Simulizi: Kurudi Kwa Moza

Simulizi: Kurudi Kwa Moza

SEHEMU YA 136



Neema alikuwa bado yupo chumbani kwake tangu muda ule walipotoka hospitali hadi anaiona jioni ikikaribia, akapigiwa simu na rafiki yake mama Pendo na kuanza kuzungumza nae ambapo mama Pendo alimkumbusha Neema swala la kumpeleka mwanae salome kwenye maombi,
“Usipuuzie Neema, mwanao anatakiwa aombewe”
“Sijapuuzia, nilisafiri ndiomana uliona kimya”
“Sasa lini utakuwa tayari ili nimwambie mchungaji wetu”
“Nitakwambia tu, siwezi kusema siku wakati Salome mwenyewe sijaongea nae chochote. Nikiongea nae nitakwambia ni lini”
Basi akakubaliana nae hivyo na kukata simu, kisha akatoka na kuanza kumuita Salome ila akaona kimya na kugundua kuwa Salome ameondoka, aliwakuta tu wanae wale mapacha wakiandika andika,
“Nyie dada yenu kaenda wapi?”
“Sijui ila ametoka”
“Yani huyu mtoto ameanza tabia ya kutoka bila kuniaga! Kweli wa kufanyiwa maombi huyu”
Ikabidi Neema aanze kufanya kazi zake za hapa na pale, ila hadi anamaliza kupika kisha watoto wake wale mapacha kwenda kulala ila Salome alikuwa hajarudi na kushangaa kuwa Salome kama alikuwa anaenda kulala huko huko si angalau angemuga basi, wakati analalamika hivyo akasikia hodi, alipoenda kufungua alikuwa ni Salome na Patrick ambapo aliwakaribisha vizuri tu kisha Salome akawaambia,
“Mi naenda chumbani kwangu, kwahiyo nyie endeleeni na mazungumzo tu”
Salome aliondoka, ila Patrick na Neema waliganda tu wakiangaliana na hakuna aliyemsemesha mwenzie kwani kwa muda huo kila mmoja alijiuliza kuwa nani anastahili kuanza kuongea kati yao. Muda nao ulizidi kwenda ikabidi Neema ajitoe muhanga,
“Nakusikiliza Patrick”
Wazo la haraka haraka la Neema alihisi kuwa Patrick ameenda kudai zile pesa zake alizomleteaga ndiomana alishindwa kuanza kuongea nae, ila Patrick leo alikuwa kama mtu aliyeshikwa na ganzi,
“Sijui hata nisemaje, ila nisamehe Neema”
“Mi nishakusamehe siku nyingi mbona”
“Nifanye nini unisamehe?”
“Wewe mbona mimi nishakusamehe jamani!”
Patrick alikuwa kimya tena kwani kadri alivyomuangalia Neema aliona anazidi kuwa mzuri, alimuona Neema akiwa mrembo zaidi kupita Yule Neema aliyemuoa akiwa na miaka kumi na sita, alijikuta akitamani kumuuliza kuwa mbona urembo ulizidi ila mdomo ulikuwa mzito, Neema nae alimuona Patrick akiwa zaidi ya vile alivyomuoa kipindi cha nyuma, alimuona Patrick amekuwa na sura ya kuvutia hatari, akajikuta anamwambia,
“Naenda kulala bhana”
Neema hakutaka tena kumuangalia Patrick kwani alihisi kumtamani ila ile alivyoinuka baada ya kumwambia naenda kulala, Patrick nae aliinuka na kufatana na Neema hadi chumbani, kwahakika Neema hakuweza kumfukuza Patrick ukizingatia alishakuwaga mume wake.

Kulipokucha, Patrick alikuwa amelala pembezoni mwa Neema na alijisikia vizuri sana, walijiona kamavile mapenzi yao ndio wametoka kutongozana. Waliamka wakitabasamu, na walipotoka chumbani walikuta Salome ameshawaandalia kifungua kinywa, kisha akawakaribisha mezani na kusema,
“Baba, kuanzia leo naomba uhamie hapa”
Patrick alicheka tu ila kicheko cha furaha kwani alijihisi kama amekuwa mtu mpya kabisa kwa siku hii na alikubaliana na kila jambo aliloambiwa na Salome.
 
