Simulizi: Kurudi Kwa Moza

Simulizi: Kurudi Kwa Moza

SEHEMU YA 155


Rose aliitwa tena na mganga ili atoe chaguo lake alilolifikiria,
“Muda unakwenda Rose, na usiku huo unaingia, chagua moja kumzika rafiki yako au kutoa kafara wanao”
“Hapana kwakweli, kuwatoa kafara wanangu hapana, nipo tayari kumzika rafiki yangu”
“Kumbuka utaenda kumzika peke yako na giza hili, hakuna wa kukusaidia. Chagua tena”
Rose hakuwa na jibu la zaidi ya kumzika rafiki yake,
“Kama umeamua hivyo sawa, inabidi azikwe leoleo yani maiti yake isilale tena maana yatatokea majanga bure”
“Majanga gani?”
“Usiniulize majanga gani, jua kuwa yatatokea majanga. Yani unatakiwa uizike maiti leoleo, ila kwa usalama wako ukiwa unatoka hapo mlangoni kwenda kuizika hiyo maiti usiongee na mtu yeyote Yule ila nenda moja kwa moja kuna mahali utakuta shimo halafu utamdumbukiza rafiki yako huku ukitaja majina yote ya watoto wako baada ya hapo utarudi na kulala hapa. Nadhani tumeelewana”
“Ndio tumeelewana”
“Haya lamba dawa hii na usiseme chochote”
Rose akalamba ile dawa na kutoka nje, ila kabla hajalisogelea gari lake akashangaa kumuona mwanae Ana akiwa amemfata kule kwa mganga, alishangaa sana na kujikuta akisema,
“Ana!”
“Ndio ni mimi mama, nimekufata nata……”
Ila kabla Ana hajamaliza sentensi yake, Rose alianguka chini na kuanza kutapatapa.

Rose akalamba ile dawa na kutoka nje, ila kabla hajalisogelea gari lake akashangaa kumuona mwanae Ana akiwa amemfata kule kwa mganga, alishangaa sana na kujikuta akisema,
“Ana!”
“Ndio ni mimi mama, nimekufata nata……”
Ila kabla Ana hajamaliza sentensi yake, Rose alianguka chini na kuanza kutapatapa.
Ana alipatwa na hofu sana baada ya kumuona mama yake katika hali ile ila gafla alijikuta akipata wazo la kutoa lile jiwe la dhahabu ila hakujua kuwa afanye nalo kitu gani.
Akalitoa lile jiwe la dhahabu na kujikuta akilishika na kuliweka kwenye kifua cha mama yake na gafla wakatoweka mahali pale.
Mganga alikuwa pembeni akiwaangalia na akiangalia kinachoendelea kwahiyo alishangazwa sana na kuona kuwa gafla watu wale hawaonekani ila gari ya Rose ilibaki pale pale na mwili wa mama Jack ulibaki mule mule kwenye gari, mganga alishangaa sana na kumwambia msaidizi wake,
“Mwanamke mshenzi sana Yule, ananiletea uchawi wake kwenye nyumba yangu pia! Kaacha maiti yake hapa, akimaanisha nini? Na nitamkomesha kwakweli yani nitamkomesha haswaa”
Msaidizi wa mganga alikaa kimya kwani hata yeye hakuelewa kitu chochote kile kinachoendelea, na pia hakuelewa kuwa yeye na mganga watafanya nini na maiti ambayo imeachwa ndani ya gari.
 
SEHEMU YA 156


Nyumbani kwa mama Jack napo hawakuelewa kabisa kuhusu mama yao, walijaribu kuulizia sehemu mbali mbali ila hakuna mahali walipopata jibu la kueleweka, ila wakakumbuka tu kuwa mara ya mwisho mama yao alimsindikiza Yule binti aliyemuokota na kuamua kumpeleka kwao, watoto wake walijiuliza kuwa bora hata wangeenda na mama yao kumsindikiza ila kwavile waliona ni mtu mzima basi wakamuacha aende mwenyewe ila kitendo cha kutokupata mawasiliano yake na kitendo cha kutokurudi nyumbani kiliwapa hofu kubwa sana, walijiuliza maswali mengi bila majibu na mwisho wa siku walipanga kuwa wakatoe taarifa polisi maana walihisi kuwa huenda mama yao ametekwa na watu wenye lengo la kumuibia gari sababu aliondoka na gari, basi wakakubaliana kufanya hivyo ila walipotoka nje walishangaa kuona gari ya mama yao iko pembeni kama vile alirudi na kuondoka tena bila ya gari,
“Jamani gari imerudije?”
“Lazima alirudi jamani, inawezekana vipi gari lirudi lenyewe?”
Wakalisogelea gari lake na kulichunguza, funguo za gari zilikuwa mlangoni na kila kitu kwenye gari kilikuwepo kasoro tu mama Jack ndio hakuwepo, ila kwavile waliona gari wakajipa matumaini kuwa atarudi tu na kuacha kwenda kutoa ripoti polisi,
“Maana kama karudisha gari basi yupo hapa hapa mtaani atakuja tu, na akiona tumeenda kutoa taarifa polisi atatuona sisi ni wajinga sana. Bora tumeona gari kidogo mioyo imetulia”
“Hivi lakini mama arudishe gari halafu asiingie hata ndani?”
“Labda sehemu aliyokuwa anaenda ni ya muhimu sana, atakuwa kwa majirani tu huko sidhani kama kaenda sehemu ya mbali aache gari”
Wakakubaliana kuwa atakuwa mazingira hay ohayo na kuwafanya hofu iondoke kwenye mioyo yao kuwa mama yao yupo.

 
SEHEMU YA 157


Wakina Rose waliamua kwenda kulala sababu usiku ulishafika, ila Salome aliwaaga kuwa anaondoka muda huo.
“Kheee mbona usiku tayari?”
“Aaah kuna umuhimu wa mimi kuondoka muda huu, natakiwa niwahi nyumbani”
“Kwanini usingelala hapa ukaondoka kesho asubuhi?”
“Hivi mmeshaniona nikilala hapa toka siku mama yenu alipotaka kufanya mambo ya ajabu kwenye chumba change? Mi naenda kulala nyumbani kwetu”
Wakatazamana ila hakuna aliyemjibu la zaidi, kisha Salome akaondoka zake na kuwaacha wakijadiliana, huku Doto akiuliza kuwa ni mambo gani ya ajabu ambayo mama yao alitaka kuyafanya chumbani kwa Salome.
“Jamani mimi kama nilisikia sikia tu kuwa eti mama alitaka kuzini na mlinzi wetu”
Wote wakashangaa na kuuliza kwa makini huku wakimfikiria mama yao na Yule mlinzi wao,
“Hivi kweli mama anaweza kufikia hatua hiyo ya kutaka kuzini na mlinzi wetu? Yule mlinzi si yupo sawa na sisi tu?”
“Hivi kama mama ameweza kutaka kututoa kafara sisi atashindwaje kutaka kuzini na mlinzi? Mama yetu kawa na mambo ya ajabu, tutakataa hilo ila ndio ukweli huo, mama amekuwa na mambo ya ajabu”
“Mimi naona tusiendelee kujadili tena mambo hayo, jamani tunataka kwenda kulala na mkumbuke kuwa mimi nalala peke yangu”
“Hivi unaweza kwenda kulala chumbani kweli leo?”
“Basi nawaomba jambo moja, tulale wote sebleni jamani”
Wakakubaliana na Sara kuwa wote walale sebleni kwa usiku wa siku hiyo.
 
