Simulizi : Elizabeth Neville

Simulizi : Elizabeth Neville

SEHEMU YA 49

" Fantastic!!!, Big up Mwanasheria mlevi kwa ugunduzi lazima tuingie humu"

"Hallo, Inspekta Jasmin bado upo hewani, njooni haraka sana Sabasaba" Daniel alisema.

Jasmin hakuwa na haja ya kuuliza kulikuwa na nini? Alikuwa amesikia kila kitu katika simu yake.

"Dokta Yusha twende Sabasaba fasta" Jasmin alisema.

"Kuna nini?" Dokta Yusha aliuliza.

"Nitakusimulia njiani"

Dakika kumi tu zilitosha kuwafikisha wakina Jasmin Sabasaba. Waliungana na wakina Daniel kuanza kuichunguza chemba ile ambayo Mwanasheria mlevi aligundua kwamba ilikuwa ni njia ya kuelekea chini ambapo bila shaka kulikuwa na handaki.

"Sasa yatupasa tuingie hapa. Maana tumejaribu kuchunguza maeneo ya jirani labda njia hii itakuwa imetokea mahali lakini hatujaona. Inaonesha ni njia ya chini iliyoenda mbali kidogo. Lazima tuingie tukawakamate hawa wanaharam" Daniel alisema.

"Tuingie wote?" Mwanasheria mlevi aliuliza. " Vipi kuhusu msako wa kumsaka Elizabeth Neville huku juu? Kwanini wasiingie wachache na wengine waendelee kumsaka Elizabeth? "

"Come on Mwanasheria! Bila ya shaka hawa watu ndio watakuwa wamemteka Elizabeth Neville pale hospitali. Tukienda na kuwaangamiza hawa tutakuwa tumemwokoa na Elizabeth. Tuingie tu humu tukaumalize mchezo" Jasmin alisema.

"Mpo kamili?" Daniel aliuliza. " Hatujui tunaenda wapi? Tunaenda kupambana na watu wa aina gani? Na wapo wangapi? Tunaenda kuweka rehani roho zetu kwa ajili ya Taifa letu. Wahitajika umakini mkubwa sana, kosa lolote lile haliruhusiwi, marufuku kufanya hata kosa dogo sana" Daniel alimalizia kwa kuonya.

Wote waliitikia kwa kichwa na kuanza kuingia kwenye lile shimo ambalo lilielekea kusikojulikana.

Mwanaume, Daniel Mwaseba ndiye alitangulia kuingia mle shimoni. Baada ya kuufunua mfuniko wa pale juu walikuta ngazi ambazo zilithibitisha hisia za Mwanasheria. Lile halikuwa shimo la kawaida. Daniel alishuka zile ngazi taratibu huku akiwa ameishika imara bastola yake kwa mkono wa kulia. Alikanyaga ngazi ya kwanza, kisha ya pili na Dokta Yusha nae akiwa na begi lake mgingoni akifuata nyuma yake. Na bastola yake iliyojaa risasi ikiwa kaishikililia kwa mkono wa kulia. Wakati Daniel anaikanyaga ardhi ya kule chini huku juu Mwanasheria mlevi ndiye aliyekuwa anaingia akiwa ametanguliwa na askari makini wa kike, Inspekta Jasmin. Mwanasheria mlevi kwa mkono wake wa kushoto alikuwa ameishikia bastola yake tayari kwa lolote lile. Dakika nne baadae wote waliikanyaga ardhi wakiwa shimoni. Kote kulikuwa na giza totoro.

Daniel aliitoa kalamu ndogo katika mfuko wake wa shati. Aliibonyaza. Mwanga mkali ulimulika kule chini. Ile kalamu ilikuwa ni kalamu ya ajabu sana. Kalamu iliyokuwa imetengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu huko nchini Urusi.
 
SEHEMU YA 50 - 54

Kule chini kulikuwa na njia moja tu iliyoelekea upande wa kulia. Wote wanne wakitanguliwa na Daniel Mwaseba walianza kuifuata njia ile. Kila mmoja akijaribu kumlinda mwenzie. Walikuwa wanaenda taratibu katika njia nyembamba iliyotengenezwa kwa ufundi mkubwa. Ilikuwa kimya, kila mmoja akiwaza lake moyoni.

Walitumia dakika arobaini na tano wakiwa wanatembea katika njia ile nyembamba. Wote walishangaa urefu wa njia ile. Kwa makadirio yao walijua kwamba walishatoka eneo la Sabasaba. Na bado mbele njia ilikuwa bado inaelekea mbele. Walizidi kutembea huku hofu ikianza kuwaingia moyoni mwao. Walianza kuhisi kwamba walikuwa wanaelekea katika kifo!!

