Simulizi - DYLAN

I gotta hand it to you man... you know your analytics
 
DYLAN

Story by Elton Tonny

Familia, Kazi, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Unyanyasaji, Usaliti, Visasi, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa

(R-rated 18+)

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA THELATHINI NA SABA

★★★★★★★★★★★★★★★★★★


NUSU SAA KABLA YA BARAKA KUPIGWA RISASI

Dylan na Grace wanafika hotelini na kupanda lifti (elevator) pamoja kuelekea ghorofa ya juu kabisa. Wanaingia chumbani na kuamua kwenda kujimwagia maji pamoja ili wapumzishe miili yao ikiwa katika hali nzuri. Baada ya wote kumaliza na kujikausha maji, wanapanda kitandani na kukaa karibu-karibu wakiwa wameshikana mikono yao na kuzungumza kidogo.

"Well... mambo yamekwenda smooth kwa njia fulani... kubwa. Sikutegemea," akasema Grace.

"Wote tulitarajia angetokea jamaa ambaye angenitandika risasi, lakini inaonekana na wao wako makini pia," akasema Dylan.

"Natumaini tutafanikiwa. Ninajua wametuona, na wakati huu watakuwa wanapanga njama fulani. Ni muhimu kuwa makini sana kwa..."

Dylan akamkatisha Grace kwa kumpiga busu mdomoni. Grace akaushika uso wa Dylan na kuanza kurudisha upendo wake kwa ulimi ndani ya mdomo wa Dylan.

"Usijali sana Grace. Ninajua tutashinda," Dylan akasema baada ya kujitoa mdomoni mwake.

"Mimi pia."

"Aam... sikukuona ukinywa wine leo, ilikuwa ni kwa nini?" Dylan akauliza.

"Sitakiwi kunywa nikiwa na mtoto, ni hatari kwake."

"Oooh... ahahah ni vizuri uko makini. Huyo dogo angepiga wine pia humo ndani sipati picha ingekuwaje, disco au?" Dylan akatania.

Grace akachekea kwa chini huku akimtazama Dylan kwa njia fulani ya upendo.

"Vipi?" Dylan akauliza.

"Leo....ndiyo kwa mara ya kwanza umeniambia kwamba...."

"Nakupenda," Dylan akamalizia.

Grace akatabasamu kwa furaha.

"Umejisikia vizuri?" Dylan akauliza.

"Sana. Sikumbuki mara ya mwisho mtu aliniambia maneno hayo nami nikaya..weka moyoni namna hii," Grace akasema kwa hisia.

"Well, itabidi uanze kuyazoea kutoka kwangu, maana nitahakikisha nakwambia kila siku," Dylan akasema.

Grace akatabasamu, kisha akaanza tena kumpiga busu Dylan. Waliendelea kudendeshana kwa sekunde chache pale simu ya Dylan ilipoanza kuita. Akajitoa mdomoni kwa Grace na kuichukua kuangalia ni nani, naye akakuta ilikuwa ni Gilbert ndiye anapiga. Akapokea na kuongea na baba yake huyo, ambaye alikuwa anauliza kama walikuwa salama huku hotelini. Dylan akamhakikishia walifika salama na ndiyo walikuwa wanajiandaa kulala, hivyo wakaagana na kuahidiana kukutana kutakapokucha.

Baada ya kukata simu na kuiweka pembeni, Dylan alijirudisha tena mdomoni mwa Grace ili kuendelea na penzi lao. Grace alitaka mambo mengi zaidi ya busu tu, huku Dylan naye akawa anatembeza vidole vyake kwenye mwili mnono wa bibie, akiyapa umakini zaidi mapaja yake yaliyokuwa nje ya 'night dress' yake fupi. Busu yao iliendelea huku Grace akiwa anapumua kwa njia ya miguno, na hapo hapo tena simu ya Dylan ikaanza kuita.

Dylan alipojitoa mdomoni mwake Grace ili aangalie ni nani, Grace akamzuia na kumgeuzia kwake ili waendelee, lakini simu ikaendelea kuita tu. Dylan akasema wacha tu apokee, lakini baada ya kuona uso wenye ishara ya kukwazika kwenye sura ya Grace, akaamua tu kuacha kuipokea ili amridhishe kwanza baby mama wake.

Hangeweza kujua ni jinsi gani simu hizo zilivyokuwa muhimu sana, kwa sababu alitaka kumwonyesha Grace kwamba yeye ni muhimu zaidi. Iliendelea kuita tu, hivyo Dylan akaichukua huku akiendelea kudodosana na mpenzi wake, kisha kwa ujuzi wake akaitolea sauti bila hata kuangalia na kuirudisha pembeni hapo.

Mapenzi matamu-tamu yakaendelea baina ya wawili hawa, bila kujua kuwa usiku huo huo walioufikiria kwamba ulikuwa umeisha ndiyo usiku ambao tatizo lingine lilikuwa limeanzishwa. Waliridhishana baada ya dakika nyingi kitandani hapo, nao wakapitiwa na usingizi wakiwa wamelaliana pamoja.


★★★


'ETHAN, TUNAHITAJI KUONGEA HARAKA NIMEMPATA MTU AMBAYE ALIJARIBU KUKUUA. NI MWANAMKE MMOJA HIVI ALIKUWA KWENYE SHEREHE PIA. UKIPATA UJUMBE HUU NIPIGIE TUONGEE KIJANA WANGU. USIKU MWEMA KWENU.'

Dylan anasoma ujumbe huu muhimu kutoka kwa Baraka baada ya kuamka kwenye mida ya saa 12 kasoro alfajiri. Alikuwa amechukua simu ili aangalie muda na kukuta missed call 23 na meseji hiyo ya Baraka. Kwenye missed call hizo, Baraka alikuwa amepiga simu mara 8, Leila mara 5, na zingine zilikuwa ni za wale walinzi aliowaajiri Grace ili wailinde familia ya Baraka. Alijinyanyua na kuketi vizuri kwa kuwa alitambua hapo bila shaka kulikuwa na kitu muhimu sana, hasa baada ya kuusoma ujumbe wa Baraka. Akaingia sehemu ya bafuni ili aweze kuongea na simu bila kumwamsha Grace; akimpigia Baraka kwanza.

Simu ya Baraka haikupatikana mara tatu zote ambazo Dylan alijaribu kupiga. Hivyo, akampigia mmoja wa wale walinzi.

"Halioo..." mlinzi huyo akasema baada ya kupokea.

"Mattias, vipi? Nimeona call zako baada ya kuamka, kuna shida yoyote?" Dylan akauliza.

"Ndiyo mkuu, kuna tatizo kubwa sana limetokea," Mattias akajibu.

"Tatizo gani?"

"Mzee Baraka ameuawa!"

Dylan aliganda akiwa haelewi jambo alilotoka kuambiwa.

"Unamaanisha nini?" Dylan akauliza.

"Amepigwa risasi usiku huu...nje ya hoteli...aliku..."

"Yuko wapi... yuko wapi sa'hivi?"

"Tuliupeleka mwili wake mochwari. Familia yake tuliilinda hapa hotelini ila..."

"Eh Mungu wangu! No, this can't be. No, no, NOOOO!"

Dylan alisema kwa sauti yenye hasira kali sana na kuirusha kwa nguvu simu yake, ambayo ilikipiga kioo cha humo na kukitia nyufa za kupasuka. Hii ilimshtua Grace, aliyekuwa bado amelala, hivyo akajinyanyua na kuvaa 'night dress' yake ili aende kuona tatizo lilikuwa ni nini.

"Dylan.... Dylan..."

Akawa anamwita huku anauelekea mlango wa bafuni humo. Alipoukaribia, akaanza kusikia sauti za vishindo kutokea humo kama kuna kitu kinapigwa kwa nguvu huku Dylan akitoa kelele zisizoeleweka, nayo hofu ya Grace ikazidi kupanda. Akaingia hapo na kumkuta Dylan akiwa anapiga kioo hicho hicho ngumi mara nyingi sana, na damu ilionekana ikimtoka kwenye kiganja chake hicho alichokunja. Grace alishindwa kuelewa ni nini kilikuwa kimempata, naye akaendelea kumwita tu na kumwambia aache.

Dylan akamgeukia Grace na kumwangalia huku analia, na hapa Grace akawa ametambua bila shaka hasira hizo zilitokana na huzuni ya jambo fulani lililompata. Dylan akawa anatangatanga tu hapo, kisha akakaa chini kwa kujitupa huku analia kwa uchungu. Grace, akaanza kumfata taratibu, kisha akapiga magoti mbele yake na kumshika usoni, akimwagalia kwa kujali sana.

"Dylan.... what's wrong?"

Akamuuliza kwa sauti ya kujali. Dylan akawa analia kwa bila kutoa sauti na kutikisa kichwa chake kwa huzuni huku anamtazama Grace kwa majonzi sana. Grace pia akaanza kudondosha machozi bila kuelewa kikamili kilichoendelea.

"Tell me..." Grace akasema huku anamfuta machozi.

Dylan akajikaza na kusema, "Wamemuua Baraka, Grace.... they killed him."

Grace akaachama mdomo akishangazwa na maneno yake. Hakuamini kabisa kwamba jambo hill lilikuwa limetokea. Dylan akaendelea kudondosha machozi huku ameinamisha kichwa, naye Grace akamkumbatia kwa upendo huku naye akilia kwa huzuni. Akawa akimbembeleza kwa kubusu kichwa chake, naye Dylan akamzungushia mikono yake mgongoni ili kurudisha kumbatio lake.



Kulipokucha hata zaidi, wawili hawa walikuwa wamemaliza kujiandaa ili waelekee kule kwa familia ya Baraka. Ilibidi Grace ashughulikie malipo ya vitu vilivyovunjwa kutokana na hasira ya Dylan kusababisha aviharibu. Alikuwa pia amemsafisha Dylan mkono na kuufunga kwa bendeji ili kusitiri sehemu iliyoumia. Dylan hakuwa na raha hata kidogo. Grace alijaribu hata kumsemesha walipokuwa wakielekea kule, lakini hakumjibu hata kidogo. Ilibidi kumwelewa tu kwa sababu alijua ni jinsi gani alivyompenda sana Baraka, na kifo chake hakikuwa cha haki hata kidogo.

Walipoifikia familia ya Baraka, ilikuwa kwenye majonzi mazito sana hotelini kwao pale. Walikuwa wakilia sana, hasa Shani na Leila, ambao hawakuweza kudhibiti hisia zao hata kidogo. Dylan alilia pamoja nao, akawabembeleza pia, na kuwahakikishia kwa kuwatia moyo kuwa wangeendelea kuwa pamoja kama familia; kushikamana.

Roho ilimuuma sana Dylan kwa sababu aliona jambo hili kuwa ni makosa yake. Alijilaumu moyoni mwake kumwingiza Baraka kwenye matatizo yake ambayo yalikuwa ni hatari sana, na jambo hili likamfanya ajichukie mno. Gilbert na Jaquelin walifika hapo pia kuwafariji wafiwa, na baada ya muda Dylan akaondoka hotelini hapo pamoja na familia hiyo ili kuwarudisha kule kwao.


★★★


SIKU 5 BAADA YA KIFO CHA BARAKA

Mazishi ya Baraka yalikuwa yamefanywa kule kwao ndani ya siku hizo, kukiwa na watu wengi waliohudhuria ili kumuaga mzee huyo aliyependwa na wengi. Ijapokuwa polisi walikuwa wakichunguza ni nani aliyemuua, Grace alimshauri Dylan asiseme kuhusiana na mambo ambayo wamekuwa wakifuatilia kwa muda mrefu na kumwacha tu Jafari ashughulikie kuwasaka maadui zao, kwa sababu kuwaambia polisi kungefanya mambo mengi yajichanganye. Dylan alijua hilo ni kweli, lakini pia kuanzia wakati huo hakuwa tena na uvumilivu wa kusema akae asubirie wakina Jafari wawatafute wabaya wao, hasa baada ya kilichompata rafiki yake kipenzi.

Dylan alihakikisha anaisaidia familia ya Baraka bega kwa bega kwa kila jambo walilohitaji, huku naye akiwa amefikiria cha kufanya ili kumpata "mwanamke" huyo ambaye Baraka alimsema kwenye ujumbe ule. Kulikuwa na wanawake wengi usiku wa party ile hivyo isingekuwa rahisi kujua alimsemea nani; labda kama angemwandikia jina. Siku hii, Jafari alikuwa amefika kwa Grace ili kumpa taarifa juu ya msako wake wa kumtafuta Mr. Bernard. Pamoja na jitihada zake zote lakini hakuwa amempata bado. Dylan alikuwepo ofisini humo pia, akisikiliza tu maongezi yalipokuwa yanaendelea baina ya Grace na Jafari.

"....hatutaweza kuendelea kusubiri. Kadiri wakati unavyopita unajua ni kama ndiyo wanazidi kuwa na nguvu. Jafari, changamka basi. Naona ni kama Bernard anakuzidi akili sasa wakati wewe ni the best," Grace akawa anamwambia.

"Naelewa boss. Bernard ametumia njia fulani ambayo.... sijajua tu kwa kweli. Lakini nahitaji tu time zaidi...."

"There's no more time Jafari," Dylan akamkatisha.

Grace na Jafari wote wakamtazama kwa makini.

"Kila kitu ambacho tumefanya imekuwa ni kujali muda na kusubiri, kusubiri, kusubiri... no more!" Dylan akasema kwa mkazo.

"Dylan naelewa. Najua..."

"No, haujui na hauelewi. Huwezi kuelewa hata kidogo. Grace aliponisimulia kwa mara ya kwanza kuhusu Bernard, nilitaka kumwambia aachane naye, kwa sababu sikuwa nimeelewa maumivu aliyopitia, na nisingeweza kamwe kuelewa. Lakini baada ya hawa washenzi kufanya hivi nimeweza sasa kuona ni jinsi gani inavyoumiza sana. Siwezi kukaa kusubiri tena," Dylan akasema kwa hisia.

"Dylan...." Grace akamwita kwa kubembeleza.

"Grace nimechoka! I can't... siwezi tena kukaa nisubiri Jafari ndiyo afanye kila kitu tu...." Dylan akasema.

"Tunafanya hivi ili kujilinda Dylan. Umeona...wameweza kumuua mtu ambaye wanajua..."

"Kwamba nilimpenda. Exactly Grace, exactly! Akili yangu ilikuwa wapi... yaani nikajitokeza, halafu nikawatambulisha na nyie... Baraka alikuwa na kosa gani Grace? Nani mwingine afuate, wewe? No. Siwezi kungoja tena Grace...."

Dylan alikuwa anaongea kwa simanzi sana. Grace alimwonea huruma, na alimwelewa mno. Akamsogelea na kumshika usoni kwa wororo ili kumtuliza.

"Dylan..."

"Nahitaji kwenda Grace," Dylan akamkatisha.

Dylan akaitoa na mikono yake Grace usoni mwake, mpaka Grace akashangaa.

"Unaenda wapi?" akamuuliza.

"Ninaenda kumchimba na kumtoa huyo bwege kwenye hilo kaburi alilojifichia," Dylan akasema kwa hasira.

"Dylan!" Grace akashangaa.

Dylan akageuka ili aondoke, lakini Jafari akamzibia njia.

"Dylan, siwezi kukubali uondoke. Ni hatari sana kwako. Wanaweza..."

"Nipishe Jafari," Dylan akamwambia akiwa serious.

Jafari akaendelea kusimama hapo hapo.

"Dylan, najua unaumia. Lakini kumbuka kwamba... tuna mtoto Dylan. Usifanye jambo ambalo litasababisha ampoteze baba yake. Uliniahidi kumlea pamoja nami, ukifanya hivi na kuhatarisha uhai wako utakuwa umeivunja ahadi hiyo," Grace akamwambia kwa hisia.

"Dylan, msikilize boss. Tafadhali usitende kwa.... jazba... tafadhali kaa tujadili zaidi," Jafari akamwomba.

Dylan akamgeukia Grace na kumwangalia machoni kwa hisia sana. Kisha akampita Jafari na kuondoka hapo, akiwaacha wawili hao wanauangalia mlango aliotokea.

"Boss, niruhusu nimzuie ikiwa..."

"Mwache," Grace akamkatisha.

"Una uhakika hiyo itakuwa sawa? Labda nimwangalie kwa ukaribu ili asiende mbali sana asije kuumia."

"Hapana. Ana uhakika na anachotaka kufanya. Acha tumwamini. Wewe endelea na ile kazi nyingine," Grace akamwambia.

Jafari akakubali na kisha kuondoka hapo.

Grace akaketi kwenye kiti chake kwa kuhisi uchovu wa kiakili. Aliwaza mengi sana kuhusu maisha haya yenye misukosuko, na hasa usalama wa Dylan pia. Lakini alijipa moyo kuwa mwanaume wake huyo angefanya kitu ambacho huenda kingesaidia, hivyo akaona asubiri tu na yeye afanye alichoridhia kwenye moyo wake ili kuwashinda wabaya wao.

Dylan aliendesha gari lake mpaka sehemu ya mbali kidogo, kisha akaegesha usawa wa miti mingi hapo. Alikumbukia mambo yote aliyofanya na Baraka; tokea alipomsaidia kumpeleka kwake mpaka naye alipokuja kuanza kumsaidia kwa mambo mengi. Alimpenda sana yule mwanaume kama baba, kaka, na rafiki wa karibu yake. Hangeweza kukubali ukatili aliotendewa mwanaume huyo mzuri uishie tu hewani; ilikuwa ni LAZIMA awapate wabaya wake mapema na kuwalipa kwa matendo yao maovu.

Akatoa simu yake na kutafuta namba fulani, kisha akaipiga na kuweka simu yake sikioni.

"Hallo... Bosco... naomba tukutane..." akasema kwa mkazo.


★★★


NYUMBANI KWA BEATRICE

Harleen akawa amerudi nyumbani mapema. Siku hii hakutaka tena kuendelea na kazi kwa kuwa hangeweza kukazia fikira mambo hayo kutokana na kumwaza sana Dylan. Aliwaza mengi kumhusu, na hasa kilichomsumbua akili ilikuwa ni jinsi gani angeweza kumpata tena mwanaume huyo ambaye alimpoteza kipindi cha nyuma kwa makosa yake mwenyewe, na sasa alikuwa mali ya Grace. Bado alimpenda sana, na ni hicho ndiyo kilimfanya akose amani kwa sababu wakati huu Dylan alikuwa wa mtu mwingine.

Baada ya kuingia ndani, alikwenda moja kwa moja chumbani kwake ili kujimwagia maji kidogo. Akatoka baada ya muda mfupi na kuelekea jikoni kuongea na wasaidizi wa kazi hapo. Wakamsalimu vizuri, naye akawaambia wamtengenezee chakula fulani kizuri. Alipomuulizia David, wakamwambia mdogo wake huyo alikuwa kwenye chumba kikubwa cha vifaa mbalimbali ndani hapo (kama stoo), akiwa anatafuta kitu fulani, nao hawakujua ni nini ambacho kilikuwa kinatafutwa.

Harleen akaona aende kumwangalia mdogo wake huko huko. Alipofika akamkuta akiwa anahangaika kutafuta kitu fulani, huku akitoa vitu vingi sehemu yake na kuvirusha ovyo ovyo tu. Alikuwa anaharibu mpangilio mzuri na kufanya mambo yawe shaghalabaaghala tu.

"Wewe, vipi?" Harleen akamuuliza.

David akamgeukia na kusema, "Sh'koo da Harleen."

"Marhaba. Mbona unapaharibu humu?"

"Natafuta Pad yangu."

"Nini?"

"Pad ya...game langu. Siioni."

"Si uiangalie chumbani kwako!"

"Haipo," David akasema kwa huzuni.

"Sasa huku nani kaileta? Ona unavyoharibu vitu... utapatengeneza?" Harleen akauliza kiukali kidogo.

David akaangalia chini.

"Ah yaani wewe! Huku Pad yako haipo. Em' ondoka humu."

"Asa' me nitachezea nini?"

"Ndiyo uwe unatunza vitu vyako. We' ukimaliza unatupa tu, unategemea nini?"

"Dah!"

David akasononeka kidogo na kuanza kutoka humo. Alipomfikia Harleen, akamkumbatia kwa njia ya kudeka.

"Kama imepotea utaninunulia nyingine, si eti?" akamwambia huku amelaza kichwa chake kwenye bega la Harleen.

"Ili upoteze tena?"

"Hamna. Me sijui iko wapi tu, ila kama imepote..."

"Haya sawa nitakununulia. Yaani wewe bado uko kama litoto," Harleen akasema.

David akafurahi sana na kuanza kumbusu dada yake usoni mara nyingi. Harleen akamwambia inatosha na aende sebuleni kwa kuwa soseji zilikuwa zinaandaliwa. Dogo akafurahi na kuondoka, akimwacha Harleen hapo anakiangalia chumba hicho jinsi kilivyovurugwa.

"Kazi wanayo."

Harleen akasema hivyo akimaanishia kazi yote ambayo wasaidizi wao watafanya kukirekebisha. Lakini alipotazama upande fulani kwa chini, aliona kitu kilichovuta uangalifu wake. Akasogea karibu zaidi na kuchuchumaa karibu, kisha akakiokota na kukiangalia. Kwa haraka aliweza kutambua ilikuwa ni 'memory' ndogo sana ya camera, na ilikuwa imebandikwa kikaratasi kidogo cheupe kilichoandikwa maneno "Alfred."

Harleen hakujua ilifikaje humo wala kuweza kukisia ilikuwa na jambo gani kwa ndani, lakini kuona jina la baba yake hapo ilimaanisha huenda kulikuwa na vitu vya zamani vya baba yake au kumbukumbu nyingi zilizotunzwa. Memory hiyo ilikuwa imewekwa ndani ya kifungio (cover) kidogo ili isiharibike, nacho kilikuwa kimechakaa sana kuonyesha ilikuwa ni ya muda mrefu. Akakibandua na kuitoa memory yenyewe, ambayo bado ilionekana kuwa nzima, kisha akatoka kwenye chumba hicho na kuelekea sebuleni akiwa nayo.

Baada ya kumaliza kula pamoja na David, alirudi chumbani kwake ili ajipumzishe, na memory ile akaiweka pembeni kwenye kitanda ili ikiwezekana aje kumpa mama yake kwa kuwa huenda ilikuwa na jambo muhimu. Lakini baada ya dakika chache akiwa ametulia hapo, akaingiwa na udadisi wa kutaka kujua kulikuwa na nini ndani ya memory hiyo, hivyo akaichukua na kuwasha laptop yake ili aweke na kuangalia. Alikuwa na kadi ndogo iliyoingiza memory za aina hiyo na kuiingiza kwenye laptop, hivyo akafanya hivyo na kufungua 'folder' lake.

Mafaili aliyoyakuta yalikuwa 13, na yote yalikuwa ni video. Chini ya kila video kulikuwa na maneno DAY kwa namba; yaani DAY 1, DAY 2, DAY 3, mpaka DAY 13. Hakuelewa maana yake, hivyo akaicheza video ya kwanza, na hapo akapata kumwona mama yake akiwa ofisini mwake. Ilionyesha karibia kila jambo aliloshughulika nalo kutokea juu, naye Harleen akawa ametambua hii ilikuwa ni camera ya kutegwa, kwa ajili ya kumfatilia mama yake.

Aliendelea kuangalia, na hakuna jambo lolote lililoonekana kwenda kwa njia ambayo haikuwa kawaida. Muda wa video hii ulikuwa ni masaa 27, na hilo likamwambia binti kuwa camera hii ingetegwa kwenye ofisi ya mama yake kwa muda mrefu sana ili kumchunguza kwa sababu fulani. Aliamua kuanza kupeleka mbele ili aone mambo kwa haraka, lakini hakukuwa na jambo lolote lenye kushtua.

