Simulizi: Jamani Mchungaji

Simulizi: Jamani Mchungaji

SEHEMU YA 23


Mama mchungaji hakuamini kuwa kundi lote lile la watu lilikuwa limemaliza safari yao mbele yake,mapigo ya moyo yaliongeza kasi sana aliukamata mkoba wake kwa nguvu mno kwani kwa upande mwingine alidhani wale pale ni wezi wanataka kumwibia kwa staili ya kumzingira.

"nini? Nini?" kwa uoga mama mchungaji alianza kujitetea mbele ya kundi lile,ile sukumwa sukumwa ya hapa na pale ilipelekea kuanguka kwake,lakini kabla hajafika chini tayari ile kanga aliyokuwa amejitanda kichwani ilikuwa imetolewa na kumwacha uso na kichwa wazi.
"ana bahati kumbe mwanamke kweli" alisema mmoja kati ya waliokuwa kwenye lile kundi kisha kila mmoja akatoweka na kumwacha mama mchungaji peke yake eneo lile. Juhudi zake za kuubana mkoba wake zilikwisha wakati anapepesuka kuelekea chini ni katika kipindi hicho hicho mikono ya kijanja ya kijana mmoja ilizama na kutoka na simu moja ya mama mchungaji.
"Mungu wangu na simu wamechukua maskini wee nitafanyaje sasa mimi" alijiuliza mama mchungaji huku akitazamwa na wananchi wengine kana kwamba ni mwendawazimu fulani aliyetoroka hospitali,mwili wake ulijaa vumbi na nywele zake zilikuwa zimevurugwa sana na wale vijana wakati wa varangati lile.
"eeh! Mwenyezi Mungu nisaidie waumini wa kanisa wasiwepo mitaa hii" huku akitetemeka alizungumza na wakati huo huo akijaribu kurudishia khanga yake kichwani na usoni. Kwa kuelewa kwamba heshima yake imeshuka tayari eneo lile mama huyu hakutaka kuongeleshana na mtu yeyote badala yake hatua kwa hatua akajitoa eneo lile kuelekea katika mitaa iliyochangamka zaidi kutokana na wingi wa nyumba zilizojengwa pale na kusababisha msongamano wa watu.

"sijui ni njia hii hapa sijui ni kule,mama yangu leo napotea hapa na sijui itakuwaje sasa..kwaheri ndoa yangu" alijisemea kwa upole na sauti ya chini mama mchungaji huku akitazama pete aliyovishwa na mchungaji siku walipofunga ndoa takatifu kanisani.

"Zinduna..nasema niachie we m¥€&** tena malaya mkubwa,niachie nisije nikakuchania blauzi yako huo mtindi ukabaki nje sasa hivi"

"umchanie nani blauzi,unaijua thamani yake wewe,nakuuliza bwana yako anaweza kununua? Ashura nitakukun'guta mpaka uione dunia chungu"
ulikuwa ni ugomvi kati ya wanawake wawili ambao kwa hali na matusi ya nguoni waliyotukanana walionekana kuwa katika mtafaruku mkubwa wa kugombea bwana,umati uliowazunguka haukuwa hata na wazo la kuwatenganisha katika ugomvi wao,zilikuwepo pande mbili na kila mmoja akishabikia mtu wake ili aweze kushinda.
Mama mchungaji alipita jirani kabisa na eneo hilo macho yake yalivutia kwenda kutazama visa alivyovikosa kwa siku nyingi tangu aolewe na mchungaji.
"he! Sio zinduna yule...ha! Na yule pale mbona ni Ashura" alisema kimoyomoyo mama mchungaji alipofika eneo lile
"au nawafananisha jamani" alizidi kuwaza.
 
