Simulizi: For You

Simulizi: For You

FOR YOU

Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Uhalifu, Mauaji, Visasi, Vita, Mambo yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA AROBAINI NA NNE

★★★★★★★★★★★★★★★★★★


"Boss, we should arm ourselves (tunapaswa kubeba silaha)," Mensah akamwambia Kendrick.

"Hapana, don't panic. Tunaweza ku-solve hili kiurahisi," Torres akasema.

"Kiurahisi jinsi gani? Nora kawaleta hao wajing...."

"Hajawaleta Nora, LaKeisha. Hao sio watu wa serikali," akasema Kendrick.

"Unajuaje hilo?" akauliza Kevin.

"Kama siyo wa serikali ni wa nani?" akauliza LaKeisha.

Kendrick akasema, "Watakuwa watu wa Salim, I don't know. Lakini tunapaswa kuhakikisha hii inakuwa mara ya mwisho wanafika hapa. Lexi, mtoe Zelda umlete huku pamoja na Azra; Victor, Kevin, tengenezeni vizuri nyumba yake, Mensah, mimi nawe tulete kila kitu wasichotakiwa kuona huku, halafu Torres na Lakeisha...."

"Tunajua la kufanya," Torres akamalizia.

Lexi akaanza kuondoka haraka.

"Kwa hiyo tunajificha tu? Tungewapa hawa wajinga wanachostahili you know," akasema Kevin.

"Mna pungufu ya dakika tatu kufanya nilichowaagiza. Harakisheni," Kendrick akaamuru.

Wengine wakaanza kuondoka pia sehemu hiyo ya chini na kuelekea juu. Lexi alikuwa amekwenda kwenye chumba cha Azra, naye akamweleza hali iliyokuwepo na kumwambia akae humo humo mpaka akimpitisha Zelda. Akaenda na kwenye chumba chake na kuwakuta Isiminzile na Nora wakiwa wamekaa, naye akamwambia Nora kuwa kuna watu walikuwa wamefika hapo katika njia ya msako. Nora akashangaa, lakini pia kwa kufikiria labda ni yeye ndiyo alifuatiliwa akaanza kujilaumu, lakini Lexi akamtuliza na kumwambia haikuwa makosa yake. Lexi akawaambia walichopaswa kufanya ni kukaa hapo hapo ndani mpaka aje kuwaita, nao wakakubali na yeye akaondoka.

Alitoka mpaka nje na kwenda kumfungulia Zelda, ambaye tayari alikuwa amelala, naye akamwamsha na kuanza kumwongoza kuelekea ndani ya nyumba. Kufikia wakati huu, wengine wote walikuwa kwenye vyumba vyao isipokuwa Kendrick na LaKeisha, kwa sababu ni wao tu na Lexi ndiyo waliokuwa wamemzoea Zelda. Hivyo Lexi akampeleka Zelda mpaka kule chini, na ingawa mwanzoni mnyama wake huyu alisumbua, lakini mwishowe akaingia huko na kumfata Lexi mpaka kwenye kile chumba kidogo cha kupasha miili joto (steam room). Lakini alimwingiza humo bila kuwasha joto la ndani, kisha akamwacha tu Zelda na kuufunga mlango. Hii ilikuwa ni kwa sababu na wengine wangehitaji kuja chini huku kujificha, kwa hiyo Zelda angetakiwa kufungiwa ndani humo ili asidhuru mtu yeyote.

Baada ya kutoka huko chini, Lexi akawafata wakina Nora, Azra, na Isiminzile, huku Mensah, Victor, Kevin, na Kendrick wakijiunga nao pia kurudi huko chini wakiwa na vifaa mbalimbali. Hii ilikuwa ndiyo mara ya kwanza kwa Isiminzile na Nora kuingia chini huko, na kiukweli walistaajabishwa kiasi na ufundi wa kundi hili katika nyingi ya njia zao. Kwa hali ya kawaida tu isingekuwa rahisi kufikiri kwamba kungekuwa na chumba kipana sana chini ya ardhi, tena kilichofichika kitaalamu mno, hivyo iliwaacha wakiwa wanajiuliza mambo yote haya yalibuniwa na nani, na lini. Waliweza kuona vifaa vingi huko kwa ajili ya dharura, mitambo mingi ya kiteknolojia, na hata sehemu zenye vitanda vichache vya kulalia. Nora alikuwa na maswali mengi sana ya kumuuliza Lexi, lakini kwanza wangehitaji kutulia ili shida iliyokuwa ikiendelea ipite.

Lexi akawaelezea jinsi mpango wao ulivyokuwa. Wengine wote wangepaswa kubaki hapo chini, isipokuwa Torres na LaKeisha. Ni wawili hao tu ndiyo angalau mpaka sasa hawakuwa wamejulikana, ingawa hakukuwa na uhakika wa asilimia mia, hivyo wangetoka na kufanya maigizo ya hali ya juu ili kuwachengua watu wale waliofika hapo. Wakati Lexi alipokuwa anawaelezea Nora na Isiminzile haya, tayari LaKeisha na Torres walikuwa wameshapanda juu. Kwa hiyo kwa huko chini wangeendelea kukaa kwa utulivu mpaka wawili hao wakirejea.



Wanaume wale waliokuwa nje, baada ya kuona dakika tano zimepita bila kujibiwa, wakatoa onyo la mwisho kwa kusema kwamba sasa wangelazimika kulifyatua geti kwa risasi na kuingia ndani kwa lazima. Lakini papo hapo geti hilo likaanza kufunguka lenyewe mbele yao, nao wakajiweka tayari na kuanza kuingia ndani hapo. Walishangaa kidogo kutoona mlinzi yeyote sehemu hiyo, na kiongozi wao akawapa ishara kwamba wangetakiwa kuwa makini, hivyo wote wakawa wanaelekea mbele huku wakielekeza bunduki zao kwa utayari.

Walipofika usawa wa geti la pili, nalo pia likafunguka, kisha wakaanza kwenda kwa pamoja. Hapo wakaweza kuiona nyumba hiyo jinsi ilivyokuwa kubwa, na mwanaume fulani akishuka kutoka kwenye ngazi kuwaelekea, yaani Torres. Wakati huu alikuwa amevalia nguo kwa ajili ya kulalia (pajamas), akionekana kama vile ametoka kupumzika au ndiyo alikuwa anajiandaa kupumzika. Wanaume wale kwa ujumla walikuwa 14, nao wakamkaribia zaidi na kusimama mbele yake.

"Habari zenu?" akauliza Torres.

"Ni nzuri. Wewe ndiyo mmiliki wa hii nyumba?" akauliza kiongozi wao.

"Ni mimi. Na nyie ni nani?" Torres akauliza.

"Tulikuwa tumeshajitambulisha kule nje. Kwa nini hakuna mlinzi getini?" mwanaume huyo akauliza.

"Walinzi wamepewa likizo fupi," Torres akasema.

"Likizo? Nyumba na sehemu kama hii inaondolewa ulinzi kwa ajili ya likizo?"

"Okay, sijui shida yenu ni nini lakini hilo ni suala la kibinafsi. Kuna tatizo lolote?" Torres akauliza.

"Hakutakuwa na tatizo lolote endapo utatuacha tufanye kazi yetu. Tunawatafuta wahalifu hatari sana, wanaojiita Mess Makers. Nadhani umeshawasikia," mwanaume huyo akamwambia.

"Ndiyo. Na sasa mnafikiri wako nyumbani kwangu... kwa nini?" Torres akauliza.

"Hili siyo suala la kibinafsi. Hii ni operesheni inayofanyika nchi nzima, kwa hiyo tunaomba ushirikiano wako tu..."

"Okay sawa. Naelewa mnahitaji kufanya kazi yenu. Mnaweza kutafuta sehemu yote, lakini ninajua mnatakiwa kuwa na mipaka. Sitazamii mharibu vitu vyangu vya gharama kutafuta kitu ambacho hamtapata," Torres akasema.

Mwanaume huyo akacheka kidogo na kuwapa wenzake ishara kuwa waingie ndani kufanya msako. Torres hata akamkaribisha kiongozi wao huyo waongozane ndani ili amwelekeze vizuri mambo ya huko, akijiweka katika hali fulani yenye kuonyesha urafiki. Wanaume wale wengine walitafuta nyumba nzima na kukosa mtu mwingine, isipokuwa LaKeisha, ambaye alikuwa chumbani akiwa amejilaza kitandani. Ikabidi naye atoke baada ya "kuvamiwa" na watu "asiowajua," naye akaelekea kule chini alipowakuta Torres na yule kiongozi wa kundi hilo. Alikuwa amevalia nguo ya kike ya kulalia pia, naye akasogea mpaka usawa wa Torres.

"Honey, what's going on? (mpenzi, nini kinaendelea?)" LaKeisha akamuuliza Torres.

"They're doing a search... Mess Makers thing (wanafanya upekuzi.. ishu ya Mess Makers)," Torres akajibu.

"Aaa... hi," LaKeisha akasema na kumsalimia hivyo mwanaume huyo.

Mwanaume huyo alikuwa anamtazama LaKeisha kwa njia iliyoonyesha upendezi, lakini akawa anajifanya kukaza.

"Unaitwa nani?" LaKeisha akamuuliza.

"Jina langu siyo muhimu hapa. Tukikosa tunachotafuta, hamtatuona tena," mwanaume huyo akajibu.

"Okay. Kwa hiyo ni nini kilichowafanya mkafikiri tunaficha wezi hapa?" LaKeisha akauliza.

"Kila mlango wa nyumba zote nchini unafanyiwa search. Siyo nyie tu..."

"Mmeshajaribu mpaka kwa Raisi?" LaKeisha akauliza kikejeli.

Torres akamkaza mkono kumzuia.

"Unasemaje?" mwanaume huyo akauliza.

"Aa... anatania tu. Kiukweli hatukufikiria mngekuja tu ghafla namna hii, kuna mambo tulikuwa tuna... si unajua? Imemkera kidogo," Torres akasema kiutani.

Mwanaume huyo akawa anamwangalia LaKeisha kwa umakini, huku LaKeisha akimpa tabasamu kwa ujasiri. Wenzake wote wakawa wamerudi, na kila mmoja wao akasema wametafuta vyumba vyote lakini hawakupata chochote chenye kutia mashaka.

"Kama tu nilivyowaambia, hapa tupo sisi tu. God, natumaini hawa Mess Makers wakamatwe haraka maana wanaumiza vichwa sana," Torres akasema.

"Nyumba yako ni kubwa sana. Ina vyumba vingi mno kuishi watu wawili tu. Una uhakika hakuna wapangaji hapa?" mwanaume huyo akauliza.

"Mimi ni mjasiriamali mkubwa ndugu yangu. Nina watu wengi, nina mikutano mingi, nina party nyingi. Napokuwa sijisikii kutoka hata kwa mwaka mzima, kila kitu kinafanyikia hapa. Kwa hiyo kuwa na vyumba vingi ni sehemu ndogo tu ya kutumia kile nilichonacho. Na hii siyo nyumba yangu pekee. Kwa hiyo... ikiwa ni hayo tu, tunawashukuru sana, na tunatumaini mtai-note sehemu hii kutokuwa nyumba ya wezi. Asanteni sana," Torres akaongea kwa uhakika.

Mwanaume huyo akamtazama kwa umakini na kumwangalia LaKeisha kwa umakini pia, kisha akatoa ishara kwa wengine kuwa wangeweza kuondoka hatimaye.

"Poleni kwa usumbufu. Mnaweza kuendelea na mliyokuwa mnayafanya," mwanaume huyo akasema.

Torres akatabasamu na kusema, "Kwa tahadhima yote, bila shaka."

LaKeisha akacheka kidogo kwa kiburi.

Mwanaume huyo pamoja na kundi lake lililojitambulisha kuwa la "serikali" wakaondoka hapo hatimaye. Baada ya hayo kuhitimika, LaKeisha akafurahi sana na kumrukia Torres, akimpa busu ya ushindi. Wakarejea kwa wenzao kule chini na kuwaambia mambo yalikuwa safi huku juu, nao wakatoka wakiwa wanauliza ni yapi yaliyoendelea. Torres akawaelezea kwamba bila shaka wanaume hao hawakuwa watu wa "serikali" moja kwa moja, bali inaonekana walikuwa ni watu kutoka kundi fulani maalum kati ya makundi ya kijeshi yaliyotumiwa kwa umakini sana.

Azra akawa ametambua kwamba hao bila shaka walikuwa ni watu wa Luteni Jenerali Weisiko, kwa sababu alifahamu njia za mwanaume yule kutokana na kutumiwa kwake kwenye mishe kadhaa, lakini hakuwaambia wengine kuhusiana na hilo. Kendrick akawaambia vijana wake kwamba wangetakiwa kuwa makini zaidi, kwa sababu kadiri siku zinavyozidi kwenda ndiyo watu kutoka nje wangeendelea kuwakaribia, kwa hiyo akawaasa waende kupumzika ili kuja kupanga mambo yao vizuri kwa kesho.

Nora mpaka kufikia sasa alikuwa anajiuliza mwanamke yule mdogo alikuwa nani, yaani Azra, kwa sababu kati ya wote waliotambulishwa kwake ni yeye tu ndiyo hakuwa ametambulishwa bado, na aliona ufanani baina yake na Lexi, lakini akakaa kimya tu ili aje kumuuliza Lexi vizuri. Wengine walipotawanyika kurudi vyumbani kwao, Lexi akamwongoza Nora pia mpaka kwenye chumba chao na kumwambia amsubiri na asitoke ili aweze kumrudisha Zelda kwenye nyumba yake ndogo. Tena na hapa Nora akawa anajiuliza Zelda ndiyo nani, na baada ya Lexi kuondoka, ikabidi asimame karibu na mlango ili aweze kumwona huyo Zelda wakati Lexi angempitisha. Si ndiyo akapata sasa kumwona akiwa na mnyama aliyefanana na simba huku akimwongoza kuelekea nje!

Nora aliendelea kuchoshwa akili na hawa watu. Yaani alianza kujiona ni kama yuko kwenye sinema fulani isiyoisha vituko kila alipodhani amejua mambo yote kuihusu. Ikabidi tu akae kitandani na kumsubiri Lexi mpaka aliporejea, na baada ya yeye kufika akaketi usawa wa kitanda pia huku akimtazama kwa umakini. Nora akaangalia chini na kutikisa kichwa kwa njia iliyoonyesha ameachwa njia panda, naye Lexi akatabasamu kidogo.