Akaitoa na kuweka video ya pili, na yenyewe ilikuwa ni kwenye siku nyingine pia, ofisini humo humo. Harleen akaanza kujiuliza ni kwa nini mama yake alikuwa anapelelezwa kwa camera ndani ya ofisi yake, na kwa kuwa memory hii ilikuwa na jina la baba yake, ilikuwa rahisi kuwaza kwamba huenda ni baba yake ndiye aliyekuwa anamfatilia. Hivyo akaendelea kutazama video hizo ili kuona ikiwa kuna jambo lingetokea ambalo liliwahusu wazazi wake kutoka kwa mama yake. Alitazama mpaka video ya 7 kwa kupeleka matukio haraka, na sasa sehemu ya kurekodia ikawa ni kwenye gari la Beatrice.

Ilifikia hatua mpaka Harleen akawa anajiuliza ni nani aliyekuwa anaipachika hii kitu sehemu hizi, kwa kuwa alijua baba yake hangekuwa na muda wa kufanya haya yote, na hivyo bila shaka kuna mtu aliyekuwa anafanya hivyo kwa ajili yake. Pole kwa pole Harleen akawa anausogelea ukweli ambao ulifichwa kwa muda mrefu bila yeyote kujua, na alipoifikia video ya 13, akaacha kupeleka mbele kama vile alivyokuwa akifanya na video zingine. Wakati huu, sehemu hii ilikuwa kwenye chumba fulani, naye akawa amemwona Gilbert ndani humo akiwa ameketi kitandani.

Harleen akashangaa. Akajiuliza baba yake Dylan alihusiana vipi na mama yake kutegeshewa camera kila sehemu, na wasiwasi wake ukaongezeka hata zaidi baada ya kumwona mama yake akiingia ndani humo na kumkumbatia Gilbert. Kilichomshtua hata zaidi, mama yake akaanza kumpiga busu Gilbert mdomoni!

Harleen akaisimamisha kwanza video hiyo. Mapigo ya moyo wake yalikimbia kwa kasi sana, kwa sababu ni jambo ambalo hakuwa ametarajia hata kidogo. Mwanzoni ilikuwa rahisi kufikiri labda baba yake anamfatilia ili kujua kama anatoka na mwanaume mwingine, lakini jambo lisilofikirika kwake lilikuwa ni mwanaume huyo kuwa baba ya Dylan.

Akaamua kuiendeleza ili aone mambo yangekwendaje, naye akaanza kusikiliza maongezi ya wawili hao kwenye chumba hicho. Alimsikia Gilbert akimwambia Beatrice kwamba walihitaji kuvunja uhusiano wao kwa ajili ya familia zao, na jinsi Beatrice alivyokataa hata kusema alikuwa tayari kumtaliki Alfred kwa ajili ya Gilbert. Harleen alianza kuona ufanani fulani kati yake na mama yake kwa kuwa hata yeye kipindi cha nyuma alikuwa kwenye mahusiano na Alex lakini kwa sababu ya kumpenda Dylan alikuwa radhi kumwacha Alex kwa ajili yake; ijapokuwa hilo halikufanikiwa. Aliendelea kuangalia jinsi mama yake alivyombembeleza sana Gilbert mpaka wawili hao wakaanza kufanya mapenzi chumbani hapo.

Harleen akaikatisha video hiyo na kukaa kutafakari mambo kidogo.

Kumbe kulikuwa na mambo mengi yenye kuvunja moyo yaliyokuwa yakiendelea ndani ya familia zao kwa muda mrefu sana. Alivunjika moyo sana alipofikiria kuhusu jinsi alivyokuwa anamheshimu Gilbert ambaye kumbe alikuwa sehemu kuu ya kuharibu ndoa ya wazazi wake. Harleen hata hakukumbuka pindi yoyote ambayo aliona wala kusikia wazazi wake wanagombana kwa sababu ya mambo haya, hivyo akaamua kuangalia ni wakati gani matukio haya yalitendeka. Alipoangalia tarehe ambayo video hiyo ilichukuliwa, alikuta ni mwaka 2012, na hapa akatambua bado alikuwa nje ya nchi kimasomo.

Alikuwa karibu kuifunga laptop yake pale jambo fulani lilipoingia kwenye akili yake. Akaitazama tena tarehe hiyo, nayo ilikuwa ni tarehe 23 kwenye mwezi wa 5 mwaka 2012. Harleen akabaki kuduwaa. Hiyo ndiyo iliyokuwa tarehe ambayo baba yake aliuawa!

Kila jambo lilikuwa linajiongeza kichwani kwake kwa njia iliyomfanya achanganyikiwe. Alianza kuwaza: ikiwa baada ya Alfred kutambua kwamba Beatrice alikuwa anatoka nje ya ndoa, basi huenda waligombana sana, na matokeo yakawa ndiyo kile kilichompata baba yake. Haikuingia akilini hata kidogo kwa Harleen kufikiri kwamba mama yake angeweza kuwa ndiyo sababu ya baba yake kupigwa risasi, lakini uwezekano huo haukuwa rahisi kupuuzia.

Dada wa watu alihisi kushuka sana moyo. Bila kujielewa akaanza hadi kulia chumbani hapo; sana. Pamoja na yote, yaani jinsi mama yao alivyojitahidi kuwatunza kwa upendo tokea baba yao alipoiaga dunia, bado alitaka kujua ukweli wote. Hivyo, akaamua kwamba angefanya uchunguzi kimya kimya kuanzia sasa ili kuweza kuupata ukweli huo, lakini akiwa pia na matumaini kwamba yale aliyohisi kumwelekea mama yake yasingekuwa ya kweli.


★★★


Baada ya Dylan kuwa amekutana na Bosco sehemu fulani wakiwa peke yao, alimweleza rafiki yake huyo kuhusu matatizo yake yote. Bosco alihuzunika sana baada ya kujua kwamba kihalisi Dylan alipangiwa ajali ile ya helicopter, na ni watu hao hao ndiyo ambao walifanya kumuua Baraka, ambaye alikuwa mpendwa wa Dylan. Akamfariji kwa maneno mazuri ya kumtia moyo, kisha Dylan akamweleza kwamba alikuwa anataka kumkamata Mr. Bernard haraka iwezekanavyo, na ni Bosco ndiye angemsaidia kufanikiwa kwa kile alichopanga.

"Umewaza nini?" Bosco akamuuliza.

"Uliniambia kuhusu lile shindano la ngumi... nililokuwaga nafanya kipindi kile..."

"Ndiyo..."

"Bado huwa linaendelea?"

"Ndiyo, linafanywa. Ila, walihitaji kubadili location maana ile ya mara ya kwanza ilivuta attention ya mapopo," Bosco akasema, akimaanisha polisi.

"Sawa. Nahitaji unikutanishe na yule mwanamke," Dylan akamwambia.

"Nani... Queen?"

"Yeah."

"Are you sure? Si ulisema hautakiwi..."

"Ndiyo, lakini now nahitaji sana kuonana naye. Ulisema alini-favour sana kipindi kile... si ndiyo?"

"Yeah... anakukubali sana. Mpaka sasa hajui kama uko hai. Atashangaa. Lakini subiri kwa nini... kwa nini unataka kumwona?" Bosco akamuuliza.

"Ikiwa ana mitandao mingi, basi ninajua atanisaidia kupata nachotafuta. Uliniambia anapenda sana kuvuna pesa nyingi eeh?"

"Sana. Alitaka kukutumia nje za nchi kule ili umtengenezee pesa maana aliona una kipaji."

"Okay. Ninahitaji kufanya makubaliano naye."

"Lakini sasa hivi Dylan una uhakika utaweza kugombana... kama zamani?"

"Usijali. Nikutanishe naye tu, mimi nitaongea naye."

Bosco akaridhia na kuanza kumweleza Dylan kuhusu sehemu ya kwenda ili akutane na Queen. Uzuri ni kwamba siku hiyo kuna mapambano matatu yalikuwa yamepangwa, hivyo Bosco akamwambia wangepaswa kuongea na Queen mapema ili liongezwe lingine lililomhusu Dylan pia, a.k.a Killmonger. Akamwambia atahitaji mask kwa ajili ya pambano, hivyo angemtafutia na kumpatia. Kisha baada ya hapo wawili hao wakaondoka na kuelekea huko kwa ajili ya kukutana na Queen.

Bosco akawa amemtafuta kwa simu Queen na kumweleza kwamba kulikuwa na jambo la muhimu sana alilohitaji kuzungumza naye. Mwanamke huyo alimwambia kwa kitisho kwamba kama lingekuwa ni jambo la kumpotezea muda wake, basi Bosco angeumia, lakini Bosco akamhakikishia kwamba hangekwazwa hata kidogo. Ilikuwa imekwishatimia mida ya saa 12 jioni wawili hawa walipofika kwenye nyumba ya kamari iliyojificha, ambayo ilikuwa ni ya Queen mwenyewe. Baada ya walinzi kuhakikisha hawakuwa na kifaa chochote chenye kudhuru, wakaongozwa mpaka ndani kwenye ofisi ya Malkia huyo.

Walipofika nje ya mlango wa kuingilia ndani ya ofisi ya Queen, Bosco akamwambia Dylan asubirie hapo kwanza ili aingie yeye kuongea na Queen, kisha ndiyo angemwita. Baada ya Bosco kuingia, Queen alimwambia aseme alichotaka, naye Bosco kwa kujivuna akasema alikuwa amepata mpambanaji ambaye angehitaji kumwongeza kwenye mechi kubwa usiku huo. Queen akamwambia hakuwa na muda wa kufanyiwa michezo ya kitoto na Bosco, lakini Bosco akamhakikishia kwamba mpambanaji huyu alikuwa bora sana; yeye mwenyewe asingeweza kukataa ofa hiyo.

Kwa udadisi, Queen akamwambia amwonyeshe ni nani, na hapo Bosco akamwita Dylan aingie humo ndani. Dylan akatii na kuingia, kitu kilichomfanya Queen anyanyuke kutoka kwenye kiti chake, akishangaa sana kumwona mwanaume huyu kwa mara nyingine. Dylan angeweza kusema kwamba sura hii ya Queen haikuwa ngeni sana kwake, lakini bado hakumkumbuka vyema.

"What... what's going on?" Queen akauliza.

"I present to you... KILLMONGER!" Bosco akamtambulisha kwa shauku.

Queen akawa haelewi kabisa. Akaanza kumfata Dylan taratibu akimwangalia kwa udadisi mwingi.

"Aren't you dead? (we si umekufa?)" Queen akauliza.

"Hakufa, Queen. Alisalimika kwenye ile ajali. Now he's back," Bosco akasema.

Dylan alikuwa anamwangalia Queen kwa umakini sana. Aliweza kutambua mwanamke huyu alikuwa ni biashara tu; yaani mwonekano wake ulionyesha kweli pesa ndiyo ilikuwa muhimu sana kwake. Queen pia alikuwa anamtazama Dylan kwa uangalifu, kama anajiuliza mambo mengi sana.

"Well, kwa hiyo... unaweza kupanga pambano lingine si ndiyo?" Bosco akamuuliza Queen.

"Kwa nini nifanye hivyo? Kwa sababu Killmonger amerudi kutoka hell?" Queen akauliza na kuanza kucheka.

Bosco akaishiwa pozi kabisa. Akamtazama Dylan akiwa na wasiwasi.

"Ninahitaji something more than just advertisements. Unataka kurudi kupigana... hiyo inanipa mimi faida gani? Maana wewe hupigani kwa ajili ya pesa si ndiyo?" Queen akamwambia Dylan.

"Naomba kuongea naye mara moja," Dylan akamwambia Bosco.

Bosco akatikisa kichwa kukubali, kisha akatoka nje.

"Najua mambo mengi yamebadilika, lakini nahitaji sana tusaidiane kwa hili," Dylan akamwambia Queen.

"Tusaidiane?" Queen akauliza.

"Ninataka nikutengenezee pesa nyingi leo, sitachukua hata mia, and in return, ninahitaji unisaidie jambo fulani."

"Jambo gani?"

"Kuna mtu nataka umkamate. Yeye ni adui yangu, na amejificha wakati huu baada ya kumuua mtu mmoja... aliyekuwa wa karibu yangu. Ninataka kumlipa kwa kila kitu alichofanya," Dylan akasema kwa hasira.

Queen akamkazia macho na kushusha pumzi.

"Anaitwa nani?" akamuuliza.

"Bernard. Yakobo Bernard Sizwe."

"Kwa hiyo... nitumie njia zangu kumpata, halafu wewe unanilipa kwa kupigana leo? Hiyo inanifaidisha nini mimi?"

"Bosco ameniambia... namaanisha, ninajua watu walikuwa wanampenda Killmonger. Kurudi kwangu kutakuwa hit kubwa, don't you agree?"

"Mm-hmm..."

"Yeah. Bet zote zitakazowekwa kwangu za ushindi, najua zitakuwa nyingi. Fanya kwa njia zako zote unazojua kuweka bet kubwa sana DHIDI yangu," Dylan akasema.

"Dhidi yako? You want me to put a huge bet against you? Huo ndiyo mpango wako wa kunilipa mimi? Kwamba, pesa nyingi niweke ili ushinde, halafu nipoteze. Akili gani hiyo?" Queen akauliza.

Dylan akatikisa kichwa kukanusha.

Queen, baada ya kutafakari alichomaanisha, akaachia tabasamu la mbali.

"Ahah... so that's your game, huh? (kumbe huo ndiyo mchezo wako eh?)" Queen akamwambia.

"So... we got a deal? (kwa hiyo... tumekubaliana?)" Dylan akauliza.

Queen akatazama pembeni, kisha akamwangalia huku anatikisa kichwa kukubali.

"Hauko vibaya, Killmonger. Fanikisha unavyopanga, halafu mimi nitamchimba huyo mtu unayemsema kutoka huko aliko," Queen akamwambia.

Dylan akatikisa kichwa kuonyesha ameelewa.

"Ngoja nikajiandae," Dylan akasema na kisha kutuoka.

Queen alibaki akitabasamu kwa kupendezwa na akili ya Dylan. Bila hata kujua kwamba mwanaume alikuwa amepoteza kumbukumbu yake, alikuwa tayari kuona maajabu ambayo angeleta usiku huo mikononi mwake.



★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★

WhatsApp +255 787 604 893
 
DYLAN

Story by Elton Tonny

Familia, Kazi, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Unyanyasaji, Usaliti, Visasi, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa

(R-rated 18+)

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA THELATHINI NA NANE

★★★★★★★★★★★★★★★★★★


Ilikuwa ni shangwe kubwa kwa mashabiki wa mchezo huu mtandaoni ambao walisisimshwa sana na taarifa kuwa Killmonger alikuwa amerejea tena. Ilikuwa ni miezi mingi imepita tokea mara ya mwisho alipoonekana, na kwa kuwa sasa alirudi, wengi walitarajia bila shaka angeleta mambo mapya kwa kishindo. Pesa za kubashiri zilimiminwa, na kama Dylan alivyotarajia, nyingi zilikuwa upande ambao ulitarajia angeshinda tu, hii ikichochewa na kumzoea Killmonger kuwa mpiganaji wa kushinda kila pambano alilohusika.

Dylan aliingia kwenye chumba cha mazoezi baada ya kufika eneo ambalo mieleka ile iliendeshwa kwa siri. Ni Bosco ndiye aliyempeleka, na kufikia wakati huu tayari mapambano mawili ya kwanza yalikuwa yamekwisha, na sasa la tatu ndiyo liliendelea. Yeye alipangiwa kupambana na mpiganaji mwingine aliyejiita Zagamba, ambaye aliongezwa katika mashindano haya kipindi kile Dylan alivyopotea.

Grace alikuwa amempigia simu Dylan mara kadhaa usiku huo, na sasa kabla pambano la Dylan kuanza akawa amempigia tena. Dylan hakuona sababu ya kuendelea kumkwepa tena mwanamke wake, kwa kuwa pia alihitaji kumwambia jambo alilokuwa amemwahidi angemwambia kila siku. Akapokea simu yake baada ya kutuliza pumzi zake za kupasha.

"Dylan... where are you?" Grace akasikika kwa sauti yake yenye kujali.

"I'm fine Grace..."

"Dylan ninaomba urudi. Tafadhali... naomba URUDI," Grace akasema kwa hisia.

Dylan akafumba macho, kisha akasema, "Usijali sana kuhusu mie, I promise nitarudi salama."

"Dylan..."

"Nilikuwa nataka nikwambie umsalimu baby Grace na.... nakupenda," Dylan akasema.

"Dylan uko wapi? I swear to God ikiwa kitu chochote kibaya kitakupata nitakuua! Naomba urudi la sivyo..."

Dylan akashusha simu kutoka sikioni mwake akijihisi vibaya kiasi kwa kuwa alijua Grace aliumizwa na kitendo cha yeye kuondoka tu bila kusema aliko. Lakini Dylan alijihakikishia moyoni mwake kwamba alichokuwa anafanya kingesaidia sana kutosababishia tena watu wake wa karibu maafa kwa sababu yake.

Mwito wa pambano lililofuata ulisikika, na hapo hapo Bosco akaingia ili kumwongoza Dylan kuelekea ulingoni. Alimtia moyo kuwa alijua ni lazima angeshinda tu hata ijapokuwa bado hakukumbuka mengi vizuri.

"Halafu bro, nimeona Queen ame-bet against you, imekuwaje, kwa nini amefanya hivyo? Nilifikiri umeongea naye..." Bosco akauliza.

"Usijali. Ndiyo lengo langu," Dylan akasema.

"Lengo... yaani... yaani unamaanisha kwamba..."

Dylan akatikisa kichwa kukubali.

Sasa Bosco akawa ameelewa mpango wake ulikuwa ni nini. Dylan akajisawazisha na kuivaa mask yake, kisha akaelekea huko sasa.

Baada tu ya kuwa ameingia, watu waliokuwepo hapo wakamkaribisha kwa vifijo vingi kuonyesha ni jinsi gani alipendwa. Mazingira haya yalikuwa yenye kusumbua sana akili ya Dylan huyu aliyepoteza kumbukumbu, lakini akajitahidi kuiweka akili yake sawa ili kufanikisha mpango wake. Zagamba alikuwa mwanaume mwenye mwili mnene kiasi, na alivaa mask nyeusi usoni huku kifua chake kikiwa wazi. Mwamuzi alipotoa kiashirio kuwa pambano lilitakiwa kuanza rasmi, kengele ikasikika, na sasa wawili hawa wakaanza kuzungukana.

Queen alikuwa kule juu kama kawaida yake, akimtazama kwa makini Killmonger wake. Zagamba alianza kumfata Dylan kwa kasi sana, lakini Dylan akamkwepa. Mara ya pili, ya tatu, ya nne, lakini Dylan akawa anakwepa tu. Hii ilishangaza wengi kiasi, siyo kwa kuwa alikwepa tu, ila ni JINSI alivyokuwa anakwepa. Ilikuwa ni kama anakimbia kabisa, kwa kuogopa, mpaka Bosco akashangaa, ijapokuwa alielewa kwamba hiyo ilikuwa ni sehemu ya mpango wa Killmonger. Wengi walimzoea Killmonger kuwa mpambanaji aliyejua kupigia mahesabu nyendo za adui zake kwa sarakasi, lakini huu mtindo wake mpya uliwaacha hoi.

Zagamba aliendelea kulazimisha mpaka akampata na kumkaba kwa nguvu. Killmonger/Dylan alijitahidi kujinasua, lakini mwanaume huyo alikuwa na nguvu nyingi mno. Alimkaba hivyo hivyo mpaka Dylan akashindwa kujua la kufanya. Kisha Zagamba akamwachia na kumtupa pembeni, huku akijisifu kuzielekea camera zilizowazunguka kwamba mpambanaji mwenzake alikuwa mdebwedo tu. Dylan akajivuta na kunyanyuka, kisha akamfata Zagamba na kuanza kurusha ngumi na mateke bila mpangilio. Zagamba alijihami vizuri na kuwa anamtandika hapa na pale, na kadiri dakika zilivyopita, ilionekana wazi kwamba Killmonger alizidiwa uwezo.

Mwishowe akawa hata hafanyi lolote ila kuruhusu adundwe tu. Alipigwa sana mpaka akadondoka chini na kutulia hivyo hivyo. Mwamuzi alipomwangalia kuona ikiwa angeweza kuendelea, akatoa ishara kuonyesha kuwa hangeweza, hivyo mshindi alikuwa ni Zagamba. Jamaa alijisifu sana na kumfanya Queen, aliyemdhamini, afurahi mno.

Huu ndiyo uliokuwa mpango wa Dylan. Sasa pesa nyingi Queen alizowekea dau kwa Killmonger kushindwa zingerudi kwake na faida kubwa kutoka kwa watu wengine wenye pesa na mashabiki walioweka dau la Killmonger kushinda. Ilikuwa ni njia iliyomletea pesa nyingi sana Queen, na kuanzia hapo dili lao lingekuwa limekamilika.

Killmonger/Dylan alijinyanyua taratibu, naye Bosco akaingia hapo pia. Watu wengi walifadhaishwa sana na Killmonger, kwa kuwa aliyaharibu matarajio waliyokuwa nayo, na pesa zao zilikuwa zimepotea. Lakini kwa Dylan hii ilikuwa ni ushindi, kwa sababu hii ndiyo iliyokuwa njia ya kumlipa Queen ili amkamatie Mr. Bernard.

Baada ya kutoka kwenye ulingo wa pambano, Dylan na Bosco wakaenda kwenye chumba cha kubadilisha mavazi. Bosco alitambua kwamba Dylan alikuwa ameumia sana, lakini akawa anajikaza tu kiume. Wakati huu alijaribu kumshauri waongee na Queen ili amletee watu wa kumtibu, lakini Dylan akakataa kwa kusema tayari Queen alikuwa na jambo anamfanyia hivyo hakutaka kumwongezea mambo mengi.

Lakini bila kutarajia, Queen alileta watu wawili wamtibu; waliokuwa na dawa za kumsaidia apunguze maumivu kwenye sehemu za mwili wake zilizoumia. Wakamsaidia kwa kumpaka dawa na kumzibia sehemu zilizovuja damu, kisha wakaondoka na kuwaacha watatu tu ndani ya chumba hicho. Queen akampongeza sana Dylan kwa kuonyesha umahiri na utayari wa kufanya lolote ili atimize malengo yake. Akamwambia angeanza kumtafuta mtu huyo aliyemtaka na kumuuliza akimpata amfanye nini. Dylan akamwambia akimpata tu amfungie sehemu fulani na kumjulisha ili yeye mwenyewe aweze kuja kushughulika naye.

Queen akatabasamu na kumsogelea Dylan karibu kabisa. Dylan hakujua atarajie nini, hivyo akatulia tu na kumsikilizia. Queen akamshika usoni kwa wororo, kisha akaanza kumpiga denda kimahaba sana! Bosco alitoa macho akiwa haamini alichoona. Baada ya kumnyonya mdomo kwa sekunde chache, Queen akajitoa na kurudi nyuma huku anamwangalia kwa macho yenye upendezi, kisha akaondoka. Dylan akamwangalia Bosco kimaswali, naye Bosco akapandisha mabega juu kuonyesha haelewi somo.

Baada ya hayo wawili hao wakatoka na kuelekea mpaka kwenye gari la Dylan, na ni Bosco ndiye angemwendesha kwa kuwa bado Dylan alihisi maumivu mwilini.


★★★


"Kipindi kile alikulamba shavu, leo kaku-smooch! Ahahah... dili lenu ni nini?" Bosco akauliza, wakati wakiwa mwendoni bado.

"Alinilamba shavu? Kwa nini?" Dylan akauliza pia.

"Ulivyowazingua wale wahuni watatu ndani ya usiku mmoja ili kunisaidia, alipenda sana. Ndo' wakati anaondoka akafanya hivyo. Hata leo nilifikiri alikuwa anataka kuku... ila ikaingia mdomoni kubabake," Bosco akasema.

"Anaonekana kuwa bonge moja la slut," Dylan akasema.

