Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Shukrani mkuu ngoja niburudike nayo...!
Huna BAYA uishi maisha marefu JDNgoja nipambanie kwanza ugali wa watoto kwanza saa kumi na mbili jioni usikose kuchungulia
[emoji120]Huna BAYA uishi maisha marefu JD
Asante Sana mkuu,tunajifunza,tunaelimika na kuburudikaSEHEMU YA HAMSINI NA NNE
Nilishangaa kumuona mtu mmoja ambaye yupo sehemu nyeti sana serikalini na sikutegemea yeye kuwepo pale hakika ilikuwa ni siku ya kipekee sana kwangu.jina lake halisi ni ngumu kuliweka hapa ila anaitwa Scorpion. Na aliitwa hivyo kwasababu alikuwa karibu na maboss akijulikana kwa sifa ya kufukuzisha wafanyakazi wenzake, hivyo akafananishwa na sumu ya Nge (scorpion)hili jina hata yeye halijui.
Tulisalimiana huku nikiwa na heshima na adabu zote, si mtu maarufu sana ila kwangu Mimi ni mtu muhimu mno kwasababu tunajuana kitambo.
Niambie Daniel mdogo wangu, imekuwaje unajiita fundi , nimeshangaa sana umeamua kuudanganya umma, maana watu walioko hapa ukumbini ni wengi sana huoni kama umejiharibia, kumbuka Mimi nakujua vizuri sana, habari za miaka mingi lakini.
alinichezesha maneno kwa kuzuga lakini nilikuwa tayari kumjibu na kumuelekeza vizuri.
Mkuu Mimi sijadanganya,
Ni kweli taaluma yangu ilikuwa ni X, ila kwa ushauri wa (jina kapuni)
Niliamua kujiongeza kwa kusomea taaluma hii. Nilimjibu.
Ok ok unawezaje kumudu kwa uweledi , maana ulichosomea ni kingine na unachofanya ni kingine je, nitaamini vipi kama unaweza kufanya hizi mambo za mechanics.
aliuliza.
Haikuwa kazi raisi bro,
Kwanza nilivyomaliza chuo sikubahatika kupata kazi mapema hii ilinifanya nijute kusomea taaluma yangu. Nikajikuta naangukia kwa mwarabu mmoja kama kibarua wake, nikiwa ni mmoja wa madereva wa familia yake.
Baada ya kufanya kazi kwa uaminifu kwake , alinipeleka kwenye kampuni ya ndugu zake ambayo ilijishughulisha na mambo ya makenika na utengenezaji wa barabara pamoja na madaraja kabla hawajafurumushwa na serikali kwakuwa walikuwa wakifanya kazi kwa kiwango duni.
Baadaye wakaamua , kujihusisha na biashara za hotel ambako Mimi nilishindwa kwani sikuwa na utaalamu hivyo nikatafuta kazi kampuni nyingine ambapo ilijihusisha na mambo ya ujenzi ikiwa ni kampuni ya mtu binafsi . Niliweka kituo.
(kwa aliyesoma simulizi ya Mimi na boss wangu atanote kitu.)
Sasa serikali uliingiaje maana Mimi nilikukuta upo kwa zaidi ya miezi nane nikitoka ughaibuni. aliniuliza Scorpion
Baadaye kampuni hii niliachana nayo baada ya kufukuzwa kwa kosa nisilolitambua, nikaamua kupeleka maombi sehemu nyingine, nikafanikiwa kuingia kwenye taasisi ya serikali nilifanya kazi mwaka mmoja tu , nikashauriwa kuwa taaluma yangu ni ngumu kunitoa kimaisha labda kwa aliyejiajiri mwenyewe nikaamua kwenda kusoma nje kwa mara nyingine hata niliporudi taasisi ilinipokea vizuri , na ndipo nilipo hata Sasa nilimfafanulia Scorpion.
Hongera sana , lakini hii kashfa ya ulevi huoni kama itakusababishia matatizo baadaye?
Hebu fikiria namna watu walivyokupigia makofi leo, unajua Kuna watu wangapi wamekuzidi wadhifa, energy, power hata pesa tu Kuna wengi wamekuacha parefu, kwasababu wewe bado umeajiriwa ni fundi lakini wenzio ni maboss ni wakandarasi, lakini hawajapigiwa makofi na kushangilia kama wewe,
Nina Imani ni bahati yako Kila mtu ana namna alivyobarikiwa na Mungu lakini kwa huo ulevi mmmmh tegemea kuwekwa pembeni ikiwa hautobadilika, Mimi binafsi nakufahamu licha ya kuwa umejieleza sana ila tambua umenificha mengi.
Sema hayo tuachane nayo , chukua namba yangu na tutawasiliana.
aliongea Scorpion ambaye alivaa kawaida huku akiwa kwenye gari ya bei nafuu mno, aliingia kwenye gari na kutokomea.
Pengine ilikuwa si rahisi watu wa Mkoa na wilaya ile kumtambua Scorpion lakini Mimi nilimtambua vizuri sana,.ni bonge la ...........
Kumbe wakati huo Fatma alikuwa akinisubiri , alikuja huku akiwa na tabasamu zuri sana, tuliongea mengi huku akilaumu kuwa kwanini nilimpa namba ambayo siyo, huku akidai hataki tena kuchukua namba toka kwangu kwani nilimdharau.
