Simulizi : Elizabeth Neville

Simulizi : Elizabeth Neville

SEHEMU YA 67

Binunu, nilikwambia hii iwe kazi yetu ya mwisho, na kweli imekuwa kazi yako ya mwisho. Najilaumu Binunu, kwanini sikukulinda, kwanini nilikuacha humu ndani peke yako. Ooooh Binunu, naumia sana na kifo chako. Ni mwanamke jasiri sana wewe hukustahili kifo hiki" Martin aliomboleza kwa uchungu.

Daniel, Dokta Yusha, Mwanasheria mlevi na Inspekta Jasmin walikuwa wamesimama wima wakiwaangalia wale wanaume wawili wakiolia mbele ya mwanamke. Mwanamke ambaye ndiye waliyemuona katika camera za hospitali kwa kujifanya nesi na kutoroka na Elizabeth Neville kwa mtindo rahisi sana.

"Inamaana wale jamaa itakuwa wametuwahi huku?" Dokta Yusha aliuliza kwa sauti ndogo.

"Haiwezekani, kuna watu wengine ndio wamefanya haya mauaji na kutoroka na Elizabeth Neville" Mwanasheria mlevi alisema.

"Hata mimi naamini hivyo Mwanasheria, kwa tulichowafanya wale wasingeweza kufika huku kwa haraka hii. Kuna watu wengine tu ambao wametuwahi" Inspekta Jasmin aliunga mkono hoja.

"Ni Elizabeth Neville mwenyewe ndiye kafanya mauaji haya" Daniel Mwaseba alisema kwa kujiamini.

Watu wote walibaki katika mshangao. Richard na Martin walitoka kwenye maiti ya Binunu na kumsogelea Daniel Mwaseba.

"Unasemaje Daniel!! Haiwezekani, katu haiwezekani. Hujabahatika kumwona Elizabeth Neville wewe. Elizabeth hajiwezi kwa lolote na alikuja hapa bado akiwa hajaamka. Katika yote hilo umekosea sana Daniel" Martin alieleza kwa kirefu.

"Umeeleza mengi sana Martin. Lakini nataka nikwambie kitu kimoja na kikae akilini mwako. Ndani ya nchi hii hakuna mtu anayemjua kwa undani Elizabeth Neville zaidi yangu. Namjua Elizabeth ndani, namjua Elizabeth nje. Na kwa kumjua huko nawaambia sasa huyu mwanamke kauliwa na Elizabeth Neville.." Daniel alisema tena kwa kujiamini.

Watu wote walibaki kimya wakamwangalia Daniel. Macho yao yalionesha kwamba wanamtumaini yeye pekee kufumbua kisa hiki cha utata.

"Elizabeth Neville yupo huru. Na hii ni nafuu sana kwetu. Uhuru wa Elizabeth unamaanisha usalama wa 001. Na hiyo kwasababu moja tu, wakiomteka Elizabeth walikuwa wanazitaka wao nyaraka za 001, wangezipata ingekuwa ni hatari sana kwetu. Ila kwa sasa nyaraka zipo kwa Elizabeth Neville mwenyewe, hivyo hiyo hatari imepungua" Daniel alisema.

"Sasa Daniel huoni kwamba Elizabeth atazipeleka nyaraka za 001 kwa watu waliomtuma?" Inspekta Jasmin aliuliza.

"Ni kweli ingawa hilo linaugumu kidogo. Elizabeth itampasa kuzisafirisha nyaraka hizo kwenda Cuba, lakini si rahisi kwa sababu atapita njia gani ya kumtoa ndani ya nchi hii salama? Vyombo vyote vya usalama vina taarifa juu ya msako huu. Hatoweza kutoka nje ya nchi hii na hizo nyaraka" Daniel alisema.

"Ni kweli Daniel. Umenena sahihi sana. Na mimi naona kazi yetu pengine imekuwa rahisi zaidi, imebaki kazi ya kumsaka Elizabeth Neville tu" Mwanasheria mlevi alisema.
 
SEHEMU YA 68

"Siyo rahisi hivyo kama unavyofikiria. Ingawa Elizabeth Neville itakuwa ngumu kutoka nje ya mipaka ya nchi hii, lakini kumkamata siyo kazi rahisi hivyo kama unavyofikiria. Elizabeth Neville ni jasusi hatari sana. Mjanja na ana mbinu za hali ya juu kuikwepa hatari yoyote ile" Daniel alisema.

