Simulizi : Elizabeth Neville

Simulizi : Elizabeth Neville

SEHEMU YA 31

Asubuhi na mapema viongozi walewale kasoro mmoja walikutana tena katika ikulu ya nchi jijini Dar es salaam. Safari hii IGP John Rondo hakuwepo. Rais Joseph alimfukuza IGP Rondo kwa uzembe wa kuleta ripoti isiyo sahihi kuhusu Elizabeth Neville na nafasi yake kuchukuliwa na Zaidi Kalinga. Katika kikao cha sasa kulikuwa na ukimya na nidhamu kubwa sana. Kila mmoja alikuwa anamwogopa Mheshimiwa Dr Joseph kupita maelezo.

"Nina imani sasa hivi tumekutana watu wazima wenye akili zetu. Utoto katika utawala wangu ni mwiko. Haiwezekani Taifa liibiwe kiasi kikubwa sana cha dhahabu halafu sisi tunaotegemewa kulilinda Taifa tunaitana kuleta utoto. Sasa tuendelee pale tulipoishia, kama alivyosema Mkurugenzi wa usalama wa Taifa njia yetu ya kutufikisha kwa wezi wetu ni moja tu. Ni kumsaka Elizabeth Neville popote pale alipo. Awe mbinguni, awe chini ya ardhi, awe nchini ama nje ya nchi lakini lazima tumpate. Nia ni kumfikia Elizabeth na kumleta mbele yetu, sasa ni nani wa kutupeleka kwa Elizabeth Neville? hili ndio swali la msingi. Mi mambo ya ripoti za kipuuzi sina haja nazo tena. Swali tunamfikiaje Elizabeth Neville??" Rais aliacha hewani swali lake. Dr Joseph alificha nia yake ya kumsaka Elizabeth Neville kwa mgongo wa wizi wa dhahabu.

"Unajua tunapata shida sana lakini hili suala tunaweza kulimaliza kwa kuwahusisha usalama wa Taifa. Mkurugenzi wa usalama wa Taifa ana vijana wengi sana ambao tukiwapa hii kazi yaweza kufanikiwa kwa asilimia mia moja" Makamu wa rais alisema.

" Ni nani anayeweza kutupeleka kwa Elizabeth Neville kati ya vijana wako Mkurugenzi wa usalama wa ndugu Christopher Mangwina? Jua lazima awe mtu imara, jasiri na mzalendo. Ni nani unayemuamini twambie tumpe hii kazi inayoonekana kuwa nzito sasa" Waziri mkuu alisema.

"Mwanasheria mlevi na Dokta Yusha bila shaka wataiweza kazi hii. Sina shaka yoyote juu yao.." Mkurugenzi alisema kwa sauti iliyosikiwa na kila mtu.

Watu wote kwenye kikao walishangaa. Ingawa walikuwa wanauliza maswali lakini majibu walikuwa nayo. Kwa jinsi mkasa huu ulipofikia waliamini ni mtu mmoja ambaye atatajwa na mkurugenzi wa usalama wa Taifa. Ni mmoja tu, ni Daniel Mwaseba. Sifa za Daniel zilikuwa zinajulikana na kila mtu mle ndani. Kuliokoa kwake Taifa katika hatari mbalimbali hakuna aliyekuwa amesahau. Misheni yake ya karibuni aliyoifanya huko nchini Ureno iliicha dunia ikiwa katika kiulizo. Dunia nzima ilijiuliza ni nani huyo

Daniel Mwaseba?. Lakini leo hii mkurugenzi wa usalama wa Taifa anaulizwa yeye anawataja
 
SEHEMU YA 32

Mwanasheria mlevi na Dokta Yusha. Ingawa hawa pia ni wakali lakini bado uwezo wao haufikii hata nusu kwa mpelelezi Daniel Mwaseba. Dokta Yusha na Mwanasheria mlevi walipambana vilivyo katika harakati za kundi hatari lilitokea huko Kilwa likilojulikana kama Six killers, katika kadhia ambayo mwandishi mmoja aliitungia kitabu na kukiita Balaa. Lakini hata katika hiyo balaa huwezi kumuacha kumzungumzia Daniel Mwaseba kwa mchango wake.

"Umesema Dokta Yusha na Mwanasheria, una hakika wataifanya hii kazi kwa ufanisi mkubwa?" Rais Joseph aliuliza.

"Bila shaka. Ni vijana mahiri sana hawa. Wataifanya hii kazi vizuri sana" Christopher Mangwina alijibu.

"Hakuna tatizo. Sasa nataka nusu saa ijayo Mwanasheria na Dokta Yusha wawe hapa. Lazima tuwaambie wote ili wajue uzito wa kazi wanayoenda kuifanya" Rais Joseph alisema.

"Ni kweli. Lazima tuone mipango ni mikakati yao katika hili suala. Nasi tuwape maoni yetu pia. Mkurugenzi wasiliana na hao watu ili wafike hapa" Waziri mkuu alisema.

Mkurugenzi wa usalama wa Taifa alitoka nje ili akawasiliana na wakina Dokta Yusha. Alipiga simu kwa Mwanasheria mlevi, hakujisumbua kupiga kwa Dokta Yusha kwani alijua amepotea kama alivyopewa taarifa na Mwanasheria mlevi. Lakini cha ajabu simu ya Mwanasheria mlevi ilikuwa haipatikani.

" Mwanasheria naye hapatikani? Kimetokea nini huko Mbeya!!" Hisia mbaya zikaanza mpata Mkurugenzi wa usalama wa Taifa. Akatafuta namba ya Dokta Yusha na kumpigia, naye alikuwa hapatikani.

Alirudi ndani ya kikao sura yake ikiwa imetahayari. Watu wote kwenye kikao walikuwa wanasubiri kauli yake.

"Both are not reachable katika simu" Alisema mzee Mangwina.

"Haina shida wasiliana na katibu mahsusi wako awaambie waje hapa kama wapo ofisini" Rais Joseph alisema.

"Nimempigia kanambia hawapo ofisini" mkurugenzi Mangwina alisema.

"Tunafanyaje sasa?" Rais Joseph aliuliza

"Nitaendelea kuwasaka. Nikiwapata nitawajulisha. Ngoja nishughulikie hilo" mzee Mangwina alijibu.

Kikao kikafungwa kazi akiwa kaachiwa Mkurugenzi wa usalama wa Taifa kuwaleta Dokta Yusha na Mwanasheria mlevi.

***

Saa nne asubuhi katika uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere. Ndege ya shirika la ndege la Algeria ilitua katika uwanja huo wa kimataifa. Walishuka watu wengi. Mtu wa kumi na sita kushuka katika ndege hiyo alivuta umakini wa watu sita waliokuwa sehemu ya kupaki magari.

"Ni yule pale" Jamaa mmoja kati ya wale sita alimuonesha kwa kidole yule kijana aliyekuwa anashuka ngazi za ndege za shirika la ndege la Algeria.

"Dalton usitoe macho yako kwa jamaa. Ukipepesa macho tu tumemkosa. Ni mjanja sana. Tutakuwa tukiwasiliana kupitia hivi vifaa vya masikioni. Nitasikia kila unachosema, nami utanisikia pia" Yule jamaa alisema.

"Usiwe na hofu Faustine. Ye si mjanja sasa amekutana na macho ya nyoka. Naenda nae ng'adu kwa ng'adu" Dalton alisema.
 
SEHEMU YA 33

"Sasa sisi tunaenda kwenye gari" Alisema Faustine. " Dalton kuwa makini makini sana. Daniel ni mtu hatari sana, hatari kuliko hilo neno hatari linavyomaanisha. Ukifanya kosa tu utalijutia milele"

"Faustine inamaana huniamini leo. Tumefanya kazi ngapi za hatari na wewe kwa ufanisi mkubwa." Dalton alisema.

Faustine na wenzake waliekekea kwenye gari. Wakimuacha Dalton akimfatilia Daniel Mwaseba.

Daniel Mwaseba alishuka ndegeni. Moja kwa moja alienda mahali wanapopaki teksi na kupanda.

"Naomba unipeleke Kawe. Sijui ni shilingi ngapi?" Daniel aliuliza.

"Elfu sitini tu boss" Dereva teksi alisema..

"Ok lets go. Haina shida" Daniel alisema huku akikaa vizuri kitini.

Gari ilianza safari kuelekea Kawe. Ndani ya gari kulikuwa kimya hakuna aliyekuwa anamuongelesha mwenzake.

"Tunafatiliwa" Daniel alisema walipofika njia panda ya Segerea.

"Umesema tunafatiliwa? Na nani?" Dereva teksi aliuliza.

"Kuna gari na pikipiki zinatufatiliwa. Sijajua nia yao ni nini lakini inaonesha si watu wema" Daniel Mwaseba alisema kwa sauti yake ya upole.

"Ni majambazi. Itakuwa majambazi" Dereva teksi alisema kwa uwoga.

"Usiogope. Naamini wewe ni dereva wa mjini. Hebu waoneshe kama wewe ni dereva wa mjini. Nataka tuwapoteze wasituone" Daniel alisema.