"Yaani Lexi kiukweli... hizi wiki chache zilizopita zimebadili kabisa aina ya mtu niliyedhani ulikuwa. Everything about you is just... a mystery (kila kitu kuhusu wewe ni fumbo)," akasema Nora.

"Pole Nora. Lakini usijali, I'll get you up to speed," Lexi akasema.

"Hicho kilikuwa ni nini? Na wewe ni Tarzan sasa?" Nora akauliza.

"Ahahah... huyo ni Zelda. Ninamfuga. Tokea Ghana. Ni kipenzi changu," Lexi akasema.

"Alikuwa wapi wakati tuko huko chini?"

"Alikuwepo huko huko... ila nilikuwa nimemfungia ili asije kuwaumiza..."

"Yaani unataka kusema kwamba tulikuwa kwenye banda moja na simba?"

"Ahahah... ndiyo..."

"Ahah... hivi hata ulimwingizaje humu nchini?"

"Njia ni nyingi. Bandarini, kwenye kontena..."

"Okay, inatosha. Sitauliza njia zenu tena," Nora akasema.

Lexi akacheka kidogo.

"Unaweza kuniambia yule msichana ni nani?" Nora akauliza.

"Anaitwa Azra. Ni mdogo wangu," Lexi akajibu.

"Yeah, nimeona mnafanana, na tayari nilikuwa nimekisia hilo. Lakini... nimesoma taarifa kuhusu familia yako, na inasemekana wote walikufa... kutia ndani wewe... miaka nane iliyopita. Mambo haya yote yaliwezekanaje?" Nora akauliza.

Lexi akashusha pumzi ya utulivu, naye Nora akawa anamwangalia kwa umakini.

"Kwanza kabisa Nora... nataka nikushukuru sana kwa kunisaidia usiku ule. Isingekuwa ya wewe labda ningekuwa nimekufa sasa," Lexi akamwambia.

"Ahah... unajua sikufikiri kiukweli kama ungeweza kuwatoroka wale wanaume, ila nikaweka tu matumaini..."

"Ndiyo Nora, naelewa. Na jambo hilo hilo ndiyo lilinipa nguvu. Nilikuwa nimeshavunjika moyo na kuamua liwalo na liwe, lakini nilivyotambua kwamba unaniamini... na mimi nikajitahidi kufanya yote ili nisikuangushe..."

"Kwa hiyo... ulipigana vile ili utoke... kwa ajili yangu?"

"Yeah... for you," Lexi akasema kwa hisia.

Nora akamwangalia kwa hisia pia.

"Nilijihakikishia kuwa kama ningetoka mikononi mwao, ningetumia kila njia ili nikufikie na niweze kukueleza kila kitu, kwa kuwa sikutaka kukuacha gizani. Nora... baba yako ni mtu anayefanya mambo mengi mabaya sana..."

"Mambo gani?"

"Unakumbuka kisa cha Demba Group kilichotokea hapa nchini miaka kadhaa nyuma?"

"Ndiyo..."

"Ni yeye pamoja na watu wengine ndiyo waliowaongoza baadhi ya wanajeshi kufanya matendo yale... wakijiita Demba Group..."

"Nini?"

"Ndiyo..."

"I don't understand..."

"Wakati huo... baba yangu na uncle Kendrick walikuwa wanajeshi pia... Uncle Kendrick akiwa kama Captain alikuja kubaini mpango wa baba yako na Lieutenant Weisiko wa kutaka kumwondoa Raisi madarakani ili wamweke makamu wake ndo awe Raisi..."

"Mdeme?"

"Yeah. Njia waliyotumia ilikuwa ni hiyo ya Demba Group, na walifanya mambo yao kwa umakini sana ili wasijulikane, lakini uncle Kendrick akajua. Walikuwa wameua watu wengi sana ili tu kupata mambo waliyotaka. Yeye ndiyo chanzo cha wazazi wangu na ndugu zangu kuuawa. Usiku ule maisha yangu yalibadilika sana. Nilimwangalia mama yangu, na baba yangu na dada zangu wawili walipouliwa na Weisiko... na mimi nisingekuwa hai ikiwa uncle Kendrick asingeniokoa," Lexi akasema kwa hisia sana.

Nora alimwonea huruma, mpaka machozi yakawa yanamlenga.

"Najua kila kitu nachokwambia huenda kikaonekana kama kimebuniwa tu... lakini usijali, nitakuthibitishia kila kitu," Lexi akasema.

"Nafahamu baba yangu siyo mtu mzuri sana kama anavyojionyesha kwa wengine... lakini sikuwahi kufikiria yeye ni mnyama kiasi hicho. Ni kwa nini alifanya hayo yote? I can't believe this," Nora akasema kwa huzuni sana.

"Yeye pamoja na wote walioshirikiana naye walinibadili sana... nilitaka sana kuwaua wote siku ambayo ningekutana nao. Lakini uncle Kendrick... yeye ndiye aliyenifundisha jinsi ya kuzuia hasira yangu... akanifundisha vitu vingi sana vilivyonifanya nitambue hasa njia nzuri ya kuwaangusha wabaya wetu wote. Kuwaua kusingetosha... nilitaka kuwafanya wajulikane kwa mabaya yao yote waliyofanya, na maumivu yote waliyosababishia mamia ya watu kwenye hii nchi wapitie na wao wangeyapitia," Lexi akasema huku chozi likimtoka.

"Oh Lexi..." Nora akamshika shavu na kumfuta chozi.

"Mhm... najua hii ni ajabu kwa kuwa nayemwongelea ni baba yako..."

"Hapana. Nakuelewa vizuri. Wakati mwingine kufuata njia ya haki hakuleti matokeo mazuri sana hasa kama unadili na mtu anayetumia ukatili kama njia yake kuu, hivyo ninafurahi kujua kwamba ulichagua kufichua mabaya yao badala ya kufanya umwagaji wa damu," Nora akasema.

"Oh Nora... mimi sitakuwa mnafiki kwako. Nitaua yeyote yule anayejaribu kuingilia kati kwenye njia yangu ya kufanya mambo. Yote niliyopitia kipindi cha nyuma... sitaki tena yeyote ayapitie. Tulijaribu kuwakomesha kwa namna yetu, lakini kiukweli...."

"Its okay. Naelewa Lexi. Naelewa," Nora akamkatisha huku akimshika usoni.

Lexi akatazama tu pembeni akiwa na huzuni.

"Nitaelewa mambo mengi vizuri ukishanipa uthibitisho zaidi. Lakini ninajua unayosema ni kweli. Nakuamini," akasema Nora.

Lexi akamtazama na kutabasamu.

"Aam... vipi kuhusu... ulichoniambia siku ile?" Nora akauliza.

"Jambo gani?"

"Ulisema kwamba wewe... unatamani kuoa. Ijapokuwa mwanzoni nilidhani labda uliongea bila kufikiri lakini baadae niliendelea sana kutafakari hayo maneno. Ulikuwa unamaanisha nini?"

"Ahah... kwani mwanamke hawezi kuoa?"

"Hapana, nilihisi ulikuwa na maana tofauti Lexi..." Nora akasema.

"Kuna jambo lilitokea... mimi na dada yangu tuli-switch miili... mpaka leo sijajua ni nini kilisababisha hilo. Mwili huu ni wa pacha wangu, na yeye ndiye aliyekuwa ndani ya mwili wangu wakati Weisiko alipomuua," Lexi akaeleza.

"What? Hiyo inawezekanaje?" Nora akashangaa.

"Ilitushangaza sisi sote, lakini hatukuweza kujua kilichotokea. Kwa hiyo miaka mingi baada ya Sandra kufa ilibidi tu nizoee kuwa ndani ya mwili wake...," Lexi akasema.

Nora akamwangalia kwa kujali.

"Maisha yangu ni kama fumbo kubwa sana, hilo ni kweli. Na najua mambo yote nayokwambia yanakuchanganya sana," Lexi akasema.

"Ndiyo ni kweli. Lakini sijui tu ni kwa nini kila kitu unachosema nakuwa... nakiamini," Nora akamwambia.

"Asante Nora. Nilitokea kuwachukia sana mapolisi na wanajeshi wengi hasa kwa sababu ya matendo ya watu kama Weisiko... lakini wewe...." Lexi akaishia hapo.

Nora akatabasamu kwa mbali.

"Kwa hiyo... ukiwa ndani ya mwili wa dada yako... bado unapata... hisia kama mwanaume?" Nora akauliza.

"Ni tofauti. Bado nahisi kuwa mimi, lakini mwili huu ni wa mwanamke kwa hiyo kuna vitu siwezi kubadili. Naishi kulingana na hali," Lexi akasema.

"Okay. Kwa uzuri wako Lexi, bila shaka umeshatongozwa karibia mara buku," Nora akasema.

"Ahahahah... ndiyo, wanaume wengi sana wamejaribu kunitokea. Wakati tumefika Tanzania, Kevin alijaribu kunitongoza eti..."

"Ahahahah... alikuwa anajibebisha?"

"Ahahahah... yeah."

"Ikawaje?"

"Nikampiga stop kali kama yule Luka wa siku ile Sea House," Lexi akasema, naye Nora akacheka.

Lexi akatulia kidogo, kisha akaanza kusema, "Ona... samahani kwa kukuambia mambo mengi yenye kuchanganya kwa..."

"Hapana, usiombe samahani," Nora akamwambia kwa sauti ya chini.

Nora akaanza kusogea karibu zaidi na Lexi na kukishika kiganja chake. Akawa ameukaribia zaidi uso wa Lexi sasa, naye Lexi akawa ameelewa jambo hili lilikotaka kuelekea.

"Nora..." Lexi akaita kwa sauti ya chini.

"Yes..." Nora akaitika na kutulia.

"Kuwa na... mimi kama mwanamke... siyo ajabu kwako?"

"Hapana, kwa nini iwe ajabu?"

"Usiku ule... ulisema ulihisi labda nimekuroga tu, kwamba haungeweza
kamwe kutoka nami katika hali ya kawai...."

"No, no, Lexi... nisamehe. Samahani sana kwa kusema maneno yale. Nilikuwa na hasira, niliumia, nilifikiri labda umeniumiza kwa makusudi maovu... sikumaanisha nilichosema," Nora akaongea kwa kujali.

"Nora... mimi ni mwanaume kwa ndani, lakini nje siko hivyo. Samahani lakini... siwezi kukupa kile unachohitaji kwa njia nayotamani kufanya hivyo," Lexi akasema kwa hisia.

"Acha kuomba samahani Lexi. Kiukweli... sijui ni kwa nini lakini wanaume wengi ambao nimekuwa nao hawajawahi kunifanya nihisi vile navyotaka kuhisi... ila kwako... ilikuwa tofauti kabla hata sijajua ndani ulikuwa mwanaume. Ni ngumu kuelezea lakini...." akaishia hapo.

"Samahani Nora..."

"Kwa nini unaomba samahani?"

"Ni kwamba tu... sina uhakika sana... yaani... samahani...."

"Agh, Lexi ukisema samahani kwa mara nyingine nitakupiga ngumi!" Nora akamwambia.

Lexi akaangalia pembeni tu.

Nora alikuwa amekwishamwelewa, na alitaka sana kumwonyesha kwamba kile alichowaza hakikuwa na shida yoyote kubwa.

"Lexi... niangalie..." Nora akasema.

Lexi akageuka na kumwangalia machoni. Nora akamshika kidevuni na kutelezesha mkono wake mpaka shavuni.

"Usijali, ninakuelewa. Ninajua yote uliyopaswa kupitia toka ulipobadilishwa mwili na dada yako hayakuwa rahisi... ninaelewa. Lakini usijifungie namna hii. Huu ni mwili WAKO sasa. Usiwaze kuhusu kile ambacho huna.... fuata tu moyo wako.... kama mimi nilivyochagua kufanya," Nora akasema kwa hisia sana.

Lexi alimwangalia sana Nora kwa hisia za upendo.

Ni kweli kwa ndani yeye bado alikuwa "Xander," na kuishi kwenye mwili wa mwanamke ilikuwa ni mtihani mgumu sana kwake tokea hali hiyo ilipompata. Alifikiria kwamba hangeweza kumfurahisha mwanamke kwa njia aliyozoea kufanya zamani, hasa kwa kuwa mwanamke aliyempenda kama Valentina hakukubaliana na hali yake hiyo mpya, hivyo aliona ni kama hata kwa mwingine ingeweza kuwa namna hiyo. Lakini Nora alionyesha kwamba hakujali kuhusiana na hilo, kwa kuwa alimpenda YEYE, yaani utu wake, na siyo kwa kuangalia sura wala mwili tu.

Nora akawa anamtazama Lexi kwa njia iliyoonyesha kwamba alimhitaji sana. Ilimchukua ujasiri kiasi kuushika mkono wa Lexi na kuuingiza ndani ya uwazi mdogo wa T-shirt yake kwa chini, na pale tu kiganja cha Lexi kilipoigusa sehemu ya mbavu yake, Nora akasisimka sana. Lexi pia alipatwa na hisia ambazo kwa kipindi kirefu aliziona kuwa za ajabu kwa sababu ya kuwa kwenye mwili wa mwanamke, lakini kwa Nora ziligeuka na kuwa nzuri sana kwake. Nora akiwa anamwangalia Lexi kama anasubiri afanye jambo fulani, Lexi akaipeleka midomo yake polepole kwenye midomo ya Nora na kumpa busu laini.

Wawili hawa wakaendelea kupeana busu kwa midomo taratibu, kisha wakaifungua midomo yao na kuanza kuzungushiana ndimi kimahaba sana. Mawazo yote ya Lexi kuwa ndani ya mwili wa pacha wake, yaliyomfanya ajizuie kujitoa kwa mtu yeyote kwa muda mrefu sana, yalififia kwa Nora. Tokea mara ya kwanza na ya mwisho alipojitoa kwa LaKeisha hakuwa amejiweka katika hali hii tena, ila sasa akajiachia tena. Alikuwa amejenga upendezi wa hali ya juu sana kumwelekea Nora. Ni jambo ambalo wote walikuwa wamejenga kwa muda fulani sasa, lakini kutokana na hali zilizowazunguka haikuwa rahisi kuonyeshana hilo.

Sasa Lexi akiwa ameondoa vikwazo vyote akilini mwake na kuamua kumwonyesha mwanamke huyu upendo, alianza kufanya mambo kwa njia ambayo angeyafanya kama Xander. Yeye kuwa "Lexi" ilimaanisha alipaswa kukumbuka kwamba kuwa ndani ya mwili wa dada yake bado kunamuunganisha naye, ijapokuwa tayari alikuwa amekufa, na ndiyo maana aliamua kuupa mwili wake heshima hiyo ya kuwa kitu kimoja tokea Alexandra alipokufa. Lakini sasa Nora alikuwa amemsaidia kuona kwamba hakupaswa kuhisi hatia ikiwa angeamua kushiriki mwili huu na mtu mwingine aliyempenda, kwa sababu kihalisi mwili huu sasa ulikuwa ni WAKE.

