Simulizi: JASMINE

JASMINE
MTUNZI BEBAS CUTELY .
SEHEMU YA 39 .
BOOKING 0756748557.

Hans alifurahi kama kabeba yeye vile hiyo mimba. Daktari alibaki kutabasamu " mnaelekea mnapenda sana". Hans alimuangalia Jasmine ambaye amekaa pembeni yake alimkonyeza . Jasmine aliona aibu na kugeukia pembeni .

Daktari aliwambia " ok mkapime vipimo vyote kumjua mtakingaje mtoto wetu" . Hans na Jasmine walikubari vizuri sana na kumshika mkono kwenda kupima . Walipima vipimo vyote kama baba na mama kumlinda mtoto wao na kupeleka kwa daktari.
Daktari aliwambia majibu yenu yapo salama usalimini nakumwambia" mkeo anaitajika kiriniki.

Hans alikubari na kumshika mkono Jasmine na kuondoka zake . Walifika nje Hans alimpa Zuri" mfikishe mama kijacho wangu nyumbani "yeye alipanda gari lake na kuondoka.

Nyumbani kwakina Hans mama Hans alíkuwa anawasiwasi kweli maana watoto wameondoka asubuhi sana awajarudi nyumbani . Baba Hans " awa awajarudi nyumbani ? aliuliza. Mama Hans" ndio awajarudi " . Najma aliingia" mimi na wambia kabisa yule mdada ni malaya kapata mimba anaogopa kurudi nyumba na kumchelewesha Zuri bure ".

Watu wote walibakia kuangaliana tu kwa maneno ya Najma anavyoropoka mbele ya wakwe zake ajui wala nini. Ilipita mida kidogo kama dakika tano Zuri na Jasmine waliingia wakiwa wameshika mkono . Zuri alimfuta mama ake kumiss mkono ndo kumsalimia na baba ake pia kumkiss mkononi na kumchukua Jasmine kutaka kuingia ndani .

Kipindi yupo kwenye ngazi kama atua mbili hivi Zuri na Jasmine. Najma alianza" hey mbona amjatupa mlejesho kuwa huyo house girl mjamzito". Watu wote walibakia kumuangalia tu Najma usoni anavyoropoka kama ayupo ukweni vile .

Zuri alimshusha na kumpandisha Najma "ni kweli lakini aikusu sababu ujanituma wewe na wala kuniagiza wewe aliyeniagiza ndo mwenye mamraka ya kupata hizi tàarifa" na kumchukua Jasmine kuingia chumbani . Najma alibakia yamemshuka adi miguuni na kukimbia chumbani kwake .

" Hiví kunasiri gani humu ndani ambayo inaendea mimi sijui na mbona Hans ukimwambia amfukuze Jasmine anakuwa mgumu hivi ? alijiuliza Najma . Alisema" sitakubari Jasmine abakie hapa nitafanya kila njia aondoke zake na Hans anirudie mimi tu.


********************

Jasmine aliingia chumbani kwake masikini akiwa analia" sasa nitafanyaje mimi kuficha aibu hii aya yote kayataka Hans " . Zuri " wewe usimsingizie kaka angu akukushikia pastora kulala chari pale mliyataka wote wawili na mle wote wawili" .

Jasmine alitabasamu tu " adi Zuri unanigeukia mara hii , aise kweli wifi anaga ushoga". Zuri alicheka sana " ebu tuzalie dume au jike acha mbambamba hapa ". Aliendelea kusema" unaogopa bure wenye mimba tumekubari tutalea sisi wenyewe sasa wewe uoga vipi ".

" Zuri mimi naona aibu isitoshe Hans ni mchumba wa mtu na baba na mama watanifikiliaje" alisema Jasmine. Zuri alimkumbatia" baba na mama awawezi kukataa damu yao ata sikumoja na wanajua Hans kapitia mitihani mingine na Najma adi kuamua kuingi mahusiano na wewe "..

" Hans sio malaya kama wanaume wengi kama aliweza kumvumilia mtu na kumuekea hadi nitakuoa tangia form three adi kamuacha juzi kavumilia sana naomba utuelewe , Hans anania njema na wewe awezi kukuterekeza mjamzito Jasmine " aliongea Zuri . Jasmine alijikuta akilia tu akiangalia kweli Hans mvumilivu sana na kamsaidia mengi sana , alimkumbatia Zuri na kulala .

