Simulizi : Elizabeth Neville

Simulizi : Elizabeth Neville

SEHEMU YA 60

"Ni refu sana. Kule lango kuu unatembea zaidi ya saa nusu saa na kutokea pembezoni mwa kambi ya jeshi. Hawa jamaa hatari sana" Richard alisema.

"Twende nyumba ya kulala wageni mbele ya Marie supermarket market. Tuone tunajipangaje" Daniel alishauri.

Haikuwa mbali hiyo nyumba ya kulala wageni akiyoizungumzia Daniel. Dakika saba tu walikuwa wamechukua chumba katika nyumba ya kulala wageni yenye hadhi ya chini.

"Dokta Yusha mtibie vizuri Richard, nitakuwa na mazungumzo naye marefu baadae" Daniel alisema.

"Naitwa Richard kama nilivyokwambia awali" Richard alianza kuelezea baada ya kuhudumiwa vizuri na Dokta Yusha. "Mimi ni mtoto wa mjini ninayeishi kwa kufanya uchunguzi na upelelezi binafsi kwa watu mbalimbali na kampuni. Mimi ni Richard Philipo yule wa Mkanda wa Siri.."

"Kumbe ndio wewe wa Mkanda wa Siri? Nilikisikia vizuri kisa kile nikiwa nje ya nchi. Mlifanya mambo makubwa sana wewe na wakina Martin Hisia. Kumbe ni wewe?" Daniel alisema kwa furaha.

"Ni mimi, na nishafanya misheni nyingi sana za hatari tofauti na ile, lakini nakiri kwamba hii misheni ni hatari kuliko zote hizo" Richard alisema.

"Hebu twambie, uliingiaje katika misheni hii? Na hii misheni inahusu nini hasa?" Daniel aliuliza. Askari wote walikuwa kimya wakimsikiliza Richard.

"Siku moja nilipigiwa simu na Zaidi Kalinga, ambaye kwa sasa ndiye mkuu wa jeshi la Polisi Tanzania. Zaidi alinambia kwamba kuna misheni ya kufanya huko Mafinga. Nilikubali bila ya kuuliza misheni inahusu nini? Misheni mimi ndio kazi yangu hivyo sikupaswa kuuliza inahusu nini? Nilisubiri maelekezo tu. Zaidi alinambia kuna mwanamke mmoja wamemshikilia lakini huyo mwanamke alikuwa hataki kusema lolote lile watakalomuuliza. Hivyo kazi yangu ilikuwa kuja kumtesa ili huyo mwanamke aseme" Richard alisema.

"Kwahiyo wewe ulikuja kwa kazi ya kutesa tu, na je ulifanikiwa?" Daniel aliuliza.

"Hapana, nikiwa katika hatua za mwanzo tu za mateso lilitokea jambo ambalo wao waliliona la ajabu sana. Lakini si kwangu, mlipuko ule haukuwa ajabu hata kidogo kwangu"

"Kwanini kwako haukuwa ajabu?" Dokta Yusha aliuliza.

Kwanini kwako haukuwa ajabu?" Dokta Yusha aliuliza.

"Tulipanga shambulio lile na wakina Martin. Mimi ndiye niliyeuza ramani kwa kina Martin wapi tulipo. Na tulipanga waje kwa namna ili kumchukua yule mwanamke. Ambaye Martin alinambia amepewa kazi na Mheshimiwa Lucas kumtafuta. Siku zote siwezi kufanya kazi tofauti na Martin, tumetoka mbali sana, hivyo nilichagua kuwasaliti wakina Sam, nilimsaliti pia Mheshimiwa Zaidi Kalinga" Richard alisema.

"Sasa Richard huyo mwanamke yupo wapi kwasasa?" Mwanasheria mlevi aliuliza.

"Elizabeth Neville bila shaka yupo mikononi kwa Martin Hisia na Binunu ambao wapo katika harakati za kumsafirisha kwenda kwa Mheshimiwa Lucas" Richard alijibu.
 
SEHEMU YA 61

"Richard unajua chochote kuhusu 001?" Daniel Mwaseba aliuliza swali jipya.

"We unajua kuhusu 001?" Richard naye aliuliza swali.

"Jibu swali Richard?" Daniel alibadilika.

"Najua kuhusu 001, hizo ni nyaraka za siri sana katika nchi hii. Siwezi kusema zaidi mpaka nijue kama ninyi ni watu sahihi kuwaambia" Richard alisema kwa kujiamini.