SEHEMU YA 137



Rose aliamshwa na sauti ya mlinzi wake aliyemuomba kwaajili ya maongezi, alipotoka alimsalimia kisha Yule mlinzi akamwambia hoja yay eye kutaka kuondoka kwenye nyumba hiyo.
“Jamani kwanini unataka kufanya hivyo?”
“Mama siwezi, sijawahi kukukosea heshima hata mara moja mama yangu ila kwa hili naomba tu nirudi nyumbani, siwezi kuendelea kuishi humu ndani”
“Jamani nimekuzoea ujue Lazaro, sipendi unavyosema unaondoka. Nitakuongezea mshahara ila usiondoke hapa nyumbani kwangu”
“Mama, hapana acha tu nirudi kwetu”
“Tumetoka mbali Lazaro, kumbuka wewe ni mtu pekee unayefahamu vitu vingi kuhusu mimi, nakuomba Lazaro usiondoke. Kumbuka umeanza kukaa kwangu ukiwa kijana mdogo sana, tafadhali Lazaro usiondoke jamani”
“Basi, naomba niruhusu niende nikasalimie tu halafu baada ya wiki nitarudi”
Kuhusu hilo ikabidi Rose akubali ila wazo la Yule mlinzi ilikuwa akiondoka tu basi harudi tena, basi Rose akampa mlinzi wake hela baadhi na kuagana nae.
Mlinzi alibeba kila kilicho chake kwani lengo lake lilikuwa ni kuondoka na kutokurudi tena kwenye nyumba hiyo, na kweli aliondoka eneo hilo na kwenda kupanda basi la kwenda kwao, ila alipofika tu stendi ya kwao na kushuka kwenye lile basi alijikuta yupo ndani kwenye nyumba ya Rose huku mizigo yake ikiwa pembeni.

Mlinzi alibeba kila kilicho chake kwani lengo lake lilikuwa ni kuondoka na kutokurudi tena kwenye nyumba hiyo, na kweli aliondoka eneo hilo na kwenda kupanda basi la kwenda kwao, ila alipofika tu stendi ya kwao na kushuka kwenye lile basi alijikuta yupo ndani kwenye nyumba ya Rose huku mizigo yake ikiwa pembeni.
Alishangaa sana na kupatwa kama na sintofahamu maana ilikuwa ni kitu cha ajabu kwake ukizingatia alipanda gari la kwenda kwao na gafla anajikuta tena nyumbani kwa Rose, kwahiyo alikuwa akishangaa shangaa tu pale huku mizigo yake ikiwa pembeni. Salome alienda pale getini na kumshangaa pia halafu akamuuliza,
“Vipi na mizigo?”
“Yani sielewi, sielewi kabisa. Nilikuwa nishaondoka kwenye nyumba hii, nilishafika hadi stendi kwetu cha ajabu nimerudishwa tena hapa”
“Nani kakurudisha sasa?”
“Sijui ni nani, ila mimi mwenyewe nakumbuka kuwa mara ya mwisho nilikuwa stendi ya kwetu nashangaa nimerudi tena hapa. Kwanza saa hizi saa ngapi?”
“Saa tisa, kwani vipi?”
“Haya ni mambo ya ajabu sana, kutoka hapa hadi kufika kwetu ni masaa saba, ni kweli hapa nimetoka saa mbili asubuhi ila nimerudishwa kwa sekunde jamani, hii si haki yani hata kijijini kwetu sikufika, nilifika tu mkoani. Hili swala sio haki kabisa”
“Sasa nani kakufanyia hivyo?”
“Sijui ila natamani nifike kwetu jamani, nimechoka mimi na maajabu ya nyumba hii”
“Unatakiwa tu uwe mvumilivu, utapoteza nauli bure tu. Wewe tulia na usifikirie kila anayerudishwa hapa ni mchawi, je wewe ni mchawi?”
Akakumbuka jana yake aliwaambia watu wa humo ndani wote wachawi kwasababu alikuwa anawaona kutoka halafu hawaoni kuingia ila leo jambo hilo lilikuwa limempata yeye, akaona kwa staili ile ni ngumu kwake kuondoka ila hapo hapo alipata wazo la kuwasiliana na kwao ili awaeleze kuhusu tatizo hilo maana limekuwa kubwa sana kwa upande wake.
 
