SIMULIZI: ELIZA NA NDOA YANGU
SEHEMU YA 21
Man Middo Tz
ILIPOISHIA………..Siku hiyo tukaenda hadi kwa wakwe na dada, ilibidi tuwahi sana maana dada alikua na watoto na hana mtu maalum wa kumwachia wanae, hivyo alipanga nanipeleke ili jioni arudi. Lakini nilikua naumia na kumuwaza tu Mudy kuwa
“Kwanini ananizungusha hivi hasemi tu ukweli kwa ndugu zangu kuwa hanipendi”
Nilikua kama mtu wa kuburuzwa tu, kwanza aliweza kuwashika ufahamu ndugu zangu akiwemo mama (wamama wakinyakyusa shikamooni kwa kuheshimu wakwe) maana Mudy aliwajua ndugu zangu kuwa wanamheshimu hivyo akinifukuza nikifika kwetu anasema “Sijamfukuza”
mama nae bila kufikiria anasema “Rudi kwa mumeo kumbe hujafukuzwa” nikirudi anasema “Nilikwambia utarudi tu na hivyo kwenu masikini utaenda wapi.”
Basi njia nzima nikiwaza hayo nilikua nalia tu, dada alinisihi kuwa maisha ndio yalivyo........SONGANAYO
Dada njia nzima alikua ananisihi tu kuwa
“Maisha ndio yalivyo mdogo wangu na siku Mudy atajua anachokufanyia ni upumbavu, ila ukifika akisema baki wewe baki ila uishi nae kwa akili sana”
Basi tukafika kwa wakwe tukawakuta, kumbe walikua wanajua ujaji wetu, wakati huo mimi nilikua na hasira zangu tu haswa nikikumbuka wamesema hawajui kama nimeondoka.
Baade tuliletewa chakula mimi hata sikula, baada ya chakula dada akaanza kujieleza kuwa
“Baba huyu Eliza ni mdogo wangu na ni kama ilivyo kwa Mudy tu, naweza sema wote wadogo zangu, tunafahamu Eliza aliondoka kwa mumewe baada ya kufukuzwa na Mumewe. Kutokana na maelezo aliyotoa na barua aliyokuja nayo kama talaka lakini pamoja na hayo imeonekana sio kweli kama amefukuzwa, sasa ikaonekana kuwa kwakua hajafukuzwa anatakiwa arudi hapa ili muyaongee kama wazazi kisha waendelee na maisha yao.
Pia sisi upande wetu nazani hata kwenu pia tunafahamu kuondoka bila taarifa kwa mumewe si vizuri na nichukue nafasi hii kwa niaba ya mama tunaomba radhi kwa mgongano wa nyie wazazi hivyo tunaomba Mudy akirudi myaongee muamalize”
Mama mkwe akadakia
“Waongee wapi? Hapa sio mahakamani hapa kwangu hatutaki vikao tena wakongee huko huko kwao hapa hakuna kitu kama hicho, kila mtu anamisha yake hatutaki ujinga hapa” baba mkwe nae akadakia
“Kwani huyo Eliza ni nani? Sisi hatumtambui! Tunamuona kama hawala tu wa mtoto wetu, hebu muulize ni lini walifunga ndoa? Na kama walifunga ndoa sisi tulikuja? Au huyo mama yake alikuja? Narudia sisi hatumtambui huyu ni kama hawala tu wa mtoto wetu lakini sio mke wa mtoto wetu, aende tu akamsubirie nje hapo akija watajuana wenyewe huko huko, sisi hatumjui hata kumkaribisha hapa tumefanya makosa mnoo alipaswa asiingie hapa”
Muda wote dada alikua kichwa chini ni kama amebeba mzigo usiomhusu kwa kweli nimelia yani nimelia nilikua siamini kama yale maneno yanatoka kwa wakwe. Baba mkwe aliyekua ananipenda vile na mama mkwe niliyekua namchukulia kama mama yangu leo hii wanaongea vile tena kana kwamba kipindi naondoka sikuondoka katika mikono yao, harafu tena kwa karatasi waliosema ni talaka, eti leo hii hawanitambui niliumia mnoo.
Baadae dada akaniomba ninyamaze akiniambia hatuwezi kupata suruhu kwa kulia hivyo. Mama mkwe akarudi tena kwa kasi kuwa
“Hapa hakuna kikao vikao mtakaa huko huko hapa tulishanawa mikono maana kila siku nyie tu, kazi ya kumtuhumu mwanangu Malaya kutwa kucha, sasaivi kuna mwanaume msafi? eti wewe dada yake kuna mwanaume msafi sikuhizi”
Baba mkwe allikua kimya kwa muda akimuacha mkwewe ajimwage aisee aliongea siku ile na nilichogundua Mudy alikua anaongea vitu vingi vya kusingizia ili mimi nionekane mbaya kwa wazazi wake. Alifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana na mimi kwa ujinga wangu nilikua sisemi makosa makubwa ukweni hapo nilijiona boya baada ya kuona Mudy ameweza kuwashawishi wazazi wake.