"Dah, malaya tu yule. Pesa nyingi kishenzi anazo lakini anataka zaidi. Hivi unafikiri ka' hangeionga serikali mihela hii ishu yake ingekuwa inaendelea? Basi tu inabidi na sisi tujumuike maana penye hela pana njia," Bosco akatania.

"Ahahah... ssss...aagh..."

"Vipi bado unaumia sana mwanangu?"

"Yeah kidogo."

"Halafu nakupeleka wapi? Hotelini au?"

"No. Sitaki attention. Nahitaji kwenda sehemu ambayo nitakuwa salama zaidi, lakini kwenda home pia namna hii hapana," Dylan akasema.

"Dah, ningesema nikupeleke kwangu ila Jessica atashangaa sana akikuona namna hiyo. Halafu pia hautakiwi kuwa mwenyewe lazima kuwe na mtu wa kukuangalia. Sa' tunafanyaje?"

"Hhh... aam, tuta... tafuta sehemu yenye... sehemu fulani tu nitalala ndani ya gari."

"Asa' na hivyo si ndiyo unakuwa mwenyewe au? Hapana. Lazima nitafute mtu wa kukuangalia," Bosco akamwambia.

"Sidhani ikiwa kuna mtu mwenye kuaminika ninayeweza ku..."

"Yupo," Bosco akamkatisha.

Dylan akamgeukia na kumwangalia kimaswali.

"Kuna... demu fulani. Anaitwa Fetty. Najua atakubali kukusaidia maana anakupenda sana," Bosco akasema.

"Fetty?"

"Ndiyo. Assistant manager wa ile hoteli yako pale.... sijui unaiitaje vile..."

"Fetty... unamjuaje? Tumesoma naye wote au?"

"Hamna. Yule nimekuja kumjua kwenye msiba wako... yaani wakati ule tunafanya msiba tukifikiri umekufa. Nilimwona akiwa peke yake amejitenga maama, analia. Kwa sababu pale hamna aliyenijua nikaona nikae naye pia. Baadae kwenye kufarijiana na nini, tukawa marafiki pia. Nilimwambia kuhusu hii mishe yetu uliyokuwa unafanya, na baada ya muda akaniambia kwamba yeye pia alikuwa anakupenda," Bosco akaeleza.

Dylan akawa ametulia tu kumsikiliza.

"Napajua kwake. Nakupeleka huko," Bosco akamwambia.

"Bosco... hapana, siyo fresh. Kumsumbua mtu sasa hivi halafu..."

"Hapana Dylan siwezi nikakuacha hivyo. Hata me nahitaji kurudi nyumbani maana Jessica hajui kuhusu hii ishu yangu nyingine, kwo' sitakuwa na amani nikisema nikuache tu kwenye gari. Fetty anakujali sana, hatakataa," Bosco akamwambia.

"Anaishi na nani?"

"Peke yake. Ana rafiki yake mmoja anaendaga pale ila sidhani kama yuko naye sa'hivi... ngoja."

Bosco akasimamisha gari baada ya dakika kama 6 hivi na kisha kumpigia simu Fetty. Dylan bado alikuwa anajihisi uchovu na maumivu kiasi, hivyo alikuwa amelaza tu kichwa chake kwenye siti aliyokalia.

"Fetty, vipi nimekuamsha?" Bosco akasema baada ya Fetty kupokea. "Ooh... okay. Sasa... niko na Dylan hapa... ameumia kidogo. Nimemleta kwako maana me kwangu pamebana anahitaji... aa... subiri... ndiyo usijali hajaumia sana yaani... Fetty calm down.... ndiyooo niko naye hapa karibu na nyumba yako ukitoka tu nje utaliona gari.... Haya poa asante sa..."

Dylan akamgeukia Bosco na kukuta ameshika simu mkononi huku anatikisa kichwa.

"Vipi?"

"Si nimekwambia? Hapo tu nimesema umeumia kaanza ku-panick utafikiri nimesema umekufa tena!"

"Kwa hiyo...."

"Anakuja. Huyo hapo."

Dylan akaangalia mbele na kumwona Fetty akiwa analielekea gari lake. Alikuwa amevalia night dress ndefu yenye kung'aa huku nywele zake ndefu akiziachia kufikia mabegani. Bosco akashuka kutoka ndani ya gari na kwenda upande wa Dylan kumfungulia mlango, kisha naye Dylan akashuka pia. Fetty akawawahi mpaka karibu na kuanza kumwangalia Dylan hapa na pale kwa kujali.

"Amefanyaje?" Fetty akamuuliza Bosco.

"Ame...amepigana...kule..."

"Nini?!" Fetty akashangaa.

"Twende tumpeleke ndani Fetty, muda umeenda," Bosco akasema.

Fetty akaona atii tu na kusaidia kumshika ili wampeleke ndani kwake.

Wakati huu, Fetty alikuwa akiishi kwenye NYUMBA ya kupanga, siyo chumba cha kupanga. Yaani nyumba yote alikuwa amepangishwa kwa kulipia kila mwezi. Ilikuwa nyumba ya kadiri tu lakini yenye kupendeza sana. Ilikuwa na sebule pana yenye meza nyeusi ya kioo, masofa machache na TV ya flat screen ukutani. Kulikuwa na sehemu ya jikoni yenye vyombo vingi, stoo ya vifaa mbalimbali, chumba chake cha kulala na kingine kwa ajili ya wageni, bafu na choo humo humo ndani na uwanja mdogo kwa nje uliozungukwa na ukuta mfupi wenye geti kwenye mwingilio. Sehemu kubwa ya chini ilikuwa ni vigae, na palikuwa pasafi sana.

Mwanadada akawaongoza wawili hao mpaka kwenye chumba chake na kuwasaidia kumweka Dylan kitandani hapo. Bosco akamweleza kuhusiana na pambano lake na kwamba alikuwa ameshawekewa dawa, hivyo alichohitaji kilikuwa ni uangalizi tu wa karibu na Fetty ndiye wa kwanza kumfikiria ilipokuja kwenye suala hilo. Fetty akasema bila shaka angemwangalia kwa umakini, hivyo Bosco akamuaga Dylan na kusema angeondoka na gari lake halafu kesho angelirejesha baada ya kulifata lake kule alipoliacha. Akaondoka zake na kuwaacha wawili hao ndani hapo, ikiwa ni saa 7 usiku sasa.

Fetty akamtolea viatu Dylan na kisha akaketi kitandani karibu yake sana, akizilaza-laza nywele zake kwa viganja vyake kwa wororo. Dylan alikuwa anamwangalia kivivu kutokana na uchovu aliohisi, naye Fetty akawa anamwangalia kwa upendo sana.

"Asante... kwa kunisaidia," Dylan akasema.

"Usijali Dylan," Fetty akasema kwa kubembeleza.

"Samahani kwa usu..."

Fetty akamziba mdomo kwa kidole chake kumzuia asiendelee kuongea.

"Usirudie tena kusema unanisumbua, la sivyo sitakusemesha milele," Fetty akamwambia kwa sauti yenye hisia.

Dylan ni kama alikumbuka maneno haya, lakini hangeweza kutambua aliyajulia wapi. Akaona macho ya Fetty yakilengwa na machozi, na kwa sababu fulani akahisi mwanamke huyu alikuwa mbali sana kihisia. Fetty yeye akamkumbatia Dylan kwa wororo sana, naye Dylan aliweza kuhisi kwamba alikuwa analia kwa sauti ya chini. Alikuwa na maswali mengi kichwani, lakini huu haukuonekana kuwa wakati mzuri wa kuanza kuuliza. Fetty akamwachia na kujipangusa machozi, kisha akamwambia alale ili kujipumzisha, na mambo mengine yangefata kesho.

Dylan akakubali, kisha akajilaza vizuri na kufumba macho yake. Aliweza kuhisi vidole vya Fetty vikiendelea kuchezea nywele zake taratibu, na hilo lilimwambia kwamba mwanamke huyu alimpenda kwa kadiri ambayo hakujua vizuri. Akaendelea kusikilizia tu vidole vyake vilivyombembeleza, na usingizi ukamjia muda mfupi baada ya hapo.


★★★


Dylan anafumbua macho yake kukiwa kumeshakucha, naye anahisi kifua chake kikikandwa kwa nguo iliyolowana. Anaangalia vizuri hapo na kukuta ni Fetty ndiye anayemkanda taratibu kwa kitambaa cheupe chenye kulowanishwa na maji yenye ubaridi kiasi. Dylan anatulia tu na kuendelea kumwangalia usoni mwanamke huyo ambaye ni mrembo sana.

Fetty anapokilowanisha kitambaa tena na kuanza kupandisha kuelekea shingoni kwa Dylan, anatambua sasa kwamba ameamka, naye anatulia akimwangalia kwa hisia machoni. Dylan pia anaendelea kumtazama tu bila kusema lolote, kisha Fetty anaendelea kumkanda taratibu.

"Saa ngapi sa'hivi?" Dylan akauliza.

"Saa 3. Unajisikiaje? Kuna sehemu inauma sana?" Fetty akauliza pia.

Dylan akatikisa kichwa kukanusha.

"Kwa nini umerudia tena kupigana Dylan? Hii haifai, ona sasa umeumia!" Fetty akasema kwa kujali.

Dylan akabaki kumwangalia tu.

Fetty akashusha pumzi na kuangalia chini.

"Unahitaji kula. Nimeandaa chakula, ngoja nikufatie..."

Wakati anataka kunyanyuka, Dylan akakishika kiganja chake ili kumzuia asiondoke. Fetty akabaki kumwangalia machoni kwa hisia, naye Dylan alikuwa akimtazama kimaswali.

"Mimi na wewe.... tuliwahi kuwa wapenzi?" Dylan akamuuliza kwa sauti ya chini.

Fetty akaonekana kubabaishwa na swali hilo kwa kuwa alishindwa kutoa jibu, hivyo Dylan akajinyanyua na kuketi, akiwa bado amekishika kiganja chake na kumwangalia usoni kwa ukaribu.

"Sikuelewa kwa nini siku ile kwenye party uliondoka ghafla tu huku unalia. Niambie tafadhali ikiwa... tuliwahi ku-share... jambo fulani..." Dylan akamwomba.

"Hapana. Mimi na wewe... hatukuwahi kuwa wapenzi," Fetty akasema.

Dylan akabaki kumtazama sana.

"Tulikuwa marafiki wazuri tu. Uli...ulinisaidia sana. Mimi na familia yangu," Fetty akamwambia.

Dylan, akiwa anakumbuka vizuri kwamba Bosco alisema mwanadada huyu alimpenda sana, akataka kujua mengi zaidi.

"Nilikusaidia kwa mambo gani?" akamuuliza.

Fetty alianza kumsimulia kuhusu jinsi alivyomsaidia mdogo wake aliyekuwa amepatwa na ajali kupatiwa matibabu mpaka wakati alipotoka hospitali, kuhusu jinsi alivyomsaidia kuipata kazi nzuri kwenye mgahawa wake ambayo ilimsaidia sana akaweza kupiga hatua kadhaa mbele kimaisha mpaka kufikia kwenye nyumba hii na kuwaendeleza wadogo zake kimasomo, na pia kuhusu jinsi alivyomsaidia kihisia kwa njia nyingi sana. Alikuwa hadi analia kadiri alivyoendelea kuongelea mambo yenye kufurahisha aliyopitia na Dylan, naye Dylan akaanza kumfuta machozi kwa huruma.

Baada ya hapo Fetty akanyanyuka na kumwambia angefata chai ili Dylan ale na kupata nguvu. Akamwacha Dylan akiwa anamtafakari sana. Ilikuwa ni hisia fulani ndani yake iliyomwambia alikuwa na ukaribu sana na mwanamke huyu, lakini bado kukumbukia mambo hayo ilikuwa ngumu sana. Mpaka akaanza kujiuliza kama kweli kumbukumbu yake ingewahi kurudi tena, maana daktari alisema zamani mno kuwa ingerudi polepole lakini mpaka kufikia wakati huu hali haikuwa imebadilika.

Mwanadada akarejea akiwa na vyakula mbalimbali vya kunywea chai, akimhudumia Dylan kama alivyokuwa anafanya zamani. Dylan alikuwa akihisi njaa sana, hivyo alikula chakula chote mpaka kikaisha. Fetty alikuwa anamtazama tu kwa upendo, akifurahia kuona jinsi mwanaume alivyokichangamkia chakula chake. Baada ya kumaliza kula akamshukuru, kisha Fetty akamwelekeza bafu lilipokuwa na kumwambia akajimwagie maji kidogo. Yeye akatoka na vyombo akimwacha Dylan anajinyanyua ili akajisafishe. Bado mwili wake ulikuwa na maumivu kiasi, lakini kujikaza ndiyo ilikuwa njia ya kuyapotezea.

Fetty hakwenda kazini siku hii. Aliamua kukaa nyumbani hapo na Dylan siku yote. Hii ndiyo ingekuwa nafasi ya kwanza kwa wawili hawa kushiriki uwepo wa kirafiki kati yao tokea muda mrefu sana. Waliketi pamoja sebuleni wakiangalia TV, na baadae Fetty alipoanza kuandaa chakula Dylan alisaidia kumtayarishia vitu mbalimbali ijapokuwa Fetty alikuwa amemzuia akifikiri bado alikuwa anaumwa sana. Dylan aliongea naye kuhusiana na jinsi alivyosaidiwa na Baraka na jinsi kifo chake kilivyomuumiza sana, naye Fetty alimfariji mno rafiki yake.

Grace hakumtafuta Dylan siku yote, na kwa sababu fulani Dylan pia aliona amwache tu ili akishapoa inavyotakiwa basi angerudi nyumbani kwake hatimaye. Baadae, Bosco alifika nyumbani hapo akiwa na gari la Dylan kulirudisha kama alivyosema angefanya, naye akakaa nao kwa muda mfupi kisha akaondoka kuelekea kwenye biashara zake.



Muda ulisonga siku hii wawili hawa wakiwa ndani ya nyumba hiyo mpaka inafika saa 4 usiku, Dylan alipoomba kwenda kupumzika chumbani. Fetty akaenda pamoja naye pia, zamu hii kwenye chumba cha wageni ambacho kilikuwa na mpangilio mzuri na kitanda kipana tu cha kulalia, kisha Fetty akamwacha mwanaume ajipumzishe. Yeye alirudi kufunga nyumba na kuzima taa za sebuleni, kisha akaenda zake chumbani ili ajipumzishe pia.

Lakini alishindwa. Alijaribu sana kutafuta usingizi lakini akilini mwake aliyezunguka tu alikuwa ni Dylan, kitu kilichomkosesha usingizi kabisa. Alitaka sana kumwambia jinsi alivyohisi kumwelekea, lakini alijua tayari ilikuwa kuchelewa mno. Akajikunyata tu kitandani hapo akiendelea kuusaka usingizi kwa lazima, maana hata simu hakuwa na hamu nayo.

Lakini baada ya dakika kadhaa, mlango wa chumba chake ukagongwa. Alijinyanyua na kukaa, akijua wazi kwamba ilikuwa ni Dylan ndiye aliyeugonga. Mapigo ya moyo wake yalimwenda kasi sana akitarajia vitu vingi mno, naye akanyanyuka na kuufata mlango kisha kufungua akiwa ndani ya night dress yake fupi kufikia mapajani.

Dylan alikuwa amesimama hapo akimwangalia mrembo machoni, kisha akatoa tabasamu hafifu kumwelekea, naye Fetty akatabasamu pia.

"Samahani kama... nimekuamsha..."

"Hapana, sikuwa...sikuwa nimelala," Fetty akamkatisha.

"Oh, okay. Najua...ni usiku na..."

"Dylan usijali kabisa. Jisikie huru kuniambia chochote wakati wowote," Fetty akamwambia.

"Sawa, asante. Ni kwamba tu, ninaondoka kesho hapa kwa hiyo nilitaka kutumia nafasi hii kukushukuru tena. Umenisaidia sana. Kuna vitu vingi ambavyo sikumbuki na hiyo inavunja moyo lakini nataka tu ujue kuwa nimethamini sana ukarimu wako," Dylan akaeleza.

Fetty akabana midomo yake na kutazama chini.

"Usijali. Nimefurahia sana uwepo wako hapa leo," Fetty akasema.

"Mimi pia, nimefurahia sana. Asante. Pia... asante kwa kunikumbushia mambo mengi ya zamani. Nikipata nafasi nzuri nitautembelea mgahawa ule ili nipate chakula hapo, maana imekuwa muda mrefu sana hahah..."

"Sawa. Nitakuandalia vyakula upendavyo siku hiyo."

"Unafahamu hadi vyakula navyopenda eh?"

"Ndiyo. Nyama sanasana."

"Ahahah... umeotea," Dylan akasema.

Fetty alishangazwa na jambo hili kwa kiasi kwa sababu Dylan alilisema bila kutambua kwamba alikuwa na kawaida ya kulisema zamani. Lilikuwa tu limemtoka kinywani kwa kuwa akili yake ilikuwa imezoea kuongea na Fetty kwa njia hiyo ijapokuwa hakukumbuka. Yeye akaona ni kawaida tu, lakini kwa Fetty ilikuwa ni kitu kilichomrudishia kumbukumbu nyingi za nyuma. Dylan akatambua kwamba binti alikuwa anamtazama kwa njia yenye uzubao mwingi.

"Vipi? Uko sawa?"

"Ndiyo... ndiyo niko sawa."

"Ni usingizi eti? Ngoja nikuache upumzike basi..."

"Dylan..."

Fetty akamwahi mkono na kumshikilia alipokuwa ameanza kugeuka ili arudi chumba cha wageni. Dylan akabaki kumwangalia tu usoni na kuona jinsi binti alivyomwangalia kwa hisia sana.

"Naomba unisamehe sana Dylan," akasema huku akilengwa na machozi.

Dylan akashangaa kiasi.

"Nikusamehe kwa lipi Fetty?"

"Siku hiyo kama ningekuonya mapema wala yale majanga yasingekukuta," akasema Fetty kwa huzuni.

Dylan akamsogelea na kumshika shavuni kwa wororo.

"Usijilaumu kwa mambo hayo. Haikuwa makosa yako," Dylan akasema.

"Siyo rahisi kwangu kukaa na rundo la hisia za majuto nikifikiria mambo mengi magumu uliyopitia kwa sababu tu nilishindwa kukua...."

"Shhh... Fetty, tafadhali... usijilaumu. Wewe haukujua kilichoendelea. Na hayo mambo yamepita... niko mzima sasa."

Fetty akaanza kudondosha na machozi kabisa. Dylan akawa anamfuta kwa huruma.

"Kama tu ninge...kama tu ningekwambia kwamba...kwamba..."

Fetty akawa anashindwa kumalizia sentensi yake, lakini Dylan akawa amemwelewa. Alijua mwanamke huyu alikuwa na mkazo wa kihisia sana, lakini haikuwa sehemu yake kumsaidia kuzituliza ukitegemea tayari alikuwa na mtu mwingine. Akashindwa amwambie nini ili kumfariji, hivyo akaona amkumbatie tu ili kumpoza kidogo. Alipomwachia taratibu ili amsemeshe, nyuso zao zikawa karibu sana kiasi kwamba maneno aliyokuwa ameandaa kumwambia yakamtoka kichwani kabisa na kubaki kuitazama sura nyororo ya mwanamke huyu.

Fetty alikuwa anamtazama Dylan kwa hisia mno, na hapo hapo akaifata midomo ya mwanaume na kumbusu kwa upendo!



★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★

WhatsApp +255 787 604 893
 
DYLAN

Story by Elton Tonny

Familia, Kazi, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Unyanyasaji, Usaliti, Visasi, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa

(R-rated 18+)

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA THELATHINI NA TISA

★★★★★★★★★★★★★★★★★★


Dylan akabaki macho wazi, akiwa hajui ni jinsi gani angepaswa kuitikia wonyesho huu wa upendo kutoka kwa Fetty.

Fetty alipouachia mdomo wa Dylan kidogo, akaubusu tena kimahaba sana huku akiwa amefumba macho yake. Sasa mwanaume akaanza kupatwa na hisia kali zilizofanya aanze kurudisha busu hii. Akili yake ilikuwa ikijaribu kupingana na kitendo hiki lakini moyo wake ukamsukuma kuendelea kuipokea midomo laini ya bibie. Fetty alianza kuitembeza mikono yake kichwani kwa Dylan, naye Dylan akamshika kiunoni taratibu huku wakiwa wanaendelea na busu yao.

Miguno ya chini kutoka kinywani mwake Fetty ilisikika vyema kwa Dylan, na sasa jamaa akawa akitambua kuwa jambo hilo lingeenda mbele sana; sehemu ambayo haikutakiwa. Kumfikiria Leila, jinsi alivyomsaliti na kusababisha aachane naye, na Grace, ambaye alikuwa amemsaidia kwa mengi mpaka kuwa naye kimapenzi, kuliighafilisha akili ya Dylan kwa kadiri kubwa na kumfanya aushike uso wa Fetty na kuachanisha midomo yao.

Fetty alikuwa anapumua kwa kasi kutokana na kupandwa na hisia nyingi, na macho yake yalionyesha uhitaji mkubwa sana wa kutaka Dylan azitulize hisia hizo.

"Fetty..."

Kabla Dylan hajamalizia alichotaka kusema, Fetty akamwekea kidole chake juu ya mdomo wake ili kumzuia. Ni kama alikuwa ameshaelewa kile ambacho Dylan alitaka kusema, lakini akawa hataki kukisikia. Akakitoa kidole chake taratibu na kuusogeza mdomo wake mpaka kwenye mdomo wa Dylan na kuigusisha kwa wororo.

Harufu nzuri ya Fetty iliingia vizuri sana puani mwa Dylan, nayo kwa kiasi kikubwa ilimfanya aufurahie zaidi ukaribu huo wa mwanamke huyu. Midomo ya Fetty ikaanza kuikandamiza ya Dylan zaidi, na ulimi wake ukawa unatafuta njia ili kuweza kuingia ndani ya mdomo wa jamaa. Dylan akafungua mdomo wake na kuupokea wa mrembo huyu, na wote wakaanza kuzungushiana ndimi zao kimahaba tena.

Jambo hili lilikuwa linatembeza hisia kali sana mwilini mwa Dylan, na kwa sababu asiyoijua ilikuwa ni kama mawazo yake yote yaliyomuandama yalitoweka kadiri alivyoendelea kupiga busu na Fetty. Wakaendelea kuonyeshana penzi la mdomo kwa sekunde kadhaa, na sasa Fetty akawa anarudi nyuma-nyuma kuingia ndani ya chumba chake bila kuuachia mdomo wa Dylan.

Dylan alijihisi utofauti wa hali ya juu sana, na hasa hii ilitokana na ukweli wa kwamba hakuwahi kufanya jambo kama hilo akiwa kwenye uhusiano na mtu mwingine, kwa hiyo ngazi za kusisimuliwa na kitendo hiki zilikuwa za juu. Hakuna hata sekunde moja iliyopita ambayo Dylan aliendelea kufanya hivi bila kumfikiria Grace. Lakini ni kama kuna kitu kilimsukuma tu aendelee licha ya kwamba akilini alijua hakupaswa kufanya jambo hilo kwa kuwa, kama ni mambo mengi aliyochukia zaidi, ilikuwa ni kufanyiwa usaliti, lakini sasa yeye ndiyo alikuwa anaufanya.

(........).

(........).

(........).

(........).

Wote walibaki wakipumua kiuchovu baada ya kupeana mapenzi kwa mara ya kwanza.

Fetty ndiye aliyejihisi furaha isiyo na kifani baada ya kushiriki mwili wake na mwanaume aliyempenda sana. Dylan kwa upande wake alihisi kitulizo pia, ingawa alielewa kwamba hii ingekuwa ni kitu ya muda mfupi sana kwa kuwa tayari alikuwa wa mtu mwingine. Mwanaume akajigeuza na kulala chali pia, akiwa karibu kabisa na kichwa cha Fetty, wote wakitazama juu huku wameshikana viganja vyao kitandani hapo.

