Simulizi: Kurudi Kwa Moza

Simulizi: Kurudi Kwa Moza

SEHEMU YA 182



Neema alipoamka alijikuta kasahau kila kitu hata kuhusu kutokuwaamsha wanae waende shule alikuwa amesahau huku akijua kuwa alishawaamsha wakaenda shule na yeye akarudi kulala, kwahiyo muda huu alioga na kujiweka sawa kisha kuanza kuandaa kifungua kinywa huku akisema kuwa yani Salome ametoka bila ya kumuaga, wakati anaandaa chai sebleni akakuta barua mezani kwake ikiwa imeandikwa kwa maneno machache tu,
“Kwako mama mpendwa, mimi naenda kuishi kwenye ile nyumba aliyokuwa akiishi baba yangu, nina maana yangu ya kufanya hivi. Nitarudi nikiwa nimekamilika. Kwaheri, ni mimi mtoto wako mpendwa Salome”
Neema alishangaa sana kwa uamuzi huo uliochukuliwa na Salome,
“Ataendaje kuishi kwenye nyumba ambayo hata baba yake hayupo, si ndio watamuua huko jamani? Kwanini kaamua kufanya hivi Salome?”
Halafu sasa akagundua kuwa hiyo sehemu wala haijui sababu hajawahi kufika zaidi ya siku waliyoenda kwenye msiba wa Moza na waliishia katikati sababu walikuta ndio wanaenda kuzika kwahiyo swala la yeye kufika nyumbani kwa Rose lilikuwa ni gumu sana, akaamua kunywa chai kwanza kisha kuchukua maamuzi mengine. Alipomaliza kunywa chai aligundua kuwa lile karatasi lenye ujumbe lilimwagikiwa na chai hivyo akachukua maamuzi ya kulitoa pamoja na vyombo vichafu kisha akaenda kulidumbukiza chooni. Kisha alienda kuchukua simu yake na kukaa sebleni ili ampigie Patrick na kumpa hiyo habari ila alipochukua alikutana na ujumbe kutoka kwa mama Pendo,
“Pole sana kwa maswahibu hayo ndugu yangu, ambayo kiuhalisia naona kama ni kiini macho kwakweli ila leo nitakuja na mchungaji hapo kwako. Mwambie mwanao asitoke, tunakuja kufanya maombi”
Neema alikuwa akishangaa huu ujumbe kutoka kwa mama Pendo kwani hata yeye hakuwa na kumbukumbu kuwa ni maswahibu gani aliyokuwa amemueleza mama Pendo,
“Kwani mama Pendo anaongelea kuhusu maswahibu gani jamani, kwani kuna maswahibu yoyote yamenipata au kaoteshwa huyu?”
Alijiuliza bila ya jibu sababu hakuwa na kumbukumbu ya aina yoyote ile kichwani mwake yani hata swala la kukumbuka kuwa alimkuta Salome amelala na gafla akamkuta mlangoni akigonga mlango haikuwepo hiyo kumbukumbu katika akili yake kabisa.

Kama ambavyo Mishi aliahidiwa na mumewe kwahiyo asubuhi asubuhi waliondoka na kwenda kwa mtaalamu lengo lilikuwa ni kuangaliziwa kuhusu huyo binti halafu na kuangaliziwa kuhusu mimba aliyokuwa nayo Mishi, walimkuta mganga na wateja wachache tu na walipoisha waliingia wao na kuanza kumuelezea matatizo yao,
“Yani cha kuwaambia tu huyo mtu ambaye mmeleta malalamiko yenu hapa, yupo nje anawasubiri”
“Anatusubiri!”
Walishtuka sana,
“Ndio anawasubiria”
“Sasa tutafanya nini?”
“Sio mtu mzuri Yule, ila yupo kwaajili ya kumkomesha mtu mmoja tu sema ukijiingiza kwenye familia hiyo imekula kwako kwahiyo na nyie swala la kuja kwangu ili niwasaidie itakula kwangu na kwenu”
“Tusaidie mganga, mi sioni kama mimba hiyo ina ukweli kwa mke wangu”
“Laiti kama mkeo akitoa hiyo mimba kaa ukijua kuwa si wewe wala mkeo utaweza tena kuwa na watoto katika maisha yenu. Mkeo alikuwa na makosa ndiomana akapewa hiyo adhabu”
“Makosa gani?”
Mishi alianza kuona aibu kwani hakumwambia ukweli mume wake kuhusu makosa yake mpaka kufikia hatua ya kubakwa ila alimwambia tu kuna vijana mapacha walidhania kuwa anawachanganya ndio huyo mtu akampa laana hiyo, basi Yule mganga akamuangalia Mishi na kumuuliza,
“Je nimwambie kuhusu makosa yako?”
Mishi alitikisa kichwa kwa ishara kuwa asimwambie, ila Yule mganga aliendelea,
“Hata nisipomwambia, ilimradi anawasuburia nje, basi napo atamwambia tu. Bora nimwambie mimi”
Mume wa Mishi akamuomba mganga amwambie maana alihisi kufichwa mambo mengine, ila Mishi aliona aibu sana na kuinuka kisha akatoka nje, ila mumewe bado alikomaa kuwa aambiwe, Yule mganga aligoma kusema sababu muhusika kainuka,
“Yani mimi kusema siwezi maana mwenyewe kainuka lakini mfate tu mtaonana na Yule mtu na atakwambia ukweli maana hatakuficha lolote”
Ikabidi mume wa Mishi ainuke tu ili amfate mkewe nje maana mkewe alishatoka eneo hilo, ila alipofika alipo mkewe alishangaa kumuona mkewe kasimama na binti Fulani ambaye yeye hakumjua binti huyo, ikabidi awafate ila huyu binti kabla hata ya salamu alianza kumwambia mume wa Mishi,
“Mkeo nimempa adhabu hiyo sababu amekuwa akiumiza moyo wa wenzie sana, bora angekuwa anajiuza tungejua moja kuliko alichokuwa anafanya huyu. Yani anakuwa na wanaume zaidi ya watano kwa wakati mmoja halafu wote anawadanganya kuwa anawapenda, je ni nafasi za mabinti wangapi anaziziba ambao wangependwa na hao wanaume? Ile familia aliumiza mioyo ya watu watatu, sasa ni zamu yake nay eye kuumia moyo. Kuhusu wanaume wengine aliokuwa nao atakwambia mwenyewe, huyu mkeo ni zaidi ya wanawake wanaojiuza ila nimemwambia akithubutu kufanya hivyo na kwenye ndoa yenu nitamkomesha”
Kisha Salome akaondoka na kuwaacha, Mishi alikuwa na aibu sana. Mumewe akamuangalia kwa jicho la gadhabu na kumwambia,
“Kumbe nimeoa changudoa, mwenyewe nilijisifu kuwa mwanamke anamsimamo hataki nimuoe ananipima kwanza kumbe ni changudoa. Kwakweli Mishi umeniangusha sana, yani unajua uovu ulikuwa unautenda nab ado bila ya aibu unataka tuje kwa mganga wa kienyeji ulidhani afanyeje sasa na wakati una laana? Unafikiri machozi ya watu wote uliowaliza yameenda bure? Tena uwe mpole kabisa maana ukileta kidomo domo chako nitawaeleza ndugu zako wote ukweli kuwa ulibakwa”
Mume wa Mishi akaondoka zake ikabidi Mishi amfate nyuma huku aibu tele ikimshika moyoni kwani hakutegemea kama angeaibika kwa kiasi hicho, alikuwa akitembea kwa aibu tele tele usoni.
 