"Kwani huyu Elizabeth Neville ni nani?" Kwa mara ya kwanza Martin aliuliza.

"Ni swali dogo lakini linahitaji majibu marefu sana. Ila usiwe na haraka utamtambua tu Elizabeth Neville. Ila kijana nakwambia, kama unataka kulipa kifo cha Binunu, hakikisha tunamkamata Elizabeth Neville, ni yeye pekee ndiye aliyemuuwa Binunu" Daniel alisema.

"Sasa nini kinafuata Daniel?" Dokta Yusha aliuliza.

"Tunaingia kazini sasahivi kumsaka Elizabeth Neville. Nitawasiliana na mkuu wa Polisi hapa ili tupate askari watakaotusaidia katika kazi hiyo. Sasa hakuna siri sana, hili jambo lishakuwa kubwa" Daniel alisema.

Watu wote walikubali kwa kichwa.

"Dokta Yusha wasiliana na Daktari mkuu wa mkoa, aje hapa wakati mimi nikiwapigia Polisi. Wakauhifadhi huu mwili wa Binunu kwa muda wakati sisi tukiingia kazini. Kwa aliyoyafanya huyu mwanamke hasa katika ile misheni ya Mkanda wa siri anahitaji kuhifadhiwa kwa heshima na kuzikwa na heshima pia na nchi" Daniel alisema.

***

Dokta Yusha wasiliana na Daktari mkuu wa mkoa, aje hapa wakati mimi nikiwapigia Polisi. Wakauhifadhi huu mwili wa Binunu kwa muda wakati sisi tukiingia kazini. Kwa aliyoyafanya huyu mwanamke hasa katika ile misheni ya Mkanda wa siri anahitaji kuhifadhiwa kwa heshima na kuzikwa na heshima pia na nchi" Daniel alisema.

***

Wakina Sam ndio walikuwa wanafika Summer night. Walikuwa ndani ya gari macho yao wakiiangalia ile baa.

"Dalton na Faustine shukeni. Ninyi hamjulikani na Richard. Chukueni hii simu ndiyo itakupeni mwongozo mahali alipo Richard. Mkimwona mnapiga risasi kisha mnaipiga picha maiti yake na mnarejea hapa. Dalton ndo utafanya kazi ya kupiga bastola wakati Faustine utamlinda Dalton.

" Sawa bosi Sam" Dalton alisema huku wakitoka nje.

Walifika mbele ya baa, kulikuwa na vijana wengi waliokuwa wakicheza mchezo wa pool. Dalton aliiangalia ile simu ya Gon. Moja kwa moja mshale ulimuonesha kijana mmoja aliyekuwa anacheza pool. Wakajua ndio Richard. Risasi moja ilididimia kifuani kwake, Faustine aliupiga picha ule mwili wa Richard harakaharaka na walitimka mbio.

Lilikuwa tukio lililodumu kama dakika moja tu, mara vurugu zikazuka pale Summer night, zogo na vilio vilitawala, huku kila mmoja akijitahidi kukimbia ili kuokoa roho yake..Maiti ya Richard ilikuwa imelala chini ikiwa haina uhai.

Gon aliyekuwa dereva wa gari aliliwasha baada ya wakina Dalton tu kuingia. Gari likatimua mbio.

"Vipi mmefanikiwa?" Sam aliuliza wakiwa wanakata kona kuelekea Iringa mjini.
 
SEHEMU YA 69

"Tumefanikiwa. Risasi moja tu kutoka kwenye bastola ya Dalton imempeleka kuzimu yule mwanaharam.

Tumeacha zogo huko sio la kawaida. Mwili wa Richard ukiwa umelala chini ukiwa hauna uhai.

Mwangalie huyu hapa, picha yake akiwa marehemu" Faustine alisema huku akimkabidhi simu Boss Sam. Sam aliichukua ile simu na kuiangalia.

"Mmefanya nini nyinyi sasa? Siyo Richard huyu!!" Sam alisema kwa nguvu.

"Whaaaaat siyee! Hebu nimwone" Gon alisema kwa nguvu.

Sam alimpa simu Gon. Akaishika simu kwa mkono wa kushoto huku wakulia akiudhibiti usukani wa gari.

"Yah siye aisee, nini kimetokea mpaka ikawa hivi?" Gon alijiuliza huku akimkabidhi simu Sam.

"Kuna mchezo tumechezewa, yatupasa tuwe makini sana ili tusiendelee kuchezewa mchezo wa kipuuzi namna hii" Sam alisema kwa hasira.