(.........).

Kisha Lexi akajitoa mdomoni mwake na kumwangalia machoni kwa hisia sana. Nora pia akawa anamwangalia huku akitabasamu kwa mbali, naye Lexi akaweka paji lake la uso kwenye paji la Nora akiwa amefumba macho. Nywele chache za Nora zilikuwa mbele ya uso wake, hivyo Lexi akatumia kiganja chake kingine kuzirudisha nyuma ya sikio la Nora taratibu. Kisha akalishika shavu la Nora na kumwangalia tena machoni, huku Nora akiwa amelegeza sana shingo yake na kumwangalia Lexi kama vile anamsubiria atende chochote kile anachojisikia.

Lexi akasogeza mdomo wake karibu kabisa na wa Nora, na hapo aliweza kuhisi joto la pumzi zake.

"This is going to be crazy... (hii itakuwa hali yenye kuchizisha)" Lexi akanong'oneza karibu zaidi na mdomo wa Nora.

Nora akatabasamu kilegevu na kusema kwa kunong'oneza, "Yeah."

(.........).

(.........).

Ndimi zao ziliendelea kuchezeana kwa sekunde kadhaa na bila papara yoyote. Lexi alianza kufurahia hata zaidi ukaribu huo, hasa kwa sababu ilikuwa ni Nora. Alipandwa na hisia nyingi sana zilizomfanya atake kufanya mambo kwa haraka, lakini alijidhibiti kwa kuwa hakutaka aongozwe na hisia za mwili wake huu ambao bado alielewa ulikuwa ni wa mwanamke. Kilichokuwepo hapa ilikuwa ni jambo moja tu; kumfurahisha Nora, na hiyo ndiyo ingekuwa furaha tosha kwake.

Ingawa alikuwa ametoka kujimwagia muda mfupi nyuma, Nora alikuwa na ngozi yenye joto sana kutokana na kusisimka mno. Lexi akaona apeleke penzi hili hatua nyingine. Mkono mmoja wa Lexi ukafungua kifungo laini cha suruali ya Nora, kisha ule ulio ndani ukashuka moja kwa moja mpaka kwenye paja la Nora lililokuwa nene kiasi na kuanza kuishusha suruali yake. Alitambua haraka kwamba Nora alijua anapoelekea kwa kuwa mwanamke huyu alijinyanyua ili yote itolewe, kisha akayaachanisha mapaja yake yaliyokuwa yamegusana na kufanya mkono wa Lexi uweze kutomasa paja moja kuelekea katikati.

(........).

Kufikia wakati huu Lexi alikuwa na T-shirt nyepesi tu ya mikono mirefu na suruali. Kisha akaacha kulitomasa paja la Nora na kumbusu, akijitoa kabisa kwake na kusimama kutoka alipokuwa amekaa.

Nora akamwangalia akiwa ameshangazwa kiasi na jambo hili, naye Lexi akaelekea upande mwingine wa kitanda hiki na kuchukua kifaa kidogo kama rimoti kutoka kwenye droo ya pembeni, kisha akarudi usawa alioketi Nora. Akampa tabasamu la mbali, kisha akabonyeza rimoti hiyo, naye Nora akatazama upande uliokuwa na sebule na kuona kitu kama pazia nene sana likishuka kutokea juu katikati mpaka chini; lililofanya kama kuitenganisha sehemu ile ya sebule na upande wa huu wa kitanda, hivyo hawangeweza kuonwa kutokea upande wa pili. Akamwangalia Lexi kwa kupendezwa na jambo hilo, naye Lexi akaketi tena kitandani karibu yake.

"Naona hii nyumba imejengwa kiteknolojia sana," Nora akasema kwa sauti ya chini.

"Yeah, ni kazi ya Torres," Lexi akajibu.

"Mbona sasa ulikuwa unaniuliza ikiwa ulitakiwa kutoka nje ili nivae... kama tu ungeweza kufanya hivyo?" Nora akamuuliza.

Lexi akachezesha macho yake huku na huku, kisha akasema, "Zilikuwa swagger!"

Nora akacheka kidogo na kumshika shavuni. Kisha akasimama karibu kabisa na uso wa Lexi, akiwa anamwangalia kwa hisia, naye akaitoa T-shirt yake na nguo yake ya ndani, akiiacha ianguke chini. Sasa mwili wake wote ukawa wazi mbele ya Lexi. Lexi aliutazama kwa matamanio mengi, akipendezwa na rangi ya maji ya kunde ya mwanamke huyu. Ijapokuwa alikuwa askari lakini aliutunza mwili wake vyema, kwa sababu haukuwa umekakamaa kama wa mwanamke mkomao.

(.........).

Alipojitoa mdomoni mwake, Nora akapanda mpaka katikati ya kitanda polepole, akiwa anatambaa na kulielekeza kalio lake kwa Lexi ili ayaone maungo hayo vizuri. Lexi akawa anamwangalia huku anatabasamu, naye Nora akakaa akiwa ameibana miguu yake, akimwangalia kwa njia fulani ya kichokozi, naye Lexi akatabasamu na kumfata mpaka hapo. Nora akaishika sehemu ya chini ya T-shirt la Lexi na kuanza kulipandisha juu, naye Lexi akamruhsu kwa kuinyoosha mikono yake juu.

Kwa mara ya kwanza, Nora (.......). Lakini alipendezwa hata zaidi na michoro ya tattoo kuzunguka kifua cha Lexi mpaka tumboni na mikononi. Yaani ilikuwa ni kama amevaa nguo nyingine kwa jinsi tattoo hizo zilivyochorwa kwenye ngozi yake nyeupe kwa ubunifu sana, kuanzia sehemu ya juu ya kifua kufikia sehemu ya chini ya tumbo, na mikononi mwake mpaka kufikia mgongoni.

Akawa anazitazama huku anatembeza kiganja chake kuzifatisha jinsi zilivyochorwa.

"Nani alikuchora hizi?" Nora akauliza.

"LaKeisha," Lexi akajibu.

"Ooooh... kumbe anajua eeh?"

"Ndiyo..."

"Lazima awe special. Wewe kumwachia akuchore hivi I mean..."

"Ndiyo, tumetoka mbali. Lakini pia tuliwahi ku.... ila siyo sana," Lexi akasema.

"Ahaaa... kumbe ndiyo maana alikuwa ananifanyia vile..."

"Ahah... yeah," Lexi akasema.

Nora akamkazia macho kwenye upande wa kushoto wa kifua chake, na hapo akaona majina fulani yakiwa ndani ya mchoro wa tattoo ya kopa (love), na kwa kuyasoma akatambua ilikuwa ni watu wa familia yake Lexi; Casmir, Alice, Sandra, Azra, Salome. Akamtazama machoni na kukuta Lexi anamwangalia kwa hisia pia, hivyo akaifata midomo yake ili waweze kuendelea na penzi lao. Lakini wakati alipoizungushia mikono yake nyuma ya mgongo wa Lexi, akahisi kitu fulani kilichofanya ajitoe mdomoni mwake kwa mara nyingine. Akamtazama kimaswali sana.

"Nini hiki?" Nora akauliza.

Alikuwa ameishika sehemu ya nyuma ya bega la Lexi. Lexi hakumjibu, bali akaangaalia tu chini. Nora akazungukia nyuma na kuangalia sehemu hiyo ya begani, na hapo akaona plasta nene ya jeraha iliyotuna kiasi, na kwa haraka alitambua lilikuwa ni jeraha la risasi.

Lexi akamgeukia taratibu.

"Hiki bado kiko fresh... Lexi... nini kilitokea?" Nora akauliza kwa kujali.

"Wakati natoroka... mmoja wao alinifyatulia...." Lexi akaishia hivyo.

"Oh Lexi... kwa nini hukuni.... sikupaswa...."

"Heey... niko sawa, kimeshapoa. Hakiko fresh kama kinavyoonekana, kwa hiyo usijali," Lexi akamwambia.

Kisha akaifata midomo ya Nora na kuanza kumbusu tena.

Nora alipenda sana jinsi Lexi alivyoupa mwili wake umakini, kwa kuwa alimshika hapa na pale kwa kuminya-minya na kumtekenya kwenye sehemu za mwili wake. Akajitahidi kurudisha upendo namna hiyo lakini akawa makini kutomkandamiza sehemu ya begani. (.........).

(........). Lakini baada ya Lexi kujitoa tu mdomoni mwake ili afanye hivyo, Nora akaendelea kuifata midomo yake na kuipiga denda tena, akikataa kuivunja busu yao tamu. Lexi alifurahi kuona jinsi Nora alivyoonyesha kupenda sana jambo hili.

(........).

(........).

(........).

Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Nora kufanya mapenzi na "mwanamke," ijapokuwa Lexi alikuwa mwanaume kwa ndani, hivyo Nora alikuwa akitaka kuona nini kingefuata ndani ya penzi hili jipya kwa kuwa hakujua sana atarajie nini kama alivyozoea kwa mwanaume. Kila kitu alichofanya Lexi kilimpagawisha sana Nora kadiri dakika ulivyozidi kwenda.

(........).

(........).

(........).

Mapigo ya moyo wake Lexi yalidunda kwa nguvu sana kwa kuwa hili ni jambo alilokuwa akitamani sana kufanya.

(........).

(........).

(........).

(........).

Lexi alipomtazama Nora kutokea katikati ya mapaja yake, akamwona jinsi alivyomtazama kwa hisia nyingi nzito za mahaba. Mkono wa Nora ulikuwa umekishika kichwa cha Lexi huku mwingine uking'ang'ania shuka kwa nguvu, naye akaliachia na kujiziba mdomo huku akikirudisha kichwa chake kitandani kwa nguvu. Lexi aliweza kusikia sauti zilizozibwa za kelele kutoka kwa Nora, lakini akautoa mkono huo mdomoni mwake, kwa sababu alijua hata kama akipiga kelele wengine hawangeweza kusikia, hivyo akawa anataka kumhakikishia hilo.

Alipenda sana sauti za Nora za miguno, ikiwa kama sauti za msichana mdogo anayedeka, naye akawa anamtekenya taratibu mwanamke huyo baada ya kuwa amemaliza kumwaga raha zake. Nora akabaki kupumua kiuchovu huku akiusugua mkono wa Lexi taratibu, bila kumwangalia, lakini akizungusha shingo yake huku na huku.

Lexi akaanza kumbusu taratibu kuanzia kitovuni kuelekea mpaka mdomoni. Wakaanza kudendeshana tena, kisha Lexi akajitoa mdomoni mwake na kumwangalia machoni. Nora akawa anamtazama huku akizichezea nywele za Lexi.

"Pelvis to pelvis," Lexi akamwambia.

Nora akacheka kidogo.

"Uko tayari kuendelea kuwa nami... hata ikiwa...."

"Lexi... stop," Nora akamkatisha.

Lexi akawa anamwangalia kwa hisia.

"Nakupenda," Nora akasema.

Lexi akaachia tabasamu kwa hisia nzuri sana aliyoipata.

Nora akatabasamu pia na kumvuta Lexi kwake, nao wakaanza kupiga busu tena.

Baada ya kuwa wamepeana mapenzi kwa mara hiyo ya kwanza, wawili hawa wakajilaza kitandani hapo pamoja na kuvuta shuka nene kuifunika miili yao; Nora akiwa amempa mgongo Lexi, na Lexi akiubana mwili wake nyuma ya mwanamke huyo huku wakiwa wameshikana.

Nora akawa wa kwanza kufumba macho yake, naye Lexi akawa kwa nyuma akizihisi pumzi za mwanamke huyo jinsi zilivyoonyesha kutulia kwake na kuridhika. Yeye pia Lexi alihisi uchovu kiasi ingawa hakuwa ametendeshwa kama yeye alivyomtendesha Nora, hivyo naye akafumba macho na kuanza kuutafuta usingizi, akihisi amani moyoni kuwa pamoja na mwanamke huyu aliyemkubali bila kujali hali aliyokuwa nayo.



★★★★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★★★★

WHATSAPP +255 787 604 893
 
Huyu isiminzile na bibi si ndio waliyemloga Lexi na pacha wake?Kama yupo hapo kwanini asimrudishie Lexi uanaume wake?Tunashukuru sana mkuu,ila kufidia ya jana ungetupia kigongo kingine.
Elton Tonny
Nadhan atakuja kukurudishia tu
Na kwel atuongeze hata kamoja tu
 
Mkuu [mention]Elton John [/mention] tushushie hata episode moja tusindikize ushindi wa Spain
 
FOR YOU

Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Uhalifu, Mauaji, Visasi, Vita, Mambo yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA AROBAINI NA TANO

★★★★★★★★★★★★★★★★★★


Nora anafumbua macho yake kukiwa kumeshakucha. Anajihisi vizuri sana ndani yake, kama vile mtu ambaye ametoka kusafishwa mwilini, lakini hisia hii kwake ni ya moyoni. Mwanga wa nje umezuiwa kupenya mpaka ndani kutokana na mapazia makubwa sehemu za madirisha, hivyo kuna hali fulani ya ugiza ndani hapo. Anapogeukia upande wa pili kumwangalia Lexi, anakuta upande huo ukiwa tupu, naye kwa haraka anatambua kwamba Lexi amekwishaamka.

Akajinyanyua taratibu na kukaa, akitabasamu kwa kuhisi furaha baada ya kumbukumbu ya mambo ambayo Lexi alimfanyia usiku uliopita kumwingia. Akajivuta polepole ili ashuke chini, na hapo akaona viatu vya manyoya vya kutembelea ndani, hivyo akavivaa na kuelekea usawa wa kabati la nguo lililokuwa upande huo wa kitanda. Akaachia tabasamu baada ya kuona kikaratasi kilichobandikwa hapo, kikiwa kimechorwa uso wa duara wenye kutabasamu na maneno "good morning" yakiwa yameandikwa, naye akakitoa na kukitazama kwa hisia.

