Simulizi: Kurudi Kwa Moza

Simulizi: Kurudi Kwa Moza

SEHEMU YA 41




Wakati anaendesha gari akasikia sauti,
“Rose, umenigonga nimekufa halafu kwenye maizishi yangu unakimbia!”
Rose alishtuka na kusimamisha gari kwa haraka huku akiwa amejawa na hofu iliyomfanya ashindwe hata kutazama nyuma ya gari kuwa hiyo sauti inatoka wapi. Akiwa amejawa na hofu zaidi, ile sauti ikajirudia tena, na kumfanya Rose ashuke kabisa kwenye gari ile, alipokuwa chini akatazama kwenye kioo cha gari gafla alimuona kama Yule babu yupo ndani ya lile gari.
Uoga ulizidi kumshika Rose na kujikuta akiacha gari kisha kuanza kukimbia hovyo, alikimbia sana hadi akachoka kwakweli. Alifika kwenye mti mmoja na kukaa chini yake huku akiwaza kuwa alikuwa anaota au ni vipi maana yale mambo yalikuwa kama ndoto.
“Hivi ni kweli au naota? Lakini mimi uoga umeanza lini kwangu? Hivi mi naweza kuwa na uoga wa namna hii kweli? Ningeweza kuwafuga wale wajinga wangu? Hapana kwakweli, mimi ndio mimi uoga kwangu ni mwiko”
Akainuka na kuanza safari ya kurudi kwenye gari yake ila aligundua kuwa ni mbali sana ameiacha hiyo gari.
Alitembea kwa umbali mrefu sana hadi kuifikia, alivyofika alikuwa amechoka vilivyo, akafungua na kuingia ndani ya gari yani ingawa milango ya gari hakufunga na funguo ila ilionyesha wazi hakuna mtu aliyeingia kwenye gari ile kwani kila kitu alikuta kama kilivyo. Aliendesha gari na kwenda moja kwa moja hotelini, hakutaka kwenda nyumbani kwake kwanza kwahiyo aliamua kwa wakati huo akalale hotelini kwanza.

Kwa upande wa nyumbani kwa Neema, ilipofika usiku Salome aligoma kwenda kulala na mamake mdogo Ashura, kitendo hiko kilimshangaza sana Neema kwani kwake ilikuwa ni ajabu,
“Kwahiyo, Salome unataka ukalale wapi?”
“Nataka leo nikalale na wewe mama”
“Una nini lakini Salome jamani?’
“Sina chochote mama ila nataka nikalale na wewe”
Neema hakuwa na jinsi zaidi ya kukubali tu vile alivyoambiwa na mtoto wake ila Ashura nae kwakweli alimshangaa sana Salome ila hakusema chochote.
Muda wa kulala ulipofika, moja kwa moja Salome alikwenda na mama yake chumbani ila walipotaka tu kulala, Salome akaanza kumwambia vitu Neema vilivyomshangaza sana, tena muda mwingine akamuuliza maswali ambayo Neema hakufikiria kama kuna siku Salome atamuuliza maswali ya namna hiyo,
“Mama, baba yangu yuko wapi?”
“Mmmh Salome, ndio maswali gani hayo?”
“Kila mtu kwenye ulimwengu huu ana baba yake, mimi je baba yangu yuko wapi?”
“Jamani, Sa lome kwanini kutaka kunikumbushia machungu yaliyopita? Wewe ni mwanamke pia, ukikua vizuri utatambua nazungumzia nini”
“Mama, mimi ni mkubwa tayari au unataka nikue mara ngapi? Nataka kujua baba yangu alipo”
“Baba yako alishakufa”
‘Si kweli mama”
“Sasa ukweli ni upi? Baba yako alishakufa, wewe huna baba”
“Sawa, baba yangu alishakufa. Je baba wa hawa wadogo zangu je nae alikufa? Maana nae sijawahi kumuona na wote tunatumia majina ya babu!”
“Salome, tafadhali niache nilale, wala sitaki maswali zaidi”
Neema aliona maswali ya Salome yanamchanganya kichwa tu, ila Salome hakuendelea na maswali zaidi halafu akajifanya muda huo huo amelala ila kumbe alikuwa kijicho kimoja akimchungulia mama yake kila alichofanya kwa muda huo, kwani Neema nae hakulala tena maswali ya Salome yalimkumbusha mbali sana hivyo hakuyataka tena, Ila kabla hajalala aliinuka pale kitandani na kupekua vitu kwenye kabiti lake, kuna kitu alikitoa kilikuwa kama daftari dogo, akakiangalia sana kisha akakirudisha na kurudi kitandani halafu akalala sasa.
Salome akainuka pia na kwenda pale alipokuwa anapekua Neema, akapata kile kitu kumbe ilikuwa ni kadi ya kliniki ya miaka ya nyuma, iliandikwa jina la mtoto Maria Patrick. Alitazama vizuri ile kadi kisha akairudisha na kwenda kulala pia.



 
SEHEMU YA 42


Leo usiku ilikuwa sokomoko pia nyumbani kwa Patrick kwani bado Sara ilionyesha hataki kulala mwenyewe ingawa kuongea alikuwa hawezi ila kila walipotaka kumpeleka akalale aliangusha machozi,
“Mmmh hapa kazi ipo, ila Sara mbona mchana ulikubali. Kwanini usiku huu unakataa?”
Sara alizidi kutokwa na machozi hivyo kufanya maamuzi ya kubaki sebleni ila Ana alitaka kwenda chumbani kulala,
“Kheee Ana, wewe si ndio ulitakiwa kubaki na dada yako hapa!”
“Hivi nyie vipi, humuoni kuwa mimi ni mtoto mdogo. Halafu huyo anagoma kwenda kulala kwa misingi ipi? Ngoja niende nikalale mie, huyo akilala mkamlaze”
“Sasa humuonei huruma kwani?”
“Namuonea huruma ila inabidi nikalale kwanza ndio huruma yangu ifanye kazi”
Ana aliwaacha pale kisha yeye akaenda chumbani kwake ila
Muda huo huo Sara alianguka na kuhisi kuwa amezimia ila walipomuangalia alikuwa kwenye usingizi mzito sana. Ikabidi wambebe na kwenda kumlaza chumbani kwake, kisha na wao kwenda chumbani kwao kulala.
Ila Patrick yeye aliamua kukaa sebleni, muda kidogo akafatwa na Ana na kumwambia,
“Nenda kalale”
“Mmmh nini tena mpaka unanilazimisha nikalale Ana!”
“Sasa sebleni unabaki kufanya nini?”
“Namsubiri mama yenu”
“Harudi leo ni hadi kesho, kwahiyo wewe nenda kalale”
“Hivi kwa mfano nikigoma kwenda itakuwaje?”
“Goma uone”
“Mmmh!”
Patrick mwenyewe aliinuka kwenye kochi na kuelekea chumbani kwani hakutaka makubwa ukizingatia huyu mtoto alikuwa na kauli sana tena kuzidi hata mama yake, kwahiyo Patrick aliona ni vyema atumie busara kuliko kugombana na huyo mtoto mdogo.
 
SEHEMU YA 43


Kulipokucha, wale mapacha walikuwa wa kwanza kutoka sebleni ila harufu ya sebleni iliwashangaza sana yani ilionekana kama kuna kitu kilikuwa kimechomwa hapo, Doto akamuuliza mwenzie,
“Hivi na wewe hii harufu unaisikia?”:
“Ndio nilitaka kukuuliza na wewe ndugu yangu, ila ni harufu ya nini?”
Hawakupata jibu ila badae wakamkumbuka dada yao ambaye haongei chumbani ikabidi waende kumuamsha na kumtoa sebleni ila hali yake iliwashtua tena kwani kwasasa dada yao hakuweza kuongea wala kufumbua macho.
“Mmmh kamuamshe baba Doto, tumpeleke huyu mtu hospitali. Mbona mambo yanazidi kuwa makubwa”
Basi Doto akenda kumuamsha baba yao ambaye nae alishangazwa na hali ya Sara kuzidi kuwa mbaya, wakakubaliana pale kuwa suluhisho ni kumpeleka hospitali tu hakuna kingine.
Wakati wanajiandaa ili kumpeleka hospitali, Ana nae aliamka na kwenda sebleni kisha akawauliza,
“Mnataka kufanya nini?”
“Tunataka kumpeleka Sara hospitali”
“Hakuna kumpeleka”
“Kheee unaongea kwa kujiamini kabisa!”
“Ndio najiamini”
“Halafu mtoto, unanyodo wewe. Hebu tupishe huko tumpeleke Sara hospitali”
“Nimesema hamna kumpeleka”
“Unaongea hivyo kama nani?”
“Naongea kama Ana, hakuna kumpeleka popote”
Kaka zake walitazamana pamoja na Patrick bila kumuelewa huyu Ana anamaanisha nini au ni kitu gani anakitaka hadi kusema vile. Ila Patrick akajikuta akiwataadhalisha wenzie,
“Jamani, Ana kashakataa tutulie tu”
“Kwani baba, Ana ni nani kwenye nyumba hii hadi tumuheshimu? Ana sauti gani kwenye nyumba hii? Ni bado kinda tu huyo, ana ukubwa gani huyu! Anajua matatizo ya mtu huyu? Sara anaumwa na hakika anajisikia vibaya sana, hospitali ndio suruhisho la pekee kwa matatizo yaliyompata kwani watachunguza kinywa na macho yake yamepatwa na nini. Achana na huyu Ana baba, tushirikiane tumpeleke Sara hospiatali”
Ana akacheka, kisha akasema
“Kwani Ana ndio nani? Ana sauti gani kwenye nyumba hii? Nadhani wote mnataka kunua nina sauti gani kwenye nyumba hii na mimi ni nani. Sasa endeleeni kung’ang’ania kumpeleka hospitali niwaonyeshe kuwa mimi ni nani”
Kaka zake walimuangalia kwa gadhabu sana, kisha wakaanza kumbeba Sara ili amtoe nje na wakampakize kwenye gari waende hospitali ila gafla wote walipiga miyeleka na kuanguka chini tena walianguka vibaya sana, halafu cha kushangaza ni kuwa kila aliyejaribu kuinuka alishindwa na kila aliyejaribu kuongea alishindwa pia. Wakabaki chini tu wakiugulia maumivu. Ila Ana alikaa na kuwacheka sana, kisha akaenda kuchukua juisi na kunywa huku akiwaangalia na kucheka.



