Simulizi: Jinsi matatizo yalivonipeleka kwenye kisiwa kilichosahaulika

Simulizi: Jinsi matatizo yalivonipeleka kwenye kisiwa kilichosahaulika

Sura ya kumi na nne

ILIPOISHIA; “hapa uko brazil, kwenye kisiwa kilichosahaulika”. Aliongea malkia kauli iliyonifanya nistuke sana kwani sikutarajia kama ningekua brazili”.

“hmmm”. Niliishia kuguna tu kwani niliona maisha yangu yanakwenda kuishia kwenye kisiwa kilichosahaulika



SASA ENDELEA;siku za maandalizi zilikwisha na hatimaye siku ya kufanya uvamizi kwenye ufalme jirani iliwadia, hatukua na lengo baya zaidi ya kufuata vyakula tu.

Baada ya maandalizi yote kukamilika uliitishwa mkutano wa kutuaga na kututakia kila laheri katika safari ambayo ingetugharimu masaa arobaini na nane majini hadi kufika kwenye ufalme huo.

Tulipanda meli kubwa ya kivita ambayo ilikua na silaha za asili ikiwemo mishale ya moto pamoja na mafuta ya petroli, safari iliaza huku kila mmoja akitupungia mkono tukiwa tunaondoka na kukiacha kisiwa kilichosahaulika.

Majira ya usiku baridi ilikua kali sana iliyoambatana na upepo mkali wa bahari ilizdi kutuandama, sikuweza kuvumilia ijapokua nilikaa kisiwani pale kwa muda mrefu lakini sikiwahii huisikia baridi kama ile. Uzalendo ulinishinda kabisa kukaa juu ya meli na kuamua kushuka chini kwa lengo la kupumzika na kuiepuka baridi ile, si mimi tu bali kila mmoja aliyekua katika meli ile alitetemeka na ilitulazimu kukumbatiana lengo lilikua moja tu, kupata joto na hatimaye kila mmoja alipitiwa na usingizi

Tulikuja kuzinduka kukiwa kumepambazuka na jua lilishaanza kuchomoza, nahodha alichoka sana na alihitaji kupumzika, hio haikua shida nilipokea usukani na safari iliendelea, nikiwa naendelea kulisongesha jahazi alikuja sia ambaye ni mmoja wa wanajeshi na kunipa taarifa ambayo ilinistua kidogo

Hususani nilikua mgeni na masuala ya usafiri wa majini.

“mkuu kuna wanyang’anyi mbele yetu tufanyeje”. Aliongea sia kauli ambayo ilinifanya niachie usukani na kutoka hadi juu ambapo nilichukua darubini na kutazama,na niliona meli kubwa kuliko yetu ikiwa mbele yetu

“mwambie nahodha akate kona haraka tubadili uelekeo”. Niliongea lakini ni kama tulishachelewa kwani kombora kubwa lilitua kwenye meli yetu na kubomoa upande mmoja na kuifaya ianze kupitisha maji kwa kasi na kuanza kuzama taratibu.

Nilichanganyikiwa sana si kwaajili ya kuzama kwa meli bali sikua na uhakika kama ningeweza kusalimika kwa mara nyingine tena.

Na swali lilikuja akilini vipi kuhusu mabinti wale nilioongozana nao? Nikiendelea kujiuliza hayo tayari miguu yangu ilishaanza kuloa na maji baridi ya bahari kisha ,apaja yangu na kiuno kikafuata, niliamua kung’ang’ania ubao mmoja wa meli ambao ulinisaidia kuelea na nisiweze kuzama

Tayari wanyang’anyi walishafika mahali meli yetu ilipozama na walianza kuokoa mmoja baada ya mwingine ikiwemo mabinti niliokua nao msafara mmoja baada ya kuokolewa mabinti hao waliokua kumi na tisa kwa idadi name nilijisogeza maeneo ya meli ile ya wanyng’anyi lakini hawakuweza kununiona

Hakika niliona roho yangu ikiwa mkononi tena mkono usio na nguvu ambao ungeweza kuidondosha siku yoyote, saa yoyote na dakika yoyote

Pembeni ya meli ile kulikua na majina makubwa yaliyosomeka MOHAMED CARGO EXPORT LIMITED

“mungu wangu”. Nilijisemea moyoni na hasira iliwaka upya kwani nilijua bila shaka ni kampuni ya Mohamed bakantan na nilijua lazima ametoka kusafirisha mabinti kwenda kuwauza kwenye madangulo nje ya nchi.

