Simulizi: Harakati za maisha

SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA

Usiku wa siku hiyo sikulala kabisa Kila nikiwaza namna Jastini alivyo nikawa napatwa na hofu.
Lakini Kuna hali fulani ya kiume ikawa inanijia.

Huwezi kunipelekesha wewe mjinga unadhani Mimi muoga kiasi hicho? Sasa jaribu kufanya unachotaka na Mimi nitakuonesha .
niliongea mwenyewe bila kujijua, kumbe mke wangu ananisikia.

Wewe vipi mbona sikuelewi,
Hebu amka kwanza, upo sawa kweli? aliuliza mke wangu.

Kwani Kuna Nini kimetokea,
Nilijibu nikijifanya sijui nini kinaendelea.

Naona unaongea peke yako!
Sijui nani hakuwezi, mara nini
Eeeeeh upo sawa kweli.
aliuliza mke wangu.

Nipo sawa, labda nilikuwa naota tu , hebu niache nilale bwana.
nilijitetea huku mke wangu akiwa hajaridhika na majibu yangu


Siku hiyo mke wangu aliamka mapema kuliko kawaida yake, akaendelea na shughuli zake ndogo ndogo za pale ndani kabla hajatoka kwenda kwenye biashara zake.

Na Mimi nilikuwa nishaamka niingie bafuni nijiswafi, mke wangu alikuja huku akiwa kabana mkoba wake kwapani .

Mimi natoka leo nataka niwahi kutokana na kuwa Kuna watu waliweka oda kwenye biashara zangu na waliniomba niwahi,lakini nikwambie tu kitu kimoja usiku wa leo nimegundua kuwa haupo sawa kiasi cha kunikosesha usingizi hata mimi, ushauri wangu ni kwamba ni vyema ukaniambia nini kinakusumbua tukusaidie. au habari za mpira nilizosema sitaki, ndiyo zinakusumbua? Lakini ujue utakuja kufa kutokana na kushindwa kuweka wazi matatizo yako mume wangu. alishauri.

Wee nishakuambia sina matatizo Sasa kwanini unalazimisha?
au unataka nizungumze uongo?
Hebu achana na mimi bwana.
nilikuwa mkali muda huo Kisha mke wangu akaondoka.

Nikiwa njiani kuelekea job, nilikuwa na mawazo sana, tena sana tu,

Mke wangu ameshagundua kuwa nina shida, halafu kajuaje?
Mbona nilijitahidi kujiweka sawa tu? au nimwambie ukweli tu, nisijekufa peke yangu, lakini nitaanzaje maana stori yenyewe ni ndefu inaanzia kwenye madini ambayo nilimficha sikutaka ajue.

Na mke wangu navyomjua kitendo Cha Mimi kumfichaficha vitu huwa hapendi kama nini, hili ni tatizo kubwa. nilijiwazia

Nilichukua simu nimpigie Jax haswa baada ya kuona huenda akawa kashusha hasira zake,lakini simu haikupatikana, nilishusha pumzi huku nikiona tayari Nina maadui wawili tena kesi moja wote wananituhumu kuwa nimeiba wake zao, na halafu ikiwa watakutana na kuambizana hili jambo si ndiyo watajua kabisa kwa asilimia miamoja kuwa ni kweli, hata yule afande ambaye hakuwa na Imani ya moja kwa moja anaweza kujua kuwa ni dhahiri shahiri Mimi nililala na mkewe, tena ni vyema kutuhumiwa na kesi nyingine lakini siyo tuhuma za wizi na wake za watu, hizi zimekaa vibaya mno. nilijiwazia huko moyo ukinidunda.

Lakini mbona inaonesha afande Hussein na Jastini wamedhulumiana pesa, huenda wakawa hawana maelewano mazuri, nikajikuta napata ahueni japo bado msala ulikuwa mkubwa.