"Naitwa Daniel Mwaseba" Daniel alisema kwa mkato.

"Hee kumbe ndio Daniel wewe. Sijawahi kuwaza kukutana na wewe katika hizi kazi aisee" Richard alisema.

"Najua sasa ni wakati sahihi wakunieleza kuhusu 001" Daniel alisema.

Richard aliwaangalia wale wengine. Daniel akaelewa kuwa ana wasiwasi na wale " Huyo anaitwa Dokta

Yusha, yule pale ni Inspekta Jasmin na yule kule ni Mwanasheria mlevi. Wote ni askari polisi waaminifu"

"Ahaa wazee wa balaa" Richard alisema huku akicheka.

"Naam, haya Richard twambie kuhusu 001" Daniel alisema.

"Kwa mara ya kwanza nilisikia 001 wakati tupo katika operesheni ya mkanda wa siri. Ni Brown mzungu ndiye aliyetwambia kuhusu nyaraka hizo za siri zilizokuwa zinahifadhiwa Ikulu. Ni nyaraka za siri na ghali sana kuliko nyaraka zozote zile duniani. Brown alinambia thamani ya nyaraka hizo ukizipata na kwenda kuziuza kwa wanaozihitaji ulikuwa na uhakika wa kupata trilion 800. Mimi nilimbishia Brown, lakini alinihakikishia hivyo. Miaka mitano sasa imepita tangu nisikie 001 kwa mara ya kwanza. Nikaja kusikia tena 001 kutoka katika mdomo wa Zaidi Kalinga, alinambia huyu mwanamke aitwaye Elizabeth Neville alikuwa anazo hizo nyaraka. Hivyo aliniasa nimtese bila kumuua ili tuzipate nyaraka hizo."

"Zaidi Kalinga anajua kuhusu 001? Ulimhoji chochote kujua kwamba anazijuaje?" Daniel aliuliza.

"Ndio, nilimuuliza na alinisimulia. Unajua yeye na rais Dr Joseph ni marafiki sana, na wanashirikiana katika mambo mengi sana. Ni rais Joseph ndiye aliyemueleza Kalinga kuhusu uwepo nyaraka hizo Ikulu. Na wiki moja tu baada ya kumueleza ndipo nyaraka hizo zilipotea. Hivyo Kalinga alianza kuzitafuta nyaraka hivyo kivyake ili ziwe mali yake. Alizisaka kwa siri bila ya rais Joseph kujua. Ndipo kwa kumtumia Gon walifanikiwa kumkamata Elizabeth Neville akiwa katika harakati za kutoroka kwenda Zambia kupitia mpaka wa Tunduma. Kwa bahati mbaya walimkamata Elizabeth akiwa yeye mwenyewe bila ya kuwa na 001. Na hapo ndipo nilipotafutwa mimi ili kuja kusaidia" Richard alisema ukweli.

" Unajua nyaraka za 001 zinahusu nini?" Dokta Yusha aliuliza.

"Hapana, sifahamu ila nasikia ni nyaraka muhimu sana hapa duniani" Richard alisema.

"Sasa hivi yupo wapi Elizabeth Neville?" Daniel aliuliza tena.

"Nikiwasiliana na Martin nitajua" Richard alijibu.

"Sawa mpigie Martin tujue wako wapi?"
 
SEHEMU YA 62

Richard alichukua simu yako na kumpigia Martin Hisia.

"Naomba usiri wakati naongea na Martin Hisia" Richard aliomba.

Walimruhusu. Richard alielekea chooni kuongea na Martin.

Baada ya dakika kumi Richard alitoka.

"Tufanyeni haraka, wakina Martin wapo uwanja wa ndege Iringa wakiwa wanaelekea Dar kwa Mheshimiwa Lucas"

Harakaharaka wakina Daniel walijiandaa na kutoka katika ile nyumba. Waliekekea Iringa mjini kuonana na Elizabeth Neville.

***

Martin, Binunu na Elizabeth Neville walikuwa katika nyumba ya wageni pembezoni na uwanja wa ndege wa Iringa. Elizabeth akiwa bado amelala usingizi kutokana sindano ya usingizi aliyochomwa hospitali. Bado Martin na Binunu walikuwa hawajaisikia sauti ya Elizabeth Neville tangu wamkamate.