"Hilo tu. Funga mkanda wako vizuri. Naitwa Andrea." Dereva teksi alisema huku akiongeza kasi gari.

Jamaa alikimbiza gari vibaya sana. Lakini wakina Dalton nao walikuwa ni watoto wa mjini, nao walienda nao sambamba.

"Hiki kitu kipya. Naingia tu jijini Dar es salaam naanza kufukuzwa. Inavyoonesha kuna watu walikuwa wanajua ujio wangu wa leo. Nani kawaambia wakati nchi nzima wanajua nina likizo ya mwezi mmoja nje ya nchi, ni mimi tu mwenyewe nimeamua kurudi mapema baada ya kupokea e-mail kutoka kwa

Mheshimiwa Dr Joseph" Daniel Mwaseba alikuwa anawaza wakati gari lao likikatiza mataa ya TAZARA.

"Unaiweza michezo hatari Andrea. Ulivyopita pale junction wakati taa zetu haziruhusu wewe jamaa kiboko. Ona tumewaacha palepale wakisubiri taa ya kijani iwake" Daniel alisema.

"Nina miaka mitatu tu katika kazi hii. Kwa sasa nina miaka thelathini na tatu. Nimetumia zaidi ya miaka ishirini katika kazi hizi za kufukuzana" Andrea alisema huku akiendesha gari kwa mkono mmoja.

"Ulikuwa unafanya kazi gani kabla haujawa tax driver?" Daniel aliuliza.

"Nilikuwa jambazi wa kuogopwa hapa jijini. Nimefanya matukio mengi sana hapa mjini. Katika tukio la kuibiwa benki gani ambayo Andrea hahusiki? Hakuna. Lakini baadae nikaona niachane na matukio yale mabaya na kuwa dereva teksi. Ingawa napata kipato kidogo lakini naridhika"

"Hiyo nzuri sana Andrea. Crime does not pay." Alisema Daniel. " Haaa anakuja, yule dereva pikipiki bado anakuja!!" Daniel alisema baada ya kuangalia side mirror"

"Ngoja nimuoneshe kazi" Andrea alisema kwa kujiamini.

***
 
SEHEMU YA 34

Ngoja nimuoneshe kazi" Andrea alisema kwa kujiamini.

***

Katika chumba kidogo kilichokuwa mtaa wa Sabasaba Mafinga walikuwa wamefungwa watu watatu.

Kulikuwa na Mwanasheria mlevi aliyekuwa amefungwa madhubuti katika kona moja ya hicho chumba. Kona nyingine alifungwa Dokta Yusha na katikati ya chumba alikuwa amefungwa mwanadada Elizabeth

Neville.

Chumba kulikuwa kiza totoro si mchana si usiku. Kila muda wa kula ulipofika walikuwa wanapewa mkong'oto wa nguvu kisha ndio wanapewa chakula. Saa kadhaa tu walizokaa mle ndani walikuwa wamechakaa haswa. Pamoja na mateso yote hayo hakuna aliyesema chochote kwa kila wakichoulizwa, wote walikuwa masugu. Hali hiyo ilizidi kuwatia hasira wakina Felix na Sam.

"Tutafanya nini sasa jamani. Majamaa wamezidi kuwa wagumu, tutumie njia gani ili tufanikiwe. Maana bila boss kugairi kuja baada ya kupanda cheo sijui tungemwambia nini? Tuna Elizabeth Neville siku kadhaa sasa lakini hakuna lolote tunalolijua" Jamaa mwembamba alisema.

"Tunamjua vizuri Elizabeth Neville ni nani?. Lakini hatuwajui hawa wengine wawili ni nani? Hatumjui huyu aliyekamatwa huko Mbeya ni nani? Na huyu aliyetuvamia jana usiku kule sabasaba pia hatumjui. Mi naona tutumie njia yoyote ile ili kutambua hawa jamaa ni wakina nani na wana lengo gani kwetu. Tukishajua tutajua way forward cha kufanya. Kwakuwa wao wamekataa kuongea lolote kwa midomo yao mi naona tuchunguze simu zao na email zao. Tutajua watu wanaowasiliana nao na mipango. Tukitoka hapo tutajua what to do" Richard alisema kwa kirefu.

"Good idea Richard. Your a brilliant boy, nakuamini sana. Zungu kachukue simu zao zipo chumbani kwangu tufanye kama alivyoshauri Richard" Mtu mfupi mnene alisema.

Zungu alitoka na kuelekea chumbani kwa mtu mfupi mnene kuchukua simu za wakina Dokta Yusha. Dakika moja na nusu baadae alirudi tena pale ukumbini akiwa na simu mbili.

"Zimezimwa zote" Zungu alisema.

"Ziwashe" Mtu mfupi mnene alisema.

Zungu aliziwasha simu. Moja akiwa kaishika kwa mkono wa kulia na nyingine kwa mkono wa kushoto. Zikawaka.

"Zinahitaji namba za siri ili zifunguke" Zungu akasema.

"Zilete hapa. Nitazifungua" Richard alisema.

Simu zote akapewa Richard ili azifungue. Alitumia dakika saba kuifungua simu ya Dokta Yusha na dakika kumi na tatu kuifungua simu ya Mwanasheria mlevi.

"Huyu mmoja ni mjanja sana. Sijawahi kutumia muda mrefu namna hii kufungua simu, dakika kumi na tatu?" Richard alisema.

Mara simu zikanza kuingia meseji mfululizo. Richard aliziweka mezani akizishuhudia jinsi zilivyokuwa zinashindana kuingia meseji.

Zilivyotulia. Kulikuwa na meseji kumi na moja katika simu zote mbili.

"Simu zote zina idadi sawa ya Meseji!! Richard alisema.
 
SEHEMU YA 35

Richard akazibofya zote na kusema " Meseji zote zinatoka kwa mtu mmoja. Maajabu hawa watu wawili wanajuana. Cha ajabu mmoja kaletwa kutoka Mbeya na mwengine tumemkamata hapa Mafinga but those wametumwa na mtu mmoja ambao wote katika simu zao wamemsave kama Chifu. Huyo Chifu ni nani?" Richard alisema.

"Tumepiga hatua kubwa sana. Sasa inabidi tuwajue zaidi hawa watu. Na tumjue huyo Chifu ni nani? Na tujue uhusiano wa hawa watu wawili ni upi?" Felix alisema.

"Huyu jamaa mwengine hajalog out upande wa e-mail" Richard alisema kwa furaha. " Kuna email nane katika simu yake. Na zote zinatoka kwa mtu mmoja mwenye email mimi@yahoo.com. Na email zote nane zinafanana zina maneno mawili tu. Nakuja kesho. Ila zimetumwa juzi. So inavyoonesha ameshaingia huyu jamaa anayejiita mimi" Richard alisema.

"Swali lengine kwetu ni Mimi ni nani? Je anahusika katika upelelezi wa hawa jamaa kwetu? Felix aliuliza.

" Kingine Felix katika orodha ya namba ya huyu mwengine kuna mtu kamsave kwa jina la Mimi. So Mimi ni mtu ingawa hatumjui. Na bila shaka Mimi yupo mjini hapa" Richard alisema.

"Je kwa huyo mwengine hakuna mtu aliyemsave kwa jina Mimi" Mtu mfupi mnene aliuliza.

"Ngoja niangalie" Richard alisema huku akiipekua simu ya Mwanasheria mlevi.

"Mmh mimi hamna lakini kuna mtu kamsave kwa jina la Me. Ngoja nizifananishe hizi namba" Richard alisema huku akiishika na simu ya Dokta Yusha. "Oooh its the same number. Mimi ni Me ni mtu mmoja. Namba zao ni sawa" Richard alisema.

"Hebu zicheck hizo namba za Mimi kwenye mtandao wa simu zinasoma jina gani?" Felix aliuliza.

"Ngoja niangalie hapa, wazo zuri Felix. Ngoja nimtigopesa"

Richard alichukua simu yake na kujaribu kuitumia pesa ile namba.

"Weeeeeeeee unajua inasoma jina ganiiiii? Richard alisema kwa nguvu akiwa amesimama wima.

" Jina gani?" Felix aliuliza.

"ELIZABETH NEVILLE!!!" Richard alisema kwa sauti kuu.

"Mimi au Me ambaye alikuja jana ni Elizabeth Neville. Elizabeth si tunaye sisi. Huyo ni Elizabeth Neville gani tena? Inamaana huyu siye Elizabeth Neville wa kweli?" Felix aliuliza.

"Haya mambo yanachanganya sana. Kuna kitu kimejificha kati ya watu wale watatu. Halafu wanajifanya hawajuani kabisa mle chumbani kumbe ni waongo" Mtu mfupi mnene alisema.

"Tumegundua mambo muhimu sana. Kwa sasa lazima tuwe makini nao sana. Pia lazima tuhakikishe kama yule ni Elizabeth Neville kweli. Maana imeshakuwa utata" Mtu mwembamba alisema.

"Felix naomba tukawabane wale jamaa watwambie kuhusu huu utata. Tukiamua tunaweza" Richard alisema.
 