Nilianza kukata mawimbi, kwa hasira iliyo kuu huku meli ile ikianza kuniacha, lakini niliamini ilikua ikielekea Tanzania hivyo niliogelea kufuata uelekeo wa meli ile hata iliponiacha sikukata tama nilizidi kunyoosha hivyo hivyo.

Nilichoka sana kuogelea, kwenye maji ya chumvi ambayo yalifanya macho yangu kuwa mekundu kama nimevuta kaya mbichi (bangi). Nilizidi kuogelea huku nikibadili mitindo mbalimbali ya kuogelea ambayo nilijifunza kisiwani ambako niliishi kwa muda mrefu sana ambao sikutambua ni ilikua miezi wiki au miaka.

Pumzi zilianza kuniisha kabisa mikono ilichoka na sikua na uwezo wa kuogelea tena, nilimuomba mungu aninusuru kwa mara nyingine kwani lengo langu ni kwenda kuwaokoa watu wengine na nafsi zao kutoka kwenye mikono ya Mohamed bakantan na nilipanga kumuadabisha mzee bakantan na kufichua maovu yake yote endapo tu ningeweza kukanyaga ardhi ya Tanzania.

Hakika hayo ni mawazo yaliyokitawala kichwa change huku baridi kali ikizidi kunipiga na nguvu zikizidi kuniisha,

kwa mbali niliweza kuona mwanga wa taa ya kandili ikija upande wangu, nami sikutaka kupoteza wakati nilizidi kukata mawimbi na hapo nguvu ziliniisha kabisa, kiza kinene kilitanda kwenye macho yangu.



Je nini kilifuata
 
Sura ya kumi na tano

ILIPOISHIA; Hakika hayo ni mawazo yaliyokitawala kichwa change huku baridi kali ikizidi kunipiga na nguvu zikizidi kuniisha,

kwa mbali niliweza kuona mwanga wa taa ya kandili ikija upande wangu, nami sikutaka kupoteza wakati nilizidi kukata mawimbi na hapo nguvu ziliniisha kabisa, kiza kinene kilitanda kwenye macho yangu.



SASA ENDELEA; Ilikua ni patashika nguo kuchanika katika jiji la dar es salaam kutokana na mauwaji yaliyokua yakiendelea na kupelekea amani ikosekane katika jiji la dar es salaam.

Kilichowashangaza wengi kila muuwaji anapoua, alikua akiacha chata iliyokua na herufi (RVM) wengi waliouawa waliachiwa alama hio kama ishara ya kwamba wameuawa na mtu mmoja.

“haloo kamanda, kuna maiti imeokotwa kigamboni, naomba msaada tafadhali”. Ilikua ni sauti ya kamanda mark ambaye alikabidhiwa jukumu la kufanya upelelezo juu ya matukio yanayoendelea.

Hakika ilikua ni kazi ngumu kumtambua mhalifu, kwani ilikua ni vigumu hata kutambua muda anaofanya mauaji zaidi miili ilikua ikiokotwa tu asubuhi na wasamaria wema.

mark akiwa ameketi jirani na eneo la tukio akisubiri gari maalum lije kubeba mwili uliojeruhiwa vibaya kwenye sehemu za kichwa na kuifanya damu igande kwani tukio lilififanyika muda mrefu uliopita, alitoa pakiti ya sugara na kuiweka mdomoni kisha kuiwasha ambapo alianza kuvuta sigara na kufanya tumbo lake lipande juu akivuta na lishuke baada ya kutoa moshi.

