Simulizi : Elizabeth Neville

Simulizi : Elizabeth Neville

SEHEMU YA 19

Na kwa bahati nzuri alifanikiwa kumpiga picha. Ni huyu hapa" Felix alisema huku akimkabidhi yule jamaa mfupi mnene ile picha.

.

Jamaa mfupi mnene baada ya kumwangalia akampa yule jamaa mrefu, naye baada ya kuiangalia akampa Richard amwone huyo jamaa.

"Ni Martin............ !!! Richard akatukana tusi kubwa la nguoni. Aiseee ni Martin Hisia!!!"

"Na wewe unamjua huyo jamaa? " Felix akauliza ingawa na yeye alikuwa anamjua Martin Hisia ni nani.

"Martin ni rafiki yangu mkubwa sana. Tushafanya misheni nyingi sana pamoja. Misheni yetu ya mwisho ni ile ya mkanda wa siri tuliyotumwa na Brown Mzungu. Martin ni mjuvi sana wa haya mambo. Yatupasa tuwe makini sana. Sio mtu wa kumuendea kichwakichwa" Richard alisema.

"Hata mimi nishasikia habari zake huyu jamaa. Ni mtu hatari na anayetumia akili sana, sasa kuanzia sasa nasi yatupasa kutumia akili. Nasikia Martin ni moto wa kuotea mbali!!" Felix alisema.

"Kwa mara ya kwanza nafanya kazi upande tofauti na Martin katika maisha yangu. Yahitaji mbinu kabambe kumshinda. Lakini kwakuwa mimi nimeanza kufahamu kama na yeye yupo katika hii misheni upande mwengine bila shaka nitamshinda. Wanasema kumjua adui ni nusu ya kumshinda!! Ila hii misheni itakuwa ya hatari sana!!" Richard aliwaza.

"Tufanye kama tulivyopanga. Felix nenda Mbeya leo ukamlete Moses Neville na familia yake. Richard na watu wawili hapo nje watamfatilia Martin na kumleta hapa." Yule mtu mnene mfupi alisema.

Na kikao kile cha watu wanne kikafungwa.

"Hawamjui Martin hawa. Martin sio mtu wa kwenda kumbeba kama mzoga wa mnyama. Lakini hivi mimi nipo sahihi kwenda kumkamata Martin? Huu ni usaliti. Tumefanya mambo mengi na Martin siwezi kumfanyia hivyo. Kaniokoa katika hatari nyingi sana. Bila Martin pengine nisingekuwa hai leo. Nakumbuka hisia zake zilivyotuokoa kule katika jumba la Chifu. Sasa leo usaliti ndio yawe malipo ya Martin toka kwangu? No! Lazima nimpe tahadhari Martin kabla haijamkuta hatari!!" Richard aliwaza wakiwa wanatoka nje na wale jamaa wawili walioshiba.

"Zungu na Seif mtafuatana na Richard kwenda kwa yule jamaa anayetupeleleza. Richard ndiye atakuwa kiongozi wenu katika kazi hii ndogo. Gon amefanya kazi nzuri sana usiku wa leo sasa nanyi msituangushe. Mpo na Richard, naamini hamuwezi kushindwa kitu chochote kile" Yule mtu mfupi mnene alisema akiwaaga pale getini.

Wakati Felix akipanda gari ndogo kuelekea jijini Mbeya kumsaka Moses Neville, Richard, Zungu na Seif walipanda gari na kuelekea Pareto kumsaka Martin Hisia. Seif ndiye alikaa nyuma ya usukani. Zungu akiwa pembeni ya Seif huku Richard akiwa katika siti ya nyuma.
 
SEHEMU YA 20

"Toka home hatari" maneno matatu aliyaandika Richard katika simu yake na kumtumia Martin.

Nusu saa baadae nyumba akiyokaa Martin Hisia ilikuwa imezungukwa na watu watatu.

"Zungu utapitia kwa nyuma. Utatumia ukuta kuingia ndani. Utavamia kutumia mlango wa uwani. Kuwa makini jembe. Seif utabaki humu ndani ya gari, tukimpata tunakuja nae mkuukuu na faster unawasha gari tunasepa. Wakati mimi nitaenda kugonga geti la mbele, na nitavamia kupitia mbele. Nyote kuweni makini sana Martin ni mtu hatari. Tufikirie kumuua kwanza ndipo tumkamate. Kosa moja tu laweza kutuadhibu" Richard aliwaeleza wenzake. Wote walikubaliana na maelezo ya Richard.

"Naenda kukutana na Martin baada ya miaka kadhaa. Siwezi kumsaliti Martin. Lazima nihakikishe hadhuruki hata kidogo" Richard aliwaza akiwa getini.

Wakati Zungu akiruka ukuta, Richard alikuwa anagonga geti kubwa la mbele.

***

Kulikuwa na utulivu mkubwa katika chumba cha upasuaji katika hospitali ya K's. Hospitali hiyo ilikuwa maarufu katika masuala ya operesheni ya kuondoa upande mmoja wa ubongo ambao kitaalam ilikuwa inaitwa hemispherectomy.

Katika kitanda ndani chumba cha upasuaji kulikuwa na mtoto aitwaye Anna amelala akiwa hana fahamu.

Anna alikuwa amezaliwa kama mtoto wa kawaida. Alianza kushikwa na kifafa akiwa na umri wa miezi kumi na tatu. Anna alikuwa na kifafa kinachoambatana na kutetemeka kwa viungo. Kwasasa alikuwa na umri wa miaka mitatu na alikuwa anashikwa na kifafa mara nyingi sana. Halafu kikawa kinabadilika na kuathiri upande wake wa kulia. Kifafa kilikuwa kinaanzia upande wa kushoto wa ubongo na kuathiri upande wake wa kulia wa mwili.

