Simulizi: Lisa

Simulizi: Lisa

LISA KITABU CHA SABA
SIMULIZI........................LISA KURASA......331 MPAKA 335
PRESENT: SIMULIZI ZA DULLY WHATSAPP: +255628924768

Sura ya: 331
Lisa alichokonoa masikio yake kwa vidole na kuhema. "Ninasikitika sana kwa kila mtu pia. Sikujua kwamba kurudi kwangu kungedhuru watu wengi, nitarudi na kufikiria njia zingine."
“Potelea mbali. Usirudi tena.” Mkurugenzi Gumbo alikasirika sana hata hakutaka kumuonyesha adabu yoyote. "Bila shaka, tunaweza kukupa nafasi ikiwa utapiga magoti na kuomba msamaha wa Bwana Kimaro na Bi. Njau."
"Hiyo haiwezekani. Ni afadhali kampuni isambaratike kuliko kuinamisha kichwa changu kwa wapenzi hao wasio na haya.” Lisa kwa ukaidi alisema hivyo na kuondoka huku kukiwa na shutuma za kila mtu.
Alipofika nyumbani, polepole alianza kutengeneza kikombe cha kahawa. Amba alikuwa kwenye hatihati ya kupiga magoti na kumlilia kumsihi ili akamwombe Alvin msamaha.

"Mwenyekiti Jones, makampuni ambayo yalikuwa yanaendelea kufanya kazi pamoja na kampuni yetu yanatishia kuvunja ushirikiano wao. Tafadhali fikiria kumuomba msamaha Bwana Kimaro...”
“Usiwe na haraka.” Lisa alikoroga kahawa yake. "Amba, ninakupa nafasi ya kuruka hadi kileleni sasa."
“Nafasi gani? Una uhakika haitanifanya niporomoke badala yake?” Amba alikuwa karibu kuachia machozi.
Lisa alimpiga jicho kali. Akatoa kadi nyeusi kwenye pochi yake na kumtupia. "Kuna shilingi bilioni sabini ndani yake. Baada ya siku mbili, nunua hisa zote kutoka kwa wanahisa wa Mawenzi Investments.”
Amba karibu adondoke magotini. "Mwenyekiti Jones, kwanini una pesa nyingi kiasi hiki?" Ilikuwa ya ajabu. Ni nini hasa kilikuwa kimempata katika miaka hiyo mitatu?
“Unataka kuchukua nafasi hii, au unataka kuniuliza maswali tu?” Lisa aliuliza.

"Ndio ndio ndio..." Amba alivutiwa kabisa.
"Kwa wakati huu, wanahisa lazima wawe na hofu. Ikiwa kuna mtu aliye tayari kununua hisa, bila shaka ataziuza kwa bei ya chini. Shilingi bilioni sabini za Kenya ni zaidi ya pesa za kutosha.” Lisa alimfafanulia.
“Lakini Bi. Jones, tukinunua hisa, utakuwa mwenye hisa pekee kwenye kampuni. Utakuwa na udhibiti kamili, ndiyo, lakini pindi Kimaro akikandamiza kampuni, Mawenzi Investments haitakuwa na mustakabali. Kwanini unataka kupoteza pesa hizi?”
“Nani alisema hakutakuwa na mustakabali?” Lisa alimtazama kwa pembeni. “Tayari nimewasiliana na kampuni za ujenzi. Ninachukua tu fursa hii kubadilisha muundo wa kampuni. Kuanzia sasa na kuendelea, sitaki kumsikiliza mtu yeyote ambaye anataka kwenda kinyume na mimi katika kampuni.”
Amba alishangaa. Hii ilikuwa mara ya kwanza kuhisi kwamba Lisa alikuwa tofauti na hapo awali.
•••

Usiku, wanaume kadhaa walikusanyika kucheza poker kwenye chumba cha hoteli ya nyota tano. Rodney alicheza kadi ya Mfalme, kisha akaanzisha mada. "Nilisikia kwamba wanahisa wa Mawenzi Investments wanauza hisa zao kwa bei ya kutupa."
Alvin alikuwa akigonga meza bila kujali. "Kuziuza ndio njia pekee ya wao kuzuia hasara zao zaidi. Kampuni hiyo ni lazima ifilisike kabisa. Hakuna mtu anayeweza kumuokoa Lisa wakati huu.
Chester aliwasha sigara. “Hebu fikiria, si umekuwa ukihisi hatia tangu alipokufa kwa miaka hii mitatu? Amefanya nini tena kukukasirisha?”
Vidole vya Alvin vikawa ngumu. Baada ya muda, alisema, “Alinitishia kwa kutumia cheti cha ndoa. Ana hamu ya kifo."
“Huogopi kwamba akikutishia tena, Sarah ata...”
“Haina maana. Hakika ninampa somo muda huu,” Alvin alisema. “Na hana pa kutokea ila