SEHEMU YA 183

Nyumbani kwa Neema alifika mama Pendo na mwanaume mmoja na wanawake wengine wawili ambao mama Pendo aliwatambulisha kwa Neema kuwa ni wana maombi, ambapo Neema aliwakaribisha vizuri sana na baada ya salamu za hapa na pale mama Pendo sasa akamwambia Neema,
“Hebu sasa elezea vizuri ili hawa watu nao wakusikie kuwa ilikuwaje jana usiku”
“Ilikuwaje kivipi?”
“Si kama vile ulivyonielezea kwenye ujumbe,hebu jaribu kuelezea vizuri”
“Ujumbe gani?”
“Kheee wewe Neema vipi tena una matatizo gani?”
Ikabidi mama Pendo achukue simu yake na kujaribu kusoma ambacho aliandika Neema ili Neema ajue hata anazungumzia nini,
“Ndugu yangu nina matatizo, nakutafuta hewani hupatikani. Mwanangu jana hakuwepo nyumabni nikafunga milango yote cha kushangaza asubuhi nimekuta chumbani kwake halafu gafla mlango uligongwa halafu aliingia yeye ndani kwakweli hiyo kitu imeniogopesha sana, naomba mnisaidie maombi nipo njiapanda”
Ila bado Neema alionekana kushangaa kanakwamba hata haelewi kinachosomwa au kuzungumzwa kisha akamwambia mama Pendo,
“Unajua hata nimeshangaa ujumbe ambao umenitumia ukinipa pole, nikajiuliza pole ya nini tena. Yani sikumbuki kabisa kama nilikuandikia hiyo meseji na wala sikumbuki kama kuna jambo kama hilo lilitokea”
“Kwahiyo wewe unakumbuka nini?”
“Nakumbuka kuwa usiku ulifika nikalala, na kuamka asubuhi nikakuta ujumbe wako hata sielewi kama nilikutumia ujumbe”
Wale watu wengine wakawa wanamshangaa Neema kama ambavyo yeye alikuwa akiwashangaa wao, ikabidi wamuulize swali,
“Kwani huyo binti yako yuko wapi?”
“Yani kuhusu binti yangu alipo, nimekuta tu ujumbe wake leo kuwa ameondoka anaenda kuishi nyumbani kwa baba yake yani hajaniaga kwa mdomo ila kaniachia ujumbe huo tu”
“Ujumbe wenyewe uko wapi?”
“Kwa bahati mbaya kile kikaratsi nimekitupia chooni maana kiliingia chai”
“Basi kalete nguo ya mwanao ili tuiombee halafu akija umpe aivae”
“Sawa, ngoja nikalete”
Neem aliinuka na kwenda chumbani kwa Salome, akafungua na kushangaa sana kwani kule chumbani palikuwa na kitanda na godoro tu, vitu vyote vya Salome havikuwepo yani nguo zake zote hata begi lake dogo halikuwepo yani Salome alikuwa kahama mazima kabisa.
Alipigwa na butwaa haswaa akarudi sebleni akiwa amenyong’onyea vilivyo ikabidi wamuulize kuwa imekuwaje tena,
“Eti mwanangu kaondoka na kabeba nguo zote”
“Halafu wewe hujui?”
“Ndio nilikuwa sijui, si ndio ujumbe tu nimekuta ameniandikia”
“Ila Neema nilikwambia mapema kabisa kuwa mwanao kutakuwa na tatizo sio swala la kawaida, kwanza mtoto akatae shule, halafu awe anatenda vitu vya ajabu lazima kuna kitu”
Yule mwanaume waliyeenda nae akasema,
“Kuna kitu kweli, tena sio cha kawaida kabisa. Naomba tuondoke tu halafu tufunge juu ya jambo hili, na wewe mama mtu ufunge”
“Mmmh kufunga tena jamani, kwani haiwezekani kuomba tu bila kufunga?”
“Hata kwenye biblia kwenye Mathayo 17:12 inasema (lakini namna hii haitoki, ila kwa kusali na kufunga). Ikimaanisha kuwa kuna maombi mengine tunatakiwa kufunga na kuomba”
“Jamani, sasa si mtafunga nyie tu wana maombi mpaka mimi nifunge jamani!”
“Hata wewe ni mwana maombi Neema”
“Ila kufunga siwezi mwenzenu yani njaa itanisumbuaje, siwezi kwakweli”
Ilibidi mpaka mama Pendo acheke maana Neema alivyotia huruma kwa kigezo cha njaa ni balaa, yani alionyesha wazi kuwa hilo swala linaloitwa kufunga kwake ni mtihani mzito.
“Yani wewe Neema itabidi nije nikupe somo kwakweli, kufunga ni kuzuri kunatuweka karibu na Mungu na pia tunasaidia miili yetu wenyewe. Yani wewe huwezi kuacha kula kwa masaa machache tu jamani kwaajili ya kujiponya mwenyewe! Natakiwa nikupe somo kwakweli”
“Basi mimi naomba tu mfanye maombi kwaajili ya mwanangu, swala la kufunga nitajifunza taratibu taratibu. Mwenzenu njaa jamani yani kufunga siwezi kabisa, ikifika saa tano tu asubuhi nahisi njaa balaa, sasa kufika hadi jioni si mtaniua mwenzenu jamani. Nawaomba tu mmuombee mwanangu”
Hawa walimuona huyu mama kuna vitu vimemfunga katika maisha yake ikabidi wakubali kuwa wao ndio wabebe dhamana hiyo, kisha Neema akawaomba wafanye maombi kwenye nyumba yake kwanza kabla ya kuondoka.

 
SEHEMU YA 184


Kulwa, Doto, na Yule mlinzi walikuwa sebleni muda huu, mara mama yao nae alitoka ikionekana kashamaliza kazi yake kwenye kile chumba chake cha siri, alipofika tu sebleni kabla hata ya salamu Kulwa alianza kumwambia mama yake,
“Mama tumeona yote uliyokuwa unayafanya, mama kuwa na huruma japo kidogo. Sara ni mtoto wako tunamuhitaji Sara”
“Sasa kwani Sara mi nimpeleke wapi?”
“Mama, usitugeleshe. Tunajua fika kuwa Sara umemfungia kwenye chumba cahko cha siri na watu wengine. Tunamtaka Sara mama”
“Nyie watoto, mimi ni mama yenu mjue. Msiniletee habari ambazo hamna ushahidi nazo”
Rose akawa akielekea mlangoni ila alivyofungua mlango tu alianza kupiga kelele huku akirudi kwa nyuma,
“Moza amerudi, Moza amerudi, Moza amerudi”
Watoto wake wakashikwa na hofu ya hali ya juu huku kila mmoja akiogopa, ila wakasikia hatua za mtu akiingia ndani.


Rose akawa akielekea mlangoni ila alivyofungua mlango tu alianza kupiga kelele huku akirudi kwa nyuma,
“Moza amerudi, Moza amerudi, Moza amerudi”
Watoto wake wakashikwa na hofu ya hali ya juu huku kila mmoja akiogopa, ila wakasikia hatua za mtu akiingia ndani.
Hakuna aliyeona kuwa kuna yeyote akiingia ndani zaidi ya zile hatua tu, Rose nae alikuwa ameganda vilevile mlangoni na baada ya muda akaanguka na kuzimia ikabidi wamsogelee na kuanza kumpepea.
Baada ya muda alizinduka na swali la kwanza alilowauliza wanae,
“Moza yuko wapi?”
“Unaongelea nini mama?”
“Mwambieni Moza simuogopi, ananitisha sana ila simuogopi. Niitieni Moza hapa”
Walimshangaa mama yao na kuona amechanganyikiwa kwli, ni kweli kulikuwa na hisia kuwa anayewasumbua humo ndani ni Moza na hata amewahi kuwatokea na kuwatahadhalisha kuwa wasihame nyumba yao ila kwa siku hiyo ya kuwa Moza yupo ndani kwao hawakuwa na uhakika kwahiyo waliona mama yao anaongea kama mtu aliyechanganyikiwa. Ila Rose aliendelea kuongea akidai kuwa aitiwe Moza,
“Kamuiteni Moza huko”
“Tukamuitie wapi mama?”
“Nendeni chumbani kwake mkamuite”
“Mmmh mama jamani, kule chumbani kwake labda uende wewe mwenyewe si umesema kuwa humuogopi kwasasa basi nenda”
“Sijaamua tu kwenda ila simuogopi, ananichezea sana akili zangu tangu amerudi, nimejipanga kwa mapambano simuogopi”
Mara kimya kikatawala ndani yani hakuna aliyeongea chochote kile halafu Rose alionekana kuanza kuogopa jambo Fulani sababu alikuwa akisikika yeye tu huku akisema,
“Nisamehe tafadhali nisamehe, naomba unisamehe nitawaachia. Unaniumiza nisamehe tafadhali”
Walizidi kuona kuwa mama yao anachanganyikiwa sasa, na gafla akazimia tena. Ila muda huu wakapata wazo kuwa wambebe na wampeleke chumbani kwake wakamlaze, ila Kulwa alitoa wazo lingine,
“Hivi kwanini tusimbebe na kumpeleka chumbani alikokuwa analala Moza maana mama inaonyesha anakisasi na huyo mtu, kwahiyo ni vyema tukimpeleka huko ili akishtuka na kujikuta huko atamalizana nae.”
Wakajikuta kwa pamoja wakikubaliana swala la kumbeba na kumpeleka chumbani kwa Moza.
 
SEHEMU YA 185



Nyumbani kwa Neema waliamua kufanya maombi kwa kifupi sana kisha kuagana na Neema halafu wao wakaondoka ila mama Pendo alibaki kidogo na Neema akizungumza nae,
“Ndugu yangu jitahidi hata kwa siku moja tu ujinyime kula na ufunge, tesa tumbo lako kwa siku hata moja upate majibu ya kile unachokihitaji”
“Inamaana mfungo wa siku moja unatosha?”
“Unatosha ndio ila ni muhimu kufunga kwa siku nyingine zaidi, kufunga sio kazi kama
unavyodhani ndugu yangu. Tusijiendekeze na kula, tunatakiwa kuwa kwenye mfungo ili kuwa karibu zaidi na Mungu wetu, Neema jitahidi utaweza. Unadhani ni jambo la kawaida hilo? Mtoto hataki shule, wewe mwenyewe unafanya vitu na kusahau. Haya sasa mtoto kahama nyumbani, yani bado tu huoni kama sio kitu cha kawaida hicho? Hiyo hali sio ya kawaida kabisa ndugu yangu, tunatakiwa kukazana na maombi tu”
“Sawa nitajitahidi basi ndugu yangu”
Basi mama Pendo alijaribu kumshawishi pale halafu aliondoka. Muda kidogo walirudi wale mapacha wa Neema, na kumsalimia mama yao, ikabidi awaulize maswali mawili matatu,
“HIvi leo nani aliwaamsha kwenda shule?”
“Ni dada ndio alituamsha na kutusaidia kujiandaa leo”
“Jana je!”
“Jana pia ni dada ndio alituamsha”
Neema akawa kimya kwa muda na kuwauliza tena watoto wake,
“Je kuna kitu chochote ambacho hamkielewi kuhusu dada yenu?”
“Hakuna kitu mama, ila mimi toka siku ambayo mamdogo Ashura kaanguka halafu dada akasema kuwa walikuwa wanacheza, na siku hiyo hiyo tukahamia hapa halafu dada akasema kuwa mamdogo Ashura kasafiri basi sijawahi kumuelewa dada tangia hapo”
“Kwanini huwa humuelewi?”
“Simuelewi tu, zamani alikuwa anakuja mara kwa mara chumbani kwetu na alikuwa akipenda kutuhadithia hadithi ila nakumbuka toka siku umerudi nae na kumkuta amelala chumbani kwetu halafu ukamwambia kuwa ni chumbani kwetu basi hajawahi tena kuja kutubembeleza kama zamani”
“Mmmh mnanifungua macho kwa kiasi fuylani, mnajua dada yenu kahama hapa nyumbani, kasema atarudi hadi akimaliza mambo yake”
“Halafu kuna jirani yetu mmoja wa kule niliwahi kumsikia akimwambia dada kuwa mbona sio Salome waliyemzoea”
“Kwahiyo nyie mnahisi ni nini?”
“Sijui labda dada kabadilika siku hizi”
Akawaruhusu tu watoto wake waendelee na mambo mengine maana kichwa chake kwa wakati huo kilikuwa kibovu kabisa maana kila alichofikiria alikosa jibu, mwishowe aliinuka tena na kwenda kwenye chumba alichokuwa akilala Salome, alikiangalia kile chumba na kuangalia kitanda vizuri ila haikuwepo nguo yoyote ya Salome, wakati anaangalia angalia chumba cha Salome kuna ujumbe mfupi alisikia ukiingia kwenye simu yake, akafungua na kuusoma,
“Mama, nimeondoka nyumbani ndio ila sio vizuri kwa wewe kuchunguza chunguza chumba changu”
Neema aliangalia kushoto na kulia kisha akatoka kwenye kile chumba cha Salome akiwa na wasiwasi kidogo kuwa huyu mtoto amejuaje kuwa atakuwa anachunguza chumba chake,
“Mmmmh labda amehisi tu, sijui”
Aliamua kwenda chumbani kwake maana alihisi kutokuelewa elewa baadhi ya mambo.
 