Kifafa ni jambo la kutisha, hasa kwa wazazi ambao hawajawahi kukiona.

Dr Yusha, daktari bingwa wa operesheni hizi alikuwa katikati ya jopo la madaktari kadhaa katika hospitali ya K's. Mtaalamu wa nusu kaputi alishafanya mambo yake ili kuhakisha operesheni hii ngumu zaidi kuwahi kufanyika katika hospitali ya K's iliyopo Mafiati jijini Mbeya inafanikiwa.

Nje ya chumba cha upasuaji alikuwepo Moses Neville. Baba mzazi wa mtoto Anna. Moses alikuwa kimya huku sura yake ikiwa ya unyonge sana akimuwaza mtoto wake wa pekee ambaye akikuwa katika chumba alichokuwa anakitazama kupigania uhai wake. Kifuani kwake kulikuwa na kichwa cha mtu kikilia. Alikuwa mkewe Joyce. Walikuwa wameomba na kuomba ili mtoto wao atoke salama katika operesheni hiyo ngumu na ya hatari. Sasa walikuwa wamemuachia Mungu kwa kupitia mikono mizuri ya Dokta Yusha.
 
SEHEMU YA 21

Operesheni hiyo ya kusisimua ilianza kama kawaida kwa kukata mstari katika ngozi ya kichwa. Daktari msaidizi alikuwa akinyonya damu kwa kutumia mpira aliokuwa ameushika mkononi wakati Dokta Yusha akiuingiza mishipa ya damu kuzuia damu isitoke. Kibano kimoja baada ya kingine viliwekwa pembezoni mwa ule mkato kuifanya iendelee kuwa wazi. Chumba kile kidogo cha upasuaji kulikuwa kimejaa utulivu na ukimya mkubwa.

Dokta Yusha na madaktari wenzake waliendelea na operesheni. Operesheni hiyo iliyodumu kwa saa tano ilimalizika salama.

Wakati operesheni inamalizika Felix ndio alikuwa anaingia jijini Mbeya kwenda kuiteka familia ya Moses. Alikuwa na ramani ya mahali alipokuwa anaishi Moses. Hivyo moja kwa moja alielekea Soweto kwenye nyumba ya Moses.

Dakika kumi baadae alikuwa mbele ya nyumba ya Moses. Aligonga na dada wa kazi alitoka nje.

"Namuulizia Moses ni rafiki yangu wa siku nyingi sana" Alidanganya Felix.

"Baba ameenda hospitali. Anna bado anasumbuliwa na kifafa" dada wa kazi aliongea kwa huzuni.

"Oooh kumbe Anna bado anaumwa. Na shemeji je yuko wapi?" Felix alitupa tena karata ya pili.

"Wote wapo hospitali. Ni mwezi sasa wanashinda huko" Dada wa kazi alisema.

"Aaah kumbe wote wapo hospitali. Ni hospitali gani ili nikipata nafasi nikawaone?" Felix aliuliza .

"Ni K's, ipo Mafiat. Ukifika Mafiat ukiuliza tu hospitali ya K's utaoneshwa" Dada wa kazi alijibu.

Felix alitia gari moto na kuelekea K's. " Naenda kuwatia katika mkono wangu wote. Kazi imekuwa rahisi kuliko nilivyotarajia. Nitahakikisha narudi nao Mafinga leoleo "

Muda huohuo, katika ofisi ya Dokta Yusha kulikuwa na watu watatu. Moses, Joyce na daktari mwenyewe. Wazazi wa Anna walikuwa wanapewa matokeo ya operesheni iliyotoka kufanyika muda mfupi uliopita.

" Tumefanikiwa kuondoa sehemu ya ubongo wake wa kushoto. Unajua watu wanaotumia mkono wa kulia hutegemea upande wa kushoto wa ubongo kwaajili ya kusema na kujongea. So lazima tusubiri mgonjwa aamke tuone kama tumeweza kudhibiti kifafa. Na pia tuone kama atakuwa na uwezo wa kuongea na kujongea. Lakini naamini kila kitu kitakuwa sawa. Mungu ni mwema kwa Anna. Mungu ni mwema kwetu sote." Dokta Yusha alisema.

"Ni kweli daktari. Tunapaswa kukushukuru sana ingawa mwanetu bado yupo katika hali ya hatari. Jitihada zako ni za kupongezwa sana. Tulikuwa tumepoteza matumaini kabisa juu ya maisha ya Anna" Moses alisema.

"Poleni sana bwana na bibi Neville" Dokta Yusha alisema. " Hivi hamna ndugu mwengine maana nawaona wenyewe tu hapa hospitali?" Dokta Yusha alichokoza.

"Sisi tulizaliwa wawili. Mimi na dada yangu Elizabeth Neville. Baba na mama yetu walifariki katika ajari ya gari. Dada yangu Elizabeth yupo Mafinga kwa muda sasa" Moses alisema.
 
SEHEMU YA 22

"Pole sana Moses kwa kufiwa na wazazi. Na je mkeo hana ndugu nae?" Dokta Yusha aliuliza tena.

"Mke wangu ndugu zake wapo Mwanza ndio maana hujawahi kuwaona hapa hospitali ila huwa tunawasiliana nao mara kwa mara" Alijibu Moses.

Waliongea mengi sana na Dokta Yusha. Huku urafiki ukichepua kwa kasi kati yao. Wakati wanaendelea na mazungumzo ghafla simu ya Dokta Yusha iliita. Alipoangalia jina lilisomeka "Mwanasheria". Akaipokea.

" Take care Dokta" Mwanasheria alisema maneno matatu tu na simu ikakatwa.