kwa kunidondokea na kuniomba msaada wangu.”
"Nilisikia kwamba maeneo muhimu ya ujenzi chini ya Mawenzi Investments yameacha kufanya kazi kwa siku tano. Wamepoteza zaidi ya dola bilioni. Watu wengi walionunua nyumba hizo wanadai kurejeshewa fedha.” Rodney alicheka na kucheza karata yake ya mwisho. "Nimeshinda. Lipa."
Wakati Alvin akitoa pesa zake nje, alitazama simu yake iliyokuwa kando yake bila fahamu. Je, mwanamke huyo hakuwa tayari kupiga simu kuomba msamaha na kukubali makosa yake bado? Hata hivyo, kuomba msamaha ingekuwa bure sasa. Lisa hakupaswa kamwe kumuumiza Sarah.
•••
Kesho yake asubuhi, nyumbani kwa Alvin, wajakazi walitoa kifungua kinywa kwenye meza. Sarah alimimina glasi ya maziwa ya moto kwa Alvin kwa furaha, kisha akasema kwa kusitasita, “Tayari ni siku ya sita. Nadhani Mawenzi Investments inapaswa tu uisamehe Hubby.”

Macho meusi ya Alvin yalimtazama. "Wewe ni mtu mpole sana."
Sarah alicheka kwa uchungu. "Nimefanya kazi huko kwa miaka miwili, baada ya yote."
"Wacha tupate kifungua kinywa." Alvin alimenya yai lililochemshwa kwa ajili yake.
“Alvinic,” Sarah alisema kwa hisia tofauti, “Je, kweli huna hisia na Lisa? Hujawahi kunisindikiza kwenda kununua chupi hapo awali. Nimekuwa nikijaribu kujishawishi siku hizi lakini bado ni ngumu kwangu kukubali. Kila nikifikiria jambo hilo, moyo wangu unauma sana hivi kwamba nashindwa kupumua.”
“Hapana.” Alvin alikanusha waziwazi. "Samahani. Sitafanya tena jambo lolote la kukuudhi.”
“Sawa,” Sarah alijibu huku akitabasamu kwa lazima.
Alvin alikuwa na hisia za huzuni moyoni mwake. Aliapa kumpa adhabu kali zaidi Lisa na kumtendea vyema Sarah.

"Bwana Kimaro, Hisa za Mawenzi Investments zilifikia kikomo mara tu soko la hisa lilipofunguliwa asubuhi ya leo," Hans aliingia ghafla na kusema kwa sauti ya chini.
“Ni nini kinaendelea?” Alvin alimtupia jicho kali.
Hans akapepesa macho. "Saa 7:00 asubuhi ya leo, Kilimani Group ilitangaza ushirikiano na Mawenzi Investments kwenye tovuti yake ya kimataifa."
Sarah alikuwa na hisia mbaya. "Kampuni ya Kilimani Group ni maarufu sana?"
Hans alielezea, "Kilimani Group sio maarufu tu, historia yao inarudi nyuma zaidi. Zaidi ya wasanifu mia moja wa juu kutoka kote Afrika Mashariki wamekusanyika hapo. Kampuni hii ndiyo kampuni ya ujenzi yenye mapato makubwa zaidi Afrika Mashariki na wana sifa kubwa. Kilimani Group imeshiriki katika takriban kila mradi wa kitambo ambao umesifiwa na watu kote hapa nchini na Afrika Mashariki kwa ujumla. Wakati huo huo, wasanifu wa Kilimani Group wamepokea tuzo zote za kimataifa kwa miaka kumi mfululizo.”

Mkono wa Sarah uliokuwa umeshika uma ulikaza, na yeye mwenyewe hakujitambua. "Kwanini kampuni kama hiyo ifanye kazi na Lisa? Hawaiogopi KIM International?"
Hans akatikisa kichwa. "Kilimani Group mara nyingi hufanya kazi na serikali kwenye nchi hizi za Afrika Mashariki. Hawaogopi mtu wala kampuni yoyote.” Alisita na kusema tena, “Zaidi ya hayo, kampuni ya Ruta Design, inayoongoza huko Uganda na yenye tawi lake Tanzania na hapa Kenya pia imetangaza kuwa wametia saini ushirikiano wa miaka kumi na Mawenzi Investments. Timu ya ujenzi ya Ruta Design iliwekwa kwenye saiti ya ujenzi ya Mawenzi Investments jana usiku.
“Ruta Design?” Sarah alishikwa na hamu ya kupiga kelele. "Hiyo ni kampuni gani ya uwongo? Sijawahi kusikia kabla.”
Hans alimtazama kwa kina. "Ingawa mkurugenzi wa Ruta Design, Joseph Ruta, ni kijana, aliwahi kuwa mmoja wa wasanifu watatu bora huko Uganda. Yeye binafsi alibuni hoteli moja na pekee ya nyota saba huko Uganda. Baada ya hapo, alianzisha kampuni ya usanifu. matawi ya kampuni yake yanaweza