SEHEMU YA 158


Swala la Neema kukuta simu ya Ashura kwenye begi la Neema ni swala lililompa wasiwasi zaidi, akajikuta akitoka nayo kwa Patrick na kumueleza kuwa ile ni simu ya Ashura na ameikuta chumbani kwa Salome.
“Hivi umesema kuwa tangia Ashura aondoke umekuwa ukiwasiliana nae kwa njia ya ujumbe”
“Ndio, hata nikashangaa kusema kuwa eti umeona picha ya maiti yake ikiwa imeoza ila nimeshangaa zaidi kukuta simu ya Ashura kwenye pochi ya Salome na kunitia uwoga zaidi kuwa huenda Salome anajua kuhusu kifo cha Ashura au huenda ndio yeye mwenyewe aliyekuwa akiniandikia ujumbe mimi. Tuseme….”
Akafikiria kidogo kuwa Salome ndio kamuua Ashura, akajikuta akitikisa kichwa chake na kusema,
“Hapana, mwanangu sio mkatili kiasi hicho. Mwanangu hawezi kuwa amemuua Ashura, kwanza kwa lipi baya alilofanyiwa na Ashura hadi amuue? Hapana kwakweli, haiwezekani yani haiwezekani kabisa”
Patrick akamshauri Neema kuwa awashe ile simu ya Ashura ili wajaribu kuangalia kuwa ni namba gani zimewahi kupigwa na ujumbe mingapi iliyowahi kujibiwa kwenye simu hiyo. Basi Neema akajaribu kuwasha simu ile ila haikuwaka na kugundua kuwa haikuwa na chaji kwahiyo ikabidi aiweke kwenye chaji huku wakiwa na hamu ya kujua kuwa ni watu gani wamekuwa wakiwasiliana nae kwenye simu ile.
Muda kidogo alijaribu tena kuiwasha ila iliwaka na ilipowaka tu kuna ujumbe ambao inaonyesha ulikuwa unasubiri kuingia kwahiyo uliingia muda huo huo, ilionekana ni namba mpya ambayo haijatunzwa kwenye simu hiyo ndio imemtumia huo ujumbe, ujumbe ule ulisema,
“Umeona mambo uliyoyafanya sasa Ashura yani umenivurugia kila kitu, huyu Salome amekuwa mtihani mkubwa sana katika maisha yangu. Nilikutuma umamalize ila ukakimbia bila ya kummaliza, sasa huyu mtoto amekuwa na nguvu za ajabu na anataka kunimaliza mimi. Je utafurahi ukisikia ndugu yako nimemalizwa na huyu mtoto wa laana? Sijapendezewa kabisa na ulichofanya”
Neema na Patrick walitazamana kwani kuelewa huo ujumbe moja kwa moja ilikuwa ngumu kabisa ukizingatia mtumaji wa ujumbe ule hawakumfahamu, hivyo wakaamua kufatia mazungumzo kwa namba hiyo na jumbe zilizotumwa, mwishowe waligundua kuwa mtuma ujumbe alikuwa ni Rose na walishangaa sana kwani waliona hadi jinsi Rose alivyopanga mipango ya kummaliza Salome kwa kushirikiana na Ashura yani hadi walijikuta wakishindwa kuangalia jumbe zingine zaidi ya zile kwani ziliwatisha kwakweli,
“Yani kumbe Ashura nilikuwa naishi nae halafu anajuana na Rose! Kumbe alipanga mipango ya kumuua mwanangu! Sielewi kabisa sielewi”
Patrick alikuwa kimya tu kwani yeye ndio hakuelewa zaidi, muda kidogo walisikia mlango wa sebleni ukigongwa kisha Neema kwenda kufungua, alikuwa ni Salome ila Neema alishindwa hata kumfokea Salome kwa kurudi usiku huo nyumbani kwani jumbe za kwenye simu ya Ashura zilikuwa zimemtisha sana, badala yake alijikuta akimkaribisha ndani na kumuuliza kuhusu Ashura kama ana mpango wa kumuua yeye alijuaje na je imekuwaje hadi simu ya Ashura ipo kwake,
“Mama na Baba naomba niwaeleze kwa ufasaha kabisa, kama mmesoma hizo jumbe mtakuwa mmapata maana kuwa Ashura alikuwa ni mtu wa aina gani katika maisha yetu. Mama ulimchukulia Ashura kama mdogo wako ila kiukweli kuna kazi alipewa ndiomana alikuja kukaa hapa, Ashura na Rose hawakumuweza Salome sababu alikuwa na kinga thabiti kutoka kwa marehemu mama yake na Patrick”
Walimshangaa kuwataja majina yao ila kwavile walitaka kujua zaidi ndiomana walikuwa wakimuuliza tu maswali kuhusu Ashura,
“Eeh mwanangu hebu nieleze vizuri, ilikuwaje tena yani ilikuwaje hadi kutaka kukuua wewe na ilikuwaje hadi simu yake ipo kwako?”
“Mama, nilimsikia kwa masikio yangu akiongea na simu kuhusu dawa ya kuweka ili wanimalize, ndipo akaandaa chakula na kuniwekea hiyo dawa kwenye chakula ila mimi nilifanya mchezo wa kumbadilishia sahani ya chakula na ndipo alipokula alianza kutoka povu na kutapatapa na akawa kimya hapo hapo kumbe ilikuwa ni sumu kali sana ya kuua kwa muda mfupi. Nikachukua simu yake na kugundua kuwa kuna vijana alizungumza nao kuja kubeba mwili wangu, kwahiyo nikampakia yeye kwenye viroba na kuwatumia wale vijana ujumbe kuwa waje wabebe tayari ila mimi niliondoka kwani nilipata pesa kwenye begi la Ashura na kuja kutafuta nyumba. Kwahiyo wale vijana walijua wameenda kunitupa mimi. Nilifanya hivyo kwasababu ni kesi kukutwa na maiti tena imeuwawa kwa sumu, nilifanya hivyo kuficha ushahidi kwani hata yeye alipanga kufanya hivyo”
Neema alishindwa kuwa alie au acheke kwani hakujielewa kabisa, siku zote alimchukulia Ashura kama mdogo wake ila hakuelewa kama Ashura alikuwa akimzunguka, ndipo akaelewa jinsi alivyoulizia habari za Ashura kwa mamake wa kambo na kuambiwa kuwa huyo mtu hawamtambui kabisa, alijaribu kuunganisha picha ya jinsi alivyokutana na Ashura na kupata jibu ya maswali aliyokuwa akimuuliza na kujua kuwa Ashura alitumwa katika maisha yake.
Salome akawaeleza vingi sana kuhusu Ashura na kuwafanya wabaki wameduwaa tu na hawakuelewa chochote kile, yani Neeema hakujua alie kwa kupata uhakika wa kifo cha Ashura au acheke sababu mwanae kanusurika na kifo, walijikuta wakikaa kimya tu wakitafakari kuhusu Ashura na kutumwa na Rose, yani Patrick alijikuta akijutia maisha yake,
“Najuta kumfahamu Rose, najuta kuanza kufanya biashara na mwanamke huyu. Alinifanya niifukuze familia yangu, amefanya nisiwathamini wanangu, amefanya mamangu auwawe kikatili, amenifanya niwasahau ndugu zangu, amefanya niwe kama ndondocha kwenye mali zangu mwenyewe. Najuta, amefanya niamini maneno ya Ashura kuwa ni ya ukweli sababu ni ndugu yako kumbe ni mtu ambaye amempanga kuja kuharibu maisha yetu, huyu mwanamke sijui nimfanye nini? Yeye ni mchawi ila mimi nitamfanyia kitu cha kawaida tu ambacho hatokisahau maishani mwake”
Patrick alionyesha kutokufurahishwa kabisa na mambo ya Rose, waliinuka na kwenda kulala ila si Patrick wala si Neema waliopata usingizi, kwani usingizi haukuwajia hata kidogo, muda wote Neema aliwaza alivyokuwa akiishi na Ashura jinsi alivyokuwa akishauriana nae halafu kumbe alikuwa na mipango ya kuuwa mtoto wake, ila tu alijiuliza kuwa kama alikuwa na mpango huo kwanini hakuweza kumuua mtoto wake wakati akiwa mdogo kabisa ndio kutaka kumuua mkubwa vile, aliwaza sana bila ya jibu la aina yoyote ile. Kwa upande wa Patrick nae alikuwa akiwaza tu toka siku ya kwanza alivyomfahamu Rose na jinsi alivyotelekeza familia yake.
 