"Kumekucha" Dokta Yusha aliwaza.

Take care Dokta" Mwanasheria alisema maneno matatu tu na simu ikakatwa.

"Kumekucha" Dokta Yusha aliwaza.

***

Kikao cha watu watatu kiliendelea katika sebule nyumbani kwa Felix iliyopo mtaa wa Sabasaba mjini Mafinga. Kulikuwa na watu walewale waliokutana asubuhi kasoro Felix mwenyewe ambaye alikuwa ameenda Mbeya kumsaka Moses Neville.

Misheni ya kwenda kumkamata Martin Hisia nyumbani kwake ilikuwa imefeli. Ndani kwa Martin walivamia lakini hawakukuta mtu yoyote. Yalikuwa mahame. Martin alikuwa ameshahama.

"Richard misheni ya kumkamata Martin imefeli. Sasa tunasubiri misheni ya Felix kule Mbeya" Mzee mfupi mnene alisema. " Kwa mujibu wa maelezo yenu inaonesha Martin aligundua kama atafatwa na kuhama. Swali la kujiuliza Martin alijuaje?"

"Sifamu alijuaje. Ila kwa mazingira tuliyoyakuta pale nyumbani kwake yaonesha Martin alihama muda mrefu. Pengine kuuwawa kwa John ndani ya nyumba yake ndiko kulimfanya achukue hatua hiyo" Richard alisema.

"Ok sasa lazima tujue Martin yu wapi? Pia ni lazima tumsake usiku na mchana ili kujua kwanini anamtafuta Elizabeth Neville? " Mtu mnene mfupi alisema.

"Yah hilo ndio la msingi. Tukifanikiwa kumdhibiti Martin na Felix akifanikiwa kule Mbeya tutakuwa tumepiga hatua kubwa sana. Kitakachobaki ni Moses kumshawishi dada yake ili aseme hiyo siri kuhusu 001. Na hii misheni itakuwa imekwisha." Mtu mwembamba mrefu alisema.

"Not easy as they think. Lazima pachimbike" Richard aliwaza.

***

Upande wa Martin ndio alikuwa anamaliza kupanga vizuri vitu katika chumba chake cha mitambo. Alihakikisha kamera zote zilizoizunguka nyumba yake zimeunganishwa vizuri na kompyuta iliyokuwepo katika chumba chake cha mitambo. Kisha alitoka na kwenda kuweka vifaa sawa katika chumba cha mateso. Aliridhika na nyumba ile mpya na mazingira yake. Sabasaba kulikuwa mahali kuzuri kwa kazi yake kuliko kule kwa awali bila kujua kwamba Sabasaba ndio mtaa aliokuwa anakaa Felix.

Mara simu yake iliita. Alikuwa Lucas...

"Vipi Martin umeonaje makazi yako mapya?" Lucas aliuliza baada ya salaam.
 
SEHEMU YA 23

"Huku ndio kwenyewe. Kuna mandhari nzuri sana rafiki kwa kazi yangu. Hakuna msongamano wa watu kama kule kwa awali. Ni patulivu sana" Richard alisema.

"Nimefurahi sana kama umeridhika na mahali hapo. Je kuna taarifa zozote kuhusu Elizabeth Neville ulizozipata?" Lucas aliuliza.

"Leo usiku ndio nitaingia kazini. Kesho asubuhi nitakuwa na lolote la kukwambia. Naamini kwa mtego nilioutega nitakuwa nimepiga hatua kubwa sana kesho." Martin alisema kwa kujiamini.

"Je kuna chochote unachohitaji?"

"Kwa sasa hapana mkuu. Nitakufahamisha nitakapokuwa nahitaji kitu"

Lucas na Martin waliagana simuni.

"Ngoja nimpigie Essau nione kama kutakuwa na lolote kule Pareto" Aliwaza. Akaiangalia simu yake ili ampigie Essau. Ndipo alipoona kuna ujumbe mpya katika simu yake. Aliusoma.

"Toka home hatari" Ilikuwa meseji kutoka kwa Richard.

"Inamaana Richard yupo Mafinga? Hii misheni naimaliza soon. Richard na Binunu ndani ya nyumba!!!" Martin alipiga kelele akiwa peke yake. "Sasa Richard kajuaje kama nyumba yangu itavamiwa? Ngoja nimpigie anieleze vizuri"

Wakiwa katika sebule ya Felix, Richard alisikia simu yake inatetema. Akaitoa mfukoni na kuiangalia. "Martin" alisema kimoyomoyo ingawa katika kioo cha simu ilisomeka Comrade. Alikuwa anatamani kupokea simu ya Martin lakini hakufanya hivyo. Ule ulikuwa sio wakati muafaka. Simu iliita hadi ikakata.

"Nitakupigia baadae" Alituma ujumbe.

Martin aliusoma ujumbe wa Richard. Akajua kuna kitu.

" Richard hajawahi kutopokea simu yake. Taratibu alielekea katika chumba cha kompyuta. Alikaa katika kitu kikichotazamana na kompyuta yake. Alibofya bofya, kwenye kioo cha kompyuta ilionekana nyumba yake ya Pareto. Akarudisha nyuma hadi alipopataka. Akatulia kitini huku akiwa makini. Ndipo alipoona kila kitu kilichotokea nyumbani kwake dakika kumi na tatu tu baada ya yeye kuhama.

"Haina haja ya kumpigia Essau, nitajionea mwenyewe" Aliwaza.

Aliona gari likiwasili pale na watu watatu kushuka. Kisha alimwona mmoja akirudi garini na mwengine akielekea nyuma ya nyumba yake. Walikuwa kwa mbali hivyo hakuwatambua. Alimwona mmoja akielekea getini. Kila jamaa akivyopiga hatua mwili wa Martin ulikuwa unasisimka vibaya sana.