Dakika kumi na tano baadae ile njia ilianza kuwa pana kidogo. Sasa walikuwa wanauweza wa kupita wakiwa sambamba wawiliwawili. Hivyo Daniel Mwaseba alikuwa bega kwa bega na Dokta Yusha na Mwanasheria mlevi alikuwa bega kwa bega na Inspekta Jasmin.

"Yaonesha twakaribia kufika walipo hawa majamaa. Umakini wahitajika zaidi" Daniel alinong'ona kwa sauti ndogo iliyosikiwa na wote.

Walitembea kama dakika tatu tangu onyo lile la Daniel.

Ghafla!! katikati ya ile njia kulikuwa amesimama mtu mwembamba aliyekuwa amevaa nguo nyeusi tupu. Alikuwa mithili ya kivuli, juu shati jeusi, chini suruali nyeusi na juu kofia nyeusi. Alikuwa amesimama upande huku akiwa ameushika ukuta kwa mkono wake wa kulia. Alikuwa anawatazama wale askari wanne akiwa kimya. Daniel Mwaseba alikuwa ndiye wakwanza kumuona mtu yule. Hakustuka.

Alilitegemea hilo. Waliendelea kusonga mbele. Yule jamaa nae akaanza kupiga hatua kuwafuata, walikutana katikati.

Hawakuongea.

Daniel alirudi nyuma na kalamu yake ikiyotoa mwanga mkali eneo lile lote. Ile nafasi yake pale mbele ikachukuliwa na Inspekta Jasmin. Na Inspekta Jasmin hakuuliza alipokuwa tu sambamba na Dokta Yusha pale mbele. Alimuelekezea bastola yule jamaa huku akiongea kwa sauti kubwa.

"Nyoosha mikono juu mbwa wewe!! Upo chini ya ulinzi!!" Inspekta Jasmin aliamrisha. Lakini hakusikilizwa.

Jamaa bado alikuwa anawafata huku akiwa kimya.

"Unaelewa unachoambiwa wewe??" Dokta Yusha nae alidakia.

Jamaa mweusi alisimama wima. Akawaangalia askari wale wanne kisha akasema...

"Karibuni sana shimoni" Jamaa alitamka maneno yake ya kwanza.

"Acha jeuri. Huu ni mwisho wako wewe na wanaharamu wenzako. Na tunaanza na wewe" Dokta Yusha alisema.

Daniel Mwaseba alikuwa pembeni akimwangalia mtu yule aliyekuwa akijiamini sana. Alikuwa anamwangalia chini hadi juu.

Aligundua kitu.

Alikumbuka nchini Cuba.

Na muda huohuo Inspekta Jasmin aliachia risasi katika bastola yake iliyoelekea moja kwa moja katika utosi wa jamaa mweusi. Jamaa haikumdhuru kabisa ile risasi, ilipita pale utosini huku ikiacha shimo dogo lisikokuwa hata na chembe ya damu. Askari wote watatu walibaki midomo wazi wakiwa hawaamini, kasoro Daniel Mwaseba tu aliyekuwa akitabasamu.

"Mzimuuuu!!" Jasmin alipiga kelele.

Ghafla yule mtu mweusi alirusha teke lilimpata dokta Yusha kifuani. Alisukumwa kwa nguvu na uzito wa teke lile na kujigonga vibaya ukutani. Inspekta Jasmin na Mwanasheria mlevi walianza kurudi nyuma kwa woga huku yule jamaa akiwafata taratibu huku akicheka. Kwa kasi yule jamaa alirusha mateke mawili yaliyowapata wale maaskari wawili sehemu ya kifua. Wote walianguka chini wakigumia kwa maumivu.

Dokta Yusha akiwa pale chini karibu na kingo ya ile njia alitoa bastola yake na kumuelekezea yule jamaa. Jamaa hakuwa hata na chembe ya hofu na ile bastola. Risasi tatu za moto zilitua katika tumbo za jamaa mweusi. Risasi zile ziliacha matundu matatu tumboni lakini bado yakimuacha yule jamaa mweusi akiwa kasimama wima. Imara kabisa.

"Mnajisumbua, mnaharibu bure risasi zenu. Sifi kwa risasi za binadamu mimi" Jamaa mweusi alisema kwa majigambo.

Daniel Mwaseba akiwa pale pembeni na kalamu yake mkononi alikuwa akiyasikia yote yale na kuona matendo ya yule jamaa mweusi.

Jamaa mweusi alimsogelea Inspekta Jasmin ambaye alikuwa katika harakati za kuinuka pale chini. Alimshika shingoni kwa nguvu na kumpeleka ukutani akiwa kawapa mgongo wakina Daniel. Hiyo ndiyo nafasi pekee ambayo Daniel Mwaseba alikuwa anaitafuta.

Kwa kasi Daniel Mwaseba alimfata yule jamaa na kuchomoa kifaa kidogo kilichokuwa mgongoni mwa yule jamaa kwa nguvu. Ghafla jamaa mweusi alimuachia Inspekta Jasmin pale shingoni na kudondoka chini.

