Simulizi: For You

FOR YOU

Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Uhalifu, Mauaji, Visasi, Vita, Mambo yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA KUMI NA NANE

★★★★★★★★★★★★★★★★


MIAKA NANE ILIYOPITA....


Turudi miaka nane nyuma kufikia wakati wa usiku ule ambao familia za Kapteni Kendrick Jabari na Meja Casmir Sona zilishambuliwa na Luteni Weisiko pamoja na wanajeshi wenzake wawili. Kapteni Kendrick aliwasikia viongozi kadhaa wa siasa na jeshi wakati huo, baadhi wakiwa ni Kanali Jacob Rweyemamu na Makamu wa Raisi Paul Mdeme, wakizungumzia kuhusu mpango wao mbaya kuwaelekea wanaume hawa wawili na familia zao kwa kuwa walihofia wangewaharibia mipango yao mibaya ambayo bado haikuwa wazi ni nini.

Ikiwa utakumbuka vizuri, Kapteni Kendrick alitoka jengoni walipokuwa na upesi kuwahi nyumbani kwake ili aiokoe familia yake, na pia alimtaarifu Meja Casmir mapema kuhusiana na mpango huo mbaya wa viongozi hao. Alipofika nyumbani kwake, aliwaasa ndugu zake wawili wanawake pamoja na mama yake mzazi waondoke haraka kwa sababu maisha yao kwa ujumla yalikuwa hatarini. Alipokwenda chumbani ili achukue vifaa vichache muhimu kwake, Meja Casmir alimpigia na kumwambia wakutane kwenye nyumba ya zamani ya mjomba wake (Casmir) ili wajipange zaidi kuhusu ni jinsi gani wangezilinda familia zao na kisha wafanye nini kuhusiana na mambo yaliyokuwa yakiwapata.

Ndipo baada ya kuwa amekata simu, Kendrick alijisawazisha na kujiuliza ikiwa kuna jambo lolote la muhimu alisahau. Alipoangalia kabati lake la nguo tena, akatuliza macho yake hapo kwa sekunde chache, kwa sababu alikumbuka kuna kitu fulani cha muhimu kilikuwa humo, kisha akavua begi na shati lake na kwenda kuifungua. Akatazama kwa makini ndani hapo, halafu akachukua VAZI lingine na kuvaa, kisha akavaa na jaketi jeusi kwa juu.

Vazi hili lilikuwa ni vazi maalumu kwa ajili ya kuzuia risasi kifuani mpaka kufikia tumboni (bulletproof vest), hivyo alilivaa kama ulinzi tu wa ziada endapo kama mbeleni yeye na Casmir wangehitaji kupambana na maadui zao, basi lingempa faida kwa kadiri fulani. Baada ya hapo alibeba begi na kutoka chumbani ili ajiunge na wengine waweze kutoroka hatimaye, lakini ndiyo akakuta Luteni Weisiko ameshafika. Alishuhudia mama yake mzazi akiuliwa kikatili mbele ya macho yake na mwanaume huyo, kisha wanajeshi wa Luteni Weisiko wakamshikilia kwa nguvu Kapteni Kendrick baada ya yeye kukasirishwa sana na kitendo hicho.

Luteni Weisiko alimwambia kwamba mambo yote aliyofanya yalikuwa ni sehemu ya wajibu wake, naye Kapteni Kendrick akamlaani na kumwambia kwa ujasiri kuwa ipo siku mambo yote ambayo walikuwa wakifanya yangewarudia tu. Luteni Weisiko alimfyatua risasi tatu; mbili sehemu ya kifua na nyingine tumboni, na wanajeshi wale wawili wakamwachia Kendrick, naye akaanguka chini. Kwa haraka waliyokuwa nayo kutokana na kutaka kumfikia Casmir upesi, wanaume hao walifikiri Kendrick alipoteza maisha pale pale, lakini kihalisi risasi zile zilikuwa zimezuiwa kwa vazi la Kendrick la ndani. Mshtuo mkubwa wa risasi karibu kabisa na mwili wake ulisababisha Kendrick apoteze fahamu, lakini hakufa.

Alipoanza kurejesha fahamu zake taratibu, alijikuta ndani ya joto kali sana, na moshi mwingi uliyachoma macho yake na pia ukamfanya aanze kukohoa. Alijisawazisha vizuri na kutambua kwamba sehemu aliyokuwepo ilikuwa ikiwaka moto mkali sana kuzunguka nyumba yote, naye akajitahidi kunyanyuka haraka ili atafute sehemu ya kutokea. Aliweza kuiona miili ya wanawake wale watatu pale chini, naye akasikitika sana, lakini akajikaza na kuanza kutangatanga huku na huko kutafuta sehemu ya kutokea.

Moto ulikuwa mkali sana, na moshi ulimfanya aishiwe nguvu. Hivyo akaona hakukuwa na njia nyingine ya kutokea ila mlangoni pale pale. Akavua jaketi, kisha akaitoa bulletproof vest na kulivaa jaketi tena. Akaitumia bulletproof vest kujikingia usoni, na kwa kupigia mahesabu sehemu ya mlango ilipokuwa, akatoka kwa kasi akikimbia kuelekea upande huo. Moto ulimuumiza sana sehemu za pembeni lakini hakukata tamaa. Ilikuwa ni kama moto unamzuia asisonge mbele, na ilionekana kama haungekwisha, lakini HAKUKATA TAMAA.

Mwishowe, alitoka mpaka sehemu ya nje na kudondokea chini, akihisi maumivu mengi mwilini kwa sehemu zilizounguzwa kwa moto. Mpaka kufikia wakati huo hakukuwa na mtu hata mmoja aliyesogea hapo kwa kuwa nyumba hii ilikuwa imejitenga na zingine. Alipumua kwa presha akihisi maumivu mengi sana, lakini akajikaza na kunyanyuka, kisha akalielekea geti na kutoka mpaka sehemu alipoegesha gari lake. Akaingia na kuliwasha, na sehemu aliyokuwa akipanga kuelekea ilikuwa ni kule kule ambako Casmir alimwelekeza.

Lakini mwanaume huyu alipata shida sana kuliendesha gari akiwa ndani ya hali yake iliyozidi kuwa mbaya. Aliendesha kama mtu aliyekuwa amelewa, hivyo akaona asimame kwanza ili atafute msaada wa maji. Alitoka ndani ya gari na kuelekea kwenye nyumba moja ambayo aliita sana wenyeji wamsaidie. Kwa sababu ilikuwa ni usiku, watu wa pale waliogopa na kufikiri labda ni mtu mbaya, lakini baada ya kuona ameumia kweli, wakamsaidia. Walipendekeza kumpeleka hospitali, lakini Kapteni Kendrick akawaambia alichohitaji ilikuwa ni maji mengi tu kwa kuwa hakuhitaji kwenda hospitali. Walimpa maji, naye akanywa na mengine kuyatumia kujikandia.

Wenyeji walimshangaa kiasi kwa sababu alionyesha ustahimilivu wa hali ya juu sana, ila sababu ilikuwa ni uimara wa mwili wake wenye uzoefu na mafunzo ya kijeshi. Akawaomba wamsaidie vitambaa vyovyote ili afunike sehemu alizobabuka, na ingawa hawakuwa na vitambaa vingi, kwa fadhili mwenye nyumba akatoa shuka moja na kulichana-chana ili wapate nguo ndefu-ndefu za kumfungia. Walikuwa ni watu wazuri, naye Kendrick akawashukuru na kuwaahidi kwamba ipo siku angewalipa kwa ukarimu wao.

Bila kukawia, Kapteni Kendrick akaondoka hapo baada ya kuwa amejisikia uafadhali. Aliendesha gari lake kwa kasi sana kuelekea kule walikoahidiana kukutana na rafiki yake; akitumaini hakuwa amechelewa mno. Roho ilimuuma sana kwamba hakuweza kuwasaidia watu wa familia yake, hivyo kama angeweza kuisaidia familia ya rafiki yake, basi ingetosha sana, kwa sababu hao ndiyo waliokuwa kama ndugu aliobakiza.

Lakini matumaini yake yaliingiwa na vikwazo pale alipokaribia maeneo ya kule walikokuwa wakina Casmir na kuanza kusikia sauti za milio ya risasi. Akaona asimamishe gari umbali fulani kutoka huko ili aweze kwenda kwa njia ambayo hangeonwa kirahisi. Risasi hizo alizosikia zilikuwa kiashirio kwamba Weisiko aliwafikia marafiki zake, naye Kendrick akaendelea tu kuomba kwa Mungu na wao wasiwe wamewaua pia, ijapokuwa nafasi ilikuwa finyu sana.

Alijongea kwa umakini sana mpaka sehemu ambayo alianza kuwaona watoto wa Casmir wakitoka ndani ya gari huku wameshikiliana, na risasi zilikuwa zikifyatuliwa kuelekea upande wao. Akaangalia upande ambao risasi zile zilikuwa zikitokea, naye aliweza kuiona miili ya watu watatu ambao aliwafahamu vizuri sana; Salome, Casmir, na Alice pia. Aliingiwa na simanzi kubwa sana moyoni, naye akaanza kutokwa na machozi kwa kuwa sasa rafiki yake kipenzi pia hakuwa hai tena. Alijilaumu kiasi pia moyoni kwa kutoweza kufanya mengi ili kuwasaidia wapendwa wake.

Aliweza kumwona Luteni Weisiko pamoja na mwenzake wakijitengeneza, bila shaka ili kuwafatilia watoto wale, naye akaingiwa na hasira kali sana kwa kumwangalia mwanaume huyo aliyetumiwa kuwafanyia mambo mabaya sana watu wasio na kosa lolote. Akawaona walipoanza kuwafatilia watoto, naye akatoka alipokuwa ili aelekee huko huko, akiazimia kuwasaidia watoto kwa kukomesha unyama wa wanaume hao haraka iwezekanavyo.

Kwa kuwa aliwahi kuja huku na kutembelea baadhi ya maeneo yenye msitu ule, alitumia njia nyingine ambayo alijua ingemkutanisha kwa mbele na watoto wa Casmir. Ambacho hangeweza kujua ni kwamba watoto wale waliamua kujigawa kwa kutumia njia tofauti ili maisha ya wawili yaweze kuokolewa; ikiwa ni wazo la Xander kwa dada zake wawili Sandra na Azra. Kendrick pia alikuwa amechoka, alihisi maumivu mwilini na hata hisia za kupoteza matumaini, lakini bado aliendelea kufanya yote ili kupigania yaliyokuwa muhimu kwake, hata kama ingemaanisha kuuhatarisha uhai wake mwenyewe.

Alizungukia upande wa mbele wenye miti mingi akiwa na matumaini kwamba angekutana na watoto na kuwasaidia kutumia njia tofauti ya kutorokea ili kuwapiga chenga wale jamaa, kisha angehakikisha wanakuwa sehemu salama ili yeye ashughulike nao hatimaye. Alifika sehemu ambayo kwa kutumia maarifa yake aliweza kujua kwamba kuna mtu alikuwa ametulia hapo, kimya, lakini bado hakuweza kubaini ilikuwa ni nani, hivyo akaona naye atulie. Haikupita muda mwingi na hatua za kukimbia kwa mtu zikasikika, na hapo akamwona mwanajeshi yule, Goko, akisimama na kutulia huku anajaribu kuangalia huku na huko.

Kendrick alikuwa ameshaanza kupiga mahesabu ya kumfata, lakini akashtushwa kiasi baada ya kusikia mlio wa risasi kutokea upande tofauti usiokuwa mbali sana na hapo. Aliporudisha macho yake kwa Goko, aliweza kumwona sasa mtu yule aliyekuwa nyuma yake akinyanyuka na kutaka kumshambulia Goko kwa jiwe, lakini Goko akamkwepa na kupiga risasi hewani baada ya jiwe hilo kupiga bega lake badala ya kisogo. Mtu yule akaanguka chini, naye Kendrick akatambua sasa ilikuwa ni Sandra (ikiwa ni Xander kwa ndani), hivyo akaanza kunyata taratibu kumwelekea Goko nyuma yake.

Mwanajeshi huyo mwenye kiburi alikuwa akimwambia maneno ya dharau Sandra (Xander) wakati Kendrick alipokuwa amekwishamkaribia zaidi, na ile Goko alipogeuka tu, Kendrick akamrukia na kuangukia naye pembeni. Alianza kumtandika ngumi nzito za kichwa na usoni pia, na kwa jicho la mbali aliweza kumwona Sandra (Xander) akikimbia kwa hofu. Lakini akaona amalize kumshughulikia kwanza mwanaume huyo, kisha ndiyo angemfata mtoto.

Goko alikuwa akijaribu kujirudisha juu kibishi lakini Kendrick akamzidi nguvu na kumvunja vidole kwenye kiganja chake, halafu akachukua jiwe zito pembeni na kumponda nalo kwa nguvu kifuani. Goko akatulia tuli. Kendrick akajinyanyua upesi na kumvuta kwa nguvu, kisha akajitahidi kumbeba begani kwake. Alianza kutembea pamoja naye kuelekea upande ambao alijua ulikuwa na bonde refu sana kuelekea chini, na akiwa bado anatembea naye, mdomo wa Goko ulitoa damu zilizodondoka ardhini kufatisha njia aliyopitia Kendrick. Kendrick alipofika usawa wa sehemu ile, akamshusha mwanaume huyo na kumsukuma chini kule kwa nguvu sana.

Kisha akageuka na kuanza kurudi kule alikoelekea Sandra (Xander). Alimwona wakati alipokuwa anakimbia kwamba "binti" huyo hakuwa na nguvu za kutosha kwa sababu fulani, hivyo akajitahidi kuwahi kabla hajaingia mikononi mwa mtu mwingine mbaya. Ilikuwa kwa tukio baya tu kwamba alisahau kuichukua bunduki ya Goko kwa ajili ya kumshambulia adui, kwa sababu kile alichowaza hasa kilikuwa ni kuokoa watoto. Lakini pia hakujua wengine wawili walikuwa wapi, ingawa mlio ule wa risasi aliosikia ulimpa wazo la kwamba huenda walikuwa upande ulipotokea.

Akiwa anamtafuta Sandra (Xander) kwa bidii, aliweza kusikia tena sauti ya risasi sehemu ambayo alitambua haikuwa mbali. Akageukia upande huo, na upesi akaanza kuuelekea lakini kwa tahadhari kubwa. Alifika sehemu ambayo ilikuwa na vichaka kumzunguka, na hapo akaweza kumwona "Sandra" akiwa amejilaza chini. Alipoangalia mbele zaidi, aliweza kumwona Luteni Weisiko akiwa amesimama tu, hivyo kwa uangalifu akaingia sehemu ile ya kichaka alipojilaza Sandra (Xander) na kufika nyuma yake taratibu.

Sandra (Xander) alikuwa ameanza kujinyanyua kivivu sana, na kwa haraka Kendrick akatambua kwamba alikuwa anataka kumsemesha Luteni Weisiko. Akasogea karibu yake upesi na kumfunika mdomoni kwa kiganja chake kutokea kwa nyuma. Alipoangalia kuelekea pale aliposimama Weisiko, sasa aliweza kuwaona Azra na Xander (ikiwa ni Sandra kwa ndani) wakiwa wamelala chini kwa ukaribu, na wakionekana kuwa mbali na uhai. Kendrick akahuzunika sana.

Sandra (Xander) alikuwa akijaribu kujinasua kutoka kwa mtu aliyemfunika mdomo kwa nyuma, lakini nguvu zake zikamwishia na kupoteza fahamu. Kendrick akaanza kumvuta nyuma taratibu, kisha akamwangalia kwa umakini. Aliona jeraha lake la tumboni sasa, naye akatambua kuwa alikuwa amepoteza damu nyingi sana. Lakini "binti" huyu bado alikuwa hai, hivyo Kendrick akajikongoja tu na kumbeba mgongoni, kisha akaanza kuondoka naye kutoka sehemu hiyo. Mambo ambayo familia zao zilikuwa zimepitia usiku huo yalikuwa mazito sana.

Kendrick alijitahidi kwa uwezo wake wote kumwahisha "Sandra" sehemu ambayo angeweza kupata tiba ya haraka, na pia ili kuokoa uhai wake kutoka kwa Weisiko. Alijua hiki ni kitu ambacho rafiki yake aliyepoteza uhai angehitaji sana amfanyie, na kumbukumbu ya mambo mengi waliyopitia pamoja ilimwongezea nguvu ya kupambania uhai wa binti yake. Aliweza hatimaye kutoka ndani ya msitu ule akiwa bado kambeba "Sandra" mgongoni. Alikuwa amechoka sana, lakini akakazana. Yaani hakutaka kugeuka nyuma kwa kuwa alielewa sasa jukumu la kuokoa uhai wa mtoto huyu lilikuwa mikononi mwake. Akampeleka mpaka kwenye gari alilokuja nalo eneo hilo na kumweka ndani yake, kwa nyuma, kisha naye akaingia kwenye usukani na kuliondoa hapo upesi.



Mwendo mzima alikuwa akimuwaza sana mama yake, Casmir, Alice, Xander, Azra na Salome. Alitiririkwa na machozi mengi sana akihisi kama ni ndoto jinsi siku hiyo iliyotakiwa kuwa ya furaha (kwa sababu ya birthday ya Alice), ilivyobadilika na kuwa anga ya umwagaji wa damu. Ilikuwa ni saa 9 iliyoelekea saa 10 usiku sasa, naye akafanikiwa kumfikisha Sandra (Xander) kwenye Zahanati fulani ya kanisa la kikatoliki, eneo ambalo halikuwa mbali sana na mpaka wa kuingia mkoa mwingine.

Alishukuru sana Mungu baada ya kukuta wauguzi wawili hapo waliomwambia kwamba kuna daktari wa Zahanati hiyo ambaye hufika mida ya saa 11 kwa kuwa huwahi kuondoka baadae tena, hivyo wakamsaidia kumwingiza Sandra (Xander) ndani na kumwekea 'drip' muhimu upesi. Wauguzi wale walitambua kwamba Kendrick na Sandra (Xander) walikuwa wameumia vibaya sana, na walipouliza tatizo, Kendrick akasema walikumbwa na mambo mabaya kutoka kwa watu fulani waliotaka kuwaumiza. Akawaomba waangalie ikiwa itawezekana kuanza taratibu za kumwongezea damu "Sandra," lakini wauguzi wakamwambia kuwa hawakujua mambo mengi ya kufanya mpaka daktari afike.

Hii ingekuwa hatari kwa sababu mwili wa "Sandra" ulikuwa umepoteza damu sana, na kumsubiria daktari kwa saa zaidi ya moja huenda kungeleta matatizo. Hivyo Kendrick akawaomba sana watafute njia yoyote ile kwa sababu alikuwa amepoteza watu wengi sana usiku huo na hivyo hangetaka kumpoteza na "binti yake." Wauguzi wale walimwonea sana huruma, na kwa neema tu ya Mungu, mmoja wao akasema anajua mambo fulani kuhusu kuwaongezea damu wagonjwa, hivyo waangalie ikiwa kundi lake la damu liliendana na la "Sandra" ili waweze kutoa ya kwake Kendrick kiasi na kumwekea "binti yake."

Kendrick akakubali na upesi muuguzi huyo akampima na kulinganisha na ya "Sandra," kukuta zinaendana. Kendrick akafarijika sana. Aliendelea kuomba kwa Mungu kuwa angalau binti huyu apone, kwa sababu alitaka sana kuuokoa uhai wake kwa kuhisi alishindwa kufanya hivyo kwa wengine. Wauguzi wale walijitahidi kumsaidia kwa kadiri ya uwezo wao, na uzuri ni kwamba angalau kwa muda huo hakukuwa na wagonjwa wengine waliohitaji huduma za dharura, hivyo walikazia uangalifu kwa hawa wawili.

Sandra (Xander) aliwekewa drip iliyomwingizia damu sasa, na kilichokuwepo ilikuwa ni kusubiri daktari afike. Lakini tena, bado Kendrick alijua yeye kuwa hapo kwa muda mrefu ingekuwa hatari zaidi kwao, hasa kama taarifa kuhusu yeye na "Sandra" kufika kwenye Zahanati hii zingewafikia wabaya wao, na hivyo hata kuhatarisha usalama wa wale waliofanyia kazi hapo. Walikuwa wemeshakaa hapo kwa saa kama moja na daktari hakuwa amefika bado kama wauguzi wale walivyosema, na ijapokuwa alijua hali ya binti wa rafiki yake ilikuwa mbaya, akaamua tu kuondoka naye kabla ya daktari kufika.

Kendrick alimbeba ''Sandra" mikononi mwake kwa uangalifu, akiwa ameshikilia kimfuko na mrija uliomwingizia damu mshipani, naye akatoka naye kuelekea kwenye gari nje. Wauguzi wale walimshangaa na kumuuliza kwa nini alifikia uamuzi huo ambao ulikuwa hatari kwa mgonjwa, lakini Kendrick hakuwajibu lolote na kumpeleka "Sandra" mpaka ndani ya gari. Kwa akili akautundika mrija ule wa damu ndani ya gari kwa njia ambayo ungeendelea kumwingizia damu "Sandra" mshipani akiwa amelala kwenye siti za nyuma. Wauguzi wakadai kwamba alihitaji kulipia, lakini Kendrick akasema ni Mungu ndiyo angewalipa kwa msaada wao, kisha akaingia ndani ya gari na kuondoka eneo hilo.



Kila mara Kendrick alipofikiria kuhusu usalama wake na wa binti huyu aliyekuwa amepoteza fahamu, alishindwa kujua ikiwa angeweza kujificha huku akielewa kwamba mtoto huyu alihitaji tiba bora zaidi, kwa sababu kama sivyo, basi na huyu angekufa akiwa mikononi mwake. Akaendelea kuomba msaada kutoka kwa Mungu kwamba "Sandra" asikate tamaa na kuendelea kupambania uhai wake ndani kwa ndani, ili yeye Kendrick atafute mazingira mazuri zaidi ya kumsaidia binti huyu. Wazo moja la mtu ambaye angeweza kumsaidia likamwingia, naye akaiwekea akili yake sehemu ambayo angetakiwa kwenda ili kujilinda kabla ya msaada kutoka kwa mtu huyo kumfikia.

Aliendelea kuendesha gari lake mpaka akatoka nje ya mkoa huo, ikiwa inaingia saa 1 asubuhi. Alifika maeneo ambayo aliona vibanda kadhaa vya simu za mawasiliano, naye akasimamisha gari lake na upesi kwenda kule. Lakini alipofika akakumbuka tena kwamba alihitaji hela ya kulipia ili aweze kupiga simu, lakini hakuwa na hela mfukoni. Akarudi tena kwenye gari kuangalia kama kulikuwa na sarafu zozote ambazo aliweka humo kipindi cha nyuma na kuzisahau, kwa kuwa kihalisi alihitaji mia mbili tu kwa ajili ya kudumbukiza kwenye mashine ile. Akatafuta na kutafuta na hatimaye akapata mia sita za sarafu, naye akamwangalia "Sandra" kiufupi. Damu ile ilikuwa imeisha kufikia wakati huu, naye "binti" hakuwa amerejesha fahamu bado. Upumuaji wake ulionekana kuwa wa kawaida tu, hivyo Kendrick akatoka hapo kwa kasi tena kuelekea kwenye kibanda kile, kisha akaweka mia mbili na kupiga namba fulani.

"Hallo..." sauti upande wa pili ikasikika.

"Hello... General... ni mimi Kendrick Jabari...." Kendrick akasema.

"Kapteni... vipi mbona mapema? Halafu kweli, umenikumbusha kuna..."

"General, yametukuta matatizo makubwa sana! Meja Casmir hatuko naye tena, familia yake pamoja na yangu zimeuawa kikatili sana usiku wa kuamkia leo," akasema Kendrick kwa huzuni sana.

Jenerali Pingu akaweka umakini wake vizuri zaidi.

"Subiri Kapteni... unamaanisha nini?" akauliza.

"General mambo ni mengi sana ya kuzungumzia, lakini siwezi kusema kila kitu hapa. Nakuomba usiseme lolote kwa yeyote yule kuhusu simu hii... tafadhali sana," Kendrick akaomba.

"Unaongelea kuhusu... Demba Group au?"

"Hapana... ndiyo... yaani... ni..."

"Kendrick jaribu kutulia. Uko wapi?"

"Sijajua sana mkuu... ila nimetoka jijini huko masaa kadhaa nyuma ninaelekea kule ambako Meja na mimi tulijenga handaki chini, si unapakumbuka?"

"Ndiyo..."

"Ninaenda huko. Tafadhali General usimwambie yeyote, maisha yako pia yanaweza kuwekwa hatarini..."

"Si uniambie kinachoendelea kwa ufupi..."

"Siyo rahisi sana... ninahitaji kuwahi kwa saba... Gen... halloo... aagh!"

Muda wa kuongea ukawa umekwisha hivyo simu ikawa imekata. Kendrick akaweka mia mbili nyingine na kumpigia tena Jenerali Pingu.

"Kendrick..." akasema Jenerali Pingu baada ya kupokea tena.

"General... ni wewe tu zaidi ya Meja ndiyo unapafahamu huko, tafadhali usimwambie yeyote na uje peke yako. Ni suala la uhai au kifo. Watu tunaowaamini ndiyo wanaotuzunguka. Tafadhali futa au hata utupe simu mbali tukimaliza maongezi haya," Kendrick akasema.

"Kendrick umenichanganya sana kwa kweli yaani... sielewi nichukulie vipi haya yote..."

"Niamini General tafadhali. Nakusihi ufanye hivyo..."

"Sawa, nitafanya hivyo. Nitakuja moja kwa moja huko ijapokuwa nilikuwa na mipango mingine leo..."

"Asante sana. Nakuomba pia ukiweza General... uje na mifuko kadhaa ya damu type B, dawa za kuongeza nguvu, glucose, na vifaa mbalimbali muhimu vya kitiba... pitia kwa hospitali, sijui kama itahitajika gharama na nini lakini... ninahitaji kwa sababu nina mtoto hapa... ametokwa na damu nyingi... ameumia sana," Kendrick akasema.

"Aisee! Sawa Kendrick, usijali niko pamoja nawe. Nitaleta kila kitu. Natumaini pia mambo yote yatakuwa wazi nikifika. Nisubirie tu kijana wangu," Jenerali Pingu akamwambia.