SEHEMU YA 138

Rose baada ya mlinzi wake kuondoka asubuhi ya siku hiyo, na yeye alifanya safari ya kumtafuta mganga wake aliyemfikiria kichwani, alimtafuta sana bila ya mafanikio ila njiani akakutana na rafiki yake wa muda mrefu sana ambaye aliwahi kumshauri kuhusu swala la waganga kwahiyo alivyokutana nae alifurahia sana, na kuanza kumshirikisha kuhusu swala lake linalomsumbua kichwa.
“Basi mwezi uliopita mwenzio nilipatwa majanga hayo balaa, yani kuna mavitu yalichanganya kichwa change kama nini ila kuna kijana huyo ni matata, kwanza kijana haogopi kitu yani hakuna takataka yoyote inayomshinda. Huyo kijana ni kimbilio la watu wengi sana, wanaotafuta watoto, wanaotafuta mali yani kila kitu. Nina uhakika huyo kijana hawezi kushindwa, hao waganga wako wamechoka halafu waoga”
“Huyo atakuwa mzuri kweli, nilijaribu kumtafuta hata Yule wa mwanzo aliyewahi kunipa dawa ya kufukia ndani kwangu ila sijampata”
“Unadhani Yule unampata kirahisi hivyo? Yule hakuwa mganga ni jinni lile, na anapatikana kwa waganga wanaojiweza tu, Yule mganga tuliyeenda kipindi kile alikuwa anajiweza ndiomana ikawa rahisi kukutana na Yule wa dawa. Ingawa masharti mengi umeyavuruga ila kwa Yule ndio kiboko”
“Naomba nipeleke ndugu yangu, nipo tayari kutoa kitu chochote kile ila niepukane na aibu hii maana kwangu ni aibu na fedheha”
Basi huyu rafiki wa Rose akajitolea kumpeleka Rose, na kwavile alimuomba ampeleke siku hiyo hiyo akajitolea kufanya hivyo ingawa ni mbali sana hiyo sehemu.

Patrick hakujisikia kuondoka kabisa nyumbani kwa Neema, na alichofanya Salome ni kwenda kumchukulia Patrick nguo zake zote na kumfanya afurahi zaidi kurudi kwa Neema, alimuomba Neema asimfukuze eneo hilo kwani alizidi kufunguka mawazo ya kuhusu mali zake na nyumba zake ambazo zingine alikuwa hata haendi kuzitembelea kwavile alishazisahau ila Neema akawa kama amemkumbusha kwahiyo alifurahi sana kumalizia muda wake kwa Neema, na pia watoto wale mapacha wa Neema aliwaona ila aliogopa kuuliza kuwa wale watoto ni wa nani, ila alijikaza na kuuliza,
“Samahani Neema, na hawa watoto wako wengine baba yao yuko wapi?”
Neema akacheka kisha akamwambia,
“Baba yao ni wewe”
“Ni mimi? Kivipi?”
“Najua huwezi kukumbuka au kujua, hii kitu niliiweka siri siku zote za maisha yangu”
“Niambie kivipi?”
Basi Neema ilibidi amueleze Patrick ilivyokuwa,
“Kuna kipindi nilikuwa nauza baa, na ulikuja kunywa sijui ulikuwa na mawazo gani ila ulikunywa sana hadi ulilewa. Ikawa kila mwanamke anayepita mbele yako unamshika, ilibidi nidanganye kuwa umenihitaji mimi na kwenda na wewe chumbani, ila kwa nguvu ya pombe uling’ang’aniza kulala na mimi, kwavile nilikuwa bado nakupenda sikuweza kukataa, nililala na wewe ila usiku wake niliondoka na kukuacha umelala fofofo. Kulipokucha uliondoka halafu na mimi niliacha kazi pale kwenye ile baa, sikuwahi kumwambia mtu yeyote kilichotokea baina yangu na yako, na baada ya mwezi nilijigundua kuwa nina ujauzito hapo ndipo nilipoamua kufanya siri hadi nimejifungua. Ilikuwa ni siri yangu hata ndugu yangu Yule Ashura sikuwahi kumwambia chochote, ingawa sasa nimegundua hakuwa ndugu yangu, yani kama hakuwa ndugu yangu alikuwa na mipango gani kwangu? Ni siri yake kwakweli, ila hakuwahi kujua kuwa watoto wangu ni wa nani sababu mar azote alizoniuliza nilimwambia kuwa nilibakwa”
Patrick alishangaa sana hii habari, na kujaribu kuvuta kumbukumbu ya siku aliyolewa sana, alikumbuka tu kuna siku alilewa sana ila hakukumbuka ni kitu gani alikifanya,
“Na hiyo siku niliyolewa sana ndio siku iliyobadilisha maisha yangu kabisa, maana tangu siku hiyo niliporudi nyumbani ndio nikafanywa kama ndondocha yani sikuwa na uwezo wa kwenda sehemu yoyote ile bila ruhusa ya Rose, yani kipindi hiko ndio mateso yalizidi kwangu maradufu”
“Pole sana, basi hivyo ndivyo ilivyokuwa kuhusu hawa watoto. Yani ni wanao kabisa”
“Kwakweli nimeteseka sana mimi, siku ile ilipelekea kunywa sana pombe baada ya kumuona mke wangu akiniwekea dawa kwa macho yangu, mimi sio mlevi kiasi kile ila siku ile nililewa sababu ya mawazo. Ila kitendo cha kurudi nyumbani ndio nikawa ndondocha kabisa, yani hakuna kitu nilichokuwa nafanya kwa akili yangu.”
Patrick aliomba aitiwe watoto wale ili awaangalie kwa karibu maana hakuamini amini kuwa alikuwa na watoto, maana alijua kuhusu Salome ila hakujua kama ana watoto wengine.
Neema aliwaita watoto wake, nae Patrick aliwakumbatia kwa furaha hata wale watoto walibaki kushangaa tu kwani hawakutegemea huyo mtu kuwafurahia kiasi kile tena huku akiwaita wanangu, walikuwa wakishangaa shangaa tu ikabidi Neema awaambie,
“Baba yenu huyo”
Na wao wakashangaa na kufurahi maana hawakufikiria kutambulishwa baba, kwani siku zote walipokuwa wakiulizia kuhusu baba yao Neema alikuwa akiwafokea sana.
Patrick akazidi kupata uchungu dhidi ya Rose na mali zake, ilimuuma sana na kumfanya sasa awaze namna ya kurudisha mali zake kwenye mikono yake ili watoto wake wafaidi.
 
