Simulizi: For You

Simulizi: For You

FOR YOU

Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Uhalifu, Mauaji, Visasi, Vita, Mambo yasiyotazamiwa

Rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA NANE

★★★★★★★★★★★★★

"Sandra... uko ndani ya mwili wangu?" Xander akauliza.

"Na wewe uko ndani ya wa kwangu! Eh Mungu, nina besi!" Sandra akasema kwa kustaajabisha.

"Sandra... nini kimetokea?"

"Sijui. Sijui. Si... sijui. Nimekuja jana humu... umenifanya nini Xander?"

"Sijakufanya chochote Sandra..."

"Oh God... hii haiwezekani. Ooooh my God!"

"Nini?"

"Hili dude lako limevimba!"

"Sandra usijali hiyo ni kawaida tu. Itaisha baada ya muda..."

"Hapana hii haiwezekani. Nini kimetokea Xander? Nini, nini... nini..."

Xander, akiwa ndani ya mwili wa Sandra, akamshika Sandra mabegani, akiwa ndani ya mwili "wake."

"Sandra calm down..."

"Calm down?"

"Nisikilize mdoli..."

"Unawezaje kuniita mdoli wakati nina lisura lako hapa!"

"Tunafanana bwana! Tulia. Shit... nina sauti ya kike! Kuna vitu huku chini vinaniwashawasha hata sielewi ni nini... kwa hiyo siyo wewe tu ambaye umeshtushwa na hili. Lakini tunahitaji kutulia ili kujua tunalitatuaje... tafadhali Sandra..." Xander akamwambia.

"Sandra" akaanza kutulia.

"Okay. Niko calm. Now what?" Sandra akauliza.

"Okay aam... jana umekuja hapa usiku... mvua kubwa ilikuwa inanyesha. Ukalala nyuma yangu... nini baada ya hapo?"

"Sijui! Ndiyo unaniamsha sasa hivi najikuta hivi. Xander tunafanyaje?"

"Usijali. Tutajua tu. Tutatafuta njia. Labda... labda tutaonana na daktari... au... sijui ikiwa itakuwa sawa kuwaambia mama na baba..."

"Watashangaa!"

"Na sijui kama hata watatuamini..."

"Kuna mtu ametufanyia uchawi Xander. Hii kitu hai-make sense!"

"Ni lazima tujue shida ni nini. Labda hatukutakiwa kulala pamoja..."

"Xander mara ngapi tumelala pamoja na hii haijawahi kutokea?"

Xander akashusha pumzi.

"Tunafanyaje? Mama na wengine hawataelewa maana hata na sisi hatuelewi. Kwa hiyo... sasa hivi nitapaswa tu kuwa wewe?" Sandra akauliza.

"Ndiyo..." Xander akajibu kiupole.

"Nini?!" Sandra akashangaa.

"Ndiyo. Itapaswa kuwa hivyo Sandra. Aisee! Sasa hivi nitapaswa kuwa nakuita Xander..."

"Eeh Mungu!"

"Usijali. We'll figure this out. Nahitaji umakini wako," akasema Xander.

"Sawa. Niambie."

"Okay. Kwa hiyo... nataka tu-test vitu fulani... kama nguvu... kumbukumbu na mambo mengine..."

"Kwa nguvu... mimi sasa hivi nina mwili wako kwa hiyo... nakubonda si ndiyo?" akasema Sandra.

"Ahahah... yeah. Na mimi sa'hivi najua kuchamba eeh?" Xander akamwambia kimaringo.

"Ahah... mimi sifanyagi hayo bwana. Lakini Xander, vipi kuhusu hiki kitu... nafanyaje... sitakiwi kuona dude lako wala kuligusa... yuck!" Sandra akasema.

Xander akacheka kidogo, kisha akamwambia, "Haina jinsi. We jisikie huru tu maana utapaswa kuoga nalo."

Sandra, akiwa ndani ya mwili huu wa kaka yake akaivuta kaptura nyepesi aliyovaa na kujiangalia.

"Eh Mungu! Ndiyo likubwa hivyo?"

"Ahahahah... asante. Hiyo hapo dada ni sifa kwangu..."

"Kwa hiyo... naenda kuoga... nafanya kila kitu nikiwa na mwili wako... na wewe je?" Sandra akauliza.

"Na mimi vice versa. Eheh... naenda chumbani kwako kuucheki mwili wangu mpya... heheheee!" Xander akasema kimasihara.

"Xander nakuonya! Usifanye jambo lolote lile la kipumbavu kwenye mwili wangu! Ukioga fumba macho, ukitaka kuvaa fumba macho, usijiangalie kwenye kioo, usishike nguo zangu za ndani, na ole wako... ooole wako umpe mjinga yoyote almasi yangu!" Sandra akamwonya.

Xander akabaki anamshangaa tu.

"Mimi sijakupa hayo masheria yote, mbona wewe unaniandama hivyo? Me sitaakiii..." Xander akaongea kwa deko eti kama mtoto wa kike kweli.

"Alexander..." Sandra akamwonyesha yuko 'serious.'

"Okay, okay usijali. Nitaulinda mwili wako. Ila kufanya hayo yote kwa njia hiyo ni ngumu. Hatuna jinsi dada yangu. Itabidi tu uniamini kama mimi navyokuamini. Usisahau... for me... for you," Xander akasema.

Sandra akabaki kumtazama tu. Xander akamshika kiganja.

"Come on say it..." akambembeleza.

Sandra akashusha pumzi, kisha akasema, "For me... for you..."

Xander sasa akiwa ndani ya mwili wa dada yake, akanyanyuka na kusimama chini. Akawa anajicheka jinsi alivyoonekana, huku Sandra naye akijiangalia pale kitandani. Kisha Xander akageuka na kuanza kutembea kimadoido kama mwanamitindo mpaka mlangoni, na alipoufikia akamgeukia "dada yake" kukuta anatikisa kichwa chake kwa kusikitika. Akaona atoke tu ndani ya chumba "chake" hiki na kuelekea kwenye chumba "chake" cha sasa. Ilikuwa ni hali moja ambayo ilifaa kupewa jina la kizungumkuti.

Xander alipofika kwenye chumba cha Sandra, akaelekea mpaka kwenye kioo na kujiangalia. Sura ya dada yake ilifanana na yake, lakini aliiona kuwa nzuri zaidi. Akatabasamu, kisha akavua T-shirt alilokuwa nalo mwilini. Kwa mara ya kwanza akayaona matiti ya dada yake, nayo yalikuwa yametuna vyema. Akaanza kuyashika na kuyavutavuta huku akicheka, lakini kadiri alivyoendelea alianza kupata hisi fulani mwilini "mwake," na kukawa na hisia kama za mtetemo fulani wenye kusisimua zilizoelekea kwenye almasi "yake."

Ijapokuwa hisia hizi zilikuwa mpya na zenye uajabu kwake, zilimfanya ajihisi vizuri sana. Akashusha kiganja chake kuelekea chini ili ajishike, lakini akili ikamrudia kukumbuka kwamba huu ulikuwa mwili wa dada yake, naye alipaswa kuuheshimu kama tu alivyomwahidi. Akajisahaulisha mambo hayo yote na kuamua kwenda kuoga haraka ili aanze kuuandaa mwili wake mpya kwa ajili ya chuo.

Kwa upande wake Sandra, aliona mambo kuwa magumu sana kuwa ndani ya mwili wa mwanaume. Hakuzoea kabisa kuwa na vinyweleo kwapani! Alipojitazama kwenye kioo, aliweza kuona jinsi mwili wa kaka yake ulivyokuwa imara, na aliweza kuhisi jinsi misuli ilivyokuwa na nguvu. Kufikia wakati huu, mashine "yake" ilikuwa imepungua, naye bado hakutaka kuiangalia hata kidogo kwa sababu aliona isingefaa. Ila kama kaka yake alivyomwambia, hakukuwa na jinsi. Kwa hiyo naye akaamua tu kwenda kuoga ili aanze kuuandaa mwili wake mpya kwa ajili ya chuo.

Ilikuwa imefika saa 1 kamili asubuhi sasa. Salome ndiye aliyekuwa akifanya shughuli za ndani baada ya kumwamsha Azra ili ajiandae na shule wakati mapacha wakiwa wanajiandaa vyumbani, naye Alice alikuwa akivuta shuka bado. Baada ya Xander kumaliza kuuandaa mwili wa Sandra vizuri, akaenda kwenye chumba "chake" alikokuwa "dada yake." Aliingia tu na kumkuta akiwa anavaa T-shirt nyeupe na chini suruali ya jeans. Akatabasamu na kumwita, naye Sandra akamwangalia.

"Vipi? Nimependeza?" Xander akamuuliza huku akiweka pozi.

"Xander ndiyo umevaaje hiyo nguo?" Sandra akamshangaa.

Alikuwa amevaa kigauni chekundu kilichombana na kuishia magotini, lakini alikuwa amegeuza.

"Kwani vipi?" Xander akauliza.

"Umeigeuza hiyo nguo..."

"Nimei... aagh... yaani nguo zenu zinachanganya kweli..."

"Kwa hiyo kama nisingekuona ungeenda chuo hivyo hivyo?"

"Ahahah... ningeweka historia leo. Lakini ingekuwa ni WEWE..."

"Acha masihara Xander, em' vua uvae nyingine..."

"Nyingine? Si naweza tu kuigeuza hii?"

"Leo nilikuwa nataka kuvaa suruali..."

"Kwani hapo umevaa sketi?"

"Namaanisha kwenye mwili wangu!"

"Ahahahah..."

"Unazingua Xander. Nenda kabadilishe."

Xander akamsogelea.

"Una mwili mzuri Sandra. Lakini kiukweli, nakuwa napata shida nikiuangalia. Ni ajabu yaani. Ni mwili 'wangu,' lakini ni 'wako.' Wewe ndiyo mmiliki halisi na haipaswi kuwa hivi..." Xander akawa anamwambia kiustaarabu.

"Ninaelewa unavyohisi. Hata mimi siko comfortable kwa kweli. Kukojoa nimesimama ni ngumu mno," akasema Sandra.

"Ahah... jaribu kuchuchumaa ndo' utaona!" Xander akasema.

"Yaani sijui itakuwaje. Wengine hapa nyumbani, wanachuo wenzetu na marafiki... walimu..."

"Inaonekana ni ubongo... akili zetu ndiyo zime-switch kwenye miili yetu... lakini kumbukumbu zetu bado zipo. Hatuna njia nyingine ila kufekisha tu tabia. Me nijifanye ndiyo wewe, na wewe ujifanye ndiyo..."

"Najua. Lakini Xander haitakuwa rahisi. Kuna vitu hatutaweza ku-control. Marafiki zangu sa'hivi watapaswa kuwa wako. Unajua vitu wanavyopenda kufanya? Hujui! Na mimi ndiyo hivyo hivyo. Sitaelewa lugha ya 'washkaji' zako wakianza kunisemesha. Halafu... eh Mungu wangu!" Sandra akasema akiziba mdomo.

"Nini?"

"Mashindano ya kuogelea! Xander mashindano ya kuogelea! Oh God what am I going to do?"

"Sandra relax. Nitaogelea, kwani shida ni nini?"

"Usifikiri ni rahisi tu au huwa ni ovyo ovyo tu. Kuna technique tunatumia. Kujua wakati wa kuruka, wakati wa kujigeuza, wakati wa kunyoosha mikono... wewe haujajifunza hayo na hauna faida ya misuli unayotumiaga kujua jinsi mwili wangu unavyofanya ka... oh my God! Jamani nilikuwa nimeji... wenzangu wananitegemea..."

Sandra, akiwa kwenye mwili wa kaka yake akawa anaongea hivyo huku analia. Xander alimwonea huruma, lakini mambo haya yote yalimshangaza. Akamsogelea karibu na kumshika mabegani.

"Sandra, kama nilivyokwambia, tutajua la kufanya. Kwanza kabisa, itabidi tutatue hili kabla ya siku ya competition. Na pili... usiwe unalialia ukiwa ndani ya mwili wangu. Watu watakuwa wanakushangaa maana watafikiri ni mimi..." Xander akamwambia.

"Sawa. Samahani," Sandra akafuta machozi.

"Ngoja tu tupitishe siku ya leo chuoni kwa njia hii. Muda wote tutapaswa kuwa pamoja... ili kuepuka zari za kushtukiza. Tukirudi tujipange vizuri zaidi," Xander akamwambia.

Sandra akatikisa kichwa kuonyesha ameelewa.

Hali hii bado ilikuwa inampa shida sana Sandra, ambaye sasa alikuwa dume. Xander akavua kigauni hicho alichovaa na kukigeuza ili akivae vizuri. Akamtania kwamba mwili wake ulikuwa unauangalia wa dada yake ukivua nguo, lakini kihalisi alikuwa anajiangalia yeye mwenyewe. Mambo yalikuwa yanachanganya sana. Baada ya kumaliza kujitengeneza vyema, mapacha wakatoka pamoja kuelekea chini ili kuondoka.

Walipofika sebuleni walimkuta Salome akiwa anasafisha meza ya chakula sehemu ya 'dining,' nao wakamsalimu.

"Azra ameshaondoka?" Sandra, akiwa kwenye mwili wa Xander, akamuuliza Salome.

"Ndiyo ameshaenda. Mama bado amelala," Salome akajibu.

"Aaaa sawa..." Sandra akasema.

"Mvua ya jana haijaangusha miti huko nje kweli?" Xander, akiwa kwenye mwili wa Sandra, akauliza.

"Mh! Kale kamvua ndiyo kakuangusha mti?" Salome akauliza pia.

"Kamvua? Ilikuwa dhoruba! Niliogopa sana jana!" Sandra akasema akionekana kama Xander.

"Ahahah... hakukuwa na mvua jana bwana. Ilinyesha kidogo tu na hata baadae usiku nilipoamka sikuisikia tena," Salome akawaambia.

Mapacha wakatazamana kimaswali. Wakahisi labda Salome alikuwa amelala fofofo mno, hivyo labda hakuisikia dhoruba ya jana. Wakaona wamuage tu, kisha wakatoka nje.

Sandra alishukuru kwamba Xander aliwahi kumfundisha kuendesha pikipiki, la sivyo asingeweza kuiendesha akiwa kwenye mwili wa kaka yake. Wakapanda pamoja, Xander akiwa kwa nyuma na kufanya kama amemkumbatia dada yake ndani ya mwili "wake" kiutundu, kisha wakaondoka ili kuelekea chuoni.

★★★

NYUMBANI KWAO ISIMINZILE

Asubuhi hii Isiminzile aliamka mapema kama kawaida na kumaliza kujiandaa kwa ajili ya chuo. Ni wakati alipokuwa anatoka ili aondoke, pale alipovutwa mkono kwa nguvu. Alipomwangalia aliyemvuta akatambua ilikuwa ni bibi yake, naye akamzungusha mpaka nyuma ya nyumba yao ili waongee. Bibi yake alikuwa anamtazama kwa njia ya kimaswali, huku yeye Isiminzile akionyesha hofu.

"Wewe kichwa chako kina nini? Eeh?" bibi yake akauliza.

"Sh'kamoo bibi..."

"Sihitaji salamu yako. Juzi umekuja hujasema lolote. Jana ukanipita tu tena, halafu na leo unataka kunikwepa. Ndiyo makubaliano yetu yalivyokuwa?"

"Hapana bibi... nisamehe..."

"A-aagh... nataka uniambie kilichotokea. Kwa nini sijaona mabadiliko yoyote? Kwa nini unanikwepa? Huendi chuo mpaka useme la sivyo utanitambua!"

Isiminzile akawa anaangalia mara chini, mara juu, mara huku na kule, kwa wasiwasi tu. Hakujua aanze vipi kumwambia bibi yake jambo hili.

"Kwa hiyo? Naongea na bubu?" bibi akamshurutisha.

"Bibi... nisamehe sana... nisamehe bibi..."

"Kwa nini nikusamehe? Umefanyaje?"

"Sikufanikiwa..." akasema Isiminzile huku ameangalia chini.

"Hukufanikiwa? Kwa hiyo bado hujampa? Unaogopa? Basi kama ni hivyo nirudishie kitu yangu, sitaki ujinga mimi," bibi akamwambia.

"Hapana bibi. Nilijaribu... nilifanya vile ila... mambo yakaharibika!"

"NINI?!" bibi akashangaa.

Isiminzile akabaki tu kimya huku mapigo yake ya moyo yakikimbia sana.

"Yameharibikaje? Sema!" bibi akasema kiukali, lakini kwa sauti ya chini.

"Hakuinywa yule... walikunywa wengine!" Isiminzile akasema.

"Toba!" bibi akashangaa.

"Nisamehe bibi... mimi siku..."

Bibi yake akamtandika kofi la kichwani kwa nguvu. Isiminzile akajishika kichwa akihisi maumivu na hofu kubwa.

"Una akili wewe? Hivi una... una akili wewe?!" bibi akasema kwa hisia kali.

"Sikutarajia bibi..."

"Naomba useme nilikwambia nini, na wewe ukafanya nini. Sema..." bibi akamwambia.

"Uliniambia... ulinipa hiyo dawa ukasema niiweke kwenye soda moja..."

"Enhe..."

"... halafu niigawanyishe kwenye vikombe viwili, nimpe kwa mkono wa kushoto... akishakunywa tu, na mimi ninywe..."

"Ndiyo. Wewe ulifanya nini?"

"Nilifanya hivyo bibi. Alikunywa ila nilivyotaka tu kunywa yangu... pacha wake akaichukua na kuinywa yeye! Sikutegemea yaani...."

"Pacha wake? Huyo mkaka ana pacha?" bibi akauliza.

Isiminzile akabaki kumtazama tu.

"Huyo nanilii... Meki sijui... si ni wa pale juu? Toka lini ana pacha?!" bibi akauliza tena.

Isiminzile akabaki tu kimya.

"Niambie mshenzi wewe! Mimi nimekupa dawa umpe huyo mjinga uliyesema anakusumbua, wewe ukampa nani?" bibi akasema kwa mkazo.

"Ni... Alexander..." Isiminzile akasema kwa sauti ya chini.

"Ndiyo nani?"

"Ni mkaka mwingine wa hapo hapo chuo..."

"Aiyayayai! We mtoto una matatizo gani? Mm? Yaani... mbona hueleweki? Wewe si tulikubaliana unaenda kumpa... niambie nilichokwambia ufanye..."

"Bibi..."

"Sema mpumbavu wewe!"

"Uliniambia nikifanya hivyo... mambo yote ambayo nilikuwa natamani kutoka kwake Mecky yangekuwa yangu. Kila kitu kizuri kilichomfanya apendwe kingekuwa... watu wangekiona kwangu, na hata msichana wake angemwacha na kuja kwangu. Ningekuwa na nguvu zake... na yeye angenyong'onyea na kuonewa kama alivyokuwa ananifanyia..." Isiminzile akasema.

"Vizuri. Sasa nataka uniambie ni mdudu gani aliyekuingia kichwani kwako mpaka ukafanya mambo kinyume..."

"Bibi nisamehe. Ningempa Mecky ndiyo lakini... Xander ndiyo huwa anapendwa zaidi. Ana hela, ana kipaji, anaongea vizuri yaani kila mtu anampenda... hata msichana ninayemtaka anampenda yeye. Kwa hiyo... nikaamua kubadilishana bahati na yeye, siyo Mecky..." Isiminzile akasema.

"Mwana huyu mupuva sana! (Litoto lijinga sana hili!)" bibi yake akasema kwa kikabila huku anazunguka sehemu hiyo.

"Bibi nisamehe... nilikuwa naogopa kukwambia tu. Nisamehe sana..." Isiminzile akasema kwa huzuni.

"Unatenda kama litoto la darasa la pili, nami nilikuona mwerevu kumbe matope tu ndiyo yamejaa kichwani kwako. Haina shida. Maji yakishamwagika hayazoleki. Nenda chuo," bibi akamwambia huku akianza kuondoka.

"Lakini bibi... vipi kuhusu Xander na pacha wake?"

"Vipi kuhusu nyoko na pacha wake! Unaniuliza mimi hivyo nilikutuma umpe huyo mwingine? Utajua mwenyewe. Alaa! Mimi nimekupa msaada ili usiwe mnyonge mnyonge sana wewe ukauchezea! Na tena hata sikutakiwa kukuonyesha njia zetu za haya mambo ila nikakuonea sana huruma... halafu wewe unajikuta mjuaji zaidi. Kwenda huko chuoni na usiniambie matatizo yako tena..." bibi akasema kwa hasira na kusonya, kisha akarudi kwenye nyumba.

Isiminzile akaachwa njia panda. Kwa woga aliokuwa nao alianza hadi kulia. Ni yeye ndiye aliyekuwa chanzo cha hitilafu ile iliyowapata mapacha kupitia kwa bibi yake. Hakujua ni matatizo gani ambayo yangewapata mapacha wale kwa sababu ya ubinafsi wake, akiwaza labda hata wangekufa, na hakujua pia angeshughulika na suala hili namna gani hasa baada ya kumfanya bibi yake amkasirikie sana.

Akavuta tu mkanda wa begi lake mgongoni na kuanza kuondoka, akiwaza mengi mno kichwani kwake.

★★★

Wakiwa bado njiani kuelekea chuoni, mapacha waliongelea kuhusu mahusiano yao kwa wapenzi wao. Sandra alimweka wazi Xander kuhusu Raymond, na kwamba ameshafanya mapenzi pamoja naye mara tatu tokea walipoanza ku-date, naye Xander akamwambia ameshafanya mapenzi mara 394 na Ramla. Sandra akacheka sana, akijua ni jinsi gani mdada yule alivyo na mchecheto, lakini pia kwamba Xander anamtania tu. Kwa kuwa hawakujua hali hii ingeisha lini, wakakubaliana kwamba hawakutakiwa kuifanyisha miili yao mapenzi na yeyote, hata kama waliwaomba kufanya hivyo.

Sandra ndiye aliyesisitiza sana kuhusu hilo kwa sababu alijua Xander ni mkorofi, lakini kaka yake akamhakikishia kuwa mwili wa dada yake kipenzi ungekuwa salama. Katika mazungumzo yao hayo, Xander alisahau kumwambia dada yake kuhusu jambo moja; madam Valentina. Hakumwambia kuhusu kilichoendelea baina yake na mwalimu wao huyo, hivyo akawa hajamweka tayari kwa lolote ambalo lingetokea baina "yake" na madam Valentina.

Walipofika chuoni, wakaegesha pikipiki ndani ya uzio wa jengo sehemu ya kuegeshea, kisha Xander akashuka kutoka kwenye pikipiki (akiwa kwenye mwili wa Sandra), naye akawa eti anajitengeneza-tengeneza na kurembua-rembua kimakusudi tu ili aonekane mrembo sana. Sandra alikuwa mrembo, lakini Xander alizidisha chumvi sana na kuanza kuutembeza mwili wa dada yake kimadoido mno. Sandra akiwa ndani ya mwili wa kaka yake akamwahi na kumshika mkono.

"Xander unafanya nini?" akamuuliza.

"Si ndo' nakuwa wewe au?" akamjibu huku anarembua.

"Naomba usinifanye nikaonekana kituko! Mimi siyo Joti..."

"Ahahaaa... unaloo..."

"Acha... mambo hayo nimekwambia sifanyagi. Kuwa kawaida tu. Ila usiwe 'wewe' sana... na penyewe utaharibu..."

