SEHEMU YA HAMSINI NA SABA
Ndugu msomaji wa simulizi hii,
Si kila jambo ni la kujaribu kwa kutaka heshima au uogopwe ohooooo...
Sasa endelea......
Nilipiga simu mara kadhaa lakini haikupokelewa,nikaamua kuendelea na kazi zingine huku kila mara nikipiga,najua yupo dukani na si rahisi kuwa mbali na simu sasa kwanini hapokei?
Nilijiuliza huku roho ya wivu ikiniingia kwa mara ya kwanza tangu nimuoe mke wangu,kwanza niliwaza namna milivyomfanyia nikawaza kuwa naye ni binadamu anayoyafanya nyuma ya pazia siyajui,na kuendelea kuleta jeuri basi nitakuwa kama nimemruhusu afanye ayawezayo . maana kwanza kuna mzigo wa pesa nimeuona ndani sijui ni sponsor gani katoa.
Na mke wangu naye ni mzuri na ndiyo maana watu hutuita mapacha,akiamua kutumia uzuri wake kujipatia riziki kwenye hii Dunia ya digitali,sina uwezo wa kubaini jambo labda kwa bahati.
Basi ikawa kila simu ikiita najua ni yeye kumbe ni watu wengine tu,
Nikituma sms hazijibiwi,weweeee siku ya jumanne ikawa mbaya kwangu huku hasira ikija na kutoka
Au nikampige maana huyu hapokei simu kisa niliyomfanyia jana,sasa nitamuonesha kuwa mimi ni nani na atanieleza zile pesa ni za nani!
Na hata kitendo cha watu kujakuja nyumbani pale ,ngoja nikampige marufuku,hawezi kuniletea mishangingi na mijitu iliyokosa mabwana ,pale ni kwangu na siyo danguro au kasino,halafu ngoja nitahakikisha anavunja urafiki na wale watu kwasababu sidhani kama ni marafiki sahihi.nilijiwazia huku nikitafuta sababu hata zisizo na mashiko lengo nikamgombeze mke wangu.
Lakini ikawa kila baada ya dakika kadhaa napiga simu,lakini haikupokelewa.
Baada ya muda fulani simu iliita mpigaji akiwa ni dada wa kazi,
Nikapokea kwa pupa.
Hey niambie kuna habari gani hapo kwema, niliuliza.
Ni kwema ilaaaaaa ,......dada wa kazi aliongea kwa kubabaika kisha akanitumia sms iliyosomeka hivi,
Dada kasema hataki usumbufu,anasema usimpigie,ila samahani shemeji mimi sijui ana maana gani na nimefikisha ujumbe tu,na kila nikimkatalia kuwa jambo hili ni gumu kwangu ananilazimisha.
Niliamua kutulia huku nikishusha pumzi ndeeeefu kwasababu nilikuwa nawaza mambo mengi sana yenye wivu ndani yake.
Muda wa lunch tuliongozana kama wanne ,wanaume watatu, mwanamke mmoja ambaye ndiye aliyetualika huku kila mtu akishangaa imekuwaje kwa Veronica tunayemjua kwa ubahili akalipe yeye ,tukajikuta kila mmoja anatabasamu.
Nilijitahidi kuificha ile hali isionekane kwa watu na kwa kiasi fulani nilifanikiwa,ila ilikuwa ni moja ya siku mbaya kwangu.
Muda wa kuondoka ulifika huku huku
Ulifika huku nikiwa nalaumu foleni kama vile ndiyo kwanza naiona kumbe ni kawaida kutokana na miundo mbinu yenyewe,lakini hata hivyo watu wanapiga hatua,ni rahisi sana mtu kumiliki usafiri tofauti na zamani,hii ni new era.
Nilifika nyumbani huku nikijaribu kuweka uso wa mbuzi , mdomoni nikipangilia maneno ya mashambulizi yatakayonipa points .
Lakini mke wangu aliinuka na kuja kunisalimia huku akinipokea handbag........
Vipi habari za kazi mume wangu ,
alisalimia.
Ni nzuri tu vipi mmeshindaje hapa,
Na mbona dukani hujaenda huoni kama utapoteza wateja, kumbuka watu tunapenda kuona sehemu ambayo iko available masaa 24.
niliongea huku nikishangaa utulivu wa mke wangu licha ya kuwa tuna kasoro zetu.
Niliingia ndani nika change nguo kisha nikatoka na panga nikiwa nazuga kukata kata majani ya mgomba huku nikimwangalia mke wangu na kilemba chake,huruma ilijaa,mawazo yaligonga kichwa, nilitupa panga pale chini na kuamua kurudi ndani kisha nikamuita mke wangu aje ndani chumbani .
