undeceivable
Member
- Dec 22, 2017
- 12
- 15
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu unaendelea lini?CHANGE
Story by Elton Tonny
Urafiki, Familia, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Ukatili, Mauaji, Mambo yasiyotazamiwa, Mambo yenye kuhofisha
R-rated 18+
Enjoy!
★★★★★★★★★★★★★★★★★★★
SEHEMU YA THELATHINI NA TATU
★★★★★★★★★★★★★★★★★★★
Manka akamsogelea Namouih na kumshika mabegani, huku naye akilia pia, na daktari akawa anawaangalia kwa simanzi. Kuna mtu aliyeingia hapo akiwa na dhumuni la kumwita daktari, naye daktari akamwonyesha ishara ya kumzuia asifike mbele na kumwambia aondoke, hivyo akafunga mlango na kutoka.
"Taratibu za kumwingiza mochwari zimemalizika nadhani. Poleni sana kwa msiba huu. Tutakuwa pamoja nanyi mkihitaji lolote lile," Daktari akasema.
Namouih akanyanyua uso wake kutoka mezani na kuanza kujifuta machozi. Manka pia akawa anajifuta machozi huku bado akilia.
"Asante doctor."
Namouih akasema hivyo na kunyanyuka kabisa, naye akatoka ndani ya ofisi hiyo ndogo akifuatwa na Manka kwa nyuma. Alijitahidi sana kujikaza ili atembee mpaka wakalifikia gari lake, naye akaingia na kuketi upande wa usukani kisha akakiweka kichwa chake hapo na kuendelea kulia kwa hisia sana. Manka alikuwa ameketi siti ya pembeni, akiusugua mgongo wa Namouih kwa njia ya kumbembeleza lakini naye akilia sana kwa huzuni. Namouih akawa anapumua kwa nguvu sana, na kila mara alipojaribu kuliwasha gari lake, angesitisha kwa kuwa angeanza kulia tena na kukosa umakini mzuri. Manka akatoa simu yake na kujaribu kumpigia Zakia, lakini ikawa inaita tu bila kupokelewa mara nyingi sana. Namouih akajikaza zaidi, kisha akawasha gari sasa na kuanza kuliondoa hapo hatimaye.
Safari yake kuja kutoa "surprise" kwa familia ikageuka kuwa ndoto mbaya tena kwake, naye akajitahidi kuliendesha gari kwa uangalifu sana ili amrudishe Manka nyumbani na ndiyo mambo mengine yafuate.
★★
Upande wa Blandina. Mwanamke alikuwa ameshaamka muda fulani nyuma na kuamua kutoka hotelini pale ili aende kukata mitaa jijini hapo baada ya kumaliza biashara zake za kikazi pamoja na Namouih muda mfupi nyuma. Na pia alikuwa anapoteza muda akimsubiri rafiki yake ili waweze kwenda kwa ajili ya matembezi ya kujifurahisha usiku. Hii ikiwa ni mida ya saa moja sasa, akawa ameingia kwenye kumbi fulani ya starehe na kuketi kwenye meza yeye pekee huku akishusha chupa moja ya bia, na ni hapa ndipo alipotaka kumjulisha Namouih kwamba yupo ili wakutane; rafiki yake akishatoka kule nyumbani kwao. Kulikuwa na watu kadhaa wakicheza muziki na wengine wakipata vinywaji, wanaume kadhaa wakimwonyesha kumtaka ila yeye anawapuuzia, naye akawa amezama kwenye simu yake akipitia mitandao ya kijamii.
Dakika kadhaa kupita akawa anaona ni kama Namouih anachelewa, na hata kuwasiliana naye hakuwa amewasiliana naye, hivyo akaamua kumpigia ili kuuliza kama alikuwa njiani kutoka kule ama ndiyo alikuwa ameng'ang'aniwa. Lakini alipokuwa tu ndiyo ameanza kumpigia, akamwona mtu mwingine hapo aliyeingia, naye akamfahamu upesi. Mwanzoni alidhani amemfananisha kwa hiyo akakata simu na kumwangalia vizuri, naye akahakiki sasa kwamba kweli Ilikuwa ni Draxton. Akashangaa kidogo lakini kwa wakati huo huo akafurahia sana, naye akanyanyuka na kuanza kumfata pale alipokuwa amesimama. Draxton alipendeza na mwonekano wake kwa kuvalia T-shirt ya mikono mirefu iliyokuwa kama sweta lenye rangi mchanganyiko, suruali ya jeans na viatu vya sneaker vyeusi vyenye mstari mweupe kwa chini. Blandina aliweza kuona namna ambavyo wanawake wengi hapo walimwangalia sana hasa kutokana na sura yake na mwili kwa ujumla kuwa nzuri, lakini mwanaume alikuwa anaangaza kwingine tu kama vile anatafuta mtu.
Blandina akamfikia kwa nyuma na kuupitisha mkono wake kuzungukia kiuno cha Draxton huku akimlalia mkononi, naye Draxton akamtazama na kuachia tabasamu. Mwanamke huyu alikuwa amevalia T-shirt nyepesi ya rangi ya kijivu iliyoacha bega lake moja wazi, suruali nyeusi ya skinny iliyochoresha hips zake na kalio vyema, na viatu vidogo vilivyoacha miguu yake wazi. Alikuwa ameziachia nywele zake za kusuka kwa mtindo wa mawimbi-mawimbi, naye akaendelea kusimama karibu sana na mwanaume huyu.
"Unafanya nini hapa?" Blandina akauliza huku anatabasamu.
"Nilikuwa nakutafuta wewe," Draxton akamwambia.
"Mh... umejuaje niko huku?"
"Huwezi amini lakini nimevuta harufu yako sehemu hii nikajua umo humu... nilikuwa nataka kuona kama kweli uko huku."
"Ahahahah... kwamba una pua kubwa sana eeh?"
Draxton akatabasamu.
"Lakini umekuja huku kufanyaje? Ndiyo sababu ulikuwa hupatikani au?" Blandina akauliza.
Draxton akabaki tu kumwangalia.
"Unanifatilia eti? Umetoka huko kote kuja kunifatilia huku eh? Kuona ka' niko na mchizi mwingine? Ahahahah..." Blandina akasema huku akicheka.
"Bahati mbaya sijamkuta, ningemuua," Draxton akasema.
"Ahahahah... kwenda huko, huna lolote. Wewe ndiyo umekuja huku kukutana na dosho. Yuko wapi? Nionyeshe nimpe vyake," Blandina akasema kimasihara.
"La, sikutani na dosho lolote. Hamna anayekuzidi hapa ndani."
"Unajihamii... nisingekufata ningemwona tu... hapo tayari umempa signal asikusogelee ili nisimwone eti? Na sikuachii mpaka akufate. Njoo huku..."
Blandina akamwambia hivyo huku akianza kumvuta mkono. Draxton akaongozana naye mpaka pale mwanamke huyu alipokuwa ameketi, nao wakasimama tu usawa wa meza yake.
"Unanifata mpaka mkoa wa mbali kuhakikisha sibebwi eeh?" Blandina akasema.
"Yah, mali yangu safi sitaki ichukuliwe hivi hivi."
"Hahah... yaani wewe unanishangaza sana. Tukiwa pamoja, unanikimbia. Ukisikia nimetoka, unanikimbilia. Ila nahisi bado hiyo siyo sababu. Uniambie ukweli, umekuja huku kufanya nini?" Blandina akauliza kwa umakini zaidi.
"Nilikuwa nimekuja huku kumwona rafiki... nilifanya jambo fulani lililomuumiza kwa hiyo nikawa nataka kumwomba samahani," Draxton akamwambia.
"Kweli?"
"Ndiyo."
"Lakini si uliniambia huna marafiki?"
"Nimeanza kuwapata toka nilipokujua."
Blandina akacheka kwa mguno.
"Nilijua na wewe upo huku maana umeniambia jana, ila sikuona haja ya kukusumbua maana upo kikazi zaidi. Lakini kweli nimehisi harufu yako wakati napita hapo nje ndiyo nikaja kuhakikisha kama ni wewe..." Draxton akasema.
"Ahahahah... lakini Drax! Kwa hiyo unaweza kuvuta harufu za watu?"
Draxton akatabasamu tu na kuangalia upande mwingine.
"Umemfanyaje huyo rafiki yako?" Blandina akauliza.
"Ni story ndefu kiasi, nitakuja kukusimulia siku moja. Na wewe? Mbona upo humu now?"
"Nimekuja na Nam huku, kuna mambo fulani tulikuwa tumeagizwa ku-handle huku kama nilivyokwambia so... namsubiri hapa afike maana alikuwa ameenda kusalimia nyumbani... familia yake ipo huku," Blandina akaeleza.
"Okay."
"Nataka nimpigie hapa amekawia kidogo..."
Blandina akasema hivyo huku akianza kubofya kwenye simu yake tena, akimpigia Namouih. Ni kweli kabisa yale yote aliyokuwa anasema Draxton. Alijua kwamba Namouih aliondoka mkoani kwao kule na kuja huku kwa ajili ya masuala ya kazi pamoja na Blandina, na kwa sababu waliachana sehemu mbaya mara ya mwisho, Draxton aliamua kuja huku huku ili ajaribu kuongea naye vizuri zaidi kusawazisha hali baina yao. Hivyo ndivyo alivyozijali sana hisia za mwanamke yule. Ndipo katika pitapita yake hapo mjini kweli akawa ameivuta harufu ya Blandina na kuamua kuingia sehemu hiyo ili kuonana naye. Mambo yao haya yalikuwa ya mzunguko sana.
Blandina akawa amepiga simu mara tatu bila kupokelewa, kisha ya nne ikapokelewa. "We' malaya uko wapi?" akasema Blandina kiutani.
"Hallo..."
Sauti hiyo iliyosikika upande wa pili haikuwa ya Namouih, naye Blandina akakunja uso kimaswali.
"Ee ndiyo hallo... nani mwenzangu?" Blandina akauliza.
"Mimi Manka..."
"Aaaa... Manka... hey hujambo?"
"Sijambo..."
"Namouih yuko wapi?"
"Anaendesha... hhh... niko naye anaendesha..."
Blandina akatambua kuwa Manka alikuwa analia. "Manka nini shida? Mbona unaongea hivyo?" akauliza kwa kujali.
"Kuna matatizo yametokea dada... kuna msiba..." Manka akasema.
Kwa uwezo wake mkuu wa kusikia, Draxton alisikia jambo hilo lililosemwa na Manka, naye akamwangalia Blandina kwa umakini zaidi.
"Nini kimetokea Manka?" Blandina akauliza akiwa ameingiwa na wasiwasi.
"Hhh... Nasma amefariki dada..."
Blandina akashindwa hata kutamka chochote tena na kuweka kiganja chake usoni.
Draxton akiwa amesikia hilo vyema, akatazama upande mwingine kwa kuhisi simanzi kwa sababu alijua huyo aliyesemwa alikuwa mdogo wake Namouih.
"Mko wapi sa'hivi? Nyumbani?" Blandina akauliza.
"Ndiyo tunaenda... tulikuwa hospitalini..."
"Okay. Okay, nakuja. Poleni sana jamani... siko mbali sana. Mwambie dada nakuja, sawa?"
"Haya..."
Blandina akakata simu na kumtazama Draxton machoni, ambaye sasa alikuwa akimwangalia pia.
"Ai jamani... Draxton... Namouih amefiwa na mdogo wake... mdogo wake wa mwisho," Blandina akasema huku akionyesha huzuni.
Draxton akakishika kiganja cha Blandina na kusema, "Twende."
Blandina akachukua mkoba wake mdogo na kuuweka begani, kisha wakaanza kuondoka na kwenda kuchukua gari lake Blandina ili kuelekea kule. Draxton hakuja mkoani huku kwa gari lake bali usafiri wa basi hiyo hiyo jana, kwa hiyo Blandina akawaendesha haraka kuelekea kule kwenye kisa chenye kuhuzunisha kilichomsibu mtoto Nasma.
★★
Namouih akawa amelifikisha gari lake nyumbani kwao, naye akashuka taratibu pamoja na Manka. Ilikuwa ikikaribia saa mbili sasa, na walikuwa wametumia dakika nyingi kufika huku kwa sababu Namouih aliendesha gari taratibu sana kutokea kule hospitalini. Manka tayari alikuwa amemwambia kwamba Blandina amesema anakuja huku, na muda wote tokea wameondoka hospitali Namouih hakuwa amesema lolote lile. Kwa kutarajia labda Zakia alikuwa amesharudi nyumbani, Manka akawahi kwenda ndani, lakini akakuta bado palikuwa pamefungwa na hata taa hazikuwashwa, kumaanisha hakukuwa na mtu hapo.
Akapafungua na kumwacha Namouih aingie ndani, naye Namouih akaelekea tu mpaka kwenye sofa moja na kukaa kama mtu mwenye uchovu sana. Macho yake yalikuwa mazito kama vile mtu aliyetoka usingizini kutokana na kulia sana, lakini wakati huu hakuwa akilia, bali alikuwa ameweka tu uso wenye kujaa huzuni huku ameangalia chini. Manka akatoka sehemu ya jikoni akiwa na glasi ya kioo, naye akaelekea kwenye friji na kuiwekea maji, kisha akaja mpaka alipoketi Namouih na kupiga magoti karibu yake; akimpa maji anywe.
Namouih akamwangalia Manka kwa ufupi, jinsi ambavyo dada huyo alikuwa na roho nzuri sana, naye akayapokea maji hayo na kunywa kidogo, kisha Manka akaichukua glasi na kuiweka kwenye meza ndogo ya kioo hapo mbele. Manka akasogea pembeni zaidi na kuanza kuwapigia ndugu zao wengi ili kuwajulisha kuhusu msiba huu, lakini alipojaribu kupiga namba ya Zakia, haikupatikana kabisa wakati huu. Akawapigia rafiki zake na kuwaambia pia, akiwaomba wamsaidie kwenda kumwambia mwenyekiti wao wa hilo eneo kuhusu msiba huu, kwa sababu kulikuwa na kawaida ya kutangaza msiba kwa vipaza sauti endapo jambo kama hilo lingetokea, na ilikuwa kupitia kwa mwenyekiti.
Namouih akiwa ameendelea tu kukaa kwenye sofa, wakaanza kuja majirani wa karibu na marafiki, wakimpa pole kwa msiba huo, na hata wengine wakilia kwa huzuni. Wengi walimfahamu Namouih na hawakujua kwamba alikuwa amerudi huku kwa wakati huu, hivyo wakawa wanaongea naye kumfariji, na Namouih hakuwa akisema lolote lile ila kutikisa tu kichwa kukubali faraja zao. Kuna watu waliokuwa wakisaidizana kutoa masofa nje sasa, na mikeka ikawa inatandikwa sehemu za nje pia kwa kuwa ndani lilikuwa zulia kubwa kutoshea sebule nzima. Namouih hakubadilisha nguo wala nini, bali akawa amekaa tu chini kwa wakati huu, akiwa ameegamia ukuta, na ni Manka ndiye aliyekuwa karibu yake zaidi pale wengine walipoendelea kutoa pole zao na kushughulikia mambo yaliyohitajika hapo.
Sasa ikiwa ni saa mbili na nusu usiku, Zakia ndiyo akawa amerejea nyumbani hatimaye. Alikuwa amefikishwa kwa bodaboda, naye akashangaa sana baada ya kukuta gari limeegeshwa hapo kwake na baadhi ya majirani zake wakiwa wamekaa kimsiba-msiba kabisa. Baada ya wao kumwona, wakamfata na kuanza kumlaki, na bado itikio lake lilikuwa la mshangao tu kwa sababu hakujua ni nini ambacho kilikuwa kinaendelea. Si ndiyo akapewa taarifa sasa!
"Uuuwiiiiii!"
Alipiga kelele ya kilio kwa kutoamini masikio yake kwa kile alichoambiwa. Alianza kutangatanga akienda huku na huko, na wale waliokuwa hapo wakawa wanajaribu kumbembeleza. Alilia kwa uchungu sana huku akiwa ameweka mikono yake kichwani, na ndiyo mmojawapo akamwambia kwamba binti yake, yaani Namouih, alikuwa ndani kule pia. Akatoka alipokuwa huku akishikiliwa na wanamama wawili mpaka sehemu ya ndani, na hatimaye akamwona binti yake. Akaanza kulia zaidi huku anamfata pale chini, na wote waliokuwa hapo waliingiwa na simanzi sana.
Zakia alipomfikia Namouih karibu, Namouih akamtazama machoni kwa hisia kali sana, na kiukweli ilimwogopesha mama huyu. Alikuwa na lengo la kumkumbatia binti yake lakini akaishia kumwangalia tu usoni huku akilia bado, naye Namouih akasimama huku akianza kupumua kwa nguvu. Jinsi alivyomwangalia mama yake kwa hisia kali ilifanya wengine waingiwe na hofu kiasi kwa sababu walijua Namouih alikuwa mkali sana, na kumwangalia mama yake kwa njia hiyo kulimaanisha tatizo kubwa baina yao.
"Ulikuwa wapi?" Namouih akamuuliza mama yake kwa mkazo.
"Nilikuwa kwenye kikundiii..." Zakia akajibu huku akilia.
"Kikundi gani?" Namouih akauliza.
Zakia akaendelea tu kulia, huku akiwa ameviweka viganja vyake mdomoni kama vile ameviuma.
"Hhh... mama... unaacha kufanya mambo ya muhimu... unaenda kutembea... na vitoto vidogo... unamwacha mwanao wa kumzaa... anakufa... hhh... unajua ni nini hata kilichompata?" Namouih akauliza kwa hisia ya huzuni kali sana.
Zakia akawa anatikisa kichwa kama kukataa.
"Mtoto amekuwa akikwambia ana... kuna mwalimu anamfanyia ushenzi shuleni... Nasma? Mama, Nasma? Kweli yule mtoto alitakiwa kupitia hali kama hiyo?"
Zakia akazidi kulia kwa uchungu.
Wengine waliopata kujua sasa ukweli wakahuzunika sana, naye Manka alikuwa pembeni akilia kichinichini.
"Miaka 11? Mama! Mtoto humwangalii... mtoto anaumia... hhh... anateseka... muda wote huo alikuwa anaja... anajaribu kukwambia yanayomsibu... hhh... lakini wewe uko bize na kucha za vidole vyako... na wanaume wa kipuuzi wasiokusaidia lolote!" Namouih akaongea kwa hisia sana huku akilia.
Zakia alikuwa bado ameweka viganja vyake mdomoni kama vile ameving'ata, huku akilia kwa uchungu mwingi.
"Unajua ni jinsi gani.... Sasha... alivyoumizwa na maneno yako mengi kwa miaka ile yote? Sikuzote ulimfanya ahisi ni kama yeye ndiyo alimuua Nasri, ukiona kila kitu ulichomtendea kuwa sahihi kabisa. Na wewe je? Leo hii umefanya nini? Niseme nini? Eh? Ni kwa sababu yako Nasma hatuko naye tena!" Namouih akafoka kwa hasira iliyoambatana na huzuni yake kuu.
"Basi dada, basi...."