"Nafurahi kuona sasa hivi wewe ndiyo unanipa ushauri, ikimaanisha utanitendea na mimi haki. Just relax... twende tuwahi kipindi..."

"Subiri. Tunahitaji kubadilishana simu," Sandra akamwambia.

"Kwa nini?"

"Kwa sababu tumebadilishwa miili mjinga wewe!"

"Ahahahah mdoli bhana... uko intense kweli badala ufurahie sa'hivi utakuwa unagonga watu..." Xander akamwambia huku anatoa simu kutoka kwenye pochi "yake."

Wakabadilishana simu zao na kuanza kuyaelekea majengo yenye madarasa pamoja. Walitembea kwa ukaribu sana. Xander alikuwa anasalimiana na kila mtu aliyepishana naye huku akijitahidi kuigiza kawaida ya dada yake ya kutembea, naye Sandra alikuwa kimya tu akitembea kawaida. Kipindi cha kwanza ambacho wangeenda kilikuwa ni cha somo la masuala ya tovuti (Web Technology). Kwa kuwa iliwabidi wabadilishane hadi madaftari, ingehitajika waandikiane na mambo muhimu pia waliyojifunza.

Marafiki zao wachache waliokuwepo hapo kabla ya mwalimu kufika, waliwachangamkia kama kawaida. Sophia, rafiki wa karibu zaidi wa Sandra, alipiga naye story nyingi bila kujua anayeongea naye ni Xander. Xander alimchekesha mno kwa maneno mengi yaliyomfanya mpaka Sophia aone ni kama "rafiki" yake amebadilika. Sophia pia alisomea kozi hii waliyosomea mapacha, kutia ndani Lucas, Bernard, Mecky na Hussein. Rafiki za Xander waliona akiwa kimya tu karibia muda wote, asichangie maongezi yao ya kishkaji kabisa. Lakini Sandra akiwa kwa ndani pia alijitahidi kuigiza kama yuko poa tu, kwa hiyo hakukuwa na shida iliyotokea, nao wakaendelea kumsubiri mwalimu.

(Note: Nitawaelezea mapacha hawa waliobadilishwa miili kwa njia hii fupi: Nikiandika "Xander (Sandra)" hiyo inamaanisha kwamba ni mwili wa Xander, lakini aliye ndani ni Sandra. Na "Sandra (Xander)" inamaanisha ni mwili wa Sandra lakini aliye ndani ni Xander. Hii itakuwa hasa kwenye sehemu ambazo wanakuwa pamoja na watu wengine au nikiwaelezea, lakini wakiwa peke yao nitatumia majina yao kawaida. Itaeleweka tu. Songa nayo)

Baada ya mwalimu kuwa amefika, wakaingia darasani na kuanza kujifunza. Mwalimu huyu, mwanaume aliyekuwa mnene kiasi, alipendwa nao kwa sababu yeye pia alikuwa mstaarabu, na alijua kufundisha. Aliwaelezea mambo vizuri sana kila alipoulizwa maswali, na jina lake lilikuwa Paul Ruta; au Sir Paul kama walivyozoea kumwita. Baada ya kuwafundisha jambo fulani siku hiyo, akawaomba wamuulize maswali, lakini hakuna hata mmoja aliyeuliza. Hivyo yeye akaona awaulize swali rahisi ili kuona kama wameshika vitu fulani kichwani.

"Haya ngoja mimi niwaulize... chemshabongo. WebKit huwa inatumika kwenye nini?"

Wote wakaendelea kumwangalia tu bila yeyote kunyoosha mkono. Kisha, Xander (Sandra) akanyoosha kiganja chake juu ili atoe jibu. Alikuwa ameketi kiti cha nyuma yake Sandra (Xander).

Sir Paul akasema, "Alexander..."

Xander, akiwa kwenye mwili wa Sandra, alikuwa ameangalia chini kwenye simu yake, lakini aliposikia jina lake likiitwa, akajisahau na kunyanyua uso.

"Naam..." Sandra (Xander) akaitika.

"Huwa inatumika kwenye browser kama Chrome na Safari," akajibu Xander (Sandra).

Jibu lilikuwa sahihi, lakini hii hali ikamchanganya kiasi mwalimu, na hata Sophia pia.

"Ndiyo ni kweli, asante. Alexandra ulikuwa unataka kusema nini?" Sir Paul akamuuliza aliyemwona kama Sandra.

"Hamna kitu," akajibu Sandra, akiwa ndani ya mwili wa Xander, kwa kujisahau pia.

Mh! Mwalimu Paul akashindwa kuelewa kwa nini amemuuliza Sandra swali lakini akajibu Xander.

"Sawa. Asante Alexander," Sir Paul akasema.

Xander, akionekana kuwa Sandra, akanyanyua uso wake tena na kusema, "Karibu sana."

Mwalimu Paul akakunja uso kimaswali. Haikuwachukua sekunde nyingi mapacha hawa kutambua kuwa walikuwa wamejisahau sana. Mwalimu akageukia ubaoni akiwa bado anajiuliza nini walikuwa wanamfanyia, naye Sandra (Xander) akamgeukia Xander (Sandra) na kumwangalia kwa yale macho ya 'tumeshaharibu.' Mwalimu Paul akawaangalia tena mapacha hawa, huku wengine darasani wakiwatazama pia.

"Okay. Alexander amesema Webkit ni kwenye Chrome na Safari. Nikumbusheni kazi yake ni nini," akawauliza.

Sophia akanyoosha mkono na kuchaguliwa.

"Inaziwekea browser HTML code na CSS. Ili kui-apply, tunapaswa kuandika -webkit pamoja na CSS kwenye code za HTML," akajibu.

"Safi sana. Vizuri sana. Nani anaweza kuniambia ni tool engine gani ambazo husaidia kuweka code hizo kwenye Opera, Firefox, na Internet Explorer?" Sir Paul akawauliza tena.

Alikuwa amefanya kusisitiza maswali ili aone itikio lingine kutoka kwa mapacha, naye akalipata. Wakati huu, aliyenyoosha mkono alikuwa ni Xander ndani ya mwili wa Sandra, naye akamchagua.

"Alexandra..." Sir Paul akaita.

"Opera wenyewe ni Presto, Internet Explorer ni Microsoft Edge, halafu Mozilla Firefox ni...." Sandra (Xander) akaishia hivyo.

'Ni Gecko,' Sandra akajisemea kichwani kwake kama anamwambia Xander.

Cha kushangaza ni kwamba, Xander akamsikia!

"...ni Gecko," Sandra (Xander) akasema kwa sauti bila kuwa na uhakika sana.

Mwalimu Paul akatabasamu tu na kumpongeza kwa kutoa majibu sahihi. Zamu hii hakuona jambo lolote lililotia wasiwasi, hivyo akaona aachane nalo tu na kuanza kujiandaa kutoka. Lakini Xander alibaki akitafakari kuhusu sauti ya dada yake aliyoisikia kichwani. Xander akamgeukia Sandra.

"Hey mdoli, ulinisemesha?" akamuuliza kwa sauti ya chini.

"Saa ngapi?" Sandra akauliza.

"Wakati natoa jibu..."

"Hamna. Sikiliza. Mazoezi ya kuogelea saa 5. Kaa karibu na Sophia ili uone atakavyofanya mambo na wewe uige. Ah yaani sijui itakuwaje..."

"Usihofu. Me nitafurahia sana kuwaona watoto ndani ya swimsuit... vinanilii vikiwa vimevimba-vimba siunajua... hwehwehwe..." Xander akatania.

Mwalimu Paul akatoka darasani.

"Acha sifa. Sitaki u..."

"Sandra, twende zetu kwa Lava," Sophia akawakatisha.

Lava lilikuwa ni jina la kijana aliyefanya kazi ya upishi kantini. Mara nyingi watu waliposema twende kwa Lava walimaanisha kwenda kula chips mayai au kavu, kwa kuwa yeye ndiyo alikaanga.

"Mh! Kwa Lava mapema hii yote kufanya nini?" Sandra (Xander) akamuuliza.

"Si kuhusu ile ishu... au umesahau?" Sophia akamuuliza.

Sandra (Xander) akamtazama Xander (Sandra), naye akampa ishara ya haraka kwamba akubali.

"Aaaa... sawa. Twende zetu best... shostito," Sandra (Xander) akamwambia Sophia.

"Mhm... sijui umekuaje leo," Sophia akasema na kuanza kuelekea nje.

"Xander, mnaenda kwa Lava ili kupokea ujumbe kutoka kwa Tobias. Anapaswa akupe wewe, na usimwonyeshe yeyote labda Sophia tu..." Sandra akamnong'oneza haraka.

"Unahusu nini?" Xander akamuuliza.

"Ukishasoma tu utauelewa halafu ujiigilizishe vizuri. Mimi..."

"Jamani twende basi!" Sophia akasema kutokea mlangoni.

Sandra (Xander) akaanza kunyanyuka, akimwambia Xander (Sandra) kwa utani kwamba anatumaini haitakuwa madawa ya kulevya. Yeye na Sophia wakaondoka pamoja kuelekea kule. Lucas na wenzake wakamfata Xander (Sandra) na kuanza kuongea naye. Wakati wakiwa bado kwenye chumba hicho hicho, akapata ujumbe wa simu kutoka kwa madam Valentina. Jina alilokuwa ametunza Xander ni "madamV" hivyo ilikuwa rahisi kwa Sandra kujua ni yeye.

'Njoo ofisini.'

Ulisomeka hivyo. Rahisi sana kuelewa. Lakini Sandra akaanza kuwaza ni nini ambacho madam wao huyo angetaka kutoka kwa Xander mpaka amwite ofisini kwake. Kwa haraka akafikia mkataa kwamba huenda kulikuwa na kazi ameiacha huko, au Xander alikuwa amemfanyia ukorofi. Akawaaga rafiki "zake" akisema yeye anakwenda ofisini mara moja, nao wote wakatoka pamoja naye kisha walipofika kule nje wakamwacha aelekee huko.

Sandra, akiwa mwilini mwa kaka yake, akafika nje ya mlango wa ofisi aliyojua ilimhusu Valentina. Akagonga mlango kidogo, naye akasikia sauti ya madam ikimwambia apite ndani. Akaingia na kuuacha mlango ukiwa wazi kidogo na kwenda taratibu kumwelekea madam Valentina. Alikuwa ameketi kwenye kiti chake huku akimwangalia "Xander" kwa tabasamu hafifu usoni. Sandra akajitahidi kuonyesha heshima na kumsalimu kwanza.

"Madam V... sh'kamoo..." akamwamkia.

Valentina akacheka kidogo huku anatikisa kichwa chake. Yeye alifikiri huu ni utani mwingine wa Xander, akimwacha Sandra anashangaa kwa nini amecheka.

"Huishiwagi vituko eti?" Valentina akasema.

Sandra, akiwa anatambua kwamba anayesemeshwa ni Xander, akatabasamu kwa njia ya kujiamini kama kaka yake tu.

"Mbona hujani-check leo?" Valentina akauliza.

"Aam... ndiyo nimetoka kwenye kipindi nika... nikaona meseji yako. Kuna jambo fulani unataka kuniambia madam?" Xander (Sandra) akauliza.

"Ndiyo mwanafunzi wangu," Valentina akasema huku anatabasamu.

Kisha akanyanyuka na kumpita ''Xander" aliposimama mpaka mlangoni, naye akaufunga na kurudi kwake. Sandra alikuwa anashangazwa na haya yote, akikisia-kisia kichwani kwamba huenda madam Valentina alikuwa anamtaka Xander, lakini hakuwa na uhakika mwingi. Ni mpaka Valentina alipomkaribia na kupitisha mikono yake kiunoni kwake ndipo akatambua kuwa wawili hawa walikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi.

"Nimekumiss... ijapokuwa ilikuwa jana tu," Valentina akasema kwa sauti yenye kudeka fulani hivi.

Sandra aliona hii kuwa ajabu, kwa sababu kihalisi huyu alikuwa ni mwanamke mwenzake akimwambia maneno ya kimapenzi. Lakini akaitikia haraka kwa kumshika mabegani na kutabasamu kiajabu-ajabu tu.

"Mimi pia," akasema bila kuelewa kilichomaanishwa hasa.

Valentina akamsogelea mdomoni na kumpiga busu laini iliyojaa upendo mwingi. Sandra akabaki kukodoa macho yake tu, akishindwa kuijibu busu hii kiusahihi. Mwili wake wa kiume ukaanza kupatwa na hisia za kimahaba ambazo zilimsisimua na kumchanganya kwa wakati mmoja. Akawa kama anamsukuma Valentina nyuma kidogo, naye madam akaivunja busu taratibu na kumwangalia kimaswali.

"Vipi?" Valentina akamuuliza.

"Aa... hamna kitu. Hapa ni ofisini kwa hiyo... niliogopa," Xander (Sandra) akajitetea.

"Ahah... toka lini umeanza kuogopa kwa sababu tuko ofisini? We ndiyo umenizoesha hivi. Au nimeshaanza kukuboa tayari?" Valentina akauliza.

"No, no, no... pfff... nani akuchoke? Siwezi. Aam... sijisikii vizuri sana leo... tuta...."

"Xander vipi, mbona hivyo?" Valentina akauliza kimashaka.

"Am sorry. Nitakwambia lakini... nahitaji kwenda... am so sorry madam," Xander (Sandra) akasema.

Akaitoa mikono ya madam Valentina kiunoni kwake na kuanza kuondoka hapo haraka, bila kugeuka nyuma hata mara moja kumwangalia mpaka alipoondoka ofisini humo. Valentina alibaki kushangaa kwa kuwa hakuelewa mpenzi wake mpya alikuwa na tatizo gani. Huyu hakuwa Xander aliyemzoea kabisa, na kitendo hiki kikamkosesha raha sana.

★★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★★

Natumaini ulifurahia sehemu ya nane. Usikose mwendelezo wa simulizi hii kali ya FOR YOU. Njoo WhatsApp for full season 1, 2, & 3 kwa bei nafuu sana.

WhatsApp +255 787 604 893
 
FOR YOU

Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Uhalifu, Mauaji, Visasi, Vita, Mambo yasiyotazamiwa

Rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA TISA

★★★★★★★★★★★★★

Sandra alikuwa haamini kama kweli pacha wake alikuwa na uhusiano na mwanamke huyu mwenye elimu sana na aliyemzidi umri. Ingekuwa kawaida kusema ni Xander kwa hiyo bila shaka aliweza kumzuzua, lakini bado ilimshangaza.

Baada ya kuondoka kwenye jengo la ofisi, akampigia pacha wake na kumwambia atoke huko aliko haraka sana ili wakutane kuongelea jambo fulani la muhimu. Akamwambia wakutane nje chini ya mti fulani, na ahakikishe anakuwa mwenyewe hata akihitaji kumkimbia Sophia.

Basi, baada ya yeye Sandra kuwa amekwenda hapo, akasubiri kwa dakika kama kumi hivi naye Xander akawa amefika. Alikuwa anatembea taratibu kama kawaida ya Sandra, naye alikuwa anatabasamu kama kawaida yake akiwa Xander.

"Yaani masela wanavyonitazaaama... wananiitaiiita... hahahah... tako lako linakuwa kubwa kila siku," Xander akasema baada ya kufika.

"Xander... kuna jambo nataka kukuuliza..."

"Na mimi nataka kukuuliza, hivi nyie wasichana mna matatizo gani? Yaani kamishe kadogo namna ile mpaka mzungushe kwa Tobias awaletee ujumbe, sijui mrudishe tena... yaani Ina maana..."

"Tulikuwa na maana yetu..."

"Maana gani?"

"Principal ananitaka. Mimi simtaki kwa hiyo ndiyo maana..."

"Anakusumbua? Kwa nini hukuniambia?"

"Kwa nini nikwambie?"

"Ahahah... okay. Kwo' kama angekuja na kunishika tako langu, yaani lako, ningemwachia tu maana ningefikiri na ye' unampa!"

"Em' toka huko! Sitaki mazoea naye kabisa. Sema sikuona haja ya hilo maana sasa hivi hatanisumbua tena..."

"Mmmm na Tobias ndo' Clerk..."

"Potezea hilo bwana. Nini kinaendelea kati yako na madam Valentina?"

"Madam Vale... ayaaa!"

"Kwa nini hukuniambia kama unatoka naye?"

"Kwa nini nikwambie? Hii ndiyo sababu sikutaka tubadilishane simu. Nipe bana amesemaje..." Xander akaichukua simu yake kutoka kwa dada yake.

"Ameniita ofisini akaanza kunipa romance. Ehehee... this is incredible. Kwa hiyo unamla madam Valentina?"

"Ndiyo, na ni kitu ambacho sikutaka ujue. Namlaani aliyenihamishia kwenye mwili wako..."

"Vipi kuhusu Ramla?"

"Agh, Ramla anazingua. Madam V namwelewa sana..."

"Ila wewe!"

"Ayaa... dah!" akasema Xander kwa kusikitika huku akiangalia simu yake.

Sandra akasogea karibu na kuona ujumbe wa Valentina kwenye simu hiyo. Ulisomeka: Xander, najua hatujawa pamoja kwa muda mrefu, lakini nimevunjika moyo sana na kilichotokea. Sijui kama kuna kitu nimefanya kukukwaza, ila naomba ujue nakuhitaji. Hata kama itakuwa kwa kipindi kifupi tu, ni sawa. Lakini bado nakuhitaji sana wakati huu.

"Ndiyo ameandika essay yote hiyo? Umeshamlaza mara ngapi?" Sandra akamuuliza Xander.

"Kwani we' umemfanyaje?" Xander akamuuliza akiwa amekerwa.

"Sijamfanya kitu. Amevunjika moyo kwa sababu sijamfanya kitu. Sijui huwa mnafanyaga nini ofisini kwake, lakini mimi nisingeweza kufanya hivyo. Si tulikubaliana hatutakiwi kufanya na yeyote chini ya hii hali?" Sandra akasema kwa sauti ya chini.

"Sijawahi kufanya naye ofisini kwake bwana. Ina maana umeshindwa hata kumpiga denda tu?"

"Ni rahisi kwako kusema... Raymond akitaka kukubusu utakubali?"

"Namkata ngumi ya pua!"

"Sasa je!"

Ujumbe mwingine kutoka kwa Valentina ukaingia. Ulisomeka: Nitakusubiri same place after hours. Please come.

Sandra alikuwa anatazama upande mwingine sana, kwa kuwa kuna jambo lilimkera sana kutokea hapo. Sasa akawa amechoka.

"Mbona huyo kaka ananiangalia hivyo?" Sandra akauliza.

"Nini?"

Xander ndani ya mwili wa Sandra akageuka na kumwona Isiminzile akiwa amesimama usawa wa maduka ya pembezoni mwa uzio wa chuo. Akamwangalia Sandra tena.

"Toka nimefika hapa namwona tu. Ananiangalia sana. Labda anakupenda!" Sandra akasema.

"Huyo ni Isiminzile. Ni rafiki yangu, kwo' igiza unamjua maana anafikiri wewe mimi. Mwite umsalimie... ni mwoga-mwoga," Xander akamwambia.

Sandra akatii na kumwita kwa ishara, lakini Isiminzile akaondoka tu kama haikuwa yeye aliyeitwa.

"Ish! Huyo mtu vipi?" Sandra akashangaa.

"Ana swaga za kiboya, achana naye. Sikiliza Sandra. Namkubali sana madam V. Sina jinsi ila kumwambia kinachoendelea..." Xander akasema.

"Nini? Yaani bado hata hatujawaambia wazazi wetu halafu unataka kumwambia mtu wa nje?"

"Sina jinsi. Mambo... yapo tight. Mama birthday kesho, anataka twende shopping najua tutakaa huko weee! Lazima tuongee na Valentina kabla ya huo muda maana mambo yatakuwa mengi kufikia kesho, si unajua mama atahitaji tuwe karibu naye zaidi?" Xander akasema kwa hisia.

"Mh! Ndiyo kusema unampenda sana?"

"Ahah... ananifanya najihisi tofauti tu. Tafadhali kubali Sandra... for me..."

Sandra akatabasamu na kusema, "For you. Sawa. Kwa hiyo tunaenda ofisini kwake sasa hivi?"

"Hapana. Ameniambia tukaongee kwake. Tukitoka tu hapa twende," Xander akasema.

"Haya sawa. Kwa hiyo wa kwanza kujua atakuwa madam Valentina. Lakini bado hatujui suluhisho la tatizo hili, sijui hata kama kuna suluhisho. Umeshafikiria itakuwa vipi kama tutakaa namna hii maisha yetu yote?" Sandra akaongea kwa hisia pia.

"Sijui kwa kweli. Lakini acha tu tuwe na imani. Mambo yatakaa sawa," Xander akasema.

Kisha akamshika Sandra kiganja kama kumtia moyo, nao wote wakapeana tabasamu la imani.

★★★

Muda ulikwenda haraka. Mpaka inafikia mida ya saa 9 mchana, mapacha walijitahidi sana kukaa kwa ukaribu, wakiwa makini kutenda kwa njia "zao" za kawaida mbele ya wengine. Walikuwa wamekubaliana kubadilishana simu, lakini wangeambiana yaliyojiri kila mara ambapo wangetafutwa na watu waliowafahamu. Wakaahidiana kutoharibiana chochote kwenye simu zao, na nyakati ambazo wangekuwa sehemu moja, basi wangerudishiana simu mpaka muda ambao wangetengana tena.

Xander alikuwa amejibu ujumbe wa Valentina, akisema angekwenda kwake ili waongee vizuri. Lakini hakumwambia kwamba angeenda na dada yake ili kutomshangaza mapema. Raymond aliwasiliana mara kadhaa na Sandra, na hata Ramla bado alikuwa akijaribu kumwomba samahani Xander ili mambo kati yao yakae sawa, lakini kijana akaendelea kumpuuzia.

Baada ya muda fulani, Xander aliliona gari la madam Valentina likiondoka hapo chuoni, naye akamuuliza kwa ujumbe ikiwa ingekuwa sawa akimfata muda huo. Valentina akapiga simu, kwa hiyo ikabidi Sandra ndiyo aipokee ili wazungumze na kumfikirisha anayeongea naye ni Xander. Valentina akamwambia kwamba ndiyo alikuwa anaelekea nyumbani, hivyo kama alikuwa anataka kuja muda huu basi amfate. Xander (Sandra) akakubali, kisha akamwambia kaka yake kile madam alichosema.

Kwa kuwa hawakuwa na kipindi kingine, wawili hawa wakaondoka pamoja kwa pikipiki ya Xander. Kiukweli watu kadhaa siku hii hawakujizuia kuwaangalia sana kwa sababu walikuwa karibu mno siyo kama sikuzote. Aliyewakazia uangalifu zaidi alikuwa ni Isiminzile, kwa kuwa alijua alichokifanya, lakini hakujua atumie njia gani ili kutambua nini kiliendelea baina yao kwa sababu aliogopa. Mapacha wakaondoka zao haraka kuelekea kwa madam.

Haikuwachukua dakika nyingi nao wakawa wamefika. Hii haikuwa mara ya kwanza kwa Sandra kufika hapa. Kipindi cha nyuma alikuja hapo mara kadhaa hasa yeye na rafiki zake walipopita kumsalimu madam wao. Aliwatendea kwa urafiki sana nao walimpenda mno. Kwa hiyo Sandra alimjua kwa kadiri fulani mwanamke huyu, na kujua kwamba Xander alitoka naye sasa ni kitu ambacho kilimshangaza kwa kuwa alihisi ni kama hawakufaana kabisa. Ila yeye hakuwa mtu wa kuhukumu hata kidogo na kuyaona yao kuwa yao tu.