 
SEHEMU YA 44


Neema alikuwa wa kwanza kuamka ila kabla hajatoka nje, mtoto wake alimuuliza
“Mama, Maria Patrick ndio nani?”
Neema akashtuka sana kwa swali lile,
“Eeeh Salome unasemaje?”
“Maria Patrick ndio nani?”
“Hata salamu hakuna? Si ndio tumetoka kuamka jamani mwanangu!”
“Ndio mama, shikamoo ila nijibu Maria Patrick ndio nani?”
“Ni mdogo wangu wa mwisho”
“Wewe mama huyo mdogo wako ni wa wapi? Kwanini hutaki kusema wazi tu kuwa Maria Patrick ni mimi”
“Salome, niache tafadhali niache. Wewe mtoto usinitafutie makubwa jamani. Wewe ni Salome, hiyo Maria imetoka wapi tena. Niache wewe mtoto nipumue”
“Mama, nahitaji kwenda kwa baba yangu”
Neema akapumua kwa hasira na kutoka nje, kisha akamuita Ashura halafu Salome nae alienda pembeni akisikiliza maongezi yao,
“Huyu mtoto mwenzangu anataka kuniletea balaa”
“Lipi tena dada?”
“Eti anataka kumjua baba yake”
“Mmmh hilo balaa kweli, mwambie alishakufa”
“Nimemwambia, ila sijui katoa wapi jina la Maria Patrick na amesema anataka kwenda kwa baba yake”
“Khee dada, hapana bhana usithubutu kufanya hivyo”
“Sasa nitafanyeje mimi?”
“Ngojea, nitajua cha kufanya dada ila usithubutu kumueleza kuhusu baba yake”
Neema aliondoka zake kujiandaa ila salome alishaelewa kinachoendelea hapo.
 
SEHEMU YA 45


Rose alipoamka hotelini, alijiandaa kwa safari ya kurudi nyumbani kwake, kwakweli alikuwa anajihisi uchovu sana ingawa alilala hotelini ila bado mwili wake uligubikwa na uchovu wa hali ya juu. Aliendesha gari yake hadi nyumbani kwake, ambapo getini alifunguliwa mlango na mlinzi kama kawaida.
“Vipi, ndani humu wote wazima?”
“Nadhani, ila leo sijamuona yeyeto akitoka nje”
“Itakuwa wananisubiria”
Aliingia ndani na kukuta wote wapo chini, tena kila mmoja na pozi lake ila kwa muda huo walikuwa wamepitiwa nausingizi. Wakati anataka kuwaamsha mara akatokea Ana na kumwambia mama yake,
“Usiwaamshe waache hao”
“Vipi tena imekuwaje?”
“Ni viburi sana hao mama”
Rose hakuelewa bado, ila Ana alimvutia mama yake chumbani na kumueleza alichowafanyia ndugu zake.
“Jamani mwanangu kumbe wewe ni fundi hivi jamani!”
“Nilikuwa sizijui vizuri nguvu zangu ila saivi nimezijua”
“Aaah wewe ni kiboko, ila mwanangu watu hawa inabidi warudi kwenye hali ya kawaida maana ndio wanaotusaidia”
“Nitawarudisha wengine ila sio dada Sara”
“Hapana mwanangu, Yule ni dada yako”
“Hata kama, labda aone tu ila kuongea ni no, Yule mdada ni mbea sana”
“Ila kwanini hatukuweza kumziba mdomo Moza?”
“Achana na habari za huyo mtu mama hakuwa wa kawaida ila cha msingi hatuponae tena hapa”
“Sawa mwanangu, ila waachilie ndugu zako”
Ana akaenda chumbani kwake kufanya dawa, na muda kidogo tu pale sebleni waliamka na waliweza kuinuka na kuzungumza ila kila mmoja aliogopa kuzungumza kuhusu kitu kilichotokea. Sara nae aliweza kuangalia ila kuzungumza hakuweza.
Wale mapacha, walipoinuka kitu cha kwanza kilikuwa ni kuondoka hapo nyumbani kwao, na kumuacha Patrick na Sara hata hawakutaka kujua kama mama yao karudi au la.

 
SEHEMU YA 46


Salome alikuwa makini akifatili mambo ya Ashura kwani alijua ni wazi angewasiliana na Rose kumwambia ile mada na kweli Ashura aliingia chumbani na kumpigia simu Rose kumbe Salome alikuwa amejibanza akisikiliza,
“Yani dada, ule wasiwasi ambao ulikuwa nao kipindi chote sasa unaenda kutokea. Kwa kifupi haka katoto kameanza kumchachafya mama yake kuhusu baba yake na kanataka kuja kwa baba yake”
Ashura akawa kimya sasa akisikiliza maelekezo ya Rose, ila Salome nae alikuwa makini kabisa kwani alijua ni wazi baada ya maelekezo hayo Ashura angeongea tu.
“Kwahiyo ndio wakati wa kuitumia ile dawa eeeh! Sawa dada nimekuelewa, si nimuwekee kwenye chakula! Sawa dada nitafanya hivyo. Lakini si siyo ya kuua? Sawa maana ingekuwa ya kuua ningeogopa kwakweli maana kesi hizi”
Kisha Ashura akakata simu na kwenda kwenye begi lake ambapo alionekana kama akipekua kitu kisha akatoa kichupa kidogo na kutoka nacho.
Muda kidogo akamuita Salome na kumwambia,
“Njoo ule Salome mzuri weee”
Salome alifika na kumuuliza,
“Sasa nakula peke yangu?”
“Hapana, tunakula wote. Chakula change si hicho hapo. Halafu cha kwako ni hiki”
“Sawa, ila wadogo zangu wako wapi nao waje nile nao bhana”
“Kawaite basi”
“Mi naona uvivu”
“Yani wewe mtoto loh!”
Kisha Ashura akaenda kuwaita wadogo zake Salome, ila kwa muda huo huo Salome aliweza kubadilisha zile sahani za chakula.
Ashura aliporudi akaenda kuwapakulia chakula chao watoto, kisha kwa pamoja wakaanza kula mara gafla Ashura akadondoka huku akitapatapa na povu likimtoka mdomoni.
 