Fetty akamgeukia Dylan, kisha kwa upendo akambusu kwenye shavu lake. Dylan akamwangalia pia, naye Fetty akaanza kuibusu midomo yake taratibu.

"Ninajua unachowaza Dylan," Fetty akamwambia baada ya kujitoa mdomoni mwake.

"Nawaza nini?"

"Kwamba haya ni makosa."

"Hapana... siyo..."

"Usijali Dylan. Ninakujua vizuri. Ninajua huwa hupendi kusalitiwa, na jambo hili tulilofanya limekufanya ujione kama msaliti. Naelewa," Fetty akasema kwa hisia.

"Unajuaje hilo?"

"Kipindi kile niliona jinsi ulivyotaabika Harleen alipokusaliti, kwa hiyo najua jinsi unavyohisi."

"Harleen? Mtoto wa rafiki yake mama?"

"Ndiyo."

"Niliwahi kutoka naye?"

"Ndiyo."

Dylan akashusha pumzi huku akimwangalia bado.

"Usijichukie wala. Nikuombe tu samahani kwa sababu nimekuwa mbinafsi. Ninajua hatukupaswa ku..."

"No, please usiseme hivyo," Dylan akamkatisha.

Fetty akawa anamtazama tu kwa hisia.

"Labda mimi pia nitakuwa mbinafsi kwa kusema hivi, lakini ukweli ni kwamba nimefurahia penzi lako Fetty. Ni sawa kusema hii haikuwa sahihi, na mimi ningejuta sana kufanya hivi wakati nikiwa kwenye uhusiano na mtu mwingine nayempenda, lakini sijui ni kwa nini tu sihisi kujuta kufanya hivi na WEWE," Dylan akasema kwa hisia pia.

Fetty akaachia tabasamu hafifu kwa kuyapenda sana maneno ya Dylan. Akaanza kuushika uso wake na kutembeza vidole vyake kwenye nywele za jamaa, akimwangalia kwa upendo sana. Alipotaka tu kuifata midomo yake ili ambusu kwa mara nyingine, simu ya Dylan ikaanza kuita. Dylan akageuka taratibu na kuichukua, na hapo akapata kuona mpigaji hakuwa mwingine ila Grace. Akamwangalia Fetty, naye Fetty akamtikisia kichwa kumwonyesha kuwa ilikuwa ni sawa akipokea tu.

Dylan akaongea na Grace, ambaye aliuliza mwanaume wake huyu angerudi wakati gani kwa kuwa alihofia usalama wake na alikuwa amem-miss sana. Dylan akamwambia kuwa ni kesho ndiyo angerudi nyumbani, na kumwambia asiwaze sana kwa sababu alikuwa sehemu salama. Kwa umalizio, kumwambia Grace kwamba anampenda kilikuwa ni kitu kilichoichoma sana nafsi ya Fetty. Hakuweza kujizuia kutamani kwamba ingekuwa ni yeye ndiyo angepaswa kuambiwa maneno hayo, na kujua kwamba jambo hili alilofanya na Dylan halingewezekana kurudiwa tena kulimfadhaisha, lakini hakukuwa na jinsi.

Baada ya Dylan kumaliza kuongea na mpenzi wake halisi, akamgeukia tena mpenzi wake wa wakati huu na kumwangalia kwa hisia sana. Fetty akampa tu tabasamu dogo, kisha akanyanyuka na kwenda zake bafuni. Dylan alijua wazi kwamba hiki kilikuwa ni kizungumkuti kikubwa sana, na hisia zake zilivurugika mno kila mara alioomuwaza baby mama wake. Alijua ikiwa Grace angetambua kuhusu kitendo hiki, basi angevunjika moyo sana na huenda hata kukasirika. Lakini kitendo chenyewe kilikuwa kimempa aina fulani ya furaha ambayo ilimfanya ajiulize ni kwa nini ilikuwa hivyo. Labda alikuwa na hisia za upendo kumwelekea Fetty pia? Kama ni hivyo, zilianza lini? Alijikuna sana kichwa kwa kukosa majibu sahihi.

Fetty akatoka kujimwagia maji bafuni na kurudi chumbani. Alivaa tena night dress yake mbele ya Dylan, kisha akapanda kitandani na kujilaza kifuani kwa jamaa, bila kumwambia lolote. Hali hii ilimshangaza kiasi Dylan. Fetty alikuwa mwanamke wa aina tofauti kabisa. Yeye akamwekea tu mkono mgongoni na kumwacha alale hapo mpaka usingizi ulipowapitia wote bila kusemeshana chochote kabisa baada ya kupeana mapenzi yao ya marufuku usiku huo.


★★★


"Kweli?" Grace akamuuliza Jafari, wakiwa wanaongea kwa simu.

"Ndiyo. Nilipata tip kuhusu alipokuwa, lakini nilipofika sehemu hiyo nikakuta hayupo. Kilichoshangaza ni kwamba mlinzi wake alikuwa amezimia hapo kwa muda mrefu sana; karibia kufa kabisa," Jafari akamwambia.

"Kwa hiyo kuna mtu, au watu walimvamia na kumteka unataka kusema?" Grace akauliza.

"Inaonekana hivyo boss. Sina uhakika sana lakini... nadhani kwamba..."

"Itakuwa ni Dylan," akamalizia Grace.

"Ndiyo. Lakini amewezaje kufanya hivyo kwa kasi sana boss? Na Mr. Bernard atakuwa amemweka wapi?"

"Ngoja niongee naye ili nijue kama kwe...."

Kabla hajamaliza maneno yake, alisikia horn ya gari nje ya geti la nyumba. Akakisia kuwa huenda Dylan alikuwa karudi, na moyo wake ukaingiwa na furaha kwa tarajio hilo.

"Nitakupigia baadae Jafari, keep me updated," Grace akamwambia.

Baada ya kukata simu, akanyanyuka kutoka sehemu aliyokuwa amekaa sebuleni hapo na kutazama nje kupitia dirisha pana na refu usawa wa mlangoni. Aliona gari likiingia ndani na kuegeshwa, kisha Dylan akashuka na kuanza kuja usawa wa mlango wa nyumba. Mwanaume alipoingia ndani, aliweza kumwona Grace akiwa amesimama hapo, akimtazama kwa njia fulani iliyo serious. Akatulia tu usawa wa mlango akimwangalia kwa hisia sana, na kumbukumbu ya kwanza akilini mwake lilikuwa ni kile alichofanya na Fetty usiku wa jana. Alijihisi vibaya kwa kadiri kubwa kwa kuwa ikiwa asingemwambia, basi angekuwa bonge moja la mnafiki kwenye uhusiano wao. Lakini tena ikiwa angemwambia huenda ingesababisha matatizo ambayo yangevuruga umoja wao ambao ulikuwa muhimu hasa kwa ajili ya mtoto aliyekuwa njiani. Akashusha tu pumzi na kuanza kumfata mwanamke wake pale alipokuwa amesimama.

Baada ya kumfikia karibu zaidi, akamkumbatia kwa upendo huku akijihisi kuwa mwenye hatia sana, mpaka akawa anakaribia kulia. Grace akajitoa kwenye kumbatio lake na kumtazama tu usoni, akionyesha wazi kwamba alikuwa ameudhika.

"I'm sorry," Dylan akasema kwa sauti ya chini.

"Jana kwa kuwa hukuwa ofisini, closure nyingi..."

"Naelewa Grace. Nitazishughulikia... ninaomba unisamehe sana Grace... sana," Dylan akasema kwa hisia.

Grace akatazama pembeni.

"Najua nimekukwaza, hapana... nimekuumiza. Grace, sitarudia tena kukutendea hivi. Nimekuwa mbinafsi sana, sana, sana. Ikiwezekana niadhibu maana... am so sorry. Yaani sijui..."

"Dylan stop, please..." Grace akamkatisha.

Dylan akabaki kumwangalia tu kwa huzuni.

"Kwa nini nikuadhibu? Ndiyo umekuwa mbinafsi, lakini ikiwa uliona ni sahihi kufanya vile ili umpate Mr. Bernard, basi hakuna haja ya kuomba samahani," Grace akamwambia.

Dylan akatazama chini kwa huzuni, akiwa anaelewa kwamba Grace hakujua samahani yake ilikuwa na mapana mengi.

"Ila usije kurudia kutoka tu... unaondoka kwa hasira... Dylan nakupenda sana. Ninajua ulikuwa na maumivu mengi kwa sababu ya Baraka lakini nami sitaki kukupoteza pia...unataka..."

Dylan akamkatisha kwa kuanza kumpiga busu taratibu kwa upendo mwingi sana. Grace aliitikia vyema pia na kuibusu midomo ya Dylan kwa shauku kubwa kimahaba, kisha Dylan akaiachia midomo yake taratibu na kuweka paji lake la uso kwenye paji la Grace.

"Nakupenda pia Grace. Sana. Hutanipoteza... I promise you that," Dylan akasema kiustaarabu.

"Shikamoo kaka Dylan," sauti ya Matilda ikasikika.

Dylan akajitoa kwenye paji la uso la Grace na kumwona msaidizi huyo wa kazi akiwa amesimama umbali mfupi kutokea walipokuwa.

"Marahaba Matilda. Za hapa?" Dylan akajibu.

"Nzuri."

"Anakula vizuri huyu?" Dylan akamuuliza Matilda.

"Ndiyo," Matilda akajibu akiwa anatabasamu.

Grace akatabasamu pia huku akiwa ameubana mwili wake kwenye mwili wa Dylan, akimwangalia kwa njia ya kudeka.

"Niwaandalie chakula?" Matilda akauliza.

"Ndiyo Matilda. Au ulikuwa umeshakula?" Grace akamuuliza Dylan.

Dylan akatikisa kichwa kukanusha.

Hivyo, Matilda akarudi jikoni kuwaandalia vyakula.

"Umetumia njia gani mpaka ukampata Bernard?" Grace akamuuliza Dylan.

"Aam... bado sijampata. Nimeomba msaada wa rafiki yangu anisaidie kumpata maana ana njia nyingi sana."

"Njia illegal?"

"Kwa kiasi fulani."

"Kwa hiyo huyo rafiki yako bado hajampata?"

"Ndiyo anamtafuta. Atanijulisha endapo..."

"Inaonekana ameshampata," Grace akamkatisha.

"What?"

"Jafari alikuwa amekaribia sana kumshika, lakini akakuta ameshachukuliwa na watu fulani," Grace akamwambia.

"Kumbe? Bado sija..."

Wakati akisema hivyo simu yake ikaanza kuita, naye akaitoa na kukuta ni Queen ndiye aliyekuwa anapiga. Akapokea.

"Queen..."

"Killmonger... we have your guy (tumempata mtu wako)," Queen akasema.

"Whoa! Mmempataje haraka namna hiyo? Nilifikiri itachukua siku kadhaa," Dylan akasema.

"Bullshit! Hapa Tanzania kuna sehemu ya kujificha sasa? Ninaye. Analetwa huku ASAP. Unataka nimfanye nini sweety?" Queen akasema.

"Nielekeze sehemu mtakayomweka ili nije hapo. Na tafadhali naomba favour moja...."

"Nini hiyo?"

"Pigeni mijeledi huo mwili mpaka nitakapofika, na asife."

Queen akacheka.

"Okay my Killmonger. Nakutumia location, wahi uje," Queen akamwambia.

Kisha Dylan akakata simu na kumtazama Grace, aliyekuwa anamwangalia kimaswali.

"Queen ni nani?"

Swali la Grace lingempa nafasi Dylan ya kuanza kumweleza kuhusu njia aliyotumia mpaka akafanikiwa kumpata Mr. Bernard, na baada ya kuwa ametumiwa kwa ujumbe sehemu aliyoshikiliwa mwanaume huyo, Grace akasema angekwenda pamoja naye pia ili hatimaye aweze kuonana naye ana kwa ana baada ya miaka mingi sana kupita.


★★★


Harleen alinunua vifaa vidogo sana vya kurekodia sauti (mini audio recorder), na kuvipachika kimoja kwenye gari la mama yake na kingine chumbani. Vilikuwa vimeunganishwa kwenye spika zake ndogo ambazo angekuwa nazo yeye muda wote ili kuweza kusikiliza mazungumzo ya mama yake wakati wowote ule. Ijapokuwa hakuwa na uhakika kama sehemu hizo alizotegeshea zingekuwa na matokeo mazuri, alitumaini angepata tu jambo fulani lenye kumjuza ni nini ambacho mama yake alikuwa anafanya wakati huu.

Sababu kuu ilikuwa hasa ni baada ya kuona video zile za kurekodiwa ambazo bila shaka alijua ni baba yake ndiye aliyezirekodi kupitia kwa mtu fulani. Lakini pia, usiku ule aliomkuta mama yake anaongea na simu chumbani, alikuwa amemsikia akisema "zote zimwishie mwilini," na kwa haraka hakuweza kuelewa maneno yake hayo yalimaanisha nini, lakini kwa sasa akayatilia maanani na kufikia mkataa kwamba kuna kitu ambacho mama yake alikuwa anafanya ambacho, hakikuwa sawa.

Ndani ya siku hizi chache ambazo alikuwa ameanza kumfatilia mama yake, hakupata kumsikia akisema jambo lolote lenye kushtusha, lakini akawa makini kutegea nyakati ambazo alikuwa angekuwa chumbani au kwenye gari ili asikilize. Ndipo siku hii ilipofika, akasikia mama yake akisema maneno yaliyomwacha akiwa haamini kabisa masikio yake, na sijui angeamini ya nani sasa!

Ilkiwa ni usiku wa siku hii sasa, wakati wote wakiwa nyumbani kwao wakila, Beatrice akapigiwa simu na kunyanyuka kwenda kuongelea chumbani kwake. Harleen naye akanyanyuka na kwenda kwenye chumba chake ili aweze kusikiliza maongezi hayo kupitia kifaa chake.

"...wakati mwingine ninatamani tu niwafate na kuwa-shoot wote! Wananikera sana.... Hakuna.... Nimesema hapana Bernard, acha nifanye mambo navyojua kuwa sahihi... hawawezi kunishinda hata siku moja.... Kama wanafikiri wamepiga hatua mbili mbele zaidi yangu wamefeli sana, mimi niko tatu mbele zaidi! Kama vipi wakamuulize yule kachero wao Baraka... na bado...."

Harleen alikuwa anajua kuhusu msiba uliompata Baraka. Kilichomshangaza ilikuwa ni kwa nini mama yake angesema maneno hayo kuhusu mwanaume huyo aliyeuawa kikatili namna ile.

"....natafuta tu nafasi nzuri nimkarabati huyo Dylan... nikimmaliza huyo nafata na Jaquelin... nimeshachoka kuigiza kuwa BFF sasa! ... Sitaki kutumia mtu kwa hili Bernard, nitadili nalo mimi mwenyewe... Una mpango gani huko uliko? ...."

Harleen aliendelea kusikiliza maongezi hayo akiwa amechoka kihisia. Ikiwa mama yake ndiye aliyemuua Baraka, na alikuwa akipanga kumuua Dylan na Jaquelin, basi ni yeye pia ndiye aliyemuua baba yake! Lakini alijiuliza ni kwa nini mama yake alikuwa anafanya haya yote. Ndiyo alielewa kwamba inaonekana zilikuwa ni hasira tu kwa sababu hakuendelea kuwa na Gilbert tena. Ila mpaka kufikia hatua ya kuua watu, tena wengine wasio na hatia, ni kitu ambacho kilimuumiza sana Harleen. Hangeweza kuruhusu maovu haya yaendelee tena, hivyo akaamua kufikisha taarifa hizi kwa Dylan ili achukue hatua ya kumdhibiti mama yake kabla hajaumiza mtu mwingine yeyote.

Wakati Harleen akijiandaa ili aondoke, Beatrice alikuwa amemaliza kuongea na simu yake pale alipotaka kuiweka kwenye meza yake ndogo ya humo na kuangusha kilainishi cha uso chini baada ya kukipamia. Akachuchumaa ili kukiokota, na hapo akaanza kuona mwanga mwekundu wenye kufifia ukitokea chini ya meza hiyo. Hii ikavuta umakini wake, naye akasogeza mkono wake na kugusa hapo kwa chini. Alihisi kitu fulani kigumu kiasi kwenye kidole, hivyo akakishika na kukichomoa hapo. Alishtuka sana baada ya kutambua kilikuwa ni kifaa cha kusikilizia sauti na kurekodi pia.

Maswali mengi yaliingia akilini mwake. Ni nani aliyeweka kifaa hicho humo, kwa usahihi kabisa kuonyesha kwamba alikuwa anamfatilia? Hakukuwa na yeyote aliyekuja kwake, na hapo kwake walioishi ilikuwa ni yeye, watoto wake wawili, na wasaidizi wa kazi, pamoja na mlinzi wa nyumba. David hangeweza kupata kifaa cha namna hiyo kwa sababu kwa kukiangalia kilikuwa na gharama. Hivyo ikawa wazi kwake kwamba ni binti yake ndiye aliyekitega humo. Lakini kwa nini angefanya hivyo? Na alikuwa ameanza kumpeleleza tokea wakati gani?

Kutokana na maswali mengi aliyokuwa nayo kichwani, na kutambua kwamba ni muda mfupi tu alikuwa ametoka kuongea na Mr. Bernard ikimaanisha alikuwa amesikiwa, akatoka haraka sana kwenye chumba chake na kukifata cha Harleen. Alipofika, akamkuta binti yake akiwa anavaa sweta jeusi, huku chini akivalia suruali ya jeans na sneaker nyeupe miguuni. Alipomwangalia machoni, alitambua kwamba Harleen alikuwa analia, na hapo hapo Harleen akaacha kumtazama mama yake na kujifuta machozi huku anaweka simu yake mfukoni.

Beatrice akaingia ndani humo akitembea taratibu, mapigo ya moyo yakimkimbia kwa kasi kutokana na wasiwasi mwingi aliokuwa nao.

"Harleen... ni wewe ndiyo umeweka hiki kidude chumbani kwangu?"

Beatrice akauliza hivyo, naye Harleen akamwangalia. Lakini hakusumbuliwa tena na hilo kwa kuwa tayari ukweli aliujua, hivyo akampita ili aondoke. Lakini Beatrice akamshika mkono na kumng'ang'ania.

"Nijibu... wewe ndiye..."

"Ndiyo. Ni mimi," Harleen akamkatisha.

Pumzi za Beatrice zikaanza kupanda. Harleen akawa anatikisa kichwa kwa kuhuzunika.

"Harleen... nisikilize. Chochote kile ulichosikia usichukulie kwa njia... haiko kama unavyofikiria..."

"Ila ikoje?"

Beatrice akashindwa kuongea.

"Nielezee. Baraka, rafiki yake Dylan, umemuua. Unataka kumuua Dylan na mama yake pia. Hebu nipe sababu moja muhimu ya kujitetea ambayo itahalalisha unyama unaofanya mama!" Harleen akasema huku analia.

"Hapana... hapana... hapana... Siyo hivyo Harley... nisikilize baby. Mimi ni mama yako. Sawa? Nina maana yangu... usiamini kila kitu ulicho..."

"Nisiamini nini mama? Kwamba wewe ni muuaji? Ingekuwa nimeambiwa tu na mtu... nimesikia mimi mwenyewe! Mama why? Just... unawezaje kufanya hivi?" Harleen akaongea kwa simanzi nzito.

"No, no, no, no.... Harleen.... baby tukae chini tuongee...nitakueleza kila kitu honey. Ona... hiyo simu... huyo nilikuwa namzingua tu, mimi siwezi kufanya mambo hayo. Kwa nini kwanza nifanye hivyo? Siwezi. Harleen...unanijua vizuri... siwezi kuua mwanadamu mwenzangu bila saba...."

"INATOSHA!" Harleen akasema kwa sauti ya juu.

Beatrice akabaki kumtazama kwa presha.

"Mimi siyo mtoto mdogo. Na uko sahihi. Nilfikiri ninakujua. Lakini kumbe sijakujua hata kidogo. Niachie... nimesema niachie! Mikono yako yenye umwagaji wa damu inanichafua!"

"Harleen...."

"Eti natafuta nafasi nzuri nimkarabati huyo Dylan! Mama, kijana wa watu amekukosea nini? Hivi kweli unataka kusema obsession yako kwa uncle Gilbert ndiyo imekupoteza namna hiyo?"

Maneno ya Harleen yakamfanya Beatrice atoe macho kwa mshangao. Hakutarajia kwamba Harleen alikuwa anajua kuhusu yeye na Gilbert.

"Ndiyo mama. Ninajua mlikuwa mna affair na baba yake Dylan. Lakini hata yeye alikuelezea kwamba hamkupaswa kuendelea kwa ajili ya familia zenu. Kwa nini umeamua kuwa chizi wa mapenzi kwa mtu ambaye ni wazi hakutaka tena kuwa na wewe?" Harleen akasema kwa hisia.

"Umejuaje hayo yote?" Beatrice akauliza kimshangao.

"Does it matter? Ni kwamba nimeshajua ukweli mama. Nini kinafata? Na mimi mtaniua kama mlivyomuua baba?" Harleen akasema kwa hisia kali.

Beatrice akaanza kurudi nyuma akiwa ameshtushwa na maneno ya binti yake. Alipandwa na presha ghafla. Harleen akawa anamwangalia huku machozi yakimtiririka

"Ni wewe na uncle Gilbert ndiyo mlimuua baba, si ndiyo? Niambie mama!" Harleen akasema kwa hisia.

Beatrice akaanza kutetemeka, hadi jasho likaanza kumtoka.

"Wewe ni mnyama mama! Najihisi kama... hhh... I hate you!" Harleen akasema kwa sauti kali sana.

Beatrice akashindwa kujikaza na kuanza kulia kwa majonzi sana.

"Ni lazima nihakikishe ubaya wako unakomeshwa. Siwezi kuruhusu uumize watu wasio na hatia kwa tamaa zako za kijinga... never," Harleen akasema.

"Harleen please... nisikilize my..."

"Don't touch me... don't..touch me!"

Harleen akamsukuma mama yake kwa nguvu na kusababisha aangukie chini.

Beatrice alikuwa analia sana.

Bila kuchelewa Harleen akatoka ndani humo ili aondoke, na mlangoni aliweza kumkuta David akiwa amesimama huku analia pia. Akamwangalia kwa sekunde chache, akishindwa hata amwambie nini mdogo wake, naye akatoka upesi na kwenda mpaka kwenye gari lake. Beatrice alibaki kulia tu ndani ya chumba cha Harleen, akihisi maumivu mengi sana kutokana na maneno ya binti yake.


★★★


Dylan pamoja na Grace walifika eneo ambalo walikuwa wameelekezwa na Queen. Kulikuwa na jengo dogo sehemu hiyo liliozungukwa na gari chache, na huu ulikuwa ni upande wa mji wao wa kule walikoishi familia yake; yaani Gilbert na Jaquelin. Eneo hilo lilizungukwa na miti mirefu na giza zito pia, lakini mwanga wa taa za gari ulimulika vyema kuwaonyesha wawili hawa mambo vizuri. Waliposhuka kutoka ndani ya gari, walifatwa na wanaume wawili ambao walikuwa ni kama walinzi wa Queen, nao wakawaambia wawafuate ili kuwapeleka hadi ndani ya nyumba ile.

Walipofika kule ndani, walikuta ilikuwa ni sehemu ya wazi kabisa isiyokuwa na vitu vingi. Queen alikuwa amesimama hapo pia na mabaunsa wengine wawili, akimwangalia Dylan kwa hamu sana kadiri alivyozidi kusogea karibu. Palikuwa na giza pia ndani hapo lililopambanishwa na mwanga hafifu wa tochi walizoshika wanaume wale. Alipomkaribia Queen zaidi, Dylan akaushika mkono wa Grace ili wawe karibu hata zaidi. Queen akaachia tabasamu la mbali huku anamwangalia Grace.