"Nitashukuru sana... kwa heri," Kendrick akasema na kukata simu.

Akarudi kwenye gari haraka na kuliwasha ili waendelee na safari. Akamwangalia "Sandra" kupitia kioo cha juu mbele ya gari.

"Usijali binti yangu, Mungu ni mwema, utakuwa sawa. Keep fighting," Kendrick akasema hivyo.

Kisha akaliondoa gari hapo upesi.



Ilimchukua masaa kadhaa kufika kule alikodhamiria. Akashuka kutoka ndani ya gari na kumtoa "Sandra" akiwa amembeba, kisha akaanza kuelekea naye kule kwenye sehemu ya kujifichia.

Handaki hilo alilosemea Kendrick (tunnel), lilikuwa ni handaki walilosaidiana na Casmir kujenga kipindi cha nyuma, kwa ajili ya kujificha nyakati za hatari. Kuna wakati ambao kulitokeaga vita na taifa jirani, na wawili hao walipokuwa wakiwakimbia adui baada ya shambulizi la kushtukiza, walidumbukia kwenye shimo refu na kukaa humo kwa siku chache. Ndipo baadae walipofanikiwa kutoka, waliamua kuifanya iwe sehemu ya maficho kwa ajili yao na baadhi ya wanajeshi wengine, lakini hawakumwambia yeyote zaidi ya Jenerali Pingu kuhusu sehemu hiyo, ambaye aliwapendekezea waitengeneze vizuri na kulipanua chini kwa chini kwa ajili ya matumizi muhimu ya wakati ujao. Ilikuwa kwenye maeneo yaliyozungukwa na misitu na mashamba makubwa ya baadhi ya watu, lakini hakukuwa na makazi ya watu maeneo ya huku kipindi hiki. Njia ya kuingilia kwenye handaki hilo la chini ya ardhi ilifunikwa kwa mawe na mimea mingi yenye miiba, na kufikia wakati huu palikuwa panaonekana kama sehemu ya kichaka; hivyo haingekuwa rahisi kwa yeyote kutambua kulikuwa na handaki sehemu hiyo kwa sababu ilifichwa vizuri.

Kendrick akamweka "binti" chini na kuanza kuyaondoa majani na mawe sehemu hiyo, kisha akaanza kufukua udongo mwingi mpaka alipofikia chuma ngumu. Akauondoa udongo wa juu uliofunika chuma hiyo na kuivuta. Ilikuwa ni aina ya chuma nzito yenye umbo la duara ambayo ilikuwa kama mlango mdogo tu wa kuingilia chini huko, naye akauweka pembeni na kumfata "Sandra." Alikuwa makini kuangalia huku na kule kuona kama kungekuwa na mtu yeyote na kukosa, hivyo akambeba na kusogea naye pale.

Ilikuwa ngumu kuingia chini huko kwa sababu ya kuwa na mtu aliyepoteza fahamu, lakini Kendrick akajitahidi sana kuingia kwa uangalifu akiwa amemweka mgongoni kwake. Kushuka chini huko zilijengwa ngazi za shaba zilizokuwa imara, na ilionekana ni kama anaingia kwenye kisima. Akiwa amefikisha kichwa kwa ndani, akauvuta mlango ule mdogo wa chuma na kupafunika, kisha akaufungia kwa ndani. Alianza kushuka taratibu; mkono mmoja angekuwa ameutumia kuishikilia mikono ya "Sandra" iliyozungikia shingoni mwake, huku mkono mwingine akiutumia kushikia sehemu zile za ngazi. Hivyo kila akiposhusha mguu chini, angebadili mkono haraka wa kumshika binti na kutumia aliokuwa amemshikilia mwanzo kushikia sehemu za ngazi.

Akafanikiwa kufika chini, pakiwa na giza haswa, lakini kwa sababu alijua jinsi mpangilio ulivyokuwa, akatembea taratibu kuelekea upande ambao alijua kulikuwa na godoro chini. Akamlaza hapo taratibu na kuanza kupapasa sehemu ambayo alijua kulikuwa na viberiti, kisha akapata kimoja na kuwasha, naye akachukua chemli iliyokuwa humo na kuiwashia moto ili wapate mwanga.

Handaki hili halikuwa kama vile mahandaki ya wazungu ambayo yamejengwa kwa utaalamu, kwa sababu waliohangaika kulitengeneza walikuwa watu wawili tu, tena kwa miaka kadhaa. Jenerali Pingu alitaka iwe siri kwa kuwa ingekuwa ndiyo sehemu maalumu kwa wakati ujao kwa ajili ya masuala ya vificho, na kwa kipindi fulani ilionekana kama mipango hiyo iliahirishwa hasa baada ya majukumu yao jeshini kuongezeka, hivyo waliliacha tu kwa muda. Kendrick akawa ameketi karibu na "Sandra" akiangalia upumuaji wake na joto la mwili. Bado kijana alionyesha uvumilivu wa hali ya juu kwa kuwa hakupoteza uhai, naye Kendrick akaendelea kuomba kwa Mungu Jenerali Pingu awahi kufika, na akiwa salama.



Ulipita muda wa kama saa zima na nusu hivi pale Kendrick aliposikia kama kimlango kile cha chuma kinagongwa kwa kule juu. Akamwacha "Sandra" na kwenda kuangalia ilikuwa ni nani. Akapanda mpaka kufikia karibu zaidi, naye akatulia kusikilizia kama ungegongwa tena. Ukagongwa tena, naye Kendrick akagonga hapo kidogo pia, na sauti ya Jenerali Pingu ikasikika kwa juu.

"Kendrick, ni mimi. Nifungulie."

Kapteni Kendrick akafungua lock kwa ndani na kukinyanyua juu kidogo kimlango hicho, naye Jenerali Pingu akakitoa chote na kukiweka pembeni. Jenerali alishtushwa kiasi baada ya kuona jinsi Kendrick alivyokuwa amebabuka sehemu za mwili na upande mmoja wa uso wake, kuonyesha aliunguzwa vibaya sana kwa moto.

"Kendrick..."

"General, ingia haraka," Kendrick akamkatisha.

Jenerali Pingu akampatia begi moja ambalo lilikuwa na vitu vingi kwa ndani, naye akaingia pia akiwa amebeba begi lingine mgongoni. Akahakikisha ameufunga kwa ndani mwingilio ule kisha akashuka mpaka kule chini. Akamkuta Kendrick akiwa tayari amelifungua begi lile na kuanza kutoa vitu alivyohitaji kama mifuko ya damu, mirija, sindano, tochi, dawa kadhaa, akifanya upesi sana ili kumhudumia "binti" huyo.

Jenerali Pingu akasogea karibu zaidi na kuanza kumsaidia.

"Huyu si ni mtoto wa Casmir? Imekuwaje... nini kimetokea?" Jenerali Pingu akauliza.

"Nitakueleza kila kitu. Tumsaidie kwanza," Kendrick akasema.

Wakafanya yote waliyoweza ili kumsaidia. Wakamwekea damu, dawa, na kukisafisha kidonda chake cha kukatwa kwa kisu tumboni na kukiziba kwa dawa. Jenerali Pingu alikuwa ameleta maji na chakula kingi pia kisichoweza kuharibika, naye akampatia Kendrick ili aweze kula baada ya kuwa wamemaliza kumpa huduma "Sandra."

"Naona kama umewahi sana kufika General..." Kendrick akasema.

"Nilitumia helicopter kufikia kambi moja. Lakini kuja huku nilichukua gari na nilihakikisha sifuatwi," Jenerali Pingu akajibu.

"Natumaini haukuvamia hospitali kwa ajili ya vitu hivi vyote," Kendrick akasema huku akijaribu kumnywesha maji "Sandra."

"Hapana, nimenunua. Kendrick... mtoto anahitaji kuwa hospitali huyu. Na wewe unaonekana kama unahitaji tiba muhimu pia. Umeungua vibaya...."

"Niko sawa General... niko sawa," Kendrick akasema.

Jenerali Pingu akabaki kimya tu huku akimwangalia kwa huruma.

Kendrick akashusha pumzi huku ameinamisha kichwa chake kwa huzuni. Alionyesha kuchoka sana. Kisha akaanza kumsimulia Jenerali Pingu kila kitu kilichotokea. Kuanzia jinsi Kanali Jacob, Luteni Weisiko, Makamu wa Raisi, na wengine ambao hakuwatambua walivyoongea kuhusu mipango yao ya kumwondoa yeye na Casmir kwenye dunia ili mipango yao ifanikiwe. Alimweleza kuhusu jitihada zake na Casmir za kuwakamata Demba Group, na kwa kuunganisha matukio kwa haraka waliweza kubaini kwamba Demba Group ilikuwa ni kitu walichofanya watu hao. Jenerali Pingu akaweka wazi kwamba hakutoa amri yoyote kwa Kanali Jacob kuwaambia Meja Casmir na Kapteni Kendrick wahamie kule kwenye ofisi jijini kwao. Hii ilikuwa ni njia tu ya watu hao kuwasogeza wawili hawa karibu ili waweze kuwaangamiza kiurahisi. Kendrick akamweleza jinsi watu hao walivyo na ufundi katika mambo wanayofanya, ikionekana wanapewa nguvu kubwa sana, hivyo hata kwenda hospitali ingekuwa shida kwao.

Jenerali Pingu alikasirika sana. Alishindwa kuelewa ni kwa upumbavu kiasi gani wanaume wale waliweza kuruhusu tamaa ziwafanye watende unyama mkubwa namna hiyo. Hakukuwa na jambo lingine walilotaka tofauti na tamaa tu za kutaka kupata mambo makubwa; Jenerali Pingu aliona hilo wazi. Akamwambia Kendrick angeshughulika nao wote haraka sana, lakini Kendrick akamwambia alipaswa kuwa mwangalifu kwa kuwa watu hao walikuwa makini mno. Hakutaka kuhatarisha usalama wao hasa kwa sababu wangefikiri wamekufa, hivyo huenda Jenerali Pingu angemhatarisha tena "Sandra." Lakini mzee Pingu akamhakikishia kwamba haingekuwa hivyo, na kwa sababu Kendrick alikuwa amejifichia mbali, hangemhatarisha mpaka ahakikishe amewakomesha wanaume wale.

Baada ya kuwa ametumia muda huu na Kendrick, Jenerali Pingu akamuaga na kumwambia asitoke hapo mpaka atakaporudi. Kama ni vyakula vilikuwepo, dawa zilikuwepo, na hata ingawa ilikuwa chini ya ardhi, bado waliweza kupumua vizuri. Jenerali akamwahidi kwenda kuizimisha mipango ya wabaya wale haraka iwezekanavyo ili Kendrick na binti ya Casmir wasiendelee kujificha tena. Akamwambia akimaliza hayo, angemsaidia yeye na "Sandra" wapate matibabu nje ya nchi kabisa, naye akampatia Kendrick simu mpya ambayo aliiwekea laini maalumu anayoweza kuitumia hata akiwa nje ya nchi, na kumwambia wakati ambao angempigia tu, basi tayari angekuwa amekwishamaliza kuwashughulikia waasi wale.

Kendrick alijua wazi kwamba sikuzote matokeo huenda yasije kwa jinsi ambavyo wangetarajia, hivyo akamsihi sana Jenerali awe makini. Jenerali Pingu akaondoka hatimaye, na wakati alipotoka alihakikisha anaweka majani na mimea mingi ya vichaka kupaziba hapo juu ili hata kama nani angepita basi pasionekane kiurahisi, ingawa eneo hilo halikutembelewa na yeyote kwa ukawaida kutokana na kuwa kama msitu tu. Kendrick akabaki akimhudumia Xander, bila shaka yeye akifikiria ni Sandra, na wakati akiwa anaendelea kumwangalia usingizi ulimpitia kutokana na uchovu mwingi.



Kendrick alipokuja kuamka, bado alikuta "Sandra" amelala. Kipimo cha damu alichokuwa amemwekea kilikuwa kimekwisha, na "binti" alikuwa anatokwa na jasho sana, naye Kendrick akatambua kuwa homa kali ilikuwa imemtawala kwa sababu alichemka mno. Kendrick alijitahidi kwa kadiri ya uwezo wake wote kumpa huduma za kwanza ili kuituliza hali yake. Hakuchoka kumsaidia mtoto wa rafiki yake kwa sababu alihisi uhai wake ulikuwa mikononi mwake. Alimkanda, alimpa dawa kwa njia ya sindano, akambadilishia pamba kwenye kidonda, na kuendelea kuhakikisha anaituliza homa yake.

Ulipita muda mrefu wakiwa chini hapo, na wazo la kuiangalia simu ile likamjia. Akaiwasha na kuona ilikuwa ni Jumatatu sasa kwenye saa 4 asubuhi, ijapokuwa chini huku ungesema muda wote ni usiku tu, na kwa haraka alitambua ulikuwa umepita muda kiasi bila "Sandra" kula chochote. Hivyo akampatia maji kidogo na juisi nzito kama chakula, huku "binti" bado akiwa amelala. Alimnywesha taratibu na kwa uangalifu ili kiasi kingi kiingie tumboni mwake, na baada ya hapo akaanza kumkanda tena.

Kendrick aliwaza mengi kuhusu ni nini kilichokuwa kikiendelea kule nje. Alijua Jenerali alisema ni yeye ndiyo angemtafuta, lakini kwa sababu ya haraka yake kutaka kuondoka hawakutilia maanani kwamba mtandao chini huku ungeleta shida kubwa. Aliangalia uwezekano wa kupata hata "baa" moja ya mtandao, lakini haikuwezekana. Akaanza sasa kujiuliza afanye nini. Hakujua ikiwa "Sandra" angeendelea kuvumilia kwa kuwa uwezekano wa yeye kufa akiwa ndani ya usingizi ulikuwa mkubwa, na muda haukuwa rafiki kwao. Hivyo akaamua kutoka nje ili atafute mtandao, halafu ampigie Jenerali Pingu yeye mwenyewe. Akamwacha "binti" katika mazingira mazuri, kisha akaenda nje kule haraka. Bado eneo hilo halikuonekana na mtu yeyote, hivyo akaamua kwenda mpaka kule alikoliegesha gari lake kwa kificho. Akaingia ndani yake na kupiga simu kwa Jenerali Pingu. Mtandao ulikuwa ukileta shida, lakini hatimaye simu ya upande wa pili ikaita.

Ilipokea sauti ya mwanamke, naye Kendrick akasema ni rafiki ya Jenerali na alitaka kuzungumza naye. Lakini mwanamke huyo akamwambia kwamba Jenerali Pingu hakuwa hai tena, kwa sababu aliuawa kikatili na watu waliojiita Demba Group. Kendrick alichoka! Akauliza ilikuwaje, na mwanamke huyo akamweleza alivamiwa wakati wa usiku na watu hao alipokuwa amefika kwake, nao watu wote waliokuwepo nyumbani kwake wakauliwa pamoja naye.

Simu ikashuka taratibu kutoka sikioni mwa Kendrick kwa mshtuko mkubwa uliompata. Alijiuliza angefanya nini sasa, kwa sababu tumaini lake la mwisho wakati huu lilikuwa limetoweka pia.



★★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★★

WhatsApp +255 787 604 893
 
FOR YOU

Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Uhalifu, Mauaji, Visasi, Vita, Mambo yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA KUMI NA TISA

★★★★★★★★★★★★★★★★


Kendrick akabaki ndani ya gari lake akitafakari na kutafakari sana, na baada ya dakika nyingi, akapata wazo lingine ambalo kiukweli halikuonekana kama lingefanikiwa. Uzuri wa Kendrick Jabari ulikuwa ni kwamba sikuzote alijitahidi sana kuyaweka kichwani mambo mengi aliyoyaona kuwa muhimu, na hiyo ilitia ndani namba za simu za watu muhimu kwake. Angeweza kukariri namba kadhaa za watu kama mama yake, Casmir, Alice, Jenerali Pingu, hasa kwa ajili ya nyakati za dharura ambazo huenda angepoteza simu na kuhitaji msaada, kwa kuwa hao walikuwa ni baadhi ya watu wake wa karibu sana. Hivyo sasa akawa akijitahidi kuikumbuka namba ya mtu mmoja, ambaye alikuwa ni yule mwanamke kutokea Ghana aliyempenda sana Kendrick, yaani Margaret.

Alijitahidi kuvuta kumbukumbu ya namba yake kwa kuwa aliiona mara nyingi pindi mwanamke huyo alipomtafuta, naye akafanikiwa kuiandika yote na kupiga. Ijapokuwa alijua huenda ingekuwa ngumu sana kumpata hasa kwa sababu alikuwa nje ya nchi, bado Kendrick alijipa matumaini kuwa angempata tu, kwa sababu sasa hakuwa na mtu mwingine wa kumpa msaada ambao ungemtoa ndani ya makucha ya wanyama wakali waliomwinda. Alijua kuendelea kuwa nchini kungeleta shida hasa kwa sababu binti ya Casmir alihitaji msaada, na kama angetafuta msaada kwa hospitali kubwa au sehemu yoyote angehatarisha uhai wa kijana huyo.

Baada ya kujitahidi sana kumtafuta mwanamke huyo, ilishindikana. Alihisi hasira mno na wasiwasi mwingi, na hata matumaini yakaanza kupotea sasa. Alianza hata kuwaza ingekuwa bora kama wangekufa tu, kwa sababu isingekuwa na maana yoyote Mungu kuwanusuru wawili hawa ili wauawe tena haraka. Alielewa vizuri kwamba Kanali Jacob na Luteni Weisiko wangetaka kuhakikisha hakuna hata mmoja wao aliyebaki, hivyo kwa sasa kilichokuwepo ilikuwa ni kutoroka nchi, lakini angewezaje kufanya hivyo bila msaada? Alihofia kutafuta mtu mwingine wa nchi hii kwa sababu ni lazima taarifa zingewafikia tu watu wale na hiyyo kumweka hata mtu huyo hatarini, kwa hiyo Margaret ndiye aliyekuwa tumaini la mwisho.

Kwa kuwa hakujua ikiwa Jenerali Pingu aliwaambia watu wengine kuhusu yeye kuwa hai au la kabla hajauawa, Kendrick akaamua kujaribu kwa mara ya mwisho kumtafuta Margaret, na ikiwa ni kama muujiza tu, simu ikaita. Aliingiwa na hamu kubwa sana, akisema kwa kurudia-rudia "pokea, pokea, pokea..." huku anapiga-piga usukani. Margaret akapokea simu, naye Kendrick akafumba macho akihisi faraja kubwa moyoni. Mwanamke huyo akauliza ni nani, na baada ya Kendrick kujitambulisha, akauliza ni nini kilichokuwa kikiendelea.

Kendrick alimweleza kila kitu alichopitia. Margaret kwa kadiri fulani alijua kuwa kwenye nchi ya "boyfriend" wake huyu kulikuwa na matatizo, lakini baada ya Kendrick kumsimulia jinsi mambo mengi yalivyomgusa vibaya, mwanamke huyo alimwonea huruma sana. Alimuuliza alikokuwa, naye Kendrick akasema amejificha sehemu ya chini ya ardhi akiwa na binti ya rafiki yake. Kendrick alimweka wazi kuhusu hali ya "Sandra," na kwamba kwa kuendelea kukaa huku angezidi kuhatarisha uhai wa mtoto, na wake pia. Alimwomba sana Margaret amsaidie kumtoa huku kisiri na kumhamishia kwenye nchi nyingine akiwa na utambulisho mwingine mpya (new identity), akimwomba pia samahani kwa kuwa uhusiano wao haukuwa ukieleweka sana kwa siku za karibuni.

Margaret hakukawia kusema kwamba angefanya yote aliyoweza ili kumtoa kwa kuwa bado alimpenda. Alimwomba uvumilivu wa siku kama mbili, naye angekuwa ameshafanya mipango ya kisiri ili kufanikisha kila kitu. Akaomba amwambie alipokuwa kihususa zaidi, naye Kendrick akafanya hivyo. Margaret alipomuuliza Kendrick ikiwa "Sandra" angeweza kuvumilia kwa muda huo, Kendrick alimwambia kwamba angejitahidi kumwangalia vyema kijana wake mpaka kufikia wakati huo. Alimshukuru sana Margaret kwa utayari wake wa kumsaidia, naye akasema angeendelea kumsubiri. Alipomaliza kuongea naye, Kendrick akafumba macho na kuinamishia kichwa chake kwenye usukani. Alikuwa akitetemeka kwa msisimko wa faraja iliyomwingia, mpaka machozi yakakaribia kumtoka. Alishukuru Mungu kimya kimya na kutoka ndani ya gari lake ili arudi kwa "Sandra" hatimaye.

Alipoanza kuingia chini kule, alitambua kwamba mwanga wa chemli ulikuwa umezimika, naye akashuka upesi mpaka chini kwa kuwa giza lilikuwa nene haswa, na aliwaza hali ya "Sandra" pia. Akawasha tochi ya simu hiyo kumulikia mbele mpaka alipomkaribia, naye akakuta bado amefumba macho. Akaangalia upumuaji wake na joto la mwili, kisha akaichukua tochi aliyoleta Jenerali Pingu na kuiwasha. Aliona kwamba chemli iliishiwa mafuta baada ya kuichunguza, hivyo angehitaji kuiacha tochi ikiwaka. Wakati alipomgeukia "Sandra" kumwangalia tena, alishtuka kiasi baada ya kumkuta akiwa amefumbua macho yake huku akimtazama!

Macho ya Sandra (Xander) yalikuwa makavu, akimwangalia Kendrick kama mtu mwenye hasira, au mwenye nia ya kikatili kumwelekea mwanaume huyo. Lakini kwa Kendrick, ilikuwa ni sababu ya kufurahia, kwa sababu sasa "binti" huyo alikuwa amerejesha fahamu. Akamsogelea karibu zaidi ili amwangalie, naye Sandra (Xander) akataka kumkwepa na kunyanyuka, lakini maumivu ya jeraha lake tumboni yakamfanya atoe kilio cha maumivu. Ikambidi Kendrick ajitahidi kumtuliza, lakini akawa anakataa na kulazimisha kunyanyuka huku anarusharusha mikono kama anapigana naye. Kendrick alielewa kwamba "Sandra" alikuwa akiogopa sana, hivyo akamshikilia kwa nguvu kiasi na kumwambia ni yeye, uncle Kendrick.

Xander, akiwa ndani ya mwili huu wa Sandra, alikuwa akipumua kwa presha sana, akiwa tu ametoka kuamka na picha ya mwisho kukumbukia ikiwa ni jinsi pacha wake alivyopigwa risasi kichwani. Alianza kupeleka macho yake huku na huko, lakini aliona tu giza zito na uso wa Kendrick bila kujua walipo, huku akiyahisi maumivu ya kisu tumboni mwake.

"Shhh... Sandra... usijali... uko sawa, uko sawa, usijali... niko nawe... usiogope... uncle Kendrick yuko nawe...."

Kendrick akaendelea kumbembeleza, na taratibu Xander akajitahidi kutulia. Alikuwa akimwangalia Kendrick kwa macho yenye huzuni sana, na machozi yakawa yakimtoka huku mdomo wake ukitetemeka. Kendrick aliingiwa na simanzi nzito sana kuona jinsi "binti" huyu alivyokuwa na huzuni. Sura yake iliongea mengi sana zaidi ya jinsi ambavyo angeyasema kwa mdomo. Kendrick akampangusa machozi taratibu, naye Xander akaelekeza uso wake juu na kufumba macho.

"Unahisije mwilini? Tumbo linauma sana? Unahisi kama hauna nguvu?" Kendrick akawa anamuuliza.

Xander akabaki kimya tu.

"Sandra... niambie unahisije... unaumia sana niku... eh Mungu yaani hata sijui... aam, una niaa? Nikupe juice? Au, biskuti?" Kendrick akaendelea kumsemesha.

"Sandra yuko wapi? Dada yangu yuko wapi?" Xander akauliza.

Kendrick akabaki kumtazama.

"Niko wapi? Mama... baba... Azra... Salome... wako wapi?" akauliza tena.

Kisha akafumbua macho na kumgeukia Kendrick tena.

"S..Sandra... unahitaji ku..rejesha nguvu mwilini. Ulipoteza damu nyingi, unahitaji kula. Usijali tuko sehemu salama kwa..."

"Siwezi kuwa hapa. Mama... Sandra... familia yangu inanihitaji..."

Xander akasema hivyo huku akijaribu kunyanyuka kwa kasi, lakini akaishia kuumia tu tumboni zaidi na kulia kwa maumivu.

"Sandra, Sandra, tafadhali tulia nakuomba mwanangu...."

"No, nahitaji kwenda aagh... aahh...."

"Umeumia Sandra, nisikilize. Tafadhali tulia nikueleze kila kitu nakuomba...."

"Hapana... ni makosa yangu.... familia yangu inanihitaji... siwezi kuwaacha..."

"Sandra dear...."

"Kwa nini niliwapeleka? Ahhh... kwa nini nisingewaacha waniue tu... kwa nini niliwapelekaaa... naahh..." Xander akawa anaongea huku analia.

"Sandra dear, tafadhali usilie.... niko..."

"Ilipaswa kuwa mimi... kwa nini lakini... Sandraaa.... haikupaswa kuwa Sandra.... naahh... haapp... siwezi... I... Azra.... uncle Kendrick... niliwapelekea kifo familia yangu.... ni makosa yangu...."

Kendrick aliendelea kujitahidi sana kumbembeleza kijana huyu, akidhani ni kwa sababu tu ya huzuni kubwa aliyokuwa nayo ndiyo maana mambo mengine aliyasema bila kufikiri. Xander alilia kwa uchungu sana. Maumivu aliyohisi mwilini na tumboni hayakuweza kulingana na maumivu makali aliyokuwa nayo moyoni. Alilia mpaka akashindwa kuendelea kulia, muda huo wote Kendrick akiwa amekikumbatia kichwa chake huku akimbembeleza. Alipoanza kutoa sauti za maumivu zilizoashiria ni tumbo lake linauma, Kendrick akaanza kumhudumia haraka ili kumpoza.

Baada ya kumtulizia maumivu kiasi, Kendrick akajaribu kumpa chakula lakini akakataa kula.

"Sandra... unapaswa kula binti yangu. Unahitaji nguvu mwilini ili..."

"Sitaki kula. Kama ni kitu nachohitaji ni kuwa na familia yangu, kwa hiyo niache tu nijiunge nao," Xander akasema.