SEHEMU YA 47



Kisha Ashura akaenda kuwaita wadogo zake Salome, ila kwa muda huo huo Salome aliweza kubadilisha zile sahani za chakula.
Ashura aliporudi akaenda kuwapakulia chakula chao watoto, kisha kwa pamoja wakaanza kula mara gafla Ashura akadondoka huku akitapatapa na povu likimtoka mdomoni.
Hapo ndio hofu iliwashika hata wadogo zake Salome waliogopa sana na kumuuliza dada yao,
“Kwani imekuwaje dada?”
“Min a mamdogo Ashura tunacheza mchezo kwahiyo hata msiwe na mashaka”
Ila Salome alikuwa jasiri sana kwa wakati huo kwani alimchukua mamake mdogo huyo na kumburuza hadi chumbani kisha akamfunika na kitenge halafu akachukua simu ya Ashura na kuifungua halafu akaangalia namba aliyoipiga mwishoni akaona ni namba ambayo haijaandikwa jina ila akahisi ndio hiyo hiyo namba ya Rose, akaamua amtumie ujumbe mfupi,
“Dada, mbona hii dawa nimempa huyu Salome ameanguka na povu linamtoka mdomoni?”
Baada ya muda ujumbe ule ukajibiwa,
“Hahaha, tayari huyo yani hapo kazi umamiliza mdogo wangu. Unaweza ukaondoka sasa”
Naye Salome akaandika ujumbe mwingine,
“Jamani dada tayari nini tena?”
“Kwani huji? Ameshakufa huyo”
“Kheee kumbe dawa ilikuwa ya kummaliza kabisa! Mbona mwanzo hukuniambia?”
“Hivi wewe Ashura unasahau sahau nini, nilishakwambia toka mwanzo kuwa huyo mtoto nataka nimmalize. Tena toka siku ya kwanza nilikwambia hiyo dawa ni ya kummaliza kabisa, wewe cha kufanya saivi ni kuondoka hapo upesi iwezekanavyo maana kazi tushamaliza. Si nilishakwambia na nguo zako upange kabisa, nakutumia na hela muda sio mrefu ili uondoke”
Na kweli baada ya muda mfupi ikaingia meseji kwenye simu kuwa amepokea milioni mbili na elfu kumi na tano. Kisha ikafatia meseji ya kawaida,
“Toa hiyo milioni mbili itakusaidia kwenye safari yako, ukishafika nishtue nikutumie hela nyingine”
“Hivi dada hawatanikamata kweli?”
“Akukamate nani bhana, kuna mtu anapajua kwenu hapo? Hakuna anayepajua kwenu, hawakukamati wala nini. Kwanza Ashura sio jina lako, kwahiyo watakutafuta hadi wachanganyikiwe”
“Ila hawa wadogo wameona kama dada yao ameanguka”
“Achana nao hao, waondoe hapo nyumbani. Wape hata hela ya biskuti ili wakatembee. Mimi hao nao nitawatokomeza ingawa sijui kuhusu ukweli wao, ila usipoteze muda saivi. Ondoka upesi”
“Sawa dada, ngoja niondoke”
Salome akamtazama Ashura waliyeishi nae kwa kipindi kirefu sana ila kumbe kuna kazi alitumwa aifanye hapo, kisha akatoka nje na kuwapa wadogo zake hela ya biskuti kama ambavyo Rose alikuwa amemshauri Ashura kwani wale watoto walipenda sana michezo na kwa vyovyote vile wamepewa na hela ndio kabisa. Hiyo hela aliipata kwa mama yake ambayo aliiacha kwaajili ya mboga ya jioni.
Kisha Salome akarudi tena chumbani kwa Ashura na kuanza kupekua begi lake, ila alikuta nguo zote za Ashura zimepangwa vizuri sana na vitambulisho vya Ashura alivikuta, na kushangaa sana.
“Hadi vitambulisho vimeandikwa Ashura kumbe sio jina lake mmmh!”
Wakati anapekua zaidi, alikutana na pochi yenye hela, alipozihesabu zile hela ilikuwa ni milioni tatu na laki saba,
“Mmh na mbona kila siku anasemaga hana hela jamani!!”
Alipopekua vizuri aliona kijitabu kimeandikwa andikwa namba za simu, halafu kiliandikwa na namba za siri za kutolea hela kwenye simu, halafu kilikuwa na namba zenye maelezo “Hawa ni watu nitakaowatumia kupoteza ushahidi” Kidogo Salome alishtuka ila swala la kukuta namba za siri kwenye kile kitabu zilimfurahisha kwani aliona kila kitu kimetimia sasa, akitoa na zile hela atakuwa na hela za kutosha, alipojaribisha ile namba kwenye simu ili aangalie tu salio lililopo kwenye simu kakuta kuna 10,050,000/= kwakweli Salome alishangaa sana,
“Kheee milioni kumi kwenye simu! Kumbewalikuwa wanaishi na pedeshee humu ndani”
Akaona ni vyema hiyo hela kabla ya kuitoa aifanyie maarifa ya kuihamisha kwenye simu nyingine halafu ndio aitoe ila kwa wakati huo akafanya namna ya kuweza kuzima lile swala la Ashura. Hivyo akatoka na kwenda kununua viroba vikubwa vya kuweza kumtumbukiza mtu, na aliifanya kazi ile mwenyewe alimtumbukiza Ashura kwenye vile viroba halafu akavifunga kwa juu halafu akamviringisha shuka na kumtumbukiza kwenye kiroba kingine. Halafu zile namba za wale watu alizozikuta kwenye kile kitabu cha Ashura ambao alikuwa ameandika historia zao, akawasiliana nao kwa njia ya ujumbe kwa kutumia simu ya Ashura kisha akawaelekeza pale kwao na mahali alipoweka huo mzigo wa mtu kwani alikuwa ameuburuza hadi sebleni. Halafu yeye akatoka kwenda kutafuta simu nyingine na laini ya kutumia yeye kwa kutumia zile hela alizozikuta kwenye begi la Ashura, hakuwa na wasiwasi na wadogo zake kwani wale huwa wanarudi nyumbani mpaka watafutwe na kuitwa. Ila alitumia ujanja wa kujificha sehemu hadi wale vijana walipofika na kutoka na ule mwili na kuupakia kwenye gari na kutokomea zao. Hapo alirudi tena pale kwao na kufunga milango halafu akatoka.


 
SEHEMU YA 48


Rose alikuwa ni mtu mwenye furaha sana kwa wakati huo hata akasahau kila kilichomtokea kwani mambo yote yalikuwa yamefutwa na kifo cha mtu mmoja tu, kifo cha Salome. Kwakweli furaha yake ilikuwa maradufu, akaenda kwa mumewe na kumwambia,
“Leo, nataka nipike mwenyewe. Sema nikupikie chakula gani?”
“Mmmh leo umefurahi na nini mke wangu jamani?”
“Wewe sema tu ni chakula gani unataka”
“Nipikie chochote tu”
Akaenda jikoni na kumuita Ana, kisha akamwambia
“Mwanangu, dadako si umuachie mdomo tu”
“Hapana mama, hawezi huyu ataropoka tu”
“Ameshajifunza mwanangu, halafu leo nina furaha sana muachie bhana”
“Furaha ya nini mama?”
“Yule mtoto aliyekuwa ananisumbua kichwa siku zote, kila nilipojaribu kummaliza nilishindwa hadi kuamua kumtafuta mtu wa kunisaidia. Ila leo naongea habari nyingine kabisa tena kwa furaha, Yule mtoto amekufa”
“Kheee mama, kweli hiyo ni habari njema tena njema haswaaa”
“Sasa sikia mwanangu, chukua simu yangu ile na utoe hela benki halafu utume kwenye namba ya Ashura. Mtumie milioni tano, nataka atulie kabisa huko alipoenda”
“Sawa mama”
Ilionyesha hii habari pia Ana ilimfurahisha sana, kwahiyo akaenda kuchukua simu ya mama yake na kufanya hivyo. Ana alikuwa ndio mtoto pekee aliyejua siri za mama yake, hata namba zake za siri zote alimwambia mwanae huyo. Alipomaliza alimfata tena mama yake na kumwambia,
“Tayari mama nimemtumia”
“Sawa, mtumie na meseji kuwa nimemtumia hela nyingine maana najua kuongea kwa sauti hawezi sababu ya hili tukio”
“Sawa mama”
Ana alituma ujumbe kwenye namba ya Ashura, na baada ya muda tu ujumbe huo ukajibiwa,
“Nimeipata asante dada, saivi ndio niko njiani naelekea kule kijijini. Nishafuta hadi ushahidi, yani hawawezi kujua Salome ametokomea wapi au amefia wapi maana nimewaagiza vijana wautokomeze mwili wake kabisa kwahiyo hakuna ushahidi, na mimi nimeondoka kabisa”
Ana alimsomea mama yake ambaye kwa hakika alikuwa na furaha zaidi, kisha akachukua simu ile kwa Ana na kuwapigia vijana ambao yeye alikuwa anawafahamu,
“Vipi mmeshafanya kazi ya Ashura?”
“Tushamaliza bi.mkubwa si unajua sisi hatucheleweshagi”
“Sasa mmemtupia wapi?”
“Kwenye mapango huko, hawezi kuonekana kamwe. Yani kama watu wataenda miaka ijayo hiyo basi watakuta mifupa. Ila Ashura ni jasiri sana kwani tumekuta amemfunga vizuri kabisa.”
“Sawa, sasa amewalipa?”
“Bado, amesema kuwa yupo safarini”
“Basi msimdai yeye hela, nawatumia sasa hivi”
Kisha Rose akakata ile simu huku akiwa na furaha zaidi halafu akawatumia hela wale vijana, kwakweli leo ilikuwa ni siku ya furaha kabisa kwake.