kupatikana karibu miji yote mikubwa nchini Uganda, Tanzania na Kenya, na yanaendelea kwa kasi miaka hii. Lazima uwe umesikia kuhusu Mradi wa Kigamboni Satelite City huko Tanzania miaka miwili iliyopita. Ilifanyika kwa ushirikiano na Ruta Design, na likawa eneo la makazi lenye gharama kubwa zaidi nchini Tanzania. Bei yake ni shilingi 140,000 kwa kila futi ya mraba, na watu hata waliingia wazimu kuinunua.”
"Joseph Ruta ... Inaonekana hanifikii kwa chochote." Alvin alicheka, lakini sauti yake ilikuwa ya kujilazimisha kana kwamba chuki ilikuwa ikipita ndani yake. Wale waliokuwa wanamfahamu walijua ni ishara kwamba alikuwa na hasira.
Hans alimkumbusha kwa kuchanganyikiwa, “Bwana Mkubwa, hukumbuki huyu jamaa?”
“Unakumbuka nini?” Alvin aliuliza kwa ukali.
Hans alipumua. “Bi. Lisa alikuwa mfanyakazi katika Ruta Design hapo awali. Joseph alikuwa mwandamizi wake.”
Sura ya: 332

Alvin alipigwa na butwaa. Hakuwa na kumbukumbu yake hata kidogo.
Hata hivyo, kutokana na ugonjwa wake mara ya mwisho, alikuwa amesahau mambo mengi. Ilikuwa kawaida kwamba hakuweza kukumbuka.
"Sijawahi kujua ... Lisa alikuwa na mwandamizi kama huyo." Sarah alikasirika kiasi cha kutaka kutema damu. Hapo awali alifikiria kuwa angeweza kumwangamiza kabisa Lisa wakati huu. Hakutarajia kamwe Lisa kuhusishwa na kampuni kubwa kama hizo za ujenzi.
Mwangaza ulipita machoni pa Sarah. Alifanya kama alikuwa na wasiwasi na akasema, "Hata kama Joseph alikuwa mkuu wa Lisa ... hana uwezo wa kwenda kinyume na Alvinic. Angalia hadhi ya Alvinic.”
Uso wa Alvin ulibadilika sana. Hiyo ilikuwa sawa. Kwanini mtu asiyefahamika kama huyo aende kinyume naye kwa ajili ya Lisa?
“Lisa asingeweza kuuza mwili wake, sivyo?” Sarha alichombeza. Alvin alipomfikiria Lisa

kuwa karibu na mwanaume mwingine, alihisi wimbi la hasira isiyoelezeka.
Hans alikosa la kusema. Sarah alikuwa amebobea kabisa katika ustadi wa kuchomekea uchochezi kati ya watu. Hakupaswa kusema chochote.
“Chunguza ni nani hasa alinunua hisa za Mawenzi Investments kwa bei ya chini." Alvin ghafla akakumbuka kitu na kumuamuru Hans.
“Sawa.” Hans akaitikia kwa kichwa. Ilikuwa kazi rahisi. Alitakiwa tu apige simu idara husika ili kupata taarifa hizo. Muda mfupi baadaye, alirudi kwenye chumba cha kulia akiwa na habari kamili. "Watu waliokuwa nyuma ya pazia ambao walikuwa wakinunua hisa walikuwa Lisa na Chris Masunga."
“Ah!” Sarah akatoa macho. Haraka akawa ameelewa kitu. "Lisa alikuwa amepanga tangu mwanzo. Kwa makusudi aliwafanya wanahisa wa Mawenzi Investments kuingiwa na hofu na kisha akanunua hisa zao kwa bei ya chini. Sasa, Mawenzi Investments ni mali ya Chris na yeye. Chris anafanya kazi chini yake."

Mshindo ukasikika! Kijiko kilitupwa kwenye sahani na kikatoa sauti ya wazi na ya kutoboa masikio. Alvin alisimama mara moja na kukipiga teke kiti kilichokuwa mbele yake. Hah! Alikuwa amemchukulia poa kabisa mwanamke huyo. Hapo awali alikusudia kumwangusha bila huruma. Alvin hakuwahi kufikiria kwamba njia zake alizokuwa akizitumia kumwangusha Lisa ndizo zilizomnyanyua mwishowe.
Kabla ya hili, Alvin alikuwa amepoteza mabilioni kadhaa kuwahonga wanahisa wa Mawenzi ili wawe upande wake. Lakini, iliibuka kuwa Lisa alikuwa akinunua hisa za wanahisa hao wasimotii kimya kimya. Aliwaondoa watu kwenye kampuni hiyo ambao hawakufuata maagizo yake na akafanikiwa kuwa mtu pekee aliye madarakani. Thamani ya soko ya kampuni ingepaa kwa urahisi hadi kufikia makumi ya mabilioni kwa kuweza pia kupata ushirikiano wa makampuni yenye sifa nzuri. Lisa, oh Lisa! Alimshangaza sana!
Sarah alikasirika kwa siri kiasi kwamba alikaribia kusaga meno hadi yakavunjika. Hapo awali, alidhani angeweza tu kumfanya Lisa afe, kama miaka mitatu iliyopita. Hata hivyo, hakuthubutu tena kumdharau Lisa.