SEHEMU YA 24


"hapana ni hawahawa wabaya wangu yaani kweli wamegawa picha zangu zile mbaya na chafu ili waniharibie ndoa yangu nasema hivi UMAMA MCHUNGAJI Pembeni ngoja niwaonyeshe nadhani wamenisahau" alijiapiza huku hasira zikimpanda kwa kasi kubwa. Taratibu alianza kuwapangua watazamaji mmoja baada ya mwingine hadi macho yake yakawaona maadui wake ana kwa ana.
"ni wenyewe ku*%$%" alitoa tusi mama mchungaji kisha kama nyati akatimua mbio kuwafuata wawili hawa kwa kasi.
***
Mwonja asali haonji mara moja na haba na haba hujaza kibaba,ni misemo hii iliyotumika kuendeleza maasi baina ya Oscar mfanyakazi katika mabanda ya mifugo na Noela ambaye ni bosi wake. Licha ya kuoneana aibu siku iliyofuata baada ya kuibanjua amri ya sita katika kitanda anachotumia Noela na mumewe Timoth ambaye alikuwa safarini kikazi,sasa Noela na Oscar walibadili na kuhalalisha wizi wao kuwa kitu halali,mara leo bafuni,kesho sebuleni,mara waoge wote. Kwa kifupi hazikuwepo aibu tena na kila mmoja alifurahia uchafu na usaliti huo mkubwa na usiofaa kuigwa hata kidogo.
"Oscar unajua tumekuwa tukijisahau sana?"

"mbona unasema hivyo Noela,kipenzi changu" alijibu kwa njia ya swali Oscar wakati wakienda kuoga na Noela katika bafu la mumewe (Timoth).

"hatujawahi kutumia kinga na leo ni mara kama sikosei ya tisa tunafanya mapenzi"

"ni mara ya kumi na moja mimi huwa nahesabu" Oscar alimkosoa Noela kwa takwimu zake alizotoa.

"mimi katika uwanja huu kwa takwimu zake Magufuli chamtoto,yaani hadi lita nilizokunywa kwako nakumbuka ni lita themanini point sita" alitania Oscar wakajikuta wote wanacheka.

"we shauri zako uje unipe mimba!" alilalamika Noela
 
SEHEMU YA 25


"aah! Noela kwani wewe siku zako hujui zinavyokwenda?" Oscar alihoji.
"najua lakini huwa nakosea siku nyingine mfano pale kwenye zizi la n'gombe siku ile usiku nilikuwa vibaya lakini ulivyoniteka mtoto wa kiume ukaweza kufanya" alijibu Noela huku akianza kumsugua mgongo Oscar ambaye alikuwa anajiamini kama vile ile nyumba ni ya kwake sembuse chumba.

"usijali baby hatutafanya makosa tena! Sawa eeh!" alijibu kwa upole Oscar na Noela akamuunga mkono.

Akiwa Mwanza Timoth aliendelea kuwa katika dimbwi kubwa la mawazo juu ya mkewe kila siku usiku alipokuwa kitandani amelala peke yake imani yake ilimwambia kwamba mkewe yupo na mchungaji kitandani,msimamo wake katika dini ulikuwa umefifia sana
"kama hawa wanaoitwa wachungaji ndio wanaochukua wake zetu na kuwafanya wa kwao nini maana ya kwenda kuabudu kanisa linaloongozwa na mnafiki mkubwa...jibu ni fupi sana ni heri kuacha kusali kabisa" alijisemea Timoth kwa sauti iliyokwaruzika kwa hasira huku akikanyagakanyaga kitanda alicholalia kwa nguvu akitumia miguu yake. "dawa ya moto ni moto aliniambia Deo nitakuwa mjinga nikipuuzia,we ngoja nikirudi Dar...yaani ngoja nirudi nasema" alishindwa kuzuia kilio chake Timoth akalia kwa uchungu wote na kutamani hizo wiki tatu zikatike upesi aweze kwenda kulipa kisasi.

Akiwa ndio anakausha machozi kwa kutumia shuka ya kujifunika simu yake iliita hakuwa mwingine bali mkewe.
 
SEHEMU YA 26



"huyu mshenzi ananipigia simu wakati yupo na jianaume hapo yaani naumia mimi...naumia jamani nyie niacheni" alizungumza kama anahadithia watu huku akiitizama ile simu.

"hellow mpenzi umelala? Nini mbona simu imeita sana" upande wa pili sauti ya Noela ilimuuliza Timoth.

"hapana nilikuwa naoga,mimi mzima namshukuru Mungu kwa ulinzi wake,nyie huko wazima?"

