitoa mkononi kwa Draxton na kutangulia kuondoka, akimwacha mwanaume anawaza ni shida gani iliyokuwepo kuwafanya watu hawa wamchukie Aysel. Lakini Aysel mwenyewe alionekana kuwa mkaidi kwelikweli, kwa hiyo bila shaka jambo alilowafanyia lazima lilikuwa zito.
Draxton akafuata nyayo za Darla na kwenda mpaka sebuleni na kuwakuta watatu hao wakiwa wamesimama usawa wa mlango. Darla sasa alionekana kuwa amempita Mark na kusimama mbele zaidi kutokea pale Aysel aliposimama, akimwangalia kiukali, na Aysel akimtazama kibabe. Mark alipomwona Draxton, akasogea nyuma kidogo akionekana kuishiwa pozi.
"I will only say this once. Get... out (Nitasema jambo hili mara moja tu. Toka... nje)," Darla akamwambia Aysel.
Aysel akamwangalia Draxton, akiona nywele zake nyeupe zilizompa mwonekano tofauti sasa, naye akasema, "Alpha Draxton, I came to see you. I really need your help, I'm regressing fast to be a feral, if you can please just... (Alpha Draxton, nimekuja kukuona. Ninahitaji sana msaada wako, ninashuka hadhi upesi mno kuwa feral, ikiwa tu unaweza tafadhali kuni...)"
"I told you I'd call you (Nilikwambia nitakuita)," Mark akamkatisha Aysel.
"When? How would you know where to find me? (Wakati gani? Utajua vipi pa kunipata?)" Aysel akamuuliza.
"I have my ways (Nina njia zangu)," Mark akasema kwa ukali kiasi.
"Didn't you hear what I said? (Hujasikia nilichokwambia?)" Darla akamsemesha Aysel.
"No one's talking to you (Hakuna mtu anayeongea na wewe)," Aysel akamwambia.
"What'd you say?! (Umesemaje?!)" Darla akauliza kwa ukali.
Akataka kumfata kwa shari lakini Mark akamzuia kwa kumshika mkono.
"That's enough (Inatosha)," Draxton akasema kwa utulivu.
Darla bado alikuwa na hasira ya kutaka kumrukia Aysel, lakini mwanamke huyo akatoka sehemu aliyokuwa amesimama na kumfata Draxton.
"Alpha... I really need you. Please... take me. I'll give you anything (Alpha... nakuhitaji sana. Tafadhali... nichukue. Nitakupa chochote kile)," Aysel akamwambia Draxton kwa kusihi.
Draxton akabaki kumtazama mwanamke huyo kwa umakini.
Darla akajitoa mkononi kwa Mark na upesi kwenda mpaka hapo aliposimama Aysel, naye akamsukuma kwa nguvu huku akisema, "F(...) off! He's mine! (Toka hapa! Yeye ni wangu!)"
Draxton akamshika Darla kiunoni kwa nguvu kiasi kumzuia asiendeleze fujo.
Aysel akajisawazisha vizuri kutokea pale alipokuwa ameangukia baada ya kusukumwa, kisha akasimama na kusema, "I don’t want him as a mate, just to keep my sanity. Why are you so clingy? (Simhitaji awe mwenzi wangu, ni ili tu niendelee kuuweka ufahamu wangu vizuri. Mbona unakuwa mwenye kumganda sana?)"
“I’m not even bonded to him yet. Wait for your turn bitch (Bado hata sijaunganika pamoja naye. Subiri zamu yako malaya wewe)," Darla akamwambia.
Mark akasogea mpaka hapo na kusema, "Aysel please... try to understand. What you're worried about is also happening to my sister, and you better than anyone know that she has every right to act this way. Draxton has already promised you to be part of his pack, trust that, and wait. Please go (Aysel tafadhali... jaribu kuwa mwelewa. Unachohofia ni kitu ambacho kinampata dada yangu pia, na wewe zaidi ya mtu yeyote unajua kabisa kwamba ana kila haki ya kutenda jinsi hii. Draxton ameshakuahidi kuwa sehemu ya kundi lake, amini hilo, na usubiri. Tafadhali nenda)."
Darla alikuwa ameanza kutokwa na machozi, na jambo hilo likamtatiza sana Draxton. Aysel akamwangalia Draxton kwa njia ya msisitizo, lakini Draxton akamwonyesha kwa ishara ya kichwa kuwa aondoke. Aysel akaanza kuelekea mlangoni, na alipoufikia akageuka kuwaangalia wote kwa ufupi, kisha akaondoka. Draxton akamgeuza Darla ili watazamane, na mwanamke huyo akawa anajifuta machozi huku akijikaza kisabuni.
"Darla... tell me why you are like this (Darla... niambie kwa nini uko namna hii)," Draxton akamsemesha kwa upole.