•••
10:00 asubuhi, Ofisi ya mwenyekiti wa Mawenzi Investments ilikuwa katika machafuko. Mkurugenzi Gumbo alivunja chombo kwa hasira. "Lisa Jones, unacheza na sisi? Kwanini hukutuambia kuwa tayari ulikuwa kwenye mazungumzo na Kilimani Group na Ruta Design tangu mwanzo? Umetutia hofu bila sababu na hata hisa zetu tukauza kwa bei ndogo. Matokeo yake, ulinunua hisa kwa bei nafuu. Wewe ni mkatili sana! Je, Sheryl alizaaje binti mpuuzi kama wewe?”
“Lazima uturudishe hisa zetu. Kama sivyo, haya hayatakuwa na mwisho.” Mkurugenzi Williams alipiga meza kwa nguvu.
“Nimeona sehemu yangu ya watu waovu, lakini sijawahi kukutana na mtu mbaya kama wewe. Mawenzi Investments ilianzishwa na sisi sote. Badala yake, unafanya chochote kinachohitajika ili kutuhadaa. Kama mtu, unapaswa kuwa na mapungufu fulani ya kimaadili.”
“Bibi mdogo, wewe bado kijana. Usiwe mkatili sana na usichome madaraja yako. La sivyo, ungekuwa umekufa kabla hujajua.”

Akiwa amekabiliwa na karipio na ukosoaji wa wanahisa wale waroho waliouza hisa zao, Lisa alikunywa kahawa polepole kabla ya kukiweka kikombe mezani kwa kishindo kikubwa.
Ofisi ilinyamaza kimya. Lisa aliinua kichwa chake. “Kila mtu anielewe, sikutaka kuwa mtu asiye na huruma lakini wakati wa mkutano wa kwanza niliporudi, niliwaambia nyote kwamba kampuni hii haikupewa jina la familia ya Kimaro. Hata hivyo, nyie bado mliwaabudu Alvin na Sarah kana kwamba ni mababu zenu. Siku chache zilizopita, Alvin na Sarah walikuwa wakinitusi kwenye ukumbi wa kampuni. Ninyi nyote wenye hisa mlikuwa kama mbwa wanaolamba miguuni mwao ili kuwafurahisha. Mliniambia hata nipotee. Kwa kuwa nyote mnapenda kuwalambalamba hao wawili, nendeni mkawatafute basi.”
“Tulifanya hivyo kwa sababu hatukutaka kuwaudhi na kupoteza nguvu ya kampuni. Ilikuwa ni kwa ajili ya kampuni,” Mkurugenzi Gumbo alisema kwa unyonge, “Kama ningejua kwamba tayari ulikuwa umepata kampuni za ujenzi, je, ningekosa aibu hivyo? Nilifanya hivyo kwa ajili ya kampuni."

"Hiyo ni sawa. Tumeifanyia kampuni mengi miaka hii mitatu. Ulikuwa wapi wakati huo?”
"Ikiwa hautaturudishia hisa zetu leo, usifikirie hata kutoka nje ya mlango huu."
“Kweli? Nataka kuona jinsi utakavyonizuia kuondoka.” Lisa alicheka. Ghafla, walinzi zaidi ya 20 waliingia na kuwazunguka wanahisa. Walipoona hali hii, zaidi ya nusu ya kiburi chao kilipungua.
Mkurugenzi Wande alifikiria kitu na kupiga magoti mara moja. "Lisa, tupe wanahisa huruma yako. Sisi ni wazee, tunataka tu kupata bonasi ili kujikimu.”
"Ndio, tutakusikiliza kuanzia leo."
"Tunapaswa kila mmoja kuchukua hatua nyuma na kuweka kipaumbele katika kuleta amani."
Lisa akasugua macho yake. Ilionekana kana kwamba walikuwa wakifanya hivyo kwa njia laini kwa sababu njia ngumu haikufanya kazi.

“Inatosha. Mkurugenzi Wande, ulienda hata kumpa Sarah zawadi jana. Na Mkurugenzi Williams, tayari wewe ni mzee sana, lakini hukuchoka kumfuatafuata nyuma Sarah kama mkia. Sijawahi hata kukusikia ukiiombea kampuni. Ulikuwa ukinifokea tu mbele ya Sarah muda mwingi.
“Si hivyo tu. Mkurugenzi Gumbo, nilikuwa nimeshachukua nafasi hii lakini kwa nini bado ulikuwa unaripoti mambo ya kampuni kwa Alvin kila siku bila kuacha chochote?” Lisa alimfichua kila mmoja wao. Nyuso zao zilikuwa na rangi nyekundu kwa aibu.Hakuna aliyetarajia Lisa kujua kuhusu mienendo yao waziwazi.
“Nimewafukuza nyinyi kutoka kwa bodi ya wakurugenzi kwa sababu mioyo yenu haipo hapa tena. Unataka tu kupata samaki wakubwa kama Alvin na Sarah. Unafikiri kila kitu kitaenda sawa mradi tu unawategemea, sivyo?" Lisa alisema kwa huzuni, "Kwenu, mimi ni mtu asiye na uaminifu wowote. Mnafanya jambo moja mbele yangu na jingine nyuma ya mgongo wangu. Sitaki kuwa na sauti nyingi katika kampuni. Nataka tu sauti yangu mwenyewe isikike. Kuanzia leo na kuendelea,