"Sandra usiongee hivyo. Nakuomba ule... la sivyo nitakulazimisha," Kendrick akasema hivyo kama kumshawishi.

Xander akafumba macho na kugeuzia tu shingo yake pembeni. Kendrick akaweka chakula pembeni na kukaa hapo hapo karibu yake.

"Najua unaumia Alexandra... najua jinsi ilivyo ngumu kwako na... ninakuelewa. Una... hhhh... Mama yangu aliuliwa usiku huo huo mbele ya macho yangu... na mimi sikuweza kufanya lolote. Sikuzote alikuwa akinifundisha kwamba... familia inakuja kwanza kabla ya mambo mengine yote... kwa sababu hakuna kitu chochote kilicho muhimu kuliko watu wa familia uwapendao, na wanaokupenda pia. Mwanangu... tumepoteza watu tunaowapenda sana. Nafikiri kama ni kitu ambacho wangetamani kuona kinatupata sisi ambao tumebaki... ni usalama wetu. Ikiwa kuna sehemu ambayo wapo sasa hivi... basi kutuona tukiwa sawa ni kitu ambacho kitawapa amani zaidi. Ni mimi na wewe tu ndiyo tumebaki.... na hiyo inafanya sisi sasa tuwe familia Sandra. Tafadhali... nahitaji uwe na nguvu..." Kendrick akasema kwa hisia.

"Nguvu kwa ajili nini? Hakuna kitu kingine kilichobaki kwa ajili yangu. Ni bora ungeniacha tu nife," Xander akasema akiwa bado amegeukia upande mwingine.

"Sandra... ninakuahidi... tutafanikiwa kutoka hapa salama, na nitafanya yote ndani ya uwezo wangu kuhakikisha haupatwi na jambo lolote baya...."

"Mambo mabaya yameshanipata. Ni kipi kingine ambacho kinaweza kuwa kibaya kwangu?" Xander akasema.

Kendrick akabaki tu kimya.

"Sitotaka kuwa mzigo kwa yeyote. Naomba... tafadhali..... niue," Xander akamwambia.

Kendrick akakunja uso wake kimshangao. Alihisi kuchoka sana kiakili kwa sababu alikuwa amejitahidi sana kumsaidia mtoto wa rafiki yake lakini kiwango chake cha kupoteza matumaini kilikuwa kimepita matarajio yake.

"Sandra... usiseme hivyo. Nakuahidi tutatoka hapa tukiwa salama. Mungu ana makusudi yake kuniacha mimi na wewe tukiwa hai. Kwa hiyo nakuomba usikate tamaa. Ishi kwa ajili ya wapendwa wetu wote walioondolewa hapa duniani bila kosa lolote. Ishi... ili tuje tuwaonyeshe wote waliotutendea hivi kwamba siku zote malipo ni hapa hapa duniani. Mimi na wewe tutayafanya maisha yao yawe kama ndoto mbaya ambayo watatamani kuikimbia ila watashindwa. Nakuahidi Sandra... tutawaonyesha. Tutawaonyesha maumivu kama waliyotupatia sisi..." Kendrick akamwambia kwa uhakika.

Xander alikuwa anadondosha machozi huku amekaza meno yake akihisi huzuni iliyoambatana na hasira nyingi. Kendrick akakishika kichwa chake na kuanza kuzilaza-laza nywele zake kama kumbembeleza, naye Xander akafumba macho yake taratibu.

Waliendelea kukaa humo kwa muda mrefu zaidi.



Baadae, Kendrick alipojaribu kumpa chakula, alikula kidogo, na hilo likamfariji mwanaume huyo. Mara kwa mara Kendrick angejaribu kumsimulia kuhusu mambo mengi aliyofanya pamoja na Casmir kwenye muda wote waliokuwa marafiki, kutia ndani jinsi walivyoitengeneza sehemu hiyo chini ya ardhi. Xander hakuwa na jambo lolote la kuongea hasa kwa sababu bado alikuwa kwenye huzuni, naye Kendrick alimweka wazi kuwa ndani ya muda mfupi msaada wa kuwatoa mafichoni ungefika.

Yaani kwa muda wote waliokaa hapo, iliwabidi kuvumilia hali kama kubana haja kubwa kwa kuwa hakukuwa na vyoo, lakini kwa haja ndogo walitumia vyombo vipana vya vyakula vilivyobaki tupu (kwa ajili ya Xander akiwa kwenye mwili wa kike), na chupa za juice au maji (kwa ajili ya Kendrick). Xander akaendelea kujitahidi kula na kutumia dawa ambazo zingemsaidia kurejesha nguvu.

Ilipofika muda ambao Kendrick alitarajia watu wa Margaret kufika maeneo yale, akamwandaa "Sandra" na kumwacha chini huko ili yeye aende nje kusikilizia. Alienda mpaka kwenye gari lake, ambalo wakati huu lilikuwa limeanza kupaushwa kwa vumbi kali. Akaingia na kujiweka humo kusubiri. Kwa mambo yote yaliyokuwa yamempata, ingekuwa rahisi kwa yeyote kukata tamaa, lakini kilichokuwa kinampa nguvu ya kusonga mbele wakati huu ilikuwa ni "Sandra." Aliendelea tu kusubiri hapo, akitumaini Margaret angetimiza ahadi yake, na baada ya masaa mawili hivi, ahadi hiyo ikatimia.

Zilifika gari mbili nyeusi pande hizo, lakini hazikwenda moja kwa moja usawa aliokuwa yeye kwa sababu inaonekana bado watu waliokuwemo hawakutambua alikokuwa kihalisi. Zikasimama tu, naye Kendrick akawaona wanaume wanne wakishuka kutoka humo, wawili wawili kutoka kila gari, nao hawakuweza kuliona gari la Kendrick. Akaendelea tu kutulia ili kuona kama wangefanya jambo fulani kuthibitisha ikiwa walikuwa kweli upande wake au la.

Simu yake ndogo ikaanza kuita, naye akapokea. Alipowaangalia tena, akamwona mmoja wao ameweka simu sikioni, na sauti iliyosema "Hallo..." ilifuatana na midomo ya mwanaume huyo. Kendrick akajibu, na mwanaume huyo akaanza kumwambia kwa kiingereza kuwa walikuwa wameagizwa na Margaret waje kumchukua na kumtoa nje ya nchi, lakini hawakuweza kutambua alikokuwa, hivyo awaelekeze kiusahihi. Kendrick akamwambia wamsubiri hapo hapo, kisha akatoka upesi na kuanza kuwafata mpaka walipokuwa. Walipomwona, wakampa pole, naye akawaelekeza shimo lile lilipokuwa ili wakamsaidie kumtoa "binti yake."

Xander, akiwa bado chini kule, alikuwa tu akiyatafakari maneno ya mwisho ya Sandra kwake kabla hajapoteza maisha. Alisema asisahau kwamba anampenda sana, na akamwomba apambane kokote aliko ili asalimike. Jambo muhimu zaidi hapa lilikuwa kwamba Sandra alikuwa amemwomba asalimike KWA AJILI YAKE, katika maana ya kwamba akisalimika yeye itakuwa ni kama amewaokoa wote. Maneno yao waliyotumia kutiana moyo, "for me, for you," Sandra hakuweza kuyamaliza na kuishia kusema "for me" kabla hajapigwa risasi, hivyo Xander akaona ni kama alinusurika ili kuja kuyamalizia maneno yale "for you" kwa vitendo.

Sauti za watu wakiingia hapo chini polepole zilianza kusikika, naye Xander akaangalia na kumwona Kendrick pamoja na wanaume wengine wakimkaribia. Kwa kuwa hakuwafahamu, akajaribu kunyanyuka ili kujihami, lakini Kendrick akamwahi na kumtuliza, akimwambia hatimaye msaada wao ulikuwa umefika......


★★★★


GHANA

Wawili hao walitolewa nchini kwao kisiri na kusafirishwa mpaka nchini Ghana. Ilikuwa ni kama ukombozi wa aina fulani, na kilichokuwepo baada ya kuwa wamewasili huko ilikuwa ni kumpeleka Xander (akiwa kwenye mwili wa Sandra) hospitali haraka iwezekanavyo. Watu wa Margaret waliwatendea kwa upole wawili hawa kwa kuwa waliona kweli walihitaji huduma muhimu sana kwa sababu ya kuumizwa kimwili, hivyo wakawapeleka moja kwa moja kwenye hospitali kubwa ya kibinafsi ili watibiwe upesi.

Margaret Dery alikuwa mwanamke mwenye pesa na mali nyingi pia. Baba yake alikuwa ni Waziri wa mambo ya ndani nchini humo, na yeye Margaret alikuwa ni mshiriki maalumu wa Bunge katika jiji la Kumasi nyanda za juu. Alipata cheo hicho si kwa sababu ya baba yake, bali kwa kuwa alikistahili na hata kuteuliwa na Raisi wa nchi hiyo yeye mwenyewe kutokana na bidii yake katika kuleta maendeleo. Alikuwa ameongoza ujenzi wa miundombinu mbalimbali sehemu za jiji hilo na hata vijiji vya mbali, kama ujenzi wa shule kwenye vijiji vya Nandom.

Kwa hiyo mwanamke huyu alikuwa na jina kubwa nchini humo. Alikutana na Kendrick kwa mara ya kwanza wakati yeye na baba yake walipokuja nchini miaka mingi nyuma pamoja na viongozi wengine, enzi hizo Margaret bado ni kijana mdogo tu asiyekuwa na cheo chochote. Wakati huo bado Casmir na Kendrick hawakuwa na vyeo vyao vikubwa jeshini pia, lakini walikuwa kati ya vijana wenye ustadi mzuri sana katika masuala ya kijeshi. Walikuwa miongoni mwa wale waliochaguliwa kuwapa ulinzi maalumu waliokuja kufanya uzuru, na Kendrick alikuwa mmoja wa wale waliopaswa kumlinda Margaret. Kwa hiyo kuna hali fulani zilizojitengeneza na kufanya binti huyo akaanza kuvutiwa na mwanaume huyo aliyekuwa ngangali kwelikweli, nao wakajikuta wanaingia kwenye mahusiano ya kisiri ndani ya muda huo mfupi.

Margaret aliikubali show ya Kendrick kiasi kwamba akamwomba namba za simu ili hata akirudi kwao waendelee kuwasiliana. Kwa hiyo mara kwa mara Margaret angetoka Ghana na kwenda Tanzania ili tu kuwa pamoja na Kendrick, na hata wakati mwingine angempeleka nchini kwao pindi ambazo Kendrick angekuwa na likizo fupi. Ijapokuwa baadae uhusiano wao ulififia, hasa kwa kuwa Margaret aliolewa na mwanaume mwingine, bado alionyesha kumpenda sana jamaa, na alimwambia hangemsahau hata ingawa aliolewa na mtu mwingine.

Walipowasiliana mara chache siku za karibuni kabla ya ishu za Demba Group kuzuka, Margaret angemwambia jinsi ambavyo ndoa yake ilikuwa ni maumivu tu, kwa sababu mume wake alikuwa akitoka nje pia, lakini waliiendeleza ili kuokoa jina zuri la hadharani (reputation). Kwa kipindi kirefu Kendrick alikuwa akifanya kama kumkwepa kwa sababu hiyo, lakini katika wanawake wote aliowahi kuwa nao baada ya mke wake kufa, Margaret ndiye aliyemwingia vizuri zaidi.

Kwa hiyo, ikiwa mume wake Margaret angejua kuhusiana na hili la kumpeleka Kendrick Ghana, maoni yake yangekuwa kwamba Margaret kamleta hawala yake. Lakini Margaret alikuwa makini sana kutofanya Kendrick ajulikane na watu ambao wangeanza kueneza porojo. Kendrick alipatiwa tiba kwenye sehemu za mwili wake zilizounguzwa vibaya kwa moto, ikiwemo upande wake mmoja wa uso. Jicho lake moja liliathiriwa vibaya na mvuke mkali wa moto, hivyo kuanzia hapo aliamua kuvaa lenzi ya kiziba jicho cheusi (kwa kukiweka ndani ya jicho).

Sandra (Xander) alipatiwa matibabu pia, na afya yake ikarudi kuwa vizuri. Madaktari waliomhudumia waliwaambia Kendrick na Margaret kwamba lilikuwa jambo lisilo la kawaida kwa mtu kupoteza damu nyingi na kukaa muda mrefu bila matibabu maalum kusalimika, kama ilivyokuwa kwa "Sandra." Walisema mwili wake ni kama ulikuwa na nguvu ya ziada ambayo haikueleweka, na ni nguvu hiyo ndiyo ilimfanya astahimili kwa muda mrefu. Kihalisi hiyo ilikuwa ni kani ya Xander ndani ya mwili wa Sandra ndiyo iliyofanya jambo hilo liwezekane kutokana na kuingiliana kwa miili yao.


★★


Basi, mwaka mmoja kutokea hapo, Kendrick na Xander waliendelea kuishi huko huko Ghana kisiri. Kendrick aliunganishwa na Margaret kufanya kazi kwenye usimamizi wa kitengo fulani kidogo cha uzalishaji wa zao la Cocoa, ambazo zingesafirishwa na kuuzwa nje ya nchi. Kazi hii ilimsaidia kuingiza kipato cha kujikimu akiwa pamoja na Sandra (Xander). Kule jijini Kumasi, Margaret alikuwa na maduka kadhaa ya bidhaa kwenye soko fulani kuu, naye alikuwa ameyaweka hayo pia chini ya uangalizi wa Kendrick, bila yeyote kutambua kwamba wawili hao walikuwa na uhusiano.

Margaret alikuwa amewatafutia nyumba fulani maalum na kubwa kwenye sehemu iliyojitenga na makazi ya watu wengine, na ambayo ilizungukwa na misitu. Kulikuwa pia na sehemu eneo hilo yenye maporomoko ya maji iliyojificha sana ambayo Xander alipendelea kwenda kutulia akiwa mwenyewe. Mara nyingi Margaret angekuja kwenye nyumba hiyo kukutana na Kendrick, nao wangepeana mahaba mazito na kufurahia wakati mwingi pamoja, kisha angeondoka tena mpaka wakati mwingine. Kwa njia fulani sehemu hiyo ilikuwa kama kichali cha mapenzi yao.

Kendrick hakutaka Xander ajihusishe na kazi zozote, zaidi ya kumletea walimu fulani hapo ambao walimfundisha mambo mengi sana. Alijifunza lugha, alijifunza mbinu na mitindo mbalimbali ya maisha, naye akapanua zaidi ufahamu na utambuzi wake. Alianza kujifunza sarakasi na mitindo ya kupigana yeye mwenyewe kwa kuwaiga wataalamu wa mambo hayo kwenye vipindi fulani vya runinga. Mwanzoni ilikuwa kama kigezo tu cha kuondoa upweke, lakini baadae aliiona kuwa njia nzuri ambayo ingemsaidia kujua jinsi ya kujilinda siku za mbeleni. Kuishi ndani ya mwili wa dada yake kulikuwa na magumu mengi, lakini mwishowe alizoea. Alikuwa pia amekwishamwambia Kendrick kuhusu yeye kuwa ndani ya mwili wa pacha wake, kwa hiyo Kendrick aliendelea kujizoeza kumwona kama mwanaume badala ya mwanamke, ingawa jambo hilo lingepaswa kuwa siri.

Mwanzoni, Xander alidhani pesa ambazo Kendrick alikuwa anatumia kufanya mambo yote zilitoka kwenye biashara zake na Margaret, lakini baadae akaanza kuhisi kwamba kuna vitu Kendrick alifanya kwa kificho vilivyomletea mali nyingi ambazo alificha. Kuna wakati alikuwa akitafuta kifaa fulani ili atumie kutengeneza banda kwa ajili ya mifugo yake michache ya sungura, pale alipojikuta ameingia kwenye chumba kidogo sana kilichofungwa kwa minyororo minene na kufuri kubwa. Alijiuliza ni kwa nini hakuwahi kuiona sehemu hiyo, naye akatafuta njia ya kulifungua kufuri hilo na kufanikiwa. Aliingia na kukuta ni chumba kilichokuwa tupu kabisa, lakini kilitunza sanduku fulani dogo la chuma.

Kwa sababu ya udadisi, alilichukua na kulifungua, na hapo akapata kuona mabamba kadhaa ya dhahabu safi kabisa. Alijiuliza maswali mengi, kutia ndani ni jinsi gani "uncle" wake alikuwa amezipata dhahabu hizo, ila akaamua kulirudisha sanduku hilo na kukaa kimya tu kama hakuwahi kuliona. Lakini kwa sababu alihitaji kujua ni jinsi gani Kendrick alikuwa akizikusanya, akaanza kumfatilia kisiri mpaka alipokuja kugundua kwamba alikuwa anaziiba dhahabu hizo. Alimsikia akitoa maelekezo ya mpango wa kuiba dhahabu kwa mtu fulani, naye akafatilia hilo kisiri pia na kupata kuwaona watu hao walipozileta dhahabu hizo. Wangegawana, kisha yeye Kendrick angetunza zile alizopatiwa kwenye sanduku lile lile.

Kwa kuwa Xander hakuelewa sababu za Kendrick kufanya haya, akaamua tu kuuliza. Kendrick naye akawa mnyoofu na kumwelezea kila kitu bila kuficha lolote. Alieleza kwamba alikuwa akijikusanyia mali nyingi ili aje kuwa na nguvu kubwa sana, na lengo lake la kuitumia nguvu hiyo lilikuwa ni kuwalipa kisasi wale wote waliomsababishia yeye na Xander matatizo. Alimwambia hakuwa amesahau ahadi yake kwake kuhusiana na hilo, na hiyo ilikuwa ndiyo sehemu ya mpango wake wa kuja kurejea nchini kwao na kuwapatia maumivu wabaya wao.

Kendrick alidhani kwamba Xander angemchukulia vibaya kutokana na mambo aliyofanya, lakini akashangaa kiasi baada ya Xander kumwambia kwamba ikiwa alitaka kufanikisha hilo, basi angepaswa kutafuta watu wenye vipaji fulani ambao wangemsaidia kukusanya mali hizo haraka, na siyo kidogo kidogo. Ushauri wake huu ulimfanya Kendrick aone kuwa Xander alimuunga mkono, naye akasema angefanya kama alivyomwambia.

Kuanzia hapo, Kendrick akawa anaendelea na kazi zake za kawaida huku kweli akitafuta watu ambao wangefaa ili kusaidia kutimiza kisasi chake yeye na Xander. Kwa upande wa Xander, tokea alipojua tu kwamba Kendrick alikuwa akifanya mipango ya kulipiza kisasi, alianza kuunda mbinu zake yeye mwenyewe zenye ufundi sana, bila hata kumwambia Kendrick, ili naye aje kutumika kwenye kisasi hicho.



★★★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★★★

WhatsApp +255 787 604 893
 
FOR YOU

Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Uhalifu, Mauaji, Visasi, Vita, Mambo yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA ISHIRINI

★★★★★★★★★★★★★


Baada ya miezi mingi kupita, Kendrick alifanikiwa kuwapata watu ambao wangemsaidia kuiba pesa au dhahabu nyingi zaidi. Alikuwa ametafuta watu wenye uzoefu mzuri katika mambo fulani hususa. Kutokea Ghana walikuwa ni Oscar, Victor na Mensah, huku Torres akitokea Jamaica. Wote hao walikuwa na aina fulani za kesi kipindi cha nyuma kutokana na kutumia vipawa vyao kufanya mambo haramu (illegal) yaliyohusisha wizi, naye Kendrick aliwaahidi kwamba wangepata faida kubwa kwa kufanya kazi pamoja naye.

Kazi ya kwanza waliyoifanya iliongozwa na Torres, nao walitakiwa kuiba pesa zilizokuwa zikihamishwa kwa kutumia magari kuelekea Manispaa fulani. Lakini mipango yao iliharibika, na ilikuwa kidogo tu Victor na Mensah wakamatwe ila wakafanikiwa kuponyoka bila kutambulika. Kwa kuwa kazi walizojipanga kufanya zilionekana kuwa ngumu, walihisi wangejihatarisha zaidi na kujadili kuhusu kuacha tu kuzifanya, na ndipo Sandra (Xander) akajiunga nao.

Kendrick hakutaka Xander ajiingize kwenye mambo hayo, lakini alikuja na mbinu mpya kisha kuiingiza katika mpango mmoja wa Torres. Aliwasaidia kuona njia nzuri zaidi ya kufanikisha kazi fulani, nao wakakubaliana kuitumia ili kuona matokeo yangekuja vipi. Walikuja kufanikiwa kuiba kontena dogo lenye dhahabu zilizokuwa zikisafirishwa kuelekea nje bila hata kujulikana kwa sababu ya mbinu hiyo aliyowapa Sandra (Xander). Walifurahi sana, nao wakamuuliza Kendrick "binti" huyo alitoka wapi, na kwa nini hakuwa pamoja nao kwenye kazi ya kwanza iliyoshindikana.

Ikambidi Kendrick akae na kuongea na Xander. Alimuuliza kama angetaka kujiunga nao kwa ajili ya kazi zingine, naye Xander akakubali. Ila akamkumbusha kwamba wangefanya kazi hizo ndiyo, lakini hawakupaswa kusahau kuwa walizifanya ili kuja kutimiza malengo yao, naye Kendrick akamwambia aondoe shaka kuhusu hilo. Alipokuja kujitambulisha vizuri zaidi kwa Torres, Victor, Mensah pamoja na Oscar, Xander alibadili jina na kujiita Lexi. Kwa hiyo, kuanzia hapo wote walimtambua kama Lexi.

Kendrick alikuja kumuuliza baadae kwa nini aliamua kujiita hivyo, naye akamwambia ni kwa sababu sikuzote Sandra alitamani jina lake lifupishwe namna hiyo, lakini kwa kuwa ilizoeleka kumwita "Sandra," basi ikawa hivyo tu. Kwa hiyo kwa kujiita jina hili, Xander angeendelea kukumbuka kwamba pacha wake ni sehemu muhimu sana kwenye maisha yake kutokea hapo na kuendelea, nayo ingekuwa ni moja kati ya njia nyingi za kuendelea kumuenzi akiwa sehemu ya mwili wake.

Katika kazi zao zote za kupokonya pesa au vito, walihakikisha hawamuumizi yeyote, isipokuwa labda kuwe na ulazima wa kuwaumiza wale waliowazingua moja kwa moja. Wangeiba vitu hivi wakiwa wanajua haingeleta hasara yoyote kwa wanyonge, bali kwa watu wabinafsi tu walioziendesha shughuli hizo. Lexi sasa akawa pamoja nao, na kutokea hapo, wizi walioufanya wa mali ulifanikiwa sana bila yeyote kuwajua. Wangefanya wizi mara moja kwa mwezi katika pindi na sehemu zisizotabirika kabisa.

Muda ulipita, nao waliendelea kuzoeana hata zaidi. Baadae, Kendrick aliwaweka wazi wengine kwamba alikuwa akisaidiana na Lexi kuunda mpango wa kulipiza kisasi utakaowapeleka Tanzania, hivyo endapo wakati huo ungefika, kama wangehitaji kurudia maisha yao mengine basi wangekuwa huru kufanya hivyo. Lakini vijana hao wakakanusha na kusema kwa lolote lile ambalo boss wao angefanya, wangekuwa pamoja naye kwa sababu aliwabadilishia sana maisha yao.

Wote kwa pamoja wakaendelea kuwa kama familia ndogo ya "wezi" wenye ufundi wa hali ya juu sana.


★★★★


Miaka mitatu kutokea hapo ilipita, na kufikia wakati huu, Kendrick Jabari alikuwa amekusanya mali yenye thamani ya dola bilioni 1 za kimarekani, yaani trilioni 2.2 za kitanzania wakati huo (2,200,000,000,000), kutokana na kutunza vitu alivyopata kwa kazi nzuri za kimya kimya walizofanya vijana wake kwa kuwaunga mkono. Alikuwa akiwapa mafungu yao bila shaka, nao walifurahia maisha mazuri lakini kwa kuwa makini sana ili wasijitie kwenye matatizo. Mwongozo walioupata kutoka kwa Torres na Lexi uliwasaidia kujiendesha vizuri wakiwa hadharani, nao wakawa wakiishi maisha ya aina mbili tofauti kabisa; wezi, na raia wema.

Mambo yote hayo yaliyoendelea gizani hayakujulikana kwa Margaret hata kidogo. Bado aliendelea kuonana na Kendrick, hasa kwa kuwa Kendrick alimwongezea ufanisi mwingi kwenye biashara zake za pembeni. Lexi alikuwa akiwafundisha wengine lugha ya Kiswahili, nao walikuwa wameanza kuizoea ijapokuwa ni Mensah ndiye iliyempa shida sana. Oscar alikuwa ndiye kijana mdogo zaidi, lakini alichangamana nao vizuri, nao walimheshimu akiwa kama mmoja wao. Victor mzee wa kutengeneza vitu bandia ndiye pekee kati yao wote aliyekuwa na watoto, wawili, nao waliishi upande mwingine wa nchi hiyo, jijini Accra. Angewasiliana nao mara kwa mara na kuwatumia pesa nyingi pia za matumizi, huku akifurahia bata na familia yake hii mpya.

Sasa ilikuwa imefikia hatua ambayo vijana hawa wangepaswa kujiandaa kwenda Tanzania ili kuanza kazi. Lexi na Torres walikuwa wamebuni mpango huu kwa umakini wa hali ya juu ndani ya miaka hiyo, na sasa wangeanza kufanya mambo kwa vitendo. Wangeanza kutengeneza na kununua vifaa muhimu walivyohitaji, kisha baadhi yao wangetakiwa kwenda Tanzania ili kuweka mambo sawa kule kwa ajili ya kuwakaribisha waliobaki. Kulikuwa na kazi moja iliyobaki ya kuiba dhahabu, kisha ndiyo wangeanza kupiga hatua za mipango hiyo ya kisasi. Mpaka kufikia sasa hawakuwa wamegundulika kwa sababu waliiba kwa kiwango hususa walichopanga kila mara dhahabu ziliposafirishwa, hivyo mara nyingi wangewaacha wamiliki na wasimamizi wa mambo hayo wakilaumiana wenyewe kwa wenyewe huku wao wakiwa wameshatembea mbele.



