Simulizi: Kurudi Kwa Moza

Simulizi: Kurudi Kwa Moza

SEHEMU YA 171


Neema alikuwa anajiuliza hadi kwenda kuoga tena alikuwa anawaza, ila badae akakata shauri na kwenda kuoga halafu akarudi akiwa anaendelea na mawazo yake, watoto wake wale mapacha walitoka shule na kumkuta mama yao pale sebleni akiwa na mawazo, mmoja akaanza kumuuliza mama yao,
“Kumbe msharudi ile safari na dada”
Akili ikamzinduka kidogo na kufanya awaulize vizuri hawa watoto wake,
“Hivi asubuhi ni nani kawaamsha na kuwaandaa muende shule?”
“Si wewe mama”
“Hivi nilirudi tena kulala?”
“Mama jamani, ulisema wewe na dada Salome mnatoka, tena hadi ukatuelekeza mahali tutakuta funguo ndiomana tumekuuliza mmesharuudi tayari”
Neema alipata kidogo mwangaza wa jambo amabalo lilitokea ingawa bado alikuwa haelewi kuwa kama jambo hilo limetokea ni hakika limemtokea yeye pamoja na Salome sasa iweje salome amwambie kuwa alikuwa anaota? Aliwaza sana, kisha akachukua simu yake na kuamua kumpigia mama Pendo ili amshirikishe hilo swala, alimpigia na kumuelezea kila kitu jinsi ilivyokuwa, kwakweli mama Pendo alishangaa sana na kuhisi kuwa huenda ni stori za kusadikika,
“Una uhakika na hayo mambo kuwa uliondoka kweli nyumbani”
“Nina uhakika, hata wanangu hawa wadogo wamenithibitishia hilo”
Akamueleza jinsi wanae mapacha walivyomwambia, yani bado mama Pendo ilikuwa ngumu kuelewa kwani mazingira ya tukio lenyewe yalikuwa ni ya utata sana,
“Sasa mi ninachoona niongee na mtumishi aje hapo nyumbani”
“Kwakweli utakuwa umenisaidia sana ukifanya hivyo, haya mambo ni ya ajabu kwangu hadi sielewi nianzie wapi na niiishie wapi”
“Pole ndugu yangu, au nije mwenyewe kuwachukua”
“Hata hivyo ni sawa ili nimwambie Salome asitoke”
“Basi nitaangalia litakalo wezekana”
Neema aliongea sana na huyu rafiki yake, basi alivyokata simu likamjia tukio la kukumbuka kuwa alishawahi kumjuangalia mwanae Salome na kumuona kama kafanana na Moza, hofu ikamshika na kujisemea,
“Hapana haiwezekani, Moza aklishakufa na mwanangu yupo hai. Haiwezekani kwakweli”
Alikuwa anajiuliza na kujijibu mwenyewe ila alipatwa na mawazo sana huku akimngoja mwanae arudi kwa siku hiyo na kumwambia kuhusu ujio wa mama Pendo kuwapeleka kwenye maombi au ujio wa mtumishi kumuombea Salome.
 
SEHEMU YA 172


Ana wakati anaongea na kaka zake alikosa raha kabisa maana yeye alionekana anajua fika alipo dada yao Sara ukizingatia nyumba nzima hakujulikana alipo. Ikabidi ainuke na kwenda chumbani kwake kufanya dawa zake.
Alifika na kuzianza dawa zake, alifanya kwa muda kidogo na kumuona kuwa dada yake Sara ni miongoni mwa misukule ya mama yao. Alishtuka sana Ana na kushangaa kwanini mama yao kafikia hatua hiyo maana aliona sasa ni hatua mbaya yani mama yao hata afikie kumuweka kama msukule mtoto wake mwenyewe, maana misukule aliyokuwa anatunza mama yake ilikuwa ni tofauti na misukule ya watu wengine maana hii ililishwa kichawi na ilimsaidia kichawi kupata nguvu za ziada kiasi kwamba ni ngumu sana kwake kuitoa misukule hiyo kwani itamgharimu maisha yake yote, kwahiyo kitendo cha mama yao kumuweka Sara msukule kilimchanganya sana Ana na kumshangaza, akamuangalia mara mbili mbili dada yake alivyokuwa akisononeka na kumuonea huruma ila hata yeye Ana hakuwa na uwezo wa kuwatoa watu kwenye kile kichumba ambacho mama yao aliwahifadhi.
Kisha akajaribu kuangalia kuwa mama yao ameenda wapi, alimuona yupo porini ambapo hata njia hakuielewa halafu alikuwa akishangaa shangaa, mara wakatokea vijana watatu na kumbana, kile kitendo kilimfanya Ana atupe dawa zake zote kwa kushtuka kwani alijua wazi kuwa mama yao yupo hatarini.

Rose alienda hadi mahali ambapo alielekezwa na Yule kijana ila alifika jioni maana sehemu yenyewe ilikuwa ni safari ya mbali sana, alishangaa sehemu yenyewe ilikuwa kimya kabisa, akaanza kushangaa shangaa, mara walikuja vijana nyuma yake wakamfunga mdomo, mikono na miguu na mwisho wakamfunga macho,
“Mama mpumbavu sana wewe na habari zako za kupenda waganga, umemuua mama yangu na wewe ni lazima ufe”
Rose hakuweza kujitetea wala nini maana wale vijana walikuwa wamemziba mdono kwa kitambaa, kisha wakaanza kumpiga ambapo walimpiga sana, halafu wakakubaliana kuwa wambake, walifanya kazi ya kumbaka kwa zamu, Rose alilia sana na kujilaumu moyoni kufika sehemu bila ya tahadhari.
Wale vijana walimpiga sana Rose, kisha wakataka kumchinja kwani lengo la mtoto wa mama jack ni kumuona huyu mtu anayeitwa Rose akifa kama alivyokufa mama yao, ingawa mama yao alikufa kichawi ila walitaka huyu mtu wamuue kimacho macho.
Alishika kisu sasa akitaka kumchoma, wakati amekiinua ili amchome alishtukia mkono wake ukishikwa na kuzuiwa kumchoma, alipogeuza macho aangalie ni nani alimuona ni binti amabaye mama yao alimsaidia usiku ambapo kesho yake ndio alitokomea nae.
 