SEHEMU YA 159

Asubuhi ilipofika walikuwa palepale sebleni yaani Sara, Doto na Kulwa. Waliamka na kusalimiana, mara wakashangaa kumuona mama yao akitoka chumbani, wakajikuta kwa pamoja wakisema,
“Mama!”
Muda kidogo wakashangaa kumuona na Ana nae akitoka chumbani, na kujikuta wakisema tena kwa pamoja,
“Ana!”
Ila Ana na mama yao walikuwa wakishangaa pia kwani ilionyesha kuwa nao hata hawakujijua kama wapo hapoa nyumbani, ikabidi Rose atoke nje ili akaangalie kama gari yake ipo, alipotoka hakuiona ile gari ambayo alienda nayo ikamfanya ajiulize sana kuwa imekuwaje yeye amerudi ila gari yake haijarudi? Halafu akakumbuka kuhusu rafiki yake aliyetakiwa kumzika wakati mwili ulikuwa ndani ya lile gari, hapo bado hakuelewa, akarudi ndani na kumtazama Ana kisha akamwambia,
“Mara ya mwisho nakumbuka nilikuona wewe ila kilichoendelea sikumbuki, imekuwaje mwanangu nimerudi nyumbani?”
“Hata mimi sielewi mama, nakumbuka ulianguka na kuanza kutapatapa. Kuna jiwe la dhahabu nililiokota mtoni, nikachukua na kukuwekea kifuani ila kilichoendelea sijui, ninachojua ni kuwa nimeamka asubuhi hii nipo chumbani mwangu”
“Unasema jiwe la dhahabu? Liko wapi hilo?”
“Sijui lilipo, yani mara ya mwisho ni kulitoa na kuliweka kwenye kifua chako ila sikumbuki limekwenda wapi”
“Unasema uliliweka kifuani mwangu?”
“Ndio mama”
Rose alikaa chini na kuanza kulia, watoto wake wote wakamshangaa kuwa anacholilia ni kitu gani maana wao hakwakuona cha kushangaza na kumfanya mama yao hata alie, walimuuliza kuwa analia nini,
“Ana mwanangu umenimaliza, yani umenimaliza kila kitu”
“Kivipi mama?”
Mara akaanza kuulizia kuhusu Salome na kuacha mada ya kuwa anamalizwa,
“Salome yuko wapi?”
“Yupo kwao”
“Sio Salome Yule, wanangu Yule ni Moza”
“Moza!!!”
Waliuliza wote kwa mshangao wa hali ya juu,
“Ndio ni Moza”
“Kivipi mama?”
“Nyie nieleweni tu, Yule sio Salome ni Moza”
“Mmmh kwahiyo Salome yuko wapi?”
“Sijui ila Yule ni Moza anatumia tu mwili wa Salome”
Wote walikuwa wanashangaa ila gafla wakasikia mtu akicheka na mara kidogo akatoka sebleni, na kusikia sauti ya Moza ikisema sasa,
“Unasemaje Rose?”
Kila mmoja alikuwa anatetemeka na hakuna aliyeweza kumtazama Moza machoni.
 
SEHEMU YA 160


Wote walikuwa wanashangaa ila gafla wakasikia mtu akicheka na mara kidogo akatoka sebleni, na kusikia sauti ya Moza ikisema sasa,
“Unasemaje Rose?”
Kila mmoja alikuwa anatetemeka na hakuna aliyeweza kumtazama Moza machoni.
Ila sauti ya Moza iliendelea kusema,
“Waambie yote watoto wako sio unawaambia tu kuwa Yule si Salome ni Moza, sasa Moza nimekuja mwenyewe na uzungumze yote mbele

yao”
Hakuna aliyeweza kuinua uso wake wala hakuna aliyeweza kusema kitu chochote na kumfanya Moza aendelee kuongea,
“Najua hapa nitakapoondoka kila mmoja atatafuta pa kwenda na kuogopa kurudi tena kwenye nyumba hii, ila niwaambie kuwa hakuna

mtakapoenda nisiwarudishe. Yani mkienda popote pale mtajisumbua tu kwani mimi nitawarudisha ndani ya sekunde. Mnashindwa kuuliza

kitu au kuongea chochote sababu mnaniogopa eeh! Naondoka ila kuanzia sasa, mkinitaja tu nakuja”
Kimya kikatanda na wote walikuwa kimya kila mmoja akiogopa kunyanyua kichwa chake na kutazama kwani hofu ilishatanda kwenye mioyo

yao. Sara aliuliza wenzie huku bado kainamisha sura yak echini,
“Jamani, ameshaondoka?”
Hakuna aliyejibu ila ikabidi Sara ainue kichwa chake na kutazama, akaona kweli ameondoka na kuwahakikishia wenzie kuwa ameondoka,

hakuna aliyeweza kucheka wala kusema neno lolote kwa muda huo kwani kila mmoja alikuwa na mashaka na nafsi yake.
Kisha aliinuka mmoja mmoja na kuelekea chumbani kwake na kuwaacha Rose pamoja na Ana kwani walikuwa kama ni watu waliopigwa na

shoti vile maana ni kitu ambacho hakikutarajiwa kabisa kwa siku hiyo.
 
SEHEMU YA 161


Walikaa kaa pale sebleni kisha Rose aliinuka na kwenda ndani kwake, kisha akachukua simu yake na kuiwasha yani ziliingia jumbe mbali mbali kwenye simu ile kanakwamba zilikuwa zikimsaubiri awashe tu simukwahiyo ziliingia jumbe nyingi hata akashindwa aanze na ujumbe upi na kumalizia na ujumbe upi, wakati anataka ajiweke sawa sasa asome akashangaa simu yake inaita, ilikuwa ni namba ngeni ila alipopokea ndio akagundua kuwa ni wale vijana wake wa kai ndio walikuwa wanapiga,
“Mama mbona hujibu ujumbe tunakutumia, hupatikani tatizo ni nini?”
“Yani nisameheni bure vijana wangu, simu ndio naiwasha leo. Nilikuwa na majanga mengi sana”
“Basi mama, ule mzoga tulioenda kutupa tumejaribu kuufukunyua ili tuone ni nini, mama ni maiti ya Ashura, yani aliyeuwawa na tuliyemtupa ni Ashura”
“Nini?”
“Ndio hivyo mama ni maiti ya Ashura, nadhani tulifanyiwa mchezo ndiomana namba ya Ashura tukipiga alikuwa haongei anatuma tu meseji”
Rose alihisi kushikwa na tumbo kabisa na kumwambia Yule kijana kuwa atampigia tena, aliinuka na kwenda chooni kuendesha yani tumbo lilimvurugika kabisa kwani alipewa habari ambazo hakuzifikiria kabisa, yani alihisi kuwa ni vitu vingine vimetupwa ila hakufikiria kama ni Ashura ndio alikuwa amekufa. Alitulia chooni kwa muda kadhaa kwani tumbo lilimvurugika vilivyo ingawa hakuna chakula kinachoeleweka alichokula ila tumbo lake lilivurugika, alirudi tena chumbani kwake na kujitupa kitandani huku akiwaza bila ya kupata jibu,
“Yani Ashura ndio amekufa!”
Hakujua kuwa aanze kupiga kelele za msiba au afanye kitu gani, alichukua tena simu yake na kupigia wale vijana kisha akaomba wakutane nae ili akaonyeshwe hapo ambapo walimtupa Ashura, nao wakakubaliana nao. Kwakweli leo Rose alichanganyikiwa kabisa, kwani aliona kama likitoka hili basi linaingia lile na kuzidi kumchanganya.
Alijiandaa na kutoka sebleni ambako aliwakuta tena wanae muda huu wamekaa sebleni kasoro Ana ndio alikuwa bado chumbani, kisha akawaaga na kuwaambia,
“Jamani natoka, nadhani badae tutaongea vizuri”
Alikuwa ni mtu mwenye hofu na mashaka halafu machozi yalionekana kumlengalenga, kitu hicho kilifanya wanae wamuulize kuwa mama yao anaenda wapi na kulikoni yani ni kitu gani kilichomsibu,
“Wanangu, Ashura amekufa”
“Ashura amekufa?”
“Ndio amekufa”
Machozi yalikuwa yakimtililika na kuondoka huku akiwaacha wanae wakijadiliana pale.
Walijiuliza kuwa huyo Ashura amekufa kivipi yani taarifa zimeletwaje maana mama yao alionekana kuchanganyikiwa kabisa na taarifa hiyo, Kulwa alijikuta akiwauliza wenzie,
“Sasa kama mama ni muoga hivi wa kifo hadi amechanganyikiwa kwa kifo cha Ashura, mbona alitaka kututoa kafara sisi? Angeweza kweli kuvumilia wakati watoto wake tumekufa kwa kutolewa kafara nay eye?”
“Unajua hata mimi mwenyewe namshangaa sana mama, kama anashtuka hivi na kifo cha Ashura je kifo chetu sisi angefanyaje!”
“Mi nadhani kwasababu kifo chetu alikuwa anakitarajia kwahiyo kisingemshtua sana, ila kifo cha huyo Ashura hakukitarajia. Sijui kafa vipi nay eye mmmh!”
Walijadiliana sana bila ya majibu yoyote yale ya moja kwa moja.