SEHEMU YA 186



Walisaidiana kumbeba Rose na kwenda kumlaza chumbani kwa Moza kama ambavyo walikuwa wamekubaliana, walimlaza kwenye kitanda cha Moza na kutoka kuelekea sebleni, ila kila mmoja hakujua ni kwanini walipata lile wazo la kwenda kumlaza mama yao kwenye chumba cha Moza.
Wakati wamerudi sebleni alifika Ana na kuwauliza kuhusu mama yao,
“Mama bado hajatoka ndani?”
Wakamuelezea ilivyokuwa hadi kufikia hatua ya kumpeleka mama yao kwenye chumba alichokuwa analala Moza,
“Kheee nyie mna akili kweli?”
“Kwanini tena?”
“Yani nyie ni zero kabisa, kumbukeni Moza alikufa na kifo chake kimekuwa na utata mkubwa sana. Nyumba yetu imekuwa ikigubikwa na mambo ya ajabu kila leo, halafu kuna siku tulisikia kabisa sauti ya Moza ikiongea na kusema kuwa tukihama tutarudishwa, halafu nyie bila hata ya huruma mnathubutu kwenda kumuweka mama chumbani kwa Moza akiwa amezimia? Hivi mama Yule mnampenda au? Mama ni mama hata akiwa mchawi bado ni mama, kumbuka ametuzaa na kutulea, na asingeweza kututoa kafara tulipokuwa watoto, kitendo cha mama kutuacha hadi leo inamaana anatupenda sana, hivi nyie mmekosa huruma hata kidogo?”
“Unatulaumu bure Ana, mama mwenyewe alisema Moza yupo humu ndani tumuitie Moza hamuogopi, halafu mama kazimia unadhani tungefanyaje?”
“Mmeshindwa kumuacha hapa hapa sebleni au basi mngempeleka chumbani kwake”
“Dah hata sijui nini kimetupitia mpaka tukakubaliana kumpeleka kule, twendeni basi tukamtoe”
Walitazamana ila walijikuta wakisita, maneno ya Ana yaliwaingia vilivyo kuwa walichofanya si sahihi ila sasa hawakujua kuwa kitu gani wanaweza wakafanya na kikawa sahihi kwa siku hiyo, wakawa wanaambizana waende chumbani kwa Moza ili wakamtoe mama yao, ila hakuna aliyeweza kusogeza hata mguu wake kwani wote walijikuta wakisita, Ana aliwatazama na kuwaambia,
“Mbona mnasita nendeni sasa mkamtoe”
Bado walikuwa wakisita yani kila mmoja aligubikwa na uoga wa hali ya juu hata wakabaki na mshangao tu kuwa imekuwaje mpaka waogope kiasi kile,
“Nyie wengi hivyo mnaogopa, ila mama peke yake mmeenda kumuacha kule. Ni nani awezaye kulala kwenye kile chumba baada ya mambo yote haya? Kwa hakika hakuna awezaye kulala pale, nendeni mkamtoe mama. Naenda chumbani kwangu, nitakaporudi muwe mmemtoa lasivyo nitakachowafanya hamtaisahau siku ya leo”
Ana aliondoka, huku nyuma kaka zake na mlinzi walikuwa wakijiuliza sana kuwa wachukue hatua gani. Ikabidi waamue kumfata mama yao chumbani kwa Moza ila tatizo lililokuwa kubwa kwao ni kwamba walikuwa wagumu sana kufanya vile ila badae walijikuta tu wakiinuka na kuanza kusogea kwenye chumba cha Moza ili wakambebe Rose na wamrudishe sebleni, kwakweli walivyofika kwenye mlango wa chumba cha moza kila mmoja alijikuta akikaa chini halafu pale pale wakapitiwa na usingizi mzito sana.
 
SEHEMU YA 187



Walikuja kuamka wakati pameshakucha kabisa, yani kila mmoja alikuwa akishangaa sahangaa tu halafu hawakujielewa kuwa pale kwenye korido wamefata nini, waliinuka na kuelekea sebleni ila walihisi njaa sana maana hawakula chochote tangu jana yake hadi muda waliopitiwa na usingizi, alianza Doto kulalamika
“Jamani nina njaa mwenzenu hadi sina nguvu”
“Hata mimi nina njaa balaa”
“Basi Kulwa kakoroge hata uji jikoni”
Kulwa wakati anainuka ili akakoroge uji, akachungulia kwenye meza ya chakula na kukuta kuna chakula kimeandaliwa, akasogea na kufunua, akakuta kuna chapati, rosti ya maini na juisi ipo kwenye jagi, akawaita wenzie kuwa mezani kuna chakula tayari,
“Mmmh itakuwa Ana ameandaa nini?”
“Jamani toka lini Ana akaweza kupika?”
Wakaona watabishana sana, bora waamini kuwa Ana ameandaa chakula kile. Walikaa na kuanza kula kwani wote walihisi njaa vilivyo.
Ana nae alitoka chumbani na kukuta wanakula, kwavile nay eye alikuwa na njaa hakusumbuka kuuliza kuwa nani kaandaa kile chakula kwani nae alikaa nao na kuanza kula, huku wakisifia kuwa chakula ni kitamu sana.
Walipomaliza kula, walikaa sebleni ila walikuwa wanaongea kwa mtindo wa usingizi kwani kila mmoja alikuwa na usingizi wa shibe, ila Ana aliwauliza sasa,
“Wote mlikuwa mnasifia kuwa chakula kitamu, nani kakiandaa sasa!”
“Kwani sio wewe umekiandaa?”
“Mimi! Toka lini mimi niweze kupika chapati, sijui mboga mboga, nimejifunza lini kupika vitu hivyo?”
“Sikia, sisi tumekuja sebleni njaa ikiwa inatuuma sana ila tukakuta chakula mezani na kuanza kula kwahiyo ndio wewe ukaja kujumuika na sisi”
“Dah jamani, nilijua ni nyie mmeandaa yani sijui tumekula mavitu yameandaliwa na nani”
Ila Doto akadakia na kuwaambia wenzie,
“Ila zile chapati radha yake ni kama zile chapati zilizokuwa zikiandaliwa na Moza”
Ila Ana aliwaambia ndugu zake kwa ukali,
“Nyamazeni na hiyo habari ya huyo mtu, eeh nimekumbuka. Mshaenda kumtoa mama!”
“Bado”
Walijibu huku wakiwa wamenyong’onyea sana, basi Ana akataka kufanya jambo juu yao ila alishangaa kuwa akishindwa kufanya jambo lolote, yani kila kitu kwake kilishindikana. Akaondoka pale sebleni na kwenda chumbani kwake, kisha akachukua ile dawa yake ambayo inakaaga chini ya godoro ila hakuikuta na kumfanya ajiulize,
“Ni nani mwenye uwezo wa kuchukua ile dawa yangu? Wengine wangeweza kuiona, ni mama tu anayeweza kuichukua na kuihamisha sehemu nyingine, tuseme ni mama! Mmh hapana”
Na kukosekana kwa ile dawa kuliharibu mambo yote ya Ana kwani kila alichokuwa akikifanya kilishindikana,
“Kosa langu ni kula yale machapati, sijui nitafanyeje mimi. Kama ile dawa ya kunisaidia nayo haipo basi nimekwisha, yani nimekwisha kabisa”
Aliwaza sana, ni kweli alipanga kuacha uchawi ila sio kwa kipindi hicho ambacho ndani kwao walikuwa wakisumbuliwa na mtu wa ajabu, kwahiyo siku zote Ana anajifungia ndani kwa lengo la kupambana na mtu huyu kwahiyo kitendo cha kukosa dawa yake aliona akishindwa mapambano kabisa maana atapambanaje bila uwepo wa hiyo dawa.
Ana akainuka na kwenda chumbani kwa Moza, alifika na kufungua mlango kisha kuingia ndani hukua akiangalia kila upande kuwa labda ataweza kuona chochote ambacho kitaweza kumsaidia.
Cha kushangaza alimuona mama yao amekaa chini halafu akionekana kama mtu anayetumikishwa ila anayemtumikisha hakuonekana, ila tu mama yao alionekana kwenye wakati mgumu sana.
Ana alimsogelea mama yao na kumuita,
“Mama, mama, mama”
Ila Rose hakumuitikia kabisa, aliendelea tu kutumikishwa, ikabidi amtingishe ila kitendo chake cha kumtingisha mama yao alijikuta akiwa katika sehemu nyingine kabisa.
 