"I will, just... not now. I need to get some rest. You two should do the same. We'll get together later, okay? (Nitakwambia, ila... si sasa. Ninahitaji kupumzika kidogo. Nyie wawili mpumzike pia. Tutakutana baadaye, sawa?)" Darla akamwambia Draxton.
Mwanamke huyo akaondoka tu kutoka hapo upesi, akiwaacha wanaume wanamwangalia mpaka alipotoka ndani ya nyumba kabisa.
Draxton akamwangalia Mark na kuuliza, "It is not gonna be easy for me to be a leader, will it? (Haitakuwa rahisi kwangu kuwa kiongozi, sivyo?)"
Mark akatazama pembeni kwa ufupi, kisha akasema, "It never is. But I believe in you. I know you will be the best leader we could never get (Haiwi rahisi sikuzote. Lakini nina imani ndani yako wewe. Ninajua utakuwa kiongozi bora zaidi ambaye hatujawahi kupata)."
"Why didn't you just take your brother's place? You are a child of an Alpha (Kwa nini haukuchukua sehemu ya kaka yako? Wewe ni mtoto wa Alpha)," Draxton akamuuliza.
"I could never even if I tried. I'm not a firstborn, so the wolf spirit would not bestow leadership upon me. After the other Alphas and their firstborns were murdered, there were few of us who tried to gain that privilege but failed. The evil leader did not want to sire a child so he could be the only one Alpha left, and now, that's gonna change (Nisingefanikiwa hata kama ningejaribu. Mimi si mzaliwa wa kwanza, kwa hiyo roho ya u-mwitu isingeniwekea uongozi juu yangu. Baada ya ma-Alpha wengine na wazawa wao wa kwanza kuuliwa, kulikuwa na wachache waliojaribu kuupata wadhifa huo na kushindwa. Kiongozi wetu mwovu hakutaka kuzalisha mtoto ili abaki kuwa Alpha pekee, na sasa, hilo litabadilika)," Mark akasema.
"Aysel is desperate for help. Won't she go back to him and tell him about me? Wouldn't that put you guys in danger? (Aysel anataka sana msaada. Vipi akirudi kwake na kumwambia kunihusu? Hilo si litawaweka nyie hatarini?)"
"She won't. You made sure of that last night that's why she was here now. Even if she did, we already have you, and in just a matter of time you will be able to protect all of us from him (Hatafanya hivyo. Ulihakikisha jambo hilo usiku uliopita na ndiyo sababu amerudi hapa tena. Hata kama angemwambia, sisi tuna wewe tayari, na ndani ya muda mfupi tu utaweza kutulinda sote dhidi yake)," Mark akasema.
"What's his name? (Jina la huyo mwanaume ni nani?)" Draxton akauliza.
"Robert. Robert King," Mark akamjibu.
Sasa Draxton akawa amelijua jina la mhasimu wake aliyewasumbua watu-mwitu wenzake kwa kipindi kirefu, na kilichokuwepo ni kuja kukutana naye ili amalize matatizo aliyosababishia wengi wa watu wake. Mark akasimama kwa njia fulani kama anajiandaa kufanya kitu, kisha akaweka mkono wake kifuani akiwa amekunja ngumi na kupiga goti moja chini, kwa njia ile ile ya heshima kama alivyofanya mara ya kwanza wamekutana Tanzania.
Draxton akamwangalia kwa umakini na kumuuliza, "What are you doing? (Unafanya nini?)"
Mark akasema, "Now that you are fully connected with your wolf spirit, I will pledge my loyalty to you Draxton. I'll officially be the first member of your pack (Sasa kwa kuwa umeunganika kikamili na roho yako ya u-mwitu, nitatoa rehani ya uaminifu wangu kwako Draxton. Nitakuwa mtu-mwitu wa kwanza rasmi ndani ya kundi lako)."
Draxton akaendelea kumwangalia kwa utulivu, naye Mark akafumba macho yake na kuyafumbua tena, sasa yakiwa yenye mng'ao wa rangi ya njano kwenye lenzi.
Mark akasema, "I fully submit myself to you. I pledge my loyalty and my life in the bond of your pack, Alpha Draxton (Ninajitoa kwako kikamili. Ninaweka rehani ya uaminifu na maisha yangu ndani ya muunganiko wa kundi lako, Alpha Draxton)."
Baada tu ya Mark kusema maneno hayo, Draxton akahisi kitu fulani kikipanda ndani ya mwili wake na kumpa kama nguvu mpya, na macho yake yakawa ya blue kwa sekunde chache, kisha yakarudia hali ya kawaida. Akaelewa kwamba hiki ndiyo kitu ambacho Mark sikuzote alizungumzia kuhusu uchochezi au uvutano ambao Alpha alikuwa nao kwa watu-mwitu wake, na sasa hivi uchochezi wake Draxton ukawa ndani ya Mark baada ya mwanaume huyo kujikabidhi kwenye muungano wake.