 
SEHEMU YA 162


Patrick siku ya leo aliomba asafiri kwani aliona ana ulazima wa kufanya hivyo ili aende kwa ndugu zake, Neema hakumpinga hata kidogo zaidi zaidi akamsaidia kujiandaa na kisha kumsindikiza kwenda kupanda magari ya kusafiri kwenda mkoa mwingine. Patrick hakuondoka na gari badala yake aliliacha gari lake nyumbani kwa Neema kwahiyo waliagana kisha Neema wakati wa kurudi akapitia tena kwa rafiki yake mama Pendo ambaye baada ya maongezi mafupi bado alimsisitizia kuwa mtoto wake ampeleke kwenye maombi,
“Sasa ndugu yangu Yule si mtoto mdogo kusema nitambeba mgongoni kwenda nae huko kwenye maombi”
“Ushawahi kuongea nae lakini kuhusu maombi?”
“Sijawahi yani kila nikitaka kuongea nae yanatokea mambo mengine najikuta sijaweza kuongea nae, yani usinione hivi nina makubwa ndugu yangu hata siju nianzie wapi na niishie wapi”
“Inatakiwa na wewe uende kwenye maombi”
“Nitakuja unipeleke, yani akili yangu haipo sawa kabisa”
Akaongea ongea nae pale kisha akaagana nae na kwenda kupanda daladala ili aweze kurudi nyumbani kwake, alipokuwa kwenye lile daladala kuna vijana pembeni akawasikia wakiongea,
“Yani muvi zingine za ajabu kweli yani, eti mtu anakufa mara mtu huyo anarudi kwenye mwili wa mtu mwingine sasa huyu mtu mwingine wanamshangaa kuwa anafanya mambo ya ajabu ambayo hajawahi kufanya kabla, unashangaa mtu alikuwa hanywi mara gafla anakuwa mlevi kupitiliza. Yale mambo ingekuwa kweli sijui ingekuwaje!”
“Lakini kuna baadhi ya vitu ni kweli sema tu tunapuuziaga vitu hivi”
“Mmmh hivi inawezekana kweli mtu akarudi kwenye mwili wa mtu mwingine? Hapo ikitokea itakuwaje?”
“Kwani hiyo picha iliishia wapi?”
Mara wale vijna kituo chao kikatangazwa na kushuka, kwa jinsi Neema alivyovutiwa na maongezi yao ni hakika kama ingekuwa ni kituo cha kushuka yeye basi angepitilizwa ili aendelee kusikiliza walichokuwa wakizungumzia. Akajiuliza mara mbili mbili kuwa inawezekana vipi kwa mtu mwingine kuingia kwenye mwili wa mtu mwingine, kisha akaanza kuwaza jinsi mtoto wake Salome alivyobadilika yani anatenda mambo ya tofauti kabisa na aliyokuwa anayafanya awali, na mara nyingine anapika chakula kinachoendana na alichokuwa akipika Moza, akaanza kujiuliza,
“Inamaana Moza… Hapana haiwezekani, ile walikuwa wanasimuliana ni muvi tu. Haiwezekani mwanangu Salome akawa Moza, Yule ni Salome na wala sio Moza, halafu Moza alishakufa”
Akawa anawaza huku akikataa majibu yake mwenyewe anayoyawaza kwani aliona akichanganyikiwa tu, kuja kushtukia kapitilizwa kituo chake sababu ya mawazo, kwahiyo akashuka na kupanda gari nyingine ili aende nyumbani kwake.
Alipokuwa kwenye gari nyingine alisikia sauti ya mtu ikimwambia,
“Pole kwa mawazo mama”
Sauti hiyo ilimchanganya vilivyo kwani ilikuwa ni moja kwa moja sauti ya Moza, kwahiyo akashindwa hata kugeuka kumtazama mtu huyo kwani hofu tayari ilikuwa imeanza kuingia kwenye moyo wake, alifika kituo chake na kushuka ila alihisi Yule mtu ameshuka nae, na kila alipotembea kwenda nyumbani kwake alihisi kuwa Yule mtu yupo nyuma. Alipatwa na uoga kadri alivyoongoza mwendo mpaka anafika kwenye geti la nyumbani kwake, bado alihisi Yule mtu yupo nyuma yake, akagonga geti kwa nguvu huku akijaribu kugeuka nyuma ili kama akikutana na maajabu basi apige kelele, ila alipogeuka nyuma hakuona mtu yeyote, kidogo moyo wake ukatulia na kujiona kuwa ni muoga sana ambapo alikuwa anaogopa kitu cha mawazoni.
Akajiona ni mjinga zaidi kugonga geti lake wakati linakuwaga wazi muda wote, akalifungua na kuingia ndani, aliwakuta wale wanae mapacha wakiwa sebleni na kuwauliza,
“Dada yenu yuko wapi?”
“Amerudi muda sio mrefu yani nadhani mliongozana mama, maana muda huu huu kaingia ndani. Yupo jikoni”
Neema bado aliganda kwani alikuwa kama haelewi elewi kitu vile, alikaa kwenye kochi huku akihema kwa nguvu ili kujitoa hofu kwanza.