SEHEMU YA 173

Alishika kisu sasa akitaka kumchoma, wakati amekiinua ili amchome alishtukia mkono wake ukishikwa na kuzuiwa kumchoma, alipogeuza macho aangalie ni nani alimuona ni binti amabaye mama yao alimsaidia usiku ambapo kesho yake ndio alitokomea nae.
Yule kijana alishangaa sana kwani haikuwa kawaida kabisa, akatupa kisu chini huku akimuangalia Yule binti aliyeonyesha yupo serious sana, kisha Yule binti akamwambia,
“Naitwa Salome, ndio mimi mwenyewe niliyekuja kwa mama yako siku moja kabla hajafa, wala hujanibahatisha. Sasa kwanini unataka kumuua huyu Rose”
“Amemuua mama yangu”
“Ulikuwepo wakati anamuua?”
“Tumeambiwa na mganga kuwa amemtoa kafara mama yangu”
“Unajua ni kwanini mama yako ametolewa kafara? Huyu mwanamke alikuwa na marafiki wangapi zaidi ya mama yako? Na mbona asiwatoe wao kafara akamtoa yeye?”
“Sijui ila ninachojua ni kuwa huyu mwanamke ni muuaji kamuuwa mama yangu”
“Ngoja nikwambie kitu, huyu mwanamke ni mchawi ila huyu mwanamke na mama yako ni bora ya huyu mwanamke, huyu hajaua watu wengi kichawi kama alivyomaliza watu mama yako, kama huamini nenda chumbani kwa mama yako halafu kuna begi lake dogo jeusi limechimbiwa chini, ni vigumu kujua lilipo ila nitakusaidia kuliona, kisha uone ni viungo vingapi vya wanadamu mama yako anavimiliki, je ndugu wa hao watu nao wangeamua kufanya maamuzi kama yako si mama yako angekuwa marehemu muda mrefu!”
“Sikuelewi”
“Huwezi kunielewa ila muachie huyu mtu aondoke zake”
“Unaniahidi nini nikimuachia?”
“Nakuahidi kuwa utaniua mimi badala yake”
Yule kijana alimuangalia Rose pale chini kisha akainua macho yake kuwaangalia wenzie ambao walimpa ishara kuwa amuachie tu, kisha akainama na kumpiga teke Rose halafu akaamua kuondoka huku akiwa ameongozana na Salome.

Rose hakuelewa chochote ila anakumbuka kuwa sauti aliyoisikia ilikuwa kama sauti ya Salome, na yale maongezi ambayo Salome aliongea na Yule kijana aliyasikia vizuri, ila hakuweza tu kuona chochote maana walimziba macho, sasa alivyopigwa lile teke akaanza kujikongoja ili ainuke na kujiona kuwa hata kuinuka hawezi kwani maguu yote ilikuwa na maumivu ukijumlisha kupigwa na kubakwa, kwahiyo Rose alikuwa na maumivu makali sana, akaamua kupiga kelele za kuomba msaada ila kumbe wale rafiki wa mtoto wa mama jack walikuwa wakimfatilia kwa nyuma kwani walifanya vile ili rafiki yao aondoke na Yule binti ila wenyewe walitaka waendelee na ule mpango wa kumuua Yule mwanamke kwani uchungu aliokuwa nao rafiki yao na wao pia waliupata na waliuhisi. Wakati Rose akipiga kelele akashtukia akizibwa mdomo na kupigwa kibao,
“Nyamaza, muuwaji mkubwa wewe”
“Jamani sijauwa mnanionea bure”
“Hujaua nini wakati umemtoa mama Jack kafara, hivi unajua ni kiasi gani Yule mama alikuwa akitusaidia. Hivi unajua ni jinsi gani tulivyokuwa karibu na Yule mama, halafu umemuua unategemea nini? Kwa taarifa yako, sisi ni makatili kupita hata Yule aliyechukuliwa na zombie lako, yani sisi hatutakuchoma kisu ila tutakuchinja taratibu ili uone kifo kina uchungu gani”
Wakaanza tena kumpiga Rose, walimpiga sana, kisha kumfungia kwenye miti kamavile wanataka kumsulubisha, yani Rose alikuwa na maumivu makali sana.
 