Turudi nyuma kidogo.............
Jastini mtu mwenye miraba minne, akiwa na asili ya Kanda ya ziwa,wapo walidai si mtanzania,ni mchizi ambaye kwa mara ya kwanza tulikutana kwenye mitambo ya kuchimba visima huku yeye akiwa anadili na madini, huku akikataliwa na mafundi wenzangu msaada pekee nikawa ni Mimi, kwakuwa alikuwa ana hela na anajiweza aliamua kuonana na bosi wetu moja kwa moja na kufanikiwa zoezi lake japo madini hakupata kwani sehemu hiyo haikuwa na mwamba jike na pia mitambo yetu haikuwa ikifika mbali sana ardhini.

Baada ya hapo aliondoka tukapoteana , hadi pale tulipoonana mwaka fulani City centre akiwa na gari ndogo BMW kipindi hicho japo sikujua ni ya mwaka gani lakini hizi gari Ukiwa nazo mtu unaonekana wa maana sana kwa kipindi kile ambacho nilikuwa sina gari.

Ndipo tulipokumbushana wapi tulionana Kisha urafiki wetu ukaanzia hapo,huku nikigundua ni jamaa lenye pesa, lakini weeeeee badala ya kufilisika yeye akaporomoka kiasi kwamba akikuona na laki moja anapagawa , tulisaidiana mambo mengi sana lakini kwa siku hiyo akawa adui yangu huku nikiwaza kujificha.

Sasa endelea.....

Nilifika ofisini Nika assemble mambo yangu Kisha huyooo kwa Da Vero mtu nayemkubali sana, ushauri na hata kutunza Siri alikuwa mwanamke wa aina yake.

Daniel my brother niambie naona kama ulisahau kuwa Mr alikupa kadi ya mwaliko,mbona hujaja sasa , au humtaki mpwa awe kama wewe , maana tulikuwa tunamfanyia sherehe ndogo kama pongezi kwa kumaliza chuo kikuu. aliweka kituo da Vero.

Nikishika kichwa na kushangaa,
Dah jamani naombeni mnisamehe sana nilisahau na sijafanya makusudi. nilijitetea.

Vipi kwani ishu ya madini inakuvuruga nini bro maana ndicho kitu nilikuwa naona kinakunyima raha, aliuliza.

Bora hata ingekuwa hiyo , japo naweza sema hicho ndiyo chanzo kilichofanya nifike kwa Jastini.
nikaanza kumweleza mwanzo mwisho na jinsi Jastini alivyonitishia.

Mmmh pole sana halafu Dani kwanini huwa una marafiki wa ajabu ajabu hebu fikiria mtu hawezi hata kukusikiliza yeye anachokazania na kuamini ndicho hichohicho,
Halafu wifi umemwambia?
(akimaanisha mke wangu)

Nimwambie? Namwambiaje Sasa na wewe, hivi wewe mumeo aje na hizi habari , utamchukuliaje?
niliuliza

Daniel acha kumtolea mume wangu mfano, yaani Mimi na yeye tuache kwanza, jifikirie wewe kwanza .
Halafu hivi umewaza mkeo akizipata hizi habari na wewe umemficha unadhani itakuwaje,

Halafu Daniiiih, hivi kwani watu wawili wakupe tuhuma ya aina moja , mbona nakuwa njiapanda , natamani nikutetee lakini mmmmh bro!
Be careful naona Kuna kitu hakipo sawa , umri wako, wadhifa wako na jinsi ulivyojenga heshima ya jina lako hizi tuhuma hazikufai hata kidogo na watu wataanza kutuhisi vibaya na Mimi, eeeh maana unapenda sana wanawake so ukaribu wetu watu watahisi vibaya. aliweka kituo.

Dada Veroooo wewe si wakusema hayo,watu watuhisi vibaya kivipi?
Mimi na wewe tunaheshimiana Dada.
niliropoka.

