Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Endeleza simulizi wewe acha manenoNi kweli kwani wapi ulishawahi ona nimesema Mimi ni mtu wa maana hapa jf?
Uliandika mwenyewe kwa kiherehere chako iweje usiimalizie?,Huoni kama unawatesa walioanza kuisoma?.Ni kweli kwani wapi ulishawahi ona nimesema Mimi ni mtu wa maana hapa jf?
Uliituma wapi?,mbona unasaundi sana wewe jamaa?hii simulizi mimi nachojua nilishaituma hadi mwishso ina episodes kumi na sita sasa sijui zilipotelea wapi ila poa tu ngoja nipekue pekue
Hapa sasa tutaenda sawa.Sura ya tatu
ILIPOISHIA; “haaaa huyo alaphat ndiyo nani?” nilihoji nikiwa nishaanza kukingiwa na wasiwasi huku giza likiwa linaanza kuingia
“Ni mpuuzi Fulani hivi”.
Kabla nasrita hajaendela na mazungumzo alistushwa na swali lilitotoka upande wa nyuma
“nas huyo ni nani”.
SASA ENDELEA; nasrita alinipa ishara ya kunikonyeza aliponigeukia kabla ya kumjibu alaphat ambaye hakuona jambo ilo.
“ni mpiga picha nimemchukua aweze kunipiga katika kila tukio ninalolifanya”.
“ujue wewe unaelekea kuwa mke wa mtu sasa inabidi uwe makini na masuala ya kujichangaya, na watu. Na mbona simu ya baba yako ulikua hupokei”.
Hapo niliona nasrita akijisachi simu na hakuiona niliona sura yake ikabadilika alike ni kama mtu aliyechanganyikiwa kabisa.
“na ulipoona nakupigia ukaamua kuizima kabisa, haya panda gari twende nyumbani haraka”.
Aliongea alaphat kwa hasira na nilimuona nasrita akitii bila kusema neno lolote lile. Kwa kua nilishachukua mawasiliano na yake na yeye kubeba yangu hakukua na shida yoyote, walipondoka nami niliingia ndani nilichoshukuru alikua alishanipa kadi ya mwaliko ya vip hivyo ningeingia ndani bila shida yoyote.
Nilipiga hatua na kufika mapokezi ambapo niliwakuta walinzi wale wale na safari hii walikuepo walinzi wanne,niliowanesha kadi waliikagua walipojiridhisha nilielekezwa mahali ambako vip walitakiwa kukaa
Nilifika na kuweka kamera zangu sawa kwa ni lengo langu halikua kukaa bali kupiga picha za caty abdul ambazo zingeniingizia pesa nyingi sana endapo ningekamilisha kuzipiga na kumpelekea Cuthbert mpangala mhariri wa magazeti pia mtu wa madili ya hatari ambaye aiweza kuijua kompyuta na editing vilivyo.
Baada ya tuki kuanza nilihakikisha nakua makini sana na umpiga picha caty abdul hususan alikua amelewa hivyo niliona ni fursa kwangu kumpiga picha za matuki ya ajabu ajabu aliykua akifanya ikiwem kunesha maungio yake hadharani na kukatika viuno hovyo.
Niliona hilo halitoshi niliamua kuchukua na mkanda wa video baada ya kuona tukio linaelekea kumalizika sikutaka kusubiri hadi tukio limalizike nilitoa memori kadi iliyokua kwenye kamera na kuihamishia kwenye simu yangu na kisha kuingia whatsapp ambapo nilimkuta Cuthbert akiwa hewani aani online
“oya mambo vipi”. Nilituma ujumbe ambap haikupita muda nilina maneno typing…. Ambapo nilikaa kusubiri ni nini Cuthbert anaandika
“oya kaka kawa umefanikisha?”. Alihoji Cuthbert
“aaaaah si unajua mambo yangu, nishamaliza na hivi sasa ndo natka kwenye party”.
“ok tuma basi”. Aliongea Cuthbert ambapo niliingia gallery na kumtumia picha nyingi sana pamoja na videos zote za tukio”.
“sasa dogo hii ni pesa ningi sana ngoja nianze kazi mapema”.
Aliongea Cuthbert na kisha baada ya muda meseji iliingia kwenye simu yangu iliyo andikwa tigo pesa imethibitishwa umepokea kiasi cha shilingi laki mbili
Sikutaka kufuatilia kwani nilijua lazima atakua Cuthbert amenilipa kutokana na kazi niliyoifanya. Nikiwa natoka nje niliona boda boda na nilimwita dereva ambaye akuremba mwandiko alikuja nipeleke tazara ilikua ni safari iliyogharimu takribani dakika ishirini kwani hakukua na foleni yoyote tulifika na nilimlipa dereva na safari ya kwenda geto iliwadia
Niliwasili majira ya saa saba usiku nilifika na kuoga kissha kuichukua simu yangu ambapo nilikutana na jumbe kadhaa ikiwem ya tigo pesa kwa mara nyingine jina la Cuthbert lilikuja ikionesha amenitumia kiasi cha shilingi laki mbili na nusu.
Swali likaja je ni nani aliyenitumia laki mbili ya awali kwani akauti yangu ya tigo pesa ilinesha nina kiasi cha shilingi laki nne.
Nikiwa naendelea kupitia meseji niliona ujumbe uliotoka kwenye namba ngeni.
“kesho tukutane royal hotel saa saba mchana, ni mimi nasrita”.
Nilipousoma ujumbe hu nilishusha pumzi zangu kwa nguvu kisha nikaurudia na kuna hakuna kilichobadilika.
Je nini kilifuata.