Lovelovie
JF-Expert Member
- Oct 2, 2021
- 12,582
- 26,053
Asante ccyBadoo hajanistua mkuu ngoja nikipata muda nitulie nisome vizuri!!
wabheja sana rafiki!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Asante ccyBadoo hajanistua mkuu ngoja nikipata muda nitulie nisome vizuri!!
wabheja sana rafiki!
Enjoy the story sis sikuhizi nina uvivu wa kusoma story balaaaAsante ccy
Same here ccyEnjoy the story sis sikuhizi nina uvivu wa kusoma story balaaa
Nishatoka church ngoja nitupieJitahidi mkuu utupie japo vipande vi2
Kula kwanza pilau halafu tupiamoNishatoka church ngoja nitupie
usinywe sana leo ukatusahau bwana.....Nishatoka church ngoja nitupie
Atakuwa tayari kashapiga ulabuusinywe sana leo ukatusahau bwana.....
Twende kazi basi mzee baba .Nishatoka church ngoja nitupie
Jumatatu tayariKiukweli sipo sawa leo sitaposti kesho Jumatatu episodes tatu zinawahusu majukumu ni mengi
Alamsiki
Msala mwingine DaniSEHEMU YA ISHIRINI NA SITA
Moyo wangu ulisisimka sana kwa kile alichokisema Jastini huku nikimuona jamaa siyo wa kawaida hana uoga kwenye Mali ya mtu.
Jastini akaendelea........
Kwahiyo baada ya kukaa lockup kule mkoani kwa zaidi ya siku tatu Kisha nikarudi Dar es salaam kwa kuungaunga, ndipo nilipomtafuta afande Hussein nimpe habari kuwa mchongo umeharibika ,
Alipokea taarifa ile kishingo upande huku nikigundua amekasirika sana Lakini hakusema chochote, tukaachana kisha nikakupigia wewe simu ili tukutane unipe madini ili tukauze nikijua Kuna chochote kitu nitapata ili nisogeze maisha Lakini ukaniambia umeuza
Hakika nilichanganyikiwa sana , Lakini nashukuru ukaniambia kama ni asilimia zangu za udalali utanipa , tukapanga tukutane kwenye hotel ya (akitaja jina)ambapo kabla hujafika tayari nilishadakwa na maaskari nikapelekwa kituoni nikitambua afande Hussein ameshanichora. alifafanua Jastini.
Maelezo ya Jastini yalitugusa wote mle ndani si mkewe, si mke wangu, Wala Mimi mwenyewe, nyuso za wanawake wawili zilionesha huruma sana hata Mimi Kuna muda nilimuhurumia Jastini licha ya kuwa ni jana tu alitoka Kunitishia Mimi na familiar yangu ila harakati zake ambazo hazikuwa na matunda zilitia huruma.
Jastini akaendelea..........
Nilikaa kituo kidogo cha polisi kwa masaa zaidi ya nane kabla sijahamishwa na kupelekwa Kituo cha kati, hata hivyo niliwaza Ina maana Dani hana taarifa yeyote kuhusu kukamatwa kwangu? shukrani ziende kwa ndugu zangu ambao walikuja kunidhamini huku wakati natoka nikakutana na wewe Daniel pale nje kabla hatujatibuana kwa kukosana kiswahili.
Nilifika nyumbani kwangu nikaangalia huku na huko sikumuona mke wangu, nikaulizia kwa majirani wakasema hawajui huku wakikuhusisha wewe Dani kuhusu kupotea kwa mke wangu maana asubuhi ya siku hiyo kabla sijadhaminiwa ulionekana nyumbani kwangu huku ukimpa kiasi kikubwa cha pesa. aliweka kituo Jastini.
Ni kweli nilionekana nikitaka kumpa taarifa za wewe kuwa mahabusu Lakini kwa hali niliyomkuta nayo , nikaona nitamuongezea matatizo zaidi na sikumpa kiasi cha pesa wanachosema, Mimi nilitoa hela ya vocha tu kuwa anitafute baadaye ili tuwe tunawasiliana, nadhani ilikuwa ni noti moja ya elfu kumi. nilifafanua huku point ile nikimlenga mke wangu na nashukuru MUNGU kwanini siku ile nilijikuta nakuwa bahili? Ni kwamba my Lord alikuwa upande wangu.
Jastini akaendelea.......
kiukweli baada ya hapo sikuwa na imani na wewe tena na nilikuchukia huku nikiwa na asilimia miamoja kuwa wewe unahusika na upotevu wa mke wangu, lakini cha ajabu jana baada ya kutoka hapa mchana nilimkuta mke wangu nyumbani ambapo aliponieleza alipokuwa niliridhika ni kwamba alikuwa kwa ndugu zangu, na nilichelewa kujua haya kwakuwa simu yangu muda mwingine naizima kwasababu ya madeni niliyokuwa nayo, na Kwa taarifa za chini chini nasikia yule mke wa afande Hussein yupo mji huu toka huko porini anakofanyia kazi na atakuwa amekuja kwaajili yangu. aliweka kituo Jastini akionesha ni mwenye wasiwasi sana.