Kukawa kimya ndani ya gari. Kila mmoja akiwaza lake kichwani. Mara simu ya Sam iliita. Alikuwa ni Zaidi Kalinga.

"Nambie Sam, vipi mmefanikiwa kumuua Richard? Zaidi alianza na swali.

" Hapana boss, jamaa wameleta ujuaji, tumeshindwa kabisa kummaliza" Sam alisema.

"Imekuwaje wakati ulinambia ndio unaenda kummaliza na kumchukua Elizabeth na mlishajua mahali walipo?" Zaidi aliuliza.

"Ni ngumu sana kuamini boss. Kile kinasa sauti kilichokuwa katika shati la Richard tumekikuta kwa mtu mwengine. Mtu asiye sahihi. Sijui kalitoa wapi shati lile!!" Sam alisema.

"Daah aisee, sasa vipi mwelekeo wa kazi hii. Tutaweza kweli kuifanikisha? Maana siku zinazidi kwenda na wale jamaa wananisumbua sana, wanautaka mzigo" Zaidi aliuliza.

"Hakuna shaka yoyote tunafanikisha hili. Tupe muda mchache tujadiliane na tutakueleza tumepanga nini" Sam alisema.

"Sawa Sam, nakuamini sana" Zaidi alisema na kukata simu.

Gari ya wakina Zaidi ilifika maeneo ya Kinyanambo C. Wakaingia katika nyumba moja ya kisasa waliyopewa na Zaidi Kalinga baada ya ile nyumba yao ya zamani kuungua. Wote wanne walijitupa sofani.

"Tumechezewa mchezo wa kijinga sana na yule mwendawazimu. Tumepoteza shabaha kabisa katika kazi hii, yaani sijui hata tunampata vipi Elizabeth Neville" Sam alisema kwa masikitiko.

"Tutampata tu boss Sam" Dalton alisema.

Mara Gon aligutuka " Nina wazo, nina wazo Sam, halafu sijui kwanini nilichelewa kuwaza hili tangu awali"

"Una wazo gani Gon?" Sam aliuliza kwa matumaini.

" Njia pekee ya kumpata Elizabeth Neville ni kwa kutumia simu ya Felix. Simu ya Felix ndio tumaini pekee la kutufikisha kwa Elizabeth " Gon alisema.

"Simu ya Felix? Kivipi? Mbona sikuelewe Gon?" Maswali mfululizo yalimtoka Sam.

"Umesahau alichomfanyia Dokta Beka Elizabeth?" Gon aliuliza.

Sam alitulia kama sekunde thelathini kisha akasema kwa furaha

"Nimekumbukaaa"

Matumaini mapya yalirejea kwa watu hawa.

"Yatupasa twende shimoni. Tukaitafute simu ya simu ile ndio pekee itakayotupeleka kwa Elizabeth Neville" Gon alisema.
 
SEHEMU YA 70

"Ni kweli Gon, yaani nilisahau kabisa. Hivi ule ulikuwa ushauri wako eeeh? Aisee una akili sana Gon" Sam alisema kwa furaha.

"Sijaelewa mnazungumzia nini?" Faustine aliuliza.

Na Sam aliwaelezea kila kitu alichokifanya Dokta Beka katika mwili wa Elizabeth Neville. Baada ya maelezo yake moja kwa moja walienda Pipeline katika njia ya dharura ya kuelekea kule shimoni njia iliyokuwa karibu na ukumbi wa Mam hall.

Ndani ya dakika kumi na mbili walifika. Walipaki gari yao mbele ya gereji moja kubwa. Na wote wanne wakiwa wamevaa maovalori ya bluu walishuka. Kitaswira walionekana kama mafundi. Hata walipofika katika chemba moja na kuanza kuufungua ule mfuniko hakuna raia aliyewatilia shaka. Wote walijua ni mafundi tu waliokuwa kazini.

Kumbe upande wa kulia, mita kama kama mia hivi katika kichochoro kimoja kulikuwa na mtu amejibanza. Pembeni, katika jalala la taka kulikuwa na mtu mwengine mchafu akiokota makopo na fuko lake kubwa.

"Daniel alikuwa sahihi aisee, jamaa wamerudi tena" Yule jamaa aliyekuwa jalalani alisema.

"Nimewaona, ni wenyewe ingawa wameongezeka na wengine wawili" Yule aliyekuwa kule kichochoroni alijibu.