Watu wakawa wanajaribu kumshika Namouih ili kumtuliza, lakini Namouih akagoma kutulia. "Msiniguse... nimesema msiniguse!" akaongea kwa ukali.
Waliokuwa wamemshikilia Namouih wakamwacha, na wakubwa wakawa wanamwambia atulize hisia na badala ya kumlaumu mama yake, wafarijiane kwa sababu msiba huu ulikuwa wao kwa pamoja.
Zakia akawa kama ameishiwa nguvu, naye akakaa chini huku akilia bado.
"Eh Mungu wangu mimi jamani... kwa nini? Nasma mdogo wangu... alitakiwa kuwa na maisha marefu jamani... hhh... aaah... hapana... Allah... yAllaah... naomba uniamshe kwenye hii ndoto tafadhali... kila kitu kwangu kinabadilika tu... aaah...."
Namouih akaongea hivyo huku akiendelea kulia kwa hisia sana. Watu waliokuwa hapo walimwonea sana huruma, naye Manka akamsogelea Namouih na kumshika mabegani ili kumfariji. Zakia alihisi uchovu wa akili. Alihisi haya yote hayakuwa kweli kabisa. Alihuzunika sana, ile huzuni ya kujilaumu kwa sababu maneno ya Namouih yalikuwa ya kweli, hakumwangalia vizuri binti yake mpaka janga hilo likawa limetokea na hivyo akaona kwamba ilikuwa ni makosa yake kabisa. Akina mama kadhaa walikuwa chini pamoja naye kujaribu kumnyanyua, lakini akawa hataki kusimama na kuendelea kulia huku anamwangalia Namouih kama mtu anayehitaji sana kusamehewa.
Namouih alikuwa analia bila kutoa sauti, na ndipo akatazama sehemu ya mwingilio wa sebule hiyo kumwona Blandina anaingia. Akasimama wima na kumtazama kwa huzuni, na upande wa nyuma yake Blandina akatokea Draxton. Namouih aliacha kulia ghafla na kubaki amemwangalia. Hakuwa ametarajia kabisa kumwona Draxton hapo, na mapigo ya moyo wake yakaanza kukimbia kwa kasi. Wengine walikuwa wanamwangalia Blandina na Draxton pia, wakiwa wageni kwa wengi wao, naye Zakia akageuka pia na kuwaona. Namouih akatoka alipokuwa na kuanza kuelekea pale wawili hao waliposimama, naye Blandina akajiandaa kumkumbatia rafiki yake, lakini Namouih akampita na kwenda moja kwa moja mpaka kwa Draxton, kisha akamkumbatia kwa nguvu huku akianza kulia upya.
Blandina alishangazwa na jambo hilo. Akabaki kumwangalia rafiki yake akiwa amemkumbatia mwanaume ambaye alikuwa ni mpenzi wake yeye Blandina, na hakuelewa vizuri kwa nini alifanya hivyo. Draxton hakurudisha kumbatio la Namouih, bali akawa ametulia tu huku akimwangalia kwa huruma. Baada ya sekunde chache, Namouih akajitoa kifuani kwake na kutazamana naye usoni, kwa ukaribu sana, na kiukweli kama ni mtu ambaye hakuwajua lazima angedhani walikuwa wapenzi, na ilikuwa sahihi kuwaza hivyo. Ila kwa Manka, Zakia, na wale waliomjua mume wa Namouih, walijua Draxton hakuwa mume wake, hivyo kwa kiasi fulani walielewa alikuwa mtu wa karibu kwake. Lakini bado Blandina angejiuliza ukaribu huo ulianza lini. Ni kitu ambacho hakuwa ametegemea kabisa.
★★★★★★★★★★★★
ITAENDELEA
★★★★★★★★★★★★
Usikose sehemu za mwendelezo wa hadithi hii kali ya CHANGE. Ni story nzuri na ndefu sana. Waweza ipata nakala yote kwa gharama nafuu sana. Karibu WhatsApp au kwa inbox ya hapa hapa JF.
WhatsApp no: +255 678 017 280
CHANGE
Story by Elton Tonny
Urafiki, Familia, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Ukatili, Mauaji, Mambo yasiyotazamiwa, Mambo yenye kuhofisha
R-rated 18+
Enjoy!
★★★★★★★★★★★★★★★★★★★
SEHEMU YA THELATHINI NA NNE
★★★★★★★★★★★★★★★★★★★
Draxton hakusema wala kufanya lolote lile zaidi ya kuendelea kumwangalia tu Namouih, naye Namouih akainamisha uso wake na kisha kumgeukia Blandina. Akawa ametambua sasa kwamba hisia zake zenye majonzi zilimwongoza afanye kitu ambacho hakutakiwa kufanya, naye akamwachia Draxton na kumfata rafiki yake taratibu. Blandina akampokea kwa mikono miwili, akiondoa fikira zingine zote akilini ili cha kwanza kiwe kumfariji rafiki yake kipenzi. Akawa anamwangalia Draxton wakati amemkumbatia Namouih sasa, naye Draxton akatoka sehemu hiyo na kwenda nje ili kuwapisha wa humo ndani.
Kwa kuwa bado ilikuwa saa mbili, wale waliofika hapo kwa wakati huo waliandaa chakula chepesi tu kwa ajili ya usiku huo, na hata Draxton alisaidiana na wengine kufanya matayarisho upesi kwa mambo kama hayo. Blandina alikwenda na Namouih chumbani ili kumtia moyo, na rafiki yake alifunguka kuhusu msiba uliompata mdogo wake na jinsi alivyokasirishwa na matendo ya mama yake. Lakini akawa anajilaumu pia kwa kuchelewa mno kumfikia Nasma kipindi chote alichokuwa anatendewa vibaya, naye Blandina akasema ni lazima wangemtafuta mwalimu yule aliyemfanyia hivyo ili alipie kwa mabaya yake.
Muda ulikwenda sana, na mpaka inafika saa tisa usiku, bado Namouih na Blandina walikuwa macho. Blandina alikuwa ameshawatafuta Efraim na Sasha kuwaeleza yaliyotokea, naye Efraim Donald akazungumza na mke pia na kumpa pole, akisema angefika hapo mapema kesho akiwa pamoja na Sasha. Zakia na Manka walipitiwa na usingizi mida ya saa kumi, na kulikuwa na watu waliolala ndani na nje ya nyumba, kutia ndani Draxton, aliyelala nje lakini siyo kusinzia. Alikuwa akimfikiria sana Namouih. Huzuni iliyompata mwanamke huyo baada ya kugundua kwamba Nasri alikufa kwa sababu yake Draxton iliongezwa zaidi sasa baada ya kumpoteza na mdogo wake mwingine, naye hakujua afanye nini ili kumpa faraja ya moja kwa moja. Ila kuwa kwake hapo kungempatia nafasi ya kuonyesha faraja, kwa sababu Namouih alionyesha wazi kwamba alimhitaji baada ya kumkumbatia muda mfupi nyuma, hivyo akaendelea kusubiri mpaka kukuche.
Namouih alikuwa amejilaza kitandani kwa kumlalia Blandina mapajani, ambaye alikuwa anazilaza-laza nywele zake taratibu mpaka usingizi ulipomchukua kwenye mida ya saa kumi na moja alfajiri. Akamgeuzia upande mwingine wa kitanda na kumwacha alale, kisha naye akaanza kuutafuta usingizi mfupi.
★★★
Hatimaye kukakucha zaidi. Watu wakiendelea kuongezeka hapo, ndiyo shughuli zilivyozidi kuendeshwa kwa ushirikiano. Wengi walichanga pesa, na Blandina pamoja na Draxton wakatoa pesa nyingi kwa ajili ya mambo yaliyohitajika hapo na kule hospitali kuelekea taratibu za mwili wa Nasma. Namouih hakutoka chumbani kwake kuanzia alipoamka mpaka inafika saa sita mchana, na Blandina alikuwa akijitahidi kumbembeleza hata ale lakini akagoma. Zakia pia alisaidiwa na rafiki zake kwa mengi hapo, huku bado roho ikimuuma kwa sababu hakukuwa na hali nzuri baina yake na binti yake mkubwa kwenye wakati huu mgumu.
Draxton alisumbuliwa sana na maneno aliyosikia baadhi ya wanawake wakisema kumhusu Namouih na mama yake. Wenye kuongea kichinichini kuhusu namna Namouih alivyomrushia maneno makali Zakia walikuwa wakisema hana adabu, hajui lolote kuhusu mambo ya huku kwa sababu anaishi mbali na hivyo hatakiwi kumlalamikia mama yake bila sababu. Walikuwa wakisema anajifanya wa kishua sana na anawaona wengine kuwa wachafu ndiyo maana alikuwa hataki hata wamguse. Walitia chumvi nyingi na kuongelea mambo mengi wasiyokuwa na uhakika nayo ili kumpakazia Namouih ubaya, na jambo hilo lilimkera sana Draxton kwa sababu walikuwa wakimhukumu mwanamke yule vibaya. Wengi wa wanawake wenye umri mdogo walivutiwa sana na Draxton, ingawa ilikuwa msibani lakini baadhi wakawa wanaongea kuhusu kupata hata namba zake. Hawangeweza kutambua kwamba yote hayo mwanaume yule aliyasikia kwa sababu ya uwezo aliokuwa nao, lakini Draxton akajitahidi kukazia fikira jambo muhimu zaidi lililompeleka hapo; kumfariji Namouih na familia yake.
Baadaye, Blandina alikuja kuongea na Draxton, akisema kwamba Namouih hakutaka kula wala kukiacha kitanda kabisa, na aliwaza mno kumhusu. Akikumbuka namna ambavyo Namouih alimkumbatia Draxton usiku wa jana, akamwambia aende pamoja naye ndani ili akajaribu kumsisitiza Namouih ale. Draxton alishangaa kiasi kwa ombi hilo na kuuliza ni kwa nini Blandina alitaka yeye afanye hicho kitu, lakini Blandina hakuweka wazi namna alivyoyaona mambo na kumsihi tu kwenda kujaribu. Mwanaume akaridhia, nao kwa pamoja wakaelekea ndani.
Chumbani alipokuwepo Namouih, Manka alikuwepo pia akimwangalia dada yao mkubwa. Kuna vyakula vya kiamsha kinywa vilivyokuwa hapo tangia saa nne asubuhi, na sasa ilikuwa inaelekea kuingia saa tisa alasiri. Baada ya Blandina kuingia na Draxton humo, Zakia akaenda pia pamoja na akina mama wengine ili kumwangalia binti yake. Yeye pia alijua kwamba Namouih hakufanya chochote siku hii, na ilikuwa kama aliogopa hata kumfata, lakini sasa akawa anataka kuona itikio lake lingekuwaje baada ya rafiki yake mwingine kupelekwa humo.
Chumba kikawa kama kimejaa kwa waliosimama hapo kuwatazama marafiki hao, naye Blandina akamsemesha Namouih, lakini hakugeuka wala kujibu. Wakati huu alikuwa amefungwa kwa khanga kiunoni, naye Blandina akamwambia Draxton kwa ishara kuwa ajaribu kumsemesha labda yeye angemsikiliza, hivyo Draxton akamwita mwanamke huyo.
"Namouih..."
Kimya.
Draxton akasogea mpaka usawa wa uso wake na kuchuchumaa, na Blandina akawa anawaangalia kwa umakini. Macho ya Namouih yalielekea tu chini, akiwa ametulia tu utadhani sanamu.
"Amka. Unatakiwa ule kitu," Draxton akamwambia.
Kimya.
"Namouih amka, la sivyo nitakunyanyua kwa lazima..."
Kimya.
"Acha kuwa mbinafsi Namouih. Haujafiwa peke yako," Draxton akamwambia.
"Drax..." Blandina akajaribu kumzuia, lakini Draxton akanyanyua kiganja chake juu kama kusema 'subiri.'
"Hasira haitakusaidia kwa lolote Namouih. Wewe kuliko watu wote ndiyo unatakiwa ujue inakuwa vipi mtu anapokasirika kwa muda mrefu."
Namouih akaendelea kutulia tu kama vile hakusikia lolote lile.
"Unataka kujua Max alikuwa na maana gani kumwambia Ramona amchore ile tattoo?" Draxton akamuuliza hivyo.
Maneno hayo ya Draxton yakamfanya Namouih amtazame taratibu machoni, kwa sababu alielewa alichomaanisha.
Blandina akakaza macho yake kwa mbali huku akimwangalia sana Draxton, kwa sababu yeye hakuelewa maana ya jambo hilo, na hivyo kama Namouih angeweza kulielewa ingemaanisha kuna kitu fulani ambacho kiliendelea kwa wawili hawa bila ujuzi wake, ingawa hakuwa na uhakika sana.
"Maneno yale... ni katika maana ya kawaida tu kwamba hata kama tukimpoteza mtu tunayempenda haimaanishi ametutoka daima, kwa sababu sehemu aliyonayo ndani ya mioyo yetu itaendelea kuishi... kwa hiyo inakuwa ni kama hajafa. Naelewa huzuni yako. Unahisi kama umeshindwa. Lakini kama tu unavyojua Namouih... mimi pia naelewa hakuna kitu kilicho kizito kuliko fikira za hatia unapohisi kushindwa kumsaidia mtu unayempemda, ila unatakiwa utambue kwamba jitihada zozote ulizofanya na unazoendelea kufanya kwa ajili ya familia yako ni za upendo, na bila shaka wanazithamini sana..."
Namouih akaanza kutokwa na machozi kwa hisia nyingi sana zilizomwingia moyoni baada ya kuyasikia maneno hayo ya Draxton. Ilimfanya akumbuke kwamba hata yeye aliwahi kumtia moyo mwanaume huyo kwa njia hiyo hiyo.
"Kila mmoja wao analijua hilo, na wote wanakupenda sana. Nakuomba tu usiuchoke upendo ulio nao kwao pia... kwa sababu sasa kuliko wakati mwingine wowote wanakuhitaji wewe zaidi Namouih.... kwa hiyo usikate tamaa," Draxton akamwambia kwa upole sana.
Watu waliokuwepo hapo walitulia sana mwanaume huyo alipokuwa akiongea hayo, naye Namouih akafumba macho yake na kuendelea kulia kwa uchungu. Draxton akamshika pande za mikono yake na kuanza kumnyanyua taratibu, na Namouih akakaa sasa. Alionyesha kuchoka kwa kiwango cha hali ya juu, na ndipo Manka akasogea karibu ili ampatie japo maji ya kunywa. Draxton akasimama na kurudi nyuma kidogo, kisha Zakia akasogea karibu ya binti yake na kukaa pembeni yake kitandani hapo baada ya Namouih kumaliza kunywa maji, naye akaishika mikono yake na kumwambia amsamehe kwa sababu ya namna ambavyo maisha yao yalikuwa yamebadilika ghafla kwa kuwa aliendekeza mambo yasiyofaa. Namouih akabaki tu kimya, naye Blandina akawaambia watu wengine waliokuwepo hapo wapishe ili Namouih ajiweke vizuri kimwili.
Watu waliokuwepo hapo wakaanza kupungua, na wakati Draxton alipokuwa anaondoka pia, Blandina akamtazama Namouih na kuona namna ambavyo alikuwa amemtazama mwanaume huyo mpaka alipotoka ndani hapo. Hali hiyo kiukweli iliendelea kuisumbua akili ya Blandina kwa kuwa ingawa hakutaka kuweka madhanio hasi kuielekea, kulikuwa na mambo mengi yaliyokuwa yameanza kumchanganya. Jinsi Namouih alivyokuwa ameanza kutenda kumwelekea Draxton Ilikuwa kwa njia iliyoonyesha hisia nyingi sana, hisia ambazo zilipita zile za urafiki wa kawaida kabisa, na hakuwahi kudhani Namouih kati ya watu wote angekuwa na uvutano wa aina hiyo kwa mpenzi wake yeye Blandina, ila bado mwanamke huyu akawa hataki kuyapeleka mawazo yake mbali sana ili asije kujikuta anamhukumu rafiki yake kwa njia mbaya. Laiti kama angejua!
★★
Ikawa imefika mida ya saa kumi jioni, na kufikia wakati huu tayari Namouih alikuwa amejisafisha na kula kidogo kwa msaada wa Blandina na Manka. Zakia hakutaka kabisa kumwacha binti yake, yaani kila sehemu ambayo Namouih angekaa na yeye angekuwepo, na sasa wanawake hawa wakiwa wanasubiria mwili wa Nasma uletwe kutoka kule hospitalini, Efraim Donald akawa amefika hapo akiwa na mama yake mzazi, yaani Halima, pamoja na binti Sasha. Ndiyo walikuwa wamefika tu jijini hapo leo na moja kwa moja kuja nyumbani, naye Sasha akamfata Namouih kwanza na kumkumbatia. Itikio la faraja aliyoipokea kutoka kwa mdogo wake lilikuwa la ndani sana kutoka moyoni kwake Namouih, naye akaendelea kumshikilia Sasha kwa dakika nyingi sana, akijitahidi kumbembeleza pia kwa sababu alikuwa analia. Halima akamfata Zakia na Namouih pia kuwafariji, kisha akina mama hawa wakamshika Sasha na kuanza kumbembeleza, nao wote wakawa karibu wakifarijiana katika msiba huo uliowachoma sana.
Wakati huu mambo mengi yalikuwa yameshatendeka hapo nyumbani kwa Zakia, watu walikuwa wameshakula, ndugu wengi wa familia ya Namouih na Efraim Donald walikuwa wameshafika, na sasa ni mwili tu wa Nasma ndiyo ulikuwa unasubiriwa kuletwa ili uhifadhiwe ndani, halafu ndiyo mazishi yafanyike kesho. Draxton alikuwa ameondoka kwa kuambatana na wale ambao walikwenda huko hospitali kuufata mwili wa Nasma, na Blandina alikuwa hapo nyumbani akiendelea kusaidia kwa mambo ya hapa na pale. Tayari mwanamke huyu alikuwa ameshawasiliana na 'boss' wao, yaani Mr. Edward Thomas, kumjulisha kuhusiana na msiba huo wa ghafla sana ambao ulifanya ratiba za mambo yaliyowaleta huku ziingiliane. Mr. Edward akatuma pole zake kwa wafiwa, naye Blandina akasema angezifikisha.
Efraim Donald alikwenda ndani pia baada ya kusalimiana na Blandina, naye akamfata mke wake pamoja na Zakia na kuwapa pole. Namouih hata hakumsemesha chochote mume wake, akionekana kuwa makini tu kwenye uimara wake wa kuendelea kuipa familia yake faraja, hivyo Efraim akamwomba waende chumbani ili wazungumze kwa kifupi. Namouih akakubali na kwenda naye, Efraim akiwa amemshikilia mkono na kutembea pamoja naye, kisha wakaingia chumbani hatimaye.
Kwanza kabisa kabla ya yote, Efraim Donald akamkumbatia mke wake kwa upendo huku akimwambia namna ambavyo alielewa maumivu yake, naye Namouih akawa anaipokea faraja ya mume wake huku akitokwa na machozi. Efraim Donald akauliza ni nini hasa kilichokuwa kimempata Nasma ghafla, na kwa kujikaza Namouih akamwelezea kwa kifupi, akisema kwamba mwalimu fulani wa Nasma aliyeitwa Joseph ndiye aliyemharibia mdogo wake maisha mpaka kusababisha kifo chake. Akamshika Efraim kwenye kola ya shati lake na kumwambia amwahidi kumsaidia ili mwanaume yule akamatwe na kumchukulia hatua iliyostahili makosa yake, naye Efraim Donald akakubali na kumwahidi kwamba haki ingetendeka.
