SIMULIZI: ELIZA NA NDOA YANGU SEHEMU YA 11
NA
Man Middo tz 0655 969 973
[emoji1427][emoji1427][emoji1427]
Baade mama mdogo akaniruhusu kwenda kwa Mudy akaniambia
“Sasa unaweza kwenda kukutana kuongeza njia”
(Aliingiza kautani kidogo) basi kabla sijaenda kwa Mudy nikaenda kliniki nikakutana na dokta akaniuliza
“Kwanini umeamua kuzaa na umri mdogo?” Nikamwambia ivyokua akaniuliza kuwa
“Mpaka imefika miezi mitatu umekutana na mhusika na je anakutafuta”
“Ndio ananitafuta” akaniambia
“Sasa jitahidi muwe mnakutana kimwili ili kuongeza njia, ili siku ya mwisho kisu kisihusike na kazi ufanye sana maana ni kama umelegea”
Na ni kweli nilipungua sana kilo na ukiniona nilikua kama mgonjwa. Nilirudi nyumani nikamtaarifu Mudy kuwa nahitaji kuja akanambia sawa, akapanga siku kweli akaja na toka siku hiyo nilisuka nywele za vitunguu.
Mudy aliniambia kwenye simu kuwa hatoshuka wala kukaa atakapofika tu ananichukua tunaenda kwa mama then tunaondoka kwake nikasema sawa.
Basi toka kipindi tunagombana kuhusu mahari na wao waje watoe mahari sijaonana na mama wala kufika nyumbani.
Mudy alikuja na rafiki yake akapiga honi nikatoka, wee! Mudy alinishangaa sana kwa hasira akaniambia
“Panda chap tuondoke”
Mimi nilijua sababu ya yeye kuchukia ni kuwa nilikua nimekonda sana na nilikua nimetoka vipele na nywele za vitunguu. Shem akashindwa kuvumilia akaniuliza
“Mbona uko hivyo unakula kweli?”
Sikua na jibu sahihi nilikaa kimya tu Mudy alikua na hasira alibakia kusonya tu.
Basi tukafika nyumbani kwa mama yangu akatukaribisha tulikuta ashapika kumbe Mudy alishampa taarifa.
Sasa mama kuniona tu ile hali yangu akaanza kulia
“Mwanagu nini! kulikoni mbona kama huli na kwanini huli?”
Bado nilibaki kimya tu mama aliumia sana pamoja na yaliyopita lakin alijua kule kwa mama mdogo muangalizi hakuna maana mama mdogo anaenda kazini na mimi kipindi kile nisingeweza kubaki kwa mama kwasababu ya maneno yake.
Ndugu zangu na mtaa mzima walijua nilimuacha yule boy wa pale mtaani kwasababu ya pesa kitu ambacho si kweli. Mama akaniuliza
“Unakula kweli?”
“Ndio Mama nakula” Mudy akasema
“Sio kweli niliongea na mama mdogo wake alinambia huwa anakunywa maziwa, maji na tikiti maji tu” nikawa kimya tu.
Basi wakandaa chakula mama akanipakulia chakula nikamwambia
“Nipe maji kwanza” Mudy akamwambia
“Mama usimpe ukimpa hatokula ale kwanza” nilinuna nikachukua ili nile lakini nilishia vijiko viwili tu, tena kwa usimamizi wa mama. Akaniambia
“Kula mwanangu, kula hiyo hali bila kula ni sawa na bure, unajua oparesheni sio nzuri” Nilijaribu nilishindwa Mudy akanambia
“Hutaki kula subiri tufike nyumani kwetu hujawahi kuonana na mama mkwe wako ndo mtaenda kuonana”
Sasa mh! kusikia hivyo niliwaza maana sikuwahi kumuona kweli, Basi tukala tukatoka nje tukaagana na mama tukanza safar ya kwenda Pwani.
Njiani ikafika usiku Mudy akasimamisha gari sheli flani hivi yenye supermarket akasema
“Haya tushuke tuchukue chakutafuna ili tufike bila njaaa”
Mimi sikushuka yani kutembea ilikua ishu harafu nilikua najihisi mbaya muda wote nilijichukia ghafla kwasababu Mudy alionyesha nimekuwa hovyo au mbaya hivi kwa hiyo nilikosa ujasiri. Nikamuomba aniletee alinijibu kwa dharau
“Sifanyi ujinga huo kama huwezi kushuka basi” Shem akasema nitakuletea, Mudy akamjibu
“Usimletee! Umletee ili iweje achana nae”
Wakaondoka mimi nikabaki nikaona sawa tu, hata wasipoleta kwanza nilikua siskii njaaa kabsaaa yani.