SEHEMU YA 188

Mishi alikosa raha kabisa baada ya siri zake kufika kwa mumewe, na akaona kuwa ile mimba ndio chanzo cha kila kitu. Akaona ni vyema kuchukua maamuzi ya kuitoa ile mimba,
“Najua Yule binti ananitokea kwa njia ya kimazingara, sasa mimi nitaenda kuitoa hii mimba hospitali. Siwezi kukubali aisee nizae kitoto ambacho nimekipata kwaajili ya kubakwa? Hapana kwakweli, naenda kuitoa hospitali”
Alimfata mumewe kwa kunyenyekea na kumuomba pesa kwaajili ya kufanya mahitaji kidogo na kusema kuwa anataka akajiandikishe na kliniki,
“Kujiandikisha na kliniki ndio hela yote hiyo!”
“Hospitali za kulipia ni gharama, ni vyema nipimwe vipimo vyote kwa usalama wangu. Hospitali za serikali hazina uangalizi mzuri”
Kwasababu huyu mwanaume alimpenda Mishi na alishakubali kuilea ile mimba kwahiyo hakuwa na pingamizi lolote la kumpa pesa, ingawa kiuhalisia moyo ulimuuma sana kuwa mwanamke anayempenda kumbe alibakwa ndio akamkubali yeye sababu alishajiona kuwa na kasoro, aliumia moyoni ila aliona cha muhimu ni kumpenda Mishi, kwahiyo akamkabidhi pesa aliyoiomba.
Mishi alienda hospitali ambazo anajua kuna daktari wazoefu na hiyo kazi ya kutoa mimba, ukizingatia bado haijawa kubwa kivile, akaonana na daktari na kuongea nae, kisha dakari akampa muda wa kwenda ili wakakamilishe hilo zoezi.
Mishi hakurudi kwake, ila alizunguka zunguka maeneo ya jirani karibu na ile hospitali ili kupoteza muda, mpaka muda ulipofika akaenda sasa kwenye chumba ambacho daktari huyo hufanyia zoezi lake hilo, na aklimkuta tayari kashaandaa na vifaa vyake,
“Kuna wenzio kama watatu tayari nishamalizana nao, yani nyie mabinti bhana mnapenda mambo yetu ila mimba hamzitaki”
“Mimba zinatuharibia ujana”
“Haya, nipe changu kabisa, nikishamaliza hili zoezi naondoka zangu maana kwa leo wewe ndio utakuwa mteja wangu wa mwisho wa zoezi hili”
Mishi alimpa pesa kisha kupanda kitandani ili daktari aanze kazi yake ya kuitoa ile mimba ambayo Mishi hakuitaka kabisa kwani kwake aliiona kama mimba ya laana.
Wakati Yule daktari akianza tu zoezi lake, Mishi alishangaa kumuona daktari akianguka chini huku akitapatapa na povu kumtoka mdomoni, wakati anamshangaa vile mara Yule daktari akawa kimya kabisa kama mtu aliyekufa.

Wakati Yule daktari akianza tu zoezi lake, Mishi alishangaa kumuona daktari akianguka chini huku akitapatapa na povu kumtoka mdomoni, wakati anamshangaa vile mara Yule daktari akawa kimya kabisa kama mtu aliyekufa.
Mishi akaanza kuogopa na kushuka kitandani, halafu akamkimbilia daktari pale chini akimshika shika huku akimuita,
“Daktari, daktari”
Ila daktari Yule alikuwa kimya kabisa, Mishi hakujielewa, alitoka kwenye kile chumba na kwenda kuita madaktari wengine ambapo walipoingia walishangaa pia, wakamchukua mwenzao kwenda kumpima ila wakati huo huo waliomba askari wa pale hospitali wamshikilie Mishi maana ilikuwa bado haijajulikana kuwa ni kitu gani kimempata mwenzao.
Mishi alikuwa kashikiliwa huku ana wasiwasi bila kiasi, alikuwa na hofu kubwa sana moyoni mwake, mara akamuona kuna daktari ambaye huwa anamfahamu akifika kama anataka kuzungumza nae ila Yule daktari alivyofika pale akamnasa kibao Mishi na kumfanya ashangae,
“Mbona umenipiga?”
“Muuaji mkubwa wewe”
“Sijaua jamani sijaua mimi”
“Mpelekeni kituoni huyu msichana ni muuaji, kamuua daktari”
Wale askari waliokuwa wamemshikilia Mishi waliita defenda kisha Mishi akapakiwa humo na kupelekwa kituoni, alijikuta akilia sana ila tu hakujua kuwa imekuwaje kuwaje maana ni kitu ambacho hakukielewa kabisa.
 
SEHEMU YA 189

Ana alikuwa sehemu ya tofauti kabisa na nyumbani kwao, na sehemu aliyojikuta yupo ni nyumbani kwa mama Jack ambapo hakujua hata imekuwajekuwaje hadi kufika pale, hakuwahi kupajua kwa mama Jack ila alitambua ni nyumbani kwa mama Jack baada ya kukuta watu kwenye nyumba hiyo wakiongelea kuhusu kifo cha mama Jack, Ana alimsogelea kijana aliyeonekana akimuhadisia mdada kuhusu kifo cha mama Jack, Ana alipowatingisha walishtuka sana na kumuuliza kuwa ameingiaje,
“Umepitia wapi wewe?”
“Sijui”
“Wewe ni mwizi?”
“Hapana, mimi si mwizi ila hata mimi sijui nimeingilia wapi. Nilikuwa kwetu ila cha kushangaza nipo huku, sipajui, sijawahi kufika ila mtu mnayemuongelea namjua tena alifia nyumbani kwetu”
Hapo Yule kijana aliacha kuwa na maswali zaidi kwani alitaka kusikia kuwa mama yao alikufaje kufaje,
“Alikufa nyumbani kwenu? Ilikuwaje?”
“Mama yenu na mama yangu ni wachawi yani hilo halipingiki ila utofauti wa uchawi wao ni kuwa, mama yenu alikuwa anafanya wa jumuiya ila mama yangu ni wa peke yake, huwa anafanya uchawi kwaajili ya mambo yake tu. Mama alipelekwa kwa mganga na mama yenu, na Yule mganga alimwambia mama kuwa atoe kafara watoto wake. Kwenye familia yetu kuna mtu wa ajabu sana ameibuka na mtu huyu ana mazuri na mabaya yake, nay eye ndiye kawaponya ndugu zangu ila akasababisha mama yenu akafa”
“Kivipi, hebu tueleweshe vizuri”
Ana aliwaambia kutokana na uelewa wake, maana kidogo yeye aliweza kuelewa kuwa kifo cha mama Jack kilikuwaje, ni baada ya mama yao kuacha kutaja majina aliyoambiwa ya kutoa kafara na kuanza kutaja jina la mama Jack sababu alimkuta ndani kwake kwa mshangao.
“Mmmh na huyo mtu anayefanya vitu hivyo hatuwezi kupambana nae?”
“Kupambana na mtu huyo ni kujiingiza matatizoni, yani mnaweza mkaingia kwenye matatizo makubwa zaidi ya haya. Mama mwenyewe kajaribu mara kadhaa kupambana nae ila mwisho wa siku ni matatizo tu na anazidi kuivuruga familia sababu ya kupambana na huyo mtu”
“Ndugu zetu wameenda tena kwa mganga, na lengo ni moja tu kupambana na huyo kiumbe na kumrudisha mama yetu kama ikiwezekana”
“Hawezi kurudishwa, kwanza kazikwa kwenye kaburi lenye maji”
“Kuna uhusiano gani wa kaburi lenye maji na kurudishwa?”
“Sijui, ila ninachojua ni hawezi kurudishwa. Waaambieni hao ndugu zenu waache tu. Mimi mwenyewe hapa sijui nitarudije nyumbani, kilichoniponza ni kutaka kumsaidia mama”
Yani Yule kijana kuna baadhi ya maneno alikuwa anamuelewa Ana ila kuna baadhi ya mambo alikuwa hamuelewi kabisa, ila kwavile Ana alifika kimaajabu Yule kaka alimwambia kuwa siku hiyo alale hapo halafu kesho yake atamsindikiza kwao.

Mume wa Mishi alishangaa kupigiwa simu kuwa mkewe yupo kituo cha polisi, ikabidi afanye hima aende maana hakuelewa ni jambo gani limempata mkewe, na kweli alimkuta kituo cha polisi na alipewa muda kidogo tu wa kuzungumza nae,
“Imekuwaje Mishi tena jamani!”
Ikabidi Mishi asifiche maana tayari alifikwa na majanga,
“Nilikuwa na lengo la kutoa hii mimba, na daktari tulielewana vizuri kabisa, kilichotokea wakati anataka kunitoa ndio sikielewi hadi muda huu maana Yule daktari alianguka chini”
Mume wa Mishi alishangaa sana na kumtaka Mishi amuelezee zaidi, ambapo Mishi alimueleza ilivyokuwa hadi yeye kufikishwa hapo kituoni,
“Inasemekana Yule daktari amekufa, lakini mimi sijamuua daktari. Kwanza nimuue kwa lipi jamani, kweli mimi naweza kuua mtu jamani! Yani nimechanganyikiwa kabisa”
“Ila na wewe mke wangu ni nani alikutuma kwenda kutoa hiyo mimba?”
“Jamani sidhani kama ni wakati muafaka wa kubishana huu, fanya hima nitoke humu Napata shida ujue, nateseka mimi. Sijamuua daktari”
“Najua kama hujamuua, na ninajua kama kuua huwezi ila sijui uliingiwa na nini mke wangu hadi kwenda kutoa mimba. Kwahiyo alikutoa?”
“Hivi jamani na wewe hunielewi au ni nini? Nimekwambia wakati anataka kunitoa akaanguka, kwahiyo hakunitoa, yani hata sielewi kuwa nijielezaje. Kwa maelezo yangu pia nitafungwa maana sharia za nchi haziruhusu kutoa mimba, yani nimechanganyikiwa hapa. Naomba ufanye kitu nitoke”
Basi mume wa Mishi akaongea pale na mke wake na kumuahidi kumtafutia dhamana ili aweze kutoka halafu wafatilie kesi, ila alipoenda kwaajili ya dhamani ilikataliwa kabisa, na kushindwa kumsaidia Mishi kwa siku hiyo, na kuamua kwenda kujipanga kwa namna nyingine.
 