 
SEHEMU YA 49


Salome aliamua kufanya jambo moja la akili sana, alitafuta dalali siku hiyo hiyo na kuulizia kuhusu nyumba, kwakweli ilipatikana yani maisha ukiwa na hela mkononi mambo mengi yanawezekana ila kama huna hela kila kitu kinakushinda. Salome alilipia ile nyumba waliyoipata kisha akatafuta vijana na usafiri wa kuanza kusafirisha vitu kwenye nyumba mpya, kisha akawaita wadogo zake na kwenda nao huko kupya. Walipofika walikuwa wakishangaa shangaa tu,
“Dada, tumehamia kwingine! Mamdogo na mama wako wapi?”
“Mama atakuja, ila mamdogo kagoma kuja huku”
“Jamani dada, mwambie mamdogo aje”
Mwingine akasema,
“Ila bora agome, Yule mamdogo simpendagi”
“John, usiwe hivyo bhana. Mama ametufundisha upendo”
“Hatakama tumefundishwa upendo na mama, ila si kagoma mwenyewe. Akiendelea kugoma dada Salome achana nae. Aje mama tu”
“Sawa sawa mdogo wangu John, wewe ndio kidume. Achana na Jose huyu anajifanya mlokole”
Basi Salome aliwaacha pale wadogo zake na kwenda kumalizia vitu kwenye nyumba yao, halafu alitafuta watu wa kuwapangia vitu vyao ndani. Yote hayo yaliwezekana kwa nguvu ya pesa tu.
Walipomaliza kupanga, alirudi pale kwenye nyumba yao ya zamani na kuwaacha wadogo zake kwenye nyumba mpya, alienda kwa lengo la kumsubiri mama yake kwani usiku tayari ulishaingia.
Kwenye mida ya saa mbili hivi, Neema alirudi na kuingia ndani. Alikuta nyumba yote nyeupe hakuna hata kitu ndani. Alipatwa na mashaka na kuhisi kuwa wameibiwa, wakati anataka kutoka ili aulize kwa majirani ndipo akakutana na Salome,
“Imekuwaje mwanangu mbona sielewi!”
“Tumehama mama”
“Tumehama, kivipi sikuelewi”
“Yani elewa tu kuwa tumehama mama, hapa nimekuja tu kukufata ili twende kwenye nyumba mpya”
“Tutahamaje wakati hapa kodi haijaisha?”
“Mama, mbona unakuwa mbishi hivyo! Nenda tu kazungumze na mwenye nyumba mkabidhi funguo atafute mpangaji mwingine, sisi tumehama”
“Wengine wote wako wapi?”
“Wapo huko kwenye nyumba mpya”
Kwakweli Neema alishindwa kuelewa kabisa kile kitendo cha kuhama kwa gafla vile halafu Salome anamwambia akakabidhi funguo.
“Hapana siwezi kukabidhi funguo wakati sijui tulipohamia”
“Inamaana mama huniamini mimi?”
“Nakuamini vizuri mwanangu ila kwa hili unanichanganya”
“Mama, tulikohamia ni mbali. Funguo twende tu ukakabidhi leoleo”
Kwavile Neema alimuamini sana binti yake, ikabidi aongozane nae mpaka kwa mwenye nyumba na kumkabidhi funguo,
“Mbona hamkusema jamani kama mnahama? Halafu mbona ni haraka haraka?”
“Nisameheni mimi ila haya ni mambo ya Salome na mdogo wangu Ashura hata sijui wamefikiria nini ila ndio hivyo tumehama”
Neema aliwaaga pale kisha akaondoka na mwanae kuelekea huko kupya walikohamia.

 
SEHEMU YA 50


Walifika kwenye mida ya saa nne usiku hata wakawakuta wale wadogo zake Salome wamelala kwenye viti,
“Mmh jamani mmewachosha watoto na kuhamahama kwenu, hivi wamekula kweli hawa? Ashura, Ashura”
Neema alijikuta akimuita Ashura kwani alitaka ndiye amjibu kwani yeye ni mtu mzima na atakuwa anjua mambo mengi sana, Salome alimuangalia mama yake na kumwambia,
“Ashura hayupo”
“Wewe si nishakukataza, ni mamako mdogo Yule. Haya hayupo yuko wapi?”
“Kuna mahali ameenda, alisema atarudi kesho”
“Sasa na kuhamia hapa nani ametoa wazo hilo?”
“Ni yeye tena tumesaidiana nae hadi kuja hapa ila baada ya kupanga kila kitu akaniaga na kuondoka. Wakati huo mimi nilikuja kukufata wewe, halafu yeye alikuwa ameondoka”
“Sasa watoto wamekula hawa?”
“Ndio, walinunuliwa chips wamekula, hata wewe za kwako zipo”
Akaenda kumletea mama yake, ambaye alikula bila kuhoji zaidi kwani njaa ilikuwa inamuuma, kisha akaenda kumuonyesha chumba cha kulala yeye. Sababu alikuwa amechoka sana akasema ile nyumba ataiangalia vizuri kesho yake, Salome akawachukua na wadogo zake na kuwapeleka chumbani kulala. Kisha yeye alienda chumbani kwake. Hiyo nyumba ilikuwa na vyumba vitatu vya kulala kama ile waliyokuwa wanakaa mwanzo ila ilikuwa ni nzuri zaidi ya ile ya mwanzo.
Neema alilala fofofo kutokana na uchovu alionao wa siku hiyo kitu kilichomfanya ashindwe hata kuhoji vizuri kuhusu ile nyumba na wazo la kuhama. Ila kulipokucha alichukua simu yake, na akashtushwa na ujumbe kutoka kwa Ashura,
“Dada samahani najua utakuwa umefadhaika sana kwa kutokunikuta ila mimi lengo langu ilikuwa ni kuona dada yangu unaishi kwenye mazingira safi na mazuri. Hiyo nyumba nimelipa kodi ya mwaka mzima kwahiyo usihangaike kabisa dada yangu. Mimi nimeamua kurudi kijijini kwetu kwa ndugu zangu nimewakumbuka sana, na huko mjini sitarudi tena. Wala usihangaike kunitafuta dada yangu. Halafu huku mtandao unasumbuaga sana kwahiyo mara nyingi nitakuwa sipatikani kwenye simu. Usihangaike kumuuliza Salome, hajui chochote kuhusu kuondoka kwangu kwani ningemwambia ukweli kama naondoka angelia ndiomana nimeondoka kimya kimya. Nawapenda sana ten asana, hata msiwe na wasiwasi na mimi nipo salama kabisa”
Neema alisoma ule ujumbe mara mbili mbili ila alishindwa hata aanzie wapi kuhoji na ukizingatia kashaambiwa hata Salome asimuulize. Kwakweli alibaki kimya tu akitazama ile nyumba kisha akatoka na kwenda kuitazama vizuri zaidi.
Wakati anaenda kwenye kila chumba kukagua aliingia na kwenye chumba walicholala watoto wake mapacha na kuwaona bado wamelala, kwakweli aliuthaminisha uzuri wa ile nyumba. Kisha akaingia chumba anacholala Salome tena aliingia bila hodi, ila alimuona Salome amesimama akiwa amempa mgongo hivi ila Neema alishtuka sana na kujikuta akisema kwa mshtuko,
“Aaah Moza!!”
Salome aligeuka sasa na kumuangalia vizuri Neema, lakini Neema alijikuta anaanguka chini.

 
SEHEMU YA 51



Kisha akaingia chumba anacholala Salome tena aliingia bila hodi, ila alimuona Salome amesimama akiwa amempa mgongo hivi ila Neema alishtuka sana na kujikuta akisema kwa mshtuko,
“Aaah Moza!!”
Salome aligeuka sasa na kumuangalia vizuri Neema, lakini Neema alijikuta anaanguka chini.
Salome akasogea na kumfata Neema pale chini, kisha akamwambia kwa sauti ya upole,
“Mama una nini jamani?”
“Mungu wangu, yani Salome ulivyosimama pale nimekuona kama Moza halafu ulipogeuka yani sura ya Moza kabisa ikanijia. Nilichanganyikiwa kabisa maana Moza ashakufa”
“Jamani mama una mawazo sana, mimi ni mwanao Salome yani hata usiwe na mashaka. Sasa mimi nawezaje tena kuwa Moza!”
“Hapana mwanangu, nahisi ni utu uzima huu”
Neema akapumua sasa hata jambo la kuongea alilokuwa nalo lilipotea kabisa kwani miguu yake ilikuwa kwenye mtetemeko wa hali ya juu, ikabidi Salome amsaidie Neema kuinuka pale kisha akampeleka sebleni ambapo alikuwa kimya kabisa akionekana kutafakari jambo Fulani. Muda kidogo wale wadogo zake Salome waliamka na kutoka pia kisha wakamsalimia mama yao na dada yao. Baada ya Salamu alianza kuongea John,
“Yani leo nimelala usingizi wa raha kweli yani!”
Salome akamuuliza mdogo wake huyu,
“Umelala usingizi war aha, hebu tudokeze kivipi?”
“Yani kule tulipokuwa tunakaa zamani, mindoo yote ya maji chumbani kwetu ila leo tumelala chumba cheupe chenye kitanda tu”
Mama yao nae akawaambia,
“Kumbe yale mandoo yalikuwa yanawakera eeeh! Mnatakiwa kuzoea maisha yote”
Kisha Salome akamuangalia mama yake na kumwambia,
“Mama unajua hawa watoto sasa wamekuwa wanatakiwa waende shule”
“Natambua hilo mwanangu, ila hela kwasasa sina”
“Sasa mama, ila nitafanya jambo na wataenda shule hawa. Wamekuwa sasa”
“Utafanya jambo gani? Wewe utapata wapi hela?”
“Mama tulia tu ila hela nitapata”
Kisha Salome akawachukua wadogo zake ili akawaandalie chai, kwakweli Neema alikuwa akimshangaa tu mwanae chauvivu alivyokuwa siku hizi.