Ulikuwa ndio mwisho wake.

"Ni nini umefanya Daniel?" Mwanasheria mlevi aliuliza akistaajabu.

"Yule sio mtu, ni machine!! Nimewahi kukutana nayo machine kama ile nchini Cuba. Nilikuwa nimeenda

Cuba miaka mitano iliyopita kurudisha nyaraka za siri zilizoibwa na jasusi kutoka Cuba ndani ya Ikulu ya Dar es salaam kipindi cha utawala cha rais Kazulu. Zilikuwa nyaraka muhimu sana kwa usalama wa nchi yetu. Jasusi wa mweusi mwenye asili ya Cuba alipandikizwa katika idara yetu ya usalama wa Taifa na kuweza kuziiba nyaraka hizo za siri. Nilitumwa mimi na rais Kazulu kwenda Cuba kuzirejesha nyaraka zetu. Ilikuwa misheni ngumu zaidi kuwahi kuifanya.

Nakumbuka nilipambana sana nami kufanikiwa kufika hadi Ikulu ya Cuba mahali ambapo zilifichwa nyaraka hizo. Haikuwa kazi ndogo hata kidogo, hadi nafika katika mlango wa chumba ambacho nyaraka za siri zilikuwa zimewekwa nilikuwa hoi bin taaban. Nimechoka kwa mapambano. Nikiwa mikono mitupu bila silaha yoyote ile. Ndipo nilipokutana na machine baada tu ya kufungua mlango. Alikuwa kama huyu mkiyepambana nae leo.

Sasa mimi nilikuwa peke yangu bila silaha huku nikiwa nimechoka baada ya kupambana na makomandoo wa Cuba wakiozilinda nyaraka zile kwa nguvu zao zote. Na kwa bahati mbaya sana nilikutana na machine bila ya kujua kwamba alikuwa ni machine.

Ilikuwa ni balaa!!!

Tulipigana kwa muda wa saa tatu mfululizo. Machine alinifanya niwe nyang'anyang'a. Nilijaribu kila mtindo wa mapigano lakini bado machine alisimama imara na kukabiliana na mimi. Mpaka nilipomchoma bomba ya kifua na kuacha tundu tu ndipo nilipogundua kuwa hakuwa binadamu. Alikuwa machine. Sasa ikanipasa kutumia akili badala ya nguvu. Nikaacha kupiga na kukwepa zaidi. Huku nikitafuta udhaifu wa ile machine. Kuna muda nilimpiga roba kwa nyuma, ndipo nilipoiona betri ndogo mgongoni mwake. Niliichomoa kwa nguvu, na machine ilidondoka chini. Nilisaka mle ndani na kufanikiwa kupata nyaraka. Nyaraka muhimu sana hapa nchini, nyaraka za 001!!! Daniel alielezea kwa kirefu.

"E bwana wee!! Zilikuwa zinahusu nini hizo nyaraka?" Mwanasheria mlevi aliuliza huku akiuhusudu uwezo wa Daniel Mwaseba.

"Katika misheni ile nilipewa marufuku ya kutozifunua zile nyaraka. Ni nyaraka nyeti sana hivyo nilisisitiziwa kutozisoma. Nilizirudisha nchini bila kuzisoma kama nilivyotakiwa na rais wa kipindi kile" Daniel Mwaseba alisema.

"Daniel we kiboko!!" Dokta Yusha alisema kwa hamasa.

"Niwaambie kitu?" Daniel aliuliza.

"Twambie" Wote walijibu.

Pamoja na kupambana kwa nguvu sana lakini juhudi zangu zimeenda bure. Nyaraka ya 001 zimepotea tena Ikulu!!"

"Heee ilikuwaje hadi zikapotea tena?" Mwanasheria mlevi aliuliza.

"Mapenzi, mapenzi ndiyo sababu. Cuba hawakukata tamaa pamoja na kuzipoteza nyaraka zile. Walidhamiria kuzirejesha zile nyaraka. Ndipo wakamtuma jasusi hatari wa kike kuja kuzisaka zile nyaraka. Bila kujua rais Dr Joseph akaingia mkenge, alianzisha uhusiano na yule mwanamke aliyekutana naye katika uwanja wa Taifa. Cuba walifanya hila zao na kuhakikisha huyo jasusi wa kike anapata nafasi ya kuwa mhudumu wa rais katika sherehe za Uhuru. Na kwa kutumia hila za kike na udhaifu wa wanaume dhidi ya wanawake rais Dr Joseph akazidiwa ujanja na kujikuta akianzisha uhusiano na yule jasusi wa kike. Alidhani dhamira ya mwanamke ni mapenzi na pengine pesa. Hakujua. Mwanamke alitumwa kuzisaka nyaraka za 001. Nyaraka nyeti na za siri sana kwa Taifa letu" Daniel Mwaseba alieleza.

