Simulizi: Harakati za maisha

SEHEMU YA THELATHINI NA TANO

Nilitoka pale taratibu huku nikigundua mtaalamu hana tamaa ya pesa nyingi kama ambavyo nilifikiri.uoga wa kumuona yule mtu bado nilikuwa nao nikawa kama nimechanganyikiwa tu nikapandisha vioo kwa uoga ,kwakuwa ilikuwa ni mchana nikaamua kukanyaga mguu kama kawaida huku nikishukuru sijachanjwa chale maana ni fedheha halafu pia mke wangu huwa hapendi nijihusishe na mambo ya shirki.

Saa kumi jioni nilikuwa kwenye lami huku nikiongeza mwendo zaidi ,ni foleni tu ya jiji ilifanya nifike nyumbani saa nne za usiku.

Nilifunguliwa geti huku kila mmoja akinishangaa ,mke wangu akaja kwangu mbiombio ,
Mume wangu karibu ,kwani ulikuwa wapi jana uliaga unaondoka lakini hukuniambia unalala,.asubuhi nimekutafuta kwenye simu zote hukupatikana,

Kwakuwa nilijua unawindwa na maaskari nimeenda hadi centra nikaambiwa kwenye Cell hakuna mahabusu mwenye jina lako,
Hebu kwanza tuingie ndani maana nina mengi ya kusema.

Tuliongea mengi na mke wangu huku akiniambia kuna muda alipokea vitisho kwenye simu na familia ya Jastini,wakidai kuwa nimemsababishia ndugu yao matatizo na watahakikisha na mimi naangukia sehemu mbaya malipo ni hapa hapa Duniani.

Mke wangu mimi nitalindwa na Mungu na pia mimi si tapeli kama watu wengi walivyosema.
Najua ni vigumu kunielewa ila tambua kuwa mimi ni Daniel nitabaki kuwa Daniel,naijua njaa,nazijua shida najua maisha magumu, lakini sijawahi kuwaza wala kutamani kudhulumu mtu, na hii ishu ya madini ni kweli niliambiwa na Jastini kuwa ninunue kwa bei fulani Kisha na Mimi nitauza kwa bei kadhaa lakini ukweli ni kwamba yale madini yalinitesa sana nikijua hela yangu nimedhulumiwa. Na hata kwenda kwa Jastini Kila saa ilikuwa ni kutaka kujua alipo kwani nilikuwa na vitu ambavyo soko lake silijui, namshukuru dada Vero alinipa mwanga nikaenda maeneo ya ushuani huko Kuna mtu huwa ananunua , nikafanikiwa kutua ule mzigo.nilimfafanulia mke wangu.

Sawa , vipi kuhusu wake za watu yaani habari zako zimetapakaa Kila kona nanyooshewa vidole Mimi, nadhalilika kuna watu wamefikia hatua ya kusema kwanini bado niko na wewe kifupi umenivua nguo.

Mke wangu,
Kwanza nikupe hongera kwa uvumilivu wako,lakini nikuhakikishie kuwa mimi najiheshimu na nakuheshimu wewe.
Unatambua fika kuwa sina maisha kivile lakini nina uwezo wa kumiliki mwanamke yeyote wa kawaida,
Hawa ambao kodi ni elfu thelathini kwa mwezi,wapo wengi mke wangu.

Ukilipa kodi miezi sita ukawa unampa hamsini kila weekend mbona atatamani umuoe,tena ni wasichana wazuri mke wangu lakini ni big no.
Watoto wetu wamekuwa wakubwa haipendezi kusikia habari za kijinga zinazonihusu mimi.nilimwambia mke wangu huku nikigundua anabadilika
Na kuonesha kunielewa .