Mambo yalikuwa ni mengi, lakini ndiyo kwanza ulikuwa mwanzo tu. Mark sasa akarejesha hali ya kawaida baada ya kuhalalisha uaminifu wake kwa Draxton, naye akatabasamu kwa kujivunia. Draxton akatabasamu kidogo pia na kutikisa kichwa kuonyesha shukrani kwa mwanaume huyo kumwamini mpaka kufikia hatua hiyo, na sasa ambacho kilibaki ilikuwa kuwaunganisha wengine pia kwenye kundi lake baada ya yeye kuungana kikamili na mnyama aliyekuwa ndani yake.
★★★★★
TANZANIA
Siku hii, Namouih aliamka mapema na kupata kiamsha kinywa nyumbani hapo kwa Salome, na alikuta mwanamama huyo akiwa ameshaondoka kwa ajili ya kazi. Yeye Namouih alikuwa na mpango wa kuchukua likizo nje ya kazi kwa mwaka mzima baada ya matukio yote yaliyompata kutokea, hivyo hakuhitaji kushughulika na kazi yoyote kwa siku hii na alipanga kwenda baadaye kuonana na Mr Edward Thomas kufikisha ombi lake. Kwa vyovyote vile ambavyo mambo yangekuwa, aliihitaji sana likizo hii ili mwili na akili yake viweze kutulia vya kutosha mpaka kufikia wakati wa kujifungua, na pesa yake ya akiba ilitosha kabisa kumsukuma kwa muda wote huo ambao angekuwa nje kikazi.
Baada ya kuhakikisha Sasha anaendelea vizuri, Namouih akajaribu kumtafuta Draxton mara kadhaa kwa simu, lakini hakujibiwa. Akaona amwache na kwenda kuzungumza na Zakia kuhusu ujio wa Halima jijini. Makadirio ya kufika kwake ingekuwa kwenye mida ya saa kumi na mbili mpaka saa moja jioni, hivyo Namouih akamwambia mama yake kwamba wangekwenda kumpokea pamoja na kumpeleka hotelini kwa ajili ya mapumziko. Akaweka wazi dhumuni la Halima kuja huku, akisema alimhitaji Zakia awepo katika mazungumzo yao hasa kwa kuwa yeye ndiye aliyekuwa shuhuda halisi wa visa vyote vilivyotokea mpaka Efraim Donald akauawa.
Mama yake Namouih hakuwa na kipingamizi kwa jambo hilo, naye akamwambia bintiye angekuwa tayari kufikia muda huo kwenda pamoja naye.
★★
Namouih alikwenda mchana kuonana na boss wake kwenye kampuni ile ambayo alifanyia kazi kupeleka ombi lake la kutaka likizo. Mr. Edward Thomas alishangazwa na jambo hilo, naye akauliza kwa sababu ipi Namouih alidhani angepewa tu likizo hiyo wakati yeye ndiye aliyekuwa mwanasheria mkuu katika kampuni hiyo. Tayari Namouih alikosa kesi kadhaa kwa wiki chache zilizopita na kulikuwa na hasara fulani zilizokuwa zimeanza kujitokeza hasa baada ya mwanasheria wake msaidizi kuacha kazi ghafla, kwa hiyo boss akasema kutoa likizo kwa mwaka mzima ni suala ambalo halingeona uafiki.
Namouih akaweka wazi kwamba alikuwa mjamzito, na pia alipima kule hospitalini na kuambiwa kwamba alihitaji muda mrefu sana wa kupumzika ndiyo sababu alifikia uamuzi huu, lakini bado Mr. Edward akagoma kumhidhinishia likizo hiyo. Kwa kuona kwamba boss wake hakutaka kumkubalia, Namouih akatoa pendekezo lingine; aache kazi.
Mr. Edward Thomas alimshangaa, akisema hakuelewa ni nini kilichokuwa kimemwingia mwanamke huyo mpaka kuchukua maamuzi bila kufikiri kwa kina, lakini Namouih akasema tayari alikuwa ameshafikiria kila Jambo kwa kina. Alimwambia kumweka mtu mwingine awe mwanasheria mkuu badala yake katika kipindi cha likizo yake lisingekuwa jambo gumu, lakini kama aliona hawezi kabisa kumpa likizo, basi angeacha kazi hapo.
Kwa kuhofia kumpoteza kabisa mwanasheria wake aliyeifanisisha zaidi kampuni yake na kupata wateja wengi kutoka sehemu za juu serikalini, Mr. Edward akaona amkubalie. Akampa likizo ya mwaka mmoja, lakini kwa sharti kwamba ndani ya huu mwezi mmoja Namouih alipaswa kuendelea na kazi kwa sababu kuna kesi kadhaa zilipaswa kumalizwa na yeye ndiye aliyekuwa tegemeo, na baada ya hapo ndiyo angekwenda kupumzika. Namouih akaona hilo halingekuwa jambo baya, naye akakubali na kumshukuru mkubwa wake kwa kumtendea wema.