Hans alirudi zake majira ya usiku kukwepa shobo za Najma. Asubuhi na mapema waliamka vizurii wakiwa na furaha sana na kufanya usafi wa nyumba nzima . Jasmine alitoka chumbani akiwa amechelewa kuamka na kuwakuta wezake wanatenga chai .

Jasmine aliona aibu kidogo Zuri alirudi akiwa kabeba supu na chapati . " Jamani hii supu ni mimi na Jasmine tu " . Hans alibakia kimya tu akimuangalia Jasmine kiwiziwizi tu .

Mama Hans " aya bhana subiri tupambane na chai na mikate yetu". Najma" sijui anampendea nini huyo Jasmine akati kazalilisha hii familia". Hans aliamua asimame aondoke chumbani bira kusema chochote . Zuri " umezidi mdomo ndo maana bwana kaondoka kwa kelele".

Watu walicheka adi mama na baba Hans waliamua kuondoka zao chumbani . " aise yule mwanamke ingekuwa amri yangu nisingekubari kijana wangu aoe ata kidogo " aliongea baba Hans . Mama Hans" bora umeyaona mwenyewe ningeongea mimi ooh mama mkwe motoni leo kiko wapi ".

Baba Hans alicheka " basi sorry mke wangu lakini ndio tuvumilie tu" . Mama Hans" Sawa " waliendea na kazi zao nyingine .

Siku zilizidi kwenda na Jasmine mimba ilizikidi kukua , Hans alizidi kumpenda baby mama wake uku watu. wakiwa wapokimya tu . Najma alizidi kuumia kuona mwezake kabeba mimba bira atua yoyote kuchukuliwa .

Najma alibidi ampigie simu Hamza bwana ake ili afanye uchunguzi Jasmine ajue histori yake . Hamza alimfanya upelelezi na kujua kuwa Jasmine alikuwa akijiuza danguro la madam Frida . Hamza alimpigia simu Najma na kumpa namba za madam Frida ambaye alitoka polisi kwa zamana na kuwa na alingumu ya Maisha.

je nini kitatokea .

itaendelea
 
JASMINE
MTUNZI BEBAS CUTELY .
SEHEMU YA 40
BOOKING 0756748557.

Najma alimpigia simu madam Frida na madam Frida aliomba waonane . Najma alitoka asubuhi siku hiyo bira kusema chochote na kwenda adi kwa madam Frida kumuona na kumtupia picha ya Jasmine. Madam Frida sababu njaa kali na anaishi nyumba ya kustiliwa pesa zote ana kakonda kama mgonjwa wa kwashako . Alipoangalia ile picha alimkumbuka Jasmine ndo sababu ya yeye kuwa masikini. " Yupo wapi huyu mtoto mpumbavu sana? aliuliza kwa hasira madam Frida.

Najma alitabasamu nakumwambia" huyu binti yupo naomba ukatoe ushaidi kuwa unamjua na aliwahi kujiuza kwenye danguro lako ". Frida alikubari " sawa ili kumkomesha Jasmine kama yeye alivyomkomesha " . Najma alitoa pesa kama laki mbili kumpa na kumuelekeza nyumba kesho aende . Frida alikubari sawa na Najma kuondoka zake.

Najma alirudi nyumbani na kumkuta Jasmine amekaa nje na wezake wakipiga stori. Alimshusha na kumpandisha kufonya bonge la fonyo na kuingia chumbani kwake . Hans alikuwa amesharudi yupo nyuma ya Najma akiangalia tukio zima . Hans alibaki kusikitika tu nakuwasalimia Jasmine na mwezake kuingia ndani .

" Hiví Hans ameachana Najma ? aliuliza Nasra . Rahma " mmmh labla maana naona tokea ile siku ya pete adi leo awaivainani " . Nasra " au kapata wifi mwingine nini ? aliuliza . Rahma alijibu'' kuna wifi mwingine zaidi ya Jasmine uoni mambo sio mabaya ". Jasmine " nyie aya bhana hii mimba nilibakwa sikuile nilivyotumwa ndizi na Najma".

" Mmmmh pole sana Jasmine ila Mungu atakutetea my dear " aliongea Nasra . Rahma na Nasra walienda kumkumbatia " tunakupenda sana Jasmine ". Jasmine alijikuta akilia " I love to you ". Walienda na mamboo yao mengi adi usiku ulipofika na kwenda kulala zao.