Nje ya simulizi,
Ndugu msomaji,mimi Jack Daniel ikitokea mke wangu Mungu amemchukua sidhani kama nitaoa mwanamke yeyote kwani sioni wa kufanana naye.(code)

Sasa endelea,
Tulilala Mida mibovu sana huku nikijiona mwepesi baada ya kuujua ukweli huku nikiwaza ,ni kweli afande Hussein alijua labda mimi nililala na mkewe,sasa kwanini aniroge.

Kwani yule Fatma huwa anampa nini tofauti na sisi ambacho kilimfanya afikirie kuniroga,
Yule mwanamke alivyo mzuri atakosaje kutongozwa , anataka kuniambia yule demu ambaye anafanya kazi mbali huko wakiwa hawaonani miezi kibao,huwa hagongwi?
Huyu pot,ataroga wangapi?
Nilijiuliza sana .huku usingizi ukikata ni kwamba pale kitandani nilijiegesha tu huku nikiwaza meengi mno.

Mume wangu,
Lala basi umeingia mida mibovu, kisha tumeongea weee , utasinzia kazini my hebu pumzika basi , nimejua ukweli wote kuwa wanakuonea tu muombe sana MUNGU.
Mwambie Yesu kuwa kwa kumtegemea yeye utayashinda majaribu .
upo wakati wako Mume wangu ukifika Kila kitu kitakaa sawa,MUNGU atakupigania ukiomba kwa Imani .

Kwenye biblia agano la kale kitabu Cha MHUBIRI sura ya tisa mstari wa kumi na moja inasema hivi,

Si wote washindao mbio, au vita na Mengine mengi yawapayo fahari au Chochote kile mume wangu,
Wamekunyanyasa, wamekufedhehesha , wamekufanya mtumwa ona Sasa hupati usingizi najua unawaza kukamatwa muda wowote. Mume wangu,
Wakati na bahati huwapata wote.
Bila kujali nani ni nani hayo wanayokusingizia upo muda, upo wakati ukifika yataisha.
Mhubiri anasema .

Maneno ya mke wangu yalinichoma huku nikiwa najua fika nimetoka kwa mganga nimejua mengi lakini nisingeweza kumwambia ningeharibu hali ya hewa kwani amenyooka mno kwenye kundi lao la wakalismatiki.

Asubuhi nilielekea kazini nikaendelea kutimiza majukumu yangu huku nikiletewa umbea fulani na madereva wa pale,

Bro Dani vipi umesikia chochote kuhusu sister Vero,aliongea yule suka.

Mimi sijui chochote kwanza siku kadhaa Mimi sikuwepo hivyo najua nimepitwa. Nilijibu.

Da Vero kaula , halafu kwanini hajakwambia hata kwenye simu watu. Wote tunajua namna mlivyo karibu , ni kwamba huyu kakatiwa ticket ya ndege anatakiwa aende sijui nchi gani Kisha kwa siku atakazokaa
Atalipwa Dola elfu kumi, Sasa niambie akichenji kwa pesa za madafu ana shilingi ngapi, ni sehemu ambayo hatamaliza wiki mbili anarudi akiwa mtamu.aliweka kituo yule jamaa .

Oyaa wewe hebu acha zako dollars elfu kumi unazijua wewe. Halafu acha umbeya wewe ni dereva mambo ya huku ndani yanakuhusu nini, kwahiyo unawaambia watu , Vero , Vero Vero kafanyaje eeenh acha umbea mtoto wa kiume. Niliongea kwa hasira

Dah samahani bro nisamehe mimi nilikwambia wewe tu lakini. Aliongea kwa upole , lakini sikumjibu nikaingia ndani huku taarifa ile ikiugusa moyo wangu wivu uliniingia nilitamani nijue kama ni kweli lakini namuanzaje Vero na Hana mazoea na Mimi nikaona kwakuwa taaluma yake ni komputa yangu siilewi lengo nijenge naye mazoea nikijua ataropoka tu
Alikuja huku akiwa mbaaali na Mimi .