"Nimeongea na Richard, Binunu" Martin alianza kuongea. " Kanambia anakuja sasa hivi tumsubiri twende wote Dar, na kanisisitizia sana tusimwambie Mheshimiwa Lucas kama tumempata Elizabeth Neville" Martin alimaliza.

"Hee kwanini sasa usimwambie. Hi misheni imeshakwisha! Mpigie Mheshimiwa Lucas aje kumchukua mtu wake sasa tuchukue kesho na kuanza maisha mengine. Tukikaa kaa ngoma itakula kwetu hii" Binunu alisema.

"Nimemwambia yote hayo lakini Richard kaomba sana. Kasema Elizabeth Neville kuna kitu cha siri ambacho ni muhimu sana kwa sisi kukijua kabla hatujamkabidhi kwa Mheshimiwa Lucas" Martin alisema.

"Haina shida tumsubiri tumsikilize. Labda ana jambo muhimu kalipata huko kwa mabosi zake" Binunu akakubali.

Martin akamimina soda kwenye glasi na kunywa kidogo. Ila hii misheni imekuwa rahisi sana unajua. Yaani tumefanya kazi mbili tu rahisi, kulipua lile jumba la wale wendawazimu na kwenda kuwalaza askari wawili hospitali. Mzigo huu hapa " Martin alisema huku akimuonesha kidole Elizabeth Neville.

"Umezoea damu wewe Martin, yaani kuteketeza watu zaidi ya kumi na tano kwako ni misheni rahisi? Una matatizo wewe ha ha ha" Binunu alisema huku akicheka.

"Rahisi hii kazi Binunu. Kumbuka misheni zetu za nyuma hivi hii utaihesabia kweli?" Martin alisema.

"Ila hii misheni bado haijafika mwisho, hatujui Richard atakuja na lipi" Binunu alisema.

"Richard anataka kampani tu ya kwenda Bongo hana lolote hahaha " Martin alisema huku akicheka.

***

Sam, Gon, Dalton na Faustine walikuwa wamekaa katika ukumbi wa Saigon. Walikuwa wameizunguka meza iliyokuwa na maji manne makubwa ya Mufindi.

"Wale wahuni wametuweza kweli. Wametubomolea nyumba yetu tukiyoitegemea, wamempora

Elizabeth Neville na kutuvuruga kabisa kule shimoni. Mbaya zaidi wamemuua Felix na kumteka na Richard. Hii ndiyo sababu ya kuwatumia ndege Dalton na Faustine muwe hapa. Sasa kazi ni moja tu, lazima tumsake Elizabeth Neville hadi tumkamate. Awe hai, awe amekufa, awe amezirai ama amezimia, Elizabeth Neville ni muhimu sana kwetu. Tuichimbue Mafinga nje ndani, nyumba za kulala wageni zote, hospitali zote, baa zote na sehemu yoyote ile Elizabeth Neville atakapokuwa. Tumpate Elizabeth, tumpate Elizabeth, tumpate Elizabeth, tumpate Elizabeth, tumpate Elizabeth!!!" Sam alisisitiza.
 
SEHEMU YA 63

"Tutaifanya hiyo kazi Sam. Na hakika tutamtia mikononi Elizabeth Neville" Dalton alisema.

"Siyo kazi rahisi lakini Dalton. Tunapambana na watu hatari sana. Wanapanga vizuri mambo yao na kutekeleza kwa ufanisi mkubwa sana. Zaidi Kalinga mwenyewe nilivyomwambia Felix ameuwawa alishangaa sana. Na nilipomweleza kwamba Richard ametekwa alitoa ukelele mkubwa. Hiyo ni kumaanisha aliwaamini sana vijana. Na kweli wale ni watu muhimu na makini sana, lakini wamefanywa walivyofanywa!" Sam alisema.

"Mimi nina wazo Boss Sam" Kwa mara ya kwanza Gon aliongea.

"Nakusikiliza fundi" Sam alijibu.

"Hivi unamkumbuka yule jamaa aliyewahi kupeleleza kuhusu Elizabeth. Alienda kwa mama yake Elizabeth mchana na usiku alienda kuvamia katika nyumba hiyo. Alifanikiwa kumteka jamaa yetu John ambaye mimi nilienda kummaliza ili kupoteza ushahidi. Nakumbuka uliwatuma wakina Richard na Zungu kwend...." Sam alimkatisha.

"Namkumbuka vizuri sana Gon, na Richard alimtambulisha kwa jina la Martin Hisia"

"Ndiyo ni Martin, hivi hawezi kuhusika na kutekwa kwa Elizabeth Neville. Kuna vitu akili yangu vinagoma kabisa kuvikubali. Akili yangu kuna vitu inaviamini" Gon alisema.