Mawazo ya wawili hawa yalikuwa tofauti, kwa kuwa Namouih alitaka huyo mwalimu akamatwe na kupewa adhabu ya makosa yake kisheria, ilhali Efraim alikuwa amepanga kumkamata na kumpa adhabu mbaya sana kwa sababu ya kumfanya mke wake alie. Akamkumbatia tena mke wake na kumtuliza kwa maneno mazuri, na ni hapo ndiyo wote wakasikia watu huko nje wakiongea kuhusu mwili wa Nasma kufika, naye Namouih akatangulia kuelekea sehemu ya sebule kuungana tena na familia yake. Efraim Donald akatoka mpaka nje ili kusaidiana na wale waliolibeba jeneza na kuliingiza ndani, na sauti za vilio kutoka kwa wanawake zikaendelea kusikika. Namouih alikuwa analia bila kutoa sauti, huku akijitahidi kumbembeleza Sasha ambaye alishindwa kuizuia huzuni yake kuu ya kumpoteza mdogo wake kipenzi.
Baada ya wanaume kutoka nje, Efraim Donald akawa amemwona Draxton hapo, naye akamsogelea karibu na kusimama pembeni yake. Draxton alikuwa amesimama kwa utulivu tu karibu na mti mkubwa uliofungwa kamba nene iliyomkaza ng'ombe-dume ambaye angechinjwa siku ya kesho, na wote wakawa wanatazama upande wa kule ndani kwa umakini.
"Umefika huku leo?" Efraim Donald akamuuliza Draxton bila kumtazama.
"La. Nilikuja jana," Draxton akajibu.
"Mke wangu amevunjwa sana na hii hali... sijui itamchukua muda gani kupona."
"Haitakuwa rahisi. Ila yuko imara. Na wewe pia utamsaidia asonge mbele," Draxton akasema na kumtazama.
Efraim Donald akatikisa kichwa kukubali, kisha akasema, "Huyu mtu aliyemfanyia Nasma hayo yote anastahili adhabu moja kali sana."
"Ndiyo. Uko sahihi," Draxton akajibu kwa uzito.
"Ikiwa ungemkamata mpuuzi wa namna hiyo aliyemharibia mtoto mdogo future nzuri mpaka akauawa... unafikiri jela ingetosha attorney Draxton?" Efraim akauliza.
Draxton akamwangalia, kisha akatikisa kichwa kukanusha.
"Sipendi kabisa mtu akimfanya mke wangu alie. Usione kama niko high ila nitakwambia ukweli kabisa... mimi ningemuua huyo mtu kwa mikono yangu mwenyewe," Efraim akasema.
"Mimi pia," Draxton akasema.
Efraim Donald akamtazama usoni kwa umakini.
Draxton akamwangalia pia, kisha akasema, "Lakini kufanya hivyo hakutatupa amani yoyote, ingawa naelewa itaridhisha."
Efraim akatabasamu kwa mbali na kurudi kutazama upande ule wa nyumba.
Wanaume hawa wakaendelea kusimama hapo mpaka Blandina alipokuja karibu nao na kumshika Draxton mkononi.
"Drax... naomba tuongee," Blandina akasema.
Efraim Donald akatoa simu yake na kuwapisha hapo, naye akaanza kuelekea mpaka kule alikoegesha gari la kukodi alilokuja nalo pamoja na Halima na Sasha.
Draxton akiwa amesimama na Blandina sasa, akamuuliza, "Vipi?"
"Kuna... hii kesi ambayo tulikuja kushughulikia huku si unajua..."
"Ndiyo."
"Well, now Namouih amebondeka sana, sidhani kama hata wazo la kuisimamia analo tena. Na hata akisema ajitahidi bado hataweza kutia nguvu yake yote kwa sababu ya huu msiba na zimebaki siku tatu tu. Ninaomba uisimamie badala yake Draxton," Blandina akamwambia.
"Umeshaongea naye kuhusu hilo?"
"Nitamwambia. Na ninajua atakubali tu."
Draxton akainamisha uso wake kidogo.
"Kwa hiyo umekubali?" Blandina akauliza.
"Ndiyo. Tutaanza kushughulikia kila kitu kinachohitajika just... utaniambia ni muda gani," Draxton akasema.
"Mbona uko hivyo?" Blandina akauliza.
Draxton akabaki kimya na kumwangalia tu usoni.
"Inaonekana kama una huzuni sana. Shauri ya Namouih eti?" Blandina akauliza tena.
Draxton akatikisa kichwa kukubali bila unafiki wowote.
"Nimeshangaa kiasi kuona jinsi alivyoonekana kutulia ulipomsemesha... tena vitu ambavyo hata me mwenyewe sielewi. Mara Ramona sijui, mara tattoo... ni kama vile mna connection ambayo sijawahi kuiona kabla," Blandina akaweka mawazo yake wazi.
"Siyo hivyo Blandina. Tumekaa kwa ufupi wakati fulani tukazungumza kwa hiyo kuna vitu nafahamu kuhusu yeye ndiyo maana...."
"Usijali Draxton, sisemi kwamba ni vibaya. Imeni-surprise tu lakini mimi nafarijika kuona umemsaidia kutuliza hisia. Sasa hivi kilichopo ni kumkamata huyo mwalimu ili haki itendeke, ila uwepo wetu sote huku ni muhimu kwa Namouih. Nafurahi kwamba uko hapa pamoja nasi Draxton," Blandina akasema kwa hisia.
Draxton akamkumbatia tu kwa wororo, naye Blandina akarudisha kumbatio lake kwa hisia.
Kutokea sehemu hiyo ambayo wawili hao walikuwa wamesimama kwa kukumbatiana, Namouih alikuwa akiwatazama dirishani kwenye nyumba yao bila wao kutambua. Alikuwa akitamani sana, sana, sana kuwa ndani ya kumbatio la Draxton kwa wakati huu, lakini alielewa hilo halingekuwa jambo rahisi hata kidogo. Akafumba macho yake na kutoka dirishani hapo, naye akaelekea chumbani na kujilaza kitandani kwa kuhisi upweke mwingi sana moyoni.
★★
Muda ulisonga mpaka inafika saa nne usiku, na Namouih pamoja na familia yake bado walikuwa ndani ya nyumba yao. Ndugu na marafiki waliofika hapo wangelala nje pamoja, kutia ndani Efraim na Draxton ambao wao wangelala kwenye magari yao (Draxton kwenye gari la Blandina). Lakini ulipofika muda huu, Efraim Donald akamwambia Blandina amwambie Namouih kwamba yeye anatoka kidogo kufata baadhi ya vitu fulani huko mjini na asingekawia kurudi. Hakuweza kumwambia kupitia simu kwa sababu Namouih aliizima yake kabisa, kwa hiyo Blandina akasema angeufikisha ujumbe, naye Efraim akaondoka.
Toka mchana huo Draxton alipoonana na Namouih na kumtia moyo hakuwa ameonana naye tena, na kiukweli, dhamiri yake ilimsumbua sana kutokana na kuhisi athari mbaya ya kuzigawa hisia zake mara mbili kwa ajili ya wanawake waliokuwa marafiki wa karibu, na hivyo kwa wakati huu kushindwa kujitoa kikamili kwa mmoja aliyemhitaji zaidi kutokana na mwingine kuwa karibu. Alihisi ni kama hakutoa faraja inayostahili kwa Namouih, lakini tena Blandina akiwa mpenzi wake halali hakutakiwa kutendewa kwa njia kama hii maana alimpenda sana. Akili yake ilimwelewa vyema kabisa Blandina. Mwanamke huyo hakustahili kuachwa gizani hata kidogo, naye Draxton akawa anafikiria labda kutafuta wakati mzuri wa kuzungumza naye kuhusu maisha yake lingekuwa jambo la busara ingawa siri nyingi zingemuumiza mwanamke huyo, ila ingekuwa bora tu aujue ukweli kutoka kwake yeye mwenyewe Draxton na siyo kuja kuujua kwa namna nyingine ambayo ingemuumiza hata zaidi.
Efraim Donald aliendelea kuendesha gari lake kuelekea upande fulani wa jiji hilo huku akifuata ramani hususa kwenye simu. Hakuwa akielekea jijini zaidi, bali sehemu ya mbali iliyokuwa na makazi yaliyoachana-achana na mitaa ambayo watu wengi hawakupita nyakati za usiku kwa sababu kulikuwa aidha na vibaka au wahuni waliosababisha matukio mabaya kwa watu. Mwanaume huyu alikuwa na lengo lake akilini kwenda huko, naye akawa amelifikisha gari usawa wa nyumba ndogo iliyokuwa na mwonekano chakavu sana kutokana na kujengwa kwa mabati kuizunguka. Mianga ya taa za gari ilimruhusu kuiona vizuri, naye akazima taa hizo na kuweka simu yake sikioni baada ya kupiga namba fulani.
"Mko wapi?" Efraim akauliza hivyo.
"Tuko ndani. Mwenye hiyo gari nje ni wewe?" sauti ya upande wa pili wa simu ikasikika.
"Ndiyo. Tokeni niwaone, na mimi natoka," Efraim akasema.
"Poa."
Efraim Donald akakata simu, kisha akashuka na kusimama nje hapo pembezoni mwa gari. Mlango wa bati wa nyumba hiyo ndogo ukafunguka, na hapo wakatoka wanaume wawili wakiwa wamevaa nguo za kawaida tu pamoja na kofia nyeusi vichwani, nao wakasogea mpaka mbele yake Efraim na kusimama huku wakimtazama kwa umakini. Lilikuwa eneo lenye giza hivyo walionana nyuso kwa mazoea tu kwa kuwa walijuana, naye Efraim Donald akatoa bahasha fulani mfukoni mwake iliyokuwa imetuna haswa.
"Mlimpatia wapi?" Efraim akauliza.
"Alikuwa sehemu fulani amejificha sijui kwa ma'mdogo wake... inaonekana tayari alijua angesakwa, au kuna mtu alimwambia kuhusu kifo cha huyo dogo," akajibu mmoja wa hao wanaume.
"Hakuna aliyewaona wakati mnamshika?" Efraim akauliza tena.
"Hapana. Tuliondoka naye nikiwa nimemwekea bastola kiunoni kwa hiyo hakufurukuta. Af' kimtu chenyewe kimekaa kiboya-boya tu, sijui hata kilimdanganyia nini huyo mtoto," akasema mwanaume huyo.
"Huwa sipendi upumbavu na vitu vinavyomhusu mke wangu. Hamjamwona na mtu yeyote huku anakutana naye labda kisiri?" Efraim akauliza.
"Nani mke wako? Hamna. Nilikuwa pale hotelini na Wachu huwa anafatilia gari lake kila akizunguka, ila hatujaona kitu cha namna hiyo. Ni kama mke wako ametulia boss," akajibu huyo mwanaume.
"Sijakupa hii kazi ili utoe maoni yako, unanielewa? Fanya unachotakiwa kufanya na kuniambia kinachoendelea... full stop," Efraim Donald akaongea kwa uzito.
Wanaume hao wakabaki kimya.
"Mashine iko wapi?" Efraim akauliza.
"Ipo huko huko ndani," akajibu yule mwanaume mwingine, aliyeitwa Wachu.
Efraim Donald akampatia mwanaume huyu wa kwanza bahasha ile, kisha akasema, "Hiyo ya kazi yenu ya leo, gawaneni mtakavyojua wenyewe. Na wewe Rama usiache kumwangalia mke wangu kwa muda wote atakaoendelea kuwa huku mpaka aondoke, inaeleweka?"
"Pamoja boss," huyo Rama akajibu.
"Ondokeni, nitamalizana naye mwenyewe," Efraim akasema.
Wanaume hao wakaondoka sehemu hiyo na kutokomea gizani, wakimwacha Efraim Donald anaelekea ndani ya ile nyumba. Hao ndiyo watu aliokuwa amewasiliana nao muda ule alipomaliza kuzungumza na Draxton kwa ufupi, naye alikuwa amewapa maagizo ya kumtafuta mwalimu Joseph kutoka katika shule aliyosomea Nasma na wamkamate, kisha wampeleke sehemu ya mbali iliyojificha ili aweze kuja kumpa malipo kwa sababu ya matendo yake yaliyosababisha mtoto yule afe. Ni hao hao ndiyo aliokuwa amewaweka huku kumfatilia mke wake toka alipoingia kwenye mji wao huu wa nyumbani, kwa hiyo walitenda kwa upesi na kufanikiwa kumkamata mwalimu Joseph kisha kumleta sehemu hii. Kifo cha Nasma kingelipwa, lakini kwa kuwa aliyetaka kukilipa kwa niaba ya Namouih alikuwa ni Efraim, ingekuwa kwa njia ambayo hakuna mtu yeyote ambaye angeweza kutazamia kabisa.
Mwanaume huyu akaingia ndani ya nyumba hiyo ndogo na kumkuta mwanaume fulani kijana akiwa amefungwa huku amesimamishwa. Yaani, mikono yake yote ilifungwa kwa kamba ngumu kuelekea juu kwenye mbao za batini, huku miguu yake ikiwa inaelea juu kidogo kutoka ardhini. Hakuwa na nguo kwa juu, kifua chake kisichokuwa na ukakamavu mwingi wa kiume kililowana jasho, na chini alikuwa amevaa suruali nyeusi ya kitambaa. Kwa kumwangalia tu, Efraim angeweza kukadiria kwamba alikuwa na miaka 25 mpaka 28 hivi, na kijana huyo alikuwa mweupe wa kadiri. Midomo ya huyo Joseph ilifunikwa kwa kitambaa kilichoibana sana, naye Efraim akaanza kupiga hatua kumwelekea huku kijana huyo anamwangalia kwa hofu nzito. Waliweza kuonana kutokana na mwanga hafifu wa mshumaa mdogo uliokuwa umesimishwa chini.
"Niaje mwanangu? Uko poa?" Efraim akauliza.
Joseph alikuwa anamtazama tu kwa woga mwingi asiweze kujibu lolote.
Efraim akatabasamu na kusema, "Sitazunguka sana bro, mke wangu ananihitaji huko nilikotoka. Ila najua angefurahi sana kuwa hapa pia maana nimemkamatia mbaya wake. Hujui ni jinsi gani ambavyo huwa napenda sana hizi drama, na kama ningeweza kumwonyesha hii ya leo... sipati picha yaani."
Joseph akawa anamwangalia huku anapumua kwa nguvu sana, naye Efraim Donald akakishika kichwa chake kwa nguvu na kusogeza midomo yake sikioni kwa kijana huyo.
"Unapenda sana kula watoto wadogo eeh? Unapenda kuwa(.....) na kuwaacha wateseke mpaka wafe, si ndiyo mpumbavu wewe? Sasa kama ulikuwa umeshazoea kuwafanyia hayo watoto wa wapuuzi wengine leo ndiyo utajua kwamba kwa Nasma umeharibu... tena umeharibu vibaya sana. Umemtia mtoto mdogo namna ile maumivu kwa sababu ya ujinga mwingi uliojaa kichwani kwako. Ngoja nikuonyeshe nini maana ya maumivu leo," Efraim Donald akaongea kwa hasira sana.
Akakisukuma kichwa cha Joseph na kusababisha mwili wake uanze kuzunguka-zunguka kama nyama iliyotundikwa buchani, naye Efraim akasogea upande wa pembeni na kuokota kifaa/mashine fulani yenye rangi ya njano na nyeusi iliyokuwa na waya mrefu. Joseph aliogopa sana, naye akaanza kujitikisa kwa nguvu akijaribu kujinasua huku akiguna kwa kwa presha.
"Vipi, mbona unacharuka hivyo? Kuna kitu unataka kusema?" Efraim akamuuliza kikejeli.
Kisha akakitoa kitambaa kilichouziba mdomo wa mwalimu huyo ili amruhusu kuongea, na ndipo Joseph akaanza kupiga yowe akiomba msaada.
"Jamani nisaidieniii.... anataka kuniuaaaa... nisaidienii jamaniii... kuna mtu anataka kuniuaaaa... msaada jamani msaadaaa...."
Efraim Donald akawa anamwangalia tu kwa yale macho ya kikatili sana, akiwa amekerwa naye kupita maelezo, kisha akakiweka kifaa hicho chini na kumshika kiunoni.
"Niachie... niachie... nisaidieniii... jamani... wewe mpumbavu niachie... mkamateni jamani... mkamatenii..."
Efraim akashusha suruali ya kijana huyo mpaka magotini, moja kwa moja ikiwa na boksa yake, na kalio lake likawa nje. Joseph akaendelea kutoa kilio cha kuomba msaada, lakini kelele hizo hazikumsumbua Efraim Donald hata chembe. Hapo alikuwepo kwa ajili ya kutoa maumivu tu, na asingeondoka mpaka ahakikishe yamemwingia kijana huyo mpuuzi vyema. Kifaa hicho kilichokuwa hapo chini kilikuwa ni mashine ndogo ya kuingizia upepo wa ujazo kwenye matairi, yaani matairi ya magari! Kilikuwa chepesi kubeba, kikiwa na mtungi mdogo tu wa gesi, lakini kilikuwa na uwezo wa kuingiza upepo ndani ya tairi kwa presha kubwa, naye Efraim Donald akauchukua waya wa kupitishia upepo kisha kuuchomeka kwa nguvu kupitia tundu la haja kubwa la Joseph!
"Aaaaaaaah!" Joseph alipiga kelele ya juu sana.
"Hahahahah..." Efraim Donald akawa anacheka tu.
Mwanaume huyo kijana akaendelea kupiga kelele kwa sababu ya maumivu makali sana aliyohisi nyuma yake baada ya chuma hicho kumwingia, lakini huo ulikuwa mwanzo tu. Efraim akachukua mnyororo mdogo uliokuwa chini pia na kuuzungushia shingoni kwake Joseph, akiikaza kwa mbali na kisha kuiachia.
"Aarrgh... nisa..nizameeegh... nizameeeggh... sita... zitarudiaa... aaaaagghh..."
Joseph akawa anaomba radhi akiwa anaumia sana, lakini kufikia hapo alikuwa ameshachelewa mno kuweza kuiona huruma ya Efraim tena.
"Hahahahah... like a squeezed on the door frog! Waswahili huwa wanasema kama chura aliyebanwa na mlango. Sasa jitazame wewe mwenyewe... nataka leo ujione namna utakavyonenepa... hahahahah..."