Tatizo ni Nini Dani, aliuliza huku akivaa miwani yake akichezea kile kipanya huku nikimsoma usoni, Computer yako haina shida labda wewe ndiye mwenye shida siku nne haupo kazini tukajua labda anarefresh mind akija atakuwa sawa kumbe ........

Kwani una shida gani , kwanza wiki ijayo nasafiri sijui utamwambia nani , na yule Mzee ukimwambia habari zako za kipuuzi nadhani unamjua wote humu tunajua kutumia hivi vitu , Kuna mahali mtu akikwama unajua yupo sahihi , lakini Daniiiii unatia huruma sana.

Nimesikia kuwa wiki ijayo hautakuwepo au nimesikia vibaya, niliongea kinafiki huku nikijichekesha.

Enhee kwani vipi unataka kunipa nauli mbona nyie Kila siku mnaenda huku na huku mnatengeneza safari ili mpate hela mnatengeneza hata vyombo vizima kwani hatujui,lakini leo mishipa ya shingo imekusimama kusikia Vero anasafiri.aliongea kwa dharau

Siyo hivyo dada halafu imekuwaje mbona unanitenga? niliuliza

Achana na mimi bwana.
Aliondoka huku nikikosa nililokusudia
Huku nikiwaza doller elfu kumi zaidi ya milioni ishirini na kitu.kila kitu anagharamiwa ,duh ngoja mimi mara ya mwisho kwenda nje nililipwa 4500 dollers halafu huyu mwenye elimu ya kuungaunga,haaaa wewe ngoja nitampeleleza tu.sijui ni shetani gani alinipata kutamani bahati za wengine.

Kwa leo inatosha,tukutane muda mwingine.

Itaendelea.............
 
Fafanua ulichoshtuka kwa faida ya wanajamvi.

Yote kwa yote stori italetwa kama ilivyo haitaongezwa jambo lolote zaidi ya kupunguza.
Ni kuhusu Mkuu Robot la Matope kukuombe uende Pm baada ya wewe kupakia sehemu iliyopita inayoelezea mganga wa kienyeji


Hivyo kukuita pm nia yake aombe connection ya mganga, kuhusu simulizi uko sawa kabisa Chief hakuna mahala nimetilia shaka[emoji120]
 
SEHEMU YA THELATHINI NA SITA

Zilipita takribani wiki tatu huku nikiendelea na majukumu yangu sikutaka kujua habari za nani wala nani nilidili na familia yangu tu huku kashikashi zikipungua, hata vitisho kutoka kwenye familia ya Jastini sikusikia na Wala sikutaka kusikia habari zao

Siku moja nikiwa kwenye ujenzi wa taifa kama kawaida.
Nakumbuka siku hiyo nilichelewa kutoka ofisini baada ya kuwa nimepokea wageni ambao , walikuwa wanarekebisha mambo fulani.

Wakati huo nilikuwa nafanya vitu kwa umakini sana haswa ukizingatia serikali ilikaa vibaya sana wakati huo, na pia kutegwa, kupelelezwa kulitamalaki hivyo nikaona lazima nifanye kazi kwa uaminifu. Bila kubagua wala kuchagua.

Nilitoka nje nikaangaza macho nikagundua watu wote wametoka tupo wawili tu mimi na jamaa mmoja ambaye alikuwa kafungua Bonet ya gari yake nisijue anafanya nini.

Mlinzi alifungua geti huku akitaka nisimame aongee na Mimi, kwakuwa hakuwa na mazoea na Mimi nikaona, huenda ana jambo la maana nikamsikiliza.

Aisee kiongozi vipi kwema?
Naomba hata ya fegi tu, maana na kibaridi hiki nahitaji kupunguza arosto. aliweka kituo yule mlinzi kijana huku akiwa kapendeza sana na sare zake.

Kwa leo nipo vibaya , labda kesho.
Nilimjibu huku nikipandisha kioo

Ahaaa sawa kiongozi , ila pia Kuna maagizo nimeachiwa. aliongea huku akiweka vizuri kofia yake kwa kujitazama kwe side mirror.