Baada ya kuegesha pikipiki nje, wakaelekea getini na kubonyeza soketi ya kengele. Walikuwa wamesimama kwa kusubiri huku Sandra akimwambia Xander asiogope sana. Jamaa akamhakikishia kwamba hakuogopa, ila wasiwasi tu ndiyo ulimjaa maana hakujua Valentina angechukulia vipi suala hili lote. Mlango mdogo wa geti ukafunguka, na wote wakamwona madam Valentina hapo. Alishtuka kiasi kwa sababu hakutazamia kuwaona mapacha wote hapo, na maswali yakaanza kupita kichwani kwake.

Xander, akiwa ndani ya mwili wa Sandra, akamkanyaga Sandra akiwa kwenye mwili "wake" mguuni kidogo ili aongee haraka, naye akasema, "Madam V..."

"Alexander..." akasema Valentina, huku akiwa na uso wenye kuonyesha hali ya kutopendezwa.

"Huyu ni pacha wangu... anaitwa..."

"Alexandra, najua. Ambacho sijui ni kwa nini umekuja naye," Valentina akamkatisha.

Xander aliona kweli mwanamke alikuwa amekerwa. Sandra akaona asogee karibu zaidi.

"Ambacho nataka kukwambia ni muhimu sana. Na Xander... I mean, Alexandra, anahusika pia," Xander (Sandra) akamwambia.

Valentina akawakaribisha ndani. Alijihisi kama mjinga kiasi kwa sababu vijana hawa bado walikuwa wadogo kwake lakini waliingia kwenye maisha yake kwa pamoja ghafla na kufanya ionekane kama walikuwa wanataka kucheza nayo. Ijapokuwa alimruhusu Xander maishani mwake, hii haikuwa ruhusa kwake kuanza kuingiza na watu wengine ambao aliona hawakupaswa kujua lolote; hasa kwa kuwa ndiyo walianza tu mahusiano. Wasiwasi pia ulimvaa akitaka kujua ni nini ambacho Xander alihitaji kusema kilichofanya na dada yake ahusike, mpaka kusababisha lile jambo lililomvunja moyo ofisini kwake asubuhi hiyo.

Walipofika ndani, Valentina akaenda kuketi kwenye sofa, akiwaambia mapacha wakae pia. Lakini wakawa wamesimama tu huku wanamtazama, naye akauliza shida ilikuwa ni nini. Xander, akiwa kwenye mwili wa Sandra, akamfata na kupiga magoti chini, karibu kabisa na alipokaa, huku akivishika viganja vyake. Valentina akashangaa.

"Alexandra... unafanya nini?" akamuuliza.

"Madam V... ni mimi. Mimi ni Xander," akamwambia kwa hisia.

Valentina akakunja uso kimaswali.

"Wewe ni Xander? Unamaanisha nini, sikuelewi..." Valentina akasema.

"Mimi ni Xander. Yule pale ni Sandra. Kuna kitu kimetokea kimesababisha miili yetu ibadilishane... sijui ibadilishanwe... ibadilishwe, ah damn it! We've switched bodies," Sandra (Xander) akasema.

Valentina akawaangalia wote kwa njia ya kawaida tu. Mapacha wakawa wanasubiri kusikia atasema nini.

"Okay kwa hiyo... wewe pacha wa kike ni Xander, na yule Xander nayemwona ndiyo wewe wa kike. Natakiwa tu kukubali like, 'sawa karibuni intertwined siblings' kirahisi tu. Ni mchezo gani mnanifanyia?" Valentina akaongea kistaarabu.

"Hapana madam, ni kweli. Mimi ni Sandra. Nimeingia kwenye mwili wa kaka yangu. Na huyo aliye kwenye mwili wangu ni Xander. Hatuwezi kukudanganya," akasema Xander (Sandra).

Valentina alianza kucheka kwa sauti ya chini huku akitikisa kichwa chake. Aliona anayemwambia hivyo ni Xander, lakini kiukweli hali hii yote ilikuwa yenye kushangaza sana. Hakuelewa vijana hawa wamepatwa na nini. Xander alikuwa anamtazama kwa hisia sana, akijua pia kwamba haingekuwa rahisi kwake kuelewa.

"Kwa hiyo... uliruka tu... mlirukiana halafu mkaishia kubadilishana miili?' Valentina akauliza.

"Siyo rahisi kuamini, naelewa. Lakini ni kweli. Jana usiku kwenye ile dhoruba, kuna kitu kilitokea. Tulikuwa tu tumelala pamoja kwa sababu dada'angu alikuwa anaogopa... tumeamka asubuhi tunajikuta hivi..." Sandra (Xander) akamwambia huku bado akiwa amemshikilia viganja.

"Dhoruba? Ile mvua ndogo ya jana ndiyo ilikuwa dhoruba?" Valentina akauliza.

Xander na Sandra wakaangaliana. Huyu alikuwa mtu wa pili kukanusha kwamba mvua ya jana haikuwa kubwa kama walivyodhani.

"Okay masihara kwisha. Xander, nilifikiri tulipaswa kukutana mimi na wewe peke yetu hapa. Sijui ni kituko gani mnataka kunifanya nionekane lakini sijapenda. Unanifanya nionekane kama mtoto mdogo. Kama unatafuta njia ya kuachana nami, niambie tu. Haya yote ya nini?" Valentina akauliza akiwa anamwangalia Xander (Sandra).

Xander, akiwa kwenye mwili wa dada yake karibu na Valentina, akamshika usoni kwa viganja vyake.

"Hapana siyo hivyo... Valentina... tafadhali niamini. Ni-test basi. Tu-test sisi wote. Kumbukumbu zetu ziko pale pale ila ni miili tu ndo' imebadilishwa. Please..." akamwomba.

Valentina akamtazama msichana huyu aliyekuwa anamwambia kwamba ndiyo mpenzi wake. Akamwangalia na "Xander," akiwa eti ndiyo "Sandra." Bado alihisi ni kama wanamchezea, lakini akaona afuate ushauri huu.

"Okay. Mara ya pili uliponishika na kunibusu, ilikuwa ni wapi, na ni nini kilifata baada ya hapo?" Valentina akauliza.

"Ilikuwa ofisini kwako. Na ilikuwa ni busu tamu sana ambayo sitasahau. Aam... principal aliingia, na mimi ikabidi niyaangushe mafaili yako chini... nikaanza kuyaokota ili kuficha... you know..." Sandra (Xander) akamwambia huku anatabasamu kwa mbali.

Valentina akamtazama sana, kisha akamwangalia yule aliyemwona kuwa Xander.

"Natumaini huwa haumwambii dada yako kila kitu ambacho mimi na wewe tumefanya," Valentina akamwambia, akiwa bado haamini.

"Hapana hajaniambia. Najua unaniona kama Xander, lakini mimi ni Sandra," Xander (Sandra) akasema.

"Ndiyo Valentina. Siwezi kumwambia Sandra kuhusu mambo yote yaliyotokea baina yetu. Lakini... kwa kuwa nahitaji kukufanya uamini... Unakumbuka mara ya pili tume... make love... nilikunong'oneza maneno gani sikioni ukasema nirudie?" Sandra (Xander) akamuuliza.

Valentina akabaki tu kumwangalia.

"Sandra" huyu akamsogelea sikioni na kumnong'oneza, 'Te amo, cariño.'

Kisha akajitoa sikioni kwake na kumwangalia tena machoni. Bado Valentina alikuwa amechanganyikiwa.

"Siwezi nikamwambia hivyo Sandra. Ni wewe tu," Sandra (Xander) akasema.

Valentina akamtazama sana "Xander" kule aliposimama. Hakuelewa nini kilikuwa kinaendelea.

"Madam, mimi ni Sandra. Unakumbuka wakati ule unatupa training usiku nyuma ya ile deck tuliona nini mpaka Asha akazimia? Na ukatuambia tusimwambie yeyote?" Xander (Sandra) akamuuliza Valentina.

Sasa Valentina akawa ameshibitishiwa hata zaidi kwamba huu ulikuwa ni ukweli. Lakini bado hakuelewa iliwezekanaje. Akawa anawatazama sana.

"Mh! Ni kitu chenye kushangaza sana. Kwa hiyo... miili yenu ime-switch vipi?" akawauliza.

"Hata sisi hatujui. Na bado hatujawaambia wazazi wetu. Xander alihofia labda utamchukia kwa kuwa kilichotokea asubuhi leo ofisini kwako... ilikuwa ni mimi. Yaani... wewe ulifikiri unanibusu mimi kama Xander na nilikuwa sijui kuhusu uhusiano wenu ndiyo maana nika-act namna ile. Sorry for that..." Xander (Sandra) akasema.

Valentina akamtazama aliyemwona kama Sandra.

"Xander..." Valentina akamwita.

"Naam..." akaitika, kwa sauti ya kike kabisa.

"Ahah... unbelievable!" Valentina akaongea kwa kustaajabu.

Xander akamkumbatia. Valentina bado aliona ni kama anakumbatiwa na Sandra lakini sasa hakuwa na jinsi ila kuzoea hali hii mpya. Xander akamwachia na kukaa naye karibu kwenye sofa.

"Kwa hiyo sasa, mtafanyaje?" Valentina akawauliza.

"Hatujui hii yote imetokea wapi na inaelekea wapi. Lakini tunahitaji msaada. Cha kwanza itakuwa ni kuwaambia wazazi wetu. Lakini tulikuwa tunataka kusubiri mpaka birthday ya mama ipite ndo' tumwambie kwanza maana atachanganyikiwa tukisema now. Baada ya hapo... nitahitaji msaada wa ukocha kidogo maana shindano la kuogelea limekaribia na Sandra anahitajika sana ili kushinda..." Sandra (Xander) akaeleza.

"Kwa kuwa uko kwenye mwili wake utahitaji kuzijua mbinu," Valentina akasema.

"Ndiyo."

"Kwa hiyo... utaogelea, ndani ya mwili wa dada yako, kwenye shindano la wanawake. Unajua kwamba kwenye vyumba vya maandalizi huwa..."

"Ndiyo tunajua madam. Lakini tutafanyaje? Xander alivyo na kichwa kibovu atafurahia sana kuona wadada wakiwa bila nguo au wakijipiga-piga makalio... na hata anaweza kuyashika-shika..." Xander (Sandra) akawa anasema kiutani.

"Sandra!" Sandra (Xander) akamkatisha.

Valentina akatabasamu kidogo.

"Usimsikilize huyu... I'd never do that," Sandra (Xander) akamwambia Valentina.

"Okay sawa nimewaelewa. Hii itakuwa challenge kubwa kwangu," Valentina akasema.

Sandra, akiwa anajua kwamba wawili hao wangehitaji kuzungumza peke yao, akamwomba Valentina amwelekeze vyumba vya haja vilipokuwa. Baada ya kuelekezwa na kwenda, Xander akamshika usoni Valentina.

"Valentina... najua hii ni ngumu kwako. Lakini ujue kwamba nakupenda sana hata kama niko kwenye mwili wa dada yangu. Hakuna kinachobadilika," akamwambia.

"Ndiyo. Najua. Ni ajabu kidogo kwa sababu... ahah... ni kama nayeongea naye ni Alexandra. Ijapokuwa mnafanana lakini ni wewe Xander, ukiwa kwenye mwili wako, ndiyo huwa unanifanya nasisimka. Hivi... sijui kama itakuwa rahisi," Valentina akamwambia.

"Usijali. Ninajua hiki kipindi kitapita. Cha muhimu ni kwamba bado tutakuwa wote madam wangu mtamu," Xander akamwambia.

Vakentina akacheka kidogo.

Xander akaifata midomo yake na kumbusu. Kwa mara ya kwanza kabisa akambusu mwanamke huyu akiwa ndani ya mwili wa pacha wake. Alijitahidi kumbusu kwa njia ile ile anayotumia akiwa kama Xander, lakini bado Valentina hakuhisi hilo; yeye aliona anapewa busu na Sandra. Baada ya Xander kukatisha denda hii, akampa tabasamu, naye Valentina akatabasamu pia lakini hakujihisi vizuri sana.

Baada ya Sandra kurejea hapo, mapacha wakazungumza na Valentina kuhusiana na jinsi ambavyo mambo yangekwenda baada ya birthday ya mama yao. Wangepanga muda fulani wa pekee ili Valentina amsaidie Xander kufanya mazoezi ya kuogelea, naye Xander akatania kwamba sasa wangetumia muda mwingi kuliko kawaida kwa sababu alionekana kuwa wa kike hivyo angemganda sana. Wakamwambia ikiwezekana wamshauri mama yao amwalike na yeye kwenye sherehe yake kesho nyumbani, ili akapate kupaona na ndani kwao kabisa, lakini Valentina akakanusha na kusema hangeweza, hivyo wao wafurahie tu.

Waliendelea kukaa hapo kwake mpaka kwenye mida ya saa 12 jioni, kisha wakaondoka kuelekea nyumbani. Valentina alibaki na vitu vingi kichwani kwake. Bado kuimeza hii hali yote haikuwa rahisi. Lakini akaamua tu kuacha mambo yawe jinsi yatakavyokuwa na kusubiri ambayo yangefuata. Akarudi ndani kupumzika.

★★★

Baada ya kufika nyumbani, mapacha walikuta mama yao pamoja na Azra wakiwa wamerudi tayari. Wakajitahidi sana kutenda kwa njia ya kawaida ili wasishtukiwe kwa kile kilichowapata. Alice akawaambia kwamba alitaka kuwatoa "out" wote ili kupata chakula sehemu fulani nzuri sana. Hili lilikuwa ni jambo lililomfurahisha sana Azra, ambaye bila kusubiri akaenda kujiandaa haraka. Salome, Xander na Sandra pia wakaenda kujiandaa kwa ajili ya matembezi hayo. Ilibidi Sandra amsaidie Xander kuvaa nguo nzuri na kumpamba usoni kiasi kwa sababu jamaa hakujua jinsi ya kutengeneza vizuri mwili wa dada yake. Walipokuwa tayari, wote wakaondoka, ikiwa ni mida ya saa 2 usiku.

Alice aliwaendesha mpaka kwenye hoteli kubwa sana ya kifahari jijini hapo. Baada ya kuegesha gari, familia hii ikaanza kuelekea ndani huko. Alice alikuwa amekwishalipia mapema sehemu waliyotakiwa kufikia kwa ajili ya mlo, hivyo walipofika tu sehemu za ndani, wakapokelewa na mhudumu maalumu aliyewaongoza kuelekea upande wa meza yao. Wanaume wengi waliwaangalia sana wanawake hawa (Alice, Salome, Azra, na Sandra (Xander), kwa sababu walikuwa wamependeza kwa mionekano yao ya gharama. Xander alikuwa anakerwa na jinsi wanaume walivyomtazama kwa njia ya utongozi kwa kuwa ni yeye ndiye aliyekuwa kwenye mwili wa Sandra, lakini Sandra akamwambia awapuuzie tu.

Wakafika kwenye meza yao, ambayo ilizungukwa na viti vyenye mtindo wa masofa vilivyokuwa virefu kuficha hadi vichwa vyao, nao wakaketi na kupewa mfululizo wa vyakula mbalimbali (menu) ili wachague walivyotaka. Wote walipomaliza kuchagua, mhudumu akaondoka kupeleka mahitaji yao kwa wapishi ili awaletee hatimaye. Lakini kuna jambo likamshangaza Alice kiasi.

"Sandra, umeagiza kitimoto? Nilifikiri huwa huli..." akamwambia Sandra (Xander).

Xander, akiwa kwenye mwili wa Sandra akasema, "Aam... sa'hivi huwa nakula. Ni nzuri."

Sandra akamkata jicho kwa sababu ni chakula ambacho hakupenda kula.

"Mama, hoteli nzuri sana hii. Kati ya zote ambazo umetupeleka, hii inafunika," Azra akasema.

"Hivyo ndivyo ulivyosema mara ya mwisho kwenye ile nyingine," Salome akamwambia.

"Hamna hii ni noma. Anaimiliki nani?" Azra akauliza.

"Anaitwa Juliana," akajibu Alice.

"Juliana wa Bushoke?" Sandra (Xander) akauliza.

"Ahahah... hapana. Juliana Kenneth. Sidhani kama mnamfahamu ni rafiki yangu pia," akajibu Alice.

"Nilikuwa najiuliza kwa nini tumekuja hapa siyo kwingine, kumbe una shosti? Angalau aone unamchangia kidogo," Sandra (Xander) akasema.

"Siyo hivyo wala. Nilikuwa nataka tu kumwona na yeye pia kwa sababu nilipanga kuongea naye. Ila ni ili nikukutanishe na mwanaye," Alice akamwambia Sandra (Xander).

Mapacha wakatazamana. Yeye Alice aliona anayemsemesha ni Sandra kumbe ni Xander.

"Kwa nini unataka kunikutanisha naye?" Sandra (Xander) akauliza.

"Ili akuoe," Alice akasema kiutani.

Sandra, akiwa kwenye mwili wa Xander, akacheka sana.

"Na wewe unacheka nini?" Salome akamuuliza.

"Hamna kitu dada. Kwa hiyo unataka kuni... unataka kumuozesha Sandra sasa hivi?" Xander (Sandra) akamuuliza Alice.

"Eeeh..." Alice akajibu.

"Mama, mimi sitaolewa na yeyote kamwe. Siwezi kuolewa. Haiwezekani kunioa," akasema Sandra (Xander).

Alice akacheka.

"Huyo kaka anaitwa nani?" Xander (Sandra) akauliza.

"Tristan," Alice akajibu.

"Wow, jina zuri. Ni mzuri?" Xander (Sandra) akauliza tena.

"Ish! Yaani Xander unauliza maswali utafikiri wewe ndiyo unaolewa!" akatania Azra.

"Hamna si namuulizia tu dada yangu jamani," akasema Xander (Sandra).

"Haolewi mtu hapa," Sandra (Xander) akasema, na wote wakacheka.

Baada ya muda mfupi, vyakula mbalimbali vikaletwa na vinywaji. Wote walikula kwa furaha sana; hasa Azra, aliyependa sana nyama ya kuku. Walikula huku wakipiga story kuhusiana na sherehe ndogo ya mama yao kesho, shule, michezo ya watoto, na maisha ya zamani ya Alice.

"Kwa hiyo kumbe lilikuwaga ni soko kubwa sana hapa?" Salome akamuuliza Alice.

"Halikuwa kubwa kihivyo. Lilikuwa dogo tu... kama vibanda vya mbogamboga na nyumba ndogo ndogo za kuuzia vyakula. Me pia nilikuwa nafanya kazi na mama kwenye mgahawa wake. Eh! Yaani palivyobadilika na kuwa hoteli kubwa hapa! Utadhani hakukuwahi kuwa na soko," Alice akaeleza.

"Kipindi hicho hata hatujafikiriwa kuzaliwa," akasema Azra.

"Ndiyo. Nilikuwa kama Sandra tu," Alice akawaambia.

"Ndiyo ulikutana na baba huku?" akauliza Xander (Sandra).

"Casmir nilikutana naye wakati nimerudi Pemba, nafikiri alikuwa kwenye masuala yao ya kuzuru. Ahah... ilikuwa kwenye daraja fulani hivi... nilikuwa nimebeba tray la mayai napeleka dukani kwa babu, nikapamiana na askari mmoja akasababisha mayai yote yapasuke. Badala aombe samahani yeye akaanza tena kuwa mkali, na mimi sikuwa nyuma. Nikaanza kumrushia maneno, eti akanitisha kunipiga, ndiyo akatokea Casmir akamkunja mkono wake kwa nguvu na kumwambia aombe msamaha...."

Watoto wakawa wameacha hadi kula, wakimsikiliza Alice kwa utulivu sana.

"Ahahah... baadae tukawa marafiki. Akanipenda. Nikampenda. Tukaanza uhusiano. Alikuwa mwelewa sana na alinisaidia kwa mambo mengi sana... mimi pamoja na familia yetu. Mwishowe... akanioa. And... here we are," Alice akawaambia huku machozi yakimlenga.

Azra akamsogelea na kumlalia begani. Alice akaanza kuzilazalaza nywele za binti yake kwa upendo. Mapacha wakatazamana kwa hisia, wakiwa wameelewa kuwa mama yao alimkumbuka sana baba yao. Kisha Alice akawaambia waendelee kula na kupiga story nyingine.

Dakika chache baadae...

"Mom, nataka niende restroom," Azra akasema.

"Okay. Sandra nenda naye," Alice akasema na kuendelea kula.

Lakini Xander, akiwa ndiyo Sandra, akawa amejisahau kwamba ni yeye ndiye aliyepaswa kunyanyuka, hasa kwa kuwa alikuwa anajibu ujumbe wa Valentina kwenye simu, naye Alice akamtazama kimaswali. Sandra, akiwa ndiyo Xander, akamwangalia pacha wake akiwa anataka kumsemesha kwamba ni yeye ndiye aliyeongeleshwa. Kutokea kichwani kwake, Sandra akasema kwa kuudhika, 'Alexander!' akiwa hajataka kuita hivyo kwa sauti.

Lakini Xander akanyanyua uso na kumwangalia Sandra. Alimsikia! Hakujua kivipi lakini aliweza kumsikia.

★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★

Full story WhatsApp +255 787 604 893
 
FOR YOU

Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Uhalifu, Mauaji, Visasi, Vita, Mambo yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA KUMI

★★★★★★★★★★★★★

"Mom, kwani lazima Sandra aende nami?" Azra akamuuliza Alice.

"Ndiyo unaweza ukapotea. Sandra ina maana hujanisikia au?" Alice akamuuliza Sandra (Xander).

"Ha..pana. Nimekusikia. Twende Azra," Sandra (Xander) akasema.

"Me siyo mtoto bwana! Siwezi kupotea," Azra akaanza kulalamika.

"Ngoja tu twende wote nami nahitaji kwenda," akasema Salome.

"Basi nenda naye tu Salome," akasema Sandra (Xander).

Salome akanyanyuka na kuondoka pamoja na Azra. Xander, akiwa kwenye mwili wa Sandra, akawa anamtazama sana pacha wake mpaka Alice akamshtukia.

"Mbona unamwangalia hivyo mwenzako?" Alice akamuuliza.

"Aa... hamna kitu," Sandra (Xander) akajibu.

Alice akaachana na hilo na kuanza kuangalia vitu fulani kwenye simu yake.

Xander bado akawa akijiuliza ni kwa nini alihisi kama alimsikia dada yake kichwani kwake. Hii ilikuwa mara ya pili; ya kwanza ikiwa kule chuoni wakati wapo darasani. Akataka kuona ikiwa naye angeweza kusikika kichwani kwa dada yake, hivyo akamwita kwa kutumia akili.

'Sandra...'

Sandra, akiwa kwenye mwili wa Xander, akanyanyua uso na kumtazama pacha wake. Alisikia! Lakini akamtazama kimaswali sana kwa kuwa hakuelewa kilichotokea. Xander akatabasamu kidogo, kisha akaona aongeze.

'Sandra, unanisikia vizuri?' akauliza kwa kutumia akili.

'Ndiyo,' Sandra akajibu kwa kutumia akili pia.

'Amazing!' Xander akawaza.

'Hii inawezekanaje?' Sandra akauliza.