"Ni mwendo wake. Ndio itakuwa ni yeye" Martin alisema huku akiangalia kompyuta yake bila kuiamini.

"Ni Richard!! Amefata nini nyumbani kwangu?" Alipayuka kwa nguvu.

***

Jua limezama. Ni saa kumi na mbili jioni jijini Dar es salaam. Mkurugenzi wa usalama wa Taifa

Christopher Mangwina alikuwa nyumbani kwake akijiandaa kuelekea ikulu kwa ajili ya kikao kingine.

Mara simu yake iliita.

"Mkuu kuna tatizo limetokea K's hospitali. Hospitali imevamiwa!!" Bila salamu alisikia sauti katika simu yake.

"Imevamiwa? Na nani? Vipi wamefanikiwa kupata chochote?" Mkurugenzi aliuliza.

"Wameondoka na Anna! Huku Moses na mkewe Joyce wakiwa wamejeruhiwa vibaya sana kwa risasi!" Mwanasheria mlevi alisema simuni.

"Mmefahamu ni kina nani hao?"

"Mimi nilikuwa katika baa nikipata vitu vyangu karibu na hospitali. Kuna gari moja ilifika majira ya jioni. Alishuka kijana mmoja ambaye nilipomwona tu nilimtilia shaka kutokana na mwonekano wake. Nilianza kumfata nyumanyuma. Nilimwona kaingia katika vyoo vya kiume, nami nilimsubiri kwa nje. Nikijifanya nimelewa tilalila. Nikiwa pale nje nilimtumia meseji Dr Yusha aliyekuwa ofisini kwake na Moses na mkewe kwamba awe mwangalifu. Nilihisi hali ya hatari. Sijui kilitokea nini lakini yule mtu hakutoka tena mle chooni.

ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 24

Baada ya dakika kumi na tano za kusubiri niliamua kuingia mle chooni nikamwangalie. Cha ajabu hakukuwa na mtu! Nilikimbia mbio kuelekea katika wodi alipolazwa mtoto Anna, naye hakuwepo pale kitandani!

Nilirudi haraka katika ofisi ya Dokta Yusha. Niliwakuta Moses na mkewe wakiwa wamelala chini. Kwa kasi nilitoka nje. Hakukuwa na kitu chochote cha kushangaza lakini gari alilokujua nalo yule jamaa halikuwepo. Yaani hadi sasa sijui Dokta Yusha yupo wapi maana simu yake haipatikani. Moses na Joyce wapo katika chumba cha upasuaji. Hali zao ni mbaya sana" Mwanasheria mlevi alisema kwa pupa simuni.

"Nimekuelewa. Sasa hivi naelekea ikulu kuna kikao cha dharura. Nitakupigia pindi tu nitakapotoka. Lakini hakikisha unajua wapi alipo Dokta Yusha na mtoto Anna. Kwa hali yake hapaswi kabisa kuwa mbali na hospitali."

"Sawa mkuu" Mwanasheria mlevi alijibu.

Simu ikakatwa.

"Ni nani hao wamewaza sawa na usalama wa Taifa. Sisi tuliamini kumweka karibu Moses ni kumweka kumpata Elizabeth. Na wao wameweza the same, ni watu gani hao? Wanaoingia chooni na kutoka bila ya kuonwa na jicho la Mwanasheria mlevi? Hii ishu sasa imezidi kuwa ngumu" Aliwaza akiwa njiani kuelekea ikulu.

Wakati huohuo, Felix alikuwa katika usukani akiendesha gari kwa kasi kubwa sana. Katika siti za katikati mtoto Anna alikuwa amelala hana fahamu. Felix alikuwa anajipongeza kwa ufundi alioutumia mpaka kumnasa Anna na kuwaacha Moses na mkewe wakiwa majeruhi.

"Yule jamaa alidhani mimi zoba? Ataenda kuwasimulia kwao. Mana jinsi nilivyomtoka pale chooni, nilipita kama upepo. Yaani sekunde kumi na tano za kuiinamia simu yake ili kubofya simu yake nilizitumia ipasavyo. Ila jamaa kanijuaje yule? Mana kaanza kunifatilia pindi tu niliposhuka garini. Jamaa ana jicho la kumjua mhalifu. Tutakutana tu!!" Felix aliwaza garini akiwa katika barabara ya Uyole akirejea Mafinga.

"Lakini je kama wale ni askari wakiweka mtego wa kiaskari mbele? Am a man nitavuka tu" Felix alisema huku akitoa sigara katika koti lake. Gari ikiwa katika kasi isiyomithilika aliachia mikono na kuwasha sigara. Aliiweka mdomoni huku akiendelea kutimua mbio. Alikuwa anarudi kambini akiwa amefanikiwa.

***

Saa moja kamili kikao kilianza huko Ikulu.

"Karibuni tena viongozi wenzangu katika kikao hiki." Rais Dr Joseph alianza kusema. "Naamini kwa sasa kikao kitakuwa na majibu mengi kuliko maswali. Bila shaka mkurugenzi wa usalama wa Taifa na IGP mtakuwa mmefanya kazi ya kutupeleka kumjua kwa undani huyo Elizabeth Neville. Naomba IGP tueleze wapi ulipofikia?"

IGP Rondo alisimama mbele ya kikao. Ukumbi ulikuwa kimya kiasi kwamba hata unyoya ungeanguka sakafuni ungeusikia. Masikio yao yote walimkabidhi mkuu wa Polisi IGP John Rondo.
 
