SEHEMU YA THELATHINI NA TANO
Nilitoka pale taratibu huku nikigundua mtaalamu hana tamaa ya pesa nyingi kama ambavyo nilifikiri.uoga wa kumuona yule mtu bado nilikuwa nao nikawa kama nimechanganyikiwa tu nikapandisha vioo kwa uoga ,kwakuwa ilikuwa ni mchana nikaamua kukanyaga mguu kama kawaida huku nikishukuru sijachanjwa chale maana ni fedheha halafu pia mke wangu huwa hapendi nijihusishe na mambo ya shirki.
Saa kumi jioni nilikuwa kwenye lami huku nikiongeza mwendo zaidi ,ni foleni tu ya jiji ilifanya nifike nyumbani saa nne za usiku.
Nilifunguliwa geti huku kila mmoja akinishangaa ,mke wangu akaja kwangu mbiombio ,
Mume wangu karibu ,kwani ulikuwa wapi jana uliaga unaondoka lakini hukuniambia unalala,.asubuhi nimekutafuta kwenye simu zote hukupatikana,
Kwakuwa nilijua unawindwa na maaskari nimeenda hadi centra nikaambiwa kwenye Cell hakuna mahabusu mwenye jina lako,
Hebu kwanza tuingie ndani maana nina mengi ya kusema.
Tuliongea mengi na mke wangu huku akiniambia kuna muda alipokea vitisho kwenye simu na familia ya Jastini,wakidai kuwa nimemsababishia ndugu yao matatizo na watahakikisha na mimi naangukia sehemu mbaya malipo ni hapa hapa Duniani.
Mke wangu mimi nitalindwa na Mungu na pia mimi si tapeli kama watu wengi walivyosema.
Najua ni vigumu kunielewa ila tambua kuwa mimi ni Daniel nitabaki kuwa Daniel,naijua njaa,nazijua shida najua maisha magumu, lakini sijawahi kuwaza wala kutamani kudhulumu mtu, na hii ishu ya madini ni kweli niliambiwa na Jastini kuwa ninunue kwa bei fulani Kisha na Mimi nitauza kwa bei kadhaa lakini ukweli ni kwamba yale madini yalinitesa sana nikijua hela yangu nimedhulumiwa. Na hata kwenda kwa Jastini Kila saa ilikuwa ni kutaka kujua alipo kwani nilikuwa na vitu ambavyo soko lake silijui, namshukuru dada Vero alinipa mwanga nikaenda maeneo ya ushuani huko Kuna mtu huwa ananunua , nikafanikiwa kutua ule mzigo.nilimfafanulia mke wangu.
Sawa , vipi kuhusu wake za watu yaani habari zako zimetapakaa Kila kona nanyooshewa vidole Mimi, nadhalilika kuna watu wamefikia hatua ya kusema kwanini bado niko na wewe kifupi umenivua nguo.
Mke wangu,
Kwanza nikupe hongera kwa uvumilivu wako,lakini nikuhakikishie kuwa mimi najiheshimu na nakuheshimu wewe.
Unatambua fika kuwa sina maisha kivile lakini nina uwezo wa kumiliki mwanamke yeyote wa kawaida,
Hawa ambao kodi ni elfu thelathini kwa mwezi,wapo wengi mke wangu.
Ukilipa kodi miezi sita ukawa unampa hamsini kila weekend mbona atatamani umuoe,tena ni wasichana wazuri mke wangu lakini ni big no.
Watoto wetu wamekuwa wakubwa haipendezi kusikia habari za kijinga zinazonihusu mimi.nilimwambia mke wangu huku nikigundua anabadilika
Na kuonesha kunielewa .
Nje ya simulizi,
Ndugu msomaji,mimi
Jack Daniel ikitokea mke wangu Mungu amemchukua sidhani kama nitaoa mwanamke yeyote kwani sioni wa kufanana naye.(code)
Sasa endelea,
Tulilala Mida mibovu sana huku nikijiona mwepesi baada ya kuujua ukweli huku nikiwaza ,ni kweli afande Hussein alijua labda mimi nililala na mkewe,sasa kwanini aniroge.
Kwani yule Fatma huwa anampa nini tofauti na sisi ambacho kilimfanya afikirie kuniroga,
Yule mwanamke alivyo mzuri atakosaje kutongozwa , anataka kuniambia yule demu ambaye anafanya kazi mbali huko wakiwa hawaonani miezi kibao,huwa hagongwi?
Huyu pot,ataroga wangapi?
Nilijiuliza sana .huku usingizi ukikata ni kwamba pale kitandani nilijiegesha tu huku nikiwaza meengi mno.