Siku fulani kabla ya kazi hiyo kufanyika, Lexi alikuwa akitembea mitaa ya mji mmoja kama kufanya mizunguko tu ya kawaida. Sikuzote wanasema kabla ya dhoruba kali hali ya hewa huwa inakuwa imetulia, na kwa timu yao ndivyo ilivyokuwa. Maisha ya kawaida waliyoishi baada ya kumaliza kuiba yasingewatia mikononi mwa sheria kwa kuwa haingekuwa rahisi kuwajua. Akiwa anapita eneo lenye soko dogo la biashara, aliweza kuwaona wanaume kadhaa sehemu iliyojificha sana.

Kwa udadisi, akapitia njia nyingine na kwenda upande ambao alijibanza ili kuweza kuwachungulia. Aliwaona wanaume hao watano wakimpa mwanamke kijana bunda la pesa kwa kificho, naye akawapatia fuko dogo lenye vitu vyeupe kwa ndani. Mwanamke huyo alionekana kuwa na haraka kutaka kuondoka, lakini wakamzuia kwanza, mmoja wao akachomeka kidole kwa ndani na kukitoa kikiwa na unga mweupe, kisha akakilamba. Kwa haraka Lexi akatambua yalikuwa ni madawa ya kulevya. Wanaume hao wakamwachia mwanamke huyo, naye akaondoka upesi.

Lexi akatikisa kichwa kidogo, kisha akajiondokea hapo. Alipokuwa akitembea njiani kurejea kwenye gari lake ili aende kule walikoishi, alishangaa kumwona tena mwanamke yule akiwa anakimbia kwa kasi sana, na ndipo wanaume wale wakaonekana wakimkimbiza kwa nyuma. Lexi alijiuliza tatizo lilikuwa ni nini, lakini kwa kuangalia sehemu ambayo mwanamke huyo alikimbilia akajua hangefika mbali nao wangemkamata na hata kumfanyia jambo fulani baya. Akaamua kuelekea huko pia ili kujua nini kingefuata.

Alifika mpaka sehemu ambayo aliwakuta wanaume wale wakipiga kitu fulani chini kwa miguu yao kikatili sana. Alizisikia pia kelele za vilio za mwanamke yule, naye akatambua watu hao walikuwa wakimpiga namna hiyo. Hakukuwa na watu wengine sehemu hiyo, hivyo Lexi akafika hapo upesi na kuwasukuma kwa nguvu, nao wakasogea pembeni huku wakimtazama. Alipomwangalia mwanamke huyo, alikuwa amejikunja chini huku akitoka damu puani na mdomoni, naye akamwonea huruma sana.

Mmoja wa wale wanaume akamfata Lexi na kutaka kumpiga, lakini akawahi mkono wake na kuukunja, kisha akauvunja. Jamaa alipiga kelele kama jogoo anayewika (ila sauti iendelezwe), naye akaanguka chini. Wengine wakashangaa sana, nao wakamfata Lexi ili kumshambulia, lakini akawachambua wote kama karanga. Walifanikiwa tu kumpiga sehemu chache za usoni na mgongoni, lakini wote wakaambulia kulala chini huku wanakoroma kwa maumivu. Lexi alikuwa anapumua kwa nguvu, kisha akamwangalia mwanamke yule, ambaye alikuwa anamtazama kwa wasiwasi.

Mwanamke huyo akajitahidi kunyanyuka na kuanza kukimbia, akifikiri Lexi ni askari. Lexi akaanza kumfukuzia pia mpaka akamshika na kumsukumia ukutani.

"Don Allah kar ka cutar da ni... (tafadhali usiniumize)" mwanamke huyo akaongea kwa kikabila.

Lexi akawa anamwangalia tu asielewe anamaanisha nini.

"Ba ma gaske ba ne... ba zan iya sake shiga kurkuku ba... don Allah.... (hata hazikuwa halisi.. siwezi kurudi jela tena.. tafadhali...)"

"Shut up!" Lexi akamwambia kiukali kidogo.

Mwanamke huyo akabaki kumwangalia huku akiwa amekunja sura kuonyesha alihisi maumivu. Lexi akamvuta na kuanza kuondoka naye. Akampeleka mpaka sehemu aliyoacha gari lake na kumwingiza, kisha akaanza kumpeleka kule walikoishi. Njia nzima hawakusemeshana lolote, na mara kwa mara mwanamke huyo angemwangalia kwa wasiwasi, lakini pale ambapo Lexi angemwangalia tu, angekwepesha macho na kutazama pembeni.

Walipofika, ilibidi Lexi alazimishe kumvuta kwa sababu alikuwa akigoma kwenda kwa kuhofia usalama wake kutokana na kutoijua sehemu hiyo iliyokuwa mbali, na imejitenga sana. Akampeleka mpaka ndani ya nyumba, na wale waliokuwepo wakashangaa. Alikuwepo Torres, Victor, na Oscar.

"Who's this? Why'd you bring her here? (Nani huyu.. kwa nini umemleta hapa?)" akauliza Victor.

"Found her getting beat up from her boyfriends. I don't think she speaks English... or not (nimemkuta anapewa kipigo na wapenzi wake. Sidhani kama anazungumza kiingereza.. au la)," akasema Lexi.

"Man! Look at her (Dah! Hebu mwangalie)," Torres akasema huku akisogea karibu.

"Well, what language does she speak? (basi anazungumza lugha gani?)" akauliza Oscar.

"Native aam... Hausa (kikabila.. kihausa)," Lexi akajibu.

"Oh..." Victor akasema na kumsogelea pia.

Mwanamke huyu akawa anawaangalia wote kimashaka.

"Menene sunanka? (unaitwa nani?)" Victor akamuuliza kwa kikabila hicho.

Mwanamke huyo akamwangalia tu.

"Kuna jin turanci? (unaweza kuzungumza kiingereza?)" Victor akauliza tena.

"Torres, help her... (Torres msaidie)" Lexi akamwambia.

"Okay. Hey... come on, let's go (Sawa.. wewe, twende)," Torres akamshika kiupole na kuanza kuondoka naye.

Wote walikuwa wanamwangalia kwa huruma kiasi. Torres akawa amempeleka kwenye chumba chenye vifaa vya kitiba ili kumpa huduma za kupunguza maumivu yake.

"You sure boss is gonna go cute with you bringing a total stranger here? (Unadhani 'boss' atapenda wewe kumleta mtu asiyefahamika hapa?)" Victor akamuuliza Lexi.

"You were a stranger (Hata wewe ulikuwa haufahamiki)," Lexi akamwambia.

"Boom! Burned... hahahahah (umeunguzwa)," Oscar akamwambia Victor kiutani.

Lexi akawaacha na kwenda chumbani kwake.

Baadae, Kendrick na Mensah wakawa wamerejea kutoka safari yao mida ya usiku. Oscar, akiwa pamoja na Victor, akamwambia Kendrick kwamba Lexi alikuwa ameleta mgeni mwingine hapo leo, naye Kendrick akamwambia amwite Lexi. Baada ya kufika, Kendrick akamuuliza ni nini kilikuwa kinaendelea. Lexi akaelezea jinsi alivyoyaona mambo yaliyotokea, na kusema alimwonea huruma kwa kuwa watu wale wangemuua ikiwa asingemsaidia.

Kendrick akamwambia Lexi halikuwa jambo la busara kuleta mtu yeyote tu hapo bila kumjua vizuri kwa sababu ingekuwa hatari kwa mambo yao mengi. Akamuuliza baada ya kumpatia huo msaada nini kingefuata sasa? Atoke nje huko na kwenda kumwambia mtu fulani ambaye atamwambia mtu fulani kuhusu sehemu hii waliyokuwa? Lexi akatazama tu chini akitafakari maneno ya "uncle" wake, naye Kendrick akamwambia Oscar akamlete mwanamke huyo hapo. Bila kukawia Oscar akamfata na kufika naye.

Mwanamke huyo alikuwa amevaa nguo safi sasa; sweta la mikono mirefu na kaptura ya kijani yenye mifuko mingi. Sehemu hii waliyokuwemo ilikuwa kama ofisi ya ndani ya Kendrick, naye Torres akafika hapo pia kukamilisha kundi lao lote. Mwanamke huyo akawa amesimama mbele ya meza pana kiasi ya kioo, ambapo alitazamana uso kwa uso na Kendrick aliyeketi kwenye kiti chake upande wa pili. Alikuwa amewekewa bendeji ndogo usawa wa jicho lake, na mdomo wake wa chini ulivimba kidogo. Akamwangalia Lexi kiufupi, kisha akamtazama tena Kendrick. Kwa kumwangalia tu alitambua kwamba Kendrick bila shaka ndiye aliyekuwa fahali kwenye zizi hili.

"What's your name? (jina lako nani?)" Kendrick akamuuliza.

"I don't think she understands English. Anaongea tu Hausa language (sidhani kama anaelewa kiingereza.. anazungumza tu kihausa)," akasema Victor.

"LaKeisha," mwanamke huyo akasema.

Wote wakamwangalia.

"What?" Kendrick akauliza.

"LaKeisha. That's my name (LaKeisha.. hilo ndiyo jina langu)," akasema tena.

"Sucks to be you," Oscar akamtania Victor, akimaanisha hakuwa sahihi kufikiri mwanamke huyo hajui kiingereza.

"Kumbe anajua... why the hell were you quiet all that time? (kwa nini sasa ulikuwa kimya muda wote huo?)" Victor akamuuliza.

LaKeisha akabaki kimya tu. Wakati huu alionekana kama vile haogopi, bali yuko makini.

"How old are you? (miaka yako mingapi?)" Kendrick akamuuliza.

"I'm 25," akajibu Lakeisha.

"I understand my niece helped you today from an unpleasant crisis. Mind telling me why those men were beating you up? (naelewa mpwa wangu amekusaidia leo kutoka kwenye shida fulani.. unaweza kuniambia kwa nini wanaume hao walikuwa wakikupiga?)" Kendrick akamuuliza.

LaKeisha akatulia kidogo, kisha akaanza kuongea.

"Those men are drug dealers. I was set by my boss to bring them a package, and in return they'd give me money to take back to him. They gave me the money, but then all of a sudden they started attacking me... until your daughter found me... and helped me... (wanaume wale wanafanya kazi ya madawa ya kulevya.. nilipangwa na 'boss' wangu kuwapelekea mzigo, halafu wangenipa pesa ili nimpelekee, lakini ghafla wakaanza kunishambulia.. mpaka mwanao alipokuja kunisaidia..)"

LaKeisha akayasema hayo na kumwangalia Lexi tena.

"Why would they just start... attacking you? (kwa nini wangeanza tu kukushambulia?)" Mensah akamuuliza.

"Because I cheated (kwa sababu nilidanganya)," LaKeisha akasema.

"With what? (na nini?)" akauliza Oscar.

"With the drugs. They were fake (na madawa.. yalikuwa bandia)," Torres akajibu kwa ajili yake.

LaKeisha akatikisa kichwa kukubali.

"Why'd you do that? What about your boss? (kwa nini ulifanya hivyo? vipi kuhusu boss wako sasa?)" Mensah akauliza tena.

"I had a huge debt... that I owed another man. I wanted to clear it out first because he was going to kill me if I didnt, and my new boss... he shouldn't have known about that. So I sold those goods elsewhere and paid off the other guy, and then... (nilikuwa na deni kubwa sana kwa mtu mwingine.. nilitaka kulifuta kwanza kwa sababu angeniua kama nisingemlipa, na boss wangu mpya hakutakiwa kujua.. kwa hiyo niliuza madawa aliyonipa kwingine ndiyo nikamlipa yule wa zamani, halafu..)" akaishia tu hapo na kuangalia chini.

"You made fake goods and went out to sell them to the men whom you were supposed to give the real ones. Good thinking! You got bruised all over your face to show that (ukatengeneza madawa bandia na kuyapeleka kwa wale uliotakiwa kuwapa yale halali.. una akili sana! uso wako wote umejaa majeraha kuonyesha hilo," Torres akasema kikejeli.

"So what happens now that you've lost your new boss' goods and the money? (kwa hiyo nini kitafuata sasa kwa kuwa umepoteza bidhaa za boss wako wa sasa na pesa yake?)" Lexi akauliza.

"He's going to kill me! I don't know what am going to do (Ataniua!.. yaani sijui nitafanya nini)," LaKeisha akasema.

"Well its your fault. I'd kill you too (ni makosa yako.. hata mimi ningekuua pia," akasema Mensah.

"I had no idea they were smuggling drugs in this country. What type were they? (sikujua kulikuwa na biashara za madawa hii nchi.. yalikuwa ya aina gani?)" akauliza Oscar.

"Cocaine... heroine," LaKeisha akasema huku akiwa ametazama chini.

"Damn!" Oscar akashangaa.

Kendrick akatazamana na Lexi kwa makini. Ni kama walikuwa wanaongeleshana kwa macho yao.

"Boss... what are we going to with her? You know we can't just let her walk out of here (mkuu, tutamfanya nini huyu? unajua hatuwezi kumwacha aondoke hapa)," akasema Victor.

"Yeah. I think we should just help her boss with the killing. She'll definitely talk this place out with the first knucklehead she meets, all thanks to Lexi (ndiyo.. nafikiri itakuwa vyema tukimsaidia tu boss wake kumuua huyu.. maana bila shaka ataenda kuropoka huko nje kuhusu sehemu hii na mpuuzi wa kwanza atakayekutana naye.. hiyo yote kwa sababu ya Lexi)," Mensah akasema.

"Aaagh... f(...) you," Lexi akamwambia Mensah.

"No... no I wouldn't. I swear. I can't go back there again, he'll kill me. I... please help me. I'll do anything for you sir. I'll be your slave if you want... I will. I won't betray you sir, please... (Hapana... sitafanya hivyo.. naapa.. siwezi pia kurudi huko, ataniua.. tafadhali nisaidie.. nitakuwa hata mtumwa wako ukitaka.. sitakusaliti bwana wangu, tafadhali..)" LaKeisha akawa anamwomba Kendrick kwa hisia.

"Betray? Bitch, you don't even know us! (kusaliti? hata hautujui, malaya wewe!)" akasema Mensah.

LaKeisha akamwangalia Lexi kwa njia ya kumwambia amwonee huruma. Lexi akamtazama tena Kendrick, naye LaKeisha akamwangalia pia.

"What's your boss' name? (boss wako anaitwa nani?)" Kendrick akamuuliza.

"Abbo-... Abbo-Pierre Kwame," LaKeisha akajibu.

Kendrick akatulia kidogo, kisha akauliza, "You'll do... ANYTHING? (utafanya.. CHOCHOTE?)"

"Yes sir... I'll do anything you want (ndiyo.. nitafanya chochote unachotaka)," LaKeisha akasema kwa uhakika.

"Take off your clothes (vua nguo zako)," Kendrick akamwambia.

"Uncle...." Lexi akasema kimshangao kiasi.

Oscar akaanza kuchekelea. Wanaume wote walikuwa wanamwangalia LaKeisha wakisubiri itikio lake, naye akaanza taratibu kuvua nguo. Alivua sweta na kubaki na T-shirt nyepesi, kisha nayo akaitoa pia na kubaki na sidiria nyekundu iliyoonyesha sehemu ya juu ya matiti yake. Kisha akaivua kaptura na kubaki na tight nyeusi iliyofikia chini ya mapaja yake, nayo pia akaitoa na kubakiza chupi nyeupe (tena kanda mbili). Oscar akamtania Victor kwa ishara kuwa alikuwa ameanza kudindisha, naye Victor akacheka kidogo. Lexi na Torres walisumbuliwa kiasi na jambo hilo, nao wakawa wanajiuliza nini maana ya Kendrick kumwambia afanye hayo. Kendrick alikuwa tu akimwangalia mwanamke huyu kwa umakini.

LaKeisha alipoanza kuishusha mikanda ya begani ya sidiria yake, Lexi akamwahi na kumzuia.

"Nafikiri hiyo inatosha," Lexi akamwambia Kendrick.

"Okay. Kama uko tayari kuvua nguo kwa ajili ya mwanaume wa kwanza anayekupatia msaada, basi wewe hauna faida yoyote kwangu," Kendrick akasema.

"What was that?" LaKeisha akauliza kwa kutoelewa.

"Its nothing, put your clothes on (siyo kitu.. vaa nguo zako)," Lexi akamwambia Lakeisha, naye akatii.

Lexi akamsogelea Kendrick na kusema, "Uncle, huyu msichana anahitaji msaada. I know, I know hujapenda mimi kumleta, lakini sikuona njia nyingine salama ya kumsaidia hasa kwa sababu ya mishe alizojiweka ndani yake...."

"Hilo siyo tatizo langu," Kendrick akamwambia.

"Basi niruhusu nilibebe mimi," Lexi akasema kwa uhakika.

"Unajua Lexi... huyu ni aina ya mwanamke ambaye akiona anakaribia kuanguka atakuangusha pamoja naye. Sitaki kukuona unaburuzwa namna hiyo," Kendrick akamwambia.

"Labda uko sahihi... labda hauko sahihi. Nipe nafasi nimsaidie. Hatuwezi kujua matokeo yatakuwa vipi sikuzote, lakini hiyo haimaanishi tuache kujaribu. Please uncle..." Lexi akamwomba.

Kendrick akashusha pumzi tu huku akimwangalia Lexi kwa umakini. Kisha akamtazama LaKeisha, ambaye alikuwa amemaliza kuvaa nguo zake zote.

"She's all yours (yeye ni wako sasa)," Kendrick akamwambia Lexi.

Kisha akanyanyuka na kuondoka hapo, akifuatwa na wengine isipokuwa Lexi na Torres. Torres akamwangalia tu Lexi kwa njia ya kuuliza kama ana uhakika na jambo alilochagua kufanya, naye Lexi akamwonyesha kwa ishara ya kichwa kuwa angefanikiwa tu. Kisha akatazamana na Lakeisha, ambaye alikuwa anamwangalia kwa matumaini mengi sana, naye akampa tabasamu dogo kama kumtia moyo.



★★★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★★★

WhatsApp +255 787 604 893
 
FOR YOU

Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Uhalifu, Mauaji, Visasi, Vita, Mambo yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA

★★★★★★★★★★★★★★★★★


Siku zilizofuata, Lexi angekaa pamoja na Lakeisha hapo kwenye nyumba na kumzoeza vitu vingi na kumfundisha mambo mengi, kutia ndani Kiswahili. Mwanamke huyu alikuwa mwepesi kujifunza mambo na hatua kwa hatua Lexi akaona jinsi alivyokuwa na bidii, na mcheshi pia.

LaKeisha alisimulia maisha yake na kusema yeye ndiye aliyekuwa mtoto pekee wa kike na wa mwisho kwenye familia yao yenye watoto sita. Walikuwa na maisha magumu, na kaka zake wote walijiingiza kwenye mambo haramu ili kuitegemeza familia yao tokea walipokuwa wadogo. Lakini baadae wote waliuawa kwa kuchomwa visu na watu waliokuwa wanawadai, hivyo hiyo ikamwacha yeye na mama yake tu, kwa kuwa na baba yake alikuwa amekufa mapema. LaKeisha alianza kufanya kazi za kucheza ngoma kwenye kundi fulani, baadae kama mhudumu wa mgahawa mdogo, mtumbuizaji wa dansi kwenye kumbi za starehe, na hizo zote zilimweka katika hali mbaya kihisia lakini hakuwa na jinsi. Alipenda masomo lakini kwa sababu ya kutopata pesa ya kutosha hakuweza kuendelea.

Baadae ndiyo alianza kuwafanyia kazi watu wakubwa ambao walitumiana bidhaa za madawa ya kulevya, yeye akiwa mhamishaji kama vijana wengine. Kipindi fulani mama yake aliumwa sana ugonjwa wa pumu na alihitaji matibabu yenye gharama, hivyo LaKeisha akamwomba boss wake kiasi kikubwa cha pesa kama mkopo ili amlipie mama yake matibabu. Boss wake alimpa, lakini pia akampa tarehe hususa ya kuzirudisha, naye LaKeisha akaenda na kumlipia mama yake matibabu. Akaanza kufanya kazi za pembeni tofauti na hiyo ili akusanye pesa kwa ajili ya kumlipa boss wake, lakini kwa tukio baya mama yake akawa amepoteza maisha. Hiyo ikamwacha akiwa peke yake tu. Muda ulifika wa kurudisha deni lakini hakuwa amekusanya pesa ya kutosha, na boss wake alimwambia kama asingerudisha basi angemuua. Kwa hiyo akajiingiza kwa boss mwingine wa masuala hayo hayo na kutafuta njia ya kuzirudisha pesa za yule wa mwanzoni, ndiyo mpaka kufikia kisa kile kilichomkuta kabla ya Lexi kumwokoa.

Hadithi ya maisha yake ilihuzunisha, lakini bado alikuwa mtu asiyekata tamaa na kuendelea kubaki imara. Wengine pia walimzoea haraka kwa sababu ya utundu wake na madoido aliyokuja nayo hapo, hadi mwisho wa siku Kendrick akaanza kumfurahia kwa sababu alionyesha kuwa mwaminifu kwake.

Ilipofika siku ambayo vijana wa Kendrick walitakiwa kwenda kuiba dhahabu kwa mara ya mwisho, LaKeisha aliomba kwenda pamoja nao. Wote walikataa, lakini akasisitiza kwa kusema alihitaji kuwasaidia ili na yeye apate chochote cha kuweza kuwalipa wanaume wale ambao mpaka kufikia muda huo wangekuwa wanamtafuta. Wengine wakamuuliza Lexi anaonaje kuhusu hilo, na baada ya kutafakari, Lexi akakubali na kumpanga sehemu mpya muhimu kwenye kazi hiyo. Walikuja kuondoka na dhahabu kilo 300 siku hiyo ilipofika, na msaada wa LaKeisha ulikuwa mzuri sana. Kendrick alianza kumfurahia hata zaidi, naye akasema sasa angekuwa mmoja wa kundi lao rasmi.

Baada ya hapo, Lexi pamoja na Mensah walikuja kumsindikiza LaKeisha alipokwenda kuwalipa wanaume wale pesa zao. Tena kwa kiburi kakawarushia usoni kwa sababu kaliwalipa mara mbili zaidi ya kile walichokadai. Alikuwa mwenye kujiamini sana wakati huu kwa sababu ya kuwa miongoni mwa kundi lenye ubora zaidi, na lililomtendea kama familia.


★★★★


Baada ya mambo yote hayo, sasa ulikuwa umefika wakati wa Kendrick na Lexi kuanza kupiga hatua za mipango yao kuelekea nchi waliyotoka. Kwa muda mrefu walikuwa wameshafatilia mambo mengi sana yaliyoendelea huko, kwa hiyo wakati huu wangeanza kujipanga ili kutimiza lengo lao. Victor, Mensah, na Oscar wangekwenda Tanzania kwanza. Mpango ulikuwa ni kwenda kujenga nyumba kubwa huko, ambayo ndiyo ingekuwa sehemu ya kufikia wengine. Walikwenda na pesa kama zote, kwa hiyo wangeajiri wajenzi wenye uzoefu ili kuanza kazi ya ujenzi wa nyumba hiyo kwa mpangilio aliowapatia Torres.

Sehemu waliyopaswa kujengea nyumba hiyo ilikuwa ni ile ambayo Kendrick na Casmir walitengeneza handaki chini ya ardhi. Kendrick alikuwa ameshakinunua kiwanja chote kuzunguka eneo hilo miaka miwili iliyopita kutokea huku huku Ghana, na hakuna yeyote nchini kule aliyejua ni yeye kwa sababu alitumia utambulisho tofauti aliokuwa akiutumia wakati huu. Kwa hiyo wakina Victor walitakiwa kusimamia ujenzi huo, lakini uliotakiwa kufanywa kwa umakini sana. Zilitakiwa kujengwa kwanza kuta za kuzunguka eneo hilo, halafu ndiyo ujenzi wa ndani ungeanza. Victor na wenzake wangetakiwa kuwa macho ili wajenzi wasitambue sehemu ile ya mwingilio wa kule chini. Yaani, wangepaswa kujenga tu nyumba na kuipangilia, lakini kufikia sehemu hiyo hawakupaswa kupagusa.

Lakini, mmoja kati ya wajenzi ambaye alikuwa makini sana aliitambua sehemu hiyo. Huyu alikuwa ni Kevin Dass. Kwa utambuzi wa haraka, alihisi ni kama watu hawa walikuwa wakifanya hivyo makusudi, naye akaona afatilie kimya kimya ili kujua nia yao ilikuwa ni nini. Alikuja kugundua kwamba wakati ambao mafundi wangeondoka, Victor, Mensah, na Oscar wangeingia kule chini ili kupatengeneza pawe pa kisasa zaidi. Alikuja kuwafuata siku moja chini huko, nao wakamkamata na kumfunga.

Kevin aliwaeleza alichofikiria, akisema inaonekana walikuwa wakificha jambo fulani muhimu, na yeye hangewasema kwa yeyote, lakini angewasaidia ili wasitambulike. Akawaambia kuendelea kuwaficha mafundi na wasimamizi wengine kuhusu jambo hili isingekuwa kazi rahisi, kama ilivyokuwa kwake tu mpaka akajua, lakini kama wangemwingiza kwenye mipango yao basi angewasaidia kuficha siri yao na hata kuwasaidia kupajenga chini huko vizuri zaidi. Alipenda pesa, na ikawa wazi kwa wengine kwamba hilo ndiyo lilikuwa lengo lake; afanye nao kazi hii ya siri ili apate pesa zaidi.

Ikabidi Victor aongee na Kendrick, ambaye bado alikuwa nje ya nchi. Alimwambia kuhusu hali halisi, naye akauliza wafanye nini. Baada ya kutafakari mambo kwa kina, Kendrick akaomba kuongea na Kevin. Alimwambia kuhusu kile kilichokuwa kikiendelea na kumuuliza kama angeweza kuwa pamoja nao mpaka mwisho, na kijana huyo akakubali. Kwa hiyo Kendrick akawaamuru wengine wafanye kazi pamoja naye, ingawa uamuzi huu haukumfurahisha kabisa Mensah. Hata akaongea na Kendrick kumwambia huu haukuwa uamuzi mzuri, lakini Kendrick akamwambia asiwaze sana, na awe anamchunga mtu huyo ili kuona kama ataleta nuksi. Kama angeleta nuksi, basi Mensah angekuwa na kibali cha kumshughulikia.