Asubuhi na mapema ilikuwa siku ya wiki end watu wote awaendi kazini na family ilikuwa ikipata chai. Najma alitoka chumbani na kuwakuta wezake wamekaa wakinywa chai na kumsalimia mama na baba Hans kuwambia kunamgeni wake nje amekuja .

Watu walikubari akamchukue mgeni wake na kuingia nae ndani. Hans alitoka kunywa chai na kuingia chumbani kwake kuchukua laptop yake . Najma alitoka nje na kumkuta Frida alimshika mkono na kuingia nae ndani kufika mlangoni tu alikutana na Jasmine .

Jasmine alipomuona madam Frida yupo pale alianza kutetemeka masikini na kujua kaja kumualibia . Najma " mbona unaniangalia sana ulijua sitojua ukweli kuwa wewe ni changudoa au vipi ? aliuliza . Jasmine alibaki kimya tu kumuangalia tu Najma aliondoka na kuingia ndani.

Najma aliwaita watu wote nyumba zima waende sebreni kuna kikao. Mama Hans , baba Hans , Zuri , dada wa kazi , Jasmine na Hans mwenyewe . Hans alipoangalia vizuri alimkuta madam Frida amekonda yupo pembeni ya Najma .


**********************

" Haa! kumbe huyu mpumbavu kaanza kunileta wapumbavu wezake kwetu eeeh anaondoka leo yeye na mpumbavu mweziwe " alijiongerea Hans. Hans " karibuni wageni " aliongea bira wasiwasi kakunja nne .

Madam Frida alibakia kumuangalia Jasmine" unanijua mimi ? alimuliza. Hans " ongea point yako ueleweke sio unanijua mimi tu utasahau vingine". Watu wote walibakia kucheka tu kwa maneno ya Hans .

Baba Hans" kimya " alitoa amri. Kila mtu alikaa kimya kumsikiliza muongeaji wao. Hans " karibu uendelee kuongea" alisema akiwa yupo busy na kuchezea simu. Madam Frida alibaki kumuangalia Hans ambaye mwenyezarau pale nakuendelea kusema" mimi nilikuwa miliki wa danguro lilokuwa posta na Jasmine ni mojaaa wapo alikuwa akijiuza danguro hapo na binti ni malaya sana afai atakurumagia kama mimi muongo mulize Hans alimpata wapi huyo binti ".

Najma aliingia "ndo maana kapata mimba kwa tabia yake ya kujiuza tu ". Jasmine alikuwa akilia kwa aibu na fedhea masikini.

" Hans ya ukweli yaliyosemwa ayo kuwa huyu binti amepatikana danguro ? aliuliza Baba Hans. Hans alijibu'' ndio baba , Jasmine nimepata danguro kweli kabisa ". Baba Hans " kwanini umeenda danguro kijana wangu "? aliuliza kwa hasira.

" I'm sorry dady nilishindwa kuvumilia feeling ambazo Najma alizonifanyia baba angu nikamua niende danguro kupunguza mawazo " aliongea akilia masikini Hans . Aliendelea kusema " nikiongea ni aibu sana Mzee wangu jinsi Najma alivyonifanyia mimi na Jasmine sio malaya kama mnavyofikilia nyie".

" Jasmine kama mwanaume amejifunzia kwangu na mimi ndo niliofundisha mambo ayo , Jasmine bado alikuwa yupo bikra licha na kukaa danguro kote nimetoa siku ile ambaye aliyotekwa na majambazi na chanzo ni Najma". Watu wote walibakia kumuangalia Najma na madam Frida akiona aibu.

Hans aliendelea " Jasmine ni mjamzito kweli ila mimba ni yangu mimi " . Najma alilia sana " Hans noo ukupaswa kunifanya hivi Hans" .

itaendelea .
 
JASMINE
MTUNZI BEBAS CUTELY .
SEHEMU YA 41
BOOKING 0756748557.

Hans alisimama na kumuangalia Najma chini adi juu " Najma nilikupenda sana mimi ukaniona sifai mbaya zaidi ulinizalilisha mbele ya wazazi wangu ukumu yako ni ondoka Najma kwangu ". Najma alibakia kumshika miguu " sorry Hans nisamehe mimi " ." Najma si umeshajenga teali ondoka kwenye maisha yangu na kwatarifa yako pesa zangu zote nimerudisha mwangu " .