Akafungua kabati na kutoa nguo ya kulalia (pajamas), naye akauvalisha mwili wake ambao haukuwa na nguo yoyote na kuzibana nywele zake kwa nyuma. Akaingia bafuni na kusafisha uso na kinywa vizuri, kisha akarudi chumbani na kuamua kuyaachanisha mapazia ili mwanga upite ndani. Kutokea hapo aliposimama, aliweza kuona kule nje, mbali sana, jinsi palivyopendeza kutokea huko juu. Akafungua mlango mpana wa kioo wa dirisha hilo, na ingawa kulikuwa na baridi, akatoka ili asimame kwenye ubaraza mdogo wa hapo juu atazame mandhari hiyo vizuri.

Wakati akiwa anatazama huko, akaanza kusikia sauti za kicheko, na sauti hiyo akaitambua kwa urahisi. Ilikuwa ni ya Lexi, na ilitokea chini upande wa kulia kutokea alipokuwa amesimama Nora, hivyo akasogea hapo na kutazama huko chini. Akamwona Lexi akiwa pamoja na mnyama wake, yaani Zelda, wakiwa wanacheza kwenye sehemu yenye kiwanja chenye majani yaliyokatwa vizuri. Lexi alikuwa anarusha mpira mdogo halafu anashindana na Zelda kuukimbilia, na kila mara Zelda angeuwahi na kuchukua kwa meno, kisha kuanza kukimbia nao akimkwepa Lexi.

Hatimaye ikafikia hatua ambayo Lexi alidanganya kuurusha mpira mbali, lakini akaurusha karibu na kuuwahi yeye, halafu akaanza kumzomea Zelda, na mnyama wake huyo akamrukia na kuanza kuzungusha kichwa chake hapa na pale kwenye mwili wa Lexi, huku Lexi akicheka. Nora akacheka kwa kustaajabishwa na jambo hilo, kwa sababu ilikuwa ni kama Zelda anamtekenya Lexi. Akavutiwa sana na urafiki huo kati ya mnyama mkali na mwanadamu, na kuona jinsi Zelda alivyoitikia mambo vizuri kulimaanisha Lexi alikuwa amemfundisha vyema.

Wakiwa wanaendelea kucheza, Zelda akamwona Nora, naye akasimama tu na kubaki amemwangalia kwa umakini. Lexi alipoangalia juu na kumwona Nora, akatabasamu na kumpungia mkono, naye Nora akampungia pia. Lexi akawa anamlazimisha Zelda eti apunge mkono pia, lakini mnyama huyu akawa tu anamwangalia Nora kama ameona chakula. Nora akatoa ishara kwa Lexi kuuliza ikiwa Zelda alikuwa anafikiria kumtafuna, naye Lexi akatoa ishara akimwambia ashuke chini ili aone. Nora akakataa, naye Lexi akacheka. Akamtolea ishara kumwambia kwamba anamalizia kutumia muda kidogo na Zelda kisha angemfata, naye Nora akakubali. Ikabidi Nora arudi tena ndani ili Zelda aache kuzubaa sana, naye Lexi akaendelea kucheza naye.

Baada ya Nora kuingia chumbani tena akaamua kwenda kuoga kabisa ili kuwa safi kimwili. Akavua pajamas na kuingia bafuni, naye akaanza kuoga taratibu. Lakini alipokuwa akiendelea, akashtuka kiasi baada ya kutambua kulikuwa na mtu anamtazama kutokea nje ya mlango wa kuingilia kwenye bafu hilo pana, naye akakata maji na kuvaa taulo, kisha akatoka upesi ili aone ilikuwa ni nani. Alipoingia sehemu ya chumba, akamkuta Kevin, akiwa amesimama karibu na kitanda huku anatafuna tofaa. Nora akakunja uso kimaswali, akiwa anahisi kuudhiwa sana na uwepo wa mwanaume huyo hapo.

"Unafanya nini humu?" Nora akauliza.

"Nilikuwa nimekuja kuongea na Lexi," Kevin akajibu kwa njia fulani ya kizembe, huku anamwangalia Nora kiutongozi.

"Yuko nje, kaongee naye huko," Nora akasema kwa uthabiti.

"Ahahah... usiku mmoja tu hapa tayari umeshaanza kujifanya mkali sana eeh?" Kevin akasema.

"Aisee, nakuomba utoke," Nora akasema kwa ukali sasa.

Kevin akakunja sura na kumsogelea karibu zaidi. "Sitoki sasa. Utafanya nini?" akamwambia kiujeuri.

Pumzi za Nora zikaongezeka kasi kwa kupandwa na hasira.

"Usinipandishie sauti mimi. Haujui kundi letu limetokea wapi, na usifikiri kwa sababu sasa hivi unachokonolewa kwa peni na huyu basi hiyo itakufanya uwe mmoja wetu... sahau," Kevin akasema kwa sauti ya chini yenye uzito.

"Aliyekwambia kwamba kilichonileta hapa ni kuwa mmoja wenu ni nani?" Nora akauliza kwa hisia kali.

"Oooh... kwa hiyo kumbe umekuja kutufanyia upelelezi wako wa kichawi, utusambaratishe kama ulivyofanikiwa kufanya kwa Oscar na kutugawanyisha kuanzia na Lexi, siyo? Mama, umekwama. Hapa kama unafikiri utaweza kutung'oa kwa uchawi wako nakwambia tena, umekwama!" Kevin akasema.

"Ninakuomba utoke sasa hivi!" Nora akasema kwa ukali.

"Ama nini?" Kevin akauliza huku akimsogelea karibu zaidi na uso kibabe.

Nora akang'ata meno yake kwa hasira na kwa kasi akamtandika kofi zito usoni. Kevin akajisawazisha na kumwangalia Nora kwa hasira sana kama anataka kumpiga, huku Nora akimkazia macho kwa ujasiri.

"Kevin..."

Sauti kutokea nyuma yake Kevin ikasikika ikimwita. Akageuka na kukuta ni LaKeisha, ambaye alikuwa ameingia ndani hapo muda huo huo.

"Victor anahitaji msaada kwa mashine, kamsaidie," LaKeisha akamwambia.

Kevin akamwangalia tena Nora kwa uso ulioonyesha chuki kali, kisha polepole akaanza kurudi nyuma huku anamwangalia na kumsonta, na baada ya hapo akatoka ndani hapo. Nora akashusha pumzi akihisi mapigo yake ya moyo yanadunda kwa nguvu kwa sababu ya hasira iliyompanda, naye akatazama pembeni akiwa anatafuta utulivu. LaKeisha akamwangalia kiufupi, kisha akamfata na kusimama mbele yake. Nora akamwangalia tu usoni.

"Huwa unakula mayai?" LaKeisha akauliza.

Nora akabaki kumtazama tu.

"Huh? Unakulaga mayai? Nijibu, nataka kutengeneza chakula cha pamoja," LaKeisha akasema.

"Ndiyo huwa nakula," Nora akajibu na kutazama pembeni.

"Mhm... inaonekana itakuwa ngumu sana kwako kuishi hapa..."

"Aagh, dada sikia. Mimi sijali agenda zenu nyote kuhusu mimi. Semeni lolote, fanyeni lolote, lakini mimi niko hapa kwa ajili ya Lexi. Nyie wote ni wa muhimu kwake, na ninaheshimu hilo. Lakini hiyo haimaanishi nitakuwa mnyonge kwenu na kuwaacha mnitendee kwa njia yoyote mnayotaka kwa sababu tu mnanichukia. Ninajua wazi kwamba mnanichukia, na nimekuja hapa nikiwa naelewa hiyo itakuwa challenge mpya kwangu. Lakini haitafanya niondoke upande wa Lexi," Nora akasema kwa uhakika.

"Kwa hiyo kumbe uko hapa kwa sababu tu ya fling uliyonayo na Lexi? Siyo kwa sababu ya kujua kwamba uko upande sahihi?" LaKeisha akamuuliza.

"Kwa mambo yote yaliyotokea, hakuna upande ulio sahihi. Sisi wote tumefanya mambo mabaya kwa kadiri fulani. Lakini nimeamua kusimama na Lexi kwa sababu nimeona aina fulani ya haki ndani ya moyo wake, na ninataka nimsaidie kufanya mambo kwa njia sahihi zaidi. Sitakataa kwamba nilikuwa upande ambao kwa njia kubwa ni mbaya sana, nikifikiri ndiyo mzuri. Ila sasa kuwa kwangu upande wenu ni nafasi mpya ya mimi kujua ukweli, na kumsaidia Lexi kutafuta haki inayostahili..." Nora akasema.

"Kwenye huu mchezo hakuna suala la haki dada'angu, ni maumivu na mateso tu," LaKeisha akasema kwa uzito.

"Najua. Lakini kama nilivyosema... hii ni nafasi tu. Nafasi mpya ya kubadili mambo. Nafasi mpya ya kubadili... kubadili aina ya mtu niliyekuwa mwanzoni," Nora akasema huku akitazama chini.

Kauli hiyo ikamfanya LaKeisha amtazame kwa uelewa mwingi. Alimkumbusha jinsi hata yeye alivyokutana kwa mara ya kwanza na Lexi, akamsaidia kubadili maisha yake, mpaka kufikia wakati huu wakiwa bado pamoja.

"Kwa hiyo... ikiwa na wewe unataka kunisema au kunichokoza au kunimeza, jitahidi tu. Lakini mambo ndiyo yako hivyo," Nora akasema.

LaKeisha akacheka kidogo huku akiwa amefumba mdomo.

"Nora..."

Wawili hawa wakageukia nyuma yake LaKeisha na kumwona Lexi akiwa amesimama hapo. Akaanza kuwasogelea polepole huku akiwa ameweka uso ulioonyesha udadisi.

"Oh well, me naenda kupika. Msichelewe," LaKeisha akasema na kuanza kuondoka.

Lakini Lexi akaushika mkono wake kumzuia, naye LaKeisha akakunja uso kimaswali.

"Kila kitu kiko sawa hapa?" Lexi akamuuliza Nora.

LaKeisha akamkazia macho Lexi kwa kukerwa.

"Yeah, kila kitu kiko sawa. Alikuwa ananiuliza ikiwa nakula mayai," Nora akasema.

Lexi akamtazama LaKeisha.

"Usiniangalie hivyo, kama ningekuwa nataka kumuua angekuwa ameshakufa," LaKeisha akasema, kisha akautoa mkono wa Lexi kwake na kuondoka.

Lexi akamwangalia Nora kwa umakini, naye Nora akatabasamu.

"Hajakusumbua huyo?" Lexi akauliza.

"No. Vipi... Zelda amelala?" Nora akauliza.

"Tss... alale sasa hivi? Hapana, yuko nje ametulia. Unapaswa ujue kwamba hutakiwi kutoka ndani mpaka kwenye mida ya kuanzia saa 6, ndiyo huwa namrudisha ndani kwake," Lexi akasema.

"Aaaa... ana ratiba zake na yeye," Nora akasema.

Lexi akacheka kidogo na kuingiza mikono yake kiunoni kwa Nora, kisha akamvutia karibu yake. Nora akaweka ya kwake kwenye shingo ya Lexi huku akitabasamu.

"Unapendeza sana ukiwa umetoka bafuni," Lexi akasema.

"Ahahah... hata wewe unapendeza sana ukifurahi. Jinsi ulivyokuwa unacheza na Zelda... maisha ya furaha kama hivyo yanakufaa sana," Nora akasema pia.

Lexi akatabasamu na kumbusu mdomoni kwa upendo.

"Tunafanya nini leo?" Nora akauliza baada ya kumaliza busu.

"Tunatulia tu hapa ndani. Tukimaliza chai, tutakuwa na maongezi pamoja na wengine. Maswali yako yote yatajibiwa," Lexi akasema kwa uhakika.

Nora akashusha pumzi na kumwangalia kwa umakini machoni, naye Lexi akaifata tena midomo ya mwanamke huyu na kuanza kumpa denda ya asubuhi taratibu huku wakiwa wameshikana kwa ukaribu.


★★★★


Muda mfupi baadae, wakati wakiwa kwenye meza ya chakula, Nora alijihisi tofauti sana kukaa pamoja na "wahalifu," kwa sababu yeye alikuwa ni askari na hali hii mpya ikamfanya ajihisi ni mmoja wao. Lexi, Isiminzile na Torres ndiyo walikuwa wanajitahidi sana kumwonyesha staha nzuri, lakini wengine hawakumjali sana. Bado alikuwa na hasira kumwelekea Kevin kwa kitendo alichomfanyia asubuhi hiyo, na ingawa bado mwanaume huyo aliendelea kumwonyesha dharau hata kwa macho yake tu, Nora hakumwambia Lexi lolote.

Ilitimia mida ya saa 5 asubuhi, na kufikia sasa wote waliokuwa kwenye nyumba hiyo ya maficho walikuwa wameshapata kiamsha kinywa na kuendelea na mambo yao ndani hapo. Nora alikuwa amepelekwa na Lexi chumbani kwa Azra, ili kufanya utambulisho rasmi. Alipata kujua sasa kwamba Azra ndiye aliyetumiwa kuwaua wanajeshi wale watatu wa timu ya Luteni Michael, Oscar, na Salim Khan, na kiukweli ilimshangaza sana kwamba mwanamke mdogo namna hiyo angeweza kufanya mambo makubwa kiasi hicho. Ikawekwa wazi kwake kwamba Azra hakuwa na kumbukumbu za maisha yake ya zamani, hivyo Lexi alimsaidia kumtoa kwenye mikono iliyomwongoza vibaya na kumleta huku ili wawe familia tena. Nora alitambua upesi kwamba Azra hakuwa mtu anayeamini watu kirahisi, na kutokana na hali alizokuwa nazo ilimbidi Nora amwelewe tu. Akamwonyesha tu urafiki na kusema alifurahi kumfahamu, kisha baada ya hapo wawili hao wakatoka na kwenda kule chini.

Huko ndiko kile kikao kifupi cha maongezi kingefanywa, na wakati huu Nora akawakuta Mess Makers wote wakiwa hapo; kutoa Azra na Isiminzile. Torres akamkaribisha aketi kwenye kiti cha pembeni yake, naye Nora akatii. Wote walikuwa wanamwangalia Nora kwa umakini sana na kumfanya adhani labda walisubiri aseme jambo fulani, lakini akamwangalia Lexi kimaswali tu. Lexi alikuwa amesimama usawa wa kiti ambacho Kendrick aliketi, naye akampa Nora tabasamu dogo tu.

LaKeisha akaanza kuongea, "ACP Nora... karibu kwenye mkutano mkuu utakaotupeleka moja kwa moja kwenye matukio muhimu ya kipindi cha nyuma mpaka kufikia sasa...."

"LaKeisha unafanya nini?" Victor akamkatisha na kumuuliza hivyo.