Sasa chagua moja , uache kuniambia stori zako au uache ukaribu na Mimi, mtu mwenyewe tayari unaonekana Malaya, mume wangu akipata hizi habari zako, unadhani atapenda tena kuweka mifupa karibu na fisi, haiwezekani. aliweka kituo huku akinitaka niondoke kabisa ofisini kwake.

Nilirudi ofisini kwangu huku nikisikia baridi na hofu kuu , why nisingiziwe?
Nina mkosi gani?
Jastini na afande sijui hata wananiwazia Nini,

Vipi mke wangu akizipata hizi habari?
Nilijikuta nakosa amani.

Itaendelea.................

Sent from my TECNO LC6a using JamiiForums mobile app
 
leo ni bandika bandua ukituzingua tunamwita Jastini akishindwa tunamuita afande hussein

shusha story Daniel
Asante.
 
Daniel ameyakanyaga 😂
 
Kazi unayo, na Justin alivyombabe atakupiga tanganyika jeki akili ikukae sawa[emoji3][emoji3][emoji3]
 
SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI

Siku hiyo nilitoka kazini huku nikipitia kwenye pub fulani ili niongeze kujiamini maana niliona kichwa changu hakipo sawa.

Nikiwa pale simu yangu iliita kuangalia mpigaji ni moja ya wale jamaa waliotaka nirudi kwenye mambo ya mpira wa miguu.

Eeeh niambie, naona umenitafuta kwa mara nyingine, niliongea mara baada ya kusalimiana.

Aisee kaka tafadhali tunakuomba sana , na hapa tumeweka loud speaker watu wote wanakusikia, ombi letu ni lilelile okoa timu yako bro, tunajua una mambo mengi lakini fanya hivyo kaka, Kuna mashindano ambayo mshindi atapata zawadi ya bajaji na kiasi fulani cha pesa na mshindi wa pili atapata kiasi cha pesa taslimu ni nyingi sana na hali kadhalika mshindi wa tatu atapata hela isiyopungua million moja.
Kaka sisi tunaomba kiasi fulani cha pesa ili tuwezeshe hii timu mbona Kila kitu kitakuwa poa tu? Na tunakuahidi kwasasa hutopata hasara. aliweka kituo yule jamaa huku nikisikia kelele za watu kusapoti kauli yake.

Halafu nyie mbona hatuelewani ni jana tu nimewaambia kuwa mnipe muda kwanza, Sasa kwanini leo tena mmepiga simu? niliongea huku nikiwa nishaanza kukolea liquid.

Basi sorry bro , ila tunaomba usikose maana ndani ya wiki mbili hizi mashindano yataanza. jamaa asiyejua kukataliwa aliongeza huku nikikata simu baada ya kuona ni ujinga

Hawa mafala wanadhani mimi naweza tena kuingia kwenye mambo ya kijinga kama hayo, watu wanadhani pesa zinaokotwa eeh, wajinga sana hawa watu. nilijiwazia huku nikiendelea kupiga vyombo.

Akaja jamaa mmoja ambaye anaitwa George ni jirani yangu karibu kabisa na nyumbani, ila kutokana na kutokuwa na mazoea naye nikajikuta kama nina aibu fulani kwani siyo Kila mtu ajue kuwa unakunywa pombe, na pia ulevi siyo sifa nzuri .

Karibu kaka, karibu sana
Kumbe na wewe huwa unakuja huku, niliongea kwa sauti ya kilevi.

Aaaaaa nikushangae wewe bro, Mimi hii ni sehemu yangu ya siku nyingi sana Kuna ndugu yangu ndiye mmiliki wa hii pub , so huwa tunakuja kimuunga mkono mara Moja moja.aliongea jamaa huku akivuta kiti na kukaa huku akiwa na tabasamu rafiki .