nyinyi hamtakuwa na uhusiano wowote na Mawenzi Investments. Usalama, wafukuzeni wote na msiwaruhusu tena katika siku zijazo."
Walinzi hao walichukua hatua haraka na kuwafukuza wanahisa wote.
Ofisi ikawa tupu mara moja. Chris alisema kwa hisia, “Lisa, unazidi kuwa mwenyekiti sasa. Una nguvu zaidi kuliko mama yako alivyokuwa wakati huo. Najiona duni ikilinganishwa na wewe sasa.”
"Mjomba Chris, kampuni itategemea mimi na wewe kuanzia sasa." Lisa alitabasamu.
Sura ya: 333
Wakati wa ukaguzi jioni, Lisa alipofika tu katika Idara ya Masoko, alimwona mwanamume akigeuka na kuondoka alipomwona.
"Meneja Halua, si vizuri kumkwepa mwenyekiti wa kampuni unapomuona, sawa?" Lisa alimwita kwa tabasamu la uwongo.
“Mwenyekiti... Mwenyekiti Jones, samahani. Kwa kweli sikukuona.” Meneja Halua alijikaza na kurudi nyuma kuomba msamaha.

"Macho yangu hayako vizuri sana."
"Nadhani sio macho yako tu ambayo hayako vizuri sana lakini mdomo wako pia." Lisa alitabasamu kwa kucheza na kusema, “Kwa mfano...
unajua sana kusema mambo ambayo ni ya uzushi.”
Miguu ya Meneja Halua ilikuwa ikitetemeka kidogo. Alikuwa amefikiria kweli kwamba Mawenzi Investments ingesambaratika au Lisa angefukuzwa nje ya kampuni. Lakini ikatokea ndivyo sivyo.
“Meneja Halua, umefukuzwa kazi. Ondoka mara moja. Ninaamini hutatilia shaka uamuzi wangu kwani tayari umeshapata mtu wa kukuunga mkono. Kampuni inayofuata hakika itakukaribisha." Baada ya Lisa kumnong'oneza sikioni, alipiga hatua za kifahari na kuendelea kuelekea Idara ya Masoko.
Meneja Halua aliuma meno. Aligeuka nyuma na kusema kwa sauti kubwa, “Kuna shida gani hata kama nikiondoka? Bi. Njau anakaribia kuwa mke wa mtu tajiri zaidi nchini Kenya.

Baada ya kuondoka mahali hapa, atanipanga kuingia KIM International.”
Wakati msaidizi wa Lisa, Amba alipokuwa karibu kumkemea, Lisa alimgonga begani na kumzuia. "Usipoteze nguvu na muda wako!"
Baada ya wao kuondoka, Amba alisema kwa hasira, “Mwenyekiti Jones, kwanini hukumfundisha somo?”
“Hakuna haja, nimeshafanya hivyo,” Lisa alisema kwa utulivu.
Nusu saa baadaye. Meneja Halua alikuwa karibu kuondoka baada ya kufunga. Hata hivyo, alipofika kwenye milango, kulikuwa na polisi wa kumkamata. “Kampuni yako imetoa ripoti polisi. Unashukiwa kufanya ubadhirifu. Tufuate kituo cha polisi.”
“Sikufanya hivyo! sitaki!” Meneja Halua alipiga kelele. Hapo awali wakati Sarah akiwa ni mwenyekiti, wale ambao walikuwa na msimamo kama wake wangeiba pesa, na kila mtu alifumbia macho. Katika kipindi hicho alipochukua upande wa Sarah, alikuwa ametapeli pesa nyingi sana kwa jina la

kampuni. Baada ya Lisa kuingia iliripotiwa kama kesi ya uchunguzi. Angelazimika kwenda jela.
“Acha kukurupuka. Tayari tuna ushahidi thabiti. Twende zetu.”
Meneja Halua alichukuliwa na polisi. Habari zilienea katika kampuni.
Amba alipojua jambo hilo, alikumbuka lile somo alilomaanisha Lisa.
•••
Jioni, gari la kifahari la lilisimama mbele ya jengo la kampuni ya Mawenzi. Lisa akaingia kwenye gari. Alipouona uso wa Joseph Ruta, ambao hakuwa ameuona kwa muda mrefu, alitoa tabasamu la kirafiki.
"Joseph, muda umepita."
Asingesahau kamwe kwamba alikuwa ni Joseph ambaye alimpa kazi wakati alipofungiwa na tasnia ya usanifu wa majengo huko Dar es Salaam wakati huo kutokana na hila za Jones Masawe. Hakutarajia kwamba wangefanya kazi pamoja tena baada ya miaka mitatu.
“Lisa, umekuwa mrembo zaidi. Ninakuona kwa mtazamo mpya.” Joseph alicheka. “Twende. Ili