Vijana hawa ambao walikuwa Tanzania waliongozwa na Victor, naye alikuwa akimwelekeza Kevin kuhusu mipango yao. Mara kwa mara wote wangemjaribu Kevin ili kuona ikiwa alikuwa mwaminifu na msiri au ni kigeugeu, lakini akawathibitishia kuwa alikuwa mwaminifu. Lexi, Torres, na Lakeisha walikuja kuambiwa kwamba kuna mtu mwingine ameongezwa kwenye kundi lao, ambaye angesaidia ujenzi wa nyumba yao kule Tanzania, nao wakaridhia pia.


★★★★


Ni Lexi, Torres na Lakeisha ndiyo pekee waliobaki na Kendrick huko Ghana. Lakini kwa muda ambao wenzao walikuwa wamekwenda Tanzania, wenyewe walikuwa wakifanya kazi ya kununua au kutengeneza vitu vingi kwa ajili ya kutumia wakati ambao wangefika nchini kule. Walikwenda sehemu kama Jamaica alikokuwa akiishi Torres, Manhattan kule Marekani, Prague huko Ufaransa, na Johannesburg Afrika Kusini. LaKeisha alifurahia zaidi safari hizi kwa sababu hakuwahi kutoka nje ya nchi aliyokulia toka azaliwe, na kuzifanya ziwe kama nafasi ya kutalii, na hata kutoka na wazungu kwenye "date."

Walipokuja kurudi Ghana, walianza kupangilia mambo na vitu kwa ajili ya kutuma kule Tanzania. Torres alitangulia huko na yeye miezi michache baadae akijiweka kama mfanyabiashara wa kawaida tu, huku vitu vingi ambavyo angeviingiza vingepitia bandarini. Walikuwa na njia nyingi sana za kuingiza mambo yao bila kutambulika, na wakati huo mambo ya ujenzi kwenye sehemu ile yalikuwa yakielekea kukamilika. Alipata nafasi ya kukutana ana kwa ana na Kevin Dass, nao wakaanza kutumia wakati pamoja ili kumzoeza vizuri hata zaidi njia zao za kufanya mambo.

Hiyo ikawaacha Kendrick, Lexi na Lakeisha huko Ghana. Kufikia kipindi hiki, Kendrick na Margaret bado waliendelea kuonana lakini hakukuwa na "mahaba" yaliyofanyika baina yao. Margaret alikuwa amejifungua mtoto wa kiume pamoja na mume wake miaka miwili nyuma, hivyo hawakutumia muda mwingi pamoja ingawa bado walijiona kuwa wapenzi. Ingawa Kendrick alihisi ni kama walikuwa wanalazimisha mambo, kuendelea kwake kuwa mtu wa pembeni wa Margaret ilitokana hasa na shukrani yake kubwa kumwelekea mwanamke huyo kwa sababu ya kuokoa maisha yake mpaka hapo alipofikia. Margaret mpaka kufikia muda huo hakujua lolote kuhusu mishe za kisiri alizofanya Kendrick na vijana wake, naye Kendrick aliona mambo yalitakiwa kubaki namna hiyo.

★★

Wakati fulani, Lexi pamoja na Lakeisha walikuwa wakifanya matembezi kwenye mitaa ya Kumasi mjini, naye LaKeisha akamwambia Lexi kwamba mapolisi waliwakamata wale wote waliofanya kazi na boss wake siku iliyopita kwa kuuza madawa. Akasema alikuwa anafurahi sana kwamba hakuwa huko tena, kwa sababu aliwahi kuwekwa jela na hakutaka kurudi huko, hivyo kama angekuwa nao kufikia kipindi hiki basi na yeye angepelekwa nao. Akiwa na furaha nyingi, akaona sehemu fulani waliyokuwa wakitengeneza nyama za kuchomwa na vyakula mbalimbali, naye akamwambia Lexi angekwenda kufata nyama ili warudi nazo nyumbani kukamua.

Lexi akamwambia aende tu naye angemsubiri, naye LaKeisha akaondoka kuelekea huko. Akiwa amesimama pembezoni mwa barabara, aliona watoto fulani ambao walikuwa wamezunguka mtaro pembeni ya barabara hiyo upande wake wa kushoto, wakiwa wanaponda kitu fulani kwa mawe madogo madogo ndani ya mtaro huo. Kwa kukisia, akadhani walichokuwa wakiponda ni nyoka labda, naye akaona asogee hapo ili aangalie alikuwa ni nyoka wa aina gani, huku akimsubiria LaKeisha.

Alipofika hapo, akakuta haikuwa ni nyoka waliyekuwa wakimponda, bali mnyama mdogo mwenye kufanana na paka. Alikuwa kama mtoto wa paka, naye alikuwa akijaribu kukimbia lakini mawe aliyopondwa yalimfanya asiweze kufanya hivyo kutokana na kuumia mguu mmoja zaidi. Lexi angeweza kuona majeraha yake yenye kutoka damu, naye akamwonea huruma sana. Akawaambia watoto hao waache kumponda, kisha akawafukuza hapo ingawa walikuwa wabishi.

Lexi akaingia mtaroni hapo na kuchuchumaa na kumwangalia, na mnyama huyu mdogo bado alikuwa akijaribu kujivuta lakini kwa maumivu. Ngozi yake ilikuwa ya rangi inayokaribiana kabisa na nyeupe, kama kijivu, na ilikuwa na madoadoa madogo madogo kuzungukia mwili wake wote. Kulikuwa na mistari ya mbali kutokea chini ya macho yake mpaka sehemu ya midomo, naye Lexi akatambua huyu hakuwa paka.

LaKeisha akafika hapo pia akiwa na mishkaki minene ya nyama ya mbuzi ndani ya mfuko, naye akauliza kwa nini Lexi alikuwa ameingia kwenye mtaro mchafu. Lexi akamwonyesha kitoto hicho, naye LaKeisha akamwambia aachane nacho tu ili waondoke wakapate chakula kule kwao. Lexi alikitazama tena, na kwa sababu asiyoijua akaanza kumfikiria Sandra. Alikumbukia jinsi mara ya mwisho kumwona alivyokuwa akiomba Weisiko asimuumize, naye kwa kumwangalia mnyama huyu, akadondosha chozi. LaKeisha mpaka akamshangaa na kumuuliza alikuwa na tatizo gani, lakini Lexi hakujibu lolote na kumbeba tu mnyama huyo, kisha akamwambia Lakeisha waondoke. LaKeisha akashangaa sana kiasi kwamba hadi akaanza kumcheka. Akamwambia wakati mwingine alikuwa anamchanganya sana ila ndiyo hivyo, alikuwa ameshamzoea.

Baada ya kumpeleka kule walikoishi, Lexi alianza kumpa huduma muhimu mnyama huyo mdogo. Alimtunza vizuri na kumpa mahitaji yake kama tu alivyofanya kwa mifugo yake ya sungura. Siku zilipozidi kusonga, afya yake ikawa nzuri zaidi. LaKeisha alikuwa anapendezwa sana na jinsi Lexi alivyowajibikia hata vitu ambavyo yeye hakuona ni muhimu kivile. Lakini pia, alianza kuona utofauti kwenye utu wake na yule aliyeonekana kwa nje. Lexi alikuwa mwanamke kwa nje ndiyo, lakini kila kitu alichofanya kilikuwa kwa mtindo wa mwanaume, na hili liliitia udadisi akili ya LaKeisha kumwelekea.

Usiku mmoja wakiwa chumbani kwa Lexi huku akicheza na mnyama wake mpya, LaKeisha alikuwa anamwangalia tu Lexi kwa umakini. Alikuwa aina ya mwanamke ambaye akitaka kujua kitu fulani, angekijua tu haijalishi nini kingehitajika. Lexi akatambua alikuwa anatazamwa sana, naye akamuuliza ana shida gani.

"Nothing," LaKeisha akasema.

"Kwa Kiswahili," Lexi akamwambia.

"Ahahah... aam... hamuna kitu," LaKeisha akasema kiutani.

"Acha masihara, najua unaweza kuongea Kiswahili vizuri sa'hivi, ila unajifanya tu," Lexi akamwambia.

"Siyo vizuri sana lakini. Ila ninajitahidi kwa sababu nina mwalimu mzuri," LaKeisha akasema.

Lexi akawa akirusha mpira mdogo upande mwingine wa chumba, na mnyama wake akawa anaukimbilia na kumletea kwa mdomo.

"Ahahahah... good girl!" Lexi akamsifia huku akichezea manyoya yake laini.

"You know, you haven't named her yet (unajua, bado haujampa jina huyu)," LaKeisha akamwambia.

"Yeah. I'm struggling to find her a good name. Something rare (ndiyo.. ninasumbuka sana kutafuta jina zuri.. jina adimu)," Lexi akasema.

"Don't... usimpe jina gumu itakuwa hard for her to get used to. And... mpe mapema ili alizoee haraka," LaKeisha akamshauri.

"Unanipa ushauri now wakati wewe ndiyo uliniambia nimwache mtaroni!" Lexi akamwambia.

LaKeisha akacheka kidogo na kuendelea kumwangalia kwa hisia. Lexi sasa akawa kama amechoshwa na jinsi LaKeisha alivyokuwa anamtazama.

"What's wrong with you? (una matatizo gani?)" Lexi akamuuliza huku anatabasamu.

LaKeisha akatabasamu, kisha akasema, "Nothing's wrong with me. I'm just weird... you know that (hakuna tatizo kwangu.. nakuwaga wa ajabu tu.. unajua hilo)."

"Yeah, no shit," Lexi akasema.

LaKeisha akatabasamu tena.

"If you want to say something, just tell me. We tell each other everything right? (kama kuna kitu unataka kusema, niambie tu.. huwa tunaambiana kila kitu, si ndiyo?)" Lexi akamwambia.

LaKeisha akavuta pumzi ya juu, kisha akaishusha na kusema, "Ina son ku."

Lexi alimtazama kiumakini. Alielewa maneno hayo ya kikabila cha Hausa yalimaanisha "I like you," njia fulani ya kumwambia mtu unapendezwa naye lakini kwa njia ya kimapenzi.

"Are you drunk? (umelewa?)" Lexi akamuuliza.

"No, I'm just serious... (hapana.. niko makini/mkweli tu)" LaKeisha akasema.

Lexi akamtazama mnyama wake tu.

"You... you're different. Its like... I don't know. Like there's something you're hiding about yourself that just... makes me like you. You never even have sex. Who does that? (wewe.. uko tofauti.. ni kama.. sijui tu.. ni kama kuna kitu kuhusu wewe unakificha ambacho.. kinafanya navutiwa nawe.. huwa hata haufanyi mapenzi.. nani huwa yuko hivyo?)" LaKeisha akasema.

Lexi akacheka kidogo. Akamtazama machoni tena na kuona kweli LaKeisha alikuwa anamaanisha alichosema, hivyo akamwambia asubiri akamwekee kwanza mnyama wake chakula ili waje kuzungumza.

Alirudi na kuanza kumweleza ukweli wote wa maisha yake. Kwa vijana wote wa kundi hili la Kendrick, walijua sababu ya wawili hawa ya kutaka kulipiza kisasi kule Tanzania ilikuwa ni ishu ile ya Demba Group miaka kadhaa nyuma iliyowaharibia maisha yao. Lakini kuhusu Xander kubadilishana miili na pacha wake, hawakujua. Sasa LaKeisha ndiyo akawa mtu mwingine tofauti na Kendrick aliyejua kuhusu hili. Ilikuwa ngumu kwake kuamini mwanzoni, lakini hakukuwa na sababu ya kukataa jambo hilo. Lexi alimwelezea vitu kwa hisia mpaka machozi yakawa yakimlenga.

LaKeisha, akiwa amepatwa na ukaribu wa kihisia zaidi kwa Lexi, akamkaribia na kumshika usoni, kisha akambusu mdomoni kwa upendo. Lexi hakuwa na itikio lolote lile zaidi ya kumwacha tu, naye LaKeisha akaendelea kulazimisha busu hiyo mpaka ikaanza kuwa denda kati yao. Pole kwa pole LaKeisha alianza kujiweka karibu zaidi ya Lexi, na wawili hawa wakaanza kupeana mahaba.

Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Lexi kufanya mapenzi na mtu tokea alipoingia kwenye mwili huu wa pacha wake. Lakini Lexi hakutaka bado kufanya mapenzi kwa njia ya wawili, yaani, yeye alimwonyesha tu LaKeisha mahaba kama jinsi ambavyo angemfanyia mwanamke wakati alipokuwa ndani ya mwili wake wa kiume, lakini hakuruhusu LaKeisha amfanyie hivyo kwa sababu kihalisi hakutaka kujua mwanamke huhisije. Kwa hiyo ilikuwa kama kumridhisha tu LaKeisha, na ilikuwa ajabu kwake kidogo kuona kwamba aliweza kumfikisha LaKeisha mahala pazuri ingawa hakukuwa na mashine iliyotumika!

Basi, baada ya mahaba yao ya KUS na KUS kama sumaku, Lakeisha alimwambia Lexi jinsi alivyofurahia burudisho hili jipya kwake. Lakini Lexi akamweka wazi kwamba hakuwa na muda wa kuwa na mahusiano, kwa sababu hali yake ya kimwili bado ilikuwa tata. LaKeisha akaonyesha kumwelewa kwa kusema jambo hilo halikuwa na tatizo, ila kama angehitaji show nyingine basi asimnyime. Kwa hiyo wangeendelea kuwa aina ya marafiki wa faida.

LaKeisha akaanza kumchora Lexi tattoo nyingi mwilini mwake kuanzia hapo na kuendelea, akiupamba mwili wa "kipenzi" chake kipya kwa umaridadi wa hali ya juu.

★★

Mwaka mmoja baada ya hayo, Kendrick alikutana na Margaret na kumwambia kwamba ulikuwa umefika wakati sasa wa yeye kurudi nchini kwao. Margaret aliuliza ikiwa hilo lingekuwa jambo la busara, naye Kendrick akatania kwa kusema kwa kuwa sasa alikuwa na miaka 56, hakuna mtu yeyote angeweza kumtambua huko kutokana na kuzeeka. Margaret alimkumbatia kwa hisia sana siku hiyo, naye akamwambia ijapokuwa safari yao ilikuwa na vikomo, bado Kendrick angeendelea kuwa moyoni mwake.

Baada ya Lexi pia kuonana na Margaret na kusema kwa heri zao, sasa Kendrick, LaKeisha na Lexi wakaelekea Tanzania hatimaye. Walikuta nyumba yao ile iliyojengwa kwa umaridadi wa hali ya juu ikiwa imekamilika, nao walipokelewa vyema na wenzao huko ambao walikuwa wamekwishaizoea nchi hiyo. Handaki lile chini ya ardhi lilikuwa sehemu za katikati ndani ya nyumba hii, na vijana wale walikuwa wameipanua na kuifanya iwe kubwa na yenye ubora huko huko chini, hasa kwa msaada wa Torres. Walikuwa wametia jitihada kubwa sana kuunda kila kitu kiwe jinsi walivyotazamia, na sasa kazi iliyokuwa mbele yao wangeanza kuipangilia vizuri hata zaidi baada ya boss wao na Lexi kufika.

Yote hayo ndiyo yaliyokuwa yamepelekea wizi wa kiasi cha shilingi trillioni 20 kutoka majengo ya benki kuu, na bado kundi hili lingeendelea kuisumbua kiaina serikali hii iliyokuwa chini ya utawala mbovu wa Raisi Paul Mdeme.......


★★★★


WAKATI ULIOPO....


Ikiwa ni siku iliyofuata baada ya Kendrick Jabari kuongea na Lexi kwenye simu usiku, Raisi Paul Mdeme alikuwa akisubiri kwa hamu mzigo wake wa dhahabu ufike. Alikuwa ametumia njia fulani ya siri kuuingiza nchini, akiwa amefanya makubaliano na watu fulani kutokea nchini Afrika Kusini ili wafanye kama "kumkopesha" madini hayo, naye angewapatia vitu fulani vya thamani kutoka nchini kwa njia haramu. Yangepitishwa DRC Congo, kisha kwa njia ya kificho yangeingizwa nchini.

Njia yenyewe ya kificho ilikuwa ni treni. Yaani tena treni zile zinazobeba kokoto nyingi tu kwenye mabehewa yaliyowazi, kutokea Kigoma mpaka Dar es Salaam. Dhahabu hizo zilifichwa chini ya behewa moja la katikati ambalo lilijazwa kokoto mpaka juu kama mabehewa mengine tu, hivyo haingekuwa rahisi kwa yeyote kutambua kuna vito vya thamani hapo. Pia, treni hii ililindwa na watu wachache wa Raisi waliojua kuhusu ishu hii, nao wangekaa mbele kule kama waongozaji wa kawaida tu mpaka wakati ambao treni ingefika ilipotakiwa na kushusha mzigo huo.

Kwa upande wa timu ya Luteni Michael, walijigawanya mara mbili siku hii ili kwenda kwenye kampuni zile binafsi zilizohusiana na masuala ya madini kutoka makampuni ya nje ya nchi. Ikiwa unakumbuka vyema, hii ilikuwa ni sehemu ya utafiti mpya uliopendekezwa na ACP Nora baada ya kufanya uchunguzi kuhusiana na nguo zile walizovaa Mess Makers ambazo zilikuwa na uwezo wa kuzuia risasi. Walitaka kwenda kuona kama kampuni hizi zingekuwa na uhusiano fulani wa kisiri pamoja na watu hawa ili waweze kuwakamata haraka.

Luteni Michael alikwenda kwenye kampuni iliyokuwa mkoani Geita, akiwa pamoja na Mario, Hussein, na Omari, naye ACP Nora akaenda kwenye ile iliyokuwa upande mwingine wa jiji la Dar es Salaam akisindikizwa na Vedastus, Mishashi, pamoja na Alex. Walimwacha Bobby kwenye jengo lao lile la uchunguzi, nao wangekuwa wakiwasiliana pamoja naye.

Upande wa treni yenye dhahabu za Raisi Paul Mdeme, ilikuwa ikitembea kwa kasi sana. Yaani siku hii hakuna treni nyingine yoyote ya abiria na mizigo iliyotakiwa kufanya safari, ni hii tu ndiyo iliyopaswa kutembea. Wasafiri kutokea Kigoma waliotaka kuchukua treni kwa reli hii ya kati kwa leo wangepaswa kusubiri mpaka kesho, au wachukue usafiri mbadala lakini siyo treni. Wengi hawakuelewa sababu, na kuchukulia ni jambo la kawaida tu; huenda kulikuwa na rekebisho likifanywa, waliwaza.

Kufikia mida ya jioni, tayari ilikuwa imeshavuka mikoa kadhaa na sasa ikawa maeneo fulani ya Morogoro yenye milima iliyo pembezoni mwa reli hiyo. Raisi Paul Mdeme aliwasiliana na watu wake walioiongoza ambao walimjulisha kwamba mzigo haukuwa mbali kufika, naye Raisi akaridhika sana.

Lakini, kutoka juu ya mlima fulani usio mrefu sana (lakini ni mrefu), kulikuwa na watu wachache wakiwa wamesimama hapo. Hawakuwa wengine ila Mess Makers. Hatari! Wahuni tayari walikuwa wameshanusa dhahabu zilipo, nao wakawa hapo wakiisubiri treni ipite usawa huo ili waanze kujichukulia madini yao. Acha kabisa! Mdeme alikuwa anawashusha thamani sana hawa jamaa, ila sasa ndiyo wangemwonyesha jina lao linamaanisha nini.

Walikuwepo watano hapo kutoka kwenye kundi lao; Lexi, Victor, Mensah, LaKeisha na Oscar. Walikuwa wamesimama huku wanaiangalia kwa umakini treni ikitembea, naye Oscar alikuwa tu ameachia tabasamu lake la masihara. Ilipoanza kukaribia usawa wao, wote wakachuchumaa, kisha wakazivaa "mask" zao usoni. Lexi akanyanyua kiganja chake juu na kuweka vidole vitatu hewani. Treni ilipoanza kuwapita, akaanza kushusha kidole kimoja-kimoja kwa kuhesabu 3, 2, 1, kisha akakunja ngumi, nao wote wakaruka kuelekea chini. Nyuma ya nguo zao maalumu kwa ajili ya mapambano walizovaa, walijifunga kamba ndefu na ngumu sana zilizoshikizwa vyema juu ya mlima huo, nao wakawa wanateremka kwa kudunda na kudunda kuelekea chini.

Kamba hizo zenye ubora ndiyo vitu waliyokuwa wamevifata kule Mwanza mpaka Kevin akakamatwa ile juzi. Walizichukulia sehemu tofauti-tofauti kwa ajili ya mishe hii, na hapa alitakiwa kuwepo Kevin pia lakini kwa sababu sasa alijulikana ilibidi wamwache kule "chini" kwenye sehemu yao ya kujificha. Hii ndiyo iliyokuwa mission ambayo Lexi na Kendrick waliizungumzia. Torres katika ufatiliaji wake wa mambo alipata kujua dili la Mdeme na watu kutoka Afrika Kusini, hivyo akafanya mipango na Lexi ili wawazingue tena kwa mara nyingine. Yaani walikuwa wanataka kuwafundisha viongozi wale waovu somo fulani muhimu kupitia haya yote waliyokuwa wanafanya, na huu ulikuwa ni mwanzo tu.

Watano hawa wakafanikiwa kufikia mabehewa na kuzifungua kamba zile, huku treni ikiendelea kusonga tu bila ya wale walioiongoza kutambua kwamba kitumbua chao kiliingia mchanga! Watano hawa wakakaribiana na kusimama juu ya behewa moja, kisha Lexi akatumia kifaa chake maalumu kumuuliza Torres dhahabu zingekuwa kwenye behewa la ngapi. Torres akamwambia lilikuwa behewa la 6 kutoka mwisho, na watano hao wakalielekea upesi. Walitaka kuwahi kwa sababu treni ilikuwa ikitembea haraka na haingechukua muda mrefu kutoka kwenye maeneo hayo yenye milima kufikia maeneo yenye watu.

Walipolifikia behewa hilo, Victor, Oscar, pamoja na Mensah wakasaidiana kuifungua sehemu ambayo ilikuwa imeliunganisha na mabehewa ya mbele. Kwa kuwa ilikuwa ngumu, LaKeisha akawapatia kifaa fulani cha kukata chuma, nacho kikasaidia kuondoa ugumu na hatimaye behewa likaachia. Oscar alikuwa kidogo aangukie kwenye reli lakini wenzake wakamwahi na kumshikilia, naye akawa anacheka huku wakiyaangalia mabehewa ya mbele yanawaacha nyuma. Mensah na Victor wakamvuta Oscar kwa nguvu na kulala juu ya kokoto za behewa hilo huku wakicheka, naye Lexi pamoja na Lakeisha wakawa wanacheka pia.

Mabehewa sita yaliyobaki sasa yakawa yakipunguza mwendo kwenye reli mpaka yakasimama hatimaye kwenye eneo lililo na uoto mwingi wa asili na miti mingi ya pori. Lexi akawaambia sasa hapo kazi ndiyo ingeanza. Wakashuka na kuanza kulifungua behewa hilo sehemu ya mbele kwa kutumia vifaa vile vya kukata chuma, na baada ya dakika nyingi likaachia. Hiyo ingefanya kokoto zote zimwagike, hivyo wakawa makini kukwepa ili zisiwaponde. Baada ya zote kumwagika, wakaanza kuzichambua sasa, nao wakaweza kuyaona mabamba madogo-madogo ya dhahabu zenyewe. Wakawa wakizitoa na kuzirusha pembeni ili kuzitenganisha na kokoto.

Oscar alikuwa anachekelea tu, huku akisifia sana jinsi kundi lao lilivyo la aina yake. Angalau walifurahishana kwa mazungumzo huku wakiendelea na kazi. Wakafanikiwa kuhamisha dhahabu nyingi mpaka giza kuanza kuingia kwa mbali.

Lexi akaangalia muda na kumuuliza Torres kupitia kifaa chake, "Yuko wapi?"

"Anakuja. Amekaribia kufika," Torres akajibu kupitia kifaa kile.

Wakaendelea tu kuzihamisha na kuzipanga, na ndipo wakasikia gari likija eneo la hapo. Lilikuwa ni lori dogo aina ya Canter, naye Oscar akaanza kushangilia kwa shauku. Wote walijua ni nani aliyekuwa amefika hapo, naye hakuwa mwingine ila Kendrick Jabari. Ilitakiwa kuwa Kevin au yeyote ambaye wangemweka pembeni ili wakishazitoa dhahabu ndiyo aje na gari hilo, lakini kwa hali iliyomkuta Kevin, ilimbidi tu Kendrick ndiyo aje.

Gari likaegeshwa usawa wa dhahabu zile, naye Kendrick akashuka na kupokelewa vyema na vijana wake. Akawapongeza na kuwaambia kiutani kwamba sasa walikuwa wameongeza utajiri mwingi hata zaidi. Kisha vijana wote wakaanza kusaidizana ili kuziingiza dhahabu ndani ya lori. Wanaume walitoa chuma bapa ya shaba kutoka kwenye lori hilo na kuiweka chini, kisha wakawa wanaziweka dhahabu hapo na kuzipandisha sehemu ya wazi nyuma ya lori, ambako Lexi na Lakeisha wangezipokea na kuzihifadhi kwenye vitu kama mabeseni yaliyopangiliwa vyema.

Baada ya kazi hiyo yenye ugumu kiasi, walifanikiwa kuziweka dhahabu zote ndani ya lori. Ilikuwa imeshafika usiku sasa, na safari ya kuondoka ikaanza. Kendrick alirudi kukaa mbele pamoja na Victor ambaye aliendesha zamu hii, huku Lexi, Mensah, LaKeisha na Oscar wakikaa nyuma ya lori sehemu yenye dhahabu hizo wakifurahia story.

Mess Makers wakawa wamechafua hali ya hewa kwa mara nyingine tena.



★★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★★

WhatsApp +255 787 604 893
 
FOR YOU

Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Uhalifu, Mauaji, Visasi, Vita, Mambo yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI

★★★★★★★★★★★★★★★★★


Luteni Michael na wenzake walirejea jijini Dar es Salaam mida ya usiku kwa kutumia helicopter, kama tu walivyokwenda kwa usafiri huo kule Geita. Waliwakuta wengine tayari wakiwa jengoni, nao wakawafahamisha kwamba baada ya kufanya upekuzi huko hawakupata jambo lenye kutia mashaka, kwa sababu nguo zile zilitumiwa tu na walinzi wa kampuni ile. Vilevile, ACP Nora na wengine walimfahamisha Luteni kuwa hata wao walikuta hali iko hivyo hivyo, kwa hiyo kwa suala hilo ilionekana kuwa kikomo kimefika.

