Simulizi: Kurudi Kwa Moza

Simulizi: Kurudi Kwa Moza

SEHEMU YA 145


Mama Jack alifika nyumbani kwakina Yule binti na kukaribishwa vizuri sana, mama Jack hakuelewa kuwa alikuwa mtegoni maana Yule binti alikuwa ni Salome ambapo alipitia hospitali kumchukua Doto kwahiyo mama Jack alifika kwenye nyumba ya Rose bila kujua kuwa pale ni nyumbani kwa Rose, na kwavile mama Jack hakuwazoea watoto wa Rose kwahiyo ilikuwa vigumu sana kwa yeye kugundua kuwa wale ni watoto wa Rose, mtoto pekee wa Rose aliyemfahamu alikuwa ni Ana na muda huo aliofika Ana alikuwa bado yupo shuleni.
Walimkaribisha vizuri sana huku Salome akiwaambia kuwa Yule mama kamsaidia sana bila ya kusema kuwa kamsaidia vitu gani, ila Salome alimuomba huyu mama asubiri mama yao atarudi nyumbani muda sio mrefu, Sara alimuuliza Salome,
“Una uhakika mama atarudi leo?”
Salome alimuangalia kwa jicho kali Sara na kumfanya Sara ainuke tu pale alipokuwa amekaa kanakwamba alimwambia kuwa aondoke, kisha Salome akabadilisha mada na kuanza kuongea na Doto habari za hospitali na jinsi anavyojisikia, kwavile habari ilibadilika kidogo, Sara alijikuta akirudi tena sebleni huku akiwa ameongozana na Kulwa ambaye alifurahi kusikia kuwa Doto ametoka hospitali.

Patrick alirudi moja kwa moja kwa Neema na kujikuta akimueleza Neema kile ambacho kaelezwa na vijana aliokutana nao, kwakweli Neema alishangaa sana na kuuliza kwa makini
“Kwahiyo Ashura amekufa?”
“Ndio, nimeona hivi picha akiwa ameanza kuoza kwakweli sijui kama ile picha itatoka akilini mwangu ila siamini kama Salome anaweza kutenda kitu cha namna hiyo”
“Nimeumia sana, ingawa kuna mengi nimeyagundua kijijini lakini Ashura niliishi nae kama ndugu yangu kabisa, alikuwa kama mdogo wangu na aliwapenda wanangu. Ila siamini kama Salome anaweza kutenda kitu cha namna hiyo, hapana kwakweli. Salome ni mwanangu, namjua vyema sana, hawezi kufanya jambo la namna hiyo. Salome hawezi kuua”
“Hata mimi nimekataa kuwa Salome hawezi kuua”
“Naomba hao vijana watupeleke huko nikaone jambo alipotupiwa ndugu yangu Ashura jamani nimeumia sana, sasa mbona nilikuwa nawasiliana nae jamani aaah haiwezekani”
Akajikuta akikumbuka kuwa wanae hawa wadogo wamewahi kumwambia kuwa mama yao mdogo Ashura alianguka na povu kumtoka halafu Salome akawaambia ni mchezo wanacheza, akajikuta anasema,
“Ina maana……”
“Ina maana nini?”
“Aaah tuachane na habari hizo, jamani Ashura ndugu yangu hapana jamani. Hata kama hakuwa ndugu yangu, hakustahili kuzikwa kinyama hivyo”
Alichukua simu yake na kujaribisha ile namba aliyokuwa anawasiliana na Ashura ila hakuipata hewani na kumfanya hadi tumbo limuume na kuzidi kuamini kuwa itakuwa kweli ashura kauwawa ila bado moyo wake ulikataa kuwa kauliwa na Salome kwani hakutegemea kama mwanae anauwezo wa kuua.
 
SEHEMU YA 146



Rose aliondoka kwa mganga na kwenda nyumbani kwake, alifika getini na kumwaga ile dawa kisha kuingia ndani, kwanza alishangaa kumuona mlinzi getini kwake wakati alimshuhudia akiwa anaondoka ila hakuweza kuongea nae kwa kuhofia kuharibu masharti ya dawa, alisalimiwa lakini hakuitikia kiasi kwamba Yule mlinzi alifikiria kuwa Rose hajapenda kumuona tena.
Rose aliongoza hadi ndani kwake na kuingia sebleni, alishangaa kumuona rafiki yake akiwa amekaa sebleni, halafu pembeni yake yupo Doto, Sara, Kulwa na Salome ila kabla hajaita hata jina moja alishangaa kuona rafiki yake akianguka chini na kuanza kujipigiza kama mtu mwenye kifafa huku mapovu yakimtoka.