SEHEMU YA 36

"Sio kwa watu wale Richard. Jamaa ni masugu, viburi na jeuri. Sio rahisi hata kidogo kama unavyofikiria" Felix alisema.

"We twende that job niachie mimi. Nitajua nafanya nini ili waseme. Nishakutana na watu wabishi ambao wale hawafikii hata nusu. Kama hufahamu mimi ni yule niliyemfanya Malkia alie. Iam a monster mimi nikiwa kazini na nimeletwa hapa kwa kazi hiyo" Richard alisema.

"Twende ukajionee mwenyewe. Maana naona huelewi ninachokwambia" Felix alisema huku akinyanyuka kutoka kitini.

Na Richard nae aliamka kumfuata nyuma Felix.

"Naitwa Daniel Mwaseba" Daniel alianza kujitambulisha kwa dereva teksi Andrea. Andrea umenisaidia sana hadi kuwatoroka wake jamaa. Ni dereva mahiri sana wewe" Daniel alisema.

"Huna haja ya kujitambulisha. Mjanja gani wa mjini asiyekujua Daniel Mwaseba. Nilikuwa napenda sana kusoma majarida ya kijasusi kutokana na kazi yangu ya zamani ya ujambazi. Huko ndipo nilipokutana na habari za kushangaza kuhusu wewe. Nilienda mbali zaidi na kukusoma, ukweli nilikuhusudu sana. Katika fukuafukua zangu ndipo nilipofanikiwa kuipata picha yako" Andrea alisema.

"Picha!! Uliipata wapi picha yangu? Watanzania wengi wanazijua sifa zangu kwa kuzisoma tu magazetini na vitabuni. Humo mote haijawahi kuwekwa picha yangu kwa sababu za kiusalama. Daniel Mwaseba hatakiwi kujulikana hovyo" Daniel alisema.

"Nilikuwa interested na mambo yako hivyo nilipiga hatua moja mbele kutaka kuona mwonekano wako. Siku ya kwanza kuiona picha yako nilishangaa sana. Jamaa ni una sura ya upole wewe unazishinda hadi sifa wakusifiazo katika vitabu vyao" Andrea alimsifia Daniel.

"Vipi nikikwambia kwamba uliiona picha yangu ulipokuwa Korea Kaskazini ulipotumwa

kwenda kuchunguza mpango wa siri uliopangwa na nchi hiyo kujaribu kombora lao moja kulipua jiji la Tanga?. Unajisikiaje kudanganya wakati mimi nimekwambia ukweli. Najua hatujakutana kwa bahati mbaya. Umetumwa na Rais Dr Joseph, kuja kunipokea uwanja wa ndege. Umejitahidi kubadili mwonekano wako, lakini still huwezi kuyalaghai macho na masikio ya Daniel Mwaseba" Wakati Daniel akiendelea kuongea Andrea alimziba mdomo.

"Ishia hapohapo. Haki ya Mungu Daniel we ni hatari sana. Sifa wakupazo hazitoshi hata kidogo. We ni zaidi ya mpelelezi, we ni zaidi ya jasusi. Nimefanya kazi na wewe mara kadhaa lakini kila siku unaonekana unazidi kuwa..." Safari hii alizibwa yeye mdomo.

"Acha mbwembwe Inspekta Jasmin. Unanibadilishia sauti mimi" Daniel alisema huku akitabasamu. "Sifa zote za nini? Hebu nambie kuna salamu gani kutoka kwa Dr Joseph" Daniel alisema.

"Daniel acha utani bwana unajifanya humjui Elizabeth Neville. Acha kunifanya mtoto mdogo. Najua unamjua Elizabeth Neville kuliko mtu yeyote yule hapa duniani. Unamjua nje, unamjua ndani. Labda nikuulize wewe, Elizabeth Neville yupo wapi?" Inspekta Jasmin alitupa swali
 
SEHEMU YA 37

.

"Hahaha mwanamke una wivu wewe, we wa nini Elizabeth Neville?" Daniel aliuliza.

"Elizabeth Neville ndio chanzo cha yote haya. Wakati tunasaka ni nani aliyebadili nyaraka kwa John

Rondo. Lazima tumtafute Elizabeth Neville"

"Very easy task. Tuingie kazini sasahivi" Daniel alisema.

"Tunaanzia wapi?" Inspekta Jasmin aliuliza.

"Makao makuu ya Polisi katika ofisi iliyokuwa ya John Rondo. Kisha nyumbani kwake. Tutapata kitu tu huko" Daniel alisema.

"Je una idea yoyote juu ya wale watu waliokuwa wanatufuata?" Inspekta Jasmin aliuliza.

"Sijui, ila tutajua tu. Najua hawatakoma kutufuata" Daniel alisema.

"Ngoja nikabadili huu mwonekano wa kiume wa Andrea. Sasa nataka niwe mtoto wa kike, Jasmin Wahab" Inspekta Jasmin alisema kwa sauti yake ya kike huku akienda ndani kubadili nguo.

Dakika sita baadae Inspekta Jasmin alitoka. " Huyo ndiye wewe, mtoto mzuri mrembo"

"Lakini simshindi Elizabeth Neville" Inspekta Jasmin alimalizia.

Daniel Mwaseba alikaa kimya.

Safari ya kuelekea makao makuu ya Polisi ilianza.

Iliwachukua saa moja na dakika kumi mpaka Daniel Mwaseba na Inspekta Jasmin wafike katika makao makuu ya Polisi.

"Jasmin tangulia mbele mimi nitakuwa nyuma yako nikikupa ulinzi. Elekea moja kwa moja zilipokuwa ofisi za John Rondo. Ukifika katika meza ya katibu mahsusi nisubiri. Hiki weka sikioni tutakuwa tukiwasiliana wakati tukiwa tunapanda. Take care mtoto mrembo" Daniel alimwelekeza Jasmin ambaye aliitikia kwa kichwa huku akiweka kifaa kidogo sikioni.

Moja kwa moja Jasmin aliongoza kuelekea ofisi ya IGP ambayo kwa sasa ilikuwa chini ya IGP Zaidi Kalinga baada ya John Rondo kutimuliwa kazi na Rais Dr Joseph.

Nyuma ya Inspekta Jasmin, kama hatua kumi na tano Daniel Mwaseba alikuwa anamfata kwa umakini mkubwa huku akiangalia pande zote. Alikuwa makini na kila hatua aliyokuwa anapiga. Jasmin ndio alikuwa wa kwanza kufika katika mlango ambako ndipo kulikuwa na ukaguzi. Jasmin alikuwa hakaguliwi kwa kuwa alikuwa anajulikana. Lakini leo hii hakupita hivihivi.

Alikaguliwa.

"Nani mwenzangu? Waenda ofisi ya nani?" Askari anayemkuta kila siku leo hii alimuuliza jina.

"Jasmin Wahab. Naenda ofisi ya kaimu IGP Zaidi Kalinga" Jasmin alijibu huku akijifanya ana haraka.

"Tulia binti. Hakuna mtu katika ofisi ya IGP" Jamaa alijibu.

"Nitaenda kumsubiri hukohuko. Naomba niruhusu" Jasmin aliomba.

"Hairuhusiwi. Wanaoenda juu wote tumeambiwa lazima wawe na kibali kutoka kwa afande Fanuel Mwalembe" Askari alisema.

"Mcheleweshe hivyohivyo, mi nitapita kwa siri" Kile kifaa cha sikioni kiliongea. Alikuwa ni Daniel Mwaseba.

"Nipe namba ya afande Fanuel basi" Jasmin alisema.

Yule askari aliangalia kwenye simu yake na kumpa Jasmin namba ya afande Fanuel. Kwa makusudi Jasmin akabadilisha namba ya mwisho. Alipiga simu kisha akaweka loud speaker. Namba ilikuwa haipatikani.
 
SEHEMU YA 38

"Mbona haipatikani sasa. Niruhusu tu niende. Sitokawia" Jasmin alisema.

"Ni kosa kutotii amri za viongozi. Siwezi kutotii agizo la afande Fanuel" Yule askari alisema.

"Nishapita naelekea katika ofisi ya IGP Kalinga. Huyo achana nae rudi kwenye gari yetu haraka" Sauti ilipenya katika kifaa kilichokuwa sikioni kwa Jasmin.

"Sawa bwana mimi naenda" Jasmin alisema huku akitoka nje.

Alipofika nje aliliangalia gari lao. Lilikuwa limepaki palepale. Alipoliangalia vizuri alimwona mtu chini ya uvungu wa gari yao.

"Kuna mtu uvunguni mwa gari yetu" Alisema Jasmin.

"Mchunguze anafanya nini? Akitoka hakikisha hakupotei. Mimi ndo nahangaika kuufungua mlango wa ofisi ya IGP" Daniel alisema.

Jamaa kule uvunguni alitumia kama dakika moja. Kisha kwa ufundi mkubwa alijibiringisha na kutoka kule uvunguni. Harakaharaka alisimama na kuelekea upande wa pili wa barabara. Kule kulikuwa na gari alifungua mlango wa nyuma na kuingia.