Wakati wakiwa wanaendelea kujadiliana kuhusu njia mpya ya kutumia ili kuwapata Mess Makers, Luteni Michael akapigiwa simu na Kanali Oswald Deule. Akapokea na kuzungumza naye, na ingawa wote hapo walisikia upande wa Luteni Michael wa mazungumzo, walielewa kuwa Kanali Oswald alikuwa akimwambia Luteni afanye upesi sana kuwakamata watu wale kwa sababu kuna mambo mengi yalikuwa yameharibika. Baada ya kukata simu, Luteni Michael akaona jinsi wengine walivyokuwa wanamtazama kama wanasubiri awaambie jambo fulani.

"Nini?" Luteni Michael akauliza.

"Sauti iliyokuwa inatoka ndani ya hiyo simu ni kali sana mpaka nimejiuliza imekuwaje sikio lako halijaziba," akasema Mishashi.

"Alikuwa anafoka nini huyo?" Vedastus akamuuliza.

"Kwamba tunachelewa kuwakamata jamaa. Anasema Raisi amekasirika sana na anataka tuwakamate haraka isivyo kawaida," akasema Luteni Michael.

"Ni nini kimemkasirisha?" ACP Nora akauliza.

"Nafikiri ni kitu inahusiana na treni ya leo," akasema Bobby.

"Treni gani?" akauliza Luteni Michael na wengine pia.

"Hamjasikia kumbe? Kuna treni ilikuwa inatoka Kigoma, imefika wapi sijui Igandu, sijui Morogoro, ikakatwa mabehewa sita ya nyuma. Ilikuwa na kokoto nafikiri za masuala ya ujenzi labda... or not," akasema Bobby.

"Imekatwa mabehewa... yaani ni ajali au?" akauliza Hussein.

"No. Imekatwa makusudi mabehewa huku bado inatembea. Waliokuwa wanaiendesha wamekuja kuona hilo tayari ishafika Ruvu. Wamekuta behewa moja limepasuliwa, sijui hata jinsi gani, na kokoto zimemwagwa chini. Halafu unajua nini?" Bobby akasema.

"Nini?" akauliza Luteni Michael.

"Kwenye hilo behewa ilibandikwa ile chata ya simba mweupe," akasema Bobby.

"Eh! Mess Makers?" akauliza Mario kimshangao.

"Ndiyo maana yake," akasema Bobby.

Wote wakaanza kuangaliana kimaswali.

"Kwa hiyo Mess Makers walikuwa wemeenda kuiba kokoto?" akauliza Omari.

"Hapana. Kulikuwa na kitu fulani ndani ya hilo behewa," akasema Nora akiwa makini.

"Kuna treni zingine zozote leo zimepita reli hiyo, hata kwenda njia za mkato?" akauliza Alex.

"Hapana. Tena, nimefatilia nikajua ni kwa agizo la Raisi hiyo treni ilipaswa kupeleka hizo kokoto Dar bila bughudhi. Leo hakuna mtu amesafiri kwa treni. Lakini... ilikuwa kitu fulani low sana... kama vile..."

"Kulikuwa na jambo limefichwa," akamalizia Alex.

"Ndiyo maana Mdeme amekasirika eeh? Kumbe kulikuwa na midoli yake humo," akasema Hussein.

"Angekuwa ameficha nini sasa?" akauliza Mishashi.

"Kiukweli, hiyo haituhusu. Kinachotuhusu ni kwamba hao jamaa leo wametoka hadharani lakini hatujawa na muda wa kutambua hilo na tumewakosa tena. Yaani... hawatabiriki. Tukisema twende huku, wenyewe tayari wako kule. Tunawapataje?" akasema Luteni Michael kwa mkazo.

Nora akaanza kusema, "Lakini Luteni... naanza kuona kama vile hawa watu hawaibi tu ili kujinufaisha. Wanaitarget serikali... kama vile wanaichallenge... na ninadhani hiyo inamaanisha kuna kitu personal kati yao na Raisi. Labda..."

"No, ACP. Nilikwambia sisi hatupaswi ku-delve kwenye mambo yao ya siasa... sisi tunatakiwa tu kufanya kazi tuliyopewa," akasema Luteni Michael.

"Luteni, nafikiri ACP anachojaribu kukwambia ni kwamba huenda kuna njia ya kufanikiwa kuwapata hao jamaa kama tutajua ni nini kinachoendelea baina yao na Raisi. Hivi vitu vilivyofichika ndiyo vinaweza kuwa ufunguo," akasema Vedastus.

"Ndiyo naelewa. Lakini hiyo haiko ndani ya description yetu. Hatutajiingiza huko," akasema Luteni Michael.

Wenzake wakawa wanaangaliana kwa kukerwa, hata Mario akazungusha macho yake.

Nora akashusha pumzi, kisha akasema, "Okay. Kuna jambo nitakwenda kufatilia kesho hospitali kuu. Labda litasaidia kwenye hii mission."

"Hospitali? Kwa nini?" akauliza Mario.

"Wacha afanye utafiti wake kwanza, ndiyo atakwambia. ACP, unastahili kupumzika. Nenda kapige juice na usingizi ili kesho ukiwashe," Alex akasema.

Nora akatabasamu, kisha akakubali na kuwaaga huku akiondoka. Luteni Michael akamwambia kama angependa basi amsindikize, lakini ACP Nora akasema haikuwa na shida kwa kuwa alikuwa na gari, kiutani tu, kisha akaondoka hapo. Luteni Michael alipowageukia wenzake, akakuta wanamcheka kichinichini.

"Mnacheka nini?" akawauliza.

"Unajua nini Luteni, ukitaka kumfanya mwanamke aone kwamba unavutiwa naye, jitahidi kuondoa hiyo superiority... yaani... onyesha wakati mwingine kwamba nawe una udhaifu ili ukianguka tu, akuokote, halafu umng'ang'anie forever," Bobby akamwambia, nao wengine wakacheka.

"Aliyekwambia nani ananivutia nani?" Luteni Michael akamuuliza.

"Siyo siri ACP ni mkali. We mwenyewe unamtamani basi tu unajishaua," Mishashi akamwambia.

"Ukija kusema hivyo tena, nakutoa meno yote," Luteni Michael akamwambia.

Mishahi akacheka.

"Hivi huwa anatoka na nani? Najua hajaolewa," akauliza Alex.

"Ana maisha ya kivyake tu. Ana hela sana lakini ni mtu mmoja asiyependa kujionyesha. Umeshawahi kufika kwake? Tena siyo kufika, umeshawahi hata kupaona?" Bobby akauliza.

"Pakoje?" akauliza Mario.

"Pazuri sana. Ana mjengo mkali Dodoma, ngoja niwatafutie hapa muuone. Lakini anaishi kivyakeee," Bobby akawaambia huku akianza kubofya 'keyboard' ya kompyuta yake.

"Siyo ajabu kuna mbunge huwa anaenda huko kum-do," akatania Hussein, nao wote wakacheka.

Luteni Michael akabaki kutafakari maneno ya Bobby. Aliona kuna ukweli mwingi ndani yake kwa sababu kiukweli Nora alimvutia. Lakini kutokana na mambo yaliyokuwa yanawazunguka ilionekana kama huu haukuwa muda mzuri kuanzisha masuala ya mapenzi, ndiyo maana alikuwa kama anampotezea tu. Baada ya wanaume hao kukaa hapo kwa dakika nyingi, nao pia wakaondoka kwenda kujipumzisha.


★★★★


Siku iliyofuata, kundi la Mess Makers tayari lilikuwa kule "chini" kwenye jengo la maficho yao. Ilikuwa ni 'full shangwe' kwa sababu kwa mara nyingine tena walikuwa wamefanikiwa kumtia hasara Raisi Paul Mdeme na serikali yake iliyoficha maovu na ufisadi mwingi. Ikiwa ni asubuhi sasa, wote walikuwa wakifurahia mlo kwa pamoja, kukiwa na vyakula mbalimbali hapo kama vile siyo asubuhi. Wapishi wa vyakula walikuwa ni Torres na Kevin, wakisaidiwa na Lexi pamoja na Lakeisha baada ya kurudi kutoka kwenye mishe yao jana.

Huu ndiyo mlo wa pamoja kama familia ambao Kendrick alimwambia Lexi wangeupata baada ya kukamilisha zoezi la kuziiba dhahabu zile. Bado Oscar alikuwa akiisifia sana timu yao hii, akisema hakutawahi kutokea watu wengine kama wao kwa sababu wamefanya vitu ambavyo hakuna mtu aliyewahi kuthubutu kufanya, huku huo ukiwa ni mwanzo tu.

"Sisi ndiyo Mess Makers!" Oscar akawa anasema huku anatafuna nyama.

"Halafu Oscar, hilo jina siye hatulitaki. Umelazimisha kutuita Mess Makers mpaka vyombo vya habari vimetukariri hivyo," Victor akasema.

"Mission ya kwanza si aliacha ile sticker yenye hayo maneno, na jana tena kayaacha kwenye treni... ndo' tushakuwa Mess Makers sijui hata alikuwa anafikiria nini..." akasema LaKeisha.

"Nyie... Mess Makers jina kali kama sura ya Zelda. Tunawaambia hao maboya kwamba sisi ndiyo wachafuzi wa hali ya hewa. Mlishaiona ile movie ya The A Team?" Oscar akauliza.

"Ile ya wale wajinga wanaofeli kama The Losers?" akauliza Torres.

"Hawafeli bwana. Ni vizuri kuwa na jina namaanisha, siyo kuitwa wezi tu wakati kazi yetu inastahili jina kubwa," akasema Oscar.

"Mh! Unajifanya mpenda kazi sana, wakati jana ulikuwa unawaza tungemaliza saa ngapi ili uwahi kwenda kutia tu hako kamguu kako kwenye tundu lolote la wale... wale wanini wa Dar?" LaKeisha akasema.

Lexi akacheka kidogo na kusema, "Wazaramo."

"Yeah... hao hao," LaKeisha akakubali.

Wengine wakacheka.

"Hivi wewe... unajua kwamba huu mkokoliko ni hatari kuliko wa yeyote nchi hii?" Oscar akasema.

"Aah wapi!" akasema Victor.

"Mkokoliko wenyewe umelala yooh," LaKeisha akasema, nao wote wakacheka.

"Ahahahah... maneno ya nani hayo?" akauliza Kendrick.

"Jamaa fulani hivi Facebook. Ndiyo mkokoliko wa Oscar ulivyo," akasema LaKeisha.

"Nikuonyeshe? Ah-aaah, nikuonyeshe?" Oscar akawa anamuuliza LaKeisha.

"Mpaka nisikie umebebesha mtu mimba, ndiyo utanionyesha," akasema LaKeisha.

"Mimba wapi wewe, unagwaya tu. Au hujui mimba huwa tunazo sisi muda wote? Nyie dada zetu huwa mnatusaidia kuzibeba tu," Oscar akasema.

"A-aaah bro, kama unayo wewe ni wewe mwenyewe," akasema Victor.

"Kwenda huko na mashavu yako kama Bambo," Oscar akamwambia Victor hivyo na kufanya wengine wacheke.

"Bwana, jana Liutenant Michael na ACP Nora wameenda kwenye kampuni za boss Geita na huko huko Dar," Torres akasema.

"Walikuwa wameenda kufanya nini?" akauliza Mensah.

"Kufatilia fabric zenye bulletproof. Nadhani wanafikiri wanaweza kutufikia sisi kwa njia hiyo kwa sababu Nora alipompiga Lexi risasi siku ile Mwanza zilidunda," akasema Torres.

"Boss, hakutakuwa na tatizo lolote hapo? Vipi kama wakipeleleza na kujua mwenye hizo kampuni ni wewe... na wakafanya uchunguzi kujua wewe ni nani..." Victor akauliza.

"Hawawezi. Boss anaziendesha kwa umakini, na hata kama angekuwa anatumia jina lake halisi hawangedhani ni yeye," akasema Torres.

"Eee kweli... bado jina lako litaendelea kuwa 'boss'," akatania Victor.

Kendrick akatabasamu.

"Ukirudi Dar baadae, mchimbe huyo malaya ujue wamepata nini kingine," LaKeisha akamwambia Lexi.

"Siyo kichwa kichwa tu. Nora ni..."

"Yeees, tunajua. Nora ni mwerevu, ana elimu kali, blah, blah, blaah... Lakini bado Lexi atajua tu," Oscar akamwambia Torres.

"Well boss, hapa tuna zigo nene. Hebu fikiria. Nimepima ounce zote za gold nimepata kilo 4000 kamili... pure kabisa. Kwa mahesabu ya haraka hizo ni 200 something million dollars, na kwa Tanzania ni kama billioni 500 huko!" Torres akasema.

LaKeisha akamwangalia na kutabasamu, kwa sababu alipendezwa na jinsi Torres alivyoongea na kasi yake nzuri ya kupiga mahesabu.

Victor akacheka na kusema, "Kwa hiyo... Mdeme alikuwa anataka kufidishia tulichochukua benki kwa hiyo shilingi mia?"

Wengine wakacheka pia.

"Bila shaka alikuwa anataka adanganye kwamba wametukamata baadhi yetu na kuzirudisha hizo, ili support kwake kutoka ndani na nje iwe kubwa," akasema Lexi.

"Lakini Mess Makers tumempika kwenye mwiko wake mwenyewe!" Oscar akasema ki-swagger.

"Lexi... Oscar akituita hilo jina tena, mwambie Zelda aitafune midomo yake," Kevin akasema.

"Zelda halagi nyama mbichi, Masai wewe," Oscar akamtania Kevin.

Wote wakaendelea kula huku wakifurahia mazungumzo yao. LaKeisha alikuwa amekaa kiti kilicho pembani ya kiti alichokalia Torres. Kiutundu, akapitisha mkono wake kwa chini na kuanza kutembeza kiganja chake juu ya paja la mwanaume huyu, naye Torres akamwangalia kiufupi, kisha akajikausha na kuutoa mkono wake kwa chini bila kumtazama. LaKeisha akacheka kidogo, kwa kuwa alikuwa anaanza kumchokoza mwanaume huyu mwenye akili nyingi sana lakini yeye akampiga chini.

Kendrick alifurahia sana muungano wao huu uliokuwa kama wa familia. Akamwangalia Lexi, ambaye alimwangalia pia, naye akamnyooshea glasi yenye juice kama kumwonyesha 'cheers,' naye Lexi akafanya vivyo hivyo pia.


★★★★


Kule Dar es Salaam, Nora aliamkia kujisafisha na kwenda kupata kiamsha kinywa peke yake ndani ya hoteli ile ile aliyokuwa amechukua chumba kwa muda ambao angekuwa jijini, kwa kuwa sasa angetumia muda mwingi pamoja na wanajeshi wale mkoani huku. Alipomaliza, alichukua gari lake na kuanza kuelekea hospitalini akiwa na lengo la kufanya utafiti fulani aliousema jana.

Wakati akiwa mwendoni, Raisi Paul Mdeme alimpigia simu yeye mwenyewe kumuuliza kama kuna maendeleo yoyote aliyofanikisha kuyafikia mpaka wakati huu, naye Nora akasema alikuwa akifuatilia suala fulani ambalo alitumaini lingeleta matokeo mazuri. Mdeme alimsihi sana atie nguvu zaidi kwa sababu Mess Makers walikuwa wanamuumiza sana kichwa chake. Ijapokuwa Nora alitaka kumuuliza kuhusiana na treni ile, akaamua kughairi tu kwa kuwa kwa kadiri fulani aliyaona maneno ya Luteni Michael kuwa kweli, ingawa alihisi kuna vitu Raisi huyu anaficha.

Basi, baada ya kuagana naye, Nora akafika hospitalini kule na kwenda moja kwa moja mpaka idara iliyotunza kumbukumbu mbalimbali za wagonjwa. Alijitambulisha kuwa Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), na hapo alikwenda kufatilia taarifa kuhusiana na wafanyakazi wa benki kuu ambao walijeruhiwa siku ile kwenye bomu lililolipuka kwenye ule wizi wa wahalifu waliojiita Mess Makers. Wale waliotunza makablasha hayo walisema isingewezekana kumpatia, lakini Nora akasisitiza kwamba ilikuwa muhimu sana kuyapata kwa sababu alikuwa akifuatilia kesi hii, na kuchunguza taarifa hizo ilikuwa ni muhimu.

Watunza mafaili hao wakamjulisha kuwa mafaili hayo hayakutunzwa hapo, bali yalitunzwa na daktari fulani ambaye kwa wakati huo hakuwepo hospitali. Nora alipouliza ni kwa nini hawakuwa wameyatunza hapo, watu hao wakamwambia kwamba hawakujua sababu, ila tu yaliwekwa huko kama kufichwa. Nora akashangaa kiasi, naye akauliza daktari huyo alikuwa nani. Wakamwambia aliitwa daktari Shani Immanuel, naye Nora akaachia tabasamu dogo. Alifahamiana naye, na alikuwa na namba zake. Hivyo akawashukuru na kuwaaga akisema angemtafuta ili wazungumzie suala hilo.

Simu yake ikaanza kuita alipokuwa ameanza kuondoka sehemu hiyo. Alipoangalia mpigaji, akakata upesi na kuirudisha mfukoni. Ilikuwa ni baba yake, Jenerali Jacob mwenyewe. Akaendelea kumpigia binti yake huyu, lakini hakupokea hata moja. Nora akarudi mpaka kwenye gari lake, kisha akamtafuta daktari Shani.

Mwanamke huyo alisalimiana naye vizuri kwa kuwa ulipita muda mrefu bila ya marafiki hawa kuongea, naye Nora akamjulisha kwamba alihitaji msaada wake katika uchunguzi mpya aliokuwa anaufanya. Shani akampa pole kwa kumkosa leo hospitalini, na kumwambia kwamba kesho angemkuta, hivyo wangeonana wakati huo. Nora hakuwa na kipingamizi, na baada ya hayo akaagana naye na kuwasha gari sasa ili aelekee jengoni kule kujiunga na timu ya Luteni Michael.

Lakini alipoiangalia simu yake tena, akakuta ujumbe kutoka kwa baba yake. Alimwambia anajua yuko Dar, na kwamba mdogo wake Nora amejiingiza kwenye shida fulani ambayo imesababisha akamatwe. Kwa kuwa Nora alikuwa huku huku Dar es Salaam, akamwomba aende kumtoa kwa sababu yeye (Jenerali Jacob) alikuwa mbali. Akamwandikia pia kwamba anapaswa kuacha utoto, awe anapokea simu zake.

Nora aliudhika sana. Alitamani hata kumjibu kumwambia aagize mtu mwingine, lakini alijua angepaswa tu kwenda kumsaidia mdogo wake. Mdogo wake huyo alikuwa wa kike, naye alikuwa mtukutu vibaya mno, aliyependa kuishi kwa kujiachia kutokana na miendekezo ya baba yake. Lakini walipendana na Nora, na ijapokuwa yeye Nora hakuwa na ukaribu na baba yao kama mdogo wake, bado alimwongoza mara kwa mara, ingawa kwa sababu ya umri mdogo wa ujana, mdogo wake huyo alikuwa na kichwa kigumu na ndiyo sababu mara kwa mara angejiingiza kwenye shida.

Nora akampigia Luteni Michael kumjulisha kwamba kuna suala fulani lilizuka alilohitaji kwenda kusuluhisha hivyo huenda angechelewa au asingefika leo, lakini kama wangepata jambo jipya ambalo wangehitaji ahusike basi angemtaarifu. Luteni Michael akamwambia hakukuwa na shida, naye Nora akaondoka hapo na kwenda mpaka kule mdogo wake alipowekwa ndani. Alikuwa ameshikiliwa na mapolisi kwa sababu usiku wa jana alikuwa kwenye club moja, ambapo fujo zilitokea, na yeye alihusika. Kwa hiyo maaskari walimkamata yeye pamoja na vijana wengine kutokana na fujo hizo walizofanya kwa sababu ya kulewa sana.

Baada ya Nora kumtoa, alikwenda naye mpaka hotelini kwake ili kumpa somo kuhusu mwenendo wake usiofaa. Alimkanya kutenda kama mtu mpumbavu, na kumwambia asingemsaidia tena wala kuongea naye endapo hali hiyo ingejitokeza. Binti akamwomba dada yake samahani, kwa kusema jana alikuwa tu na misongo kwa kuwa alimwomba mpenzi wake watoke, lakini mpenzi wake huyo akamkwepa na kusema hangeweza kutoka naye kwa jana kwa kuwa angeenda sehemu nyingine, hivyo aliudhika tu na kwenda na vijana wengine ambao wangekuwa ndiyo njia rahisi ya kumsaidia kuchangamsha akili.

Binti huyu alikuwa ndiyo wa mwisho kuzaliwa, na ijapokuwa alikuwa na miaka 23, bado mambo mengi aliyafanya kama mtoto kwa sababu ya kuwa kitindamimba. Alikuwa mrembo kama dada yake tu, "black beauty," naye aliitwa Asteria. Nora akaongea naye na kumpa ushauri mzuri kuhusu kujidhibiti, kisha baada ya maongezi yao, wakatumia muda pamoja kufurahia undugu wao kama dada. Asteria hata akamsuka Nora kwa mtindo mzuri wa rasta, kisha baadae Nora akampeleka mpaka kule Asteria alikoishi, yaani kwenye nyumba waliyokuwa wamejengewa na baba yao. Nora hakuwahi kabisa kukanyaga ndani huko, na hii ikiwa ni kwa sababu ya chuki yake kumwelekea Jenerali Jacob. Hivyo akampeleka tu na kumshusha njiani, kisha akajiondokea zake.

★★

Kufikia wakati aliporudi upande wake wa jiji hili, giza tayari lilikuwa limeshaingia kutokana na yeye kutumia muda mwingi na mdogo wake. Akaamua tu kuelekea kule kwenye bar/mgahawa ule, yaani Sea House, ili kuichangamsha akili kidogo kwa kuwa hakutafutwa na Luteni Michael. Hakutaka pia kusumbuliwa na yeyote, bali kuwa peke yake tu na kupiga kilevi kwa kadiri ambayo ingemfanya atulize akili kutokana na mambo mengi yaliyokuwa yanamzunguka. Alifika tu kwenye meza ya bartender na kumwambia Elias amwekee kama kawaida yake, naye jamaa akamsogezea kinywaji.

Akiwa bado amekaa huku akinywa taratibu, akasemeshwa na sauti aliyoikumbuka haraka.

"Habari mheshimiwa?"

Nora akageuka na kukuta ni Lexi. Alikuwa tayari amerudi jijini na kuja kujifanya raia mwema mbele ya Nora. Alivalia suruali ya kardet, sweta la rangi ya blue lenye sehemu ya kufunika mpaka kichwa (hood), lakini alikuwa hajakifunika. Uso wake mzuri mweupe usio na make up ya aina yoyote ulimwambia Nora kwamba kiukweli "mwanamke" huyu hakuwa na uhitaji wa kujionyesha sana kwa kuwa alijikubali.

"Safi, vipi?" Nora akajibu, lakini bila kuonyesha hisia yoyote.

"Fresh. Naona umekuja kujichimbia tena huku," Lexi akasema huku akichukua glasi ya wine.

"Yeah... unaweza kusema hivyo," Nora akasema na kukirudia kinywaji chake.

"Umependezea hivyo ulivyosuka," Lexi akamwambia.

"Nashukuru," Nora akajibu bila kumtazama.

"Naona unapendelea ladha asili za nchi... Dane red wine. Dodoma wamepiga hatua," Lexi akasema.

"Yeah ni nzuri. Ulishawahi kuonja?"

"Naaah... me za nchi hii sigusagi."

"Unaonekana kama vile haupendi mambo mengi ya Tanzania. We ni mhamiaji au?"

Lexi akacheka kidogo.

"Hata wewe unaonekana kama vile umetoka kulazimishwa kumeza tango huko ulikotoka," Lexi akatania.

"Leo umetoa wapi ujasiri wa kuongea nami namna hiyo?" Nora akauliza huku amekaza macho.

"Oh, shit sorry... nilikuwa tu natani..."

"Mimi siyo rafiki yako, kwa hiyo usinitanie. Hatujuani," Nora akasema kiukali kidogo.

Lexi akatazama tu pembeni na kuangaliana na Elias, ambaye alikuwa amemsikia Nora akisema hivyo. Baada ya kutambua kwamba alimfokea Lexi pasipo sababu yoyote, Nora akajihisi vibaya kwa kadiri fulani. Akatazama tu chini na kujituliza, akifikiria kumwomba samahani kwa kumsemesha kwa njia hiyo. Lakini akaanza kusikia wanaume fulani waliokuwa wamekaa meza za pembeni nyuma yao wakiongea mambo yaliyomhusu Lexi.

Walikuwa wakisema mara eti demu ni mkali sana, anaonekana ana kalio jeupe sana kama uso wake, anaonekana ndiyo ametoka tu kuvunja ungo, na kwamba hapo hakuwa akitafuta chochote zaidi ya mtu wa kumhonga, hivyo yeyote kati yao angekubali tu kutoka naye. Walikuwa wakiutania mwonekano wake kwa kusema amejiweka kama mwanaume fulani hivi ili asifuatwe, lakini kihalisi anataka kufuatwa. Nora alipomwangalia Lexi, alitambua yeye pia alikuwa akiwasikia lakini akawapuuzia tu. Alipowaangalia wanaume hao, walikuwa ni watano, watu wazima kabisa kwenye miaka ya 40 mpaka 50 huko, wakiwa wameweka vilevi vingi mezani kuonyesha wazi pombe pia ilikuwa ikiwasumbua.

Nora akawa anatafuta njia ya kumsemesha Lexi ili amwombe samahani, lakini mmoja wa wanaume wale akanyanyuka na kwenda mpaka nyuma yake Lexi. Akamshika kiunoni kiutongozi na kuegamia sehemu ile ya bartender huku anamwangalia kwa tabasamu la uchokozi, lakini Lexi akaendelea tu kunywa wine yake bila kufanya lolote. Nora akawa ameingiwa na hasira kiasi bila hata kujua sababu ni nini kwa kuwa kama alivyosema, yeye na Lexi hawakuwa marafiki. Lakini ni hali hiyo tu ndiyo iliyomkera sana na kumfanya atamani ingekuwa ni yeye wamemfanyia hivyo ili awanyooshe, ila akataka kuona Lexi alikuwa mwanamke wa aina gani; kama ni kweli walichosema wanaume hao kumhusu, au la.