SEHEMU YA 139


Ana alishaamua kujitoa kabisa kwenye maswala ya waganga na kumkataza mama yake kwa kadri awezavyo lakini mama yake alikuwa mbishi sana, yeye Ana alikuwa na uwezo wa kupata hisia za mama yake alipoenda kwahiyo siku hiyo akapata hisia kuwa mama yake kaenda tena kwa mganga ila inaonyesha wazi alishindwa kumuaga sababu alijua angemzuia.
Ana alikuwa chumbani kwake, alifunua godoro lake na kutoa dawa yake, kwa mara ya kwanza aliamua kutumia dawa yake ili avuruge akili ya mama yake na kumfanya arudi nyumbani na ili aweze kubaini ni nani anaewaumiza kwenye nyumba yao. Aliamua kwanza abaini ane waumiza katika nyumba yao,
“Jitokeze nikuone wewe unayetusumbua humu ndani”
Alisema maneno hayo kama mara tatu na gafla alihisi kuna mtu kasimama mbele yake, aliinua kichwa chake huku amejawa hofu ila alijitia ujasiri na kumtazama mtu huyo, alikuwa ni Moza kwakweli Ana alishtuka sana na kumfanya ashindwe hata kumuuliza chochote zaidi ya kutetemeka tu. Moza alimuangalia Ana na kucheka ila Ana hakuweza kumtazama zaidi Moza, na badala yake alijikuta akizimia tu pale ndani kwake.
Muda huu Sara alikuwa nje ya chumba cha Ana akigonga na aligonga kwa muda mrefu sana bila ya kufunguliwa hadi ikabidi afungue mwenyewe, alishtuka sana alipoingia ndani kwani alimuona Ana akiwa kajifunika makhanga halafu kuna kitu pembeni yake ambacho alikishangaa sana Sara kwani hajawahi kuona kitu cha namna ile tangia azaliwe, alipiga kelele na kumfanya kaka yao Kulwa aje ndani pia ila alishangaa alichokiona pembezoni mwa Ana muda huo Ana akiwa kazimia, alimshika mkono Sara na kumtoa nje haraka haraka kisha kumwambia,
“Yule mdogo wetu ni mchawi, yani bila ubishi Yule ni mchawi, sasa ndugu yangu maswala ya kumfatilia mchawi ni maswala mazito sana. Pale tunamuona kama kaanguka ila huwezi jua labda ameenda kwenye uchawi wake utashtukia anashtuka na kuanza na wewe, tukae mbali dada yangu tunaishi na nyoka humu ndani”
Sara hakuweza hata kuchangia hoja kwani kiukweli mambo ya nyumbani kwao yalimchosha tena sana tu ila hakuwa na jinsi na hakuwa na pakukimbilia, muda kidogo Salome nae alitokea nje na kuwafata sebleni Sara na kaka yake kisha kuwauliza kuwa kuna nini, ila Sara nae alimuuliza,
“Hili hujalijua au?”
“Ningelijua ningeuliza?”
“Na sisi hatujui kuna nini”
Salome alicheka kisha akaelekea njia ya vyumbani, ila Sara alimuangalia sana Salome kwani siku hizi alianza kuwa na mashaka nae pia.
 