"Who's your good looking friend? (rafiki yako huyu mzuri ni nani?)" Queen akauliza.

"Huyu ni Grace. Grace, huyu ni Queen," Dylan akasema.

"Sikujua ulikuwa unakuja na dada yako," Queen akasema.

"Mimi siyo dada kwake. Ni mpenzi wake," Grace akasema.

"Ooooh... kweli? Too bad. The boy was already turning me on (...basi hiyo mbaya. Huyu kijana alikuwa ameanza kunipagawisha sana)," Queen akasema kikejeli.

"Mimi na Grace letu ni moja. Tunamtaka huyo mpumbavu kwa hali na mali," Dylan akasema.

"I can see that... all the desperation. Amewafanya nini kwani?" Queen akauliza.

"Amefanya vitu vingi vibaya. Amewatesa wasichana wengi na kuwadhulumu watu haki zao. Na hata alijaribu kuniua mimi na Dylan," Grace akasema.

"Oh! Kumbe ndiyo hivyo? Alijaribu kukuua kwa sababu gani?"

"Hakuwa na sababu yoyote zaidi ya kuwa mwenye tamaa za kibinafsi," Grace akajibu.

"Mmmm... so all this is to exact revenge? You could have just told me to handle him for ya...(kwa hiyo hii yote ni kulipiza kisasi? si mngeniambia tu mapema ili nimshughulikie kwa ajili yenu...)" Queen akauliza.

Grace akamsogelea karibu zaidi.

"I want to make him feel all the pain he has caused many people. Killing him will not make him feel it. I'll deal with him in such a way that he'll wish it was better if he was dead! (ninataka kumfanya ahisi maumivu aliyowasababishia watu wengi. Kumuua haitamfanya ayahisi. Nitashughulika naye kwa njia ambayo itamfanya aone kifo kuwa bora!)" Grace akasema kwa mkazo.

"You talk big, girl. Ungekuwa na fire ya namna hiyo hiyo kwenye kumtafuta mbona ungekuwa umempata tayari? Ni kama ulikuwa ume-relax tu," Queen akamwambia Grace.

"Nilikuwa napanga mambo mengi carefully. Mpelelezi wangu alikuwa ameshampata wakati wewe ulipomteka," Grace akamwambia kwa uthabiti.

"Ahahahah... kwa hiyo nilipomchukua tu ndiyo huyo mpelelezi wako akampata? What a coincidence," Queen akasema.

"Unataka kusema nini?" Grace akauliza.

"You gotta be careful on whom you put your faith in sweetheart (kuwa mwangalifu kuhusu watu unaowaamini mpenzi)," Queen akamwambia.

Dylan alihangaishwa na jinsi wanawake hawa walivyopeana maneno kwa njia hiyo. Lakini alianza kuona ni kama Queen alikuwa sahihi. Jafari alikuwa akiwasaidia ndiyo, lakini ilipokuja kwenye suala la Mr. Bernard, ni kama alikuwa anajirudisha nyuma. Alifikiria wakati ambao Pius alikufa, yeye ndiye aliyempatia taarifa mapema, lakini bado kutokea wakati huo mpaka sasa eti hakuwa amempata Mr. Bernard. Kwa upande mwingine, haikuonekana kwamba ingewezekana kumfikiria Jafari kuwa mtu anayemlinda Mr. Bernard, kwa kuwa kama ingekuwa hivyo basi huenda Grace asingekuwa hai leo. Kwa hiyo Dylan akayaona maneno ya Queen kuwa kama ya tahadhari tu isiyokuwa na hatari kubwa.

"Unataka kusema nini? Kwamba mpelelezi wangu ananisaliti?" Grace akauliza.

"Wewe ndiyo umesema hivyo," Queen akamwambia.

Wanawake hawa walikuwa wanatazamana kwa hisia kali, ikionekana wazi kila mmoja alionyesha yuko makini sana. Dylan akasogea karibu yao ili kuvunja hali hiyo tata.

"Queen, yuko wapi huyo mpumbavu? Ninataka kumuuliza mambo mengi," Dylan akasema.

Queen, akiwa bado anamwangalia Grace machoni, akatoa ishara kwa kupiga vidole vyake viwili vilivyotoa sauti iliyosikika vyema, na hapo hapo taa zikawashwa kuelekea mwishoni mwa nyumba hii. Dylan na Grace waliweza kumwona Mr. Bernard akiwa kwa mbele kule, mikononi akifungwa kwa kamba nene zilizokazwa kwenye nguzo za ndani hapo; zilizoinyanyua mikono yake juu. Alikuwa amepiga magoti chini, huku kichwa chake akiwa amekiinamisha, na kifua chake chenye vinyweleo vingi kilikuwa wazi.

Queen akaanza kuwaongoza kumwelekea, na walipomkaribia, akawaangalia wawili hao huku anatabasamu.

"Here's your guy. Fucker was hiding in a truck self-contained room... what a bitch! (huyu hapa mtu wenu. alikuwa anajificha kwenye chumba cha kontena kubwa la gari..malaya kweli!)" Queen akasema.

Grace alikuwa akimwangalia kwa hasira sana.

"Amezimia?" Dylan akauliza.

"Amesinzia. He's all yours," Queen akamwambia.

Dylan akamsogelea Mr. Bernard karibu, kisha akamwasha kofi la nguvu usoni na kusababisha mzee huyo akurupuke kutoka usingizini. Akawa anawaangalia wote hapo kwa taharuki kubwa, lakini alipomwona tu Grace, akagandisha macho yake kwake kiudadisi. Alitambua kwamba mwanamke huyu alimjua, lakini hakuweza kukumbuka kikamili alikomjulia.

"Dylan... kijana wangu... naomba tuongee... usichukue hatua ambayo...."

"Shut up!" Dylan akamfokea.

Mr. Bernard akawa anaogopa sana huku akimwangalia tena Grace.

"Ninakuuliza swali moja. Ninataka jibu moja. Ni wewe ndiyo ulimuua Baraka?" Dylan akauliza.

Mr. Bernard akawa anapumua kwa presha kubwa tu. Hakujua aseme nini.

"Sidhani kama leo ndiyo siku yako ya kwanza kuwa na hizo lips nyeusi... ongea," akasema Queen.

"Siyo mimi!" Mr. Bernard akasema.

"Ni nani?" akauliza Dylan.

"Nitakwambia. Lakini kwanza, nifungue... halafu unilinde kwa kuwa..."

"Hivi we ni mshenzi eti? Mlijaribu kuniua mimi, mkamuua Pius na Baraka, halafu unajifanya unaweza ku-demand chochote kutoka kwangu? Niambie ni nani aliyekuwa akikusaidia... NOW!" Dylan akapaaza sauti kwa hasira.

Mr. Bernard akawa kimya tu, kama hataki kujibu.

"Okay this is getting old. You want me to make him talk? (hii inaboa. Nikusaidie kumfanya aongee?)" Queen akamwambia Dylan.

"Hapana. Ataongea tu," Dylan akasema.

Kisha akamshika na kumnyanyua ili asimame, na hapo hapo akaanza kumtandika ngumi nyingi sana hasa tumboni na usoni. Mr. Bernard alitoa kelele nyingi za maumivu, huku Dylan akiwa anamwambia aseme ni nani aliyekuwa akimsaidia. Mwishowe, alipoona hangeweza kuendelea kuficha tena kutokana na maumivu ambayo alipata, akamwomba Dylan aache kumpiga, naye angemwambia ni nani. Dylan akaacha, huku Mr. Bernard sasa akiwa amepiga magoti chini na damu zikimtoka mdomoni na puani mwake.

"Ongea..." Dylan akamwamuru.

Mr. Bernard akawa amelegea kwelikweli huku akiyasikilizia maumivu aliyohisi. Hapa hakuwa na ujanja tena kwa kuwa siku za wizi wake zilikuwa zimefikia arobaini.

"...ni... ni Beatrice... ni Beatrice ndiyo ana.... ndiyo amenisaidia... amemuua yule mwanaume..."

"Beatrice gani?" akauliza Dylan.

"Rafiki yake na mama yako..." akajibu Mr. Bernard.

Dylan akashindwa kuelewa.

"Beatrice?!" Grace akauliza.

"Kwa nini afanye hivyo?" Dylan akamuuliza Mr. Bernard.

Mzee akawa anapumua kivivu tu. Dylan akamshika kichwa na kumtazama usoni kwa ukaribu.

"Sitaki unifanye mimi fala mwenzio. Niambie ukweli," Dylan akamwamuru.

"Ni kweli... ni yeye. Mimi sijaua mtu... sijafanya chochote kibaya Dylan niamini..."

Dylan akakisukumiza kichwa chake kwa kukerwa.

"Nipe sababu moja kuu ya kuamini maneno yako," Dylan akamwambia.

"....yule mwanamke anataka... anamtaka baba yako. Anataka... anataka kuivuruga familia yenu... Anaweza kuwafanya chochote anachojisikia... ni mkatili sana ndiyo maana me nikaogopa hata... nikafanya mabaya yake lakini..."

"Acha kujifaraghua, fala wewe. Umekuwa mtoto upelekeshwe kwani? Tunajua nature yako Mr. Bernard wala usijilambe-lambe. Huyo Beatrice ndiyo wa kuua mtu kisa tu anamtaka baba yangu? Bado hujani-convince," Dylan akasema.

"Hapana sikudanganyi. Ni yeye...aah ssss...alinitafuta nika... alinipanga ili tuwaangushe Gilbert na Jaquelin kwa pamoja. Mpango ulikuwa kuichukua kampuni... mimi sikutaka kuhusika kwenye mauaji ila yeye ndiye aliyesema ufe kwa kuwa aliogopa ungemletea matatizo. Yule ndiyo mbaya wenu... siyo mimi. I'm a victim here too..."

Grace akasonya kwa kukerwa sana na mwanaume huyo. Dylan akamwangalia Grace akiwa anayatafakari maneno ya Mr. Bernard kuhusu Beatrice. Hili kwa kweli lilikuwa ni jambo lisilowazika kabisa.

"Msinifanyie kitu kibaya tafadhali nawaombeni. Yule mwanamke ni sumu, niko tayari kufichua mabaya yake ili...."

"Huyo Beatrice... mpaka sasa... oh God! Nahitaji kuwaonya wazazi wangu," Dylan akamwambia Grace.

"Kikulacho hah..." Queen akasema.

"Ndiyo. Ni jambo la muhimu sana kuwaambia haraka. Halafu inabidi tuhakikishe anakamatwa bila yeye kutarajia," Grace akasema.

Dylan akatoa simu yake ili ampigie Gilbert.

"Vipi kuhusu huyu? Nitafurahi mkiniambia nimkatekate ili nimtengenezee mbwa wangu supu," Queen akawaambia.

"No please... tafadhali nina..." Mr. Bernard akawa anaomba asidhurike.

Dylan alimpigia baba yake simu, lakini hakupokea. Hivyo akaona ampigie mama yake badala. Ila kabla hajafanikiwa, simu yake ikaanza kuita, na mpigaji alikuwa ni Harleen. Dylan alikumbuka vizuri kuwa huyu alikuwa ni binti wa Beatrice, ambaye sasa alikuwa amepata kujua kuwa ndiye adui yake mkubwa. Akapokea akiwa makini sana.

"Hello... Dylan?" sauti ya Harleen ikasikika.

"Naam..." Dylan akaitikia.

"Dylan... kuna jambo muhimu nataka tuzungumze. Naomba tukutane."

"Jambo gani?"

"Tafadhali Dylan, naomba tukutane. Ni muhimu mno kwa kuwa... inahusiana na mtu anayejaribu kukuua. Nimemjua... nataka nikwambie ni nani, na nina ushahidi wa kukusaidia ili akamatwe. Please kutana na mimi," Harleen akaomba.

Dylan akamwangalia Grace, ambaye alikuwa anamtazama asijue mwanaume anaongea na nani, kisha Dylan akakubali na kumwambia Harleen wakutane. Kwa kuwa alikuwa jijini kwao, Harleen alimwelekeza sehemu ya kukutana ambayo haikuwa na watu ili aweze kumpa kile alichomwambia. Baada ya hapo, Dylan akakata simu na kumsogelea Grace.

"Grace, huyo alikuwa ni Harleen. Anasema ana ushahidi wa kunipa kuhusu mtu anayetaka kuniua," akamwambia.

"Nini?" Grace akauliza akiwa hajaelewa.

"Mtoto wa Beatrice yule wa kike, Harleen, anataka kunipatia ushahidi wa mtu aliyekuwa...."

"Una uhakika hiyo ni genuine? Je kama yeye na mama yake wanakuzunguka?" Grace akauliza.

"I'm not sure, sijui lakini... kuna chance kwamba anachosema ni ukweli. Nahitaji kujionea," Dylan akasema.

"Okay. Twende wote. Ikiwa kweli..."

"No Grace. Hatutaenda pamoja," Dylan akamkatisha.

"What?"

"Nahitaji kuwa mwangalifu. Kama ulivyosema, ikiwa ni mchezo nafanyiwa basi nahitaji kuwa makini. Lakini... wewe na hali yako, haitakuwa salama..."

"But Dylan..."

"Usijali Grace, mimi nitakuwa sawa. Nachohitaji zaidi wakati huu ni wewe kuwa salama, tafadhali."

Grace akashusha pumzi.

"Kwa hiyo unaenda mwenyewe?" Queen akamuuliza.

"Hapana. Nipe wanaume wako niende nao, just in case," Dylan akasema.

"Ahahahah... unavyoongea utafikiri umewaajiri. Wakifa huko?"

"Hawawezi, nawajua wako vizuri sana. Nisaidie Queen tafadhali, ninataka kuikomesha hii hali yote milele, please..."

"Okay fine. Jacob na Hussein, nendeni na Killmonger. Mpeni protection endapo kutatokea shida," Queen akawaambia walinzi wake, nao wakakubali.

"Killmonger?" Grace akauliza.

"Aam... hiyo ni nickname yangu... nilikuwa natumia zamani. Queen, thanks, I really owe you a lot," Dylan akasema na kumshukuru Queen.

"Yeah you do. Nenda kashughulike na huyo mwingine, na sisi tutashughulika na huyu, au siyo... Grace?" Queen akasema.

Grace akatikisa kichwa kukubali, kisha akamgeukia Dylan na kumpiga busu ya kumuaga, na hapo hapo Dylan akatoka akiwa na wale wanaume kwenda mpaka kwenye gari ili waelekee kule walikokubaliana kukutana na Harleen.


★★★


Harleen alikuwa akisubiri ujio wa Dylan usiku huo peke yake. Sehemu hii ilikuwa ni ya jengo la ofisi lililoachwa na kutotumiwa kwa muda mrefu. Alikuwa peke yake nje hapo, akimsubiria Dylan ili aweze kumwambia ukweli wote, haidhuru ikiwa mama yake angechukuliwa hatua ya kisheria, kwa kuwa aliyoyafanya hayakuwa mazuri hata kidogo. Ilipita zaidi ya nusu saa tokea Harleen alipomwambia Dylan wakutane hapo, na sasa aliweza kusikia gari ikiwa inakuja upande huo alipokuwa. Likafika hatimaye na kuingia sehemu hiyo mpaka nyuma ya gari lake na kusimama hapo.

Lakini gari hili alilijua vizuri sana, na kwa haraka angeweza kusema halikuwa la Dylan hata kidogo. Lilikuwa gari la mama yake. Akaingiwa na hasira hata zaidi baada ya kumwona mama yake akishuka na kumfata, huku nyuma akisindikizwa na yule mlinzi wake gaidi. Alikuwa ametumia simu yake kumfatilia Harleen, na hivyo ndivyo alivyoweza kumpata huku. Mikononi mwake Harleen alikuwa ameshika kile kifaa cha kurekodia sauti alichotoka nacho nyumbani, naye akakirudisha nyuma ili kukificha.

Beatrice akamsogelea mpaka karibu akiwa na uso ulioonyesha mfadhaiko mkubwa sana.

"Harleen..."

"Unataka nini?"

"Harleen nisikilize. Mimi ni mama yako..."

"Kwa hiyo?"

"Nakupenda Harleen. Kila kitu nachofanya ni kwa ajili yako... na David..."

"Bullshit!"

"Harleen, tafuta kote utakapoenda lakini hautapata mama mwingine zaidi yangu. Mimi nimekuzaa, nimekulea, nimekutunza mpaka umekuwa hivi, huwezi kusema utanichukia kwa sababu... hhh... Look, hayo ni mambo yaliyopita binti yangu... eeh? Yasahau, mimi niko tayari..."

"Yaani yooote unayoyasema hayana faida yoyote kwangu mimi. Ongea chochote kile unachotaka, lakini kuanzia wakati huu sitaki tena kuwa na lolote la kufanya linalokuhusu. Hesabu hauna binti hapa, kwa sababu mimi siwezi kuwa na mama ambaye ni mfano wa Shetani!" Harleen akamwambia.

"Harleen usiongee hivyo. Kumbuka mambo yote ambayo..."

"Ninachokumbuka tu sasa hivi ni kile nilichokiona kwenye zile video. Ninachoona ni wewe ukimuua baba. Hakuna chochote kingine ninachoona zaidi ya ushetani wako mkubwa!" Harleen akaongea kwa hisia sana.

Beatrice akaanza kulia.

"Siwezi kukuachilia uendeleze mabaya haya. Nitayaweka wazi kwa wote uliowakosea..."

"Harleen..."

"....kama ndiyo itakuwa fundisho kwako ni bora uende jela kabisa ili ulipwe kwa mabaya yote uliyoyafanya. Unanifanya najihisi mchafu sana mama... how could you do this?" Harleen akawa anasema huku akilia.

"I'm sorry... I'm sorry...I'm...I'm...I'm sorry... Harleen please...."

"Mm-mm...usiniguse... don't touch me..."

"Harleen my baby... usimpe yeyote hiyo record... mimi ni mama yako... huna... tafadhali..."

"Niache. Ni lazima ufundishwe somo... siwezi kukubali umuumize Dylan hata siku moja..."

"Yaani... kwa ajili ya Dylan uko tayari kuni..."

"Ndiyo!"

"Harleen...."

Kulikuwa na hali nzito sana ya kihisia baina ya wawili hawa wakati huu. Beatrice akawa aking'ang'aniza kumkumbatia Harleen ambaye hakutaka hilo hata kidogo. Alimsukuma mara kadhaa ili kukataa kumbatio lake, lakini bado Beatrice akaendelea kulazimisha. Mwishowe, Harleen akatulia tu na kumwacha mama yake amkumbatie huku analia sana na kuomba amsamehe na asifichue mabaya yake.

"...please... baby I love you.... please usifanye hivi...."

"Its too late mommy. Siwezi kurudi nyuma tena..."

Beatrice akakaza macho yake kwa nguvu sana akihisi uchungu mwingi moyoni mwake.

"I'm sorry... nisamehe Harleen... nisamehe.... nakupenda my daughter... nakupenda sana...."

Mkono mmoja wa Beatrice ulirudi mpaka nyuma ya kiuno chake, naye akatoa bastola yake na kuipandisha taratibu mpaka usawa wa tumbo la binti yake. Harleen aliweza kuhisi kitu kigumu kikigusa tumbo lake, na ijapokuwa aliingiwa na hofu kubwa baada ya kutambua ilikuwa ni nini, akatulia tu hivyo hivyo na kufumba macho yake huku akitokwa na machozi. Beatrice alikuwa analia huku mkono wake mwingine ukizishika-shika nywele za kichwani za binti yake kwa wororo, kisha akavuta kidole chake kwenye kivutio cha bastola yake.

"Paahh!"



★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★

WhatsApp +255 787 604 893
 
Waoo what a step, a mom kills her own daughter to cover her wrongdoings up.!! Ngoma inakuwa nzito zaidi ingawa Bernard ameshabwabwaja kule.... Ngoja tuone yatakayojiri in next episode
 
DYLAN

Story by Elton Tonny

Familia, Kazi, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Unyanyasaji, Usaliti, Visasi, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa

(R-rated 18+)

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA AROBAINI

★★★★★★★★★★★★★


Harleen alianza kulegea baada ya kuhisi maumivu makali sana yaliyommaliza nguvu mwilini. Risasi iliyompiga ilitoboa tumbo lake mpaka kufikia mgongoni, hivyo damu nyingi zilivuja. Beatrice alikuwa bado amemkumbatia huku akilia sana, na taratibu wote wakaanza kushuka chini pamoja. Harleen alikuwa amelegea mno huku machozi yakimtoka, na ni giza fulani zito tu ndiyo lililokuwa likionekana mbele ya macho yake; kila akijaribu kufumbua macho ndivyo lingezidi kuyafunika.

"Boss, tuondoke. Mlio wa risasi ulikuwa mkubwa kuna watu wanaweza kuja hapa," akasema mlinzi wake Beatrice.

Lakini Beatrice alikuwa kama hamsikii kutokana na kuhisi uchungu mwingi wa kile alichokifanya. Akaendelea tu kumshikilia binti yake chini hapo huku akilia sana. Hivyo mlinzi wake akamfata na kumvuta ili waondoke haraka, huku mwanamke huyu akiweka mgomo wa kutotaka kumwacha binti yake. Lakini mlinzi wake akatumia nguvu zaidi na kumbeba mpaka kwenye gari, kisha akarudi kwa Harleen na kukichukua kifaa kile cha kurekodia sauti ambacho kilikuwa kimedondoka chini na kurudi kwenye gari tena, kwa sababu alijua ndiyo hicho ambacho Beatrice alikitaka. Akaliwasha na kuwaondoa wote hapo.

Harleen alibaki chini pale akiwa ametazama juu kilegevu, akihisi kani yote ya dunia inamvuta kutoka ndani yake.


★★★


DAKIKA 20 KABLA YA HARLEEN KUPIGWA RISASI

"Kwani leo kulikuwa na mechi?"

"Eeh! Kariakoo Derby! We vipi ina maana ulikuwa hujui?"

"Aah sijaamkia magazetini leo. Kwa hiyo wametoka ngapi?"

"Tatu bila. Morrisson anachelewaga sasa?"

"Pimbi tu yule na midevu yake. Unamshadadiaga kweli utafikiri yeye peke yake ndiyo club nzima ya msimbazi."

"Kwendraa huko! Tako lako linakuuma tu kwa kuwa timu yako hiyo ya vyura wamegalagazwa."

"Hauna lolote... we ndala tu."

"Fetty unashabikiaga ipi?"

"Mimi sifatilii mpira," akajibu Fetty.

"Ahahaaaa... hicho ni kilio tosha cha tatu bila!"

"Kweli bwana. Me mpira hapana. Jamani tufanye haraka, usiku huo. Harakisheni tuondoke," Fetty akasema.

"Halafu Tony amewahi kuondoka leo."

"Mechi hiyo. Anashabikiaga Yanga ndo' maana hajarudi."

Wote wakacheka.

Haya yalikuwa ni maongezi baina ya Fetty pamoja na waajiriwa wa mgahawa wa Dy-Foods. Zilikuwa ndiyo dakika za mwisho wakimalizia mambo hapo kama vile usafi na kupangilia vitu ili waweze kwenda nyumbani. Siku hii biashara ilikwenda vizuri kwa kuwa walipata wateja wengi mpaka inafika usiku, hivyo walikuwa wamechoka na wenye uhitaji mkubwa wa kupumzika. Fetty akiwa kama msimamizi msaidizi, alipendwa na waliofanya kazi hapo kwa kuwa aliwatendea kwa urafiki sana, na hata alisaidiana nao kazi kadha wa kadha.