Wakati alipoaga ili aondoke, Mr. Edward akamuuliza ikiwa taarifa zozote mpya kumhusu Efraim Donald zilikuwa zimeletwa, lakini Namouih akakataa, akisema bado hakuwa amesikia chochote kile, naye akaondoka hapo.
★★
Basi, muda ukasonga kama kawaida mpaka jioni ikaingia. Namouih na Zakia walifika stendi kuu ya mabasi na kusubiri lile ambalo Halima alikuwa amepanda lifike. Namouih alikuwa amejaribu kwa mara nyingine tena kumtafuta mpenziwe aliyekuwa Marekani, lakini kwa sababu asizofahamu bado akawa hajibiwi.
Zakia alikuwa anamtia moyo binti yake, akisema Halima alikuwa mwanamke mwelewa na hata kama taarifa ambazo wangempa zingemuumiza sana, bila shaka angekubaliana naye kwamba kila jambo lililotokea halikuwa makosa ya Namouih, bali mwana wake mwenyewe. Namouih akaendelea kuzituliza hisia zake mpaka pale mama wa aliyekuwa mumewe alipofika hatimaye.
Haikuwa kukutanika kwa shangwe kama ilivyokuwa zamani, ingawa Zakia alijitahidi kumwonyesha Halima shauku kiasi baada ya kuonana kwa mara nyingine. Halima alionekana kuwa makini, na hata waliposaoimiana na Namouih, mtu angedhani ndiyo walikuwa wamekutana kwa mara ya kwanza na ndiyo wakatambulishwa. Kulikuwa na hali ya umbali baina yao hata walipoingia ndani ya gari lake Namouih na kuanza kuelekea jijini zaidi, ikiwa ni Zakia sanasana ndiye aliyekuwa akiongea zaidi na mwanamama huyo.
Namouih akaendelea kuendesha gari na ukimya wake mpaka walipoifikia hoteli aliyokusudia kumchukulia Halima chumba. Ilikuwa ni kwenye hoteli ile ile ambayo Namouih alikaa mwanzoni kabla ya kuhamia pale kwa Draxton, na baada ya kupata chumba kizuri, wakaingia humo na Halima kuingia kuoga kwanza.
Namouih akamwambia mama yake kwamba anatoka kwenda kuandaa sehemu nzuri ya kupata chakula hapo hapo hotelini, lakini Zakia akamshauri abaki kwanza. Alielewa binti yake alikuwa na wasiwasi, naye akamtuliza tu na kumwambia wamsubiri Halima amalize kujiweka sawa kisha mengine yafuate.
Kilikuwa ni chumba chenye upande wa sebule na sehemu ya kulala kwa upande mwingine, ambao ndiyo ulikuwa na bafu, hivyo wawili hawa walimsubiri Halima sebuleni mpaka alipokuja tena akiwa ameshajimwagia na kubadili mavazi.
"Angalau sasa hivi mwili uko fresh, eti? Maana kuna joto huku..." Zakia akamsemesha Halima kirafiki.
Halima, akiwa anaketi kwenye sofa moja, akasema, "Ndiyo, angalau. Me mwenyewe napenda kweli maji yaani kidogo tu nakuwa nataka kuoga kama bata."
Zakia akacheka kidogo na kusema, "Sisi kwa uchafu ndiyo tunaongoza kwa hiyo usafi muda wote inakuwa lazima."
"Ni kweli," Halima akasema hivyo, kisha akamtazama Namouih.
Namouih akamwambia, "Nilikuwa nakusubiri umalize... twende tukapate chakula kwanza halafu..."
"Binti yangu, haina haja. Sihisi njaa. Mimi nataka tu tuongee," Halima akamwambia kwa upole.
Zakia akamtazama Namouih kwa kujali.
"Ni mambo gani yanaendelea huku? Inaenda wiki ya tatu sasa sijampata Efraim, kuna watu mpaka wananitafuta wanamuulizia, na wewe unasema hujui... halafu mara sijui nasikia mmetalikiana... naomba unielezee jamani... mimi... sina amani..." Halima akazungumza kwa hisia.
Namouih akaanza kulengwa na machozi, hata pumzi zake zikaanza kutetemeka na kushindwa kutoa jibu lililonyooka.
Halima alipoona hilo, akauliza, "Shida ni nini? Eh? Mama Nam... mbona sielewi?"
Zakia akamtazama Namouih na kumwambia, "Jikaze mama... unahitaji umwambie ukweli."