SEHEMU YA 140


Rose kule alipopelekwa kwa mganga walifika jioni kabisa karibia na usiku hata hivyo mganga mwenyewe hawakumkuta, ni baadae ambapo giza lilikuwa limeingia kabisa ndio alirudi na kukuta kuwa anangojwa kwa hamu zote. Rose alitaka kuhudumiwa usiku huo huo ingawa Yule mganga pia alikataa kumuhudumia kwa usiku huo kutokana na mlolongo wa matatizo yake.
“Labda tuanze tiba saa nane usiku”
“Nipo tayari hata saa ngapi ila hili jambo liishe, nateseka sana”
“Litaisha tu, hapa ndio mwisho wa matatizo yote”
Rose alisubiri kwa hamu zote hata kulala kidogo hakutaka, rafiki yake aliyempeleka aliamua kuondoka na kumuacha Rose muda uleule, kwahiyo Rose alibaki peke yake kwa Yule mganga huku akisubiri tiba, hakujali kukoje kukoje kule ila alichojali yeye ni kupata tiba tu.
Rafiki wa Rose alijulikana kwa jina la mama Jack, muda aliokuwa anarudi kwake ni usiku tayari ulishaingia kutokana na kwake kuwa mbali kidogo na kwa mganga huyo, ingawa alitumia usafiri wa kukodi ila alichelewa sana kufika nyumbani kwake.
Alipofika tu alimuona mtu yupo pembezoni mwa nyumba yake akilia kanakwamba ni mtu aliyekuwa na shida, alipomuangalia alimuona ni binti mdogo tu, alimfata na kumuuliza tatizo,
“Vipi binti?”
“Nimefukuzwa na mama wa kambo”
Huku Yule binti akiendelea kulia, mpaka mama Jack alimuonea huruma kwani alijua wazi kuwa ikiwa atamuacha hapo nje binti huyo anaweza kubakwa na vijana wasio na huruma kwahiyo alimwambia aingie nae ndani kisha kuzungumza nae na kumuahidi kuwa kesho atamsaidia afike kwa mama yake. Yule binti alikubali na kumshukuru sana huyu mama, kisha Yule mama akamuandalia sehemu ya kulala binti Yule. Hakuwahi kumuona, hakuwahi kumfahamu ila ni huruma tu ndio iliyomfanya amsaidie. Yule binti alionyesha kumshukuru sana Yule mama kiasi cha kumfanya Yule mama ajisikie vizuri na ajione kuwa katenda jambo jema sana kumsaidia Yule binti.
 
SEHEMU YA 141

Ilipofika saa nane usiku Yule mganga alianza kufanya dawa zake, Rose alikuwa macho kabisa kwani alitaka kwanza kushuhudia anavyofanyiwa dawa. Yule mganga alijifungia kwa mud, kisha akatoka na kumwambia Rose,
“Unahisi ni nani anayekufanyia mambo ya ajabu?”
“Ni Yule binti Salome, sijui kapata wapi uchawi”
“Hapana, anayekuchezea wewe ni Moza”
Rose alishtuka na kumuuliza mganga kwa mshangao,
“Moza”
“Ndio Moza, amerudi kwa lengo moja tu la kukutesa wewe”
“Kwahiyo Moza alikufa na kurudi?”
“Hapana, Moza hakufa kama unavyofikiria ila Yule unayemsema Salome si Salome ni Moza Yule. Nimekwambia amerudi kwa kasi ya ajabu”
“Kheee, kwahiyo Salome yuko wapi?”
“Salome yupo mahali na amelala usingizi mzito sana, si mimi wala si wewe tunaoweza kumuamsha labda Moza mwenyewe apende kumuamsha na atamuamsha endapo azma yake ikikamilika”
“Mmmh ana azma gani kwangu?”
“Anataka uwaachie wale watu uliowafungia kwenye kichumba”
“Mmmh siwezi mganga, itanigharimu maisha yangu yote, siwezi”
“Anatambua hilo kuwa itakugharimu maisha yako yote ndiomana anataka wewe mwenyewe uwatoe, huyu Moza ni amejipanga yani amejipanga haswaaaa”
“Sasa nitafanyaje?”
“Inahitajika kafara”
“Nipo tayari kuwatoa kafara wale niliowafuga”
“Hapana hawatakiwi hao, kafara inayohitajika ni kafara ya mtoto wako”
Rose alipata hofu kusikia habari ya kutoa mtoto wake kafara tena, uoga ulimshika kwani hakutaka kuona mtoto wake yeyote anakufa kwaajili yake.
“Hakuna njia nyingine?”
“Hakuna, zaidi ya kutoa kafara. Ikiwa unahitaji kuendelea kubaki kwenye nafasi yako, toa mtoto wako kafara”
“Mmmh sasa nitamtoa mtoto wangu gani?”
“Mtoe mwanao wa hospitali, kwani itakuwa rahisi sana kusema kuwa kafia hospitali sababu ya kuungua maji moto”
Kidogo maneno ya huyu mganga yalikuwa yakimuingia vilivyo Rose na kuanza kuhisi kuwa huyu mganga ni mkweli, akafikiria kuhusu mwanae Doto ila badae akaona ni vyema kumtoa kafara mwanae Yule mmoja na kuokoa maisha yake na maisha ya watoto wake wengine, akamkubalia mganga na kusubiria maelekezo atakayompa. Ila mganga alikubaliana nae kumpa masharti asubuhi ya siku inayofuata.