Baada ya wote kuwa wamemaliza na kutoka nje, walipafunga na kuagana, kila mtu akielekea upande tofauti. Ni Fetty pekee ndiye aliyeondoka na rafiki yake, Patricia, ambaye alitaka kwenda naye kulala kwake. Wakapata bodaboda wawili nao wakaanza kuelekea upande ambao Fetty aliishi. Lakini wakiwa njiani, bodaboda aliyokuwa amepanda Fetty ikashindwa kusonga mbele kutokana na shida fulani, hivyo ikabidi ampe Patricia funguo ili atangulie. Ijapokuwa Patricia alishauri wapande ile ile aliyopanda yeye, Fetty alikataa na kusema hakutaka kubanana, hivyo angesubiri tu kwa kuwa boda alimhakikishia haingechukua muda mrefu kuitengeneza.

Wakati wakiwa hapo bado baada ya Patricia kuwa ametangulia, Fetty pamoja na bodaboda walisikia mlio wa risasi ukitokea upande wa jengo moja ambalo lilikuwa upande wa mbele kidogo. Kutokea upande huo hawakuona mtu yeyote, lakini mlio huo ulikuwa mkubwa kuwaambia kwamba kuna hatari fulani ilikuwa hapo.

Fetty alishtuka sana, na baada ya kuangalia pikipiki, akakuta mwanaume ambaye ndiyo alikuwa bodaboda akikimbia kuelekea upande walikotokea, bila shaka akikimbia hatari iliyokuwepo eneo hilo. Mwanadada hakujua la kufanya kwa kuwa alihitaji sana kurudi nyumbani, hivyo akaamua kujibanza sehemu ya pembeni ili kuficha uwepo wake na kusikilizia ni nini ambacho kingefuata.

Baada ya kama dakika mbili, akaona gari likitokea upande huo na kuanza kuja upande wake, nalo lilipokaribia usawa wake kwa macho ya haraka aliweza kumwona Beatrice akiwa siti ya mbele, akionekana kulia sana. Gari likapita na kuondoka. Fetty alibaki hapo akijiuliza mwanamke yule aliwahi kumwonea wapi, kwa sababu sura yake haikuwa ngeni sana ijapokuwa aliiona kwa ufupi mno wakati huu. Akaangalia upande ule ambao gari lile lilikuwa limetokea, na udadisi ukamfanya anyanyuke ili kwenda pale kuangalia ni nini kilikuwa kimetokea. Hakukuwa na mtu mwingine eneo la hapo, na ijapokuwa wasiwasi ulikuwepo moyoni, bado akajitia ujasiri ili kwenda kuona kama yeyote alikuwa ameumia.

Fetty alitembea kwa uangalifu mpaka kufika pale, na hapo akaweza kuona mtu akiwa amelala chini. Kwa haraka aliweza kutambua kwamba ilikuwa ni mwanamke, na woga mwingi ulimwingia baada ya kuona damu nyingi pale chini mwanamke huyu alipolala. Akatoa simu yake haraka na kupiga 112 ili kupata msaada wa polisi na ambulance. Akawaambia kilichotokea na maeneo aliyokuwepo, akiwasihi wawahi kwa sababu kuna mtu alikuwa amepigwa risasi. Wakamwambia wangefika upesi, naye akakata simu na kuendelea kuuangalia mwili ule pale chini.

Fikira ya kutaka kusogea karibu zaidi ilimwingia, kwa sababu alitaka kujua ni nani ambaye alikuwa amepigwa risasi pale chini, na kama ikiwa bado alikuwa hai basi ajaribu kutoa msaada wa mapema. Akasogea polepole na kuukaribia mwili huo, na mkono wake ukafumba mdomo kwa mshangao baada ya kutambua kwamba ilikuwa ni Harleen. Aliogopa sana. Akamfata haraka na kuanza kumwamsha, akimwita kwa sauti ili aamke. Harleen alikuwa ametokwa na damu nyingi sana. Fetty akajaribu kumgeuza ili alaze kichwa chake kwenye mapaja yake, huku akijaribu kuzuia damu tumboni mwake zisitoke kwa kukandamiza na kitambaa chake.

"Harleen... Harleen.... Harleen...."

Akaendelea kumwita tu huku akimwonea huruma sana. Lakini wakati akiendelea kufanya hivi, akatambua kwamba macho ya Harleen yalikuwa yanatikisika kwa mbali, kama vile anataka kuyafumbua. Hii ikamfanya Fetty atambue kuwa binti bado alikuwa hai, hivyo akaendelea kujitahidi kumwamsha. Alimwita na kumwita mpaka Harleen akaweza kufumbua macho yake kwa mbali sana.

"Harleen.... Harleen.... nini kime.... nani amekufanya hivi? Mm? Harleen? Harleen?"

Harleen akaendelea tu kuonyesha jinsi alivyokuwa ameishiwa nguvu.

"Usijali.... mapolisi wanakuja. Nimewaambia waje na ambulance... jikaze dada'angu... tunakupeleka hospitali sawa?" Fetty akasema kwa hisia.

"Mm... ma.... mm... mau..."

Harleen akawa anajaribu kusema jambo fulani, lakini Fetty akawa anashindwa kuelewa kwa sababu sauti yake ilikuwa ya mbali iliyoonyesha maumivu makali.

"Nini? Nini unataka kuniambia Harleen? Nani amekufanya hivi?" Fetty akauliza.

Kifua cha Harleen kilikuwa kinashtua kila alipojaribu kusema kitu hicho kwa shida sana. Hivyo, Fetty akasogeza sikio lake karibu na mdomo wa Harleen, na hapo Harleen akamtamkia maneno hayo ambayo Fetty hakuelewa yalimaanisha nini.

"Unamaanisha nini? Harleen... unamaanisha nini? Eeh? Nani amekufanya hivi?" Fetty akauliza huku machozi yakimtoka.

"Ina... uma..." Harleen akasema kwa maumivu makali sana.

Fetty alihisi simanzi nzito sana moyoni. Alijua kwa jinsi mapolisi wanavyojivuta hawangefika hapo kwa muda mwafaka. Alimwonea huruma sana Harleen. Hakujua afanye nini usiku huo maana haingekuwa rahisi kumpatia msaada wa haraka, na hali yake ilikuwa mbaya sana. Hivyo, akafanya kama kumkumbatia, akiweka kichwa kwa kichwa huku anambembeleza taratibu. Akamwambia kila kitu kitakuwa sawa, na ajitahidi kuyaachia maumivu yote aliyohisi badala ya kuyasikilizia sana. Hata akaanza kumwimbia kwa sauti ya chini huku analia kwa huzuni nyingi sana. Simu ya Fetty ilikuwa ikiita sana, na ilikuwa ni Patricia ndiye aliyekuwa anampigia kuuliza yuko wapi, lakini Fetty hakuweza hata kuichukua kuangalia mpigaji.

Kutoka kwenye usawa wa shavu lake aliweza kuhisi pua ya Harleen ikiwa imekata pumzi ndogo iliyokuwa ikitoa nje. Alilia sana Fetty. Ilikuwa ni kama alijuana na Harleen sana lakini hata hawakuwahi kukaa kupiga naye story yoyote ile; labda maongezi kidogo kipindi kile wako hospitalini kwa ajili ya Sophia wakati Harleen akiwa kama daktari pale. Ni simanzi kubwa iliyojaa moyoni mwake ndiyo iliyofanya alie mno, kwa sababu alihisi ni kama alishindwa kumsaidia dada wa watu kwa lolote lile wakati huu ambao alikuwa akiteseka mpaka kufa.

Kutokea nyuma yake aliweza kusikia sauti ya gari, naye akajua bila shaka mapolisi walikuwa ndiyo wamefika, lakini kwa kuchelewa mno. Ni baada ya kugeuka nyuma ndipo akatambua kwamba haikuwa gari la polisi, bali la mtu binafsi kabisa. Akaendelea kulitazama, na hapo akamwona Dylan akishuka pamoja na wanaume wengine wawili, nao wakaanza kumfata. Dylan alikuwa akishangaa sana baada ya kumwona Fetty hapo akiwa amemshika Harleen, aliyeonekana kutokwa na damu nyingi sana na kuwa mbali na uhai. Akasogea mpaka karibu akiwa anajiuliza maswali mengi, huku Fetty akiwa anamtazama kwa huzuni.

"Fetty.... what happened?" Dylan akauliza.

"Hata sijui Dylan. Nime... nimekuta tu amelala hapa.... nimesikia risasi.... Dylan nilikuwa nataka tumuwahishe hospitalini lakini mapolisi na ambulance zimechelewa.... mimi sielewi...."

"Fetty usijali... usijali..." Dylan akamtuliza.

Alipomwangalia Harleen, aliingiwa na simanzi kubwa sana. Akamshika Fetty na kumnyanyua ili asimame.

"Umeita mapolisi?" akamuuliza.

Fetty akatikisa kichwa kukubali.

"Okay. Twende," Dylan akasema.

"Lakini... vipi kuhusu Harleen.... tunamwacha tu ha...."

"Usijali Fetty. Twende. Now," Dylan akamkatisha ili wawahi.

Alijua mapolisi wangeanza kumpeleleza binti wa watu wakati ni wazi haikuwa yeye aliyehusika, hivyo akaanza kumwongoza kuelekea kwenye gari mpaka siti za nyuma na kuketi naye; wale wanaume wengine wakiingia mbele, nao wakaliondoa gari hapo haraka sana wakimwacha Harleen amelala pale nje; akiwa marehemu. Fetty alikuwa akilia kwa sauti ya chini huku mikono yake ikitetemeka sana, hivyo Dylan akamtuliza kwa kuishika na kumfuta machozi. Walienda mpaka sehemu fulani isiyokuwa na nyumba zozote wala watu na kuegesha gari huko, kisha Dylan akaanza kumuuliza Fetty ni nini hasa kilichokuwa kimetokea. Binti alimweleza ukweli wote, na akagusia pia kuhusu gari aliloona likiondoka pale ambalo lilikuwa na mwanamke aliyelia ndani yake.

"Ni mwanamke mtu mzima?" Dylan akauliza.

"Ndiyo. Alikuwepo hata siku ile kwenye party yako... nilimuona. Sijui kama ndiyo yeye aliyempiga risasi lakini," Fetty akamwambia.

"Kama ni yeye basi ni mtu mwenye roho ya kikatili sana," Dylan akasema.

"Kwa nini? Kwani Harleen alikuwa amemfanyaje?" Fetty akauliza.

"Sijui sana. Harleen amenipigia simu kuniita tukutane ili aniambie jambo muhimu sana. Ni muda mfupi tu nimetoka kujua kwamba mama yake ndiyo amekuwa akifanya yale yote mabaya yaliyonipata..."

"Kweli?"

"Ndiyo. Sasa kama mwanamke huyo uliyemwona ni yeye inamaanisha amemuua mtoto wake..."

Fetty akashangaa.

"Nilikuwa sijui kama huyo mmama ndiyo mama yake Harleen," akasema Fetty.

"Sijui alikuwa anataka kuniambia nini Mungu wangu! Najilaumu kutoweza kufika kwa wakati. Ikiwa ni kwa sababu yangu ndiyo amepatwa na haya... yaani... aah..." Dylan akawa anasikitika.

"Siyo makosa yako Dylan... usijilaumu. Harleen... hajastahili kufa namna ile... ila kuna kitu alikuwa anataka kuniambia lakini sikumwelewa," Fetty akasema.

"Alikusemesha?"

"Ndiyo... kwa pumzi yake ya mwisho."

"Alisema nini?"

"Alikuwa anasema... maua... sielewi alichokuwa anataka ku... yaani inaonekana kilikuwa muhimu lakini," Fetty akamwambia.

"Maua?" Dylan akauliza.

Fetty akatikisa kichwa kukubali.

"Sasa tutafanya nini Dylan?" Fetty akauliza.

Dylan akawa anatafakari ujumbe wa Harleen kwa Fetty. Alijua bila shaka Harleen alikuwa anataka kufikisha jambo muhimu kwa binti labda ili amfikishie yeye pia. Lakini wakati huu, jambo la muhimu lilikuwa kumnasa Beatrice, hivyo akatoa simu yake na kupiga kwa mtu muhimu.

"Halloo... Dylan mwanangu, vipi?" akasema Jaquelin baada ya kupokea.

"Mama... naomba unisikilize kwa makini...."


★★★


Upande wa Beatrice. Alipelekwa na mlinzi wake sehemu kama msitu ili aweze kuwa mwenyewe kuutoa uchungu wa kumpoteza binti yake. Beatrice alilia sana akikumbuka kitendo alichofanya muda mfupi uliopita. Alihisi majuto kiasi kwamba akaichukua bastola yake na kujiwekea kichwani, akitaka kujipasua kichwa kwa kuwa hisia za hatia zilimlemea mno. Lakini mlinzi wake akamshawishi kuwa asifanye hivyo kwa sababu bado David alimhitaji na hakuna yeyote ambaye alijua kuhusu kitendo kile, hivyo azitulize hisia zake nao waendelee na mambo mengine.

Beatrice akaanza kuielekeza hasira yake kwa Dylan hata zaidi, akilaumu kwamba kama isingekuwa ya kijana huyo, basi hangehitaji kumuua binti yake mpendwa, hivyo akaapa kuwa ni lazima angemfata Dylan huko huko aliko na kumsambaratisha haraka iwezekanavyo. Lakini wakati akiwa anajiandaa kuingia kwenye gari, simu yake ikaita, na mpigaji alikuwa ni Gilbert. Akashangaa kiasi, lakini akapokea na kuiweka simu yake sikioni taratibu.

"Beatrice...."

"Bee..."

"Beatrice... kuna jambo limetokea huku... uko wapi?" Gilbert akauliza.

"Niko... niko ofisini... kuna mambo mengine mengi.... nilikuwa namalizia. Jambo gani... limetokea?" Beatrice akaongea kwa kujikaza.

"Ooh... Beatrice... Harleen... Harleen amepigwa risasi!" Gilbert akamtaarifu.

Beatrice akafumba macho yake kwa kuhisi uchungu. Lakini alijua angepaswa kuigiza kwamba hajui hilo, hivyo akajikaza.

"Nini! Harleen amepigwa risasi?" akauliza kimshangao wa kinafiki.

"Ndiyo Beatrice. Wamempeleka mochwari. Tunaenda huko. Pole sana Beatrice," Gilbert akasema kwa hisia.

Beatrice akaanza kulia kwa sauti sana.

"Beatrice... tafadhali njoo. Njoo kwa binti yako... Niko pamoja nawe dear," Gilbert akamwambia.

Beatrice akaishusha simu kutoka sikioni na kuendelea kulia sana. Akakaa na chini kabisa akijiona kama Shetani kwa mambo yote aliyoyafanya. Lakini baada ya dakika chache, akaanza kujifuta machozi na kujikaza, kisha akanyanyuka akiweka uso ulio serious, naye akamwambia mlinzi wake ampeleke hospitali kule ili akaigize vizuri kwamba anaumizwa na kilichompata binti yake. Mpango ukawa kwamba akishamaliza kuonyesha maombolezo kwa ajili ya msiba uliompata Harleen, basi angeanza kushughulika na wote aliowaona kuwa ndiyo chanzo cha kumsababishia amuue binti yake; hasa Dylan.

Lakini kabla hajaingia kwenye gari, mlinzi wake, ambaye aliitwa Seba, akamwambia kwamba kwenye kifaa kile cha sauti alichokichukua kutoka kwa Harleen, hakukuwa na kitu chochote kilichoweza kusikika. Beatrice akashangaa na kukikwapua haraka, kisha akakifungua na kukuta betri liko vizuri tu. Akalitoa kuangalia sehemu ya kupachikia memory, na hapo akakosa kuiona. Akapiga kelele kwa hasira sana baada ya kutambua kuwa Harleen alikuwa ameitoa memory hiyo, na bila shaka kuna sehemu alikuwa ameiweka. Lakini haingewezekana kujua ilikuwa wapi tena maana tayari binti yake hakuwa na uhai. Akakitupa chini kwa nguvu kisha akaingia ndani ya gari kwa hasira. Sasa akaona kumuua binti yake ilikuwa kazi bure kwa kuwa hakupata kile ambacho kingeweza kutumiwa kama ushahidi dhidi yake, na endapo kama kuna mtu angeipata basi isingekuwa jambo zuri kwake.

Wakaondoka hapo na kuelekea hospitali baada ya Beatrice kumpa Seba maagizo kuifukia bastola yake udongoni, chini sana, ili isije kutokea akakamatwa nayo.

Ikawachukua kama nusu saa kuweza kufika hospitalini kule. Beatrice akashuka na kumwambia Seba amsubirie hapo nje ili yeye aende kutengeneza show nzuri kule ndani. Alikwenda kwa njia ya kinyonge sana, na ijapokuwa alikuwa na maumivu moyoni, bado alifanya mambo kwa kuigiza sana. Beatrice alikuwa ni nyoka! Akafika kwa wauguzi wa hapo na kuulizia kuhusu mwili wa binti yake, nao wakamwelekeza kwenye chumba ulipolazwa. Akaanza kwenda, huku akilini mwake picha za jinsi alivyompiga risasi Harleen zikiendelea kuonekana na kumtia uchungu maradufu.

Baada ya kufika usawa wa korido lililoelekea kwenye vyumba vile, aliweza kuwaona Gilbert pamoja na Jaquelin wakiwa wamesimama usawa huo pia. Jaquelin alikuwa wa kwanza kumwona Beatrice, naye akamwambia Gilbert kuwa mama ya binti marehemu alikuwa amefika. Wote wakawa wanamwangalia kwa umakini sana, naye Beatrice akaanza kuwafata upesi huku akilia. Lakini hakumfata "shosti" yake, akaenda moja kwa moja mpaka kwa Gilbert na kumkumbatia huku analia.

Gilbert akamtazama Jaquelin, naye Jaquelin akamtazama Gilbert. Utizami wao uliongea mengi sana ambayo haingekuwa rahisi kwa yeyote kuelewa walichoambiana. Beatrice akajitoa kwa Gilbert na kuanza kuwaangalia wawili hao kwa huzuni huku akilia kwa kwikwi.

"Mwanangu... mwanangu wamemfanyaje? Harleen wangu jamani..." Beatrice akawa anasema kwa huzuni.

Gilbert na Jaquelin wakawa wanamtazama tu kwa makini.

"Yuko humo? Nataka nimwone binti yangu... wamemuua amewakosea nini jamani? Aaah.... Harleen... nataka..."

Akiwa bado anajifaraghua hivyo, akatambua kwamba Gilbert na Jaquelin wote walikuwa wanaangalia nyuma yake. Akashindwa kuelewa ni kwa nini, na ile anageuka, akashtuka sana baada ya kukuta Dylan akiwa amesimama hapo, pembeni yake kukiwa na mwanamke (Fetty), na nyuma yake wakiwepo mapolisi watatu wenye silaha. Mapigo ya moyo yalikuwa yanakimbia kwa kasi sana kifuani kwa Beatrice, na moja kwa moja akawa ameelewa hii ilikuwa ni mtego kwake. Askari wale wakaanza kumfata mpaka karibu kabisa, na mmoja akamshika kwa nguvu mikononi.

"We vipi? Mbona siwaelewi? Gil, nini hiki... kwa nini mapolisi wanani..."

"Kaa kimya!" askari akamkatisha.

"Ndiyo yeye, siyo?" Dylan akamuuliza Fetty.

"Ndiyo," Fetty akajibu.

Askari yule akatoa pingu na kumfunga Beatrice mikono kwa kuizungushia nyuma ya kiuno chake.

"Nini kinaendelea? Mtoto wangu ameuawa nyie... em' niachie nitawafunga wote! Jaquelin... what's this supposed to mean... Gilbert?"

Beatrice akaendelea kulalamika sana. Jaquelin na Gilbert walikuwa wanamtazama kwa hasira nyingi, naye Dylan akamsogelea karibu zaidi. Beatrice akatulia.

"Ningekuwa na roho kama yako ningekuua kwa kila kitu ulichofanya. Haustahili kuwa mwanadamu kabisa. Nitahakikisha unalipia mambo yote uliyofanya kwa kuishi maisha yako yote yaliyobaki ndani ya cell," Dylan akasema.

Beatrice akawa anamtazama huku anapumua kwa hasira kali.

Maaskari wakaanza kuondoka na Beatrice huku akigoma na kusema anataka kumwona binti yake kwanza. Hatimaye, Beatrice akawa ametiwa mikononi mwa sheria. Gilbert na Jaquelin walimkumbatia mwana wao kwa faraja. Matatizo yote ambayo yalikuwa yamewapata kwa sababu ya mwanamke huyo sasa yalionekana kufikia hatamu.

Muda mfupi baadae, Dylan alikutana tena na Grace, ambaye alikuwa pamoja na Queen kwenye hoteli yake (hoteli ya Queen). Alimsimulia kila jambo lililotokea, na wanawake hawa wakamjulisha kuwa Mr. Bernard alikuwa bado amefungiwa ndani ya jengo lile, hivyo wangeweza kumtumia kwa ajili ya kutoa ushahidi dhidi ya Beatrice. Queen alishauri tu kuwaua kwa kuwa hakuona sababu ya kusumbuka sana kuanza kuwapeleka mara mahakamani au jela, lakini Dylan akasisitiza kwamba njia hii ndiyo iliyokuwa sahihi ili wabaya wao hao waishi maisha yao sehemu ambazo zingewafanya wajute kwa yale yote waliyofanya.


★★★


Mambo yalikwenda kwa uharaka sana baada ya Beatrice kuwa amefungwa kwa mashtaka ya uuaji na mambo mengine haramu. Msiba wa Harleen ulipofanyika, aliruhusiwa kwenda kuhudhuria pia huku akiwa na pingu mikononi akisubiri kesi zake kusikilizwa. Kwa kuwa sasa yeye alikuwa ameshikiliwa na polisi na binti yake hakuwa hai, lilizuka suala la ni nani ambaye angemtunza mwana wake, David, endapo angeishia jela. Uamuzi wa haraka ungekuwa ni kumwekea waangalizi anaowaamini, labda ndugu wa kiukoo, kwa kuwa bado Beatrice pesa nyingi alikuwa nazo.

Katika siku hizi chache ambazo walisubiri kesi ya Beatrice kuendeshwa, kuna jambo ambalo bado lilikuwa linaisumbua akili ya Dylan, nalo lilikuwa ni Harleen. Aliendelea kujiuliza ni nini ambacho binti yule alitaka kumwambia kilichokuwa na umuhimu sana mpaka kusababisha mama yake mzazi amuue kikatili vile. Alielewa kuwa huenda ilihusiana na mambo yote aliyojua Beatrice amefanya, lakini bado akawa anataka majibu zaidi kwa kuwa kifo cha Harleen kilimvunja sana moyo. Grace alikuwa amemshauri aache kuwaza sana kwa sababu tayari binti alikuwa amepoteza maisha, na hivyo asingeweza kujua mambo hayo, lakini Dylan akaazimia kuendelea kufanya utafiti zaidi ili ajue ukweli.

Grace alikuwa na kawaida ya kwenda kule walikomweka Mr. Bernard. Yeye pamoja na Queen ni kama walikuwa mashosti sasa, kwa sababu mambo mengi aliyotaka Grace yafanywe kwa mwanaume huyo, Queen aliyafurahia na kuyatekeleza kwa ajili yake. Mr. Bernard alipewa adhabu nyingi haswa. Alipigwa mara kwa mara, alinyimwa chakula na kupewa kidogo mara moja moja sana, na mara nyingine Grace aliamuru aunguzwe kwa pasi mgongoni na atetemeshwe kwa shoti za umeme ili ayahisi maumivu ambayo alimfanya apitie kipindi kile anamtesa. Mr. Bernard alitamani hata kufa kabisa, lakini Grace alihakikisha hakioni kifo kabla ya kujua nini maana ya mateso.

Wakati huu, zikiwa zimebaki siku tatu kabla ya kesi ya Beatrice, Grace alimfata tena Mr. Bernard na kumwambia kwamba angeacha kumtendea vibaya ikiwa angefanya kama anavyotaka. Mwanaume huyo, akiwa amechoka haswa, alimwambia angefanya lolote ili tu aache kuteseka namna hiyo. Grace akamwambia angeanza kumtendea vizuri na kumpa chakula kizuri ikiwa angekuwa tayari kusimama mahakamani na kutoa ushahidi dhidi ya Beatrice.