Maagizo?
Maagizo gani na kutoka kwa nani.
Niliuliza.

Kuna muda wakati naingia hapa kubadilishana na mlinzi mwenzangu ambaye kapata dharula, Kuna watu wawili walikuja hapa wakakuulizia wakisema wanakuhitaji.
Ikabidi niwakague Kisha nikawataka waeleze shida yao.
Cha ajabu wamegoma wakidai wanataka kuonana na wewe mwenyewe eti niwaitie.
Ila nimewakatalia kuwa si utaratibu wetu.lakini babu mlinzi mwenzangu aliwafukuza,huku wakisema nikwambie.uwapigie kwa namba hii waliyoniachia aliweka kituo yule mlinzi huku akinitajia namba fulani ambayo sikuitambua.

Dah ahsante sana, unavuta sigara gani ? Niliuliza

Asee Mimi navuta hizi za bei rahisi kaka , alinijibu Kwa bashasha,

Nikampa ya pakiti nzima akafurahi sana huku nikitoka taratibu na kutafuta njia ya nyumbani huku nikipiga ile namba niliyopewa na mlinzi.

Nani mwenzangu, maana namba nimeikuta kwa mlinzi, niliongea mara baada ya mtu yule kupokea simu.

Sihitaji hata ujue jina langu, unahitajika ufike hapa kituo cha polisi cha (akitaja jina) Kisha akakata simu.

Hawa nikiwadekeza wataniona Mimi boya na mtumwa wao Sasa ngoja nitamuonesha. Nikapiga ile namba.

Ee bwana kwanza naomba tuheshimiane,
Unaniita sijui una shida gani,
Na maelezo gani,
Halafu kwanini tunafatana maeneo ya kazini ? Sasa nikwambie tu kuwa kwa leo siji hapo.
Pia nahitaji kujua Nini unataka kwangu. Nilikuwa mkali.

Daniel huna haja ya kujiuliza kosa gani , una makosa chungu mzima, na tumekuheshimu tu muda ule tungetaka tungeondoka na wewe, usijifanye mbabe Cha muhimu fika hapa Leo hii. akakata simu.

Nilimpigia simu mke wangu namna nilivyoongea na maaskari na kusema kuwa naelekea kituo X na akiona nachelewa anaweza kunifuatilia .

Dah Hawa watu si wakufunge tu mimi nijue moja? Mambo gani haya mtu unaishi kama digidigi kwanini?
Baba rudi kijijini tukapumzike nipo tayari jiji halikutaki hili. aling'aka mke wangu lakini nikaona kuendelea kumsikiliza hatomaliza maneno nikaamua kukata simu.

Nilifika kwenye kituo husika nikashangaa kumkuta afande Hussein ambaye kwanza sijawahi kumuona akiwa na sare ndiyo kwanza siku hiyo, huku nikitambua bado ni askari wa cheo Cha chini kabisa kwani sare zake zilionesha. Na hata muonekano wake alionekana bado anatumwatumwa tu.yaani alikuwa ni single phase bado nilishangaa mtu anawaza kuroga kwaajili ya wanawake, si angeroga apande cheo. Loh kweli akili ni nywele Kila mtu na zake.

Karibu sana ndugu yang, Mimi ndiye niliyekuita , hata yule afande mliyekuwa mnakwazana nilimtuma Mimi na mbaya zaidi namba yako nilipoteza sikuwa nayo ila ofisini kwako tunapafahamu, aliongea kwa upole afande Hussein huku tukiingia chumba fulani chenye mafaili mengi sana ya kizamani pamoja na computer ambazo hazikuwa latest version.