SEHEMU YA 25

"Ahsante sana Mheshimiwa Rais na wanajopo wote. Mimi kwa upande wangu tangu tulivyoachana hapa nilienda kulifanyia kazi hili suala. Na kwa hakika nimemjua Elizabeth Neville ni nani???"

Nyuso zote mle ndani zilionesha mstuko.

"Nilivyotoka hapa moja kwa moja nilienda makao makuu ya Polisi. Niliitisha kikao kidogo na wapelelezi watano ninaowaamini sana. Wakiongozwa na Fanuel Mwalembe. Kazi yao ilikuwa moja tu, kuchunguza na kupekua ili kumfahamu huyo Elizabeth Neville ni nani? Na kweli hapa nina kurasa mbili zenye kumuelezea kwa kirefu huyo kiumbe" IGP John Rondo alisema huku akimkabidhi zile karatasi mbili Mheshimiwa Dr Joseph.

Rais alizipokea na kuzigeuza geuza mbele na nyuma. Kisha aliongea " Pongezi sana IGP kwa kazi uliyoifanya wewe na vijana wako. Hakika hii ni hatua kubwa sana. Kumfahamu Elizabeth Neville ni hatua muhimu ya kwanza kuelekea kwa wezi wa dhahabu zetu. Mheshimiwa Dr Jeska hebu tusomee hizi karatasi mbele ya kikao ili wanakikao wote tujue kilichoandikwa humo" Rais alisema na kumkabidhi zile karatasi Dr Jeska Mlamka.

Jeska alizichukua zile karatasi na kuziangalia. Ukumbi wote ulikuwa kimya ukimsikiliza yeye. Aliiangalia karatasi ya kwanza kisha akafunua kuiangalia karatasi ya pili. Akarudia tena ya kwanza. Ghafla akasema "Khaaaa mbona siyaelewi haya maandishi?" Mheshimiwa Jeska alisema kwa sauti kubwa. Watu wote walishangaa. Jeska aliziangalia tena zile karatasi. "Imeandikwa kwa lugha gani hii?" Aliuliza tena.

"Mbona ni Kiswahili, ni Kiswahili mkuu" IGP Rondo alijibu harakaharaka.

"Hiki sio kiswahili" Jeska alisema huku akizirudisha kwa rais zile karatasi. Rais nae aliziangalia zile karatasi kwa umakini.

"Sio Kiswahili. Naona tunaleteana utani hapa!!" Alisema kwa sauti kuu huku akizirejesha kwa IGP Rondo mwenyewe.

Uso wa IGP Rondo ulikuwa katika mshangao. Kahamanika. Hakuelewa nini kimetokea. Alikabidhiwa ripoti ya Elizabeth Neville na Fanuel ikiwa katika lugha ya Kiswahili kumbukumbu zake zilimwambia hivyo. Aliisoma na kukubali kwamba ilikuwa ripoti nzuri na iliyojitosheleza kwa kila kitu. Leo hii ripoti ileile aliyokabidhiwa na Fanuel imebadilika lugha. Yalikuwa maajabu!!!

Aliishika ile ripoti na kuitazama. Akageuza ile karatasi upande wa pili. Hakuamini na wala kuelewa nini kimetokea.

"Wameibadilisha!!" IGP Rondo aling'aka. " Kuna watu wamenichezea mchezo. Unamchezea mchezo IGP? Watajuta. Hakika watajuta kuzaliwa"

"Hii habari kuhusu Elizabeth Neville imekuwa ikigubikwa na utata kila siku. Tazama, ripoti ya IGP Rondo eti anatwambia imebadilika lugha. This is too much. Hii ni aibu kwako Rondo. Aibu kwa timu yako yote" Rais Joseph alisema kwa kughadhika. "Hii ndio aina ya watu wanaoongoza nchi hii. Wazembe wazembe wazembe!! Huu ni uzembe wa kiwango kikubwa sana kuwahi kufanywa na IGP"
 
SEHEMU YA 26

"Samahani Rais. Samahanini wanajopo wot..." IGP Rondo alikuwa anaomba samahani lakini rais akamkatisha.

Kwa hasira akasema" Nafunga hiki kikao hadi kesho saa mbili usiku!!"

Kikao kilifungwa namna hiyo. IGP Rondo alikuwa ameharibu hali ya hewa. Rais Joseph alikuwa katika rundo la hasira. Hatazamiki.

Saa mbili usiku ya siku hiyohiyo ilikuja habari iliyomsitua kila mtu. Kupitia kwa mkurugenzi wa habari wa ikulu ilisambaa habari kwamba Rais wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania amfuta kazi mkuu wa Polisi nchini, IGP John Rondo! Huku nafasi yake ikikaimiwa na ndugu Zaidi Kalinga"

Ulikuwa ni uamuzi mbaya kuliko yote katika utawala wake.

***

Felix na mtoto Anna waliingia ndani ya nyumba huko Sabasaba. Huku Anna akiwa hana fahamu kabisa. Alikuwa katika hali ya hatari ambayo Felix hakuonesha kuijari hata kidogo. Yeye dhamira yake ilikuwa moja tu, kumfanya Elizabeth Neville aseme kwa njia yoyote. Bila ya kujari kwamba njia hiyo ina madhara gani kwa wengine. Hiyo ndio ilikuwa tabia halisi ya Felix. Mtu katili asiye na huruma hata chembe.

"Wooow Felix umefanya kazi kubwa sana we jamaa ni kiboko. Hakika umefanya kazi kubwa sana. Wewe kweli ni fundi makini katika hizi mambo. Umeifanikisha hii kazi ya Mbeya kwa asilimia zote. Hongera sana Felix!!" Mtu mnene mfupi alisema kwa mbwembwe zote.