Aliendelea na zoezi hilo hadi alipobakiza kipisi kidogo ambacho alikikanyaga na buti lake kubwa, baada ya kumaliza aliangaza huku na kule, na kichwani aliendelea kuwaza na kuwazua ni jinsi gani ataweza kumpata mhalifu, na hakuweza kupata jibu lolote mwisho king’ora cha gari la polisi kilisikika



Pembeni mark alimuona kijana aliyevalia koti jeusi na kofia nyeusi iliosindikizwa na mwiwani myeusi, hakika haikua rahisi kumtambua kijana Yule, hata mark alishaanza kuingiwa na wasiwasi,juu ya kijana Yule kwani alikua akimtazama muda wote na pia walikua jirani lakini hakua amesema chochote.

mark hakua na budi kuondoka na gari la polisi lililokua limekuja kubeba mwili ule ambao hata kuutambua ilikua ni vigumu, lakini ulikua na chata ilioandiwa vizuri RVM.

“YALE YALEE”. Aliongea mark walipokua ndani ya gari la polisi wakati akiukagua mwili ule ambao ulikua umevaa prova lililoku na mifuko.

Mark alijikuta akiingiza mikono kwenye mifuko ya sweta hilo na kukuta karatasi iliyoandikwa maneno ambayo yalimstua kila mmoja.

“najua mtahangaika sana kumpata muuwaji, lakini niko pamoja nanyi katika kumdibiti Mohamed cargo export limited”.

Hakika baada ya kila askari kusoma ujumbe huo alipagawa na kuanza kutambua kwamba wanacheza na muuaji mwenye akili nyingi sana.

“simamisha gari mimi nirudi ufukweni”. Aliongea mark na hakuna aliyepinga gari lilisimama na mark akashuka na kupanda bajaji kurudi ufukweni ambapo alifika kwenye eneo alilokuepo Yule kijana ambaye awali aliweza kumtilia shaka, lakini hakumkuta,na baada ya muda mfupi mari alishangaa umati wa watu ukimfuata na kumwambia kuna mauwaji yametokea muda sio mrefu.

Mark hakua na budi kuelekea eneo la tukio, alienda na kukuta maji yamebadilika na kuwa ndani ya damu na juu ulioneka na mwili ukielea, alisaidiana na watu kuutoa mwili huo ambao ulikua umebandikwa karatasi, huku ukiwa na alama ile ile ya RVM.

Ujumbe huo ulisomeka hivi,



“ooooh afadhali umerudi, naomba askari mfanye kazi ya kufuatilia meli ya Mohamed ina watumwa ndani ambao wamekaa sio chini ya mwezi mmoja humo ndani”.



Moyo wa mark ulipasuka paa! Na alijaribu kuhusianisha matukio yaliyokua yakiendelea na kuona yalikua na muunganiko mkubwa sana, alikua akiyawaza hayo wakati ametulia sehemu moja ufukweni akiwa nanapata samaki choma na soda.

Baada ya muda gari la askari liliingia mahala pale na mark aliwashirikisha askari wenzake juu ya ujumbe ulitoka kwa muuwaji na mwisho walikubaliana kuvamia meli ile usiku na kuianyia ukaguzi wa hali ya juu.



Kazi iliyobaki ni kufuatilia kibali cha ukaguzi toka kwa mkuu wa jeshi la polisi bwana eif mmari ambaye hakuwa na hiyana ya kutoa arrest warranty kwa askari, baada ya kupewa kibali, mark hakuweza kulaza damu alichukua kikosi na kwenda kuvamia meli iliyokua ufukweni .

“wewe utakaa nje na utahakikisha unamkamata yeyote atakaejaribu kutoka nje, mimi nitaenda pamoja na makamanda wengine kwaajili ya kuwakamata, atakae kusumbua mpige risasi ya mguu”.



Aliongea mark na zoezi la uvamizi likaanza, hakuna kilichosikika zaidi ya milio ya risasi wakati huo mimi nikiwa jirani kabisa na eneo la tukio nikiwa na kamera yangu kwaajili ya kupiga picha ambazo zingekua ushahidi tosha kwa jeshi la polisi ili kumkamata Mohamed bakantan.



Je nini kilifuata.
 
Sura ya kumi na sita

ILIPOISHIA; Aliongea mark na zoezi la uvamizi likaanza, hakuna kilichosikika zaidi ya milio ya risasi wakati huo mimi nikiwa jirani kabisa na eneo la tukio nikiwa na kamera yangu kwaajili ya kupiga picha ambazo zingekua ushahidi tosha kwa jeshi la polisi ili kumkamata Mohamed bakantan.