"sisi wazima sana tu japo Oscar aliugua kidogo mafua"

"ooh! Mpe pole,nitamletea dawa nzuri za kienyeji kutoka Mwanza,bado siku nne nimalize hizo wiki tatu huku"

"karibu sana mume wangu nimekumis sana"

"nimekumis pia mpenzi wangu,usiku mwema mamaa"

"na wewe pia babaa" alimalizia Noela kisha akakata simu.

"mh! Amesema bado siku nne arudi,tumalizie malizie kwa usongo lakini salama " Noela alimwambia Oscar aliyekuwa kifuani pake akimchezea chezea anavyotaka.
"dah! Siku nne chache jamani sasa inabidi dozi iwe alfajiri,asubuhi,mchana,adhuhuri,jioni na usiku eti eeh!" alijibu Oscar kwa kibesi.
***

Kama vile watoto wake wa kuwazaa mama mchungaji alifika na kuwafinyangafinyanga wawili hawa waliokuwa wanapigana
"Mtanieleza leo,mkipenda hapa hapa hadharani na mkiamua mwaweza kufanya hivyo majumbani kwenu" mama mchungaji aliwaambia wawili hao wakati huo mtandio ulikuwa umeanguka tena na kubaki wazi kichwani na usoni.
 
SEHEMU YA 27



"he! Rehema jamani ni wewe kumbe kulikoni tena" Zinduna ndiye aliyekuwa wa kwanza kumtambua akasema hayo.
"ha! Da Rehema jamani kulikoni" alidakia Ashura ambaye tayari alikuwa amechubuka usoni. Umati uliongezeka kwani burudani ilikuwa imeongezwa ladha na ujio wa mama mchungaji ambae jina lake halisi ni Rehema.
"jamani Rehema twende basi nyumbani tunaaibika hapa dada Rehema" kwa sauti ya chini Ashura alimwambia mama mchungaji naye akamuelewa taratibu bila kuhoji akawaachia wakaongoza njia kuelekea nyumbani kwao maeneo hayo hayo ya uswahilini.
"he! Kumbe wanajuana jamani" washakunaku waliokuwa eneo hilo kushuhudia mpambano huo. Kila mmoja alibaki mdomo wazi wakati mama mchungaji,Zinduna na Ashura walivyokuwa wanatoweka ghafla tena kirafiki

"ni lini mmeniomba pesa nikawanyima? Mara ngapi mmetuma please recharge me nikajikausha eeh! Nawauliza nyie vibwengo msokuwa na haya hata kidogo" mama mchungaji alianza kuongea hayo baada ya kuingia katika kijumba kidogo walichoishi Ashura na Zinduna,midomo yake ilikuwa inatetemeka sana na macho yalikuwa mekundu.
"ujue shoga hatukuelewi hata kidogo" walisema kwa pamoja Ashura na Zinduna.
"ambacho hamuelewi ni nini hapo nyie wanafiki mlidhani sitajua?...haya ni shida gani mlipata hadi mkaziuza zile picha chafu nilizopiga wakati ule Maisha club,na Masai club na zile nyingine siku zile kwenye kitchen party Lango la jiji Magomeni" alijaribu kujieleza kwa sauti ya chini kidogo mama mchungaji ili aweze kueleweka mbele ya wawili hawa waliokuwa wanashangaa tu jinsi mama huyu alivyokuwa anapepeta mdomo.
"jamani jamani jamani,nani huyo anataka kutuchonganisha? Nani huyo anataka kuuvuruga urafiki wetu? Nani nauliza" Ashura alistukia na tayari akawa ameamka kutoka alipokuwa amekaa na kujishika nyonga zake.

Lilikuwa ni jambo la kushangaza sana na kwa jinsi walivyojieleza hatimaye mama mchungaji akaamini kuwa huenda kweli hawajui lolote.
"lakini ndo hivyo mwenzenu maji ya shingo tayari yamenifika huyo kijana aliyeleta hiyo barua ametoa maneno makali na kuwa ataisambaza picha yangu mbaya sasa hapo nitafanya nini mnadhani kama sio aibu ya mwaka,ni nyie tu mnaonifahamu kama Rehema huko pote naheshimika kama mama mchungaji hebu jenga picha ya hiyo aibu jamani" aliongea akiwa amekata tamaa kabisa mama mchungaji.
 