Karibu mezani vipi huwa unatumia?
nilimkaribisha ule mzinga huku nilijichekesha

Aaaah hapana bro huwa situmii na sijawahi kutumia na sidhani labda kama kutakuwa ulazima, Mimi nafuata nyama tu hapa , Kuna jamaa anajua kutengeneza nyama ya ng'ombe vizuri mno ,halafu pia bei ni very cheap huwezi amini bei za hapa ni za kawaida sana hivyo huwa napitia kupata chochote kitu . alijibu

Kiufupi uwepo wake ulinikosesha amani na kuninyima uhuru maana mtu ambaye hanywi pombe huwa sipendi kuchangama naye lakini pia ni jirani yangu hilo ndilo lilininyima raha.

Jamaa aliagiza akatengenezewa nyama ile iliyochanganyikana na ndizi kisha akanikaribisha tukaendelea kugonga ile nyama, huku tukipiga stori za hapa na pale.

Bro nasikia wanaume wengi wanakufa mapema kutokana na stress za maisha kutokana na ile kujiita mwanaume ana kifua cha kustahimili mambo, hivyo kujikuta tunakosa amani ya moyo kwa muda mrefu. aliongea yule jamaa huku nikitingisha kichwa kukubaliana naye huku nikiagiza soda ili nisiwe mnyonge .

Lingine bro ni nyama hizi tunazokula zinawahisha sana wanaume, ndiyo maana wajane ni wengi sana,
Hata kwenye mlolongo wa viongozi wa taifa hili waliotangulia mbele za haki asilimia nyingi wanawake bado Wapo. aliweka kituo.

Yeah hilo linajulikana je nyama inaingiaje hapo na nini madhara yake kwani wanawake huwa hawali?
niliuliza.

Tatizo siyo kula tu Bali ni kwa kiwango gani?
Wanaume tunakula nyama kama hivi za kuchoma, mara mchemsho , mara supu ya nini sijui, kama nyie watumiaji wa vilevi huwa mnakula sana nyama kwa kiasi kikubwa na mara kwa mara. Mambo haya ni aghalabu kwa wanawake wengi haswa wake za watu, kwanza out zao siyo za mara kwa mara, pili hata nyama ikiwepo home wake zetu siyo walaji unaweza Kuta ni mara tatu kwa wiki au hata chini ya hapo. Lakini sisi men haipiti siku mbili hujatia kipande cha nyama mdomoni , siyo mjini tu, hata vijijini kuna watu huwinda wanyamapori na kurudi na nyama majumbani mwao, huku wakiwa wamekula na kusaza huko porini.

Wanawake wao mboga za majani na vitu vya maajabu ajabu ndiyo huvitumia na pia hapohapo wengi wao siyo walaji, unaweza toka out na mwanamke akaagiza vitu na kuishia kugusa gusa tu, siyo kushindilia kama sisi so hii huwafanya wao kubalance vitu mwilini. aliweka kituo yule jirani yangu.

George bwana!! umeongea saaaana je wewe huu utafiti ulifanya au kusikia wapi,au ni chuo gani, ni Havard? Oxford? au chuo changu UDSM? mbona sijasikia? au ndiyo vijiwe vya kahawa vinakuharibu , kwahiyo Mimi na mke wanguuuuu, mmmmh unataka kusema nitaanza kufa Mimi siyo? niliongea huku nikicheka sana.

Brother Dani eeh kifo anapanga MUNGU . Ila tuachane na hayo, ni kwamba pale nyumbani kwako Kuna Bomba sijui limepasuka? au kufanyaje sijui, ila linatiririsha maji kuja kwenye ukuta wa fence yangu hivyo kiasi cha kutia ukungu na uvundo hivyo ningekuomba bro ukashughulikie suala lile. aliongea Kisha akainuka na kuondoka huku nikipata picha kuwa ni hayo aliyokujia kwangu.

Baada ya kuondoka niliimalizia ile nyama huku nikiagiza local beer ili nibalance mambo yangu,

Eti nyama zinaua mapema, wanadanganyana kweli hawa? naachaje kula nyama, yaani ilivyo na pilipili hivi na bia za baridiiiii wewe hapana.