"Aisee kumbe nchi ina mambo ya siri sana ambayo sisi wengine hatuyajui. Ndo nasikia leo habari kuhusu hizo nyaraka. Wananchi pia bila shaka nao hawaelewi, maana wao wanahangaika tu na habari za kina Dokta Luis Shika" Mwanasheria mlevi alisema.

"Jasusi wa kike alifanikiwa kuziiba nyaraka za 001. Na ni yeye huyohuyo alifanikisha wizi mkubwa wa dhahabu huko Geita. Cha kushangaza sasa. Alitoa taarifa kabla kwa katibu mahsusi wa machimboni aitwaye Bertha Fidelis kabla wizi wa dhahabu haujatokea. Bertha nae alitoa taarifa serikalini lakini hazikupewa uzito unaotakiwa. Tani mbili za dhahabu zikaenda na maji.."

"Sasa usalama wa Taifa haukunusa kabisa harufu ya wizi huo. Na inamaana hadi leo hawajagundua kitu? Na vipi kuhusu hizo nyaraka?" Inspekta Jasmin aliuliza.

Idara ya usalama wa Taifa walianza kumsaka huyo jasusi kimyakimya ili wajue kuhusu wizi wa Dhahabu, huku ishu ya 001 ikiwekwa siri kwa watu wachache sana, kwakuwa kulikuwa na uzembe katika ngazi za juu, lakini hawakufanikiwa. Elizabeth Neville alikuwa kayeyuka mithili ya upepo. Walishindwa kazi, ndipo nikarudishwa mimi kutoka huko Faro, Ureno. kumsaka huyo jasusi wa kike. Maana rekodi zilionesha bado yupo hapahapa nchini, hakuwa ametoka nje ya mipaka yetu"

"Hivi mlisikia kifo cha Jane Munuo?" Daniel aliuliza " najua hakuna anayejua. Ninyi mmeletwa katika operesheni hii mkiwa hamjui chochote. Mnatumiwa tu na viongozi kwa maslahi yao.

Sasa baada ya kuiba nyaraka ya 001 ikulu jasusi huyo wa kike alianzisha uhusiano na Mheshimiwa Lucas. Najua mnajua kwamba kila mtu anajua Lucas ndiye atakuwa mrithi wa rais Joseph. Hivyo huyo jasusi alienda kwa Lucas sio kwa bahati mbaya, alienda kutafuta siri ambayo itawafanya wamwendeshe Lucas watakavyo pindi atakapokuwa rais. Ili wizi wa 001 uendelee kuwa siri. Rais ajaye asithubutu kusema wala kuhangaika kuisaka. Na walifanikiwa. Jasusi huyo alifanikisha Lucas kutekwa na kwenda kufanyiwa kitendo kibaya sana. Mheshimiwa Lucas aliingiliwa kinyume na maumbile na watu huku akirekodiwa, na hizo records anazo huyo jasusi wa kike.

Lakini pamoja na hayo yote huyo jasusi alizidiwa ujanja. Katika uhusiano wao Mheshimiwa Lucas alifanikiwa kuiba nyaraka za 001 kabla hazijasafirishwa kwenda Cuba..

Hapo ndipo shughuli ilianza. Jasusi wa kike alikuwa anazihitaji sana zile nyaraka, huku Lucas akiihitaji sana ile records.

Lakini jasusi wa kike alifanya ujanja.

Unajua sisi wanaume ni dhaifu sana kwa wanawake. Jasusi alimtumia mwanadada changudoa aitwaye Jane Munuo. Huyo ndiye aliyefanikisha kuibiwa tena nyaraka za 001 mikononi mwa Lucas na kuzirejesha kwa jasusi wa kike. Mheshimiwa Lucas alikasirika sana baada ya kugundua zile nyaraka zilikuwa zimeibwa na Jane Munuo. Alidhamiria kumuua!

Na alimuua kweli katika baa ya Hongera!

Bila kujua kwamba alikuwa anarekodiwa na mwandishi wa habari wa gazeti la udaku, Zulfa, wakati anafanya mauaji. Na wakati Zulfa akirekodi hakujua kwamba macho ya yule jasusi wa kike yalikuwa yanamwona pale Hongera baa. Hakufika nayo popote ile video ya mauaji aliyoyafanya Lucas. Maisha ya Zulfa yaliishia Sinza Madukani baada ya kusababishiwa ajari mbaya ya gari na yuleyule jasusi wa kike. Na ndipo alipotokomea na ile video pia. So huyo jasusi alikuwa na vitu vitatu vya siri sana, na alikuwa anatafuta njia ya kutoka nchini na kuelekea Cuba.

Hakufanikiwa.
 
SEHEMU YA 55

Ndipo hawa watu ambao hatujui wametumwa na nani wakamteka!!"

"Ni nani huyo jasusi mwanamke? Una picha yake? Sasa utamjuaje Daniel ili kuikomboa nyaraka ya 001?