SASA ENDELEA; nilizipiga picha hizo kwa umakini wa hali ya juu ijapokua ilikua ni usiku na nilihakikisha hakuna aliyekua akiniona.



MWEZI MMOJA NYUMA

“Jamani, kijana mzuri hivi nini kimempata”. Alisikika mama mmoja mjasiliamaji aliyekua akifanya kazi za kuuza samaki feli

“huyu atakua alijatribu kuogelea akashindwa na maji yalimpeleka mbali maana tumemkuta mbali sana akiwa hana nguvu kabisa ja[o alikua ni mzima”. Aliongea mmoja moingoni mwa wavuvi waliokua maeneo yale ya feli

Wakati huo nilikua chini nimelala mna maneno hayo niliyaskia kama ndoto yenye ukweli ndani yake. Hali ya ubaridi na upepo mkali wa bahari vilinifanya nipige chafya kadha wa kadha na hatimaye kuzinduka nikiwa natetemeka sana, ambapo wasamaria wema waliweza kunipa nguo na wengine chakula huku wakiniuliza ni nini kilichonisibu.

Sikutaka kuwaambia mazito niliyoyapitia zaidi ya kusema nilikua katika starehe zangu za kuogelea na nilishindwa na maji yalinipeleka mbali, watu walisikitika sana na hapo nilitumia njia hio kuomba nauli iweze kunirudisha nyumbani tazara kwani sikua na pesa hata mia.

Kwa msaada wao niliweza kupata pesa ambayo ilinitosha kupanda kivuko na kufanikiwa kupanda daladala ambazo zilinifikisha tazara. Kisha nilianza safari ya kuelekea maeneo ilipokua nyumba niliyokua nikiishi.

Nilishangaa sana kukuta kufuli kwenye chumba changu ambalo linaonesha lilifungwa muda mrefu uliopita, hapo nililazimika kumtafuta mwenye nyumba na kwakua sikua na simu nilienda moja kwa moja nyumbani kwake

“hodiii”. Nilibisha ambapo ndani ilisikika sauti ya kunikaribisha sikuingia hadi sauti iliporudia tena kunikaribisa

“karibuu”. Aliongea mwenye nyumba lakini sikuingia pia nilingoja atoke

“mungu wangu”. Ilikua ni sauti ya mama mwenye nyumba baada ya kuniona, ambapo almanusura azimie kisha alirudi ndani na kumuita mumewe mzee sentimbili

“haa, mwanangu rahim ulikua wapi miezi saba bila taarifa?” aliongea mzee sentimbili na kunifanya nitambue kwamba ni miezi saba tangu nimeondoka na kupotela kisiwani baada ya kutekwa.

“maisha baba binadamu wabaya”. Niliongea kwa ufupi na kuwaacha na maswali wenye nyumba

“karibu ndani mwanangu”. Aliongea mzee sentimbili ambapo sikusita nilikaribia

“ehee mwanangu ulipotelea wapi? Nilijua umekufa maana si kwa hali niliyoikuta ndani mwako pindi umeondoka ndiyo maana nikaamua kufunga mlango lakini cha muhimu nilivitunza vitu vyako simu pamoja na kadi zako za benki”.

Aliongea mzee senti mbili na kufanya uso wangu uchanue kwa tabasamu kwani niliona saa kisasi changu dhidi ya alaphat pamoja na mohamed bakantan kikienda kukamilika.

Baada ya kupata chakula nilimuomba anipe vitu vyangu ambavyo ilikua ni simu na kadi za benki, baada ya hapo tuliondoka na kurudi kwenye geto ambapo mzee sentimbili alifungua chumba na kuniambia niangalie kama kuna kitu kimepungua, nilimshukuru sana kwani nilikuta kila kitu kipo sawa godoro langu lilikuwepo na vitu vingine pia acha vile nilivyovihifadhi kwa Cuthbert.

Baada ya kukabidhiana chumba mzee sentimbili aliniambia amefanya wema huo kwa sababu alikua akinipenda sana na alinisihi niwe makini sana.

