Simulizi: For You

Simulizi: For You

FOR YOU

Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Uhalifu, Mauaji, Visasi, Vita, Mambo yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA THELATHINI NA MBILI

★★★★★★★★★★★★★★★★★★★


MIAKA NANE ILIYOPITA....


Turudi tena mpaka usiku ule ambao familia ya Meja Casmir ilishambuliwa na Luteni Weisiko pamoja na wanajeshi wake wawili. Baada ya Weisiko na Goko kuwaua wazazi wa watoto wale watatu, Casmir na Alice, pamoja na msaidizi wao wa kazi Salome, watoto walikimbilia msituni huku Xander, akiwa ndani ya mwili wa Sandra, akiwa na maumivu tumboni kutokana na kuchanwa kwa kisu, naye Sandra, akiwa ndani ya mwili wa Xander, akihisi maumivu pia kwenye paja lake baada ya kuchunwa na risasi aliyofyatuliwa na Goko.

Kutokana na jinsi watoto walivyokuwa wakikimbia polepole hasa kwa sababu ya Sandra kumshikilia Xander kutokana na mwili wake kuishiwa nguvu kwa sababu ya kisu alichochomwa tumboni, Xander akawaambia wenzake wamwache nyuma ili dada zake wakimbie pamoja. Sandra akawa anakataa, lakini Xander akamshawishi kwa kumwambia ni bora hata kama akifa yeye lakini ndugu zake wawe na nafasi kubwa ya kupona kuliko ikiwa wote watauliwa. Kwa hiyo akamwambia waelekee upande mmoja, halafu yeye atajitahidi kuelekea upande mwingine akiacha viashiria kwa wanaume wale ili wamfate yeye tu. Sandra akiwa kwenye mwili wa Xander alilia sana. Azra alilia pia mno, nao wote wakamkumbatia ndugu yao, kisha akawasihi wawahi haraka maana alijua Weisiko na mwenzake walikuwa nyuma yao.

Sandra, akiwa kwenye mwili wa pacha wake akaondoka na Azra kuelekea upande mmoja, wakimwacha Xander anajiandaa kuelekea upande mwingine. Alijitahidi kukimbia pamoja na Azra kwa uangalifu ili kuwaepuka maadui, huku Azra naye akijikaza sana kukimbia ingawa alikuwa amechoka. Walikimbia na kukimbia bila ujuzi wowote wa walikokuwa wakielekea, na kwa sababu ya kutotambua uelekeo wao ikawa ni kama wanazunguka msitu tena na kurudia njia ile ile waliyotokea. Azra akafikia ukomo wa pumzi zake, naye akamwomba "Xander" wapumzike kidogo kwa kuwa hangeweza kuendelea kukimbia. Sandra kwa kuhofia usalama wao, akaamua tu kumbeba mgongoni ili waendelee kukimbia, akitumia vizuri nguvu ya mwili wa kaka yake ili iwafikishe mbali. Kichwani kwake alimuwaza sana Xander, angekuwa kwenye hali gani kwa hizo dakika chache walizotengana.

Wakati akiendelea kukimbia hivyo, akaukwaa mguu wake na kudondoka pamoja na Azra. Bado alihisi maumivu kwenye paja lake, lakini akawa anajitahidi kumnyanyua mdogo wake ili waendelee kukimbia. Azra sasa akasema angeweza tena kukimbia, lakini shida ikawa kwa Sandra. Alihisi mguu wake ukiwa mzito sana, kama vile ulikuwa umeanza kufa ganzi, kwa maana kila alipojaribu kusimama vizuri asingeuhisi vyema, na hilo likasababisha awe anadondoka tu. Azra akajitahidi kumsaidia ili waondoke pamoja, na ni hapa ndipo wakaanza kusikia sauti za hatua zikija upande wao. Kwa kutambua bila shaka ilikuwa ni adui, wakaendelea kujivuta kwa pamoja ili kumwepuka, lakini Sandra akamwambia Azra wajifiche tu sehemu fulani ili adui yao awapite, kwa kuwa kuendelea kukimbia namna hiyo hakungeleta matokeo mazuri sana.

Kwa hiyo wakaketi kwenye kichaka kimoja ambacho kilikuwa na miiba midogo-midogo, na ingawa iliwachoma lakini wakajikaza tu na kuendelea kutulia. Kutulia huku kulifanya maumivu kwenye paja la Sandra yasikike zaidi, lakini akajitahidi tu kujikaza pia. Hazikupita sekunde nyingi, nao wakamwona mtu fulani akifika hapo kando yao. Kwa haraka wakatambua ilikuwa ni Luteni Weisiko, naye Sandra akambana zaidi Azra kwake ili wasitikisike. Luteni Weisiko akasimama hapo kwa sekunde chache, kama akitathmini watoto walikuwa wameelekea wapi, kisha akaendelea kukimbilia upande mwingine.

Baada ya Sandra na Azra kuona ameondoka, wakajitoa kwenye kichaka hicho, naye Azra akamwambia aliyemwona kama Xander kwamba wangepaswa kurudi nyuma ili kumtafuta "Sandra." Lakini Sandra akasema hata hakujua walikokuwa, hivyo hangejua wapite wapi labda mpaka wasubiri kukuche, lakini Azra akasisitiza kwamba walipaswa kurudi kumsaidia ndugu yao hasa kutokana na jinsi alivyoumia. Sandra akiwa anafikiria nini cha kufanya, wote wakastushwa na sauti ya Luteni Weisiko ikisema, "Njooni na mimi, nitawapeleka kwa dada yenu."

Wawili hawa walishtuka sana na kutazama upande ambao walimwona Luteni Weisiko akiwa amesimama huku anawaangalia. Hofu ikawajaa sana, naye Sandra akamwambia Azra akimbie haraka. Azra akaanza kukimbia kuelekea upande mmoja, naye Sandra akaanza kuelekea huko huko. Luteni Weisiko akaendelea kusimama hapo hapo na kutabasamu tu, kisha akaikoki bunduki yake na kuanza kuwafata kwa kasi. Ilikuwa ni kama alipenda sana mchezo huu wa paka na panya, na baada ya kuwakimbiza kwa hatua kadhaa, akawaona wakiwa kwa mbele wanakimbia, wakijitahidi kuokoa maisha yao.

Walikuja kufika sehemu ambayo ilikuwa na eneo lenye uwazi kidogo bila kuwa na miti bali majani tu chini, na baada ya Luteni Weisiko kuingia hapo akasimama na kuielekeza bunduki yake kwa Azra, aliyekuwa mbele zaidi, naye akafyatua risasi iliyompata nyuma ya mguu wake wa kushoto. Azra alipiga kelele ya maumivu na kudondoka chini, lakini ni wakati tu amedondoka chini ndiyo akapiga kichwa chake kwa nguvu sana kwenye jiwe dogo na kupoteza fahamu.

Sandra akiwa ndani ya mwili wa Xander alipiga kelele ya kilio baada ya kushtushwa na sauti ya risasi hiyo, naye akaanguka chini akiwa amejikunja kwa woga mwingi. Luteni Weisiko akajisawazisha na kuanza kumwelekea mpaka pale alipokuwa, na alipofika karibu, akamwelekezea bunduki yake kichwani kama anataka kumfyatua kwa risasi. Sandra akawa anamwangalia huku analia na kuficha uso wake kwa mikono. Weisiko akawa anataka kukivuta kifyatulio cha risasi, lakini akasikia mlio wa risasi nyingine kutokea upande tofauti na huo. Akatazama upande huo wa msitu na kukisia kwamba bila shaka ilikuwa ni Goko ndiye aliyempata pacha wa kike na kummaliza, hivyo akaishusha bunduki yake na kumtazama tu pacha huyu wa kiume.

"Umebaki wewe," Luteni Weisiko akamwambia hivyo "Xander" huku akitabasamu.

"Tafadhali... usiniue... please..." Sandra akawa anaomba kwa sauti tetemeshi.

Luteni Weisiko akachuchumaa na kumtazama kwa ukaribu. Sandra akawa anajivuta nyuma kwa woga.

"Unajua hapa ni sawa na kama umeshakufa kwa sababu... hata nikisema nikuache, huu msitu una wanyama wakali. Ni bora tu nikusaidie ili wasikutafune..." Weisiko akasema.

Sandra akawa anatikisa kichwa kukataa.

"Cha risasi ni rahisi zaidi kuliko meno. Au unataka kutafunwa? Si bora hivi?" Weisiko akauliza kikejeli.

"Una watoto?" Sandra akauliza.

Luteni Weisiko akabaki tu kumtazama.

"Ikiwa ungekuwa nao... na uko sehemu fulani ukijua kabisa wanapatwa na mambo kama haya yanayotupata sisi... ungefanya nini?" Sandra akauliza.

Luteni Weisiko akainamisha uso wake kama anatafakari jambo fulani. Yeye aliona ni kama Xander ndiyo anamuuliza hivyo, na kiukweli maneno yake yalimgusa kwa kiwango fulani.

"Nitakupa dakika mbili tu za kufanya chochote kile unachotaka kufanya. Baada ya hapo...." Luteni Weisiko akaishia tu hivyo na kusimama.

Sandra akaanza kujivuta kuelekea kule alikoangukia Azra. Akafika mpaka karibu yake na kuanza kumpepesa ili aamke, lakini akawa ametulia tuli tu. Aliposikiliza mapigo yake ya moyo, akatambua kwamba bado alikuwa hai, naye akamgeukia Luteni Weisiko kukuta tayari akiwa amewakaribia.

"Please usiniue... please... I'm begging you..."

Luteni Weisiko akaonekana kutojali kilio cha kijana huyu na kuielekeza bunduki yake kwake kwa mara nyingine. Sandra akajisawazisha na kupiga magoti, akiwa ameviunganisha viganja vyake.

"Usiniue tafadhali. Azra... mdogo wangu ananihitaji. Ana tatizo la upumuaji, ana... ana... ananihitaji... tafadhali...." Sandra akaendelea kuomba.

Maneno haya ya Xander (Sandra) yakamfanya Luteni Weisiko aishushe bunduki yake kidogo. Ni kama alikuwa anatafakari jambo fulani baada ya Xander (Sandra) kusema kwamba mdogo wake alikuwa na tatizo la upumuaji, naye akamwangalia Azra pale chini. Lakini akayakaza meno yake na kumwangalia tena "Xander." Akainyanyua bunduki yake kwa njia yenye uhakika zaidi wakati huu, naye akaikoki tayari kumfyatua risasi.

"Usiniueee... pleeease... please usi... usiniueee..." Sandra akaendelea kumwomba hivyo Luteni Weisiko, naye Weisiko akawa kama anataka kufyatua lakini anasita.

Kutokea kichwani kwake, Sandra akasikia sauti ya pacha wake ikimwita, 'Sandra... Sandra...' na kwa sababu hakujua ilitokea wapi, akatafuta utulivu kidogo ili aweze kumsemesha pacha wake pia.

Luteni Weisiko akawa bado amemwelekezea bunduki, naye akasema, "Nisamehe... hii ni sehemu tu ya kazi yangu."

Sandra akafumba macho yake na kuamua kujaribu kuongea kwa kutumia akili yake pia, akiwa ameshakubaliana na matokeo. Ilikuwa ni muhimu sana kwake pacha wake asikie maneno yake ya mwisho.

'Xander... popote ulipo... jua nakupenda sana pacha wangu... tafafhali pambana usalimike... usisahau hili kamwe... for me...'

Lakini kabla hajamaliza maneno yake, Luteni Weisiko akamfyatua kwa risasi kichwani, naye akaanguka chini karibu kabisa na alipokuwa amedondokea Azra. Luteni Weisiko akakaza meno yake kwa nguvu na kutazama pembeni, akiwa kama mtu aliyefanya jambo hilo kwa shingo upande. Lakini akajikumbusha yeye ni nani, mwanajeshi mtiifu ambaye hakupaswa kuruhusu hisia zimkengeushe kutoka kwenye "mission" aliyopewa, hivyo akajisawazisha akili tu na kuwaangalia tena watoto hao, kisha akaanza kuwasogelea chini hapo. Mkono wake uliokuwa umepigwa kwa risasi bado ulitoa maumivu, lakini akawa anaupuuzia tu.

Alipowakaribia zaidi, akachuchumaa na kumwangalia Azra. Kwa hapo angeweza kuhisi tu kwamba binti huyo bado alikuwa hai, naye akaushika uso wake mweupe ambao ulionekana vyema kwenye giza hilo la msitu. Alimwangalia mno binti huyo mdogo, na kumbukumbu kadhaa za matukio ya kipindi cha nyuma zikamwingia akilini mwake.

Luteni Weisiko alikuwa na mtoto wa kike, ambaye kwa sasa hakuwa hai. Binti yake huyo alikuwa mweupe kufata weupe wa mama yake, ambaye Luteni Weisiko aliachana naye kwa kuwa mwanamke huyo hakupenda tabia za kitemi-temi za mwanaume huyu. Lakini Weisiko alimpenda sana binti yake ingawa hakumpa muda mwingi wa kuwa pamoja naye kama mzazi. Binti yake huyo aliitwa Mary, naye alikuwa na tatizo la upumuaji ambalo liliongezeka sana kufikia wakati alipokuwa na miaka 13; rika kama la Azra tu.

Kipindi fulani Weisiko alipokuwa kazini, binti yake alishikwa na mkazo mbaya sana kwenye mapafu, na mama yake alijaribu kumtafuta Weisiko ili amsaidie kuweza kumpatia matibabu ya haraka, lakini Weisiko alichelewa, na hivyo mtoto huyo akapoteza uhai. Mzazi mwenza alimlaumu sana Weisiko kwa kifo cha bintiye, akisema alikuwa na uwezo mzuri tu wa kumpatia matibabu mapema sana hata nchi za nje, lakini akampuuzia. Ila ukweli ni kwamba Luteni Weisiko alikuwa na deni kubwa wakati huo ambalo alikuwa akilipia fidia mfululizo, ndiyo sababu hakuweza kulipia matibabu ya hali ya juu kwa ajili ya binti yake.

Mwanamke huyo aliyezaa naye alikuwa msusi tu kwenye saluni za wanawake, hivyo hakuwa na kipato cha kutosha na alihangaika kwa muda mrefu na binti yake. Kwa hiyo alimlaumu sana Weisiko kwa kuwa aliona kwamba mwanaume huyo kwa mtoto wao alikuwa baba jina tu. Weisiko pia alijilaumu mno kwa kukosa kumsaidia binti yake, na ndiyo kutokea hapo akaapa kufanya kila alichoweza ili kupata pesa nyingi zaidi kwa sababu aliona jinsi maisha yalivyokuwa na hasara bila kuwa na pesa ya kutosha. Akaanza kujihusisha na masuala haramu ya chini chini ambayo ndiyo mpaka yakapelekea yeye kujiingiza katika visa hivi viovu ili tu apate jambo ambalo aliona ndiyo muhimu zaidi lililobaki kwenye maisha yake: pesa.

Kwa hiyo kumwangalia Azra kulimfanya aone ni kama anamtazama Mary kwa mara nyingine tena. Maneno ya "kaka yake" kwamba Azra alikuwa na tatizo la upumuaji, yalichochea hata zaidi hisia hizo kumwelekea binti huyu, naye akahisi eti ni kama alipaswa "kumsaidia," kana kwamba anapewa nafasi ya pili ya "kumsaidia" mtoto huyu kwa kuwa wa kwake alishindwa. Akili yake ilikuwa imeingiwa na suto kubwa kwa sababu ya mambo maovu aliyofanya, kwa hiyo fikira ya "kumsaidia" mtoto huyu ikaonekana kama njia yake ya kujiaminisha kwamba alikuwa na moyo mzuri.

Akatoa simu maalumu ya kijeshi (walkie talkie) na kupiga kwa Kanali Jacob Rweyemamu ili kumtaarifu kwamba mambo yalikamilika. Baada ya kupokelewa, Luteni Weisiko akasema tu, "Mission Accomplished," kisha akarudisha kifaa hicho mfukoni na kuanza kumnyanyua Azra kwa mkono mmoja. Aliweza kuona jinsi ambavyo damu nyingi zilivuja mguuni kwake, naye akachana sehemu ya nguo ya "Xander" na kumfunga Azra sehemu iliyovimba kwa risasi. Akambeba begani kwake kama vile windo la swala, kisha akaanza kuondoka naye.

Alikwenda taratibu kama vile hakukuwa na tatizo lolote kabisa mpaka akafika kule ambako kulikuwa na nyumba ile alikowaua wazazi wa watoto hawa. Akampeleka Azra mpaka ndani ya gari walilokuja nalo hapo, naye akaanza kumtafuta Goko kwa kifaa kile cha mawasiliano. Alifikiri angemkuta huku tayari kwa sababu alisikia risasi ile iliyofyatuliwa kutokea upande ambao alimwambia aende. Kwa sababu hakuweza kumpata, akaona tu aondoke hapo ili kumpeleka binti huyu kwenye matibabu. Alimwangalia kwa mara nyingine na kuona bado yuko hai, naye akawasha gari na kuondoka hatimaye.


★★★★


Akiwa bado mwendoni, Weisiko aliongea na baadhi ya vijana wa kundi lao na kuwaeleza kile yeye na wengine wawili walichofanya usiku huo, naye akawaamuru baadhi kwenda sehemu ile alikotoka ili kuteketeza miili ya wale waliowaua. Akawapa maagizo hususa kabisa kwamba walipaswa kupeleka na miili mingine ya watu waliokufa ili kuichoma kwa moto pamoja na ile ambayo wangeikuta, na walipaswa kumaliza hayo yote kabla ya jua kuchomoza. Akamalizana nao na kuendelea na safari yake, akiwa na lengo la kumpeleka Azra kwenye hospitali ya jeshi. Yaani ilikuwa ni kama akili yake imekufa ganzi kabisa, akifanya mambo kwa njia aliyoona kuwa sahihi, na hakuna kitu chochote ambacho kingemzuia.

Alifika kwenye hospitali ndogo ya jeshi na kupokelewa na baadhi ya vijana ambao alikuwa ameshawapanga. Walimpokea kwa njia yenye umakini ili kuwaficha wengine ambao hawakuwa wa kundi lao kuhusiana na yaliyotokea. Eneo la huku lilikuwa kwenye kambi kubwa sana ya kijeshi ambako wanajeshi wengi waliishi. Kwa hiyo vijana wake hao wakampeleka Azra kwenye chumba cha matibabu, na daktari wa upasuaji (akiwa ni mwanajeshi pia) akafika na kuanza kumhudumia mtoto.