Asubuhi yake, mganga alimtaka Rose kwenda mtoni na kumwambia kuwa huko ndiko ambako ataenda kutoa kafara, kuna dawa alimpa na kumwambia kuwa ataenda kuinyunyiza mtoni halafu kingetokea kitanda cha hospitali ambacho kalazwa Doto kisha kitanda hicho akisukumie mtoni hapo atakuwa amefanikiwa na kumtoa kafara mtoto wake, Rose aliona hilo swala ni jepesi kwake kwani halikuwa sharti gumu kumfanya shindwe kulitekeleza, kwahiyo alichukua hiyo dawa na kuanza safari ya kwenda mtoni.
Alivyofika mtoni alimwaga dawa ile kwenye mto, ni kweli kikatokea kitanda pembeni na alipoangalia aliyelala kwenye kitanda hicho hakuwa Doto bali alikuwa ni Moza.
 
SEHEMU YA 142




Alivyofika mtoni alimwaga dawa ile kwenye mto, ni kweli kikatokea kitanda pembeni na alipoangalia aliyelala kwenye kitanda hicho hakuwa Doto bali alikuwa ni Moza.
Rose aliogopa na mkono wake kuanza kutetemeka hata akashindwa kukisukuma kile kitanda mtoni badala yake alikimbia haraka haraka kurudi nyumbani kwa Yule mganga.
Alifika anahema sana, ila alimkuta mganga amechukia vilivyo,
“Umefanya nini wewe?”
“Nimemwaga dawa ila hakutokea Doto, bali alitokea Moza”
“Hata kama ungemsukuma mtoni hivyo hivyo, yani ushaharibu kila kitu”
“Nisamehe”
“Nikusamehe nini na ushaharibu”
“Sasa hutotoa kafara mtoto wako mmoja, itabidi utoe wawili”
Rose alishtuka sana kusikia atoe kafara ya watoto wake wawili ukizingatia huyo mmoja tu alikuwa anafikiria sasa kuhusu wawili ataweza kweli, ikabidi amwombe mganga akafikirie kwanza.
“Hili si jambo la kufikiria ila ni jambo la kufanya maamuzi”
“Mganga nina watoto wane tu, watoto wangu wote ni wa muhimu kwangu”
“Kwahiyo wanao ni wa muhimu kuliko maisha yako?”
“Sikia ndugu yangu, yani watoto hawa ndio wamefanya siku zote hizi nihangaike sababu yao. Yani yote haya ninayoyafanya kwenye maisha ni sababu yao, yani leo nikawatoe kafara kweli?”
“Chagua moja, kuwatoa watoto wako kafara au wewe kuumbuka”
Yule mganga akainuka na kumuacha Rose akiendelea kuwaza kuhusu kuwatoa kafara watoto wake, aliwaza sana bila ya kupata jibu na kufanya kama akili yake kukosa uelekeo.
Yule mganga alirudi tena na kumuuliza Rose kuwa amechagua jambo gani sasa,
“Hapana kwakweli, siwezi kuwatoa kafara watoto wangu”
“Yani hapo watoto wawili tu unasema huwezi, je ukiambiwa wote?”
“Hapana siwezi”
“Basi wewe ndio utolewe kafara”
Rose akashtuka na kuuliza kwa makini,
“Nitolewe kafara kwanini?”
“Umekiuka masharti yangu, na mimi sipo tayari kufa kwaajili ya ujinga wako kwahiyo nitakutoa kafara wewe”
Katika vitu ambavyo Rose alikuwa anaviogopa katika maisha yake basin i kifo, yani kwake ilikuwa ni rah asana kusikia wengine wamekufa ila yeye hata akianza kuumwa tu basi hofu ya kifo humkaa kichwani, kwahiyo swala la kuambiwa kuwa atolewe kafara yeye lilimchanganya akili vilivyo hadi akajikuta anakubali kuwatoa kafara watoto wake.
“Nitawatoa hao wanangu wawili kafara”
“Kwahiyo utamtoa yupi na yupi?”
“Wale mapacha”
“Mapacha hata ukiwatoa wote bado utaonekana umemtoa mmoja sababu wale wamezaliwa siku moja, kafara yao inabidi iwe ya siku tofauti ili iwe na nguvu ila kwa siku moja itakuwa haina nguvu na kafara ninayoitaka mimi ni ya siku moja. Mweke mwingine wa kumtoa kafara hapo”
“Ana najua haiwezekani ila Sara, jamani yani nimtoe mwanangu Sara kifungua mimba wangu! Nampenda Sara jamani, tafadhari nisimtoe Sara”
“Unatakiwa kumtoa, ndiomana nimekwambia kama huwezi basi kafara tukutoe wewe”
Kwa kuhofia kifo akajikuta anakubali kuhusu kuwatoa watoto wake kafara, kwahiyo kilichofatia ni mganga kumpa masharti ya kafara anavyoitaka iwe, kwahiyo Rose alikuwa makini kabisa kusikiliza mlolongo wa kafara.
 