"Kumbe ni wale jamaa waliotufuata kule uwanja wa ndege. Wapo katika gari ileile" Jasmin alisema.

"Itakuwa wamekuona hapo mlangoni kama walikuwa wamepaki sehemu. Rudi tena ndani kuwapoteza maboya" Daniel alisema.

"Sawa Daniel vipi wewe huko?" Jasmin aliuliza.

"Nipo ndani ya ofisi ya kaimu IGP Kalinga. Nimeikuta laptop ndogo hii nitaibeba tutaenda kuichunguza home" Daniel alisema.

"Kuwa makini wewe mwanaume" Jasmin alisema kwa upole.

Ilichukua dakika tano. Jasmin akimsubiri Daniel pale mapokezi.

"Toka nje, tayari nishatoka" Jasmin alisikia katika kile kifaa.

"Hee umepita wapi Daniel mbona sijakuona?" Jasmin aliuliza.

Daniel alikaa kimya.

Jasmin alitoka nje na kumwona Daniel amesimama karibu na kibanda cha walinzi akiwa kabeba begi dogo mkononi.

"Gari yenyewe ni ile kule ya njano?" Daniel aliuliza.

"Ndio" Jasmin alijibu akiwa anaelekea upande aliosimama Daniel.

"Haitakiwi kupanda gari hapa. Si salama kwetu. Wale jamaa watakuwa wanatuangalia inabidi tuwapige chenga kisha tuanze kuwafatilia sisi" Daniel alisema.

"Wewe elekea upande wa kulia. Mimi naelekea upande wa kushoto. Tuone watamfata nani? Wakija kwako nitawafata nyumanyuma kisha tutawashambulia wakija kwako hivyohivyo. Watakuwa katika..."

Jasmin hakumaliza alichotaka kusema. Ulisikika mripuko mkubwa sana. Gari walilokuja nalo wakina Daniel lilirushwa juu huku likipasuka vipandevipande. Magari mengine yaliyokuwa pembeni nayo yalishika moto na kuanza kuungua. Eneo lote la parking ya jeshi la polisi ilikuwa moto mtupu.

"Wanakimbiaaa!!" Jasmin alisema kwa nguvu.

Daniel aliangalia ule upande wa pili wa barabara lile gari la njano ndo lilikuwa linaondoka.

"Ama zao, ama zetu" Daniel alisema kwa sauti ndogo.

Pembeni kulikuwa na pikipiki aina ya boksa ikiwa na dereva juu yake. Daniel alimvuta yule dereva na kumuangusha chini. Alipanda yeye juu ya pikipiki na kuifukuzia ile gari ya njano.
 
SEHEMU YA 39

"Chukua hilo begi lenye laptop kalihifadhi home" Daniel alimwambia Jasmin katika kile kifaa.

"Nimekusoma. Nimekusoma" Jasmin alijibu.

Gari ya njano ilikata kushoto, ndani ya gari walikuwa wanalaumiana wenyewe. Kwa mara nyingine tena walikuwa wameshindwa kumuua Daniel Mwaseba.

"Sasa tutamwambia nini Boss Sam. Katupa nafasi nyingine tena ili tuumalize mchezo tumeshindwa" Dalton alisema.

"Daniel sio kiumbe wa kawaida yule. Sasa kitu gani kilichomfanya asiingie ndani ya gari na kuanza kuzungukazunguka. Kapoteza muda hadi muda tuliouseti lile bomu umeisha na kulipuka" Jamaa mwengine alisema.

"Sasa what is our next plan. Mara ya pili tumeshindwa kumuua Daniel Mwaseba kwa leo. Inabidi tumtaim kwa mara ya tatu ambayo tuhakikishe tunaondoka na roho yake" Dereva naye alishauri.

"Tumdungue tu kwa risasi tuumalize mchezo. Ahhh lakini tatizo sasa Bosi Sam anataka tumpeleke kwake akiwa hai. Hapo ndo pagumu lakini kama ingekuwa ni kumuua tu sahivi tungekuwa tunaongelea habari zingine" Dalton alisema.

"Kumtega Daniel kama ndege mkiwa sio jambo la kitoto. Yatupasa kufanya kazi" Dereva alisema.

Daniel akiwa juu ya pikipiki aliikaribia kabisa ile gari ya njano. Akawa yupo nyuma yake wakati gari likiwa mitaa ya faya. Zilipofika mataa gari zote zikasimama. Hiyo ndiyo nafasi pekee akiyoihitaji Daniel. Aliweka pikipiki pembeni na kuifata ile gari ya njano. Akachomoa kisu mfukoni, aliikaribia kabisa ile gari. Alilichoma kwa nguvu tairi la nyuma la gari lile. Gari lilitoa mlio uliomstua kila mtu.

"Nini hiko?" Ndani ya gari Dalton aliuliza.

"Itakuwa pancha" Dereva alisema huku akijishughulisha kufungua mlango. Alitanguliza mguu wa kulia mbele. Alikutana nayo. Risasi ilitua katika mguu wake. Damu zilimwagika!! Alitoa ukelele huku akianguka chini. Alikuwa hajiwezi.

"Wamemdungua!!" Dalton alisema ndani ya gari.

"Tunafanyaje sasa?. Gari haiwezi kuondoka na kutoka nje ni kujianika ili tupigwe risasiii !!!" Jamaa mmoja aliongea kwa pupa.

Mara risasi zikaanza kuvurumishwa katika gari yao. Wote waliinama vichwa chini. Risasi zilirindima bila kujua adui yupo upande gani.

"Inameni hivyohivyo. Kila mmoja aweke bastola yake stand by tutashambulia kwa pamoja" Dalton alisema.

"Wale jamaa wawili walifanya kama walivyoagizwa.

" King tambaa hadi kwa dereva jaribu kuliondoa gari hivyohivyo. Tupo katika hatari na hatujui risasi zitakoma muda gani, tusije kukamatwa hapahapa"Dalton alisema.

King akasogea kwa kutambaa hadi katika kiti cha dereva. Alifunga mlango ambao uliachwa wazi na yule dereva wa awali. King akazungusha funguo, gari likawaka, akatia moto ili gari liondoke. Halikusogea. Daniel Mwaseba alikuwa amepasua tairi zote nne.

"Limekuwa zi..." King hakumakizia alichotaka kusema. Risasi ilitua juu kidogo ya sikio lake la kulia. Hakuomba hata maji. Alilalia usukani akiwa mfu. Sasa walibaki wawili ndani ya gari wakiwa wamejisweka chini ya viti. Risasi mfululizo zikielekezwa katika gari yao.
 
SEHEMU YA 40

"Mpigie boss Sam" Yule jamaa alishauri.

Harakaharaka Dalton alichukua simu yake na kumpigia boss Sam. Simu iliita tu haikupokelewa. Akapiga tena. Safari hii ilipokelewa. Bila salamu Dalton alilia simuni.

"Sam tunashambuliwa na askari polisi. Tupo mataa ya Faya hapa. Dakika yoyote tunauwawa. King na Dereva tayari washauwawa!!"

Sam akakata simu " Bullshit amekata simu pumbavu. Tupambane wenyewe kujiokoa"

Wakina Dalton walikaa tayari kwa lolote. " We shambulia upande wa kushoto mi nashambulia upande wa kulia. Piga mtu yeyote yule awe askari ama raia, we piga tu!!" Dalton alisema.

"Niko sawa" Jamaa alijibu.

Ghafla risasi zilikoma. Wakina Dalton wakapumua. "Wameacha kutushambulia. Ila tufanye kama tulivyopanga" Dalton alisema.

***





SEHEMU YA 8

Ghafla risasi zilikoma. Wakina Dalton wakapumua. "Wameacha kutushambulia. Ila tufanye kama tulivyopanga" Dalton alisema.

***

Richard na Felix walifika katika chumba walichofungiwa wakina Elizabeth Neville. Waliingia chumbani kukiwa kimya kabisa. Mateka wote watatu wakiwa wamefungiwa katika viti ambavyo havikuruhusu kujisogeza hata kidogo. Richard alisimama mlangoni akitanguliwa na Felix. Felix akiwa amefura kwa hasira.

"Naitwa Richard" Richard alisema akimtambuka Felix pale mlangoni. "Nimekuja hapa ili tuongee kistaarabu. Sitaki tuumizane" Richard alisema huku akimsogelea Elizabeth Neville.

"Felix, niachie nafasi ya kuongea na mmojammoja, nitaanza na huyu, kisha yule na nitamalizana na

Elizabeth Neville" Richard alisema. "Hawa watoeni nje kwanza"

Felix alibonyaza swichi ukutani. Dakika moja baadae wakaja walinzi wawili. Felix aliongea nao.

Mwanasheria mlevi na Elizabeth Neville walitolewa nje. Mle ndani alibaki Richard, Felix na Dokta Yusha.