 
SEHEMU YA 52


Siku ya leo, Rose aliruhusu watoto wake kutoka pia alimruhusu Patrick kutoka kwani alikuwa na furaha sana, kasoro kwa Sara tu ambaye hakuweza kuongea ndio alikaa ndani kama mwali hivi, kwa upande mwingine wa moyo wake alimuhurumia mwanae Sara ila kwa upande mwingine aliona ni vyema apate adabu kidogo kwani ni yeye aliyevuruga mwenendo mzima wa mazishi ya Moza, hakutaka mtu yeyote kwenda nyumbani ila Sara sababu ya kiburi chake akaenda.
Akiwa ametulia zake sebleni, huku Sara nae yupo sebleni akiangalia tu Tv ila kuongea ndio alikuwa haongei, mara ujumbe mfupi ukaingia kwenye simu ya Rose, alipoangalia ulikuwa unatoka kwa Ashura,
“Dada niongezee hela kidogo, halafu huku mtandao unasumbua sana yani nitakuwa sipatikani kabisa. Ukiniongezea hiyo hela sitakusumbua tena”
Rose alisikika akisema,
“Aaah huyu nae kashafanya ndio kitega uchumi wake mimi loh! Namtumia hiyo hela na bora asipatikane kabisa maana sasa anaanza kuniudhi. Miela yote niliyokuwa nampaga halafu kazi yenyewe kaichelewesha hadi leo”
Sara alikuwa akimsikia tu mama yake huku akitamani kumuuliza kitu ila alishindwa, basi Moza akatuma hela na kumuandikia ujumbe,
“Nimekutumia hiyo milioni tano nyingine najua itakusaidia, na wewe kuwa makini huko utafute biashara ufanye maana kazi yangu huku mjini ushamaliza.”
Alipotuma kidogo tu akajibiwa ule ujumbe,
“Asante dada wala usijali sitakusumbua tena dada yangu”
Basi Rose akapumua sasa, ila kila alipomuangalia mtoto wake alimuonea huruma sana.
Muda mfupi wakapata mgeni, alikuwa ni Ommy. Rose alipomuona hakupendezewa nae wala nini ila alimkaribisha tu kwa shingo upande. Basi Ommy akamsalimia Sara pale ila Rose akajibu kwa niaba ya Sara,
“Anaumwa kifua huyo, sauti haitoki”
“Jamani hata kidogo ya kunijibu tu!!”
“Hivi Kiswahili unaelewa wewe, nishakwambia anaumwa kifua huyo sasa akujibu nini?”
“Sawa mama, ila ameshaenda hospitali?”
“Kwahiyo wewe ndiye unayejali afya yake sana kushinda mamake mzazi niliyemzaa! Yani nikae na mgonjwa mpaka muda huu nikisubiria ushauri wako tu! Naomba uondoke, kwanza sikupendagi wewe kijana basi tu”
Ommy akaomba msamaha, kisha akainuka na kuaga na kuondoka zake. Sara machozi yalikuwa yakimtoka tu, mamake akamuangalia na kumwambia
“Sasa kinachokuliza ni nini? Unafikiri mimi sikuhurumii? Mdomo wako ndio haukuhurumii ila mwanangu usijali nitamwomba Ana akirudi akusamehe mwanangu”
Halafu Rose akainuka na kwenda chumbani kwake, kile kitendo tu cha Rose kuinuka na kwenda chumbani, Sara nae aliinuka na kutoka nje.
Alipofika getini, mlinzi alimuuliza,
“Madam vipi unashida na Yule rafiki yako nimkimbilie”
Sara akaitikia kwa kichwa tu, ila mlinzi akaelewa na kuona kuwa kaitikiwa vile kutokana na mapozi ya matajiri ila alitoka na kumkimbilia Ommy, bahati nzuri hakuwa amefika mbali, naye ommy akasikia wito na kurudi ambapo Sara alitoka nje ili aweze kuzungumza na Ommy japo kwa vitendo.
Ommy alivyofika pale, alimkumbatia Sara na kumwambia,
“Nieleze Sara umepatwa na nini tena?”
Ila Sara hakuweza kumjibu ila alimuomba simu yake kwa vitendo, kisha alivyompa akafungua sehemu ya ujumbe na kumuandikia,
“Mdogo wangu ni mchawi Ommy, ndio amenifanya hivi. Kanifunga mdomo nisiongee kabisa. Nisaidie”
Ommy alishika simu na kusoma ule ujumbe, kwakweli alishtuka sana na kujikuta akimuuliza kwa sauti ya chinichini,
“Mdogo wako yupi? Ana au?”
Sara aliitikia kwa kichwa, ila muda si muda Ana nae alirudi kutoka shuleni hata wakamshangaa maana sio kawaida yake kutoka shuleni mapema hivyo.
Ana akamuangalia Sara kwa jicho kali sana, Sara alijikuta akitetemeka na kuingia ndani bila kujidhania kisha Ana nae akaingia ndani na kumuamuru mlinzi afunge geti. Ommy aliweza kuelewa kinagaubaga kuhusu kinachoendelea mule ndani, basi akaondoka zake.

 
SEHEMU YA 53


Ana alimtanguliza Sara mbele na walipofika sebleni tu akaanza kufoka hadi mama yake akatoka nje.
“Vipi tena mwanagu kuna nini?”
“Mama, ndio mtu wa kumsamehe huyu!”
“Kafanyaje tena?”
“Nimemkuta nje ya geti anaongea na kale kamchumba kake”
“Khee alitoka nje ya geti, weee Sara wewe jamani kwanini lakini? Yani kwenda chumbani tu kidogo ukaamua ukifate kile kibwana chako? Na utaendelea kuwa bubu mpaka akili ikukae sawa”
Sara machozi yalikuwa yakimtoka tu na kwenda chumbani kwake huku akitokwa na machozi zidi ila bado kuongea hakuweza. Pale sebleni alibaki Ana na mama yake,
“Mwache nimkomeshe mama”
“Ila namuhurumia mwanangu jamani, ila mbona leo umewahi kurudi?”
“Nishawavuruga na huko shuleni”
“Kheee umewavuruga!”
“Ndio, mwlimu mkuu na walimu wake leo hawaelewani”
“Kwanini umefanya hivyo mwanangu?”
“Nimejisikia tu, kwahiyo wenyewe wameturuhusu shule nzima turudi nyumbani”
“Mmmh mwanangu, sasa huko siko. Wale ndio walimu wenu sasa ukiwafanyia hivyo mtafundishwa na nani?”
“Mama hujui tu, kuna mwalimu bonge huyo kanifokea leo yani yeye ndio kanifanya nijaribishe vitu vyangu. Kwanza nimemfanyia mchezo akaanguka chooni halafu nimetoa maelewano kwa walimu wote hadi wameturuhusu turudi nyumbani, nina hakika atajutia mule mule chooni maana sidhani kama atapata wa kumtoa”
“Mmmh mwanangu umekuwa kiboko, yani saivi sijui kama kuna mtu atatubabaisha tena”
Ana akacheka kisha akaelekea chumbani kwake.
Sara nae alikuwa chumbani kwake huku akiwaza cha kufanya akaamua kuwasha simu yake kwani alihisi huenda Ommy akamtafuta, na kweli alipowasha tu akakutana na ujumbe wa Ommy,
“Pole sana Sara kwa tatizo lako, ila kuna mzee nimekutana nae nimemueleza. Basi badae nitakupigia simu akuelekeze namna ya kufanya halafu utafanya na amesema utaongea tu”
Sara nae akamjibu Ommy,
“Nashukuru sana, simu niko nayo hapa kwahiyo ukipiga tu nitapokea yani nikipokea uanze kuongea kwani itakuwa tayari sikioni mwangu”
“Sawa, usijali Sara”
Basi Sara akaiweka ile simu makini kabisa ili akipigiwa na Ommy apokee.

 
SEHEMU YA 54


Siku ya leo, Neema hakutoka kwenda popote alibaki tu nyumbani kwake akitafakari kisa na mkasa halafu akishindwa hata kumuuliza Salome kwani akikumbuka ule ujumbe ulimwambia kuwa asijisumbue kumuuliza Salome.
Akiwa amekaa sebelu yao hiyo mpya, kwenye mida ya jioni alikuja Salome na kumwambia habari ambayo alipoisikia hakuipenda hata kidogo,
“Mama, kesho nataka kwenda kwa baba yangu”
“Unasemaje wewe?”
“Kesho nataka kwenda kwa baba yangu”
“Hivi wewe Salome una matatizo gani jamani, baba yako unayemuongelea ni yupi!”
“Patrick mama, najua baba yangu anaitwa Patrick. Nataka kesho niende kwa baba yangu”
“Unapajua?”
“Ndio napajua, wewe subiria tu kesho nikienda kwa baba yangu”
“Salome una nini lakini mwanangu, mwenzio nakupenda sana na sitaki kukupoteza. Aliyekwambia baba yako ni Patrick nani?”
“Mamdogo Ashura aliniambia ukweli wote hadi anapoishi baba yangu alinielekeza, aliniambia kila kitu kuhusu baba yangu”
“Mmh haiwezekani, Ashura akwambie wewe haiwezekani”
“Sasa mimi nimejuaje?”
“Sijui ila Ashura, labda lakini siamini nitamtafuta badae aniambie vizuri”
“Wewe mtafute tu ila kesho naenda kwa baba yangu. Yule ni baba yangu mama utanificha hadi lini? Mimi ni binti mkubwa sasa”
“Salome tafadhali usinitafutie makubwa”
“Yani mama huna cha kunishawishi kwakweli hata useme nini ila kesho naenda kwa baba yangu”
Neema hakuongea neon la zaidi, akainuka na kwenda chumbani kwake. Muda huo Salome nae aliinuka na kwenda chumbani.
Basi Neema akaanza kupiga simu ya Ashura ila iliita sana bila ya kupokelewa mara akapokea ujumbe,
“Tuma meseji nipo kwenye kelele”
“Ashura mdogo wangu umeanzaje kumwambia ukweli Salome kuhusu baba yake jamani! Unajua ni mabalaa unayaanzisha, kumbuka Yule mama alisemaje!”
Muda kidogo ujumbe ule ukajibiwa,
“Dada, Salome amekua sasa ana haki ya kumjua baba yake ndiomana nimemwambia. Na ukae nae chini umueleze ukweli wote, amekua huyo dada tutamficha hadi lini? Nimemwambia ukweli kuwa baba yake yupo na anitwa Patrick halafu anapokaa nimemuelekeza. Mwache mtoto amtafute baba yake. Kila mtu ana haki ya kumjua baba yake”
Neema aliposoma huu ujumbe akapumua kidogo kwani siku zote aliyekuwa mkali kwa Salome kumjua baba yake ni Ashura sasa ilimradi huyo Ashura amekubali basi hakuna wa kupinga.