Wakati nawaza hayo nilimuona mwanamke ambaye namfahamu akija upande wangu huku akiwa kapendeza sana, tena mno .
Maziwa yake madogo yaliyoshikiliwa vizuri na sidiria, yalinitoa udenda huku suruali yake ya jinsi iliyobana mapaja na kufanya nyonga zake zionekane vizuri ikaamsha hisia zangu kama vile nimetoka jela.

Alieleaelea akitafuta meza ya peke yake Kisha akaipata ni karibu na zilipo speaker akiwa peke yake huku akibonyeza simu yake, Kila nikimwangalia nikawa namfananisha kama Kuna mahali niliwahi kumuona,yeye alikuwa bize akiangalia nje huku akiongea na simu hakuwa ameniona bado.

Baada ya dakika kadhaa niliinuka na kwenda Kaunda ile niletewe bia zingine.

Mmmh kaka ungemuita muhudumu angekupatia tu siyo lazima uje hapa mwenyewe, hawa wapo kwaajili ya Kazi hii. alishauri dada wa kaunda.
Kumbe lengo langu lilikuwa nisogee kule ili nimuone vizuri yule mwanamke, tukagongana macho yetu akatabasamu huku meno yake mazuri yanayong'aa yakiupasua moyo wangu.

Nilimtambua ni Fatma, mke wa afande Hussein tuliwahi kusafiri pamoja last year, nilirudi kwenye meza yangu huku, nikiwa namtazama
Kila muda huku zile taa zikimmulika nikamuashiria kwa kufumba na kufumbua kiganja cha mkono akaja nilipo huku Kwa mbwembwe nikifuta kiti kwa kutumia kitambaa changu, hakika alifurahi sana.

Vipi upo mwenyewe dada.
niliuliza.

Yeah ila Kuna watu nawasubiri.
alijibu kiufupi.

Kunywa pombe maisha ni haya haya ukifa umekufa tu hakuna starehe huko, akadai zile lager zitamchukua mapema akaagiza bia ya bei ghali, kutokana na vitu vilivyo kichwani sikujali niliagiza. Sikujali muda wala nini , sikujali ni mtu alitaka kunisababishia matatizo pombe nazo zilichukua nafasi yake .baada ya dakika mbili yule mwanamke aliniazima simu ili apige baada ya kuwa ya kwake imezima, Kisha akatoka akiwa anaongelea pembeni .

Cha ajabu nilishangaa
Kumuona mke wangu akiwa anaangaza macho akiangalia huku na kule pia akiwa anabonyeza simu kama anapiga. nikagundua ananitafuta na Mimi simu ipo na yule mwanamke.

Wakati huo my wife keshaniona huku akiwa na uso uliokasirika, akaja huku nikiwaza, tangu lini huyu kunifuata?

Na kaelekezwa na nani, na pia mbona siyo kawaida yake hata siku ambazo huwa narudi usiku sana?

Itaendelea.............
 
Daniel hukomi tu wewe sikio la kufa na wasiwasi ni Simon yule wa Baba Mkubwa alimleta mjini kumsomesha 😂sio kwa kurudia makosa kama ni mtego he.
 
Huishiwi majanga
 
SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU

Habari za saizi mume wangu, mbona upo hapa muda wote? nimekupigia zaidi ya mara tatu hujapokea,na huyo mwanamke wa watu kwanini umemtorosha?

Hivi hapa ninapoongea nasikia Jastini alikuja mida ya asubuhi na kutoa lugha zisizofaa pale nyumbani, na pia mida ya saa kumi na mbili jioni ya leo hii amerudi tena na anaonekana ni mwenye shari sana.
Lakini my kwanini uanze kumtorosha mke wa mtu, kweli?
Hata kama wenyewe wana maisha magumu ndiyo uingilie ndoa za watu?