SEHEMU YA 190


Wakati mume wa Mishi anaondoka njiani alikutana na Salome aliyekuwa akitabasamu, kisha akamsalimia mume wa Mishi,
“Habari yako?”
“Hivi tunajuana mimi na wewe?”
“Ndio tunajuana, au umechanganyikiwa sababu ya mkeo kuwa rumande!”
“Umejuaje”
“Najua”
Yani akili ya mume wa Mishi kwa wakati huo hata haikuwa ya kawaida kabisa kwani iligubikwa na mawazo mengi sana ya jinsi gani atamsaidia mkewe, kwahiyo hata hakuwa na kumbukumbu kuwa Salome ndiye aliyemwambia ukweli kuhusu mke wake kule kwa mganga,
“Nimechanganyikiwa kweli, mke wangu hata sijui nitamsaidiaje”
“Utamsaidia vipi muuwaji!”
“Sio muuwaji mke wangu, daktari alianguka mwenyewe”
“Mkeo sio muuwaji, na kile kiumbe alichotaka kukitoa sio uuwaji ule? Au kwavile unadhani mkeo ni mimba yake ya kwanza ile? Unajua ni ngapi ametoa? Mkeo ni muuwaji na kumsaidia itakuwa ni ngumu sana”
“Sikuelewi, inamaana wewe unajua kilichotokea?”
“Najua ndio”
“Basi usitangaze hivyo kuwa mke wangu alitaka kutoa mimba”
“Sasa nimetangaza au nimekwambia wewe muhusika, unaona sababu viumbe vya tumboni haviwezi kulilia haki zao, haviwezi kushtaki kuwa vimeuliwa kwa makusudi kabisa, mkeo ni muuwaji. Yule daktari nae anahaki ya kufa maana kashaua watoto wengi wasio na hatia kwa tamaaa ya pesa. Hata ufanyaje mkeo kwasasa hatotoka mule ndani mpaka ajifunze adabu na aelewe anapoambiwa kitu, maana kichwa chake ni kigumu kuelewa. Nishamwambia mara nyingi asiitoe ile mimba, najua ni mchezo wake ndiomana nikamuonya sana kuwa asiitoe ile mimba, halafu wewe unakazana kuugua moyo sababu ya Yule muuwaji! Ukitaka msaada wangu zaidi utanitafuta”
Kisha Salome akaondoka, mume wa Mishi alimuangalia Salome hadi alipoishia ndio akakumbuka kuwa ni huyu binti aliyemwambia tabia za mkewe ndipo alipokumbuka maneno ya mkewe kuwa huyo binti hakuwa mtu wa kawaida, ikabidi aendelee kwenda nyumbani ila alijipanga kwenda tena polisi ili akamuulize vizuri Mishi anapoishi Yule binti na aweze kwenda tena kuongea nae.

Nyumbani kwa Rose, walikaa watoto wake sebleni na muda kidogo alikuja Salome na kuwafanya wote washtuke maana wakikumbuka yale maneno kuwa Salome ndiye Moza walipatwa na mashaka ila Salome akawauliza,
“Mbona mnaonekana kuniogopa?”
Walikaa kimya hakuna aliyeweza kumjibu, na kufanya Salome aendelee kuongea
“Najua mama yenu atakapotoka kwenye adhabu ambayo amejipa kutokana na matendo yake yasiyoeleweka, ataenda kuwafungulia wale watu aliowafungia kwa miaka mingi”
Walikuwa kimya tu wakimsikiliza, hakuna aliyeongea chochote kwani ilionyesha wazi wanamuogopa Salome kutokana na hoja kwamba ndiye Moza, baada ya kimya kidogo Kulwa aliuliza kwa mashaka,
“Wewe ni Moza?”
Sauti yake ilikuwa ya kutetemeka sana,
“Kwa mfano mimi nikiwa ndiye Moza mtafanyaje?”
Wakawa kimya tu, na kufanya Salome aendelee kuongea
“Mimi nikiwa ndiye Moza, inamaana kuwa Moza mwenyewe yuko wapi, na Salome mwenyewe yuko wapi? Je Moza alikuwa ni jinni kiasi kwamba aweze kuingia kwenye mwili wa mtu mwingine na kufanya mambo yake? Msiniogope, mimi sipo kwaajili ya kuwatisha ila nipo kwaajili ya kuwasaidia, na kikubwa kinachonisumbua ni kuhusu hao watu ambao mama yenu kawatunza ndani, sishindwi kuwatoa ila nikiwatoa mimi nitasababisha madhara makubwa sana ndiomana nataka awatoe yeye mwenyewe”
Kidogo Salome alivyosema hivi walipata hata kauli za kuongea nae kwani uoga uliwaondoka kwa kiasi Fulani tofauti na mwanzo walivyokuwa wamejawa na uoga usio kifani, kisha akawaambia kuwa ni yeye ndiye aliyewaandalia chakula cha asubuhi, wakatamani kumuuliza kuwa mbona chapatti zilinoga kama zimepikwa na Moza, ila hakuna aliyeweza kuuliza hilo swali ingawa kwa wakati huu uoga ulikuwa umepungua.
Salome aliwaambia kuwa kwa siku hiyo wote walale hapo sebleni, yani hapakuwa na cha mlinzi wala nani kwani hakutoka tena kwenda getini, ni toka siku ile ya majanga ya kumuokota Rose, alikuwa akiishi tu mule ndani.

ITAENDELEA
 
Hayawi hayawi sasa yamekuwa, ZIMEBAKI SEHEMU 10 TU ZA MWISHO SIMULIZI IFIKIE TAMATI,
Je utabiri wako umetimia/Utatimia? ........

Hakuna kulaza damu, tukutane saa 6 usiku.... tumalize simulizi yetu [emoji91] [emoji91] [emoji91] [emoji91]
Sawa mkuu nipo seat ya mbele apa
 
SEHEMU YA 191

Kulipokucha mume wa Mishi alienda tena kituoni na kuongea na mkewe ambapo mkewe alimpa maelekezo ya anapopatikana Salome, kisha mume wa Mishi alimuahidi kufanya hivyo kwa muda huo maana hakuwa na namna nyingine yoyote, kesi ya Mishi ilikuwa ni kubwa sana na kama ikisomwa yani Mishi ana kifungo cha maisha pale, kwakweli mume wa Mishi alikuwa akihofia sana swala la mkewe kufungwa maisha ukizingatia ni siku chache tu tangu aoane na huyo mwanamke.
Aliondoka pale na kufata maelekezo hadi nyumbani kwa Rose, ila kabla hajagonga geti Salome alikuwa ameshamfungulia,
“Nilijua tu utakuja, na kwa hakika unajutia makosa ya mke wako nay eye anajutia makosa yake”
“Ni kweli anajutia sana mke wangu, mimi nipo tayari kuilea ile mimba na kulea mtoto na tena nitampenda kama mwanangu ila sasa mke wangu anawakati mgumu sana hata sijui nitafanyaje kumsaidia”
“Sasa umenifata mimi ndiyo hakimu wa kesi ya mkeo kusema nitaamuru asifungwe?”
“Najua kuwa wewe sio hakimu, ila wewe ulimpa laana mke wangu na laana hiyo ikampata. Ulimkataza mke wangu kufanya jambo lolote kinyume, na amefanya amepatwa na mabalaa makubwa sana, najua unauwezo wa kufanya mke wangu asikutwe na hatia”
“Lakini mkeo katoa mimba nyingi sana, hata akikutwa na hatia ni halali yake”
“Hawezi kurudia tena, ni ujana ndio ulikuwa unamsumbua. Naomba umsamehe mke wangu”
Mume wa Mishi alipiga magoti kwa Salome huku akionyesha simanzi ya hali ya juu,
“Nihurumie mimi, nampenda sana Mishi. Yeye ni mwanamke nimpendaye, ndoa yetu ni changa kabisa, hata miezi miwili haina ila majanga kama haya. Nakuomba nihurumie tafadhali”
Salome alicheka sana na kumwambia mume wa Mishi ainuke kisha akamwambia,
“Nenda nyumbani kwako”
“Halafu badae niende polisi!”
“Sijakwambia uende polisi, nenda nyumbani kwako kunguni wewe.”
Mume wa Mishi hakubisha na moja kwa moja alifanya safari ya kwenda nyumbani kwake, alipofika alifungua mlango na kushangaa mkewe kasharudishwa nyumbani.