Rose aliongoza hadi ndani kwake na kuingia sebleni, alishangaa kumuona rafiki yake akiwa amekaa sebleni, halafu pembeni yake yupo Doto, Sara, Kulwa na Salome ila kabla hajaita hata jina moja alishangaa kuona rafiki yake akianguka chini na kuanza kujipigiza kama mtu mwenye kifafa huku mapovu yakimtoka.
Alijikuta anainama kumpa rafiki yake huduma ya kwanza huku akimuita,
“Mama Jack, jamani mama Jack”
Kile kitendo cha kumuita tu kilimfanya awe kimya gafla hata kule kujipigiza aache, kwakweli Rose alichanganyikiwa yani kama kuchanganyikiwa sasa hapa alichanganyikiwa tena sio kwa kujifanyisha ila ni kuchanganyikiwa kweli.
Alijikuta akikazana kumita ila kadri alivyomuita ndivyo alivyozidi kukauka, yani watoto wake wote walikuwa wakishangaa lile tukio huku wakitaka kwenda kumsaidia mama yao ila Salome aliwazuia,
“Muacheni”
Sara alimuangalia kwa gadhabu Salome na kumwambia,
“Hivi una nini wewe? Yani mama yetu yupo kwenye matatizo unasema muacheni, unataka tukusikilize au?”
Sara akataka kwenda, ila Salome aliwazuia na kuanza kuwaambia,
“Hivi nyie hata hamjui mtu ameanza kutapatapa sababu ya nini halafu manataka mkamsaidie, mkipata kesi ya kujibu je?”
Walitamani kwenda kumsaidia mama yao ila kuna uzito uliingia ndani kwao na kujikuta wakiishia kuongea tu bila ya kwenda kumsaidia.
Rose alilia sana huku akimuita rafiki yake, yani kwa muda huu hata hakukumbuka kama kakosea masharti au vipi maana alishachanganyikiwa kuwa rafiki yake kaanguka ndani ya nyumba yake, ila kwavile yeye alikuwa na mwili na rafiki yake alikuwa mwembamba, alijikuta akimbeba bila hata msaada wa watoto wake, alimbeba na kumtoa nje kisha akampakiza kwenye gari na yeye kupanda kwenye gari na kuondoka.
Njiani alikuwa akiendesha kwa kasi sana kwani alikuwa anamuwaisha rafiki yake kwa mganga kwani alijua akichelewa tu ataharibu kila kitu na rafiki yake anaweza akapoteza maisha kweli.
Ila leo ilimchukua muda mrefu sana kufika kwa mganga kiasi kwamba aliendesha gari hadi alichoka huku ana machungu kuhusu rafiki yake ila mara kidogo alipofika mbele ya safari yake alijikuta akishindwa kuendesha gari tena halafu akapitiwa na usingizi mzito sana.



 
SEHEMU YA 147


Pale ndani walibaki watoto wa Rose wakiwa na Yule Salome huku wakimlaumu Salome kwanini kawakataza kumsaidia mama yao,
“Hivi nyie hamuwezi kujiongeza au? Mama yenu anajua kilichompata rafiki yake ndiomana kambeba hapa bila msaada wa mtu yeyote sababu anajua ni kipi kimempata nan i wapi atampeleka”
“Kwani wewe Salome kuna chochote unatambua?”
“Mngekuwa misukule leo ndio mngeniuliza kuna kuna chochote natambua, mama yenu alitaka kuwatoa kafara”
Wote wakashangaa, kuwa mama yao awatoe kafara kwa misingi ipi na kumbishia Salome kuwa mama yao hawezi kuwatoa kafara,
“Aaah ningemuacha awatoe eeh!”
“Mama anatupenda sana, hawezi kufikia hatua hiyo. Kwanza atutoe kafara kwa lipi!”
“Sasa nitamuacha awatoe kafara halafu hayo maneno yenu mkayazungumzie kuzimu huko”
“Sidhani kama umetuelewa Salome, tunauliza mama atutoe kafara kwasababu ipi!”
“Tulieni tu tena mnishukuru mie, la sivyo mngekuwa marehemu nyie. Mnafikiri Yule mama anaenda kupona? Yule ndio basi tena, mama yenu akirudi hapa muulizeni kuhusu Yule mama atawaambia”
Walikaa kimya, baada ya muda mfupi Ana nae alirudi ila leo ndio hakuongea na mtu yeyote kwani alipitiliza chumbani kwake hata ndugu zake wakamshangaa kwani walijipaga moyo kuwa Ana amebadilika ila kitendo cha kupitiliza bila kuwasalimia kiliwafanya waanze kuhisi kuwa amesharudi kwenye matendo yake.
Ana hakuwaongelesha sababu alikuwa akienda kwenye dawa zake, na aliweza kutazama na kuona mama yake alipewa masharti ya aina gani na alitaka kufanya nini na kitu gani kimetokea, Ana kwa kutumia dawa yake mara nyingine alikuwa na uwezo wa kuona matendo yaliyotokea ila tu hakuweza kuona matendo yatakayotokea, kwahiyo aliweza kuona masharti ambayo mama yake alipewa na alichokifanya hadi ameondoka.
Ana akahisi kuwa mama yake amerudi tena kwa Yule yule mganga, aliweza kuangalia njia vizuri kwa dawa zake na kuiona, kisha akabalisha nguo za shule na kuondoka tena bila ya kuongea chochote maana alitaka akakutane na mama yake na amzuie kutokwenda tena kwa Yule mganga kwamaana kunapoendelea aliona mama yao anaweza kumtoa kafara hata yeye ukizingatia anaogopa kufa.
Kwahiyo aliwaacha wote wakiwa wanamshangaa anatoka hadi anaishia zake, walimuangalia tu na hawakuelewa kuwa alikuwa anaenda wapi.