 
SEHEMU YA 163

Rose alikutana na wale vijana wake na moja kwa moja wakampeleka kule wakikotupa ule mwili, nay eye aligundua tu nguo za Ashura,
“Jamani ni kweli Ashura wangu”
“Ndio mama, ni Ashura kumbe ndio tulimtupa na tukajua ni kile kitoto”
“Jamani nani kamuua Ashura wangu?”
“Mama itakuwa ni kile kitoto tu ndio kimetuchezea mchezo mchafu, labda ndio kamuua Ashura halafu akatuma ujumbe kuwa tukambebe na kumtupa”
Yani Rose hakujua cha kufanya kwa muda huo kwani vitu hivyo vilikuwa vikimchanganya sana, hawa vijana walimuuliza kuwa ni kitu gani kifanyike kwa mwili wa Ashura ulioharibika na kuwaomba kuwa wachimbe hata shimo na kumzika kwani hakuelewa kuwa hata wafanyeje,
“Sisi tutachimba mama ila mshiko ndio tunaouhitaji”
“Nitawapa jamani, naomba tu mchimbe bora kidogo niwe na amani kuwa ndugu yangu hata alizikwa, yani roho inaniuma sana kumuona Ashura katiaka hali hiyo.”
Wale vijana hawakupoteza muda na kuanza kuchimba shimo, ila wakati wanataka kumzika Ashura lile shimo lilijaa maji na kumfanya Rose ashangae kuwa shimo limechimbwa vizuri halafu lijae maji tena, akawaomba wale vijana wachimbe tena. Walichimba mashimo kama matatu na yote yalijaa maji wakamwambia,
“Nadhani tuzike hivyo hivyo tukisema tuchimbe chimbe tutabambwa hapa, ujue vitu vya magendo hivi tunafanya? Na tukikamatwa ni kifungo cha maisha hakuna atakayetuelewa, tutaonekana tuliua na ndio tumeamua kuja kuzika mtu tuliyemmaliza”
Rose hakuwa na jinsi ikabidi wazike hivyo hivyo kwenye mimaji na kufukia, roho ilimuuma sana kuona ndugu yake amezikwa kama mnyama, ndugu yake kazikwa kikatili na ameuwawa ingawa bado hakuelewa kuwa dawa aliyoweka ili auwawe Salome ndio dawa hiyo hiyo iliyomuua Ashura.
Walimaliza, akawalipa wale vijana na kuondoka, alikuwa anarudi nyumbani kwake huku ana mawazo mengi sana haswaa akiwaza kuwa afanyaje na huyu mtu wa kuitwa Salome ilihali kashaujua ukweli kuwa huyo Salome ndio Moza ila huyo Moza akija kwenye umbile lake la Moza asilia anatisha sana bora akija kama Salome, na hapo akajiona mapambano ya kupambana na Salome yakimshinda kabisa.
“Natakiwa nimtafute Patrick nimwambie ukweli kuwa mwanae Salome ni mtu mwingine”
Alipanga kumtafuta Patrick ila alijaribu kupiga simu za Patrick kwa wakati huo hakuzipata hewani zilikuwa hazipatikani.
 
SEHEMU YA 164


Neema alikuwa pale sebleni ila ndani ya muda ule ule, Salome alikuja kumwambia kuwa chakula ni tayari na kumfanya uoga umshike zaidi kuwa amekipika saa ngapi ikiwa watoto wale wamemwambia kuwa karudi muda sio mrefu, ila kabla hajamuuliza chochote Salome akamwambia,
“Mama unajiuliza kuwa chakula nimepika muda gani, unafikiri nimekipika sasa hivi basi? Nilikiacha jikoni, na mimi nilienda dukani”
Kidogo alivyosema hivyo hofu ilimuisha Neema na kujikuta akiinuka kwenda kula, ila macho yake hayakuisha kumuangalia Salome, alikuwa akimuangalia kwa jicho la wizi lakini alikuwa akimuangalia haswa wakati anakula alimuangalia sana, kwa kawaida Salome hakuwa na utaratibu wa kula ila alishangaa Salome wa sasa hivi alikuwa na utaratibu wa hali ya juu hata wakati anakula hakuwa akiongea wakati Salome hadi alikuwa akipaliwa kwa mtindo wake wa kula na kuongea.
Walipomaliza kula aliamua kuzungumza na Salome kuhusu swala aliloambiwa na mama Pendo la maombi,
“Sawa nitaenda, ila nipe sababu ya kunipeleka mimi kwenye maombi?”
“Salome umekataa kusoma, sasa unafikiri nisikupeleke kwenye maombi kweli!”
“Kusoma sijakataa ila nimekwambia nimechoka kwa kipindi hiki na nitasoma mwakani, kwani mbali jamani mwakani si hapo tu. Halafu kitu kingine kwani mtu asiposoma ndio ana matatizo hadi aombewe? Wangapi hawajasoma na maisha yao ni mazuri tu”
“Hatakama Salome, ila mimi ni mama yako naomba twende kwenye maombi”
“Sawa mama tutaenda”
“Kesho jiandae nikupeleke kwenye maombi”
Salome alimuitikia Neema bila ya pingamizi lolote ila muda wote Neema alikuwa akijiuliza maswali bila ya majibu huku akijaribu kuhusisha stori za wale vijana na jinsi alivyo Salome wake, ila alijikuta akipinga kuwa Salome wake hawezi kuwa amevamiwa na mzimu ila ni Salome Yule Yule sema kabadilisha matendo yake.

 
SEHEMU YA 165


Kwa Yule mganga ambapo Rose aliacha lile gari likiwa na mwili wa mama Jack, mganga akataka afanye jambo la kichawi ili mwili ule urudi kwa Rose kisha Rose angejijua mwenyewe, mganga alimchukua msaidizi wake na ule mwili kisha wakauweka kwenye kile chumba cha mganga na kuanza kufanya dawa zake ili ule mwili uende nyumbani kwa Rose, basi alifanya dawa zake kwa muda kama wa nusu saa na ule mwili ukatoweka machoni mwao, mganga alijisifia,
“Mimi ndio kiboko wa kila kitu”
Mara gafla ule mwili ulirudi kibandani kwake na kumfanya mganga na msaidizi wake wabaki wanashangaa,
“Imekuwaje tena?”
“Nadhani kuna mtu anacheza na akili yangu, ila sikubali”
Akafanya tena dawa zake kama kwa nusu saa hivi, na mwili ukatoweka kweli. Sasa muda huu alitaka kujua kuwa ulipo mwili ni kitu gani kinatokea, akachukua kioo chake na kuangalia alishangaa sana kuwa muda huo mwili wa mama Jack ulionekana nyumbani kwa mama Jack na watu kwenye nyumba hiyo walikuwa wakishangaa tu.


Akafanya tena dawa zake kama kwa nusu saa hivi, na mwili ukatoweka kweli. Sasa muda huu alitaka kujua kuwa ulipo mwili ni kitu gani kinatokea, akachukua kioo chake na kuangalia alishangaa sana kuwa muda huo mwili wa mama Jack ulionekana nyumbani kwa mama Jack na watu kwenye nyumba hiyo walikuwa wakishangaa tu.
Mganga alishtuka sana na kumuangalia msaidizi wake,
“Sijui ni wapi nimekosea yani sijui, badala mwili uende nyumbani kwa Rose eti umerudi kwa familia yake”
“Sasa tutafanyeje?”
“Sijui ila kuurudisha huku siwezi, hata mwanzo nimeshangaa ulirudi huku sasa sijui ndio ulienda nyumbani kwa Rose au ni kitu gani halafu saivi umeenda nyumbani kwa mama jack. Sina jinsi itabidi tu nikubali kuwa anaenda kuzikwa nyumbani kwake ingawa ni mbaya sana ila sina cha kufanya”
Msaidizi wa mganga alikuwa kimya tu huku akishangaa matukio ya siku hiyo.

Nyumbani kwa mama Jack, walishtushwa sana na kitendo cha kukuta mwili wa mama yao upo ndani tena inaonyesha alikufa siku mbili au tatu zilizopita, kwakweli walilia sana na kufanya wakose hata la kufanya na mwili huo, wengine wakawaambia wakazike tu maana utakuwa na harufu, ila walikataa kuwa haiwezekani kuzikwa bila ya kuchunguzwa kwanza, kwahiyo wakakubaliana kuwa mwili ule ukafanyiwe uchunguzi maana hata ulivyofika pale nyumbani ilikuwa ni kiajabu ajabu kwahiyo wakaita watu na kusaidiana kupakia kwenye gari ili kuupeleka hospitali kwaajili ya uchunguzi, kila mmoja alikuwa haelewi na watoto wa mama Jack walilia tu kuwa mama yao umekuja mwili amekufa wakati walijipa moyo kuwa yupo, na kama mama yao kauwawa hao waliomuuwa walikuwa na lengo gani maana gari halikuibiwa lilikutwa tu nyumbani ila mwili wa mama yao umekutwa ndani, hakuna aliyeelewa moja kwa moja kuwa yale ni mambo ya kishirikina.
Basi walipanda kwenye gari na ule mwili wa mama yao ila wakati wanakaribia hospitali ule mwili ulitoweka kwahiyo walifika hospitali bila ya ule mwili kuwepo kwenye gari, kila mmoja alimtazama mwenzie na kufanya waanze kuogopa sasa, huku wakirudi na gari upesi upesi nyumbani n hakuna aliyeweza kubaki nyumbani hapo kwani wote walikuwa na mashaka muda wote, ndipo kuna ndugu yao mmoja aliyetoa wazo kuwa waende kwa mganga wa kienyeji ili wakaangalie maana yake hayakuwa mambo ya kawaida.