"Vitu gani vinagoma kuvikubali akili mwako? Na vitu gani inaviamini?" Sam aliuliza.

"Akili yangu inaamini kwamba tulisalitiwa!" Gon alisema kwa kujiamini.

"Kusalitiwa? Na nani? Kwanini?" Sam aliuliza maswali mfululizo.

"Tulikuwa tunaishi na nyoka nyumbani kwetu. Amini Sam. Richard hakuwa mtu mzuri kwetu. Richard alitusaliti!! Kwa namna gani mimi sijui, ila naamini yule jamaa alitusaliti!!" Gon alisema.

"Hilo linawezekana vipi Gon? Unajua Richard kaletwa na Chifu mwenyewe. Bila shaka alikuwa anamwamini sana ndio maana alimleta katika misheni hii ya siri. Sasa iweje tena aweze kufanya hayo unayoyasema?" Sam aliuliza.

"Mwanzoni nilikuwa namwamini sana yule bishoo" Gon alieleza. "Lakini imani yangu kwake ilipungua siku ambayo camera zetu zilinasa picha za mvamizi kule kwa mama yake Elizabeth. Na picha za mtu yule ambaye Bishoo alisema kuwa zilikuwa za rafiki yake. Unajua ninyi hamkumchunguza. Ile kauli ilimtoka bila kutarajia, kisha uso wake ulionesha kujuta kwa kutoa kauli ile. Sikumwacha hivihivi, nilipiga hatua ya ziada mbele kwa siri bila ya kumwambia mtu. Nilienda katika chumba namba moja na kuchukua vifungo kumi vya kunasa sauti na mahali mtu alipo. Nilivipachika vifungo vile katika shati kumi za Bishoo akizozipenda sana kuzivaa huku nikilink vile vifungo katika simu yangu. Nia ni kujua nini anaongea, na nani? na eneo gani yupo?" Gon alinyamaza.

"E bwana wee Gon we ni kiboko!! Eeh ulinasa nini kutoka kwa bishoo?" Sam alisema kwa hamasa.

"Tokea nimefanya ile ishu mambo yalienda kwa haraka sana. Kazi zilikuwa nyingi na nilishindwa kabisa kusikiliza nini alichokuwa anaongea yule jamaa. Ila tunaweza kusikiliza hapa leo" Gon alisema.
 
SEHEMU YA 64

"Naam ni maamuzi sahihi. Na hata kama alikuwa upande wetu tutajua hao waliomteka walimpeleka wapi? Ulifanya jambo la maana sana Gon, Big u man" Sam alisema.

Gon hakujibu. Aliitoa simu yake mfukoni na kuanza kuichezea. Ilimchukua nusu dakika tu akasema.

"Richard ameongea na simu mara kumi na moja baada ya mimi kuweka vile vifaa vyangu akiwa amevaa yale mashati yaliyotegwa. Mara kumi aliongea na mtu mmoja na hii nyingine ndio aliongea na mtu mwengine tofauti" Gon alisema.

"Weka tuanze kusikiliza moja baada ya nyingine" Sam alisema.

Gon, Sam, Faustine na Dalton walianza kusikiliza zile sauti zilizowaacha katika bumbuwazi.

" Pumbavu!! Tumesalitiwaaa" Sam aling'aka baada ya kusikiliza zile sauti kumi za awali. "Richard katusaliti!! Hebu angalia upande wa kifaa kinapodaka mahali alipo tujue yuko wapi? Pumbavu sana yule 'Sam akamalizia na tusi zito la nguoni'"

Gon alikuwa kimya. Makini na simu yake. " Yap tumemnasa, vinasa eneo tisa vinaonesha Richard yupo shimoni. Hivyo inamaana mashati yale hayakuyavaa. Ila ili moja inaonesha Richard yupo mitaa ya

Summer Night, bila shaka hili ndio shati alilotoka nalo kule shimoni na kutoroka nalo" Gon alisema.

"Ulikuwa sahihi Gon kuhusu Richard. Najuta kukukwepesha mkono ulivyotaka kummaliza Richard kule shimoni. Mimi niliamini yule ni mtu imara na atavumilia mateso hivyo tumwache hai, nilikose.."