 
SEHEMU YA 148



Usiku ulimkuta Ana akiwa njiani na kuamua kwenda kulala hotelini, ingawa alikuwa anajiamini sana ila hakutaka kutembea usiku ule peke yake. Alijiaminisha kuwa asubuhi ya siku hiyo angeondoka zake, pale hotelini alienda kula kwanza na kusikia watu wakipiga stori huku wakisema kuhusu wachawi,
“Yani wachawi bhana hakuna kinachowashinda, natamani kuwa mchawi”
“Mimi ningekuwa mchawi ningekuwa naingia benki kuchukua hela si mchawi bhana hawanioni”
“Mimi ningekuwa mchawi wangenikoma mtaani kwangu, yani ukiwa mchawi hakuna kitu kinachokushinda”
Ana alitabasamu na kuinuka kisha kuingia kwenye chumba alichokodi huku akijaribu kuzitafakari akili za wale watu kuwa wana akili mbovu na wanaona kuwa mchawi hakuna kinachoweza kukushinda wakati wao Salome tu anawatoa jasho. Ila kadri alivyokaa mule ndani alijisikia kwenda kuwafundisha adabu wale wote waliokuwa wanazungumzia mada za kichawi, na usiku wake alienda kuwatembelea kwa uchawi na kwa bahati mbaya alimuua mmoja wao na kurudi kwenye chumba chake huku akijiambia kuwa hakutaka kuua ila Yule mmoja kiherehere chake kimemponza ila yeye binafsi hakutaka kuua, toka muda huo hakuweza kulala hata alivyorudi kwani muda mwingine roho ya kibinadamu inamjia na anaona huruma ila muda mwingine anaona ni sawa kwa Yule mtu kufa. Kulipokucha alisikia kelele za vilio sehemu ile na kuamua kuondoka zake kwani hakutaka kusikiliza kelele za vilio vya msiba aliosababisha mwenyewe.
Kwahiyo aliendelea na safari yake ya kwenda alipoenda mama yake.

Salome alirudi nyumbani kwao siku ya leo na kumkuta mama yake na baba yake wanataka wajiandae kwenda kuwatafuta wale vijana ili wawaonyeshe ile maiti ya Ashura na waifanyie utaratibu wa maziko, aliwauliza kuwa wanajiandaa kwenda wapi,
“Mwanangu, kumbe mamako mdogo Ashura amekufa”
“Kwani nyie mmejuaje?”
Wakamshangaa vile ambavyo hajaonyesha kushtushwa hata kidogo, kisha Patrick aliamua kumueleza vile ambavyo alikutana na wale vijana na jinsi walivyomueleza na kushutumu kuwa atakuwa ni Salome ndio kahusika na kumuua Ashura, ila cha kushangaza Salome akacheka na kuwafanya waangaliane kwa zamu maana hawakumuelewa anachochekea kisha akamuuliza Patrick,
“Ni ushahidi gani wamekuonyesha kuwa Ashura amekufa?”
“Wamenionyesha picha ya maiti yake ikiwa imeharibika sana”
“Matapeli hao”
“Matapeli! Kivipi?”
“Msiwafatilie hao ni matapeli, watawatapeli na kuwafanya muumie tu. Hakuna cha mwili wa Ashura wala nini, amekufa wakati tunawasiliana nae kila siku! Achana na hao”
Kisha Salome akaenda chumbani kwake na kufanya Patrick na Neema wazidi kupatwa na maswali, ila bado hawakutaka kubadili wazo lao la kuwatafuta hao vijana ili kama ni kweli basi wamzike Ashura sehemu stahiki, kwahiyo wakaondoka hivyo hivyo.
Walifanya ile safari yao, ila wakiwa njiani wakashangaa gari yao ikisimamishwa kisha kijana mmoja wapo kati ya wale vijana ambao Patrick aliwaona jana aliwasimamisha halafu akawasalimia na kuwaambia kuwa ataenda kuwaonyesha ulipo mwili wa Ashura kwahiyo walipanda nae kwenye gari na kuanza safari ila walivyofika mbele ya safari, walishangaa wakishikwa na usingizi na kulala kwenye gari tena fofofo kamavile wapo kitandani.

