Abdallahking
JF-Expert Member
- Mar 19, 2018
- 3,985
- 10,840
- Thread starter
- #81
SEHEMU YA 60
"Ni refu sana. Kule lango kuu unatembea zaidi ya saa nusu saa na kutokea pembezoni mwa kambi ya jeshi. Hawa jamaa hatari sana" Richard alisema.
"Twende nyumba ya kulala wageni mbele ya Marie supermarket market. Tuone tunajipangaje" Daniel alishauri.
Haikuwa mbali hiyo nyumba ya kulala wageni akiyoizungumzia Daniel. Dakika saba tu walikuwa wamechukua chumba katika nyumba ya kulala wageni yenye hadhi ya chini.
"Dokta Yusha mtibie vizuri Richard, nitakuwa na mazungumzo naye marefu baadae" Daniel alisema.
"Naitwa Richard kama nilivyokwambia awali" Richard alianza kuelezea baada ya kuhudumiwa vizuri na Dokta Yusha. "Mimi ni mtoto wa mjini ninayeishi kwa kufanya uchunguzi na upelelezi binafsi kwa watu mbalimbali na kampuni. Mimi ni Richard Philipo yule wa Mkanda wa Siri.."
"Kumbe ndio wewe wa Mkanda wa Siri? Nilikisikia vizuri kisa kile nikiwa nje ya nchi. Mlifanya mambo makubwa sana wewe na wakina Martin Hisia. Kumbe ni wewe?" Daniel alisema kwa furaha.
"Ni mimi, na nishafanya misheni nyingi sana za hatari tofauti na ile, lakini nakiri kwamba hii misheni ni hatari kuliko zote hizo" Richard alisema.
"Hebu twambie, uliingiaje katika misheni hii? Na hii misheni inahusu nini hasa?" Daniel aliuliza. Askari wote walikuwa kimya wakimsikiliza Richard.
"Siku moja nilipigiwa simu na Zaidi Kalinga, ambaye kwa sasa ndiye mkuu wa jeshi la Polisi Tanzania. Zaidi alinambia kwamba kuna misheni ya kufanya huko Mafinga. Nilikubali bila ya kuuliza misheni inahusu nini? Misheni mimi ndio kazi yangu hivyo sikupaswa kuuliza inahusu nini? Nilisubiri maelekezo tu. Zaidi alinambia kuna mwanamke mmoja wamemshikilia lakini huyo mwanamke alikuwa hataki kusema lolote lile watakalomuuliza. Hivyo kazi yangu ilikuwa kuja kumtesa ili huyo mwanamke aseme" Richard alisema.
"Kwahiyo wewe ulikuja kwa kazi ya kutesa tu, na je ulifanikiwa?" Daniel aliuliza.
"Hapana, nikiwa katika hatua za mwanzo tu za mateso lilitokea jambo ambalo wao waliliona la ajabu sana. Lakini si kwangu, mlipuko ule haukuwa ajabu hata kidogo kwangu"
"Kwanini kwako haukuwa ajabu?" Dokta Yusha aliuliza.
Kwanini kwako haukuwa ajabu?" Dokta Yusha aliuliza.
"Tulipanga shambulio lile na wakina Martin. Mimi ndiye niliyeuza ramani kwa kina Martin wapi tulipo. Na tulipanga waje kwa namna ili kumchukua yule mwanamke. Ambaye Martin alinambia amepewa kazi na Mheshimiwa Lucas kumtafuta. Siku zote siwezi kufanya kazi tofauti na Martin, tumetoka mbali sana, hivyo nilichagua kuwasaliti wakina Sam, nilimsaliti pia Mheshimiwa Zaidi Kalinga" Richard alisema.
"Sasa Richard huyo mwanamke yupo wapi kwasasa?" Mwanasheria mlevi aliuliza.
"Elizabeth Neville bila shaka yupo mikononi kwa Martin Hisia na Binunu ambao wapo katika harakati za kumsafirisha kwenda kwa Mheshimiwa Lucas" Richard alijibu.