***
Baadae dada akaanza kuomba msamaha akawambia
“Msameheni huyu bado ni mtoto na hata hiyo ndoa kaikimbilia tu hebu msameheni au nisameheni kwa niaba yake” basi baba mkwe akasema
“Nimekusamehe wewe dada mtu kwakua unaheshima sana lakini Eliza angekua peke yake nisingempokea hapa, sasa utalala tu hadi kesho kwakua muda umeenda huyo Mudy akirudi nitamuliza anatakaje akikataa unarudi kwenu asubuhi”
Dada akashukuru pale na akaomba kuondoka ili awahi watoto wake, Baadae usiku Mudy alirudi kwake akamuita baba yake na mdogo wake wakiume wakaenda kuongea huko kwake mimi nilibaki tu kuwaza kama atanirudisha au kuamua tu nirudi kwetu hata usingizi haukuja. Baadae walirudi saa 8 usiku ila Mudy hakuja, na usiku huo huo wakawa wanajadili kitu na mama mkwe nikahisi labda nitaitwa ila walikua kama mipango flani wanapanga.
**
Baadae wakaingia zao kulala bila kuitwa, basi asubuhi ilivyofika nikaamka nikafanya usafi nikapika chai tukanywa ndipo baba mkwe akanita akanipa tena elf 20 hapa niliwaza “Narudi nyumbani lakin pia hawazi hata huyu mtoto wananipa hela ya nauli tu” basi baba mkwe aliniambia kuwa
“Hii hela uende nyumani Mudy amesema atakuja huko huko sasaivi yupo bize na kazi”
Nikapoke ile hela nikaenda zangu kuvaa na mwanangu tukapelekwa hadi staendi nikapanda gari nikarudi Morogoro.
****
Nilivyofika na maumivu yangu nikamlilia mama kwa uchungu nikimwambia
“Mama naomba unipeleke kusoma Mudy ameamua tu kufanya dharau nimeenda kule lakini hakuna jipya zaid ya kutukanwa na kuonyesha dharau ya pesa zao, naomba sana mama nipeleke chuo mimi sio wa kuitwa hawala mama yangu naomba please nipeleke chuo nikiwa na kazi haya yataisha”
Mama nikama hakuona uchungu nilionao wala yale machozi yangu, achilia mbali yale ya kila siku lakini muda ule yalikua ya uchungu mno.
Basi mama akaniambia “Subiri kikao! Wewe bado ni mke wa mtu nitapoteza pesa zangu bure kwako ngojea aje huyo mwenzako tujue kuwa unarudi au hurudi”
Niliumizwa sana na maneno ya mama, nilitarajia angekua na maamuzi magumu juu yangu lakini ndo hivyo. Dah! Baadae nilikaa tu mtaani bila cha kufanya kila siku kazi yangu ilikua kumkumbusha mama ampigie Mudy nijue kama anakuja lakin cha ajabu Mudy alikua anatangaza mtaani kuwa sitaki asome nataka maisha yampige kwanza mpaka aombe msamaha.
*
Nilizidi kukonda siku hadi siku, nikawa mweusi chu wakati hata sio mweusi. Muda wote huo hajawai kumkumbuka mwanae hata kwa chochcote, nikazoea tu maisha ya mtaani kama ndio yalivyo na tukakaa kimya hatuwatafuti. Sasa walivyoona tupo kimya siku hiyo wakapiga simu kuwa
“Tunakuja kuyaongea wiki ijayo” basi siku ikafika wakaja kwaajili ya kikao…….ITAENDELEA.
JE UNAJUA KWENYE KIKAO WALIAMUA NINI? JE ELIZA ATARUDI TENA KWA MUDY? SOMA NUKUU HARAFU USIKOSE SEHEMU YA 22.
NUKUU “Kumbuka Mwishoe utaishia kuumia tu kama unafikiri watu watafanya wema kwajili yako Kama wewe ujitoavyo kwajili yao, SIO KILA MTU ANAMOYO SAWA NA WAKO” ELIZA ametenda wema mwingi kwa wakwe zake lakini hakuna malipo yoyote, hapa ndio unaweza kuchukua ile dhana kuwa “Tenda wema harafu nenda zako na usubiri malipo kwa Mungu” lakini Mungu anaona kila chozi lilidondokalo na sababu za chozi hilo, Nyie mabingwa wa kumwaga machozi ya watu hakika malipo yenu yapo hapa hapa duniani.
Kumbuka “Mtu kufikia hatua ya kulia sio kwamba ni dhaifu NOO, Ila hii ni kwakua amebaki imara kwa muda mrefu”
Kama unahitaji episode ijayo kujua maamuzi ya kikao nicheki Inbox
man Middo au Whtasapp 0655 969 973 Upate mwendelezo.
Usikose kujua waliamua nini katika kikao chao, Je Eliza atarudi tena kwa Mudy au atabaki,
hakikisha unalike ukurasa wangu wa
Man Middo tz