Namouih akajifuta machozi upesi na kushusha pumzi ndefu.
"Ni mambo mazito dada yangu. Ni vitu ambavyo nikikumbukia nakuwa nashindwa hata kujua ikiwa inawezekana kuelezea... na hata kwa Namouih inakuwa ngumu zaidi maana yaliyotokea siyo mazuri," Zakia akasema.
"Nini kimetokea mama'angu? Niambie," Halima akamsemesha Namouih kiupole.
Namouih akatulia zaidi na kusema, "Efraim hakuwa mtu niliyedhani alikuwa mama. Ali... hhh... alinioa kwa misingi ya kishirikina ili apate mali nyingi zaidi."
Halima hakuonekana kushtuka kusikia kauli hiyo, lakini akauliza kwa utulivu, "Unamaanisha nini?"
"Alinioa kimasharti. Sijui kama ni ya waganga au vitu gani, lakini yalihusisha mambo mengi mabaya sana mama. Alikuwa anaua... wasichana wadogo... akiwatoa kama kafara kila mwezi... na mimi... nilikuwa kwenye hilo sharti alilopewa kwamba... anioe tu na kunitunza bila kunipa haki yangu ya ndoa mpaka amalize kutoa kafara zote alizotakiwa... kutoa..." Namouih akaongea huku midomo yake ikitetemeka kiasi.
Halima kiukweli alishangazwa na jambo hilo, lakini hakushangazwa na ukweli wenyewe. Tayari alikuwa anafahamu kwamba mwana wake alijiingiza katika masuala ya namna hiyo ili kutajirika ingawa hakuwahi kumuuliza wala kujua alitumia njia zipi, kwa hiyo kuelewa sasa kwamba mambo hayo yalihusisha vifo na maumivu kwa wengi kulimvunja sana moyo, naye akaangalia chini kwa huzuni.
"Nayokwambia yote ni kweli mama... hhh... Efraim alikuwa na roho ya kikatili... alimuua baba yangu, alimuua rafiki yangu, akalala na mdogo wangu, halafu akapanga kumuua na yeye pia kwa ajili ya hizo kafara... alikuwa ameniweka mimi ndani kama hirizi yake ya bahati katika kujizolea mali za kudumu kutoka kuzimu mama... yaani sikuamini kabisa kama alikuwa wa namna hiyo!" Namouih akaongea huku akitokwa machozi.
Halima akamwangalia, machozi yakianza kumlenga pia, naye akawa anatikisa kichwa kwa kusikitika.
"Ni kweli Halima, ni kweli kabisa. Nitaendelea kubeba majuto mengi mno moyoni mwangu kwa sababu ya ujinga mwingi nilioufanya maishani. Na moja kati ya majutio makubwa ni kumruhusu mwanao aniingie kimwili pia..." Zakia akasema.
Halima akamwangalia kimshangao.
"Ndiyo dada. Efraim alilala nami. Baada ya kutimiza haja yake akaniambia mipango yake pia na ndiyo kuanzia hapo nilijua hakuwa mtu niliyemdhania kabisa... sikudanganyi... najutia sana... sana," Zakia akaongea huku akilia.
Halima akafumba macho yake na kushusha pumzi kiutetemeshi, kisha akajikaza na kumwangalia Namouih tena kwa uimara, naye akauliza, "Kwa hiyo Efraim yuko wapi?"
Zakia akamtazama Namouih, na binti yake akaangalia chini.
"Niambieni aliko. Mmeshatalikiana, si ndiyo? Kama... mmemfichua maovu yake, sawa, nimekubali, lakini nataka kujua yuko wapi... hicho tu," Halima akasema.
Bado ikawa ngumu kutoa jibu.
"Mmemfunga au?" Halima akauliza.
"Efraim amekufa mama..." Namouih akamwambia moja kwa moja.
Halima akabaki kumtazama kana kwamba hajamsikia.
"Amekufa," Namouih akasema kiuhakika.
Halima akaanza kububujikwa na machozi mengi, na bila kutoa sauti yoyote ya kilio akainamisha tu kichwa chake na kuuegamiza uso kwenye viganja vyake. Mwili wake ulitikisika taratibu, ikionyesha dhahiri kwamba alikuwa analia, lakini hakutoa sauti. Namouih akawa analia pia bila kutoa sauti, na Zakia akamsogelea Halima na kuketi pamoja naye kumpa faraja kwa ukaribu.
Ingawa ni kweli Efraim Donald alkuwa mbaya, bado alikuwa ni mwanaye, na kifo chake kingemuumiza sana kwa maumivu yale yale kama aliyopitia wakati akimzaa. Aliendelea kulia ndani hapo kwa dakika nyingi huku Zakia akimfariji, na Namouih alikuwa pembeni tu mpaka alipotulia kiasi. Kisha akamuuliza Namouih ilikuwaje mpaka Efraim akafa.