Nilikaa kwenye godoro ambalo lilifuka vumbi, sikujali hilo nilianza kutafakari mlolongo wa matukio yaliyokua yakinitokea kwenye maisha yangu, niliona kama ni ndoto na kama ni kweli basi mungu alikua upande wangu sana.

Nilifikiria hayo hadi usingizi uliponipitia na nilikuja kuamka majira ya saa tisa alasiri, ambapo nilipiga mihayo mingi sana na niliamua kwenda kupata maji ya kuoga.

Baada ya kumaliza nilijihisi kuwa fiti kuliko awali, uchovu ulipungua kiasi na nilihitaji kuwasha simu yangu.

Baada ya kuwasha nilikutana na jumbe nyingi sana toka kwa nasrita,na nilifarijika sana kuona ujumbe wa mwisho ulikua umetumwa asubuhi ya siku hio

“rahim, nimefanikiwa kujifungua mtoto wa kiume nijibu basi maana sio kwa kunisusa huko”.

Baada ya ujumbe huo nilishusha pumzi ndefu na kujiuliza maswali mengi sana lakini niliyapotezea, na kuamua kumjibu ujumbe nasrita

“hongera, muite clever”. Nilituma ujumbe huo ambapo hazikupita sekunde nyingi simu yangu iliita sikuipokea zaidi nilimwabia atume picha za mtoto.



Je nini kilifuata?
 
Sura ya kumi na Saba

ILIPOISHIA; “hongera, muite clever”. Nilituma ujumbe huo ambapo hazikupita sekunde nyingi simu yangu iliita sikuipokea zaidi nilimwabia atume picha za mtoto.

SASA ENDELEA; Sikutaka kujihusisha sana na nasrita mpaka mipango yangu ya kumsambaratisha Mohamed bakantan itakapotimia, baada ya muda uliingia ujumbe katika uwanja wangu wa whatsapp ulikua umeambatanishwa na picha za mtoto zilizotumwa na nasrita.

Nilizitazama kwa makini na kufarijika sana moyoni kwa kuweza kumpa ujauzito masrita ikiwa ni siku ya kwanza tu baada ya kufanya mapenzi.

Nilishusha pumzi ndefu na kutoka kwenye katika uwanja wa whatsapp kisha kuingia katika account yangu ya istagram ambapo nilikuta matukio mengi sana likiwemo la Cuthbert kupata ajali ya gari, moyo uliniuma sana na nilipanga kwenda kumtembelea nyumbani kwake mbezi, pia nilikutana na picha ambazo Mohamed bakantan amezituma huku akimpongeza alaphat kwa kufunga ndoa na binti yake miezi kadhaa iliyopita, hapo ndipo nilipopata picha ya kwamba nasrita alikua ameshafunga ndoa na alaphat muda mrefu, na mpango wa alaphat kuniteka ilikua ni kumuepushia aibu ya kwamba mkewe amezaa nje ya ndoa.

Mpaka hapo nilikua nishapta mahali pa kuanzia kulipa kisasi kwa alaphat na mzee bakantan,nilitoka kwenye uwanja wa instagram na kumpigia simu Cuthbert ambaye alishangazwa sana na simu yangu , simu iliita na kupokelewa,

“haloo wewe dogo upo kweli dunia hii”. Aliongea Cuthbert

“dah kaka ni stori ndefu sana nitakutembelea kesho hapo kwako”. Nilimwambia Cuthbert

“aise nimekukumbuka sana mdogo angu, karibu sana nyumbani”. Aliongea alaphat na mazungumzo yaliishia hapo, kwakua ilikua ni usiku nilitoka chumbani na kwenda kupata chakula mgahawani kisha kurejea chumbani ambapo niliwasha gemu na kucheza kidogo kisha kujilaza kitandani.

Nasrita hakuacha kunitumia ujumbe kila dakika lakini nilikua nikizipuuzia jumbe zake na nilipanga kutomtafuta hadi nikamilishe kazi yangu.

Asubuhi kulikucha na baada ya kuamka nilifanya usafi kisha kumpigia simu Cuthbert ambaye aliniambia niende nyumbani kwake kwani hakua na zamu ofisini siku hiyo.