"Nampa utangulizi kwa njia atakayoelewa, au umesahau kama yeye ni police? Unajua ACP Nora... kiongozi mmoja wa jeshi aliwahi kusema kwamba...."

"LaKeisha acha mambo yako bwana," Torres akamwambia.

Kendrick, Mensah na Lexi wakawa wanachekea kwa chini, huku Nora akitabasamu kwa mbali.

"ACP Nora, asante sana kwa kuwa pamoja nasi wakati huu..."

Torres akaanza kuongea hivyo, naye LaKeisha akamwonyesha Kendrick kwa ishara kuuliza kwamba kulikuwa na utofauti gani na utangulizi alioutoa yeye na wa Torres, naye Kendrick akatabasamu.

"Tutakuelezea mambo mengi ambayo huenda yakakuchanganya, lakini kwa akili yako nzuri ninajua utaelewa haraka. Hatuna muda mwingi wa kukusanya kila kitu na kukurushia, hivyo nafikiri itakuwa vyema tukifanya hii kama interrogation... wewe ndiyo uulize maswali vital zaidi, ili upate majibu unayotaka. Sounds okay?" Torres akamwambia.

Nora akatikisa kichwa kukubali, kisha akasema, "Sawa, nimeelewa."

"Safi. Kwa mambo mengi nafahamu tayari unajua kuhusu sisi kuwa "wezi," lakini hujui kwa nini sisi ni "wezi." Sikiliza kwa makini kila mtu atakapoongea kwa upande wake ili wewe mwenyewe uwe ndiyo kama hakimu... uamue ikiwa yale unayosikia ni kweli au la," Torres akasema.

Nora akamtazama Lexi, naye Lexi akamwonyesha kwa ishara ya kichwa kuwa aanze.

"Okay. Kwa nini mnajiita Mess Makers?" Nora akauliza.

"Yaani katika maswali yoote muhimu ukaona uanze na hilo?" Kevin akamuuliza.

"Kevin!" Mensah akasema kiukali.

"Nini? Hapa naona kama tunapoteza muda tu. Tungekuwa tunautumia huu kwa ajili ya mambo muhimu zaidi," Kevin akasema.

"Kama nini? Kufokea wanawake kwenye nyuso zao?" LaKeisha akamuuliza.

Swali la LaKeisha likavuta umakini wa Lexi.

"Unajua, sasa naelewa ni kwa nini mliamua kumfanya huyu mwanaume aigize kuwa kichaa. Hakuna mwingine kati yenu ambaye angeweza kuigiza vizuri kama yeye kwa sababu tayari yeye ni kichaa," Nora akasema kwa uhakika.

Kevin akamtazama kwa kuudhika. Wengine wakaanza kucheka kwa kuelewa vizuri maneno yake.

"Ahahahah... dah, hadi nam-miss Oscar. Kama angekuwepo angesema...."

"Boom! Burned," LaKeisha akamalizia maneno ya Victor.

"Ni Oscar ndiye aliyetuita hivyo. Haikuwa kitu chochote rasmi lakini baada ya vyombo vya habari kuanza kulisambaza zaidi... jina hilo likageuka kuwa letu," Torres akasema.

"Unajua nini... mwanzoni sikulipenda hilo jina. Lakini baada ya kifo chake... ilikuwa ni kama alituachia alama yake kwa njia hiyo pia. Kiukweli jina Mess Makers linaleta msisimko fulani hivi... sasa hivi mtu yeyote akilisema atakachowaza tu ni sisi... na sisi ni hatari," akasema LaKeisha kwa hisia.

"Na picha ya kwenye sticker... ilikuwa reference kwa Zelda, si ndiyo?" Nora akauliza.

Lexi akatikisa kichwa kukubali.

Nora akatazama chini kiufupi, akitafakari jambo fulani lilitokeza swali muhimu zaidi ambalo tokea alipoanza kushughulika na msako wa kundi hili ndiyo lilikuwa likimchanganya zaidi. Akamwangalia Kendrick, kisha akauliza, "Mliiba vipi zile trilioni 20 benki kuu?"

Kendrick akatabasamu kidogo, kisha akamwambia Torres amwelezee kila jambo kwa njia nzuri sana ambayo ingemwelewesha mwanamke huyu njia waliyotumia ili kufanikiwa kufanya jambo lililodhaniwa kutowezekana. Torres akaanza kumweleza Nora jinsi walivyofanikiwa kuziiba pesa zile kwa kusema kwamba hawakuziiba moja kwa moja, bali ni kama WALIPEWA.

Kwa kuwa hii ilimchanganya Nora, akauliza ni nini maana yake, naye Torres akaanza kumtembeza taratibu kwenye kujua kuhusu njia walizotumia kupata pesa hizo.....


★★★★


JINSI MESS MAKERS WALIVYOIBA TRILIONI 20 BENKI KUU


Baada ya Kendrick na vijana wake kuwa wamefika nchini na kukamilika, ilikuwa ni wakati wa kuanza kupiga hatua za mipango yao waliyokuwa wameandaa tokea wakiwa Ghana, na hasa Kendrick, Torres pamoja na Lexi ndiyo waliohitajika kuwaongoza vizuri wengine ili kufanikiwa. Kufikia wakati huu, wale ambao tayari walikuwepo huku kabla ya Kendrick, Lexi, na Lakeisha kufika, walikuwa wameshakamilisha baadhi ya mambo muhimu yaliyohitajika, ili siku ya kupiga hatua ikifika wawe tayari kwa asilimia zote. Kila mmoja alikuwa na mgawo muhimu katika suala hili lilioonekana kuwa gumu sana, lakini wote waliazimia kuhakikisha linafanikwa.

Kevin alitengenezwa vizuri sana na kupewa mwonekano uliomfanya aonekane kama kichaa, akiwa mchafu na aliyenuka sana. Mgawo wake ulimtaka awe akitumia muda mwingi eneo ambalo lilizunguka majengo ya benki kuu, ili aweze kuona taratibu za pale nje, na jinsi usalama ulivyowekwa, halafu angekuwa anawapa taarifa wenzake ili kuongeza njia za kuimarisha zaidi mpango wao.

Victor alikuwa ameweza kutengeneza sura bandia na zenye kufanana kabisa na watu wawili waliofanya kazi kwenye benki ile; Eunice Shirima na Nathan Masunga. Alitumia umakini sana kuzitengeneza kwa kuiga picha zao na kutumia vifaa alivyozoea, na pia akatengeneza vitambulisho bandia ambavyo vingefanana na vile ambavyo wafanyakazi hao walitumia kwa ukawaida kazini.

Wakati hayo yakiwa yanakamilishwa, ni Lexi pamoja na Oscar ndiyo waliotumia muda wao kujiweka karibu na wawili hao na kujenga urafiki pamoja nao. Lexi alijenga urafiki na Eunice Shirima, ambaye alikuwa mwanamke mstaarabu sana, na Lexi alijitambulisha kwake kama Nadia. Mwanamke huyo alipendelea kwenda kwenye mgahawa fulani wa kisasa kila siku kwenye mida ya mchana ili kupata chakula, na ndiyo hapo Lexi alikutana naye kila siku na kufanya mazungumzo naye. Vilevile, Oscar alijenga urafiki pamoja na Nathan Masunga, akijifanya kama kijana fulani tajiri aliyeitwa Erick na kutumia muda mwingi kujifurahisha naye. Watu hao walikuwa sehemu muhimu ya mpango huu kwa kuwa Lexi na Oscar wangekuja kuigiza kuwa wao, ili waweze kuingia ndani ya majengo yale bila kutambulika na kufanya kilichowapeleka.

Kwa hiyo baada ya kuhakikisha kila jambo limepangiliwa vyema kwa kila mmoja wa kundi hili, ikafika siku ambayo mpango huu ungeanza kazi. Lexi alikuwa amehakikisha kwamba siku hiyo Eunice hangekwenda kazini kwa kuwa siku iliyopita aliweka dawa fulani kwenye kinywaji chake ambayo ingesababisha asumbuliwe na tumbo la kuhara kwa siku mbili mfululizo. Alikuwa ametumia njia tofauti na ya Oscar, kwa kuwa yeye alicheza mchezo wa ku-bet na Nathan Masunga ili kumzuia kwenda kazini siku hii, na wote wakawa wamefanikiwa.



Baada ya Victor kuwaandaa vyema wawili hawa na kuwapa mwonekano uliofanana kabisa na wa Eunice Shirima pamoja na Nathan Masunga, Lexi na Oscar wakatoka na kwenda kwenye majengo ya benki kuu na kuingia wakiwa wamevaa vitambulisho vyao, nao wakawa wakiigiza kama kawaida ya watu waliochukua utambulisho wao, na hakuna mtu yeyote aliyehisi kuna jambo haliko sawa. Walikuwa wameshapitia mambo mengi kuhusu kile walichotakiwa kufanya kwa sehemu za kazi walizokuwa nazo hapo, hivyo wakaendelea kujiweka hapo na kupoteza muda ili ufike wakati mwafaka wa kupiga hatua.

Eunice Shirima ndiye pekee ambaye alitaka kutoa taarifa kwa wakuu kwamba hangeweza kufika ofisini siku hiyo, lakini Torres alikuwa ameunganisha mitambo yake kwa simu ya Eunice, hivyo alipopiga namba za mkuu wake, simu hiyo ikaenda kwa Torres, ambaye akapokea na kuweka programu maalum iliyoruhusu kuigiza sauti ya mtu yeyote, naye akaweka sauti ya mkuu wa Eunice na kumwambia haikuwa na shida; apumzike nyumbani kwa siku mbili zaidi. Kwa hiyo kwa hapo kukawa hakuna tatizo lolote tena, na sasa Torres akatoa maagizo kwa Lexi na Oscar kuanza kazi iliyowapeleka kule ndani.

Mpango ulikuwa ni kuingia ndani ya vyumba vilivyoshikilia masanduku makubwa sana (vaults) yaliyobeba pesa nyingi mno. Eunice Shirima alikuwa na ruhusa ya kuingia sehemu hiyo kutokana na kitengo cha kazi alichokuwa nacho, hivyo hiyo ndiyo ikawa shabaha ya Lexi. Kuna kitu fulani kilichokuwa kimefichwa kwa umakini sana ndani ya chumba maalum ambacho ni Gavana wa benki kuu tu ndiye aliyeweza kufungua, yaani Gavana Laurent Gimbi. Oscar alikuwa ametengeneza kifaa ambacho kingemsaidia Lexi kuweka viingizi vya utambulisho bandia uliofanana na wa Gavana Laurent, kama neno la siri na alama za vidole vyake ili Lexi aweze kufungua na kuchukua kitu hicho cha muhimu sana.

Kitu hicho kilikuwa ni boksi dogo lililotunza vifaa vichache vyenye taarifa za siri za hali ya juu za mambo mengi ambayo kundi la kufanya maovu la Raisi Paul Mdeme lilikuwa limefanya. Waingereza huita taarifa hizi "top secret" au "classified," na kwa kipindi fulani cha wakati zilikuwa zikifichwa ndani hapo na kundi hili kupitia Gavana Laurent. Muungano wao ulihitaji sana uaminifu wa hali ya juu kwa mipango yao, na hii ilikuwa ni njia ya kuhakikisha kwamba hawasalitiani kwa lolote, kwa sababu endapo yeyote angefanya usaliti basi taarifa za mambo aliyofanya zingetumiwa kumuadhibu. Ilikuwa kama uhakikisho wa kwamba wangeendelea kuaminiana, kwa hiyo kila mara walipofanya jambo fulani haramu, rekodi zozote zilizobaki zilitunzwa humo; hasa mafaili na "flash disc" za kompyuta. Katika utafiti wake mwingi miaka michache iliyopita Torres alikuwa amepata kujua kuhusu jambo hilo, na kwa pamoja yeye na Lexi wakawa wameliweka kuwa shabaha muhimu zaidi katika mpango huu.

Lexi sasa alitakiwa kuingia ndani ya chumba hiki, aibe taarifa hizo, kisha ndiyo waondoke. Kutoka na trilioni 20 hapo ni kitu ambacho hakikuwezekana, lakini kuiba taarifa hizi na kuzitumia dhidi ya Raisi Paul Mdeme ndiyo kungefanya watoke na hizo pesa. Huo ndiyo uliokuwa mpango wao.

Wakati Lexi alipokuwa anajipanga sasa kuingia huko, Oscar tayari alikuwa ameshatega mabomu yake mawili katika majengo hayo kwa umakini na tahadhari kubwa, na ilikuwa kwenye sehemu za pembeni ya vyumba vilivyotunza pesa nyingi sana. Kulikuwa na walinzi na watu kadhaa kwa ndani kwa hiyo bomu la kwanza lilipolipuka, mshtuko mkubwa bila shaka ungeleta taharuki nzito hapo, na ndiyo Lexi akaitumia nafasi hiyo kupenya ndani kule na kufungua kile chumba wakati wengine walipokuwa wakikimbia kwa ajili ya usalama. Akafanikiwa kukifungua na kuingia ndani, kisha akachukua boksi hilo dogo na kuanza kupekua humo, akitaka kuchukua flash chache na makaratasi hususa, kisha akayaficha vyema ndani ya nguo zake na kutoka.

Akaenda mpaka usawa wa eneo ambalo alijua angemkuta Oscar, na sasa eneo lote hilo la hayo majengo lilikuwa linakaribia kuwa tupu kwa sababu ya watu wengi kukimbia, bila kuwa na mtu yeyote aliyejeruhiwa. Lexi akampata Oscar, ambaye alikuwa kwenye chumba cha walinzi wa mifumo ya digitali ili kuharibu mifumo ya kamera za CCTV za ndani ya eneo la majengo hayo, kutia ndani chumba alichokwenda Lexi, ambazo zilikuwa ni nyingi sana. Alipomaliza, alitakiwa kuanza kuziharibia na zile za nje ya eneo hilo, lakini muda ukawa hautoshi baada ya wawili hawa kuanza kusikia sauti za ving'ora vya zima moto, polisi, na magari ya hospitali.

Ikambidi Oscar abonyeze mtambo wake mdogo uliofanya bomu lingine lilipuke upande mwingine wa jengo, kisha wawili hawa wakaelekea sehemu iliyokuwa imelipuka na kuanza kuangalia ikiwa kuna watu walikuwa wamejeruhiwa, ili kujaribu kuwasaidia. Ndani ya ngozi bandia walizokuwa wamevalishwa ili kuwafananisha na Eunice Shirima na Nathan Masunga walikuwa wamevaa nguo zao maalum za mapambano, hivyo joto la moto halikuwaunguza sana. Oscar alikuwa ametega mabomu yake kwa umakini sana ili kuhakikisha hakuna mtu aliyekufa, lakini bado alijihisi vibaya kwa sababu kuna baadhi waliokuwa ndani bado na hivyo kuumia, kutia ndani wachache waliokuwa wameanza kuingia ndani ya eneo hilo alipolipua bomu la pili.