" Dokta Yusha aliuliza kwa kupagawa.

"Misheni ya kusaka nyaraka za 001 kutoka kwa jasusi hatari wa kike ndio hii. Na huyo mwanamke, jasusi hatari wa kike aliyetumwa na serikali ya Cuba ndiye anayeitwa ELIZABETH NEVILLE!!!" Daniel Mwaseba alisema.

"Wee! Daniel..unasema kweli? Inamaana, yaani..sijakuelewa Daniel, Elizabeth Neville? Yaani...." Mwanasheria mlevi alishindwa kuongea.

"Ninyi mmeingia kwenye misheni hii kwa bahati mbaya tu. Aliyewatuma ndio anajua kwanini anamsaka Elizabeth Neville. Ishu ya Elizabeth Neville ni kubwa sana tofauti kabisa na mnavyofikiria. Mtu asiye sahihi kuzipata nyaraka za 001 ni hatari sana kwa nchi yetu. Hatari kuliko neno hatari linavyomaanisha!!!!!" Daniel Mwaseba alisema.

"Ni kweli Daniel. Lakini wewe na Elizabeth Neville si wapenzi?" Inspekta Jasmin aliuliza.

"Ha ha ha umeanza wivu Jasmin" Daniel alisema huku anacheka.

Askari wanne walisonga mbele wakiwa na nguvu mpya sasa. Habari ya Daniel Mwaseba ya huko nchini Cuba iliwasisimua sana. Walijiona wana dhima ya kuhakikisha nyaraka za 001 haziendi katika mikono michafu. Kalamu ya Daniel iliendelea kuwapa mwanga katika safari yao ya kusonga mbele. Walitembea dakika kumi tu ndipo lilipotokea jambo la kushangaza. Kifusi kilianza kujifunika kule walipokuwa wanatokea.

"Daniel kifusi kinashukaaa!!!" Inspekta Jasmin alisema kwa nguvu huku akiwasukuma wakina Daniel kwa pupa. Bila kushangaza nao walianza kukimbia kuokoa roho zao. Dakika kumi tu kila kitu kilibadilika mle shimoni. Mbio zikaanza huku mchanga ukioporomoka kutokea juu ukiwafata kwa kasi!!

"Tunakufa jamaniiii, tunakufaaaa" Inspekta Jasmin aliendelea kupiga kelele.

"Kelele Jasmin!!" Daniel alisema kwa ukali.











Tunakufa jamaniiii, tunakufaaaa" Inspekta Jasmin aliendelea kupiga kelele.

"Kelele Jasmin!!" Daniel alisema kwa ukali.

Sasa zikawa mbio za kimyakimya bila makelele, miguno na pumzi zilisikika wakati askari wale wanne wakijitahidi kuokoa maisha yao.

Kile kifusi hakikuwa upande wao. Sasa kiliwafuata kwa kasi na kiliwakaribia, ilibaki miguu kama sita tu ya mtu mzima kabla haijawafikia. Dakika saba za kukimbia mbio za fadhaa zilikuwa zinafikia ukingoni.

"Ongezeni mwendo hali ni ya hatari!!" Hatari alisema kwa nguvu akiwa amegeuka nyuma. Askari walijitahidi kuongeza mbio, lakini wapi....Hali ya vumbi ilikuwa mbaya sana kwao, walianza kuishiwa pumzi na mwendo ukapungua.

"Ndo nakufa mimi maskini Jasmin. Nakufa kifo kibaya sana jamanii" Hayo ndio yalipita kichwani kwa Jasmin. Hali ilivyokuwa ilikuwa dhahiri kifo kilikuwa kinawakaribia. Askari wote waliingiwa na hofu, isipokuwa Daniel Mwaseba.

Sasa kifusi kilikuwa hatua tatu tu nyuma yao. Askari walizidi kukimbia, lakini matumaini yakiwa yameisha kabisa moyoni mwao.

"Wote ruka mbele kwa nguvuuuuu" Daniel alisema huku mwenyewe akijirusha kwa mbele. Na askari wengine wote walijirusha mbele.

Kukawa kimyaaaa...

***

ITAENDELEA

BURE SERIES
SIMULIZI
 
Noma mwanangu
hatariiiii
emoji91.png
emoji91.png
emoji91.png
 
SEHEMU YA 56

Huko ndani shimoni ilikuwa ni makelele. Wakina Felix walikuwa na furaha isiyo na kifani. Waliamini kwamba wamewamaliza maadui zao kwa kufukiwa na kifusi cha mchanga.

"Kazi nzuri sana, tumewamaliza wale marhuni waliotukurupusha kule Sabasaba" Sam alisema.

"Ni kweli yatupasa kujipongeza. Lakini lazima tujiulize mara tatu, wale watu waliwezaji kupita kwa machine? Machine kawahi kushindwa mara moja tu huko Cuba alipopambana na Jasusi wa Kimataifa. Leo hii hawa wapuuzi wameweza sana. Yaani lazima tujitathmini tena" Felix alisema.