 
SEHEMU YA 55


Kwenye mida ya jioni kabisa, Sara akiwa chumbani kwake akaingia Ana na kumuangalia dada yake. Muda kidogo simu ya Sara ikaanza kuita basi Sara akaichukua ila alienda Ana na kumpora kisha akaipokea na kuiweka sikioni ili amsikie mpigaji anasemaje maana aliona jina Ommy, kwakweli Sara aliona kabisa mwangaza wake umetoweka kwani Ana ndio alkuwa akisikiliza kila kitu ambacho mzee aliyetafutwa na Ommy alikuwa akimwambia Sara basi alipomaliza kumsikiliza akakata ile sime kisha akamuangalia dada yake na kumwambia,
“Yani wewe hukomi, hukomi kabisa eti umeamua utafutiwe mganga wa kienyeji akusaidie. Hivi hujui kuwa huyo mganga nikiamua hata yeye namfanya mbaya! Ila wewe nitakukomesha maana kinachokupa jeuri sasa ni hayo macho, na hutatazama tena”
Pale pale macho ya Sara yakajifunga na hakuweza kuangalia tena, kwakweli machozi yalikuwa yakimtoka tu.
Kisha Ana akaondoka zake na kwenda sebleni, hata kaka zao walivyorudi siku hiyo na kutaka kwenda kumtazama Sara walizuiliwwa na Ana, walitii kutokana na kile kitendo alichowafanyia siku ya kutaka kumpeleka Sara hospiatali.
Rose alijifanya kama hayupo kwenye matatizo ya mwanae huyo na wala hakuonekana kumsaidia tena, wala kwenda kumuona alivyofanywa kipofu amakweli mtu akishakuwa na roho ya kichawi anakuwa mnyama na huruma inamtoka kabisa.
Usiku ulifika na wote kwenda kulala.

Asubuhi kulivyokucha kama kawaida, watu waliondoka wote mule ndani tena na siku ya leo hata Rose aliondoka ingawa mwanae alikuwa haoni na yuko ndani.
Ila tu alimtoa na kumuweka sebleni kisha akamuacha hapo na kuondoka, kwahiyo mlinzi alikuwa anajua ndani kabakia Rose ila hakujua kama hakuwa na uwezo wa kuongea wala kuona.
Muda kidogo wakati Yule mlinzi yupo pale getini akamuona Salome na kumfanya amshangae,
“Karibu ila umekuja wakati Moza alishakufa”
“Nilipata habari ila mimi sijamfuata Moza”
“Umemfata nani kwani?”
“Kuna nani ndani?”
“Yupo Sara peke yake, wengine wote wametoka”
“Sawa, basi huyo ndio nimemfata”
Mlinzi hakuwa na jinsi zaidi ya kumkaribisha tu, ambapo Salome aliingia moja kwa moja ndani hadi sebleni na kumkuta Sara amekaa tu kwa kujiinamia huku machozi yakimtoka. Salome alimfata Sara pale alipokaa,
“Ni wewe ndiye umenifanya nije kwa wakati huu”
Sara alitamani kuongea lakini, alishindwa akaendelea tu kumsikiliza huyu Salome,
“Funua kinywa chako”
Sara alifunua kinywa na akanyunyuziwa dawa kama matone halafu gafla akajikuta akiweza kuongea, na kuuliza kwa sauti ya upole,
“Wewe ni nani uliyekuja kunisaidia?”
“Unataka kuniona?”
“Ndio nataka kukuona”
Basi Salome akachukua dawa na kunyunyiza kwenye macho ya Sara, na hapo hapo Sara akafikicha macho yake na kuona ila alipoinua macho vizuri ili amtazame aliyemsaidia alishtuka sana na kusema kwa nguvu,
“Kheee Moza!”
 
SEHEMU YA 56



Basi Salome akachukua dawa na kunyunyiza kwenye macho ya Sara, na hapo hapo Sara akafikicha macho yake na kuona ila alipoinua macho vizuri ili amtazame aliyemsaidia alishtuka sana na kusema kwa nguvu,
“Kheee Moza!”
Sara alikuwa akihema juu juu na muda kidogo akazimia ila Salome akammwagia maji na kuzinduka, Sara akawa anamuangalia Salome sasa, na kumuuliza
“Mara ya mwisho nilikuona na Moza eeh!!”
“Ndio nilikuwa na Moza”
“Ila mbona wakati ule nilipoanza kuona nimekuona kama Moza!”
“Sijui, labda mawazo yako unamfikiria Moza”
“Inawezekana, ila asante kwa kunisaidia maana nilihisi ndio mwisho wangu”
“Usijali, sikuweza kuvumilia ilihali najua unateseka ingawa nataka hapa niletwe na mama yangu”
“Aaah unataka kuja kuishi hapa eeeh!”
“Ndio si kwa baba yangu, nataka niishi na baba yangu”
“Karibu sana, hivi unaitwaga nani vile maana mimi najua jina la Maria ndio alikuwa mtoto wa baba ila Moza alisema jina lingine”
“Naitwa Salome ingawa sijui ni kwanini walinibadilisha jina”
“Na umejuaje kama baba ni baba yako?”
“Siku nyingi sana nilitamani kumjua baba yangu, ila sasa nimemjua ni furaha kubwa sana kwangu. Je wewe unatambua chochote kuwa kwanini walinificha nisijue?”
“Hata sijui kwakweli, hata mimi sielewagi ni kwanini ila nilikuwa namsikia mama na Ashura wakiongea kuwa haipaswi kabisa wewe kuujua ukweli”
“Sawa, ila saivi nimeshajua. Naomba ndugu zako wasijue kama nilikuja na nimekufanya uone na kuongea”
“Hawa si ndugu zangu kwakweli, ni wachawi. Kumbe mdogo wangu Ana ni mchawi sana, hata sikujua kama nitapona. Sijui wewe ni mganga?”
“Hapana ila nimewasikia wakikuongelea roho ikaniuma sana, ndio nikaamua nikusaidie. Ila usiseme kama ni mimi nimekusaidia”
“Sawa sisemi, ila wewe utakuja lini kuhamia hapa nyumbani?”
“Nitakuja tu hata usijali!”
“Niambie ni lini bhana, mimi nitaondoka humu nyumbani hadi urudi”
“Hata usiondoke, wakukute hapa hapa na kwa hakika hawatakufanya chochote halafu wakirudi jifanye haujapona uweze kuwasikiliza maongezi yao yote kwanza. Hata usiwe na mashaka nitakusaidia, ila usimwambie yeyote kama nimekuja hapa. Kwaheri, mimi naondoka hadi wakati mwingine nitarudi rasmi”
Salome aliondoka, ila Sara alijiangalia mara mbili mbili na kwenda chumbani kujiangalia kwenye kioo ila bado hakuamini kama amepona kabisa na anaona na kuongea. Akachukua simu yake na kumpigia Ommy kuwa aje nyumbani kwao, kwakweli Ommy alifurahi sana na kumuahidi kufika muda sio mrefu.
Basi Salome nae alitoka getini na kumuangalia Yule mlinzi kisha akamwambia,
“Wewe si upendi umbea eeh halafu umbea ufanyagi, tafadhali iwe ni siri yako kama nilifika hapa siku ya leo”
Salome akaondoka zake huku mlinzi akimshangaa na kujiuliza,
“Huyu dogo aliambiwa na marehemu Moza nini kuwa mimi sipendi umbea mmmh!”
Alimshangaa sana na kumuangalia hadi alipoishia kuondoka.