kusherehekea ushirikiano wetu, nitakuandalia chakula.”
“Joseph, mimi ndiye ninayepaswa kukuhudumia. Kampuni yako ndiyo pekee nchini Kenya ambayo ingejitokeza kuniunga mkono,” Lisa alisema kwa unyoofu, “Wewe ndiye mfadhili wangu.”
"Watu wa nje hawajui utambulisho wako kama mkurugenzi wa muundo wa Kilimani Group." Joseph alitania.
"Tuendelee kuweka wasifu wa chini tu." Lisa alisukuma kidole kwenye midomo yake na kufanya sura ya kushangaza. Vicheko vilisikika ndani ya gari.
Saa moja baadaye, gari liliingia uani kwenye hoteli kubwa. Magari machache ya kifahari yalikuwa yameegeshwa uani. Lisa alifahamu hoteli chache zilizotoa huduma nzuri za chakula kama ile. Japo ilikuwa katika eneo lililojitenga, chakula chake kilikuwa na ladha nzuri.

Waliposhuka kwenye gari, kuna mtu alikuja kuwapokea. Alikuwa ni Sam Harrison. Lisa alishangaa kumuona pale maana kumuona Sam maeneo hayo pia ilimaanisha kuwa Alvin na genge lake wangekuwepo pia. Alijikuta anakosa raha ghafla maana kila alipokuwa na wakati mzuri basi Alvin angekuwepo tu ili kumharibia.
“Lisa nilikukumbuka sana. Njoo, nikukumbatie.” Sam alimlaki kwa furaha.
“Bwana Harrison...” Lisa alikunja uso kuonyesha kutofurahishwa kwake.
“Usinifikirie sana Lisa. Najua unahofia kukutana na Alvin na wengine,” Sam akaeleza haraka ili kusafisha hali ya hewa, “nilikuja Nairobi nna Bwana Joseph na hivyo nilimwalika kwa chakula hapa na marafiki zangu. Sikuwa naelewa kama nyie tayati mmekutana na angekuja na wewe hapa!”
“Basi itabidi niondoke, wewe mwenyewe unajua namna mambo yanavyokuwaga nikikutana na genge la Alvin.” Lisa alitoa wasiwasi wake.

“Usijali, mimi nipo nitasuluhisha hilo.” Sama alimtoa wasiwasi.
“Kwani....” Joseph alitaka kuongea kitu lakini kabla hata hajamaliza usemi wake, sauti kali ilisikika.
“Nyie...” Alvin akageuka. Alishangaa kumuona Lisa akitoka na kijana mtanashati. Mwanaume huyo alikuwa amevaa suruali ya jeans na shati la khaki. Nywele zake fupi zilikuwa zimekunjamana kidogo, na alionekana kama mtu mashuhuri—aliyekuwa na mvuto mzuri!
Kwenye mkono wa kijana huyo kulikuwa na mkoba wa wanawake wa rangi ya zambarau, na ni wazi ulikuwa wa Lisa.
Mwanamke huyo... Hawakuwa wametalikiana bado lakini tayari alikuwa akishirikiana na wanaume wengine. Ubaridi ulitanda kwenye macho meusi ya Alvin. Wakati huo, Lisa aliona kundi la watu pia. Alipepesa macho na kumtazama Sam bila la kusema neno. Sama aligusa pua yake kwa unyonge.
Sarah ghafla akasema, “Sam, marafiki uliosema unakuja kuwapokea sasa hivi walikuwa... ndo hawa?”

“Ndiyo.” Sam aliitikia kwa kichwa tu. "Lisa anafahamiana na Bwana Joseph Ruta. Nilikuwa nimepanga nikutane naye kwa chakula. Lakini najua wewe na Lisa hamna maelewano mazuri, kwa hiyo tutaondoka sehemu nyingine.” Akapunga mkono na kuelekea upande wa Lisa.
Cindy alisema kwa kusitasita, “Kwa kuwa kila mtu anamjua mwenzake, hakutakuwa na shida. Kwanini tusiende pamoja kwenye jumba la klabu? Tukiwa wengi zaidi ndivyo inavyopendeza zaidi.”
Macho ya kila mtu mara moja yalitua kwake. Chester alikunja uso huku Alvin akitabasamu. “Siyo jambo lisilowezekana. Inatokea kwamba nina kitu nataka kujifunza kutoka kwa Mkurugenzi Jones. Ulianza lini kupanga hila hiyo ya biashara ili kufufua kampuni licha ya kuwa katika hali isiyo na matumaini? Nadhani tukijumuika pamoja itakuwa vizuri zaidi.”
Lisa aliinua macho yake kwa uvivu. Alipotaka kuongea, ghafla alifoka. “Samahani, sikukusikia vizuri, ulikuwa unasema?"