SEHEMU YA 143


Mr.Patrick alimuaga Neema kuwa anaenda kumchukulia kitu Fulani ila hakutaka kumtajia, ukweli ni kuwa alijiona mwenye bahati sana kupokelewa tena na Neema na alimuona Neema ni mwanamke mwenye upendo sana juu yake.
Aliondoka nyumbani hapo kwa Neema na alienda kwenye nyumba nyingine aliyowahi kujenga ili aiangalie kama inafaa kumuhamishia Neema hapo, ila wakati yupo kwenye ile nyumba mara wakaja vijana watatu na kumsalimia kisha wakajitambulisha kuwa wao ni wafanyakazi wa Rose, kwahiyo Patrick alitulia akiwasikiliza kwa makini kuwa wana jambo gani wanalotaka kuongea nae,
“Sikia tukwambie, kuna kazi mama alitupa ila kazi yenyewe sijui alipanga yale mazingira tumekuta mambo hayaeleweki kabisa, halafu tunamtafuta hewani hatumpati”
“Hata siwaelewi mjue”
“Hutuelewi kivipi kwani kazi za mkeo huzijui?”
“Bado siwaelewi”
“Sisi tunamtafuta hewani tumpe habari kuwa ile maiti tuliyoendaga kuitupa tumeenda kuifukunyua tumekuta imeoza na ananuka vibaya ila sura ni ya Yule ndugu yake aliyetupa kazi”
“Maiti? Bado siwaelewi”
“Huyu mzee vipi jamani, hatuelewi nini? Hebu toa simu yako umuonyeshe picha za ile maiti tulivyoikuta”
Mmoja akatoa simu na kumfungulia picha Patrick aione, kwakweli Patrick alitamani kuruka, picha ilionyesha maiti kaoza oza ila sura yake inatambulika bado na ilikuwa ni sura ya Ashura. Kwakweli Patrick hakuweza hata kuitazama mara mbili na kuamua kuwauliza tena,
“Inamaana mmemuua Ashura?”
“Hapana ila sisis tulipewa kazi tu ya kutupa ile maiti na tuliambiwa ni maiti ya mtu mwingine halafu tulikuwa tunawasiliana na huyo huyo Ashura nahisi kuna mtu katuzunguka kamuua Ashura halafu kataka sisi tubebea maiti tukijua ni yeye kumbe ni Ashura”
“Mtu gani huyo?”
“Sisi tulitumwa kubebe maiti ya binti mmoja anaitwa Salome, na tulivyobeba tulijua ni Salome kumbe ni Ashura”
Yani hapo ndio walizidi kumchanganya kabisa Patrick kwani hakuelewa kitu chochote kile, halafu wale vijana wakaanza kumueleza kwa utaratibu sasa jinsi ilivyokuwa ambapo kwa mujibu wa maelezo ya wale vijana inaonyesha wazi mtu aliyemuua Ashura atakuwa ni Salome.
“Hapana, hapana kabisa haiwezekani, mwanangu Salome hawezi kuwa muuwaji”
“Kumbe ni mwanao!”
“Ndio ni mwanangu”
“Kama ni mwanao kwanini mkeo alitaka tumuue?”
Patrick hakuwa na jibu kwani muda huu akili yake kama ilipoteza majira hivi, alikuwa haelewi kitu chochote kile hakuendelea hata kuangalia nyumba aliamua tu kuondoka zake eneo lile.
 