Namouih akaelezea kwa kina namna ambavyo siri za Efraim Donald zilivuja kutokana na kikwazo cha kutompa mwanamke huyo haki yake ya ndoa. Alieleza jinsi alivyokuwa anampenda Efraim toka alipojitokeza kumsaidia baba yake, na alitaka kumwonyesha upendo huo kwa matendo kama tu mwanamke anavyotakiwa kufanya pia lakini ndiyo sharti la mumewe likasababisha amnyime kwa muda mrefu sana mpaka akatumbukia kwenye penzi la mwanaume mwingine. Kutoka kwake ndani ya ndoa hiyo ndiyo kulisababisha Efraim Donald afichuliwe, naye akaeleza kwamba ni mwanaume aliyekuwa akitoka naye ndiye aliyemuua Efraim baada ya mumewe kuwateka yeye, Zakia na Sasha, na hata kujaribu kumuua Sasha kikatili sana.
Halima aliumia sana. Alijihisi vibaya mno kwamba mambo yote hayo mabaya yalimhusu mwanaye pekee aliyekuwa amebaki kuwa nguzo kuu ya maisha yake, na sasa hakuwepo tena kwa sababu ya kujiingiza kwenye mambo yasiyofaa kabisa. Na alikuwa amemwonya. Alimwonya mapema kwamba kujiingiza kwenye masuala ya kishetani kungemwathiri vibaya, na sasa matokeo yakawa wazi. Sasa Halima akawa ameachwa bila mtoto hata mmoja, wote watatu aliozaa wakiwa marehemu. Iliuma sana.
Namouih akamsogelea Halima na kupiga magoti chini karibu kabisa na miguu ya mama huyo, naye akamshika mikononi na kumwomba samahani kutokana na kuwa chanzo cha kati kwenye matatizo yaliyotokea. Akamwambia kwamba angeendelea kumwona kuwa mama yake haijalishi nini kilikuwa kimetokea, na kumwomba asimchukie kwa sababu ya kilichompata Efraim.
Halima alimtazama sana Namouih, akiwa ametafakari suala zima kwa kina na kulielewa vizuri kabisa, naye akamkumbatia kwa upendo. Namouih alifarijika mno kupata jibu lake kwamba mwanamke huyo hakumchukia. Alilia kwa faraja aliyohisi moyoni, naye akarudisha kumbatio lake kwa hisia. Zakia alikuwa akitokwa na machozi pia, naye akajiunga kukumbatiana pamoja nao kwa furaha.
Ahueni Namouih aliyohisi moyoni baada ya kumaliza mambo haya upande wa mama-mkwe wake kwa njia nzuri ilimsaidia kuona vitu kwa njia chanya zaidi, naye angekuwa tayari kushughulika na kila kitu ambacho Halima angehitaji kutokea hapo ili wakivuke kipindi hiki wakiwa pamoja kwa umoja na uimara.
★★★★★
MAREKANI
Masaa kadhaa yakapita kutokea wakati ambao Mark alijitoa rasmi kuwa mwaminifu kwa Draxton. Wanaume hawa waliingia kujipumzisha, yaani kulala, kwa sababu walikuwa wamepitisha masaa mengi bila kufurahia usingizi na ndiyo wakajipa nafasi hiyo baada ya kumaliza kumsaidia Draxton kujiunganisha na upande wake wa kiroho.
Draxton alilala kwa muda mrefu sana. Alikuwa akiamka mara kwa mara na kurudi usingizini tena mpaka ilipofikia mida ya saa kumi na mbili jioni, ikiwa kama alipitia ugonjwa fulani mbaya. Ilikuwa ni uchovu tu, na hata baada ya kuamka muda huo akaendelea kujilaza kitandani mpaka kufikia saa moja, akiwa amejipa muda wa kutafakari kwa kina kuhusu suala la kutakiwa kumwachilia Namouih katika muungano wake wa kiroho.
Alikuwa anahofia labda jambo hilo lingekuja kusababisha amsahau mpenzi wake kabisa, na ni kitu ambacho hakutaka, kwa hiyo angefanya yote awezayo ili kisitokee. Ulikuwa umepita muda fulani hajamtafuta Namouih kutokana na mambo kuwa mengi, hivyo akajinyanyua na kwenda kuchukua simu yake ili afanye jambo hilo.
Alipoifungua, akakuta kwamba Namouih alikuwa amemtafuta mara nne jana usiku, na leo asubuhi pia, naye akatikisa kichwa kwa kusikitika kutokana na kushindwa kuijali simu kwa masaa mengi. Alipopiga hesabu ya haraka kichwani alielewa kwamba kwa muda huu, Tanzania ingekuwa aidha saa nane au saa tisa usiku, hivyo bila shaka Namouih angekuwa amepumzika.
