Kushoto kabisa mwenye masharubu ni hayati jeneral Waden Marwa{kamanda kambale}aliyekuwa na uwezo kusafiri hadi Kampala na kurudi bila kukamatwa na Nduli AMINI, akapewa jina la Kambale kwa uwezo wake huo,akifatiwa na jenerali Mayunga Sailas{kamanda mti mkavu kwa tabia yake ya kutembea na mkongojo mkononi kila alipo}.
Anayefatia hapo baada ya Msekwa ni jeneral David Musuguli{kamanda Mutukula}aliyekuwa mTz wa kwanza kuingia nchini Uganda kwa mbwembwe akivuka vitongoji vya Mtukula tena mchana kabisa huku akitafuna muwa alioupata kwa kuvuna kutoka shamba la serikali ya kijiji},,anafatia ni Rais mteule Geofrey Kakongwa Binaisa aliyeteuliwa Rais toka kuwa mwanasheria mkuu wa serikali ya Uganda,baada ya hayati Lule kugombana na hayati Mwl.
Anayefatia ni aliyekuwa mkuu wa majeshi ya Tz hayati Twalipo,aliyerudi nyumbani Tz baada ya picha hii, baada ya kuteuliwa kuwa mkuu wa majeshi ya Tz wkati huo.