"Ndugu yangu nasikia u mgumu kidogo kuongea. Lakini uligoma kwa Felix sio kwa Richard. Nilikwambia naitwa Richard na ni kweli naitwa hivyo. Sasa ninaomba ujibu kila ninachokuuliza. Ninaomba kwakuwa nakuonea huruma sana endapo hautosema nitakufanya kitu kibaya sana. Mimi sitaki tufike huko kwakuwa wewe unaonesha u rafiki mzuri sana. Swali langu la kwanza ni hili" Richard alimtazama yule jamaa kisha akatikisa kichwa kusikitika.

"Unaitwa nani?" Richard alidondosha swali. Lilikuwa swali rahisi sana pengine kuliko yote duniani lakini pamoja na urahisi wake Dokta Yusha hakujibu.

"Nimekuuliza unaitwa nani?" Richard alirudia tena swali. Dokta Yusha alimwangalia tu Richard hakusema chochote.

"Kwa mara ya tatu nakuuliza unaitwa nani?" Richard aliuliza huku akimsogelea Dokta Yusha.

Bado Dokta Yusha alikaa kimya. Alikaa tu pale kitini akiwa hana wasiwasi wowote.

"Lile si jiko la umeme Felix?" Richard alimuuliza Felix huku akilionesha jiko lilikuwa pembeni mwa chumba kile.

"Ndio" Felix alijibu.

"Niletee kisu kikubwa kidogo" Akasema Richard.

Felix alitoka nje akiwaacha mle ndani watu wawili tu. Richard na Dokta Yusha.

"Utasema brother" Richard alisema kwa kujiamini.
 
SEHEMU YA 41

Mara Felix aliingia na kisu mkononi.

"Washa ile swichi pale jiko lipate moto" Richard alisema huku Felix alitelekeza.

Dakika chache tu jiko lilishika moto.

"Liko fresh jiko" Felix alisema.

"Weka kisu hapo juu ya jiko" Richard alisema.

Felix alifanya kama alivyoagizwa. Kisu kilianza kushika moto taratibu. Dakika kumi baadae kisu kilikuwa chekundu, kimeshika moto hasa.

"Mfunge pingu mikono na miguu" Richard akasema.

Felix alienda kwenye kabati lililokuwemo mle chumbani na kutoa pingu mbili. Moja alimfunga mikono na nyingine miguuni.

"Mfungue huo mkanda uliombana hapo kwenye kiti" Richard alisema. Na Felix alifanya kama alivyoagizwa. Dokta Yusha sasa akawa huru ingawa alikuwa amefungwa miguu na mikono kwa pingu.

"Mvue hizo nguo" Richard akasema.

Felix akasita kidogo. Alimwangalia Richard kwa mshangao.

"Mvue hizo nguo zote" Richard alirudia tena kwa sauti ya upole.

Safari hii Felix alitekeleza. Alimvua nguo zote ingawa kwa kuzichana maana zilikuwa zinashindwa kupita kwenye zile pingu. Dokta Yusha akabaki uchi, uchi wa mnyama akiwa na pingu zake.

"Unaitwa nani ndugu?" Richard alirudia tena swali.

Bado Dokta Yusha alikaa kimya.

"Lete hiko kisu Felix" Richard akasema.

Felix alikitoa kile kisu pale jikoni. Kisu kilizidi kuwa chekundu. Akampa Richard.

"Ninakutoa uzazi jamaa yangu. Si umejifanya jeuri nakukata uume leo!!" Richard aliongea akiwa anamaanisha.

"Msimamishe vizuri Felix. Huyu hanijui mimi. Namkata uume serious. Atanijua mimi leo kuwa ni kichaa" Richard alisema.

Felix alimsimamisha Dokta Yusha. Kwa mara ya kwanza Dokta Yusha alianza kutetemeka. Katika adhabu zote hii hakuitegemea.

Kule katika chumba walichofungiwa wakina Elizabeth Neville waliona kila kitu kupitia kwenye runinga.

"Dokta Yusha anaogopa" Mwanasheria mlevi alisema kwa sauti ndogo.

"Lazima aogope, huyu Richard ni mwendawazimu. Atamkata kweli uume" Elizabeth Neville alisema.

"Daaah tumekwisha" Mwanasheria mlevi alisema akiwa amekata tamaa.

"Naomba nikwambie kitu kaka. Maana wewe ni mtu pekee ninayeweza kumwambia kitu nikiwa katika safari ya kifo. Naziona dalili zote kwamba ninaenda kufa leo. Naomba nikwambie siri hii endapo utafanikiwa kutoka hai uipeleke sehemu" Elizabeth Neville alisema.

"Huwezi kufa, ninaamini tutatoka salama" Mwanasheria mlevi alisema.

Elizabeth Neville hakutaka kuyasikiliza maneno ya kutia moyo ya yule jamaa. Alidhamiria kumwambia siri ambayo hakuwa tayari kuitoa nje siku zote. Alidhamiria kumwambia mtu mmoja tu ambaye hakuwa na uhakika kama watakutana.

"Siri yangu ni kwamba..." Elizabeth Neville alianza kusema.

"Nooooo! Usinambie hiyo siriiii" Mwanasheria mlevi alipiga kelele.

"Kwanini nisikwambie? Wewe ni mtu pekee niliyotokea kukuamini. Naomba nikwambie na uyafanyie kazi nikwambiayo. Naona maisha yangu hayana muendelezo. Siwezi kuvumilia maumivu ya kile kisu cha moto. Am going to die today" Elizabeth Neville alisema kwa uchungu.
 
SEHEMU YA 42

"Usinambie Elizabeth. Usinambie hiyo siri sina haja ya kuijua. Don't tell me Elizabeth" Mwanasheria mlevi alisema kwa nguvu.

"Wewe ni mtu wa ajabu miongoni mwa watu wa ajabu. Nataka nikwambie kitu ambacho kila mtu anataka kujua. Nataka nikwambie kuhusu 001. Kubali nikwambie ili ujue utafanya nini?. Nitakuwa nimefanya dhambi kubwa sana endapo nikifa bila kumwambia mtu kuhusu 001. Sikili..." Elizabeth Neville alitaka kusema lakini Mwanasheria mlevi alimkatisha.

"Don't tell my sister pleeease. Don't tell meeee" Alisema kwa nguvu Mwanasheria.

Katika chumba kingine kilichokuwa na watu wawili katika nyumba hiyohiyo kulikuwa na taharuki. Watu hao walikuwa mbele ya kompyuta zao huku wakiwaangalia Elizabeth na yule jamaa. Mwanzoni sura zao zilikuwa zimejawa na furaha pale Elizabeth alipokuwa tayari kutoa siri kabla ya yule kijana kukataa kuambiwa hiyo siri.

"Huyu jamaa anazingua. Tulikuwa tunaimaliza kazi hii leo. Elizabeth Neville alikuwa tayari kutoa siri kuhusu 001 ila huyu jamaa katurudisha nyuma.

"Sasa tufanyaje. Naona na mpango huu unaelekea kufeli" Zungu alisema.

"Elizabeth Neville apelekwe katika chumba cha mateso akakutane na Richard, nahisi leo atasema kila kitu. Ameingiwa na uwoga kuona kile anachotaka kufanywa mwenzie. Mpeleke kule leo atatapika" Sam aliamrisha.

Simu ikapigwa kule chumba cha mateso. Felix naye akapiga kwa walinzi wakiowalinda wakina Elizabeth Neville. Harakaharaka Elizabeth alitolewa katika kile chumba na kupelekwa katika chumba cha mateso. Na Dokta Yusha akarudishwa kule katika chumba cha awali.

"Aisee that man is monster. Na ujanja wangu wote leo mkojo umenitoka. Ni nani yule Richard. Sura yake nzuri lakini inabadilika awapo kazini. Maneno yake hatanii, ananena atakacho kutenda. Alikuwa ananitumbua korodani leo!" Dokta Yusha alisema pindi tu alipopelekwa kile chumba kingine.

"Tumeona kila kitu. Tumeona ukivyotetemeka pindi alivyotaka kukufanya yule jamaa. Hata Elizabeth huku alikuwa anatetemeka. Akataka kunambia siri lakini nikakataa" Mwanasheria mlevi alisema.

"Hee! Kwanini umekataa sasa. Hiko ndio kitu tulichotumwa na Chifu. Tumeishi miezi kadhaa Mbeya kuisaka hiyo siri. Kwanini sasa umeikataa?"

"Nimekataa kwa sababu ya Camera hizo. Ningesema tu nikubali kuambiwa basi tungewarahisishia kazi hawa jamaa. Hawa nao bila shaka wanaisaka hiyo siri. Sikutaka kuwasaidia kwa namna hiyo" Mwanasheria mlevi alisema.

"Sasa Elizabeth kapelelekwa kule. Je hawezi kuisema hiyo siri baada ya kupewa mateso?" Dokta Yusha aliuliza.

"Ni suara la kuangalia mbele kwenye ile runinga tutapata jibu" Mwanasheria mlevi alisema.

Wote macho yao yalielekea mbele. Kushuhudia Richard akiwa amekutana na Elizabeth Neville. Kuona je atasema?"

***

ITAENDELEA

BURE SERIES
SIMULIZI
 
SEHEMU YA 42

"Usinambie Elizabeth. Usinambie hiyo siri sina haja ya kuijua. Don't tell me Elizabeth" Mwanasheria mlevi alisema kwa nguvu.