'Sijui ila... inaweza kuwa njia nzuri ya kuwasiliana kati yetu...'

'Kwa hiyo mawazo yangu yote unayasikia?'

'Hapana... sijui. Em' jaribu kuwaza kitu bila kuniambia,' Xander akasema akilini.

Sandra akafanya hivyo.

'Umenisikia?' akamuuliza.

'Hapana,' Xander akajibu.

'Mmmm... basi inaonekana ni mpaka tuwe tunaambiana...' Sandra akasema kwa akili.

'Yeah. Hili jambo linaloendelea kati yetu linazidi kuchanganya sana!' Xander akasema kwa akili.

'Sana!' Sandra akakubali.

'Kwa hiyo... sasa hivi tutakuwa tuna...'

"Nyie vipi? Mbona mnaangaliana hivyo?" sauti ya Alice ikasikika.

Mapacha wakaacha kutazamana na kukuta mama yao anawaangalia sana. Wote wakabaki tu kimya na kuendelea na chakula kilichobaki. Alice akaingiwa na mashaka kwa sababu sasa akawa ametambua kuna kitu hakikuwa sawa kati ya wanaye. Azra na Salome wakaonekana wakirejea, naye Alice akasema anatoka kwanza kwenda kumwona rafiki yake kule kwenye ofisi yake. Baada ya wawili wale kufika, Alice akaondoka, akiwaacha wanamalizia chakula.

Alexander na Alexandra wakaendelea kufanyiana majaribio ya kuongeleshana kwa kutumia akili, na lilikuwa ni jambo lenye kustaajabisha sana. Sandra akamkumbusha Xander kwamba kesho angepaswa kutoka na mama yake na Azra kwa ajili ya shopping yao, hivyo angetakiwa kumchagulia mavazi mazuri na siyo yoyote tu.

Baada ya wote kumaliza chakula, wakaendelea kukaa hapo na kupiga story mpaka Alice aliporudi. Kwa kuwa yeye hangeendelea kula, akawaambia waondoke kuelekea nyumbani sasa ili kuweza kupumzika.

★★★

SIKU ILIYOFUATA

Ikiwa ni Jumamosi yenye upekee kwa Alice kwa sababu ya kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa, maandalizi yalianza kufanywa mapema nyumbani kwao; usafi, mapambo, vifaa vya matumizi, vyakula, vinywaji, na burudani ndogo ambazo zingekuwepo. Mida ya mchana Alice aliondoka pamoja na Azra na Sandra (Xander) kuelekea kwenye moja ya duka lake kubwa la nguo ili kuchagua nguo nzuri za kuvaa, kisha baadae wakarejea nyumbani.

Marafiki wengi wa Alice walikuwa watu wenye maisha ya hali ya juu, lakini alialika pia na wale ambao hawakuwa na uwezo mkubwa sana kifedha. Sandra na Xander waliona ni bora kutoalika mtu yeyote, hasa rafiki zao, kwa kuwa waliona suala lao la kubadilishana miili kuwa tatizo ambalo lingewachanganya sana. Mpaka inafika mida ya jioni ndiyo watu wakaanza kufika kwa kuwa sherehe hii ililengwa hasa kwa ajili ya mida ya usiku.

Alice alipendeza sana kwa nguo alizovalia. Watoto wake wa kike walipendeza sana kwa magauni, huku Xander akichukia kuvalishwa gauni namna hiyo kwa kuwa ndani ya mwili wa pacha wake ilikuwa ni yeye. Sandra aliuvalisha mwili wa kaka yake nguo za kawaida tu kwa pendekezo la Xander, naye Azra alipendeza kupita maelezo. Alice akaamua kumpigia Casmir simu ili kuuliza ikiwa mume wake angefika, na wakati akifanya hivi, watoto wake wote walikuwa pamoja naye chumbani. Casmir akapokea, na kwa sababu ilikuwa ni kwa njia ya "video call," wote wakamwona akiwa ndani ya gari lililokuwa mwendoni pamoja na Kendrick.

"Uncle Kendrick!" Azra akamwita Kendrick kwa shauku.

"Azra! Umefutuka mtoto, unaenda wapi?" akasema Kendrick kupitia simu.

Wote wakacheka kwa furaha.

"Mwanagalie na huyo kadadaa! Alexandra umekua mkubwa jamani!" akasema Kendrick.

"Asante uncle K. Wewe pia unang'aa," akajibu Sandra (Xander).

"Ahahahah... unaongea kama mzee mzima hapo," Kendrick akasema.

"Nakuona uncle Kendrick," akasema Xander (Sandra).

"Nakuona pia mzee wa fujo," akasema Kendrick.

"Mmependeza sana wapendwa wangu," akasema Casmir.

"Baba, uko njiani eeh?" akauliza Azra.

Kendrick na Casmir wakaonekana wanaangaliana kifupi. Hii ikamfanya Alice ahisi kuna shida.

"Ndiyo sweetheart. Hapa ndo' tuko tunawahisha kuja," Casmir akasema.

Azra akafurahi sana.

"Mtafika saa ngapi?" akauliza Xander (Sandra).

"Aam... labda saa 1, saa 2..." Casmir akajibu.

Alice akatazama chini kwa kuvunjika moyo kiasi. Casmir akatambua hilo.

"Baba, Uncle Kendrick, msiache kuja na zawadi," Azra akasema.

Kendrick akajifanya kuziba mdomo kwa mshangao na kusema, "Ayaaa! Nimesahau! Sasa tutafanyaje?"

"Yaani usionekane hapa! Urudi huko huko mpaka ulete zawadi," Azra akaamuru.

"Basi sasa itabidi tu nirudi nyuma kweli..."

Kendrick akasema hivyo huku akionekana anarudisha mikono yake nyuma ya gari na kuirudisha akiwa ameshikilia boksi kubwa la zawadi. Wote wakacheka, huku Azra akifurahia sana.

"Kwa hiyo niahirishe tu kuja eti?" Kendrick akamuuliza Azra.

"Wee! Ole wako," Azra akamwonya.

Wote wakacheka tena.

"Sandra, nakuletea na Vaziri. Niliipata," Casmir akasema.

"Sawa. Asante," Sandra (Xander) akajibu kibaridi-baridi tu.

"Alice umependeza sana. Happy birthday," Kendrick akasema.

"Asante. Tunawasubiri kwa hamu sana," Alice akawaambia.

"Ndiyo sana. Mwahi kufika. Nyie ndiyo mtafanya party iwe party zaidi," akasema Xander (Sandra).

Casmir na Kendrick wakacheka.

"Alice my dear, happy birthday. Tuko njiani," Casmir akamwambia mke wake.

"Asante Casmir," Alice akajibu.

Kisha wote wakaagana na kukata simu. Watoto wakaelekea nje ya nyumba wakimwacha mama yao chumbani. Bado alihisi kama vile mume wake alikuwa anasema tu yote yale ili kumridhisha, lakini akajifariji tu kuwa hata kama nini kingetokea, angejitahidi kuwa sawa kwa ajili ya wanaye.

★★★

Baada ya simu kuwa imekatwa, ndani ya gari hili walilokuwemo Casmir na Kendrick kukawa na hali ya umakini zaidi. Kendrick akarudisha boksi lile la zawadi nyuma ya gari na kumtazama Casmir.

"Vipi kama tutachelewa?" Kendrick akamuuliza.

"Hapana Ken. Ni lazima tutawahi tu. Lazima nifike," Casmir akasema huku akiongeza mwendokasi.

"Yaani hata sielewi. Nini kinaendelea? Tunapofikiri tu tuko right on track, mambo yanaharibika," akasema Kendrick.

"Hii ishu imekuwa mbaya tena kwa njia ambayo inashangaza sana. Just... how?" Casmir akasema kwa mkazo huku anaupiga usukani kwa kiganja chake.

"Hapa Kanali atashangaa sana kwa hii ripoti. Unajua hawa Demba Group wanaanza kuonekana kama mashetani, maana wanafanya mambo yasiyoeleweka halafu wanatoweka tu, tena kwa watu fulani wanao... wanawalenga watu fulani kwa nini? Hawamtaki Raisi, si wamfate? Wale wanaume wamewakosea nini? Halafu wanafanyaje haya mambo bila kupatikana? Aagh... yaani me nashindwa kuelewa!" Kendrick akasema kwa kuudhika sana.

"Ningetakiwa kuwa nimetulia angalau kwa wiki hii na Alice wakati wanasakwa, ila sasa tena itabidi..." Casmir akasema kwa huzuni.

"Usijali Meja. Tufike kwa Kanali kwanza, then birthday, mambo mengine yatafuata," akasema Kendrick.

"Yeah. Baada ya birthday nataka kuhakikisha huu utumbo unamalizika haraka sana," akasema Casmir kwa uhakika.

"Nimeona kama Alexander anakuchangamkia. Ana Fever?" Kendrick akatania kidogo.

"Ahahah... sijui sana, lakini nimependa. Matumaini waliyonayo... yaani sitaki kuwaangusha kabisa," Casmir akasema kwa hisia.

Wawili hawa walikuwa na mzigo mzito sana kuhusiana na suala hili la Demba Group. Siku mbili zilizopita baada ya Kanali Jacob kuwahamishia jijini kwao, walikuja kupewa taarifa siku iliyofuata juu ya mauaji ya wapelelezi wale wa kijeshi waliowatuma kwenye mikoa ambayo walihisi Demba Group wamejifichia. Hawakuwa na jinsi ila kuondoka na kwenda huko kuchunguza mambo zaidi. Ila baada ya kuwa wamefika, leo tena wakapokea taarifa juu ya wanajeshi wengine 9 waliouawa na Demba Group.

Wanajeshi hao 9 walikuwa ndiyo wale ambao waliongoza msafara ule wa silaha siku ile Casmir alipoenda kuuchunguza, na wote waliuliwa kimya kimya na kuchorwa maandishi meusi juu ya paji la nyuso zao yaliyosomeka "Demba Group." Yalikuwa ni mambo yenye kushangaza sana, kwa sababu watu hao mpaka sasa hawakujulikana, na kwenye mauaji yote hayo hawakuacha kitu chochote cha kusaidia kuwafuatilia; kama tu msemo wa Kendrick, walikuwa kama mashetani.

Mambo haya yote yalimsumbua sana Casmir. Alikuwa amekwishapokea amri ya kuanza kazi baada ya yeye kuianza kisiri, na sasa wanajeshi wake aliowachagua wakauawa. Ikiwa ingejulikana kwa Raisi kuwa alifanya hivyo kabla ya kupewa amri, ingezua tatizo. Lakini Casmir alikuwa tayari kuwajibika. Hata kama angepewa adhabu. Alijilaumu sana kwa vifo vya wapelelezi wake. Alijiuliza watu hawa walijua vipi mipango yake na hatimaye kuikomesha kabla haijafikia hatamu nzuri.

Meja Casmir na Kapteni Kendrick walitakiwa kushughulika na mambo yote yaliyotokea haraka, lakini wakaamua kuyaacha kwanza ili Casmir atimize ahadi kwa mke wake ya kuwepo kwenye sherehe ya siku yake ya kuzaliwa. Hapo walikuwa wakitokea Singida upesi ili kuwahi jijini kwao. Walijua wangepaswa kwanza kwenda kwenye ofisi za Kanali ili kutoa ripoti ya ana kwa ana, na ndiyo maana Casmir alikuwa akiwahisha sana ili asiikose sherehe ya Alice.

Ilifika mida ya saa 1 usiku, na wawili hawa wakawa wamefikia kwenye jengo hilo. Walielekea ndani upesi, wote wakiwa wamevalia suti nadhifu. Casmir alitambua kwamba ni kama wanajeshi wa ulinzi sehemu hii walikuwa wamepungua, lakini hakukazia fikira sana jambo hili na kwenda mpaka kwenye ofisi ya Kanali. Bado Kanali Jacob alikuwepo, hivyo wote wakaruhusiwa kuingia ndani. Casmir akaeleza hali halisi ilivyokuwa, na kusema kwamba ni makosa yake kwa kila kilichotokea, hivyo kama ni adhabu basi apewe; angekubali yoyote ile.

Kendrick naye vilevile akasema alistahili adhabu, lakini Kanali Jacob akawaambia hakukuwa na haja ya adhabu. Akasema kwamba walitakiwa kulificha jambo hilo lililowapata wanajeshi wale kwanza, ili "mission" yao ya kuwakamata Demba Group ikamilike. Meja na Kapteni wakashangaa. Walitarajia labda Kanali Jacob angekuwa mkali, lakini haikuwa hivyo. Tena akawakumbusha kwamba anajua ni muhimu sana kwa Casmir kuwa na mke wake leo, hivyo waende kujifurahisha, kisha wangerejea ili kupiga kazi kiusahihi zaidi.

Casmir na Kendrick hawakujua ikiwa wangepaswa kushukuru au la, lakini Kanali Jacob akaomba kuongea na Meja Casmir peke yake kwanza, kisha ndiyo wangeondoka. Kwa heshima, Kendrick akamwambia Casmir kuwa angemsubiri ofisini kwake (ofisi ya Kendrick), naye akapiga saluti na kutoka akiwaacha wawili hao humo ndani.

"Meja Casmir..." Kanali Jacob akaita.

"Naam Kanali..." Casmir akaitika.

"Unakumbuka kipindi kile cha zile fujo? Jinsi wanajeshi walivyoweka mgomo na kuharibu mambo mengi sana ya wazungu ili kuwafanya waache kutukandamiza?" Kanali Jacob akauliza.

Casmir akabaki tu kimya na kuangalia chini.

"Hivi kweli tulikuwa tunakandamizwa, au labda walikuwa tu hawaridhiki?" Kanali Jacob akauliza tena.

"Watu... huona mambo kwa njia tofauti na jinsi wengine huyaona. Wengine waliona wanatendewa vizuri, na wengine kinyume. Inapofikia wakati mtu amechukua hatua fulani kwa sababu ya maoni yake, basi huwezi... kuibadili akili yake kwa sababu anaona anachofikiri kuwa sahihi," Casmir akasema.

Kanali Jacob akamtazama kwa tabasamu la pembeni, naye Casmir hakupendezwa na jambo hilo.

"Sikuzote majibu yako huwa unayapangilia au? Ahahah... napenda sana akili yako. Ndiyo sababu General anaku-favour sana. Utafika mbali Casmir. Usipoteze matumaini," Kanali Jacob akamwambia.

"Hapana mkuu, sijapoteza matumaini. Najua maisha yana kusudi. Huko kote tulikopita, tulipo, na tunapoenda, hatuwezi kupanga sisi wenyewe. Wakati mwingine ni muhimu kuwa na imani kwamba kila kitu kitakuwa sawa hata ijapokuwa inaweza ikaonekana kama hakuna njia. Sijui ni kwa nini umenikumbusha jambo hilo, lakini ninakuhakikishia, ipo siku wale WOTE wanaohusika na haya watateketea vibaya sana. Imani tu," akasema Casmir kwa utulivu.

Kanali Jacob akamtazama kwa umakini, kisha akatabasamu na kutikisa kichwa chake.

"Ama kweli wewe ni mtu imara sana. Endelea hivyo hivyo, ipo siku utakaa kwenye kiti hiki... au cha General kabisa," Kanali Jacob akasema kwa njia yenye kejeli kiasi.

Casmir akatabasamu na kusema, "Asante mkuu."

"Okay. Waweza kwenda, najua mke wako anasubiri. Na kumbuka, usiseme kuhusu yaliyot..."

"Ndiyo najua Kanali. Nitafanya hivyo. Asante sana," Casmir akasema na kupiga saluti kwa heshima.

Kisha akatoka ofisini humo na kuelekea mpaka ofisini kwa Kendrick. Bado akili yake ilisumbuliwa sana na njia ya Kanali Jacob ya kufanya mambo. Hakujua ni kwa nini lakini ni kama Kanali alificha kitu fulani, ila hangeweza kutambua ni nini hasa. Akamkuta Kendrick akiwa amesimama na kijana fulani nje ya mlango wa ofisi yake, aliyekuwa kama msaidizi wa Kanali Jacob, ambaye pia alikuwa akiondoka jengoni hapo. Casmir akamwambia Kendrick waondoke upesi sasa ili kuwahi kule, na bila kuchelewa wakaelekea kwenye gari lake.

★★★

"Huyo kijana ndiyo amekwambia hivyo?" Casmir akamuuliza Kendrick wakiwa mwendoni.

"Ndiyo. Amesema eti Kanali ana mkutano muhimu na watu fulani hapo ndo' maana hajaondoka mpaka sa'hivi," Kendrick akasema.

"Na ndiyo maana ni kama watu wote wamewafukuza. Hao watu watakuwa nani?" Casmir akauliza.

"Sijajua. Ila kuona kwamba sisi hatujui inamaanisha ni watu special, sisi mtumba," akasema Kendrick.

"Yeah."

"Kwa hiyo sisi ndiyo wakatuona makolo sana au? Kwamba tusijue kuhusu hilo?" akauliza Kendrick.

"Ahah... sidhani kama inajalisha. Kanali Jacob... ni mtu mtata sana. Kuna vitu vingi ambavyo anaficha. Na hiyo inakwambia kwamba kuna ishu nyingine itafanyika, labda hata ni viongozi wengine wanakuja kujadili hili suala tunaloambiwa tupige kimya kulihusu. Sisi tusubirie tu kupewa order... au labda kutimuliwa," akasema Casmir.

Kendrick akacheka kidogo. Casmir akaichukua simu yake ili kuiwasha, lakini haikuwaka.

"Aaagh... simu yangu imeshiwa chaji saa ngapi? Imezima halafu sijamtext Alice, yaani atanitafuna mzima mzima nikichelewa bila taarifa aisee. Mpigie basi hapo mwambie tupo njiani. Mwambie pia tulikuwa tumepitia zawadi kwa ajili yake ndiyo maana...."

"Aah shit!" Kendrick akamkatisha Casmir.

"Vipi?" Casmir akauliza.

Kendrick alikuwa anatafuta-tafuta kitu fulani mifukoni.

"Nafikiri nimesahau simu yangu ofisini," akasema.

"Dah! Uliingia na ofisini? Basi siyo mbaya..."

"Naihitaji kaka..."

"Uifate? Si utaikuta kesho?" Casmir akasema.

"Hamna bwana, naihitaji. Usifikiri ni wewe peke yako ndiyo unapenda ku-chat," Kendrick akamwambia kiutani.

"Ulishawahi kuniona na-chat?"

"Mm... unajikana eti? Hapo ukikuta Alice anakwambia uwahi ili akakupe malavii hadi maudende yanakutokaga heheheee..." Kendrick akatania.

"Ahahahah... mbwa wewe."

"Geuza bana niifate."

"Acha hizo Ken... unajua nawahi birthday ya Alice. Tumeshachelewa tena unataka niirudie simu yako... kisa ku-chat tu! Utaikuta kesho bwana..."

"Hamna siyo kihivyo Meja... sema... kuna jambo la muhimu nahitaji kufanya kwa simu ndiyo maana..."

"Nini? Umeshampatia Margaret au siyo?"

"Ahahahah... achana na habari zake huyo. Ila ni muhimu sana. Fanya kuniacha hapo hivi nichukue boda nirudi kule fasta..."

"Unajua hawaruhusu kufika maeneo yale na boda, umechanganyikiwa?"

"Hatutafika pale kabisa bana... ananifikisha pembeni natembea kwa guu mpaka kule."

"Mh! Yote hiyo kwa ajili tu ya simu? Si ungesubiri mpaka kesho ina maana ni muhimu kiasi hicho cha huo usumbufu wote?"

"Ndiyo kaka ni muhimu."

"Dah! Ahahah... haya bwana. Me yangu masikio nitajua tu ni nini."

"Ufe!"

Wote wakacheka, kisha Casmir akaegesha gari usawa wa sehemu ambayo ilikuwa na shughuli-shughuli za watu. Marafiki hawa wakaagana vizuri huku Kendrick akisema angejitahidi kuwahi kwenye sherehe ya Alice, kisha akashuka na kumsindikiza Casmir kwa macho alipoondoka eneo hilo. Akaangalia eneo hilo na kufanikiwa kuona taxi upande wa pili wa barabara, hivyo akafata moja na kuingia; akimwambia dereva ampeleke eneo fulani ambako angemwelekeza jinsi ya kufika.

Baada ya mwendo wa dakika kadhaa, dereva akawa anatambua walikuwa wakielekea kwenye makao ya kijeshi, hivyo akaonya kwamba asingeweza kumfikisha kule kabisa. Kendrick akamwambia asihofu kwa kuwa yeye ni mwanajeshi, na angemwelekeza sehemu nzuri ya kuegeshea ili asije akajikuta anaingia sehemu hiyo iliyozuiliwa na hivyo kukamatwa kimakosa. Wakiwa wanakaribia huko, Kendrick aliweza kuona gari mbili nyeusi zikiwa karibu na jengo lile. Akamwambia dereva asimame haraka, kisha akamlipa na kushuka.

Taxi ikaondoka, naye Kendrick akaanza kuelekea huko kwa umakini. Hakujua ikiwa kulikuwa na shida wala nini, lakini alielewa kwamba hakutakiwa kuwepo hapo kwa sababu aliambiwa kwamba mkutano huu uliwahusu wakubwa wake tu, hivyo akawaza kwamba labda ingeleta shida kama angeonekana tena hapo. Lakini akaamua tu kutowaza mambo mengi mno na kwenda pale kwa sababu kihalisi shida yake ilikuwa ni simu tu, kwa hiyo angeichukua na kuwahi birthday ya mke wa rafiki yake.

Baada ya kufika karibu na mwingilio wa eneo la jengo lile, akakuta wanajeshi wawili aliowajua vizuri wakiwa wanalinda bila shaka, na gari tatu nyeusi; mbili aina ya V8, na moja aina ya TOYOTA MARK X zikiwa pembeni. Aliweza kutambua kwa kuzipiga macho haraka kwamba V8 moja kati ya hizo ilikuwa na kibendera kidogo cha kupamba mbele ya gari, hivyo wazo la kwanza la mmiliki wake ingekuwa ni mtu kutoka serikalini na siyo jeshini; ingawa hakuwa mwenye uhakika na hilo. Akawasogelea wajeshi wale, nao wote wakapiga saluti ya heshima kwake; na yeye vile vile. Akataka kuwapita, lakini wakafanya kama kumzuia.

"Samahani mkuu. Tumepewa amri kuwa hatupaswi kuruhusu yeyote kuingia hapa," mmoja wao akasema.

"Ndiyo najua. Lakini kuna kitu cha muhimu sana nimesahau ofisini kwangu. Ninakwenda kuchukua kisha naondoka haraka," Kendrick akasema.

"Hiyo itakuwa kuvunja amri ya mkuu Kanali. Tusamehe sana lakini hakuna uwezekano wa kukuruhusu kupita..."

"Mimi ni superior kwenu. Mnajua hilo. Kwa nini mnanizuia wakati ninaweza kuwapa amri na mtapaswa kuifuata?"

"Hapana mkuu, siyo kihivyo. Ni kwamba amri ya Kanali ni ya juu zaidi... Hata Luteni amesema tuhakikishe hakuna kitu kinaingia hapa, hivyo ni lazima amri itekelezwe."

"Luteni? Luteni Weisiko yuko hapa?" Kendrick akashangaa.

Wanajeshi wale wakatazamana, kisha wakamwangalia tena Kendrick.