Efraim Donald akaongea hivyo akiwa hana hata chembe ndogo ya huruma kumwelekea kijana huyo, halafu akakanyaga kifaa kile kwenye sehemu ya kukiwasha, nacho kikawaka. Kisha, akainama na kuzungusha sehemu iliyotoa upepo, na hapo kikaanza kazi yake! Joseph alipiga yowe la nguvu sana kwa kuwa alihisi maumivu yasiyo na kipimo ndani ya mwili wake. Efraim Donald akaanza kurudi nyuma huku akicheka, na upepo uliotoka kwenye mashine ile ukaendelea kumwingia mwanaume yule na kusababisha mwili wake uanze kujaa kama puto. Mnyororo Efraim alioufunga shingoni kwake Joseph ulifanya upepo uliomwingia usipite kwa kasi sana kuelekea kichwani, na mwili wa mwanaume huyo ukaendelea kutanuka na kutanuka huku sasa Efraim Donald akichukua video ya jambo hilo kwa simu yake. Tayari Joseph alikuwa amepoteza maisha baada ya dakika moja tu ya kuyahisi mateso hayo makali sana, na ndipo mwili wake wote ukalipuka na kusambaratika kwa nguvu!
Kupasuka huko kwa mwili wa Joseph kulirusha damu nyingi na vipande vingi vya nyama kutoka kwake, na hata kiasi fulani kikamfikia Efraim pale alipokuwa amesimama na kummwagikia usoni na kwenye nguo zake. Alikuwa ameelekeza uso wake juu huku amefumba macho wakati huo mwili wa Joseph umelipuka kwa kishindo, naye akajilamba juu ya mdomo wake ili kuionja damu iliyommwagikia hapo. Kisha akafumbua macho yake na kutazama pale ambapo mwili wa Joseph ulikuwa umetundikwa na kuona imebaki mikono yake tu iliyokuwa imefungwa kwa juu, naye akakaza macho yake na kuweka uso makini sana.
"Anything for you... Namouih."
Akasema maneno hayo kwa uzito, akimaanisha kwamba chochote kile kwa ajili ya mke wake atafanya tu, kisha akatoka ndani humo na kuelekea mpaka pale alipoegesha gari lake lile. Akairusha simu yake ndani ya gari na kwenda kufungua buti la nyuma na kutoa dumu dogo lenye maji, naye akajimwagia na kuanza kunawa vizuri kabisa, halafu akazivua nguo alizokuwa nazo na kuzikunja, kisha akaziweka kwenye fuko lililokuwa nyuma kwenye buti la gari hilo. Akaingia ndani ya gari na kuvaa nguo zingine za ziada alizokuwa ameweka humo, kama kawaida yake akiwa mtu wa mahesabu alielewa kila alichotakiwa kufanya kabla ya mambo kama hayo ili akimaliza aweze kurudi alikotoka bila doa lolote.
Baada ya kujiweka vizuri, akawasha gari na kuanza kuondoka sehemu hiyo, akiwa ametoka kulipa kisasi cha kifo cha mtoto Nasma kwa njia mbaya sana lakini aliyoona kuwa ya haki kwa asilimia zote. Unampa ngapi Efraim Donald?
★★★★★★★★★★★★
ITAENDELEA
★★★★★★★★★★★★
Usikose sehemu za mwendelezo wa hadithi hii kali ya CHANGE. Ni story nzuri na ndefu sana. Waweza ipata nakala yote kwa gharama nafuu sana. Karibu WhatsApp au kwa inbox ya hapa hapa JF.
WhatsApp no: +255 678 017 280
CHANGE
Story by Elton Tonny
Urafiki, Familia, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Ukatili, Mauaji, Mambo yasiyotazamiwa, Mambo yenye kuhofisha
R-rated 18+
Enjoy!
★★★★★★★★★★★★★★★★★★★
SEHEMU YA THELATHINI NA SITA
★★★★★★★★★★★★★★★★★★★
Ijumaa ilipita upesi, bila ya kuwa na mambo mengi sana ya kufanya kwa upande wake Namouih, aliyekuwa tu nyumbani hadi mume wake aliporudi. Ila kwa Blandina, ilikuwa ni siku ambayo haikwenda vyema sana baada ya kilichotokea baina yake na Draxton usiku wa kupambazia siku hiyo, na toka walipokuwa wameachana pale nyumbani mwanaume huyo hakupatikana kwa simu kabisa. Kwa mara nyingine tena Blandina alikuwa amewekwa solemba na mpenzi wake kutokana na shida isiyoeleweka vizuri iliyolitesa penzi lake, kwa hiyo kama kawaida alitakiwa tu kusubiri mpaka wakati ambao Draxton angemtafuta.
Sasa ikawa imefika Jumamosi, na ni siku ambayo Efraim Donald alikuwa ameandaa kutoa mambo mazuri kwa ajili ya ujio wa wageni muhimu hapo nyumbani kwake, yaani Zakia na Sasha. Haikuwa imewachukua muda mrefu wawili hawa kuandaa mambo waliyohitaji kwa ajili ya ujio wao huku, na ni asubuhi tu ya siku hii tayari walikuwa wameshaianza safari ya kuja jijini ili kumtembelea Namouih na mume wake; Manka akiwa ndiyo amebaki kule nyumbani kwao. Namouih alikuwa na furaha kwamba angalau angekuwa na familia yake iliyosalia hapo nyumbani kwa siku kadhaa, na jambo hili lilimsukuma hata afanye maandalizi ya vyakula vitamu sana kwa ajili yao ili wasuuzike mioyoni watakapofika.
Mida fulani ya mchana, Blandina pamoja na mama yake mdogo, yaani Natasha, wakawa wamefika hapo kwake Namouih ili kumtembelea pia kwa kifupi. Hii haikuwa mara ya kwanza Namouih kukutana na Natasha, walifahamiana kwa muda mrefu sana kutokana na urafiki wa wanawake hawa kuwa wa kitambo, na Namouih akawashukuru kwa kuendelea kumwonyesha wanamjali. Wakala pamoja naye, wakaongea pamoja naye, wakamtia sana moyo Namouih, naye akawajulisha kwamba siku yake ya kuzaliwa ingefanyiwa kumbukumbu hapo kwake kwa hiyo wanakaribishwa sana. Namouih hata akajaribu kumuulizia Draxton kwa Blandina, kwamba wanaendelea vipi, naye Blandina akasema wako poa tu. Natasha akaanza kumsimulia Namouih jinsi ambavyo Blandina anadeka sana akiwa pamoja na mwanaume huyo, nao wakawa wakicheka sana pamoja huku kihalisi Namouih akiwa ameficha kitu kizito sana rohoni.
Efraim Donald akawa amerejea nyumbani jioni ya mapema tu na kuwakuta marafiki za mke wake hapo, naye akajiunga pamoja nao na kuendeleza mazungumzo yao mpaka ilipofika mida ya saa moja jioni, ndiyo wakaaga kuondoka. Namouih na Efraim walitaka wawili hao wabaki ili wajiunge pamoja nao kwa ajili ya mlo wa jioni wakati ambao mama yake Namouih na mdogo wake wangefika, ila Blandina akagusia kwamba kuna sehemu alihitaji kumpeleka mama yake mdogo kwa wakati huo kwa hiyo wangepanga pindi nyingine ya kujumuika pamoja nao, na kwa hilo wanandoa hao wakaridhia. Wakaagana na marafiki zao vizuri mida hiyo, kisha wanandoa wakakaa kusubiri ujio wa Zakia na Sasha.
Imefika mida ya saa mbili usiku, gari maalumu lililowabeba wageni wa Namouih likawa limefika hapo nyumbani kwake na kuingia mpaka sehemu ya maegesho. Aliyekuwa akiendesha gari hilo ni mmoja kati ya wale wanaume ambao Efraim Donald aliwatumia kumkamata mwalimu Joseph kule walikotoka, aliyeitwa Wachu, lakini hakuna yeyote hapo aliyejua kuhusu hilo isipokuwa yeye na 'boss' wake. Zakia na Sasha wakashuka, wakiwa wamependeza wenyewe, na hapo nje tayari Namouih na Efraim walikuwepo ili kuwapokea. Namouih akawasogelea na kumkumbatia Sasha kwa upendo huku akikishika kiganja cha mama yake pia na kuwapa pole ya safari ndefu. Efraim Donald akawasalimu vizuri na kuwakaribisha pia, wakati huo Suleiman akiwa ametoka pia na kusaidia kubeba mizigo ya wawili hao ili ipelekwe ndani.
Namouih akaanza kuelekea ndani pamoja na mama na mdogo wake pia, wakati huo Efraim akizungumza kiufupi na Wachu. Akampatia pesa na kumwambia aondoke, na jamaa akatii. Huko ndani, Esma akawa amewakaribisha wageni vizuri sana, na hii haikuwa mara ya kwanza kwake kukutana nao maana kipindi fulani cha nyuma waliwahi kufika hapo, hivyo hata salamu zao zilijaa shauku. Namouih akawaongoza wawili hao mpaka kwenye vyumba ambavyo wangetumia, kila mmoja cha kwake peke yake, naye akawaambia wajimwagie kisha warudi kule chini ili kujumuika pamoja kama familia.
Zakia alifurahia sana mazingira ya nyumba ya binti yake, yaani kila kitu kilikuwa cha gharama na kilipangiliwa vizuri sana. Sikuzote alitamani kuishi namna hiyo, na kujua binti yake aliishi maisha yaliyoonekana kuwa ya starehe kama hivyo kulimfanya awe na kiwango fulani cha wivu mzuri wa kutaka kuendelea kujiachia ndani yake, hata kama ingekuwa ni kuyaonja kwa muda mfupi. Sasha yeye alikuwa mpole tu kama kawaida yake, akiwa anahisi amani kuwa huku karibu na dada yake tena ingawa kuna mambo fulani alikuwa akimficha. Ni mambo mengi yaliyokuwa yametokea hapa katikati lakini hakuwa amesahau kuhusiana na lile suala la mpenzi wake kumwibia pesa na kutokomea kusikojulikana. Kwa kuwa alimwomba msaada kaka-mkwe wake juu ya hilo na kuupata, ijapokuwa alimdanganya kwa kutunga kisa cha uwongo, angalau alihisi amani fulani moyoni kujua hilo lilikuwa limeshapita, kwa hiyo angejitahidi kuelekeza fikira zake kwenye kufanya ujio wake huku ulete furaha tu kwa dada yake.
Basi, baada ya wawili hao kumaliza kujisafisha na kwenda kujiunga pamoja na Namouih, walimkuta akiwa anasaidizana na Esma kuandaa meza ya chakula, na wakati huu Efraim Donald alikuwa sehemu ya nje akizungumza na Suleiman. Zakia na Sasha wakaketi masofani huku Namouih akiwasemesha kuhusiana na mambo ya hapa na pale, kisha baada ya kumaliza kuandaa meza vizuri akatoka hapo ili kwenda kumwita mume wake kwa ajili ya chakula. Alipofika nje ya mlango, aliweza kutambua kwamba Efraim alikuwa anamsemesha Suleiman kwa njia fulani ya ukali kidogo, naye akamwita na kuwaambia wote waingie ndani ili wapate chakula. Efraim Donald akatabasamu na kusema wanakuja, akijifanya kama kila kitu kiko sawa, naye Namouih akaona apuuzie tu hayo mambo ya wanaume na kurudi ndani.
Efraim Donald akamwangalia Suleiman na kusema kwa sauti ya chini, "Hakikisha unaenda na haurudi tena kwangu bila kuwa na kichwa cha huyo mshenzi, unanielewa?"
Suleiman akatikisa kichwa kukubali, naye Efraim akageuka na kuanza kuelekea ndani tena huku akifuatwa naye.
Wawili hao walikuwa wanazungumzia suala lile la mtu aliyekuwa anatoka kimapenzi na mke wake Efraim. Suleiman ndiye aliyekuwa anakaa na kifaa cha kumwonyesha camera ile ya mtego aliyoiweka kule kwenye nyumba ya msituni, na leo baada ya kukiangalia alitambua kwamba kilikuwa kimeharibiwa. Kwa sababu ilikuwa ni camera ya kurekodi, alitazama matukio yaliyopita na kuona namna ambavyo mwanaume fulani aliyejificha sura kwa nguo alipofika na kuinyofoa na kuipasua kabisa. Alijaribu kutazama umbo la mwanaume huyo kwa umakini lakini hakuweza kugundua ni nani, na ndiyo sasa alikuwa amepata nafasi ya kumwambia 'boss' wake, maana alikuwa na mambo mengi.
Efraim Donald alikuwa amekasirika sana, akielewa kwamba mtego wake huo mdogo ulikuwa umeshampa mbaya wake tahadhari, na bado hakuitambua sura yake. Kwa hiyo hapo alikuwa anamwamuru Suleiman ahakikishe anakwenda kule tena upesi, labda kesho, ili afanye jambo fulani litakalomlazimu huyo mtu ajikamatishe tu halafu ndiyo amuue. Alimpa maagizo ya kuwa makini sana, hakutaka kumpoteza tena huyo mpuuzi hasa kwa sababu alionekana kuwa mwerevu, na ndiyo Suleiman akawa ametii juu ya hilo.
Efraim akajitahidi kuvaa ngozi ya kondoo na kwenda kuketi mezani pa chakula ili wale pamoja na familia yake ya ukwe. Alimwongelesha Zakia kwa staha sana, hata Sasha pia. Yaani hakuna mtu mwingine hapo ambaye angeweza hata kukisia kwamba mwanaume huyo alikuwa wa rangi tofauti kabisa na ile aliyoionyesha kwa nje isipokuwa Suleiman pekee. Baada ya mjumuiko huo wa pamoja, wote wakaendelea kupata maongezi ya hapa na pale ili kupatana kimawazo na kupisha muda, kisha wakaelekea vyumbani kupumzika.
★★
Basi ikawa imefika mida ya saa saba usiku, Sasha akiwa amelala chumbani kwake hakuweza kupata usingizi haraka tokea alipoingia kitandani, naye akawa amefikiria labda angetakiwa kunywa maji kidogo ili aendelee kupambana kuutafuta. Alikuwa amemaliza kutumiana jumbe za kirafiki na kuperuzi mitandao ya kijamii dakika chache nyuma, na kiukweli bado jambo lile lililompata baada ya mpenzi wake kumsaliti na kumwibia pesa nyingi ambazo alikuja kufidishia kwa kumdanganya Efraim Donald kuhusu rafiki yake anayeumwa, ni kitu kilichokuwa kinamkosesha amani kwa kadiri fulani. Kwa sababu ya jambo hilo alijiona kuwa mnafiki wa hali ya juu, hasa kumwelekea Namouih, ambaye hakutambua lolote kati ya mambo yote hayo. Lakini kwa sababu muda ulikuwa umepita na wakati huu familia yao ilikuwa ikijitahidi kurudisha uimara baada ya kifo cha Nasma, aliona ni vyema kuliacha jambo hilo lipite tu, na yeye angejitahidi kulisahau.
Akaamua kushuka kitandani na kuelekea mpaka kule chini ili achukue maji kidogo kupoza koo yake. Alipofika sehemu ya jikoni na kuingia, akashtuka kiasi baada ya kumkuta Efraim Donald hapo, akiwa amesimama karibu na friji huku ameweka glasi kwenye kibonyezeo cha kutoa maji. Sasha akatulia kidogo na kumtazama kwa umakini. Taa hazikuwa zimewashwa, lakini aliweza kumwona kwa usahihi kabisa, akiwa amevalia nguo nyepesi ya kulalia iliyotoka juu ya mwili wake mpaka chini moja kwa moja. Alikuwa amempa mgongo, na kwa sababu hakugeuka, Sasha akafikiria kwamba hakuwa ameonwa hivyo akataka kurudi sehemu ya sebule ili ampishe kwanza, na ile amerudi nyuma kidogo tu....
"Sasha..."
Efraim Donald akaita hivyo. Binti alikuwa ameshika kingo ya mlango wa kuingilia ndani hapo, naye akatulia kidogo na kugeuka kumtazama. Efraim Donald hakuwa hata amemgeukia Sasha, akionekana kukinga maji bado, naye Sasha akaona aitike.
"Bee..."
"Unakosa usingizi?" Efraim akauliza.
"Aa... ahah... hapana, nilikuwa nimekuja kuchukua maji kidogo...."
Maneno ya Sasha yakakatishwa baada ya Efraim Donald kumgeukia. Binti alianza kumwangalia kwa aibu kiasi, kwa sababu kaka-mkwe wake alionekana sasa akiwa kifua wazi, na akiwa amevaa boksa nyeusi pekee mwilini tofauti na hicho kinguo chepesi alichokivalia mabegani. Akaangalia chini kidogo, naye Efraim akasogea pembeni ya friji.
"Njoo uchukue," Efraim Donald akamwambia.
Sasha alihisi aibu, lakini haikuonekana kama kaka-mkwe wake huyo alikuwa na tatizo hivyo yeye binti akaanza kuelekea hapo kwenye friji. Alionekana kubabaika kiasi kutoka kwenye fikira za kile alichohitaji, naye Efraim akamwambia pa kuchukulia glasi, hivyo akafata na kuja kuanza kukinga maji kwenye friji. Kwa kuwa Efraim Donald alikuwa pembeni yake, Sasha akawa anamwangalia kwa kuibia na kumwona alipokuwa akinywa maji yake taratibu, na ndipo akashtuka baada ya kupitiliza kuweka maji kwenye glasi kwa sababu ya kuzubaa, nayo yakaanza kumwagika.
Akatoka hapo na kuiweka glasi pembeni, kisha akatafuta kitambaa na kuanza kupafuta hapo kwenye friji huku akimwangalia Efraim kwa woga kiasi, na sasa kaka-mkwe wake alikuwa anamtazama pia.
"Uko sawa Sasha?" Efraim akauliza.
"Ndiyo... samahani... nilizubaa tu..." binti akasema.
"Inaonekana una mambo mengi kichwani," Efraim Donald akamwambia.
Sasha akatabasamu haraka na kushuka chini ili apafute pia, lakini akakumbuka kwamba hicho kilikuwa kitambaa cha kufutia vyombo na siyo chini, hivyo akanyanyuka ili atafute mfagio wa kudekia. Efraim akawa anamwangalia kwa umakini tu, jinsi ambavyo alikuwa anababaika mara huku, mara kule, mwishowe akamwambia atulie.
"Acha tu Sasha... Esma atapatengeneza kesho," Efraim akasema.
"Hapana, ngoja tu nipasafishe, niko careless kweli," Sasha akasema.
"Hamna, hauko careless. Ni vitu vingi vinakuchanganya I know," Efraim akamwambia.
Sasha akawa amemaliza kufuta sasa, naye akampita Efraim na kuweka ufagio huo pembeni, kisha akayarudia maji yake tena na kuanza kunywa. Alipomaliza, akakuta kaka-mkwe wake anamtazama tu kwa umakini, naye akaweka glasi pembeni na kuanza kuondoka.
"Usiku mwema kaka," Sasha akasema na kumpita Efraim.
"Sasha..."
Efraim Donald akaita hivyo kwa sauti ya chini, naye Sasha akasimama kwanza. Akageuka taratibu na kumtazama tena usoni.
"Rafiki yako anaendeleaje?" Efraim Donald akauliza.
Sasha akabaki kimya tu. Hakuwa ametarajia kabisa kwamba Efraim angeuliza swali hilo wakati huu, naye akabaki tu kumwangalia.
"Wameweza kuitibu saratani?" Efraim akauliza tena.
Sasha akaacha kuzubaa na kusema, "Ndiyo... wame... wamemtibu."