"Tunafanyaje sasa Daniel?" Yule wa jalalani aliuliza.

"Tunataka mtuletee maiti tatu na mmoja akiwa hai" Daniel alisema.

"Sawa Daniel" Yule jamaa wa jalalani aliitikia.

Wakati huo wale jamaa watatu walikuwa wameshaingi mle shimoni huku wakimwacha mmoja kama mlinzi pale juu. Aliyeachwa juu alikuwa ni Dalton alitulia pale huku akiangaza huku na kule. Yule jamaa aliyekuwa kule jalalani alianza kutembea taratibu na fuko lake mkononi kuelekea pale karibu na chemba. Alikuwa anaimba wimbo usioeleweka huku akipiga mluzi. Dalton hakuwa na mashaka nae hata kidogo mtu yule ambaye alionesha dalili zote kwamba maisha yamempiga kisawasawa.

"Mkaribie hivyohivyo kisha muoneshe kazi. Mimi na wenzangu tutawaingilia wale jamaa shimoni" Yule jamaa wa kule kichochoroni alisema.

"Washafika kwani?" Muokota makopo aliuliza.

"Tupo karibu, tupo karibu" Mtu mwengine alijibu.

Muokota makopo alimkaribia kabisa Dalton. Dalton alipomwangalia yule jamaa alistuka sana. Alikiona kifaa cha mawasiliano sikioni mwa yule jamaa.

"Jamaa ni shushushu" Aliropoka Dalton, na lilikuwa kosa.

Sekunde ileile, jamaa akiyejifanya muokota makopo na vyupa jalalani, ambaye alikuwa ndiye mwanasheria mlevi alimtupia lile fuko la makopo na vyupa huku likiambatana na teke la nguvu lililompata Dalton mbavuni. Teke lile lilimpeperusha Dalton kidogo. Kisha akajiweka sawa, alikunja ngumi huku akimwangalia yule jamaa. Mwanasheria mlevi hakujiuliza, alirusha teke lengine la nguvu kwa mguu wake wa kulia. Dalton aliliona, aliinama kidogo na teke lile lilipita. Dalton naye alijibu mapigo, alirusha teke lililonaswa na mkono wa Mwanasheria mlevi.
 
SEHEMU YA 71

Mwanasheria aliufyetua kwa nguvu kwa mguu wake wa kulia ule mguu uliobaki chini. Dalton alienda chini mzimamzima. Mwanasheria alimsogelea yule jamaa na kumkandamiza na goti kifuani.

"Tuliaaa, huna ujanja mbwa wewe!!" Mwanasheria mlevi alisema.

Dalton alikuwa anafurukuta pale chini. Lile goti la Mwanasheria lilikuwa linamuumiza vibaya sana pale kifuani. Ghafla, aliukunja mguu wake na kuachia teke lililompata Mwanasheria mlevi mgongoni. Mwanasheria alirushwa mbele kidogo huku akimruhusu yule jamaa kujipanga upya. Mara, Mwanasheria mlevi aliruka juu huku akitanguliza mguu wake wa kulia mbele. Teke lile lilimpata Dalton usoni. Teke lile lilimpoteza uelekeo Dalton. Mwanasheria alirusha tena teke lililompata kichwani Dalton na kumtupa chini. Mwanasheria mlevi alimkimbilia pale chini na kumkandamiza tena Dalton. Harakaharaka alimfunga pingu katika mikono yake yote miwili. Wakati uleule Dokta Yusha na Martin Hisia walifika pale kulipokuwa na mpambano.

"Mdhibiti huyo paka Mwanasheria, Daniel na Inspekta Jasmin wanakuja sasahivi." Dokta Yusha alisema.

Dokta Yusha na Martin Hisia waliingia mle shimoni kwenda kupambana na wakina Sam.

***

Kule shimoni, Gon, Sam na Faustine walikuwa katika mwili ukiotoa harufu wa Felix.

"Mpekue mfukoni Faustine" Sam alisema.

Faustine aliipekua mifuko yote ya Felix. Hakukuwa na simu.

"Hana simu jamaa" Faustine alisema kwa fadhaa.

"Twendeni ofisini tukaangalie" Sam alisema.