SEHEMU YA 174


Salome aliondoka na Yule kijana mpaka nyumbani kwa mama Jack, kisha akaenda nae hadi chumbani kwa mama jack, ndugu zake na Yule kijana walikuwa bado hawajarudi kutoka kwa Yule mganga, basi akamuonyesha sehemu kuwa afukue, na Yule kijana akafanya hivyo kisha kukutana na mfuko mkubwa chini yake ambao kwa hakika kwa kawaida hata wasingeweza kudhania kuwa kuna mfuko wa aina ile ndani mwao haswa chumbani kwa mama yao, ilikuwa ni ajabu sana. Kisha Salome akamwambia Yule kijana afdungue ule mfuko, na alipoufungua alishangaa sana,
“Usishangae, hivyo ni vitu ambavyo mamako alikuwa anaamini kuwa vinamletea utajiri, mama yenu kashamaliza watu wengi tu kwa kuwatoa kafara akiangalia kupata mali na utajiri, unafikiri mali hizi mama yenu kazitoa wapi? Ngoja nikuulize, baba yenu yuko wapi?”
“Alikufa”
“Sasa unajua kuwa baba yenu alitolewa kafara”
“Kafara?”
“Ndio kafara, unakumbuka baba yenu alikufaje?”
“Alipata ajali yani gari walilopanda lilipinduka na alikufa baba peke yake”
“Wakati baba yenu anakufa, mama yenu alikuwa wapi?”
“Hakuwepo alikuwa safarini”
“Ila ndiye aliyekuja kuwapa taarifa kuwa baba yenu amekufa?”
“Ndio, anasema alioteshwa ndio akarudi na kukuta kumbe kuna ajali ilitokea na baba alikufa”
“Sasa kaa chini uelewe kuwa mama yenu alikuwa ni mchawi tena mchawi haswaaa na alikuwa anatamani amuachie mtoto mmoja uchawi wake sema katolewa kafara nay eye, na mama yenu kauwawa sababu yangu yani mimi ndio nimemsababishia mama yenu auwawe. Sipendi uchawi, nauchukia uchawi na nipo kwaajili ya kumkomesha Rose na marafiki zake, mama yenu alimshauri Rose aende kwa mganga, na Yule mganga ndiyo aliendaga yeye na kufikia hatua ya kumtoa mume wake kafara, halafu Rose naye aliambiwa awatoe watoto wake wawili kafara ila mimi nilikuja kumchukua mama yenu na akatoka badala ya watoto wawili wa Rose. Je bado unataka kuniua na mimi?”
Yule kijana alikaa chini kwanza kwani alihisi kuwa anaota, vile viungo vya binadamu kuvikuta kwenye chumba cha mama yao vilimshangaza sana, hadi akajikuta hana jibu kwa huyu mtu, kisha Rose akamuuliza tena,
“Dada yenu wa kwanza yuko wapi?”
“Alikufa”
“Hajafa”
“Hajafa! Kivipi?”
“Ngoja uone”
Muda kidogo alitokea mdada akiwa amechafuka sana, alikuwa dada yao na alikuwa hajielewi wala nini, Yule kijana bado kidpogo aanze kukimbia kwani hakutegemea kama wangefikia hatua hiyo,
“Nenda mkamshughulikie dada yenu arudi kwenye hali ya kawaida, mama yenu alimfanya msukule wake ampatie mali sababu dada yenu alikuwa na damu kali sana. Nenda mkashughulikie dada yenu, mnyoeni nywele hizo, mkateni kucha arudi kwenye hali yake ya kawaida, ila swala la mama yenu kurudi hilo halipo maana haiwezekani akarudi”
“Nitawezaje?”
“Utaweza tu, ila cha kuongezea, msimpeleke kwa mganga yoyote huyu dada yenu kama bado mnampenda. Na wala usishiriki dawa yoyote watakayokwambia ushiriki”
Kijana Yule alitia huruma zaidi kwani hata hakuelewa kama aendelee na kuchunguza ile mifupa au amsaidie dada yake, ila Salome aliondoka na kumuacha pale akitafakari bila hata kuelewa ila mwisho wa siku aliamua kumchukua dada yake na kubeba na mkasi kisha kutoka nae nje na kuanza kumkata nywele maana hata uoga ulimuisha muda huu ukizingatia alimuona dada yake akizikwa kabisa halafu katolewa akiwa mzima, ilimshangaza sana ila alijivika moyo wa ujasiri na muda mwingine kujihisi kuwa labda yupo usingizini na anafanya vile vitu ndotoni.
 
SEHEMU YA 175


Wale vijana waliendelea na kumtesa Rose, kisha kila wakitaka kumuua wanajikuta mikono yao ikiwa mizito sana, na mwisho wa siku wakati wanafikia hatua kuwa wamuue kwa pamoja, Salome alitokea katikati yao na kuwafanya waogope kwani hawakuwa kwenye lile eneo la mwanzo walilokuwa kwahiyo walijiuliza kuwa huku huyu binti kapajuaje,
“Nilisemaje? Si nilisema huyu mama aachiwe?”
Wale vijana walimuangalia Salome na kumshangaa kuwa binti mdogo vile anawezaje kuwa na amri juu yao, yani anasemaje bila ya kuwa na uoga hata kidogo, wakakonyezana kuwa wamvamie na huyu Salome wamdunde ili akili yake ikae sawa, sasa ile wanataka kufanya mashambulizi kwake wakashangaa wakianza kupigwa viboko, yani walicharazwa viboko vingi vingi kisha walishangaa kuona Yule mama waliyemfunga akitoweka na hata haikujulikana ni wapi ameenda ila wao walikuwa wakitrandikwa tu viboko halafu walikuwa hawawezi kuondoka eneo lile, yani hawawezi kwenda popote ila walikuwa wakipigwa tu hadi walianguka chini na kuzimia.
Ila walipokuja kushtuka kila mtu alikuwa nyumbani kwao, kila mmoja alitafakari na kukosa jibu ya kilichotokea siku hiyo.