"Mambo vipi joto?" mwanaume huyo akamwambia Lexi huku anatabasamu.

"Oy Elias, niongezee kinywaji," Lexi akasema kwa kumpuuzia mwanaume huyo.

"Usijali dear, naweza kukuagizia kreti zima ukitaka. Sema chochote unachotaka," mwanaume huyo akamwambia.

"Nataka uutoe mkono wako kiunoni kwangu," Lexi akamwambia bila kumwangalia.

Nora akamtazama mwanaume huyo. Alikuwa amelewa kiasi lakini siyo ya kuyumba.

"Aaaa... lakini si unapenda nikikubinya-binya kama hivi..." mwanaume huyo akasema huku akiwaonyeshea wenzake sasa ili wampe sifa.

"Luka, em' mwache dada wa watu. Mkeo atamuua," Elias akamwambia mwanaume huyo.

"Hahahaaa... Elias, we kaa kutumiminia tungi, njugu tuachie sisi," Luka akasema.

Nora mpaka hapo alikuwa tu akisubiria zari lianze ili atembeze maumivu haswa. Lexi yeye alikuwa ametulia tu kama haelewi somo vile. Mwanaume huyo, Luka, akamsogelea Lexi karibu zaidi na sikio akitaka kumsemesha kiutongozi, naye Lexi hakutikisika.

"Niambie mrembo... unanionaje? Kama John Cena mweusi au siyo? Nakwambia huko chini nina mdudu muhogo uhogo yaani... utafurahia sana leo," Luka akasema.

Wenzake wakacheka kwa sifa.

"Aliyekwambia me nataka muhogo nani?" Lexi akamuuliza.

"Najua umenipenda tayari, na sikulaumu maana ndiyo sipeshilialiti yangu. Dada mzuri kama wewe unahitaji mwanaume ngangali kama mimi.... eeh...."

"Mm-hmm..." Lexi akasindikiza.

"Yeah. You know... kuna watu huwa wananichanganya na mwanaume fulani hivi lakini siyo mimi. Kwanza me sina mke. Mke wangu alikufa mwaka kesho siku kama ya leo, kwa sababu ndiyo siku niliyokutana na wewe...."

Nora akatikisa kichwa akimwonea huruma Luka kwa kuwa alianza kuona mwanaume hakuwa kitisho kikubwa sana kama alivyodhani, na kufikiri huenda hata Lexi alikuwa akifurahishwa naye.

"Hebu niambie... unaponiona mimi hivi... hivi unavyoniona... nakupa hisia gani nzuri? Mmm? Sema tu nijue..." Luka akasema.

"Hapana hautaki kujua," Lexi akamwambia.

"Come oooon... niambie bwana... tell me...." Luka akawa anabembeleza kilevi-levi.

"Mmm... okay. Kiukweli hisia nayopata ni kama kupigia punyeto kichwani lakini ubongo haufiki kileleni kwa sababu uso unaouona ni wako," Lexi akamwambia hivyo.

Luka akabaki kutumbua macho.

Elias pamoja na watu wengine waliomsikia Lexi wakacheka kwa sauti sana na kuendelea kumcheka Luka. Jamaa akaanza kuangalia huku na huko kama kujiona amekuwa kituko kikubwa. Nora alikuwa akitabasamu kwa kufurahishwa na maneno ya Lexi, naye Lexi akampa Luka tabasamu la kumwambia kwa heri. Luka akasonya na kusema 'Malaya wewe' na kuanza kuondoka, kitu kilichofanya watu waendelee kumcheka. Nora naye akachekea kwa chini huku akimwangalia sana Lexi, naye Elias na wengine wakawa wanamtania jamaa aliporudi kuketi na wenzake.

Lexi akamwangalia Nora na kutabasamu kirafiki, naye Nora akatabasamu pia.

"Ona... samahani kwa kuwa sikukusemesha vizuri sana muda ule..." Nora akasema.

"Siku ngumu kazini eh?" Lexi akauliza.

"Yeah..."

"Twende, nifate..." Lexi akasema huku akinyanyuka.

"Kwenda wapi?" Nora akauliza.

"Kuna sehemu hapo nje imetulia zaidi. Twende tukakae maana hapa naona kuna kelele tu za hawa mbwa," Lexi akasema huku anamwangalia Luka na wenzake.

Nora akatabasamu kwa kuona jinsi Lexi alivyokuwa mwenye kujiamini. Akamalizia wine yake yote kwenye glasi na kunyanyuka pia, kisha akatoka pamoja na Lexi kuelekea nje. Walikuwa wakielekea taratibu upande wa fukwe za bahari.

"Umeoga?" Lexi akauliza wakati wakiendelea kwenda.

"Hapan... yaani, kuoga asubuhi au?"

"Namaanisha ulipotoka kazini..."

"Ahah... hapana. Nimekuja moja kwa moja hapa..."

"Okay, basi ndiyo maana moody ilikuwa high..."

"Kwa hiyo kuoga ndiyo ingeituliza eeh?"

"Nothing a good shower won't solve."

Nora akatabasamu.

"Nina mambo mengi wakati mwingine inaweza kupita hata siku nzima sijaoga," akasema Nora.

"Mwenzako ziliwahi kupita wiki 3 sijaoga, nilipokuja kuoga nilimaliza tank zima la maji..."

"Ahahah... aa wapi. Haiwezekani..."

"Kwamba nilikaa wiki zaidi ya tatu bila kuoga au kumaliza maji tank zima?"

"Vyote..."

"Well, angalau nimekufanya utabasamu. Nilifikiri wewe huwa ni makwenzi na pingu tu..."

"Ahahah... no, huwa siko hivyo. Siku hazifanani kwa hiyo wakati mwingine inaweza kunikuta vibaya... hata wewe una siku za namna hiyo bila shaka..."

"Yeah, najua unachomaanisha. Its okay. Mimi napenda sana utani... na ijapokuwa sisi siyo marafiki nilitaka tu kuchangamsha mazungumzo. Ila ushauri kidogo; kama unataka kutuliza akili basi tafuta sehemu iliyotulia maana hapo ndani ni kwa machizi kama sisi..."

"Ahahah... basi na me ni mmojawapo kwa kuwa nilikuwa humo pia..."

"Yeah, sema we ukiingia tu inabidi mbwa mwitu wengi humo wavae ngozi ya mbuzi... angalau Luka kajitahidi leo," akasema Lexi, naye Nora akacheka kidogo.

"Nilidhani angekusumbua. Nilikuwa nimeshajiandaa kumfumua," Nora akasema.

"Ahah... ningekuwa shabiki wako mkubwa kama ningeona hilo," Lexi akamwambia.

Simu ya Nora ikaita, lakini baada ya kuangalia aliyepiga, Nora akakata tu na kuirudisha kwenye mfuko wake.

"Boyfriend?" Lexi akauliza.

Nora akatabasamu na kusema, "Sina huo muda."

"Kwa nini?" Lexi akauliza.

"Kama nilivyokwambia... mambo mengi."

"Mmmm... okay.

"Nini... mbona unaguna?"

"Hamna kitu. Ni kwamba tu nimeenda moja kwa moja kwenye 'boyfriend' bila kufikiri uwezekano kuwa ni 'husband'..."

"No, mimi sijaolewa. Au naonekana kama nina miaka 70?"

"Aam... kiukweli nilikuwa nafikiri 90 umeshafikisha..."

Nora akacheka.

"Asante. Huku tunakoenda ni ili ukaogelee au?"

"Na hii baridi? La. Nilikuwa tu nataka kukuonyesha sehemu fulani nzuri sana hapa..."

"Hapa pote napajua vizuri sana. Nimetembelea sehemu hii mara nyingi na kuzunguka mno..."

Wawili hawa walifika sehemu yenye miti na giza kiasi nyuma ya jengo fulani dogo la mbao. Kulikuwa na mti katikati ya bonde dogo, sehemu ambayo mtu angeshuka kama ngazi, na mwanga wa mwezi ulimulika vizuri sehemu ya mbeleni. Wakapapita, naye Nora akaona sehemu nzuri yenye vichaka, miti na beach kwa mbele. Kulikuwa na viti viwili vya beach vilivyowekwa kutazama upande waliotokea, na moto wa kuni uliwaka chini baina yavyo.

Nora alipofika pale, Lexi alimtazama na kuona jinsi mwanamke alivyopendezwa sana na mandhari hiyo.

"Karibu kwenye sehemu yangu ya siri," Lexi akamkaribisha.

"Ahahah... eti sehemu ya siri. Hivi vitu umeviweka hapa wewe mwenyewe au?" Nora akauliza.

"Ndiyo. Ona nimeficha na chupa za wine hapa," Lexi akachuchumaa kumwonyesha chupa zenye wine zilizokuwa zimefukiwa chini.

"Ahahah... unazitoleaga wapi? Sikujua kama una kiwanda," Nora akauliza.

"Huwa naziiba hapo House. Siku ukikuta sina sikio moja ujue tu ni Elias!" Lexi akatania.

Nora akacheka kisha akaketi kwenye kiti cha pembeni. Aliiona bahari mpaka mbali, na sauti ya mawimbi ikamfanya atulie. Lexi naye akaketi na kumpa chupa moja ya Dompo.

"Asante. Kwa hiyo... hii ndiyo... sehemu ya... kuwa kivyako?" Nora akamsemesha.

Lexi akajibu, "Ndo' nayopenda zaidi, na ndo' rahisi kuifikia. Zipo nyingine kibao kuzunguka fukwe. Unajua wakati mwingine huwa nawaza naweza kukaa tu siku moja nikashtukia nafumuliwa na mtu kwa sababu ya kuingia kwenye sehemu yake."

Nora akacheka kidogo na kusema, "Nafikiri hii beach iko free kwa kila mtu kwa hiyo usiwaze kuhusu hilo."

"Yeah, ni moja kati ya sehemu tulivu. Nzuri kwa ajili ya romance," Lexi akasema.

"Kweli. Ni vizuri ukimleta boyfriend wako hapa..."

"Ahah... sina boyfriend mie..."

"Kwa nini?"

"Basi tu. Sijawahi kuwa na boyfriend maisha yangu yote..."

"Mmm..."

"Nini sasa?"

"Hamna kitu..."

"Ni ngumu kuamini?"

"Sidhani kama kuna mtu atakayeweza kuamini hilo. Unaplay hivyo kwa kuwa me ni askari au?"

"La. Nachokwambia ni kweli. Kuwa na boyfriend siyo kitu yangu kabisa..."

"Sawa..."

"Ahahahah... hutaki kuamini. Hutaki sina boyfriend, unataka nina boyfriend..."

Nora akacheka kidogo.

"Sitakulazimisha. We inaonekana ushaweka hadi na mpango wa ndoa kabisa..." Lexi akamwambia.

Nora akacheka tena na kunywa wine kidogo.

"Kuwa care usiitamani sana, nasikia hizo zinawahi kuwazeesha wanawake hatari..." Lexi akatania.

"Ikifika itafika tu, lakini siyo sasa. Baada ya muda. Bila shaka hata wewe unatamani siku moja kuolewa, kuzaa watoto, kuwa na mume wako, si ndiyo?"

Lexi akamtazama kwa sekunde mbili tatu, kisha akasema, "Hapana. Hiyo siyo kitu yangu kabisa mheshimiwa."

"Mh? Ina maana hautaki kuolewa? Kila mwanamke anataka kuolewa, kuwa na familia," akasema Nora.

"Ndiyo najua, hata ma-sister pia... lakini siyo mimi..."

"Ahahahah... ila wewe! Kwa nini sasa?"

"Wanaume siyo type yangu."

"Kwa hiyo type yako ni nani... wanawake?"

Lexi akamtazama kwa umakini kiasi, kisha akasema, "Ndiyo."

Nora akapandisha nyusi juu kidogo kwa kuwa hakuwa ametarajia jibu hilo.

"Okay. Kumbe wewe ni Bi?" Nora akauliza.

"Hapana. Yaani... inachanganya kidogo lakini..."

"Usijali. Nimekutana na watu wengi kama wewe na ni kawaida tu," Nora akasema.

Lexi alijua kwamba kwa yeye ilikuwa tofauti si kwa sababu alizofikiri Nora, lakini akamwacha afikiri hivyo hivyo.

"Kwa hiyo na wewe unayesema unataka kuolewa lakini kwa sasa mambo mengi... utafika huko lini? Miaka 40?" Lexi akauliza.

"Ahahah... sijui. Nachojua tu ni kwamba kwa sasa hapana," akajibu Nora.

"Wanaume wengi wanaumiza vichwa eeh?"

"Yeah. Nafurahia zaidi kuwa mwenyewe kwa sasa..."

"Umekuwa mwenyewe kwa muda gani?"

"Ni muda mrefu..."

"Alright. Una uhakika hautaumwa? Mwanamke anahitaji show za hapa na pale mara kwa mara..."

"Ahahahah... basi nitakuwa naukaribia ubikra tena maana ni miaka imepita..."

"Damn! Uko vizuri. Unakumbuka hata mara ya mwisho show ilikuwa vipi?"

"Agh... yaani mimi kwenye uchaguzi sikufichi, nilikuwa ovyo sana. Punda wote niliopanda walikuwa na miguu kama ya panzi..."

Lexi akacheka.

"Angalau wa mwisho alikuwa na jiti kali, lakini kulitumia hakujua..."

"Ilikwendaje?"

Nora akasema, "Yaani tulimaliza muda siyo mrefu hata wa mimi kufika kileleni. Hilo linakuambia nini?"

"Oooh shit, dakika nne! Ahahahah... alijitahidi," Lexi akasema.

"Huyo jamaa hapana. Like, alikuwa na dude zuri tu ila muda kwake ndo' ilikuwa shida. Halafu eti likajitoa akili kabisa. Eti linafikiri nimeenjoooy, linasema tupige nyingine kesho, ya dakika mbili?" Nora akasema na kumfanya Lexi acheke.

"Akakuacha unajisikia kama shimo tu eeh," akasema Lexi akamwambia.

"Wee! Acha yaani..."

"Ahahah... pole. Mapenzi ni mapenzi tu lakini. Huwezi jua lipi litakuwa zuri au baya mpaka uingie...au niseme... ufanye..."

Maneno ya Lexi yakamfanya Nora awaze kuwa huenda "mwanamke" huyu alikuwa ni mmoja wa wale wanaojua kutoa raha haswa. Nora akashindwa kujizuia kuzama sana kwenye kuyaangalia macho mazuri ya Lexi. Alipatwa na hisia fulani hivi kama vile yuko na mtu anayemfahamu vizuri sana, na kufikia hapa alitambua kuwa Lexi alimfanya ajiachie kwa kadiri fulani na kupunguza mikazo yake kiasi.

Wakaendelea na maongezi ya kirafiki kwa dakika kadhaa, kisha Nora akamuaga akisema alihitaji kupumzika kwa ajili ya kazi muhimu kesho. Akamwacha Lexi akiwa amemwambia wangeonana tena endapo angerudi hapo Sea House au sehemu nyingine.

Lexi sasa akawa ameshaanza kufanikiwa kumwingia Nora. Alianza kuona aina ya utu aliokuwa nao mwanamke huyu, naye akawa anatafakari atumie njia zipi ili kuweza kupata taarifa mpya kutoka kwake kuhusu tafiti zao kuwaelekea Mess Makers.


★★★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★★★

WhatsApp +255 787 604 893
 
FOR YOU

Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Uhalifu, Mauaji, Visasi, Vita, Mambo yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU

★★★★★★★★★★★★★★★★★


Asubuhi ilipofika siku iliyofuata, ACP Nora aliamkia kule kwenye jengo lile ilipokuwepo timu ya Luteni Michael. Aliwakuta baadhi yao tu; Bobby, Mario, Hussein, na Omari, nao wakamwambia alipendeza sana kwa msuko wake mpya, kisha wakamjulisha kwamba Luteni Michael na wengine walielekea kule alikokuwa Kanali Oswald Deule kwa kuwa walihitaji kumpa taarifa za maendeleo yao katika msako huu, na ili awapatie mbinu na mwongozo mpya pia kusaidia. Nora akamjulisha Bobby kwamba jana alitingwa na mambo fulani, hivyo utafiti wake kule hospitalini ulikwama, lakini leo angerudi tena ili kuukamilisha, kisha angekuja na mambo mapya pia. Mario akatania kwa kusema siku ya leo ingekuwa kama siku ya mapumziko kwao kwa sababu wasingepiga hatua yoyote mpaka Luteni Michael arudi.

Baada ya hapo, ACP Nora akawasiliana tena na daktari Shani kumuuliza ikiwa angekuwa na muda wakati huo ili aonane naye, na daktari huyo akamwambia angepata muda wa kuwa huru kwenye saa 8 mchana, hivyo aende wakati huo. Nora akakubali, kisha akawaaga wengine kwa kusema anaenda kufatilia mambo mengine. Kihalisi alitaka kwenda kumwona Asteria tena, naye akamtafuta na kumwambia watoke kupata chakula sehemu fulani.

Walikutana muda mfupi baadae, naye Asteria akamwambia dada yake kuwa alijisikia vizuri zaidi sasa, na kwamba mpenzi wake alimwomba samahani na kumpa zawadi nzuri sana. Nora akafurahia sana kwa ajili yake, huku Asteria akimwambia na yeye pia atafute mwanaume kwa sababu alipitwa na mambo mengi. Nora akasema wakati huo ungefika tu, ila kwa sasa alihitaji kupiga kazi kwanza, na mapenzi yangefuata baadae.



Walikuja kuagana kwenye saa 7 ya saa 8, naye ACP Nora akaenda hospitalini kuonana na daktari Shani. Alipokelewa vizuri na mwanamama huyo, ambaye alibobea kwenye masuala ya upasuaji, kisha wakaanza mazungumzo kuhusiana na historia yao ya urafiki. Shani pia alisomea Marekani kama Nora, na kwa kipindi fulani walipatana sana kule ijapokuwa walisomea masuala tofauti na kuonana mara chache. Baada ya kukumbushia, Nora sasa akaja kwenye pointi iliyompeleka. Akamweleza alichohitaji, lakini Shani akasita kumpatia. Alimwambia alipewa jukumu la kuzilinda taarifa zile na watu wa "juu," yaani watu wenye nguvu, naye hakupaswa kuzitoa ovyo kwa yeyote.

Nora alishindwa kuelewa sababu ni nini kwa kuwa hata Shani hakujua sababu ni nini, lakini alijua tu kwamba hakupaswa kuyatoa bila idhini ya watu hao. Nora akalainisha mambo kwa kumwambia amwamini tu, kwamba alihitaji taarifa fulani tu ndogo, na baada ya hapo angemrudishia bila yeyote kujua. Akamwomba sana, naye Shani akalegeza. Akampatia mafaili yenye taarifa za majeruhi wale na kumsihi azirudishe kufikia kesho muda kama huu. Akamwomba sana asimwonyeshe yeyote yule, naye Nora akakubali na kumhakikishia kila kitu kingekuwa sawa.

ACP Nora akamuaga daktari huyo na kuondoka hapo hospitalini. Alikuwa anatamani sana kumuuliza ni nini na ni nani waliomzuia mwanamke huyo kuzitoa taarifa hizi, lakini hakutaka kumshurutisha kufanya mambo ambayo huenda yangemsababishia mama wa watu matatizo asiyokuwa na uelewa wowote kuyahusu. Akaona ni vyema tu aende yeye mwenyewe kutafiti alichohitaji kisha amrudishie mafaili hayo kabla ya jambo lolote lisilotazamiwa kutokea.

Lakini Nora hakuweza kuyapitia mafaili hayo baada ya Inspekta Jenerali wa Polisi, IGP Donald Ngassa, kumtafuta na kumwomba akutane naye ili ampatie msaada kwa jambo fulani. Yaani Nora hakuwa mtu wa kupumzishwa kabisa. Kwa kuwa ni siku chache zilikuwa zimepita tokea mara ya mwisho walipoonana, akakubali tu kwenda upande wake kuona angeweza kusaidia vipi. Akaahirisha kuyasoma mafaili yale na kuyapeleka tu hotelini kwake, kisha akaelekea kwa IGP.


★★★★


Muda ulisonga, naye ACP Nora akawa amemaliza kumpatia IGP Donald Ngassa msaada aliohitaji kwenye masuala ya kuwaongoza baadhi ya polisi wa kitengo fulani upande mwingine wa jiji. Alikuwa amemwomba msaada huu Nora kwa sababu alijua kipawa chake cha kuongoza mambo kilikuwa kikubwa, lakini pia ni kwa sababu tu ya uvivu akaona ampe dada wa watu kazi zaidi.

ACP Nora akaanza kurejea upande wake wa jiji hatimaye. Aliwasiliana na Luteni Michael, ambaye alimwambia kwamba walikuwa wamerejea huku baada ya mkutano wao mfupi na Kanali Oswald, hivyo wangeendelea na kazi. Lakini akamwambia Nora apumzike tu kwanza kwa leo, ili kesho ndiyo wakutane na kujipanga vizuri zaidi. Nora akaafikiana na hilo, akisema pia utafiti wake aliotaka kuufanya ungekuwa mezani kwao kufikia kesho, naye akamshukuru Luteni Michael kwa kumpa muda wa kupumzika.

Giza lilikuwa limeshaingia kufikia wakati huu, naye Nora akaamua kwenda kule Sea House kwanza ili ajipe muda wa kutuliza akili yake kama kawaida. Alikuwa na wazo pia la kuonana na Lexi, kwa sababu ni kama alianza kumzoea "mwanamke" huyo ambaye alikuwa ameanza kuwa njia nzuri ya kumsaidia kusafisha akili yake kutokana na misongo mingi. Hakuwa na ukawaida wa kupendezwa na watu mpaka kutamani kuwaona tena, lakini kwa Lexi sasa ilianza kuwa tofauti.

Alipofika pale, alikaribishwa na Elias na jamaa kumuuliza ikiwa angependa amwekee kinywaji kama kawaida yake. Nora akakubali na kuketi, kisha akaendelea kuwa hapo akinywa wine yake taratibu kama anasubiri mtu. Lakini wakati huu Lexi hakufika hapo, hivyo akamuuliza Elias ikiwa leo angefika, au kama ratiba yake haikueleweka. Elias akatania kwa kumuuliza ikiwa alitaka kumkamata labda, lakini Nora akasema alikuwa tu anataka kumwona, naye Elias akamjulisha kuwa Lexi alifika hapo kabla yake kisha akaondoka kuelekea sehemu fulani za beach, lakini hakujua ni wapi.

Moja kwa moja Nora akakumbuka sehemu ile ambayo Lexi alimpeleka usiku wa jana, naye akamalizia kinywaji chake na kuondoka ili aende kujaribu kuona ikiwa alikuwa huko. Ilikuja kwa kumshangaza kiasi kwa nini alitia jitihada za kutaka sana kumwona "mwanamke" huyo, kwa sababu hata hakumfahamu vizuri namna hiyo. Lakini bado tu ikawa ni kama kuna kitu kinamsukuma kuendelea kumtafuta, akitarajia kuwa na mazungumzo mazuri pamoja naye kama usiku uliotangulia.

Baada ya kufika sehemu ile, alivikuta viti vile pale, na chini kukiwa na moto uliowaka katikati ya kitu kilichochengenezwa kama mafiga madogo. Nora akatabasamu baada ya kumwona Lexi akiwa ameketi kwenye kiti kimojawapo kwa kumpa mgongo. Alikuwa amevalia nguo nyeupe yenye kubana mwili kwa juu, iliyokuwa yenye mikono mirefu na kufunika mpaka sehemu ya shingo yake. Suruali ya jeans nyeusi ilionekana pia miguuni mwake, na viatu vya raba vya rangi nyeupe pia. Kulikuwa na chupa mbili za wine chini pamoja na vikombe viwili pia. Akaanza kusogea taratibu kumwelekea.

Lexi akahisi kabisa kwamba kulikuwa na mtu anakuja nyuma yake, na kwa sababu hakujua ni nani, akaishika chupa ya wine na kuikaza kiganjani mwake bila kugeuka ili kama ni adui basi amshambulie kiaina.

"Nimekubamba..."

Sauti ya Nora ikasikika kwake ikisema hivyo, naye Lexi akatenda upesi na kujifanya kashtuka na kugeuka nyuma.

"Hey! Don't do that... umenishtua!" Lexi akasema.

"Ahahahah... pole. Mambo vipi?"

"Safi. Karibu..."

"Asante. Kuna mtu unamsubiri?"

"Hapana..."

"Mbona naona chupa na vikombe viwili?"

"Labda nilikuwa nakusubiri wewe..."

"Ah wapi! Polisi huwa hasubiriwi..."

"Ahahah... ila anakimbiwa tu..."

Nora akaketi kwenye kiti cha pembeni.

"Unapenda kuwa hapa peke yako tu kwa nini sasa?" Nora akauliza.

"Nafikiri nilikwambia sababu ile jana..."

"Eeh kweli... kwa sababu pametulia..."

"Angalau lakini umekuja. Za huko? Unaonekana kama vile umetoka kukimbizana na akina Mess Makers ahahahah..." Lexi akatania kimakusudi.

"Ahahah... ungejua..." Nora akasema.

Lexi akaanza kuwekea kikombe cha pili wine, naye Nora akawa anamwangalia kichwani, akipendezwa na jinsi nywele laini za Lexi zilivyopeperushwa na upepo wa bahari.

"Hao jamaa bado wanawasumbua sana mapolisi, eti?" Lexi akauliza.

"Agh... achana na habari zao. Tuongelee mambo mengine lakini siyo kazi, sawa?" Nora akamwomba.

"Okay," Lexi akasema na kumpatia kikombe chenye kinywaji.

"Nywele zako ni natural, eti?" Nora akauliza.

"Naam? Ndiyo. Ni zangu," Lexi akajibu.

"Ni nzuri. Nafikiri ungependeza zaidi kama ungeziacha zote zikue badala ya kupiga duku hilo," Nora akamtania.

"Ahahah... asante kwa ushauri..."

"Asili yenu... asili yako ni ya wapi?"

"Kwa kina bin Laden kule..."

Nora akacheka.