SEHEMU YA 28



"wasikutishe sana hao Rehema,cha msingi we onana nao na uwafanyie yale yaliyomsababisha yule diwani amwache mkewe unakuwaje wewe mbona mwoga? Au ndo dini imekukaa kichwani tayari?" alichombeza Zinduna aliyekuwa kimya muda mwingi.

"kwa hiyo Zinduna una maanisha ni....."
"ndio namaanisha hivyohivyo" alijibu Zinduna hata kabla mama mchungaji hajamalizia

"na tena inabidi iwe fasta fasta maana uzito wa hiyo aibu nina imani huwezi kuubeba,utaishia kujiua na sie bado tunakupenda shoga yetu,kuliko kujiua ni bora urudie enzi zako tu" alielezea Zinduna.

"mh! Kweli nitaweza jamani,imepita miaka kumbukeni" alijitetea mama mchungaji.
"utaweza tu ujuzi hauzeeki kamwe!!" alisisitiza Ashura.

***

"Nina mimba Oscar" ndio maneno mafupi lakini makali yaliyopenya katika sikio la Oscar kutoka kwa Noela,na ilikuwa imebaki siku moja mwenye mali (Timoth) aweze kurejea tena Dar-es-salaam.
Hakuweza kuficha hata nukta moja uoga wake wa waziwazi,
"Noela sasa itakuwaje,au unatania?" aliongea Oscar akiwa amekaa kitako katika kitanda.

"ndio maana nimekwambia ili tushauriane ehe! Niambie tunafanyaje sasa mpenzi wangu" alijieleza Noela.
"sina hata jibu moja la kutoa mbele ya suala zito kama hilo isitoshe wewe ni mke wa mtu" alizidi kujikanyagakanyaga Oscar wakati huo yupo mbali kidogo na Noela
 
SEHEMU YA 29


"kwa hiyo Noela nitafanyaje mimi hapo unadhani...eh! nitafanyaje?" Oscar alimuuliza Noela kwa sauti iliyotetemeka kwa uoga.

"kwa kweli hatuhitaji kukurupuka katika hili inabidi tujipange sawasawa" alijibu Noela.

"tujipange? Huo muda wa kujipanga uko wapi? Timoth anarudi sijui keshokutwa utamficha kwa staili gani?"

"haya we hilo niachie mimi na hofu ondoa cha msingi uwe thabiti sana na utoe ushirikiano" alijieleza Noela huku akitabasamu kwa mbali,Oscar hakumwelewa.

"sasa si uniambie huo ushirikiano nijue mapema kwa sababu Timoth akija sitapata muda wa kuongea na wewe kama ninavyofanya hapa"

"ushirikiano wenyewe ni ujiandae kulea mwanao!" alijibu Noela.Ni kama vile jibu lile lilimtia ganzi Oscar,aliamini kama Noela alikuwa hana utani basi labda hakumsikia vizuri.

"yeye ni bosi wangu,sina hata chumba cha kupanga,kamshahara kote natuma nyumbani,sasa nitaanzia wapi mie kuhudumia mtoto,nimekwisha mie Oscar na tamaa zangu,ah! Lakini mimi sikutamani si alinilazimisha kufanya ah! Ona sasa" alisema kimoyomoyo Oscar huku uso wake ukiwa umejawa na simanzi,haikuwepo furaha hata kwa mbali.

"Noela hivi unanipenda kweli?"
 
SEHEMU YA 30



"ningekuwa sikupendi ningekubebea huu mzigo"

"he! Kumbe umefanya maksudi Noela jamani sasa ndio nini hicho?" alilaumu Oscar.

"nimebeba bahati mbaya lakini nitailea maksudi Oscar nimekwambia ondoa hofu" alizidi kusisitiza Noela hakujua ni jinsi gani Oscar alikuwa amejawa uoga kwa tukio la kumpa mimba bosi wake ambaye alikuwa kwenye ndoa tayari.

"najua atatoka huko Mwanza na mahamu yake na mimi bila hiyana nampa hivyo hivyo,akijichanganya tu hii kitu inakuwa ya kwake kwa muda lakini ni yako milele" Noela alimwambia jambo hilo Oscar,ambapo kwa upande fulani lilisaidia kurejesha furaha japo kidogo.