"Kwa hiyo anaendelea vizuri?"
"Ndiyo."
Efraim Donald akatabasamu kwa chini, na kiukweli jambo hili likaanza kumtia wasiwasi mwingi huyu binti.
"Vipi kuhusu Shomari... amesharudi?"
Sasha alihisi kama kitu fulani kikiruka ndani ya kifua chake kwa nguvu, na mapigo yake ya moyo yakaanza kwenda kasi. Swali hilo moja tu lilimaanisha kwamba kaka-mkwe wake alijua kila kitu. Kama alimjua Shomari, basi ilimaanisha alijua wazi kabisa kwamba kila kitu ambacho Sasha alimwambia siku ile ili apate pesa kilikuwa ni uwongo. Woga wa hali ya juu ukamwingia mwanadada huyu, naye akabaki kumtazama tu Efraim kwa hofu.
"Hautaniuliza nimemjua vipi Shomari?" Efraim akamuuliza.
Sasha akabaki kimya tu.
"Unajua kwa nini watu wengi wanaofanya mabaya hufanikiwa zaidi ya wale wanaojifanya ni wazuri sana? Ni kwa sababu wao huwa ni waongo wazuri. Wewe Sasha... siyo mwongo mzuri... ndiyo maana haukufanikiwa kunidanganya," Efraim Donald akasema hivyo.
Sasha akaangalia chini, mapigo ya moyo yakiendelea kumkimbia kwa kasi.
Efraim akaanza kumfata huku akisema, "Usiogope Sasha... mimi sijakuhukumu kwa sababu ulinidanganya. Wewe ni binti mwenye akili sana kama dada yako tu, ndiyo maana nilishangazwa kidogo baada ya wewe kutumia njia isiyokuwa na utimamu kunidanganya. Ungetafuta kisingizio kingine lakini ukaona useme saratani... kwa nini? Ili kunikumbusha kuhusu baba-mkwe wangu?" Efraim akaongea hivyo.
Sasha akawa anatikisa kichwa kukataa, huku machozi yakianza kuvizia macho yake, naye Efraim akawa amemkaribia zaidi.
"Jambo ulilofanya halikuwa zuri Sasha. Ulidanganya kuhusu maisha ya mtu mwingine ili tu upate laki tisa?" Efraim akasema.
Sasha akaangalia chini.
Efraim Donald akashusha pumzi na kusema, "Kiukweli niliumia sana. Ila nilikupa milioni mbili kwa sababu nilitaka kukusaidia wewe na siyo kisingizio ulichonipa, kwa hiyo kwa hilo usiwe na wazo dear. Ila kama wewe ungekuwa mimi baada ya kudanganywa hivyo... ungejifanya nini?"
Sasha akamwangalia usoni.
"Nikimwambia Namouih itakuwa jambo sahihi?"
Sasha akamshika kiganjani huku akitikisa kichwa kukataa, naye Efraim Donald akauangalia mkono wa binti.
"Hutaki nimwambie dada yako? Sasa utafanya nini ili kulipia uwongo wako kwangu?" Efraim akauliza.
Sasha akakiachia kiganja chake na kubaki amemwangalia machoni tu.
"Niambie..." Efraim akasema.
Sasha akatikisa kichwa kukanusha, kisha kwa sauti ya chini akasema, "Sina chochote cha kukupa kaka."
"Ouh lazima kuwe na kitu Sasha. Please recall maneno yako. 'Nitakulipa tu kaka, upende usipende.' Ninataka niyapende hayo malipo Sasha... na hiyo ndiyo itakuwa ransom ya kilichotokea kwa sababu ya wewe kunidanganya," Efraim Donald akasema.
Sasha akaendelea kumtazama tu usoni akihisi kuchoka sana kihisia. Hivi siyo alivyotarajia kabisa safari yake ya kuja huku kwa dada yake kugeuka. Usiku mmoja tu hapo tayari mambo yakawa yamevurugika.
"Hauna clue ya kile nachotaka unipe Sasha? Ngoja nikwambie..."
Efraim akasema hivyo, kisha akaanza kumsogelea Sasha karibu kabisa na aliposimama. Binti akaanza kurudi nyuma taratibu mpaka hatua zake zilipozuiwa na kuta ndogo ya vigae vya sinki kubwa lilikokuwa katikati ya sehemu hiyo ya jikoni, naye Efraim akamkaribia mpaka karibu kabisa na uso wake. Sasha alikuwa na wasiwasi mwingi. Huu ulikuwa ni usiku wa manane, nyumbani kwa dada yake, halafu mume wake akawa anaomba kitu fulani ambacho binti huyu alielewa wazi kilikuwa cha marufuku kabla hata hajaambiwa ni nini. Kwa kuwa ni kweli alimdanganya Efraim, hapa Sasha aliona kabisa kwamba hakuwa na njia ya kutoroka.
"Nisingehitaji kitu kama hiki kutoka kwako Sasha... lakini naweza kusema haya yote ni makosa yako. Ulipochuchumaa kuokota cheque siku ile my Goood... girl you are so sexy," Efraim akamwongelesha binti karibu na mdomo wake.
Sasha akamwangalia kimaswali kiasi.
"Ndiyo. Ulipochuchumaa nilikuona. Ilikuwa ni kama... hhh... harufu yako nyuma iliingia puani mwangu yaani... so sweet," Efraim akaongea kwa njia ya utongozi.
Wakati huu, mwanaume huyu alikuwa amepitisha mkono wake kiunoni kwa Sasha taratibu, naye Sasha akaibana midomo yake na kufumba macho.
"Mmmm... unanukia vizuri sana..." Efraim akasema hivyo huku akizungusha pua yake shavuni kwa Sasha.
"Kaka... mbona... lak... mi... naogopa... dada ata... atajua..."
"Hapana Sasha, ondoa hofu. Namouih hawezi kujua lolote..."
"Kaka... unahitaji nikupe nini... nimebakiza pesa nyingi tu... nitakupa... niki... nikija kuanza kazi nita...."
"Ahahahah... usiwe na hofu, mrembo wangu. Pesa ipo tu. Cha muhimu wakati huu... ni mimi na wewe," Efraim akamwambia hivyo na kuushika uso wake.
Sasha aliogopa sana. Kuwa karibu na uso wa shemeji yake ni jambo ambalo hakuwahi kutazamia, na angeweza hata kutoka hapo na kukimbia upesi, lakini njia ya Efraim Donald yenye mtego mkali sana ilikuwa imemnasa binti huyu sehemu hiyo na kumfanya asiweze kujongea kabisa; yaani alikuwa kama ameishiwa nguvu. Binti alikuwa amevaa T-shirt nyepesi sana na suruali ya kulalia, hivyo Efraim akauingiza mkono wake ndani ya T-shirt hiyo na kuushika ubavu wa Sasha, akiusugua taratibu huku amemwangalia machoni.
Kisha mwanaume huyu akaanza kumlamba Sasha sikioni, taratibu, akishuka mpaka shingoni na kupalamba, naye Sasha akawa ameipindisha tu shingo yake huku machozi yakimtoka. Halafu mwanaume akamfata binti mdomoni na kuanza kumdendesha kwa uzito, huku mkono wake uliokuwa ubavuni kwa binti ukiwa umeshapanda kufikia kwenye kifua chake laini na kuanza kuzungusha kiganja chake hapo. Sasha alikuwa akizipokea busu za Efraim huku amefumbua macho yake, kama vile hahisi chochote kabisa, naye Efraim akaacha kuibusu midomo hiyo na kumwangalia usoni. Akampa tabasamu fulani hivi la hila, naye Sasha akawa anamtazama kwa kufadhaika.
"Its okay. I understand the toll. Lakini nakuahidi... utafurahia sana mambo nayotaka kukuonyesha..."
Efraim Donald akamwambia hivyo huku akizivuta-vuta nywele za binti, kisha akamshika mabegani na kuanza kumkandamiza kuelekea chini, naye Sasha akashuka mpaka chini na kuwa kama amekaa kwa kuchuchumaa, yaani akiegamia sinki lile. Akawa anamwangalia Efraim Donald usoni huku akiwa amevurugika kihisia, akielewa vizuri sana kile ambacho kingefuata, na mwanaume huyo akaona asimcheleweshe. (........)
"You turn me on so bad. Nahitaji joto la midomo yako na msuguo wa meno yako mrembo wangu. Nipe nachohitaji... nami nitakupa unachostahili mama," Efraim akasema maneno hayo kwa sauti tulivu.
Sasha alikuwa anamtazama kwa njia fulani legevu sana, naye Efraim akakishika kichwa chake kwa nyuma (.........).
"Come on," Efraim Donald akasema hivyo kwa ushawishi, naye Sasha akaufungua mdomo wake kwa kusita sana.
(........).
(........).
"Hiyo ilikuwa nzuri sana mrembo wangu. Sasa ni zamu yako."
Sasha akatikisa kichwa kukanusha kile ambacho Efraim alitaka kufanya kutokana na kuyaelewa maneno yake, lakini mwanaume huyo akatabasamu tu (.......).
(.......).
Sasha alikuwa akiangalia mlangoni kwa wasiwasi mwingi akihisi kwamba huenda dada yake, mama yake au Esma angefika hapo, (.......).
(........).
(........).
(........).
Chumbani, Namouih akawa ameshtuka kifupi kutoka usingizini, kisha akajigeuza ili aendelee kuutafuta usingizi. Lakini jicho lake zito la usingizi likamwonyesha kwamba mume wake hakuwa kitandani, naye akageukia upande wa sehemu ya bafuni kupaangalia, lakini taa haikuwa imewashwa kwa hiyo akaelewa kwamba hakuwa humo. Kwa kufikiri kwamba mume wake alikwenda chini kupata maji, mwanamke huyu akaamua kuendelea tu kupiga usingizi. Wakati huu sasa kule jikoni, Efraim alikuwa amemgeuza Sasha kwa nyuma, yaani binti alikuwa amempa mgongo huku akiegamia sehemu ile yenye sinki kwa kulaza tumbo na kunyanyua mguu mmoja hewani, halafu mwanaume akawa anakula raha zake kutokea nyuma. Sasha alikuwa anaguna kwa njia ya taratibu yenye deko nyingi, kama tu Namouih, huku macho yake yakiwa yamelegea sana na akihisi raha nyingi ambayo ilikuwa imelazimishwa kutoka ndani yake.
Harakati ya kuutafuta usingizi kwa mara nyingine ikamgomea Namouih kwa kuwa alianza kusikia sauti ambazo hakuzielewa vizuri. Akajinyanyua na kuketi, kisha akaichukua simu yake na kutazama muda; saa tisa. Akaweka umakini wake zaidi ili kujua zilikuwa sauti za nini lakini hakuweza kutambua kwa urahisi. Akaamua kushuka kutoka kitandani ili kwenda kuangalia ni jambo gani ambalo mume wake alikuwa anafanya huko au sauti hizo zilitokea wapi, na hata kumbukumbu ya ile ndoto mbaya sana aliyoota usiku ule yeye na Blandina wamemgonga Draxton kwa gari ilikuwa akilini mwake kutokana na namna ambavyo mazingira yale ya ndoto yalitaka kuendana na hali hii ya sasa.
Akatoka chumbani kwake kwa ujasiri na kutembea kuelekea kingo za ngazi, naye akaangalia kule chini na kuona kwamba hakukuwa na taa yoyote iliyowashwa. Sauti alizokuwa amesikia ziliendelea kusikika, naye akatambua zilikuwa ni za mtu au watu lakini hazikueleweka vyema, hivyo akaamua kutowasha taa ili aende kuona mume wake alikuwa akifanya nini huko chini. Akashuka ngazi taratibu na kuangaza huku na huko, kisha akaamua kuelekea sehemu ya jikoni. Alipoingia tu hapo, akamkuta Efraim Donald akiwa amesimama usawa wa sehemu ile yenye sinki huku akitazama kifaa chake cha tablet, ikionekana alikuwa anatazama video fulani hapo.
Namouih akamwangalia kwa umakini sana, kisha akaingia ndani hapo. "Efraim..." akaita.
Efraim Donald akamgeukia, naye akatoa tabasamu hafifu tu na kuendelea kumwangalia.
"Mbona uko huku?" Namouih akauliza.
"Nilikuwa nimekosa usingizi... ndiyo nikaona nishuke tu kunywa maji," Efraim akasema.
Namouih akakitazama kifaa kile Efraim alichoshika mkononi, kisha akamwangalia usoni kwa udadisi.
"Nilikuwa tu naangalia video za ndugu yangu... aliyekufa kwenye ajali. Nimemkumbuka sana, ni miaka mingi... nimemuota dakika chache nyuma... ilikuwa ni kama nimetoka kumwona live," Efraim Donald akaongea kwa hisia.
Namouih akaangalia chini, kisha akasema, "Pole. Una... unahitaji muda wa kuwa peke yako labda...."
"Oh no, twende tu tukalale... nilikuwa napanda tu sasa hivi," Efraim akasema na kuanza kumwelekea mke wake.
Namouih alikuwa anamwangalia kwa mashaka kiasi, kama vile kujua kwamba kuna kitu mume wake alikuwa anaficha hapo, lakini hakuona haja ya kuumizwa kichwa kwa sababu hata yeye alikuwa na yake aliyoficha. Efraim Donald akamkaribia na kumshika kiunoni, nao wakaanza kwenda pamoja kuelekea juu huku Efraim akimsimulia kwa uwongo kuhusu ndoto aliyosema ameota. Chini ya sehemu ile ya sinki kwa upande mwingine, binti Sasha alikuwa amejibana kwa hapo huku ameuziba mdomo wake kwa viganja, na alikuwa akilia sana. Ni muda mfupi tu nyuma alikuwa ametoka kutandikwa penzi la lazima na kaka-mkwe wake, na lilikuwa limekatishwa na Efraim baada ya yeye kutambua kwa machale yake ya hali ya juu kwamba Namouih alikuwa anakuja. Mzee wa mahesabu tayari alikuwa na njia mbadala ya kujihami, hivyo akamficha binti na kukaa kuigiza alikuwa anatazama video.
Binti Sasha alijihisi vibaya sana. Alihisi ni kama amechafuka mno na hakukuwa na njia ya kuweza kujisafisha tena. Baada ya kilichotokea kati yake na mume wa dada yake usiku huu, nini kingefuata? Vipi kama mama yake angejua? Vipi kama dada yake angejua? Alijiuliza sana. Akajilaza hapo hapo huku akiendelea kulia sana mpaka inafika saa kumi usiku, ndiyo akajitahidi kunyanyuka na kurudi kwenye chumba chake taratibu. Nani alipaswa kulaumiwa?
★★★★★★★★★★★★
ITAENDELEA
★★★★★★★★★★★★
Usikose sehemu za mwendelezo wa hadithi hii kali ya CHANGE. Ni story nzuri na ndefu sana. Waweza ipata nakala yote kwa gharama nafuu sana. Karibu WhatsApp au kwa inbox ya hapa hapa JF.
WhatsApp no: +255 678 017 280
Mkuu ukisoma vizuri alianza kumpa maji kujisukutua kama mara tatu na pia mtu mwenyewe Mwamba Efraim kinyaa anakipata wapi?Daaah! We jamaa,atakama ni ficition story,yani mtu atoke kutapikiana uko haraf upate ujasir wa kumpiga denda,realy???, apa alipaswa kupewa chakula 2, na siyo denda bwana. Jaribu kukumbuka kile ulichokisimulia nyuma bwana
Mbona kama haujasoma vizuri Mkuu ?😄Daaah! We jamaa,atakama ni ficition story,yani mtu atoke kutapikiana uko haraf upate ujasir wa kumpiga denda,realy???, apa alipaswa kupewa chakula 2, na siyo denda bwana. Jaribu kukumbuka kile ulichokisimulia nyuma bwana
🙏 Mheshimiwa Elton Tonny 😂😂😂CHANGE
Story by Elton Tonny
Urafiki, Familia, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Ukatili, Mauaji, Mambo yasiyotazamiwa, Mambo yenye kuhofisha
R-rated 18+
Enjoy!
★★★★★★★★★★★★★★★★★★★
SEHEMU YA THELATHINI NA SABA
★★★★★★★★★★★★★★★★★★★
Asubuhi ikafika, ikiwa ni siku ya Jumapili. Wanandoa Efraim Donald na Namouih waliamka mida ya saa tatu na kukaa kwa ufupi kitandani kuzungumzia kuhusu sherehe ndogo ya kuzaliwa Namouih, hasa kuhusiana na marafiki ambao mwanamke huyu alikuwa anataka wawepo. Ingawa Namouih alichangia kuongelea mambo aliyopenda yafanywe, Efraim aliona wazi kwamba mke wake aliongea vitu ili kumridhisha tu, na akili yake haikuwa kwenye jambo hilo kabisa. Pamoja na hayo, Efraim Donald akaendelea kufanya mchezo wake wa kuwa mume mzuri ili aendelee kupoteza muda na Namouih kwa ajili ya malengo yake binafsi.
Muda mfupi baada ya hapo, wawili hao wakaelekea chini kule ili kwenda kupata kiamsha kinywa, na tayari Zakia, Esma na Sasha walikuwa wameamka na kuendelea na mambo mengine. Esma kama kawaida alikuwa amemaliza kuandaa mahanjumati ya asubuhi, na alikuwa amepewa msaada na Sasha katika jambo hilo leo. Lakini baada ya Namouih kumsalimu Sasha, aliona jinsi mdogo wake alivyoonekana kukosa raha, naye akamuuliza ikiwa alikuwa na tatizo. Sasha hata hakumwangalia dada yake usoni alipomwambia kwamba hakuwa na shida yoyote ile, naye akaelekea tu upande mwingine na kuwaacha wakubwa wakiongea. Efraim Donald alikuwa anaongea na mama-mkwe wake kwa urafiki mpaka wote walipoketi mezani kwa ajili ya kupata chai. Namouih akawa anamwangalia mdogo wake na kuona namna ambavyo alikuwa ametulia mno, kupita kiasi, yaani alikuwa amenyong'onyea kuzidi ile hali ya kawaida. Alikuwa ameweka chai tu kwenye kikombe lakini hakutoa vitafunwa.
"Sasha... mbona huweki mkate?" Namouih akauliza hatimaye.
Sasha akamwangalia tu usoni na kutazama chini tena.
"We' dada yako si anakusemesha, mbona unaleta ujeuri?" Zakia akasema hivyo kwa uthabiti kiasi.
Namouih akamwangalia mama yake kama kusema hakuhitaji aongee kwa niaba yake, kisha akamtazama mdogo wake na kusema, "Sasha, weka chakula ule."
"Hapana dada. Nitakunywa chai tu," Sasha akaongea.
"Kwa nini?" Namouih akauliza.
Sasha akamwangalia tu.
"Unaumwa Sasha?" Efraim Donald akauliza swali hilo.
Sasha akaendelea kubaki kimya tu huku sasa akiangalia chini.
"Niombe radhi kwa ajili yake, Sasha siyo mwongeaji sana. Ni ugeni kama unavyojua," Zakia akamwambia Efraim.
"Usijali, naelewa. Nadhani ni uchovu wa safari pia," Efraim Donald akasema.