Ndugu wa mama jack baada ya kumaliza kwa Yule mganga na kupewa dawa wakaamua sasa warudi nyumbani ili wapange mipango vizuri kwa kile walichoambiwa na mganga wao, walishangaa kufika nyumbani wakamkuta Yule aliyewakimbia kule kwa mganga na kabla hawajamuuliza chochote akawaambia,
“Kuna kitu nataka niwaonyeshe”
“Kitu gani?”
Kila mtu alikuwa na shauku ya kujua kuwa ni kitu gani ambacho alitaka kuwaonyesha, basi Yule kijana, alienda kumchukua dada yake ambaye alimuacha chumbani kwa muda, yani alivyofika ukumbini tu wote walianza kupiga kelele na wengine kukimbia kimbia mpaka pale alipowaita na kuwaambia kuwa wasiogope ila bado walishikwa na uoga wa hali ya juu ukizingatia ni mtu ambaye wamemzika miaka mitano iliyopita kwahiyo kitendo cha kumuona mzima kiliwaogopesha sana,
“Jamani msiogope, ni mzima kabisa huyu sema saivi kuongea ni mgumu ila ataongea tu”
“Tuambie imekuwaje kuwaje?”
Ikabidi huyu kijana awaeleze ukweli wa mambo ya jinsi ilivyokuwa kuanzia alivyowasiliana na Rose hadi alivyotaka kumuua na jinsi Yule binti alivyotokea.
“Huyo binti ni nani?”
“Hata mimi mwenyewe simjui ila anasema kuwa yeye ndiye aliyempeleka mama akatolewe kafara kwa madai kuwa mama alikuwa mchawi ndio kwa kunithibitishia kamtoa huyu dada yetu kuwa alichukuliwa msukule na mama”
Wote walishangaa na ilikuwa ngumu sana kuamini ingawa uwepo wa Yule dada uliwashangaza sana ila ilikuwa vigumu sana kwao kuamini kuwa mama Jack alikuwa mchawi, ikabidi Yule kijana awaletee na ile mifupa ambayo ilikutwa chumbani kwa mama yao.
“Kwahiyo na wewe unaamini kuwa mama alikuwa mchawi?”
“Siamini ila kuna vitu sivielewi”
“Kama huamini huenda hata huyu dada alichukuliwa msukule na huyo huyo rafiki wa mama, kesho tumpeleke kwa mganga, halafu tuendelee na mipango ya dawa tuliyotoka nayo kwa mganga”
“Hapana, mimi sitashiriki hizo dawa na wala huyu dada msimpeleke kwa huyo mganga”
“Kwahiyo tumpeleke wapi?”
“Yule mtu amekataa kabisa kuhusu swala la kumpeleka dada kwa mganga wala mimi kushiriki dawa mlizokuja nazo”
“Mbona unatuambia mambo ya ajabu wewe, kama ukikataa shauri yako ila dawa tutafanya tu, hakuna anayeamini kuwa ndugu yetu alikuwa mchawi na alimuuwa na kumfanya msukule huyu mwanae mpendwa, lazima mwanae alichukuliwa na huyo huyo mtu wa ajabu lazima twende tena kwa mganga”
Walikuwa wanaongea ila huku wana hofu nyingi sana kuhusu Yule dada aliyerudi maana wote walimshuhudia akizikwa, kwahiyo hofu waliyokuwa nayo ilikuwa kubwa sana kiasi kwamba wote waliaga na kuondoka wakijifanya wanarudi tena kwa mganga halafu pale nyumbani walimuacha Yule Yule kijana na ndugu yake aliyetoka kwenye usukule kwani wote walikuwa wanamuogopa.
 
SEHEMU YA 176

Neema alimpigia simu binti yake kuwa anarudi nyumbani muda gani kwa siku hiyo maana alishaongea na mama Pendo kwahiyo alitaka aongee na huyu binti yake ila binti yake alimshangaza sana kwani alimwambia kuwa kwa wiki hiyo atalala kwenye nyumba ya baba yake,
“Sasa wewe kwenye hiyo nyumba ya baba yako unamfata nani wakati baba yako hayupo?”
“Nawafata hawa watu wa huku nimezoeana nao sana, wananihitaji niwe karibu nao”
“Unajua unanipa mashaka wewe Salome”
“Mashaka ya nini?”
“Umeanza lini tabia ya kulala mbali na nyumbani?”
“Basi nitarudi”
“Utarudi muda gani?”
“Saa mbili usiku”
Kisha Salome akakata ile simu ila Neema alishukuru hata kwa huu muda aliyomwambia kwani alihitaji sana huyu binti yake hata akutane na mama Pendo ili nae ajaribu kumuhoji kidogo na kuona tofauti yake na kuangalia ni jinsi gani watamsaidia. Neema akampigia simu mama Pendo na kumuomba afike kwake saa mbili usiku, naye mama Pendo hakugoma bali alikubali kufanya vile.

Rose alitupwa getini kwake akiwa hajitambui kabisa, mlinzi akiwa anataka kutoka nje ili aende dukani akashangaa kumkuta bosi wake amelala chini na akiwa ameumia sana na ubaya zaidi hakujitambua, ikabidi mlinzi amuite Kulwa ambaye alikuja kisha wakaanza kusaidiana ili kumbeba wamuingize ndani ila alikuwa mzito sana kiasi kwamba aliwashinda kumbeba, Kulwa aliona ni vyema wakatafute msaada wa watu wengine wambebe kwakweli iliwashangaza sana kwa Yule mama kuwa mzito kisi kile, ila kabla Kulwa hajatoka kwenda kuomba msaada mara alifika Salome ila Kulwa alipomuona Salome ikamjia kumbukumbu ya Moza alivyowajia siku maa yao aliwaambia kuwa Salome ndiye Moza, kwahiyo kitendo cha kumuona tena Salome hapo kilimtia mashaka Kulwa na kujikuta akiacha kufanya chochote na kukimbilia ndani, mlinzi alikuwa anashangaa tu na kuuliza
“Mbona amekimbia?”
“Nikuulize wewe maana mimi ndio nimefika sasa hivi”
Mlinzi alitaka kwenda tena kumjuita Kulwa ila alipofika mlangoni, akageuka nyuma na kumkuta Salome kambeba mwenyewe Rose.
Mlinzi alishangaa sana ila kila alipozidi kumuangalia Salome akija na Rose ndani alimuona akibadilika na kuwa Moza.
 