 
SEHEMU YA 57


Muda kidogo Ommy alifika na kugonga geti kisha kuingia ndani, na alipoingia tu akamuita sara ambaye alitoka sebleni,
“Eeeh Sara unaongea?”
“Ndio naongea”
Ommy akamkumbatia sara, pale kisha akakaa nae,
“Eeeh niambie ni dawa za Yule babu eeh!”
Sara akatamani kumueleza yaliyojiri ila akahofu kwamba Salome alimwambia kuwa asiseme,
“Mbona kama unasitasita hivi?”
“Natamani kukueleza yaliyotokea ila nashindwa sababu nimeambiwa nisiseme”
“Aaah jamani Sara umenza kunificha tena mpenzi!”
“Hapana sikuficha, ila kiukweli Yule babu amenisaidia sana. Ndio kafanya nipone kwakweli”
Ommy alifurahi sana na kumkumbatia tena Sara, kisha wakaenda pamoja jikoni na kupika chakula na kula, chakula kilikuwa kingi tu kwahiyo walikula na kubakisha kisha Sara akafunika kile chakula jikoni kwao. Kwakweli walikuwa na furaha sana, tena siku hiyo Ommy alishinda nae sana Sara hapo nyumbani kwao, hadi alivyoona jioni jioni akaaga na kuondoka zake.
Kwahiyo sara akabaki mwenyewe ndani, tena alienda kukaa pale pale sebleni, muda kidogo mama yake pamoja na Ana walikuwa wamerudi na walikaa pale pale sebleni wakizungumza kwani Sara alikuwa kama mtu aliyelala,
“Leo shuleni mwanangu imekuwaje maana sijaelewa eti”
“Mama nadhani kuna walimu pale wachawi pia”
“Kwanini?”
Nilitaka kwenda ofisini ila nikajibanza na kusikia mazungumzo yao, eti Yule mwalimu niliyemuangusha jana chooni leo kaja kazini”
“Kheee kaja kazini wakati ulisema hata kuinuka hatoweza?”
“Ndio ilitakiwa iwe hivyo mama, sasa nikamkuta Yule mwalimu akiwasimulia wenzie. Kuwa jana shule nzima ilikuwa kimya nay eye ameanguka choono mara gafla akatokea binti mmoja ambaye hamjui na hajawahi kumuona, eti binti Yule alimuinua na kumpaka dawa halafu akamwambia amepona. Eti Yule binti akaondoka na kumuacha Yule mwalimu akienda nyumbani kwake”
“Jamani mbona hiyo habari ya ajabu sana, au kuna waganga pale shuleni kwenu?”
“Mama, kwa uchawi wangu hakuna mganga anaeuweza hata nashangaa imekuwaje. Ndio wamenibamba pale nasikiliza umbea ndio wamenipa adhabu ya kukaa ofisini mpaka wewe ulipokuja kunichukua. Kwakweli wale walimu wamenikera sana ila sijawafanya chochote sababu nilikuwa na mawazo”
“Ila mwanangu inabidi tujue huyo mwalimu kwanini imekuwa hivyo. Na huyo binti aliyemtokea ni nani”
“Mama hata usijali, nitahakikisha najua kila kitu na kama ni mganga huyo mtu nitamkomesha”
“Yani nimeshangaa sana mwanangu jinsi ulivyo hatari saivi eti vinatokea vitu vya kuzuia mambo yako. Nimeshangaa sana”
“Mama tulia, nitafanya kitu utaona tu”
Akainuka na kwenda ndani, kisha Rose akamuangalia Sara aliyeonekana amelala pale kwenye kochi halafu akainuka na kwenda chumbani. Sara alikuwa akiwasanifu tu maana alisikia kila kitu walichokuwa wakiongea. Walipoenda chumbani, nae akainuka sasa na kwenda chumbani kwake.
Ila muda kidogo akakumbuka kile chakula ambacho alikifunika jikoni, basi akataka kwenda kukitoa ili wasielewe kama alipika siku hiyo, alipofika jikoni kile chakula hakukikuta ila aliona sahani nyeupe kabisa kanakwamba kuna mtu amekula,
“Inamaana muda huu huu Ana au mama ametoka kula au ni nini? Hivi wanaweza kula chakula bila kuuliza nani kapika?”
Akajiuliza na kuondoka kule jikoni kisha akarudi chumbani kwake, ila ilikuwa ngumu sana kwake kuelewa kuwa kile chakula kimeliwa na nani maana hakutegemea kutokukikuta ukizingatia mama yake pamoja na Ana walishaenda chumbani. Alikaa chumbani kwake akitafakari tu ila aliweza kuhisi sasa kuwa nyumba yao ni zaidi ya anavyoifikiria yeye.

 
SEHEMU YA 58


Salome akiwa amefika nyumbani kwao, akamkuta mama yake yupo ndani, kisha Salome alipoingia tu akamuanza na maswali,
“Unajua sehemu niliyokuaga naenda asubuhi, nimeenda na kurudi. Ila sasa niambie ukweli wewe ulikuwa wapi?”
“Nilienda kwa baba”
Neema akashtuka na kujikuta akimuuliza tena,
“Unasemaje Salome?”
“Nilienda kwa baba”
“Unaoajua?”
“Napajua ndio, si mamdogo Ashura alinielekeza!”
“Wewe mtoto wewe usiniletee makubwa mimi”
“Makubwa yapi mama? Yani baba kafurahi sana kuniona na alitaka nikae pale moja kwa moja nikamwambia bado sijamuaga mama”
“Nitolee balaa lako hilo Salome”
“Sio balaa mama, yani baba kwa furaha aliyokuwa nayo kanipa hadi pesa za matumizi”
“Pesa za matumizi? Ziko wapi?”
Salome akatoa pesa ambazo zilikuwa ni elfu kumi kumi, akampa mama yake. Kwakweli Neema aliishiwa nguvu kabisa kuona zile hela akataka aanze kuzihesabu,
“Hata usijisumbue kuhesabu, kaniambia ziko milioni tatu”
“Milioni tatu? Yani Patrick akupe wewe milioni tatu! Wakati huo mke wake alikuwa wapi?”
“Mkewe alikuwepo na mbona kasapoti tu, tena alitaka niongezewe ila baba akasema hizo za kuanzia”
“Mmh Salome wewe unanishangaza”
“Mama hata usishangae ila nieleze ukweli kwanini ulinificha kuhusu baba yangu?”
“Aaah unajua mwanangu, aaah yani hata sijui nianzie wapi. Achana na hizo habari bhana”
Salome akachukua zile hela kwa mama yake,
“Sasa mbona umechukua tena wakati ulinikabidhi mwanangu!”
“Mpaka uniambie ukweli, mimi ni binti mkubwa sasa. Nataka kujua ukweli wa kwanini ulikuwa unanificha kuhusu baba yangu”
“Basi naomba nikuelezee kwa kifupi, si utanipa hizo hela eeh!”
“Mi nitakupa ila niambie ukweli”
“Ni hivi, Patrick amewahi kuwa mume wangu, tena ni mume wa ndoa kabisa. Nilifunga nae ndoa ya kanisani huko kijijini kwao. Ila niliishi nae muda mrefu sana bila ya kupata mtoto, yani mimi na Patrick tulioana mapema sana. Kipindi hicho nilikuwa na miaka kumi na sita halafu yeye alikuwa na miaka ishirini. Baada ya kuishi muda mrefu bila kuzaa takribani miaka kumi ilipita ndipo tulipohamia mjini na kuendelea tena na maisha ila sikuwahi kupata mimba hata ya kusingiziwa hata mwenyewe nilikuwa nashangaa maana sikuwahi kutoa mimba maishani mwangu. Miaka ilienda tu sibebi mimba wala mdudu wa mimba, basi mjini hapa biashara za Patrick zikaanza kutanuka akawa na mali nyingi na biashara kubwa kubwa ila kilichokosesha furaha ndoa yetu ni mtoto tu. Siku moja mume wangu alizna kufanya biashara na mwanamama aitwaye Rose, Yule Rose alikuwa Rose kweli kipindi hicho alikuwa mzuri haswaaa sio kama siku hizi hata mimi mwenyewe nikawa na mashaka ya kuibiwa penzi langu na rose ingawa alikuwa ni mkubwa sana tu kwangu. Ila naye alikuwa mfanyabiashara, gafla nikaja kusikia Patrick kuna mjengo amejenga huko anaishi na Rose kumbe mimi ananiaga kuwa anasafiri halafu anaenda kuishi na Rose, kuna kipindi alipotea kama miaka mitatu kumbe ndio yupo huko anaishi na Rose. Akarudi na kuishi na mimi kama wiki kumbe ananitafutia sababu ya kunifukuza. Siku hiyo Patrick alikuja na kuniambia wazi kuwa amechoka kuishi na mwanamke asiyezaa, miaka inaenda lakini mwanamke sizai na akaniambia ameamua kuwa na huyo Rose mwenye watoto tayari kwani anaamini huyo atamzalia ukizingatia tayari ameshazaa watoto watatu, nilisononeka sana. Patrick akanifukuza pale nyumbani kama mbwa kisha ile nyumba nasikia alipangisha. Nilianza maisha ya kutangatanga na badae nikajigundua kuwa nina ujauzito, nilijua ile mimba ni ya Patrick nikawa nataka niende kumwambia ila siku hiyo nilikutana na Rose akaniambia nikithubutu kusema basi ataninyonga na kukinyongelea mbali kitoto changu. Ila bado nilijipa matumaini kuwa Patrick akigundua atafurahi, nilihangaika na ile mimba, nakumbuka nilienda kujifungulia kijijini kwa kina Patrick, na mtoto nilimuita Maria Patrick. Jina Maria ni jina ambalo mwanangu ulipewa na bibi yako yani mama mzazi wa Patrick nami nililifurahia sana. Yule mama alinipenda na ndio akaanza kumsumbua Patrick kuwa anirudie mimi na tulee mtoto wetu lakini mambo yakawa si mambo tena, siku hiyo isiyo na jina walikuja vijana na kuvamia pale nyumbani kwa mama Patrick na ndani tulikuwa tunaishi mimi, na mtoto mdogo ambaye ni wewe pamoja na mama yake Patrick. Wale vijana walimchinja mama Patrick mbele ya macho yangu, kwa hakika siwezi kusahau kamwe na nikaambiwa niondoke tena nisionekane kabisa hapo kijijini kwani nitachinjwa na mwanangu kama walivyofanya kwa huyo mama. Walinitishia na niliogopa sana, ingawa ulikuwa ni usiku nikatoka na kukimbia kwa bahati nilikuta watu njiani wakisubiri gari lao nikawaomba lifti na kuja nao mjini. Niliteseka sana na wewe mwanangu yani sikuwa na raha ya maisha kabisa, sikutaka tena kurudi kwa Patrick wala ndugu zake kwani nilihofia yasije yakawapata kama kilichompata mama Patrick. Nilikaa kama miaka mitatu au mine mjini nikitangatanga, ndio kwa bahati nikampata Ashura aliyejitambulisha kama mdogo wangu na toka siku hiyo nikaanza kuishi na Ashura tena ni yeye aliyenishauri nikubadilishe jina ili tusifatiliwe tena. Badala ya Maria tukuite Salome tena akaniambia kuwa Rose amezaa na Patrick mtoto anaitwa Ana basi nikajua furaha ya Patrick imetimia sasa maana kama mtoto ameshapata, basi ndio imekuwa hivyo hadi leo. Naomba nisiendelee sana mwanangu, mengine utayajua taratibu tu. Basi nipe hizo hela”
Salome alichukua zile hela na kumkabidhi mama yake, kisha akainuka na kwenda chumbani ambako alikuwa akipanga mipango mipya sababu ameshajua yote aliyotaka kuyajua.
“Sasa nimeelewa kwanini Ashura alitumwa, lakini lazima kuna kitu kilikuwa kizuizi cha kuwachinja wahusika na kuishia kumchinja mamake Patrick. Hivi Patrick anajua kweli kama Yule mwanamke ndiye alimuulia mama yake? Najua hajui ila atajua tu”
Ila kumbe alikuwa anawaza kwa sauti halafu Neema nae alikuwa amekuja chumbani kwa Salome na kujikuta akimuuliza,
“Kujua nini?”
“Hamna mama kuna kitu nafikiria tu, ila mama na wewe jiwekee utaratibu basi wa kugonga mlango kabla ya kuingia ninapolala”
“Hivi wewe Salome utanificha nini mimi, maana mimi ni mwanamke na wewe ni mwanamke. Hakuna cha kufichana”
“Hatakama mama ila ni vizuri kuwe na utaratibu huo”
“Basi nitakuwa najitahidi, ila hizi pesa zimenichanganya yani hadi najiona kama namiliki dunia vile”
“Yani mama milioni tatu tu ndio inakuchanganya hivyo!”
“Kwa mimi ni kubwa sana, ten asana yani hapa hadi sina maneno. Ngoja kesho nikafungue akaunti benki”
Salome akacheka tu jinsi mama yake alivyopagawa na zile hela ila ukweli wa hela zile angeujua sijui angefanyeje.