"Ahsante sana boss Sam. Lakini haikuwa rahisi sana. Pale hospitaki K's nimeuwa wawili nimeteka hiki kifaranga na kuacha kizaazaa kikubwa sana ambacho mtakiona magazetini kesho. Kwasasa nina mtoto wa Moses ambaye ni mgonjwa lakini nina hakika atatusaidia sana. Cha msingi boss tafuta daktari sasahivi arekebishe hali yake ili tumtumie baadae" Felix alisema huku akiingia ndani.

Harakaharaka mtu mfupi mnene alipiga simu kwa rafiki yake ambaye ni daktari wa wilaya Mafinga.

"Dokta Beka uko poa" Sam aliongea simuni baada simu yake kupokelewa.

"Niko poa, vipi pande gani?"

"Niko kwa Felix waweza kuja kuna ishu. Mambo yetu yale yanakuhitaji tena" Sam alisema.

"Nitakuwa hapo baada ya dakika kumi. Nije na vifaa?" Dokta Beka alisema

"Ndio. Kuna ishu critical kidogo" Sam alisema.

"Sawa. Am on the way Sam"

Sasa pale nyumbani walitulia wakimsubiri daktari ili aje kumsaidia mtoto Anna.

"Vipi kuhusu Moses Neville?" Mtu mrefu mwembamba alivunja ukimya.

"Nimemwua!" Felix alisema " nimemwua yeye na mkewe waliniletea ujuaji. Tutamtumia tu huyo mtoto kama mtego ili Elizabeth atwambie tutakacho. Atasema tu ni mjomba wake" Felix alisema kwa kujiamini.

"Sidhani" Richard alisema kwa sauti ndogo lakini iliyosikuwa na kila mtu. "Its not easy like that"

Watu wote walimwangalia Richard. Wakiwa hawayaamini masikio yao.
 
SEHEMU YA 27, 28, 29, 30

"Unasemaji wewe bishoo" Felix aliuliza kwa dharau.

"Ni mimi ndiye niliyebuni mbinu ya kumtumia Moses ili kumfanya Elizabeth Neville aseme kila kitu. Ni Moses nilisema sio mtoto mdogo wa Moses mgonjwa asiojiweza kwa lolote. Mpango haukuwa huo" Richard alisema.

"Sikiliza we bishoo. Mpango 'A' ukifeli siku zote tunaingia katika mpango 'B'. This is our principle katika hizi kazi. Usituletee mawaidha ya huruma hapa. Hapa hatuhubiri" Felix alisema.

"Mpango huu niliubuni mimi narudia tena. Na haukuwa na plan 'B'. Plan ilikuwa ni 'A' tu ambayo ilikuwa kumleta Moses hapa. Sio huyu mtoto asiye na hatia. Ni plan 'A' tu na tumeshafeli" Richard alikuja juu.

Kule nje. Katika gari alilokuja nalo Felix kutoka Mbeya kulikuwa na mwinuko mdogo katika buti la gari la Felix. Ulitokea mwinuko na kisha buti kurudi tena chini. Ilikuwa ni ishara kwamba ndani ya buti kulikuwa ni mtu. Ni nani? Ameingiaje? Hakuna aliyekuwa anajua.

Baada ya dakika tano buti la gari likainuka tena. Kwa kutumia macho mawili ambayo yalikuwa kwenye buti yaliyachunguza mazingira yale. Yalikuwa macho ya kijasusi. Yakitathmini nini sasa cha kufanya kwa wakati ule.

"Hapa ndipo anapoishi jamaa. Yaani nimekaa kwenye buti kwa muda mrefu sana. Sijui nini kinachondelea huko duniani. Sijui Moses na Joyce kiliwakuta nini pale ofisini kwangu. Lakini kwakuwa nipo hapa majibu ya maswali yangu yote yatajibiwa nikipita mlango ule" Dokta Yusha aliwaza peke yake akiwa ndani ya buti katika gari la Felix.

Akiwa bado anachungulia kupitia upenyo mdogo alilishuhudia gari lengine liingia mle ndani. Alimwona daktari akishuka kutoka siti ya mbele.

Kumbe baada ya meseji ya Mwanasheria mlevi Dokta Yusha alipiga hatua moja mbele. Aliingia kwenye buti la gari la Felix bila mwenyewe kujua.

"Wamemleta daktari bila shaka kwa ajili ya mtoto Anna. Sasa kwanini wamteke Anna? Wana lengo gani hawa jamaa?" Dokta Yusha alijiuliza maswali mfululizo akiwa katika buti.

Alimshuhudia yule daktari akikaguliwa pale mlangoni na kisha kuingia ndani.

"Tutaonana giza likitawala" Aliwaza.

Saa sita kamili usiku giza likiwa totoro Dokta Yusha alitafuta namna ya kutoka nje ya buti ya gari bila kujulikana. Taratibu alifungua buti na kujitupa chini mithili ya mzigo. Harakaharaka alijiviringisha hadi uvunguni mwa gari. Akiwa kule uvunguni aliiona miguu ya mtu ikielekea kule kwenye gari. Akajua kwa vyovyote jamaa kasikia kishindo chake wakati alipojiangusha. Akakaa tayari kukabiliana nae. Jamaa alisogea hadi katika gari ya Felix. Aliwasha tochi na kuanza kulimulika gari. Kule chini Dokta Yusha alijibana vizuri ili asimulikwe. Akajisogeza kuelekea upande wa pili. Jamaa na tochi yake akaelekea ule upande aliokuwa kajificha Dokta Yusha. Kwa kasi Dokta Yusha akajiviringisha kurudi ule upande akiotokea jamaa. Jamaa akasimama, akainama kidogo ili achungulie uvunguni. Lilikuwa ni kosa la mwaka. Alikutana na teke la uso! Lililoipangusa vizuri pua yake. Jamaa aliona vimulimuli. Alikosa umakini kabisa. Lilikuwa kosa lengine. Harakaharaka Dokta Yusha alitoka uvunguni na kumkaba yule jamaa kwa nyuma. Bonge la kabali. Jamaa alijitahidi kujitoa lakini wapi. Dokta Yusha alikaza hasa. Jamaa alianza kuishiwa nguvu. Hewa ilikuwa ngumu kuipata. Dokta Yusha alikaza roba kwa mkono wake wa kushoto, huku mkono wake kulia akipeleka usoni. Kwa kutumia vidole vyake viwili aliviingiza machoni kwa jamaa. Aligandamiza. Jamaa akataka kupiga kelele. Kelele hazitoki kutokana na ile roba. Ilikuwa kasheshe!