Baada ya dakika kadhaa wawili hawa wakatambua kwamba kundi lingine la kutoa msaada lilikuwa likija. Kwa kuwa wangehitaji kujifanya wameumia pia, wakatafuta sehemu ya kujilaza na kujipaka vumbi jeusi usoni na mwilini kuonekana walipondwa na matofali labda. Sehemu hiyo ilikuwa ni hususa, kwa sababu watu ambao wangekuja kuwasaidia waliojeruhiwa wangeanza kutafuta huku na kule, lakini Mess Makers walikuwa wanajua wenzao wangefika hapo moja kwa moja. Kwa hiyo walipoanza kuingia, Mensah, Victor, na Kevin ndiyo waliofika wakijifanya kuwa waokoaji kwa kuvaa nguo maalumu za wafanyakazi wa hospitali, nao "wakawasaidia" kunyanyuka; Mensah na Victor wakimbeba Lexi, na Kevin akitembea pamoja na Oscar kwa kumpa egamio.

Wakatoka pamoja nao katikati ya watu wa usalama na kuwapeleka kwenye 'ambulance' moja, huku na majeruhi wengine wakiwa wanapelekwa kwenye zingine, kisha Mess Makers wakaingia kwa pamoja ndani ya gari hilo, na dereva hakuwa mwingine ila LaKeisha. Akalitoa gari hapo kwa kasi huku ikipiga king'ora chake, naye akaanza kuelekea upande mwingine tofauti na barabara ambayo ingewapeleka hospitali na kisha kukizima king'ora hicho. Akawaendesha mpaka sehemu iliyokuwa na miti mingi sana, kisha wote wakashuka na kwenda mpaka kwenye gari lingine walilokuwa wameliacha hapo, naye Victor akashika usukani na kuwaingiza barabarani kuelekea upande mwingine tena ili watoke jijini hapo.

Safari hii ilikuwa na vifijo sana kwa vijana hawa kwa kuwa walifanikiwa kupata kilichowapeleka, nao wakamtaarifu Torres na Kendrick kuwa "mission" ilikamilika. Wakawapongeza na kuwaambia wawahi ili kuweza kupiga hatua ya pili ya mpango wao upesi sana.



★★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★★

WHATSAPP +255 787 604 893
 
FOR YOU

Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Uhalifu, Mauaji, Visasi, Vita, Mambo yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA AROBAINI NA SITA

★★★★★★★★★★★★★★★★★★


Baada ya kuwa wamefika kule mafichoni kwao, Lexi akampatia Torres "data" zote alizoiba ndani ya chumba kile kule benki kuu, naye Torres akazibusu kwa furaha kwa sababu ushindi wao ungefanikishwa na vitu hivyo. Kwa hiyo sehemu ya pili ya mpango wao ukaanza bila kuchelewa.

Kwa kutumia mifumo yake ya kompyuta iliyofichwa vyema, Torres akampigia simu Raisi Paul Mdeme na kumwambia kwamba walikuwa wameiba taarifa zao muhimu sana siku hiyo. Kila jambo ambalo lingefichua maovu yake yote lilikuwa mikononi mwake, na alitaka kitu kimoja ili asizisambaze taarifa hizo hadharani. Mdeme akamuuliza yeye ni nani na alifikiri anataka kumfanyia mchezo gani, naye Torres akamwambia angemthibitishia kwamba kila kitu alichomwambia ni kweli na siyo mchezo. Akamwambia aangalie kwenye simu yake, kwamba kuna jambo alikuwa amemtumia, na baada ya Mdeme kuangalia, akakuta baadhi ya picha na video chache ambazo alijua vyema kwamba Gavana Laurent alitakiwa kuwa amezificha. Alipojaribu kupiga simu kwa Torres, hakumpata, lakini simu yake ikaita, ikiwa ni namba ngeni tena, naye akapokea na kukuta ni Torres.

Mdeme akamuuliza kwa mara nyingine tena yeye alikuwa ni nani na alitaka nini, ndipo Torres akamwambia kwamba alichotaka ilikuwa ni kiasi cha trilioni 20 za pesa kutoka kwenye benki hiyo, zote zikiwa za karatasi (in cash). Mdeme alishangazwa na jambo hilo na kuuliza ikiwa mtu huyu alikuwa amechanganyikiwa kufikiri angekubali kufanya kitu kama hicho, lakini Torres akamwambia ana SIKU MBILI tu za kufanya hivyo, la sivyo angeziachia taarifa zile hadharani.

Torres akampa Mdeme maelekezo hususa kwa kumwambia aanze kazi haraka kwa kuhakikisha hakuna vyombo vya habari vinapita pale na ahakikishe anaweka ulinzi wa hali ya juu kupazunguka ili taarifa yoyote ya kinachoendelea isitoke nje, na ili watu wake Mdeme wafanye kazi ya kuzikusanya pesa hizo na kuziweka ndani ya magari yenye makontena makubwa, halafu baada ya hapo angemjulisha cha kufanya. Torres akakata simu hiyo baada ya kumwambia Mdeme aharakishe kufanya mambo hayo kwa kuwa aliona kila kitu.



Raisi Paul Mdeme alichanganyikiwa sana. Hapo tayari kulikuwa na taharuki nzito baada ya kupokea taarifa kwamba majengo ya benki yamelipuliwa kwa mabomu, halafu sasa tena akapokea ujumbe huo kutoka kwa watu hao asiowafahamu kabisa. Lakini kwa kuzingatia kile alichokuwa ameonyeshwa kwenye simu yake, alijua alitakiwa kuwahi kufanya jambo fulani ili taarifa hizo kweli zisitoke, hivyo akamtafuta Jenerali Jacob na Luteni Jenerali Weisiko na kuwapa maagizo ya kuweka ulinzi mkali sana kwenye eneo lile la benki kuu na kuwaondoa watu wengine waliokuwa wameanza kwenda huko. Kisha akawaambia wangepaswa kukutana naye haraka sana ili wazungumze kuhusiana na jambo muhimu.

Jenerali Jacob alitii na kufuata maagizo aliyopewa, na upesi eneo lile la benki kuu liliwekewa ulinzi wa hali ya juu kutoka kwa wanaume maalumu wa kikosi cha Jeshi la Nchi. Yaani hakukuwa na ruhusa kwa yeyote kuingia hapo isipokuwa wale tu ambao wangeruhusiwa na Jenerali, hivyo hata maaskari wa Jeshi la Polisi waliagizwa kukaa mbali. Jenerali Jacob, Makamu Eliya, Waziri Mkuu Yustus na Gavana Laurent Gimbi walikutana na Mdeme haraka sana baada ya mwito wake, naye akawaeleza hali iliyokuwa imewakumba. Luteni Jenerali Weisiko alikuwa kule kwenye majengo ya benki, na kwa wakati huu Salim Khan alikuwa nje ya nchi.

Wote walishangaa sana, hasa Gavana Laurent, ambaye ndiye aliyekuwa mtunzaji wa siri hizo. Akasema haingewezekana kuingia kwenye chumba kile alichoficha taarifa zile kwa kuwa ulinzi ulikuwa wa kitaalamu, na hata kama ni mabomu ndiyo yalilipua yasingeweza kuvunja chuma ngumu ya chumba kile. Jenerali Jacob akawaambia kwamba Weisiko aliangalia kila kitu huko kwa umakini, lakini hakupata kitu chochote chenye kusaidia kuwaonyesha wezi wao, kwamba watu hao walioiba walitumia umakini wa hali ya juu, na kitu kilichopatikana ilikuwa ni sticker ndogo tu yenye maneno "Mess Makers." Kwa hiyo Mdeme akawaambia wenzake wampe ushauri achukue hatua gani, kwa sababu hata alipojaribu kufatilia chanzo cha simu iliyompigia, hakuweza kukipata, hivyo isingekuwa rahisi kujua maadui hawa wako wapi.

Jenerali Jacob akashauri kwamba, wacheze mchezo huu jinsi watu hao walivyotaka uchezwe, halafu wangetumia njia za kitaalamu zaidi ili kuweza kuwakamata. Alikuwa anajiamini kwamba wangeweza kuwashika watu hao kwa sababu trilioni ishirini zisingekuwa rahisi kuhamishika nje ya nchi, ikiwa lengo la wezi hao lingekuwa ni kukimbia baada ya kuzipokea, hivyo akasema wangetumia kila njia kuziba mipaka, kuweka mitego kwenye kila mfumo wa akaunti za benki endapo tu tuseme watu hao wangefanikiwa kuzipata na kujaribu kuziweka kwenye akaunti zao kwa njia fulani, na kuhakikisha kila aina ya mifumo ya kiteknolojia nchini inachunguzwa kupitia rada. Wengine wakakubaliana na mawazo hayo, ikionekana kama kweli wasingeweza kushindwa, bila kutambua kwamba walikuwa wanashughulika na watu walioelewa yale waliyoyafanya.

Baada ya upande wa Mdeme kuwa umejipanga vyema, walituma agizo sasa kule benki ili zile pesa zianze kuhamishwa na kuwekwa ndani ya magari, huku wakisubiri mbaya wao awatafute. Ilikuwa ngumu kwao kumpata Torres kwa sababu alificha vyanzo vyake kwa ufundi wa hali ya juu kupita hata ule ulio bora zaidi wa nchi hii, hivyo hawakuwa na jinsi ila kusubiri.

Salim Khan, akiwa nje ya nchi, alitaarifiwa kuhusu janga hili lililokumba kundi lao, naye akasema angewahi kufika nchini upesi sana. Gavana Laurent alikuwa ameshauri wasiweke pesa hizo zote ndani ya magari yale, kwamba waweke kidogo tu ili kuwadanganya watu hao, lakini Mdeme akaweka wazi kwamba hawa watu bila shaka wangekuwa na njia ya kujua ikiwa pesa zote zimewekwa kikamili, hivyo walipaswa tu kufuata walichosema kwa sababu aliona hata hivyo hawangefika mbali na haya yote. Wangewakamata tu, kwa hiyo akamsihi Gavana aache kuwa na wasiwasi.


★★


Baada ya siku hizo mbili kupita, yaani ikiwa ni saa 6 usiku ya siku mpya ya tatu, Mdeme akatafutwa na Torres. Tayari simu ya Mdeme ilikuwa imeunganishwa kwenye mifumo ambayo ingewaruhusu watu wake kuona ni wapi aliyepiga alikuwa, lakini hata baada ya kupokea bado hawakuweza kutambua kwa urahisi. Maeneo ya aliyepiga yalionyesha kuwa Uholanzi, mara Canada, mara Eldoret, yaani sehemu nyingi zilizowachanganya wataalamu hawa na kushindwa kujua chanzo kipi kilikuwa kweli. Torres akaanza kutoa maelekezo. Sauti aliyotumia ilikuwa imeundwa na kompyuta, kwa hiyo wataalamu upande wa Mdeme walipojaribu kutafuta ufanani wa sauti yake na ya mtu halisi, hawakupata lolote. Hao jamaa walijua walichokuwa wanafanya, na huo ulikuwa mwanzo tu.

Torres akamwambia Mdeme kwamba alijua magari yale yalikuwa yamekamilisha kuwekewa trilioni 20, na kwa kejeli akampongeza kwa kazi nzuri. Akamwambia sasa kwamba alitakiwa kutoa agizo kwa madereva wawili, waanze kuyaendesha magari hayo kutoka eneo la benki na kuelekea eneo lingine, na hakutaka wafatiliwe, wala barabara zozote kuwekewa vizuizi. Akamwambia ikiwa angetambua wamewafatilia, basi angeachia video kumi mitandaoni. Mdeme akamwambia haingekuwa na shida kabisa, naye akauliza baada ya kufanya hivyo ingekuwaje sasa kwa sababu alitakiwa kuzipata taarifa zile na uhakikisho kwamba hawangeziachia mitandaoni, naye Torres akamwambia wakishazipata tu pesa, angemwambia la kufanya.

Mdeme alikuwa pamoja na Jenerali Jacob wakati Torres anaongea naye, na baada ya kukata simu, Jacob akatuma maagizo kwa Luteni Jenerali Weisiko kuwa huko waliko wajiweke tayari. Walikuwa wameweka mpango wa kuyafatilia magari hayo bila kuyafatilia moja kwa moja, yaani kwa kuweka vifaa vya ufatiliaji ndani yake kwa umakini, ili kuona kule ambako yangeishia. Walitaka kuwafanya wabaya wao wafikiri kwamba wamewaachia, halafu baadae wakishatambua magari yalikokwenda basi wawakamate, maana walijua haingekuwa rahisi kuzihamisha pesa hizo upesi sana. Kwa hiyo Weisiko alikuwa pamoja na kikosi chake makini sana chenye watu waliosambaa maeneo mbalimbali wakitazama mwelekeo wa magari hayo ili yakitulia tu sehemu moja, waanze kuyafata kimya kimya sana. Hiyo ndiyo ikaonekana kuwa njia nzuri sana ya kutatua tatizo lao bila kuharibu mambo.

Magari yale yakaanza mwendo kutokea kwenye majengo hayo ya benki kuu usiku huo. Yalikuwa mawili, kila moja likibeba trilioni 10 kwenye makontena yake. Madereva wawili walioyaongoza walikuwa ni wanajeshi pia, lakini walitakiwa kujifanya kama madereva wa kawaida tu. Torres alikuwa amemwambia Raisi Paul Mdeme kwamba madereva hao wangepaswa kuwa na simu ili aweze kuwapa maelekezo ya njia za kupita, na ndicho walichokuwa wakifanya. Mdeme na wenzake walikuwa bado wakishangazwa na ni jinsi gani mtu huyo aliweza kuyaendesha mambo na kuwapa maelekezo bila wao kuweza kutambua alikuwa wapi. Lakini kadiri magari hayo yalivyozidi kutembea, ndivyo Weisiko na watu wake walivyozidi kuona yalikokuwa, na kujulishana kisiri ili kuyasogelea taratibu.