Kendrick akajua bila shaka kulikuwa na mambo mengi ya siri yaliyoendelea hapo mpaka kufanya yeye azuiwe na watu ambao alipaswa kuaminiana nao, na mtu mwingine ambaye alikuwa chini yake. Lengo lake kufika hapa ilikuwa ni simu, lakini sasa akataka kulazimisha mambo ili ajue kilichoendelea hasa.

"Jamani... sijui niwaambieje. Ninahitaji sana kuingia ofisini kwangu... nimeisahau simu yangu. Kuna dada yangu yuko mkoa mwingine anajifungua leo, nahitaji kujua hali yake kwa sababu mtoto amekuja kabla ya wakati..." akadanganya.

"Si utumie simu ya mtu mwingine umpigie mkuu?"

"Ndiyo hicho sasa. Mimi sijaikariri namba ya kule na waliopo huko bila shaka wananitafuta kwa kuwa mimi ndiyo wanategemea nigharamie kila kitu. Nahitaji kujua mambo yanayoendelea huko kwa sababu nimeondoka upesi ili niwahi kufanya malipo lakini kwa bahati mbaya nikawa nimesahau vitu vyangu kwa sababu ya haraka. Ninawaomba mnisaidie siyo kama Kapteni wenu ila kama kaka na mzazi hapa... tafadhali..."

Kendrick alibuni uwongo huu haraka-haraka kiasi kwamba akawa hajawapa nafasi nzuri ya kukaa kutafakari mambo kwa kina kuelewa kuwa alikuwa anawadanganya tu.

"Goko... eeh... Rama... nisaidieni basi. Nahitaji kwenda kuchukua haraka. Kama vipi twendeni wote... au mmoja wenu anipeleke nichukue halafu niondoke... maana hata hivyo wengine si wako upande mwingine wa ofisi? Kwa hiyo tunafanya tu upesi halafu naondoka... come on guys..." akawashawishi.

Ilikuwa rahisi kwao kukubali maneno yake hasa kwa kuwa walimfahamu akiwa kiongozi hapo na alionyesha unyonge ijapokuwa yeye alikuwa mkubwa wao kiumri na hata kwa vyeo. Hivyo, Goko akamwambia Rama amsindikize Kapteni mpaka ofisini kwake ili achukue vifaa vyake haraka na kurudi naye ili hata ikitokea ameonwa basi awe karibu yake kusema alikuwa akimwangalia. Kendrick akashukuru, kisha akaanza kuongozana na Rama kuelekea ndani kule. Wakiwa wanaenda aliangalia mazingira ya hapo, naye hakuona mtu mwingine akilinda eneo la hapo; kana kwamba haikuwa sehemu ya kijeshi kabisa.

"Wanajeshi wote wa ulinzi wameondolewa?" Kendrick akauliza wakiwa wanaelekea ndani.

"Ndiyo. Luteni alituweka sisi tu na wengine wa kwao," Rama akajibu.

"Kwa hiyo amefika Luteni Weisiko, Kanali, na nani mwingine?" Kendrick akauliza.

"Wengine siwajui. Walikuwa watatu wote wamevaa suti. Ila kati yao kuna mbaba mwingine mnene nafikiri nilishawahi kumwona lakini sijui wapi tu..." akasema Rama.

"Viongozi viongozi..." akasema Kendrick kiudadisi.

"Inawezekana."

Kendrick akahisi ni kama Rama anaficha jambo fulani, ila anajifanya kila kitu kiko sawa.

"Nilifikiri anakuja Jenerali Pingu... kumbe wengine kabisa..." Kendrick akajifanya anajisemea.

Rama akabaki kimya akitembea sambamba naye.

Walifika kwenye ofisi ambayo ndiyo ilikuwa ya Kapteni Kendrick mwenyewe, naye akaingia na kumwacha Rama nje ya mlango. Alipofika mezani akachukua simu yake haraka, kisha akafikiria afanye nini ili aweze kufika sehemu waliyokuwepo watu wale ili ajue ni nini kilichoendelea. Akaikoki vizuri bastola yake na kuiweka kwenye mkanda wa kiuno chake, kisha akasogea mlangoni na kusema kwa sauti ya chini, "Rama, njoo mara moja kijana wangu."

Rama akiwa anafikiria labda mkubwa wake huyo alihitaji msaada na jambo fulani, akaingia upesi na kukuta pakiwa tupu sehemu hiyo ya ofisi. Lakini ghafla akahisi kitu fulani kimempiga na kwa mbali alihisi maumivu nyuma ya shingo yake, na papo hapo akalegea na kupoteza fahamu. Ilikuwa ni Kendrick ndiye aliyempiga hivyo, akiwa amejibanza nyuma ya mlango muda ule alipomwita kijana huyu. Akamvuta mpaka kwenye kona pembeni na kumlaza hapo, kisha akaichukua bunduki yake (ya Rama) na kuiweka ndani ya kabati yake na kuifunga kwa funguo.

"Nisamehe kijana wangu... lakini ni lazima nijue ukweli."

Kendrick akanena hivyo, naye akaitolea simu yake sauti, kisha akatoka kwenye ofisi yake na kuifunga kwa funguo kabisa. Akaanza kuelekea upande wa jengo ambako alijua bila shaka kikao hicho kilifanyikia, yaani ofisi ya Kanali. Hawakuwa wameachana sana kiofisi, hivyo ilikuwa rahisi kuifikia. Alipokaribia aliwaona wanaume wanne wakiwa wamevalia suti, pamoja na Luteni Weisiko, na kwa haraka akajibanza ukutani ili wasimwone. Akawachungulia tena ili kuwasoma vizuri, na upesi akatambua wale walikuwa walinzi maalumu wa mtu, au watu hawa muhimu waliokuja.

Kwa kuwa haingewezekana kuwapita hapo, na alijua bila shaka Goko kule nje angeanza kuona yeye na Rama wanachelewa, akatumia njia mbadala ili kuweza kufikia chumba kile. Kwa sababu alikuwa ametumia siku yake ya kwanza kufika kwenye jengo hili kulifahamu vizuri, alijua kwamba ofisi ya Kanali ilikuwa na uwazi juu ya dari, uliozibwa kwa njia fulani ambayo angeweza kufungua ikiwa angekuwa kwa juu. Hii ndiyo ilikuwa kama njia ya ziada ya kupitisha hewa, hivyo ikiwa angeweza kuingia humo basi angepata kusikiliza maongezi ya kikao hicho.

Upesi akatoka hapo na kuelekea upande mwingine uliokuwa na ngazi ili aelekee juu kisha atumie njia nyingine kufika juu ya dari la ofisi hiyo. Alitumaini kwamba hakuwa amechelewa sana, na kwamba kwa vyovyote ni lazima tu kulikuwa na nuksi hapa katikati. Mambo ambayo Casmir alimwambia kuhusu utendaji wa viongozi wao yalikuwa ni kweli, na ijapokuwa alimwambia kwamba walitakiwa tu kufanya wajibu wao na kufuata amri, alitaka sasa pia kujua mambo mengi sana yaliyoonekana kuwa na utata ndani yake.

Baada ya kufika kule juu, akafanikiwa kupenya ndani ya njia zile na kuingia mpaka sehemu ya karibu zaidi na chumba cha ofisi ile. Aliweza kuwaona wanaume wale wanne waliolinda pale nje ya mlango kutokea alipokuwa, pamoja na Luteni Weisiko, lakini akawapuuza na kujitahidi kusogea karibu zaidi kwa umakini wa hali ya juu. Kupitia njia hiyo iliyokuwa na matobo madogo kiasi, alianza kusikia sauti za watu humo ndani zikiongea pamoja kuhusiana na operesheni fulani ambayo hakuweza kuelewa kikamili ilikuwa nini.

"...lakini una uhakika tunaweza kumwamini huyu kijana katika hili?" mmoja wa watu hao akasema.

"Ndiyo. Asilimia mia," ikajibu sauti ya Kanali Jacob.

"Unajua hatuwezi kuafford makosa. Mipango yote imewekwa kwa umakini wa hali ya juu. Kinachobaki sasa ni kuhakikisha wote waliohusishwa wafutwe... hiyo inatia ndani na huyu kijana," ikasema sauti nyingine.

"Hapana mheshimiwa. Ninaelewa process nzima. Lakini nakuhakikishia, Weisiko hatakuwa tatizo. Wale wengine ndiyo tutakaowafuta kwa sababu wako keen sana na Jenerali. Tukiwamaliza hao ndiyo mambo yatakwenda bila shida kabisa..." akasema Kanali.

Kendrick akatilia mkazo maneno hayo. Kanali Jacob alimaanisha nini kwamba wengine wafutwe isipokuwa Luteni Weisiko? Mipango gani iliyokuwa ikiendeshwa kinyume na utaratibu ambao hawakutaka Jenerali Pingu afahamu? Na hawa watu ambao Kanali aliwaita "mheshimiwa," walikuwa ni akina nani? Wakati akiendelea kujiuliza, akasikia sauti ya mmoja wao ikisema, "Mwite." Akatega sikio vizuri zaidi na kusikia sauti ya mlango ukifunguliwa kisha kufungwa.

"Kazi uliyokabidhiwa ilikamilika jana. Kuna changamoto zozote zilizotokea kinyume na mpango mzima?" Kanali Jacob akasikika akisema hivyo.

"Hapana mkuu," Luteni Weisiko akasikika akijibu.

Sasa Kendrick akatambua aliyeingia alikuwa ni yeye.

"Umekuwa ukifanya kila jambo uliloambiwa kufanya, na mengi yamefanikiwa kwa msaada wako. Tunajuaje hautatugeuka mbeleni Luteni?" sauti ya "mheshimiwa" ikasikika.

"Mimi pia ninataka kile kile mnachotaka. Kila mtu anajua kupanda ngazi ni muhimu ili kufika juu, kwa hiyo niko tayari kufanya lolote chini yenu ili nifike juu. Na ikiwa nitashindwa, basi maisha yangu mnayo nyie," akasema Luteni Weisiko kwa uhakika.

Sauti za vicheko vya kuridhika vikasikika.

"Mnaona? Jamaa yuko vizuri sana. Anaelewa sehemu itakayompa faida ni ipi," akasema Kanali Jacob.

"Indeed. Sisi tuna motto moja. Maneno yakatwe, kazi ifanywe. Tunachotaka ndani ya masaa 24 ni kwa wale wote WALIOONA ile kitu watoweke. Sijali ni nani, ni wangapi, na wako wapi. Hakikisha unawamaliza wote kabla ya kesho kutwa, do you understand?" ikasikika sauti nyingine ikiongea kwa uzito.

Sauti hii haikuwa ngeni sana kwenye masikio ya Kendrick, lakini akawa bado hajatambua ni nani.

"Ndiyo mheshimiwa, imeeleweka. Jenerali Pingu anajifanya anajua sana kukaza, sasa atalazimika kulegeza tu," akasema Kanali Jacob.

"Mipango ya kesho?" ikauliza sauti ya "mheshimiwa."

"Kila kitu nyendoni. Mimi na Luteni Weisiko tuna vijana wetu watiifu ambao wako tayari kufa kwa ajili yenu wakuu. Kwa hiyo nyie mtakachotakiwa kufanya ni kunyoosha tu miguu na kuangalia maua mazuri yakimeremeta," akasema Kanali Jacob, nao wote wakacheka.

"Silaha za leo zimepita pia tayari?" akauliza mwanaume mwingine.

"Mapema. Kesho kazi inaanza," akajibu Luteni Weisiko.

"Na target wako wa kuwaondoa kimya kimya unawajua vizuri?"

"Nyayo mpaka nywele. Walikuwa 9, tayari nimeshawaondoa. Nimebaki na Meja na Kapteni kwa kuwa wenyewe ndiyo walilazimisha mizigo ile ifunuliwe, lakini Kanali akahakikisha hawasemi lolote kwa Jenerali. Ila sasa nitahakikisha hawasemi lolote tena milele!" Luteni Weisiko akasema.

Kendrick alibaa! Alishtushwa sana na kile alichosema Weisiko kiasi kwamba akajigonga hapo juu.

★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★

Usikose mwendelezo wa simulizi hii kali ya FOR YOU. Njoo WhatsApp or Inbox for full season 1, 2, & 3.

WhatsApp +255 787 604 893
 
FOR YOU

Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Uhalifu, Mauaji, Visasi, Vita, Mambo yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA KUMI NA MOJA

★★★★★★★★★★★★★★★★

Kendrick akatulia kidogo akisikilizia ikiwa walikuwa wamemsikia alipojigonga, lakini wakaendelea kuongea tu.

"...mpumbavu anajiona sana anajua kutoa lecture za maisha. Ni vyema wamerudi huku, hii kazi kwa Luteni itakuwa rahisi zaidi...."

Kanali Jacob akawa anaendelea kuzungumza tu, naye Kendrick akaanza kujirudi taratibu nyuma ili aondoke hapo haraka. Hakujali tena kilichoendelea baada ya kutoka hapo, kwa kuwa alijua alikuwa amepangiwa kifo pamoja na rafiki yake ndani ya saa 24. Hivyo alipaswa kuhakikisha anamwonya Casmir upesi kisha wamwambie na Jenerali Pingu pia kuhusu haya yote.

Akafanikiwa kufika chini kule na kuanza kuelekea nje, na alipokaribia pale aliposimama Goko, akaanza kujifanya kama ameumia hivyo akawa anachechema. Baada ya Goko kumwona, akamwahi na kuanza kumuuliza nini kilitokea maana yeye na Rama walikuwa wamechukua muda mrefu mno; na Rama alikuwa wapi. Kendrick akamdanganya kwamba kuna shida kule ndani, kwamba inaonekana kuna mtaalamu wa mauaji ya kimya-kimya (assassin) aliyeingia na kutaka kuwadhuru, lakini yeye akafanikiwa kumponyoka, hivyo Goko awahi ili kutoa msaada maana waliopo kule bado wanahangaika naye.

Goko akatoka nduki na bunduki lake akiwahi kwenda kutoa msaada, akiwa ameamini kabisa kile ambacho Kapteni wao huyu alikuwa amesema, naye Kendrick akaharakisha mpaka kwenye magari yale pale nje na kuanza kuangalia kama kuna mlango ulio wazi. Yote yalikuwa yamepigwa funguo, hivyo, akiwa kwenye Mark X ile nyeusi, akavunja kioo na kuifungulia kwa ndani, kisha akaingia na kuanza kujaribu kuliwasha gari kwa kuziunguza nyaya za "ignition system." Akafanikiwa kuliwasha na kuliondoa hapo haraka sana, akiendesha kama anashindana vile!

Kendrick alichoka sana kiakili. Akaanza kuyarudia tena maneno ya watu wale aliyotoka kusikia, na baada ya kutafakari kwa kina, akawa ameitambua sauti ile iliyotoa amri ya kwamba yeye na wengine wafe kabla ya kesho kutwa kufika. Ilikuwa ni sauti ya Makamu wa Raisi, a.k.a mheshimiwa Paul Kalebu Mdeme. Akajiuliza maana yao kufanya yote haya ilikuwa ni nini. Alihofia mambo mengi mno; hasa familia zao.

Akatoa simu yake upesi na kupiga namba ya Casmir ili aweze kumwonya mapema kuhusu mambo yote aliyosikia, lakini akawa hampati. Alijaribu sana mpaka kumbukumbu ilipomjia kuwa simu ya Meja wake huyo ilikuwa imezima, kwa hiyo huenda alikuwa ameshafika nyumbani na kuiweka moja kwa moja ipate "charge." Akaamua kupiga namba ya Alice, nayo ikaita. Hakupokea mara ya kwanza na ya pili, lakini ya tatu akapokea.

"Alice..."

"Yaani wewe mbwa wewe ndiyo ukaamua kutokuja leo eti? Nikikata simu hapa usinisemeshe tena kamwe..." Alice akaongea kimasihara upande wa pili.

"Alice... nisamehe sana shemeji kwa kutofika. Lakini nahitaji kuongea na Cas sasa hivi! Ni muhimu sana tafadhali..." Kendrick akasema kwa presha.

"Kuna tatizo gani?" Alice akauliza.

"Ni kuhusu maisha yake... yako hatarini. Please mpe simu muda hautoshi..."

Kukawa na sekunde kadhaa za ukimya, kisha sauti ya Casmir ikasikika...

"Ken vipi?"

"Kaka ondoka haraka sana hapo! Mambo yamechacha..." Kendrick akasema.

"Kuna matatizo gani tena? Mbona umemfanya Alice ameogopa sana?"

"Samahani. Lakini maisha yako... labda hata ya familia yako nzima yako hatarini. Kaka, Kanali amefanya mpango kutuua mimi na wewe ndani ya masaa 24!" Kendrick akamwambia.

"Nini?" Casmir akashangaa.

"Ondoka haraka sana hapo maana tunavyoongea hivi inawezekana wameshaanza ku-move..."

"Ken, subiri. Nini... umetoa wapi taarifa hizi maa..."

"Nisikilize Casmir! Hakuna muda wa kuanza kuuliza maswali. Fanya haraka sana utoke huko. Hakikisha unaondoka na familia yako hata ukihitaji kuwaburuza sawa tu lakini mwondoke haraka. Nitakueleza kila kitu. Niamini Meja..." Kendrick akasema kwa heshima.

Simu ilikatwa, naye Kendrick akawa anatumaini kwamba Meja Casmir alikuwa amemwelewa vyema na kuanza harakati za kuondoka haraka sana. Kwa mbali aliweza kusikia mlio wa helicopter, naye akawa makini zaidi kwenye kuendesha huku anaangalia juu ili asije kutunguliwa kutokea angani. Alikokuwa anawahi ni kwenye nyumba yake, ambako aliishi mama yake na wasichana wale wawili ambao walikuwa ni ndugu wa kiukoo.

Baada ya mwendo wa kama nusu saa, alifika maeneo ya nyumba yake na kuliegesha gari nje. Akawahi mpaka getini na kuanza kugonga kwa fujo akiwaita wadada wale ili wafungue upesi. Mlango mdogo wa geti ukafunguka, naye akaingia ndani haraka akimpita dada mmoja hapo ambaye ndiye alimfungulia, na akiwa anashangaa kwa nini kaka anapita kama anakimbizwa. Kendrick alifika mpaka ndani na kwenda moja kwa moja chumbani kwa mama yake, kisha akamwamsha akisema walihitaji kuondoka haraka sana.

Mama yake alikuwa anamshangaa mno, hasa ukitegemea ilikuwa usiku na hakujua mwanaye alikuwa anataka waende wapi. Akamuuliza tatizo lilikuwa nini, lakini Kendrick akamwambia tu kwa ufupi kwamba ikiwa wangeendelea kukaa hapo basi wangeuawa. Wadada wale wawili walikuwa mlangoni wakitazama mambo haya, naye Kendrick akawageukia na kuwaambia wamsaidie mama yake kujiandaa haraka ili waondoke kwa kuwa maisha yao yalikuwa hatarini. Akawaambia akihakikisha amewapeleka sehemu salama zaidi, ndiyo angeanza kufanya jitihada za kupambana na watu waliotaka kumdhuru.

Upesi akaelekea chumbani kwake haraka akiwaacha wanawake wanajiandaa. Aliwaambia wasibebe makolokolo yoyote bali wavae tu nguo nadhifu na yeye angeenda kuwapatia kila kitu walichohitaji mbele ya safari. Akiwa anaweka vitu vichache vya muhimu kwenye begi lake dogo, simu yake ikaita. Ilikuwa ni Casmir ndiye aliyepiga.

"Meja..." Kendrick akasema baada ya kupokea.

"Ken, tumeshatoka kule, lakini Alexandra hatuko naye," Casmir akasikika upande wa pili.

"Nini? Amekwenda wapi?" Kendrick akauliza.

"Alitoka kwenda kukutana na rafiki zake, lakini tumemtafuta na kumwambia asirudi nyumbani ila atukute kule kwenye ile nyumba ya mjomba wangu ya zamani... si unapakumbuka?"

"Ndiyo napakumbuka..."

"Basi nilikuwa nafikiri na wewe uje tukutane huko ili tupange mambo vizuri, halafu tuhakikishe tunawapeleka mahala salama zaidi..."

"Sawa kaka, nitafanya hivyo. Lakini Sandra akichelewa je? Umemwambia uzito wa suala hili?"

"Ndiyo nimemwambia na amesema ameelewa. Ana akili, ninajua atawahi..."

"Okay basi, na sisi tunaelekea huko sasa hivi. Umeongea na Jenerali kuhusiana na haya tayari?"

"Bado. Familia kwanza Kendrick. Wakiwa salama ndiyo tutajua jinsi ya kushughulika na hao washenzi. Wahi tafadhali..."

"Ondoa shaka Meja..."

Casmir akakata simu.

Kendrick akajisawazisha na kujiuliza ikiwa kuna jambo lolote la muhimu alisahau. Hapana. Alipoangalia kabati yake tena, akatuliza macho yake hapo kwa sekunde chache, kisha akavua begi na shati lake na kwenda kuifungua. Akatazama kwa makini ndani hapo, kisha akachukua vazi lingine na kuvaa, halafu akavaa na jaketi jeusi kwa juu. Akabeba begi lake na kutoka chumbani kuelekea sebuleni ili aondoke na wapendwa wake, pale aliposimama ghafla baada ya kukuta jambo lenye kushtua sana.

Luteni Weisiko alikuwa amefika. Alikuwa amesimama nyuma ya mama yake Kendrick, huku ameweka bastola nyuma ya kichwa chake. Mama yake Kendrick alikuwa anatetemeka kwa hofu huku analia kwa sauti ya chini. Hofu ilimwingia zaidi Kendrick kwa kuwa wadada wale wawili walikuwa wamelala chini, bila kuonekana kwa damu zozote, na hiyo ikamwambia kwamba walikuwa wamepigwa sehemu fulani mwilini na kupoteza fahamu haraka au maisha kabisa. Pembeni yake Weisiko walikuwepo wanajeshi wengine wawili, mmoja wao akiwa ni yule Goko, nao walikuwa wameelekeza bunduki zao kwa Kendrick.

"Kapteni Kendrick. Habari za wakati huu?" Weisiko akamsalimu.

"Luteni, nakuomba umwache mama yangu," Kendrick akamwambia.

"Nami nakuomba utoe bastola yako na kuirusha pembeni Kapteni," Weisiko akamwambia.

"Kwa nini unafanya hivi? Eeh? Unawaumiza watu wasio..."

"Bastola yako. Tupa chini pembeni," Weisiko akamkatisha kwa mkazo.

"Kenddd... hhh... Kennnn..." sauti yenye utetemeshi ya mama yake ikasikika.

Kendrick akatoa bastola yake na kuitupa pembeni. Luteni Weisiko akatoa ishara ya kichwa kwa Goko kuwa amfate Kendrick, naye akatii na kumfata. Akaanza kwa kulitoa begi mgongoni kwake, kisha akampapasa mwili mzima akitafuta kama alikuwa na silaha nyingine lakini akakosa. Kendrick alikuwa anamtazama mama yake kwa huruma, kwa sababu alijua kwa vyovyote vile watu hawa wasingemwacha akiwa hai. Akaanza kujilaumu moyoni mwake kuwa yeye ndiye amemsababishia mama yake mambo haya wakati angetakiwa kumalizia siku za uzee wake kwa amani.

Goko akamwambia Weisiko kuwa Kendrick hakuwa na chochote tena mwilini.