Dokta Yusha akakaza zaidi ile roba. Jamaa alienda kuzimu taratibu. Dokta Yusha akamvuta yule jamaa na kumsweka uvunguni mwa gari. Kwa kunyata akaanza kuelekea katika ile nyumba. Akazunguka na kuelekea upande wa kushoto wa nyumba. Akalikuta dirisha. Akachungulia. Kilikuwa chumba kitupu. Hakuna kitu. Akasogea kwa mbele kuelekea nyuma ya ile nyumba. Akaliona dirisha lengine lakini lilikuwa limefungwa. Akazidi kuelekea mbele, dirisha la tatu. Alichungulia. Uso kwa uso alikuwa anatazamana na Elizabeth Neville!!!

"Elizabeth Neville" Dokta Yusha alisema kwa sauti ndogo. "Kumbe Elizabeth yupo humu?"

Dokta Yusha akaona hatari iliyopo kuendelea kukaa katika nyumba ile. Sehemu aliyopo Elizabeth Neville lazima itakuwa sehemu ya hatari.

"Nitaweza kweli kumkomboa Elizabeth Neville mwenyewe. Hapana. Namhitaji Mwanasheria mlevi" Dokta Yusha akawaza. "Peke yangu itakuwa ngumu. Lazima nitafute namna ya kutoka humu. Lazima nirejee na Mwanasheria mlevi kuja kuumaliza mchezo. Sasa nitatokaje?"

Dokta Yusha akaelekea ukutani. Alienda kutafuta namna ya kutoka nje kupitia ukutani. Ulikuwa ukuta mrefu ambayo kwake hakuwa anashindwa kuupanda. Alipougusa tu. Akahisi kitu cha baridi kikigusa shingo yake.

Bastola.

Mwanasheria mlevi bado alikuwa katika harakati za kumsaka Dokta Yusha pamoja na yule jamaa mvamizi aliyemteka mtoto Anna na kuwaacha Moses na mkewe wakiwa majeruhi. Alitafuta kwa kila namna lakini hakujua kabisa wameelekea wapi. Mwisho aliamua kumpigia Mkurugenzi wa usalama wa Taifa ili kumueleza kilichotokea.

"Mzee za sahivi" Mwanasheria mlevi alianza simuni baada ya simu yake kupokelewa.

"Nakusikiliza Mwanasheria" Aliitika.

"Huku Mbeya bado hali mbaya. Moses na mkewe hali zao sio nzuri hata kidogo. Mtoto Anna hajapatikana hadi sasa sambamba na Dokta Yusha. Nimejitahidi kadri niwezavyo ili kupata angalau fununu kwamba watakuwa wapi lakini sijafanikiwa" Mwanasheria mlevi alisema.

"Mmh this is unbelievable!! Wamepoteaje hao watu? Sasa una shauri ofisi ifanye nini kwa sasa?"

"Hii vita imekuwa ngumu sana. Tunapambana na watu tusiowajua lakini pengine wao wanatujua. Sasa ili twende sawa naomba uniongezee mtu. Kwa sasa nipo peke yangu bila dira yoyote. Lazima tuongeze mtu kwa ajili ya ushauri na mapambano. Hivi Daniel yu wapi. Daniel Mwaseba anatosha sana kuumaliza mchezo" Mwanasheria alisema huku sauti yake ikionesha matumaini.

"Daniel yupo likizo katika mji mmoja huko Ureno unaitwa Faro. Ana likizo ya mwezi mmoja ambao hata wiki mbili hana tangu ameondoka. Lakini neno langu ni amri kwake. Nitahakikisha anarejea, akusaidie kuifanya hii kazi kisha arejee tena huko Faro"

"Nashukuru sana mkuu kwa kuwa na nia ya kutekekeza ombi langu. Mlete Daniel mjini hapa aturahisishie kazi, lazima akate mizizi" Mwanasheria alisema.

Wakaongea maongezi kidogo kesho wakatakiana usiku mwema na kulala.

"Daniel Mwaseba again. Hawa sasa wamezoea vibaya. Huku ni kumpa kichwa tu Daniel kila kazi yeye. Safari hii simwiti ng'o. Wataifanya kazi wenyewe" Mkurugenzi wa usalama wa Taifa alikuwa anawaza wakati akiutafuta usingizi.

"Siwezi kulala wakati mwenzangu sijui yupo wapi? Siwezi kuwa msaliti kiasi hicho. Lazima nipambane usiku huu kujua mbivu na mbovu" Mwanasheria alitoka katika hoteli aliyopanga na kutoka nje. Aliangalia saa yake, ilikuwa saa nane na dakika tisa usiku. Alichukua pikipiki yake na kuelekea katika hospitali ya K's.