Weisiko aliketi kwenye kitanda cha pembeni ndani ya chumba hicho hicho, akiwa anatolewa risasi mkononi mwake, na hakuna yeyote aliyepaswa kuuliza ni nini kilikuwa kimetokea. Walipaswa kuwapa tiba, halafu waendelee na mambo mengine. Weisiko akawaambia watu wake wamwangalie vizuri sana huyo mtoto, yaani wafanye lolote lile lakini asife, nao wakaendelea kujitahidi kumpa Azra huduma mpaka inafika asubuhi. Walifanikiwa kuitoa risasi mguuni kwake na kumshona, nao wakatibu sehemu ya kichwa chake iliyoumia na kuifungia bendeji. Sasa mtoto akawa anasubiriwa kurejesha fahamu.

Taarifa kumhusu Azra kuwa hapo zilipaswa kuwa za siri sana, ikiwa ni amri kutoka kwa Luteni Weisiko. Lakini alijua kwamba huenda asingefanikiwa kuficha hili kwa wakuu wengine kwa muda mrefu sana, hivyo asubuhi hiyo akaamua kumwambia Kanali Jacob Rweyemamu kila kitu akichofanya. Kanali Jacob kiukweli alimshangaa na kuuliza ikiwa akili yake ilikuwa imekongoroka au alikuwa anataka kuwaletea matatizo mapema. Lakini Luteni Weisiko akamwambia kuna hali ilimsukuma kumsaidia mtoto huyu, hasa kwa sababu alimkumbusha kuhusu binti yake aliyeshindwa kumwokoa.

Kanali Jacob akamwambia kwamba hilo halikujalisha hata kidogo. Ikiwa msichana huyo angeamka na kusema kila jambo lililotokea basi mambo kwao yangeharibika. Akamuuliza Luteni Weisiko angewezaje kuzuia hilo, ndipo Weisiko akamwambia kwamba alipanga KUMSAHAULISHA Azra mambo yote yaliyotokea. Yaani alitaka mtoto huyo apoteze kumbukumbu ya mambo yaliyotokea, lakini pia kuhusu yeye ni nani KABISA. Kanali Jacob alipouliza nia yake ya kufanya hayo kiukweli ilikuwa nini, Weisiko akasema alitaka kumfanya Azra kuwa kama "binti yake," kwa sababu kila kitu kumhusu huyo mtoto kilimkumbusha kuhusu Mary. Akamwomba sana Kanali Jacob amkubalie kuhusiana na hili, akisema ana njia ya kufanya hivyo, na hakuna jambo lolote ambalo lingeharibika kwa kuwa amehakikisha mipango yao yote imekwenda "salama."

Pamoja na kwamba Kanali Jacob aliona suala hili kuwa upuuzi wa hali ya juu, akamkubalia tu, naye akamwambia angetumia uchochezi wake kuhakikisha Azra anaendelea kuwa siri hapo kwenye hiyo hospitali. Lakini akamweka wazi kwamba Azra kuendelea kuwa hai nchini humu hata kama asingekumbuka lolote bado kungekuwa hatari kwao, hivyo akapendekeza kwamba walipaswa kumhamisha na kumpeleka nje ya nchi. Akiwa nje ya nchi kwa kipindi kirefu ingesaidia kumfanya asahaulike kabisa hasa kwa sababu watu wangefikiri ameshakufa kama tu watu wa familia yake, naye Weisiko akakubaliana na hilo.

Lakini kwanza wangehitaji kumalizia sehemu muhimu ya mipango yao iliyobaki, yaani, kuwaondoa Jenerali Pingu Senganya na Luteni Jenerali Geneya Oyayu, ndiyo wangeanza harakati za kumsafirisha Azra.


★★★★


Baada ya wiki moja hivi kupita, Azra alirejesha fahamu zake. Alijikuta akiwa ndani ya chumba cheupe, kilichokuwa na mwonekano kama wa vyumba vya hospitali lakini cheupe kupita maelezo. Alikuwa amewekewa 'drip' kwenye mishipa, na aliweza kuhisi jinsi ilivyokuwa ngumu kunyanyua baadhi ya sehemu zake za mwili. Alikuwa akijiuliza alifikaje humo, na kitu chenye kumhofisha hata zaidi ni kwamba hakuwa na kumbukumbu yoyote ya mambo yaliyompata mpaka kufika sehemu hii. Alijaribu na kujaribu kuvuta taswira ya vitu vingi kuhusu yeye, lakini ilikuwa ni kama kichwa chake kilikuwa tupu kabisa.

Hali hii ya kutojielewa ilimfanya aogope sana, hasa kwa sababu alikuwa binti mdogo mno. Akaanza kujaribu kunyanyuka, lakini akashindwa. Akaanza kulia sana, kwa sauti ya chini, na ndipo akaingia mtu aliyemwona kama mwanaume wa kawaida tu. Kwa sababu hakumtambua, mwanzoni alionyesha kuogopa, lakini mwanaume huyo akaanza kumtuliza kwa kumwambia yeye alikuwa ni baba yake. Huyu alikuwa ni Luteni Weisiko.

Akaanza kumdanganya Azra kwa maneno mazuri sana na kumfanya atulie. Akamdanganya kwa kumwambia kwamba jina lake lilikuwa ni Mary. Alimweleza kwamba alipatwa na ajali mbaya sana na ndiyo maana alikuwa kwenye hospitali hiyo kimatibabu. Akasema kwenye hiyo ajali waliwapoteza mama yake na ndugu zake wengine, kwa hiyo walikuwa wamebaki peke yao tu. Azra hangeweza kukumbuka chochote wakati huu kwa sababu ndani ya wiki hiyo tayari Luteni Weisiko alikuwa amefanya ule mpango wake wa kuipoteza kumbukumbu ya binti kwa kutumia madawa fulani. Kwa hiyo yeye kuwa hapo peke yake na kuonyesha anamjali sana Azra, kukafanya binti amwone kuwa mtu wa kuaminika na wa karibu zaidi kwake, hivyo kujihisi salama.

Weisiko akaendelea kukaa na Azra hapo kwa muda mrefu, akimwambia kwamba angempeleka nje ya nchi apate matibabu bora zaidi ili apone haraka. Azra hakuweza kusema lolote lile kwa kipindi hiki. Muda wote alikuwa kimya tu, na akiitikia mambo machache kutoka kwa Luteni Weisiko kwa kutumia ishara. Hata wakati ambapo watu wengine kama wauguzi wangeingia, angeonyesha kuwahofia na kujificha kwa Weisiko, naye angemtuliza. Mambo yote mabaya yaliyompata kwa sababu ya mwanaume huyu yakawa yametoweka kwake, na sasa ikawa kama vile huyu ndiyo mkombozi wake.

Siku kadhaa zilizofuata, Luteni Weisiko, kwa msaada wa Kanali Jacob, akawa amefanya mipango tayari ili kumtoa Azra nchini huku na kumpeleka nchini India. Kanali Jacob alijuana na watu kule ambao wangeweza kumhifadhi binti huyo sehemu ya mbali kwa muda mrefu, naye Weisiko akamhakikishia Azra kwamba angekwenda huko pia baada ya kumaliza kazi fulani huku ili wawe pamoja, kwa kuwa Azra angetangulia. Binti bado hakujihisi usalama mikononi mwa watu wengine, hivyo kwenda na hawa wageni ndiyo ilimfanya aogope hata zaidi. Lakini Weisiko alikuwa amemwambia asiogope, kwa sababu alipaswa kujitahidi kuwa imara zaidi kwa ajili ya "baba yake" ili waje kuwa pamoja.

Kwa hiyo binti akapaa kuelekea kwenye himaya mpya kabisa kwenye maisha yake, akiyaacha maisha ya zamani na kwenda kuanza mapya kabisa.


★★★


Mwanaume aliyekuwa amemchukua Azra na kumpeleka India aliitwa Vivek Nambiar. Huyu alikuwa ni mshiriki mkubwa kutoka kwenye shirika kubwa la kimisaada kutokea India, ambalo lilikuwa na sehemu kubwa pia nchini Tanzania kwa miaka mingi. Lakini kama vile Makamu wa Raisi Paul Mdeme na Kanali Jacob tu, mwanaume huyo alikuwa ni mfisadi wa hali ya juu, akitumia njia mbaya kujipatia mali huku akijifanya mwema kwa kujihusisha na utoaji wa misaada.

Kikundi cha watu wa jamii yao kilikuwa nchini Tanzania, na ingawa wengi walifanya mambo mengi kama kusaidia katika sekta za elimu, afya, na mahitaji mbalimbali kama maji, bado watu kama Nambiar walifanya uovu usioonekana kwa njia ya moja kwa moja kupitia shughuli hizo hizo. Kwa hiyo lengo la Kanali Jacob Rweyemamu la kumpeleka Azra mafichoni lakini kwa mwanaume huyo kihususa, ilikuwa ni ili amjenge kuwa aina ya mtu ambaye angekuja kuwa msaada katika mipango yao ya baadae.

Sehemu ambayo Azra alipelekwa ilikuwa kwenye eneo lililojulikana kama Kerala, lakini ilikuwa ndani sana kwenye milima na misitu. Huko kulikuwa na majengo ya kale ambayo yalionwa kama mahekalu, na yalitunzwa kisiri sana kwa muda mrefu. Nambiar alijuana na baadhi ya watu wa huko, ambao walikuwa na tamaduni zile za ndani sana. Mara nyingi walipeleka watu fulani huko ili kuwatengeneza kwa njia mbalimbali kuendana na viwango vyao kiakili na kimwili, lakini hasa watoto wadogo. Wangefundishwa tamaduni za hapa na pale, kisha baadae wangekuja kutumiwa katika masuala mbalimbali kijamii ili kuonyesha tamaduni hizo, au watu hao waliowatunza kupata malipo ya hali ya juu kutoka kwa watu waliowapeleka watoto hao huko.

Kulikuwa na mafunzo ya aina mbalimbali hasa kwa ajili ya maonyesho, muziki, kupigana, na kujihami, na baada ya Azra kukaa huko kwa kipindi cha mwaka mzima, mwanamke mmoja mzee aliyeitwa Madhava Gopinath, ambaye alikuwa mmoja wa walimu huko, aliona kitu fulani ndani ya Azra ambacho kilimwambia kwamba binti huyo angeweza kujifunza mtindo fulani wa kupigana uliokuwa nadra sana kwa wengine kufundishwa.

Mtindo huo ulifundishwa karne na karne nyingi zilizopita, lakini ulikuwa ni mtindo hatari sana endapo ungetumiwa vibaya. Hivyo kwa muda mrefu uliacha kufundishwa, na hata wengi walidhani haukuwahi kuwepo. Ni mtindo uliohitaji kiwango cha juu cha imani kutoka kwa mwalimu ili amfundishe mwanafunzi ambaye alionekana kuwa na utu unaofaa ili kutoutumia vibaya. Na mwanamke huyo akaona jambo hilo kwa Azra.

Kwa muda wote ambao Azra aliishi huko, hakuwa akiongea. Mwanzoni alikuwa akijitenga lakini baada ya muda akawa akichangamana na wengine na kufuata maagizo yote aliyopewa, lakini bado alikuwa haongei kwa mdomo. Mwanamke huyo mzee alianza kujenga ukaribu naye zaidi na hivyo kumwelewa vizuri hata zaidi, kwa hiyo baada ya muda alianza kumfundisha njia hiyo pekee ya kupigana na kujihami. Hii haikuwa kati ya mitindo ambayo Kanali Jacob na Weisiko walitazamia Azra kufundishwa, kwa hiyo ikawa ni nyongeza ya siri kwenye mafunzo yake.

Mwanamke huyo alimfundisha mambo mengi sana, na Azra akampenda kama bibi yake. Weisiko alikuwa na kawaida ya kwenda India ili kutumia muda pamoja na "binti yake," na kwa kipindi cha miaka michache ambayo Azra aliendelea kuishi India, alipata aina fulani mpya ya furaha na kujihisi huru na salama. Lakini hilo lisingechelewa kuharibiwa.


★★★


Baada ya Azra kuwa ameishi India kwa miaka zaidi ya saba, Weisiko, sasa akiwa ni Luteni Jenerali, alikwenda na kumchukua kutoka huko ili kumrudisha nchini. Sasa akiwa ni mwanamke mdogo, aliyekuwa na sura nzuri na mwonekano wenye kuvutia, alirudi kwenye nchi yake ambayo hakuwa na kumbukumbu ya mambo mengi kuihusu. Hii Ilikuwa ni kwa sababu kwa kipindi chote alichoishi India alikuwa akipewa dawa kupitia Weisiko ambazo alifikirishwa zilikuwa zinamsaidia kiafya, lakini ndiyo zilikuwa zinafanya asikumbuke maisha yake ya zamani. Angalau wakati huu aliweza kuzungumza tena, na alijua lugha tatu; Kiingereza, Kihindi, na Kiswahili, ingawa hakuzungumza Kiswahili kabisa.

Luteni Jenerali Weisiko alimpeleka binti yake huyu kwenye makao yake mapya, ambako Ilikuwa ni kwenye moja kati ya nyumba za kifahari za Weisiko. Hii ingekuwa nyumba ya Azra pekee, naye alifurahia sana kuona kwamba "baba yake" alikuwa amempatia zawadi nzuri kama hiyo kwenye siku yake ya kwanza nchini humu. Alitarajia kwa hamu sana kuanza kukutana na watu wengine na hata kujenga marafiki, lakini matarajio yake yakazimwa baada ya Weisiko kumwambia kwamba asingeweza kwenda sehemu yoyote ile na kuchangamana na watu isipokuwa mpaka amwambie kufanya hivyo.

Kwa kutoelewa sababu, Azra aliuliza ni kwa nini, na ndiyo hapa Weisiko akaanza kuijaza akili yake kwa uwongo mwingi sana kuhusiana na maisha yake ya nyuma. Alimwambia sababu iliyofanya mpaka akashindwa kukumbuka mambo ya nyuma ni kutokana na ile "ajali" iliyompata, lakini kuna watu ambao waliisababisha ajali hiyo na hivyo kuharibu maisha yao wakiwa familia. Alimwambia kuwa watu kama hao wangetaka kumdhuru endapo wangejua aliokoka, na ndiyo sababu alimhamisha kutoka huku na kumpeleka Kerala. Akamwambia mafunzo aliyopokea kule yalikuwa ili kumsaidia awe imara, lakini pia endapo maadui wao wangewazingua basi amsaidie kuwafutilia mbali.

Azra alichanganywa sana mwanzoni. Alikuwa amefundishwa kutumia vipawa vyake KUJIHAMI na siyo KUUMIZA mtu, lakini Weisiko alichokuwa anamwambia ilikuwa kwamba endapo angemwomba amshughulikie mtu na kumwondoa kabisa, basi atii. Weisiko alijiweka kwenye upande ulioonekana kuwa mwema, akisema hangemwomba kamwe aue mtu asiyekuwa na hatia, bali wale tu ambao walifanya mambo mabaya kupitiliza. Akamwambia ndiyo sababu alihitaji kukaa kwa siri ili kulinda utambulisho wake. Kwa sababu Azra alimheshimu kama "baba yake" aliafikiana na yale aliyokuwa amemwambia, ijapokuwa moyoni mwake hakuhisi amani.

Kwa hiyo baada ya muda fulani kupita akiwa nchini, Azra aliendelea kukaa mwenyewe, na maisha kwake yalikuwa mazuri na ya hali ya juu kutokana na vitu alivyopewa na Weisiko. Hakuwa tu mtu wa kukaa ndani ya nyumba asubuhi mpaka asubuhi, kwa sababu mara kwa mara alitoka na kwenda kutembea sehemu mbalimbali akiwa mwenyewe, lakini kwa umakini wa hali ya juu. Aliwakumbuka sana baadhi ya watu waliokuwa kama marafiki kwake kule India, na hata mara kwa mara angehisi uhitaji wa kujenga marafiki huku, lakini Weisiko aliendelea kuwa karibu naye kama "baba" ili kutomfanya ahisi upweke.

Ndipo baada ya siku kadhaa kupita baada ya tukio la wizi wa trilioni 20 kwenye benki kuu, Luteni Jenerali Weisiko alikuja kwake na kumwambia kuwa angempa "mission" mpya iliyomhitaji kuwakamata watu wa kundi la Mess Makers na kuwaua. Azra alihofia kwamba huenda asingeweza kutimiza aliyotaka "baba yake," lakini Weisiko akamwambia hakupaswa kuogopa. Alimwambia njia walikuwa wameshamtengenezea, hivyo yeye angepaswa kufanya vitendo tu na kujiondoa sehemu za tukio haraka bila kutambulika. Alitumia kigezo cha kwamba Mess Makers waliumiza na kuua watu wengi tokea walipolipua mabomu kwenye majengo yale, na bado walikuwa wakiendelea kuisumbua serikali, hivyo msaada wake wa siri ungethaminiwa sana.

Azra alikuwa amefunzwa kuwa makini sana, hivyo aliuliza kwa kina mambo aliyohitaji kufanya, ikiwa labda angeshambuliwa na mtu ambaye hakutakiwa kumuumiza, naye Weisiko akatoa kibali cha kuua tu. Alimwambia ilikuwa ni muhimu kwake kufanikiwa katika yote aliyotakiwa kufanya, kwa sababu Raisi alikuwa ameiharibu nchi sana. Ijapokuwa mwanzoni Weisiko alimshawishi kwa kusema anafanya hayo kama njia ya kuwasaidia watu, Azra alikuwa na akili kutambua kwamba kwa jambo hili Weisiko alikuwa anamtumia kama silaha yake maalum, lakini akaacha iwe hivyo tu ili kumridhisha "baba yake" huyo.

Kazi ya kwanza katika mishe hiyo ilikuwa ni kuiweka timu ya Luteni Michael na ACP Nora karibu na macho yake, ili hatimaye aweze kuwafikia Mess Makers. Haikuwa rahisi kwake hata kidogo mara ya kwanza kabisa alipolazimika kuwaua wanajeshi wale watatu, Vedastus, Omari, na Mishashi, pamoja na Oscar Amari wa Mess Makers. Usiku huo alipotoka kwenye mauaji hayo aliyoyafanya kwa mikono yake mwenyewe, alikwenda sehemu ya mbali na kuanza kulia sana. Alilia mno, kwa kuwa ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kuondoa uhai wa wanadamu wenzake. Tokea alipopelekwa India, Azra alikuwa mwenye uhitaji wa kujua ni nini lililokuwa kusudi la maisha yake, na sasa ikawa ni kama limefunuliwa wazi mbele yake. Akaamua tu kuliishi sasa, kwa kuwa hicho ndiyo kitu alichotengenezwa kuwa; muuaji.