"Wewe ni mtu wa ajabu miongoni mwa watu wa ajabu. Nataka nikwambie kitu ambacho kila mtu anataka kujua. Nataka nikwambie kuhusu 001. Kubali nikwambie ili ujue utafanya nini?. Nitakuwa nimefanya dhambi kubwa sana endapo nikifa bila kumwambia mtu kuhusu 001. Sikili..." Elizabeth Neville alitaka kusema lakini Mwanasheria mlevi alimkatisha.

"Don't tell my sister pleeease. Don't tell meeee" Alisema kwa nguvu Mwanasheria.

Katika chumba kingine kilichokuwa na watu wawili katika nyumba hiyohiyo kulikuwa na taharuki. Watu hao walikuwa mbele ya kompyuta zao huku wakiwaangalia Elizabeth na yule jamaa. Mwanzoni sura zao zilikuwa zimejawa na furaha pale Elizabeth alipokuwa tayari kutoa siri kabla ya yule kijana kukataa kuambiwa hiyo siri.

"Huyu jamaa anazingua. Tulikuwa tunaimaliza kazi hii leo. Elizabeth Neville alikuwa tayari kutoa siri kuhusu 001 ila huyu jamaa katurudisha nyuma.

"Sasa tufanyaje. Naona na mpango huu unaelekea kufeli" Zungu alisema.

"Elizabeth Neville apelekwe katika chumba cha mateso akakutane na Richard, nahisi leo atasema kila kitu. Ameingiwa na uwoga kuona kile anachotaka kufanywa mwenzie. Mpeleke kule leo atatapika" Sam aliamrisha.

Simu ikapigwa kule chumba cha mateso. Felix naye akapiga kwa walinzi wakiowalinda wakina Elizabeth Neville. Harakaharaka Elizabeth alitolewa katika kile chumba na kupelekwa katika chumba cha mateso. Na Dokta Yusha akarudishwa kule katika chumba cha awali.

"Aisee that man is monster. Na ujanja wangu wote leo mkojo umenitoka. Ni nani yule Richard. Sura yake nzuri lakini inabadilika awapo kazini. Maneno yake hatanii, ananena atakacho kutenda. Alikuwa ananitumbua korodani leo!" Dokta Yusha alisema pindi tu alipopelekwa kile chumba kingine.

"Tumeona kila kitu. Tumeona ukivyotetemeka pindi alivyotaka kukufanya yule jamaa. Hata Elizabeth huku alikuwa anatetemeka. Akataka kunambia siri lakini nikakataa" Mwanasheria mlevi alisema.

"Hee! Kwanini umekataa sasa. Hiko ndio kitu tulichotumwa na Chifu. Tumeishi miezi kadhaa Mbeya kuisaka hiyo siri. Kwanini sasa umeikataa?"

"Nimekataa kwa sababu ya Camera hizo. Ningesema tu nikubali kuambiwa basi tungewarahisishia kazi hawa jamaa. Hawa nao bila shaka wanaisaka hiyo siri. Sikutaka kuwasaidia kwa namna hiyo" Mwanasheria mlevi alisema.

"Sasa Elizabeth kapelelekwa kule. Je hawezi kuisema hiyo siri baada ya kupewa mateso?" Dokta Yusha aliuliza.

"Ni suara la kuangalia mbele kwenye ile runinga tutapata jibu" Mwanasheria mlevi alisema.

Wote macho yao yalielekea mbele. Kushuhudia Richard akiwa amekutana na Elizabeth Neville. Kuona je atasema?"

***

ITAENDELEA

PSEUDEPIGRAPHAS
SIMULIZI
Aisee kitu kinazidi kuwa kitamu yani nasoma huku natamani isiishe
 
SEHEMU YA 43

Daniel Mwaseba alikuwa nyumbani kwake. Alikuwa amekaa kwenye sofa moja huku Jasmin akiwa katika sofa lengine.

"Vipi umewakosa wale jamaa?" Jasmin aliuliza.

"Yah, nilikuwa nimefanikiwa kuwadhibiti. Na askari wa pale mataa waliungana na mimi kunisaidia wakiamini wale ni majambazi. Tukiwa tunawashambulia ghafla askari mmoja alipigiwa simu na kupewa amri tuache kuwashambulia wale jamaa" Daniel alisema.

"Ha!! Mkaacha!!" Jasmin alishangaa.

"Askari hana ruhusa ya kupinga amri ya mkuu wake. Waliacha. Nilijaribu kuwatahadharisha kuwa wale watu ni hatari. Lakini hawakunielewa."

"Ni nani aliyewapigia simu hao askari?" Jasmin aliuliza.

"Kamanda wa Polisi wa Kinondoni. Tutamfuta baada ya kutoka hapa kujua kwanini alitoa hiyo amri. Sasa hivi tushughulikie hiyo kompyuta" Daniel Mwaseba alisema.

"Sawa Daniel "

Jasmin aliingia ndani na kurejea na laptop nyeusi aina ya Toshiba. Aliiwasha.

"Inahitaji password aisee.." Jasmin alisema.

"Hebu ilete hapa" Daniel alisema.

Akamsogezea ile laptop Daniel. Alitumia dakika tatu kubofyabofya na laptop ilifunguka.

"Shaabbaash kumbe nawe mtundumtundu"

Macho manne yalikuwa mbele ya laptop. Kila mmoja akiwa na kimuhemuhe cha kutaka kujua ni nini kilikuwepo kwenye ile laptop. Iliwachukua dakika ishirini kusoma kila kitu kilichokuwa katika ile laptop. Wote jasho liliwatoka kwa mambo mazito waliyoyasoma katika ile laptop.

"Sasa kumekucha" Daniel alisema. " lazima twende Mafinga kufumbua hili fumbo"

"Na hawa wahalifu je tunawaacha?" inspekta Jasmin aliuliza.

"Hao wote tutakutana nao Mafinga. Yaonesha mipango yao yote inafanyika huko. Bila shaka hata Elizabeth Neville atakuwa huko, lazima twende Mafinga leo" Daniel alisema kwa msisitizo.

"Ok Daniel, na tujiandae. Ila Zaidi Kalinga ni mtu mbaya sana!!" Jasmini alisema kwa hasira.

Saa mbili baadae Daniel Mwaseba na Inspekta Jasmin walikuwa ndani ya ndege ya Coastal aviation wakielekea Iringa, na hatimaye Mafinga. Kwenda kumsaka Elizabeth Neville na kufumbua fumbo la 001.

***

Elizabeth Neville alikuwa amekaa katika kiti mbele yake kukiwa na Richard. Sura ya Richard ikiwa imebadilika vibaya sana. Akiwa anatamani kumchakaza yule mwanamke ili aweze kumwambia kuhusu siri za Mheshimiwa Lucas na 001.

"Sina haja ya kujitambulisha" Richard alisema. " Lakini ukiwa na hamu ya kutaka kunijua mimi nani leo utanijua. Mimi ni katili kuliko katili yeyote yule unamyejua hapa duniani. Sina huruma na sijawahi kuwa na huruma tangu nizaliwe. Sina haja ya kukutisha maana utaona nitakachokufanyia, in short kitabaki katika kumbukumbu za maisha yako..."

"Usinitolee risala ndefu. Fanya unachotaka kufanya, sisemi chochote kile kwakuwa sijui chochote kile" Elizabeth Neville alijibu kwa hasira.

Richard hakuongea tena. Alienda kwenye kabati na kuchukua mkasi. Akaanza kuubonyaza bonyaza mithili anamnyoa mtu. Mkasi ulikuwa unatoa ukelele kila ukibonyazwa.

"Ninakata chuchu zako leo na kuyang'oa maziwa yako!!!" Richard alisema kwa ukali.
 
SEHEMU YA 44

Elizabeth Neville alikuwa anamwangalia Richard kwa sura ya nipo tayari kwa lolote. Richard alimsogelea taratibu, alipitisha mkasi kwenye ile blauzi aliyokuwa ameivaa Elizabeth. Akaivuta ile nguo na kumvuka. Elizabeth sasa alibaki kifua wazi, huku mwili wake mzuri ukitazamwa na macho mabaya ya Richard.

Kule ndani, Dokta Yusha na Mwanasheria mlevi walikuwa wanaangalia yote yake kwa macho ya kukata tamaa. Walijua ile ndio ulikuwa mwisho wa maisha yao. Waliamini kwamba baada ya Elizabeth kusema kila kitu, basi wao watauwawa sambamba na Elizabeth Neville kwakuwa watakuwa hawana thamani tena. Ulikuwa wakati mbaya sana kwao. Walishuhudia mkasi ulioshikwa na Richard ikielekea katika chuchu za Elizabeth Neville.

Ilikuwa balaa!!!

Sekunde hiyohiyo, Nje ya nyumba waliyokuwemo wakina Elizabeth Neville kulikuwa watu wawili wakiwa wanaizunguka nyumba hiyo. Martin Hisia na Binunu Issa walikuwa wamejiandaa kuivamia nyumba hiyo na kumuokoa Elizabeth Neville.