Torres akiwa anawaongoza madereva wale wawili kuelekea upande fulani, wakafika sehemu pana zaidi lakini yenye misitu pembezoni, na hapo wakatokea watu wachache mbele ya barabara wakiwa wamevaa nguo nyeusi huku wakiwaelekezea bastola madereva hao kuwa wasimamishe magari haraka. Dereva mmoja akamjulisha Torres kilichokuwa kinaendelea, naye Torres akasema wasimame. Baada ya kuyasimamisha magari hapo kwa ughafla, timu ya Luteni Jenerali Weisiko iliona jambo hilo kwenye mitambo yao, nao wakaanza kutumiana maagizo ya kuanza kusogea mpaka eneo la huko wakifikiri hapo ndipo maadui wao walipodhamiria kusimama kabisa.

Waliokuwa wamefika hapo ilikuwa ni Lexi, LaKeisha, Oscar na Mensah, nao wakawaamuru madereva wale washuke upesi. Waliposhuka huku wakiwa wamenyanyua mikono yao juu, Mensah na LaKeisha wakawaamuru walale chini na kuweka mikono yao vichwani, nao wakatii. Madereva hawa wakiwa ni wanajeshi walijiamini sana kwa kuhisi wabaya wao hawangefanikiwa, wakidhani kwamba walikuwa wanapanga kuanza kuzihamisha pesa au kuondoka na magari hayo yaliyokuwa yakifatiliwa. Lakini huo haukuwa mpango wa Mess Makers.

Oscar na Lexi waliyafata magari yale mawili upesi na kuingia sehemu za mbele, kisha wote wakatoa vifaa vidogo vyenye kufanana na kifaa cha kuchomekea USB flash, nao wakaviweka kwenye sehemu inayotoa nguvu ya ziada ya umeme wa gari (Auxiliary Power Outlet), kisha wakachomeka vifaa fulani vidogo vya kiteknolojia ambavyo vilikuwa na kusudi la kuzuia mawimbi (signal) kwenye vifaa vya ufatiliaji vilivyokuwa vimewekwa kwenye magari hayo (GPS blockers). Walijua isingekuwa rahisi na ingekuwa kupoteza muda kuanza kuvitafuta vifaa hivyo vya ufatiliaji, kwa hiyo walikuwa wameamua kuikorofisha mitambo kabisa. Wakazima na kuwasha magari tena, na hapo kifaa chao kikawa kimevuruga mambo tayari. Hawa watu walijua!

Weisiko na wenzake waliokuwa wakifanya unyatiaji walishangaa tu mitambo yao inavurugika na kupoteza eneo ambalo magari yale yalikuwa, maana alama za yalikokuwa zilifutika. Wakajiuliza shida ingekuwa ni nini maana walivificha vifaa vile vya ufatiliaji kwa ndani sana, naye Weisiko akatoa agizo kwa wale waliokuwa wamesogea karibu na eneo hilo la mwisho magari hayo yalipokuwa wawahi kuona kama bado yalikuwepo au la; kwa maana kuanzia hapo hawakuwa na njia nyingine rahisi ya kujua.

Baada ya Lexi na Oscar kumaliza kukorofisha mitambo, wakashuka, naye Oscar akaanza kutoa mabomu mawili makubwa sana kutoka kwenye begi lake dogo na kuanza kuwafunga wanajeshi wale waliolala chini. Waliogopa kwa kiasi kikubwa, lakini hawakuwa na ujanja ila kutulia tu kwa sababu Mensah na Lakeisha walikuwa wamewaelekezea miguu ya kuku kwa umakini. Mmoja wao akauliza kwa nini walikuwa wanawafunga kwa mabomu, naye Lexi akawafata na kuwafunga wote midomo kwa gundi ya karatasi. Yaani walikuwa hapo kwa ajili ya kazi na siyo kuongea.

Wanajeshi hao wawili wakatazama upande mwingine wa barabara na kuona magari mawili makubwa yakija usawa huo. Iliwashangaza kidogo kwa sababu magari hayo yalifanana kabisa na haya yaliyokuwa yamebeba pesa, nao wakanyanyuliwa na kuanza kuongozwa kuyaelekea. Kwenye magari hayo walishuka wengine wawili waliokuwa wamevalia kama wakina Lexi, ikiwa ni Victor na Kevin, ambao ndiyo waliyaendesha.

Wanajeshi wale wakapelekwa kila mmoja kwenye gari mojawapo, naye Oscar akafanya kama kuchomeka waya mmoja uliotokea kwenye mabomu yaliyowafunga wanaume hao na kuuungsnisha na mfumo wa magari hayo, kisha akawataarifu wote kwamba alikuwa ameyaunganisha mabomu hayo na gari, hivyo likiwashwa tu halingepaswa kuzimwa kwa kuwa mabomu yangelipuka. Akaweka wazi kwamba pindi ambapo wangeanza kuyaendesha magari hayo, hawakutakiwa kupunguza mwendo wala kuongeza zaidi ya kikomo ambacho angekuwa amewawekea, la sivyo mabomu yangelipuka. Ikiwa wangejaribu kujitupa nje kupitia mlango na nyaya ikatike, yangelipuka. Kwa hiyo wangepaswa kuendelea tu kuyaendesha magari hayo kuelekea upande mmoja.

Wanajeshi hao wawili walikuwa aina ya watu ambao walikuwa tayari kufa kwa ajili nchi yao, lakini ikiwa wangeamua kufa tu wakati huu isingekuwa na faida yoyote, kwa sababu sasa walikuwa wameuelewa mpango wa hawa jamaa. Wakati Oscar alipokuwa akifanya hayo yote, Lexi alikuwa ameunganisha vifaa vidogo vya ufatiliaji kwenye zile simu ambazo wanajeshi hao walikuwa wakisikiliza maelekezo ya Torres wakati wakija huku, halafu akaziweka ndani ya haya magari ambayo Victor na Kevin walileta. Torres akaunganisha mitambo yake na kuipeleka moja kwa moja kwenye mifumo ya timu ya Weisiko ili waone kwamba signal ya vifaa "vyao" vya ufatiliaji imerudi, yaani wafikiri kwamba ilipotea na kurudi tena.

Kwa hiyo magari haya mengine ambayo sasa madereva hao wanajeshi walipewa kuyaendesha ndiyo yangeonekana kuwa yenye zile pesa, hivyo Mess Makers wakayatia mwendoni na kuwaacha madereva wale wawili wakiyaendesha kwa uangalifu kama walivyoelekezwa ili mabomu yasiwalipukie. Wangepaswa kuendelea kuyaendesha tu bila kusimama, la sivyo wangekufa vibaya kwa kulipuka. Kwa hiyo upande wa Weisiko ukaanza kuona kwamba "magari yenye pesa" yalianza tena kutembea, hivyo Weisiko akabadili maagizo na kuwaambia wale waliokuwa wanakaribia kwenye eneo hilo yaliposimama na kupoteza signal kwamba watulie na kufuata maagizo yake mapya kwa kuwa magari yaliendelea na safari kuelekea upande mwingine.

Bila kupoteza muda, Lexi na wenzake wakawa wameyachukua magari yale mawili yenye pesa na kuanza mwendo, wakitumia njia nyingine isiyo rasmi ili kuingia upande mwingine wa jiji, kisha wakaanza kuelekea mpaka kwenye eneo la bandarini. Kwa sababu hakukuwa na watu wengine waliojua kuhusu mchakato huu usiku huo, hakukuwa na vizuizi sehemu hiyo, kwa sababu tayari Kendrick alikuwa amefanya mipango kwa kutumia pesa zake ili kuwapokea vijana wake huko. Alikuwa ameagiza meli kubwa ya mizigo iwasubirie kwa kuwalipa wamiliki pesa nyingi kwa njia isiyo ya moja kwa moja ili aitumie kwa ajili ya mambo yake, bila wao kujua kuhusu ishu hii kubwa sana. Lakini upande wa bandari waliotumia haukuwa ule rasmi kabisa, bali kwenye sehemu iliyokuwa imejitenga kiasi na zile nyingine.

Ikiwa ni mida ya saa 8 usiku sasa, waliyafikisha magari yale mawili yenye pesa huko, kisha wakayapeleka mpaka usawa wa gari kubwa sana lenye mashine ya kunyanyulia makontena, na ndani yake alikuwepo Kendrick Jabari mwenyewe. Vijana wake wakavunja vyuma vilivyoyakaza makontena kwenye magari kwa kutumia mashine za kukata chuma, kisha Kendrick akaanza kuyanyanyua makontena yale na kuyapakiza kwenye meli ile, na baada ya kumaliza akatoka kwenye gari hilo na kwenda pamoja na vijana wake ndani ya meli; isipokuwa Victor na Kevin. Wawili hawa walibadili mavazi yao na kuvalia kwa njia ya kawaida tu, kisha wakaingia kwenye yale magari yaliyokuwa yamebeba pesa na kuyaondoa eneo hilo mpaka kufikia sehemu nyingine na kuyatelekeza, kisha wakaondoka kwa kutengana kama raia wema, huku Kendrick na wengine wakiwa wameshaondoka kwa meli yenye yale makontena yenye pesa. Ilikuwa ni jambo hatari sana kwao kufanya haya yote, na ingawa hawakuwa na uhakika kama kila jambo lingekwenda kwa usahihi, wakawa wamefanikiwa kwa asilimia kubwa.

Madereva wale wanajeshi waliendelea kuyaendesha magari yale mawili barabarani kwa umakini, na kwa kuwa ilikuwa ni usiku hakukuwa na magari mengi ya kupishana nayo njiani, lakini shida ingekuja endapo magari yangeanza kuwa mengi barabarani, na walijua hawangeweza kuyaendesha magari hayo milele. Kihalisi walikuwa wakiogopa sana kwa sababu ilionekana hakukuwa na njia ya kutoroka janga hilo, nao wakaendelea tu kuendesha taratibu kwa mwendo waliopewa, wakitumaini wenzao wangetambua kuna tatizo na kuwapatia msaada.

Mawazo yao yalikuwa sahihi, kwa sababu baada ya Luteni Jenerali Weisiko kumtaarifu Jenerali Jacob kuhusu hitilafu ile ndogo ya vifaa vyao vya ufatiliaji iliyotokea, upesi Jenerali Jacob alitambua kwamba walikuwa wamefanyiwa mchezo. Akauliza magari yale kwa sasa yalikuwa wapi, naye Weisiko akamjulisha kwamba aliona kupitia vifaa vyao kuwa yalikuwa barabarani bado yakitembea, taratibu, kwenye barabara kuu kama yanaelekea nje ya jiji. Jenerali Jacob akatoa maagizo kwa Weisiko kuwa wayavamie upesi magari hayo kwa sababu alihisi kuna kitu kilikuwa kimefanyika, ingawa Weisiko hakuona kama kuna tatizo bado. Lakini akatii na kuwaagiza watu wake waliokuwa wakitumia njia zingine kwenda na magari hayo sambamba, wayafate na kuyazingira upesi. Mdeme alikuwa anang'ata tu kucha zake kwa kuhisi wasiwasi mwingi sana, kwa sababu Torres hakuwa amemtafuta tena, na hata kama yeye angejaribu kumtafuta, asingempata.

Kikosi maalumu cha Weisiko kikawa kimeyafikia magari yale kujaribu kuyazuia kutembea, lakini wakashangaa kuona tu yakiwa bado yanaendeleza mwendo. Ikawabidi wayafyatue kwa risasi sehemu za matairi kutokea kwenye bunduki zilizozibwa sauti ili yasimame kwa lazima, na hasa kwa sababu yalikuwa yakitembea bila mwendokasi mwingi hakukuwa na hatari yoyote ya kuyaangusha. Yote mawili yakatoka nje ya barabara baada ya matairi kupigwa pancha namna hiyo, na wale madereva wanajeshi waliogopa sana kwa sababu walijua kusimama huko kulimaanisha vifo vyao. Lakini mpaka yanasimama kabisa, mabomu yale hayakulipuka. Wanaume hao wakaendelea tu kutulia ndani ya magari hayo, huku nyaya ile ikiwa imeunganika bado kutoka kwenye bomu mpaka kwenye gari, na midomo yao ikiwa imezungushiwa gundi kuziba sauti.

Wanaume wa kikosi cha Weisiko wakayasogelea magari hayo wakiwa wameyaelekezea bunduki, kisha baadhi wakafungua milango ya madereva na kuwaona wakiwa wamefungwa mabomu na kuzibwa midomo yao. Iliwachukua tahadhari ya hali ya juu kuanza kuwafungua midomo na kuhakikisha hawayatibui mabomu, nao wakauliza ni nini kilichokuwa kimetokea. Madereva wale wanajeshi wakawaelezea kila kitu, wakisema jinsi hao "wezi" walivyoyaiba magari yenye pesa na kuwawekea vifo vyao kifuani.

Weisiko alifika hapo upesi baada ya kuwa amepewa taarifa hizo, naye akiwa pamoja na wataalamu wa masuala ya mabomu, wakaanza kuyafungua kwa umakini ili yasilipuke, kwa sababu hawakuweza kuelewa kikamili lugha iliyoandikwa kwa namba-namba nyingi zilizoonekana kwenye mifumo yake. Wakamtolea mmoja lake, lakini walipokuwa wanamtolea mwingine wakakosea mahesabu na kusababisha lifyatuke, na wote wakajirusha chini wakihofia mlipuko ambao ungetokea. Lakini cha kushangaza ni kwamba halikulipuka, bali likatoa kama cheche tu kiasi na kunyanyua kiwaya fulani chenye kichwa cha katuni lenye kucheka likiwa na maneno "Mess Makers!"

Wote hapo walijiona kama wapumbavu sana, kwa sababu hayo hayakuwa mabomu halisi. Ni kwamba tu kuna ile hali ya hofu ambayo tayari kundi la Kendrick lilikuwa limeshaijengea nchi hii, nayo ilikuwepo mpaka miongoni mwa watu kama hawa waliokuwa wapiganaji wa nchi, kwa hiyo Oscar alikuwa ameitumia vizuri sana kwa kuwafikirisha kwamba yale yaliyotokea kwenye majengo ya benki kuu yangeweza kujitokeza tena, ndiyo maana ilikuwa rahisi kuamini kwamba mabomu yale yalikuwa halisi.

Weisiko alichoka. Alikuwa anaenda kuyaangalia mara kwa mara magari hayo kwenye makontena na kukuta yakiwa tupu kabisa. Akaanza kuwalaumu wanaume wale kwa kuuliza ni kwa nini hawakufanya lolote kutoa kama ishara kwa wenzao kwamba kulikuwa na tatizo, lakini wakasema kwamba wale wezi waliwazidi akili kwa njia ambayo hawakutarajia. Kama kawaida, mwanaume kama Weisiko sikuzote angetaka kuitoa hasira yake kwa kuua tu, hivyo akawaua wanaume hao wawili papo hapo. Hii bado ilikuwa ni saa 8 hiyo hiyo ambayo wenyewe wakiwa wanapoteza muda hapo, Kendrick na vijana wake ndiyo walikuwa wakifanikisha mpango wao wa kuyaondosha makontena yale nchi kavu.