Namouih akaendelea kumwangalia mdogo wake kwa kujali. Alihisi kabisa kwamba kuna kitu kilikuwa kinamsumbua maana hivi siyo alivyokuwa jana walipoagana kwenda kulala.
"Honey, kwa kuwa leo hatuna kazi vipi tukifanya matembezi ya split?" Efraim Donald akamwambia Namouih.
Namouih akamwangalia na kuuliza, "Unamaanisha?"
"Vipi ukienda na mama kumpa tour hapa na pale, halafu mimi niende na Sasha... then kesho tufanye vice versa?" Efraim akasema.
Sasha akamwangalia Efraim kimaswali kiasi.
"Yaani leo niende kutembea na Namouih halafu kesho na wewe?" Zakia akamuuliza Efraim.
"Mmmm..." Efraim akatoa mguno wa kukubali.
"Aa... kwa leo...."
"Vipi una mipango mingine?" Efraim akamkatisha Namouih.
Namouih akabaki kimya, kwa sababu ni kweli alikuwa na mpango wa kutoka baada ya kunywa chai ili aweze kumtafuta mtu aliyempatia burudisho ambalo mume wake hakumpa, yaani Draxton, kwa kuwa zilikuwa zimepita siku chache bila ya wawili hao kufanya hata mawasiliano. Alikuwa amemkosa sana mwanaume huyo.
"Ha..pana... sina mipango... ila..."
"Wonderful! Ninajua itapendeza sana mki-bond na Zakia, unajua kuna sehemu nzuri sana huku ambazo Namouih atakuonyesha yaani utafurahia sana mama..." Efraim akamwambia Zakia.
Zakia akatabasamu kwa furaha na kumwangalia Namouih, lakini binti yake alionyesha kutopendezwa sana na wazo hilo ila ikawa kama limetiwa tiki kwa shingo upande.
"Sisi pia tutaenda kutembelea sehemu nzuri Sasha... nyingi tumeshaenda na Esma pia, utafurahia," Efraim akamwambia Sasha.
Sasha akamwangalia Namouih na kusema, "Mimi... nitabaki tu... sijisikii kwenda...."
"Sasha nawe unapaswa ukatembee bwana. Uchovu wa safari sidhani bado unasumbua sana mbona me niko safi kabisa? Em' kubali, ujiandae tukatembee," Zakia akamsisitizia.
Sasha akamwangalia dada yake kwa njia fulani kama anahitaji amuunge mkono katika ombi lake la kutotaka kwenda.
Namouih mwenyewe akiwa amehisi kukerwa na wazo la kwenda na mama yake, akamtikisia tu kichwa Sasha mara moja kama kusema akubali ili kumridhisha mama yao.
Sasha akamtazama Efraim kwa ufupi na kuona namna mwanaume huyo alivyomwangalia kwa umakini, na tabasamu la pembeni likaonekana midomoni mwake kuonyesha jinsi alivyofurahia kumwonyesha hila zake waziwazi. Namouih akaangalia simu yake kuona kama Draxton alituma ujumbe wowote, lakini haikuwa hivyo. Akamaliza kula haraka kabla ya wote na kuamua kwenda chumbani kuanza kujiandaa, kwa kuwa Zakia tayari alikuwa amejisafisha na kuvaa vizuri kabla hata ya wazo la kwenda kutembea halijatolewa. Sasha akamaliza chai yake na kwenda chumbani pia ili ajiandae kwa kuwa mama yake alikuwa anamsukuma mno kuwahi, na hapo wakawa wamebaki mtu na mama-mkwe wakipiga story.
★★
Asubuhi hii, Suleiman alikuwa amekwenda kule kwenye nyumba ya msituni ili kuhakikisha anammaliza kabisa mtesaji wa penzi la 'boss' wake, hasa kwa kuwa Efraim Donald alimtaka arudi akiwa na kichwa cha mtu huyo. Suleiman hangejali ni nani ambaye angekutana naye huko, yaani alitakiwa kumshika na kumuua, kisha arudi kwa mkubwa wake akiwa na jambo ambalo lingempa tabasamu. Aliendesha gari kwa umakini, akiwa pia hajasahau kwamba mtu anayekwenda kushughulika naye alionekana kuwa na akili sana hivyo na yeye Suleiman angepaswa kujiweka katika utayari wa lolote lile ili aweze kufanikiwa. Kama angemkuta mtu huyo, huu ndiyo ungekuwa mwisho wake, kituo kikuu. Lakini kama asingemkuta, basi angekaa kumsubiri mpaka afike sehemu hiyo na kutekeleza alichoagizwa kufanya. Huyu ndiyo alikuwa kikaragosi mtiifu.
Alipofika eneo la karibu zaidi na nyumba ile, aliweza kuliona gari jeusi likiwa limeegeshwa usawa wa nyumba, naye akalisimamisha lake mbali kiasi ili aweze kwenda pale kwa tahadhari; ikimaanisha atembee. Akashuka, huku akiwa ameshikilia bastola yake mkononi, kisha akaanza kwenda taratibu mpaka alipofika kwenye mti mmoja wa karibu na kujibanza hapo. Alilitazama gari hilo na kuanza kufikiria ikiwa angetambua mmiliki wake ni nani, ila haingekuwa rahisi maana ni wengi waliokuwa na magari ya aina kama hilo kwa hiyo ingeweza kuwa yeyote. Kuona kwamba mtu huyo aliendelea kuwepo hapo licha ya kukuta amewekewa mtego wa camera juzi kulimaanisha alikuwa anajiamini sana, naye Suleiman akawa anajishauri ikiwa aende kwenye nyumba hiyo moja kwa moja au atulie kusikilizia hali.
Lakini hazikupita dakika nyingi na mlango wa kuingilia kwenye nyumba ile ukafunguka, na ndipo sasa akaweza kumwona mtu aliyetakiwa kuwa mlaji wa keki ya 'boss' wake. Suleiman hakuweza kujizuia kushangaa. Alimtazama Draxton, akiwa amevalia nguo za kawaida kabisa kama mwenyeji wa huo msitu, naye akatabasamu kwa kutoamini kama kweli mwanaume huyo ndiyo alikuwa anakula mali ya Efraim Donald. Alijua kwamba Draxton ni mpenzi wa rafiki wa karibu wa Namouih, na kwa kiasi fulani alifikiri Namouih hata hakupendezwa naye, ila sasa tamthilia iliyokuwa mbele yake ilielekea kuwa yenye kuburudisha zaidi kuliko alivyodhani.
Draxton alikuwa ametoka nje hapo siyo kama vile anatoa uchafu labda, ila ni kwa sababu masikio yake yenye uwezo wa hali ya juu wa kusikia yalipigwa na mawimbi ya mbali akiwa ndani ya nyumba yaliyomwambia kwamba kuna gari lilikuwa limekaribia eneo lake. Kwa hizi siku mbili tokea aliporudi huku na kukuta amewekewa mtego, hakuwa ameondoka kwenye nyumba hiyo kabisa, na sasa akiwa hapo ndani baada ya kusikia mngurumo wa gari na kuona halijafika karibu zaidi, alitambua mmiliki wake hakuwa Namouih, bali adui. Alikaa kwa muda mfupi ndani kuona nini kingefuata bila kukipata, hivyo akaamua kutoka nje kwa ujasiri ili kuweza kukipata. Akatoka sehemu ya mlangoni na kulielekea gari lake, na kabla hajalifikia, akasimama kwanza huku ametazama chini kwa umakini.
Suleiman alikuwa anamtazama huku bado akiwa amejibanza nyuma ya mti kwa uangalifu, naye akawa anamsoma mwanaume huyo bila kutambua kwamba yeye tayari alikuwa ameshasomwa. Draxton alikuwa ameivuta harufu ya kibinadamu ya Suleiman, na kwa haraka akawa ametambua ni nani, na yuko upande gani. Akafumba macho yake na kushusha pumzi, kisha akapiga hatua chache akilikaribia gari lake na kusimama huku anautazama mti ambao Suleiman alikuwa amejifichia.
"Vipi ukitoka hapo ulipo ili tuongee vizuri?"
Maneno hayo yalisemwa na Draxton, na kwa kiasi kikubwa Suleiman akawa ameshangaa namna gani mwanaume yule aliweza kutambua kwamba yeye yuko hapo. Ila hiyo haikujalisha tena. Suleiman akavaa ujasiri wake wa kikatili na kutoka hapo kwenye mti, kisha akaanza kuelekea sehemu ile aliyosimama Draxton huku akitembea kwa kujiamini na bastola yake mkononi.
"Una mambo mengi we' kijana. Yaani mimi huwa ni mgumu kushangazwa na vitu kama hivi ila wewe leo umejitahidi," Suleiman akamwambia.
Draxton akawa anamwangalia kwa macho yake makini sana.
"Sijaja kuongea mrembo. Ila kama wewe una cha kusema unaweza kuongea," Suleiman akasema.
"Kwa nini uko hapa?" Draxton akauliza.
"We' hujui?"
"Nisingeuliza."
"Unajifanya una akili sana eti? Ulitumia dawa gani kumroga bibi wetu?"
"Ona... kuna mambo mengi sana ambayo siyo rahisi kuelewa, na kiukweli...."
"Hivi unafikiri huto tumaneno twako mimi tunaweza kunimaliza nguvu? Usiniongeleshe ka' me demu, malaya wewe!" Suleiman akasema.
Draxton akabaki kimya.
"Kwo' dogo una machale sana mpaka ukavaa kitambaa ili kuficha uso, ukafikiri umemaliza eti? Hahah... hii nyumba nani alikujengea? Umeanza kumla Namouih lini?" Suleiman akauliza kwa dharau.
"Siyo jinsi unavyofikiria," Draxton akasema.
"Ila?"
"Ni ngumu kuelewa. Namouih hana makosa katika hilo, tafadhali, ananisaidia tu ku...."
"Msenge wewe! Anakusaidia na nini kama siyo kukunyonya mavi yako huko? S'kiza. Pale umebugi. Unanisikia? Umebugi vibaya mno. Hakuna mtu anayecheza na mali ya 'boss' wangu akaachwa salama, kwa hiyo utambue kwamba leo ndiyo mwisho wako kujitawazia chakula chake. Af' yaani me nilikuwa namwona mke wake kama mtu fulani anayejielewa kumbe anatoka hadi na kivuruge wa rafiki yake! Ama kweli ni mavi ya kunde tu ndiyo yamemjaa kichwani!" Suleiman akaongea kwa dharau.
"Usimwongelee Namouih kwa njia hiyo, nitakuumiza!" Draxton akasema kwa hisia kali.
"Unasemaje?!"
"Nilichosema!"
Suleiman akainyanyua bastola kumwelekea, akiwa ameingiwa na hasira.
Draxton akanyanyua mkono kidogo na kusema, "Tafadhali... nakuomba... usifanye hivyo. Tunaweza kuongea vizuri... lakini ukifanya hivyo utajihatarisha kwa...."
Kabla hajamaliza kuongea, Suleiman akafyatua risasi iliyompata katikati ya tumbo lake! Ilisikika kwa nguvu sana na hata kufukuza ndege wengi waliokuwa mitini, na kwa sekunde hizo chache Draxton akawa amekaza shingo yake ili asitoe sauti kwa maumivu aliyohisi, naye akajiangalia tumboni na kuona jinsi damu ilivyomtoka kwa wingi. Mwili wake ukaanza kuhisi udhaifu, hasa miguuni, naye akashuka chini taratibu na kupiga magoti huku amejishika tumboni, na kadiri ambavyo maumivu yake yalikuwa yanasambaa mwilini, ndivyo joto lake la mwili lilivyoongezeka, naye akatambua hiyo ilikuwa inamaanisha nini.
Suleiman akaanza kumfata huku akimwangalia kikatili, na alipomkaribia zaidi akaiweka bastola yake kichwani kwa Draxton, aliyekuwa ameinamisha uso wake huku anapumua kwa nguvu sana. "Ningekupasua hili bichwa ila nataka nikuchinje huku bado unapumua. Haki ya baba hii zawadi itamshangaza boss," akasema.
"Aahh... kaka... nakuomba ukimbie... sss... haujui ni jinsi... gahh... unajihaahh..tarisha..." Draxton akasema kwa maumivu.
Suleiman akacheka.
Draxton akamshika mguu na kusema, "Ingia kwenye... gari sss... ondoka...."
Suleiman akaupiga mkono wake pembeni na kutumia uchuma wa bastola kumpiga nao kichwani, naye Draxton akahisi maumivu makali na kudondokea pembeni, lakini akiwa amejitahidi kuishikisha mikono yake chini na hivyo kutolala kabisa. Suleiman akatoa kisu kutoka kwenye mkanda wa suruali yake, chenye makali kuwili, naye akaanza kumfata Draxton taratibu akiwa na lengo la kwenda kuanza kuikata shingo yake. Wakati huu, Draxton alisikika akipumua kwa njia zilizotoa muungurumo, lakini Suleiman hakujali kelele hizo. Akafika karibu yake zaidi na kunyanyua kichwa chake ili aanze kumchinja, na ile Draxton aliponyanyua tu uso wake, Suleiman akashtuka kidogo.
Macho ya Draxton sasa yalikuwa ya blue, huku pembezoni mwake ukianza kuonekana ule weusi uliyofanya yatishe. Suleiman hajakaa sawa akaanza kuona ngozi ya mwanaume huyo inabadilika rangi na kuwa nyeupe, huku nywele za kichwa chake zikirefuka na kuwa nyeupe pia. Butwaa lililompiga Suleiman lilikuwa kubwa sana, lakini siyo kama pigo lililofata baada ya hapo. Draxton akiwa katikati ya badiliko lake sasa, akamtandika mwanaume huyo ngumi nzito sana tumboni iliyofanya mwili wake urushwe kuelekea juu hewani na kurudi chini kwa kishindo. Bastola na kisu alichokuwa ameshika mwanaume huyo vikadondokea pembeni, naye akawa anaugulia maumivu aliyohisi kwa kutoa miguno ya sauti ya juu.
Draxton akasimama taratibu, akiwa amempa mgongo Suleiman, naye Suleiman akaanza kujivuta-vuta huku ameshika tumbo lake kwa kuhisi maumivu makali sana. Huyo aliyekuwa mbele yake alikuwa kiumbe wa aina gani? Kwa usawa huu aliokaa aliweza kuona namna ambavyo makucha kwenye vidole vya Draxton yaliongezeka urefu, naye akaingiwa na hofu sana. Mnyama-Draxton akamgeukia taratibu, akiwa mweupe kama mzungu, macho na meno yake makali yakionekana vyema, na akimwangalia mwanaume huyo kwa njia isiyokuwa ya kirafiki hata chembe. Suleiman akajitia ujasiri na kusimama tena, halafu akakunja ngumi kibabe kuonyesha hamwogopi na yuko tayari kupambana naye.
Akili ya Draxton bado ilikuwepo kwa wakati huu, lakini endapo kama Suleiman angejichanganya tu basi matendo yake yangekuwa ya kinyama. Alikuwa amesimama tu akiendelea kumwangalia mwanaume huyo, naye Suleiman alipomwangalia tumboni akaona risasi aliyompiga jamaa ikitoka yenyewe na kudondoka chini. Hapa ndiyo akawa ameelewa kwamba Draxton hakuwa kiumbe wa kawaida kabisa, na kama risasi tu haikumdhuru, ngumi zingesaidia nini? Ila hiyo haingemaanisha akae tu kusubiri lolote, kwa sababu hapa njia ya kutoka kati yao ilikuwa moja tu kati ya hizi; uhai, au kifo. Akatazama pale ambapo bastola yake ilikuwa imeangukia, akijishauri aifate ili zamu hii amfyatue kichwani maana aliona huenda kwa kumtandika risasi kichwani ndiyo angemuua, lakini alikuwa amekosea sana.
Suleiman akapiga mahesabu ya haraka, kisha akafata bastola yake upesi na kuiokota tena, na alipoinyanyua tu kumwelekea Draxton akaanza kufyatua risasi nyingi zilizompiga kupitia usoni, shingoni na kifuani. Alikuwa anamtandika risasi huku anapiga kelele kama jemedari aliye vitani, na zilionekana kumtoboa Draxton vibaya sana na kuuharibu uso na kichwa chake, lakini hakudondoka chini wala kuweweseka hata kidogo. Suleiman akawa amemaliza risasi zote, naye akabaki kupigwa na butwaa baada ya kuona mwanaume yule amesimama tu, na ndipo mwili wa Draxton ukafumuka kwa nguvu sana na kuwa mkubwa zaidi, huku ngozi yake ikitawaliwa na manyonya meupe. Suleiman alishtuka sana baada ya kuona kilichokuwa mbele yake, bonge moja la mnyama mwenye kutisha kupita maelezo, naye akaidondosha bastola yake akihisi kama nguvu zote zimemtoka.
Draxton sasa hakuwa Draxton tena. Baada ya siku nyingi kuwa zimepita, hatimaye upande wake wa mnyama ukawa umetoka tena, siyo kwa kulazimisha, ila kwa kulazimishwa. Mnyama ambaye sasa alikuwa ameuvaa mwili wa Draxton akawa anamwangalia Suleiman kwa njia ya kikatili sana, kisha akatoa muungurumo mkali sana kumwelekea mwanaume huyo. Suleiman aliogopa mno na kuanza kukimbia kulielekea gari lake, lakini kutokea hapo lilikuwa mbali mno. Akawa anakimbia huku anapumua kwa hofu, akielewa bila shaka kwamba kilicho nyuma yake kingekuwa kinamfata, na alikuwa sahihi. Hakusikia sauti yoyote ya hatua za mnyama huyo mkubwa, lakini akashtukia mwili wake unapigwa kwa nguvu sana na kumfanya arushwe mpaka kuangukia chini ya mti mmoja.
Akaanza kulia kwa maumivu sana, kwa kuwa kipigo hicho kiliambatana na mkwaruo wa makucha marefu ya mnyama huyo kwenye mwili wake, na hapo hapo mguu wake ukakamatwa kwa nyuma na yeye akaanza kuburuzwa akiwa amelalia tumbo. Alipiga kelele sana, lakini tena mguu wake ukanyanyuliwa na kuvutwa kwa kasi, na kilichofuata ilikuwa ni mwili wake kujikuta umebamizwa kwenye gari lile la Draxton baada ya kurushwa upande huo kwa nguvu. Suleiman hakuweza kuona mambo vizuri sasa, maana kizunguzungu kilitawala kichwa chake, na maumivu aliyohisi mwilini yalikuwa makali sana kiasi kwamba ukawa unakufa ganzi. Akawa anahisi muungurumo wa taratibu karibu yake, mara alambwe-lambwe, mara apigwe-pigwe kidogo, mara kucha ndefu ikitembea mwilini mwake kwa njia fulani kama inamtekenya, na ingawa alikuwa ameshahisi kuchoka alielewa kwamba mnyama huyo alikuwa anacheza na "windo" lake, kama paka afanyavyo akishamkamata panya. Uso wake ulikuwa umeshavimba sana, damu nyingi ikimtoka, na hakuna kitu kingine alichokuwa anaombea kifuate zaidi ya kifo cha haraka, ila mnyama huyo alionekana kutaka amfanye ahisi maumivu kwanza.