Baadae wakarudi huku wanakula Mimi nikaa kimya tu, Mudy alijua nitachukia au nitadai lakini nilikua kimya akanza kuongea
“Mimi siwezi kukaa na mtu asie kula yani twende lakin ukizidi kukaa bila kula nitakurudisha kwenu, siwez Mimi ujinga huo yani tumbo lako kula tuhusike wengine. Nakwambia nitakurudusha kwenu labda kwenu ndo utakula yani umeniuzi sana, inafikia hatua mpaka mama yako analia mbele yangu kana kwamba sijui unakosa nini”
Aliongea mpaka nilijiskia vibaya nikajiona kama nimemkosea sana mama nikaumia sana kwa kitendo kile mpaka mama kulia. Akamwambia Godii
“Hebu mpe”
Kumbe walinunua vitu vingi tu waliweka kwenye mifuko nikachukua nikawa natafuta huku natafakari ukali wake kuwa haoni kuwa mimi sipendi pia hiyo hali.
Baadae mama yake akampigia simu akamuliza
“uko wapi?” Akajibu
“Tupo njiani tunakaribia”
“Sawa amekula huyo?” akaanza kumwambia sasa
“Hali yani tumetoka kwao hajala chochote hapa nimenunua vitu vya kijinga ndo anajifanya kupapatikia yana anauzi sana ngoja aje uone”
Basi tukaendelea na safari tukafika njiani akashuka shem tukafika nyubmani.
Usiku ule alienda kwao kuchukua chakula sikuweza kula kabisa yani ikabidi aagize tu chipsi na mshikaki zilipanda kidogo nikala nusu tu harafu nikatapika alikua anakunja sura huyo, basi nikaenda kulala.
Nikakumbuka kuongeza njia basi tukafanya wee!!! Asubuhi niliamka nguvu sina wakati nimekaa sebleni Mudy anajiandaa kwenda kazini nikasikia hodi! Kumbe alikua mama mkwe akaingia nikamsalimu pale alionekana kuwa na taarifa zangu zote basi akaanza kunipa risala ya vyakula maana yeye alikua nesi mstaafu akaniambia
“Ni lazima ule bila hivyo itakua ngumu kuwa salama na mtoto tumboni cha msingi useme chochote unachotaka harafu usilale muda wote” akaongea weee! Aksema
“Ngoja nikuetee chai unywe” Nilianza kusema
“Haya sasa ya kusimamiwa ni mateso”
Baade akaleta trei la chakula yani kuna kila aina ya vitafunwa viwili viwili na chai aina tatu nichague kipi kinapanda nilionja kila kitu nikaona bagia na uji ndo vinapanda kidogo lakini nilitaka sana ubuyu na soda………. ITAENDELEA
HIVI MIMBA ZINAKUAGA HIVI UNAPENDA TU UBUYU NA SODA? WANAWAKE TUAMBIE YAKO ILIKUAJE?
MWANAUME TUAMBIE MKEO ALIKUA ANAPENDA NINI KIPINDI MJAZITO MPAKA UKANZA KUCHUKIA?
JE UNAJUA KIFUATACHO?BASI UKO TUELEKEAKO NIKUTAM BALAA, KUNAHUZUN ISHA NA KUNAFURAHISHA.
NUKUU “Katika maisha wakati wa furaha, Rafiki na ndugu zako watapata kujua WEWE NI NANI. Wakati wa matatizo utapata kujua yupi ni rafiki yako”
Hata Eliza mama yake alishamgombeza kwa kupata ujauzito lakini barua ilivyokuja akapiga vigelegele.
(Hapa tunajifunza wazazi wetu kuna muda wanangalia maslahi kuliko utu wa mwanae)
Kingine Mudy anakunja sura mke wake akitapika lakini akiwa faragha mambo yanakua mazuri
(Jifunze kumpenda mwenzi wako katika kila hali anazopitia, jitahidi sana kumjua mpenzi wako, jitahidi uwe rafiki wa mpenzi wako kwani ukiwa rafiki utajua matatizo yake yote”
Whatsapp 0655 969 973