Kwahiyo hiyo million tatu shemeji huwezi kuilipa kwa namna yeyote ili uwe na amani? mke wangu aliuliza.
Lakini Jastini alicheka kidogo Kisha akaniangalia mimi na huku akikohoa kidogo.
Ndugu zanguni Mimi nadhalilika hapa mjini Nini million tatu? Kwa hela anazonidai yule mwanamke ni nyingi yaani million tatu ni kama elfu tatu tu kwa hela anazodai ni kwa kipindi kirefu, mbaya zaidi alishakataa ushirikiano na mimi, halafu Nina madeni kwa watu wengine pia hakika safari na nyumba ile naona inaenda kuuzwa. aliongea kwa hisia kali Jastini kiasi cha kudondosha chozi.
Jastini mtu mwenye kiburi na anayejiamini pande la mtu,jitu lenye kipara muda wote, aliwahi kusema huwa hapendi kufuga nywele kwani huwa zinachukua asilimia kadhaa za ubongo,na pia mwenyewe aliwahi kusema kamwe hawezi kudondosha machozi kizembe ,akidai machozi ni ya thamani kubwa kwa mwanaume lakini,hatimaye alilia mbele ya wanawake wawili,huku aibu nikiiona Mimi, hakika hakuna kitu kibaya sana kama shida.
Wakati huo mke wangu alikuwa na imani tena kwangu kwani maelezo ya Jastini yalijitosheleza mno. Kazi ilikuwa kwa mke wa Jastini ambaye alikuwa analia kama mfiwa haswa baada ya kusikia kuwa nyumba wanayoishi huenda ikauzwa muda si mrefu.
Tulifanikiwa kumbembeleza Kisha yale mambo yakawa yameisha na tukaendelea kupiga stori za kawaida tu, hakuna aliyewaza kwenda polisi eti Jastini aliyetutishia hatimaye yupo mikononi mwetu kama ambavyo mke wangu alishauri tupige simu polisi kimya kimya then waje wamkamate, lakini kwa harakati za maisha yake hakuna aliyewaza mambo mengine yasiyofaa.
Lakini hofu ya Jastini bado niliiona nilitambua licha ya kutueleza mambo mengi lakini bado Kuna vitu anaficha ikabidi nimuulize haswa baada ya kuwa wanawake wameondoka.
Jax haupo sawa hebu niambie Kuna nini kingie tofauti na maelezo yako kama ni m3 nipo tayari kulipa niliropoka.
Daniel mwanangu,
Fatma yupo mjini, na amekuja kwaajili yangu nilimdhulumu pesa nyingi sana,na kumbuka Hawa wote ni maaskari yeye na mumewe hivyo Wana msaada mkubwa sana, wanaweza kunipoteza mara moja.
aliongea kwa upole Jastini.
Niliinama chini nikawaza sana, nakumbuka ni Jana tu nilionana na Fatma, pisikali ya maana almanusura nijipendekeze kwa mara nyingine jana lakini mpango uliharibika baada ya mke wangu kuja kunipa taarifa za kusema kuna vitisho nyumbani , nilishawahi kutengeneza mazingira ili nilale naye lakini ilishindikana, Fatma mbona kama ni zaidi ya nimuonavyo kwanini Jastini anamuogopa hivi?
nilijiuliza sana.
Kumbe wakati tupo ndani Kuna mtego uliwekwa nje na hakuna aliyejua, geti liligongwa wakaingia watu watatu mbavu kwelikweli wakasalimia huku haraka wakitoa vitambulisho vyao na kunionesha.
Walikuwa ni askari polisi sura ngeni hakuna niliyemjua hata mmoja.
Bila shaka wewe ni Daniel (akitaja majina matatu)
Yeah ni Mimi karibuni.
Niliwakaribisha huku nikimuona Jastini akija tulipo
Kwahiyo kumbe plan na mipango yenu huwa mnafanyia hapa si ndiyo?
Yaani nyinyi mnajifunza utapeli,Wala si wazoefu Sasa jeshi la polisi linawasaka watu kama nyinyi , Tena mlivyo wajanja Kuna muda mnajifanya mmegombana ili kutuzuga lakini timu yetu imefanikiwa kujua mbinu zenu.jana tu umeenda kituo cha polisi eti unamshitaki huyu jambazi mwenzio kakutishia, kumbe lengo mnatuchezea ili tusijue mipango yenu. aliongea huku akikunja sura akionesha hatanii.
Afande unaongea nini na Hawa?
Maelezo haya watapewa kituoni . aliamrisha askari aliyekuwa na silaha akisema muda unapotea.
Licha ya kujaribu kutaka kuuliza Kuna Nini lakini nilitishiwa na kubwa zaidi baada ya kujaribu kugoma kwenye gari lao lenye vioo vya tinted. Nilipigwa vizuri nikaona isiwe tabu na nitaumia nikaingia kwenye gari.
Itaendelea.................