Mr. Bernard akakubaliana na Grace haraka sana na kusema angekuwa tayari kufanya hivyo kwa kuwa hata yeye hakumpenda sana Beatrice bali alifanya tu mambo mabaya kwa kushurutishwa naye. Grace aliona hiyo kama njia ya kujikosha tu kutoka kwa mwanaume huyo mnafiki, hivyo akampuuzia na kuwaambia waliomchunga waanze kumpa mahitaji kwa njia nzuri, lakini wahakikishe kwamba haondoki kutoka kwenye nyumba hiyo aliyofungiwa.

Siku hiyo Dylan aliamua kwenda pande za nyumbani kwao kuwatembelea wazazi wake. Kwa sababu hakuwa amewaambia kama angewatembelea, alikwenda moja kwa moja kwenye kampuni ya baba yake na kuwakuta huko wakiendesha masuala ya kikazi. Kufikia sasa, Gilbert na Jaquelin walikuwa wamerudisha ukaribu kimahusiano baada ya kutambua mwiba uliokuwa ukiwasumbua kwa muda mrefu na kuweza kuudhibiti hatimaye; yaani Beatrice. Dylan alikuwa amewaambia kuhusu kile Mr. Bernard alichosema, kwamba Beatrice alikuwa tu anamtaka Gilbert ndiyo maana akafanya yote yale, lakini ukweli mzima hakuujua.

Wazazi wake walifurahi sana baada ya Dylan kufika pale, nao wakakaa pamoja naye kuzungumzia maisha yao sasa na kesi itakayosikilizwa kesho kutwa. Wote walikuwa na uhakika kwamba Beatrice angepatwa akiwa na hatia tu, lakini bado Dylan alitaka sana kujua ni nini hasa kisa kilichofanya mpaka mtu ambaye alikuwa ni rafiki yao atake kumuua yeye. Jaquelin alimweleza kwamba hata yeye alitaka sana kujua ni nini iliyokuwa sababu, na kwamba alijaribu kumfata Beatrice kule alikofungiwa ili aongee naye, lakini mwanamke huyo aligoma kuonana naye. Hivyo haingekuwa rahisi kujua kisa kilichofanya mpaka akawatendea kwa unafiki mwingi vile maana kusema tu sababu ilikuwa anamtaka mume wake haikutosha.

Gilbert alijua ukweli moyoni mwake, lakini hakutaka kuwaambia kwa sababu alihofia huenda mambo yangeharibika tena ikiwa angesema vitu alivyofanya pamoja na Beatrice wakati ule ndoa yake iko matatizoni. Aliona kukaa tu kimya kuhusiana na mambo yaliyopita kulikuwa jambo bora zaidi ili waendelee tu kusonga mbele vizuri kimahusiano yeye pamoja na familia yake. Alijua pia huenda kwenye kesi mambo hayo yangehitajika kufunuliwa, hivyo akajiweka tu tayari kwa lolote; yaani ikiwa angehitaji kusema ukweli, basi angesema. Lakini kwa wakati huu hakutaka kuvuruga mambo kwanza, hivyo akaamua kuwa tu mkimya.

Basi, baada ya kama masaa mawili ya kuwa hapo kwenye kampuni, Dylan akawaaga na kusema angekwenda Dy-Foods ili kupata mlo pale. Wazazi wake wakamwambia nao wangekwenda baadae pia, hivyo mwana akatangulia. Alifika kwenye mgahawa wake na kuingia hapo, na wote waliofanya kazi hapo wakamfata ili kumsalimu. Walimpenda sana, na hata wateja wangeweza kukisia kwamba huyu alikuwa mtu muhimu mpaka wote waliofanyia kazi pale wamfuate kwa shauku ili kumsalimu. Patricia aliamua kumfata Fetty, ambaye alikuwa kwenye kiofisi chake kidogo hapo alichotumia na Tony, yule msimamizi mkuu. Wakati huu Tony hakuwepo, hivyo ni kama Fetty aliachiwa ausimamie mgahawa huu sasa.

Baada ya mwanadada kuambiwa kwamba Dylan alikuwa amefika hapo, akafurahi sana na kuamua kumfata pia. Alimkuta ameketi kwenye meza ya chakula, akisubiria huduma aliyoagiza. Fetty akamfikia karibu akiwa anatabasamu, naye Dylan akamkaribisha aketi ili ale pamoja naye. Ijapokuwa mwanzoni Fetty alisema hangeweza, Dylan alimsihi sana, hivyo binti akalegeza na kuamua kukaa pamoja naye. Walikuwa wakitazamana kwa njia nzuri sana, na kwenye akili zao wote walikuwa wakifikiria kuhusu usiku ule walioshiriki penzi kwa mara ya kwanza; penzi la marufuku.

Baada ya vyakula kuletwa, wakaanza kula pamoja huku wakiongelea mambo kadha wa kadha, hasa kuhusiana na familia ya Fetty.

"Okay... kwa hiyo hivi sasa anaweza kutembea bila egamio?" Dylan akauliza, akimaanishia mdogo wake Fetty aliyemsaidia kipindi kile alipopata ajali, yaani Sophia.

"Hapana, bado anatumia gongo mguu wake wa kulia. Mguu haujakaa sawa kivile," Fetty akajibu.

"Lakini ana-heal haraka! Wengine huwachukua muda mrefu sana kuweza tu hata kusimama hivyo, lakini yeye miezi michache tu," Dylan akasema.

"Ndiyo, anajitahidi mazoezi. Na pia... huduma zote ulizomlipiaga kipindi kile zilisaidia sana ndiyo maana."

"Nataka uje unipeleke kwenu ili niwasalimu. Ijapokuwa sitawakumbuka vizuri lakini, nitafurahi kuwa pamoja nao tena."

"Ndiyo mimi pia nitafurahi. Tutapanga twende... kama ukiwa huna mambo mengi."

"Well... mambo mengi bado nayapanga. Kampuni, kesi kesho kutwa, familia ya Baraka, mama na baba... ninataka kuhakikisha kila jambo linakuwa vizuri... ili tusije kupitia tuliyopitia hizo siku za nyuma."

"Kila kitu kitakuwa sawa. Usijali sana... me naona kama mambo yameshaanza kwenda vizuri mno. Huyo mwanamke atafungwa tu," Fetty akamhakikishia.

"Yeah..." Dylan akasema na kunywa juice kidogo.

"Grace anaendeleaje?" Fetty akauliza.

"Yuko poa. Ana mizunguko siku hizi kwa hiyo mara nyingi ananiachia niangalie kampuni yote."

"Wacha! Ninadhani itakuwa yako pia muda ukitimia."

"Ahahahah... anapenda kazi huyo! Sema siku hizi anapenda kwenda kutembelea sehemu fulani sana kwa hiyo ananiachia majukumu... majukumu majukumu," Dylan akasema huku akitabasamu.

"Nafurahi kujua una...furahia maisha yako... ukiwa pamoja naye," Fetty akamwambia kwa sauti ya chini.

Dylan aliweza kutambua kuwa maneno hayo yalikuwa yamebeba aina fulani ya hisia za kuvunjika moyo, ijapokuwa Fetty hakuwa mtu mnafiki. Akatabasamu tu, kisha akaona abadili mada na kuanzisha mazungumzo ya kile ambacho hasa ndiyo kilikuwa kimefanya afike hapo mgahawani.

"Aam... Fetty... naomba nikuulize kitu," akamwambia.

"Ndiyo... uliza tu."

"Nahitaji unielezee tena ni nini ambacho kilitokea usiku ule ambao Harleen alipigwa risasi na mama yake."

"Kwa nini?"

"Kuna... kuna jambo ambalo natafuta. Na ninahitaji kujua tu hasa mambo yalikwendaje maana nahisi ndiyo hapo napoweza kuupata ukweli zaidi... if you don't mind," Dylan akasema.

Fetty akaangalia chini, kisha akashusha pumzi ndefu na kuanza kukumbukia yaliyotokea usiku ule.

"Kiukweli... sikuona mambo mengi pale. Yaani nilikuwa ndiyo nimetoka hapa, mimi na Patricia... tukiwa tunaenda nyumbani pikipiki niliyopanda ikapatwa na shida. Nikashuka... wakati anaiangalia huyo bodaboda ndiyo tukasikia sauti kubwa ya risasi. Ye alikimbia, ila mimi kwa sababu nilishindwa kujua la kufanya pia nikajificha pembeni chini ya kibanda kidogo... Baada ya hapo ndiyo nikaliona gari la mama yake...na mama yake akiwa humo... sijui tu hata niliingiwa na nini yaani... nikaenda tu pale kuangalia ni nini kilikuwa kimetokea kwa sababu hakukuwa na watu hiyo sehemu... palikuwa kimya sana. Ndiyo nikamkuta sasa amelala pale chini... damu nyingi... nikamfata na kuwapigia simu polisi. Lakini kwa sababu walichelewa... sikujua la kufanya...."

Fetty akaishia hivyo na kubana midomo yake tu akijihisi vibaya kutokana na yote aliyoyaona siku ile.

"Its okay Fetty, haikuwa makosa yako. Kilichotokea kilitokea, na ilikuwa ni kwa sababu ya ubinafsi wa hali ya juu wa mama yake. Harleen alikuwa amenipigia simu usiku huo huo kuniambia tukutane pale kwa sababu alitaka kuniambia jambo la muhimu. Nadhani mama yake hakutaka nijue hicho kitu ndiyo maana akamuua," Dylan akasema.

"Inawezekana ni kuhusiana na mambo yote Beatrice aliyokufanyia..."

"Ndiyo, inaonekana. Lakini nahisi ni kama vile kuna kitu kingine... sielewi tu ni kwa nini..."

"Hata me nilipomshika... ni kama alikuwa anataka kuniambia kitu... ila akashindwa kwa sababu alikuwa ameishiwa nguvu..."

"Subiri... uliniambia siku ile alikwambia nini wakati umemshika?"

"Alisema... maua..."

"Eee ndiyo... maua."

"Yeah... sijui labda tu fahamu zake zilikuwa zimeshapotea ndiyo maana akawa anatoa labda... maneno yasiyoeleweka."

Dylan akaonekana kutafakari jambo fulani.

"Dylan..."

"Naam..."

"Unawaza nini?"

"Oh... yaani... namwaza sana Harleen. Najilaumu kwa nini sikuwahi kumfikia mapema siku hiyo."

Fetty akamshika kiganja.

"Hayakuwa makosa yako, kama tu ulivyoniambia mimi. Usiwaze sana kwa sababu hatuwezi kurudisha tena wakati huo nyuma," akamwambia kwa hisia.

Maneno ya Fetty yakaiingizia akili ya Dylan kitu fulani upesi. Hakuwa amefikiria jambo hili; kurudi nyuma, kuangalia vizuri mambo ambayo Harleen aliyaacha kama viashiria kwa ajili ya kile alichotaka kumwambia. Aliwaza kuwa maneno hayo, "maua," yalimaanisha jambo fulani, na kwa haraka akasimama akiwa anaonyesha nia ya kutaka kuondoka baada ya wazo moja kumwingia akilini. Fetty naye akasimama akiwa hajatarajia jambo hilo, naye Dylan akaweka pesa mezani ya chakula.

"Dylan... vipi?" Fetty akamuuliza.

"Nahitaji kwenda... kuna kitu nimefikiria nahitaji kuchunguza..."

"Kitu gani?"

"Ni...."

Kabla hajamwambia alichofikiria, akawaona wazazi wake wakiingia pale, naye akawapungia mkono wake huku akitabasamu. Fetty akawaona pia, naye akawapa tabasamu dogo huku wao wakija upande wao. Walipowafikia, Fetty akawasalimu, nao wakamwitikia vizuri.

"Afadhali tumekukuta... tukae wote... au umeshamaliza kula?" Jaquelin akamuuliza Dylan.

"Ndiyo... Samahani kuna sehemu nahitaji kwenda haraka... nyie kaeni m-enjoy msosi... nitapita GJD baadae kabla ya kurudi home..."

Dylan akasema na kuwapita wote upesi, akiharakisha sana na kuwaacha wanamwangalia tu kimshangao.

"Anaenda wapi? Mbona anakimbia?" Gilbert akamuuliza Fetty.

"Sijajua... tulikuwa tunaongea tu mara akanyanyuka..." Fetty akaishia hapo.

Wazazi wa Dylan wakaona wakae tu ili wapate mlo mzuri hapo kabla ya kurejea kazini. Wakafikiria kuwa huenda kijana wao alikuwa na mambo mengi tu, hivyo wakamwacha ayafuatilie.

Dylan aliendesha gari lake mpaka kwenye jengo lile ambalo ni usiku ule ambao Harleen alipigwa risasi ndipo alipokubaliana kukutana naye. Bado sehemu hiyo haikuwa ikitumiwa rasmi na watu, hivyo alikuta tu baadhi ya watu wakifanya mambo yao na wafanyabiashara upande wa barabara walioendelea na pilikapilika zao. Akaegesha gari hapo na kushuka, kisha akaelekea mpaka sehemu ile aliyoikumbukia kuwa ndiyo alimkuta Harleen akiwa amepotezea uhai. Wakati huu alama za damu zilibaki kuonekana kwa mbali chini hapo.

Akatulia kidogo akijaribu kutathmini mambo kwa kina, kisha akaanza kuzungusha macho yake eneo hilo kutafuta kigezo alichohitaji. Aliweza kuona pembezoni mwa jengo lile ndoo kadhaa zilizowekewa udongo, zikiwa na maua ya aina mbalimbali na yaliyopangiliwa kwa njia ya kupendeza. Ilikuwa ajabu kidogo kwa kuwa yalisitawi vizuri ijapokuwa haikuonekana kama kuna mtu aliyekuwepo wa kuyatunza. Ni wakati huu ndipo Grace akampigia simu kumuuliza angerudi wakati gani kwa sababu alitaka kuwa pamoja naye, naye Dylan akamjulisha kuwa haingechukua muda mrefu sana angekuwa amesharudi.

Baada ya kuagana na 'baby mama' wake, akazielekea ndoo zile, na moja baada ya nyingine akawa anazipepesa kutafuta kitu chochote ambacho huenda kilikuwa kimefichwa. Aliwaza kuwa inawezekana Harleen alificha kitu fulani kwenye maua hayo ili kiwe salama mpaka wakati ambao angeweza kumpa, lakini hakufanikiwa baada ya mama yake kumfikia kwanza. Hivyo akaendelea kutafuta-tafuta kwenye maua hayo akiwa na matumaini kwamba alichowaza kilikuwa sahihi.

Baadhi ya watu waliomwona walifikiri labda amepoteza kifaa chake, kwa kuwa alionekana kuwa mtanashati mno kufikiri labda amerukwa na akili kucheza na maua. Aliendelea kutafuta ndoo moja baada ya nyingine, na hatimaye akafanikiwa kugusa kitu fulani ndani ya ndoo moja kilichokuwa kigumu kiasi. Matumaini yake yaliongezeka hata zaidi baada ya kukivuta na kupata kuona kwamba ilikuwa ni kiboksi kidogo cha plastiki kilichofunikwa vyema; bila shaka kukiwa na kitu fulani kwa ndani. Akanyanyuka na kulifata gari lake, na baada ya kuingia, akakifungua taratibu na kukuta memory mbili ndogo.

Sasa akawa amejihakikishia kwamba alikuwa sahihi kufikiria kuwa maneno ya mwisho ya Harleen yalikuwa na maana fulani, na angeweza kujua hasa maana hiyo ilikuwa nini baada ya kuona yale yaliyokuwa ndani ya memory hizo.


★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★

WhatsApp +255 787 604 893
 
Huu mkasa ni hatari sana. Elton Tonny umetisha sana.

Yaani visa vimepangiliwa na vinasisimua mno. Uzuri ni kuwa Gilbert ni honest man, atajieleza vyema tu mahakamani kikimnukia, na hata kwa Dylan na Jaquiline kabla ngoma haijafika mahakamani nao atawaeleza kwa utuo watamuelewa
 
Very well put my friend
 
DYLAN

Story by Elton Tonny

Familia, Kazi, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Unyanyasaji, Usaliti, Visasi, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa

(R-rated 18+)

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA AROBAINI NA MOJA

★★★★★★★★★★★★★★★★★★


Kesi ilisikilizwa kwenye mahakama kuu baada ya siku mbili kupita. Familia ya Baraka ilikuwepo pia, yaani Shani, Leila, na Emilia; Steven akibaki nyumbani. Beatrice alikuwa ameajiri mwanasheria bora asimamie upande wake, na vile vile Dylan alikuwa ameajiri mwanasheria mzuri upande wake. Alikuwa akitoa mashtaka ya uuaji wa watu kama Pius, Baraka na Harleen, biashara haramu za Mr. Bernard ambazo Beatrice aliziunga mkono pia, na pia kuhusu mpango wa kutaka kumuua yeye kwa kuihujumu helicopter kipindi kile. Upande wa Dylan ulionekana kuwa na nguvu sana kwa kuwa ushahidi mwingi uliotolewa ulithibitisha kwa kiasi kikubwa hatia za Beatrice, ijapokuwa naye upande wake ulijitahidi kupambana haswa ili kumtetea.

Dylan, akiwa wa kwanza kutoa ushahidi, aliongelea kuhusiana na safari yake kipindi kile, ambayo ilihujumiwa na Beatrice pamoja na mwenzake ili auawe. Alisimulia jinsi alivyookolewa, na pia kwamba ni Beatrice ndiye aliyemuua yule aliyemwokoa, yaani Baraka. Maneno yake yalikuwa ya hisia sana na yaliwagusa wengi, huku Beatrice akichukizwa naye sana na kutamani hata amuue pale pale.

Fetty alitoa ushahidi juu ya kile alichokiona usiku ule ambao Harleen aliuawa. Aliweka wazi kwamba baada ya kusikia mlio wa risasi, aliliona gari la Beatrice likiwa linatoka sehemu ile, na Beatrice mwenyewe alikuwa ndani ya gari hilo.

Mr. Bernard alifikishwa pale pia na kutoa ushahidi dhidi ya Beatrice, akisema juu ya kifo cha Pius na Baraka. Alikiri kwamba walishirikiana kutaka kuwaangusha Gilbert na Jaquelin, na hata kupanga kifo cha Dylan. Mwanasheria wa Beatrice alimuuliza maswali mengi yenye kuchanganya ambayo yalisababisha akose mwelekeo mzuri wa majibu yake, na hata kusababisha awekwe chini ya ulinzi kwa kukiri makosa hayo, na kufanya ionekane kwamba Beatrice hakuwa na ubaya.

Ndipo mwanasheria wa Dylan akamwomba hakimu kuwasilisha ushahidi wao wa mwisho, ambao ulikuwa ni kwa njia ya maongezi yaliyorekodiwa. Beatrice alishtuka sana, kwa sababu alielewa inawezekana ndiyo yale yale maongezi ambayo binti yake alimrekodi usiku ule. Baada ya hakimu kukubali, mwanasheria akachukua kifaa kidogo cha spika na kuweka memory humo, kisha akaicheza (play) rekodi hiyo ili watu wote waisikie kila jambo vizuri.

""....wakati mwingine ninatamani tu niwafate na kuwa-shoot wote! Wananikera sana.... Hakuna.... Nimesema hapana Bernard, acha nifanye mambo navyojua kuwa sahihi... hawawezi kunishinda hata siku moja.... Kama wanafikiri wamepiga hatua mbili mbele zaidi yangu wamefeli sana, mimi niko tatu mbele zaidi! Kama vipi wakamuulize yule kachero wao Baraka... na bado.... natafuta tu nafasi nzuri nimkarabati huyo Dylan... nikimmaliza huyo nafata na Jaquelin... nimeshachoka kuigiza kuwa BFF sasa! ... Sitaki kutumia mtu kwa hili Bernard, nitadili nalo mimi mwenyewe...."

Sauti hiyo ilisikika vyema, na kila mtu angeweza kutambua yalikuwa ni maneno ya Beatrice. Hakukuwa na njia ya kukataa tena kwamba mwanamke huyo hakuhusika na mambo haya mabaya hata kidogo! Mwanasheria wa Dylan alimweleza hakimu baada ya kuifunga rekodi hiyo kwamba ni binti yake Beatrice ndiyo aliyerekodi sauti ya mama yake akiongea kwenye simu usiku ule aliouawa. Akamweleza kuwa inaonekana baada ya Beatrice kutambua binti yake amemrekodi, alimfata ili auchukue ushahidi huo, lakini kwa sababu mwanamke huyu mbinafsi alijua Harleen aliazimia kumfikisha kwenye vyombo vya kisheria, akaamua kumnyamazisha milele.

Beatrice alichoka. Hakuwa na ujanja tena. Hata mwanasheria wake alipoulizwa ikiwa alikuwa na jambo la kusema kupinga, akakanusha kwa kuwa ilikuwa wazi hata kwake kwamba mwanamke huyu hakustahili kuachiwa huru. Hivyo, hakimu akasema kwamba kesho wakati kama huo wote wangepaswa kurudi ili kusikiliza hukumu dhidi ya mtuhumiwa. Beatrice alimlalamikia sana mwanasheria wake kwa kutofanya lolote lile ili kumtetea mwishoni hapo, lakini mwanasheria akamwambia hakukuwa na njia nyingine. Mwanamke huyo akarudishwa rumande kufungwa ili asubirie hukumu yake. Mr. Bernard pia alitiwa mikononi mwa polisi kwa kuwa naye alikuwa na hatia, hivyo ni kama Grace na Dylan walikuwa wameua ndege wawili kwa jiwe moja.

Baada ya kurudi nyumbani, Grace alimuuliza Dylan alitolea wapi rekodi ile ya sauti ya Beatrice, naye jamaa akamweleza kila kitu. Mwanamke huyu alivutiwa na hekima ya Dylan, na akampongeza kwa kuwa alikuwa amewahakikishia ushindi kwenye suala hili. Sasa walichokuwa wakisubiri ni hukumu kesho dhidi ya mbaya wao.


★★★


"... Ninakwenda kuwasomea sheria zilizohusika katika kuamua kesi hii. Ili kuthibitisha mashtaka yaliyofikishwa dhidi ya mtuhumiwa Beatrice Mahone Elifazi, idara ya hukumu imepitia mambo makuu matatu yaliyofikishwa hapa dhidi yake. Kwanza, kwamba mtuhumiwa alihusika na kushiriki katika mpango wa kutaka kumuua kijana aitwaye Dylan Gilbert Mushi. Pili, kwamba mtuhumiwa alihusika moja kwa moja katika kifo cha wanaume wawili kwa majina ya Pius Ernest Shabani na Baraka Steven Majaliwa, na binti yake wa kumzaa mwenyewe kwa jina la Harleen Alfred Maganga. Na tatu, mtuhumiwa alihusika katika biashara haramu zilizofanywa kisiri kupitia fedha zake mwenyewe. Kutokana na ushahidi uliotolewa upande wa mtoa mashtaka, vigezo vyote vilivyofikishwa ili kuthibitisha kwamba haya mambo yote matatu yalikuwa na ukweli ndani yake unaopita maelezo, mahakama inamtia hatiani Beatrice Mahone Elifazi, na kumpa kifungo cha maisha jela."

Hakimu akagonga nyundo ya sheria mara mbili kuhalalisha hukumu hiyo iliyosomwa na msomaji wa hukumu siku hiyo. Familia ya Dylan, familia ya Baraka, Grace, Fetty, na wote waliokuwa upande wao walifurahi sana baada ya kuwa wamefanikiwa hatimaye kumweka chini mbaya wao. Beatrice alilalamika kwa sauti ya juu sana, akisema alionewa na hakustahili hukumu hiyo. Mapolisi walijitahidi kumdhibiti na kumvuta kuelekea nje ili wamweke kwenye karandinga na kumpeleka rumande; na baada ya hapo asafirishwe mpaka gerezani.

