Simulizi: Jinsi matatizo yalivonipeleka kwenye kisiwa kilichosahaulika

Simulizi: Jinsi matatizo yalivonipeleka kwenye kisiwa kilichosahaulika

DR SANTOS

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2019
Posts
12,846
Reaction score
28,106
Mwanzo


“Huyu tumuue kwani bosi amemleta huku lengo lake afe tu”.
“Hapana nafikiri kumuua sio jambo jema, kiubinadamu pia huyu ni mwanaume mwenzetu”
“Kibarua kitaota nyasi shauri yako,sasa unashauri nini”.
“Tumtupe kwenye maji tu akacheze na papa huko”

Mabishano hayo niliweza kuyapata vyema, yalipenya kwenye ngoma za masikio yangu barabara kabisa kwani hakukua na kelele yoyote ambayo ingeweza kufanya nisisikie kilicho zungumzwa zaidi ya sauti za mawimbi ya bahari ya hindi, pamoja na injini ya boti ambayo ilizidi kuchanja mbuga kwani mlio wa injini ulionesha dhahiri boti hio ilikua ikienda kwa kasi sana, baridi njaa kali pamoja na kiu vilizidi kuniandama.

Nikiwa kwenye chemba ndogo ya boti maalum kabisa kwaajili ya kuhifadhi vifaa vya ukarabati , pamoja na madumu ya mafuta na makorokoro mengine yaliyofanya chemba hio kuwa na harufu ya dizeli na mafuta ya petrol ambayo ilifanya mavazi yangu yaweze kunukia petrol vile vile.

Muda mchache baada ya mazungumzo hayo kusikika mlango wa chemba ile uliweza kufunguliwa na kijana mmoja ambaye kwa makadirio alikua na umri wa miaka ishirini hadi ishirini na nne, ambaye alinipokea kwa maneno ya kejeli “nataka leo nikupigishe stori na papa mzee baba”.

Aliongea kijana huyo ambapo sikutaka kubishana nae kwanza nilihitaji kukusanya nguvu pia kunyoosha viungo vyangu vizuri na ukizingatia nilikua sijaona jua kwa muda mrefu sana zaidi ya kukaa kwenye chumba chenye kiza kinene cha boti ile.

Tofauti na nilivyotarajia kijana Yule alizidi kunipa kejeli na sikujua kwanini alifanya hivyo kwani nilimuona ni mbwa tu tena koko aliyejishikiza kwenye utajiri haramu wa Mohamed bakantan.

Nilimtazama kwa hasira sana kijana Yule ambapo niliona akizidi kunishuhia maneno ya matusi, hakika kwa binadamu wa kawaida asingeliweza kuvumilia kabisa, kutukanwa na mwanaume ambaye anaona angeweza kummudu.

Nilimkadiria nikatazama na kamba walizonifunga niliwaona ni wazembe sana na sikutaka kupigana wala kujibizana na yoyote kwa chochote, nilichohitaji kwa muda huo ni kuhakikisha najitoa mikononi mwa Mohamed bakantan na timu yake.
“nifungue hizi kamba kama wewe ni mwanaume, nikuzibue”.

Niliongea kwa hasira nikimchimba mkwara kijana huyo ambapo hii ilipelekea apunguze kuongea kwani nilimtisha sana na aliweza kutambua mimi ni mtu wa aina gani, jua lilizidi kuwaka na kukomaa kabisa hii ilionesha ulikua ni wakati wa mchana.

Nikiwa sielewi nini hatma yangu,njaa nayo ilikua kama rafiki yangu wa karibu hakika nilikua na wakati mgumu sana, bado boti ilizidi kuchana mawimbi kabla ya kijana mmoja kunifuata na kunipa chakula nile ambapo ilikua ni mkate na soda kama kawaida na maneno ya kejeli yalihusika.

“Wewe fala kula kwa mara ya mwisho tutakutupa kwenye maji ukawe rafiki wa papa mkapige soga huko majinii mbwa wewe, ili siku nyingine uache kufuatilia mabinti za watu. Unajifanya unajua kupenda eeeeh”.