Watu wale watatu waliongozana na kuelekea ofisini kule chini. Wakiwa njiani ghafla Faustine akadondoka huku ukisikika mlio mkali. Risasi ya kisogo ilikichimba vibaya kichwa cha Faustine kwa nyuma na damu kumwagika hovyo. Harakaharaka Felix na Gon walilala chini huku wakitoa bastola zao. Wakati Gon akijibiringisha kuelekea upande wa kushoto, Sam kwa mtindo uleule wa kujibiringisha alielekea upande wa kulia. Kila mmoja akafikia nguzo za kuzitumia kama ngao. Jambo moja tu likilowasumbua hawakujua adui yupo wapi.

Kwa nafasi aliyokuwa Dokta Yusha alikuwa na nafasi nzuri ya kumdungua Sam. Huku kwa nafasi aliyokuwa Martin Hisia mwili wa Gon ulikuwa wazi kabisa.

"Mkiwaona wauweni haraka hao. Dalton katueleza kila kitu" Walisikia sauti kwenye masikio yao. Ilikuwa sauti ya Daniel Mwaseba.

"Tuumalize mchezo" Dokta Yusha alisema. Na sekunde ileile risasi mbili zilitua katika miili ya wale watu. Ndio ulikuwa mwisho wao.

Dakika mbili baadae Daniel Mwaseba na Inspekta Jasmin waliingia mle shimoni. Baada ya kuwapekua wale watu na kuchukua vitu kadhaa walivyokuwa navyo zikiwemo simu na silaha. Daniel alisema.

"Kazi nzuri vijana. Sasa yule mshenzi wa juu kaanika kila kitu. Twendeni ofisini, kuna simu muhimu sana inabidi tuipate" Daniel alisema.

Askari wale wanne walielekea kule ofisini. Hawakupata shida sana, waliipata simu ya Felix ikiwa katika chaji na kutoka nayo nje.

SIMU hiyo ndiyo iliyomaliza utata wote.
 
SEHEMU YA 72

" Mheshimiwa rais. Naomba mumuweke chini ya ulinzi Kaimu IGP Kalinga, Waziri wa ulinzi Lucas na

Mkurugenzi wa usalama wa Taifa mzee Mangwina"

"Kwanini wawekwe ndani viongozi wote hao Daniel. Hao ni watu wakubwa sana hapa nchini. Lazima tuwe na maelezo ya kutosha ya kuwaeleza wananchi sababu ya kuwaweka ndani hao watu" Rais Dr Joseph alisema.

"Naomba waweke chini ya ulinzi tena haraka sana. Baada ya saa mbili nitakuwa hapo kuwaelezea kwanini wamewekwa ndani" Daniel alisema.

"Ok, uwe hapa muda huo Daniel. Nitakuwa pamoja na makamu wa raisi pamoja na Waziri mkuu. Na sasa natekeleza maombi yako" Rais Dr Joseph alisema.

"Nina ombi lengine Mheshimiwa rais " Daniel alisema.

"Nakusiliza Daniel, na kama lipo ndani ya uwezo wangu nitalitekeleza" Rais alisema.

"Najua ni nje ya utaratibu na wewe kama rais hupangiwi, lakini kwa heshime yangu naomba utengue nafasi ya Zaidi Kalinga, na umrejeshe John Rondo" Daniel alisema.

"Kwanini Daniel?" Rais aliuliza.

"Nitakuja kukwambia usiku" Daniel alisema na kukata simu.

***

Ilikuwa saa moja jioni katika ikulu ya jiji la Dar es salaam. Rais Dr Joseph, makamu wa rais, Waziri mkuu Dr Jeska Mlamka na IGP aliyerudishwa kazini John Rondo walikuwa wamekaa huku mbele yao kukiwa na vijana watano, alikuwepo Daniel Mwaseba, Inspekta Jasmin, Martin Hisia, Dokta Yusha na Mwanasheria mlevi.

"Tunashukuru sana Mheshimiwa rais kwa kutekeleza ombi langu kwa kuwaweka chini ya ulinzi viongozi wale watatu. Na kumrejesha kazini IGP John Rondo" Daniel alisema. "Sasa ninaomba waletwe hapa ili tukuambie tuliolikusudia hadi nikafikia hatua ya kukwambia uwaweke chini ya ulinzi" Daniel alisema.

IGP John Rondo alipiga simu kwa kamanda wa mkoa wa Kinondoni na kumwagiza wale viongozi waliokamatwa waletwe ikulu.

"Mwambie na yeye aje" Daniel alirukia.