Neema alikuwa nyumbani kwake na siku hiyo aliamua kuanza kufunga kama ambavyo alikuwa ameshauriwa na mama Pendo, alijitahidi afunge ingawa ilikuwa vigumu sana kwake kupambana na njaa yake, kwenye mida ya saa kumi jioni alishikwa na usingizi na kuamua kujilaza ila alijiwa na ndoto ambapo kwenye ndoto hiyo alimuona binti yake Salome amelala tena amelala kwenye kilekile chumba chake ila amelala usingizi mzito sana kiasi kwamba hashtuki kabisa, halafu akamuona Moza ambaye alionekana akibadilika kwa pembeni na wakati mwingine kuwa na mwili wa Salome na wakati mwingine kuwa na mwili wake, Neema alishtuka sana kutoka usingizini, na moja kwa moja akachukua simu yake na kumpigia mama Pendo huku akimueleza vile ambavyo ameota kwenye ndoto,
“Usihofu ndugu yangu, tunatakiwa kuingia kwenye maombi”
“Lakini naogopa”
“Usiogope, muombe Mungu akupe ujasiri na utaweza kupambana na hali yoyote. Kesho tutakuja huko”
Basi Neema alikuwa na mashaka ya hali ya juu, akaamua kwenda tena chumbani kule alipokuwa analala Salome, huku akitembea na tahadhari kubwa sana, akafungua chumba na kumfanya ashtuke vilivyo maana alimuona kweli Salome amelala hoi kitandani.
 
SEHEMU YA 192

Basi Neema alikuwa na mashaka ya hali ya juu, akaamua kwenda tena chumbani kule alipokuwa analala Salome, huku akitembea na tahadhari kubwa sana, akafungua chumba na kumfanya ashtuke vilivyo maana alimuona kweli Salome amelala hoi kitandani.
Neema hakuweza kuvumilia, alikimbia hadi nje huku akihema juu juu, akaunganisha matukio ya jinsi Salome wake alivyoanguka na kukauka kwenye kaburi la Moza, na jinsi alivyoota kuhusu Salome kulala chumbani kwake halafu Moza kuonekana akiingia kwenye mwili wa Salome na vile alivyoenda chumbani kwa Salome na kumkuta kuwa ni kweli amelala chumbani kwake, Neema alikuwa na hofu kubwa moyoni huku akijikuta akiogopa kuingia ndani kwake, akaita mmoja wapo wa wanae mapacha kuwa aende ndani akamletee simu kwa madai kuwa yeye alikuwa na kazi nje kumbe kiukweli alikuwa anaogopa ndani, Yule mtoto aliingia ndani ila ilichukua muda mrefu sana na hakurudi pale nje, ikabidi amuite pacha mwingine na amuagize ila naye ikawa hivyo hivyo na kufanya hofu kubwa itande kwenye moyo wa Neema, alikuwa na uoga wa hali ya juu. Badae akajiuliza kuwa yawezekana alichokiona ni maruweruwe ya usingizi kutokana na ile ndoto aliyoota,
“Ila wanangu niliowatuma ndani mbona hawajarudi?”
Akajaribu kuwaita lakini hawakumuitikia, alikaa nje mpaka mida ya saa moja jioni badae akajisemea,
“Natakiwa niwe jasiri,hivi mama gani mimi naogopa ndani na kuwatuma watoto! Haya sasa watoto hawajarudi halafu mimi bado naogopa na cha kushangaza kabisa huko ndani kwangu eti namuogopa mtoto wangu mwenyewe Salome, itabidi tu nijiweke ujasiri”
Akajitia ujasiri na kuingia ndani kwake, kisha akawasha taa za nyumba nzima na kuanza kuwaita wale wanae mapacha ambao aliwakuta chumbani kwao wamelala hoi, akawaamsha wakaamka huku wakidai kuwa na usingizi sana,
“Amkeni mle kwanza ndio mtalala”
Akatoka nao hadi sebleni, kisha akamuagiza mmoja wao,
“Nenda chumbani kwa dadako kamuamshe nae aje kula”
Basi yeye alikuwa na hofu sana pale wakati mwanae mwingine ameenda kumuita Salome, baada ya muda kidogo mwanae alirudi na kumwambia,
“Mama, mbona dada hayupo chumbani kwake? Una uhakika alikuwa amelala?”
“Mmmh labda ametoka”
Kisha Neema akaenda jikoni kuandaa chakula cha usiku huo kwani hata kufuturu hakufuturu kutokana na uoga wake, akijipa matumaini kuwa huenda ni mawazo yake tu kuwa alimuona Salome.
 
SEHEMU YA 193


Muda huu Salome aliingia ndani na moja kwa moja alienda chumbani kwake, ila Kulwa alimfatilia Salome kwa nyuma na alipofika kwenye mlango wa chumba cha Salome alichungulia kwa kutumia kitasa cha mlango, akamuona mama yao akiwa anafanya shughuli zisizoonekana ila alikuwa amechoka sana, halafu akamuona Salome akimfata mama yao, na walisikika wakiongea ambapo Salome alimuuliza Rose,
“Umechoka?”
“Nimechoka ndio”
“Upo tayari kuwaachilia wale uliowafungia?”
“Naogopa maisha yangu”
“Kwahiyo maisha yako ni bora kuliko maisha ya wale uliowafungia?”
“Naogopa tu”
“Rose, jua naweza kufanya kwa lazima ila itakugharimu maisha yako kupita vile unavyofikiria, hebu waza jinsi nitakavyowatoa wale watu kinguvu nini kitatokea kwako”
“Najua nitakufa”
“Sasa kufa na kufilisika kipi bora”
Rose alionekana kukaa kimya na kufanya Salome aendelee kuongea,
“Mali nyingi umezipata kwa njia isiyo ya halali, umetesa watu. Umefanya wengine kuwa mandondocha yako sababu tu upate mali unayoitaka. Haya sasa kuna hasara gani ya hizi mali zikipotea?”
“Mali zangu zikipotea nitaweka wapi sura yangu, siku zote nimekuwa nikihangaika sababu ya hizi mali. Nihurumie Moza”
Hapa Kulwa alishtuka sana ila kwavile aliyemuona yeye kupitia kile kitasa cha mlango alikuwa ni Salome, aliendelea kujipa moyo kuwa huenda mama yao amechanganyikiwa tu kumuita Salome kuwa Moza. Ila huyu Salome aliendelea kuongea na Rose,
“Nakupa leo tu, ukishindwa basi mimi kesho nitafanya ninavyojua mimi. Nimekuvumilia sana Rose, unatesa watu, unawaumiza watu wasio na hatia ili wewe ufurahie maisha yako, waachie watoto wa watu, wanahitajika pia kwenye familia zao. Yani watu hawajulikani walipo kwao, familia hizo zimelia hadi basi kumbe wapo kwako huku umewafungia. Waachie watoto wa watu Rose”
“Basi nitafanya hivyo leo usiku”
“Mimi nakwambia kweli usipofanya hivyo unajitafutia mabalaa, kesho nitafanya mwenyewe na utaogopa sana”
Rose alionekana kutetemeka kiasi, Kulwa nae aliondoka pale kwenye kitasa cha mlango na kwenda kuwapa taarifa wenzie kuhusu kile alichokiona na kukisikia.
 
SEHEMU YA 194


Neema akiwa bado na mashaka ya maisha ingawa muda tayari ulikuwa umeenda, akataka tena kwenda kuangalia kwenye chumba cha Salome kwani muda wote alisikia kama aende kuangalia ilia one kuwa atakutana na maajabu gani, ila kabla hajaenda popote uliingia ujumbe mfupi kwenye simu yake, alipoangalia ulikuwa unatoka kwa Salome,
“Mama nimeshakwambia, achana na maswala ya kufatilia chumbani kwangu. Hakuna chochote utakachokipata zaidi zaidi kujiweka kwenye mawazo tu”
Neema aliogopa sana huku mapigo yake ya moyo yakienda kwa kasi ya ajabu, akaamua kuchukua simu na kumpigia mama Pendo ila hakumpata hewani kwa wakati huo, basi ndio moyo wake uligubikwa na uoga mwanzo mwisho. Akajikuta akiogopa kwenda kulala mwenyewe kwenye chumba chake hivyo alienda kulala na watoto wake mapacha.

Mume wa Mishi alistaajabu sana kwa uwepo wa mke wake nyumbani, akamuuliza kwa mshangao kuwa amefanikiwa vipi kupata dhamani,
“Sio kupata dhamana tu mume wangu bali sina kesi tena”
“Kivipi?”
“Unajua alikuja Yule binti niliyekwambia, ndio kanitoa polisi hata sijui kaongea nao nini ila ndio kanitoa polisi na hakuna tena kesi wala kuripoti siendi kuripoti, kwa kifupi nimefutiwa kesi”
Mume wa Mishi alishangaa sana, ikabidi amueleze Mishi kuwa alienda kupatafuta hapo anapoishi huyo binti ili kumuomba amsaidie mke wake, kwahiyo swala la kusema kuwa Yule binti alishaenda polisi na kumsaidia lilimshangaza sana, akamuuliza tena mke wake kuwa hilo swala lilitokea muda gani,
“Kwanza asante sana mume wangu maana sikujua kama ni wewe ulienda kuzungumza nae, ila nilimuona polisi pale askari waliponifungulia na kumkabidhi kuwa niondoke nae. Nilipotoka nae alinipa onyo moja kuwa nisijaribu kuitoa hii mimba tena na nisijaribu kutoka nje ya ndoa yangu. Ila aliposema hapo tu kama kawaida kimaajabu nimejikuta nipo hapa ndani, mume wangu Yule binti sio mtu wa kawaida kabisa. Mume wangu, nakuhakikishia kuanzia muda huu, mimi ni Mishi mpya tena mpya kabisa, sitashawishika tena na chochote. Hii mimba nitalea na mtoto nitampenda kupita maelezo ya kawaida, sirudii kutoa mimba, sirudii tena kuhangaika hangaika na wanaume”
“Kwahiyo Yule daktari amekufa kweli”
“Ndio Yule daktari kafa kweli, tena nasikia leo ndio ilikuwa mazishi yake. Ni amekufa, ila inasemekana Yule daktari kashiriki sana kutoa wanawake mimba, yani Yule daktari nimemjua kupitia rafiki zangu, ni wengi sana kawatoa”
“Hapo sasa unatimia ule msemo usemao, mshahara wa dhambi ni mauti. Mke wangu tabia ya kutoa mimba uache, tutaliliwa siku ya mwisho na watoto mbalimbali tuliokatisha maisha yao”
Mishi alimuahidi mumewe kubadilika kabisa kwani kwa muda aliokaa kule rumande hakutamani kurudi tena kwani aliona kama dunia ikimuelemea ukizingatia yeye alikuwa anajiona kuwa hana hatia.
Siku hiyo waliwahi sana kulala ili kupata muda wa kupumzika kutokana na ile misukosuko ya siku hiyo na zile siku za nyuma.