Weisiko alimmwagia sifa baada ya matokeo ya kwanza ya kile alichofanya, akifikiri kwamba Azra alifurahia sana, lakini kiukweli alikuwa amembomoa kupita maelezo. Furaha aliyokuwa amekuja nayo nchini ilitoweka kuanzia usiku huo alipowaua wanaume wale, na moyo wake ukaanza kugeuka kuwa mgumu zaidi kwa sababu ya hisia za kujichukia. Hakuwekwa wazi kuhusu mambo ambayo Mdeme alikuwa amefanya pamoja na kundi lake kwa muda mrefu, akifikirishwa kwamba yeye yuko upande sahihi kwa sababu ya uwongo ambao "baba yake" alikuwa akiilisha akili yake.

Kwa hiyo kutokea hapo angeendelea kutulia mpaka akiambiwa cha kufanya na Weisiko, naye angetekeleza aliyoambiwa ili tu kumfurahisha, mpaka wakati ambao aliagizwa kumuua Salim Khan....


★★★★


WAKATI ULIOPO....


Siku hiyo ambayo Salim Khan alinyongwa kwenye lifti kikatili sana, Azra alipatwa na jambo fulani ambalo liliisumbua akili yake baada ya kufanya mauaji hayo. Wakati akiwa anapigana na mmoja wa Mess Makers, yaani Lexi, alishindwa kuelewa ni kwa nini mwanamke huyo alijifichua kwake, halafu akaanza kumwita kwa jina la "Azra." Aliendelea kupigana naye, huku Lexi akijitahidi kumwambia aache, lakini Azra hakusikiliza na kufanikiwa kumpiga kwa mtindo wake uliommaliza nguvu Lexi mikononi.

Azra aliposhika kisu na kumfata Lexi akiwa na nia ya kuikata shingo yake, mkono wake ukasita baada ya akili yake kuanza kumwonyesha picha fulani ya mwanamke huyu, kama vile aliwahi kumwona kipindi cha nyuma. Alishindwa kuelewa hiyo ilikuwa ni kwa nini, lakini hisia aliyoipata ilimfanya ahisi ni kama anamfahamu, tena vizuri sana. Akashindwa hata kupitisha kisu kwenye shingo yake kutokana na kuchanganywa na hali hiyo, na ndipo wenzake na Lexi wakafika hapo.

Kwa sababu ya kutotarajia, Azra alishtuka na kuwa kama amepoteza umakini wake, na wakati Mensah alipomwelekezea bastola, akashangaa sana baada ya Lexi kumkinga na kupigwa yeye badala yake. Hapa ni kama umakini ndiyo ukamrudia, naye akatoka eneo hilo upesi na kukimbia kwa kasi yote. Akiwa anakimbia alisikia vizuri sana jinsi mwanamke yule aliyekuwa anakaribia kumchinja alipomwambia mwenzake kwamba asimpige (Azra) risasi, naye Azra akafanikiwa kukimbilia upande mwingine wa uwanja huo na kujificha pembeni ya ukuta; pakiwa na giza.

Maswali mengi sana yalipita kwenye kichwa chake. Mwanamke huyo alikuwa ni nani? Na kwa nini alimkinga asipigwe na risasi? Ni kwa nini alimwita kwa jina ambalo hakuwa na utambuzi wowote kulihusu? Na jambo la muhimu hata zaidi, ni kwa nini yeye Azra alishindwa kumuua alipopata nafasi rahisi zaidi? Kwa kukosa majibu sahihi na kufikiria hali aliyokuwa ndani yake, akaamua tu kuondoka eneo hilo haraka.


★★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★★

WHATSAPP +255 787 604 893
Mkuu hongera sana yaani unaandika simulizi kiuhalisia kabisa kama kweli vile.

Sent from my SM-J700H using JamiiForums mobile app
 
FOR YOU

Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Uhalifu, Mauaji, Visasi, Vita, Mambo yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA THELATHINI NA TATU

★★★★★★★★★★★★★★★★★★


Upande wa jengo lile ambalo mauaji ya milionea Salim Khan yalifanyika, maafisa wa usalama walikusanyika hapo muda mfupi tu baada ya tukio. Tayari baadhi ya waandishi wa habari waliokuwepo walichukua picha na video za lifti ile iliyoanguka kutoka juu ya ghorofa, na mambo mengi yaliulizwa kuhusu ni nini kilichotokea. ACP Nora alikwenda kule juu pamoja na Emiliana Ngoyi, Secretary Joachim, na maaskari wengine ili kuchunguza mkasa huo, na baada ya muda wakawa wamefanikiwa kuutoa mwili wa Salim kwa uangalifu sana; uliokuwa umejeruhiwa vibaya sehemu ya mkono.

Nora alighafilishwa sana na mambo aliyoona. Jambo hili lilimkumbusha kuhusu usiku ule ambao mmoja wa wale Mess Makers alimsaidia kwa kuwaua wanaume waliotaka kumtendea vibaya kimwili, naye akawa anajiuliza ikiwa ni huyo ndiye aliyefanya na ukatili huu pia. Lakini kwa nini? Mess Makers wangepata faida gani kwa kumuua Salim Khan, mwanaume ambaye alikuwa hagusiki? Alijadiliana na Emiliana pamoja na Joachim na kuona hata wao walihisi kuna mchezo mkubwa uliofanyika nyuma ya pazia. Kila shuku ilimwelekea mtu mmoja tu; Raisi Paul Mdeme, kwa kuwa ilikuwa wazi kwa mtu yeyote kwamba jambo alilofanya Salim la kuiachia miradi ya serikali halikumfurahisha Raisi, hivyo tukio la namna hii moja kwa moja lingefanya aelekezewe vidole. Lakini muda si mrefu lawama ikapata mfadhili.

Maaskari waliochunguza chuma la lifti iliyoharibiwa walipata kibandiko (sticker) cha aina ile ile walichotumia Mess Makers kila walipofanya tukio fulani, yaani sura ya simba mweupe anayenguruma. Kilikuwa kimebandikwa kwenye sehemu ya chuma iliyokunjika, na mkataa wa haraka uliofikiwa ukawa kwamba Mess Makers ndiyo waliohusika na mauaji ya Salim Khan pamoja na walinzi wake. Jenerali Jacob na Luteni Jenerali Weisiko wakaongea mambo machache kuhusiana na "ushahidi" huo, wakisema kwamba kwa sababu ya kitendo hicho, Mess Makers walihitajika wakiwa hai au wamekufa. Jenerali Jacob akaahidi kwamba angewakamata wote na kuhakikisha wanalipia kwa kifo cha Salim, na baada ya hapo yeye na Weisiko wakaondoka tu.

Kibandiko hicho chenye picha ya simba kilikuwa ni uthibitisho kwa wengi hapo kwamba Mess Makers ndiyo waliohusika na mauaji, lakini kwa Nora haikuwa hivyo. Alielewa kwamba kuna mambo ambayo yaliingiliana baina ya serikali, milionea huyo, na hao Mess Makers, lakini bado uthibitisho huo haukumshawishi kabisa kwamba ni Mess Makers ndiyo waliofanya haya. Akili yake ikamwambia kwamba kuna mtu alitaka ionekane hivyo ili kuficha utambulisho wake, na hakuna yeyote ambaye angefikia kiwango cha juu cha kushuku isipokuwa Raisi Paul Mdeme. Lakini akaona akae kimya kuhusiana na wazo hilo.

Baada ya muda, wengi waliokuwa eneo hilo wakatawanyika, naye Nora akarejea kule hotelini kwake kupumzika. Gumzo lililokuwa limeanzishwa kwa sababu ya tukio hilo lingeendelea kwa muda mrefu sana, Nora alijua hilo. Kwa hiyo kuanzia sasa alitambua angepaswa kuzama zaidi kwenye utafiti wake wa matukio haya, hasa kwa sababu mambo mengi yalikuwa yanaingiliana kwa njia zenye kuchosha sana akili. Jambo lingine muhimu zaidi kwake ilikuwa ni kujua Lexi ni nani hasa, kwa sababu baada ya kugundua kuwa naye alitokea Ghana kama tu Oscar Amari, kichwa chake kilimsumbua mno kwa maswali.

Uwezekano wa mwanamke yule kuingia kwenye maisha yake ili kumzunguka ulionekana kupatana na akili, lakini bado alitumaini yale yote ambayo alihisi kumwelekea hayakuwa ya kweli. Akaamua kuingia kulala tu, ili kesho aanze kutafuta ukweli kwa nguvu zote.


★★★★


"CHINI"


Mess Makers wanne waliokuwa kwenye tukio lililompata Salim Khan walikuwa wamefanikiwa kuondoka Dar es Salaam na kufika kule kwenye nyumba yao ya maficho, a.k.a "chini." Ilikuwa imewachukua masaa kadhaa kama kawaida, na sasa Lexi alikuwa amerejesha nguvu mwilini mwake. Safari nzima ya kuelekea huko, wengine walikuwa wakiongelea kuhusu jambo lililompata Salim Khan, huku mara kwa mara Lexi akisemeshwa, lakini hakutoa jibu lolote. Alikuwa kimya mwanzo mwisho mpaka wanafika huko.

Kendrick, Torres, na Kevin waliwapokea wenzao, ikiwa inakaribia alfajiri kabisa sasa, naye Victor akaanza kuwasimulia jinsi mambo yalivyokuwa huko kwa mara nyingine tena. Akaeleza jinsi Lexi alivyofanikiwa kumkamata muuaji yule, na kwamba alikuwa ni mwanamke, lakini kwa sababu fulani isiyojulikana Lexi akamwachia akimbie, huku tayari akiwa ameiona sura yake. Kendrick alishangaa na kumuuliza Lexi, ambaye alikuwa ameegamia ukuta kwa njia legevu, aeleze ni sababu gani iliyomfanya afanye uzembe wa hali ya juu namna ile.

Mensah hata akaongeza kwa kusema kwamba alikuwa anamfyatulia risasi mtu yule lakini Lexi akamkinga ili zisimpate. Kendrick alijua Lexi asingefanya hayo bila kuwa na sababu kuu, hivyo akasisitiza Lexi ajieleze. Lexi alikuwa anatafuta namna ya kusema kile alichoona, lakini hisia zikamlemea na kusababisha aanze tu kulia. Alikuwa akijaribu kutoa maneno lakini yanazibwa kwa kilio cha chini kilichoonyesha uchungu mwingi, na hali hiyo iliwatatiza sana wengine. LaKeisha akasogea karibu yake na kuanza kumpangusa machozi kwa kujali, akimuuliza pia tatizo lilikuwa ni nini, naye Lexi akamwangalia Kendrick kwa huzuni na hatimaye kumwambia ukweli.

"Huyo mwanamke... uncle Kendrick... huyo mwanamke ni Azra!" Lexi akamwambia huku akilia.

Kendrick akabaki kushangaa. "Nini?" akamuuliza.

"Azra? Nani Azra?" LaKeisha akauliza pia.

"Lexi unamaanisha nini?" Kendrick akamuuliza tena.

"I don't know... sielewi yaani... oh God!" Lexi akaongea na kuinamisha uso wake kwa huzuni.

"Boss... what is she talking about? (anaongelea nini?)" Mensah akamuuliza Kendrick.

Kendrick akashindwa ajibu nini. Hiki ni kitu ambacho hata yeye kilimchanganya sana. Akamsogelea Lexi karibu zaidi na kumshika mabegani.

"Lexi... unamaanisha kwamba... mtu aliyemuua Oscar... ni Azra?" Kendrick akauliza.

Lexi akatikisa kichwa kukubali.

Kendrick akachoka. "How is that possible? (hiyo inawezekanaje?)" akauliza.

"Jamani, si mgetuambia nini kinaendelea... hii show yote ya nini?" Kevin akauliza.

"Kevin, nakuomba uondoke hapa sasa hivi kabla sijageuka!" Kendrick akasema kwa hasira.

Kevin akashangaa. Alipomwangalia Torres, akamwonyesha kwa ishara ya kichwa kuwa aondoke, naye Kevin akatii na kuanza kuondoka. Lakini alijifanya tu kuondoka, kwa kuwa alipofika usawa wa kuta nyingine alijibanza na kutulia hapo ili ajue kilichoendelea.

"Lexi... una uhakika? Una... una uhakika kabisa na ulichokiona?" Kendrick akamuuliza.

"Ndiyo. Nimemwona usoni uncle. Ni yeye kabisa!" Lexi akamwambia.

"Boss, Azra ndiyo nani?" LaKeisha akauliza.

"Azra ni mdogo wake Lexi," Torres akasema.

LaKeisha akamwangalia kimaswali. Hata Victor na Mensah wakashangaa pia.

"Mdo...? That bitch is your sister?! (yule malaya ni dada kwako?)" LaKeisha akauliza akiwa haamini.

"LaKeisha!" Kendrick akamzuia kuongea vibaya.

"Kivipi? Si ulisema... familia yako na hata ya boss ziliuliwa na Weisiko na Jacob? Huyo Azra ni wa wapi?" akauliza Victor.

Lexi akakaa chini akihisi uchovu wa hali ya juu; siyo wa akili, siyo wa mwili. Kendrick akachuchumaa na kumtazama usoni.

"Lexi... tuliwaona. Mimi na wewe tuliwaona wote wakiwa... hii inawezekanaje?" Kendrick akauliza tena.

"Boss... hapa kuna mchezo umefanyika. Inawezekana hata huyo assassin amevaa tu sura inayofanana na mdogo wake Lexi. Tusiwe emotional sana labda ndiyo kitu maadui zetu wanachotaka," akasema Victor.

"I agree (nakubali)," LaKeisha akasema.

"Hapana. Hapana, ilikuwa ni yeye. I know her. Najua ilikuwa ni yeye," akasema Lexi.

Kutokea pale Kevin alipokuwa amejibanza, alikuwa amesikia mambo yote yaliyosemwa, naye akatikisa kichwa chake kwa kukerwa sana, kisha akaondoka tu na kuelekea chumbani.

Torres akasogea mpaka Lexi alipokaa na kumshika begani.

"Lexi... najua kuna vitu vingi sana unawaza. Lakini kwanza, unahitaji kurudisha uimara wako mwilini na akilini. Kuna jambo ninataka tuzungumze, wote kwa pamoja, na nitahitaji focus yako nzuri, kwa hiyo nakuomba ujitahidi kuiweka akili yako sawa kwa sababu kuna mambo mengi tunahitaji kufanya. Please..." Torres akasema kwa ustaarabu.

"Unahitaji tuongelee kuhusiana na Salim Khan?" akauliza Lakeisha.

"Ndiyo. Kutia ndani na Azra pia," Torres akasema na kumwangalia Lexi.

Lexi akamtazama kwa umakini, kisha akaanza kujinyanyua taratibu.

"Umepata nini kuhusu Azra?" Lexi akauliza.

"Unahitaji kupumzika kwanza Lexi. La sivyo sitakwambia lolote," Torres akasema.

"Ndiyo Lexi. Hapo najua una maumivu. Unahitaji kupumzika. Twende," LaKeisha akamwambia huku akimvuta taratibu.

Lexi akawa anaangaliana sana na Kendrick, ambaye alibaki kumwangalia tu kwa hisia mpaka LaKeisha alipofanikiwa kuondoka naye na kuelekea upande wa juu wa nyumba hiyo. Torres akamtazama tu Kendrick kwa ufupi, naye akamshika begani kama kumpa kitia moyo, kisha yeye pamoja na Victor na Mensah wakamwacha peke yake akiwa amesimama hapo mwenyewe. Akaanza kumkumbuka sana rafiki yake kipenzi, ambaye alipoteza maisha kikatili na kumwachia malezi ya mwanae huyu ambaye alikuwa akipitia mambo mengi magumu kihisia.

Kendrick akashusha pumzi kwa kufadhaika sana na kuuliza hivi, "Kwa nini mambo yanakuwa magumu namna hii kwa huyu mtoto Casmir?"


★★★★


Siku hii mpya ilipoendelea kupitisha muda, tayari baadhi ya mashirika ya serikali yalikuwa yamesafisha "uchafu" uliokuwa umebaki baada ya tukio lililompata Salim Khan. Kwa sababu ilionekana kwamba ni Mess Makers ndiyo walimuua mwanaume huyo, Raisi kupitia wawakilishi wake alitoa tamko kwamba kuanzia wakati huu, wangefanya msako wa hali ya juu kupita maelezo kwenye nchi yote ili kuwakamata hao watu. Yaani wananchi waliambiwa mapema kuwa wasishangae endapo maaskari au wanajeshi wangeingia kwenye nyumba zao kama migambo, kwa sababu msako huu sasa ungekuwa mkubwa kuliko mwanzoni. Lakini hii yote ilikuwa ni njia ya serikali ya kujikosha tu ili kuwapa watu matumaini bandia.

Raisi Paul Mdeme alikutana na wenzake waliobaki kwenye kundi lao siku hii huko Ikulu. Gavana wa Benki Kuu Laurent Gimbi alikuwa na mashaka kuhusu jambo lililompata Salim, naye aliuliza ikiwa Raisi alihusika katika kifo chake. Mdeme kama kawaida alikataa, akiwashawishi wengine wakubali kwamba ilikuwa ni Mess Makers, huku Jenerali Jacob na Luteni Jenerali Weisiko wakiwa wanaujua mkanda mzima.

Kwa hiyo sasa swali likabaki kuwa baada ya kifo cha Salim ni nini kingefuata, naye Mdeme akawaambia kwamba angetumia uchochezi wake ili kujiingiza katika sehemu ya mali ambayo Salim aliacha. Yaani, angeongea na baadhi ya watu au wanasheria wa Salim Khan waliosimamia miradi yake ndani na nje ya nchi, kwa njia ya kuwalaghai ili sehemu kubwa ya mali za Salim zitumike kumuunga mkono yeye na serikali yake tena.

Hii ilikuwa ni kwa sababu Mdeme alijua kuhusu mambo mengi haramu aliyofanya Salim na kumfichia kwa kipindi kirefu, kwa hiyo angeyatumia hayo kuwalaghai watu waliobaki kusimamia mali na miradi ya Salim. Hangeweza kufanya hivyo wakati Salim alipokuwa hai kwa kuwa jamaa pia alijua mambo mengi kumhusu Mdeme na alikuwa na nguvu sana, lakini kifo chake kilifanya nguvu hiyo ipungue kwa sababu wengine hawakujua kuhusu muungano wao.

Ingawa Makamu Eliya, Waziri Yustus na Gavana Laurent waliona hilo kuwa hatari, Jenerali Jacob na Weisiko wakamuunga mkono Raisi Mdeme na kuwashawishi wengine kufanya hivyo. Kihalisi, hiyo yote ilikuwa ni sehemu ya mpango wa Jenerali Jacob, ambao alimpatia Mdeme na kumfanya aridhike nao. Kwa hiyo baada ya wengine kumuunga mkono Raisi pia, sasa ambacho kingefuata ingekuwa ni utekelezaji tu.