Saa moja na nusu usiku Zaidi Kalinga, Lucas Mohamed na Christopher Mangwina waliletwa mbele ya Rais na askari kumi wakiongozwa na kamanda wa Polisi wa Kinondoni. Daniel Mwaseba aliwaangalia viongozi wale kwa jicho la hasira na kuanza kuongea..

"Nashukuru sana Mheshimiwa rais Dr Joseph kwa kutekeleza nilichokuagiza. Nilikuwa nataka nikueleze haya mbele yao kama kuna yoyote atakayeona namsingizia aseme hapahapa. Mheshimiwa rais, viongozi hawa watatu wamekusaliti na kulisaliti Taifa. Najua kila mmoja anajua jinsi Mheshimiwa rais alivyoingia katika mtego wa Elizabeth Neville na kuweza kuibwa 001. Nikwambie kwamba ile ilikuwa ni kazi ya Zaidi Kalinga.."

"Muongo, ananisingizia huyo kijana!! Mimi siyajui mambo hayoo" Zaidi Kalinga aliropoka.

"Tulia Zaidi, utafika muda wako wa kujielezea" Mheshimiwa Dr Joseph alisema.
 
SEHEMU YA 73

" Ipo hivi, Zaidi Kalinga ametusaliti kwa kushirikiana na waCuba. Amekuwa kibaraka wa waCuba kwa muda mrefu sana, tangu alivyokutana na mtu anayeitwa Salvador Raul.."

Uwoga wa wazi ulionekana usoni kwa Zaidi alipolisikia jina hilo likitajwa na Daniel.

"Salvador Raul aliingia nchini kwa njia ya panya akitokea Kenya katika mpaka wetu wa kule Namanga. Salvador ni jasusi wa Cuba aliyekuwa anafanya kazi maalum mjini Nairobi. Lakini alikuja nchini kwa kazi mbili, kazi moja ni kumtambulisha mwanadada Elizabeth Neville kwa Zaidi Kalinga na kazi yake ya pili kuratibu wizi wa dhahabu kule Geita kwa kushirikiana na Zaidi huyuhuyu" Daniel alisema.

"Muongo huyo msimuaminii" Zaidi Kalinga alisema kwa kukata tamaa.

" Elizabeth Neville yeye aliingia nchini wiki moja baada ya mimi kurudi Cuba na nyaraka ya 001. Kitu cha kwanza kukifanya alipoingia nchini ni kuanzisha uhusiano na mimi. Kwa kuwa nilionekana ni mwiba mchungu kwao. Nia yao ilikuwa Elizabeth aanzishe uhusiano nami ili iwe rahisi kwao kunimaliza. Nilistukia mpango huo miezi mitatu baadae kwamba yake hayakuwa mapenzi, na Elizabeth baada ya kugundua hilo alinikimbia huku akiicha hii simu yake nyumbani kwangu. Hapo ndipo Elizabeth alipowasiliana na wenzake na kuletwa Salvador. Kwa kutumia pesa zao walimshawishi Zaidi Kalinga naye alikubali kuwa upande wao. Akampenyeza kwa siri Elizabeth Neville kuwa mhudumu ili awe karibu na wewe na iwe rahisi kwake kuiba nyaraka za 001..."

"Wewe ni mtu mbaya sana Kalinga. Nimekuwa nakuamini sana Zaidi kumbe wewe ni nyoka!! Umenisaliti Zaidi" Rais Dr Joseph alisema kwa hasira.

Zaidi Kalinga alibaki kimya. Aibu ikiwa imemjaa usoni.

Elizabeth Neville alifanikiwa kuchukua 001 lakini baadae Zaidi Kalinga ilimjia tamaa ya kuipata yeye 001badala ya kuipeleka Cuba. Alitengeneza mazingira yote ya Elizabeth Neville kutoka nje ya nchi kupitia mpaka wetu wa Tunduma. Lakini ni yeye huyohuyo aliyepanga kutekwa kwa Elizabeth ili kumpora 001. Hivyo ndio namna Elizabeth alivyopotea na sisi kuanza kumtafuta." Daniel Mwaseba alimaliza.

"Christopher Mangwina tamaa ya kuipata 001 ili kuitumia kama silaha katika mchakato wake wa kuwa rais naye imemuumbua" Dokta Yusha naye alizungumza.