Sikua na budi kuchukua pikpiki ambayo ilinipeleka hadi nyumbani kwa Cuthbert

“woow dogo” Cuthbert alinikumbatia kisha akanitazama mara mbili

“yes ndo mimi bro sema hapo kati nilipata matatizo ndo maana nikapotea mjini”. Niliongea

“oooh pole sana dg ndo maana nakucheki simu haipokelewi mwisho ukawa kimya kabisa but thks gd umerudi mjini tupige pesa”. Aliongea Cuthbert kwa uchangamfu wa hali ya juu

“pole kaka nasikia ulipata ajali”. Niliongea

“yes dogo si unajua shemeji yako ndiye aliyeababisha yote hayo, baada ya kushauriwa na mchepuko wake akaniwekea cocaine kwenye maji ya kunywa hivi nimemaliza dozi ya methadone mwezi uliopita, maana nilishakua teja”. Aliongea Cuthbert kwa hasira sana

“pole sana kaka nipe uelekeo sasa tunapigaje pesa”. Niliingiza mada za pesa

“yes dogo tena bora umekuja, unamjua huyu mzee bakantan?” alihoji Cuthbert

“ndio kafanyaje”.nIlihoji

“hapa kati kuna mtoto wa kigogo alipotea sasa jamaa anahusishwa na biashara za wanawake nje ya nchi polisi wanamfanyia uchunguzi”. Aliongea Cuthbert

“duh huyu mzee hafai lakini watamtia nguvuni tu njia ya mwongo fupi”. Niliongea huku nikiwa nishapata mahali pa kuanzia juu ya kuanza kumsaka mzee bakantan

Baada ya kuongea na cuthbert na kumaliza karibu siku nzima nyumbani kwake nilimuaga na kuondoka, nilipofika nyumbani nilijilaza na usingizi ukanipitia.

Kulipokucha asubuhi nilidamka mapema na kufanya usafi kisha kwenda kwenye minada ya nguo na kununua koti kubwa jeusi na kwa bahati nzuri nililipata pia nilinunua miwani pamoja na kofia nyeusi mwisho nilimalizia na kununua buti kubwa jeusi na kisha kurudi nyumbani .

Ambapo majira ya usiku nilibeba camera na kutoka kuelekea maeneo ya ufukweni ambapo nilikuta boti nyingi zikiwa zimetia nanga maeneo ya ufukwe, nami nilizipiga hatua zangu kuelekea ilipo meli kubwa iliyoandikwa Mohamed cargo export limited ambapo nilitafuta ngazi na kupanda juu kabisa, ambapo nilikutana na mlinzi aliyenizuia kuingia.

Sikutaka kuchelewa nilimpiga ngumi nzito na kumziba mdomo asije piga kelele, kwa mbali niliweza kusikia muziki ndani ya meli ile, haraka nilimsachi mlinzi Yule na kupata kadi ambayo niliitumia kufungua mlango mkuu wa kuingilia ndani.



Je nini kilifuata?
 
Sura ya kumi nane



Asante kwa kufuatilia kisa hiki Cha kufikirika kwanzia mwanzo mpaka sehemu hii ya mwisho.



ILIPOISHIA; Sikutaka kuchelewa nilimpiga ngumi nzito na kumziba mdomo asije piga kelele, kwa mbali niliweza kusikia muziki ndani ya meli ile, haraka nilimsachi mlinzi Yule na kupata kadi ambayo niliitumia kufungua mlango mkuu wa kuingilia ndani.

SASA ENDELEA;sikutaka yoyote anitilie shaka ndani ya meli kwani kulikua na anasa ya kila aina, madawa ya kulevya, pombe bangi pamoja na kamari, nilifika na kuagiza pombe kubwa aina ya dompo huku nikiendelea kusoma mazingira ya eneo lile, baada ya kukaa kwa karibu nusu saa niliweza kumwomba mhudumu anioneshe mahali maliwato yalipo ambaye alinipa kadi maalum ya kuingilia maliwatoni.

Nikiwa njiani niliweza kumwona mlinzi akiingia ndani ya maliwato nami nilimuwahi kabla mlango haujafunga, ambapo nilimpiga ngumi ya shingo iliyompeleka hadi chini.