"Tunaelekea pale getini. Yatupasa tuwe sharp sana mana hawa watu ni hatari sana. Tuwe makini, kosa moja tu laweza kufelisha hii mission. Mipango yote ni kama tulivyopanga, naamini kwa asilimia 100 tunaenda kulifanikisha hili, nakuamini Binunu" Martin alisema.

"Nakuamini Martin" Binunu naye alijibu huku wakipeana mikono. Walitazama machoni, macho yao yalionesha matumaini makubwa.

Binunu alienda nyuma ya nyumba ile. Baada ya dakika tatu akarejea tena mbele.

"Tayari?" Martin aliuliza.

"Yap" Binunu alijibu kwa kifupi.

"Lets go" Martin alisema.

Walisogea taratibu kuelekea getini.

Ghafla!!! Mlipuko mkubwa ukasikika nyuma ya ile nyumba. Sekunde tatu baadae ulisikika mlipuko mwengine mkali zaidi. Moto mkubwa ukazuka ulioteketeza ukuta wa ile nyumba, muda uleule magari yaliyokuwa kule nyuma yamepaki yakashika ule moto. Ikaanza kutokea milipuko mikubwa sana. Kelele zikalipuka toka kwa majerani wa ile nyumba. Moto ulisambaa kwa kasi, ukidaka gari moja baada ya jingine. Harakaharaka wakina Martin walitoka pale getini. Baada ya kutoka tu dakika mbili mbele ulisikika mlipuko mkubwa sana pale getini. Walinzi ndani ya ile nyumba walichanganyikiwa. Hawakuelewa chanzo cha moto ule.

Kule ndani ya nyumba watu wote walikuwa wamepigwa na butwaa, hawakuelewa kabisa nini kimetokea. Hawakupata nafasi ya kutafakari. Ving'ora gari za Polisi vilikuwa vinasikika kwa nguvu kuelekea pale. Martin Hisia na Binunu walipishana na ile gari wakiwa wanarejea mjini. Walikuwa wameacha tafrani isiyo na kipimo huko Sabasaba.

"Polisiii!! Polisiiiii wanakujaa" mtu mwembamba mrefu alipiga kelele.

"Wote kimbilia chumba namba moja" Festo alisema.

Ndani zikawa pilipilika za kuelekea chumba namba moja. Kila mmoja alikimbia kuikoa nafsi yake. Walipofika chumba namba moja ambacho kilikuwa kimejaa silaha lukuki, Felix alibonyaza swichi moja ukutani. Sakafu ikafunguka na wote wakaingia ndani ya shimo. Yeye alikuwa wa mwisho, aliacha ametega bomu moja zito mle chumbani na kusahau kwamba walikuwa wamewasahau mateka muhimu sana mle ndani.
 
SEHEMU YA 45

Dakika nne baadae gari tatu za polisi na gari mbili za zimamoto zilikuwa zimewasili. Zimamoto walifanya kazi yao ya kuzima moto ambao sasa ulikuwa umeanza kuiunguza na ile nyumba. Hakuna aliyejua aliyewaita Polisi wale. Majirani kadhaa walikuwepo kusaidia katika uokoaji. Ndipo katika chumba kimoja walipomkuta Elizabeth Neville huku chumba kingine wakiwakuta Dokta Yusha na Mwanasheria mlevi wote wakiwa wamefungwa vitini. Katika chumba kingine walimkuta mtoto Anna akiwa kalala kitandani. Harakaharaka wote walipakiwa katika ambulance na kupelekwa katika hospitali ya wilaya ya Mafinga.

"Tafuteni kama kuna watu wengine humu" Koplo Adrian alisema katika lile jumba.

"Koplo njoo uone" askari mmoja aliita kutoka katika chumba kimoja. Koplo Adrian alienda, alipigwa na butwaa, alikuwa anatazama na chumba kilichojaa silaha mbalimbali za kivita.

Ghafla ulitokea mlio ulioambatana na mlipuko mkubwa wa bomu zito na kuiteketeza kabisa ile nyumba na vyote vilivyomo mle ndani.

Balaaa!!!

Askari wote waliteketea katika nyumba ile.

***





Askari wote waliteketea katika nyumba ile.

***

Daniel Mwaseba na Inspekta Jasmin ndio walikuwa wanaingia katika mji wa Mafinga. Taarifa ya kwanza kuipokea wakiwa ndani ya tax ilikuwa ni kuungua kwa nyumba moja huko Sabasaba. Katika redio ya Ebony FM walikuwa wameipa habari hiyo uzito mkubwa. Hadi mtangazaji aliposema ndani ya nyumba hiyo waliokolewa watu watatu tu huku wakimtaja kwa jina mwanamke aliyejitambulisha kwa jina la Elizabeth Neville ndipo wakastuka. Harakaharaka walimwambia dereva teksi waelekee Sabasaba. Waliyoyakuta huko ilikuwa ni hali ya kutisha sana. Ilikuwa kimeungua kila kitu mahali ambapo majirani walimhakikishia kwamba kulikuwa na nyumba. Kulikuwa na mabaki machache huku miili kumi na nane ikiwa imeungua tikitiki. Daniel alishangaa zaidi alipoambiwa wale wote walikuwa ni askari wa jeshi la Polisi pamoja na zimamoto.

"Kuna kitu!!" Daniel Mwaseba alisema.

"Hao watu waliookoka katika ajari hii wako wapi?" Daniel alimuuliza jirani mmoja.

"Wamekimbizwa hospitali" Jirani alisema.

"Twende haraka hospitali tuwawahi" Daniel alimwambia Jasmin.

Harakaharaka Daniel Mwaseba na Inspekta Jasmin waliingia kwenye gari na kuelekea hospitalini. Wote wakiwa na hamu ya kwenda kukutana na Elizabeth Neville..

Laiti wangejua......

Walifika hospitali, wakamtafuta daktari wa zamu na kumueleza lengo lao la kwenda kuwaona majeruhi wa ajari ya moto. Baada ya kuona vitambulisho vyao Dokta Kitange akiwapeleka moja kwa moja wale askari wawili wodini.

"Umewaonaje majeruhi, watapona kweli?" Inspekta Jasmin aliuliza wakiwa njiani.

"Watapona bila shaka, ila hawaoneshi kama ni majeruhi wa ajari ya moto. Hasa yule mwanamke inaonesha ameteswa sana. Sio moto ule" Dokta Kitange alisema.

Daniel alikuwa kimya akiwasikiliza. Walifika wodi namba mbili, wodi ya kiume waliyokuwa wamelazwa Dokta Yusha na Mwanasheria mlevi. Daniel aliwatambua..Pamoja na yote Daniel na Jasmin walifurahi sana kumpata Elizabeth Neville.
 
SEHEMU YA 46

"He vijana mmekuja huku? Ni nani kawatuma mje huku? Nakumbuka mara ya mwisho niliwatumia meseji kwamba narejea kutoka Ureno, lakini hamkunijibu wote" Badala ya kuwa kuwajulia hali Daniel aliuliza kwa wahka.

" Daniel Mwaseba!! Umekuja huku. Nawe umekuja kwa ajili ya Elizabeth Neville?? " Dokta Yusha aliuliza kwa nguvu.

"Hii ishu imekuwaje?, na wakina Mwanasheria mpo?" Inspekta Jasmin nae aliuliza.

Nusu saa baadae wanaume watatu na mwanamke mmoja walikaa katika ofisi ya Dokta Kitange. Dokta Yusha ndiye alikuwa muongeaji mkuu.

"Sisi tupo hapa kwa muda mrefu sana. Tulianza kufanya kazi hii miezi mingi iliyopita. Tulianza kufanya upelelezi wetu huko Mbeya na kutuleta hadi huku. Dhima yetu kuu ni kumsaka Elizabeth Neville kama tulivyotumwa na Mkurugenzi wa usalama wa Taifa. Tulianza kumpeleleza kaka yake Elizabeth Neville huko Mbeya, tulihisi kupitia yule tutampata Elizabeth Neville. Na ilikuwa hivyo...Siku moja tulivamiwa ambapo mtoto wa kaka yake Elizabeth aitwaye Anna alikuwa amelazwa. Tuliwafatilia wale wauaji ambapo walitufikisha mpaka pale kwenye kambi yao. Wale jamaa ni watu hatari sana. Kumbe ndio walikuwa wanamshikilia Elizabeth Neville. Tulimkuta mle bhana lakini akiwa katika mateso makubwa sanaaa. Tulishindwa kumuokoa Elizabeth kwakuwa nasi tuliingia katika mikono yao. Tulitekwa wote kirahisi sana. Tulikaa mle hadi jana usiku ambapo ulitokea mlipuko. Wakati huo Elizabeth alikuwa yupo katika mateso ili atoe siri waitakayo. Hawakuwahi. Mlipuko ule uliharibu kila kitu. Dakika chache baadae walikuja askari kule chumbani tulipokuwa na kutuleta huku. Hatujui chochote kilichoendelea kule"

"Mmesema mmetumwa na mkurugenzi wa usalama wa Taifa. Yeye alikuwa anamtaka wa nini huyo Elizabeth Neville kwa alivyowaeleza?" Daniel Mwaseba aliuliza.