Upande wa Yule mganga, walitulia kwa muda na kuhisi kuwa ule mwili wa mama jack utakuwa tayari umeshazikwa kwake ila walishangaa gafla mwili ukirudi kwenye kibanda chao, kwakweli mganga hakutaka tena kushindana na zile nguvu zaidi ya kumuomba kijana wake watafute vijana wawasaidie kuchimba kaburi kisha auzike huo mwili,
“Nitamkomesha huyu mwanamke aitwaye Rose, anadhani ni rahisi rahisi hivi kunitesa mimi! Nitamkomesha”
Yule msaidizi akaenda kutafuta vijana nao wakachimba kisha kwenda kwaajili ya kuzika ila kaburi lilijaa maji, mganga hakutaka kujisumbua zaidi kuwa wachimbe kaburi lingine badala yake aliwaambia wazike hivyo hivyo kaburi likiwa na maji, nao wakafanya hivyo ili wakimbizane na muda kwani giza lilikuwa linaanza kuingia, na walipomaliza waliondoka zao.

 
SEHEMU YA 166


Rose alifika nyumbani kwake na kukutana na watoto wake getini wanataka kuondoka, ikabidi awaulize kulikoni,
“Mama kuna vioja huko ndani, unajua tulikuwa tumekaa pale sebleni mara ikaletwa maiti ya Yule rafiki yako na kuwekwa pale kati kati yetu yani kila mmoja hapa alichanganyikiwa na gafla ikapotea tena”
“Mmmh jamani, sio mawazo yenu tu!”
“Mawazo yetu! Mawazo wapi? Kila mmoja ameona kwakweli ni mambo ya ajabu, hakuna anayeweza kuishi tena humo ndani”
“Kwahiyo na Ana yuko wapi?”
“Yupo chumbani kwake, yeye hajatoka kabisa tangia muda ule”
“Wanangu tafadhari msiondoke, maana hata mkiondoka hamtatui tatizo kabisa, hili ni tatizo ila halimalizwi kwa kuondoka”
“Mama tunaondoka”
Mlinzi akawaambia,
“Hata msijisumbue kuondoka, mtashtukia mmerudishwa hapa hapa”
Ndipo wakakumbuka na maneno ya Moza kuwa wasikimbie nyumba hiyo kwani hata wakikimbia watarudi, pia wakakumbuka siku ambayo walikimbia na kwenda kulala hotelini ila wote walirudishwa nyumbani kwenye vyumba vyao, mwisho wa siku wakaona hata kukimbia ni kazi bure na kuamua kurudi na mama yao ndani, ila walipoingia tu ndani wakamwambia mama yao,
“Mama tafadhali toa ile misukule yako kwenye kile chumba cha siri maana ndio vitu vinavyotumika kututesa sisi”
Rose aliwashangaa wanae kuwa wamejuaje kuhusu kile chumba chake cha siri, ila Kulwa aliendelea kujua,
“Usishangae tu kuwa tumejuaje kuhusu kile chumba cha siri ila ujue kwamba tumejua kuwa ulitaka kututoa kafara watoto wako. Mama umeugua sana na kifo cha Ashura, hivi watoto wako sisi sio zaidi ya huyo Ashura? Sisi si ndio uliotutolea uchungu mama, ila ukataka kututoa kafara mama ili upate faida gani? Na kama kupata mali, utumie na nani wakati watoto wako umetutoa kafara”
Rose alikaa chini kwanza kwani hakufikiria kuwa watoto wake wamejua habari zake za kutaka kuwatoa kafara pia, yani habari za chumba hazijaisha zimekuja habari zingine za kutaka kuwatoa kafara. Akajikuta tu akiongea kwa unyonge,
“Nani amewaambia habari hizo wangu?”
Kulwa ndiye aliyemjibu mama yao maana leo alijitoa muhanga haswaa kwa hakika alichoshwa na kilichokuwa kinaendelea kwenye nyumba yao.
“Mama sekeseke lilianzia kwenye chumba chako cha siri ambako mtoto wako nilipigwa na shoti, sijui umeweka nini kwenye kile chumba. Nilizimia ila nililetwa ulipo kwa mganga na alikupa machaguo mawili kuwa umzike rafiki yako au uwatoe kafara watoto wako”
“Lakini sikuchagua kuwatoa kafara wanangu”
“Mama hukuchagua ndio ila kumbuka kuwa ulishataka kuwatoa kafara Doto na Sara, hivi wewe ni mama wa aina gani ambaye huna upendo na watoto wako? Siku zote umekuwa ukihangaika kwaajili ya maisha yetu, kuhangaika kwako huku ili tule vizuri na tulale vizuri, leo hii uliowahangaikia uwatoe kafara kweli?”
“Nisameheni wanangu”
Rose alijikuta akitoa machozi tu, muda ule ule Ana nae alitoka chumbani na kusema,
“Tena nisingekuwahi mama, ungeenda tu kumzika Yule rafiki yako basi ungetutoa kafara na sisi maana uliambiwa utaje majina wakati unamzika, yani ungemtaja mwanao mmoja mmoja na huku ingekuwa kwaheri”
“Umejuaje Ana?”
“Mama, tambua kuwa mimi nina utambuzi mkubwa sana. Nashukuru lile jiwe la dhahabu nililoliokota maana lilikuwa na nguvu za ajabu, mwanzoni tulipotoweka nilijilaumu kuliokota lile jiwe ila baada ya kujua ukweli nashukuru kwa kuliokota lile jiwe. Mama hata mimi uchawi umenichosha sasa, jamani ndugu zangu msiniogope ila nisaidieni natamani kuacha uchawi”
Wote walimshangaa Ana kuwa amebadilika hivyo kwa muda mfupi tu, na amekubali kuacha uchawi, Sara alijikuta akimsogelea mdogo wake ingawa kwa uoga uoga ila alimkumbatia na kumpongeza kutaka kuachana na uchawi, ila alikuwa anampongeza huku ana mashaka bado, sema Kulwa hakuacha hoja yake kumwambia mama yao kuwa atoe misukule aliyoiweka kwenye chumba chake cha siri, mama yao akawaomba kuwa wampe muda kidogo ajifikirie kwanza, akainuka na kwenda chumbani kwake.
 