"ngo ngo ngo ngo" ulisikika mlio huo kutokea sebuleni wakati Noela akiwa amekumbatiana na Oscar.
"he! Nani tena huyo" Noela alijiuliza haikuwepo kawaida ya kupata wageni katika nyumba yao tena ilisikika hodi iliyorudiwa rudiwa kuonyesha msisitizo.
***

Mama mchungaji aliondoka mitaa ya Temeke akiwa bado mwingi wa mawazo,mawazo yaliyohitaji umakini mkubwa katika kuyatatua. Katika mkoba wake alibeba kifurushi cha zana za kazi alizopewa na shoga zake Zinduna na Ashura,alikuwa hata hajafungua kuangalia kulikoni humo ndani.
Majira ya saa kumi jioni mama mchungaji alikuwa tayari amerejea kwake.
"sina njia ya ziada lazima nifanye kama walivyonishauri wenzangu labda ndio ponea yangu" mama mchungaji alijisemea wakati anaitua pochi yake kubwa kitandani.
"ngoja niwapigie waheshimiwa" taratibu mama mchungaji akachukua simu yake iliyosalia na kupiga namba alizopewa na Desmund siku ile kanisani.
"halo,nani mwenzangu" upande wa pili ulipokea na kuhoji. Mama mchungaji hofu ikamtanda akashindwa kujitambulisha.
 
SEHEMU YA 31


"we nani tafadhali namba yako ni mpya huku kwangu" sauti iliendelea kuhoji.

"ha ha ha ha ha ok! Hata kama hutaki kujitambulisha najua wewe ni mama mchungaji" kicheko na maelezo kutoka upande wa pili vilimshtua mama mchungaji.

"Mungu wangu amenijuaje!!" alijikuta akisema baada ya kukata simu kwa mshtuko.

Deo ama Desmund kama alivyojitambulisha kwa mama mchungaji alikuwa amejiandaa ipasavyo na aliamini janja yake itamleta mama mchungaji katika mstari anaoutaka yeye. Namba ya simu aliyoiandika katika kibarua kifupi alichokipeleka kwa mama mchungaji ilikuwa ni mpya kabisa na hakuna hata mtu mmoja aliyeitambua zaidi ya yeye (Deo) na mama mchungaji. Siku zilikatika bila mama mchungaji kupiga simu ile,Deo akaanza kuhisi huenda alikosea kuandika namba katika ile karatasi. Zilipita siku tatu matumaini yakizidi kufifia kuwa huenda mama mchungaji ameushtukia mchezo ndipo majira ya jioni ile simu ambayo alikuwa ameweka lain ya tigo anayoitambua mama mchungaji,mara simu iliita.Deo hakukurupuka kuipokea taratibu akainyanyua na kuhakikisha kuwa mpigaji wa hiyo simu alikuwa habip bali anapiga. Kwa uzoefu wa harakaharaka baada ya kupokea alizisikia pumzi za upande wa pili zilivyopishana kwa kasi."bila shaka ni yeye" alifanya utabiri wake kisha akaongea kwa kujiamini kama vile anamfahamu fika alizepiga hiyo simu.
Punde tu baada ya kufanya ubashiri wake alishtukia simu imekatwa,akiwa bado anajiuliza nini tatizo hadi simu imekatwa kwa mara nyingine tena iliita simu yake.

"samahani simu imekatika bahati mbaya"

"usijali hata kidogo una shida gani" alihoji Deo.

"mimi ni yule mama wa siku....." alianza kujieleza mama mchungaji lakini kabla hajamaliza alikatishwa

"nakufahamu vizuri sana,kwa nini umepuuzia maagizo niliyokutumia au ulidhani ni maigizo?" alihoji Deo kwa sauti iliyojaa hasira za kuigiza.

"samahani baba,nisamehe sasa lini nikutafute,nisamehe baba yangu" alijitetea mama mchungaji

"baada ya siku tatu nipigie simu nikueleze wapi pa kunikuta,ole wako upuuzie au utoe taarifa yoyote" alitoa karipio Deo.

"sitapuuzia mheshimiwa tafadhali nioneeni huruma hizo picha mimi nitajificha wapi?" kwa sauti iliyojaa majonzi na iliyobembeleza mama mchungaji alimjibu Deo.