Alitutuma mimi na Mwanasheria mlevi kwa siri kumtafuta Elizabeth Neville bila kuishirikisha ofisi. Alitutuma Mbeya kumsaka Elizabeth Neville ili tuipate 001 naye aitumie kwa malengo yake ya kuwa rais, kwakuwa alijua kwamba akiipata 001 na kuiuza atapata hela nyingi sana ambazo zitamsaidia katika kampeni zijazo za urais. Hivyo Christopher Mangwina nae ameitumia ofisi kwa manufaa yake binafsi" Dokta Yusha alisema.

Christopher Mangwina alikuwa kimya. Alikuwa amepatikana.
 
SEHEMU YA 74

"Lucas Mohamed ndiye aliyemuuwa mwanadada Jane Munuo pale hongera baa. Na alifanya yote hayo katika kuisaka 001 kwa malengo sawa kama ya Christopher Mangwina. Na mbaya zaidi ni yeye ndiye aliyemtorosha Elizabeth Neville jana akiwa na 001" Martin nae alisema.

"Ahaaa!! Rais Dr Joseph alistuka. " kwanini umemtorosha Elizabeth Neville? "

"Ilinipasa kufanya hivyo Mheshimiwa rais. Yule mwanamke alikuwa na records zangu za mambo ya siri sana. Jana asubuhi Elizabeth Neville alinipigia simu na kunambia atazipeleka kwa waandishi wa habari la sivyo nitafute nje ya kumtoa nje ya nchi. Na nilifanya hivyo kwa makubaliano hayo" Lucas alijitetea.

"Swali la msingi ni ziko wapi nyaraka za 001?" Inspekta Jasmin aliuliza.

"Ameondoka nazo. Ameondoka nazo yule mwanamke" Lucas alisema kwa majuto.

"Kwa sasa yupo wapi Elizabeth Neville?" Rais Dr Joseph aliuliza akimwangalia Daniel.

"Kwasasa atakuwa nje ya mipaka yetu. Kule Mafinga tuliipata simu moja ambayo iliunganishwa na detector iliyochimbiwa katika mwili wa Elizabeth Neville. Tulijaribu kumfatilia. Tuliikuta ile detector ikiwa mpakani Tunduma. Elizabeth Neville sijui kwa namna gani aliitoa detector ile iliyowekwa mwilini mwake na kutokomea" Daniel alisema.

"Tumemkosaa. Na hii yote kwa sababu ya upumbavu wenu. Ninyi ni watu mliokuwa nawaamini sana. Mmeniangusha sana viongozi. Mmefanya usaliti mkubwa sana kwa Taifa letu. Na mbaya zaidi mmemtorosha mtuhumiwa mwenye nyaraka za siri za 001. Hatuwezi kuziacha bure zile nyaraka. Kesho asubuhi vijana wote sita mtaelekea nchini Cuba kuzika nyaraka za 001 kwa mara ya pili, wakati ninyi wasaliti wa nchi hii mtakuwa mkipelekwa mahakamani" Rais Joseph alisema.

"Nina swali la mwisho kwako kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni." Daniel alisema huku akimwangalia. "Kwanini ukitoa oda ya kusitisha mapigano kwa askari pale Faya tulivyokuwa napambana na wahalifu?"

Kamanda alikumbuka " Nilipigiwa simu na Zaidi Kalinga. Mimi nilitekekeza oda tu" Kamanda alisema. "Na pia ngoja niseme hili ili nisiwe mmoja wa wahalifu katika sakata hili, ni hivi kabla ya hapo Zaidi Kalinga alinituma kazi ya kubadilisha ripoti kuhusu Elizabeth Neville" Kamanda alisema huku akiogopa.

IGP John Rondo macho yalimtoka!!!

***

IGP John Rondo macho yalimtoka!!!

***
BURE SERIES
 
SEHEMU YA 75

Daniel Mwaseba, Inspekta Jasmin, Martin Hisia, Richard, Dokta Yusha na Mwanasheria mlevi waliagana pale ikulu. Kila mmoja alirudi nyumbani kwake kwa ajili ya kujiandaa na safari ya kesho yake asubuhi. Daniel aliingia katika nyumba yake iliyopo huko Mikocheni saa sita usiku. Alipitiliza sebuleni na moja kwa moja kuelekea chumbani. Jicho lake lilipotua kitandani, alistuka sana! Katika kitanda chake alikutana na bahasha ambayo haikuwepo hapo siku aliyoondoka. Aliichukua ile bahasha. Akaisoma. Juu ya bahasha iliandikwa Daniel Mwaseba.