Yaani amenitisha na kaongea kwa sauti kiasi cha baadhi ya majirani kusogea pale, licha ya kukupigia mara nyingi hujapokea........................

Wewe dada sijui mmama mbona unaongea sana sema uhudumiwe. aliongea muhudumu huku akiwa kabinua midomo yake kwa dharau huku akikatisha maongezi yetu.

Baada ya muda kidogo alikuja yule mwanamke ambaye ana simu yangu, lakini alikaa kwenye meza nyingine huku akiwa hanipi simu, nadhani muonekano wa Mimi na wife ulimpa jibu kuwa tuna mahusiano gani.
hakika nilimsifu sana.

Mimi sihitaji chochote dada, nimemfuata mume wangu tu hapa.mke wangu alimjibu muhudumu.

Mume, mume, angekuwa anakupenda mngefuatana mpaka huku loh, ndiyo maana sihitaji kitu kinaitwa ndoa. aliongea yule muhudumu mwenye kimini anayeonekana umri umesogea huku akirudi kwenye meza yake .

Basi, mke wangu hebu tuondoke na hizi bia siwezi tena kunywa maana haiwezekani Jastini anitafute Mimi kama Simba anawinda mnyama, ina maana hawezi kuongea na Mimi Hadi tutishane?
Kwa mke yupi hasa wakunitishia Mimi, hebu tangulia kwenye gari mke wangu naenda toilet kwanza.
si kwamba nilikuwa naenda toi kweli Bali nilitaka wife atangulie then nichukue simu yangu kwa yule mwanamke.
Ni kweli nilifanikisha huku nikimpa heko yule mwanamke kwa kucheza kama Pele. hakika alijiongeza sana.

Mke wangu akiwa anaendesha gari Mimi niliamua kuketi siti ya nyuma kabisa kwasababu zangu huku nikimtaka awe makini.

Mume wangu unanidhalilisha sana, lazima nikwambie ukweli.
alivunja ukimya mke wangu.

Kwanini,?
Niliuliza.

Yapo mengi ambayo kiukweli hayapo sahihi, na kuna vitu unafanya sijui kama unawaza hatma na mustakabali wa maisha na familia yako, unalewa sana mume wangu, tena saizi umezidi ni tofauti na zamani, kiukweli unanifanya ninyong'onyee sana, naona hata aibu yaani, hebu fikiria yule muhudumu alivyosema, Eti mume, mume ungekuwa wa maana ningekufuata bar? Ni dhahiri Mimi naabika na nitaaibika hadi lini? kwanini usiache
Pombe mume wangu, ni kitu ambacho usipotumia hupati madhara, haya Sasa kwa mfano hivyo ulivyolewa ndiyo mnakutana na Jastini si atakuua wewe? aliweka kituo mke wangu.

Aniue, hivi mama Jack Mimi huwa unanichukuliaje, kirahisi tu mtu anipige , weeeee never, hicho kitu hakitowezekana na yote kwa yote nitakufa naye labda. nilijibu kwa kujiamini

Halafu mke wangu nani kakuelekeza pale bar na tangu lini tunafuatana sijapenda. niliongea kwa sauti ya juu kidogo

George ndiye kanielekeza , si mlikuwa pamoja? baada ya vurugu na vitisho vya Jastini majirani walitoka na Kila nikipiga simu kwa ushauri wa watu kadhaa ukawa hupokei ndipo George aliponielekeza. alijibu mke wangu.

Sasa huko wapi unaenda mbona hivyo? eeeeeh njia ya nyumbani ni hii kunja kushoto bwanaa. nilimwambia mke wangu huku nikimshangaa wapi anaenda.

Huwezi kuelewa chochote kwa hali uliyokuwa nayo, lakini ukweli ni kwamba kwa vitisho hivi ni vyema tukaripoti polisi kwanza , Mimi mwenzio Sina amani kabisa .
alijibu mke wangu.