Sikuyajali maneno hayo nilichojali nimekula chakula ambacho niliamini kitaniongezea nguvu. Kwakua ilikua ni kipindi cha baridi kali kuna maeneo jua halikuwaka kabisa siku hio na kupelekea maji kuganda na kutengeneza miamba migumu ya barafu, boti yetu iligonga moja ya mwamba na kutoboka kupelekea maji yanze kujaa nayo kuzama taratibu.

Haraka nilijifungua kamba zile nilichojali ni kujiokoa nafsi yangu tu bila kusahau kumlipa fadhila Yule aliyenitukana
“wewe mbwa wa bakantan hebu kafie mbele, na utaliwa na papa leo nyau wewe”.

Baada ya kumaliza kumpa maneno ya kejeli nilijitosa baharini bila kusahau kubeba koti maalumu kabisa kwa kutozama majini, nikiwaacha wakiendelea kuhaha na boti lao.
 
Sura ya pili
ILIPOISHIA; Baada ya kumaliza kumpa maneno ya kejeli nilijitosa baharini bila kusahau kubeba koti maalumu kabisa kwa kutozama majini, nikiwaacha wakiendelea kuhaha na boti lao.

SASA ENDELEA; nilianza kuogelea huku nikiwa sijui naenda wapi kwani hakukua na dalili yoyote ya kupata msaada jua lilizidi kutokomea hii ilionesha wazi ilikua ni jioni na giza lilianza kuitawala dunia hakika sikua na matumaini ya kuiona siku ya kesho kwani nguvu zilianza kuniisha ilifika wakati nilikosa nguvu hata ya kuogelea.
Hapo ndipo nilanza kumkumbuka mpenzi wangu nasrita ambaye alinipenda sana na ndiye aliyenifanya niwe mahali hapo nilikumbuka jinsi nilivokutana nae kwa mara ya kwanza.

MIEZI MITATU ILIYOPITA.
Baada ya kuzuiliwa na walinzi kuingia kwenye party ya mtoto wa msanii mkubwa caty abdul ambaye ilikua ni siku yake ya kuzaliwa, nilitoka kinyonge nje ya geti la jumba kubwa lilopo maeneo ya mbezi beach nikiwa nime vaa kamera yangu na nyingine nikiwa nimeiweka kwenye begi dogo.
Nilitoka nikiwa na uso wa huzuni na kwenda kwenye mgahawa mmoja,mkubwa ulioko jirani na eneo lile, ambapo nilifika na kuagiza maji makubwa ili niweze kutuliza ghadhabu iliyoko ndani yangu juu ya wale walinzi wa geti ambao hata ningweza kuwadunda kwani walionesha kunidharau na kujivunia wadhifa waliopewa kwa siku hio.
Mhudumu baada ya kuleta maji baridi nilikunya funda moja lililoyafiksha maji hale hadi nusu hadi niliposikia kuitwa.
“kaka habari”.
“poa tu vipi!”
nilijibu huku nikimtazama aliyenisabahi kwa makini, hakika alikua binti mrembo mwenye uzuri wa kipekee alikua na hips zilizotanuka na kufanya gauni la kuvutika lililombana vema kuonesha umbile lake barabara kabisa kiasi kwamba mwanaume yeyote rijali angeweza kusisimka
“eti wewe ni mpiga picha? Nataka uwe mpiga picha wangu siku ya leo kwenye matukio yote ya kwenye party hii”.
“ndio mimi ni kamera mani lakini sina tiketi wamenitoa nduki mle na ndo maana niko hapa”.
Niliongea kwa upole sana huku nikimtazama ambaye alitabasamu usijali niko na kadi mbili tena za V.I.P ambapo name nilitabasamu kwani wale walinzi waliniharibia pesa nyingi sana kwani kamera ilikua ndiyo kila kitu kwangu na picha za tukio hilo zilikua ni za muhimu sana kwenye kazi yangu kwani nilitakiwa kuzituma kwa ripota mmoja wa gazeti ambaye angezitumia kuandika habari za udaku

