SEHEMU YA HAMSINI
Walitafuta meza wakakaa Kisha wakamuita jamaa fulani ambaye nadhani ndiye alikuwa meneja wa pale, waliongea naye kama dakika kumi na tano hivi Kisha wakatoka huku wakinitazama Mimi hadi wanapotelea,
Kengele ya hatari ililia huku nikijua napelekezwa ama nafuatiliwa , nikajikuta hata yule mwenyeji wangu ambaye alinipokea kwa mara ya kwanza huenda lao Moja ila wanajifanya kama wapo tofauti lengo tu huenda wananipeleleza hivyo nikaongeza umakini ila baada ya muda kadri alivyokuwa anakata maji yule Medi nikatambua huyu ni mlevi tu Wala hayupo na wale,
Nilipiga maji sawasawa siku hiyo haswa ukizingatia nina zaidi ya miezi kadhaa sikugusa kilevi,
Piga maji haswa kama nilipania
na baada ya kukuta mimi na mwanangu Medi tunaongea
Broken English zaidi kuliko kiswahili nikaona ni muda wa kuagana ili tuondoke, na ikawa hivyo huku nikichukua usafiri maarufu kama bodaboda nirudishwe napokaa
Asubuhi niliwakuta saiti wale jamaa huku wakiwa wamechangamka fulani hivi yaani ile kumchangamkia mtu kinafiki . tulisalimiana
Sasa Dani ee au leo upumzike tu maana pengine utakuwa haupo sawa maana Jana Kuna sehemu tulikuona tulishangaa hata hujatupungia mkono tunywe soda? aliongea mmoja wapo.
Nipumzike?
Ili iweje na nyinyi ni kama akina nani Hadi mniambie hivyo, Mimi waajiri wangu ndiyo walionituma hii kazi na ndiyo nitakaowapa mrejesho wa kile walichonituma, ndiyo wenye mamlaka ya kusema nipumzike, sasa siwaelewi. Niliuliza kwa sauti yenye ukali kidogo
Hapana kaka sisi tumeshauri tu kuwa kwa hali tuliyokuona nayo jana ni vema ungepumzika hii kazi ni yako na siku zipo nyingi, hivyo kwakuwa ni kazi inahitaji utimamu tukaona kwa leo ungepumzika tu.
waliongea kwa sauti ya upole haswa baada ya kuona Mimi nakuja juu.
Sikilizeni, siku zote mtu asiye kunywa pombe huwaona au kuwachukulia watu wote ni walevi, na huwa mnashindwa kutofautisha Kati ya mtu mnywaji na mlevi, Sasa tambueni kuwa Mimi ni mnywaji wa pombe na si mlevi.
Nayajua majukumu yangu, natambua Nini kimenileta huku na nitakabidhi kazi kwa muda niliopangiwa kama ambavyo nimeaminika na walionituma,
Sidhani kama Kuna haja ya nyinyi kuweza kunishauri chochote kile. Na nawaombeni tuheshimiane, na kuwe na mipaka baina yetu sihitaji maneno wala ushauri usiozingatia nidhamu.
niliongea kwa jazba na Kwa kujiamini.
Waliondika huku wakiwa na aibu kwanza hawakuwahi kufikiri kama ningewatolea shombo, na nilifanya makusudi maana walizidisha dharau .
Nilitoka na kwenda kutafuta mchemsho ili kutoa hangover maana ukweli niliamka nazo siku ile nikiwa kwenye mgahawa ulioonekana si wa siku nyingi huku watu wenye nafuu wakipata vifungua kinywa pale nilitulia , kwenye kitu huku hata mchemsho wenyewe ukinishinda.
Mmmh pombe hizi halafu nimeleta ukali tu lakini wale jamaa wamegundua kuwa sipo vizuri,
Ila si mbaya , jitihada za unachokifanya huwa hazionekani hata utumie nguvu kiasi gani huwezi kuwaaminisha watu, Bali ni matokeo ya kile ulichofanya,
Results matters only .
Hata ukilima ekari mia kama kipato chako ni gunia moja tu basi huna ulichokifanya.
Nitahakikisha kila kitu kipo sawa na wale wambea walitaka niwakubalie eti nipumzike kwa amri yao ili waanze kusema mtu mwenyewe hafanyi kazi analewa tu ,never haiwezekani kwanza sihitaji mazoea nao kabisa.nilijiwazia.
Nilirudi kisha tukaendelea na kazi na vijana wangu huku nikigundua ile rangi yangu niliyowaonesha kuwa ni mkali, nikagundua design fulani wananiogopa lakini nilianza kuwatania huku kazi zikienda hata chakula cha mchana tukawa tunapiga pale pale ili wasiniogope.