“Mohamed bakantan yuko wapi?” .

nilimhoji yue mlinzi ambaye hakutaka kusema ambo ambalo lilinikasirisha sana na kumtandika buti la uso lililomfanya agalegale sakafuni.

“nakupa nafasi ya mwisho kuongea la sivyo shingo yako halali yangu”.

Mlinzi bado alionekana kua mgumu kumtaja mdosi wake hivyo niliinama na kuinyonga shingo yake kisha kupiga chata kwenye mwili wake kutumia kifaa maalum iliyosomeka “RVM”.

Kisha kuondoka haraka sana eneo lile kwani niliona hatari iliyopo mbele yangu kwani ni dhahiri shahiri wangeanza kunishuku.

Baada ya kushuka ngazi za meli ile sikutaka hata kugeuka nyuma niliondoka na kuanza kuzipig hatua ndefu kabla ya kukutana na gari jeusi aina ya mistubis outlander ambalo lilisimama na nilimuona mzee bakantan akishuka kisha wakafuata na vijana wengine ambao walitoa mfuko mkubwa ambao kwa mbali ilionesh ni maiti kisha kwenda kuitupa majini.

Hakika hasira iliwaka dhidi ya mzee bakantan na nilitamani nimmalize hapo hapo lakini sikua na namna zaidi ya kuondoka na kusubiri wakati wa mpango wa kumkamatisha bakantan kwenye mkono wa sheria.



Baada ya kufanikiwa kuzipiga picha za tukio zima la uvamizi wa meli, nilipanga kumtumia max mpelelezi mkuu aliyekabidhiwa dhamana ya kuchunguza sakata zima la mauaji yaliyokua yakiendelea jijini dar es salaam.

Polisi walifanikiwa kuwatia mbaroni watu watano baada ya wenngine wawili kujitosa majini, pia walifanikiwa kukuta kete za unga, bangi na mirungi.

Miongoni mwa watu waliokamatwa alikuwepo alaphat chande, moyo wangu uliridhika na kisha niliweka vizuri kamera yangu na haraka nilirudi nyumbani mbapo niliwasha laptop na kuzihamisha picha zote na nilizozipiga kabla.

Niliziambatanisha na kuzituma moja kwa moja kwa max mkuu wa upelelezi, baada ya hapo nilijiegesha kitandani hadi kulipokucha.

Niliwasha televisheni mbapo habari iliyokua ikiruka wakati huo ni kuhusu uvamizi wa meli ambapo licha ya polisi kuwakamata watu watano, walifanikiwa kuwaokoa mabinti ishirini ambao walikua si raia wa Tanzania, nilipata shauku ya kuwajua kwani nilihisi huenda walikua ni wale mabinti kutoka kisiwa kilichosahaulika.

Baada ya serikali kuruhusu mwenye chochote aweze kuwapelekea hospitali ndipo nilipoamua kwenda na nilistaajabu bada ya kukutana na mabinti wa kisiwa kilichosahaulika

Ambapo kila mmoja alionekana kulitaja jina langu, kana kwamba wananijua, watu wote waliokuwepo eneo lle la hospitali walistaajabu kwani mabinti hao hawakua wakingea Kiswahili lakini mimi niliweza kuwaelewa.

Taarifa zilifika kituo cha olisi ambapo nilitakiwa kuhojiwa juu ya mabinti wale wa kigeni hapo sikusita kuwasimulia mkasa mzima ulionikuta kadi kupelekea mimi kufika katika kisiwa kilichosahaulika, hakika ilikua ni simulizi ya kusisimua na hakuna ambaye aliamini kwamba kijana mdogo kama mimi ningweza kupitia mkasa kama huo.



Bada ya kupatikana na ushahidi wote alaphat alihukumiwa kifungo cha maisha jela, huku Mohamed bakantan akihukumiwa kunyongwa.

Kisha zilifanyika harakati za kuwarudisha mabinti hao katika kisiwa kilichosahaulika, nami sikua na budi kujiunga nao kwani nilitokea kulichukia jiji la dar es salaam na nilitamani kuanza maisha mapya katika kisiwa kilichosahaulika.

Hivyo nami nilitokomea katika kisiwa kilichosahaulika!



mwisho
 
unaweza skiza youtube kwa mfumo wa audio
 
Back
Top Bottom