Lakini akaamua kumtumia video ya kujirekodi, akimwambia kwamba amemkosa sana, na wanapishana mno kutokana na mambo mengi ya huku kuingiliana na ratiba ya muda anaotakiwa kumtafuta kila siku, ila akamhakikishia kuwa anampenda mno na atajitahidi kuwahi kuyamaliza mambo yote ili arudi kwake haraka.
Baada ya kumtumia video hiyo, akaingia bafuni kujiweka katika hali ya usafi, kisha akavaa T-shirt nyeusi na bukta nyepesi, naye akaelekea sebuleni. Nywele zake nyeupe alizibana kwa nyuma kama mkia, na alipofika hapo akamwona Mark sehemu ya jikoni akiwa anatengeneza nyama kama kawaida. Mark alipomwona pia, akamwonyesha ishara ile ya heshima kwa kuweka ngumi kifuani kwake, naye Draxton akamtikisia kichwa mara moja kama kumpa salamu ya mbali na kisha akakaa kwenye sofa.
Baada ya dakika chache, Mark akafika hapo alipoketi Draxton akiwa na sahani yenye nyama nyingi zilizotengenezwa vizuri, naye Draxton akamtazama usoni.
"Did you wake up long? (Umeamka zamani?)" Mark akamuuliza.
"Like an hour ago. You? (Kama saa moja lililopita. Wewe je?)" Draxton akauliza.
"Three hours back. I slept like a baby, and then went to fetch this steak. It even rained a little (Masaa matatu nyuma. Nililala kama mtoto, na ndiyo nikaenda kuifata hii nyama. Mvua imenyesha kidogo pia)," Mark akamwambia.
Draxton akatikisa kichwa kuonyesha uelewa.
"How do you feel now? (Unajihisi vipi sasa?)" Mark akauliza.
"Normal, and too good to be true (Kawaida, na vizuri mno kiasi cha kunipotosha)," Draxton akajibu.
Mark akatabasamu na kusema, "I'm glad. In a few, Darla is gonna come and help you with the change. She serves as your better half and will make sure everything goes according (Nafurahi. Ndani ya muda mfupi, Darla atakuja na kukusaidia kwa badiliko lako. Anatumika kama kikamilisho chako na atahakikisha kila jambo linakwenda kwa namna linavyotakiwa)."
Draxton akatikisa kichwa kukubali, na wote wakaanza kula.
"It feels wonderful sharing a meal with you. It was something I never thought would see the light (Inanipa hisia nzuri sana kushiriki mlo pamoja nawe. Ni kitu ambacho sikuwahi kufikiri kingekuja tokea)," Mark akamwambia.
Draxton akamwangalia na kusema, "You don't need to be formal with me Mark. I'm still Draxton. And you are a friend to me, so just be yourself and treat me like a normal person (Hauhitaji kutenda kwa njia ya ugeni kwangu Mark. Mimi bado ni Draxton. Na wewe ni rafiki kwangu, hivyo kuwa tu namna ulivyo na unitendee kama mtu wa kawaida)."
"Oh no, I wouldn't dare. You are very special, in ways yet unseen to yourself, and you deserve all the respect you are going to get (Oh hapana, siwezi thubutu. Wewe ni wa pekee sana, katika njia ambazo bado hujazitambua, na unastahili heshima yote utakayotakiwa kuipata)," Mark akasema.
Draxton akatabasamu kidogo, naye akaendelea kula pamoja na mwanaume huyo.
"I really can't wait for the time you'll start kicking ass! (Yaani siwezi kusubiri utakapofika muda uanze kutandika watu!)" Mark akaongea kwa shauku.
Draxton akatabasamu, akiwa ameelewa hilo lililoongelewa lilimaanisha kuwaangusha wabaya wao, naye akamuuliza, "Is everything okay with you? (Kila kitu kiko sawa kwako wewe?)"
Mark akasema, "Yeah. I'm good (Ndiyo. Niko poa)."
"How's Nina doing? (Nina anaendelea vipi?)"
"Ahah... she's fine. Once all of this is over, I'm going to tell her... well... if you'll allow me... (Ahah... yuko sawa. Mara tu haya yote yatakapokwisha, nitamwambia... yaani... ikiwa tu utaniruhusu ni...)"
"Of course. You'll tell her anything you want. I know you can't wait for me to kick ass so you can finally be with her freely, and I fully support that (Bila shaka. Utamwambia lolote unalotaka. Najua hauna subira kwangu mimi kuwaangusha wabaya wetu ili hatimaye uweze kuwa naye kwa uhuru zaidi, na mimi naliunga mkono kabisa jambo hilo)," Draxton akasema.
Mark akatabasamu na kusema, "Thank you (Asante)."