 
SEHEMU YA 149


Nyumbani nako ambapo walikuwepo Kulwa, Doto na Sara walikuwa wakizungumzia kuhusu tukio la jana yake, kuhusu Yule mtu ambaye alienda na Salome nyumbani kisha kurudi mama yao na Yule mtu kuanguka akitapatapa kisha mama yao kumbeba na kuondoka nae, walikuwa wakijiuliza sana kuhusu lile tukio na jinsi mdogo wao alivyorudi kutoka shuleni na kuondoka ambapo mpaka siku hiyo hakuwa amerudi nyumbani,
“Ila jamani mara nyingine kwenye hii nyumba tunafanya vitu kama tumerogwa vile, hivi kweli sisi tunalala kabisa wakati mdogo wetu hatujui alipo! Bora mama ni mtu mzima ila Ana bado mdogo sana”
“Weee Kulwa nawe umeanza kuugua kichaaa nini, si ulimuona mwenyewe akitoka hapa jana mbona hukumuuliza mdogo wangu unatoka unaenda wapi?”
“Yani wewe Sara badala umuhurumie mtoto wa kike mwenzio eti na wewe unamkandamiza na kuona ni sawa kabisa Yule mtoto kutokurudi nyumbani”
“Mimi dada ila nyie ni kaka zake, mmeshindwa kuwa na sauti kweli kwa mdogo wenu wa kike? Kumbukeni nishawahi fanywa kipofu, nishawahi fanywa bubu na huyo mnaemuita ni mtoto, Ana ni mtoto kwa nje ila ndani ni mkubwa”
“Mmmh jamani Sara, sasa unashauri nini?”
“Mimi mwenyewe roho inaniuma sana kuhusu mama na Ana, mama yetu amekuwa mtu wa kutojielewa kabisa siku hizi kwakweli roho inaniuma sana ila nashindwa cha kusema. Kuna kitu nikiwaonyesha kaka zangu na nyie pia mtashangaa sana”
“Kitu gani hicho?”
“Ndani ya nyumba hii, kuna chumba cha siri cha mama ambacho hatukijui ila cha kushangaza Salome alikijua”
Wote walishangaa kusikia habari za chumba cha siri na wakatamani kwenda kukishuhudia hiko chumba cha siri walichoambiwa.

Patrick na Neema walikuwa kwenye usingizi mzito sana, ila aliyekuwa wa kwanza kushtuka alikuwa ni Neema ambaye alimuamsha Patrick walishangaa wakiwa nyumbani tena wakiwa wamechoka sana hata vichwa vilikuwa vinawauma na kuwafanya kutokukumbuka kwa muda huo huo kuwa walikuwa wapi mara ya mwisho, muda kidogo Patrick akakumbuka tena akiwa na macho ya usingizi bado na kumwambia Neema,
“Si tulikuwa kwenye gari sisi?”
Neema nae akakumbuka vilivyo ila nay eye macho yalikuwa mazito hatari, yani yalizingirwa na usingizi,
“Ndio tulikuwa kwenye gari tunaenda kufata mwili wa Ashura. Yuko wapi Yule kijana wa kutupeleka? Halafu mbona tuko nyumbani?”
“Hata mimi sielewi kabisa, tumerudije hapa? Gari yangu imepona kweli”
Patrick akataka kuinuka ili akaangalie kama gari yake ipo lakini usingizi ukamzidia na kumfanya ashindwe hata kuinuka zaidi ya kulala vizuri, Neema nae alipomuangalia Patrick amelala akajikuta nay eye akilala usingizi wa nguvu tena usingizi wa safari hii haukuwa sawa na ule usingizi wa kwanza kwani huu ulikuwa mzito zaidi.
Kwahiyo wenyewe walilala chumbani kisha Salome akawaandalia wadogo zake chakula ambapo walikula bila kuhoji zaidi kuhusu wazazi wao, halafu akawapeleka nao kulala huku yeye akiondoka kabisa hapo nyumbani kwao.