★★

Kwa upande wa timu ya Luteni Michael, mambo hayakuwa mazuri sana kwake ijapokuwa kiujumla hayakuwa mabaya. Baada ya tukio la Salim Khan, alitafutwa na Kanali Oswald Deule kwa njia ya simu na kuambiwa aende kukutana naye kwenye jengo maalum la kijeshi, ambako ndiko ofisi za viongozi kama yeye zilikuwa. Luteni Michael alikwenda huko siku hii, na baada ya kukutana na Kanali Oswald, akaambiwa kwamba kuanzia sasa msako huu wa Mess Makers angeushughulikia yeye moja kwa moja. Yaani, uhuru aliokuwa amempatia tokea ACP Nora alipojiunga na msako huo sasa ungeondolewa, kwa hiyo kila jambo lingefanywa kwa mwelekezo wake moja kwa moja na si vinginevyo.

Hii ilimshangaza kiasi Luteni Michael, kwa sababu ilikuwa ni kama anaondolewa kwenye uongozi wa msako huu kwa njia isiyo ya moja kwa moja. Kanali Oswald akamwambia hiyo ilikuwa ni kwa sababu kwa muda sasa Luteni Michael amekuwa hafanyi kazi aliyopewa na badala yake kuendekeza hisia za kijinga, yaani kumwelekea ACP Nora. Luteni Michael alishangazwa na ni jinsi gani Kanali Oswald angejua kuhusu hisia zake kwa Nora, lakini akamwambia kwamba hilo lilikuwa nje ya masuala ya kazi, na hajaliingiza popote kwenye msako wao muhimu.

Ndipo Kanali Oswald akamwambia anajua Luteni Michael alikuwa anapoteza tu muda wake kumfata ACP Nora na kupiga mwanamke mwingine ambaye ni rafiki tu, kwa sababu alikuwa anasumbuliwa na wivu wa kipuuzi. Akamwambia kama Jenerali Jacob angepata kujua kuhusu mambo aliyokuwa anafanya basi anafahamu ni jinsi gani hiyo ingemwathiri vibaya. Luteni Michael akaomba tu samahani kwa heshima, naye Kanali Oswald akamwambia hahitaji samahani yake bali utekelezaji wa kazi. Akamwonya kwa kusema ikiwa angepata tena taarifa kuhusu mambo hayo aliyoyaona kuwa ya kitoto, basi angemjulisha Jenerali Jacob ili amshughulikie yeye mwenyewe. Alimwambia ajitahidi kukaa mbali na ACP Nora, kwa sababu baba yake hakuwa mtu wa kucheza naye kabisa.

Luteni Michael hakuwa aina ya mwanaume wa kuogopa vitisho vya "nitakusema kwa baba" hata kidogo, lakini kwa sababu ya nidhamu yake ya kijeshi, akakubali ushauri wa Kanali na kumwambia makosa ya namna hiyo hayangejitokeza tena. Kwa hiyo baada ya hapo Kanali Oswald akamruhusu aondoke ili akawajulishe na wengine kuhusu "mabadiliko" hayo.

Luteni Michael alirejea kwa timu yake akiwa amekwazika kiasi. Siyo kwa sababu ya Kanali Oswald kumwambia angepaswa kujiweka chini kwenye msako huu, ila ni jinsi ambavyo watu walihukumu hisia zake. Kuanzia kwa Nora, baadhi ya vitu wanajeshi wa timu yake walivyomwambia, na hata maneno ya siku ile ya Lexi, yalimfanya ajiulize ikiwa labda kweli hakujua alipotakiwa kuwa. Lakini akajikaza tu kiume na kwenda kuwafikishia wengine taarifa mpya. Bobby, Alex, Mario na Hussein walishangaa kiasi, wakiuliza ikiwa hiyo ilimaanisha kwamba hangewaongoza tena, lakini akasema ni kwenye msako huu tu na si vinginevyo.

Akawaita Mario na Hussein pembeni baada ya hapo na kuwauliza ikiwa walimwambia yeyote kuhusiana na yaliyotokea kwenye chumba cha Nora siku ile, lakini wote wakakanusha. Akawauliza kwa mkazo iliwezekana vipi Kanali Oswald akajua kuhusu hilo, kwa sababu Nora hakuwa aina ya mwanamke ambaye angemwambia mwanaume yule. Mario alisema wazi kwamba hakuna yeyote aliyemwambia, naye Hussein akakataa pia. Lakini Hussein akawa ametambua kwamba huenda alifanya makosa makubwa, kwa sababu ni yeye ndiyo aliyesema kuhusu kilichotokea siku ile kwa Aliyah; mpenzi wake mpya. Akajiuliza ikiwa Aliyah alimwambia mtu mwingine, na kama alifanya hivyo basi mapenzi yote aliyomwonyesha usiku ule yalikuwa ni kwa ajili ya kumpeleleza.

Baada ya Luteni kuwaacha, Hussein alikwenda faragahani kuongea na Aliyah na kumwambia anajua ni yeye ndiye aliyefanya uchongezi. Alimwambia kwa njia ya moja kwa moja kama vile anajua kila kitu tayari, naye Aliyah akafunguka kwa kusema ni kweli; alimtaarifu Tariq kwa kuwa Kanali Oswald aliwaweka wampe taarifa zilizofichwa kwake. Kufikia wakati huu Aliyah alikuwa amempenda sana Hussein, hivyo akamwomba samahani na kuahidi hangemchongea tena. Hussein alikasirika na kumwambia asingeweza kuendelea naye tena kwa sababu uhusiano wao ulijengwa kwa uwongo, kwa hiyo kuanzia siku hii wangekuwa wamemalizana kimapenzi, na kubaki kuwa na uhusiano wa kikazi pekee.

★★

Kwa upande wake Nora, alikuwa ameamkia ofisini kwake kuendelea na uchunguzi wa hapa na pale kuhusiana na Lexi, Kevin Dass, pamoja na Oscar Amari. Alikuwa akijaribu kuunganisha mambo ambayo yangepatana kuhusiana na watatu hawa ili kubaini ikiwa Lexi alikuwa ni mmoja wao. Tokea walipoachana jana asubuhi na Lexi kusema alikwenda nje ya mkoa, Nora hakuwa amempata tena kila alipojaribu kumpigia.

Baada ya tukio lililotokea usiku wa jana kiukweli mashaka kumwelekea yaliongezeka, lakini bado Nora hakuwa amepata jambo lolote lenye kuongezea mashaka yake kumhusu "mwanamke" huyo. Kama tu jinsi ambavyo taarifa nyingi kuhusu maisha ya zamani ya Kevin Dass na Oscar Amari zilivyokuwa zimefichika, ilikuwa namna hiyo hiyo kumwelekea Lexi ingawa mengi ya maisha yake ya kawaida akiwa huku kwa wakati huu yalikuwa wazi.

Wakati akiendelea na tafiti za Mess Makers na Salim Khan pia, akapigiwa simu na Kanali Oswald Deule, ambaye alimtaarifu kwamba sasa taarifa zozote za kazi alizofanya angempatia yeye na siyo Luteni Michael. Nora akauliza sababu ya badiliko hilo, naye Kanali akamwambia ni ili wafanikiwe zaidi wakati huu kwa sababu ilionekana kama kazi imemlemea sana Luteni Michael. Jeshi la Nchi mpaka sasa halikuwa limepata matokeo mazuri, na Jeshi la Polisi nalo ndiyo kabisaa, kwa hiyo akasema kwamba yeye kuingia tena moja kwa moja kungebadili mambo.

Nora hakuwa na kipingamizi, naye akamwambia kufikia sasa bado hakuwa amepata jambo lolote jipya. Kanali Oswald akamwamuru afanye kazi kwa uharaka kwa sababu walikuwa wameshawadekeza hao Mess Makers vya kutosha, na sasa eti chini ya utawala wake hilo lingekwisha. Nora alimwona kuwa aina ya wale viongozi wanaojali sana sifa, kwa hiyo akampuuzia tu na kukata simu.

Wazo la kumuuliza Luteni Michael ni kwa nini mambo yalikuwa yamebadilika ghafla lilimwingia, lakini hakuona umuhimu wa kumtafuta mwanaume huyo hasa ukitegemea na jinsi hali ilivyokuwa mbaya baina yao. Alijua Michael alisema alitazamia wangeongea tena vizuri, lakini yeye Nora bado hakuwa tayari. Akaendelea tu kutulia ofisini kwake akiitazama moja kati ya picha za Lexi, akimtafakari sana mwanamke huyu aliyekuwa "ameuteka moyo wake."

Baadae alitoka na kuelekea kule Sea House. Wakati huu angekuwa peke yake, lakini ni kama kila kitu kuhusu sehemu hiyo kilimkumbusha mara zote alizokutana na Lexi. Akapata vinywaji, kisha akaenda mpaka ile sehemu ya fukwe ambayo Lexi alimwonyesha. Alikumbukia maongezi yao, alikumbukia kuhusu jinsi Lexi alivyoficha tattoo zake, na jinsi alivyombusu kwa mara ya kwanza kabisa wakiwa sehemu hiyo. Kuwaza kwamba huenda kila kitu kuhusu jinsi mahusiano yao ya kirafiki yalikuwa yamejengwa kwa uwongo kulimtatiza sana, naye akajikuta anakaa tu hapo kwa muda mrefu mno akitafakari vitu vingi.

★★

Upande wa Mess Makers. Siku hii ilikuwa imeanza kwa kikao kidogo cha kundi hili kilichoongozwa na Torres. Alikuwa anataka kuwaeleza mambo fulani kuhusiana na yaliyotokea siku ya jana, na angalau kwa wakati huu Lexi alikuwa ametulia zaidi kihisia baada ya kutumia muda fulani kupumzika.

Torres kama kawaida alianza kuyaorodhesha mambo kwa jinsi yalivyotokea mpaka Salim Khan kuuawa, naye akafikia mkataa kuwa huo ulikuwa ni mpango wa Jenerali Jacob bila shaka. Aliwaeleza kwamba kwa kumuua Salim, hii ingempa Raisi Mdeme nafasi ya kujiingiza kwenye mfumo wa mali alizoacha milionea huyo na hivyo kuiinua miradi ya serikali, lakini kwa sababu lawama ya kifo cha Salim ilielekezwa kwao, hii sasa ilimaanisha hata watu wa nje waliokuwa na ukaribu na mwanaume huyo wangeingizwa ili kuwasaka Mess Makers kwa njia tata zaidi, na hiyo ingeongeza hatari kwao zaidi ya ilivyokuwa mwanzo.

Kwa misingi hiyo, Torres akawaambia ingebidi waharakishe zaidi mpango wao wa mwanzo, mpango uliofanya waibe zile trilioni 20, kwa sababu muda usingekuwa rafiki kwao na ingefika tu siku ambayo sehemu yao ya maficho ingejulikana. Walitakiwa kuharakisha mpango wao ili isiwafikie wakiwa hawajaukamilisha.

Baada ya wote kuonyesha wamemwelewa, sasa Torres akaanza kuzungumzia kuhusiana na helicopter ile iliyofika kule juu ya ghorofa usiku wa jana na kutokomea. Aliwajulisha kuwa alifanya uchunguzi na kubaini kwamba Salim Khan hakuwa na nia ya kuondoka kwa gari tena. Alikuwa ameagiza helicopter ifike pale ili akimaliza mahojiano apande kuelekea juu na kuingia, kisha ndiyo aondoke; kimtindo yaani. Lakini helicopter ambayo ilifika haikuwa ile iliyotakiwa kwenda hapo, kwa sababu ilifika dakika 30 kabla ya muda hususa ambao ile halisi ilitakiwa kufika.

Bila shaka helicopter hii ndiyo iliyomshusha mwanamke yule ambaye Lexi alimtambua kuwa Azra, naye Torres akawaambia baada ya kuifatilia na kujua ilikotokea, alitambua ni nani aliyeiendesha, mwanaume aliyeitwa Khalid Juma, ambaye ni mmoja wa wanajeshi maalumu wa vikosi vilivyoongozwa na Luteni Jenerali Weisiko. Akasema inaonekana Azra alipotoka kwenye jengo lile na kuelekea kwenye ule uwanja, hiyo helicopter ilitakiwa kuwa hapo ikimsubiria, lakini kwa sababu Torres alikuwa ametumia njia za kiteknolojia kupata taarifa hizo, aliyeiongoza helicopter hiyo alitambua hilo, na hivyo akaona asirudi nyuma kwa kuwa alihofia labda ni vyombo vya usalama ndiyo vilikuwa viki-hack mifumo yake. Kokote Khalid alikoipeleka helicopter baada ya hapo Torres hakuweza kuifatilia tena, na huenda hiyo ilimaanisha waliiharibu mifumo yake au labda helicopter nzima kama tu Lexi alivyokuwa ametabiri.

Kwa hiyo, kilichokuwepo sasa ilikuwa ni kumkamata mwanaume huyo wa kijeshi, Khalid Juma, ili awaambie ni nani aliyempa amri ya kuiongoza helicopter ile kumpeleka Azra mpaka jengoni pale kufanya mauaji, na huenda taarifa ambazo wangezipata zingewasaidia kumkamata Azra. Lexi akakubaliana na hilo upesi na kusema wangepaswa kuanza kulishughulikia haraka, lakini Kevin akawaambia wote kwamba haikujalisha muuaji huyo alikuwa ni nani, walipaswa kumlipizia kisasi Oscar kwa sababu aliuliwa kikatili kupitia mtu huyo. Hawakupaswa kumfata ili kumkamata, bali kumuua. Kevin hakuelewa uzito wa kile alichokuwa anasema, kwa sababu alipenda sana kutanguliza maoni ya kibinafsi, na ingawa ilionekana hoja zake zina usahihi, hicho ni kitu ambacho hata yeye mwenyewe alijua kingepingwa tu.

Lexi akamuuliza Kevin vipi ikiwa angegundua kwamba muuaji wa rafiki yake ni dada yake wa damu, angefanya nini? Kwa kiburi Kevin akajibu kwamba angemuua tu. Lexi akamsikitikia sana, naye akamwambia alikuwa amepanga kumtumia na yeye kwenye mishe hii ya kumkamata Azra, lakini kwa sababu ya jibu lake lisilo la akili, angeendelea kubaki huko huko "chini." Kevin akaudhika sana, lakini hakuwa na njia ya kuweka kipingamizi. Lexi akamwambia Torres ampe maelezo kuhusu huyo Khalid Juma, na baada ya Torres kumweleza mambo machache kumhusu mwanajeshi huyo, Lexi akasema angekwenda leo leo kumfata; yeye pamoja na Victor na Lakeisha pekee.

Torres angetakiwa kubaki huko "chini" ili Lexi akifanikiwa kumpata mwanaume huyo na kumnyonya ukweli basi ampe taarifa (Torres) ili wapange njia nzuri ya kumkamata Azra. Kendrick akakubaliana na mawazo hayo, naye akasema kuna mambo anahitaji kuendelea kupangilia kwenye zile kampuni zake, hivyo angeondoka pamoja na Mensah kuelekea Geita kwanza. Kwa hiyo kwenye maficho yao wangebaki Torres na Kevin mkalia ndoo.

Hivyo bila kuchelewa, Lexi, LaKeisha na Victor wakaondoka hapo na kurudi Dar kumsaka Khalid Juma, ili hatimaye waweze kumpata Azra.


★★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★★

WhatsApp +255 787 604 893
 
FOR YOU

Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Uhalifu, Mauaji, Visasi, Vita, Mambo yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA THELATHINI NA NNE

★★★★★★★★★★★★★★★★★★


Kutokana na maelezo kuhusu Khalid Juma ambayo Torres alikuwa amewapatia, Lexi, LaKeisha na Victor wakaunda mpango mdogo tu wa kuweza kumnasa mtu huyo. Kama ni kitu ambacho watu kama Khalid walipenda, basi ilikuwa ni starehe na wanawake. Torres alikuwa amemsoma na kujua kuwa alipenda sana kwenda sehemu za starehe pamoja na marafiki zake wa jeshini, na mara nyingi walichukua wanawake kwa ajili ya kujitumbuiza. Kwa siku za karibuni mwanaume huyo hakuwa akienda sehemu aliyozoeleka, lakini bado angetafuta wanawake wa kujifurahisha pamoja nao.

Lexi alitaka kujua kwa nini mtu wa namna hiyo aliyejiachia kipuuzi tu angepewa "mission" ya kumwongoza muuaji hatari sana kwa helicopter. Huenda labda ilikuwa ni yeye tu ndiye aliyejua kuongoza helicopter, au katika kundi la wanajeshi waliotumiwa kufanya maovu ya Jenerali Jacob na Weisiko na yeye alikuwemo, na hivyo alijiamini kupita kiasi. Kwa vyovyote vile, siku ya leo isingekwenda vizuri kwake kwa sababu hiyo hiyo ya kujiachia sana.

Ikiwa imeshafika usiku, Mess Makers walipata kujua kwamba sasa Khalid Juma alikuwa amekwenda kwenye kumbi moja kubwa ya starehe, ambapo wengi wa "marafiki" zake walikuwepo pia. Wangechezewa dansi na wanawake waliovaa nusu utupu kwenye zile sehemu za watu muhimu zaidi (VIP), kisha wangechagua mwanamke wa kutoka naye ili kwenda kula bata, yaani bata.

Mpango rahisi wa Mess Makers hapa ulikuwa ni LaKeisha. Dada aliingia kwenye kumbi hiyo, akiwa amevalia nywele za wigi jekundu, na akiwa na mwonekano wenye kuamsha hisia sana. Alikwenda mpaka sehemu iliyoelekea kwa ma-VIP, lakini akazuiliwa kupita. Ila baada ya mmoja wa wanaume waliokuwa huko kumwona jinsi alivyokuwa mrembo, akawaambia mabaunsa wamruhusu apite, naye akaenda hapo na kuanza madoido sasa.

Kulikuwa na wanawake kadhaa hapo wakicheza na wengine wakiwa wamewakalia wanaume hao, naye LaKeisha akaanza kucheza pia. Siyo kwamba wengine walikuwa hawachezi vizuri, lakini LaKeisha alikuwa mtaalamu sana. Alikuwa anatumia mitindo mingi iliyowavutia wanaume hao, mitindo ya Ghana huko, na wengi wakawa wanamwangalia kwa matamanio. Baada ya karibia wanaume wote hapo kuonyesha kumtaka, yeye LaKeisha akamchagua Khalid Juma, ambaye alifurahi kupita maelezo. Mwanamke alimchezea mwanaume huyo mpaka akawa anamwaga tu hela kama kichaa vile, lakini LaKeisha hakujali pesa.