"Kwa mambo yote Kapteni, ninataka tu ujue kwamba hili suala si la kibinafsi. Niko hapa kutimiza wajibu tu," akasema Weisiko.

"Kuua watu wasio na hatia kwa tamaa za kibinafsi za wengine toka lini imekuwa ni wajibu wa mwanajeshi? Nyie vijana wote hamstahili kuitwa watumishi wa nchi hii. Nyie ni mashetani. Na ipo siku... IPO SIKU... yote mnayofanya yatawarudia..." Kendrick akasema kwa hisia sana.

Weisiko akang'ata tu meno yake huku anamwangalia Kapteni wake, na papo hapo akafyatua risasi iliyopasua kichwa cha mama mzazi wa Kendrick mbele ya macho yake. Mwili wake ukadondoka chini kwa kishindo kikubwa. Kendrick alifumba macho yake huku machozi yakitiririka kwa kuhisi huzuni kubwa sana. Kwa mtu mwenye mafunzo ya kivita kama yeye ilikuwa jambo la kawaida kuona watu wakifa, na hata alihusika kuwafundisha wanajeshi kuwa wanapaswa kujikaza sana kifo cha mwenzao kikitokea, lakini kifo kama cha namna hii kilimuumiza sana. Hakuweza kujikaza, akaanza kulia kwa uchungu.

"Nilitaka kufanya mambo kwa njia rahisi. Bila kuumiza mwingine yeyote. Lakini wewe kuja jengoni leo kumebadili hilo. Sina namna nyingine..."

"Huna namna??? Mshenzi wewe!!!" Kendrick akafoka kwa hasira.

Goko akamshika mikono kwa nguvu, na yule mwanajeshi mwingine akawahi kumsaidia. Kendrick sasa akawa anapumua kwa kasi huku akijaribu kujivuta, lakini wakamzidi nguvu kwa pamoja.

"Nakulaani Weisiko... ninalaani kizazi chako chote na yote ambayo unafikiri utayapata kwa kufanya unyama huu... Nilikuwa mwalimu wako... nilikutendea kama mdogo wangu... lakini umechagua ku..."

Kabla Kendrick hajamaliza kuongea, Weisiko akamfyatua risasi kifuani! Akaongeza mbili nyingine zilizompata sehemu ya tumbo na upande wa kushoto wa kifua akilenga moyo. Wanajeshi wale wawili wakamwachia na kumlaza hapo chini baada ya maneno yake kukatishwa kikatili namna hiyo.

"Usisahau kwamba hata mwanafunzi anaweza kuja kumzidi mwalimu... Lala salama... Captain," akasema Weisiko huku akirudisha bastola yake kiunoni.

Luteni Weisiko akatoka ndani ya nyumba hiyo pamoja na wanajeshi wake hao. Wakaenda mpaka kwenye gari walilokuja nalo; Weisiko akiingia na kuketi, lakini wanajeshi wale wakichukua madumu mawili ya mafuta na kurejea kwenye nyumba ile. Walienda na kuanza kuimwagia mafuta nyumba, mmoja nje, mwingine ndani; na baada ya kumaliza madumu yote mafuta, Goko akafyatua risasi kutokea nje kuelekea mlangoni iliyofanya moto mkali uanze kuwaka. Wote wakarudi upesi kwenye gari lao na kuondoka kutoka eneo hilo.

★★★

MASAA MAWILI KABLA YA KENDRICK KUPIGWA RISASI

"Happy birthday to you! Happy birthday to you! Happy birthday, Happy birthday... Happy birthday to you!"

Makofi yalisikika na vigelegele vya shangwe kutoka kwa familia na rafiki za Alice, waliokuwepo kwenye sherehe hii nzuri ya siku ya kuzaliwa kwake. Sasa ulikuwa ni wakati wa yeye kupuliza mishumaa na kutoa maneno ya kile ambacho angetamani kitokee (wish), lakini ijapokuwa alitakiwa kufurahia, hakujihisi vizuri kwa sababu mume wake hakuwa amefika bado. Watu wakawa wanamwambia apulize mishumaa midogo-midogo iliyowaka ambayo iliyozungushiwa kwenye keki yake kubwa, lakini yeye akawa anawaza tu mume wake yuko wapi kwa sababu aliahidi angewahi kufika, lakini mpaka sasa hakuwa amefika.

Watoto wake walimwangalia kwa huruma sana kwa kuwa walijua aliumia mno. Kwa kupoteza matumaini, akaona tu ainame kuelekea keki yake ili apulize, na hapo hapo sauti ikaanza kusikika ikiimba "happy birthday to you." Wote walitazama kutokea getini na kumwona Casmir akiwa amesimama huku anaimba wimbo huo kwa ajili ya mke wake. Wengi walifurahi sana kumwona, hasa watoto wake na mke wake pia. Alice alifurahi mno mpaka machozi yakaanza kumlenga kwani alikuwa amemkosa sana mume wake.

Azra pamoja na Sandra (akiwa ndani ya mwili wa Xander) wakamkimbilia baba yao na kumkumbatia kwa furaha. Kidogo hii ilimshangaza sana Casmir kwa sababu hakutegemea "Xander" angemkumbatia, bila kujua kihalisi aliyekuwa ndani humo ni binti yake. Xander akiwa ndani ya mwili wa Sandra akabaki tu kuwaangalia, nao dada zake wakaanza kutembea pamoja na baba yao kuelekea mpaka aliposimama Alice huku Casmir akimwimbia wimbo huo wa 'birthday,' na mikononi alibeba zawadi kubwa iliyofungwa kwa karatasi za urembo, kisha akaiweka chini na kumwambia Alice, "Make a wish."

Alice akainama kuelekea keki na kuipuliza mishumaa, na marafiki zake wote wakamshangilia sana. Yeye akamkumbatia mume wake kwa furaha sana huku Casmir akiomba samahani kwa kuchelewa. Kisha wakaanza kukata keki kwa pamoja, na wa kwanza kulishwa alikuwa ni Azra. Wakafata mapacha, kisha baba yao, na marafiki zao wote pia. Kila mmoja aliyelishwa alimlisha Alice pia, hivyo alikula keki nyingi sana.

Casmir hakuwa amechelewa mno kwani hata chakula walikuwa hawajala bado, hivyo ni wakati huo ndipo watu wakaanza kufata misosi huku wakiburudishwa na muziki. Casmir alikuwa akiongea na baadhi ya watu waliofahamiana naye sana, na baada ya hapo akaenda kuketi pamoja na familia yake ili wapate chakula na vinywaji pamoja. Maongezi yao yalitawaliwa zaidi na Azra, Sandra (ndani ya mwili wa Xander), na Alice. Xander akiwa ndani ya mwili wa Sandra hakuzungumza sana, na hii ilikuwa mpya kwa Casmir kwa sababu alizoea Sandra kuwa mchangamfu kwake, lakini sasa Xander ndiyo akawa mchangamfu kwake badala.

"Sandra, nakumbuka competition yenu ni Jumamosi. Najua umeshajiandaa vyema. Sijaisahau na Vaziri yako ipo kwenye gari," Casmir akamsemesha.

Xander akabaki kimya tu akiwa amejisahau kwamba alipaswa kujibu kwa kuwa mwili wa dada yake ndiyo ulikuwa unasemeshwa, hivyo ikabidi Sandra amshtue kwa kutumia akili.

'We Xander! Baba amekusemesha mjibu!' akaongea kwa kutumia kichwa.

Sandra (Xander) akashtuka na kukuta wengine wanamtazama.

"Aaa... ndiyo. Nimeshajiandaa. Asante," akajibu.

"Nitajitahidi kuwepo pia," Casmir akasema.

"Sawa," Sandra (Xander) akajibu.

"Baba, siyo kujitahidi. Ufike bwana. Hii ni muhimu sana kwangu, nahitaji wote mwepo," akasema Xander (Sandra), akiwa amejisahau pia.

"Ahahahah... muhimu kwako? Siyo kwa dada yako?" akauliza Casmir.

"Oh, namaanisha... ndiyo, ni muhimu kwa Sandra... kwa sisi wote. Ataumia sana usipofika, si eti Sandra?"

"Yeah, yeah, nitaumia. Usiache kuja," akasema Sandra (Xander) bila kuwaangalia.

Mbadiliko huu wa tabia kati ya mapacha ulizidi kumchanganya Alice, ambaye bado alikuwa akijiuliza ni nini kilikuwa kinaendelea kati ya wanae hawa. Casmir yeye alikuwa anaishangaa tabia mpya ya Sandra, ya kutojali, bila kujua kihalisi aliyekuwa humo ni Xander.

"Okay. Niliongea na Rojas wakati ule nimeenda Moshi, akaniambia nikusalimu. Unamkumbuka?" Casmir akamwambia "Sandra."

"Ndiyo, namkumbuka," Sandra (Xander) akajibu.

"Ndiyo nani huyo?" Alice akamuuliza Casmir.

"Ni jamaa fulani anaye... em' Sandra mwambie mama yako," Casmir akasema huku akiingiza chakula mdomoni.

Xander akaingiwa na wasiwasi kwa sababu alipaswa kujibu kuhusu mtu huyo asiyemfahamu kwa kuwa wazazi wake walifikiri wanaongea na Sandra. Lakini kabla hajaropoka, msaada ukaingia kichwani kwake...

'Rojas ni mkuu wa TUSA,' sauti ya Sandra ikasikika kichwani kwake.

"Aaam... Rojas ni mkuu wa TUSA. Anajuana na... baba pia... na mimi..." Sandra (Xander) akajibu bila kuwa na uhakika sana.

Alice aliweza kuhisi kuna hali fulani ya sintofahamu hapa katikati, naye akataka kuthibitisha zaidi.

Akamuuliza Sandra (Xander), "Kirefu cha TUSA ni nini?"

Sandra (Xander), akamwangalia kwa ufupi Xander (Sandra), naye Alice akatambua hilo. Kutokea kichwani kwa Sandra alimsemeshea Xander kirefu cha neno hilo.

'TUSA ni Tanzania University Sports Association...'

"TUSA kirefu chake ni Tanzania University Sports..."

'Association!'

"Association," Sandra (Xander) akasema.

Alice akatikisa kichwa kuonyesha ameelewa, akijifanya kama hakuhisi lolote na kuendelea kula tu.

Waliendelea kupata mlo, na baada ya kutosheka wote wakanyanyuka na kuendelea na vitumbuizo vingine vichache kwenye sherehe hiyo. Alice alikuwa akiwatazama mapacha wake mara kwa mara ili kuona matendo yao. Kwa sababu aliwajua vizuri sana, angeweza kuona kwamba walikuwa wamebadilika kwa kiwango fulani kilichomfanya akose amani. Hivyo akaona amwambie Casmir kuhusu jambo hilo ambalo lilikuwa linamsumbua sasa. Akamwomba waende ndani ya nyumba ili wazungumze kwa ufupi. Casmir akafurahi sana akifikiri mke wake anaenda kumwambia ni jinsi gani alivyokuwa amem-miss sana.

Wakafika mpaka ndani na kuelekea kwenye chumba chao. Walipoingia tu Casmir akambana mke wake kwa nyuma huku akiibusu shingo yake kwa fujo nyingi, kitu kilichofanya Alice acheke kwa furaha. Akamgeukia mume wake wakiwa wameshikana kwa ukaribu namna hiyo, kisha Casmir akaanza kumpiga busu ya upendo. Alice aliifurahia busu hii iliyogeuka kuwa denda taratibu, lakini siyo kitu kilichokuwa kimemleta hapa. Baada ya kujitoa mdomoni mwake, akamwambia anataka waongee.

"Kunimiss sana kusifanye tuwaache wengine nje ili tu tujinome huku," Casmir akatania.

"Ahahah... hapana, siyo hivyo. Kuna jambo fulani nahitaji tuzungumzie. Ni kuhusu Alexander na Alexandra," Alice akasema.

"Ndiyo..."

"Unajua... sijui tu nikuelezee vipi, ni kama kuna jambo fulani wanaficha... au wanatuficha..."

"Kwa nini unasema hivyo?"

Simu yake Alice ikaanza kuita. Alikuwa ameishikilia mkononi lakini akaipuuza.

"Behavior zao zimebadilika. Wakati mwingine mpaka wananiogopesha..." akamwambia mume wake.

"Kwani kuna jambo baya wamefanya?"

"Hapana. Ni tabia... yaani... zimebadilika. Nawajua vizuri... na hizi siku mbili wamekuwa wanaonyesha tabia tofauti sana na jinsi ninavyowajua..."

"Umejaribu kuongea nao?"

"Ndiyo nilijaribu kuongea na Sandra lakini alisema kila kitu kiko sawa. Pamoja na yote lakini bado sikuridhika kwa kweli..."

Simu ilikuwa imeacha kuita muda huu, kisha ikaanza tena kuita. Alice akaitolea sauti bila kuangalia mpigaji.

"Labda unawaza kupita kiasi. Am sure wako fine. Jeez yaani hata Xander amenikumbatia leo..." Casmir akamwambia.

"Ndo' hicho Casmir. Hujiulizi inawezekanaje Xander akukimbilie kukukumbatia halafu Sandra abaki kukuangalia tu? Me naona kuna kitu hakiko sawa Cas..."

"Mh... okay usiwaze sana. Tutaongea nao ili kujua mengi zaidi. Lakini sasa weka worries zote pembeni darling... enjoy party yako!" Casmir akasema na kumtekenya kidogo.

Alice akacheka na kumsukuma nyuma kidogo. Simu yake ikaendelea kuita tena.

"Pokea simu, utanikuta nje sawa?"

"Haya..."

Casmir akatoka chumbani hapo na kuelekea kwa wengine. Alice alipoiangalia simu yake, akakuta mpigaji ni Kendrick. Akachekea kwa chini na kusonya kidogo, kisha akapokea huku akitabasamu....

Casmir alifika mpaka nje na kukuta watu kadhaa wakiwa bado wanajifurahisha kwa muziki na vinywaji. Akamwona Azra, ambaye alikuwa amekaa kwenye viti vya nje karibu na mwingilio wa mlango wa ndani akibofya simu yake ya kioo. Akamfata hapo na kumshika begani.

"Baba..." Azra akamgeukia.

"Wewe, hausikii usingizi?" Casmir akamwambia.

"Ahah... hapa mpaka kukuche... ndiyo wamesema hivyo..." Azra akajibu.

"Mmmm... yaani utaweza kweli kukesha? Na unavyopenda kulala hivyo? Halafu kuna baridi kwa nini usivae...."

Kabla hajamaliza kuongea, Alice akafika nyuma yake na kumwambia kwamba Kendrick alikuwa anataka kuzungumza naye. Baada ya Casmir kuona uso wa mke wake ukionyesha wasiwasi, akajua kulikuwa na shida. Akamuuliza ni nini kilikuwa kinaendelea lakini Alice akamwambia tu rafiki yake huyo alisema kuna jambo la muhimu sana alihitaji kumwambia. Akaichukua simu upesi na kurudi ndani ya nyumba haraka, huku Alice akimfuata taratibu.

"Ken vipi?" Casmir akasema baada ya kuiweka sikioni.

"Kaka ondoka haraka sana hapo! Mambo yamechacha..." Kendrick akasema upande wa pili.

Ni wakati huu Alice akawa amemfikia mume wake huku akionyesha sura ya wasiwasi.

"Kuna matatizo gani tena? Mbona umemfanya Alice ameogopa sana?" Casmir akauliza.

"Samahani. Lakini maisha yako... labda hata ya familia yako nzima yako hatarini. Kaka, Kanali amefanya mpango kutuua mimi na wewe ndani ya masaa 24!" Kendrick akamwambia.

"Nini?" Casmir akashangaa.

"Ondoka haraka sana hapo maana tunavyoongea hivi inawezekana wameshaanza ku-move..."

"Ken, subiri. Nini... umetoa wapi taarifa hizi maa..."

"Nisikilize Casmir! Hakuna muda wa kuanza kuuliza maswali. Fanya haraka sana utoke huko. Hakikisha unaondoka na familia yako hata ukihitaji kuwaburuza sawa tu lakini mwondoke haraka. Nitakueleza kila kitu. Niamini Meja..." Kendrick akasema kwa heshima.

Casmir akakata simu, naye akamshika mkono Alice na kuanza kwenda naye chumbani haraka sana. Alice alikuwa haelewi kinachoendelea.

"Alice, kuna jambo fulani haliko sawa. Maisha yetu yanaweza kuwa hatarini... tunahitaji kuondoka haraka!" Casmir akamwambia.

"What? What's going on? Nani anataka..."

"Listen, nahitaji uniamini katika hili. Wakusanye watoto tuondoke haraka sana. Kendrick amenionya kuwa wanaotaka kutuumiza wako karibu, kwa hiyo hatuna muda wa kupoteza. Please Alice... fanya haraka... Azra, mapacha, Salome..."

"Sawa, sawa, nafanya hivyo..." Alice akasema na kutoka chumbani upesi.

Casmir akaanza kuchukua vitu vya muhimu ambavyo angehitaji kwa ajili ya safari hiyo ya ghafla. Kichwani kwake yalipita maswali mengi sana ambayo hayakuwa na majibu sahihi. Kwa nini Kanali alitaka kuwaua? Tena hata na familia yake nzima? Kendrick alitoa wapi taarifa hizo? Ijapokuwa tahadhari hii ilikuja kwa kushtukiza sana, alimwamini Kendrick. Alijua rafiki yake angekuwa na vigezo vilivyojitosheleza vya kuamini kwamba maisha yao kweli yalikuwa hatarini, hivyo jambo la muhimu kufanya ilikuwa kutii onyo hilo haraka iwezekanavyo.

Casmir akiwa anaweka vitu kwenye begi dogo, wakaingia watoto wake pamoja na mama yao. Akashangaa kutomwona Sandra hapo.

"Alexandra yuko wapi?" akauliza.

"Ameondoka baba," akajibu Xander (ikiwa ni Sandra).

"Ameenda wapi?! Xander unawezaje kumwacha dada yako aondoke usiku huu wote?" Casmir akauliza kwa ukali.

"Amechukua tu gari akaniambia ameenda pale kona kuna rafiki yake anakutana naye..."

"Kona wapi?!" Casmir akafoka.

"Casmir, tulia. Cha muhimu sasa tumtafute, tumpate, tuondoke, sawa?" akasema Alice.

"Mama, baba, nini kinaendelea?" akauliza Azra.

"Kuna watu wanataka kutuumiza. Tunahitaji kuondoka upesi ili muwe sehemu salama..." akajibu Casmir.

"Wakina nani?" akauliza Azra.

"Ni wale waasi... Demba Group?" akauliza Xander (Sandra).

"Umemtafuta Sandra?" Casmir akauliza.

"Ndiyo, lakini hapokei simu..." akajibu Alice.

"Eh Mungu wangu!" Casmir akaishiwa nguvu.

"Xander mpigie simu dada yako mpaka apokee... Azra twende kumsaidia Salome kuweka vitu vyetu," Alice akasema.

"Salome yuko wapi? Msiweke vitu vingi sana tusichelewe..." Casmir akasema.

Alice na binti yake mdogo wakatoka na kuwaacha "Xander" na baba yake chumbani humo. Xander (yaani Sandra) akawa anaipigia sana simu yake mwenyewe, kwa kuwa sasa walikuwa wamebadilishana simu na kaka yake kutokana na yeye kuwa mbali naye. Casmir baada ya kukamilisha vifaa vyake muhimu akatoka pamoja na mwanaye na kufika mpaka sehemu ya sebule. Wanawake nao wakaja hapo wakiwa wamebeba mabegi yenye vitu vichache. Baadhi ya watu waliokuwepo sehemu hiyo wakawa wanawashangaa.

"Xander..."

"Bado hapokei mama!" akajibu.

"Casmir... isije ikawa kwamba...." Alice akaishia hapo.

"No, hapana. Yuko sawa. Tutampata tu. Mpigie rafiki yake," akasema Casmir.

Sandra, akiwa kwenye mwili wa Xander, akawaza ni wapi ambapo Xander angekuwa amekwenda. Akasogea pembeni.

"Alice vipi? Mbona kama mnataka kuondoka?" rafiki yao mmoja akawauliza.

"Party imeisha. Jamani... kila mmoja anaweza kwenda nyumbani sasa, party imekwisha. Usiku mwema. Harakisheni," Casmir akaongea kwa sauti ya amri.

Wote waliokuwepo walibaki kushangaa tu, na mmoja baada ya mwingine wakaanza kujiondokea. Baadhi waliwauliza shida ilikuwa ni nini, nao wakawaambia tu kulitokea dharura ghafla. Sandra alitambua sasa baada ya kufikiria sana kuwa Xander hakukutana na "rafiki" yoyote, bali madam Valentina, hivyo akampigia madam ili kuuliza ikiwa bado alikuwa naye. Hakuwa amefanya hivi mapema kwa sababu ya kuchanganywa na hali nzima, ila sasa akakumbuka. Simu ya madam Valentina iliita bila kupokelewa mara ya kwanza, kisha mara ya pili akapokea.

"Hallo... Madam V..."

"Ndiyo... Alexandra mwenye besi..." akasema Valentina upande wa pili.

"Samahani... Xander yuko kwako?"

"Ndiyo..."

"Tafadhali naomba kuongea naye... ni muhimu sana..."

Baada ya sekunde kadhaa...

"Sandra vipi?" Xander akasikika (ikiwa ni sauti ya kike).

"Xander toka huko haraka njoo nyumbani!" Sandra akamwambia kwa sauti ya chini.

"Mzee ameshaanza kumtafuta mdoli wake eeh?"

"Acha masihara. Kuna shida imetokea. Wahi nyumbani sasa hivi..." Sandra akasema kwa mkazo.

"Yeah... actually... sidhani kama n'tarudi leo maana huku mambo ni fire!"

"Xander... maisha yako yapo hatarini! Unapaswa kuni..."

"Xander, umempata dada yako?" Casmir akamkatisha huku anamfata.

Ikabidi akate simu haraka ili baba yake asije kuanza kuuliza "Sandra" alikuwa anafanya nini kwa mwalimu wake usiku huu wote ikiwa angeichukua simu.

"Hapana... ngoja niendelee kumtafuta..." akamjibu baba yake.

"Sasa tunafanyaje?" akauliza Alice.

Kufikia sasa, watu wote walikuwa wamekwishaondoka nyumbani hapo, hivyo Casmir akasema waende tu kwenye gari upesi na Sandra wangempata mbele kwa mbele. Wakawahisha mpaka ndani ya gari lao na kuliondoa hapo haraka sana. Casmir alikuwa ameongea na na walinzi wa nyumbani kwake kuwaambia wafunge nyumba vizuri kisha waondoke pia, naye angewatafuta baadae. Wakiwa ndiyo wameianza barabara tu, simu ya Xander (yaani Sandra) ikaita, na mpigaji alikuwa pacha wake. Akawaambia wazazi wake kwamba "Sandra" alikuwa anapiga sasa, naye Casmir akamwambia ampe Alice apokee kisha aweke sauti ya juu.

"Halloo..."

"Sandra... uko wapi?" akauliza Alice.

"Mama... niko huku kwa..."

"Unawezaje kuondoka bila kusema unakoenda? Una matatizo gani wewe siku hizi? Unajua kwamba lolote baya linaweza kukupata? UKO WAPI?!" akauliza Alice kwa hisia kali.

"Mama punguza jazba... niko kwa rafiki yangu. Kwani shida gani mpaka unafoka hivyo wakati hii siyo mara yangu ya kwanza?"