Daniel bwana tatizo wewe hujiamini na Kila mwanamke huwa unamtaka, hivi hatuwezi kuwa na mawasiliano bila kuwa na mahusiano ya kimapenzi,? Hilo linakukwamisha sana Dani acha kuishi kiswahili hivyo,
Najua unamuogopa mume wangu ndiyo maana hutaki kunipa namba zako, na niseme tu kuwa sitaki tena namba zako. aliongea Fatma Kisha tukaongea mambo mengi Kisha akaondoka.
Watu walinifuata tukapeana mikono na kuongea mawili matatu huku wakitamani kunijua zaidi lakini nikaamua kuondoka kuepusha maswali mengi.huku nikimpigia simu Medi mwenyeji wangu, lakini hakupokea simu na gari lake nilikuwa nalo Mimi. Nikaamua kuondoka kwani nilipo anapajua nikaona muda na saa yeyote atafuata usafiri wake .
Saa tano usiku alinipigia akiwa amelewa sana huku akidai atakuja asubuhi. (Dah Kuna watu wa ajabu sana mtu unawezaje kuwa na Imani na watu kiasi hiki huyu hajawahi kuibiwa nini? Nilijiwazia.
Asubuhi na mapema nilipokea simu kuwa nijiandae, kwani kesho yake ambapo ni jumatatu nitafuatwa na dereva ili nirudi kwenye jiji lenye fujo zake.
Wakati nikimsubiri Medi nilipiga simu kwa mtaalamu wangu , ikapokelewa tuliongea kifupi Kisha nikaamua kumtumia muamala fulani kama ambavyo nilipanga maana Kuna vitu nilianza kuviona , nikaamini kuwa yule hakuwa mtu wa kawaida.
Saa nne asubuhi Medi alifika huku akiwa na aibu fulani maana Jana si alinitelekeza?
Tukasalimiana
Oyaa samahani sana yaani Jana Kuna tamaa iliniingia baada ya kupokea simu ya mchongo wa hela nikaona nisiiache. Nisamehe sana ndugu yangu. Medi alikuwa mtu wa ajabu sana.
Usijali bro kama ulipata simu ya kukupatia maisha, ni vyema ulifanya hivyo kuhusu kuonana si ndiyo kama hivi tumeonana?
sisi wote wanaume michongo tunaijua na maisha tunayajua hivyo usijali mwanangu. Nilimtoa wasiwasi huku akifurahi na kunipa tano.
Ila mwanangu Mimi kesho naondoka nadhani natakiwa nionane na wale jamaa zako kesho asubuhi na mapema ili niwakabidhi vifaa. Niliweka kituo.
Dah mbona mapema chaliangu, Sasa tunafanyaje, ila bro ana zawadi yako kwa kumfichia aibu maana tayari lawama zilianza watu wakidai amechukua tenda ilihali ana vifaa vibovu.
Pia Mimi mwenyewe Nina zawadi yako na pia twende ukapajue nyumbani na umuone na shemeji yako, Mimi mwenyewe si mzaliwa wa Mkoa huu nimekuja tu kwasababu braza wangu ana kampuni yake hapa miaka mingi.
Siku hiyo tulizunguuuka huku nikitamani nipumzike lakini sikuwa na namna hatimaye tulifika kwa Medi nyumbani kwake ,
Dah kweli umdhaniaye siye...
Jamaa alikuwa vizuri licha ya kuonekana mwezi mchanga hivi kutokana na namna alivyo lakini alikuwa na life zuri kabisa ,
Pia nikagundua wale watu wahuni wahuni ndiyo ambao huwa na wake wazuri sana kuanzia sura hata akili,dah kweli Mungu hakunyimi vyote (hapa nisiongee sana).
Siku inayofuata nilikuwa nishakabidhi vifaa na pa kusaini nikasaini huku nikiwasilisha mambo kwa njia ya Email. Nikawa nishamaliza kazi .
Nilianza na Mungu nikamaliza na Mungu japo changamoto huwa hazikosekani maana Kuna watu wawili nilitakiwa nishirikiane nao kazi lakini mmmh tangu nafika Hadi naondoka jamaa hawakunikubali kabisa lakini sikushangaa sana maana binadamu ndivyo tulivyo.
Saa sita dereva alinipigia simu kuwa Kafika , nikamuelekeza nilipo akaja,huku nikishangaa kuona kaja mtu mgeni kabisa ambaye simfahamu.
Safari ikaanza huku Medi akitusindikiza hadi barabara kuu eti,
Yule mjuba sitamsahau,alikuwa na visa mno,kila nikichungulia kwenye side mirror naona gari hii hapa,kabla hajatuwashia taa kuashiria ndiyo anaishia.
Kwani huyu jamaa yako tupo safari moja eeh dereva aliuliza.
Nikajikuta badala ya kujibu nacheka tu,Medi alikuwa mtu wa aina yake.
Nini kitajiri baada ya kurudi ofisini?
Usikose next episode.
Jifunze,
Elimika,
Burudika.
Itaendelea.................
Saa mbili usiku usikose kuchungulia.Samson embu Leo furahisha watu kwa niaba ya team ya wananchi [emoji23]
Saa mbili usiku usikose kuchungulia.
Ila omba Yanga ashinde asiposhinda..,.....(joke)[emoji23]
Almerrikh 0. 2.YangaSaa mbili usiku usikose kuchungulia.
Ila omba Yanga ashinde asiposhinda..,.....(joke)[emoji23]