Jaquelin aliwaomba samahani wote kwa sababu ya kufanywa kipofu na rafiki yake huyo mnafiki, na hivyo ni kama matatizo yaliyowaandama yalichangiwa naye kwa kuwa kilichokuwa kinawala kilikuwa nguoni mwake. Lakini wote wakakubaliana kusahau yote na kuendeleza maisha yao kwa furaha, kwa sababu sasa adui alikuwa ametoweka maishani mwao. Jaquelin akapendekeza wafanye sherehe ndogo nyumbani kwake kufurahia ushindi wao, akisema wote walitakiwa kuwepo kesho ili waburudike pamoja.

Wakakubaliana na jambo hilo, kisha wote wakarejea sehemu zao za makazi.


★★★


Sherehe hii ndogo iliyofanywa kwa Jaquelin iliwaburudisha sana wote waliohudhuria. Wakati huu Jaquelin alikuwa mwenye urafiki sana kwa wote, akiwa ameachana na ubaguzi aliokuwa nao kipindi cha nyuma. Dylan alikuwa pamoja na Grace, Gilbert bila shaka na Jaquelin, na Shani, Leila, Emilia, Steven, Fetty, Patricia, na Bosco walikuwepo pia. Walifurahia mlo mzuri, vinywaji na maongezi; na wageni hapo walionyeshwa mambo mazuri ya nyumba ya wazazi wake Dylan.

Ijapokuwa hii ilikuwa pindi yenye uchangamfu, Gilbert alitambua kwamba ni kama Dylan alikuwa anamkwepa. Kuna wakati angemsemesha na kijana wake kumwitikia kwa njia iliyoonyesha hakuwa na furaha naye. Aliangalia jinsi alivyotenda kwa wengine, ilikuwa vizuri, lakini kila mara alipojaribu kuonyesha ukaribu kwake, ni kama kijana huyu alifanya mambo kwa kujilazimisha. Hivyo, wakati wengine wakiendelea kuburudika hapo, Gilbert akamwomba Dylan aende pamoja naye ndani ya nyumba ili amsaidie na jambo fulani. Dylan akatii na kumfata mzee wake, wakiwaacha wengine sehemu ya nje.

Walipofika chumbani kwa baba yake, Dylan akatambua kuwa aliitwa bila shaka kuzungumzia jambo fulani, hivyo akaiweka akili yake sawa ili atulie.

"Dylan... nimekuita ili tuongee kidogo," Gilbert akamwambia.

"Ndiyo..."

"Well... nimeona ni kama hauna amani hivi... kila nikikusogelea ni kama unanikwepa... hiyo ni kwa nini?"

Dylan akabaki kimya tu. Akatazama pembeni akiwa anatafakari jambo fulani.

"Kama kuna tatizo mwanangu, niambie. Nahitaji kujua ikiwa kuna sehemu labda sijatenda vyema... basi unirekebishe. Napenda amani kati yetu," Gilbert akamsihi.

"Nimejua ni kwa nini Beatrice alifanya hayo yote... na sababu ni wewe," Dylan akasema.

Gilbert akatazama chini kwa huzuni.

"Hiki ni kitu ambacho kimedumu kwa muda mrefu sana. Na kwa sababu sikumbuki mambo mengi, huenda hata ukanificha na kuwaficha wengine ukweli halisi, lakini hiyo haimaanishi kwamba...."

"No Dylan... sina haja ya kuficha lolote," Gilbert akamwambia kwa unyoofu.

Dylan akawa anamtazama kwa uangalifu.

"Ni kati ya mambo ninayojutia sana kufanya maishani mwangu. Beatrice... ni mwanamke ambaye nilimpenda kwanza... zamani sana kabla sijakutana na mama yako. Kwa hiyo baadae tulipokutana tena... shinikizo lilikuwa kubwa, hasa kwa sababu mimi na Jaquelin tulikuwa kwenye matatizo ndani ya ndoa yetu. Sitajitetea... ninajua nilikosea. Lakini sikufikiria makosa yangu yangewaletea watu wengi madhara ijapokuwa nilijitahidi kuyaficha... na kwa hilo naomba unisamehe," Gilbert akasema kwa hisia.

"Mama anajua?" Dylan akauliza.

Gilbert akatikisa kichwa kukanusha.

"Mambo kati yetu yalikuwa yameanza kwenda vizuri. Sikutaka... kuharibu. Najua ni ubinafsi sana lakini, niko tayari kuendelea kuwa mbinafsi ili amani iliyopo wakati huu idumu. Nataka kila kitu kiwe sawa tena," Gilbert akamwambia.

Dylan akamshika baba yake begani kama kumpa faraja.

"Usijali baba, ninaelewa. Mimi pia kuna vitu nimefanya ambavyo najua ikiwa Grace angefahamu basi... huenda hata ningempoteza. Inaonekana ni kama tunakuwa wabinafsi... lakini kihalisi tunakuwa tunataka kulinda vile vitu tunavyothamini zaidi. Samahani kwa sababu... nilifikiri ulifanya makusudi... ila sasa nimehakikisha kwamba ulichomwambia Beatrice kilikuwa ni ukweli. Natumaini itaendelea kuwa hivyo... for everybody's sake," Dylan akasema.

"Asante Dylan. Lakini... unamaanisha nini nilichomwambia Beatrice... kitu gani?" Gilbert akamuuliza.

"Harleen aliacha memory mbili, ile yenye sauti ya Beatrice, na nyingine ya video mliyorekodiwa wewe na yeye mwaka 2012; kwenye chumba fulani."

Gilbert akakunja uso wake kimaswali.

"Kwenye video hiyo unazungumza na Beatrice kwamba mnapaswa kuachana kwa ajili ya familia zenu, lakini anakushawishi mwendelee bila kujali mtu mwingine yeyote."

"Kwa hiyo... yaani... nani alirekodi?"

"Sijui. Lakini ndiyo vitu ambavyo Harleen alitaka kunipa kabla... mama yake hajamuua."

Gilbert akatazama chini kwa huzuni.

Dylan akamwambia warudi kwa wengine maana walikuwa wamekawia. Alipoanza kuondoka, Gilbert akamwita, naye akageuka nyuma.

"Ikiwa ulikuwa na memory hizo zote mbili, kwa nini haukuitumia na hiyo mahakamani?" Gilbert akamuuliza.

"Hakukuwa na haja. Sidhani kama ingethibitisha lolote lile. Na pia... kama ulivyosema... wakati mwingine ni bora kuwa mbinafsi ili kudumisha amani iliyopo," Dylan akamwambia.

Kisha kijana akatoka chumbani humo, akimwacha baba yake anahisi majuto moyoni mwake.

Baada ya Dylan kurejea kwa wengine pale nje, mama yake akamuuliza Gilbert alikuwa wapi, naye akamwambia chumbani. Hivyo Jaquelin akamfata mume wake ili aweze kurudi pamoja naye. Alimkuta akiwa ameketi tu kitandani akiwaza mambo, naye akamuuliza ikiwa alikuwa sawa. Gilbert akamwambia alikuwa sawa tu, na ni hapa ndiyo akatumia fursa hii kumwomba samahani kwa mambo mengi ambayo alifanya kipindi cha nyuma yaliyomuumiza sana mke wake; ijapokuwa hakusema mengi kuhusiana na Beatrice.

Jaquelin akamwomba samahani pia na kumuahidi kuendelea kuwa mke bora kwake licha ya kwamba naye alifanya mambo mengi yenye kumvunja moyo kipindi cha nyuma. Wawili hawa wakakumbatiana kwa upendo, kisha wakarejea kwa wengine.

Grace alikuwa pamoja na Leila na Fetty, wakionekana kuzungumza kirafiki licha ya kwamba ni mwanaume mmoja tu hapo wote walimpenda, lakini chaguo lake wakati huu lilikuwa ni Grace pekee. Jaquelin alikuwa ameleta vinywaji akisaidiana na Shani alipofika hapo na kujiunga nao kwa ajili ya maongezi, kisha Dylan, Bosco pamoja na baba yake wakajiunga nao pia huku Patricia, Emilia na Steven wakiwa wanaogelea kwenye swimming pool.

"Mimi nilipenda sana jinsi yule aliyesoma hukumu alivyosema... eti uthibitisho uliopita maelezo... hahahahah... yaani alivyoisema ni kama alikuwa anafurahia pia yule mchawi kufungwa," akasema Shani.

Wote wakacheka, naye Dylan akasogea karibu ya Grace.

"Wanaopelekwaga magereza ya wanawake na penyewe huwa wanafanyishwa kazi mashambani kama wanaume?" akauliza Leila.

"Wanafanya kazi ndio, lakini siyo zile ngumu kama wanaume," akajibu Bosco.

"Wanaitaga utumishi kwenye jamii," Gilbert akaongezea.

"Wanalipwa?" akauliza Leila.

"Ndiyo huwa wanalipwa. Lakini siyo mara zote," akajibu Gilbert.

"Tena kwa hii serikali yetu sijui sana hata ikiwa huwa wanapewa hamsini. Kwa wenzetu wanapewaga tuvisenti twa kutumia familia zao," akasema Jaquelin.

"Hmmm lakini huyo kikongwe nasikia ana hela sana kwa hiyo sidhani kama ataishi kwa shida huko," akasema Leila.

Ni wakati huu ndipo Shani akawa amemfikishia kinywaji Grace (yaani bia).

"Oh... asante Shani," Grace akashukuru, lakini hakupokea kinywaji.

"Mbona haunywi eti? Toka tumekuja hujaonja hata. Em' chukua buanaa..." Jaquelin akambembeleza.

"Siwezi kunywa kileo. Me nakunywa juice tu," akasema Grace.

"Hauwezi? Unamaanisha nini?" Jaquelin akamuuliza.

Grace akabana midomo yake akitabasamu, kisha akamtazama Dylan. Dylan akatabasamu pia na kumshika mkono, kisha akawaangaalia wote na kutumia kiganja chake kuligusa tumbo la Grace. Wote waliweza kuelewa alimaanisha nini, na sura zao zilionyesha mshangao wenye shauku kubwa sana. Jaquelin akamfata Grace na kumkumbatia kwa furaha kubwa. Gilbert alikuwa anafurahia sana pia, naye akamshika Dylan begani akimpongeza.

"Jamani! Hongera dada," Shani akamwambia Grace.

"Asante," akasema Grace.

"Ni miezi mingapi sasa?" akauliza Jaquelin.

"Miwili," akajibu Grace.

"Wow! Nyie wasiri sana... yaani muda wote huo kweli tulikuwa gizani jamani..." akasema Jaquelin.

"Tuliona tusubirie wakati mzuri wa kuwaambia," akasema Dylan.

"Nina uhakika atakuwa bonge la baunsa! Gilbert, unazeeka sasa. Ndani ya miezi michache utaitwa babu," Jaquelin akatania.

"Ahahahah... lakini wewe utabaki kuwa binti tu eeh?" akasema Gilbert.

"Ndiyo maana yake," Jaquelin akasema, kisha akamkumbatia tena Grace.

"Grace anataka awe mdada, siyo baunsa," Dylan akasema.

"Ndiyo, ningependa hivyo lakini... kwa vyovyote itakavyokuwa itakuwa sawa tu," Grace akasema.

"Ahahahah... amebadili msimamo ghafla..." Dylan akatania.

Leila na Fetty walimpongeza mwenzao pia, wakimwonea fahari kwa kuwa angekuwa ndiyo mama wa mtoto wa kwanza wa Dylan; kitu ambacho hata wao walitamani lakini haingewezekana tena. Kilichokuwepo ilikuwa ni kufurahia tu kwa ajili ya furaha ya mwenzao, nao bila shaka wangeipata ya kwao mbeleni pia.

Burudani za hapa na pale ziliendelea kwa siku hiyo mpaka wakati ambapo familia hizi na marafiki ziliachana, huku Grace akibaki hapo kwa "wakwe" siku hiyo kwa msisitizo wa Jaquelin. Mambo yalionekana kuanza kuwaendea vyema sana, nao walitazamia siku zenye furaha hata zaidi mbele ya safari ya maisha yao.


★★★


MIEZI SITA BAADAE......

Maisha yaliendelea vizuri kwa watu ambao Dylan aliwapenda.

Wakati huu, Grace alikuwa amebakiza wiki kama mbili kufikia wakati wa kujifungua, na tumbo lake lilikuwa kubwa haswa. Ili kumpa nafasi ya kutulia mpaka wakati huu, alikuwa akiishi nyumbani kwa Gilbert na Jaquelin, akitunzwa vyema na Jaquelin ambaye alitazamia kwa hamu sana mjukuu wake azaliwe. Dylan ndiye ambaye alishughulika na mambo mengi ya kampuni ya Grace, kule kule walikoishi pamoja mwanzoni, hivyo angefika mara kwa mara nyumbani kwa wazazi wake ili kuwa na "baby mama" wake kwa muda fulani kabla ya kurejea tena kule kuendelea na masuala ya kazi.

Gilbert aliendelea kuiongoza kampuni yake ya ukandarasi kama kawaida. Ilizidi kuongeza ufanisi mwingi na kukua hata zaidi hasa kwa kuwa alishirikiana na Dylan katika mambo ya kushauriana kimipango ya uendeshaji. Kwa kuwa Jaquelin alitumia muda mwingi akiwa na Grace, binti-mkwe wake wa baadae, mambo mengi ya kikazi angeyagusia mara moja moja sana au angeyafanya akiwa nyumbani, na kwa muda wote alioutumia na Grace ilikuwa ni kununua vitu kwa ajili ya mtoto na kujifurahisha kwa kadiri fulani pamoja naye.

Fetty, alikuwa ameachiwa na Dylan mgahawa wa Dy-Foods uwe wakwake kabisa. Yule msimamizi aliyekuwepo mwanzoni, yaani Tony, alikwenda sehemu nyingine kimasomo, hivyo kwa miezi michache baada ya kuondoka ni Fetty ndiye aliyeusimamia mgahawa huu, na baada ya hapo Dylan akona ampatie haki za kuumiliki kabisa. Mgahawa wa Dy-Foods ulikuwa mkubwa, wa kisasa, na ulivutia wateja wengi wenye pesa. Fetty alijitahidi kuuendesha vizuri akiwa na wafanyakazi wazuri wenye bidii na kuajiri msimamizi msaidizi pia, naye hakuwa mwingine ila Leila mwenyewe. Jaquelin na Grace wangekwenda hapo kupata msosi mzuri kila nafasi waliyopata, hivyo wanawake hawa walikuwa na ukaribu sana kufikia kipindi hiki.

Dylan alikuwa amewapa familia ya Baraka, yaani Shani, Leila, Emilia, na Steven, ile nyumba aliyoachiwaga na baba yake. Hivyo Leila angekuwa karibu na Dy-Foods kwa ajili ya kazi. Emilia alikuwa amefaulu vizuri kidato cha nne na kuchaguliwa kwenye shule moja nzuri ambayo haikuwa mbali sana na sehemu hii waliyoishi kwa ajili ya kuendelea na kidato cha tano. Kwa sababu Steven alikuwa anaendelea na darasa la saba, yeye na Shani bado walikaa kule kule kwao, na mara kwa mara walikuja kwenye nyumba yao hii mpya ambayo waliifurahia sana. Ilitakiwa mpaka Steven amalize darasa la saba ndiyo waweze kuhamia huku moja kwa moja kwa kuwa haingekuwa rahisi kumhamisha shule kipindi hiki.

Sophia, yule mdogo wake Fetty, alikuwa akiendelea vizuri kufikia kipindi hiki. Bado aliendelea kutumia dawa na vifaa vilivyomsaidia kutembea vizuri kiasi, na angalau aliweza kujitegemeza mwenyewe katika mambo kadhaa aliyohitaji kufanya. Dylan alikuwa ameahidi kumhudumia kimasomo atakapokuwa na nafuu zaidi, na jambo hilo lilimpendeza sana Fetty. Familia ya Fetty ilikuwa ikiendelea kuishi kule kule kwenye nyumba yao ambayo wakati huu Fetty alijitahidi kuiboresha. Pia, alikuwa amemsaidia mama yake kufungua duka la nguo, na hivyo mama yake akawa akiendelea na biashara hiyo na ushonaji kama kawaida.

Kipindi hiki cha siku za karibuni, familia ya Dylan ilikuwa na sababu nyingine ya kuwa na furaha kwa kuwa mdogo wake Gilbert, yaani Camila, alikuwa amekuja na mchumba wake huku kufanya kama 'sendoff' kwa ajili ya ndoa yao. Dylan bado hakuweza kukumbukia mambo aliyowahi kufanya pamoja na shangazi yake huyu, na hii kidogo ilimpa ahueni Camila kwa kuwa hangejihisi uajabu kama ule ambao angekuwa nao ikiwa Dylan angekuwa mwenye king'ang'anizi kama kipindi kile.

Wakati huu, Dylan alimtendea Camila kama mtu anayemzidi umri kwa heshima kubwa, akielewa kuwa aliishi naye Brazil kama mama yake mdogo, bila kukumbuka mapenzi yao ya marufuku. Na mambo kuwa hivyo ilifaa ili kuendeleza furaha baina yao kwa sababu sasa Camila alikuta Dylan pia ana mwanamke wake aliyempenda sana.

Mipango ya sherehe ilikuwa imefanywa, kukiwa na waalikwa wengi waliotakiwa kuhudhuria. Mchumba wa Camila alikuwa amekuja na mama yake na ndugu wengine wachache kwa ajili ya tafrija hii nzuri. Walikuwa ni watu wazuri na walifurahia uwepo wao huku nchini baada ya kuchangamana na familia ya Camila. Dylan, Gilbert, na baba yake Gilbert na Camila walishirikiana kuandaa sehemu na mambo ya kufanyia sherehe hii. Walichagua hoteli kubwa ya kifahari, na kupangilia vitu vingi kwa msaada wa kamati iliyoundwa kushughulika na mambo yaliyohitajika. Vitu vingi kama vyakula na burudani zilihakikishwa kuwa za kipekee na kwa wingi sana ili kila mtu ambaye angehudhuria afurahie vilivyo.


★★★


Siku ya sendoff ikafika. Wanaume walijiandaa mapema kwa kupendeza sana na mavazi yao ya suti. Wakati huu Dylan hakuwa akifuga rasi, bali alinyoa nywele zake za mtindo huo na kuacha nyingi katikati, huku pembeni akizipunguza kiasi. Babu yake, Gilbert, Bosco, Steven, na bila kumsahau Jafari, wote walikuwa pamoja naye kuelekea ukumbini mapema. Waliambatana na mume mtarajiwa wa Camila, ili kumtafutia sehemu nzuri ya kumficha kwa bibi harusi, kama ilivyo desturi ya sendoff nyingi, mpaka wakati ambao bibi harusi angemtafuta na kumfichua kwa watu.

Wanawake maalum, yaani Jaquelin, Grace, na Camila, walitumia muda mrefu kuandaliwa na wapambaji wenye uzoefu pale pale nyumbani kwa Gilbert. Kwa kuwa nyumba yao ilikuwa kubwa, walifanyia mambo hapo kwa kujinafasi na kwa shauku kubwa, wakitazamia kwa hamu sherehe hii. Pesa ni nzuri sana. Yaani wangeweza kufanya lolote na popote walipojisikia ili kuziridhisha nafsi zao. Grace alipendeza sana pamoja na tumbo lake kubwa. Jaquelin kama kawaida alionekana kama mwanadada badala ya mwanamama, na Camila ndiye aliyependeza hata zaidi akiwa bibi harusi. Wakawa hapo wakimalizia mambo yao huku wakisubiri wakati mwafaka wa kuanza kuelekea kule kwenye hoteli.

Ukumbini, mambo yalianza kwa burudani za hapa na pale kutoka kwa MC wa sherehe na muziki pia. Marafiki wengi wa Camila, Jaquelin, Dylan, Gilbert, Grace, na baba yao Gilbert walikuwepo hapo pia. Leila, Shani, Emilia, Fetty, Patricia, na wengine waliokuwa karibu na Dylan walifika wakiwa wamependeza sana, na wageni wote wakatulia kusubiria bibi harusi afike hatimaye.

Lakini mambo yalianza kwenda kinyume na matarajio. Bibi harusi pamoja na watu waliotegemewa kufika naye walichelewa sana. Mpaka inakaribia kufika saa mbili na nusu usiku, bado Camila na wengine hawakuwa wamefika. Dylan na baba yake waliwatafuta sana kwa simu, lakini kwa sababu fulani hawakuwa wakipatikana. Walijaribu hata kuwatafuta madereva wao na wengine waliokuwa karibu nao, lakini bado hawakupata itikio lolote. Baadhi ya wapambaji walipigiwa simu kuulizwa kama bado walikuwa wanaendelea kuwapamba, lakini wakasema walikuwa wameshahitimisha mambo hayo na kuondoka huko mapema tu.

Wakati bado kukiendelea kuwa na hali ya sintofahamu, Jafari, ambaye alikuwa ametoka kwenda kuongea na simu pembeni, akaja upesi kumwelekea Dylan akiwa na habari fulani zenye kushtua sana. Akamwongoza kuelekea pembeni ili aweze kumwambia.

"Vipi Jafari?" Dylan akauliza.

"Nimepigiwa simu kuambiwa kwamba Beatrice ametoroka gerezani!" Jafari akamtaarifu.

"What?!" Dylan akashangaa.

"Ndiyo Dylan. Ametoroka jana usiku eti," Jafari akamhakikishia.

"Kivipi?"

"Hawajabaini njia aliyotumia, lakini inawezekana kuna maaskari amewalipa wakamtengenezea njia... labda hata wakuu."

"Kwa hiyo katoroka tu halafu wamemwach...."

"Dylan, nini kinaendelea?" Gilbert akawa amefika hapo.

"Baba, tumepata taarifa kwamba.... oh my God!" Dylan akaishia hapo baada ya wazo fulani kuingia akilini mwake.

"Nini?" Gilbert akauliza.

Dylan akaonekana kutahamaki sana. Alitoa macho na kujishika kichwani kwa kuhofu.

"Dylan... Jafari, nini tatizo?" Gilbert akamuuliza akiwa amechanganywa.

"Beatrice ametoroka jela," Jafari akamjulisha.

"Nini?!" Gilbert akashangaa.

"Ni Beatrice! Beatrice ndiyo.... atakuwa amewafiki... oh my God... Grace!" Dylan akawa anaongea kwa wasiwasi.

Ilikuwa wazi akilini mwake sasa kuwa bila shaka Beatrice aliyetoroka ndiyo amefanya jambo fulani lililosababisha mpaka wanawake wao wakawa wamechelewa vile. Alihofia sana usalama wa mama yake, shangazi yake mdogo, na mama wa mtoto wake ambaye hakuwa mbali sana kujifungua. Bila kusubiri lolote, alitoka hapo haraka na kukimbilia nje kwa kasi sana, akiwaacha watu wanamwangalia kwa mshangao. Jafari pamoja na Gilbert walimfuata pia mpaka nje, wakiwa wanaelewa kwamba alichowaza Dylan huenda kilikuwa sahihi.

Dylan alitaka kuharakisha nyumbani kule, akiwa na matumaini ya mbali kwamba huenda bado Beatrice hakuwa amewafikia wapendwa wake, au kama alikuwa huko basi afanye yote awezayo kuwatoa mikononi mwa mwanamke huyo mkatili. Akaingia ndani ya gari na kuliwasha upesi, na hapo hapo Gilbert na Jafari wakaingia ndani ya gari hili pia ili waelekee pamoja naye kule.

Dylan akakanyaga mafuta na kuliondoa gari hapo kwa kasi sana, akitaka kuwahi wapendwa wake kabla kitu chochote kibaya hakijawapata.


★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★

Usikose sehemu kali zitakazofuata!

DYLAN ▶WhatsApp +255 787 604 893
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…