SEHEMU YA 167


Ana alibaki na wale ndugu zake huku akiwauliza kuwa atawezaje kuacha uchawi,
“Si unaacha tu”
“Haiwezekani kuacha uchawi kirahisi rahisi hivyo jamani”
Wakaangaliana kwa muda kisha kuulizana kuwa uchawi unaachwa vipi kirahisi, hakuna aliyekuwa na jibu,
“Ni vigumu sana kuacha uchawi kirahisi rahisi hivyo, itanigharimu maisha yangu yote. Natamani kuacha uchawi ila ni vigumu kwangu kuacha uchawi kirahisi rahisi”
“Mfano mama akiacha uchawi, na wewe si utaacha?”
“Mama hataki hata kusikia habari za kuacha uchawi ingawa unamtesa sana sasa hivi, ila mkiweza kumshawishi aache basi mtakuwa mmefanya vyema”
Ana aliondoka na kuelekea chumbani kwake, ila bado ndugu zake walijiuliza kama kweli Ana ana lengo la kuacha uchawi huku Sara akikumbuka alivyopofushwa na ndugu yake kichawi pia akawasimulia ndugu zake jinsi Ommy alivyopotea kwenye nyumba yao na kuwaambia kuwa nae ni mmoja wapo wa misukule wa mama yao, walikuwa wakishangaa tu uchawi wa mama yao jinsi ulivyo na bila wao kujua kama mama yao ni mchawi tena wa kudumu kiasi kile.
Waliongea sana ila badae walipoona muda umeenda sana wakakubaliana kuwa waende wakalale ila Sara akatoa tena ushauri,
“Jamani na leo kwanini tusilale wote sebleni?”
“Bado unaogopa tu kulala mwenyewe?”
“Ndio naogopa”
“Basi kalale na Ana”
“Weeee hapana jamani, siwezi kulala na Ana jamani”
“Kwanini lakini wakati kasema anaacha uchawi”
“Hata kama siwezi kulala na Ana kwakweli, bora nikalale ndani kwangu peke yangu”
Sara akainuka na kwenda ndani kwake kisha wale mapacha nao waliamua kuondoka na kwenda chumbani kwao kwahiyo pale sebleni kwao palibaki hapana mtu.
Baada ya muda kupita kidogo na kimya kutanda ndipo Rose alipoamua kwenda kufanya mambo yake sebleni sasa na kwavile aliona hakuna mtu hata mmoja akahisi ni vyema kufanyia vitu vyake hapo kwani yeye alikuwa anapenda zaidi kufanyia mambo yake sebleni kisha yanatawala nyumba nzima ila siku za hivi karibuni hakufanya sababu ya kutingwa na mambo mengi sana, taratibu alianza kufanya mambo yake pale kwa kuwasha dawa zake za kujifukiza na kuanza kujifukiza sasa.
 
SEHEMU YA 168


Sara hakupata usingizi kabisa kwa usikiu huo kwani yeye alihisi kutokewa na vitu vya ajabu ajabu tu na kufanya ashindwe kulala, mara akasikia harufu kuwa kama kuna kitu kimewashwa hivi, uoga ukamshika kwani alihisi kuwa ndio huenda ni yale mambo ya ajabu yameanza tena, akatamani kujificha ila hakuwa na pakujificha ila akajivika ujasiri na kusema kuwa atatoka ili aende kuona kinbachoendelea.
Akanyanyuka taratibu huku akiwaza kuwa kama ataona vitu visivyoeleweka basi atapiga kelele ili kaka zake nao waamke na wamsaidie.
Taratibu akatoka chumbani kwake na kugundua kuwa ule moshi unatoka sebleni, kwahiyo akanyata hadi sebleni akashangaa kumuona mama yao akiwa mtupu kabisa akijifukiza na dawa zilizokuwa zikifuka moshi, akasema kwa hamaki,
“Mama!”
Mama yake aligeuka na kumtazama ila sura yake ilikuwa tofauti na alivyoizoea, ilikuwa ni sura ya kutisha sana, Sara akajishangaa kuwa anaanza kukimbia na badala ya kukimbilia chumbani alikuwa akikimbilia mlango wa kutoka nje ilia toke nje na kukimbia ila kabla hajafika mlangoni alijikwaa na kuanguka halafu mguu wake ukaanza kutoka damu, alimuona tu mama yake akiweka mikono kichwani na kusema,
“Masikini mwanangu jamani! Na yeye ndio anapotea hivyo!”
Mara gafla akatoweka, hakuwepo tena pale sebleni wala uwepo wake haukuonekana kama hata amechungulia mahali hapo, Rose aliacha kuendelea na zile dawa zake, alibeba vitu vyake na kwenda chumbani, alijibadilisha na kuwa kawaida kisha akaanza kulia huku akiumia sana moyoni,
“Sara mwanangu jamani kwanini lakini! Kwanini unataka kunifedhehesha mama yako? Kwanini unataka nikose raha mama yako, unajua ulipoenda ni pagumu sana, unaweka maisha yangu klwenye ugumu wa hali ya juu”
Rose alilia sana na kumfanya ashindwe kabisa kulala wala kuendelea na jambo lolote kwa usiku huo hadi panakucha.

Ndugu wa mama Jack walienda kwa mganga ila Yule mganga aliwatahadhalisha sana,
“Ndugu yenu aliingia kwenye mtego mbaya sana, na hata hivi ninavyoongea ameshazikwa”
“Amezikwa?”
“Ndio kazikwa, na sehemu aliyozikwa ni kaburi lenye maji kiasi kwamba siwezi hata kufanya dawa yoyote kwaajili yake, hata hivyo alikaa muda mrefu sana kabla ya nyie kugundua kifo chake.”
“Sasa tutafanyaje?”
“Sijui cha kufanya ila hata huyu mganga aliyechukua jukumu la kumzika mama yenu kwenye kaburi lililojaa maji ana jambo gumu sana na kubwa linaenda kumpata”
“Sasa ndugu yetu tutamkoa vipi?”
“Jamani ngojeni pakuche, usiku mzima nitafanya dawa zangu ila huyu aliyemfanyia mama yenu hivi lazima aumbuke kabla hapajakucha. Ngojeni nifanye dawa zangu, leo msiondoke hadi kesho tutakuwa tumepata majibu ya kueleweka”
Ndugu wa mama Jack waliamua siku hiyo kulala nyumbani kwa mganga ili kujua hatma ya ndugu yao maana kifo chake kilikuwa na utata sana.
 
SEHEMU YA 169



Kulipokucha, Neema alienda kumuamsha Salome na kumkumbusha kuhusu lile swala la kwenda nae kwenye maombi, ni kweli Salome hakubisha kabisa halafu wakaanza kujiandaa walipomaliza safari yao ikaanza huku Neema akimsisitiza mwanae kuwa wakifika huko aeleze kila jambo linalomsibu ili iwe rahisi kuombewa, Salome alimuitikia mama yake na alikubaliana nae kwa kila kitu.
Walifika kituoni na kushuka kisha safari ya kuelekea kwenye maombi ikaanza sehemu yenyewe haikuwa mbali na kituo cha basi, wakati wanakaribia kufika Salome alimuomba mama yake kuwa aende dukani kununua maji mara moja kwani alikuwa na kiu sana, Neema alikubali kisha Salome akaanza kwenda dukani ambako napo hapakuwa mbali sana, ni nyuma kidogo tu na walipokuwa.
Neema akaona kama mwanae anakawia dukani na kuamua kumfata, ile anafika dukani tu alishtukia akiwa nyumbani kwake tena bado yupo chumbani kitandani yani ndio anaamka.