"Naonekana kama mhindi eti?" Lexi akauliza.

"Tena wale weupe..."

"Nimeshaambiwa na wengi niwape ushauri kuhusu dawa nayotumia usoni ili wawe kama mimi. Wanafikiri najichubua..."

"Ahahahah... hamna wamekosea. Ngozi yako ni nzuri sana lakini..."

"Asante. Hata we siyo mbaya sana," Lexi akatania.

Nora akacheka na kunywa wine kidogo.

"Kwa nini dada mzuri kama wewe ukaamua kuwa polisi? Si ungepiga hata modelling?" Lexi akauliza.

"Ahahahah... wewe ni mtu wa ngapi sijui kuniambia hivyo," Nora akasema.

"Wote waliokwambia hivyo ujue wanasema kweli. Hauonekani kama type za mapolisi wanawake..."

"Kwa nini? Kwani type zao zikoje?"

"Manene manene, meusi, pardon me lakini, wengi wanaonekanaga kama hawawezi kukaa dakika zaidi ya mbili bila kuomba hela madereva wa magari barabarani..."

Nora akacheka.

"Siyo wote wako hivyo bwana. Na mimi siko kundi hilo," Nora akasema, naye Lexi akacheka pia.

"Kiukweli ndiyo moja ya mambo yaliyonifanya nisiamini kwamba wewe ni askari mara ya kwanza tulipoonana. Yaani dada uko vizuri kisura na kimwili. Hata ukisema uombe kupiga u-video vixen, wasanii watapanga foleni ili kukuchukua," Lexi akatania.

Nora akacheka na kusema, "Flattery ni nzuri kwa mwanamke wa aina yako Lexi. Kiukweli mimi nilipenda sana kuja kuwa askari tokea nilipokuwa mdogo."

"Kwa nini?"

"Mmmm... naweza kusema tu kwamba nilipenda kusaidia watu. Mara ya kwanza nimeokoa uhai wa mtu nilijisikia vizuri sana, nikataka kufanya mengi zaidi kiutumishi ili kuweza kuwasaidia wengi zaidi," Nora akaeleza.

"Mara ya kwanza umeokoa mtu ilikuwa wapi?"

"Ilikuwa... kwenye hoteli fulani hivi wakati niko mdogo. Tena nilikuwa na miaka 14 tu. Kuna mtoto mdogo alikuwa kwenye swimming pool, akashindwa kuji-handle vizuri na kuzidiwa na maji. Ndiyo nikaingia kumwokoa. Ni siku ambayo sitasahau yaani. Ilinifanya nijihisi vizuri sana," Nora akasimulia.

Lexi akabaki kukunja uso kwa kutafakari. Kisa alichokisimulia Nora kilifanana na kisa alichojionea yeye mwenyewe wakati alipokuwa mdogo. Akakumbuka pia kwamba aliwahi kukiandika kisa hicho kwenye moja ya kazi za madam Valentina wakati yuko chuo. Nora alipomwangalia Lexi, akatambua alikuwa amezubaa.

"Hey vipi?" akamuuliza.

"Oh, oh nothing. Aam... nimependezwa tu na hadithi yako. Umeanza kuwa hero tokea udogoni kumbe..." Lexi akajibu.

"Huwa sijioni kama hero, ila kama mtumishi tu wa kawaida..."

"Unaonekana kuwa na life ya juu pia..."

"Mh... hapana. Kawaida tu..."

"Kwani huwaga mnasema sasa..."

"Ahahahah... haijalishi. Mimi napenda kuishi maisha ya kawaida tu..."

"Mmm... ya kivyako pia eeh?"

"Yeah..."

"Hauna ndugu wengine wanaong'ang'ania chenji ya mshahara?"

"Ahah... wapo. Nina wadogo zangu wa kike wawili. Mmoja yuko Marekani kimasomo, na mwingine yupo huku... yeye ni kula bata tu. Sina ukaribu sana na ndugu wengine wa kiukoo... tuko distant. Ni wadogo zangu tu ndiyo niko in touch nao mara kwa mara," Nora akasema.

Lexi alikuwa anataka kuuliza kuhusu baba yake Nora, lakini akaona akaushe tu kwanza.

"Lakini life ya kujitenga unaonekana kuishikisha sana mizizi. Hawawezi kuona kama vile dada hatupendi?"

"Ahahah... hapana. Nawapenda wadogo zangu. Ila, kwa mambo mengi wanayofanya... mara nyingi yanawaleteaga hasara, na mimi nakuwa sitaki kujiingiza huko, si unaelewa? Wanapenda kujiachia sana na kutupa pesa mpaka inakuwa too much. Me nakuwa tu bize kuwasaidia wasije kufanya mambo yatakayosababisha wafungwe au hata wafe," akasema Nora.

Lexi akashusha pumzi na kusema, "Yeah, hata mimi ilikuwa hivyo na baadhi ya rafiki zangu tulipokuwa tunafanya kazi kwenye gereji ya mjomba wangu. Me ndo' nikawa kama mama yao pale."

"Subiri, wewe unafanyaga nini kwenye gereji ya mjomba wako?" Nora akauliza.

"Nafanyaga kazi, mezani, ku-order part za magari na kuhudumia wateja; wakati mwingine nashughulikiaga magari pia kama panakuwa pamejaa wateja."

"Basi me nikafikiri labda wewe mtoto wa boss tu unakaa na kuletewa kila kitu... yaani hauhitaji kufanya kazi," akasema Nora.

"Ahahah... naonekana wa kishua sana eeh?"

"Sana..."

"Well... hivyo ndivyo vitu nilivyofanya; na kuhakikisha familia inakaa kwa amani na kusaidia biashara isife..." Lexi akasema, akimaanishia wenzake kwa njia ya fumbo.

"Kumbe... okay. Nafurahi umeniambia hayo kuhusu wewe. Napendezwa na wewe zaidi sasa kama rafiki..."

"Wow! Unaniona kama rafiki sasa hivi?" Lexi akauliza kichokozi.

"Naapa kabisa kwamba kuanzia sasa sisi ni marafiki, siyo kwamba pombe imenichanganya," Nora akatania.

Lexi akacheka kidogo. Baada ya kutazama baharini kwa ufupi, akamuuliza, "Hivi ni kitu gani kuhusu huku Sea House kinachokufanya uonekane kuwa mtu tofauti sana?"

"Tofauti kivipi?"

"Tofauti na mapolisi wengine ambao nimeshawahi kukutana nao yaani..."

"Mmm... kila mtu nayefahamiana naye hapo ni kama familia. Unajua, niliwahi kuzimia hapa karibu kabisa na bahari, lakini badala ya kujikuta naelea kwenye maji bila nguo, kuna watu walinichukua na kunipeleka ndani na kunifunika na blanket kabisa... akiwemo Emmanuela. Kwa hiyo... ahah... samahani, sijui hata kwa nini naongelea hilo, naonekana kilaza kweli..." Nora akasema kwa haya kiasi.

Lexi akatambua kuwa sasa mwanamke huyu angalau alikuwa kamzoea sana.

"Hamna, wala hata. Nimeshakuchunguza mheshimiwa na, siyo kwamba tu unakuwa na furaha ukilewa, ila unapendeka kwa kukuangalia tu," Lexi akatania.

"What! Lini uliniona nimelewa?" Nora akauliza.

Lexi akacheka na kusema, "Ni siri yangu!"

Nora akatabasamu na kusema, "Haya bwana, asante. Point ni kwamba, watu kadhaa hapo House wananijua mimi kama Nora, na siyo kuniona kama Kamishna tu. Ni kama ndo' kwetu vile."

"Inaonekana kama unataka kuja kuishi sehemu ya namna hii siku moja..."

"Ndiyo, labda miaka michache baadae. Nimejipangia ku-retire nikifikisha miaka 40, hata niiuze na nyumba yangu kabisa, ili baada ya hapo niishi maisha niliyotamani kutokea zamani..."

"Ya kujiachia..."

"Ahahah... unaweza ukasema hivyo..."

Lexi alipendezwa sana na mtazamo wa Nora. Alianza kuvutiwa naye hata zaidi, kiasi kwamba ikabidi aangalie pembeni kwa kukumbuka kuwa hakupaswa kujiachia sana kwa mwanamke huyu huku akijua kwenye upande wa maadui wao, yeye pia alikuwemo.

"Nimefurahi sana pia kujua hayo kuhusu wewe," akasema Lexi.

Nora akatabasamu.

Kisha Lexi akataka kuichukua chupa ya wine chini ili aongeze, lakini kwa tukio baya akaipiga kwa vidole nayo ikaanguka na kuanza kumwaga kinywaji. Akanyoosha mkono wake ili aiokote upesi, na hiyo ikafanya nguo yake ivutike sehemu iliyofunika mpaka mwanzo wa kiganja chake, na hapo Nora akaona jambo fulani. Lexi hakutambua na kuiokota tu chupa haraka, kisha akamwangalia Nora na kukuta anamwangalia kwa umakini.

"Vipi? Unawaza kuniponda na ndala kisa share yako ya wine imemwagika?" Lexi akauliza kiutani.

"Hizo ni tattoo?" Nora akauliza.

Tabasamu la Lexi likafifia, kisha kwa haraka akaivuta sehemu ile ya nguo ili kuficha.

"Aam... yeah. Nilichoraga zamani... kama kupaka tu yna... hahah..." akasema na kuanza kumimina wine kwenye kikombe.

"Zinaonekana vizuri sana. Ulizichorea wapi?"

"Ni rafiki ya... mjomba wangu ndiyo alinichora. Nikuongeze wine?"

"Hapana, asante. Naweza kuziangalia?"

"Oh, wala usijisumbue... siyo hata nzuri, wala muhimu. Okay. Mmm... you're missing out. Ijapokuwa wine imemwagika lakini ladha bado ni tamu... na mchanga tu kidogo," Lexi akajitahidi kubadili mada.

Nora akatabasamu na kuangalia chini.

"Lakini kama umefikiria kuja kuishi sehemu kama ya namna hii, vipi Mr. Right wa baadae akikataa? Akitaka mjenge state kama Illinois hivi utafanyaje?" Lexi akauliza.

"Ikiwa haupendi niangalie tattoo zako haina shida Lexi. Kila mtu ana siri zake," Nora akamwambia kiustaarabu.

Lexi akamtazama tu kwa umakini, naye Nora akaangalia muda kwenye simu yake.

"Asante Lexi kwa company yako. Nimefurahi kukuona leo," Nora akamwambia.

"Mimi pia mheshimiwa," Lexi akajibu.

Nora akatabasamu na kusema, "Naomba namba yako tafadhali. Tutakuwa tuna..."

"Tunachekiana... fresh kabisa. Ni vizuri kuwa na rafiki polisi... sasa hivi wanaonionea watanitambua," Lexi akasema.

Nora akacheka huku akimpa simu, naye Lexi akampatia namba yake. Baada ya Nora kujaribu kuipigia, simu aliyokuwa nayo Lexi hapo ikaita, naye akamwambia angeitunza yake pia. Nora akanyanyuka.

"Nahitaji kukimbia sasa. Wewe bado upo?" Nora akauliza.

"Ndiyo, ila sina muda mrefu nitaondoka pia..."

"Okay..."

Nora akabaki kumtazama tu Lexi kama anataka kusema kitu kingine, huku Lexi akimwangalia pia kwa njia ya kawaida.

"Okay... usiku mwema," Nora akasema kiajabu-ajabu.

"Kwako pia mheshimiwa rafiki," Lexi akamwambia.

Nora akatabasamu na kuanza kuondoka tu. Mara kwa mara angegeuka nyuma kumwangalia Lexi na kukuta bado anamtazama pia huku anatabasamu, na Lexi akampungia mkono wa kwa heri.

Baada ya Nora kuondoka, Lexi akabaki kutafakari mambo yote yaliyotokea hapo. Alijilaumu kiasi kwa sababu ni kama alikuwa anapoteza muda wake kupiga story na Nora badala ya kutafuta njia ya kunyonya taarifa kutoka kwake zenye umuhimu kwa timu yao. Ilikuwa wazi sasa kwamba alipendezwa na utu wa Nora, kwa kuwa alijionea jinsi mwanamke huyu alivyokuwa mnyoofu kwa kadiri kubwa. Lakini Lexi akajiahidi kuwa imara zaidi wakati mwingine, hasa kwa kuwa Nora mwenyewe aliomba namba yake, hivyo njia zingekuwa nyingi za kupata taarifa za nyendo zao.

Simu hii ambayo alimpatia namba Nora, aliitumia kwa mawasiliano ya kawaida katika "maisha ya kawaida" ambayo yeye na kundi lake waliishi ili kutojulikana. Hangewasiliana na wenzake kupitia simu hii, bali wote walikuwa na vifaa vingine maalumu walivyotumia kuwasiliana ambavyo viliunganishwa moja kwa moja na Torres kwa ajili ya kupeana taarifa muhimu. Lakini kama ni namba za simu za kawaida walizotumia, kila mtu alikuwa nazo, ila wangechekiana tu kwa jumbe fupi ambazo hazingekuwa na nuksi yoyote ile ili kuzuia kutambulika.

Walikuwa makini sana hawa watu, lakini sikuzote huwa hakuna uhakika wa kujua ni wakati gani mambo yangekuja kuharibika, na kwa Mess Makers, hilo halingechukua muda mrefu.


★★


Nora aliporudi kwenye chumba cha hoteli alikokaa, alianza tena kupitia mafaili ya wafanyakazi waliojeruhiwa wa makao ya benki kuu. Alijua kwamba wafanyakazi wengi wa pale walishikiliwa kwa muda fulani baada ya tukio lile la wizi kwa ajili ya mahojiano, na matokeo yalikuja kwamba hakuna hata mmoja aliyejua kilichotokea kwa sababu baada ya mabomu yale kulipuka, wengi walikimbia kuokoa uhai wao, isipokuwa labda wale waliojeruhiwa ndani huko.

Nora akaanza kupitia taarifa za wale waliojeruhiwa, nao walikuwa ni watu 11 tu; wanaume saba, wanawake wanne. Tokea mwanzo ilisemwa tu kwamba waliojeruhiwa walikuwa wengi sana, lakini namba hii ilikuwa ndogo kulinganisha na "wengi sana." Hakukuwa na mambo mengi kwenye mafaili hayo kama alivyotarajia, hivyo akatafuta rekodi za watu hao waliojeruhiwa kwenye laptop yake, lakini kwa sababu fulani zikawa zimefungiwa.

Hii ilimshangaza kiasi. Ni kwa nini taarifa za watu hao zilifungiwa? Alitaka sana kujua ili kuipa nguvu kauli yake ya mara ya kwanza kwamba wezi wale walitoka kwa kujifanya wamejeruhiwa, kwa sababu ambulance zilizofika kuwachukua walioumia zilirudi hospitalini pungufu ya moja. Alitaka kujua kwenye ambulance iliyotokomea ni wafanyakazi gani WALIOTAKIWA kuwa mule, kwa sababu isingepatana na akili kwamba hawakufika hospitalini halafu waje kudai kuwa siku hiyo walikuwepo kazini. Aliwaza huenda kati ya wafanyakazi waliojeruhiwa, wale waliotoroka kwa kujifanya wamejeruhiwa ndiyo walikuwa wezi waliofanya jambo fulani kuwaziba mdomo wafanyakazi halisi wa hapo ili kufanikisha mipango yao.

Wazo la kwamba huenda hata ni baadhi ya watu wa hapo hapo ndiyo walifanya mpango wa kuiba pesa hizo kijanja halikuwa mbali na akili yake, na labda ndiyo sababu zilipita siku mbili kabisa baada ya wizi huo pakiwa kimya, na waandishi wa habari kuzuiwa kufika huko ili kuficha yaliyoendelea pale, ambayo ndiyo yaliyozusha utata mkubwa wa suala hili lote. Yeye alitakiwa tu kusaidia kuwakamata wezi, sawa, lakini alitaka kujua anamkamata nani hasa. Mambo yote yalionekana kuzama kwenye suala zito mno zaidi hata ya ugaidi.

Kwa hiyo akaamua kwamba angemjulisha Luteni Michael kesho ili amsaidie kupata taarifa hizo bila kuhusisha mtu mwingine zaidi ya timu yake, wapate taarifa alizohitaji, kisha wachimbe zaidi ili kupata ukweli. Akaingia kujipumzisha tu baada ya hapo.


★★★★


Asubuhi na mapema ACP Nora akawa amefika kwenye jengo lile na kuikuta timu yote ya Luteni Michael ikiwepo. Wakamsalimu na kumkaribisha vizuri, nao wakamwambia kuhusu njia kadhaa ambazo wamejaribu kufanya ili kupata chochote kutokana na uchunguzi wao wa mara nyingine tena wa kampuni zile za madini bila mafanikio yoyote, kwa sababu hawakupata kiashiria chochote chenye kuwaongoza kwa Mess Makers.

Nora bila kuchelewa akaweka wazo lake jipya mezani. Baada ya kuwajulisha kuhusu uchunguzi wake, wote waliona kweli hapo katikati kulikuwa na nuksi, lakini baadhi wakasema inaonekana taarifa hizo zimefichwa kwa sababu fulani ambazo hazikuwahusu wao, kwamba wenyewe walitakiwa tu kukamilisha "mission" waliyopewa. Ijapokuwa hata Luteni Michael kipindi cha nyuma alikuwa na mtazamo huo, sasa akasema kwamba wazo alilotoa Nora kweli lingetakiwa kufanyiwa kazi, kwa kuwa muda ulikuwa unasonga na walihitaji kutafuta kila njia ya kupata matokeo mazuri. Akawakumbusha kuhusu jinsi mara ya kwanza Nora alivyotumia hekima kutambua Kevin Dass alijifanya kichaa mpaka wakamkamata, hivyo hata kwa hili akaunga mkono kwa sababu aliheshimu kipawa chake katika kuona mambo kwa njia pana. Nora akafurahi baada ya kuona Luteni Michael alibadili mtazamo wake, naye akamshukuru kwa hilo.

Basi baada ya kukubaliana, upesi Bobby akaingia kwenye kompyuta na kuanza yake ili kuzipata taarifa zilizofichwa. Baada ya dakika mbili za kubofya hapa na pale kwenye "keyboard" huku screen ikileta taarifa za mambo kadhaa, akasitisha zoezi hilo na kubaki ameitazama tu kompyuta.

"Vipi mzee?" akauliza Omari.

"Luteni... hizo taarifa zimefichwa kwenye database za Ikulu," Bobby akasema.

"Nini?" Luteni Michael akashangaa.

"Kwa nini?" Mario akauliza.

"Me nitajuaje sasa? Nenda ka-date na mmoja wa ma-IT wa huko atakwambia," Bobby akamwambia Mario.

Nora akatazamana na Luteni Michael kimaswali.

"Ina maana... yaani watu kujeruhiwa tu ndiyo taarifa zinafi... hapana... hii harufu mbaya siyo ya panya aliyekufa, ni mzoga mkubwa sana umefichwa," Alex akasema kitamathali.

"Ingia sasa uziangalie," Mishashi akamwambia Bobby.

"Acha bangi kaka. Wakigundua nimeingia na kuiba hizo info, sisi wote hatuna kazi hapa. Ni kama unaniambia ni-hack Ikulu mzee," akasema Bobby.

"Dead end kwa hiyo? Tunafanya nini sasa Luteni?" akauliza Alex.

Luteni Michael bado akawa anaangaliana na Nora, akiona jinsi mwanamke huyu alivyotaka sana afanye uamuzi ambao huenda ungewaletea shida. Lakini kiukweli hata yeye alitaka sana kujua ni nini kiliendelea mpaka taarifa hizo kufichwa Ikulu, hivyo akaamua kuuchukua huo huo uamuzi.

"Bobby... ingia," Luteni Michael akasema.

"Nini?!" Bobby akashangaa.

"Umenisikia," Luteni Michael akasema.

"Luteni, nina watoto watano, mmoja ni mlemavu, na...."

"Do it!" Luteni Michael akamkatisha Bobby.

Bobby hakuwa na jinsi ila kutii tu japo kishingo upande, naye akaingia kwa njia ya marufuku ili kupata taarifa hizo. Alifanya mambo chap chap na kufanikiwa kuipata orodha ya wafanyakazi wale waliopelekwa hospitali siku hiyo, kisha akatambua kwamba ma-IT wa ikulu walimgundua na kuanza kumzibia njia.

"Shit!"

Bobby akatamka hivyo na kufungia kila kitu haraka ili wasifanikiwe kumpata, ingawa alielewa kwamba hicho ni kitu ambacho hakingewashinda. Uzuri ni kuwa tayari alikuwa ame-copy orodha hiyo, naye akairusha moja kwa moja kwenye tablet (kama simu) nyingine.

"Luteni, kazi yangu..." Bobby akasema.

"Usijali Bobby kuhusu hilo, nita-handle mimi. Mpe ACP aangalie," Luteni Michael akamwambia.

Bobby akampatia Nora taarifa zile, naye akaanza kuzipitia.

"Okay, so genius wetu, unaona nini hapo?" akauliza Hussein.

"Walitakiwa kuwa 11, lakini ni 9 tu ndiyo waliofika hospitalini," Nora akasema.

"Nini? Kwa hiyo inamaanisha nini?" akauliza Vedastus.

"Inamaanisha kati ya hao, wawili ndiyo wezi wetu!" Mishashi akamwambia.

"Siyo uhakika Misha. Nafikiri kuna kitu hawa Mess Makers walifanya ili wenyewe ndiyo waingie kazini sehemu ya hawa wawili siku hiyo... ila sijajua ni jinsi gani," Nora akasema.

"Majina?" Luteni Michael akauliza.

"Nathan Masunga... na Eunice Shirima," Nora akasema.

"Bobby, tafuta waliko hawa," Luteni akasema.

Bobby akaanza kuwasaka upesi, naye akafanikiwa kupata anwani zao.

"Luteni nimewapata. Lakini, huyu Shirima amekufa," Bobby akasema.

"Tokea lini?" akauliza Luteni Michael.

"Ana kama wiki sasa. Tena siku nne baada ya wizi," Bobby akasema.

"Harufu ya huo mzoga bado inaingia vizuri puani mwako?" Hussein akamuuliza Alex kiutani.

Alex akamwonyeshea dole la kati.

"Kwa hiyo ni kusema kwamba hawa Mess Makers ndiyo wamemuua au?" akauliza Vedastus.

"Amekufa vipi?" akauliza Nora.

"Aliumwa. Kifua. Ndiyo ilivyoandikwa," Bobby akasema.

"Huo msiba basi ulifanywa kimya kimya sana aisee, maana haujasikika popote," Mario akasema.

"Kama kweli angekuwa mmoja wa majeruhi wa bomu, basi mpaka muda huo angekuwa hospitali labda. Na lazima tu kifo chake kingetangazwa. Lakini prrrrr... Ikulu," Omari akasema.

"Vipi kuhusu Nathan?" akauliza Mishashi.

"Yupo. Yupo maeneo siyo mbali na Kivukoni. Bado anasomeka kama mfanyakazi mwaminifu, lakini kwa sasa haendi kazini maana alivunjika mguu kwenye bomu," Bobby akasema.

"Kwa hiyo, unasema kwamba hatoki nyumbani?" akauliza Luteni Michael.

"Ndiyo inavyoonekana," Bobby akajibu.

"Nipe address yake haraka. Veda, Omari, Hussein, mko nami. Tunamfata huyo pimbi. Mario, Omari, nendeni na ACP pande za huyo Shirima mwangalie kama kuna nuksi zingine huko. Bobby, usiache kutupa touch zozote mpya," Luteni Michael akanena.

"Luteni, usisahau kuhusu ka-hacking nilikotoka kufanya hapa..."

Bobby akawa anamkumbusha kuhusu hilo huku tayari Luteni Michael akiwa ameanza kuondoka na wengine. Nora akamshukuru Bobby kwa kazi nzuri, kisha naye akaelekea nje kwa wengine ili kwenda walipoambiwa.

★★

Iliwachukua kama nusu saa kwa ACP Nora na wenzake kufika maeneo alikoishi Eunice Shirima kutokana na msongamano wa magari barabarani. Walipata kuwaona baadhi ya watu wa familia yake, ikiwemo mkane aliyemwacha na watoto watatu. Waliongea na mwanaume huyu ambaye aliwaeleza kwamba mke wake alikufa siku chache baada ya kujeruhiwa vibaya kwenye bomu lile, naye alizikwa kule kwao Arusha. Walimuuliza ikiwa alikwenda hospitali kumwona, na kama alimwona, lakini akasema ijapokuwa alijaribu, hakuweza kabisa kumwona mpaka alipopewa taarifa kwamba alipoteza maisha kutokana na mapafu yake kuingiwa na moshi mwingi.

Nora aliweza kugundua kwamba mwanaume huyo aliongea mambo ambayo ALIDHANI ni kweli kabisa, kwa hiyo akaamua tu kuwaambia wenzake wamwache kwa sababu kwa hapo hawangepata jambo lolote lenye nuksi, hasa kwa kuwa mkane huyu alionekana kuwa mwenye huzuni bado.

Upande wa Luteni Michael, akiwa amesindikizwa na Vedastus, Omari na Hussein, alifanikiwa kufika mpaka kwenye nyumba waliyoitambua kuwa ya Nathan Masunga. Ilikuwa kubwa kiasi yenye uzio wa kuta kuizunguka, nao wakafika getini na kugonga mlango mdogo wa geti hilo. Wakaendelea kuligonga bila kujibiwa kwa dakika mbili zaidi, ndipo likafunguliwa.

Wote wakashangaa baada ya kumwona mwanaume huyo ambaye walijua wazi ni Nathan Masunga mwenyewe. Alikuwa nzima kabisa, akisimama vizuri, bila kuonekana na kitu chochote kilichoashiria kwamba mguu wake ulikuwa umevunjika. Cha ajabu hata zaidi baada tu ya kuwaona wanajeshi hawa, mwanaume huyo akafunga mlango wa geti upesi, lakini Vedastus akawahi na kuanza kubishana naye kuusukuma ili asiufunge kwa ndani, ila Nathan akafanikiwa kuufunga.

Sasa nuksi wakawa wameipata huku.



★★★★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★★★★


Usikose mwendelezo wa simulizi hii kali ya FOR YOU. Njoo WhatsApp for the full season, bei kwa kila msimu ni nafuu. Karibu.

WHATSAPP +255 787 604 893
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…