Lakeisha akaonyesha wazi kwamba alitaka watoke, naye Khalid hakukwaza. Akanyanyuka na kutoka naye sehemu hiyo ili waelekee kwenye vyumba, lakini LaKeisha akamwambia alitaka waende sehemu tofauti na kumbi hiyo ili ampe burudani bila makelele ya watu wengine. Khalid hakupinga, naye akatoka pamoja na "bebe" wake mpya na kwenda mpaka kwenye gari lake, na safari kuelekea kwenye hoteli ikaanza. Njiani LaKeisha alikuwa anamwambia Khalid maneno mengi yenye kusisimua, huku sikioni mwake akiwa na kifaa kidogo cha sauti kilichounganishwa kwa Lexi na Victor, ambao walikuwa wanasikia kila kitu anachosema ili kujua walikuwa wamefika wapi.

Baada ya mwendo wa dakika chache, gari la Khalid lilifika sehemu ya barabara isiyokuwa na makazi kwa pande hizo na kukanyaga kitu kama msumari kilichosababisha pancha. Ikabidi wasimame kwanza, naye Khalid akamwambia Lakeisha angeenda kubadili tairi upesi. Lakeisha akamwambia angemsaidia, hivyo wote wakashuka na kurudi mpaka nyuma ya gari. Lakini wakati tu Khalid alipotoa tairi, akashtuka sana baada ya kugeuka na kukuta watu wengine wawili waliovalia nguo nyeusi mwili mzima, na vitu usoni vilivyoficha nyuso zao, huku mmoja akiwa amemwelekezea bastola. Ilikuwa ni Victor na Lexi, na Victor akiwa ndiyo ameishikilia bastola akamwamuru Khalid anyooshe mikono yake juu.

LaKeisha akaanza kujifanya kuogopa, akimng'ang'ania Khalid huku anatetemeka eti, naye akamuuliza wangefanya nini. Khalid akamwambia asiogope kwa sababu hao wahuni hawakujua yeye ni mwanajeshi, hivyo angejifanya kuwatii halafu angewazunguka haraka na kuwadhibiti. Victor akarudia kumwambia anyooshe mikono yake na kugeukia gari, naye Khalid akafanya hivyo. Victor akaigiza kumwambia LaKeisha kwa ukali kwamba akimbie haraka sana la sivyo angemfyatua kwa risasi, lakini Khalid akajifanya mkaidi na kugeuka nyuma huku akiwaambia wawili hao kwamba kama walitaka pesa basi angewapa, lakini wasimuumize mpenzi wake. LaKeisha akazungusha macho kikejeli, kisha akaendelea kujifanya anaogopa.

Lexi akaushusha mkono wa Victor ulioshika bastola, naye akaanza kumfata Khalid. Akakunja ngumi kuonyesha anataka wapigane, naye Khalid akakunja ngumi kwa kujiamini na kumwambia LaKeisha kwa sauti ya chini angewashughulikia wote kwa zamu kisha wangeondoka, hivyo asiwaze. Yaani walikuwa wanamfanya jamaa kuwa mpumbavu sana, kwa sababu pale tu alipomfata Lexi ili kumpiga, Lexi akamzunguka na kumpiga kwa mtindo mmoja tu uliofanya jamaa apoteze fahamu. LaKeisha na Victor wakaanza kucheka, kisha Victor akamsaidia Lexi kumfunga Khalid mikono na miguu kwa kamba ngumu, na mdomo na macho yake pia kwa kutumia kitambaa, halafu wote wakasaidizana kumweka kwenye buti la nyuma la gari walilokuwa wameegesha upande wa pembeni kwa kificho.

Wakaondoka eneo hilo na kumpeleka sehemu ya mbali iliyokuwa na msitu wenye giza zito, nao wakamtoa na kumkalisha kwenye kiti cha chuma walichokuwa wamekiweka huko tayari. LaKeisha alikuwa ameshavua nguo zile zilizomfanya aonekane kama anajiuza. Kuigiza kwao kwamba LaKeisha hakujuana nao ilikuwa ni kwa sababu Khalid alikuwa ameiona sura yake. Hivyo ilitakiwa ionekane kwamba LaKeisha kweli alikuwa mtu wa kawaida tu, ili hata wakimwachia Khalid baadae basi asifikiri LaKeisha alikuwa mmoja wao.

Baada ya sekunde chache, Khalid akarejesha fahamu na kujikuta akiwa amefungwa huku ameketi sehemu asiyokuwa na utambuzi kuihusu. Bado macho yake yalifunikwa kwa kitambaa, lakini kutokana na upepo mkali na baridi alilohisi aliweza kutambua kwamba wako nje. Akaanza kusikia hatua zikimkaribia, na hofu yake ikapanda kwa kiasi fulani. Akahisi mdomo wake ukitolewa kitambaa kilichomfunga, naye akawa anapumua kwa kasi.

"Nyie ni akina nani? Mnataka nini?"

Khalid akauliza hivyo kwa sauti ya chini. Hakupata jibu lolote, lakini akasikia sauti za vitu kama cheche karibu yake.

"Hey! Nimewauliza nyie ni nani? Mnataka nini? Yule mwanamke mmemweka wapi?" Khalid akauliza tena.

"Tumemuua," Victor akajibu.

"Nini? We ni nani? Kwa nini mmemuua mwanamke asiye na hatia?"

Swali hilo la Khalid likamfanya Lakeisha acheke bila kutoa sauti huku akimwonyesha Lexi kwa ishara kwamba eti ameguswa sana.

"Alikuwa hana hatia? Au ndiyo ulikuwa unaenda kumfanya awe na hatia?" Victor akauliza.

"Nini? Wewe unataka nini? Niambie kama ni pesa nikupe," Khalid akasema.

"Sihitaji pesa. Ninachotaka ni kukuua wewe..."

"Nini?!" Khalid akauliza huku pumzi zake zikipanda.

"Nataka kuikatakata miguu yako kwanza, halafu mikono yako. Nikimaliza nakatakata milango yako yote ya fahamu, na nikisema yote namaanisha hadi ngozi naichuna, na hapo bado utakuwa haujafa. Nataka ufe huku unahisi kabisa kwamba unakufa," Victor akamalizia.

LaKeisha akawa anacheka huku ameziba mdomo.

"Wewe! Wewe ni nani? Mimi ni mwanajeshi, unajua utaumia sana ndugu yangu kwa huu upuuzi ni bora uniachie sasa hivi!" Khalid akatoa kitisho.

"Aaa... kwa hiyo unafikiri nakutania eeh?" Victor akauliza.

Kisha akamfanyia ishara Lakeisha, ambaye akasogea karibu na hapo huku akiwa ameshika kifaa kimoja cha kukatia chuma, kisha akakiwasha. Sauti ya jinsi kilivyozunguka kwa kasi ikamfanya Khalid ahofie sana. Akaanza kujivuta-vuta kwa woga.

"Wewe... nyie... subiri... mnataka kuniua kwa nini? Nimewafanya nini?" Khalid akauliza huku anababaika.

"Nataka uniambie ni kwa nini ulimuua Salim," Victor akasema.

"Nini? Salim gani?"

"Huyo huyo gani..."

"Mimi sijui unachokiongelea. Haloo... nakuombeni..."

LaKeisha akasogeza mashine hiyo karibu zaidi na sikio la Khalid ili kumtisha, naye Khalid akaogopa sana na kujaribu kufurukuta, lakini Victor akakishikilia kiti alichokalia kwa nguvu.

"Kwa nini ulimuua Salim?" Victor akauliza kwa ukali.

"Sijamuua!" Khalid akasema kwa hofu.

"Kata hilo sikio!" Victor akaongea.

"Subiri, subiri, subiri, subiri... sijamuua Salim mimi. Sikumuua mimi..."

"Alimuua nani?"

"Ni... ni Luteni...."

"Ongea!"

"Ni Luteni Jenerali Weisiko. Weisiko," akasema Khalid.

"Acha kumsingizia Weisiko. Ni wewe ndiyo uliyeenda na kumnyonga Salim. Sasa tutakuonyesha kifo kibaya zaidi ya hicho," Victor akaongea kwa kitisho.

"Hapana, hapana, ni Weisiko... siyo Weisiko yaani... ni Weisiko ndiyo alitutuma, lakini mimi sikumnyonga. Ni yule anayemwita silaha yake... huyo ndiyo alimnyonga..." Khalid akasema.

"Silaha yake? Nani, Black Widow?" Victor akauliza kama vile hajui.

"Sijui... si..si... sijamwona sura. Mimi nilimpitia tu na kumpeleka pale kama nilivyoambiwa, basi," Khalid akasema.

Victor akamtazama Lexi, naye Lexi akamwonyesha kwa ishara ya kidole kuwa aendelee.

"Kwa hiyo... mkajiunga ili kumuua boss wetu si ndiyo? Sasa tunaanza na wewe, halafu tunamfata na huyo mtu wako!" Victor akamwambia.

"Hapana sikia, mimi ninafuata maagizo tu ndugu yangu. Ninafuata amri, siyo kwamba ninapenda..."

"Siyo kwamba unapenda? Mmewaua watu nyie halafu mnawasingizia wengine mkafikiri hatutajua? Yaani leo tunaondoka na viungo vyako vyote vikiwa vimeachana..."

"Hapana msiniue! Tafadhali jamani, nina familia..."

"Sikuzote mkiwa kwenye matatizo ndiyo mnakumbuka familia nyau nyie!"

"Nawaombeni jamani! Nitafanya chochote kile lakini msiniue... tafadhali...." Khalid akaendelea kuomba.

"Sawa. Kama ni kweli haikuwa wewe uliyemuua, basi tuambie aliyemuua yuko wapi, labda ndiyo tutakuacha," Victor akamwambia.

Khalid akaanza kuwaelezea tu jinsi siku hiyo alivyopewa maelekezo ya kuipeleka helicopter mpaka juu ya nyumba fulani ya kifahari iliyokuwa imejitenga kwenye eneo fulani, na baada tu ya kutua, mtu huyo asiyefahamika aliingia kwa nyuma, kisha ndiyo akaipeleka helicopter kwenye jengo lile alikomuua Salim Khan. Akasema alipewa maelekezo ya kuwa makini sana na baada ya kumaliza jambo hilo aipeleke helicopter sehemu ya mbali ili iweze kuharibiwa huko. Alipoulizwa aliahidiwa kulipwa pesa kiasi gani, akasema tayari alikuwa ameshalipwa, kwa sababu alikuwa amefanya kazi nyingi haramu kwa ajili ya Weisiko kwa muda mrefu na hivyo aliwekwa kuwa kama mtu wa muhimu kwa ajili ya mishe za namna hiyo. Kwa hiyo wakati wowote ambao angehitajika basi angewajibika. Akawaambia ikiwa Weisiko angejua amemchongea namna hii, angeuawa.

Victor akamwambia tu ampe maelekezo ya ni wapi nyumba hiyo ilipokuwa kwa usahihi, naye akamwahidi wakishamkamata mtu yule aliyemuua Salim basi wasingemuua yeye, na hata Weisiko asingejua. Khalid akawapa maelekezo ya ni wapi nyumba hiyo ilipokuwa, na baada ya hapo Lexi akawapa ishara wenzake wamfunge Khalid kwa bomu dogo la bandia walilokuja nalo, halafu Victor akamdanganya Khalid kwamba endapo angejaribu kutoka kwenye kiti hicho, basi bomu lingelipuka, kwa hiyo alipaswa kukaa hapo hapo mpaka warudi kuja kumtolea. Khalid aliwaomba sana wasifanye hivyo, lakini hii ilikuwa ni njia ya Mess Makers kuhakikisha hawampotezi mwanaume huyo wakati ambao wangekwenda kumtafuta Azra.

Wakatoka hapo na kumwacha akiwa ameketi kwenye kiti usiku katikati ya msitu huo mdogo, nao wakawasiliana na Torres na kumpa taarifa mpya waliyopata, ambaye akaanza kuwaongoza vizuri kuelekea kule kwenye nyumba hiyo waliyotumaini kumkuta Azra.


★★★★


Siku hii haikuwa na mambo mengi sana upande wa Azra. Kutokea asubuhi, alikuwa ndani ya nyumba yake tu akifanya mambo ya hapa na pale yenye kuburudisha kiasi ili kupoteza muda. Alikuwa akihisi upweke wa hali ya juu, na hii hasa ilitokana na yeye kutokuwa na mtu wa kuzungumza naye kuhusu hisia zake.

Tokea alipofanikiwa kuwatoroka Mess Makers usiku wa jana, tena kwa msaada wa mmoja wao, alikuwa hajaondoka kwenye nyumba hiyo kabisa. Mara chache ambazo Weisiko alifika hapo ili kumpa ushirika wake hazikuondoa hisia nzito za majuto alizokuwa nazo moyoni, zilizomfanya ahisi ni kama amebeba mzigo mzito sana. Alijiona kuwa kama adui wa dunia yote iliyomzunguka, kwa kuwa alishinikizwa kufanya mambo mabaya yasiyokuwa na faida yoyote kwake, na hivyo kuhisi labda anastahili kuwa mwenyewe tu.

Kama ni jambo ambalo liliendelea kuzunguka akilini mwake, basi ni kitendo ambacho "mwanamke" aliyepambana naye usiku ule alifanya. Kutokea mara ya kwanza kabisa walipopigana, Azra alikuwa akijiuliza ni mafunzo ya aina gani ambayo mwanamke yule aliyapata mpaka kuzidi ya kwake yenye ubora zaidi, lakini sasa kilichosumbua akili yake kuhusu mwanamke huyo ilikuwa ni kwa nini aliokoa maisha yake baada ya kujaribu kuyaondoa mwanzoni. Kuna hisia fulani zilijijenga kwake, hisia ambazo zilikuwa ngeni kabisa kwake, lakini hakujiruhusu zimpoteze, kwa kuwa alifunzwa kutoruhusu jambo lolote limfanye kuwa dhaifu. Akajihakikishia kwamba endapo angekutana naye tena, basi asingesita kummaliza kabisa kwa sababu alikuwa ameanza kuwa tatizo kwake.

Wakati huu alikuwa amekaa tu kwenye chumba chenye TV kubwa sana, akitazama katuni ya Tom and Jerry, ambayo ilikusudiwa kufurahisha sana mtazamaji, lakini yeye hata kutabasamu hakutabasamu. Alikuwa tu anakula chips zilizokaushwa taratibu akiwa ameboeka sana, na baada ya kuangalia muda, akakuta ni saa 7 usiku tayari. Akaamua tu kuzima na kwenda kuutafuta usingizi kitandani.

Makao yake haya yalikuwa makubwa kweli, lakini ni yeye peke yake ndiye aliyekuwa ndani ya nyumba. Eneo la nje lililindwa na wanaume maalum wa jeshi waliowekwa na Weisiko, lakini hakuna hata mmoja kati yao aliyeruhusiwa kuingia kule ndani. Hivyo kumwona binti huyu ilikuwa ni mpaka wakati alioamua kutoka kwenda "misele" mara moja moja sana, lakini walinzi hao hawakuwahi hata kumsemesha "mtoto wa boss."

Baada ya Azra kupanda kitandani na kuanza kutafuta usingizi, haikumchukua dakika nyingi sana naye akawa ametambua kuwa kuna jambo halikuwa sawa. Ilikuwa ni kama machale yake tu ndiyo yalimwambia hivyo, kwa sababu kwa mtu wa kawaida asingefikiria kulikuwa na tatizo lolote hapo kutokana na utulivu wa hali ya juu uliokuwepo. Akajinyanyua na kuketi, akiwa amevalia tu T-shirt nyeusi na kikaptura chepesi kilichoishia mapajani, na udadisi wake ukamfanya anyanyuke na kuchungulia nje kutokea kwenye dirisha pana la chumba chake kilichokuwa kwenye ghorofa. Alitazama mazingira ya hapo nje, na kwa uhakika akawaona walinzi wakiwa wanazunguka kwa zamu kulinda eneo la nyumba.

Akaamua kurudi kitandani tena, lakini bado akawa haupati wepesi wa amani kwenye machale yake. Akajiuliza ni kwa nini, naye akatoka kitandani ili aelekee sehemu za chini ya ghorofa hilo kuangalia kama kuna jambo halikuwa sawa. Alishuka ngazi na kuzunguka huku na huku, kukiwa na giza lakini mambo mengi yakionekana vizuri kutokana na mwanga hafifu wa taa za nje, naye akakosa jambo lolote lenye kutia mashaka.

Akaamua kurudi juu tu ili alale, na ile alipofika usawa wa korido pana lililoelekea mpaka kwenye chumba chake, akahisi mtu akitokea upande huo wa ukuta na kutaka kumshambulia, na kwa kasi akajirusha sarakasi na kuangukia upande mwingine. Alipojinyanyua ili amwone adui, akahisi kitu fulani kikimchoma kwenye shingo yake kutokea kwa nyuma, na kwa kasi akageuka na kumtandika mtu aliyemchoma kwa mtindo wake wa kumaliza nguvu, kisha akajiviringisha upande mwingine na kuzikaribia ngazi. Akajaribu kunyanyuka lakini nguvu zikaanza kumwishia na kusababisha ashindwe kusimama vyema, naye akawaona watu wawili waliovaa nguo nyeusi wakiwa wamesimama mbele yake, huku mwingine akiwa amepiga goti chini pembeni.

Hao walikuwa ni Lexi, Lakeisha na Victor. Tayari walikuwa wamefika hapo na kufanikiwa kuingia kwenye nyumba bila kutambulika, na ni Victor ndiye aliyemchoma Azra kwa sindano yenye dawa ya kulewesha baada ya LaKeisha kumzubaisha Azra kwa kujaribu kumshambulia. Azra akadondoka chini akiwa amejishika shingo, na ilikuwa kidogo tu aanze kudondoka kuelekea chini ya zile ngazi, lakini akahisi mkono ukimshika na kumvuta ili kuzuia hilo. Akiwa anahisi kichwa chake ni kizito sana, akawa anaangalia juu na kumwona mtu aliyemshika mkono, naye akatambua ilikuwa ni yule mwanamke aliyepanga kummaliza endapo wangekutana tena, yaani Lexi. Giza zito likafunika macho yake, naye akapitiwa na usingizi bila kupenda.

Lexi alikuwa ameshaitoa 'mask' yake wakati alipomfata Azra kuzuia asianguke kwenye ngazi, naye akamshika usoni huku akimwangalia kwa huruma.

"Damn! How does she do this? (hivi huwa anafanyaje hivi?)"

Victor akaongea hivyo akiwa amekaa chini sasa. Alikuwa analalamika kwa sababu mkono wake ulikuwa umekufa ganzi kabisa baada ya Azra kumpiga muda mfupi nyuma, naye akawa anashindwa kuunyanyua mpaka kutumia mwingine.

"Shh! Punguza sauti, walinzi nje," LaKeisha akanong'oneza kwa tahadhari.

"We gotta go (tunahitaji kwenda)," Lexi akasema.

"Tunamtoaje sasa huyo akiwa amelala, unajua jinsi ilivyokuwa ngumu kuingia hapa," Victor akasema.