 
SEHEMU YA 150


Ana ilikuwa inamchukua mud asana kufika kwa Yule mganga sababu alitumia usafiri wa jumuiya tofauti na mama yake alitumia gari lake, Ana alikuwa anapanda kwenye gari hii na kushuka mbele sababu safari yenyewe kwa kutumia madaladala ilikuwa ni ya kuunganisha unganisha, ila Ana alikuwa akisumbuliwa sana kichwa na Yule mtu aliyemmaliza kichawi usiku uliopita, ilikuwa ni kwenye hasira tu akajikuta akimmalizia ila hakupanga kummalizia. Ila damu ya huyu mtu ilimuumiza sana kichwa Ana, ikabidi atafute mto kwanza kwahiyo alivyofika kwenye maeneo ya karibu na kwa mganga alitafuta mto kwanza na kwenda kuoga mtoni kwani yeye aliamini kuwa unapooga kuna vitu vinaondoka kwenye mawazo yako haswa kumfikiria huyo mtu ambaye alimuua bila ya hatia.
Alichukua muda mrefu sana kuoga huko mtoni kisha alipomaliza akavaa nguo zake vizuri tu, ila kuangalia pembeni akaona kitu kinang’aa sana na kuhisi kuwa huenda ikawa dhahabu na kwavile kule kulikuwa sehemu ya ndani ndani kwahiyo uwezekano wa kitu hicho kuwa dhahabu ulikuwa mkubwa sana, ingawa Ana ni mtu mwenye machale sana ila kitendo cha kuona dhahabu kilimaliza machale yake, akainama na kuiokota kisha kuiweka vizuri kwenye mifuko yake kuwa ataenda nayo kila mahali na atarudi nayo mjini kwaajili ya kuiuza, baada ya kuiweka vizuri ndipo akaendelea na safari yake ya kufika kwa mganga.

Sara aliwachukua wenzie mpaka ile sehemu aliyochukua funguo na Salome kisha kufungua hiko chumba na kuingia ndani, wote wakashangaa,
“Inamaana siku zote hizi tulikuwa hatujui kama hiki chumba kinaingilika au ni nini jamani mbona sielewi yani hatujawahi kukihisi hata mara moja!”
“Sasa nasikia kuna watu mama kawafungia kwenye hiki chumba, unaambiwa ukisukuma lile kabati utaona mlango mwingine na hapo kuna chumba kingine”
Ikabidi Kulwa asukume kabati kwani hawakutaka kuandikia mate wakati wino upo, na kweli alivyosukuma kabati aliona mlango wa chumba kingine kinachoonekana kama choo cha ndani, Kulwa alitaka kuwa shahidi bado na kukisogelea kile chumba kisha akashika ule mlango ila aliganda pale pale, akawa anajaribu kuutoa mkono wake ila haikuwezekana na mara chumba kile kikaanza kutingishika na kuwafanya wengine yaani Sara na Doto waanguke chini huku Kulwa akiwa kaganda pale pale mlangoni na mara akaanza kukauka kama anapigwa na shoti ya umeme.

ITAENDELEA
 
Hivi mkuu kama hutojali, hizi simulizi mnazotuburudisha nazo humu JF nyie mnapata return vipi?
Zipo faida nyingi mkuu, nitakujia mbili.
1. Mwandishi/mtunzi anakuwa anatangaza kazi zake au kipaji, kwani waandishi ni wengi, na akitoa vitabu basi vitanunuliwa sana kwasababu watu wanajua umahiri wa kazi zake.
2. Unatengeneza marafiki katika jamiiforums, unawakutanisha wapenzi wa simulizi kwa pamoja. unaiishi katika kijiji cha Jamiiforums
 
SEHEMU YA 151