Zuri " eeeh makubwa Najma adi kutubia tena ulikuwa unatuibia tena " aliingia chumbani na kumtolea nguo zote na kupeleka mabegi yake nje . Najma alichukua mabegi yake akuamini kuwa anaondoka kwenye chumbani nzuri kama ile . Watu wote walimcheka na kumjambisha " ilo kiko wapi sasa ".

Baba Hans" ufanye umuoe huyu binti sitaki tena maswala ya madanguro nyumbani kwangu ". Hans " sawa baba nimekuelewa na kumkonyeza Jasmine ". Baba Hans na mama Hans waliondoka zake wakimuacha Hans na mchumba ake wamekaa wakifurahi wenyewe na kukumbatia .

Najma alivyotoka pale alienda moja kwa moja adi kwa Hamza . Alipiga odi odi na kuja kumfunguliwa mlango na mwanamke ." Hamza yupo ? aliuliza . Mwanamke alimuangalia juu adi chini " baby kuna mgeni wako " .

Najma alibakia kushangaa ! baby tena , kidogo Hamza alitoka akiwa anadunduki mwenyewe. Hamza alimkuta Najma amekaa nje na mabegi yake " hey mbona unabegi vipi ? aliuliza. " Hamza nimefukuzwa na Hans naomba nipite" aliongea nakutaka kuingia ndani .

Hamza alimzuia asipite " toka nyumbani kwangu Najma ". Najma " hivi unaakili kweli Hamza nimekwambia nimefukuzwa ebu acha utani bhana " . Hamza alisema" nipo serious naomba utoke nyumbani kwangu , Najma mimi ni masikini niache nioe masikini mwezangu ambaye atanipenda na kunijari endelea kutafuta pesa ". Najma alimpigia kofi Hamza la shavu " Hamza kumbuka wewe ndo chanzo cha kunialibia kwa Hans mimi. Hamza " niumalaya wako uliyekutuma umsaliti bwana ako ondoka Najma". Najma alibakia kasimama " naomba nyumba yangu ".

Hamza alicheka" nyumba gani unayenidahi mimi ? aliuliza kwa zarau . " Ok nenda mahakamani sawa eeeh si unapesa eeeh " alimsukumiza na kumtupia mabegi nje . Najma aliondoka akiwa analia masikini akiangalia anapesa pesa zote kamuonga Hamza na Hamza kamgeukia . Najma alikuwa na mawazo sana naenda wapi mimi nitaishije ingawa sinapesa palepale kizungu zungu kilimshika na kudondoka chini kufa kwa presha .

Watu walienda kumkota Najma ameshakufa akiwa sehemu anamtu anayemjua na kuzikwa na serikali.

Upande wa Jasmine.
Jasmine aliolewa na Hans ndoa ya kitajiri sana viongozi mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi walikuja kuuzulia ndoa ya Hans. Walitunzwa sana vitu vya thamani sana na ndoa iliishia . Marafiki zake walifurahi sana Jasmine kuolewa na Hans.

Jasmine alijifunga mtoto moja wa kiume na Hans furaha ilizikidi kuwa kubwa nyumbani . Mama Hans alibidi awafunguze nyumbani kwake na wakajitegemea kutoka na Hans alíkuwa ajui kuna wazazi muda wote kubebika tu .


******************

BAADA YA MIAKA 2
" Sasa my wife kesho tenaenda mahakamani ili kudahi vitu vya wazazi wako" aliongea Hans . Jasmine " asante mume wangu Hans kwa yote uliyonifanyia" . Hans " sawa njoo tulale Amita ameshakuwa teali njoo tumtafutie mapacha".

Jasmine " ndo maana tulifukuzwa nyumbani kule sababu ukishinda nyumbani dah " aliongea akivua nguo moja moja na kwenda kulala. Hans alicheka sana" nikajua utaki utanibania ". Jasmine " ebu tufanye haraka haraka ujui Amita achelewi kuamka ". Hans alitabasamu" nakupenda sana mke wangu unastairi kuwa mama bora wa familia" . " Napenda pia baby mume wangu asantee kwa yote iliyofinyia " .Hans aliendelea kupunguza shibe ya chakula cha mchana maana alitoka kula.

Kesho yake asubuhi ilikuwa jumatatu Hans alienda moja kwa moja adi mahakamani kufungua kesi ya milasi ya mkewe na kuuzwa bila izini yake. Mahakama ilitoa amri aitwe baba na mama mdogo Jasmine wapelekwe kizimbani . Wakili wa Jasmine alifanya hivyo na kutoka kwenda kwakina Jasmine kuwapeleka karatasi ya mahakamani.