"Sio muda wa kuomboleza huu Sam, twende Summer night sasahivi tukamwoneshe Richard malipo ya usaliti!" Gon alisema kwa hasira.

Harakaharaka waliingia katika gari na kuelekea Summer night mahali walipoamini Richard alikuwepo. Wakiwa ndani ya gari simu ya Sam iliita. Alikuwa ni Zaidi Kalinga.

"Sam nipe maendeleo ya Msako wa Elizabeth Neville" Zaidi aliuliza simuni.

"Tunaelekea kumkamata sasa. Tushapata location walipo" Sam alijibu.

"Mmejuaje Sam? Na yupo wapi Elizabeth Neville?"

"Boss mtu wako katusaliti. Kumbe Richard alikuwa anawasiliana na watu ili waje kumkomboa Elizabeth Neville. Ni yeye na hao watu waliopanga lile shambulio la kule Sabasaba hata ule uvamizi wa kule shimoni" Sam alisema.

"Aiseee mjinga sana yule mwanahizaya. Mmeyajuaje hayo yote Sam?" Zaidi aliuliza.

"Kazi ya Gon hiyo. Kumbe Gon alianza kumhisi zamani yule jamaa kuwa msaliti, akampachika kwa siri vinasa sauti, hivyo ndivyo vimemuumbua" Sam alijibu.

"Kwahiyo mmejua huyo msaliti yupo wapi?"

"Ndio, Richard yupo Summer Night Club muda huu, ndio tunaenda kumfundisha adabu" Sam alijibu.

"Muue kabisa huyo, muue kinyama sana!!!" Zaidi alisema kwa hasira.

Simu ikakatwa.

"Boss katoa kibali cha kumuua kinyama" Sam alisema kwa sauti ndogo.

Garini ilikuwa kimyaa.

***
 
SEHEMU YA 65

"Mbona huyo Richard anachelewa sana? Hebu mcheki kwenye simu tujue yupo wapi?" Binunu alimwambia Martin.

Martin alichukua simu yake na kumpigia Richard.

"Shabash, kumbe simu imeisha Salio, ngoja nichukue hapo nje" Martin alisema.

"Poa Martin, usichelewe" Binunu alijibu.

Martin alitoka na kumwacha Binunu peke yake. Alikosea sana. Lilikuwa ni kosa kubwa sana ambalo Martin alilijutia milele.

Kumbe Elizabeth Neville alikuwa ameamka muda mrefu sana. Alijifanya kulala ili kuvuta muda kuona kama anaweza kuicheza karata yake ya mwisho na kujiokoa kutoka mikononi mwa wale watu ambao alikuwa hawatambui. Alifungua macho taratibu sana, alimwona yule mwanamke aliyemtambua kwa jina la Binunu akiwa amekaa katika kiti akiingalia miguu ya Elizabeth ambayo ilikuwa imejaa majeraha. "Nitaweza" Elizabeth Neville alijiambia neno alipendalo.

"Nitaweza" Alirudia tena.

"Nitaweza!!!" Safari alisema huku akikurupuka pale kitandani na kumvaa Binunu. Binunu hakujiandaa kabisa na shambulio lile. Msukumo ule pamoja na mstuko ulimpeleka chini moja kwa moja. Kidogo chake kilijigonga vibaya sana sakafuni na kuleta jeraha la kutisha likilomwaga damu. Binunu aliumia mahala palepale alipoumia miaka mitano iliyopita. Elizabeth Neville hakujiuliza mara mbili, alifungua ule mlango wa kile chumba na kutoka nje. Akimwacha mhudumu wa mapokezi mdomo wazi alipomwona yule mtu mgonjwa akitoka nje kwa kujikokota.

"Napunga hewa nje" Elizabeth alisema bila kusubiri jibu la yule mhudumu. Elizabeth Neville alikuwa huru baada ya kutekwa kwa miezi kadhaa. Alijokokota taratibu na kuzunguka kichochoro cha nyuma cha nyumba ile ya kulala wageni. Aliondoka huku akisema

"Nitaweza!!"

Martin alikuwa dukani akinunua vocha. Alipoishika tu ile vocha simu yake iliita. Aliangalia kwenye kioo, alikuwa Richard.

"Ndio nilikuwa naweka vocha hapa nikupigie. Upo wapi? Mbona mmechelewa sana?" Martin aliuliza.

"Nipo Ipogolo hapa ndio napandisha huko. Ila nipo na wageni wangu Martin" Richard alisema.