"utanipa maelezo hayo siku tukikutana" alijibu Deo kisha akakata simu.
 
SEHEMU YA 32


"Oscar hiyo hodi ni kama ya mume wangu mh! Ingia uvunguni haraka tafadhali ukijidanganya tu kutoka tu,kwisha habari yetu" Noela alimwambia Oscar kwa sauti ya chini,jasho lilikuwa linawatoka kwa sana,kila mmoja alikuwa mdogo kama pilton,hakuna aliyekuwa mjanja mbele ya mwenzake.
Oscar hakupinga haraka akajiviringisha na kutosha chini ya uvungu wa kitanda walichokuwa wamelalia. Huku hodi ikiwa imetulia sasa,Noela alichukua haraka nguo yake ya kulalia akaivaa na kisha kwa mwendo wa kuigiza kuwa ametoka usingizini alianza kwenda sebuleni ambapo ndio hodi imetokea. Huku uvunguni,Oscar alikuwa hasumbuliwi hata kidogo na vumbi lililojihifadhi uvunguni,uoga uliziba pua zake na kuhisi hilo vumbi halikuwepo hata kidogo.
"eeh! Mungu niepushe na janga hili mbele yangu" Oscar alijikuta akimkumbuka muumba wake wakati wa matatizo.

Hatua za kurejea chumbani kwa kunyata zilizidi kumwogopesha Oscar maeneo ya uvunguni alipokuwa."huwa nasoma kwenye magazeti ya udaku juu ya mafumanizi sasa leo ni la kwangu nitakoma" aliwaza Oscar huku akijizuia kuzitoa pumzi zake kwa nguvu.

"Oscar bora uje mwenyewe tumegundulika tayari mi nilikukataza usije chumbani ukalazimisha" sauti iliyosindikizwa na kilio cha kwikwi ilisikika vyema katika masikio ya Oscar pale alipokuwa,alitamani iwe ndoto lakini ni kweli alikuwa chini ya kitanda cha mke wa mtu.
"siamini Noela amenisaliti yaani mimi ndio nilimlazimisha!! Dah! Nauwawa leo" aliwaza huku akiwa ameuma meno yake kwa hasira,mikono haikuwa na nguvu tena huku tumbo la kuhara likiwa limemshika tayari.

"huyu hapa yuko humo humo uvunguni amejificha" ilisikika tena sauti ya Noela kana kwamba kuna mtu pembeni anamwambia. Bila kujizuia papo hapo haja ndogo ikaanza kuchuruzika katika kaptula ya Oscar

Pensi yake ikiwa imelowana mkojo tayari Oscar alikuwa ameamua kutoka pale uvunguni ili akutane na adhabu aliyotakiwa kupewa na mwenye mali. Macho yake yalikutana na jambo asilolitegemea uso wa Noela ulikuwa umezibwa na kalenda kubwa kiasi ambayo kwenye moja ya tarehe ilikuwa imezungushiwa alama ilikuwa ni tarehe 17 mwezi wa 11. Oscar hakuelewa haraka maana ya tarehe ile hadi Noela alipotoa kalenda usoni huku akijizuia kucheka japo macho yake mekundu yalidhihirisha kwamba ametoka kucheka muda si mrefu.
"kuna nini Noela"

"happy birthday to you" alijibiwa

"kuna nini?" aliendelea kuhoji Oscar.

"ni siku yako ya kuzaliwa" alijibu Noela na kuangua kicheko kikubwa.

"na aliyekuwa anagonga mlango ni nani?"

"ni mlio nilioweka kwenye simu yangu hakuna mtu humu ndani"

"umeniweza Noela,yaani hadi nimejikojolea mwenzako" kwa sauti ya kinyonge alijibu Oscar huku akijitizama katika bukta yake jinsi alivyoilowanisha,wakati huo Noela alikuwa hacheki tena bali alimwonea huruma Oscar.
 