Ikabidi Kulwa asukume kabati kwani hawakutaka kuandikia mate wakati wino upo, na kweli alivyosukuma kabati aliona mlango wa chumba kingine kinachoonekana kama choo cha ndani, Kulwa alitaka kuwa shahidi bado na kukisogelea kile chumba kisha akashika ule mlango ila aliganda pale pale, akawa anajaribu kuutoa mkono wake ila haikuwezekana na mara chumba kile kikaanza kutingishika na kuwafanya wengine yaani Sara na Doto waanguke chini huku Kulwa akiwa kaganda pale pale mlangoni na mara akaanza kukauka kama anapigwa na shoti ya umeme.
Sara na Doto walitamani wakamsaidie ndugu yao lakini hawakuweza kwani chumba kilikuwa kinatingishika na wao wapo chini, ile hali ilizidi kuwa mbaya kwa upande wao na gafla ikakatika mara tu ya mlango wa kuingilia chumba kile ulipofunguliwa na aliyeingia alikuwa ni Salome, walibaki wakimtazama tu kasoro Kulwa kwani hata kilichoendelea hakujua na alikuwa amekauka kama kapigwa na shoti ya umeme, alionekana Salome akipuliza upepo kutoka mdomoni kwenda kwenye mkono ambao Kulwa alishika kitasa cha ule mlango mwingine, na gafla alijikuta kakiachia na kuanguka chini ila akiwa vile vile hajitambui, Salome akamwamuru Sara amkongoje Kulwa kutoka kwenye kile chumba kwani Doto alikuwa bado na maumivu ya kuungua.
Kwahiyo Sara aliinuka na kuanza kumburuza Kulwa nje huku hofu ikiwa mmemtanda moyoni kuwa huenda Kulwa amekufa maana alikuwa kimya kabisa kama kabigwa shoti ya umeme na alikuwa amekauka kabisa, ila Salome alimwamuru Sara amvutie hadi nje kabisa ambapo Sara alimburuza Kulwa hadi nje kabisa, kwa hakika alichoka maana Kulwa alikuwa mzito sana, alimuhurumia kumburuza ila ilibidi afanye vile kwani hakuwa na jinsi zaidi ya kumburuza tu, ukizingatia alishapewa amri na Salome kuwa afanye hivyo kisha akarudi sebleni ambako Salome alikuwa amekaa na Doto, hapo Sara akauliza,
“Hivi Kulwa atapona kweli?”
“Angekuwa haponi wala nisingekusumbua kuwa umbebe. Na ulianzaje na wewe kuwapeleka wenzio kwenye kile chumba?”
“Hata sijui kwakweli, ila nilitaka kuwaonyesha kuwa kuna chumba ambacho hatukifahamu humu ndani”
“Haya sasa, faida yake umeiona? Kaka yako atapona ila itamchukua muda sana kurudi kwenye hali ya kawaida, familia mnazidi kuugua magonjwa yasiyoeleweka”
“Sikuelewi”
“Si huwa mnabisha nyie siku zote kuwa mama yenu ni mchawi! Haya sasa kama mama yenu si mchawi, kile chumba kwanini kipo kisiri? Na kwanini mtake kuumia sababu ya kukichunguza kile chumba?”
“Unajua ni vigumu sana mtu kuamini kuwa mama yako mzazi ni mchawi”
“Basi ndio hivyo, wakati nafanya kazi hapa kwenu. Siku niliyoamua kukichunguza kile chumba nilizimia muda mrefu sana”
“Wakati unafanya kazi hapa kwetu!!!”
Sara na Doto walijikuta wakishangaa kwani waliona Salome anaongea maajabu ukizingatia kwenye nyumba hiyo wamemjua badae sana ila yeye anawaambia wakati anafanya kazi pale kwao, ila Salome hawakuwajibu chochote ila aliwaambia wasitoke nje mpaka Kulwa atakapozinduka.
 