SEHEMU YA 177

Mlinzi alitaka kwenda tena kumuita Kulwa ila alipofika mlangoni, akageuka nyuma na kumkuta Salome kambeba mwenyewe Rose.
Mlinzi alishangaa sana ila kila alipozidi kumuangalia Salome akija na Rose ndani alimuona akibadilika na kuwa Moza.Hofu ilitawala kwa mlinzi kiasi kwamba hakuweza kumuangalia tena na kujikuta akitimka mbio huku akipiga kelele, na alitimkia ndani akabamiza mlango akiendelea na kelele zake. Kulwa akamuona mlinzi mlangoni sebleni kwao akipiga kelele, akamuuliza kwa mshangao,
“Vipi wewe una mashetani?”
“Kuna makubwa huko nje”
Alikuwa anaongea huku akitetemeka,
“Makubwa gani?”
“Sijui, sijui kabisa”
“Sasa wewe mlinzi gani mama amekuweka muoga muoga hivyo? Sasa wewe ukiogopa kitu sisi tufanyeje? Hebu toka hapo mlangoni tuone kuna nini”
Doto nae alitoka ndani ili kuangalia zile kelele zilikuwa za kitu gani, Kulwa alimtoa Yule mlinzi kwa nguvu na kufungua mlango ila cha kushangaza hakuona chochote cha ajabu nje, akamuangalia mlinzi na kumwambia,
“Hivi wewe Lazaro una matatiozo gani, mbona hakuna chochote cha kuogopa nje? Yani wewe sio mlinzi sio chochote, mtu mwenyewe muoga tu”
Doto aliuliza kuwa kuna nini lakini Kulwa alimjibu kuwa ni mawenge tu ya mlinzi wao, sema Yule mlinzi alikuwa kimya kabisa kwani alipigwa na butwaa asijue ni imekuwaje kuwaje na kujisemea moyoni kuwa ile nyumba ni ya kuondoka huku akikumbuka kuwa alipoondoka alirudishwa kimazingara, alipofikiria hapo alikosa raha kabisa na kujikuta akikaa chini tu. Kulwa na Doto walibaki wakimshangaa na kuona kuwa anaanza kuchanganyikiwa.
Wakakaa nae pale sebleni huku wakimuangalia jinsi alivyotoa mimacho, mara kidogo wote wakashtuka baada ya kumuona mama yao yani Rose akitoka maeneo ya chumbani huku akipiga kelele ilionyesha kama alikuwa akitandikwa viboko na mtu ambaye haonekani ila kilichosikika ni sauti ya viboko nay eye akipiga kelele, swala hilo liliwachanganya sana mule ndani ukizingatia mama yao hakuwepo ndani, sasa imekuwaje akitoka chumbani tena akionekana anatandikwa viboko huku akilia kwa maumivu, wakajikuta wakikimbilia nje, ila Rose nea alikimbilia nje huku viboko vikiendelea kumchapa, wakajikuta wakikimbia hovyo hovyo kwani mama yao alitafuta msaada kwa yeyote aliyekuwa mbele yake, ila walipofika getini ili watoke nje kabisa walishangaa kuwa geti lilifungwa kitu hicho kiliwastaajabisha sana na kuwafanya waendelee kukimbia hovyohovyo, hadi mama yao akaanguka na kutulia huku ile sauti ya viboko nayo ikiwa imetulia.
 
SEHEMU YA 178


Neema aliona usiku umeingia ila mwanae hakuwa nyumbani na kumfanya ajiulize tena kuwa huyu mtoto ana nini kiasi kwamba anashindwa kurudi nyumbani kwa wakati, ila wakati anawaza hivyo akasikia mlango ukifunguliwa na Salome akiingia,
“Jamani wewe mtoto kwahiyo ndio saa hizi unarudi?”
“Mama jamani kwani kuna ubaya gani?”
“Wewe ni mtoto wa kike halafu unasema kuna ubaya gani!”
“Basi nisamehe mama”
“Mbona umekuwa mwepesi hivyo wa kuomba msamaha!”
“Kwahiyo mama ulitaka niendelee kubishana na wewe bila kukuomba msamaha!”
“Haya yaishe, kesho asubuhi mama Pendo anakuja kutufata twende kule kwenye maombi. Tafadhali kesho usiondoke”
“Sawa nipo, sitaenda popote kesho”
Kisha Salome akaelekea chumbani kwake, ila Neema alimuangalia sana mtoto wake huyu bila ya kummaliza kwani vitu vingi sana alikuwa kabadilika kiasi kwamba Neema alijikuta akipata mashaka, akainuka na kwenda chumbani kwake huku swala la kuombwa msamaha na Salome likimjia,
“Salome ni mgumu sana kuomba msamaha, au ndio kukua! Kama ndio kukua basin i vizuri maana kawa mtoto mzuri ingawa nina mashaka nae mmmh!”
Neema alijikuta akiwaza sana bila ya majibu, akatamani kumuuliza maswali kadhaa mtoto wake ilia one atamjibu nini, kwahiyo akainuka tena na kuongoza chumbani kwa Ssalome.
Alipofika alifungua mlango akijua kuwa Salome atakuwa amelala ila hakumkuta Salome kitandani,
“Kheee ametoka tena! Huyu mtoto jamani mbona ananitania. Yani arudi usiku na aondoke tena!”
Akarudishia ule mlango wa chumbani kwa Salome, na kumuangalia kila mahali mule ndani ila hakumkuta na kupata uhakika kuwa ni wazi Salome ametoroka nyumbani kwahiyo akaenda kukaa sebleni huku akisema atakaa hapo mpaka pale Salome atakaporejea, akainuka na kufunga mlango kabisa na funguo ili atakaporejea amsikie.
 