"Alisema Elizabeth ana siri kubwa ambazo zinahitajika kwa usalama wa nchi yetu"

"Nyinyi mmepata bahati ya kukutana uso kwa uso na Elizabeth Neville. Je kwa anavyoonekana ni mtu wa aina gani?" Inspekta Jasmin aliuliza.

"Elizabeth ni mtu mpole kwa mwenekano. Lakini ni sugu hasa. Inaonesha kuna vitu vya siri anavijua maana kuna wakati alitaka kunieleza lakini nilikataa" Mwanasheria mlevi alisema.

"Kwanini ulikataa?" Daniel aliuliza

"Hapakuwa sehemu sahihi mahala pale. Maana siri ile isingekuwa siri tena, chumba kile kulikuwa na camera za siri ambazo zikichukua kila kitu" Mwanasheria mlevi alisema.

"Sasa watu wanne kwa umoja wetu tuwasake hao watu waliomteka Elizabeth. Ambao bila shaka hawakuwepo katika mlipuko ule" Daniel Mwaseba alisema.

Ghafla mlango wa ofisi ulifunguliwa. Dokta Kitange alikuwa anapiga kelele.

"Wamemtekaaa, wamemtekaaa"

"Tulia Dokta, nani wamemteka?" Dokta Yusha aliuliza.
 
SEHEMU YA 47

"Elizabeth, Elizabeth Neville ameibiwa wodini!!" Dokta Kitange alisema kwa nguvu.

Watu wote wanne walitoka kwa pupa mle wodini. Nyuma wakifuatwa na Dokta Kitange. Moja kwa moja walielekea katika wodi aliokuwa amelazwa Elizabeth Neville. Hakukuwa na mtu.

"Ilikuwaje hadi Elizabeth Neville akachukuliwa humu?" Daniel Mwaseba aliuliza kwa ukali. "Si kulikuwa na ulinzi?"

"Hata sisi hatuelewi. Tumewakuta askari wawili wakiwa wamesinzia mlangoni huku Elizabeth Neville akiwa ametoweka. Lakini tunaweza kuona kila kitu maana tu CCTV humu hospitali" Dokta Kitange alijibu.

"Sasa ametekwa au ametoroka" Jasmin aliuliza.

"Bila shaka ametekwa, kwa hali yake ilivyo hawezi hata kutembea. Hana nguvu kabisa" Dokta Kitange alisema.

"Tupeleke katika chumba chenye TV ili tuone nini kilitokea. Huu utakuwa udhaifu mkubwa sana kumpoteza Elizabeth Neville mikononi mwetu. Hatupaswi kujisamehee kwa makosa haya" Dokta Yusha alisema.

Harakaharaka walienda katika chumba cha mitambo ambako ndipo kulikuwa na TV zikizoonesha kila kitu ndani ya ile hospitali huku ikirekodi kila kitu. Wote watano walikaa mbele ya TV moja na kuangalia matendo yaliyotokea nusu saa iliyopita katika wodi aliyokuwa amelazwa Elizabeth Neville.

...alionekana Elizabeth Neville akiwa amelala kitandani. Mkononi mwake kulikuwa na dripu ya maji yaliyokuwa yanaingia taratibu. Elizabeth Neville alikuwa amelala usingizi akiwa amefunikwa na shuka nyeupe za hospitali. Mwili wake ukiwa dhaifu sana...mara mlango wa wodi ile ulifunguliwa na aliingia nesi wa kike akiwa na kiti chenye matairi cha kubebea wagonjwa. Nesi alienda moja kwa moja katika kitanda alichokuwa amelazwa Elizabeth. Aliitoa ile dripu ya maji taratibu na kumkalisha kitako Elizabeth kwenye kile kiti. Taratibu alitoka nae nje yule mwanamke. Ilikuwa ni rahisi kama kumsukuma mlevi....

"Ni nesi wenu yule?" Daniel alimgeukia Dokta Kitange.

"Hapana, hatuna nesi kama yule hapa hospitali" Dokta Kitange alijibu kwa uwoga.

"Nataka kuona TV itakayoonesha yaliyotokea nje ya wodi hii" Daniel alisema.

Dokta Kitange alichukua rimoti na kubonyazabonyaza. TV ilianza kuonesha tena.

TV ilionesha askari wawili wakiwa wamekaa nje wodi aliyokuwa amelazwa Elizabeth Neville. Mara alitokea yule nesi aliyeonekana awali akiongea nao. Baada ya dakika tano askari wale walikubaliana na yule mwanamke kisha nesi aliingia ndani ya wodi. Wale askari walibaki wamelala vitini sekunde tano baadae. Baada ya dakika tano alionekana yule nesi asiyejulikana akitoka mle wodini akiwa anamsukuma Elizabeth Neville. Alipita nae kwenye korido ndefu huku akipishana na watu kadhaa ambao hawakuwa na wasiwasi hata kidogo na yule nesi. Alikata kushoto njia ikiyoelekea nyuma ya hospitali ile. Ikatokea mlango wa nyuma ambapo hakukuwa na watu. Camera zilimuonesha yule nesi akimshusha yule Elizabeth Neville na kumuingiza ndani ya teksi. Gari likaondoka...

"Hebu rudisha nyuma kidogo hadi kwenye ile teksi" Daniel alisema.

Dokta Kitange alirudisha nyuma.
 
SEHEMU YA 48

"Gandisha...gandisha hapohapo" Daniel alisema.

"Jasmin andika hizo namba za hiyo gari"

Jasmin alizinukuu zile namba.

T 345 CJA..

"Huyu mwanamke ni nani? Halafu anajiamini sana. Anajua nini kuhusu Elizabeth Neville? Haya mambo yanazidi kuchanganya" Dokta Yusha alisema.

"Yes, wakuu tuna pa kuanzia. Lazima tugawane majukumu katika kufanikisha hili. Dokta Yusha na Jasmin mtalifuatilia hili gari. Mimi na Mwanasheria mlevi tutaenda Sabasaba kule katika eneo la tukio. Wakina Jasmin mtaripoti kila kitu kwangu. Kuweni makini sana katika nyendo zenu, kosa moja tu laweza kuleta madhara makubwa sana"

Jamaa waliagana na kila mmoja kuingia kazini.

Safari ya Jasmin na Dokta Yusha iliwafikisha hadi stendi ya Mafinga katika kituo pekee cha madereva teksi. Waliwakuta madereva wakiwa katika makundi makundi wakizungumza. Walimwita dereva mmoja pembeni.

"Habari yako kaka" Jasmin alianza kwa kusalama.

"Salama kabisa dada yangu sijui ninyi?"

"Nasi tuko poa. Tuna shida moja ndogo" Jasmin alisema. "Jana tulikodi teksi hapa mida ya usiku lakini kwa bahati mbaya tulisahau mzigo wetu mmoja"

"Teksi gani hiyo" Dereva teksi aliuliza.

"Ni teksi nyeupe, Toyota mark 11 yenye namba T 345 CJA. Unaijua?" Jasmin aliuliza.

"Ya Shabani, teksi ya shabani hiyo. Mbona hiyo teksi ina siku ya tatu sasa imekodishwa. Na majamaa wanaiendesha wenyewe. Ngoja nimuite Shabani"

"Haina haja ya kumuita. Labda itakuwa tumekosea namba kama imekodiwa"

"Sawa haina shida wakuu, poleni sana kwa kupoteza mzigo wenu"

Wakaagana.

"Hii ishu ishakuwa ngumu. Sijui tutampataje yule nesi nwanaharamu" Jasmin alisema kwa hasira.

"Yaani hii habari ya Elizabeth Neville ni yenye utata sana. Mimi siku zote yaniacha na maswali kadhaa yasiyo na majibu" Dokta Yusha alisema.

"Tutajua tu mbivu na mbichi" Jasmin alisema kwa hamasa.

"Sasa nini kifuatacho?" Dokta Yusha aliuliza.

"Ngoja tumpigie Daniel tumpe habari hii"

Jasmin alipiga simu kwa Daniel. Huko walipata habari mpya kabisa iliyobadilisha mipango yao.

"Daniel mambo vipi?" Inspekta Jasmin alianza simuni.

"Mambo safi. Vipi habari kuhusu ile teksi"

"Bado tunaendelea kuifatilia ile teksi. Ingawa yule dada inaonesha ameikodi siku tatu kabla. Sidhani hata kama huyo dereva atakuwa anamjua yule dada. Lakini tunataka tumbananishe atatapika tu kila kitu...." Mara ikasikika simuni sauti.

"Daniel, Daniel inaonekana kuna handaki hapa " sauti ya Mwanasheria mlevi ilisikika simuni.

"Hee kweli !!! Kumbe huu sio mfuniko wa chemba?"

"Ndio, nimejaribu kuchunguza na nimegundua kuna njia. Sasa lazima tuingie humu tujue huko ndani kuna nini? Bila shaka wahalifu watakuwa humu?
 
Back
Top Bottom