Tuliinuka nakuanza safari huku tukimuacha kila mtu aliyekua eneo li
le mdomo wazi watu wengi walinishangaa wani binti niliyekua nae walikua wakimuona kwenye magazeti na televisheni lakini mimi sikulitambua hilo

Safari yetu iliishia mbele ya gari la kifahari aina ya Toyota athlete ambapo nilipigwa na butwaa kwani sikujua kama binti Yule angeweza kuwa na gari hapo nilianza kupata picha kwamba niko na mtu wa aina gani. Akili yangu iliwaza pesa tu kwa wakati ule kwani nilijua ningempiga picha nyingi pamoja na kumchukua pesa za kutosha.
Tulifika nje ya geti na kupiga honi ambapo mlango ulifunguliwa na tuliingia safari hii magari yalikua mengi sana tofauti na nilivoyaacha awali hii ilionesha tayari party ilishaanza. Tukiwa tunaingia nilimuuliza jina lake
“dada unaitwa nani”
“naitwa nasrita na wewe je”.
“naitwa rahim”.
Nilimjibu kwa kifupi na yeye alienda kwenye maegesho ghafla baada ya kushuka nasrita alistuka sana na nilimsikia akiongea mwenyewe
“mmmh alaphat yuko hapa, kafuata nini? Lazima ananitafuta mimi”.
“haaaa huyo alaphat ndiyo nani?” nilihoji nikiwa nishaanza kukingiwa na wasiwasi huku giza likiwa linaanza kuingia
“Ni mpuuzi Fulani hivi”.
Kabla nasrita hajaendela na mazungumzo alistushwa na swali lilitotoka upande wa nyuma
“nas huyo ni nani”.

Je nini kilifuata?
 
story yako inakosa uwasilia
Kwanza bahari yetu ya Hindi hakuna kipindi cha baridi ikaganda mpaka barufu
bahari yetu ina vipindi viwili kusi na kaskazi ni (vipindi vya upepo na shwari ☀️ Joto ☀️)
Pia kule baharini kuna mafungu ya mchanga na miamba

Kingine bora ungesema hao wabaya wako walikutesa na kukupa chakula pia wakakupa na maji na kuvisha life jacket na kukutupa baharini kidogo ungelete uwasilia fulani

Pia ukitunga story kama muhusika ni nini wewe pendelea sana kuwa chini yaaan wewe uwe mnyonge usipende sana sifa nimekushangaa sana inakuwaje mtu ufungiwe ndani zaidi ya masaa 24na chakula usipiwe umefungwa na makamba magumu unapata jeuri gani ya kumjibu mtesi wako na pia unapataje nguvu ya kuchukua boya na kujitupa baharini
 

Attachments

  • IMG_1902.JPG
    IMG_1902.JPG
    6.7 KB · Views: 28
story yako inakosa uwasilia
Kwanza bahari yetu ya Hindi hakuna kipindi cha baridi ikaganda mpaka barufu
bahari yetu ina vipindi viwili kusi na kaskazi ni (vipindi vya upepo na shwari ☀️ Joto ☀️)
Pia kule baharini kuna mafungu ya mchanga na miamba

Kingine bora ungesema hao wabaya wako walikutesa na kukupa chakula pia wakakupa na maji na kuvisha life jacket na kukutupa baharini kidogo ungelete uwasilia fulani

Pia ukitunga story kama muhusika ni nini wewe pendelea sana kuwa chini yaaan wewe uwe mnyonge usipende sana sifa nimekushangaa sana inakuwaje mtu ufungiwe ndani zaidi ya masaa 24na chakula usipiwe umefungwa na makamba magumu unapata jeuri gani ya kumjibu mtesi wako na pia unapataje nguvu ya kuchukua boya na kujitupa baharini
Kwani wapi nimesema stori yangu ni ya kweli
 
Njoo uendeleze uongo wako sasa mbona umeutelekeza?,Kumbe upo baki bencha unapiga chabo tu ila kuendeleza mpaka usifiwe?,Umeamua kuleta uongo njoo uumalizie
Wewe nioneshe wapi nimesema story ni ya kweli sio unakimbilia kuropoka tu apa 😳😳
 
Back
Top Bottom