Si taarifa hizo zikamfikia Jenerali Jacob! Alikasirika sana na kuuliza ni nini hasa ambacho Weisiko alikuwa anafanya mpaka akaruhusu hilo kutokea, naye Weisiko akaeleza kwamba kiukweli hata yeye alishangaa sana. Mdeme ndiye aliyehisi kama vile presha imepanda baada ya kuambiwa trilioni 20 zimekwenda hivyo. Ilikuwa ni usiku ambao uliwatia pigo kubwa sana wanaume hao, nao wakashindwa kujua la kufanya. Lakini Jenerali Jacob na Weisiko wakaanza kutoa maagizo haraka ya kufunga mipaka yote ya jiji kuzuia gari lolote lisipite, na wanajeshi wote waingie kwenye msako wa kutafuta magari yoyote makubwa, na kabla ya asubuhi kufika wawe wameyapata. Wakaja kuyapata magari yale ambayo walitumia kuhamisha zile pesa na kuwapelekea Mess Makers wao wenyewe, yakiwa bila makontena na yakiwa yametelekezwa. Ndiyo uchizi wa viongozi hawa ulianzia hapo.

Wakiwa bado wamechanganyikiwa, Mdeme akapigiwa na Torres. Raisi huyu aliuliza kwa hasira ni kwa nini mbaya wake alikuwa amekwenda kinyume na makubaliano, lakini Torres akaweka wazi hakukuwa na makubaliano yoyote kutokea mwanzo. Akamwambia kwamba pesa kazichukua, na bado ushahidi wa mambo maovu ya Mdeme na wenzake anao, lakini hangeuachia hadharani. Akasema ikiwa Mdeme alitaka kuanza kumtafuta, basi afanye hivyo, kwamba amempa ruhusa kabisa. Kisha Torres akakata simu hiyo, na kuanzia hapo hakumtafuta tena Mdeme.

Jenerali Jacob alianza kufanya mipango mingi ili kuhakikisha kwamba hakuna mtu yeyote tofauti na vikosi vyao ambaye angejua kuhusu jambo hilo, na njia ya kwanza ilitakiwa kuwa kuondoa ulinzi ule waliouweka kwenye majengo ya benki kuu na kuruhusu vyombo vya habari vifanye kazi zao kwa undani zaidi, halafu waanze msako wa hadharani wa wezi hao kupitia njia zilizoonekana kuwa rasmi zaidi (maaskari, Kanali Oswald, Luteni Michael, n.k). Pia, wangetakiwa kuhakikisha kwamba taarifa za kile kilichotokea hasa siku ile mabomu yalipolipuka zinafichwa, kutoka kwa watu ambao walibaki kule ndani, hasa wale majeruhi. Wakaamua kuzificha Ikulu taarifa kuhusu majeruhi hao na kubuni za uongo, kisha wakafanya mpango maalum wakitumia watu wao "kuwaziba" mdomo majeruhi wale kuhusu yale yaliyotokea hasa (kwa kuwalipa pesa au kutoa vitisho).

Haikuwachukua muda mrefu kwa Jenerali Jacob na wenzake kugundua kwamba wawili kati ya wezi wale walijifanya kama Eunice Shirima na Nathan Masunga ili kuiba taarifa zao, kwa hiyo ikabidi wawili hawa watafutwe upesi ili wajieleze, kwa sababu ilionekana labda walihusika kwa njia fulani. Lakini walipokosa hatia kwao, wakawapa maonyo ya kutoondoka makwao mpaka waambiwe, na kutosema lolote kwa yeyote kuhusu walichojua, na kwa woga Nathan Masunga alikubali, lakini Eunice Shirima ndiye aliyekuwa na ujasiri wa kuuliza ni kwa nini watu hawa walikuwa wanafanya mambo haya yote. Kwa kutokupewa maelezo yenye kujitosheleza, Eunice alikataa kuafikiana na agizo lao la kukaa ndani tu bila sababu yoyote, kwa hiyo watu wa Weisiko wakamuua mwanamke huyo. Halafu wakaja kutoa taarifa za uongo kwamba alikuwa mmoja wa majeruhi, na alifia hospitalini siku nne baada ya tukio la wizi, ambalo kufikia wakati huo lilikuwa limezua gumzo kubwa sana.

Hivyo ndivyo mambo yalivyokwenda, njia ya wizi wa matrilioni ikiwa imepitishwa kwa msaada wa mkono wa Raisi Paul Mdeme mwenyewe. Hiyo ndiyo iliyokuwa sababu iliyofanya Salim Khan amlaumu sana Mdeme na wengine kwa kufanya yale ambayo walielekezwa na Mess Makers, akiona lilikuwa ni jambo la kipuuzi kwao kudhani wangeweza kuwazunguka watu hao waliowaona kuwa wadogo sana. Lakini baada ya hayo mambo yote sasa wakawa wamegundua kwamba ni wao ndiyo waliofanywa kuwa wadogo....


★★★★


Torres sasa akawa amemaliza kumsimulia ACP Nora kuhusu njia walizotumia kuiba pesa zile, hasa akiwa amezungumzia mambo yaliyofanyika kwa upande wao. Nora alishangazwa sana na mambo mengi aliyoambiwa. Ilikuwa ngumu kuamini kwamba kundi hili la watu wachache lingeweza kufanya mambo ambayo yaliizidi mifumo mikubwa ya ujuzi ya nchi kwa ujumla (intelligence), tena hadi na baba yake kabisa. Lakini pia ilikuwa ni ukweli wa kwamba tokea mwanzo alikuwa akidhani anatumikia upande ulio sahihi, ila sasa akatambua hakujua lolote kabisa.

Wengine wakawa wanamwangalia kwa umakini alipokuwa akiendelea kutafakari mambo mengi baada ya kupewa ufunuo huo tata sana. Akamwangalia Lexi, ambaye alikuwa anamtazama kwa njia iliyoonyesha alisubiri kusikia maoni yake.

"Vipi askari? Umeimeza hiyo fresh?" LaKeisha akamuuliza Nora.

"Nafikiri anawaza atoke hapa jinsi gani ili awakimbizie hizo taarifa watu wake," Kevin akasema.

"Hapana, hawezi. Tulifanya makubaliano mazuri jana," Kendrick akaongea.

"Nora... unaonaje kuhusu hayo yote?" Torres akamuuliza.

"Nimeshangaa... sana. Ni nani aliyefanya mipango hiyo yote... ni wewe?" Nora akamuuliza Torres.

"Ni sisi wote," Torres akajibu.

"Mlikaa kuangalia series ya Money Heist ndiyo mkaweza kufanya hayo yote?" Nora akauliza tena.

Wote wakacheka kidogo, isipokuwa Kevin.

"Hapana. Siyo kitu tulichopanga kwa miaka zaidi ya 20 lakini ilichukua miaka kadhaa kupangilia na kuhakikisha kila jambo lingekwenda according to plan. Kiukweli, nafikiri ni Mungu tu pia alikuwa ametuwekea mkono wake," Torres akasema.

"Kwa hiyo baada ya kutoka na meli mlipeleka wapi makontena hayo?" Nora akauliza.

"Mwanzoni mwa kisiwa cha Pemba, kuna sehemu ambayo Lexi alikuwa ameweka kama makazi ya muda mfupi alipotoka Ghana na kuja huku, ikionekana kama garage kubwa ya biashara ya magari. Hapo ndiyo tuliyapeleka, tukazihamishia pesa kwenye kontena lingine kubwa, na uzuri ni kwamba walikuwa wameziweka kwa mpangilio mzuri ndani ya mifuko mikubwa... kwa hiyo wenye ile meli walipokuja kuichukua sisi tayari tulikuwa tumesambaa," akasema Torres.

"Ina maana mlikuwa mnazunguka na trilioni 20 huko kisiwani?" Nora akauliza.

"Hapana, boss tayari alikuwa ameweka gari kubwa lenye kontena na kufanya mipango kwa meli nyingine ili tulipeleke huko. Hii ilikuwa ya kibinafsi, na tungeitoa huko na kuipeleka kupitia fukwe za mwisho za mkoa wa Tanga, kisha kutokea hapo ningeanza kuwaongoza wenzangu kupitia njia ambazo zingewaleta huku bila kukamatwa. Tulitumia gari lingine tena lenye kontena. Ahah... nakumbuka siku hizo hatukulala kwa siku nne mfululizo," Torres akasema.

"Sisi wengine, Victor na Kevin wali-enjoy vitanda vyao," akasema LaKeisha.

Victor akatabasamu.

"Kwa hiyo kumbe mlizileta pesa hapa?" Nora akauliza.

"Ndiyo," Torres akajibu.

"Vipi kuhusu yule mwanamke... Eunice Shirima?" Nora akauliza.

"Amefanyaje?" akauliza LaKeisha.

"Najua unahisi labda tulifanya jambo fulani kwa mwanamke huyo, lakini haikuwa sisi. Ni Weisiko bila shaka. Walipodanganya kuhusu waliojeruhiwa na kutupa sisi lawama sana, inaonekana Eunice hakutaka kucheza muziki waliokuwa wamemwekea, kwa hiyo hata sisi tulikuja kutambua baadae kwamba walimuua," Torres akasema.

Nora akamwangalia Lexi.

"Unajua naona kama vile haya maongezi hayafiki popote walahi! Huyu atakaa hapa kuuliza chochote anachojisikia mpaka kesho asubuhi. Kwa nini tunajisumbua sana kuthibitisha kwake kwamba sisi ndo' tuko fair?" Kevin akauliza.

"Ulipojiunga na sisi Kevin tulikupitisha kwenye darasa letu karibia mwaka mzima. Unachoogopa ni nini kuhusu hili darasa fupi tunalompa Nora?" Victor akauliza.

"Ni tofauti. Huyu ni askari, na amesha...."

"Stop whining, you idiot!" Lexi akamkatisha Kevin kiukali.

Wengine wakawa wanamwangalia Kevin huku wanatikisa vichwa kwa kusikitika.

"Nora samahani. Kevin yuko..."

"Usijali naelewa," Nora akamwambia Lexi huku akimwangalia Kevin.

Kevin akacheka kwa kuguna na kukunjia mikono yake kifuani.

"Nitakuonyesha kila file kati ya yote tuliyochukua ili kukuthibitishia zaidi. Lakini kwa sasa... ACP Nora... tunahitaji kujua ikiwa uko tayari kufanya kazi na sisi, ili tuweze kuukamilisha mpango wetu," akasema Torres.

"Mpango gani?" Nora akauliza.

"Mpango uliofanya tukachukua hizo trilioni 20. Hatukuzichukua ili kula bata, tulizichukua ili kuwarudishia wale WOTE waliodhulumiwa ndani ya hiki kipindi cha miaka nane iliyopita," Torres akamwambia.

Nora akashangaa na kuuliza, "Wote?"

"Ndiyo... wote," Kendrick akajibu.

Nora akatikisa kichwa kama vile mtu ambaye haamini. "Kumbe hilo ndiyo lililokuwa lengo lenu?" akauliza huku anatazama chini.

"Yeah, we steal from the rich and give to the needy... sisi ndiyo ma-Robin Hood," LaKeisha akasema.

"Lakini kwa nini trilioni 20? Hicho ndiyo kiasi cha pesa mnachosema watu wamedhulumiwa kwa hiki kipindi cha utawala wa Mdeme?" Nora akauliza.

"Kwa makadirio ya haraka ingekuwa kwenye trillion 18 and something, lakini sisi tukaamua kubeba 20... 2 kwa kwa ajili ya usumbufu waliotupatia," Lexi akasema.

Wengine wakacheka kidogo. Nora akatabasamu pia.

"Ahahah... kwa hiyo... unasemaje?" Torres akamuuliza Nora.

Nora akamtazama Kendrick, ambaye alikuwa anamwangalia kwa umakini sana. Kisha akamwangalia na Lexi, aliyekuwa anamtazama kwa umakini pia.

Nora akaanza kusema, "Baada ya mambo yote uliyonielezea... siwezi kuuliza ni njia gani mtatumia kuwarudishia watu hao pesa zao kwa sababu najua bila shaka hiyo njia mnayo tayari..."

Wengine wakacheka kidogo.

"Kuwa pamoja nanyi itakuwa experience mpya kwangu, na ingawa najua hii ni hatari lakini najua pia itaburudisha. Kwa hiyo jibu ni ndiyo... nitafanya kazi pamoja nanyi," Nora akasema.

"Wonderful!" Torres akafurahi.

"Haukuwa na njia ya kukataa hata hivyo maana unajua tungeku...kiiih!" Victor akatania huku akitoa ishara ya kuikata shingo.

Nora akacheka kidogo, kisha akamtazama Kendrick. Mwanaume huyo alikuwa anamwangalia kwa umakini uliopitiliza, naye Nora akaangalia pembeni.

"Okay, kuanzia sasa wewe hautakuwa ACP Nora tena hapa. Wewe ni Nora, Nora wa Mess Makers," Torres akasema na kutoa ishara kama anamwapisha Nora.

Nora akatabasamu na kuuliza, "Kwa hiyo... nini kinafuata sasa?"

Wengine wakamwangalia Kendrick.

"Kama Torres alivyokwambia, kitakachofuata ni kuukamilisha mpango huo... halafu tutamwangusha Mdeme, Weisiko... na Jacob," Kendrick akaongea kwa uzito.

Kevin akatabasamu kwa kejeli.

Nora akaangalia chini tu akiwaza mambo mengi. Hakuelewa kikamili maana ya kuwaangusha watu hao, lakini kama hiyo ilimaanisha kuwaua, basi kwa kadiri kubwa hiyo ingekuwa hali tata. Ingawa alifahamu kwamba Jenerali Jacob alihusika na mambo mengi mabaya, bado alikuwa ni baba yake, na hata kama alimchukia bado lisingekuwa jambo zuri kwake ikiwa angekufa.

Lakini tayari alikuwa ameshajiweka ndani ya makubaliano mapya na kundi hili, kwa hiyo kuanzia hapo angetakiwa kushirikiana nao katika mipango yao; haijalishi nini kingetokea mbele ya safari.



★★★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★★★

WHATSAPP +255 787 604 893
 
Back
Top Bottom