 
SEHEMU YA 59


Mapacha wa Rose walirudi na moja kwa moja wakaenda kumsalimia dada yao chumbani,
“Sara tumekuja kukujulia hali. Najua unatusikia tu ila kuongea na sisi huwezi ila tunakupenda dada yetu. Bado tunazunguka sehemu mbalimbali tukiulizia tiba ya tatizo lako.”
Sara akainua kichwa na kuwatazama, kisha akawaambia,
“Asanteni kwa upendo wenu”
“Khee Sara unaongea!”
“Ndio naongea”
Kwakweli walifurahi sana na kumkumbatia dada yao, yani ile furaha yao hata ikawashtua Rose na Ana. Walishtuka na kujikuta kwa pamoja wakienda chumbani kwa Sara, kwakweli nao walishangaa sana kumuona Sara anaona na kuzungumza. Naye Sara aliwauliza,
“Sasa mnashangaa nini jamani? Hamjapenda nilivyopona!”
Ana alisonya yani sonyo ambalo hata kaka zake walishtuka ila hakuna aliyemkaripia, basi Sara akaongea tena,
“Hata ukinisonya ni kazi bure tu, nimeshapona yani nimepona kabisa na huniwezi tena”
“Unasemaje wewe Sara?”
“Huniwezi tena”
Ana akataka kufanya jambo pale ila mama yake akamzuia kuwa asifanye kisha akatoka nae na kumuacha Sara na kaka zake. Mmoja akamwambia,
“Dada unajiamini sana eeh! Yule mtoto kawa noma”
“Kuna noma zaidi yake, aliniweza mwanzo ila kwasasa haniwezi tena”
Sara aliongea kwa kujiamini, hadi kaka zake wakataka sara awatajie huyo aliyemfanyia dawa akapona na huyo noma wa Ana.
“Nyie subirini tu, akija nitawaambia kwamba huyu ndio kiboko ya Ana. Anajifanya mjanja sana kumbe kuna wajanja zaidi yake, najua hata akinifanyia kitu atakuja Yule na kunisaidia. Kma ameweza kumsaidia mwalimu asiyemfahamu sembuse mimi”
Mara Ana akaingia tena chumbani kwa Sara na kusema,
“Nimekusikia yote, subiri nikuonyeshe”
Kabla hajaanza kufanya chochote chumba cha Sara kikaanza kutikisika.

 
SEHEMU YA 60



Mara Ana akaingia tena chumbani kwa Sara na kusema,
“Nimekusikia yote, subiri nikuonyeshe”
Kabla hajaanza kufanya chochote chumba cha Sara kikaanza kutikisika, wote walichanganyikiwa cha kushangaza hata ile hali ilimchanganya pia na Ana hadi akajikuta akipiga kelele ambazo zilimshtua hadi mama yao chumbani. Kelele za Ana zilifanya watu wote mule chumbani wazimie. Rose aliingia chumbani na chumba kikaacha kutikisika, alikuwa akishangaa sana na kumuuliza Ana aliyekuwa amesimama na hasira,
“Kuna nini Ana?”
Ana alimpushi mama yake na kutoka nje, kwakweli Rose alikuwa akishangaa tu na kwenda kuwagusa wanae ambao walikuwa wamezimia wote. Kiukweli hakuelewa kabisa kwani kabla aliwaacha wakiwa wanaongea na Sara ambaye kapona kimuujiza halafu akakumbuka kuwa Ana alibaki nje wakati amemwambia kuwa waondoke.
Ikabidi atoke mule chumbani kwakina Sara na kwenda tena kumfata Ana chumbani kwake, aliingia na kuongea nae kwa utaratibu kabisa,
“Mwanangu Ana niambie tatizo ni nini?”
“Mama niache, tafadhali niache”
“Sawa mwanangu, ila mimi ni mama yako mwanangu jamani. Usiponiambia na mimi utamwambia nani mwingine! Mimi na wewe ndio wa kusaidiana mwanangu. Kumbuka nakupenda sana mwanangu, ndiomana wote wale nimeachana nao ingawa wamezimia ila nimekuja kuzungumza na wewe”
“Mama, kuna mtu ananichezea akili halafu Sara anajua ukweli wote”
“Mwanangu, kama Sara anaujua ukweli najua cha kumfanya aseme ukweli kwetu hata usijali”
“Kwahiyo mama utanisaidia!”
“Ndio nitakusaidia mwanangu”
“Sasa hivi hakuna siri mama, yani watoto wako wanaelewa fika kuwa mimi ni nani na nina uwezo gani. Sasa nadhani wametafuta vya kuwasaidia ndiomana imekuwa hivi, hebu fikiria mama kabla sijafanya chochote eti chumba cha cha Sara kikaanza kutikisika kwakweli nimechukia sana”
“Kheee makubwa, sasa mbona wamezimia?”
“Sauti yangu ya kelele imewafanya wazimie, ndiomana nakwambia saivi washanijua kuwa mimi ni mtu wa aina gani. Tafadhali mama fanya kitu nijue ukweli maana nasikia aliyemfanya Sara apone ndiye aliyemuokoa Yule mwalimu aliyeanguka chooni”
“Kheee mwanangu, atakuwa jinni huyo sidhani kama ni mtu wa kawaida”
“Hata kama ni jinni sidhani kama anaweza kunishinda kiasi hiki halafu kwanini nisipate hata kengele ya hatari kuwa kuna kitu kinatendeka nyuma yangu!”
Basi Ana na mama yake wakajadili sana siku hiyo, na mama yake akamwambia atakachokifanya ili Sara aseme ukweli.
Muda kidogo Patrick nae alirudi ila aliamliwa akalale siku hiyo bila hata ya kula chochote kile humo ndani.

 
Back
Top Bottom