"Ni kweli Felix. Ngoja tumalize hii shughuli kisha tutoe tathmini yetu. Sasa lazima tuweke akili zetu katika kuimaliza hii shughuli" Sam alisema.

" Nini kifuatacho sasa?" Richard aliuliza.

"Lazima tumsake Elizabeth Neville kwa mara nyingine tena. Waliomteka ni wale ambao tushawauwa kwenye kifusi. Twendeni tukawafukue ili tupate chochote katika maiti zao ili iwe njia ya kutupeleka kwa Elizabeth Neville" Sam alisema.

"Ni wazo zuri sana, twendeni" Felix alisema.

Watu saba wakielekea kule katika njia ya kuingilia shimoni. Kwenda kuzikagua maiti za wale wavamizi.

Wakina Daniel walikuwa wameangukia katika uwanda mpana. Kule kujirusha katika hatua ya mwisho ndio ilikuwa usalama wao. Njia ya handaki ilijengwa kwa kanda tofauti, kujirusha kule kuliwatoa kutoa katika kanda moja kwenda katika kanda nyingine, walitoka katika sehemu ambayo ilikuwa inalindwa na machine ambayo wakina Felix waliamua kuisambaratisha kwa kuiporomosha na kifusi yote.

"Tumepona, tumepona aisee, ilikuwa tufe yaani daah" Jasmin alisema huku akijifuta vumbi.

"Tuna bahati sana. Nimefanya kazi nyingi sana ambazo huwa zinanifanya nikikaribie kifo lakini leo hii ilikuwa ni hatari zaidi. Yaani ujanja wote uliniisha daaah" Mwanasheria mlevi naye alisema huku akijipangusa vumbi usoni.

"Daniel wewe ni kiongozi. Umetuongoza vizuri sana katika kukikimbia kifo cha kufukiwa na mchanga. Bila wewe hakika tunge..."

Wakati Dokta Yusha akiendelea kuongea ghafla peni ndogo ya Daniel ilitoa mlio huku ule mwanga ambao ukitumika kuwamulikia ukizimika na kuwaka mara tatu.

"...wanakuja!!" Daniel alimkatisha Dokta Yusha. " Wanakuja hawa wanaharam. Tujipange kupambana nao. Ni kufa au kupona" Daniel alisema huku akiwaangalia kwa zamu wale maaskari watatu.

Askari wote wakajipanga imara. Kila mmoja alikaa nyuma ya nguzo wakiwa na bastola zao. Walikuwa katika eneo pana lenye zaidi ya mita mia tano. Likiwa na nguzo kadhaa zilizoelekea juu. Daniel aliizima tochi katika peni yake. Ukabaki mwanga hafifu wenye kuwezesha kuona. Hakukuwa na giza sana kama kule walipotoka.

"Kila mmoja aweke kifaa cha mawasiliano sikioni kwake. Tutakuwa tukiwasiliana kwa njia hiyo" Daniel alisema kwa nguvu kidogo. Na askari wote watatu walimtii.

"Tayari" Jasmin alisema na Daniel na wengine wote walimsikia kupitia vifaa vyao vidogo vikivyoning'inia sikioni.
 
SEHEMU YA 57

"Nami tayari" Dokta Yusha nae alisema.

"Nami tayari, mnanipata?" Mwanasheria mlevi aliuliza.

Wote walisikiana. Ikimaanisha kila kitu kilikuwa sawa.

"Wanakuja wale kule mbele" Daniel alisema kwa sauti ndogo.

Watu saba walikuwa wanakuja bila wasiwasi wowote ule. Walikuwa wanaamini wavamizi wao walikuwa wameuwawa katika kifusi. Kumbe haikuwa hivyo.

"Tulifanya jambo zuri sana ingawa tulikuwa na udhaifu" Felix aliyekuwa ndio kiongozi wa wale watu saba alisema.

"Kwanini?" Richard aliuliza.

"Unajua alam ya kutustua kwamba machine amesambaratishwa imelia saa moja baada ya machine kuuwawa. Hii ni hatari sana. Mtu angeweza kuiuwa ile machine na kusonga mbele kutufikia tulipo, sijui kwanini hawa walichelewa kutufikia"

"Daah kumbe ndo mlifanya kosa kubwa hivyo? Kwanini sasa?" Richard aliuliza.

"Zamani ilikuwa inalia kwa haraka. Lakini ilikuwa inatakiwa kuupdate kila baada ya mwezi, jambo ambalo tulipitiwa kabisa kufanya" Felix alisema.

"Sasa hawa watu tutawakuta kweli?" Richard aliuliza.

"Tutawakuta. Ingekuwa wametoka ule ukanda ukiolindwa na machine wangekuwa wameshatufikia. So bila shaka kifusi kiliwafukia"

"Ahaa ni kweli. Kwa umbali huu ingekuwa washafika kule" Zungu alisema.