Naam,
baada ya siku kumi na moja niliwapigia simu maboss zangu na kuwaambia kuwa kazi imekamilika,nikaambiwa nisubiri wawasiliane na watu wa kule niliko,kisha nikaambiwa nitabaki zaidi ya wiki mbili ili nijiridhishe juu ya utendaji wa kazi wa vitu nilivyorekebisha.
Hii ilinipa unyonge sana nilikosa raha,
Haya mambo gani tena?
Mbona sehemu nyingine unatengeneza chombo unakabidhi kisha unafuatwa na kurudi,leo imekuwaje,yaani nianze kwenda saiti tena na mimi ,ama kweli hii kazi huenda inataka kunitoka ,naona watu wananitafutia kila aina ya makosa ili tu nifukuzwe kazi.nilijiwazia moyoni.
Baada ya siku mbili vyombo viliingia site huku mimi nikienda na kwa bahati nzuri siku iliisha hakuna kifaa kilizingua ikawa karibu Kila siku naenda ili kusikilizia muungurumo tu, chombo gani hakipo sawa ili nitimize azma niliyoambiwa.
Siku moja nikiwa kwenye mti fulani nachezea simu Kuna gari ya maliasili land rover ilikuwa inakuja huku ikichepuka kuingia kwenye Diversion ilitengenezwa mahususi kwa muda ili kupisha matengenezo ya kipande kikuu.
Nikiwa sina hili wala lile kwani niliona ni gari tu kama gari zingine sikuwa na time nayo ila ilisimama karibu na Mimi nikisikia naitwa kwa sauti ya kike Daniiiiii huku anayeita akifungua mlango na kushuka .
Naam, ilikuwa ni sura ya mtu ninayemfahamu si mwingine alikuwa ni Fatma au Fetty mke wa afande mmoja wa jeshi la polisi aitwaye Hussein.
Tulisalimiana huku moyo ukinidunda kwa kukataa kitu, sikujua moyo wangu unakataa Nini wallah,
Daniel unafanya nini hapa, wewe ni mkandarasi , ni nani labda ningependa nijue na unakumbuka siku zile ulinificha kabisa kazi yako.
aliuliza kwa sauti yake ya kike nzuri.
Nipo tu ni Harakati za maisha tu, nipo nasaka vibarua dada yangu. Nilimjibu kifupi huku nikimtazama mwanamke ambaye alivaa sare zilizoiva huku ile kofia yao ya duara aliyovalia pembeni ikimpendeza sana .Kwa mara ya kwanza nilimuona Fatma akiwa kwenye mavazi ya kazi yake.
Dah basi sawa karibu kwenye Mkoa wetu ndugu , na hii ndiyo wilaya yetu. Aliongea kwa madaha huku vijana maaskari waliokuwa nyuma ya ile gari wakinitazama sana .
Kwani unatoka wapi dada yangu. Niliuliza.
Aaaaa unajua huku upo karibu sana na hifadhi , na geti letu halipo mbali sana ni kilomita chache tu kutoka hapa, na Mimi mwenzio nimepanda cheo(huku akicheka)hivyo sikai Tena kota za kule nakaa hapo center, karibu sana . alifafanua huku nikimtazama mabegani akiwa
Mashallah ni afisa mkubwa tu kiasi chake nikampa hongera zake huku nimeduwaa.
Mwanamke mzuri ambaye alidai ana mtoto mmoja tu, akiwa hataki kuzaa tena kwaajili ya kuwa bize kulitumikia taifa. Kweli afande Hussein alikuwa sahihi kuwa na wivu
Mwanamke English figure, weupe wa asili akiwa na tumbo zuri flat
(Siyo Hawa vitumbo mchongoma)
sauti tamu, sura tamu yaani mtamu nilitamani utamu wake, lakini moyo ulikuwa unakataa akili zangu ndogo zenye kusahau jambo haraka zilitaka ila Sasa moyo haukutaka kabisa.
Naona Dani Mimi nikuache tutawasiliana,sema nipe namba zako sina ni Mr alifuta kipindi kile.
aliongea kwa sauti tamu huku nikishindwa Cha kufanya.
Je nitatoa namba Mimi Daniel kweli?
Ni huyu mwanamke ambaye mumewe alidhani nimetembea naye kiasi cha Mimi kuwekewa mtego, mganga aliniambia kuwa ni chanzo cha matatizo yangu.
Ni Fatma huyu ambaye kamsababishia matatizo jamaa yangu Jastini, huku Mimi mwenyewe nikiponea kwenye tundu la sindano.Leo nimpe namba?
Kumbuka Daniel napenda wanawake wazuri bwana, maisha yanahitaji vitu vizuri tafuta pesa,tumia pesa , nimezaliwa, naishi , nitakufa.
Hapa katikati kwenye kuishi lazima nile maisha.
Mimi ni mwanaume, sijazaliwa ili nije kushangaa. Sasa itakuwaje nitatoa namba?
Weekend njema wadau wangu.
Jifunze,
Elimika,
Burudika.
Itaendelea.................................