SEHEMU YA 179

Mishi akiwa na mume wake, leo alijipanga kumwambia mumewe kuwa ana mimba ila alikuwa na hofu kubwa sana ya kumwambia kuwa alibakwa, kwahiyo alianza kuongea nae kwa utaratibu,
“Kuna jambo nataka nikwambie”
Huku machozi yakimlengalenga hata mumewe akawa na mashaka kuwa ni jambo gani,
“Nini tena Mishi wangu jamani!”
“Mwenzio nina mimba”
“Wow, hilo ni jambo la kheri sana. Mungu amesikia kilio changu”
Yule mwanaume akamkumbatia Mishi kwa furaha, huku akimwambia ataje zawadi yoyote akamnunulie kwani ni kipindi kirefu sana amekuwa akitafuta mtoto kwahiyo swala la Mishi kupata mimba kwa kipindi kifupi hivyo kilimpa furaha ya ajabu.
“Sema zawadi utakayo nikakutafutie kesho mke wangu”
“Sitaki zawadi yoyote zaidi ya kunitunzia siri yangu”
“Siri! Siri gani tena”
“Sitaki watu wajue kama nina mimba mpaka pale itakapokuwa kubwa”
“Sasa hiyo ni siri ya kukusumbua akili mke wangu, usijali hakuna nitakayemwambia. Sema tu zawadi yoyote mke wangu”
Mumewe akamlazimisha sana aseme zawadi ikabidi tu Mishi aseme zawadi kisha mumewe akamuahidi kuwa kesho ataenda kumnunulia zawadi hiyo, mumewe alikuwa na furaha sana kiasi kwamba Mishi hakuweza kumwambia ukweli kuwa alibakwa kabla ya ndoa yao, na mimba aliyonayo ni matokeo ya kubakwa na sio sababu ya kuolewa.
Mishi akakubaliana na moyo wake kuwa hatomwambia ukweli wowote mume wake, ila gafla mumewe aliinuka na kwenda chumbani halafu Mishi nae alijisikia kutapika na kutoka nje.
Yani alipofika nje hali yote ya kutapika iliisha, kichefuchefu chote kiliisha kwani mbele yake alimuona Salome na kumfanya aogope sana,
“Unaogopa kwavile hutaki kumwambia ukweli mumeo. Mwambie ukweli mume wako uone kama mimi nitakufata tena”
“Kwani wewe ni binadamu wa kawaida?”
“Hilo halikuhusu kabisa kabisa, unachotakiwa kufanya ni kumwambia ukweli mumeo, mwambie kuwa una mimba ya kubakwa”
“Naogopa”
“Unaogopa nini? Unaogopa mimba ya kubakwa! Mbona wakati ulikuwa ukichanganya vijana wa watu hukuogopa? Umewaweka roho juu vijana wa watu wote wakikufikiria wewe, je wewe ndiye msichana mrembo pekee ulimwenguni? Mwambie ukweli mumeo, na ole wako uanze kumchanganya mumeo na vijana wengine nitakufundisha pia. Haya niambie mumeo utamwambia ukweli humwambii?”
“Nitamwambia”
“Tena umwambie leoleo, Yani unavyoingia ndani tu umwambie”
Mishi aliitikia kwa kichwa tu kuwa atafanya hivyo na akaona ni wazi kama asipofanya hivyo huyu mtu ataendelea kumsumbua sumbua, muda kidogo Salome aliondoka halafu mume wa Mishi nae alitoka pale nje ila Mishi alimdanganya kuwa alitoka kupunga upepo kidogo na kumtaka warudi tena ndani huku akijaribu tena kuongea nae,
“Kuna jambo nataka nikwambie sijui utanichukuliaje?”
“Jambo gani tena?”
Mishi alimueleza mumewe kwa kirefu kidogo ya jinsi alivyochanganya wale mapacha na jinsi alivyopewa laana na mdada aliyemkuta nyumbani kwa wale mapacha na jinsi alivyobakwa na kujikuta kuwa ana mimba,
“Mmmh tuseme hiyo mimba ni ya kubakwa?”
“Ndio”
“Na huyo binti anayekutokea tokea ni binti wa aina gani?”
“Nilimkuta tu nyumbani kwa wale mapacha na ndio akanipa laana hadi nikabakwa na akaja kuniambia kuwa nina mimba tayari”
“Mmmh hayo mambo sio ya kawaida, sasa kesho nitakupeleka mahali”
“Wapi?”
“Tulia tu, nitakupeleka mahali kesho maana hivyo vitu sio vya kawaida. Huyo binti ni jinni hilo, na laana ya majini sio ya kuichekelea, yani tutaenda mahali hata usijali usikute wala huna mimba”
Mishi alihisi tu anaambiwa na mumewe kuwa wataenda kwa mganga, ila kwa upande mwingine alifurahia kwani alijua ndio utakuwa mwisho wa Yule binti kumfatilia fatilia.
 