"Tunatoka kama tulivyoingia," akasema LaKeisha.

"Nimevunjika mkono, sitaweza kuning'inia," Victor akasema.

"Basi utabaki," LaKeisha akamwambia huku akienda kumsaidia Lexi kumnyanyua Azra.

"Victor get yourself together, we don't have much time (Victor, jisawazishe vizuri, hatuna muda mwingi)," Lexi akamwambia.

Victor akasimama na kuanza kuwaongoza wengine kuelekea juu kabisa ya ghorofa hilo, Lexi na Lakeisha wakiwa wamembeba Azra. Walikuwa wametumia nyaya nene za nguzo kuingia hapo, ambazo zilipita karibu kabisa na jengo hilo. Wakati walipokuja, walitumia mahesabu kwa umakini sana kujua muda uliofaa kupita juu ya nyaya hizo, yaani nyakati ambazo walinzi wangefanya mizunguko na kuipa mgongo sehemu hiyo, ndiyo wao wangepita. Lakini wakati huu walikuwa na mtu aliyepoteza fahamu, hivyo ingekuwa ngumu sana kumtoa hapo kwa njia waliyotumia kuingia. Kwa sababu walinzi wale walikuwa na silaha nzito, kutafuta njia chini kusingekuwa na faida, hivyo njia ingepaswa kuwa hiyo hiyo. Kwa hiyo baada ya kuwa wameongea na Torres, akawaelekeza cha kufanya, ingawa hakuwa na uhakika kwa asilimia zote kama wangefanikiwa.

Mpango ukawa kwamba, wawili wangepaswa kutoka hapo kama walivyoingia, lakini mmoja wao azikate nyaya zile na kuzifunga kwenye mwili wake pamoja na Azra, halafu waitumie kama kamba ya bembea kujitupia upande wa pili wa kuta za nyumba hiyo, ambako wenzao tayari wangekuwa wameshasogeza gari ili wakitua tu wawaingize na kuondoka upesi. Lilionekana kuwa moja kati ya njia ngumu sana ambazo wangetakiwa kuchukua, lakini Lexi akakubaliana nalo na kusema yeye ndiyo angejifunga pamoja na Azra, hivyo Victor na Lakeisha ndiyo watangulie.

LaKeisha pamoja na Victor waliliona kuwa wazo baya sana, kwa sababu kwa kukata nyaya huenda wangesababisha shoti ambayo ingewaua wawili hao wakijifunga kwa huo waya. Torres akasema wangepaswa kuifunga sehemu hiyo kwa nguo nyingi kabla ya kuizungushia kwenye miili yao, na walipaswa kuwa makini sana. Akawapa matumaini kuwa kwa kukata nyaya huenda hata umeme ungekata, hivyo ingepunguza nafasi ya walinzi kuwaona wakitumia nyaya kama bembea. Lexi akawaambia wenzake kuwa yote yangepaswa kufanywa kwa umakini, lakini matokeo wangepaswa kuyaacha mikononi mwa Mweza yote, kwa sababu asingeondoka hiyo sehemu bila Azra.

Kwa kuwa muda ulizidi kuyoyoma, LaKeisha akaharakisha kurudi ndani ya nyumba hiyo na kufata mashuka manne marefu kabisa, kisha akapanda tena mpaka kule juu. Bado alikuwa na kile kifaa chake cha kukata chuma, hivyo akampatia Lexi na kumsihi sana awe mwangalifu. Mkono wa Victor ulikuwa umeanza kurudisha nguvu, na baada ya kuona upande huo ukiwa umepitwa na mlinzi tayari kule chini, akarukia nyaya hizo na kuanza kuelekea upande wa nguzo, kwa njia ya kuning'inia na kuibana miguu yake kwa pamoja. Lexi na Lakeisha wakamwangalia mpaka alipofanikiwa kuifikia nguzo upande wa pili wa kuta zilizozunguka nyumba hiyo, naye akashuka huko chini bila kutambulika. Upesi akawahisha kwenda walipoliacha gari lao na kuingia kumsubiri LaKeisha.

Lexi na Lakeisha walibaki kule juu na kusubiri walinzi wamalize zamu ya pili ya kuzungukia upande huo, na baada ya kuondoka, LaKeisha akafuata kuzirukia nyaya na kuanza kuielekea nguzo mpaka na yeye alipofanikiwa kufika upande wa pili. Haingekuwa rahisi kuwaona kwa sababu palikuwa parefu na nguo zao nyeusi zilifanya wafichwe vyema kwa giza la huko juu, lakini kimbembe kingekuja kwa Lexi. Angehitaji kumbeba Azra, kujifunga kwa nyaya za umeme zilizokuwa hatari sana, na kubembea naye mpaka nje ya kuta za nyumba hiyo kama Tarzan.

Ingehitaji umakini wa hali ya juu kwa sababu kama angekosea mahesabu basi angeangukia ndani ya kuta hizo na siyo kule nje. LaKeisha akiwa ameshafika kwenye gari pamoja na Victor, akamjulisha Lexi, naye Lexi akasema akiwaambia tu waanze kulisogeza gari upesi mpaka upande ambao alitazamia kuangukia, basi wafanye hivyo haraka. Uwezekano wa kuonwa ulikuwa mkubwa sana, hivyo wangetakiwa tu kudondoka, kunyanyuka, na kuondoka.

Baada ya kujiweka sawa, Lexi akazirukia nyaya hizo akiwa ameshayafunga-funga mashuka yale kwa pamoja, naye akaanza kuyafungia karibu na sehemu aliyokusudia kuzikata. Wenzake walikuwa wametulia tu wakisikilizia mambo kama vile waliona kilichokuwa kinaendelea, na kiukweli ilikuwa ngumu sana kwa Lexi kufanya hivyo. Kwa kukadiria muda ambao walinzi wangepita upande huo, akajiachia kutoka huko juu na kuangukia ghorofani tena ili kujificha kwanza, na baada ya mlinzi kupita, akapanda tena na kukiwasha kifaa kile cha kukata chuma. Kilitoa sauti kali kiasi, hivyo akapitisha tu mkono wake haraka na kujiachia huku akiwa ameshikilia sehemu ya shuka iliyofungwa hapo kama kamba, na kuangukia ghorofani tena.

Hii ilifanya nyaya zikatike, naye akiwa bado amelishika shuka akawa anaona cheche zikipiga kutoka kwenye waya uliodondokea karibu na alipoangukia. Kwa haraka alijua walinzi wangekuwa wamesikia na hata kuanza kuja juu kuangalia nini kilikuwa kimetokea, hivyo akanyanyuka ili aanze jitihada za kuifungia miili yake na Azra kwa nyaya hizo na hatimaye wabembee mpaka nje. Lakini baada ya kunyanyuka, akatambua kwamba umeme haukukatika kwenye nyumba hiyo baada ya yeye kuzikata hizo nyaya, na alipochungulia kule chini, akaona walinzi wakiendelea na biashara zao tu, kuonyesha hata hawakusikia kilichotokea.

Sauti za shoti zilizotoka kwenye nyaya hizo zilizibwa na fundo la shuka lililokuwa limezungushiwa kwa ukaribu, hivyo Lexi akaona azidishe fundo hilo hapo ili zisisikike hata zaidi. Ilimshangaza kiasi kwamba umeme haukukatika, lakini labda hiyo ilimaanisha umeme wa nyumba hii haukuhusiana na nyaya hizo, au kulikuwa na jenereta la dharura endapo umeme ukikata linawaka moja kwa moja. Kwa vyovyote vile hii ilikuwa na faida kwake, kwa sababu angekuwa na muda wa kutosha kumweka Azra mwilini mwake vyema ili hatimaye waondoke.

Kutokea kule nje, LaKeisha na Victor waliona nyaya hizo zikilegea kule juu, nao wakawa wanamuuliza Lexi kama kila kitu kilikuwa sawa. Akawajibu mambo yalikuwa safi, hivyo akiwaambia tu "now" waanze kuendesha. Lexi alikuwa anahangaika kuhakikisha sehemu ya nyaya iliyokatika haingewagusa moja kwa moja kwa kuyarundika mashuka hapo. Sasa akaona kwamba ingekuwa ngumu kuubananiza mwili wake na wa Azra kisha aifunge kwa pamoja, kwa hiyo ili kuokoa muda akaamua kwamba angemweka mgongoni.

Kila kitu alichowaza alijua kingekuwa na hatari fulani, lakini akaazimia kufanya yote awezayo kutoka sehemu hiyo na mdogo wake. Akaziunganisha vizuri nyaya hizo, kisha akamnyanyua Azra na kumweka mgongoni, naye akatumia sehemu ya shuka kumfunga kiunoni kwake na kuikaza mikono ya Azra shingoni kwake kwa mkono mmoja, halafu akaishikilia nyanya hiyo kwa mkono mwingine na kusimama, naye akasema kwa sauti ya chini, "Now!"

Papo hapo akashika nyaya hizo kwa mikono yote na kujirusha kwa nguvu sana. Nyaya ikaanza kuwapeleka kuelekea chini kwa kasi sana, na walipoukaribia ukuta, miili yao haikuwa juu vya kutosha kuweza kuuvuka, hivyo wakaishia kujigonga karibu kabisa na mwisho wa kuta hizo!

Mlinzi mmoja aliona jambo hilo, na kutokea alipokuwa akawapa tahadhari wengine kwamba kuna jambo lilikuwa linatokea upande wa Lexi, nao wakaanza kukimbilia huko. Lexi alikuwa amejitahidi kuendelea kuzishika nyaya hizo, huku akihisi kabisa jinsi Azra alivyoanza kuteleza kutoka mgongoni kwake, lakini akajivuta kwa nguvu kuelekea juu na kufanikiwa kuishika chuma iliyochongoka juu ya kuta hizo. Kulikuwa na seng'eng'e zilizozungushiwa pia kwa juu, hivyo kwa kiasi fulani zikawa zinachoma vidole vyake vilivyokuwa ndani ya 'gloves' ngumu.

Ukuta huo ulikuwa mrefu sana, na baada ya walinzi kufika usawa huo, wakamwamuru aliyembeba Azra ajisalimishe la sivyo wangempiga kwa risasi. Lexi hakutaka kukata tamaa. Kutokea juu hapo aliweza kusikia sauti ya gari kwa kule nje, naye akatambua ilikuwa ni Victor na Lakeisha, hivyo akaongeza bidii ya kujivuta na kufanikiwa kupigisha goti lake juu ya kuta hizo. Mlinzi mmoja kati ya sita waliokuwa hapo alimlenga Lexi kwa umakini sana na bunduki yake ili amfyatue yeye na siyo Azra, huku walinzi wawili wakikimbia kuelekea geti ili wafike kwa nje. Mlinzi huyo akafyatua risasi iliyofanikiwa kumpiga Lexi sehemu ya juu ya mbavu yake, lakini haikuweza kumdhuru kutokana na nguo yake kuzuia risasi hiyo ingawa ilikuwa na nguvu kali sana. Msukumo wa risasi hiyo nzito ukasababisha Lexi asukumwe kwa nguvu sana na hivyo yeye pamoja na Azra wakaangukia upande wa pili wa kuta hizo, yaani kwa kule nje!

Ilikuwa ni shukrani kwa Mungu tu kwa sababu tayari Victor na Lakeisha walikuwa wamesimama sehemu waliyoangukia kwa huko nje, na hivyo Victor akajiweka vizuri na kufanikiwa kumdaka Azra, nao wakadondokea pembeni bila ya Azra kuumia vibaya sana, ingawa alikuwa na mikwaruzo kwenye miguu kutokana na seng'eng'e zile za juu kumkwarua. LaKeisha hakuwa na uwezo wa kumdaka Lexi vizuri, lakini kwa ujasiri alijiweka sehemu ambayo Lexi angeangukia na hivyo akamdondokea na wote kuanguka kwa pamoja. LaKeisha aliumia kiasi kwenye mkono wake, naye Lexi alihisi maumivu kichwani na msuguo mkubwa kwenye nyonga, lakini wote wakajitahidi kunyanyuka na kuambiana walikuwa sawa.

Lexi akaonya kwamba walinzi wale walikuwa wanakuja, hivyo upesi wakamwingiza Azra kwenye gari, naye Victor akawaondoa hapo haraka isivyo kawaida. Aliendesha kwa kasi sana na kufanikiwa kufika mbali bila kuwaona walinzi wale wakija, na baada ya kufika sehemu walikoacha gari lingine, wakalifata na kuliacha hili walilotumia, kisha Victor akafanya kama kulilipua kwa kupiga risasi sehemu ya tenki la mafuta kwa bastola yake ndogo.

Wakawa wamefanikiwa kuondoka na Azra, ambaye bado alikuwa mbali kiusingizi. LaKeisha akamuuliza Lexi ikiwa aliumia sehemu yoyote kwa sababu walisikia mlio wa risasi kule ndani, naye akasema hakuumia. Victor akaweka wazi kwamba mchezo waliokuwa wametoka kufanya ulikuwa hatari sana, hivyo walistahili mambo mazuri kutoka kwa mdogo wake Lexi na siyo wamfikishe huko halafu awazingue. Torres kupitia kifaa cha mawasiliano, akawapongeza sana kwa kazi nzuri na kusema angemjulisha "boss" wao kuhusu mafanikio waliyopata.

Lexi alikuwa amekaa siti ya nyuma ya gari hilo, huku Azra akiwa amelaza kichwa kwenye mapaja yake, naye akatabasamu kwa hisia huku akipitisha kiganja chake kwenye nywele laini za mdogo wake. Hatimaye akawa pamoja na mdogo wake tena.



★★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★★

WhatsApp +255 787 604 893
 
Mkuu Elton Tonny shukrani sana kwa simulizi tamu ambayo ukiisoma unajenga na picha as if unaangalia movie. Tuongezee episodes hata mbili Basi mkuu
 
IMG_9645.jpg
 
FOR YOU

Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Uhalifu, Mauaji, Visasi, Vita, Mambo yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA THELATHINI NA TANO

★★★★★★★★★★★★★★★★★★


Alfajiri na mapema tu, tayari Luteni Jenerali Weisiko alikuwa amefika kwenye nyumba ya "binti yake" baada ya kupewa taarifa kwamba alikuwa ametekwa. Alifika akiwa na hasira kali siyo mchezo, akiwa pamoja na walinzi wake maalum, na walinzi wale wa nyumba ya Azra walikuwa wamepigishwa magoti ndani ya geti la nyumba hiyo kama vile wanafunzi waliochelewa kuhesabu namba shuleni. Weisiko alitaka kujua ilikuwa vipi "mtoto wake" akatekwa wakati walinzi hao walikuwepo muda wote, nao wakamweleza kwamba waliomchukua walitumia nyaya za umeme kuingia na kutoka, na kwamba walikaribia kuwakamata lakini wakawaponyoka kimuujiza.

Weisiko hakuwa aina ya mtu aliyeamini miujiza, ila kama ni muujiza aliotaka utokee ilikuwa ni "Mary" wake kurudi hapo haraka iwezekanavyo. Akawauliza watu hao walitoroka vipi eneo hilo, nao walinzi wakamwambia walitumia gari ambalo baada ya kulifuatilia walikuta limelipuka, bila kuwa na miili yoyote ndani. Weisiko alichanganyikiwa sana. Silaha yake muhimu zaidi ilikuwa imeibiwa, lakini kilichomfanya ahuzunike hata zaidi ilikuwa ni ile hisia kama vile amempoteza mtoto wake kwa mara nyingine tena. Akawauliza walinzi hao ikiwa wangeweza kuwatambua watu waliomteka binti yake, lakini wakakanusha.

Kwa jazba kali sana, akachukua bastola kutoka kwa mmoja wa walinzi wake yeye na kuanza kuvifyatua vichwa vyote vya walinzi wale sita kwa risasi! Wote wakaanguka chini wakiwa wamepoteza maisha yao, naye Weisiko akaendelea kuimiminia miili yao risasi huku akipiga makelele kwa hasira mpaka bastola ikawa tupu. Akawaambia walinzi wake washughulikie miili hiyo, kisha yeye akaenda pembeni na kumpigia simu Jenerali Jacob. Akamweleza yaliyokuwa yametokea, naye Jacob akakasirika sana.

Moja kwa moja wote wakawa wamefikia mkataa kwamba ni Mess Makers ndiyo waliomteka "Mary," kama jinsi walivyomwita Azra. Jenerali Jacob akamwambia Weisiko wangepaswa kufanya juu chini kufahamu ni jinsi gani Mess Makers walijua mahali ambapo "Mary" angekuwepo, na labda kwa njia hiyo wangeweza kuwapata pia. Weisiko alihofia sana kwamba huenda watu hao wangemdhuru "binti yake," kwa hiyo akaapa kuwapata wote mapema na kuwaua, kwa sababu kumgusa Azra ilikuwa ni kama wamemgusa yeye moja kwa moja.

Lakini hakujua kwamba kama tu ilivyokuwa ngumu kwa serikali yote ya nchi kuwapata wahuni wale, ingekuwa tata hata zaidi kwake. Akaondoka tu kwenye nyumba hiyo akiwa na hasira kali huku akiwaza afanye nini ili kumpata "Mary" wake.


★★★★


Mess Makers wakawa wamemfikisha Azra kule "chini" kwenye nyumba yao ya maficho kwenye mida ya asubuhi, wakipokelewa vyema na Torres. Mpaka wakati wanafika Azra hakuwa amerejesha fahamu bado, na wakati huu mikono yake ilikuwa imefungwa pamoja na miguu kama tahadhari tu.

Walimwingiza kwenye chumba fulani kidogo kilichokuwa kimejengewa kule kule chini ya handaki lile pana, ambacho kilikuwa ni aina ya chumba chenye kusaidia kupasha miili joto kwa muda mfupi (steam room, siyo sauna). Kutokana na jinsi mwili wa Azra ulivyoshikwa na baridi baada ya safari ndefu ya usiku kutoka kule kwenye nyumba yake, lilikuwa wazo la Torres kumweka ndani hapo ili mwili wake upate joto la taratibu kadiri ambavyo fahamu zake zingekuwa zinarejea.

Kevin kama kawaida yake bado alikuwa akisema kwa msimamo wake kwamba wazo la kumpeleka mwanamke huyo hapo akiwa hai halikuwa zuri, na badala yake walitakiwa kumpa kifo tu kama vile alivyomfanyia Oscar. Mwanaume huyu alikuwa ameshaanza kumkera sana Lexi, lakini Lexi alikuwa imara vya kutosha kumpuuzia tu kwa sababu aliielekeza zaidi akili yake kwa mdogo wake.