SEHEMU YA 152


Rose alikuja kushtuka na kugundua kuwa alilala pale usiku mzima na kazinduka kesho yake huku mwili wa mama jack ukiwa kwenye siti ya nyuma ya gari lake kama alivyouweka, alishangaa sana kisha kuanza tena kuendesha gari kwa haraka haraka hadi akafika nyumbani kwa mganga ila alimkuta akiwa amechukia sana, kwani aliposhuka tu kwenye gari lake na kukutana uso kwa uso na Yule mganga alishangaa akifokewa na Yule mganga,
“Ndio umefanya nini sasa Rose?”
“Sielewi”
“Huelewi nini na umemtoa kafara rafiki yako? Nenda kamzike sasa”
Rose alihisi kuishiwa nguvu kabisa kwani hakutegemea kama rafiki yake atakuwa amekufa,
“Nisamehe mganga”
“Na bora ungewahi jana ile ile, sasa mwili umeshapoa kabisa ndio unamleta kwangu? Nenda kazike tu”
“Nisamehe tafadhari sijui cha kufanya”
“Hujui nini? Nenda kazike”
“Sijapanga kumtoa kafara rafiki yangu hata sijui imekuwaje”
“Hivi wewe mwanamke una akili gani? Mwanzo si nilikutuma na dawa mtoni wewe nikakwambia ukimwaga utamuona mwanao kitandani halafu msukume mtoni, ila wewe ukamuona sijui Moza wako ukakimbia na hukuweza kumsukuma, sasa nimekupa dawa umwage mlangoni kwako, usiongee na mtu yeyote zaidi ukifika ndani uanze kutaja majina ya unaowatoa kafara. Ni kweli hujaongea chochote ila umeanza kumtaja rafiki yako huyu, ulikuwa na mpango gani nay eye zaidi ya kumtoa kafara tu. Na hiyo kafara haikusaidii chochote ni kama umetoa sadaka tu, haya nenda kazike mzoga wako”
Rose alijikuta akikosa nguvu kabisa kwani haya mambo yalivyoenda ndivyo sivyo yalizidi kumchanganya akili na akaona kunapoelekea sasa hata yeye binafsi atajikuta amejiua kwa presha au kwa namna nyingine yoyote maana hakuelewa chochote, hakujua aanzie wapi kuzika au aishie wapi.
“Sasa mimi nitamzikaje?”
“Kwani hujui watu wanazikaje? Wewe mwanamke ni mjinga sana, rafiki yako kakusaidia kakuleta kwangu halafu umemtoa sadaka, yani wewe mwanamke ni mpumbavu”
“Nakuomba mganga tumsaidie rafiki yangu kwa namna yoyote ile”
“Tumsaidie nini na mwili umepoa huo? Labda utoe kafara ya watoto wako wote”
Rose alichanganyikiwa kabisa, ila Yule mganga aliondoka na kwenda kwenye chumba chake cha uganga na kumuacha Rose akiwa na mawazo yasiyo na kifani.
Aliwaza kuhusu watoto wake na kuona kuwa vyote alivyovifanya kwa kipindi chote ni kazi bure,
“Hivi mimi si ndio nilimtesa yule mwanaume yani Patrick na kumfanya kama ndondocha sababu ya watoto wangu! Nilitaka waishi vizuri, wale raha ya maisha, yani leo nikawatoe wote kafara kweli! Hao wawili wenyewe nilikubali kwa shingo upande, naweza kuwatoa kafara watoto wangu kweli! Kuna sababu gani ya mimi kuendelea kuishi na kutafuta mali kwa haj azote ikiwa watoto angu nimewatoa kafara, kuna faida gani ya kuishi vizuri huku nikinyooshewa vidole na watu kuwa niliwatoa kafara watoto wangu! Nawapenda sana, niishi bila Sara, Kulwa, Doto na Ana kweli! Hapana kwakweli, na huu mwili wa rafiki yangu sijui nitafanya nao nini”
Aliwaza sana bila ya jibu la mawazo yake na alijihisi ni mkosanji kila alipofikiria kwani aliona anapoelekea sasa sio kuzuri, yani awatoe watoto wake wote.
Yule mganga akamtuma mtu ambaye alienda kumuita Rose na kuingia kwenye chumba cha mganga, na baada ya kuingia tu aliulizwa alichokiamua,
“Utaenda kumzika rafiki yako au utawatoa watoto wako kafara?”
“Nitaenda kumzika rafiki yangu”
“Yani wewe naelewa sasa kwanini wachawi wenzio hawashirikiani na wewe, yani wewe uchawi wako mkubwa ni kutegemea nguvu za waganga wa kienyeji, hakuna mchawi ambaye hatoi kafara, wewe ni mchawi gani wewe? Nakuuliza mara ya mwisho, utaenda kumzika rafiki yako au utawatoa watoto wkao kafara?”
“Nitaenda kumzika rafiki yangu”
Mganga ilibidi acheke huku akisikitika, alimuangalia kwa makini sana Rose halafu akamwambia tena,
“Nakupa machaguzi ya mwisho, nenda kafikirie kati ya kumzika rafiki yako na kuwatoa kafara watoto wako”
Rose alitoka tena na kukaa chini ya mti huku kichwa chake kikiwa kimejawa na msongo wa mawazo.
 