Suleiman akawa anawaza namna ambavyo amejitahidi kumtumikia Efraim Donald kwa utiifu mwingi tokea alipomwajiri, akimfanyia mambo mengi sana na kumtunzia siri nyingi, na sasa huu ndiyo uliokuwa mwisho wake, mwisho wa yote aliyofanya, mwisho wa yote aliyotaka kufanya, mwisho ambao ulikuwa mbaya kuliko namna ambavyo angeweza kutazamia. Ndani ya hizi dakika chache za kuisikilizia pumzi aliyokuwa amebakiza, aliweza kukiona kichwa cha mnyama huyo karibu na uso wake, naye akafumba macho na kuhisi namna ambavyo kichwa chake kiliingia ndani ya kinywa kikali cha mnyama huyo na kuanza kutafunwa. Ikawa ndiyo habari kwisha ya Suleiman.
★★
Familia ya Namouih ilikuwa imeachana kwa kugawana wawili-wawili ili kwenda kufanya matembezi. Ingekuwa ni kwa masaa machache tu, kisha wote wangetakiwa kurejea nyumbani kabla ya jioni ili kuwa pamoja tena. Efraim Donald alikwenda pamoja na Sasha sehemu ya mbali kiasi kutoka maeneo walikoishi, na kiukweli binti huyo hakuwa akijihisi amani kuwa pamoja na mwanaume huyo aliyefanya sehemu fulani ya maisha yake ibadilike ghafla, na kwa njia mbaya sana.
Wakati wote waliokuwa mwendoni, Efraim aliongea mambo mengi yenye kuamsha upendezi kuhusu mafanikio yake, tamaduni alizopenda, safari, na umuhimu wa familia, lakini Sasha hakuchangia lolote lile hata kidogo. Hata mara ambazo Efraim Donald alimuuliza maswali, binti hakujibu lolote utadhani haikuwa yeye aliyesemeshwa. Sasha alielewa kwamba mwanaume huyo hakuwa na nia nzuri kwake bali kumtumia tu kama chombo cha starehe, na ilimuumiza kwa sababu alijiacha afikiri kwamba hakuwa na njia ya kumwepuka, hasa kwa kufikiria kuhusu jinsi ambavyo Namouih angehisi endapo kama angejua kilichotokea baina yao. Kwa upande wake Efraim, ilikuwa ni jambo lililompa furaha sana kucheza na hisia za binti huyu mdogo, kwa sababu alijua kulikuwa na chuki kuu moyoni mwa Sasha kumwelekea, naye alikuwa na mipango ya kuitumia chuki hiyo hiyo kwa njia ambayo ingempa faida za kichoyo zaidi. Na hilo ndiyo lililokuwa lengo la safari hii ya "matembezi" ambayo Sasha hakujua ingemfikisha wapi.
Walifika sehemu fulani yenye mgahawa wa kisasa, naye Efraim Donald akamwambia Sasha ashuke ili waende kula kitu, lakini binti akagoma kutoka ndani ya gari. Efraim akatabasamu tu, kisha akatoka na kwenda kununua chakula na kukifunga, halafu akarudi kwenye gari na kumpa sehemu, akimwambia binti kwamba angepaswa kula kwa kuwa huko waendako angehitaji nguvu nyingi. Sasha alifumba tu macho yake, akihisi hasira na huzuni kwa wakati mmoja, kwa sababu alijua huko waendako ilikuwa ni kwa madhumuni ya kumfanyia kile alichofanyiwa usiku wa jana. Efraim Donald akalitia tu gari lake mwendoni huku akila, lakini Sasha hakugusa chakula alichopewa.
Ikiwa imetimia mida ya saa saba mchana, Efraim Donald akalifikisha gari lake mahali kulikokuwa na nyumba fulani kubwa yenye ghorofa tatu, na mwonekano wake ukiwa kama nyumba ya zamani sana. Hakukuwa na nyumba zingine eneo hilo, na sehemu za pembeni kulizunguka palikuwa na miti tu na vichaka. Walikuwa wameiacha barabara ya lami mbali kiasi, na mpaka kufikia sasa, Sasha hakuwa amekula chakula alichonunuliwa hata kidogo. Aliitazama tu nyumba ile, akielewa kuwa hapa aliletwa ili kufanywa kuwa chakula pia. Efraim Donald akalizima gari baada ya kulisimamisha umbali mfupi kutoka kwenye nyumba hiyo, naye akamgeukia Sasha na kumwangalia kwa macho yenye matamanio.
"Tumefika. Ingekuwa afadhali kama ukila hata kidogo mrembo wangu," Efraim akamwambia.
Sasha akabaki kutulia tu, akitazama chini kuelekea viganja vyake alivyovishikamanisha.
"Usiwe hivyo bwana. Hujasema lolote safari nzima mpaka huku... siyo vizuri. Unanifanya nihisi labda nimekutendea vibaya wakati sijafanya kitu cha namna hiyo," Efraim akaongea.
Sasha alihisi hasira sana, lakini kama tu alivyokuwa na utu wenye upole, akaendelea kujizuia kutokufanya wala kusema lolote lile.
"Najua unachowaza... au niseme... unavyohisi. Unahisi hasira sana, una... unachukia kwamba niko nawe huku usikokujua kabisa. Yaani akili yako inakutaka ufanye mambo mengi lakini... unaizuia kufikiria mabaya, au siyo?"
Sasha akaendelea kubaki kimya.
"Naelewa unavyohisi. And believe me... sipendi kabisa kuona unaumia. Nataka kukusaidia kuiondoa hiyo chuki na hasira iliyo ndani yako kwa njia nzuri sana darling..."
Binti akameza mate tu na kuangalia upande wa kioo cha mlango wa gari.
"Unanichukia, siyo? Akili yako inatamani hata kunifanyia jambo baya eeh? Hhahahahah... ngoja nikwambie kitu fulani kuhusu akili. Kati ya mwanaume na mwanamke, ni mwanamke ndiye mwenye akili zaidi ya mwanaume, na iko hivyo kwa sababu mwanamke ana faida nyingine juu ya mwanaume. Mwanamke ni mtamu... sana. Kama wewe. Lakini unajua ni kwa nini huwa inaonekana kwamba mwanaume ndiyo mwenye akili kuliko mwanamke? Ni kuwa mwanamke anajua kabisa kwamba utamu wake ndiyo kitu kinachomfurahisha mwanaume, kwa hiyo katika mambo mengi mwanamke hutegemea zaidi kuwa mtamu tu mbele ya mwanaume na siyo kutumia akili superior aliyopewa ambayo angeweza kuitumia juu ya mwanaume. Hivyo ndiyo mzee wetu wa kwanza alivyopagawishwa na mwanamke mpaka akajisahau na kula tunda lililosababisha matatizo, ndiyo maana baada ya hapo wanaume wakaingiwa na akili ya kujua jinsi ya kuwa na akili dhidi ya wanawake," Efraim Donald akaongea kwa njia yake aliyoiona kuwa ya busara.
Sasha alikerwa sana na maneno yake. Hayakuwa na maana yoyote ile kwake, na ingawa alitamani hata kumwambia jinsi alivyomchukia kweli, akaendelea kunyamaza.
Efraim Donald akatabasamu huku akimwangalia kwa macho yenye hila, kisha akamuuliza, "Unaweza kuotea ni kwa nini tumekuja huku?"
Sasha akaendelea tu kuangalia upande wa kioo.
Efraim akapeleka mkono wake kwa binti huyu na kukishika kidevu chake, kisha akakigeuzia upande wake ili watazamane. Akaendelea kukishikilia, huku Sasha akimwangalia kwa hisia iliyoonyesha kutopenda kabisa jambo hilo. Efraim Donald akashusha kiganja hicho mpaka shingoni kwa binti, akikiweka hapo kama vile anataka kumkaba, naye Sasha akawa anamwangalia kwa njia fulani hivi ya ujasiri huku akikaza ngumi kwenye kiganja kuzuia hisia zake.
Efraim Donald hakuikaza shingo ya Sasha kwa nguvu, badala yake akawa kama anaisugua taratibu tu huku akimwangalia kwa macho yanye hila kali na tabasamu lililojaa uovu haswa, kisha akamwambia, "Leo nataka kukufundisha jinsi ya kuitoa hasira yako... mrembo wangu."
Sasha akiwa hajaelewa kikamili jambo alilomaanisha mwanaume huyu, mkono mwingine wa Efraim ukapita kwa chini, chini ya usukani, naye akawa kama anajaribu kuvuta kitu fulani, kisha akautoa huku ukiwa umeshikilia bastola ndogo sasa. Sasha akaiangalia kimaswali kiasi na kumtazama tena Efraim, aliyekuwa ameishikilia kwa ukaribu na uso wake mwenyewe.
"Ushawahi kuziona hizi kwa ukaribu?" Efraim akauliza.
Sasha akaendelea tu kuitazama.
Efraim akakitoa kiganja chake kingine kwenye shingo ya binti na kukaa sawa kwenye siti yake. "Dada yako alikuwa anapenda kuichezea sana kwa hiyo nikaificha humu. Nikikupa uitumie, utaweza?" akamuuliza.
Sasha akaanza kuingiwa na wasiwasi mwingi.
"Utaitumia vipi nikikupa? Utanipasua hili bichwa eti?" Efraim akauliza tena.
Binti akaangalia chini huku mapigo yake ya moyo yakianza kukimbia kwa kasi zaidi.
Efraim akamtazama na kusema, "Usiogope. Nataka kukuonyesha kitu fulani. Labda baada ya hapo ndiyo utaweza kula."
Mwanaume huyu mkatili sana akashuka kutoka ndani ya gari akiwa na bastola yake, akimwacha binti ndani ya gari akiwaza kuhusu ni nini mwanaume huyo alichokuwa anapanga kumfanyia. Kufikiri kwamba Efraim Donald hakuwa mjinga vya kutosha kumleta huku ili labda amuue wakati akielewa kabisa kwamba mama yake na dada yake walijua aliondoka pampja naye, ni jambo lililokuwa rahisi kuingia kichwani, lakini haikuwa kitu kisichowezekana. Sasha akawaza kwamba ingekuwa bora kama angekataa mapema kabisa kuja naye, kwa sababu wakati huu aliona tayari alikuwa ndani ya shida isiyo rahisi kutorokwa. Akafumba macho huku akijikaza sana asilie, ngumi akiikaza kwa nguvu zaidi, na sauti ya mlango wa upande wake kufunguka ikamfanya ayafumbue macho yake tena. Hapo nje alikuwa amesimama mume wa dada yake kipenzi, akiwa ameshika bastola, na akimwangalia kama kusema "toka."
Sasha, akiwa ameshaamua kukubaliana na lolote lile ambalo lingetokea, akashuka taratibu. Kuwaza kwamba haya yote alikuwa amejisababishia mwenyewe kulifanya ajione kuwa mstahili wa mabaya ambayo angepitia, hivyo kama ni kuyaacha yampate basi angeyaacha yampate tu. Efraim akaufunga mlango wa gari na kukishika kiganja cha Sasha, kisha akaanza kutembea pamoja naye kuielekea nyumba ile. Ilikuwa ni kama jinsi ng'ombe anayepelekwa machinjioni anavyokwenda kwa hiari bila kujua, isipokuwa kwa Sasha ilikuwa tofauti kwa kuwa alijua kabisa kwamba aliongozwa kuelekea sehemu hiyo kama machinjioni, na bado hakufanya jitihada yoyote ya kujaribu kuepuka hilo. Yaani liwalo na liwe. Efraim Donald akawa anamwambia kuhusu jinsi jengo hilo lilivyotumiwa zamani kama nyumba ya kupangisha, lakini yeye akaja kulinunua na kuliacha tu, hiyo yote kuonyesha alikuwa na pesa nyingi sana za kufanya chochote alichotaka, na bado asingepungukiwa. Akamwambia anataka kumwonyesha jambo fulani litakalomsaidia agundue yeye (Sasha) alikuwa nani hasa, yaani mtu wa aina gani, kitu ambacho binti huyo aliona ni kama kimesemwa kwa njia ya fumbo ili kuficha jambo fulani zito sana hapo, na ndivyo ilivyokuwa.
Wakalifikia jengo hilo baada ya hatua hizo chache. Sehemu ya ardhi kulizunguka ilijaa majani mengi sana ya matawi ya miti yaliyokauka. Haikuonekana kama kulikuwa na mtu au watu walioishi hapo, lakini baada ya wao kuufikia mlango, Efraim akabisha hodi kwa nguvu. Bado alikuwa amekishika kiganja cha Sasha, na bastola ikiwa kwenye kingine, na mlango huo ukafunguliwa taratibu na mtu fulani kuonekana humo ndani. Alikuwa mwanaume, mweusi, mwenye mwili mkubwa zaidi kuzidi wa Efraim, na alikuwa na sura makini sana. Sasha akamwangalia kwa wasiwasi kiasi baada ya mwanaume huyo kumtazama kwa sura ngumu, lakini Efraim akawa anamwangalia kwa njia ya kawaida tu. Jamaa akaufungua mlango zaidi, kama kuonyesha ruksa kwa wawili hawa kuwa waingie ndani, naye Efraim akaanza kupiga hatua kuingia lakini Sasha akaweka mgomo kiasi. Efraim Donald akamgeukia na kumwambia asiogope, kisha akatumia nguvu kiasi kumvuta na hatimaye kuingia pamoja naye, na yule mwanaume akaufunga mlango.
Sasha aliiangalia sehemu hiyo hapo ndani kwa hofu kiasi. Hapakuwa na aina yoyote ya samani (furniture), yaani palikuwa tupu kabisa isipokuwa sehemu za milango iliyoonekana kuingia ndani ya vyumba vingine vya jengo na ngazi zilizoelekea juu kwa mbele zaidi ukutani. Efraim Donald na mwanaume huyo hawakusemeshana lolote kabisa, na jamaa akazielekea ngazi na kuanza kupanda, akitokomea kutoka chini hapo. Efraim akaachia kiganja cha binti na kuzishika nywele zake laini huku akimwangalia kwa upendezi, naye Sasha akawa mtulivu tu kusubiri hatma ya haya yote.
Kutokea kwenye ngazi zile, wakaanza kushuka wanaume wengine watatu huku wakifuatwa na yule jamaa wa mwanzo, nao wote wakafika mbele ya Efraim Donald na kusimama. Akiwa ameingiwa na hofu zaidi, Sasha akarudi nyuma kidogo, lakini Efraim akakishika kiganja chake kwa mara nyingine tena.
"Tulia mpenzi. Tulia," Efraim akamwambia.
Wanaume hao wote walitoa harufu za pombe na sigara, lakini walionekana kuwa watu makini sana.
"Yuko wapi?" Efraim Donald akamuuliza mmoja wao.
"Yupo juu. Chumba cha pili. Anakusubiria," mtu huyo mwenye sura ngumu akajibu.
Efraim akatabasamu na kusema, "Kazi nzuri. Nendeni kwenye gari mkachukue kitu yenu. Nataka kutumia muda kidogo na mpenzi wangu hapa."
"Pamoja sana boss," mwanaume huyo akasema.
Sasha alishindwa kuelewa ni nini kilichokuwa kinaendelea kabisa. Wanaume hao wakawapita na kutoka hadi nje kabisa, naye Sasha akamwangalia Efraim kimaswali.
Efraim akamwangalia, kisha akasema, "Wewe na dada yako ni warembo sana. Na mnafanana kwa vitu vingi. Mna... kau-special fulani hivi ambako ni adimu kukuta kwa wengine, ingawa siyo ngumu. Na ningesema nyie wote ni watamu lakini kwa dada yako bado sijajua."
Sasha akabaki kumwangalia kwa kutomwelewa kabisa.
"Ila unajua nini... pamoja na kwamba mnafanana sana... wewe umemzidi jambo fulani. Wewe Sasha... uko... kama.... mimi," Efraim akasema kwa uzito.
Sasha akaendelea kumtazama kwa makini.
"Uko kama mimi Sasha... ila bado haujui hilo. Niko hapa pamoja nawe kukusaidia ulitambue. Utajua wewe ni nani sasa," Efraim akasema.
Sasha akaangalia chini, akiwa anajiuliza ikiwa kaka-mkwe wake alikuwa na matatizo ya akili ama vipi, lakini muda siyo mrefu angepata jibu.
Efraim Donald akaanza kumvuta kistaarabu kuzielekea ngazi, nao wakapanda kwa pamoja kuelekea juu. Sasha akijua wazi kwamba huko juu kulikuwa na mtu aliyewasubiria ni jambo lililomwongezea wasiwasi kwa kuwaza ingekuwa nani, na alikuwa anataka nini kutoka kwake. Hili janga alilokuwa amejileta yeye mwenyewe ndani yake lilionekana kuwa kubwa kuliko alivyodhani. Baada ya kufika ghorofa ya pili, wakaelekea kwenye mlango wa pili kutoka kwenye korido fupi lililoelekea kwenye ngazi za kwenda juu zaidi, naye Efraim Donald akaufungua mlango na kuingia huku Sasha akimfuata kwa nyuma kutokana na mwanaume huyo kuushikilia mkono wake bado.
Chumba hiki kilikuwa kipana na tupu pia, isipokuwa ya kiti kimoja kilichokuwepo humo ambacho alikalia mtu fulani. Sasha alitoa macho kwa mshangao, mapigo ya moyo wake yakianza kudunda kwa kasi zaidi, baada ya kumtambua mtu huyo kuwa Shomari! Yule mpenzi wake aliyekimbia na kiasi fulani cha pesa ambazo binti alipewa na dada yake kwa ajili ya matumizi yake ya shule wakati fulani nyuma. Alishangaa sana kumwona hapo, naye akamwangalia Efraim Donald akiwa na maswali mengi kichwani.
"Mwana mpotevu apatikana. Ila huyu bwege hakurudi mwenyewe. Alitafutwa," Efraim akaongea maneno hayo kwa kejeli, naye Sasha akamwangalia mtu ambaye alikuwa wa karibu sana kwake.
Shomari alikuwa ameketi kwenye kiti, mikono yake ikirudishwa kwa nyuma huku ikiwa imefungwa, na miguu yake ikifungwa kwa pamoja chini. Hakuwa na nguo yoyote mwilini isipokuwa boksa nyeusi tu iliyoficha sehemu za siri, na mdomoni mwake alifungwa kwa gundi ya karatasi. Sasha alimtazama sana, asiamini kabisa kwamba ni yeye huyo ndiyo alikuwa mbele yake. Jamaa alikuwa na mwili mkakamavu kiasi, na vinyweleo sehemu ya kifuani vilionekana kulowana kwa jasho. Alikuwa anajaribu kujinasua hasa baada ya kumwona Sasha, na binti huyu akaingiwa na hasira iliyofanya aanze kupumua kwa nguvu huku machozi yakivizia machoni mwake.
"Surpriiise..." Efraim akamwambia Sasha kikejeli.
Sasha akakunja ngumi kwa kuhisi hasira hata zaidi.