"Wageni? Ni wakina nani hao? Unajua ni jambo la hatari sana unalifanya Richard, mimi nilitegemea unakuja wewe peke yako" Martin alisema kwa hofu.

"Ni wageni wema. Nitawatambulisha kwako. Nimekwambia mapema ili usishangae endapo utatuona watu watano badala ya mmoja" Richard alisema.

"Basi tukutane mashine ya mpunga Richard. Nitakaporidhika na wageni wako ni watu sahihi ndipo tutaenda kule nyumba ya kulala wageni alipo Elizabeth Neville" Martin alisema.

"Sawa haina shida"

Dakika tano baadae, Martin alikutana na wakina Richard mashine ya mpunga. Richard ndiye alikuwa muongeaji na kuwatambulisha askari wale wanne.

"Nimewaelewa Richard. Ila tatizo mimi nimetumwa na Mheshimiwa Lucas kumpeleka Elizabeth Neville, na tayari nishamjulisha kuwa nimempata. Na kwa bahati mbaya zaidi kashanilipa tayari kwa hii kazi" Martin alisema.

"Sikiliza Martin" Daniel alisema. "Sisi hatumtaki Elizabeth Neville, hatuzitaki hizo records za siri ambazo Elizabeth anazo zinazomhusu Mheshimiwa Lucas. Sisi tunahitaji nyaraka za serikali tu, Elizabeth akitukabidhi hizo nyaraka tutakuachia"
 
SEHEMU YA 66

"Sawa tunaenda kule, ila sitaki utokee usaliti wowote ule" Martin alisema.

"Hilo haliwezekani Martin. Siwezi kukusaliti wewe ndugu yangu" Richard alisema.

Watu wote sita walipanda kwenye gari na kuelekea katika nyumba ya kulala wageni aliyopanga Martin kwa muda, waliyoyakuta huko.

Martin ndiye alikuwa wa kwanza kuingia ndani baada ya kugonga mlango mara tatu bila majibu. Bastola yake ikiwa kaishika imara kwa mkono wake wa kulia. Alikaribishwa na damu zilizotapakaa mle ndani. Pembeni aliuona mwili wa Binunu ukiwa unaogelea katika dimbwi la damu! Ilikuwa ni picha ya kutisha sana kuitazama.

"Dokta Yusha, mcheck yule majeruhi" Daniel Mwaseba alimwambia Dokta Yusha.

Wakati Dokta Yusha akivaa gloves ili kumhudumia yule mgonjwa. Wakina Daniel waliendelea kupekua mle ndani. Hakukuwa na kitu chochote kile cha maana.

"Katoroshwaaa!! Elizabeth Neville katoroshwaaa" Martin alisema kwa uchungu huku akiwa anachungulia uvunguni.

Mara sauti kutoka kwa Dokta Yusha ilisikika " Huyu mwanamke amefariki!! Amepoteza sana damu, tumechelewa"

Kauli ya Dokta Yusha ilibadilisha upepo wa mle ndani. Richard na Martin waliungana pamoja katika mwili wa Binunu. Waliufikia muda gani hakuna aliyekuwa anajua. Wote kwa pamoja waliutikisa mwili wa Binunu wakiwa na matumaini kwamba ataamka. Macho ya Binunu yaliwaangalia katika hali ya mshangao, mshangao uleule wa kumwona Elizabeth Neville akinyanyuka pale kitandani kama mzimu.

"Binunu, amka Binunuuu" Richard alisema kwa uchungu.

"Comrade, usife comradeee" Martin nae alisema kwa majonzi makubwa mno.

Binunu aliwashangaa tu, kwa macho yasiyo na uhai. Martin aliyafumba yale macho ya Binunu kwa mkono wake.

"Rest in Peace Binunu" Martin alisema kwa sauti ndogo.

"Siamini, siamini huu ndio mwisho wa Binunu, haiwezekani, haiwezekani. Mtakilipia kifo hiki. Yeyote yule aliyemuuwa Binunu lazima alipe kifo hiki. Kifo cha Binunu hakiwezi kupita hivihivi tu" Richard alisema.

Martin alishindwa kuvumilia, chozi la kiume lilidondoka na kudondokea katika maiti ya Binunu.

"Ni mimi, ni mimi ndiye niliyesababisha ufe Binunu. Nilikulazimisha uje katika kazi ambayo uliikataa.

ITAENDELEA

BURE SERIES
 
Pseudepigraphas
poor bununu
 
Back
Top Bottom