Mume wangu,
Lala basi umeingia mida mibovu, kisha tumeongea weee , utasinzia kazini my hebu pumzika basi , nimejua ukweli wote kuwa wanakuonea tu muombe sana MUNGU.
Mwambie Yesu kuwa kwa kumtegemea yeye utayashinda majaribu .
upo wakati wako Mume wangu ukifika Kila kitu kitakaa sawa,MUNGU atakupigania ukiomba kwa Imani .
Kwenye biblia agano la kale kitabu Cha MHUBIRI sura ya tisa mstari wa kumi na moja inasema hivi,
Si wote washindao mbio, au vita na Mengine mengi yawapayo fahari au Chochote kile mume wangu,
Wamekunyanyasa, wamekufedhehesha , wamekufanya mtumwa ona Sasa hupati usingizi najua unawaza kukamatwa muda wowote. Mume wangu,
Wakati na bahati huwapata wote.
Bila kujali nani ni nani hayo wanayokusingizia upo muda, upo wakati ukifika yataisha.
Mhubiri anasema .
Maneno ya mke wangu yalinichoma huku nikiwa najua fika nimetoka kwa mganga nimejua mengi lakini nisingeweza kumwambia ningeharibu hali ya hewa kwani amenyooka mno kwenye kundi lao la wakalismatiki.
Asubuhi nilielekea kazini nikaendelea kutimiza majukumu yangu huku nikiletewa umbea fulani na madereva wa pale,
Bro Dani vipi umesikia chochote kuhusu sister Vero,aliongea yule suka.
Mimi sijui chochote kwanza siku kadhaa Mimi sikuwepo hivyo najua nimepitwa. Nilijibu.
Da Vero kaula , halafu kwanini hajakwambia hata kwenye simu watu. Wote tunajua namna mlivyo karibu , ni kwamba huyu kakatiwa ticket ya ndege anatakiwa aende sijui nchi gani Kisha kwa siku atakazokaa
Atalipwa Dola elfu kumi, Sasa niambie akichenji kwa pesa za madafu ana shilingi ngapi, ni sehemu ambayo hatamaliza wiki mbili anarudi akiwa mtamu.aliweka kituo yule jamaa .
Oyaa wewe hebu acha zako dollars elfu kumi unazijua wewe. Halafu acha umbeya wewe ni dereva mambo ya huku ndani yanakuhusu nini, kwahiyo unawaambia watu , Vero , Vero Vero kafanyaje eeenh acha umbea mtoto wa kiume. Niliongea kwa hasira
Dah samahani bro nisamehe mimi nilikwambia wewe tu lakini. Aliongea kwa upole , lakini sikumjibu nikaingia ndani huku taarifa ile ikiugusa moyo wangu wivu uliniingia nilitamani nijue kama ni kweli lakini namuanzaje Vero na Hana mazoea na Mimi nikaona kwakuwa taaluma yake ni komputa yangu siilewi lengo nijenge naye mazoea nikijua ataropoka tu
Alikuja huku akiwa mbaaali na Mimi .
Tatizo ni Nini Dani, aliuliza huku akivaa miwani yake akichezea kile kipanya huku nikimsoma usoni, Computer yako haina shida labda wewe ndiye mwenye shida siku nne haupo kazini tukajua labda anarefresh mind akija atakuwa sawa kumbe ........
Kwani una shida gani , kwanza wiki ijayo nasafiri sijui utamwambia nani , na yule Mzee ukimwambia habari zako za kipuuzi nadhani unamjua wote humu tunajua kutumia hivi vitu , Kuna mahali mtu akikwama unajua yupo sahihi , lakini Daniiiii unatia huruma sana.
Nimesikia kuwa wiki ijayo hautakuwepo au nimesikia vibaya, niliongea kinafiki huku nikijichekesha.
Enhee kwani vipi unataka kunipa nauli mbona nyie Kila siku mnaenda huku na huku mnatengeneza safari ili mpate hela mnatengeneza hata vyombo vizima kwani hatujui,lakini leo mishipa ya shingo imekusimama kusikia Vero anasafiri.aliongea kwa dharau
Siyo hivyo dada halafu imekuwaje mbona unanitenga? niliuliza
Achana na mimi bwana.
Aliondoka huku nikikosa nililokusudia
Huku nikiwaza doller elfu kumi zaidi ya milioni ishirini na kitu.kila kitu anagharamiwa ,duh ngoja mimi mara ya mwisho kwenda nje nililipwa 4500 dollers halafu huyu mwenye elimu ya kuungaunga,haaaa wewe ngoja nitampeleleza tu.sijui ni shetani gani alinipata kutamani bahati za wengine.
Kwa leo inatosha,tukutane muda mwingine.
Itaendelea.............