Eti nini? Kwahiyo Mimi nitishiwe na yule mpuuzi Kisha nimuogope, yaani Hadi polisi kabisaa kisa Jastini, wee upuuzi huo Mimi sifanyi hata kidogo na nikwambie tu kuwa leo nitakuonesha kuwa Mimi ni nani. Niliongea kilevi huku mke wangu akisimama alishindwa aelekee wapi.

Kwahiyo twende nyumbani siyo, lakini taarifa hizi usidharau mume wangu, lazima polisi wajue ili lolote likitokea basi inakuwa ni vyepesi kutoa taarifa. alisisitiza huku akigeuka na kuniangalia.

Weweeee huko huendi hebu twende nyumbani ,kama huwezi kuendesha gari nipe niendeshe mwenyewe,uoga tu eti nianze kutoa maelezo polisi kisa kutishiwa na Jastini,yeye ndiye wa kwenda polisi ili ampate mkewe,na hivi anavyohangaika na mimi anazidi kujichelewesha tu.niliongea kwa jazba huku mke wangu akiwa kimya kwa muda huo.

Lakini baba Jack,unaniumiza sana moyoni nashindwa kuelewa ni kwanini,uhusishwe na kupotea kwa mke wa mtu,kwahiyo umemfungia lodge au?maana kwa maelezo aliyotoa Jastini,kuwa alisafiri kwenda mkoani lakini cha ajabu ukawa unaonekana nyumbani kwake,pia aliwekwa mahabusu kwa matatizo fulani bado hukumsaidia ila ukatumia mwanya huohuo kumtorosha mkewe,hakika inaumiza sana.

Yaani mimi naishi maisha ya kukuheshimu wewe kama mume na kuishikilia ndoa yangu lakini wewe unahangaika na wanawake tena wake za watu? huogopi? hunifikirii mimi? huwazi kuhusu wanao? Mume wangu kiukweli unanisononesha mno unaniumiza .ila nadhani mwisho wangu umefika mbona kuna watu wanaishi bila waume na maisha yanaenda ,naamini kila jambo hutokea kwasababu zake.siwezi tena nasema siwezi kuaibika tena.
aliongea kwa uchungu mke wangu huku sura yake ikibadilika.

Hapana mke wangu nitatulia nitakuelekeza Kila kitu, najua utapata picha nzima Nini kinaendelea.
na huyu mpuuzi Jastini kwasasa atanielewa tu kuwa Mimi ni nani
Nilitoa vitisho vya kilevi.

Baada ya kufika nyumbani, nilishangaa geti kuwa wazi, ikabidi nimuulize mke wangu.

Hivi huyu msichana anajielewa kweli, tukiibiwa? yaani anawezaje kuacha geti wazi na hili ni wewe mke wangu humwambii ,unaishi naye kama ndugu ,hamuishi kama mtu na boss wake,nilishuka kwenye gari na kukuta na mlango wa barazani upo wazi .hapa nilishtuka na hata mke wangu alishangaa.

Wote wawili tulishuka na kumuita dada wa kazi lakini hatukusikia chochote ,mke wangu bila tahadhari akataka kuingia ndani lakini nilimzuia huku pombe zikikata kabisa.
niliingia mwenyewe ndani huku kukiwa shwari tu, hata vyumba vyote vilikuwa safi kabisa. Kisha nikatoka na kwenda kwenye mabanda yangu kule uani nikamuita dada wa kazi lakini ikawa kimya.

Mume wangu hupaswi kujifikiria mara mbili,amua moja kwanini tusiripoti polisi? bado huioni hii hatari? Sasa Irene wangu yuko wapi? Mtoto wa watu yuko wapi?
Tutawaambia nini wazazi wake? aliongea kwa kulalamika mke wangu.

Sikuwa na pingamizi nikafunga milango yote, tukaenda polisi muda huo ni saa nne za usiku.

Itaendelea.................
 
Aiseee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…