Mke wangu mbona hukupokea simu nimepiga zaidi ya masaa manne kila baada ya dakika kadhaa ,vipi niambie kulikuwa na tatizo gani.
Niliuliza kwa upole.
Tatizo lipo,ila labda nikuulize kitu Mume wangu, kwasababu nakuogopa nahisi nipo na mtu mwenye ukichaa ,japo samahani kama nakutukana ila tambua nashindwa kabisa nikuweke kwenye fungu gani.aliweka kituo mke wangu.
Sawa ,najua umegundua kuwa nimechukia lakini hujui sababu .
Ila naomba kujua pesa ambazo zipo humu ndani ni za nani.
hapa nilibadilika kidogo sikuweka sura ya masihara.
Mbona hukuuliza mara tu baada ya kuziona huoni kama utapoteza ushahidi ,hivi kwa mfano tupo mahakamani unaweza kuonesha hizo pesa? Mke wangu ajibu kiupole.
Niliinuka kama kipanga na kwenda kufungua droo ya lile kabati lakini ilionesha imefungwa.
Pesa niliziona humu ,hebu nioneshe funguo na leo utanieleza nani kakupa hizo hela.sikuonesha utani.
Aliinuka na kutoa funguo zilizokuwa kwenye mkoba wake na kunisaidia kufungua huku nikiziona zile pesa kama nilivyoziona jana.
Haya (huku nikitaja jina lake halisi)
Niambie umepata wapi pesa zote hizi ? niliuliza nikiwa sina masikhara kabisa
Daniel,wewe ni mume wangu tena nakupenda sana,si kwasababu unanifanyia mazuri sana ila ni kwasababu kuu mbili,
Kwanza wewe ni baba wa wanangu na unawajibika vyema kama mume na baba wa familia.
Pili ni kwasababu tu nimekuzoea ,yaani naishi na wewe kimazoea.lakini kiukweli nje ya hapo sikupendi Daniel,laiti ningeambiwa nirudi zama za usichana wangu halafu nichague ni mume gani niolewe naye , sidhani kama kwenye miamoja bora ungekuwepo.
Naomba usichukie kwasababu nimekuambia sikupendi,
Bali nimeamua kukwambia ukweli,
Tabia zako haziniridhishi ,hebu fikiria umekaa huko mkoani kwa wiki tatu halafu unafika hapa unanuna tu ,
haya tufanye hizi pesa za watu ndiyo zimekuudhi kwanini usingeuliza,
Mbona kama siyo Daniel ninayekujua au unayejulikana na wengi.
Ni mjanja,ni mwenye ushawishi,ni mtu msomi kiasi chake,unaaminiwa lakini sasa hizi umekuwa kama mlevi wa vilabuni haupo kama zamani au unataka kuoa,maana kuoa ndiyo maana unanicharura charura kisha uone nitafanyaje.
Mtu nakungojea kwa hamu akili yangu inajiandaa kwa hamu mume anarudi,lakini badala yake unarudi na kuniongezea maumivu,sasa nagundua huenda hata ulikoenda hukwenda kazini bali ni kwa mwanamke mwingine.
Sasa nikwambie hivi mimi (akijitaja jina halisi) nakuruhusu fanya chochote kuanzia muda huu kama unataka kuniacha niache tu baba,hakuna sababu ya kujisumbua kutafuta visingizio visivyo na msingi ,nipo radhi kuondoka sitajuta kuyaanza upya maisha.
aliongea kisha akainuka na kuchukua Documents fulani kwenye mkoba wake akanipa.
Hizo karatasi ni za kikundi chetu cha kipindi kile na hizi ni pesa tumekopeshwa na kama mbunge alivyokuwa ametuahidi ,na jana tulifanikiwa kutoa hicho kiasi unachokiona ili tujue pakuanzia,kuna watu walikuja kwaajili ya kikao tupange tuanze na mradi gani kati ya miradi kadhaa tuliyonayo.na leo ilikuwa ni siku ya kikao husika ila nimeshindwa kwasababu Daniel umeharibu siku yangu vilivyo nashindwa nifanyeje.
Najua kikundi hiki hukukipenda tangu mwanzo na ndiyo maana hata hujui nina nafasi gani au naaminika vipi kwenye chama.
Tukiwa tunaendelea na maongezi dada wa kazi aliita kuashiria kuna ugeni nje.nilitoka na kukutana na sura za akina mama kama nane zikiwa hazina tabasamu kabisa.
Mkeo yuko wapi , anapigiwa simu hapokei tangu asubuhi na hatumuelewi.waliongea huku wakilazimisha kuingia ndani kwa nguvu.
Jifunze,
Elimika,
Burudika.
Itaendelea.............