SEHEMU YA 144


Rafiki wa Rose, leo aliamka na kumkuta Yule binti aliyemkaribisha kwake akiwa ameamka pia huku akifanya shughuli za mule ndani hadi mama Jack akashangaa kuwa huyu mgeni ni wa wapi kiasi cha kufanya shughuli za nyumbani kwake, kwahiyo alisalimiana nae na kumsikiliza kuwa anataka amsaidiaje,
“Mimi naomba unipeleke kwa mama yangu”
“Lakini kwa mama yako si unakujua, kwahiyo nitakupakiza tu gari uende”
“Nakuomba twende wote, napenda mama asikie mtu aliyeniokoa alinikuta kwenye mazingira gani. Naomba unipeleke, mama yangu ana hela na atakulipa kwa shukrani ulizomfanyia”
Mama Jack akasikiliza maneno ya Yule binti ila muda mwingine kama moyo wa imani ulimshika kwahiyo akamuomba waende mchana mchana na Yule binti alionyesha kufurahishwa sana,
“Asante sana mama yangu, nitakumbuka ukarimu wako siku zote za maisha yangu”
“Usijali binti mzuri”
Kwahiyo mama Jack alijikuta akisaidiana na Yule binti kwenye kila kitu hadi muda ulipofikia wa kwenda nyumbani kwa binti, ila wakiwa njiani binti alimuomba mama Jack amsindikize hospitali kumuona ndugu yake nae alifanya hivyo bila hiyana yoyote, walifika hospitali na kumuomba mama Jack amsubiri nje ya wodi, huyu mama alikubali ila hakuelewa kitu chochote wala hakumuelewa huyu binti sababu hakumjua ila alimsaidia, baada ya muda kidogo Yule binti alitoka huku akimsaidia mgonjwa wake kujikokota na kusema kuwa karuhusiwa, sababu mama Jack alikuwa na usafiri hakuona hiyana ya kumsaidia Yule binti kumrudisha na huyo anaedai ni kaka yake nyumbani.

Rose alitulia akisikiliza dawa anazopewa na Yule mganga, ambapo alianza kwa masharti,
“Hakikisha siku ya leo hakanyagi rafiki yako yoyote nyumbani kwako”
“Hata hivyo hakuna rafiki yangu anayepajua nyumbani kwangu”
“Sawa, ukifika tu getini utapuliza dawa hii”
“Sawa, baada ya hapo”
“Utaingia ndani bila kuongea na yeyote ila cha kwanza kabisa, utaanza kumuita jina mwanao aliyeko hospitali maana ukifanya hivyo tu mwanao kule atakufa. Kisha unajifanya ulikosea unaanza kumuita mwanao mwingine wa Kafara, ataanguka alipo na kufa. Hakikisha unaita majina wakati ushaingia ndani kabisa na kwenye kochi umekaa, yani ita kamavile huna wasiwasi na kilichopo au kitakachotokea. Ukipata habari ya msiba wa watoto wako, jifanye umechanganyikiwa na upotee nyumbani kwako yani uje huku mpaka watakapozika. Utakaporudi watakuonyesha tu makaburi ya watoto wako ila baada ya hapo, kila mtu mjini atakujua wewe ni nani maana mali zako zitaongezeka maradufu na utazidi kuheshimika”
“Nimeipenda hiyo ingawa wanangu wananiuma ila hiyo ya mali zangu kuongezeka nimeipenda sana”
“Ila hakikisha nyumbani kwako asifike mgeni wa aina yoyote”
“Haiwezekani mganga, kwanza saivi watoto wote wanapaogopa pale nyumbani kwahiyo hata kualika rafiki zao ni ngumu”
“Sawa, na rafiki zako pia wasifike”
“Hawatofika, yani hakuna anayepafahamu pale”
Rose alijiaminisha vilivyo kuwa hakuna anayepajua nyumbani kwake, mganga alimpaka dawa nyingine ya kumkinga akimwambia kuwa hiyo itamsaidia zidi ya Moza kwani hatomuona tena kwenye macho yake na hatoweza tena kumsumbua.

 
Back
Top Bottom