"Lakini hawa jamaa walijuaje kama tulikuwa tunaishi pale Sabasaba na kuja kutulipua? Ile ilikuwa ni nyumba ya siri ambayo ni vigumu sana kwa mtu yeyote yule kuihisi. Yatupasa kujitathmini upya" Felix alisema lakini hakujibiwa.

Muda uleule watu wake wanne walipigwa risasi nne kila mmoja ya utosi na kuanguka chini mithili ya mizigo. Harakaharaka Felix, Richard na Zungu, kila mmoja alijificha nyuma ya nguzo huku wakitoa silaha zao.

"Good job. Sasa wahitajika umakini zaidi. Kumbukeni tunamwitaji mmoja akiwa hai" Daniel alinong'ona huku akisikiwa vizuri na wale askari watatu.

"Tunashambuliwaaa" Felix alisema simuni akimtaarifu Sam.

"Na nani tena? Wamekuja wengine? Sam aliuliza.

" Walewale wahuni, washaangusha watu wetu wanne" Felix alisema.

"We Felix? Watu wanne? Imewezeka..." Sam hakumaliza alichotaka kusema. Milio ya risasi ilisikika mfululizo. Yule jamaa mwengine aitwaye Zungu alifanya kosa moja kubwa sana. Alihama nguzo kutoka nguzo aliyokuwa kwenda nyingine ili kujipanga vizuri. Risasi kutoka katika bastola ya Daniel Mwaseba ilichana vibaya sana katika kifua cha yule jamaa. Damu ziliruka hovyoooooo! Na wakati huohuo Richard alianza kushambulia kwa fujo kuelekea katika nguzo aliyokuwa amejificha Daniel. Risasi hizo ndizo zilizokatisha simu ya Felix. Naye alitupa simu chini na kupiga risasi kuelekea katika ile nguzo ya Daniel Mwaseba. Katika nguzo aliyosimama Mwanasheria mlevi ambayo ilikuwa kwa pembeni kidogo, jicho lake lilitua katika goti la Richard lilijitokeza kidogo katika nguzo. Mwanasheria mlevi aliitumia nafasi ile kwa kulenga bastola.

Akafyatua!!!
 
SEHEMU YA 58

Richard alirushwa juu na kujitupa chini kwa nguvu huku akipiga kelele za maumivu. Bastola akiwa kaitupa mita chache pembeni yake. Pigo lile lilimstua sana Felix. Alikoma kupiga hovyo na kubaki amekaa kimya. Huku akitweta na jasho likimtoka.

"Dokta Yusha msogelee, wewe upo katika engo nzuri hapo" Daniel alisema katika kile kifaa.

Dokta Yusha alipiga hatua kutoka nguzo moja kwenda nyingine kuelekea kule alipokuwa Felix.

"Tunaomba ujisalimishe kijana kabla hatujakuuwa. Hauna ujanja tena" Daniel Mwaseba alisema.

Felix aliisikia ile sauti lakini hakutekeleza. Bado alijificha huku bastola yake ikiwa mkononi.

"Felix, Felix unanipata?" Ile simu pale chini iliendelea kuita. Felix alikaa kimya.

Dokta Yusha ambaye alikuwa upande ambao Felix hakuwa na umakini nao alisogea tena. Yeye Felix bastola yake ilikuwa palepale katika nguzo aliyokuwa Daniel, akiamini pale ndipo adui wake alipo.

Alikosea.

"Namwona na nampata hapa vipi nimshoot" Dokta Yusha aliuliza.

"Mshoot!!, Tutamtumia yule jamaa aliyempiga Mwanasheria mlevi mguuni" Daniel alitoa amri.

Dokta Yusha alilenga vizuri shabaha ambapo sehemu ndogo ya mbavu alikuwa anaiona. Akabonyaza trigaa.

Huo ndio ulikuwa mwisho wa Felix. Risasi ilivunja vibaya sana mbavu za Felix. Damu ilimwagika.

Askari wanne walisogea mbele kuelekea pale alipokuwa amelala Richard akiugumia kwa maumivu. "Mfunge hilo jeraha likome kutoa damu" Daniel alisema. Dokta Yusha alifanya kazi hiyo kwa ufanisi mkubwa sana. Huku moyoni akimwangalia kwa hasira mtu yule aliyetaka kunkata uume kwa kisu cha moto. Dakika mbili tu zilitosha kuisimamisha damu ile.

"Tuondokeni hapa siyo mahali salama" Richard alisema kwa uchungu.

"Twende wapi mbwa wewe!! Tumekuja kuteketeza kila kitu hapa! We si ulijitia mtesaji!! Utajuta leo!!" Dokta Yusha alisema kwa hasira.