"Yalipoanzia mambo haya ndipo patakaponipa majibu. Mtu hawezi kufanya mambo yale mchana kweupe bila kuacha alama yoyote nyuma yake"

Dakika kumi baadae alikuwa nje ya hospitali ya K's. Alikaa katika kibanda kidogo ambacho mchana hutumiwa na mshona viatu. Alitulia tuli huku akiangalia kwa makini hospitali ile iliyoleta kizaazaa mchana. Alitumia dakika thelathini na moja tu. Ndipo alipoona tukio la kushangaza.

Aliiona gari aina ya Noah ikija kwa kasi. Kisha wakashuka watu wanne waliojazia wakiwa na mavazi meusi. Walisimama nyuma ya Noah yao wakipeana maelekezo.

"Wale sio watu wazuri. Kuna kitu kinaenda kutokea hapa. Ngoja niwe na subira" Mwanasheria alijionya mwenyewe.

Baada ya majadiliano jamaa waliingia ndani ya hospitali. Waliingia watu watatu wakimuacha mmoja palepale ndani ya gari. Ilichukua dakika saba tu, wale watu walitoka mkukuumkukuu, waliingia katika gari yao na kuondoka kwa kasi, Mwanasheria mlevi naye alikuwa nyuma yao juu ya pikipiki.

***

"Sasa tumekamilika. Hapa Martin Hisia, pale Richard Phillipo na kule Binunu Issa. Soon tunaenda kuimaliza hii kazi ya Mheshimiwa Lucas, na pengine ikawa ndio kazi yangu ya mwisho kama nilivyomuahidi Binunu" Usiku wa manane akiwa kitandani Martin alikuwa anawaza. "Kesho asubuhi tunaianza hii kazi. Kwa mikakati tuliyoipanga na Binunu jioni, hii misheni imekuwa soft sana. We are going to make it hureeeh"

Upande wa Mwanasheria bado alikuwa juu ya pikipiki yake akiwafata wale watu wanne waliokuwa ndani ya Noah nyeusi. Jamaa walipofika Mafiat walikata kulia njia iliyokuwa inaelekea Tunduma. Dhamira ndani ya moyo wake ilimwambia wale majamaa wana kitu na kule hospitali walifanya kitu. Ni kitu gani hiko? Swali hilo lilimfanya Mwanasheria aongeze kasi ya pikipiki kuwafata wale jamaa ili kukifahamu.

Noah ilipofika katika kituo cha daladala cha Kadeghe ilisimama kidogo. Mwanasheria naye alisimama ghafla usawa wa ukumbi wa Dhando akiwa makini na wale jamaa. Alimwona mtu mmoja akishuka ndani ya ile Noah huku akiwa ameweka simu yake sikioni.

" Hawa jamaa ni wakina nani lakini? Hawaaminiani hata wenyewe. Wako pamoja lakini kuongea na simu tu imebidi wasimame ili aongelee nje" Aliwaza Mwanasheria akiwa kaiinamia pikipiki yake akijifanya kuitengeneza.

Majamaa wawili walishuka kwa siri katika ile Noah na kuchepuka katika barabara inayoelekea mahakama kuu. Walienda kidogo na kukata kulia njia iliyokuwa inaelekea hosteli za Goodwill. Walipofika usawa wa uwanja wa mpira wa kikapu wa chuo kikuu cha Mzumbe walikata tena kulia na kuifata barabara iliyowafikisha tena katika barabara kuu.

Ghafla! Mwanasheria mlevi akiwa kaiinamia pikipiki yake alijikuta akipigwa teke la nguvu la makalio. Aliruka juu kilevi huku akitoa makelele ya ajabu.

"Yeleuwiii Mambo gaani haya mbona hatujapinga boko na nyinyi?" Mwanasheria mlevi alisema kimasihara.

"Usijifanye chizi. U mzima na umekuwa ukitufatilia tangu K's hospitali. Ukiwa mpole waweza kutoka katika mikono hii mibaya. Twambie ukweli kwanini unatufatilia?" Jamaa mmoja kati ya wake wawili aliuliza.

"Mimi natoka zangu Mbeya Carnival kupata kinywaji. Nimefika hapa pikipiki yangu imezinguaa. Mimi sijui mambo ya K's wala kufatilia. Mimi ni Mwanasheria, Mwanasheria lakini mlevi" Mwanasheria alisema huku akilia kilevi.

Jamaa walipata utata juu ya yule mlevi anayejiita Mwanasheria. Wamchukue ama wamwache.

"Twende naye Ngome huyu ndo ulevi wake wa kuwafatilia watu asiowajua utakwisha. Ni mjanja tu huyu lakini anakijua anachokifanya" mmoja wa wale watu alisema.

Walimbeba juujuu Mwanasheria na kuelekea naye katika gari lao. Walipofika naye tu yule jamaa akiyejifanya akiongea na simu naye aliingia na safari ya kuelekea Ngome ilianza.

Gari ilipofika Nzovwe jamaa mmoja akamnusisha kitambaa cheupe Mwanasheria. Baada ya sekunde thelathini alilala na hakujua tena nini kilikuwa kinaendelea hapa duniani.

Muda uleule wakati Mwanasheria mlevi akidhibitiwa na majamaa wanne wenye Noah na ndio ulikuwa muda uleule Dokta Yusha alihisi ubaridi katika shingo yake. Ubaridi wa bastola. Alijaribu kuangalia kwa jicho la wizi alishangaa. Alikuwa anatazamana na mtu asiyevaa nguo lakini alikuwa na viatu chini. Alikuwa anaitwa Gon!! Naye alitekwa na kuingia katika mikono haramu.

***

ITAENDELEA BAADAE KIDOGO
BURE SERIES
 
Pseudepigraphas
nakungoja sibanduki hapa
 
Back
Top Bottom