Kulwa alipowaeleza wenzie kwahiyo wakawa tayari kwa kuona maajabu kwa usiku huo huku uoga ukiwa wa hali ya juu, wakakubaliana kulala sebleni tena ila usiku huo Salome hakulala nao sebleni maana hakutoka kabisa chumbani kwake, kwahiyo walibaki wenyewe ila walijawa na hofu ya hali ya juu kiasi kwamba hata wakisikia mjusi anapita wanatamani wakimbie, yani siku hiyo hakuna aliyelala kabisa hadi kuna muda walisikia mlango unabamizwa walijikuta wakikimbia wote na kukimbilia mlango wa kutokea nje ila walishangaa mlango haukufunguka yani hofu ikawajaa huku wakiwaza kuwa wataona vitu vya ajabu ila muda kidogo wote watatu wakasikwa na usingizi mzito sana.
Kesho yake walishtuka kila mtu akiwa amelala sehemu yak echini pale sebleni ila hakuna cha tofauti ambacho walikiona kwenye nyumba yao kwahiyo walijiona kuwa ni uoga tu ndio uliowasumbua ndiomana walikuwa na hali ile usiku.
 
SEHEMU YA 195

Ilikuwa ni siku nyingine tena ambapo Ana alimuomba Yule mkaka amsindikize sasa nyumbani kwao, ila ndugu mmoja wa Yule kaka akajaribu kumkumbusha kuwa hata mama yao kilichomponza ni kumsindikiza Yule binti,
“Ila mimi sio mchawi”
“Sasa unauhakika gani kuwa mama yetu alikuwa mchawi?”
“Mifupa tuliyoikuta chumbani kwake, na huyu dada aliyetolewa msukule”
“Wewe ndugu yangu wewe, hakuna mwenye uhakika kuwa mama alikuwa mchawi, amesingiziwa tu na Yule binti ila mimi cha kukushauri usiende peke yako huko. Nenda na mtu mwingine”
Yule kijana alikubaliana na wazo la ndugu yake huyo, ila Ana aliuliza jambo moja kwao,
“Mama yenu alizoeleka kwa jina la mama Jack, huyo Jack ndio yupi kati yenu?”
“Jack ni mtoto wa mama aliyezoeleka sana, alikuwa na mapenzi na watu wengi ndiomana mama hakuitwa majina yetu yote ila aliitwa mama Jack, tena alikuwa ni mtoto wa mwisho kwa mama yani ndio mdogo wetu. Ila cha kushangaza, mdogo wetu huyo alipoteaga na hadi leo hatujui alipo”
“Kheee kumbe! Au nae katolewa kafara?”
“Hata hatujui kwakweli, dada yetu huyu tulijua amekufa kumbe yupo katolewa kafara, ila kuhusu Jack hakuna anayejua alipo Jack, alipotea kwenye mazingira ya kutatanisha na hadi leo hajawahi kuonekana”
“Mama yenu alichukua hatua gani kuhusu kupotea kwa huyo Jack?”
“Hatujawahi kumuelewa zaidi ya kusema ataenda kuagua kwa mganga ili ajue mwanae Jack yuko wapi, ila kila siku alisema bado haijajulikana alipo”
Ana aliwaelewa kisha akaondoka nao na kuanza safari ya kuelekea nyumbani kwakina Ana.
 
SEHEMU YA 196

Leo mapema kabisa Neema alimpigia simu mama Pendo kisha akamuelezea kuhusu ndoto ambayo aliota jana yake na jinsi alivyoenda chumbani kwa Salome na kukuta amelala, akamuelezea jinsi alivyowatuma wanae na kugundua kuwa ni maruweruwe,
“Hapana Neema, hapo lazima kuna kitu wala sio maruweruwe”
“Mmmh unanitisha sasa, si mtakuja leo?”
“Kuna udhuru kidogo imetokea, tutakuja kesho”
“Sasa mimi nifanyeje, jamani naogopa mwenzenu”
“Cha kukusaidia ni kuwa uendelee na mfungo leo”
“Mmmh jamani nifunge tena?”
“Ndio funga tena, halafu hujui tu unafikiri hiyo ndoto umeota burebure, ni faida ya kufunga hiyo. Kufunga kuna faida”
“Mmmh haya”
“Funga bhana, usikate tama kuna faida ya kufunga. Kuna faida ya kufanya maombi, yani wewe usijali kuwa sisi hatujaja nyumbani kwako, unaweza kuomba mwenyewe na Mungu akakusikia, cha msingi kuwa na imani tu”
Neema alimkubalia mama Pendo na kukubali kuwa siku hiyo ataingia kwenye mfungo tena ingawa mwanzoni alikuwa anaona kuwa mfungo ni swala gumu sana kwake kwani aliona njaa ndio kitu cha kusumbua zaidi akili yake.
Wakati amekaa kwenye mida ya mchana mchana alisikia hodi, na alipofungua alikuwa ni Patrick amerudi, kwa upande mwingine Neema alifurahi sana kwani aliona sasa ataishi bila uoga sababu kuna mtu mkubwa ndani ya nyumba yake, ila kwa upande mwingine aliona ni mtihani kwake kwani atatkiwa kumpikia Patrick chakula wakati yeye amefunga, kwahiyo anaweza akajikuta anaonja na kufungulia.
Alimkaribisha vizuri sana, ambapo alipoingia tu cha kwanza alidai kuwa ana njaa sana, kwahiyo ikabidi Neema aende kumuandalia chakula,
“Mmmh huu ni mtihani sasa, nitaweza kuandaa chakula kweli bila kuonja? Huu ni mtihani kwangu”
Neema alijiona akianza kushindwa kufunga kwa siku hiyo mapema sana kabla hata siku haijaenda ukingoni.
 
SEHEMU YA 197

Nyumbani kwa Rose, leo aliingia jikoni Salome na wote walikuwa sebleni kwa wakati huo kasoro Ana ambaye hakuwepo nyumbani, kwahiyo pale sebleni alikuwepo mlinzi, Kulwa na Doto.
Leo Salome alipika chakula na kila mmoja alisikia harufu ya kuungua kwa kile chakula,
“Jamani kama chakula kinaungua?”
“Ni kinaungua kweli”
“Ila si Salome yupo jikoni”
Ikabidi mmoja aende akamuangalie Salome jikoni, akashangaa sana kwani hakuwa Salome tena bali alikuwa ni Moza.


Ikabidi mmoja aende akamuangalie Salome jikoni, akashangaa sana kwani hakuwa Salome tena bali alikuwa ni Moza.
Uoga ulimshika na akarudi haraka haraka huku akiwapa wenzie ishara kuwa wakajishuhudie wenyewe kwa macho yao halafu yeye alikimbilia mlangoni kwa lengo la kutoka nje, nao waliinuka na kwenda jikoni, ila walipomuona Moza walipatwa na uoga wa hali ya juu, wakarudi haraka haraka na kuanza kugombeana mlango wa nje ambapo Kulwa nae alikuwa akihangaika nao ila haukufunguka ilikuwa kamavile vile usiku kuwa umejikaza na kufanya uoga uwazidi hata wasiweze kusogea kwenda mahali popote.
Wakiwa pale sebleni wakamuona Moza akitoka jikoni na kwenda pale walipo, kwa uoga waliokuwa nao hakuna aliyeweza kumtazama Moza, ila Moza aliwaambia
“Leo lazima nimalize kazi yangu, sitaweza tena kukaa, kwani Salome anatakiwa kurudi kwao”
Wote hawakuweza kumjibu kitu chochote na uoga waliokuwa nao ulikuwa ni maradufu, huku wakijiuliza kuwa Salome ni nani na Moza ni nani, iweje Salome ageuke na kuwa Moza na iweje Moza aseme kuwa Salome anatakiwa arudi kwao, hawakuweza kuuliza ila walibaki wakitetemeka kwa uoga.

Neema akiwa nyumbani kwake, gafla alijihisi kutetemeka mwili mzima halafu akawa na shauku ya kwenda tena kuchungulia chumbani kwa Salome, akainuka na kwenda kuchungulia akamuona Salome amelala, alipiga kelele za uoga ambapo Patrick nae alimfata ili kujua tatizo ni nini,
“Ni Salome”
“Kafanyaje?”
“Salome sio Salome wa kawaida”
“Kivipi sio wa kawaida?”
“Muone”
Neema alionyesha kidole alipo Salome pale kitandani, Patrick aliangalia kisha akamwambia Neema,
“Mbona mtoto amelala kawaida tu”
“Sio wa kawaida Patrick”
Patrick hakumuelewa kabisa Neema, ikabidi asogee kwenye kitanda cha Salome kisha alijaribu kumuamsha bila ya kuamka na alionekana amelala usingizi mzito sana, ndipo Neema akatoa tena wazo la kumpigia mama pendo ili awaite tena wale waombaji wamsaidie binti yake.
“Kuna tatizo huku naomba msaada wenu”
“Lakini ni mpaka kesho”
“Haiwezekani kuvumilia, Salome kalala haamki, tunamuita haitiki, sio kwamba amekufa ila kalala haamki”
Mama Pendo alishangaa sana kwa jinsi alivyoelezewa na Neema hivyo kumuahidi kuwa wanaenda na wale waombaji.
 