SEHEMU YA 180

Nyumbani kwa Rose, walisaidiana kumuingiza mama yao ndani, huku wakiwa na hofu kubwa na kutamani kuongea nae kuwa kulikoni,
“Mama pole sana, kitu gani kimekupata?”
Mama yao alikuwa kimya, na kuwafanya wagundue kuwa mama yao kaumia mdomoni ndiomana hawezi kuwajibu kitu chochote, walikaa nae pale sebleni ila kiukweli walikuwa na wasiwasi mkubwa sana, kwa wakati huo hata Yule mlinzi wao nae aliogopa kwenda kukaa getini, ilibidi wamuulize naye kwa makini,
“Uliona nini na wewe?”
“Nilimwona mama yupo chini akiwa hajitambui, nikawa nakuja ndani ili nikuite tukambebe ila kabla sijafika sijui kinini kikanishawishi kugeuka nyuma, mara nikamuona Salome akiwa kambeba mwenyewe mama wakati mimi nilimshindwa alikuwa ni mzito sana halafu kadri Yule Salome alivyokuwa akisogea alikuwa akibadilika na kuwa kama Mo…..”
Kulwa alimzuia mlinzi asiendelee kuongea,
“Ishia hapohapo tushakuelewa, usituletee makubwa bure. Usiku ushaingia sasa”
Doto akamuulizia Ana,
“Hivi na Ana yuko wapi?”
“Yupo chumbani kwake toka asubuhi, ila Yule mtoto anajijuaga mwenyewe”
Wakakubaliana kwa pamoja kuwa usiku huo walale wote sebleni hapo ukizingatia hata mlinzi alishagoma kulala kwenye lindo lake.

Palipokucha asubuhi waliamka ila mama yao hakuwa pale sebleni na wakahisi kuwa ameenda chumbani,
“Au mama aliamua kwenda kulala chumbani!”
“Jamani ningekuwa mimi nisingeweza yani kupigwa kote kule ila mama bado kaenda kulala chumbani! Kwakweli ningekuwa mimi nisingeweza jamani”
“Tumetofautiana mioyo, Lazaro kaona maajabu tu kaogopa kwenda kulala kwenye lindo lake”
“Ila inataka moyo nyie, yani haya mambo ni makubwa ila wenyewe tunayachukulia kawaida”
“Sio tunayachukulia kawaida ila hatuna cha kufanya, tukiondoka tunarudishwa unafikiri tutafanyaje”
Mlinzi ndio akashangaa hapa kuwa hata hawa nao wakiondoka wanarudishwa ila Doto akasema,
“Jamani mbona Sara kafanikiwa kuondoka na hajarudishwa?”
Ana akafika pale sebleni na kudakia zile habari za Sara,
“Jamani Sara sio kwamba ameondoka hapa nyumbani ila Sara kafungiwa na mama”
“Kafungiwa na mama!”
“Ndio kafungiwa na mama, yani mama ndiye mtu pekee wa kumtoa Sara. Hajatoroka wala nini, yupo humu humu ndani ila kafungiwa na mama”
Kulwa na Doto wakapata picha ya kile chumba ambacho Sara aliwahi kuwaonyesha na wakaganda huko, moja kwa moja wakajua kuwa ni chumba kile kile amabacho mama yao amemfungia Sara. Ila Ana alivyomaliza kuwaambia hayo aliondoka zake na kwenda jikoni kisha kwenda chumbani kwake.
Kulwa na Doto walitazamana kisha wakamwambia mlinzi,
“Inabidi ukatusaidie sasa”
“Sasa niwasaidie kufanyeje?”
“Kumtoa Sara”
“Tutamtoaje?”
“Twende tukakuonyeshe”
Walienda mpaka mlangoni mwa chumba kile na kuchukua fungua kisha kufungua na kuingia ndani ya kile chumba, halafu wakamwambia mlinzi,
“Umeona pale nyuma ya kabati kuna mlango mwingine, sasa ule mlango ndio yupo Sara. Nenda kaufungue umtoe”
“Kheee nyie vipi, kwanini msiende kufungua na kumtoa wenyewe!”
“Sisi haturuhusiwi”
“Na mimi siwezi”
Yule mlinzi akatoka nje ya kile chumba, ila alipopiga jicho pembeni akamuona mama mwenye nyumba yani Rose akija kule walipo huku amevaa kaniki.

ITAENDELEA
 
mmh! ngoma nzito...

Ila Rose analo...maana hapo lazima awafungue mateka..hii ni shida kwake na ataadhirika... labda yule Salome Moza ..akaombewe..nguvu zimtoke!

Kila mtu hapo naona analipwa uovu wake..
SIMULIZI INAELEKEA UKINGONI [emoji91] [emoji91] ...... WEKA UTABIRI WAKO..
TUKUTANE SAA 3 USIKU !!
 
SEHEMU YA 181

Neema aliamka pale sebleni kwahiyo siku hiyo alilala pale sebleni huku ameshika funguo, alipoamka akakumbuka matukio vivuri sana,
“Yani huyu mtoto hajarudi mpaka muda huu!”
Akainuka na kwenda kuchungulia tena chumbani kwa Salome, akashangaa kwani alimkuta amelala, akaangalia ufunguo wake mkononi ambao ulikuwa vilevile alivyoushikilia toka mwanzo, hilo swala lilimfanya ashikwe na hofu huku akijiuliza,
“Amepitia wapi huyu mtoto wakati milango yote nilikuwa nimefunga?”
Akatoka haraka chumbani kwa Salome huku uoga mwingi ukimjaa, mara akasikia mlango wa sebleni ukigongwa na kuhisi kuwa huenda ni mama Pendo amefika ingawa alishangaa kuwa mbona ni mapema mno, akaenda kufungua na kushangaa ni Salome ndio alikuwa amerudi.