"Hawa watu sio watu wazuri, watakuja kutuua sasahivi hapa" Richard aliendelea kulalama bila kumjari Dokta Yusha.

"Anatuchezea mchezo" Daniel aliwaza.

Ghafla risasi moja ilipita pembeni kidogo kwa kichwa cha Richard. Askari wote walilala chini huku wakijipanga kwa mashambulio.

"Lala watakuuwa!" Daniel alimwamrisha Richard naye akatii. Alilala huku akijisogeza kujificha kwa kutumia ile nguzo.

Askari wote wanne walitembea kwa kutumia matumbo yao kuzifuata nguzo ili kujilinda. Kila mmoja alikaa sehemu sahihi na kutafuta wapi alipo adui.

Kulikuwa kimyaa.

Askari walikaa kimya vilevile dakika tano. Hakikutokea kitu.

"Kila mmoja asake kwa macho na hisia mahali alipo adui" Daniel alisema.

Kila mmoja akafanya kazi hiyo. Lakini bado kulikuwa kimya.
 
SEHEMU YA 59

Daniel akaitoa peni yake iliyokuwa mfukoni. Peni ilikuwa imetulia tuli ishara kwamba hakukuwa na hatari yoyote. Daniel alibonyaza ile peni. Aligundua kwamba ilimtaarifu wakati wale watu wanakuja lakini hakusikia. Bila shaka kutokana na kelele za mashambulizi. Lakini sasahivi peni ilikuwa haioneshi hatari yoyote. Bila shaka wakina Sam walikuwa hawapo maeneo yale.

"Jamaa itakuwa wamekimbia, hawapo kabisa katika mazingira haya" Daniel alisema.

"Kifuatacho nini sasa Daniel?" Jasmin aliuliza.

"Tusubiri kidogo kama dakika mbili" Daniel alisema.

"Jamaa itakuwa alikuja kwamwangamiza yule majeruhi, na baada ya kushindwa bila shaka kaamua kukimbia" Mwanasheria mlevi alisema.

"Ndiyo, jamaa alikuja kupoteza ushahidi" Dokta Yusha alidakia.

"Huyu jamaa ni nani? Yupo nao lakini inaonesha si mmoja wao. Si mmesikia hata kauli zake" Mwanasheria mlevi alisema.

"Ni monster huyo!!" Dokta Yusha alisema kwa ukali. Bado kumbukumbu za akichotaka kufanywa na Richard zilikuwa kichwani mwake.

Dakika mbili ziliisha na hali ilikuwa ileile.

"Jamaa wametoweka, twendeni kwa yule jamaa" Daniel alisema.

Askari wote wanne kwa mwendo wa kunyata. Silaha zao zikitangulia mbele walielekea pale Richard alipokuwa amelala. Richard aliwaangalia watu wale kwa macho ya kukata tamaa.

" Mpe sapoti ya kutembea Dokta Yusha " Daniel alisema bila kujari uhasama wao.

Dokta Yusha alimnyanyua yule majeruhi kwa hasira na kuweka mkono wake begani kumsaidia. Askari wote wakiwa makini na silaha zao mbele walianza kusonga mbele.

"Watakuwa wamekimbia" Richard alisema.

"Ni wakina nani?" Daniel aliuliza.

"Gon na boss Sam" Richard alisema.

"Goon! shabash! Gon kaja Mafinga?" Daniel aliuliza kwa hamaki.

"We jamaa" Richard akamwangalia Daniel kwa kumstaajabu. " Inamaana unamjua Gon? Nyi ni wakina nani hivi?" Richard aliuliza.

Daniel hakujibu. Waliendelea kwenda mbele hadi wakafika mahali ambapo walikuwa wanaishi wale jamaa.

"Hapa ndipo tukipoishi, wamekimbia wakina Gon" Richard alisema.

"Sasa yatupasa tutoke nje. Isije wakatuzika humu. Jamaa waitwa nani?" Daniel Mwaseba akimuuliza yule majeruhi.

"Naitwa Richard" Alijibu.

"Ok Richard tuoneshe njia ya kutoka humu ya haraka. Hawa jamaa wakitoka nje wanaweza kutuzika humu" Daniel alisema.

"Ok twendeni ule upande wa mashiriki ndio kuna njia ya dharura, njia kuu kwa vyovyote itakuwa imeshazibwa" Richard alisema.

" Twendeni mashariki" Daniel alisema.

Wote watano waliekekea upande wa mashariki ambapo kulikuwa na mlango wa dharura kutoka nje. Iliwachukua dakika kumi kufika katika lango la mashariki. Walifunua mfuniko ni kutoka nje. Walikuwa duniani. Ilikuwa ni pambezoni mwa ukumbi wa sherehe wa Mam ukumbi unaomilikiwa na J.J Mungai.

"Aisee tumetoka Sabasaba mpaka Pipeline. Hili handaki ni refu sana" Dokta Yusha alisema.
 
Back
Top Bottom