"Uliaga? Uliaga?"

"Basi Alice, inatosha. Sandra, uko wapi?" Casmir akauliza.

"Niko huku... mitaa siyo mbali sana na chuo..."

"Kote huko umeenda kufanya nini? Oh God... Sandra... nisikilize kwa makini. Kuna watu wanataka kutudhuru, na wanaweza kuwa popote pale muda wowote ule. Nahitaji kuwapeleka kwenye usalama. Sandra unanielewa? Maisha yako yapo kwenye hatari! Nataka ufanye kile ambacho nitakwambia haraka sana..." Casmir akasema.

"Ndiyo baba... nakusikiliza..."

"Unakumbuka nyumba ya babu yako Daudi ilipo? Kule tulipokuwaga tunawapeleka mkiwa wadogo kumtembelea?"

"Mjomba wako yule?"

"Ndiyo..."

"Yeah... napakumbuka. Lakini baba..."

"Nisikie. Nataka uje huko haraka sana. Ndiyo tunakoenda sasa hivi. Usiende nyumbani, na uhakikishe huongei na yeyote kuhusu hili. Sandra unanielewa dear? Harakisha mpenzi..." Casmir akaongea kwa hisia.

"Sawa baba. Nakuja..."

"Sawa," akasema Casmir.

"Kuwa mwangalifu Sandra. Nakupenda," akasema Alice huku machozi yakimlenga.

"Nakupenda pia mama..."

Kisha simu ikakatwa. Ndani ya gari hili walilokuwemo palijaa hali nzito ya wasiwasi. Casmir na Alice walimwaza sana binti yao. Sandra, akiwa ndiye Xander ndani ya gari, alimwaza pia kaka yake ambaye alikuwa mwenye mwili wake. Azra aliogopa, na Salome pia alikuwa na wasiwasi mwingi.

"Casmir... kwa nini usiongee na watu unaofahamu juu ya hili? General Pingu bila shaka anaweza kukusaidia, au marafiki zake wengine ambao..."

"Hapana Alice. Siyo rahisi kama unavyodhani. Sijui wa kumwamini. Ninaweza kuongea na mtu nikifikiri ni msaada kumbe ndiyo tatizo lenyewe. Singetaka kuwaweka nyie hatarini. Nataka kuhakikisha hamfikiwi na yeyote ndiyo nianze kudili na hawa wapumbavu sasa..." akasema Casmir.

"Baba nani anataka kutuua?" Azra akauliza.

"Sijui mpenzi. Lakini watu wanaoshirikiana naye pia tulidhani ni marafiki, kumbe ndiyo maadui. Isingekuwa ya Kendrick sijui ingekuwaje..."

"Kendrick yuko wapi?" Alice akauliza.

"Atakuwa amekwenda kwa mama yake, ndiyo yuko karibu zaidi. Ni yeye tu ndiyo ninayemwamini... wengine wote sijui... yaani sijui imekuwaje hivi... eti Meja nakimbizwa na... ahah... I can't believe this!" Casmir akaongea kwa masikitiko.

Alice na wengine walibaki kimya, wakimwonea Casmir huruma sana.

Waliendelea na mwendo kwa zaidi ya dakika 30 bila kusemeshana lolote, nao wakawa wamefika eneo ilipokuwepo ile nyumba. Azra alikuwa amesinzia pamoja na Salome wakati huu. Wengine waliweza kuona nyumba ile ndogo kiasi ikiwa imetawaliwa na giza, na pembeni mwake hakukuwa na nyumba zingine kwani ilijitenga sana. Pande za huku kulikuwa tu na miti mingi iliyofanya paonekane kama msitu, lakini haikuwa ule wa kina sana.

Baada ya kuwa amesimamisha gari, Casmir akatoa simu yake na kumtafuta "binti yake" tena. Wakaongea, naye Sandra (Xander) akamwambia alikuwa njiani. Baada ya hapo, akaona ampigie na Kendrick ili kumwambia jambo la muhimu pia.

"Meja..." Kendrick akasikika baada ya kupokea.

"Ken, tumeshatoka kule, lakini Alexandra hatuko naye," Casmir akasema.

"Nini? Amekwenda wapi?"

"Alitoka kwenda kukutana na rafiki zake, lakini tumemtafuta na kumwambia asirudi nyumbani ila atukute kule kwenye ile nyumba ya mjomba wangu ya zamani... si unapakumbuka?"

"Ndiyo napakumbuka..."

"Basi nilikuwa nafikiri na wewe uje tukutane huko ili tupange mambo vizuri, halafu tuhakikishe tunawapeleka mahala salama zaidi..."

"Sawa kaka, nitafanya hivyo. Lakini Sandra akichelewa je? Umemwambia uzito wa suala hili?"

"Ndiyo nimemwambia na amesema ameelewa. Ana akili, ninajua atawahi..."

"Okay basi, na sisi tunaelekea huko sasa hivi. Umeongea na Jenerali kuhusiana na haya tayari?"

"Bado. Familia kwanza Kendrick. Wakiwa salama ndiyo tutajua jinsi ya kushughulika na hao washenzi. Wahi tafadhali..."

"Ondoa shaka Meja..." Kendrick akasema.

Casmir akakata simu na kumwangalia mke wake. Alipotazama saa, ilikuwa ni kasoro dakika chache itimie saa 8 kamili usiku. Akamwambia Alice asubiri kwanza ndani ya gari, kisha yeye akashuka na kuanza kuelekea kwenye nyumba ile huku akiwa makini. Mikononi alishika bastola kwa ajili ya tahadhari, naye akazunguka nyumba hiyo kwa umakini akiangalia kama kuna nuksi yoyote. Mjomba wake Casmir, yaani Daudi, alikuwa amekufa siku nyingi na nyumba hii hakumwachia yeyote. Wapo ndugu kadhaa ambao waliendelea kuishi hapo lakini baadae ikaachwa tu bila kuwa na yeyote wa kuitunza kwa sababu ilikuwa ya siku nyingi mno.

Baada ya kuhakikisha pako salama, akarejea kwenye gari na kuwaambia washuke ili kwenda kule ndani ya nyumba. Azra akiwa na usingizi sana akaamshwa pia na kutembea pamoja na wengine mpaka ndani kule. Baada ya kuwa wameingia, walikuta vifaa vingi vikiwa vimechakaa na vumbi likitawala sehemu kubwa. Alice akamuuliza Casmir ikiwa lilikuwa wazo zuri kwenda hapo, lakini mume wake akaweka wazi kuwa sehemu hii ilikuwa salama zaidi kwa wakati huu kwa sababu maadui zao wasingejua wapo huku.

Basi, Salome pamoja na "Xander" wakafanya-fanya usafi wa kadiri sehemu fulani za makochi yaliyokuwa ya zamani sana, kisha Alice akaketi huku Azra akijilaza hapo pia akiwa amemlalia mama yake mapajani. Kwa kuwa walibeba mashuka machache na blanketi, wakayatumia kumfunika Azra na kujifunikia pia mwilini. Casmir alikuwa anawaangalia wote kwa huzuni sana, akiwaza imekuwaje mpaka wakajikuta kwenye hali hii ghafla. Lakini akajifariji kuwa kila kitu kingekuwa sawa; cha muhimu kwanza ni kuwasubiria wakina Kendrick na "Sandra."

Zilipita dakika kadhaa wakiwa hapo, na kufikia wakati huu ni Casmir na Xander (yaani Sandra) ndiyo walikuwa macho bado. Wengine walikuwa wamepitiwa na usingizi kutokana na uchovu wa usiku. Kulikuwa na giza ndani hapo na mwanga pekee uliokuwepo ulitoka kwenye tochi ya simu ya "Xander." Casmir akamtazama mwanaye, ambaye alikuwa ametulia tu kwenye kiti huku amekunjia mikono kifuani.

"Unajua muda mrefu sana umepita, sikuwa hata nimetambua kwamba umenizidi urefu," Casmir akamsemesha.

"Ahahah... ndiyo. Hadi na ndevu nitakuzidi," Xander akatania, ikiwa ni Sandra ndiyo anaongea.

Casmir akatabasamu kidogo, kisha akasema, "Mama yako alikuwa anawaza kuhusu nyie wawili. Anasema hizi siku chache ni kama mmebadilika sana kitabia. Siwezi kujua mengi kwa sababu nakuwa mbali lakini nilitaka tu kujua ikiwa kila kitu kiko sawa."

"Ndiyo baba kila kitu kiko sawa. Ni kwamba tu mama... anatupenda sana kwa hiyo... hata kitu kidogo tu kinamhangaisha," Sandra akaficha ukweli.

Casmir akabaki kimya kwa ufupi, kisha akasema, "Unakumbuka kipindi kile tumeenda Serengeti?"

"Ndiyo! Nakumbuka... ahahah... wakati tumelala kwa tent wale nyani wakaanza kutufanyia fujo jinsi Azra alivyokung'ang'ania yaani..."

Casmir akacheka kidogo.

"Yeah ilikuwa ni kipindi ambacho nilifurahia sana. Kuwa pamoja nanyi. I wish siku zingerudi nyuma wakati ambao nilitumia muda wangu mwingi na nyinyi..." Casmir akasema kwa huzuni.

"Usijali baba. Cha muhimu ni kwamba tunajua upendo wako kwetu haubadiliki... hata ukiwa mbali kiasi gani..." Xander (Sandra) akasema.

"Mhmm... nilifikiri bado ungekuwa unanichukia kwa sababu ya hilo," akasema Casmir.

"Hapana baba... sikuchukii."

"Najua kwa sababu ya... hali tuliyopo... inawezekana... Ulikuwa sahihi kuniambia niachane na hii kazi... nisingeendelea nayo huenda haya yasingetupata..."

"Hapana baba siyo..."

"Ndiyo ukweli Xander. Nimetumia muda mwingi kutumikia wengine, kwa faida gani? Ili familia yangu ije iwekwe shabaha? Hakuna wa kulaumu kuhusu hili isipoku..."

"No baba nisikilize. Haya siyo makosa yako. Sisi sote tunakupenda sana. Inaweza ikaonekana kama Xander anakuchukia, lakini siyo hivyo. Anakuwa anataka tu ujiingize zaidi kwenye maisha yake. Naweza kusema kati ya sisi wote yeye ndiye anakupenda zaidi..."

"Ahah... unavyojiongelea ni kama unasemea mtu mwingine..."

"Aam... yeah, napenda kufanya hivyo. Sote tunakupenda baba. Tunajua utapambana kwa ajili yetu no matter what. Pambana Meja... ninajua utashinda..."

Sandra akiwa ndani ya mwili wa Xander aliongea maneno hayo yaliyomtia sana moyo baba yake. Casmir akafarijika sana na kuhisi amepata nguvu zaidi kwa sababu alifikiri anayemwambia hivyo ni mwana wake ambaye kwa kipindi kirefu alihisi anamchukia.

"Kwa hiyo baada ya hapa tutaenda wapi?" Xander (Sandra) akauliza.

"Mimi na Kendrick tuliwahi kuwa na sehemu fulani iliyojificha chini ya ardhi kipindi kile wahamiaji haramu na waasi wamevamia. Nafikiri hiyo itakuwa ya kuanzia," Casmir akajibu.

"Ahahahah... tutaishi mapangoni sasa..."

"Ndiyo, kwa muda mfupi tu lakini. Na haitakuwa mbaya sana kwa sababu mtapata supply nyingi nzuri tu. Sema roho inaniuma kwa sababu Sandra anaweza kukosa competition yao Jumamosi na alikuwa amejiandaa sana..."

Maneno ya Casmir yalimhuzunisha sana Sandra kwa kuwa baba yake hakujua ilikuwa ni yeye ndiyo yuko hapo. Akaanza kuona ni kama hakukuwa tena na sababu ya kumficha baba yake ukweli wa kile kilichowapata yeye na Xander, hasa ukitegemea hali hiyo hawakujua jinsi ya kuitatua. Akanyanyuka ili amfate baba yake na kumweleza ukweli, pale alipohisi kitu fulani. Akatulia kwanza, na baada ya Casmir kumwangalia, akatambua kwamba mwanaye alikuwa anafikiria kitu fulani. Kisha Casmir akamwonyesha kwa ishara ya kidole kuwa asiseme lolote na ainame chini taratibu. Hii ilikuwa ni baada ya Casmir kusikia hatua za mtu fulani nje.

Baada ya Xander (Sandra) kuinama, Casmir akawa anaelekea dirishani ili kuchungulia nje, akiwa ameishika bastola yake kwa utayari. Akachungulia upande ule ambao aliegeshea gari lake lakini hakuona chochote kulizunguka. Sandra akiwa ndani ya mwili wa Xander akawasogelea mama yake, mdogo wake, pamoja na Salome, kisha akawaamsha polepole akiwapa tahadhari kuwa wakae kimya na kujiweka tayari kwa lolote. Wakajitahidi kuuondoa usingizi na kujiweka tayari, wakimtazama Casmir kwa umakini.

Casmir akahisi hatua zimefikia mlangoni, hivyo akawahi upande huo na kujibanza ukutani, huku akiwapa ishara ya mkono wengine kuwa wasogee mwishoni mwa kona ya nyumba wajifichie hapo. Wote wakatii na kuelekea huko, huku Azra akiwa amemkumbatia Alice kwa hofu. Casmir akaendelea kujibanza karibu na mlango akisubiri jambo fulani litokee, na papo hapo mlango ukagongwa. Akawaza kwamba huenda ilikuwa ni Kendrick au Sandra ndiye aliyefika, lakini bado alihitaji kuwa na uhakika kwa sababu ingeweza kuwa adui. Ila kabla hajafikiria la kufanya...

"Baba..."

Akasikia sauti hiyo ikiita, aliyoitambua upesi kuwa ni sauti ya binti yake kipenzi, Sandra. Alice pia alisikia, naye akaanza kufurahi sana pamoja na wengine.

"Sandra!" Casmir akasema akihisi faraja moyoni mwake.

Alice akatoka pale alipokuwa na kusogea mpaka karibu yake Casmir. Casmir akaanza kuufungua mlango upesi akiwa anataka kumwingiza binti yake ndani haraka, lakini papo hapo, Sandra, akiwa kwenye mwili wa Xander ndani hapo akatoka pale alipokuwa na kusema kwa sauti kubwa...

"Baba subiri!"

Tayari Casmir akawa ameshaufungua mlango na kukuta "binti" yake amesimama huku kichwani kwake akiwa amewekewa bastola! Aliona mkono tu ukiwa umetokezea upande wa ukutani, kisha mwenye mkono huo akajitokeza pia. Casmir akamtambua upesi, naye alikuwa, si mwingine, ila Luteni Weisiko mwenyewe.

"Habari za wakati huu Meja..." Luteni Weisiko akamsalimu.

Casmir alichoka. Alice aliogopa sana na kuanza kulia, huku mapacha nao wakiangaliana kwa huzuni sana....

★★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★★

WhatsApp +255 787 604 893
 
Jamani [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
FOR YOU

Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Uhalifu, Mauaji, Visasi, Vita, Mambo yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA KUMI NA TATU

★★★★★★★★★★★★★★★★

"Mamaaaa!"

Watoto walitoa vilio vya huzuni baada ya kuona mama yao akilegea na kuangushwa chini. Xander akiwa kwenye mwili wa Sandra bado alihisi maumivu tumboni mwake, lakini baada ya kuona mama yake amepigwa risasi alihisi uchungu hata zaidi. Casmir aliona hilo, na kwa sababu ya hasira kali iliyomwingia alitumia nguvu zake zote kumshinda jamaa uwezo na kumnyang'anya bunduki ile, kisha akamtandika risasi kifuani akiwa karibu naye; kitu kilichofanya damu zake zimrukie usoni. Kisha papo hapo akageuka na kufyatua risasi iliyompiga Luteni Weisiko na kumwangusha chini.

Mambo haya yote yalimwogopesha sana Azra. Alikuwa anapiga kelele nyingi sana huku amemng'ang'ania Salome. Sandra akiwa ndani ya mwili wa kaka yake akamfata pacha wake pale chini na kumsaidia anyanyuke, naye Salome akaenda hapo pamoja na Azra. Wote wakawa wanamwangalia mama yao akiwa amelala pale chini, akiwa ametulia tuli. Walilia sana. Casmir pia alikuwa akilia mno, naye akausogelea mwili wa mke wake na kumwangalia kwa huzuni nzito sana.

Watoto walipoanza kumsogelea, akawazuia na kuwaambia waondoke haraka sana.

"Lakini baba..." akasema Sandra (Xander).

"No. Xander, mwahishe dada yako hospitali hilo jeraha ni kubwa. Nahitaji kumwondoa mama yenu hapa. Salome mwangalie sana Azra... nendeni... now!" Casmir akawasihi huku akiwapa funguo za gari lake.

Salome akaanza kuwasaidia Xander na Sandra kutembea, huku Azra akiwa ametangulia mbele na funguo za gari. Walikuwa wakielekea kwenye gari la baba yao huku Casmir akiurudia mwili wa Alice pale chini, na wakati tu walipolifikia sauti ya juu ya mlio wa risasi ikasikika. Ilifuatwa na kilio cha maumivu kutoka kwa Salome, ambaye alikuwa ametandikwa risasi mgongoni kwake. Wote wakaanguka chini, huku mapacha na Azra wakiwa wameshtushwa sana na jambo hilo. Casmir aligeukia upande wa nyumba na kumkuta Goko akiwa amesimama hapo, huku akiikoki bunduki yake kubwa ili afyatue risasi nyingine tena.

Lakini Casmir akaanza kufyatua risasi za kwenye bastola aliyokuwa nayo kumwelekea pia, huku Goko akirudi ndani ya nyumba kujificha ili zisimpate. Mapacha wakanyanyuka ili kuweza kuingia kwenye gari pamoja na mdogo wao, lakini ni hapa ndipo wakasikia mlio wa risasi ukifuatwa na kelele ya maumivu kutoka kwa baba yao!

Wote walipotazama upande huo, waliweza kuona baba yao akiwa amepigwa risasi mgongoni, na aliyemfyatulia alikuwa ni Luteni Weisiko kutokea pale chini. Kumbe wakati ule Casmir alipompiga risasi, ilimpata sehemu inayokaribiana na begani, siyo moyoni kabisa, hivyo hakuwa amekufa bali alipoteza tu fahamu baada ya kuanguka kwa nguvu.

Watoto walibaki kumwangalia baba yao akidondoka chini, na hapo Goko akatoka kule ndani na kuanza kuuelekea mwili wa Casmir pale chini kuhakikisha kama alikuwa amekufa. Xander, akiwa kwenye mwili wa Sandra uliokatwa kwa kisu tumboni, alijua wazi wenyewe ndiyo wangefuata, hivyo akajitahidi kuwaondolea butwaa dada zake ili wakimbie haraka.

Goko alipofika karibu kabisa na mwili wa Casmir, akamtandika risasi nyingine mgongoni kuhakikisha hainuki tena. Watoto hawa watatu sasa wakawa mayatima. Goko akamfata Weisiko ili kumsaidia anyanyuke, lakini jamaa akamwambia awashughulikie kwanza wale watoto na asimpoteze yeyote.

Goko alipowaangalia watoto, aliwaona wakiwa wameingia kwenye gari tayari, na hapo hapo akaichukua bastola ya Weisiko na kuanza kufyatua risasi kulielekea gari hilo; hasa kwenye vioo na matairi. Kwa kuwa gari lilikuwa halijageuzwa bado ili kuondoka, risasi zilipiga tairi na kufanya lisiweze tena kutembea, huku ndugu hao watatu wakiwa wameinama kwa ndani ili risasi zisiwapate. Xander akawaambia wenzake watoke kupitia milango ya upande mwingine, na ni hapa ndiyo akatambua kwamba Sandra alikuwa amechunwa na risasi moja pajani.

Ilikuwa ni shida juu ya shida. Sandra, akiwa ndani ya mwili wa kaka yake akajikaza na kutokea upande wa pili wa gari pamoja na wenzake, nao wakaanza kukimbia kuelekea kwenye miti mingi; ikionekana kama msitu wa eneo hilo. Weisiko akajinyanyua na kuchana sehemu ya nguo ya Alice, kisha akaanza kujifunga sehemu ya jeraha lake akisaidiwa na Goko. Akamwambia hawakupaswa kuwaacha watoto hao watoroke, hivyo upesi wakabeba silaha zao na kuanza kuwafata huko huko.

Baada ya mapacha na mdogo wao kujitahidi kukimbia msituni hapo penye giza kwa sekunde kadhaa, mambo yalizidi kuwa magumu kwao hasa kwa sababu ya mwili wa Sandra (Xander) kuishiwa nguvu kutokana na kisu alichochomwa tumboni. Pacha wake alijitahidi kumkokota hivyo hivyo ili watoroke, lakini Xander alijua angewafanya wakamatwe upesi kwa sababu ya yeye kuwa mzito. Walifika sehemu fulani naye Xander akamwambia Sandra amwache nyuma ili dada zake wakimbie pamoja.

Sandra akawa anakataa, lakini Xander akamshawishi kwa kumwambia ni bora hata kama akifa yeye lakini ndugu zake wawe na nafasi kubwa ya kupona kuliko ikiwa wote watauliwa. Kwa hiyo akamwambia waelekee upande mmoja, halafu yeye atajitahidi kuelekea upande mwingine akiacha viashiria kwa wanaume wale ili wamfate yeye tu. Sandra akiwa kwenye mwili wa Xander alilia sana. Azra alilia pia mno, nao wote wakamkumbatia ndugu yao, kisha akawasihi wawahi haraka maana alijua wale wapumbavu walikuwa nyuma yao.

Sandra akaondoka na Azra kuelekea upande mmoja, kisha Xander, akihisi udhaifu mkubwa sana kwa sababu ya kupoteza damu nyingi kwenye mwili wa dada yake, akajitahidi kulivua sweta alilopewa na Valentina, kisha akapiga hatua chache kuelekea upande mwingine na kuliangusha chini makusudi, ili wale watu wakiliona upande huo waendelee kuufuata huo huo. Alijikongoja kilegevu tu huku akitumaini dada zake wangefika mbali sana, kwa sababu alijua yeye asingeweza. Akafika sehemu fulani na kujikalisha chini ya mti akiugulia maumivu makali ya kidonda chake kikubwa tumboni.

Weisiko na Goko walikuwa wamefika sehemu ile na kuliona sweta pale chini, na upesi Goko akamwambia Luteni wake huyo kwamba watoto watakuwa upande huo, hivyo wawawahi. Lakini Weisiko akamzuia kwanza. Kutokana na mafunzo yake, aliweza kubaini kwamba huo ni mpango wa kuwachengua, na kwa haraka akakisia kwamba watoto walijigawa na kwenda pande tofauti. Akaangalia upande ule ambao Sandra na Azra walielekea, naye akamwambia Goko afatilie ule ambao ulikuwa na sweta pale chini, halafu yeye angeenda huu mwingine. Balaa!

Goko akaanza kuelekea kule alikoenda Xander, huku Luteni Weisiko akitoka kwa kasi zote kuelekea kwa dada wale wawili. Goko alifika mpaka sehemu ya msitu ambayo ilimchanganya sana na hakujua aelekee wapi tena. Akawa anaangaza huku na huko akitumaini kuona jambo lolote, hasa kwa sababu alikuwa ameyazoesha macho yake giza la msitu. Kutokea aliposimama, mti wa nyuma yake ndipo alipokuwa amekaa Xander, na alikuwa akijikaza ili asitoe sauti yoyote ile, na akiomba Mungu mjinga huyo apitilize. Lakini eti ndiyo likasimama hapo hapo kabisa huku linajiuliza pa kwenda.