"Oh dear... naelewa unavyohisi. Kuwa... face to face na mtu aliyekusaliti vibaya sana... inauma. Na tena unadhani basi hata alikuwa amekimbilia mbali? Laki tisa ile ikampa kiburi cha kufikiri amemaliza maisha, akaenda zake wilaya nyingine na kujitafutia kachumba na kademu kake kakizaramo... ahahahahah... ai watoto nyie! Hivi hata ulimtolea wapi huyu mpuuzi? Mbona haendani kabisa na hadhi yako? Labda ndo' kusema moyo hauna hiyana eeh? Hhahahahah..."
Efraim alionekana kuufurahia sana mchezo huu aliokuwa ameanzisha, lakini akili ya Sasha ilikuwa imehama ghafla kutoka kwenye kuwaza kuhusu usalama wake akiwa na Efraim, na sasa alikuwa ameielekeza yote kwa kijana huyo aliyeuvunja moyo wake. Alikuwa akimpenda sana, na hakuna kitu kilichoisumbua akili yake kama swali la ni kwa nini aliamua kumtendea kwa njia ile yenye hila wakati yeye alionyesha kumwamini sana.
"Utanishukuru baadaye kwa kukusaidia kumpata, lakini hapa ndiyo mahali unapopaswa kujiuliza swali hili: utafanya nini sasa?" Efraim akamuuliza.
Sasha akamtazama, huku sasa machozi yakianza kutiririkia kwenye mashavu yake.
Efraim akampangusa machozi kwa kidole na kusema, "Hapa ndiyo sehemu unayotakiwa kukumbuka kwamba wewe ni kiumbe mwenye akili, na siyo mtamu tu. Mambo yote yaliyokupata mpaka sasa ni kwa sababu yake. Ameuvunja moyo wako, yeye. Amesababisha ukaacha kumsikiliza dada yako wa damu na bado akakusaliti, yeye. Amefanya ukadanganya, ukanidanganya ili upate pesa kwa ajili ya kufidishia makosa yake, yeye. Na hiyo ikakuweka wapi? Kwangu. Ni kwa sababu yake mimi na wewe tumefanya jambo ambalo hukuwahi kufikiri ungekuja kufanya kabisa... yeye Sasha."
Sasha alikuwa anabubujikwa na machozi hata zaidi, kwa kuwa maneno ya Efraim yaliyojaa uchochezi yaliiongezea hasira yake moto mkali hata zaidi. Efraim akamkabidhi bastola taratibu kiganjani mwake, huku binti akimwangalia tu kwa hisia nyingi zilizovurugika.
Akiwa bado anamkabidhisha bastola, Efraim akaendelea kusema, "Wewe uko kama mimi Sasha. Dada yako... dada yako anani-cheat. Unajua jinsi gani ilivyo ngumu ku-share kitanda kila siku na mtu huku ukijua kwamba mali yako anaigawa kwa wengine? Haujui kwa kiwango changu lakini hata kwa chako ninajua unaelewa. Ulipokuja ofisini kwangu siku ile, kunidanganya... Sasha kuanzia hapo nilijua kabisa kwamba uko kama mimi. Uko tayari... uko tayari kufanya lolote lile ili Namouih asivunjike moyo, hata mimi... hata mimi kuna mambo nimefanya, na siko radhi mke wangu ajue. Ni bora tu kuendelea kutoa tabasamu la unafiki lakini faida yake maishani iwe na mantiki... na dada yako ni kitu chenye faida sana kwangu, ndiyo maana bado niko naye. Lakini unajua nini Sasha? Haupaswi sikuzote kufanya mambo kwa kujali tu namna mtu mwingine atakavyoyaona. Fanya vitu vitakavyokupa wewe faida, siyo kwa kuwaza tu kwamba hata ukidanganya, unafanya hivyo kwa ajili ya Namouih, au Zakia, au Sabrina, au fulani... no. DANGANYA KWA AJILI YAKO MWENYEWE. Na kama kutatokea jambo fulani linalokufanya ufikie hatua mbaya sana, kihisia, kimwili, kiakili...."
Efraim akaishikisha mikono yote ya Sasha bastola taratibu na kuigeuzia kumwelekea Shomari, huku akiwa nyuma ya binti.
"....ni lazima ufanye kila uwezalo kuliondoa," Efraim akamalizia maneno aliyokuwa akimwambia.
Sasa binti huyu mdogo akawa ameelekezeshwa bastola kwa mpenzi wake aliyemfanyia usaliti kwa kuendekeza pupa, akiwa analia kwa kuhisi huzuni na hasira kwa wakati mmoja. Efraim Donald akawa ameweka kichwa chake karibu na cha Sasha kutokea nyuma, akimshawishi binti huyu afanye jambo ambalo halikuwahi kuingia akilini mwake toka ameingia ndani ya dunia hii.
"Iko tu kama kwenye movie Sasha. Unaweka kidole chako hapa, unavuta, kisha tatizo linalokukosesha amani linatoweka kabisa. Ni rahisi sana mrembo wangu..."
Efraim akaendelea kumshawishi kwa kunong'oneza sikioni namna hiyo. Mapigo ya moyo wa Sasha yalidunda kwa nguvu na kwa kasi sana. Aliogopa. Kumwangalia Shomari akionekana kulilia msaada hapo mbele yake siyo jambo lililompendeza hata kidogo, lakini ni kama maneno ya Efraim yalikuwa yameanza kuitia sumu akili yake ifikiri kwamba kweli hata yeye alitaka kufanya jambo hili. Akiwa anakumbukia jinsi alivyojitoa kwa kijana huyo kumwonyesha jinsi alivyompenda, kumpa kila kitu cha kihisia na kimwili haikutoaha kuthibitisha kwa Shomari kwamba anapendwa mpaka akaamua kuusaliti upendo wa binti, tena kwa pesa kidogo tu. Shomari mwenyewe alionekana kama mtu aliyebanwa na haja kubwa ila kakosa choo cha kuingia mbele ya watu wengi kutokana na jinsi alivyojivuta-vuta kwa hofu huku akiguna ndani ya gundi ya karatasi iliyomfunika mdomo.
"Alikuwa na deni la laki sita, na angefilisiwa kila kitu. Ulipompa laki tisa aliamua kuwaacha wamfilisi ili yeye aondoke akaanze maisha mapya. Na hilo wazo la kishenzi alilipata kutoka kwa chakubimbi wake huyo aliyekuwa anakula wakati huo huo yuko nawe. Kwa mambo mengi anakuona kama kitega uchumi maana alikupulizia dawa huyu... akutumie kukudolishia kwa wasela, akutafune weee... halafu mwishowe akubwage. Kama kawaida yao. Mimi nakujali sana Sasha kutoruhusu mpuuzi yeyote aurushe-rushe moyo wako kama yoyo. Moyo wako ni wa kipekee sana. Mtu kama huyu hastahili kupendwa na mtu special kama wewe... na ndiyo maana nimemleta huku ili umwonyeshe. Mwonyeshe. Mwonyeshe inamaanisha nini kucheza vibaya na moyo wako... nakuapia Sasha, hisia utakayopata baada ya hapo, hakuna yoyote inayofanana nayo. Utaridhika," Efraim akamwambia binti kwa ushawishi.
Mwanaume huyu alikuwa na nia ya kumpitisha mwanadada mdogo kwenye njia mbaya sana, njia ambayo ingeyabadili kabisa maisha yake endapo kama binti angeamua kuifuata. Sasha alihisi hasira kali isiyoelezeka, na hiyo ni kwa sababu yeye alikuwa mtu aliyezifungia sana hisia zake nyingi ndani tokea zamani, na sasa Efraim alikuwa akimlazimisha azitoe zote wakati huu. Ilikuwa ni kama Efraim pekee ndiye aliyeelewa namna alivyohisi, kwa kuwa hata hakudhani kuna mtu angetumia muda wake kujaribu kutafuta ukweli kuhusu matendo ya mpenzi wake huyo aliyemkimbia. Moja, aliusaliti upendo wake. Mbili, akamfanya yeye Sasha amsaliti dada yake. Na tatu, akaingiliwa kimwili na mtu asiyekuwa na upendo wowote wa kimahaba kumwelekea. Alijihisi mchafu sana, na sababu ya yeye kuhisi hivyo ilikuwa mbele yake, au tu jinsi Efraim alivyotaka binti ayaone mambo. Akaanza kumwangalia Shomari kwa chuki kali sana, huku bado akiielekeza bastola kwake, naye Efraim Donald akaviachia viganja vya binti na kusogea pembeni kidogo. Bado Sasha akawa ameendelea kumwelekezea jamaa silaha hiyo, huku akihisi mtetemo mikononi, mapigo yake ya moyo yakifanya riadha kwa kasi, na Shomari akiendelea kuguna kwa nguvu pale alipoketi.
"Unataka kusema kitu? Haya."
Efraim akamwambia hivyo Shomari, kisha akaanza kumfata kijana huyo na kumfikia karibu, naye akaibandua gundi ile ya karatasi iliyoufunika mdomo wake na kusogea pembeni kidogo. Sasha akiwa amesimama vilevile bado, akawa anamtazama Shomari kwa mkazo sana, aliyekuwa anapumua kwa nguvu.
"Sasha... Sasha usi... usimsikilize huyu. Kila kitu alichokwambia ni uwongo. Mimi sijafanya hivyo," Shomari akaongea kwa hofu.
"Mwambie basi wewe ulichokifanya," Efraim akamwambia jamaa.
"Sasha... mimi sikukukimbia mpenzi wangu. Nilitoka tu kidogo, nilikuwa narudi..."
"Kwa wiki zaidi ya mbili? Bila kupatikana, bila kuacha ujumbe, na ukiwa na mwanamke mwingine, ulikuwa unarudi wapi?" Efraim akauliza.
"Sasha... usimsikilize. Yeye ndiyo mbaya, mm..mimi sikufanya hivyo. Anakulaghai tu. Nilikuwa narudi kwako mpenzi. Kumbuka tulikotoka, ni mbali. Hakuna mwanamke mwingine zaidi yako Sasha... wewe ndiyo wangu wa moyoni..."
"Hhahahahah... oh God, nazipendaga sana hizi drama," Efraim akaongea kwa kufurahia.
"Sasha mpenzi wangu, niamini. Nakupenda sana. Mimi siyo mbaya. Hawa watu walioniteka ndiyo wabaya, huoni hilo? Unahitaji kuwaita mapolisi... wameniteka, wakanipiga Sasha... mama yangu atakuwa anawaza sana juu yangu... Sasha... kwanza huyu ni nani? Anakurubuni tu. Mimi na wewe tumetoka mbali, usisikilize uzushi... niamini, unanijua vizuri...."
Sasha akapeleka macho yake kwa Efraim wakati huo Shomari akiendelea kujitetea, na mwanaume huyo alikuwa anamwangalia kwa umakini kama anasubiri binti atende jambo hilo kwa hamu. Lakini kwa usawa huu, Sasha akawa ametambua jambo fulani. Efraim bado alikuwa anacheza na akili yake. Kwa jinsi walivyokuwa wamejiweka, ni kama Efraim alifanya makusudi kabisa kuwa pembeni ya Shomari, ikionekana alikuwa anampa Sasha jambo lingine la kufikiria, yaani, amuue yeye badala ya Shomari, au awaue wote. Uamuzi ulikuwa ni wake.
Binti huyu akaendelea kumtazama Efraim Donald kwa mkazo, kisha akageuza uelekeo wa silaha hiyo mikononi mwake na kumnyooshea kaka-mkwe wake! Efraim akanyanyua kidevu juu kiasi, akiwa anamwangalia kwa njia fulani kama ya mtu aliyeridhika kabisa.
"Ndiyo... ndiyo Sasha... huyu ndiyo mbaya. Mpige... mpige asiendelee kukudanganya. Me ni mpenzi wako, yeye siyo kitu chochote kwako. Mpige mpenzi wangu... mpige risasi ili tuwe huru tena... tuendelee... tuwe pamoja...." Shomari akaendelea kuongea hivyo ili kumchochea binti amuue Efraim na kuunusuru uhai wake yeye.
Sasha akawa anapumua kwa hisia kali sana, macho yake yakiwa kwa Efraim, na masikio yake yakiingiwa vyema na yale ambayo Shomari alisema. Efraim Donald akiwa anamwangalia binti huyo kwa umakini bado, akaachia tabasamu hafifu lililopeleka ujumbe fulani wenye hila ndani ya akili ya mwanadada huyo mdogo. Sasha akang'ata meno yake kwa nguvu sana, huku akimwangalia Efraim kwa hasira kali, na papo hapo akageuza mikono wake na kufyatua risasi, iliyompata Shomari kichwani na kukitoboa kufikia kisogoni!
Msukumo wa risasi hiyo ulifanya kijana aanguke moja kwa moja na kiti chake kwa kurudi nyuma, na maisha yake yakawa yametoweka hapo hapo. Sasha alikuwa kama mtu aliyerukwa na akili, akipumua bila utaratibu mzuri, naye akaiachia bastola hiyo na kuidondosha chini. Jasho likawa linamtoka sehemu ya kichwani, huku akiangalia jinsi mwili wa Shomari ulivyoeneza damu nyingi sakafuni hapo, naye akaanza kushtuka-shtuka kifuani kama jinsi ambavyo mtu hufanya anapohisi kutaka kutapika.
Efraim Donald akatoka pale alipokuwa amesimama na kumfikia mpaka nyuma yake, kisha akalibana tumbo lake kwa nguvu huku akimwinamisha mbele kiasi, naye Sasha akaanza kutapika. Alikohoa sana, na ikawa kama vile mwili wake umeishiwa nguvu kutokana na kuwa ndani ya mshtuko mkubwa kwa alichokifanya yeye mwenyewe. Akawa anapumua kwa nguvu huku ameelekeza uso wake chini, naye Efraim Donald, akiwa bado amemshikilia, akatabasamu kwa kuridhishwa na matokeo ya jaribio lake. Sasa alikuwa amefanikiwa kumgeuza msichana mdogo, aliyeonekana kuwa bila dosari, awe kitu kibaya kama yeye alivyokuwa, na angeendelea kumjenga awe namna hiyo hata zaidi.
Ni muda huo huo ndipo wanaume wale wanne wakawa wameingia ndani hapo, kama vile walijua yaliyokuwa yametokea, kisha wakausogelea mwili wa Shomari na kuanza kufungua kamba zilizoufunga ili wakautupe mbali. Efraim Donald akaokotewa bastola yake na mmoja wao, akampa, kisha Efraim akamwongoza Sasha taratibu kuelekea nje ya chumba hicho. Binti alikuwa amelegea kiasi, hivyo egamio kutoka kwa kaka-mkwe wake lilisaidia kumfanya atembee vizuri. Wakiwa wametoka ndani ya chumba hicho, Efraim akatoa kitambaa mfukoni mwake na kumfuta binti mdomoni, kisha wakaanza kushuka ngazi mpaka walipotoka kabisa ndani ya jengo hilo.
Akamwongoza mpaka kwenye gari lake, na walipolifikia, Efraim akatoa chupa yenye maji na kumpa anywe kidogo. Sasha hakuweza hata kutoa itikio lolote lile kwa sababu ya kulemewa na hisia nyingi mvurugo, hivyo Efraim akamnywesha na kumwambia ateme. Wakafanya hivyo mara tatu, halafu ya nne akamnywesha fundo tano kabisa ili apate utulivu kiasi. Bado Sasha alikuwa haamini kama alifanya kitendo kile kule ndani, naye akawa anapumua kwa utaratibu kiasi wakati huu ingawa bado bumbuazi halikumwondoka.
"Umefanya vema sana mrembo wangu. Am so proud of you."
Efraim akamwambia binti maneno hayo, naye Sasha akamtazama machoni.
"Najua umeshaambiwa sana kwamba kuua ni kitu kibaya. Lakini kamwe siyo kibaya endapo kama unaua mtu anayestahili kufa. Huyo bwege amestahili kilichompata, kwa sababu amecheza na wewe. Sikuzote kumbuka hili Sasha. Wewe ni special. Hakuna kitu, wala mtu yeyote anayepaswa kukuchezea halafu umwangalie tu. Kwa hall na mali yoyote ile, mtu yeyote akikuchezea, mwonyeshe wewe ni nani. Na mimi... mimi nitakusaidia ujue jinsi ya kuwakomesha wale wote wanaojaribu kukuonea. Unanielewa?"
Sasha alimtazama mwanaume huyo kwa umakini sana, akiyatilia maanani maneno yake kwa uelewa mpana zaidi.
Efraim akakishika kichwa cha Sasha kwa nyuma kama anazivuta nywele zake kiasi, kisha akamuuliza, "Unahisije now? Unahisi kuridhika, siyo?"
Sasha hakutoa jibu, ball akampa tu utizami ambao ulimwambia Efraim kwamba kweli aliridhika.
Efraim Donald akatabasamu na kusema, "Hivyo ndivyo inavyotakiwa kuwa. Hautawaza tena kuhusu Shomari, itakuwa kama hukuwahi kumjua kabisa, na utaweza kujichagulia yeyote unayetaka na kumtema wakati wowote unaotaka. Hivi ndivyo unavyotakiwa kuwa, siyo kuonwa kama kitu cha kinyonge, au tuzo tu, wakati wewe unaweza hata kuwa na watu wa juu zaidi kuliko yeyote ndani ya hii serikali. Nataka ufurahie hii side yako ambayo sikuzote umekuwa nayo lakini hukutambua hilo. Ni kitu kizuri sana Sasha... sana."
Sasha akashusha pumzi, kama vile kuonyesha ameanza kupata utulivu.
"Niambie mrembo wangu... unataka nini now? Chochote kile... nitakupa. Umenifurahisha sana leo," Efraim akamwambia huku akiutoa mkono wake kwenye nywele za binti na kuanza kutelezesha kidole chake kwenye shavu laini la binti.
Sasha, aliyekuwa kimya tokea mwanzo mpaka sasa, akatazama jengoni pale na kuwaona wanaume wale wakitoka, huku wawili wakiwa wamebeba gunia lenye kitu kizito na kuelekea nalo upande mwingine. Alijua kabisa kwamba humo kulikuwa na maiti ya mpenzi wake wa zamani, aliyemuua kwa mikono yake mwenyewe. Akamwangalia Efraim machoni kwa umakini, kisha akasema, "Nataka kula."
Efraim Donald akaachia tabasamu kwa kuhisi furaha sana, kisha akamwambia, "That's my girl."
Mwanaume huyu akamshika binti shingoni kwake, kisha akamsogelea mdomoni na kuanza kumbusu kimahaba sana. Sasha alikuwa haipokei busu ya mwanaume huyo mwanzoni, lakini baada ya sekunde chache naye pia akaanza kuirudisha, akimnyonya mdomo kimahaba sana na kumshika kiunoni mpaka mgongoni. Efraim Donald akawa amekamilisha mpango wake kwa ushindi.
★★★★★★★★★★★★
ITAENDELEA
★★★★★★★★★★★★
Usikose sehemu za mwendelezo wa hadithi hii kali ya CHANGE. Ni story nzuri na ndefu sana. Waweza ipata nakala yote kwa gharama nafuu sana. Karibu WhatsApp au kwa inbox ya hapa hapa JF.
WhatsApp no: +255 678 017 280
Efraim ni mwisho. Na hapo bado🙏 Mheshimiwa Elton Tonny 😂😂😂