Wakati kila mtu alipofikiri kwamba Alvin alikuwa karibu kuachia hasira yake kwa Lisa, ghafla alitabasamu. "Unafikiri kwamba hali yako itabadilika kwa sababu tu thamani ya soko ya Mawenzi Investments imeongezeka? Lisa, kukuangamiza ni rahisi kama vile kumkanyaga sisimizi chini ya miguu yangu.”
Lisa alisafisha sikio lake kwa kidole. "Nadhani sasa nimeelewa maneno yako, na ninakushukuru sana kwa kweli. Bila wewe kunipa changamoto nisingepata akili hii. Ningekuandalia chakula cha jioni ukipendacho kama shukrani lakini naogopa kundi hili la watu ulilofuatana nalo. Je, ninahitaji kuwahudumia pia? Hata nikiwa na pesa nyingi, hazikuanguka kutoka angani.”
Sarah, Chester, Rodney, na Cindy walichukulia maneno ya Lisa kama dhihaka kwao. Nyuso zao zilibadilika.
Chester alisema kwa sauti isiyo ya kirafiki kabisa. “Lisa, ni miaka mitatu imepita bado haujaonyesha maboresho. Umeuchoka ulimi wako?”
“Kwa kweli siwezi kuthubutu kuwaudhi nyie. Kazi yenu ni kuharibu tu makampuni ya watu wengine na kutishia kukata ndimi zao." Lisa

alishtuka na kutikisa kichwa. Akamgeukia Joseph na kusema, “Joseph, twende zetu.”
Joseph? Alvin alimtazama kwa ujeuri. "Wewe ni Mkurugenzi wa Ruta Design?"
Joseph alitabasamu kwa unyonge. Hakukubali wala kukanusha.
Alvin alitikisa kichwa na kusema kwa ukali, “Vema sana, wewe ndiye mtu pekee ambaye unathubutu kwenda kinyume na mimi katika Kenya yote.”
“Lisa nimetoka naye mbali. Kwake, siogopi vitisho vyovyote.” Joseph alitabasamu na kumgeukia Lisa ambaye alishikwa na butwaa. “Twende zetu.”
“Sawa.” Lisa aliondoka naye wakitembea sambamba.
Sura ya: 334
Wakiwa wanatembea kuelekea kwenye gari, mwanga wa mwezi uliwaangazia kana kwamba walikuwa wanandoa wakamilifu. Kifua cha Alvin kilihisi kana kwamba kuna mtu

amewasha moto ndani yake. Alikasirika. Sarah alimtazama na kukunja ngumi kwa siri.
“Um...mimi naondoka pia. Tuliahidina na Joseph kuwa na chakula cha jioni pamoja.” Sam aliondoka haraka baada ya kusema. "Sam hasomeki kabisa siku hizi," Rodney alisema kwa hasira na kuwageukia wenzake, "Bado tunaenda kwenye jumba la klabu kujiburudisha?"
"Inachosha kwenda kwenye jumba la kilabu kila wakati. Sarah, twende zetu nyumbani.” Alvin alifoka na kuingia ndani ya gari.
Muda mfupi baadaye, gari lilisimama mbele ya jumba la kifahari. “Unaweza kutangulia ndani. Nina miadi na mtu mwingine kujadili mambo kadhaa ya kikazi sasa hivi."
“Mbona sikusikia kuwa ulikuwa na miadi hapo awali?” Sarah aliuliza, nusu-utani.
"Nilisahau kukuambia kuhusu hilo hapo awali." Alvin aliwasha sigara. Alionekana kutokuwa na raha kabisa. “Usinisubiri usiku huu. Lala mapema.”

Sarah akauma meno na kujilazimisha kushuka kwenye gari. Alitaka kusema maneno machache zaidi lakini alichosikia ni exhaust ya gari tu.
Alikanyaga miguu kwa kufadhaika. Hakujua ni kwanini, lakini alikuwa na hisia kali kwamba Alvin alikuwa anaenda kumtafuta Lisa.
Nusu saa baadaye, gari la Alvin lilifika kwenye Hoteli ya Silverland.
Sam ndiye aliyependekeza waende hapo. Sam aliipenda baa hii zaidi katika Nairobi nzima ndiyo maana Alvin alijua kulikuwa na nafasi kubwa sana ya kuwakuta hapo.
Alipousukuma mlango na kuingia ndani, sauti ya kupasua anga ilisikika ikiimba.
'"Ingawa rohoni nimekwisha....
Namuomba Mola anisaidie... Niweze kukusahau kabisaaa ...
Nipate mwingine kushinda weweee "

Alvin akatazama katikati ya ukumbi wa baa. Mwanamke kijana mwenye nywele ndefu zilizomwagika alikuwa ameketi kwenye kiti kirefu. Kichwa chake kilikuwa chini na alikuwa akiimba kwenye kipaza sauti. Alikuwa amevaa suruali ya jeans ya buluu. Mguu wake mmoja uliegemea kwenye kiti kirefu huku mguu wake mwingine ukigusa chini. Alikuwa amevaa jozi ya viatu vya turubai vyenye rangi nyeusi na nyeupe ambavyo vilifichua sehemu ya vifundo vyake vya mguu vilivyo maridadi.
Mwangaza hafifu wa taa za rangi ulioanguka juu yake ulikuwa kama maua ya waridi yaliyochanua usiku. Alishika gitaa la acoustic na kutekenya nyuzi zake kwa vidole vyake vyembamba.
Wanaume walivutiwa na uzuri wake. Wanawake walipiga mayowe kwa sauti nzuri iliyomtoka.
"Kila mtu, wacha tuimbe pamoja." Lisa alisimama kutoka kwenye kiti kirefu. Kasi aliyokuwa akiipiga gitaa ilikuwa inaendana na kasi ya wimbo. Ujuzi wake haukuwa mkubwa sana na wala si duni sana, lakini wimbo ulivutia sana.