"Nini hii, kaleta nani? Kaingiaje humu?" Daniel Mwaseba alisema huku akiifungua ile bahasha. Alitoa karatasi kumi nyeupe ndani ya ile bahasha, juu ya karatasi ya kwanza kuliandikwa maneno kwa herufi kubwa NYARAKA ZA 001.

Daniel alistuka sana "Zimefikaje hapa hizi bahasha?" Nani kazileta?" Daniel Mwaseba alijiuliza maswali ambayo hakuwa na majibu nayo. Daniel alinyanyuka na kwenda chumba chake cha mitambo. Huko ndipo aliona kila kitu.

.....Video ilimuuonesha sebuleni mwanamke mmoja akiingia. Moja kwa moja bila wasiwasi mwanamke yule alienda chumbani kwake na kuiweka ile bahasha kitandani. Kisha alikaa kitandani na kuanza kuongea.

" Najua hapa namulikwa na Camera zako Daniel, na ndio maana naongea haya maana najua utakuwa unaniangalia muda huu. Kwa majina naitwa Elizabeth Neville. Mwanamke ukiyemsaka usiku na mchana tangu siku ile nilivyotoroka kwako baada ya kujua umenigundua kwamba mimi ni spy kutoka Cuba. Ulikuwa sahihi Daniel, sikuja kwako kwa bahati mbaya, nilikuja kwako kukumaliza kama nilivyotumwa na wakuu wangu na nilikuwa na uwezo wa kukuuwa lakini sikufanya hivyo. Sikukuuwa sio kwamba nakuogopa, la hasha! Sikukuuwa kwa sababu moja kuu Daniel, MAPENZI. Nilitokea kukupenda sana Daniel, na sikuona kama nitaweza kujisamehe endapo nitakuuwa mwanaume kama wewe ninayekupenda kuliko kitu chochote kile duniani. Ndoto yangu ni kuja kuishi mimi na wewe kama mke na mume, sikutaka kumuuwa mume wangu mtarajiwa.

Daniel, kuonesha upendo wangu wa dhati kwako nimeamua kukuachia nyaraka za siri za 001. Nyaraka muhimu sana kwa nchi yenu. Ila nakuomba ukamshauri rais akaziweke mahala sahihi nyaraka hizo kwani ni nyaraka muhimu sana ambazo serikali yangu ya Cuba wanazihitaji kwa udi na uvumba. Mimi ninarudi kwetu Daniel, nina asilimia ndogo sana za kusamehewa nitakavyorudi bila nyaraka za 001, lakini najua cha kusema na naamini watanielewa na kunipa nafasi nyingine, hapo ndipo nitakuja na kuishi na wewe kama mke na mume. Na kuachana sana mambo haya. Nakupenda sana Daniel, amini nakupenda kiasi cha kuisaliti nchi yangu. Na hiyo ni zawadi pekee niliyokuachia. Ngoja nikuibie siri Daniel, ni mimi ndiye niliyevujisha mpango wa wizi wa dhahabu Geita kabla hukatekelezwa, lengo ni kuinusuru nchi ya mwanaume ninayempenda. Ni mimi ndiye niliyemwambia msichana Bertha Fidelis kuhusu wizi ule.

Ahsante kwa kunisikiliza Daniel Mwaseba, mme wangu mtarajiwa"

Daniel Mwaseba alihemwa. Hakuamini kabisa macho yake. Elizabeth Neville alimwacha katika mshangao mkuu.

Harakaharaka alimpigia simu Rais Dr Joseph na kumueleza kila kitu. Dakika ishirini baadae Daniel Mwaseba alikuwa ikulu na kumuonesha rais Dr Joseph ile video na kumkabidhi nyaraka za 001. Rais Dr Joseph hakuamini macho yake. Alimshukuru sana Daniel.

Kwa furaha alisema" Kesho mtazikuta zawadi zenu katika akaunti zenu. Nimeshaongea na hazina" Rais Joseph alisema huku akizirudisha zile nyaraka za siri mahali pake.

Mwisho

Imeletwa kwenu kwa udhamini wa BURE SERIES

Ahsanteni sana kwa kuwa wote mwanzo hadi mwisho.
 
Imeletwa kwenu kwa udhamini wa Pseudepigraphas

Ahsanteni sana kwa kuwa wote mwanzo hadi mwisho.
Noted
 
Ahsante kwa burudani japo kuna makosa makubwa na madogo ya hapa na pale ila kazi nzuri kwa mwandishi
 
Safi sana...

Chapter Closed...
 
Back
Top Bottom