SEHEMU YA 153


Kulwa alishtuka kama mtu aliyeshtuka usingizini halafu moja kwa moja akakimbilia ndani huku akihema sana, ni Sara aliyeenda kumdaka maana haikujulikana kuwa alitaka kukimbilia chumba gani ukizingatia Salome alishawaambia kuwa akili yake itakuwa kidogo inasumbua kufanya kazi kwa kipindi hiko kutokana na kuanguka kwenye kile chumba.
Kwahiyo Sara alimshikilia kaka yake huku akimsihi kuwa akae kwanza akili itulie, ila Kulwa alipokaa tu alianza kuropoka kuwa kuna vitu aliviona wakati amelala,
“Vitu gani hivyo?”
“Kwanza mama yuko wapi?”
“Hayupo, unajua fika mama tangu jana aliporudi na rafiki yake kuanguka akaondoka nae ndio hajarudi hadi leo”
“Basi nilichokiona ni cha kweli”
“Kitu gani hicho?”
“Nimeona mama yupo kwa mganga, yani Yule rafiki wa mama wa jana eti amekufa”
Wenzie wakashangaa na kuuliza,
“Amekufa!!”
“Ndio nilivyoona, na mama kapewa achague chaguo moja na Yule mganga, yani aende akamzike rafiki yake au atutoe sisi wanae kafara. Kwenye kumuona kwangu yani bado mama anafikiria kuhusu hilo swala kuwa atutoe kafara au akamzike rafiki yake”
“Yani mama yetu atutoe kafara sisi!”
Doto aliuliza kwa mshangao, na Kulwa akamjibu
“Ndio, kapewa chaguo hizo kuwa atutoe kafara au akamzike rafiki yake”
“Haiwezekani, haiwezekani mama kututoa kafara sisi. Hayo ni mawazo yako tu yasiyokuwa na maana yoyote Kulwa”
Salome aliyekuwa akiwasikiliza tu akacheka sana kisha kumuangalia Doto na kumwambia,
“Tena wewe ndio usiseme kabisa, nadhani leo ndio ingekuwa mazishi yako. Mama yako alishakubali muda mrefu sana kukutoa kafara wewe, na badae akakubali kukutoa wewe na Sara, ila kwa ninavyomjua angekutoa wewe kwanza”
Wote walikaa kimya kwanza baada ya kusikia kuwa walikuwa kwenye orodha ya kutolewa kafara, na lile swala aliloongea Kulwa kuwa mama yao yupo kwenye machaguzi ya kuwatoa kafara wao au kumzika rafiki yake. Doto alijikuta akiuliza,
“Jamani sasa tutafanyaje ikiwa mama atapanga kututoa kafara wote?”
Kulwa akawaambia wenzie kwa msisitizo,
“Jamani sikilizeni, kama mama alipanga kuwatoa kafara nyie mwanzoni ila Salome alipokuja na Yule mgeni wote tulimshangaa ila kumbe ndio ametolewa sadaka kwaajili yenu. Hapa hatuna budi zaidi ya kumwambia Salome atusaidie”
Kisha akamgeukia Salome na kumwambia,
“Salome tusaidie maana kwajinsi nilivyomuona mama anasuasua kwenye ndoto kwa hakika atachagua kututoa kafara tu, naomba utusaidie”
Sara nae akachangia,
“Kweli Salome tusaidie”
Sasa nyie mnaniombaje hivyo binadamu mwenzenu badala mmuombe Mungu awasaidie, ombeni Mungu awasaidie na muelewe kuwa mama yenu sio mtu mzuri, kila siku nawaambia kuwa mama yenu sio mtu mzuri ila hamtaki kuelewa ila muelewe sasa, na mkitaka niwasaidie tushirikiane kwa pamoja ili mama yenu aachane na uchawi na arudi kwenye maisha wanayoishi binadamu wa kawaida”
“Kwahiyo ni kweli mama kahifadhi watu kwenye kile chumba kidogo?”
“Yani siku wakitoka mtashangaa sana, kwanza ni wamekonda mno halafu watu wengine hata hamuwezi kuwadhania kama wapo humo”
“Mmmh hivi wewe Salome ni mtu wa kawaida kweli?”
Salome akacheka na kuwaambia,
“Mimi ni mtu wa kawaida ila ipo siku mtanijua mimi halisia kuwa ni nani na kwanini nilikuwa nafanya yote haya”
Walijikuta wote wakitamani kumjua Salome halisia ni nani ila Salome aliwabadilishia mada na kuwataka kuwa wakapate chakula ila alimtaka Sara akamuite mlinzi ili siku hiyo ale chakula pamoja na mlinzi.
Sara alifanya hivyo kwenda kumita mlinzi ila mlinzi aligoma na kusema kuwa hawezi kwenda kula ndani kwenye nyumba hiyo.
“Kwanini?”
“Sitakli tu, na siwezi kuja”
Sara alirudi na kumpa huo ujumbe Salome ambaye alisema, sawa hakuna tatizo ila muda mfupi tu mlinzi alikuwa mezani akishangaa shangaa kuwa ameingiaje ndani ya nyumba wakati alikataa.
 
SEHEMU YA 154


Patrick na Neema muda huu waliamka tena na kujiona kuwa sasa wapo sawa kiasi yani ule uchovu umepungua pungua ila muda nao ulikuwa umeenda sana yani giza lilishaanza kutanda, waliamka na uchovu na kutoka sebleni ambapo Neema alianza kwa kumuita Salome ila ilikuwa kimya na kuhisi kuwa Salome hakuwepo,
“Unajua huyu mtoto kipindi cha nyuma alisema kuwa anakuja kukaa nyumbani kwako ili akae karibu na baba yake, sasa kipindi hiki uko hapa ila mbona haonekani nyumbani?”
“Labda kaenda kujisomea na wenzie”
“Aende kujisomea wapi? Yule mtoto amekataa kwenda shule kama hujui, na ndio kwanza yupo kidato cha tatu ila kwenda shule amegoma sijui ataingiaje hiyo kidato cha nne mwakani maana miezi inazidi kukatika tu”
“Kumbe hasomi? Kwanini umeacha mtoto hasomi?”
“Sassa kakataa shule mwenyewe unadhani mimi ningefanyaje? Hivi unakumbuka kwanza mara ya mwisho kabla hatujarudi nyumbani tulikuwa wapi?”
“Hata safari ya kurudi nyumbani sijui imefanyajwe fanyajwe. Ila Neema mchunguze mtoto, haiwezekani mtoto akatae tu gafla kwenda shuleni halafu wewe ukae unamchekelea tu, labda kaanza wanaume usikute wanamuongopea”
“Mmmh kama nakumbuka kitu hivi, Salome aliniambiaga ana simu umemnunulia wewe”
“Mmmh sijawahi kumnunulia Salome simu”
Neema machale yakamcheza na kuanza kuhisi vile alivyoambiwa na Patrick kuwa usikute mwanae ana mwanaume ndiomana hataki shule, akaamua kwenda kupekua chumbani kwa Salome kuwa pengine anaweza kukuta hata barua ya mapenzi na ajuwe ni wapi aanzie na mtoto wake huyu.
Wakati ameenda kupekua chumbani kwa salome, aliona begi dogo na kulifungua, alikuta simu ila alishtuka sana kwani ilikuwa ni simu ya Ashura.
 
Back
Top Bottom