Ndugu yangu kwanza pole na kazi na pole kwa usumbufu, nimekuita hapa ili tufanye jambo moja,ni kweli Mimi na mke wangu tulikuwa tunamdai Jastini pesa nyingi tu kama ulivyosikia kiufupi katudhulumu sana ila wewe hauhusiki tumejua baada ya kufanya upelelezi, lakini hata hivyo Jastini tupo gerezani hadi muda huu tunapoongea , ni baada kupelekwa mahakamani wiki iliyopita na kujikuta anakosa dhamana kwani licha ya kuwa kwetu ni kesi ya madai lakini alikuwa na jinai pia, kwani inasemekana anamiliki pia silaha kinyume cha sheria .

Sasa ndugu zake pamoja na mkewe wanatia huruma mno wamechanga wamepata kiasi fulani kisichofika hata million tano ila mke wangu karidhika na yupo tayari kusamehe kiasi kilichobaki ili maisha mengine yaendelee.sasa nilichokuitia ni kwamba tunamtoaje jela? Mimi Kiukweli nipo kwenye sehemu ambazo siwezi kubeba dhamana ya mtu kama Jax na mbanga zake .ila ndugu zake wapi tayari ishu ni kwamba anakabiliwa na mashtaka mengi mno ingekuwa deni letu wala asingefika huko,ila natamani Jax awe uraiani.silali Wala Sina furaha. aliweka kituo afande Hussein.

Kwani yuko gereza gani?
Niliuliza huku akinitajia.

Lakini afande Mimi sina undugu na Jastini hata kidogo pia Sina ushikaji naye kivile ni kwamba hata kipindi kile ilikuwa ni biashara tu ambayo nayo Almanusra niishie pabaya, kiufupi tafuta mwingine ambaye anaweza kumsaidia Jastini. Niliweka kituo huku nikiinuka tukaagana nikaondoka.

Huyu afande Hussein fala kweli , Sasa kama ana huruma aliwezaje kuruhusu jamaa yake aingie jela, kwanini asingemshawishi mkewe wasimpeleke huko. Kwanza nitampiga marufuku asipende kunizoea sana wanga wakubwa hawa.

Nikiwa home nilianza kumfikiria Jastini starehe,fujo zote tulizofanya mjini huku mademu wakimuita handsome ingawaje alikuwa na sura ya kazi yote ilikuwa ni pesa aliyokuwa nayo,hela za Jastini nilikula sikatai , lakini pia Kuna siku watoto wangu wakiwa wanapokea sakramenti ya kipaimara Jastini aligharamia Kila kitu huku tafrija ndogo ikifana pale nyumbani, tulikuwa marafiki haswa , alinizudi hela kiasi cha kunidharau kwamba kwanini nasubiri pesa ya mwisho wa mwezi huku akinicheka na kusema yeye asingeweza kwani ana uwezo wa kutengeneza ten milioni kwa siku, ikichelewa sana siku tatu. Lakini Leo Jastini yupo gerezani mke wake, watoto wake wanaishije?
Halafu kumbe fujo zote za kipindi kile familia yake na ndugu zake wana maisha magumu tu,maana kundi lote lile nililiona pale kituoni,wameshindwa kufanya maamuzi hadi mtu anaishia jela?

Lazima Jastini atoke gerezani ,hata kama sitaonekana mimi huko gerezani nitatuma watu ngoja nitaazima,nitakopa ila lazima atoke jela maisha ni haya haya hakuna atakayezikwa na pesa, tulikuja watupu tutaondoka watupu,.

Mume wangu unawaza nini ,umewasha kompyuta halafu umejiinamia tu,sijui unasinzia eeh,na hujaniambia huko kituoni walikuitia nini.aliongea mke wangu huku akiisogeza PC yangu pembeni.

Itaendelea................
 
Asilimia sabini watu wengi wanategemea waganga kwenye mambo yao,why watu wajifanye kushtuka, wanafiki [emoji23][emoji23][emoji23]
Hakuna aloshtuka ila,kukuita inbox tumehisi kwa ishu hio tu 😂hatuna unafki wowote na upande wangu ilikuwa utani.weka Vyombo JD.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…