Sura ya kumi na mbili
ILIPOISHIA; Nilikaa juu yake tayari kwa kumkabili roda kabla siza na anne hawajarudi, na hilo lilifanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani baada ya kufanya yetu ya kikubwa na roda ambaye niliula uroda wake, mlango wa chumba kile ulifunguliwa na aliingia mwanamke mrembo aliyevaa kidani cha malkia kichwani.
SASA ENDELEA; roda aliinama huku ameshika kifua chake kama ishara ya salamu kwa malkia huku akiongea maneno ya kikabila ambayo ndiyo ilikua lugha ya eneo lile.
“habari yako kijana”. Alinisalimu malkia ambapo nilimjibu huku nikiona aibu na kuficha mkuyati wangu uliokua ukibembea kwani sikua na nguo yoyote malkia aliliona hilo na aliagiza nitengenezewe nguo mara moja.
“salama tu, nashukuru sana kwa msaada wenu wa kusaidia maisha yangu”. Niliongea kwa umakini sana na kumfanya malkia Yule anitazame kwa umakini pia.
“usijali, lakini mshukuru mungu wetu aliyekuokoa maana sisi hatuwezi chochote”. Aliongea malkia hukua akiinama nilipo na kunishika mkono kisha kuniinua, wakati huo nguo zilishaletwa ambazo ziliziba sehemuz angu za siri pekee.
“twende nifuate”. Aliongea malkia ambapo tulianza kuongozana nikiwa pembeni ya malkia na nyuma walikuwepo wanawake wanne ambao walikua na jukumu la kumlinda malkia.
Njiani tukiwa tunaelekea hekaluni, nilishangaa kupewa heshima ya hali ya juu lakini nilijua huenda ni kwasababu ya malkia, niliyekua nimeongozana nae.
Tulifika nje ya mlango wa hekalu lililonakshiwa kwa michoro na uremboo mbalimbali, lakini ajabu sikupata kumuona mwanaume hata mmoja, zaidi ya kukutana na mabinti warembo kila kona tuliyokua tukikatiza, hali hio ilinifanya nijawe na maswali mengi kichwani kuhusu eneo lile abao sikutambua ilikua ni nchi gani au bara gani. Tayari nilishaanza kuingiwa na wasi wasi endapo wanawake wote watanitaka itakuaje, wangeweza hata kuniua.
Lakini niliamua kupiga moyo konde na kuendelea na safari hadi nilipoambiwa na malkia niketi, na baada ya kuketi malkia alitoa agizo kwa vijana wake
“atakua ana njaa sana, leteni chakula cha kutosha”. Baada ya kusema hivyo mabinti hawakuchukua muda mrefu walilleta chakula pamoja na matunda ya kutosha. Nilifakamia chakula kile hususani nilikua na njaa ya shilingi elf kumi, kama sio bilioni moja kabisa. Baada ya kutosheka na chakula nilikaa hadi niliposikia sauti ya malkia ikinisemesha
“natumai tunaweza kuongea sana”. Alianza mazungumzo malkia.
“ndio malkia wangu”. Niliongea kwa upole
“hiki ni kisiwa kilichosahaulika, kwani hakijawahi tembelewa na mtu yeyote Yule na hata tumeshangaa kukukuta hisiwani ukiwa huna fahamu”. Aliongea malkia na hapo ndipo nilianza kupata picha na lait kama kissiwa hicho kingelikua kwenye ramani ya dunia basi vijana wote wangekwenda kule kwa lengo la kubeba wanawake wazuri wa kuwaoa.
“mbona sijapata kumuona mwanaume hata mmoja maeneo haya”. Nilihoji
“kijana wangu, ni hadithi ndefu sana lakini nitakusimulia kwa sababu umetaka”. Aliongea malkia na kisha kuanza kusimulia.
Miaka mingi iliyopita, kisiwa hiki kilikua chini ya utawala wa familia Fulani ya kifalme ambayo iliendesha utawala wake kwa mabavu huku ikiwapa kipaombele wanaume zaidi. Wanaume walionekana ni muhimu kuliko wanawake na kupelekea kutokua na usawa katika kisiwa hiki
Wanawake walifanyiwa vitu vibaya ambavyo wanaume walijisikia ikiwemo kubakwa, na kulazimishwa kuolewa, kupigwa pamoja na kufanyiwa udhalilishaji wa kila aina.
Alitokea binti mmoja, shujaa nasema shujaa kwa sababu ndiye aliyeweza kufanya mapinduzi ya kuwatoa wanaume wote kisiwani hapa, alikua ni shupavu, na hodari katika vita.
Hakika tunaishi tukimuenzi sana katika kisiwa hiki.
Baada ya malkia kumaliza kutoa historia hio fupii tuliendelea na mazungumzo na malkia
“na mnawezaje kuishi bila ya wanaume, pia vipi kuhusu usalama wendu hapa endapo akitokea mvamizi”. Nilihoji
“tunalo jeshi na maadui wetu wakubwa ni wanaume tuliowatimua katika kisiwa hiki, mara nyingi huja na kufanya uharibifu pia kuchukua wanawake kinguvu”. Aliongea malkia
Ambapo baada ya muda kelele zilianza kusikika nje ya hekalu lile ambapo malkia alichungulia kupitia dirishani na kisha akasema
“tayari kumekucha”. Nikiwa naendelea kuzubaa nilikoswa na mshale uliopita pembeni yangu
Je nini kilifuata,