SEHEMU YA 181
Neema aliamka pale sebleni kwahiyo siku hiyo alilala pale sebleni huku ameshika funguo, alipoamka akakumbuka matukio vivuri sana,
“Yani huyu mtoto hajarudi mpaka muda huu!”
Akainuka na kwenda kuchungulia tena chumbani kwa Salome, akashangaa kwani alimkuta amelala, akaangalia ufunguo wake mkononi ambao ulikuwa vilevile alivyoushikilia toka mwanzo, hilo swala lilimfanya ashikwe na hofu huku akijiuliza,
“Amepitia wapi huyu mtoto wakati milango yote nilikuwa nimefunga?”
Akatoka haraka chumbani kwa Salome huku uoga mwingi ukimjaa, mara akasikia mlango wa sebleni ukigongwa na kuhisi kuwa huenda ni mama Pendo amefika ingawa alishangaa kuwa mbona ni mapema mno, akaenda kufungua na kushangaa ni Salome ndio alikuwa amerudi.
Akatoka haraka chumbani kwa Salome huku uoga mwingi ukimjaa, mara akasikia mlango wa sebleni ukigongwa na kuhisi kuwa huenda ni mama Pendo amefika ingawa alishangaa kuwa mbona ni mapema mno, akaenda kufungua na kushangaa ni Salome ndio alikuwa amerudi.
Neema alishindwa kabisa kuvumilia na kujikuta akipiga kelele kwa uoga aliokuwa nao kwani kilikuwa ni kitu cha ajabu sana machoni pake, ila Salome alimuuliza
“Vipi mama mbona hivyo?”
Alikuwa akiongea huku akimsogelea ila Neema aliendelea kupiga kelele huku akisema,
“Usinisogelee, usinisogelee kabisa. Wewe ni nani?”
“Jamani mama imekuwaje tena? Mimi si mwanao Salome?”
“Hapana”
Neema alikimbia na kuelekea chumbani kwake, yani leo hata kuwaamsha wale wanae kwaajili ya shule hakufanya hivyo, kisha Yule Salome nae alielekea chumbani kwake.
Neema akiwa chumbani kwake akachukua simu na kumpigia simu mama Pendo huku akihema sana ila simu ya mama Pendo haikupatikana hewani na kuzidi kumchanganya, ikabidi amtumie ujumbe mfupi ili akiwasha tu simu basi apate ule ujumbe, alikuwa na mashaka sana ila baada ya muda kidogo akashikwa na usingizi na kulala.
Mlinzi alipomuona Rose akija halafu amevaa kaniki akaogopa sana kwani ni wazi ilionekana uchawi wake bila chenga, mlinzi alimuangalia kwa hofu kubwa sana huku uoga ukimtawala na kusema kuwa akimbie au afanye nini ila cha kushangaza Rose alimpita Yule mlinzi kama hamuoni kisha akaingia kwenye kile chumba ambamo walikuwemo Kulwa na Doto ila nao walishangaa kumuona mama yao akiwa amevaa kaniki ambapo aliwapita nao kama hawaoni vile, kitendo kile kiliwashangaza sana wakabaki wakiangaliana ila hawakuondoka kwani walitaka kujua kuwa mama yao ameenda kufanya nini.
Wakamuona akikaa chini kisha kuita vitu vilivyokuja kama dawa, halafu akapuliza ambapo kabati lile lilisogea halafu ule mlango wa kile chumba ulifunguka, Kulwa na Doto walishangaa sana na kujikuta wakitaka kusogea zaidi kwenye kile chumba ili kuona kuna nini ndani yake, ila kabla hawajasogea alikuja Ana kwa haraka sana na kuwashika mikono kisha akawatoa nje kinguvu na kuwaambia,
“Nyie msithubutu kusogelea”
“Kwanini?”
“Tuondokeni”
Akawavuta kaka zake mikono hadi sebleni ambapo Yule mlinzi nae alifata nyuma,
“Mmemuona pale mama sio akili zake zile, kashapandwa na kinyamkera yani anaweza akafanya kitu chochote pale bila kutarajia. Msishangae hajawaona, ila nyie mmemuona sababu kuna dawa iliwekwa leo na mtu anaetikisa nyumba hii. Subirini mama akitoka akiwa na akili zake timamu, tumwambie ya kuwa wote tumemuona alichokuwa anafanya, ila kitendo cha nyie kutaka kuingia kule kitawamaliza”
“Hatukuelewi”
“Nieleweni tu, mnajua Sara yuko wapi? Nadhani mnajua kuwa Sara amepotea kwenye mazingira ya kutatanisha, mnajua kapotea vipi? Je mama alitaka kumpoteza na Sara? Hapana, hata yeye kitendo cha kupotea Sara kinamuuma sana, ila kitendo cha kuachia watu kwenye chumba hiko kinamshinda sababu kitayagharimu maisha yake, ila tunatakiwa kusimama pamoja. Mama akiwa tu na akili zake timamu yani kinyamkera kikimtoka tumwambie ukweli kuwa tumemuona halafu akibisha nitawaambia cha kufanya”
“Kwanini usituambie kabisa maana mama kubisha ni lazima”
“Sitakiwi kuwaambia sasa hivi ila nyie jueni kuwa nipo upande wenu”
Walitulia wakimsikiliza Ana kwani waliamini kuwa Ana anajua mambo mengi kupita wao, ila mlinzi akawaambia jambo,
“Jamani zamani nilipokuwa mtoto nilikuwa napelekwa kanisani, na nilifundishwa kuwa vitu vya ajabu vikitokea yatupasa kufanya sala ila toka nianze kazi kwenye nyumba hii sijawahi kuwaona mkienda kanisani wala msikitini, tuseme nyie hamna dini?”
Ana akamjibu,
“Hebu tutolee habari zako na wewe, mbona wewe huendagi Kanisani wala Msikitini tuseme na wewe huna dini au? Badala ya kuangalia jinsi gani tutapambana na haya mambo kwenye nyumba yetu unatuletea habari za makanisa hapa”
Yule mlinzi ilibidi tu awe kimya kwani hakuweza kuendelea kubishana na vitu ambavyo hata yeye mwenyewe alikuwa havijui.