Habarini za kutwa wanajamvi ,bila shaka wote mko bìèn!. Kwanza kabisa nianze kwa kusema ninayo mikasa miwili ambayo nimewahi kuishuhudia kwa macho yangu na kuifanya kwa mikono yangu mwenyewe,mkasa wa kwanza ulituhusu mimi na ndugu zangu ambapo wakati huo nikiwa nina miaka 14 - 15 mwaka 2000 -...
www.jamiiforums.com
Kwangu Mimi hii ni the best kuliko zote,japo jamaa alizingua hakumaliza nadhani kutokana na ujuaji mwingi was watu.
Ni stori ya kweli.
Sijawahi vutiwa kusoma stori,
Hata hizo alizoweka jamaa pale juu nilijaribu kusoma nikashindwa .
Lakini hii ndiyo stori pekee niliyoshawishika kuisoma mstari kwa mstari.
Habarini za kutwa wanajamvi ,bila shaka wote mko bìèn!. Kwanza kabisa nianze kwa kusema ninayo mikasa miwili ambayo nimewahi kuishuhudia kwa macho yangu na kuifanya kwa mikono yangu mwenyewe,mkasa wa kwanza ulituhusu mimi na ndugu zangu ambapo wakati huo nikiwa nina miaka 14 - 15 mwaka 2000 -...
www.jamiiforums.com
Kwangu Mimi hii ni the best kuliko zote,japo jamaa alizingua hakumaliza nadhani kutokana na ujuaji mwingi was watu.
Ni stori ya kweli.
Sijawahi vutiwa kusoma stori,
Hata hizo alizoweka jamaa pale juu nilijaribu kusoma nikashindwa .
Lakini hii ndiyo stori pekee niliyoshawishika kuisoma mstari kwa mstari.
Huyu lwanda Magere yuko radio free Africa akisimulia hiki kisa kila jumapili SAA nne. Kamili asubuhi Mimi naendelea nae...majamaa walikuwa wanachonga mpaka lwanda akaikatisha dohh
Story za kweli ndiyo zenyewe, binafsi na story ya kweli kwenye life yangu ila sijui kuandika, kuandika ni upako aisee, na hivi watu wanajua kuzodoa nitishia episode 1 tu.
Story za kweli ndiyo zenyewe, binafsi na story ya kweli kwenye life yangu ila sijui kuandika, kuandika ni upako aisee, na hivi watu wanajua kuzodoa nitishia episode 1 tu.
Habari wapendwa? Poleni na jukumu zito la ujenzi wa nchi yetu nzuri ya Tanzania. Ama baada ya salamu niende kwenye maada moja kwa moja. Leo nimeona nilete simulizi kumi kali nilizowahi kusoma hapa JF. Haimaanishi kwamba hizi ndio bora kuliko zingine ambazo sijazitaja hapana bali nimeamua tu kushare hizi chache na nyie mpate kuburudika kama ni mpenzi wa masimulizi najua zipo zingine kali sana nawewe pia sio vibaya ukitaja hapa nasisi pia tupate kuburudika.!
Karibuni
10.Goodness of fit:Love,Loyalty na Betrayal
Shukurani kwake KigaKoyo kwa hii simulizi niliipenda sana hasa namna anavosimulia inavutia sio siri. Anazo simulizi zingine kali lakini kwangu hii niliipenda zaidi.
Ladies and gentlemen, its me again. The creater of stories like “How I met my wife” na “Cheaters: the series”. Nakuleteeni Goodness of fit. A story of love, blackmail, betrayal and politics. Pamoja na kua moderators wamekua wananyofoa nyuzi lakini naona mwaka huu wamelegeza kidogo na kutoa...
www.jamiiforums.com
9. THE LAST SUMMER IN TANZANIA
Kutoka kwa mtunzi Nyemo chilongani hii simulizi ni habari nyingine kabisa nazani bongo movie wamtafute huyu jamaa wafanye nae kazi trust me it will pay more! Asante kwa Abdallahking kwa kuileta hapa JF.
SIMULIZI HII IMEKAMILIKA IMEANDIKWA NA : NYEMO CHILONGANI CHANZO : BURE SERIES SEHEMU YA KWANZA Matangazo yalikuwa yamebandikwa kila kona ndani ya Jiji la Dar es Salaam yaliyokuwa yakihusu ujio wa mjasiriamali mkubwa, Potter Mickey aliyejulikana duniani kote kutokana na mafundisho yenye nguvu...
www.jamiiforums.com
8.MSAKO WA HAYAWANI
Hii ililetwa na idawa lakini mtunzi ni Eddie Ganzel. Najua wahenga mnayo mengi kuhusu huyu mtunzi alikua balaa. Alale pema peponi.
KAMBI YA NDALA. MWANGAZA hafifu wa mapambambazuko uliwafanya Luten Dennis Raymond Makete na wenzeke waonekane kama vivuli.Walikuwa katikati ya msitu wa Ndala wakienda mbio za mchakamchaka. Wote walikua katika vazi kamili la kombati,bunduki mkononi ,mkoba mgongoni. Rekuruti au...
www.jamiiforums.com
7.SAFARI SABA ZA SINBAD
Hii ni simulizi ya kusisimua sana hasa inatukumbusha kua tusikate tamaa kwenye maisha. Ni kisa cha kale kilicholetwa hapa JF na mkuu Bujibuji. Itafute utafurahi
SAFARI 7 ZA SINBAD BY RAJABU ATHUMAN SAFARI SABA ZA SINBAD SAFARI SABA ZA SINBAD Katika nchi ya Baghdad kulikuwepo na kijana aliyejulikana kama Sinbad mbeba mizigo. Kijana huyu alijaaliwa kuwa na uwezo mkubwa wa nguvu za kuweza kubeba mizgo. Pia alikuwa na uwezo mzuri wa kiakili. Sinbad...
www.jamiiforums.com
6. PENZI LA MFUNGWA
Kwa wale wapenzi wa masimulizi huko FB jina la mtunzi Alexis wa milazo sio geni ila ilieletwa humu na Sharobaro la jf. Simulizi ya kichawi inayosisimua sana.