Victor akaondoka pamoja na Kevin ili kuziondoa kero za jamaa hapo, na wengine wakamkalisha Azra vizuri tu kwenye kiti na kumfungulia kamba baada ya Lexi kusema wafanye hivyo. LaKeisha akasema angekwenda kujimwagia baada ya usiku wenye kuchosha, akimwomba Torres waondoke pamoja kwenda kujisafisha pamoja kwa kuwa Azra hangechukua dakika nyingi kuamka, ili pia kumwacha Lexi na mdogo wake peke yao. Wakamsihi Lexi awe mwangalifu naye, kisha wakaondoka sehemu hiyo.

Lexi alikuwa anamwangalia Azra sana huku anatafakari mambo mengi, na baada ya sekunde kadhaa kupita, yeye pia akavuta kiti kidogo na kuketi. Akaendelea kumwangalia mpaka alipoanza kugeuza shingo yake taratibu, lakini ghafla akashtuka na kudondokea chini, akijaribu kujiweka katika hali ya kujihami. Lexi akasimama na kuanza kumwambia asiogope kwa sababu alikuwa sehemu salama, lakini Azra akachukua kile kiti na kujaribu kumponda nacho, naye Lexi akakikwepa.

"Calm down! Listen to me! I'm not gonna hurt you. I'm not (Tuliza hisia! Nisikilize. Sitakuumiza. Sitakuumiza)," Lexi akasema kwa kumtuliza.

Azra akawa anarudi nyuma nyuma huku anapumua kwa nguvu, na akiwa anamwangalia Lexi kwa hasira.

"I'm sorry. I'm sorry I attacked you. But it was the only way to bring you with me (samahani... samahani kwa kukushambulia.. lakini ndiyo ilikuwa njia pekee ya kukuleta pamoja nami)," Lexi akamwambia.

Azra akawa anamtazama tu kama hamwelewi.

"Look... I know this is all messed up... and a lot is going on even I don't understand, but one thing I know for sure... is that you're my sister. I know you probably don't know me... but I know you. I do. Let's just... I just want us to talk. Please (ona... najua mambo yote haya ni mvurugo.. na mengi yanaendelea hata mimi mwenyewe sielewi, lakini kitu nachojua kwa uhakika ni kwamba wewe ni dada yangu. Najua labda hunifahamu.. lakini mimi nakujua. Nakujua. Tu.. nataka tu tuzungumze.. tafadhali)," Lexi akamwomba.

"Who the hell are you? (Wewe ni nani?)" Azra akauliza.

Hapo ndiyo alikuwa amemwongelesha Lexi kwa mara ya kwanza, na Lexi kuisikia sauti yake kulifanya afarijike sana moyoni. Bado ilikuwa jinsi ile ile alivyoikumbuka kabisa.

"My name is Lexi. Well... its my new name. You used to know me as... Sandra (naitwa Lexi.. ni jina langu jipya.. wewe ulikuwa ukinijua kama Sandra)," Lexi akamwambia.

Aliona ampe utambulisho wa yeye kuwa Sandra kwa sababu suala la kubadilishana mwili na pacha wake lingemchanganya kwa wakati huu.

"I'm your sister (mimi ni dada yako)," Lexi akamwambia.

"I don't have a sister (sina dada)," Azra akamwambia kwa mkazo.

"Azra... we're siblings. We're... from the same womb. I don't know what happened to you, but everything I'm telling you is the truth. Azra our parents we're killed right in front of us.... our parents died that night... that horrifying night of our entire lives... that changed everything about who we've become now. It was never supposed to be like this.... (Azra sisi ni ndugu. Tumetoka tumbo moja. Sijui ni nini kilikupata lakini kila kitu nachokwambia ni kweli. Azra wazazi wetu waliuliwa mbele ya macho yetu.. usiku ule walikufa.. usiku ule wenye kuogopesha sana katika maisha yetu uliobadilisha kila jambo kuhusu watu ambao tumekuwa sasa.. Haikupaswa kamwe kuwa namna hii)" Lexi akawa anazungumza kwa hisia.

"What the hell are you talking about? (Unaongelea nini?)" Azra akauliza.

"I need you... to look deep down in you even if you don't remember... I know your heart knows its the truth. What those people did to you... might have erased all of your memories about our family. Azra... I am your family. I mean come on, we even look alike, don't you see? We share the same blood (Nakuhitaji ujichunguze ndani yako kabisa.. hata kama haukumbuki.. ninajua moyo wako unajua nayokwambia ni kweli. Mambo ambayo watu hao wamekufanyia huenda ndiyo yamesababisha upoteze kumbukumbu kuhusu familia yetu. Hebu tazama, yaani mimi na wewe tunafanana kabisa, au huoni? Sisi ni wa damu moja..)," Lexi akasema.

Alikuwa akiongea hivyo huku akipiga hatua chache kumfata Azra.

"Stay back! (Tulia huko huko!)" Azra akamwonya.

"Azra..."

"I'm not! Don't call me that! (Mimi siyo! Usiniite hivyo!)" Azra akamwambia kiukali.

"Its your name! You're my sister, you're Azra (ndiyo jina lako.. we ni dada yangu, we ni Azra)," Lexi akasisitiza.

"No, no, I'm not. Whoever you are, or whatever game you think you're playing with me its not gonna work. I will kill you, do you understand me? (Hapana, hapana, mimi siyo. Sijali wewe ni nani au ni mchezo gani unafikiri unanichezea, lakini hautafanikiwa. Nitakuua, unanielewa?" Azra akaonya.

"Really? You'd kill me? (kweli? utaniua?)" Lexi akauliza.

"Without a blink (bila kukonyeza)," Azra akajibu.

"Then why didn't you? (mbona haukufanya hivyo basi?)" Lexi akauliza.

Azra akabaki kimya.

"The other night when I found out it was you... you had a knife on my neck.... why didn't you do it? (Usiku ule nilipojua ni wewe.. uliweka kisu kwenye shingo yangu.. kwa nini haukufanya hivyo?)" Lexi akauliza.

"Ahah... you really just love acting don't you? (unapenda sana kuigiza, siyo?)" Azra akauliza.

"Azra, I'm your sister. If I wanted to harm you, I would have. My only goal coming after you was to avenge my friend's death, but when I found out it was you.... I thought you were dead. I thought all of you were. Everything is a shock to me the same as it may apply to you, but I'm telling you the truth. You gotta believe me. Azra... (Azra mimi ni dada yako. Kama ningekuwa nataka kukudhuru ningekuwa nimefanya hivyo. Lengo langu kukufata mwanzoni lilikuwa ni kulipiza kisasi kwa kifo cha rafiki yangu lakini nilipojua ni wewe... nilidhani ulikuwa umekufa. Nilidhani nyote mlikuwa mmekufa. Kila jambo limenipa mshtuko kama jinsi inavyoweza kuwa kwako pia.. lakini nayokwambia ni kweli. Unapaswa kuniamini. Azra...)" Lexi akaishia tu hivyo.

Machozi yalikuwa yamejaa kwenye macho yake kwa sababu ya hisia nyingi sana za huzuni. Azra alikuwa anamwangalia kwa kutomwamini bado, na jambo moja lililokuwa akilini mwake ilikuwa ni kutoroka sehemu hiyo waliyokuwepo haraka iwezekanavyo.

"Azra look... I can show you some of the things that... may help you see that what I'm saying is true... if you'll let me (Azra ona.. ninaweza kukuonyesha baadhi ya mambo ambayo yanaweza kukusaidia uone kwamba nayosema ni kweli.. ikiwa utaniruhusu)," Lexi akamwambia.

"Like... what? (kama nini?)" Azra akauliza.

"I'll ask my friend to... get some old photos of us. You used to love to take many photos of us and post them on Facebook back then... (nitamwomba rafiki yangu atafute baadhi ya picha zetu za zamani. Ulikuwa ukipenda sana kuchukua picha zetu nyingi na kuzirusha Facebook kipindi hicho..)" Lexi akasema.

"I don't know what you're saying (sijui unachokionhelea)," Azra akamwambia.

"Its true. I can prove it to you (ni kweli.. ninaweza kukuthibitishia)," Lexi akamhakikishia.

"And then what? I become... Azra... your beloved sister? Everything'll just change... your gang'll just forget I killed one of you? That I'll switch sides, join you, and live happily ever after? (Halafu baada ya hapo? ndiyo nitakuwa.. Azra.. mdogo wako kipenzi? Kila kitu kitabadilika tu.. genge lako litasahau kwamba niliua mmoja wenu? Halafu nitakuja upande wenu, tuishi maisha ya raha mustarehe milele?)" Azra akauliza.

Lexi akabaki kumtazama kwa hisia.

"Ahah... there's no such thing as that. What you're saying, even if it was true, won't change anything. I'm not your sister. I'm not... Azra. I don't want you to prove anything to me. What we've become now has to stay as it is... enemies. You and I, we're enemies. That's the only relationship we got (hakuna kitu kama hicho. Unachokisema hata kama kingekuwa ni kweli, hakitabadili lolote. Mimi siyo dada yako. Mimi siyo Azra. Sitaki uthibitishe lolote kwangu. Tulicho kwa sasa kitapaswa kubaki hivyo hivyo.. maadui. Wewe na mimi ni maadui)," Azra akamwambia.

Lexi akadondosha chozi la huzuni. Azra akakunja ngumi na kujiweka katika hali ya pambano.

"I'm getting out of here. Alive or dead (ninatoka hapa.. nikiwa mzima au nikiwa nimekufa)," Azra akamwambia.

Lexi akainamisha uso wake chini kwa huzuni. Alitambua kiukweli huyu aliyekuwa mbele yake hakuwa na chembe yoyote ya hisia kumwelekea. Jinsi watu wabaya walivyokuwa wamembadili mdogo wake ilimuumiza sana, na ijapokuwa ilivunja moyo, Lexi hangekata tamaa. Kwa sababu ni Azra pekee kati ya watu wote wa familia yake ndiyo alikuwa amebaki, naye hangekuwa radhi kumpoteza kwa mara nyingine tena. Azra alikuwa amejiweka tayari kuanzisha mapigano na Lexi ili atoroke hapo, lakini Lexi akawa amesimama tu huku anamwangalia kwa hisia.

Ile tu Azra alipotaka kumfata, kengele ndogo ya chumba hiki ikaanza kutoa sauti, na kwa haraka Lexi akatambua kwamba hiyo ilikuwa ni wonyesho kwamba mlango wa chumba ulitaka kufunga. Yaani kutokea alipokuwa amesimama, mlango wa humo haukufungwa, na hiyo ilikuwa ni kwa sababu hakukuwa na mtu mwingine kwa nje. Ikiwa ungejifunga wakiwa ndani bado, basi wangechemshwa wazima wazima kwa kuwa hawangeweza kuufungua wakiwa kwa ndani.

Sehemu ya kibonyezeo cha kuufunga na kuufungua kilikuwa kwa nje, kwa hiyo Lexi akatoka kwa kasi sana kuwahi kabla haujajifunga. Ulikuwa wa chuma na ulifunga kama milango ya lifti ifanyavyo lakini kwa upande mmoja, naye akawahi ulipokuwa karibu kabisa kujifunga na kuuingiza mwili wake katikati, akikanyaga kwa mguu sehemu iliyobaki ili kuacha nafasi kidogo. Hii ilimuumiza sana, lakini akajikaza na kujikakamaza kutokana na msukumo wa mlango.

"Azra... get out!" Lexi akasema huku amekaza meno.

Azra alitenda upesi na kukimbia mpaka hapo, kisha kwa wepesi wake akajitelezesha chini ya uwazi mdogo aliouacha Lexi na kutokea upande wa nje wa chumba hicho. Akanyanyuka na kumwangalia Lexi, ambaye alihitaji msaada wa kuvutwa kwa nguvu, lakini Azra akamsogelea na kumsukumia ndani!

Mlango ukajifunga, Lexi akiwa ameangukia ndani kule, naye Azra alipoangalia kifaa kile kinachoonyesha kiasi cha joto, akaona kiko mwisho kabisa. Akashindwa kuelewa iliwezekanaje mtambo huo kujiweka namna hiyo wenyewe tu, lakini akaamua kuacha hivyo hivyo ili mwanamke aliye ndani aive vizuri. Alimwona Lexi kupitia kioo kidogo sana cha mlango huo akisimama na kumtazama tu kwa hisia, naye Azra akampuuzia na kuanza kuondoka hapo kwa uangalifu. Hangeweza kutambua kwa urahisi mwanzoni kwamba alikuwa chini ya ardhi, kwa sababu palikuwa na mwonekano kama wa nyumba ya kawaida, lakini kadiri alivyosonga akatambua alikuwa chini ya ardhi. Akaziona sehemu za ngazi kuelekea juu, naye akazipanda ili aondoke upesi.

Lexi alihisi kuchanganyikiwa. Alihofia mengi sana kuhusu Azra, lakini pia hali yake ndani hapo. Joto lilizidi kuwa kali na kama angeendelea kukaa humo kwa dakika zaidi ya 15 basi angekufa kwa kukauka. Hakuwa na kifaa cha mawasiliano hapo, na hata kama angepiga kelele wenzake wasingesikia, na alijua wasingekuja huku chini kwa sababu ya yeye kuhitaji muda wa kibinafsi na mdogo wake ambao sasa ulikuwa umevurugika. Ambacho kingekuwa msaada ni ikiwa Azra angefika huko juu na kukutana na mmoja wao, ambaye labda ndiyo angekuja kumsaidia, ila tena na hapo akawa anahofu sana kwa sababu huenda Azra angewaumiza wenzake vibaya mno. Ikaonekana kama ni muujiza tu ndiyo ungepaswa kutokea la sivyo hakuna jambo lolote ambalo lingekwenda vizuri.

Torres ndiyo alikuwa ametoka tu kuoga na kumwacha LaKeisha bafuni kwa sababu walikuwa wanaoga pamoja, na sasa akiwa kwenye sehemu ya chumba chake anajipangusa maji kutoka kwenye nywele zake, akaona jambo fulani lililomshtua sana. Kutokea aliposimama kulikuwa na dirisha pana la milango ya vioo, na kwa hapo aliweza kuona jambo hilo ambalo alijua halingekuwa zuri hata kidogo ikiwa lingefika ndani.

"Holy shit!"

Torres akatamka maneno hayo na kwa kasi akatoka kwenye chumba hicho akiwa ndani ya taulo tu. Alikimbilia upande ule wa kule chini ili kwenda kumwambia Lexi alichoona, lakini njia aliyotumia kufika huko ilikuwa tofauti na ile ambayo Azra aliitumia baada ya kufanikiwa kutoka kule chini. Kwa hiyo wakapishana kidogo tu, naye Azra alimwona Torres, hivyo akajibanza na kumwacha apitilize kwenda huko. Kwa kuwa alitambua angekwenda kwa Lexi, akaona awahi kutafuta njia ya kutokea nje, naye akatoka haraka na kuanza kuelekea sehemu za mbele ya nyumba hii.

Torres alifika kule chini upesi na kukuta taa nyekundu ya chumba kile cha joto ikiwaka. Akashangaa kidogo, naye akasogea karibu zaidi na kumwona Lexi akiwa kwa ndani huku ameinama, akionekana kukosa hewa. Upesi Torres akaizima na kuufungua mlango, kisha akaingia ndani hapo na kumshika Lexi.

"Lexi..." Torres akaita.

"Torres... Azra... she's gone... (Azra amekimbia)" Lexi akasema kivivu.

"Lexi... Zelda's out! (Lexi.. Zelda ametoka nje!)" Torres akasema.

Lexi akamwangalia kwa mshangao, kisha akajitoa mikononi mwake na kuanza kukimbilia nje. Alijitahidi kuwahi kwa kuwa alijua ikiwa angechelewa, basi shida ambayo ingetokea asingeweza kuirekebisha.

Azra ndiyo alikuwa amefika tu usawa wa sehemu yenye eneo pana kidogo lililoelekea mpaka kwenye milango ya kuingilia kwenye nyumba hii, pale aliposimama na kutoa macho kwa mshangao baada ya kushtushwa na kile alichokiona. Milango ilikuwa wazi, na kwenye mwingilio wa hapo alisimama mnyama mwenye kufanana na simbamarara (tiger), lakini ngozi yake ilikuwa nyeupe kiasi yenye madoa meusi yaliyoonekana kwa mbali kutokea mgongoni mpaka miguuni. Mwili wa mnyama huyu haukuwa mnene wala mwembamba sana, akionekana kama duma mweupe. Huyo ndiyo alikuwa Zelda!

Azra alikuwa amesimama, akimwangalia kwa hofu iliyokuwa imeanza kumpanda, naye Zelda akawa anamtazama kwa macho makali. Umbali mfupi ambao Azra alisimama kutoka kwa mnyama huyu ulimwambia kwamba hata akijaribu kufanya nini, asingeweza kushindana na kasi ya mnyama huyo, hivyo ilikuwa ni kifo tu. Ni kama Zelda alikuwa anasubiri mtu huyu mbele yake afanye jambo fulani, lakini Azra akajitahidi kutulia tu kwanza kwa sababu alijua hata akitenda chochote haingekuwa na faida kwake. Woga ule wa msichana wa kawaida ulikuwa umemwingia, ikionekana kama hakuwa na njia ya kuepuka janga hilo mbele yake.

"Zelda!"

Sauti ya Lexi ikasikika kutokea upande mwingine wa sehemu hiyo, akiwa tu ndiyo amefika hapo. Azra akamwangalia, naye akamwona na Torres akiwa nyuma ya Lexi kwa njia ya kujificha, huku Lexi akipiga hatua taratibu kuja mbele. Azra akatambua sasa kwamba Zelda alikuwa ni huyu mnyama, na aliyemfuga ni huyo mwanamke aliyekuwa anasisitiza wao ni ndugu.

"Zelda... look at me. Look at me girl... look at me..."

Lexi akawa anajaribu kumsemesha Zelda ili asimkazie fikra Azra, naye Zelda akamwangalia Lexi. Victor alikuwa anatokea chumbani kwake kule juu huku akitafuna nyama ya kwenye paja la kuku, na baada ya Torres kumwona akamwonyesha kwa ishara kuwa arudi upesi. Ijapokuwa hakuelewa, akarudi na kuchungulia kutokea huko huko kuona yaliyokuwa yakiendelea, naye akashtuka sana.

"That's it... that's it... look at me. That's a good girl..." Lexi akaendelea kumsemesha Zelda huku akipiga hatua za taratibu kumwelekea.

Azra, kwa kufikiria sasa angeweza kujitoa hapo, akapiga hatua mbili nyuma, naye Zelda akamwangalia.

"No! Azra... don't... move!"

Lexi akamsemesha Azra kwa sauti yenye tahadhari kubwa sana kumzuia asijongee, na pumzi za Azra zikaongeza uzito kwa kuwa sasa Zelda alimwangalia kwa ile njia ambayo alijua ni ya mauaji.