Mama mdogo Jasmine alishangaa ! baada ya kuona karatasi ile na yeye alikuwa kachoka kachakaa jasho la mtu alimuachia salama nakupokea barua . Wakili alitoka na kuwambia kesho ndo kesi yenu .

Baada ya miaka kumi na mbili .
Jasmine aliiuzwa na miaka kumi na sita adi sasa anamiaka 28 ndo wanakutana tena mama ake mdogo mahakamani akiwa kapeteza sana yupo na mume Hans . Mama mdogo Jasmine alipomuona Jasmine alimfata na kumpiga magoti maana alikuwa muhasirika wa ukimwi na bwana aliyekuwa nae alimtapeli pesa zote . Hans " hii kesi imefika vyombo vya sheria twende mahakamani" na kumchukúa mke wake kuondoka zao.

Mama ake mdogo aliingia adi mahakamani na kusomewa mashitaka yake. Alibidi akili na kuomba msamaha mahakama . Mahakama ilimpa kifungo cha miaka 10 kumi sababu mgonjwa na kuamuru amrudishie vitu vyake vyote vya ulithi . Mama mdogo alifungua pingu na kupelekwa gerezani .

Jasmine alikuwa akilia tu masikini kwani akuamini kuwa atampata mume bora kama Hans. Hans " na surprise nyingi mkewe wangu nataka nikimfanyie . Jasmine "ipi hiyo baby ? aliuliza. Hans " acha mchechetu panda kwenye gari.

itaendelea.
 
JASMINE
MTUNZI BEBAS CUTELY
SEHEMU YA 42.
BOOKING 0756748557.

Hans alimchukua Jasmine adi nyumba moja nzuri kiasi japo sio sana. Jasmine alibaki kushangaa ! " uku wapi mume wangu? aliuliza . Hans alishuka kwenye gari na kumshusha Jasmine kwenye gari.

" Usiogope niamini mimi " alisema Hans . Jasmine kwa vile yupo na mume wake alibidi ashike mkono na kwenda adi kwenye nyumba hiyo . " Hodi , hodi hodi " aligonga odi .

Mdada alitoka" ooooh brother Hans karibu ". Hans " asantee dada yupo ? aliuliza. Mdada " ndio yupo ila kalala. Hans " ok " nakumshika mkono Jasmine kuingia nae ndani . Jasmine akiwa anashangaa Mazingira kidogo yule dada aliingia chumbani .

Jasmine kipindi anashangaa! mazingira mwenyewe akiwa alewi alishangaa mtu anatoka chumbani akiwa anakohoa sana masikini. Jasmine alibidi amuangalie vizuri akuamini macho yake kumkuta Zawadi . Zawadi nae akuamini macho yake kumkuta Jasmine amependeza sana walikumbatia na kuanza kulia masikini .

Zawadi alilia masikini" mwezako nimeathirika na virusi vya ukimwi" alimuhadithia. Jasmine" pole sana usijali kuugua sio kufa rafiki angu " nakumfuta machozi. Jasmine na Zàwadi walijikuta wote wakimuangalia Hans .
" Asantee mume wangu kwa surprise nzuri uliyoniletea ".

Zawadi alijikuta akimpigia magoti Hans " sijui nikuite nani kwenye maisha yangu baba , kaka au Shemeji kwa uzito na wema uliyonifanyia. Hans alitabasamu " usijali shemeji yangu mtu mwema ulipwa kwa wema " .

Jasmine wawooow na kumkumbatia " baby sijutii kukupenda na wala sitamani mwingine zaidi yako ". Hans " usijali nakupenda sana my wife " . Zawadi " mdogo wangu Jasmine pls naomba usimuache Hans ana moyo wa pekee mimi naishi sababu ya Hans , nyumba nzuri sababu ya Hans mimi nilikuwa mtu wa mkufa " aliongea uku akiwa analia .

Jasmine " bàsi rafiki angu nakuaidi sitomuacha na kumuuzi adi kifo kitutenganishe ". Zawadi alitabasamu" nakumkumbatia rafiki ake na Hans alienda kuwakumbatia wote wawili .

The end .
 
[emoji1787]basi nitume ya saida Ile ndefu ndefu [emoji847]

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] we tuma bwanaa shida sio zako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…