Wakuu karibuni katika riwaya hii inayoitwa 'Kijijini kwa Bibi', au 'mnyonya damu', kama ambavyo wengine hupenda kuiita. Mtunzi wa riwaya hii ni yule yule wa 'Mkono wa Chuma' na 'Sala ya Sarah', Alex Kileo. the Legend☆
www.jamiiforums.com
4. TAI KWENYE MZOGA
Kama unapenda simulizi za kijasusi basi hii n "baba lao". Bonge moja la riwaya toka kwa mtunzi nguli wa stori za kipelelezi muite KELVIN e. MPONDA ama jasusi kama yeye mwenyewe anavopenda kujiita. Shukurani kwake the banker kwa kiluleta huu uhundo hapa JF. Ukipata muda kaipitie utanishukuru nakwapia.
Wadau kama nilivyoahidi leo naanza kuishusha riwaya ya tai kwenye mzoga mpaka mtunzi atakavyonielekeza tofauti. Mtunzi wa riwaya hii ni yule yule KELVIN e. MPONDA. Wasiliana naye kwa namba 0688058669 VITABU vya TAI KWENYE MZOGA, MIFUPA 206 na UFUKWE WA MADAGASCAR sasa vinapatikana sehemu...
www.jamiiforums.com
3. BAO TATU ZA MGENI
kama unazani ni zile bao za chota chama wa simba au za saidoo yule wa yanga basi unakosea sana. Hapa kuna mwamba alipiga mabinti wa watu mimba karibia kijiji kizima. Yaani alikua anakula tunda kimasikhara sana. Wanawake walidata na bao tatu za mgeni. Chombezo hili ni balaa la mtunzi Jack Mambo lakini lililetwa hapa na madau wa kuitwa Dampa. Isome utafurahi mwenyewe ila kama hauna mpenzi bro! My sister chunga sana utajikuta upo ngome kongwe ya CHAPUTA.
Chombezo………….BAO TATU ZA MGENI! Umri…………………..18+ Sehemu ya 1 Ngurumo na radi vilitawala,huku wingu zito likitanda,ilikuwa ni dalili kuwa muda wowote mvua itanyesha,tena siyo ya rasharasha ilikuwa ya uhakika! Muda huo ndiyo nilikuwa nimeshuka kwenye basi lililonileta mpaka Sumbawanga,ilikuwa...
www.jamiiforums.com
2. ANGA LA WASHENZI NA JOANA ANAONA KITU USIKU.
Ohoo! Unawajua washenzi kweli wewe? basi tulia usije ukaniuliza kwani washenzi wenyewe wanasemaje? Hilo swali tayari mtunzi kichwa SteveMollel alishalijibu. Hii ni moja kati ya stori za hapa JF iliyonifanya nikeshe usiku kucha kuisoma maana ni full mzuka ndo maana Zuchu alipoisoma akajua utamu wake balaa tupu yaani ni su..ka..ri. Sugar sukari!!!...
Uzi huu utakuwa mahususi kwa ajili ya kutuma simulizi hizi mbili kwa wapenzi wasomaji wangu. Simulizi hizo nazo ni: ANGA LA WASHENZI na JOANA ANAONA KITU USIKU mpaka vikomo vyake. Karibu tufurahie.
www.jamiiforums.com
1. PENIELA
Hili dude nililisoma hapa mwanzoni mwa mwaka 2017 hakika ni hadithi ya kiwango cha nyota maana iko juu sana. Ndio ilinifanya nianze kupenda hadithi za kipelelezi heko kwake PATRICK CK. nazani wadau wadau wa JF tulipaswa kutoa tuzo kwa huyu mtunzi maana hii simulizi iliyotikisa zaidi anga la wasomaji hapa JF hadi neno "alosto'' likaingizwa kwenye urahibu wa kumiss simulizi. Kama unazani ni hadithi ya kuipotezea tu unakosea sana mazee! maana hadi leo ilishagonga " Viewers" zaidi ya milioni moja na ushee wa hapa jukwaani. Shukurani kwake mkuu LEGE kwa kutuletea hii burudani na nyingine nyingi kali. Ipitie utafurahi sana.
SEASON 1 SEHEMU YA KWANZA MTUNZI : PATRICK.CK Ni saa sita za usiku sasa bado jaji Elibariki chukuswa yuko sebuleni akiendelea kupitia kitabu chake cha sheria .Katika meza ndogo kulikuwa na vitabu vingine zaidi ya saba vya sheria.Aliendelea kufungua ukurasa baada ya ukurasa.Alionekana kuwa na...
Habari zenu wakubwa kwa wadogo. Kwanza napenda kutoa pole na shughuli za kutwa kwa wale wahangaikaji wote kama mimi ambao kila siku lazima tutoke ili tuweze kujipatia riziki halali kila siku iendayo kwa mungu. Tuseme wote asante mungu. Nisiwachoshe niende moja kwa moja kwenye mada,mdaa huu...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.