Walifika kituoni na kushuka kisha safari ya kuelekea kwenye maombi ikaanza sehemu yenyewe haikuwa mbali na kituo cha basi, wakati wanakaribia kufika Salome alimuomba mama yake kuwa aende dukani kununua maji mara moja kwani alikuwa na kiu sana, Neema alikubali kisha Salome akaanza kwenda dukani ambako napo hapakuwa mbali sana, ni nyuma kidogo tu na walipokuwa.
Neema akaona kama mwanae anakawia dukani na kuamua kumfata, ile anafika dukani tu alishtukia akiwa nyumbani kwake tena bado yupo chumbani kitandani yani ndio anaamka.
Neema alishangaa sana na kujiangalia mara mbili mbili, ni kweli alikuwa ametoka kuamka ysni hata kuoga alikuwa hajaoga,
“Jamani haiwezekani, yani iwe sijaamka mpaka muda huu kweli!”
Akachukua na simu yake kuangalia saa, akaona ni saa tano asubuhi na kuzidi kushangaa kwani hata kwakama kwa kawaida hana tabia hiyo ya kulala mpaka saa tano asubuhi, mara nyingi akichelewa sana basi anaamka saa mbili ila siku hiyo ilimchanganya zaidi, akajaribu kukumbuka kuwa alishajiandaa na Salome walikuwa wanaenda kwenye maombi na mara ya mwisho Salome alimuomba kuwa anaenda kununua maji halafu alikawia sana dukani, ila alipomfata dukani ndio akajikuta yupo kitandani tena akiwa naio kwanza anaamka, akajiuliza
“Hivi naota au ni kitu gani? Lakini sioti jamani mbona nilikuwa macho jamani ndoto gani hii?”
Neema alijiuliza maswali kadhaa bila ya majibu, akaamua kutoka ili ajaribu kuona kama anaota au la.
Alitoka na kumkuta Salome akiwa anaandaa kifungua kinywa, na alipomuona tu alimuamkia, Neema alishangaa sana na kumuuliza Salome,
“Inamaana bado hatujaonana?”
“Tumeonana muda gani tena mama? Si ndio umetoka kuamka?”
Neema akaganda kwa muda kisha akamwambia Salome,
“Hivi mimi na wewe hatujaenda mahali leo?”
“Mama unaota ua?”
“Sijui mwanangu, yani sijui kabisa ila ninachojua ni kuwa tulijiandaa kwenda kwenye maombi, na tulifika kabisa ila wewe ukataka kununua maji, nimekufata gafla nikajikuta kitandani ndio naamka”
Salome alicheka sana, kisha akamuangalia mama yake na kumwambia,
“Mama jamani mbona vichekesho hivyo yani uende mahali halafu ujikute gafla umelala ndani yani ndio unaamka! Unaona hilo jambo linawezekana kweli?”
“Hata mimi nashangaa mwanangu, yani sielewi kabisa”
“Hiyo ni ndoto mama isikupe presha”
“Yani hata sijui, sijui kabisa yani”
“Usijali mama ni ndoto hiyo”
Neema alikaa kwenye kochi sasa, huku akiwa na mawazo tele kuhusu yale mauzauza aliyoyapata maana hakuelewa kama ni ndoto au ni kitu gani.
Alijifikiria sana bila ya majibu, wakati anawaza vile akashtuliwa na Salome na kumwambia,
“Natoka mama”
Alitaka kuongea jambo ila hakuweza kuongea chochote zaidi ya kumuitikia mwanae tu kuwa wataonana badae.
 
SEHEMU YA 170


Ndugu wa mama Jack leo waliendelea kufanyiwa dawa na Yule mganga, Yule mganga aliwaambia kuwa anaona kitu sio cha kawaida kimefanyika kisha akawaambia,
“Inaonekana mama Jack katolewa kafara na rafiki yake”
Wakashangaa sana, na kuuliza kuwa ni rafiki yake yupi ambaye kamtoa kafar mama yao,
“Huyo rafiki yake anaitwa Rose”
Watoto wa mama Jack wakashangaa sana kwani mama yao siku zote alikuwa akimsifia huyo Rose ingawa hawakujua kuwa Rose anapatikana sehemu gani. Yule mganga aliendelea kuongea,
“Yani huyo Rose anapenda sana mambo ya waganga wa kienyeji ndiomana kajikuta kamtoa rafiki yake kafara, mama yenu kosa lake ni kumsindikiza huyu Rose kwa mganga yani huyo Rose anapenda sana mambo ya waganga ndio yanayomghalimu.”
Walimshangaa mtoto mmoja wa mama Jack akishindwa hata kuendelea kumsikiliza mganga bali aliinuka na kuondoka zake.
Alienda moja kwa moja nyumbani kwao na kuchukua simu ya mama yake kisha kupekua jina la Rose, na alipolipata alimpigia simu,
“Hallow”
“Samahani nani mwenzangu?”
“Najua mama una shida, mimi ni mganga wa kienyeji. Naomba tukutane nikusaidie”
“Jamani umejuaje dah! Nashukuru sana, nielekeze ulipo nije”
Basi Yule kijana akamuelekeza Rose mahali ambapo yeye aliona panafaa kukutana na huyo Rose kwani alikuwa na uchungu sana wa mama yake kutolewa kafara ukizingatia maiti ya mama yake ilifika kwao na kutoweka kwahiyo mama yao walijua tu amekufa ila hata nafasi ya kuzika mwili wa mama yao hawakuipata, yani kijana huyu alijikuta ana uchungu uliopitiliza moyoni mwake haswaa swala la kumfikiria Rose.

Rose muda aliokuwa nyumbani kwake na mawazo sana kuhusu kutoweka kwa Sara ndio muda aliopigiwa simu na Yule kijana kwahiyo alihisi kupata mkombozi ukizingatia hakutaka kuchukua hatua ya kutoa wale misukule wake kwavile anahisi kuwa atapata matatizo ndiomana alikuwa anaogopa kuwatoa, kwahiyo ile simu aliona kama ya ukombozi kwake.
Alijiandaa haraka haraka na kutoka, ila sebleni alikuta watoto wake wale mapacha wamekaa na baada ya salamu walimuuliza mama yao,
“Mama, Sara kaenda wapi?”
“Jamani Sara ni mtu mzima, mimi siwezi jua alipoenda”
“Mama, Sara hajatoka humu ndani. Tumeenda kumuuliza mlinzi kasema hajatoka, tumemuangalia chumbani kwake hayupo pia. Sara kaenda wapi mama?”
“Jamani hebu subirini hadi jioni moune hatorudi, mtoto wa kike yule labda karuka ukuta huko kaenda kwa wanaume”
Kisha akatoka zake na kuwaacha, walijiuliza sana maswali ni kwanini mama yao kawajibu kirahisi kiasi kile maana swala la kutokuonekana kwa Sara ilitakiwa hata yeye ashtuke lakini cha ajabu yeye alikuwa akiwajibu kirahisi rahisi tu, wale mapacha walijiuliza sana kuhusu ndugu yao na kukosa jibu.
Mama yao alipoondoka, Ana nae alienda sebleni, ikabidi kaka zake wamuulize yeye,
“Sara kaenda wapi?”
“Sara!!! Sijui mimi”
“Ana, ulisema kwa uzuri kabisa unataka kuacha uchawi, Sara haonekani ndani. Mlinzi hajamuona akitoka, na kama angeenda mahali kwa hakika angetuaga hata simu yake ipo ndani, Sara yuko wapi?”
“Jamani sijui, mtanilaumu bure tu”
Hawa mapacha waliwaza sana cha kufanya ila hawakuwa na jinsi maana hakuna mwenye uhakika wa alipo Sara.

Salome leo alienda kumtembelea Mishi na kumshtua sana kwani hakutegemea kutembelewa tena na Salome, aliamini kuwa ameshamalizana nae, kwahiyo kitendo cha kumuona kaenda tena kumtembelea kilimshangaza sana, akashindwa hata kumkaribisha,
“Usishikwe na uoga Mishi, ila kilichonileta leo ni jambo moja tu. Kwanini unataka kumdanganya mzee wa watu?”
“Kumdanganya nini?”
“Si unataka kumwambia kuwa mimba hiyo ni yake!”
“Tafadhali naomba nisaidie, sitaki kuumbuka mimi, sitaki watu wajue kuwa nilibakwa ndiomana nataka kumwambia kuwa mimba ni yake”
“Msamaha wangu kwako ni kumwambia ukweli, yani wewe mueleze ukweli wote. Anakupenda, kukuacha hawezi, nataka tu ajue mtu anayempenda ni mtu wa aina gani, usimdanganye kuhusu mimba uliyobeba, mwambie ukweli wote”
Mishi alikuwa kimya tu maana huu ulikuwa ni mtihani mkubwa sana kwake, na alijua kama atamwambia huyo mzee ukweli basi ni lazima huyo mzee akikutana na mama yake Mishi atamueleza halafu yeye alitaka iwe siri,
‘Nihurumie tafadhali”
“kama husemi, nitakuumbua. Nakupa siku moja tu ya kumwambia mzee wa watu ukweli”
Ilibidi Mishi akubali kuwa atamueleza Yule mzee ukweli wa mambo ingawa alikuwa anaumia sana.
 
Back
Top Bottom