Kutokea upande mwingine wa msitu, Xander na Goko waliweza kusikia sauti za milio ya risasi, nao wote wakashtushwa na hilo. Goko aliwaza huenda ni Luteni Weisiko ndiyo amewapata vijana wale wengine, naye Xander ndiyo akatambua kwamba mpango wake wa kuwachengua wawili hawa haukufanikiwa na inawezekana ndugu zake walikuwa wamepatwa na baya. Maumivu yalimzidia, naye alijua hangeweza kuendelea kujificha, kwa hiyo kama angekufa, basi angekufa kibishi.

Chini hapo aliweza kushika jiwe kubwa kidogo, naye akaanza kujinyanyua taratibu huku akikaza kichwa chake sana ili asitoe sauti yoyote, lakini Goko akahisi kuna jambo fulani nyuma yake. Ile Xander alipotaka tu kumpiga nalo kwa nyuma, Goko akawahi kugeuka, hivyo likampiga sehemu ya bega huku naye akifyatua risasi iliyopiga hewani. Xander akadondoka chini kiudhaifu, naye Goko akajiweka sawa na kuikoki tena bunduki yake ili wakati huu asifanye makosa tena.

"Mmetusumbua sana nyie madogo... yote haya ya nini kama kifo kitawapata tu?" Goko akamwambia.

Xander akawa anajivuta-vuta hapo chini huku anamwangalia kilegevu, akiwa anajua huo ndiyo ulikuwa mwisho wake. Lakini, mara ghafla akaona kama kitu fulani cheusi kinatokea nyuma ya Goko, na kilikuwa kinajongea taratibu sana kwa njia ya kuvizia. Akatoa macho kwa hofu kwa kuwa hakuweza kukiona vizuri, naye Goko akatambua hilo. Ile naye amegeuka tu, kitu hicho kikamrukia na kuanguka naye pembeni, jambo lililomwogopesha sana Xander (akiwa ndani ya mwili wa Sandra).

Akaanza kujivuta kutoka hapo huku akisikia sauti za Goko za maumivu, na kukuru-kakara zikitokea hapo. Hakuweza kujua kitu hicho ni nini, lakini ilionekana kama ni mtu; ila bado hakuwa na uhakika. Aliwaza labda ilikuwa ni mnyama, lakini bado alionekana kama mtu. Alijitahidi kujongea kwa nguvu ndogo alizobakiza, naye sasa akawa anakwenda ovyo ovyo tu bila kujua anakoelekea. Wazo lililokuwa kichwani mwake ni kwamba ingekuwa bora kufa kwa risasi, siyo kutafunwa na mnyama. Kwa hiyo bado akawa anajaribu kunusuru uhai wake masikini.

Ilifikia hatua akaishiwa nguvu kabisa na kuanguka chini. Alikuwa anapumua kwa shida huku macho yake yakifumba na kufumbua kilegevu sana kutokana na kuhisi kizunguzungu. Lakini kutoka masikioni mwake, aliweza kusikia sauti za vilio, na moja kwa moja akatambua sauti hiyo kuwa "yake." Yaani, sauti ya mwili wake, hivyo akajua huyo alikuwa ni Sandra. Akafumbua macho kwa nguvu, naye akaanza kujitahidi kufatilia upande sauti hiyo ilikotokea. Akajigeuza taratibu na kuanza kujiburuza, akiumia sana tumboni, lakini akawa anataka sana kumwona pacha wake.

"Usiniueee... pleeease... please usi... usiniueee...

Sauti hiyo ikawa inasema maneno hayo kwa kilio. Xander akaweza kujivuta mpaka sehemu ambayo ilimwezesha kumwona Sandra, akiwa amekaa chini huku ameviunganisha viganja vyake kama anaomba sana aonewe huruma. Huo ulikuwa ni mwili wake wa kiume, na chini yake akamwona Azra akiwa amelala tuli. Xander akaanza kulia kwa maumivu sana, akishindwa hata kunyanyuka ili kwenda kutoa msaada. Akasema kwa kutumia akili yake 'Sandra... Sandra...'

Xander akasikia sauti ya Luteni Weisiko ikisema, "Nisamehe... hii ni sehemu tu ya kazi yangu."

Hakuweza kumwona Luteni Weisiko, lakini sasa akajua kuwa huyo ndiye ambaye 'dada yake' alikuwa anamwomba asimuue. Kutoka kichwani kwake, Xander akasikia sauti ya dada yake ikimwambia, 'Xander... popote ulipo... jua nakupenda sana pacha wangu... tafafhali pambana usalimike... usisahau hili kamwe... for me...'

Xander alijua dada yake alikuwa anamkumbusha msemo wao waliopenda sana kuambiana, na kabla hajaweza kumjibu kwa kichwa, hapo hapo ikasikika sauti ya risasi, naye akauona mwili wake, ukiwa na dada yake kwa ndani, ukianguka chini karibu kabisa na Azra. Xander alihisi uchungu mwingi sana, kwa kutambua kwamba sasa alikuwa amebaki peke yake, na akiwa hana matumaini yoyote ya kupona. Aliumia sana moyoni.

Hivyo, akaona ni bora tu kama na yeye akienda hapo ili afe akiwa pamoja na ndugu zake. Akaanza kujiburuza tena, naye akavuta nguvu yote ndogo iliyobaki mwilini mwake ili amwite Luteni Weisiko, pale mkono fulani ulipouziba mdomo wake kutokea kwa nyuma! Xander alijaribu kufurukuta, lakini akawa hana nguvu za kufanya hivyo. Aliishiwa nguvu kabisa, huku akihisi mwili wake unavutwa kwa nyuma, na giza zito likafunika macho yake.

Kutokea pale alipokuwa amesimama Luteni Weisiko, aliwaangalia sana watoto wale pale chini. Yeye aliona ni Xander na Azra, bila kujua aliyekuwa ndani ya mwili wa Xander ni Sandra. Alikuwa ameusikia mlio ule wa risasi aliyopiga Goko hewani muda ule amemkosa Xander (akiwa kwenye mwili wa Sandra), hivyo alikuwa amechukulia kwamba Goko alimkamata Sandra na kumuua.

Weisiko akawasogelea wawili wale pale chini na kuwatazama sana, naye akachuchumaa na kuushika uso wa Azra. Alimwangalia mno binti huyo mdogo, kisha akatoa simu maalumu za kijeshi (walkie talkie) na kupiga kwa mtu fulani. Baada ya kupokelewa, Luteni Weisiko akasema tu maneno haya:

"Mission Accomplished."

★★★★

WIKI CHACHE ZILIZOFUATA....

Mambo yalizidi kuwa mabaya sana ndani ya serikali. Kundi la Demba Group, ambalo lilikuwa lenye baadhi ya wanajeshi mahiri na waasi wakiongozwa na Luteni Weisiko na Kanali Jacob Rweyemamu kisiri, lilifanikiwa kuiua familia nzima ya Jenerali Pingu, ikiwemo na yeye pia, na Luteni Jenerali Geneya Oyayu. Waliacha ujumbe kuwa taratibu wangehakikisha viongozi wengi wanauawa pia. Haikujulikana waliweza vipi kufanya hivyo, lakini njia zao zilikuwa zenye urahisi fulani kutokana na wenyewe kuonekana kuwa wanajeshi walioaminika. Wanajeshi wengi waliingia kwenye msako wa hadharani nchi nzima ili kuweza kuwakamata, lakini waliambulia patupu.

Raisi alikuwa ametoa tamko kuhusiana na maovu hayo, kwa kusema kwamba angehakikisha vitendo hivyo vinakomeshwa, lakini hofu ikazidi kutanda baada ya mabomu yaliyotegeshwa kwenye mabweni ya shule maalaumu za kutunza watu wenye ulemavu (upofu, viungo vya mwili, na akili), yaliyosababisha maafa ya watu 210 ndani ya siku moja; na yote yakilipuka sehemu tofauti ndani ya muda ule ule. Watu hawa walikuwa wakatili sana, na bado hawakuweza kukamatwa.

Wananchi wengi walianza kufanya fujo kwa sababu waliilaumu serikali kuwa iliangalia tu vitendo hivyo bila kufanya lolote zaidi ya kubwabwaja tu. Walishangazwa sana na jinsi ambavyo mambo haya yalikuwa yakiendelea bila serikali yao kufanikiwa kuwakamata waasi hao, hivyo wengi wakawa wakiandamana na kufanya fujo nyingi wakitaka Raisi ajiondoe madarakani kama Demba Group walivyotaka. Walijaribu kutulizwa sana lakini ghasia walizofanya zilisababisha taifa liwe chini ya msukosuko mkubwa kupita maelezo.

Raisi aliyekuwepo madarakani, alitoa video fupi iliyomrekodi yeye akizungumza maneno yaliyowalenga Demba Group, akitaka kujua kwa nini walitaka aondoke madarakani na ni nani ambaye walimtaka awe Raisi sasa. Jibu lilikuja kupatikana kupitia video iliyosambazwa mitandaoni, ya kundi hilo, na kiongozi wao aliyeficha uso wake akasema kwamba wenyewe walichotaka ni Raisi kujiondoa, mengine yangefuata, la sivyo visa vya kikatili kutoka kwao vingeendelea.

Muungano wa nchi za mashariki ulijaribu kutoa msaada maalumu kwa Raisi ili kushughulika na suala hili, lakini hiyo haikusaidia kwa lolote kwa sababu watu hawa walijua vizuri sana nyendo ambazo zingefuatwa, hivyo wenyewe wangetokeza njia zingine za kufanya maovu yao. Raisi alikuwa akipewa ulinzi mkubwa sana pamoja na viongozi wengi, lakini bado Demba Group wakafanikiwa tena kuwaua wabunge kadhaa na madiwani.

Hali hii ilitisha na ilichosha! Vurugu zilitanda kila kona, ilikuwa ni kama Taifa limeingia kwenye kipindi cha maafa, kwa sababu ijapokuwa hii ilikuwa vita, bado haikueleweka ni vita ya aina gani. Sehemu nyingi kama mashule na vyuo vilifungwa ili kuepushana na watu wengi kuendelea kuumia.

Kwa sababu mambo yalizidi kuwa mabaya sana, Raisi alitangaza kujiuzulu yeye mwenyewe, na kwa sababu haikuwa kipindi cha uchaguzi, kisheria sehemu yake ingepaswa kuchukuliwa na Makamu wake, mheshimiwa Paul Kalebu Mdeme. Huu ndiyo uliokuwa mpango mzima. Makamu huyu wa Raisi mpaka sasa alikuwa akijifanya yuko upande wa serikali yao, na Raisi pia, lakini kihalisi ni yeye ndiye aliyeongoza mambo yote hayo ili kuweza kuinyakua nafasi ya Raisi mapema.

Kwa hiyo baada ya Raisi kujiuzulu, Mdeme akaichukua ngazi ya uraisi kwa urahisi. Lakini mambo aliyokuwa amefanya kufanikisha yote haya yalikuwa ni mabaya kupita maelezo. Kabla ya kujiuzulu kwake, Raisi aliyepita alikuwa ametoa onyo la wazi kwa wananchi kwamba hata nani aingie madarakani, sikuzote watu hawangeridhishwa tu. Yeye alikuwa amejitahidi sana kulijenga-jenga taifa, na wengi walimpongeza kwa jitihada zake. Lakini matatizo haya yalipoanza, mazuri yake hayakuonekana tena. Ila alielewa fika kuwa hofu iliyokuwa imejengwa ilikuwa kubwa, na ndiyo maana akaachia tu cheo chake.

Baada ya Makamu Paul Mdeme kuwa Raisi rasmi, alitoa ahadi kwa wananchi kwamba mambo mengi yangekuwa sawa zaidi sasa, na hawangeacha kuwatafuta wabaya wao. Alisema hakujua ni kwa nini Demba Group walifanikiwa kufanya mambo yote hayo bila kukamatwa, ila kama kuna mtu au watu waliokuwa wanawaficha, hata kama ilikuwa chini ya mahandaki, wangewakamata tu. Akaongea kinafiki kwamba vifo vilivyotokea haviwezi kusahaulika, hivyo alijua kuwapata waasi hao na kuwaadhibu ilikuwa jukumu lake.

Wananchi hawakujali nani ni Raisi, walichokuwa wanaangalia sasa ni kama hali zingetulia kwa kuwa Demba Group waliahidi Raisi akijiondoa tu, wangeacha mambo hayo. Hakukuwahi kutokea tukio kubwa namna hiyo la uasi bila waasi kukamatwa, hii ndiyo ilikuwa mara ya kwanza. Kwa hiyo wengi bado walishangaa sana iliwezekanaje watu hao kutojulikana mpaka wakati huu. Wafiwa walifanya misiba kwa ajili ya wapendwa wao wengi waliopoteza uhai, na Raisi mpya alitoa msaada mkubwa wa njia ya rambirambi kwa pesa kwenye KILA familia iliyopatwa na matatizo hayo.

Mambo ambayo "Raisi" Paul Mdeme alikuwa ameanza kuyafanya yaliwafanya watu wamwone kuwa mwenye hisia-mwenzi sana (compassion), bila kujua kihalisi yeye ndiye shetani aliyesababisha vifo hivyo vyote.

Kwa kuwa sasa Paul Mdeme alikuwa na nguvu sana kama Raisi, alitumia uchochezi wake kuwapatia vyeo vya juu Kanali Jacob Rweyemamu na Luteni Weisiko. Ni mambo yaliyoshangaza baadhi ya watu jeshini kwamba Kanali Jacob alipandishwa cheo na moja kwa moja kuwa Jenerali wa jeshi la nchi baada ya kifo cha Jenerali Pingu, naye Luteni Weisiko akawa ndiye Luteni Jenerali baada ya Geneya Oyayu kuuawa. Lakini bado ukweli ulikuwa umefichika mpaka wakati huu, hivyo watu hawa wabaya wakawa juu zaidi na kuendelea kufanya mipango yao mingine ya kibinafsi.

Tokea Raisi aliyepita alipojiuzulu, Demba Group hawakusikika tena. Yaani walikuwa wametoweka tu mbele ya maisha ya watu baada ya Raisi mpya kuingia. Paul Mdeme alijitahidi sana kujifanya ni Raisi mwema kwa wananchi, ikionekana kuwa baada ya yeye kuingia aliweka mfumo mkali sana wa ulinzi uliowafanya Demba Group waogope, hivyo watu wengi walimsifu. Kihalisi, wanajeshi wale waliokuwa wakimuunga mkono kwa matendo hayo, ambao ndiyo walijifanya kuwa Demba Group, walikuwa wamepewa pesa nyingi sana kwa kazi zao. Hivyo nao wakaendelea kuwepo tu jeshini bila kutambulika, kwa hiyo ishu ya Demba Group ikaanza kuonekana kuwa historia.

Ndugu na marafiki wa familia ya Casmir waliwaombolezea sana kwa siku nyingi. Valentina na Raymond waliumia sana kujua kwamba hawangeweza kuwaona wapenzi wao tena. Sophia, Mecky, Lucas, Benjamin, Bernard, Hussein, na Ramla pia, walihuzunishwa sana na habari za vifo vyao. Waliowaua walifanya vilevile walivyoifanyia familia ya Kendrick; waliwarudisha kwenye nyumba ile ya mjomba wake Casmir na kuwaingiza, kisha kuichoma kwa moto. Kwa hiyo kihalisi miili iliyozikwa ilikuwa imekauka sana mpaka kufikia hatua ya majivu.

Kukawa na vipindi maalumu vya televisheni vilivyozungumzia maisha ya viongozi wa serikalini na jeshini waliokufa kwenye matukio hayo ya uasi. Na ingawa bado Demba Group hawakufichuliwa, ilitiliwa mkazo sana kwamba jambo hilo halingekuja kutokea tena chini ya utawala wa Paul Mdeme. Ahadi nyingi ambazo Raisi huyu mpya alitoa zilianza kutimizwa kwa kasi sana, hivyo watu wengi walizidi kumpenda, ilhali baadhi waliona makosa mengi pia kwenye njia zake za kuongoza mambo.

★★★

OFISI YA JENERALI

Jenerali Jacob Rweyemamu, akiwa amejaa mafanikio sasa baada ya "kupanda juu," akawa kwenye ofisi yake akifanya kazi fulani kwa utulivu mida ya jioni. Ni baada ya kujulishwa na msaidizi wake kwamba mgeni aliyekuwa anamsubiria amefika, ndipo akaachana na kazi zake na kuamuru mgeni huyo afike ndani ya ofisi. Baada ya msaidizi wake kuondoka, akaingia mwanaume aliyemfahamu vizuri sana, na kwa furaha akanyanyuka ili kwenda kumlaki. Mwanaume huyu akapiga saluti ya heshima kumwelekea Jenerali, naye Jenerali Jacob akasimama mbele yake akiwa anatabasamu na kumpiga-piga mabegani kirafiki.

"Luteni Jenerali Weisiko! Aah... inapendeza sana hahahahaaa," Jenerali Jacob akamsifia.

"General... habari za siku?" Luteni Jenerali Weisiko akamsalimu.

"Ni nnnzuri sana! Tena zinazidi kuwa nzuri kwa sababu yako. Unapiga sana kazi kijana wangu. Unastahili wake 10 kabisa," Jenerali Jacob akamwambia.

"Kama msemo wa mwanafalsafa, bado nipo nipo kwanza," Luteni Jenerali Weisiko akatania.

Jenerali Jacob akacheka na kumpiga-piga bega tena, kisha akamwambia waketi ili wazungumze.

"Singida wanasemaje?" Jenerali Jacob akamuuliza.

"Wako poa. Hawatangulizi mapenzi, ila vitunguu tu. Sebastian amenipa salamu zake nikufikishie pia," Weisiko akajibu.

"Hahahah... Unamwonaje Brigedia wetu huyo?" Jacob akauliza.

"Anapiga kazi... anawaongoza vizuri sana vijana wake na..."

"Nilikuwa namaanisha, na yeye anaweza kuwa asset nzuri upande wetu, au?" Jacob akamkatisha.

"Mmm... kiukweli... sina uhakika sana General. Bado na yeye ana mwelekeo wa Pingu-Pingu hivi. Kwa hiyo kwa masuala yetu sidhani kama itakuwa sawa kumwingiza," Weisiko akamwambia.

"Hmm... Okay. Lakini ninafurahi sana kwamba Mdeme ametuongezea na ally wengine. Viongozi wengi wanamkubali sana lakini kwenye hili game ni sisi saba tu. Yeyote atakayejaribu kutuzingua... you know the drill," Jacob akasema.

"Ndiyo Jenerali. Mambo yote tunayafanya kwa umakini sana. Mdeme kweli anajua kututunza," akasema Weisiko.

Jenerali Jacob akacheka.

"Ni nzuri sana ukifanya kazi ngumu na kuibuka mshindi. Vijana wetu wako vizuri sana. Mdeme alikuwa anahofia kwamba labda baadhi ya hao waliotumika wangetusaliti, lakini nikamhakikishia wote tunao mfukoni. Usiache kusisitiza umuhimu wa wenyewe kuwa kimya kuhusu mambo yote, la sivyo..."

"Ndiyo najua General. Nitahakikisha mambo yote yanakuwa sawa."

"Ulifanikiwa kumpata?" Jacob akauliza.

"Hapana, lakini nafikiri nimetambua alikoishia. Baada ya kukuta Goko amekufa, nilijua huyo msichana amemtoroka kwa hiyo nikafatilia trace zake za damu. Sehemu zilipoishia ni kwenye bonde refu sana kuelekea chini. Inaonekana alidondokea humo," Weisiko akaeleza.

"Inaonekana? Weisiko tunatakiwa kuwa makini sana. Vipi kama huyo binti alisalimika?"

"Hapana General, haiwezekani. Ilikuwa ni usiku, na nilikuwa nimemkata vibaya sana tumboni. Sijui alimshinda vipi akili Goko, lakini asingeweza kufika popote maana huo msitu ulikuwa ni dead end... na kudondokea kwake kule ni kifo moja kwa moja," akasema Weisiko.

"Okay sawa. Mlitumia akili kuweka miili ya watu wengine ichomwe ili ionekane ndiyo wenyewe. Kazi nzuri kwa hilo. Ninatumaini mambo haya hayatasikika tena," Jacob akasema.

"Ondoa shaka General. Huu ndiyo mwanzo tu wa kufurahia matunda ya jasho letu..."

"Hahahahah... kweli kabisa," Jacob akasema kwa furaha.

"Vipi kuhusu.... ameshafika India salama?" Weisiko akauliza kwa hisia.

"Ndiyo. Ameshafika," Jacob akajibu.

Weisiko akaangalia chini kwa utulivu.

"Nini hasa kilichosababisha ukashindwa Weisiko? Usiniambie ulikuwa soft..." Jacob akamuuliza.

"Hapana siyo hivyo. Ni kwamba tu..." akaishia hivyo.

"Alikukumbusha kuhusu Mary?" Jacob akasema.

Weisiko akatikisa kichwa taratibu kukubali.

"Well... nimefanya vile kwa ajili yako kwa kuwa uliniomba. Ila jambo hili linapaswa kuwa siri kati yetu, hata Mdeme hapaswi kujua. Nambiar anajua njia watakazotumia ili kumfanya awe kama tunavyotaka, kwa hiyo najua kila jambo litakuwa sawa," Jenerali Jacob akasema.

"Amefikia wapi?" Weisiko akauliza.

"Nimeongea na Nambiar akanijulisha wamempeleka Kerala kwenye sehemu ya siri sana kwa ajili ya hiyo ishu. Anaaminika, najua ata-deliver," Jacob akasema.

"Ni wapi kabisa?"

"Itakuwa bora usipojua. Focus kwanza kwenye mambo unayohitajika kufanya, yeye atakuwa salama. Ikiwa mambo yataenda vizuri, basi atakuwa msaada kwetu mbeleni. Trust that," Jenerali Jacob akasema.

Wawili hawa walikuwa wakizungumzia jambo fulani kubwa sana walilofanya kutokana na matukio yale ya kikatili waliyoshiriki kutenda. Na kama Jenerali Jacob alivyomwambia Weisiko, ilifaa kubaki kuwa siri ili kuja kuanza kuitumia kwa wakati unaofaa. Wakaendelea na maongezi yao mengine kuhusiana na kazi, kisha Luteni Jenerali Weisiko akamuaga Jenerali Jacob Rweyemamu na kuondoka jengoni hapo.

Siku zikazidi kwenda, na Taifa likaonekana kuanza kujinyanyua tena kutoka pabaya pale lilipokuwa kwa kipindi kile kifupi na kusonga mbele. Wenye kufanya maovu sasa ndiyo wakawa juu zaidi, wakifurahiwa na watu ambao hawakujua mabaya yao kwa sababu walijionyesha kuwa watetezi wazuri wa haki na walijali mahitaji yao, na muda ukazidi na kuzidi kusonga mbele kukiwa na mambo mengi sana yaliyojificha, ambayo muda ungekuja kuyafichua mbele ya safari......

★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★

Huo ndiyo mwisho wa msimu wa kwanza. Sehemu zitakazoendelea zitaanzisha msimu wa pili.

Tunalipia sh ngap kuipata hii
 
Back
Top Bottom