Akatoka haraka chumbani kwa Salome huku uoga mwingi ukimjaa, mara akasikia mlango wa sebleni ukigongwa na kuhisi kuwa huenda ni mama Pendo amefika ingawa alishangaa kuwa mbona ni mapema mno, akaenda kufungua na kushangaa ni Salome ndio alikuwa amerudi.
Neema alishindwa kabisa kuvumilia na kujikuta akipiga kelele kwa uoga aliokuwa nao kwani kilikuwa ni kitu cha ajabu sana machoni pake, ila Salome alimuuliza
“Vipi mama mbona hivyo?”
Alikuwa akiongea huku akimsogelea ila Neema aliendelea kupiga kelele huku akisema,
“Usinisogelee, usinisogelee kabisa. Wewe ni nani?”
“Jamani mama imekuwaje tena? Mimi si mwanao Salome?”
“Hapana”
Neema alikimbia na kuelekea chumbani kwake, yani leo hata kuwaamsha wale wanae kwaajili ya shule hakufanya hivyo, kisha Yule Salome nae alielekea chumbani kwake.
Neema akiwa chumbani kwake akachukua simu na kumpigia simu mama Pendo huku akihema sana ila simu ya mama Pendo haikupatikana hewani na kuzidi kumchanganya, ikabidi amtumie ujumbe mfupi ili akiwasha tu simu basi apate ule ujumbe, alikuwa na mashaka sana ila baada ya muda kidogo akashikwa na usingizi na kulala.

Mlinzi alipomuona Rose akija halafu amevaa kaniki akaogopa sana kwani ni wazi ilionekana uchawi wake bila chenga, mlinzi alimuangalia kwa hofu kubwa sana huku uoga ukimtawala na kusema kuwa akimbie au afanye nini ila cha kushangaza Rose alimpita Yule mlinzi kama hamuoni kisha akaingia kwenye kile chumba ambamo walikuwemo Kulwa na Doto ila nao walishangaa kumuona mama yao akiwa amevaa kaniki ambapo aliwapita nao kama hawaoni vile, kitendo kile kiliwashangaza sana wakabaki wakiangaliana ila hawakuondoka kwani walitaka kujua kuwa mama yao ameenda kufanya nini.
Wakamuona akikaa chini kisha kuita vitu vilivyokuja kama dawa, halafu akapuliza ambapo kabati lile lilisogea halafu ule mlango wa kile chumba ulifunguka, Kulwa na Doto walishangaa sana na kujikuta wakitaka kusogea zaidi kwenye kile chumba ili kuona kuna nini ndani yake, ila kabla hawajasogea alikuja Ana kwa haraka sana na kuwashika mikono kisha akawatoa nje kinguvu na kuwaambia,
“Nyie msithubutu kusogelea”
“Kwanini?”
“Tuondokeni”
Akawavuta kaka zake mikono hadi sebleni ambapo Yule mlinzi nae alifata nyuma,
“Mmemuona pale mama sio akili zake zile, kashapandwa na kinyamkera yani anaweza akafanya kitu chochote pale bila kutarajia. Msishangae hajawaona, ila nyie mmemuona sababu kuna dawa iliwekwa leo na mtu anaetikisa nyumba hii. Subirini mama akitoka akiwa na akili zake timamu, tumwambie ya kuwa wote tumemuona alichokuwa anafanya, ila kitendo cha nyie kutaka kuingia kule kitawamaliza”
“Hatukuelewi”
“Nieleweni tu, mnajua Sara yuko wapi? Nadhani mnajua kuwa Sara amepotea kwenye mazingira ya kutatanisha, mnajua kapotea vipi? Je mama alitaka kumpoteza na Sara? Hapana, hata yeye kitendo cha kupotea Sara kinamuuma sana, ila kitendo cha kuachia watu kwenye chumba hiko kinamshinda sababu kitayagharimu maisha yake, ila tunatakiwa kusimama pamoja. Mama akiwa tu na akili zake timamu yani kinyamkera kikimtoka tumwambie ukweli kuwa tumemuona halafu akibisha nitawaambia cha kufanya”
“Kwanini usituambie kabisa maana mama kubisha ni lazima”
“Sitakiwi kuwaambia sasa hivi ila nyie jueni kuwa nipo upande wenu”
Walitulia wakimsikiliza Ana kwani waliamini kuwa Ana anajua mambo mengi kupita wao, ila mlinzi akawaambia jambo,
“Jamani zamani nilipokuwa mtoto nilikuwa napelekwa kanisani, na nilifundishwa kuwa vitu vya ajabu vikitokea yatupasa kufanya sala ila toka nianze kazi kwenye nyumba hii sijawahi kuwaona mkienda kanisani wala msikitini, tuseme nyie hamna dini?”
Ana akamjibu,
“Hebu tutolee habari zako na wewe, mbona wewe huendagi Kanisani wala Msikitini tuseme na wewe huna dini au? Badala ya kuangalia jinsi gani tutapambana na haya mambo kwenye nyumba yetu unatuletea habari za makanisa hapa”
Yule mlinzi ilibidi tu awe kimya kwani hakuweza kuendelea kubishana na vitu ambavyo hata yeye mwenyewe alikuwa havijui.
 
Back
Top Bottom