"Zelda... look here, look here... she's my sister... don't you dare...."

Lexi alipokuwa anaendelea kumsemesha hivyo, LaKeisha akawa amefika hapo, karibu na Torres, na baada ya kuona hayo, akaanza kumsogelea Lexi pia taratibu.

"Lexi... ametokaje huyo?" LaKeisha akauliza.

Lexi alipokuwa anaendelea kukaribia zaidi upande wa Zelda, hofu ikamjaa baada ya kuona jinsi Zelda alivyochezesha mkia wake na kuonyesha utayari wa kumshambulia Azra kwa kunguruma kidogo.

"Shit!"

Lexi akapiga kelele hivyo na kujirusha kwa kasi yote baada ya Zelda kujifyatua na kumfata Azra kwa kasi. Lexi alijirusha upande aliosimama Azra, ambaye alikuwa ameanguka chini kwa hofu kubwa iliyompata, naye Lexi akakutana hewani na Zelda, hivyo akampamia na kuanguka naye sakafuni na kufanikiwa kumshikilia shingoni.

"Keish!"

Lexi akapiga kelele namna hiyo, naye Azra akashtukia anashikwa mkono wake na Lakeisha, ambaye alianza kumvuta ili waelekee chumbani upesi pamoja na Torres. Lexi akajitahidi kumng'ang'ania Zelda ili kumzuia asimuumize mtu, lakini Zelda akamshinda nguvu na kwa hasira kumkwarua sehemu ya juu ya kiganja chake. Lexi akahisi maumivu sana na kumwachia, naye Zelda akaanza kuelekea kule mbele kuifata nyama yake.

"Anawafata! Pigeni lock!"

Lexi akawaonya wengine namna hiyo kwa sauti ya juu kutokea alipokaa. Torres, Lakeisha na Azra waliingia kwenye chumba kile ambacho Mess Makers walikuwa na kawaida ya kufanya mikutano kwa pamoja na kukifunga kwa ndani. Kilikuwa na milango ya vioo, hivyo ni wakati tu wamerudi nyuma ndipo wakamwona Zelda akifika hapo na kutishia kupita lakini akajigonga. Azra alikuwa anapumua kwa hofu sana, huku Torres nusu adondoshe taulo! LaKeisha akasogea mpaka karibu na mlango huo na kuanza kumfokea Zelda, akimwambia aondoke haraka sana. Mnyama huyu alikuwa anamwangalia tu kwa njia ya hasira, naye akaanza kuzunguka kuzunguka hapo kwa dakika kadhaa, kisha akaondoka.

Kwa hapo, ni Lexi na Lakeisha pekee ndiyo ambao Zelda alikuwa amewazoea, na mtu mwingine aliyemzoea alikuwa ni Kendrick, kwa sababu kwa muda ambao Lexi alimchukua na kumfuga, ni watatu hawa tu ndiyo ambao alikua akiwa karibu nao miaka michache nyuma. Kwa hiyo wengine angewaona kama maadui, na ndiyo sababu muda mwingi alifungiwa kwenye nyumba yake ndogo mpaka aidha ya watatu hao washughulike naye. Mara zote ambazo wengine wangeambiwa kumsafisha, haikumaanisha walimkaribia na kumsafisha yeye Zelda, bali kusafisha sehemu aliyokaa kwa kutumia njia za uangalifu.

Baada ya Zelda kuwa ameondoka hapo, LaKeisha akamgeukia Torres na Azra, ambao walikuwa wanatazamana kwa njia yenye kuonyesha uajabu fulani hasa kutokana na hali ya Torres ya kuwa kifua wazi na kuvaa taulo tu, naye Torres akaelekea upande mwingine wa chumba hicho na kuketi.

"Are you okay? (uko sawa?)" Lakeisha akamuuliza Azra.

Lakini binti akabaki tu kumtazama.

"Don't worry. Your sister will take care of that. Just stay here (usijali.. dada yako atashughulika na hilo. Wewe kaa tu hapa)," LaKeisha akasema.

Kisha akatoka hapo mlangoni na kumfata Torres. Torres akamwambia LaKeisha aende kuangalia kama Lexi alihitaji msaada, lakini LaKeisha akagoma kwa kusema Lexi angemalizana na Zelda mwenyewe. Kihalisi alikuwa hataki tu kumwacha Torres peke yake na Azra huku akiwa bila nguo, kwa kuhofia labda eti kuna vitu vingetokea baina yao. Wivu huo.

Ilikuwa ni ajabu sana kwa Azra kwa sababu hakuelewa nia ya watu hawa kufanya mambo yote haya ilikuwa ni nini. Bado alihisi ni kama anafanyiwa mchezo, lakini akifikiria jinsi ambavyo mwanamke yule alijitoa kuokoa uhai wake, akili yake ikazidi kuchanganywa sana. Akakaa tu kwenye kiti kimoja humo, ikiwa ni kama ameshasahau kuwa dakika kadhaa nyuma lengo lake lilikuwa ni kutoroka hapo, naye akatulia tu akitafakari mambo mengi.

Zelda aliporudi kule alikomwacha Lexi, alimkuta akiwa amejiegamiza kwenye ukuta huku ameshika kiganja chake kusitiri maumivu. Pamoja na huyu kuwa mnyama, lakini alielewa kwamba mtu huyo aliyempenda alikuwa akiumia, naye akamsogelea mpaka karibu na kuanza kufanya kama jinsi paka huwa wanafanya wanapokuwa na mtu waliyemzoea. Akawa anasugua-sugua kichwa chake kwenye shingo ya Lexi, lakini Lexi alionyesha wazi kwamba alikuwa amekasirika kwa kuwa hata hakumwangalia.

"I told you to stop. Why didn't you listen to me? (nilikwambia uache.. kwa nini hukunisikiliza?)"

Lexi akamuuliza hivyo kwa sauti ya chini. Lakini mnyama huyu alikuwa anamwangalia tu, naye akaketi pembeni yake kwa njia ya kujilaza akimuegamia. Lexi alikuwa na hasira, lakini hakuwa na hasira na Zelda, bali baada ya kuwa ametafakari mambo yote yaliyotokea na kujua chanzo chake ni nini, ndiyo ikamfanya ahisi hasira kali sana. Lakini kwanza, angehitaji kumshawishi mnyama wake arudi kwenye nyumba yake ndogo kule nje ili aje kushughulika na mambo mengine. Kutokea vyumbani, sauti ya Victor ikasikika ikiuliza kama mambo yalikuwa shwari, naye Torres akasema atulie mpaka Lexi aseme jambo fulani.

Lexi akajinyanyua taratibu, naye Zelda vile vile akasimama. Akaelekea pamoja naye mpaka sehemu ya jikoni na kutoa mfuko wenye nyama iliyochomwa na kuhifadhiwa, kisha akaanza kuelekea nje pamoja naye mpaka kwenye nyumba yake ndogo. Akamfungulia, na upesi Zelda akaanza kula. Lexi akamwangalia sana mnyama wake, akijua hakuwa na makosa katika haya yote, ila aliyekuwa na makosa alikuwa ndani. Akamwacha na kuufunga mlango wa hapo kisha kurejea kule ndani. Alipokuwa akielekea kwenye chumba ambacho Torres na wengine walikuwa, akapaaza sauti kwa Victor kumjulisha kwamba mambo yalikuwa sawa, naye akafika kwenye chumba kile.

LaKeisha akamfata na kuuangalia mkono wake uliokuwa umeumia, naye akatoka haraka kwenda kufata boksi la huduma ya kwanza. Torres akasema angekwenda kuvaa nguo na kurejea, hivyo hapo akabaki mtu na "dada yake." Wakawa wanaangaliana sana, naye Lexi akamsogelea karibu zaidi. Wakati huu Azra hakujiweka tayari kwa pambano, kwa kuwa kufikia hapa aliona kweli Lexi hakuwa na nia mbaya naye.

"Are you okay?" Lexi akamuuliza.

Azra akaangalia tu pembeni.

"I'm sorry. That won't happen again (samahani.. hiyo haitatokea tena)," Lexi akamwambia.

"So you set loose your pet lion and put on a show in order to win my trust? (kwa hiyo ukamwachia simba wako wa kufugwa na kufanya hayo maigizo ili kunifanya nikuamini?)" Azra akauliza kimtego.

"Look bitch... (Ona malaya wewe...)" LaKeisha akawa amefika na kuanzisha maneno, "This woman here just bust her ass to save yours and that's how you thank her? (huyu mwanamke hapa ameumia ili kukuokoa wewe, halafu hivyo ndiyo unavyomshukuru?)"

"Keish..." Lexi akajaribu kumzuia.

"Keish nini? Unajaribu kumsaidia halafu anazingua kifala tu? You should have just let Zelda eat her! (..ungemwacha tu Zelda amtafune!)" LaKeisha akasema kwa kuudhika.

Azra akawa anamwangalia kwa hisia kali.

"Okay inatosha. Siyo makosa yake, you know that," Lexi akamwambia Lakeisha.

"Whatever," LaKeisha akasema.

Akauchukua mkono wa Lexi ili aanze kuupaka dawa. Lexi akamtazama mdogo wake kwa hisia sana, huku Azra akimwangalia kwa njia ya kufikirisha kwamba hakujali.

"Look... a lot is going on that I haven't figured out yet. But that's not going to stop me from doing what I know to be right... make up to you. I wanna make up for all that time that we've spent apart. I want to show you what we were... and what we can become... together. I want you to stop thinking of yourself as nothing but a weapon. I don't think of you as a weapon. You're not a weapon. You're my sister Azra. And I'm never ever giving up on you... ever," Lexi akamwambia kwa hisia.

Alikuwa akisema ingawa kuna mambo mengi yaliyoendelea ambayo hata yeye hakuelewa, hangeacha kufanya jambo lililo sahihi na muhimu zaidi, yaani kumwonyesha upendo aliostahili na alioukosa kwa muda mrefu kwa sababu ya kutengana kwao. Akamhakikishia kwamba yeye hamwoni kama silaha, hivyo naye alipaswa kuacha kujiona kama silaha tu. Hangemkatia tamaa kamwe, kwa sababu alikuwa ni mdogo wake kiukweli.

Azra akaanza kulengwa na machozi, lakini akageukia upande mwingine ili kutoonyesha hisia zake. Hata akawa anajiuliza alikuwa amepatwa na nini. LaKeisha akaangaliana na Lexi, naye akampa tabasamu hafifu la kumtia moyo.

"What happened here? (nini kimetokea hapa?)"

Wote wakasikia swali hilo kutokea nyuma, na baada ya kugeuka wakakuta ni Victor pamoja na Kevin. Ni Kevin ndiye aliyekuwa ameuliza hivyo.

"Zelda ndiyo amekufanya hivyo? Dada yako amekuletea majanga huyo," Victor akamwambia Lexi.

"Na wewe ulikuwa wapi?" LaKeisha akamuuliza Kevin.

"Chumbani... nimelala. Hizo vurugu zote zilikuwa za nini?" Kevin akauliza.

"Zelda kaingia ndani. Una bahati haukutoka la sivyo angetafuna scones zako hahahahah..." Victor akatania.

Lexi akawa anamtazama Kevin kwa mkazo sana.

"Ni sawa kumwachia huyo mdogo wako namna hiyo? Ameshaiona na nyumba hii, na sura zetu, sasa nini kitafuata?" Kevin akauliza.

Wakati huu LaKeisha akawa amemaliza kuufunga mkono wa Lexi kwa bendeji, naye Torres akaingia hapo tena.

"Kufikia hapo inamaanisha Lexi anamwamini vya kutosha kutotusaliti, si ndiyo?" Torres akaongea.

"Kwa jinsi mambo yalivyo, sidhani kama kumwamini inahusu. Ni suala la yeye kutotusaliti. Lexi, huyu ni mdogo wako sawa, lakini kwa hii miaka yote ambayo imepita hajakuwa pamoja nawe. Ameishi maisha tofauti, na anafanya kazi na maadui. Anaweza hata kuigiza kwamba atakuwa upande wetu halafu akatugeuka. Umeshawaza kuhusu hilo?" LaKeisha akamuuliza.

Lexi akamtazama Azra, ambaye sasa alikuwa anamwangalia pia.

"Ndiyo. Nimeshawaza kuhusu hilo. Nitafanya kila kitu ndani ya uwezo wangu kumfanya anikumbuke," Lexi akasema.

"Lexi... amejaribu kukuua mara kadhaa, hata leo. Una hakika gani hatafanya kitu kibaya kwako au kwetu? Huyu siyo mtu uliyekua naye, ni mtu tofauti sasa. Amefundishwa kulenga tu shabaha, na siyo kuingiza hisia. Utambadilisha vipi?" Torres akauliza.

Lexi akamsogelea karibu zaidi Azra.

"Sitambadilisha. Atabadilika yeye mwenyewe. I know her. I believe in her," Lexi akawaambia huku anamtazama Azra.

"Yaani kama siyo yeye, basi ni huyo simba wako ndiyo atakuja kutumaliza. Lexi dada yangu naheshimu sana mambo yako, lakini kiukweli unapotea, sitakuficha," Kevin akaongea.

"LaKeisha, take her to your room (mpeleke chumbani kwako)," Lexi akasema.

"What?!" LaKeisha akauliza kimshangao.

"Tunamfunga au hivyo hivyo tu?" akauliza Victor.

Lexi akamwangalia mdogo wake kwa umakini, kisha akasema, "Hakuna haja ya kumfunga. She needs to be free (anahitaji kuwa huru)."

Azra akaangalia chini tu.

"Free? Ahahahah... boss atapenda sana hii. Yaani nawaambia kesho kesho-kutwa sisi wote tutakuwa mikononi mwa Jacob kwa sababu ya huu upuuzi," Kevin akasema.

Torres akamsogelea Lexi karibu na kumuuliza, "Are you sure? (una uhakika?)"

Lexi akatikisa kichwa kukubali. Alionyesha kwamba anamwamini Azra, kwamba ingawa yeye bado alionyesha ugumu wa kuamini yale aliyoambiwa, lakini moyo wake ulijua ni ya kweli. Aliamini kabisa kwamba Azra alimwelewa, na hapa alikuwa anafanya kama kipimo cha imani yake kwa mdogo wake. LaKeisha akamwambia Azra amfuate ili ampeleke kwenye chumba kimoja hapo, na baada ya Azra kumtazama Lexi kwa kifupi, akawapita wote na kumfata LaKeisha taratibu.

"Yaani ni katoto tu lakini mambo kanayofanya! Hivi ana miaka mingapi?" akasema Victor.

"Atakuwa kwenye 22 sasa, si ndiyo?" Torres akauliza.

Lexi akatikisa kichwa kukubali.

"Mtakuja kujijambia katakapowafanya myeyushwe. Sasa hivi mnaniona mjinga, lakini mtakuja kuona," akasema Kevin.

"Ah, we kijana, yaani huachi tu!" Victor akasema kwa kukerwa.

Lexi akashusha pumzi, kisha akamfata Kevin na kumtandika kofi zito usoni!

Torres na Victor wakashangaa kiasi, na wakati tu Kevin alipomwangalia Lexi kwa hasira, Lexi akampiga ngumi mbili za kasi usoni, kisha akamtandika teke la tumbo, na hapo hapo kumnyanyua kwa nguvu sana na kumrusha mezani! Kevin alidondokea mpaka kwenye viti na kusababisha vishindo vilivyosikika mpaka kwa Lakeisha na Azra walipokuwa wamefika tu huko juu, naye LaKeisha akamwambia Azra waendelee tu kwenda kwa sababu hakukuwa na shida.

Kevin akajinyanyua akiwa amechanganywa sana na Lexi, hata Torres na Victor wakawa wanamuuliza anafanya nini, lakini akamfata tena Kevin na kuanza kumtandika hapa na pale kwa hasira sana, na kwa kiburi Kevin akawa anarusha ngumi pia. Akampiga moja usoni, na kwa hasira Lexi akamtandika kwa mtindo wa haraka uliosabahisha amuumize Kevin sehemu ya nyonga. Jamaa akaanza kujivuta chini hapo akishindwa kunyanyuka, hivyo ikabidi Victor aende kumsaidia. LaKeisha akawa amerejea na kukuta hilo zari, naye akauliza nini kilikuwa kinaendelea bila kupewa jibu. Torres akamshika Lexi na kumuuliza alikuwa ana tatizo gani, naye Lexi akauvuta mkono wake kwa hasira kutoka kwake na kumsogelea Kevin usoni.

"Najua ni wewe ndiyo uliyeifunga steam room. Najua ni wewe ndiye uliyemfungulia Zelda. Kevin ninakuonya. Ukija rudia kufanya jambo lolote lile kumwelekea Azra, au hata kusema tu, hautapaswa kuwaza tena kuhusu sisi kuyeyushwa. Kwa sababu nitahakikisha wewe ndiyo unayeyuka... milele," Lexi akamwambia kwa mkazo.

Wote wakawa wanamwangalia kimaswali sana, naye akaondoka hapo akiwa ameudhika haswa. Victor akamwachia Kevin kwa njia ya kumsukuma kidogo, naye akamwangalia huku anatikisa kichwa kwa kusikitika. Wote wakaondoka na kumwacha jamaa humo akiwa anaugulia maumivu kwenye kiuno chake, lakini pia akihisi aibu na hasira kwa sababu ya kile alichofanya kutofanikiwa na kuumbuliwa.

Lengo lake siku hii lilikuwa ni kuwamaliza dada wawili bila yeye kujulikana, lakini tena mpango wake ukakwama. Alidhani hakuna mtu ambaye angetambua ilikuwa ni yeye ndiyo alifanya yale, lakini sasa akatambua kwamba alikosea sana. Kuanzia wakati huu kiwango cha kumwamini kutoka kwa wengine kingepungua, naye alijua kuna siku tu ambayo watu hawa wangeamua kumalizana naye, hivyo kwa jinsi akili yake ilivyokuwa mbovu, akaanza kufikiria tena cha kufanya ili kuwakomoa.

Hakuna yeyote aliyekuwa ametambua kuwa wakati LaKeisha aliporejea huku, Azra alikuja pia na kuona kilichotokea. Alimwona Lexi alipomwongelesha Kevin maneno yale, naye upesi alirudi kwenye chumba kile alichopewa na kujifungia. Alikaa akiwaza mambo mengi sana. Bado akili yake ilimwambia alipaswa kujihami mno, hasa kutokana na mafunzo yake ya kutomwamini yeyote yule, lakini kuna hali fulani ndani ya moyo wake iliyokuwa ikimsukuma kuamini kwamba Lexi alikuwa ni mtu mzuri kwake.

Sasa alichobaki akijiuliza kilikuwa ni kitu kimoja; angefanya nini kuhusu haya yote?


★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★

WHATSAPP +255 787 604 893
 
Back
Top Bottom