Wakiwa mbioni kumaliza nyama, mlango ukafunguliwa, na hapo ndani akaingia Darla. Draxton akamwangalia kwa upendezi mwingi. Wakati huu alionekana kutulia zaidi kihisia, na alipendeza kwa kuvaa blauzi nyepesi ya kijani pamoja na sketi fupi ya blue-bahari yenye mtindo wa marinda ya sketi ya shule iliyoyaacha mapaja yake wazi, na kama kawaida harufu yake nzuri ikazitia pua za Draxton sumu tamu ya hewa isiyoepukika kuvuta. Alikuwa ameziachia nywele zake ndefu kwa nyuma, naye akaelekea mpaka hapo wanaume walipokaa na kusimama pembeni kwake Draxton.
Mark akamwambia akae, lakini Darla akaendelea tu kusimama. Draxton akaitazama miguu mizuri ya mwanamke huyo na kupatwa na msisimko wa ajabu ndani ya mwili wake, na Mark akalitambua hilo na kutabasamu kiasi.
"You ate it all without inviting me? (Mmekula yote hata kunialika hamna?)" Darla akasema hivyo.
Draxton akampandisha mpaka usoni.
"Figured you guys had your own stuff there, so don't blame me (Nilionelea kwamba na nyie mtakuwa na mambo yenu huko, kwa hiyo usinilaumu)," Mark akamwambia.
"Whatever. Edmond went out with Gia again. I thought this would be a good time to come over... or am I too early? (Vyovyote. Edmond na Gia wametoka tena. Nikaona huu ndiyo wakati mzuri wa mimi kuja... ama nimewahi sana?)" Darla akauliza.
"No, perfect timing. I was just about to leave too (Hapana, ndiyo muda mwafaka. Mimi pia ndiyo nilikuwa nataka kuondoka)," Mark akasema.
Draxton akamwangalia Mark na kuuliza, "Where to? (Wapi unaenda?)"
"I'm off to the hospital again (Ninaenda hospitalini tena)," Mark akamjibu.
"And let me guess, it's a voluntary shift. What is it with you and this new obsession, huh? (Na ngoja nikisie, ni zamu ya kujitolea. Ni nini kilichokupa huu upendezi mpya uliopitiliza, eh?)" Darla akauliza huku sasa akikaa.
Mark akashusha pumzi taratibu na kuangalia chini kama anatafakari jambo hilo.
Draxton akamwangalia na kuona kama akili ya Mark ilivutwa na jambo zito, naye akauliza, "Is there something serious going on? (Kuna jambo lolote zito linaloendelea?)"
Mark akamtazama na kusema, "Yeah. The town hasn't said anything so people don't panick, but bodies have been showing up at the hospital. All of them are from cases of severe animal attacks (Ndiyo. Mji bado haujatangaza suala hili ili watu wasihofie kupitiliza, lakini kuna miili imekuwa ikifikishwa hospitalini. Yote imetokana na majanga ya kushambuliwa vikali na wanyama)."
Draxton na Darla wakatazamana machoni kwa umakini, kisha mwanaume akauliza, "And? (Na?)"
"The town sheriff and his men are doing a quiet manhunt to find the animal, they think it's a bear (Sherifu wa mji na maaskari zake wanafanya msako wa kimya-kimya kumkamata huyo mnyama, wanadhani ni dubu)," Mark akajibu.
"But it's not a bear, is it? (Lakini siyo dubu, ama ndiyo?)" Darla akauliza.
"Could there be any of our kind to do such things? (Watakuwepo wa aina yetu wanaofanya hayo mambo?)" Draxton akauliza.
"No, the Alpha would not allow it. Something else is going on (Hapana, huyo Alpha hangeruhusu jambo hilo. Kuna kitu kingine kinaendelea)," Mark akasema.
"It could be Aysel (Inaweza ikawa ni Aysel)," Darla akasema kwa mkazo.
Mark akamtazama dada yake kwa ufupi, kisha akasema, "It could be (Inawezekana)."
Hilo lilikuwa kweli, kwa sababu Aysel alikuwa anakaribia kupoteza ufahamu wake mzuri kama Gianna tu na alikuwa huko nje anazurura sana bila kupata msaada aliohitaji, kwa hiyo kuua au kuumiza watu ovyo ovyo lingekuwa jambo ambalo huenda angekuwa anafanya.
Kwa kufikia mkataa huo, watatu hawa wakawa wamekubaliana kuharakisha badiliko la Draxton ili aanze kuwashughulikia watu wake vizuri ili kama matatizo yaliyokuwa yameanza kutokea mjini yalisababishwa nao, basi aweze kuyakomesha upesi na kuendelea kuhangaikia mengine pia.
★★★★★★★★★★★★
ITAENDELEA
★★★★★★★★★★
WHATSAPP +255 678 017 280