SEHEMU YA 35
Richard akazibofya zote na kusema " Meseji zote zinatoka kwa mtu mmoja. Maajabu hawa watu wawili wanajuana. Cha ajabu mmoja kaletwa kutoka Mbeya na mwengine tumemkamata hapa Mafinga but those wametumwa na mtu mmoja ambao wote katika simu zao wamemsave kama Chifu. Huyo Chifu ni nani?" Richard alisema.
"Tumepiga hatua kubwa sana. Sasa inabidi tuwajue zaidi hawa watu. Na tumjue huyo Chifu ni nani? Na tujue uhusiano wa hawa watu wawili ni upi?" Felix alisema.
"Huyu jamaa mwengine hajalog out upande wa e-mail" Richard alisema kwa furaha. " Kuna email nane katika simu yake. Na zote zinatoka kwa mtu mmoja mwenye email
mimi@yahoo.com. Na email zote nane zinafanana zina maneno mawili tu. Nakuja kesho. Ila zimetumwa juzi. So inavyoonesha ameshaingia huyu jamaa anayejiita mimi" Richard alisema.
"Swali lengine kwetu ni Mimi ni nani? Je anahusika katika upelelezi wa hawa jamaa kwetu? Felix aliuliza.
" Kingine Felix katika orodha ya namba ya huyu mwengine kuna mtu kamsave kwa jina la Mimi. So Mimi ni mtu ingawa hatumjui. Na bila shaka Mimi yupo mjini hapa" Richard alisema.
"Je kwa huyo mwengine hakuna mtu aliyemsave kwa jina Mimi" Mtu mfupi mnene aliuliza.
"Ngoja niangalie" Richard alisema huku akiipekua simu ya Mwanasheria mlevi.
"Mmh mimi hamna lakini kuna mtu kamsave kwa jina la Me. Ngoja nizifananishe hizi namba" Richard alisema huku akiishika na simu ya Dokta Yusha. "Oooh its the same number. Mimi ni Me ni mtu mmoja. Namba zao ni sawa" Richard alisema.
"Hebu zicheck hizo namba za Mimi kwenye mtandao wa simu zinasoma jina gani?" Felix aliuliza.
"Ngoja niangalie hapa, wazo zuri Felix. Ngoja nimtigopesa"
Richard alichukua simu yake na kujaribu kuitumia pesa ile namba.
"Weeeeeeeee unajua inasoma jina ganiiiii? Richard alisema kwa nguvu akiwa amesimama wima.
" Jina gani?" Felix aliuliza.
"ELIZABETH NEVILLE!!!" Richard alisema kwa sauti kuu.
"Mimi au Me ambaye alikuja jana ni Elizabeth Neville. Elizabeth si tunaye sisi. Huyo ni Elizabeth Neville gani tena? Inamaana huyu siye Elizabeth Neville wa kweli?" Felix aliuliza.
"Haya mambo yanachanganya sana. Kuna kitu kimejificha kati ya watu wale watatu. Halafu wanajifanya hawajuani kabisa mle chumbani kumbe ni waongo" Mtu mfupi mnene alisema.
"Tumegundua mambo muhimu sana. Kwa sasa lazima tuwe makini nao sana. Pia lazima tuhakikishe kama yule ni Elizabeth Neville kweli. Maana imeshakuwa utata" Mtu mwembamba alisema.
"Felix naomba tukawabane wale jamaa watwambie kuhusu huu utata. Tukiamua tunaweza" Richard alisema.