SEHEMU YA 198

Ana alikuwa ameongozana na wale vijana hadi nyumbani kwao, alipofika mlangoni alishangaa harufu ya kuungua kwa chakula ambapo harufu hiyo ilikuwa ni kali kiasi kwamba ilimchanganya na yeye kwani anajua fika masharti ya nyumba yao kutokuunguza chakula cha aina yoyote halafu siku hiyo chakula kilikuwa kinaunguzwa kwa hali ile, akafungua mlango ila ulikuwa mgumu kwahiyo ikabidi agonge, alifunguliwa na kushangaa sana,
“Moza!!”
“Ndio ni mimi, nimekuja kumaliza kazi yangu”
Ana alitaka kukimbia ila miguu yake iligoma kwenda popote na kujikuta akiingizwa ndani pamoja na wale vijana, wakiwa wanashangaa shangaa kwa uoga pale sebleni mara walianza kuona watu wa ajabu wakitokea kwenye korido ya nyumba yao kama wakitokea vyumbani, wale watu walikuwa wakitoka mmoja mmoja na walipofika pale sebleni walikaa chini, ni hapo ndipo walipomuona Ommy na Sara wakiwa wameambatana na wale watu wengine, kiukweli kila mtu alishangaa, ila cha kushangaza zaidi ni kwa wale vijana kumuona mdogo wao jack akiwa ameambatana na wale watu,
“Mungu wangu, jamani si Jack huyu”
Walikuwa wakishangaa sana ila wale watu walitoka wote na kukaa chini pale sebleni ilionyesha kama akili zao bado haziko sawa kwani hakuna kati ya waliotoka aliyekuwa akishangaa kuwa yupo wapi na anafanya nini.
Moza aliingia jikoni na kutoka na sufuria ambayo mboga ilikuwa inaungua kisha akaweka maji halafu akaanza kummwagia mmoja mmoja kwa wale waliokaa chini ambao wametoka vyumbani, yani kitendo cha kumwagiwa kila mmoja alijikuta akili zake zikirudi timamu na kujishangaa zaidi kuhusu mahali alipo na jinsi alivyo, walikuwa jumla watu kumi na tano.
Wale vijana walimsogelea ndugu yao Jack, wakati huo Kulwa na Doto walimsogelea dada yao Sara huku wengine wakibaki wanajishangaa na kuona kuwa wamepata uhuru wa gafla bila ya kutegemea.
Moza alikuwa akitabasamu tu, na kupiga mluzi mkali ambapo Rose alitokea chumbani baada ya mluzi huo, ila alipowaona watu hao alishtuka sana na kupiga magoti kwa Moza,
“Umenimaliza Moza, umenimaliza Moza”
“Angalia ulivyowatesa watu hawa, wengine wana miaka mitano kwenye chumba chako kile kidogo umewafungia kimazingara. Unajiona bado una faida?”
“Umenimaliza Moza”
Rose alikuwa na kauli moja tu kuwa Moza umenimaliza yani alionekana kuteseka sana na kile kitu alichokifanya Moza.
Ila Moza alionekana kumpulizia kitu machoni ambapo Rose alianguka chini na kuonekana kama amezimia, watoto wake wakataka kwenda kwa mama yao ila Moza akawaambia kwa ukali,
“Asimsogelee mtu yeyote, hakuna kumsogelea Rose ni hatari kwa maisha yenu kwasasa. Haya wote tokeni nje ya nyumba hii, na mkae mbali kabisa”
Ana alijaribu kumtetea mama yake,
“Msamehe mama”
“Nyamaza na wewe, tena wewe kila kitu chako kinaenda kuteketea pamoja na uchawi wa mama yako. Hivi unadhani kuwatesa watu hawa kwa miaka yote ni vizuri? Mama yenu amekuwa mtu war oho mbaya sana kwa muda mrefu, aliweka zindiko baya kwenye nyumba yake hii, mtu usijikwae kwenye nyumba hii unapotea ili yeye azidi kufurahia maisha ya kutesa viumbe visivyokuwa na hatia. Nasema hivi ondokeni wote, tokeni nje, hapa mtuache sisi wenyewe. Nyie kakaeni mbali kabisa”
Macho ya Moza yalikuwa yanawaka kama moto hivyo kufanya wote washikwe na uoga, hakuna aliyeweza kubaki mule ndani ukizingatia Moza alikuwa anaongea kwa ukali sana halafu alikuwa anatisha, wote wakatoka nje ya nyumba yao na kukaa mbali kabisa, mara gafla wakiwa nje walishangaa kuona nyumba yao ikilipuka na moto mkubwa ukiwaka, moto ambapo uliwaka kwa muda mchache tu lakini kila kitu cha kwenye nyumba ile kiliteketea, yani kilibaki kiwanja na majivu, ilikuwa ni kitendo cha kufumba na kufumbua kila kitu hakikuwepo tena.
 
SEHEMU YA 199

Wana maombi na mama Pendo walifika nyumbani kwa Neema na kwenda chumbani kwa Salome, ambapo walimkuta vile vile amelala wakambeba na kwenda nae sebleni halafu wakaanza maombi huku wakimuita Salome kuwa arudi kwani ilionyesha wazi kuwa Salome pale yupo kimwili tu.
Baada ya maombi ya muda kidogo, Salome alionekana kuamka na kukaa huku akishangaa kila alichokiona mbele yake, mama yake alikuwa bado na uoga ila alimfata na kumkumbatia.
Salome alimuangalia mama yake na kumuuliza,
“Mama niko wapi na kuna nini”
“Salome mwanangu, ulikuwa umelala ndio nimewaita waombeaji waje wakuombee”
“Nililala? Muda gani? Na kwanini niombewe?”
“Ulibeba vitu vyako vyote ukaondoka mwanangu ukaniachia ujumbe tu, ila nikakukuta umelala chumbani kwako”
“Sikuelewi”
Neema akaamua kumshika mwanae mkono ili ampeleke chumbani kwake huenda labda akamuelewa, ila alipofika kwenye chumba cha Salome alishangaa kuona kuwa nguo za Salome na vitu vya Salome vyote vilikuwepo mule ndani yani hakuna kitu ambacho kilihamishwa kama yeye alivyofikiria mwanzo, Neema alipiga kelele na kuwaita wale wanamaombi chumbani kwa binti yake, ila walimtaka awe mpole kwanza na akae chini atafakari huku akifanya mambo taratibu taratibu,
“Ukifanya kwa papara hutaelewa chochote kile, unatakiwa kuwa mpole na utafakari. Mungu ni mwema, na mwanao ni mzima kwahiyo swala la kuanza kumkandika maswali utashindwa kuelewa kipi ni kipi”
Ikabidi Neema akubaliane na ushauri wa mama Pendo ingawa kiuhalisia hali ya mwanae ilimchanganya sana kwani mwanae hakuwa na kumbukumbu yoyote ile.
Basi wale wanamaombi na mama Pendo wakaaga huku wakimsisitiza Neema ampelekage mwanae kwenye maombi hadi atakuwa sawa kabisa.

Neema alibaki ndani, yeye, mwanae na Patrick ila aliendelea kumuhoji Salome ambaye alionyesha kila kitu hakijui hata uwepo wa Patrick hakuuelewa kabisa, kwani kila kitu kilikuwa kigeni machoni mwake. Alianza kumuhoji mama yake kuhusu Patrick,
“Mama, huyu ni nani?”
“Ni baba yako huyu”
“Baba yangu! Mama si ulisemaga kuwa sina baba!”
Neema akawa kimya kwa muda kisha akamuangalia mwanae na kumwambia,
“Si wewe Salome uliyeamua kwenda kumtafuta baba yako hadi kuamua kuhamia nyumbani kwake. Huyu ni baba yako uliyemtafuta kwa kipindi chote, na ni wewe ndiye uliyemleta hapa nyumbani”
“Sikuelewi mama”
Neema alijaribu kumuelewesha vilivyo ila Salome hakumuelewa kitu chochote, halafu akauliza tena maswali yaliyomchanganya kabisa Neema,
“Vipi kule nyumbani kwetu? Mbona tuko huku, ni kwa nani huku? Yuko wapi mamdogo Ashura?”
“Mmmh hata sijui nikujibu vipi Salome yani vitu vingine unauliza wakati ulifanya mwenyewe, wewe si ulisema Ashura alitaka kukuua ukamuwahi na kummaliza”
“Kummaliza! Kivipi sikuelewi mama”
“Ashura alikufa”
Salome alianza kulia baada ya kusikia kuwa Ashura alikufa, kwakweli Neema alimshangaa sana mtoto wake na kuhisi kama kuna mchezo mbaya kachezewa mwanae,
“Mmmh wale wa maombi nao au wamefanya kitu kibaya kwa mwanangu”
Patrick aliamua kumkanusha Neema,
“Usiwaseme vibaya watu wamekuja kutusaidia, wameshasema kuwa kuna kitu hakipo sawa kuhusu mtoto wetu huyu sasa maneno ya nini. Mimi naona cha msingi labda tumpeleke Salome kule nilipokuwa naishi mimi labda ataweza kuweka kumbukumbu zake sawa na kuelewa kila kitu”
Neema aliona hilo ni wazo jema sana kwa wakati huo, kwahiyo akaenda kujiandaa kisha kuondoka kwenye gari na Salome ili wakamuonyeshe walipokuwa wanaishi.
 
Back
Top Bottom