SEHEMU YA 33


Deo alijikuta hisia za mapenzi zilizokuwa zinamtawala tangu aone paja la mama mchungaji zilizidi ghafla akajikuta yuko wima akimkabili mama mchungaji aliyekuwa ameinama taratibu akichukua kanga yake,uoga ulikuwa kwa mbali na akajikuta tayari amekikamata kiuno cha mama mchungaji ambaye badala ya kushtuka aligeuka na kuikutanisha midomo yake na ya Deo,kighza tayari kilikuwa kimeanza kutawala pale ndani hivyo kilichangia wawili hawa kutokwa na uoga na aibu. Deo tayari alikwisha sahau mpango kabambe uliokuwa mbele yake hivyo aliamini alichotaka kufanya ni halali yake kabisa. Mikono yake tayari ilikuwa imezunguka katika kiuno cha Mama mchungaji,mapigo ya moyo ya Deo yalikuwa kasi sana joto la mama mchungaji lilikuwa limemchanganya Deo.

***

Kelele za hapa na pale kutoka chumbani zilimvuta Timoth kutaka kujua kulikoni na nini kinatokea humo ndani,giza lililokuwa mbele yake halikumtia hofu sana na aliamini hatua zake za miguu zitakuwa zitakuwa sawa kabisa hadi atakapoufikia mlango wa chumba kile.
"kuuuu!!!! Kaaaaa!!" ulisika mlio pale chumbani Timoth mbio mbio aliondoka kwa mshtuko mkubwa hakujua ni nini kinatokea pale ndani ulikuwa mlio mkubwa sana.
"puuu!"ulifuata mlio mwingine na safari hii alikuwa ni Timoth akiwa anasalimia na sakafu baada ya kujikwaa kwenye kochi lililokuwa limepangwa vibaya pale sebuleni. Maumivu makali aliyoyapata yalimsababishia kilio cha kimya kimya,licha ya kujikaza sana ilishindikana alikuwa ameumia sana goti lake pamoja na kifua chake. Akiwa bado anagumia kwa maumivu makali pale chini mara mlango aliokuwa anaufuata kwa ajili ya kujua kulikoni ulifunguliwa baada ya kimya kirefu kuwa kimetawala na hatua za binadamu zikaanza kusikika kuanzia mbali na sasa zilizidi kusikika kusogea eneo ambalo alikuwa ameanguka. Timoth alijaribu kuinuka lakini maumivu yalizidi kumweka pale chini.
 
SEHEMU YA 34


"Timo vipi kaka mbona upo hapa eeh!"

"kiajali kidogo kaka!" alijibu kwa sauti iliyojaa maumivu baada ya kugundua aliyekuwa anauliza swali lile ni Deo.

"Pole sana kaka lakini jikaze sasa uamke mambo tayari huko ndani,ebwana! Unasubiriwa wewe tu kuamua mwisho wa mchezo huu" alizungumza Deo kwa sauti ya kunon'goneza,maneno yale ni kama yalitibu majeraha na maumivu ya Timoth japo yaliongeza hasira zaidi kwa mama huyo ambaye aliamini mume wake ndiye anayefaidi mwili wa mkewe (Noela). Kama vile amepigwa shoti ya umeme aliinuka pale na kukaa kitako.

"hebu ongeza sauti ya redio nikupe mchakato sasa" Deo alimwambia tena Timoth ambaye tayari hamu zilikuwa zimempanda juu ya kulipiza kisasi. Timoth haraka haraka akaongeza sauti ya redio na kusababisha lugha ya kunon'gonezana ikome na kuwapa uhuru mkubwa wa kuongea.

"nimemwacha yupo pale kitandani sasa ni wewe kwenda kumtoa pale na kumweka chini sakafuni kwa sababu kitanda kile ni kibovu. Umenielewa" alitoa maelekezo Deo yaliyoeleweka vizuri kwa Timoth,kwa mujibu wa saa zao ilikuwa saa tano usiku.

"mimi hata bafuni sawa tu,nia yangu ni kulipiza kisasi" alijibu Timoth huku tayari akiwa wima.

"hakuna kuongea neno we ukifika ni shughuli tu sawa" alisisitiza Deo

"haina tatizo"

***
Deo hakuchukua muda mrefu kuingia katika majaribu joto la mama mchungaji lilimmaliza kabisa akajikuta palepale waliposimama akithubutu kuibanjua amri ya sita,mara wakahamia sakafuni,ujuzi wa mama huyu ulikuwa wa hali ya juu
 
Back
Top Bottom