Banio la nywele lilitoka nyuma ya sikio lake na nywele zikasambaa kufunika uso wake mzima. Alizirudisha nyuma kwa kutingisha kichwa chake, akifunua uso wake wa kushangaza na wa kuvutia. Uso huo mdogo uling'aa chini ya mwanga hafifu wa rangi, na ilikuwa kana kwamba nyota bilioni zilikuwa zikimulika machoni pake.
Miguu ya Alvin ilikuwa imekwama palepale. Lisa alionekana kama amesimama kwenye jukwaa la tamasha. Mwili wake mzima ulionekana kung'aa. Hakujua kuwa uimbaji wake ulikuwa wa sauti na ustadi zaidi kuliko hata baadhi ya wasanii maarufu. Hakujua kuwa Lisa ndiye alikuwa mwalimu wa Cindy enzi hizo wakiwa shule ya sekondari, akimfundisha kuimba na kumtungia nyimbo pia. Hakujua kuwa angeweza kucheza gitaa pia. Hakuwahi kugundua kuwa anaonekana mrembo sana alipotkuwa akiimba na kucheza jukwaani huku akitabasamu.
Moyo wake ulipiga kwa nguvu. Wimbo ulipoisha, akabaki akitamani zaidi. Sio yeye tu, bali watazamaji wote walihisi vivyo hivyo.

"Msichana mzuri, uimbaji wako ni mzuri sana. Imba wimbo mmoja zaidi!”
"Ni kweli, unaimba vizuri zaidi kuliko hata wale waimbaji kwenye matamasha ya moja kwa moja."
“Msichana mzuri, mimi ni meneja katika kampuni ya muziki. Unataka kusaini mkataba na sisi?"
“Hakuna haja, naimba kwa ajili ya kujifurahisha tu. Nimechoka, hivyo nitapumzika kwanza.” Lisa alishuka kutoka jukwaani. Ngazi za jukwaa zilikuwa za juu sana, na Joseph akaenda mara moja ili kumsaidia kushuka.
Tukio hilo lilimchoma macho vibaya sana Alvin. Watu waliokuwa karibu nao walianza kunong'ona.
“Huyo lazima awe mpenzi wake. Ninamuonea wivu sana kwa kuwa na pisi kali kama hii, utasema ni mungu wa kike!”
"Ndio, sura yake inaonekana nzuri sijawahi kuona! Kwanini sina bahati kama hiyo?"

Alvin akakunja uso. Alitembea kwa hatua ndefu. Wakati Lisa, ambaye ndo kwanza alikuwa ameketi tu anainua glasi yake ili kunywa mvinyo wake, nguvu kali ilimrudisha nyuma kwa ghafla. Mvinyo mwekundu kwenye glasi ulimwagika kote kwenye fulana nyeupe kifuani mwake.
Sehemu ya shati lake iliyolowa sana ilinasa kifuani mwake, ikionyesha mikunjo yake ya kuvutia na mistari iliyofifia chini.
Lisa alipiga kelele. Aligeuka nyuma kwa hasira na kumuona Alvin akiwa na sura yenye hasira na nyororo. "Alvin, una wazimu?"
Baada ya kumkazia macho, kwa haraka Lisa alichukua kitambaa ili kufuta madoa kwenye shati lake. Hata hivyo, haijalishi aliifuta kwa bidii kiasi gani, bado ilishikamana na kifua chake kwa nguvu. Ilifanya hata matiti yake kuonekana kwa mbali kupitia kitambaa laini cha fulana kilicholowa.
"Vaa hii." Mara moja Joseph alivua shati lake la khaki na yeye akabaki kwenye fulana ya ndani. Alitaka kumfunika Lisa, lakini mikono mikubwa ya Alvin ilimzuia kufanya hivyo. Macho ya kina Alvin yalikuwa yakimtazama kwa onyo.

“Bwana Kimaro, si tayari una mpenzi wako? Unaingilia mambo mengine ambayo hayakuhusu kwanin?” Joseph alitabasamu kwa utulivu.
"Unapaswa kumuuliza Lisa kwanini ninaingilia mambo yake." Alvin akalishika lile shati la Joseph na kulitupa huko. "Tuondoke!"
Alipokuwa akiongea, macho yalimtoka Lisa na kuyafanya macho ya Alvin yakawa na joto. Hakuwahi kutarajia kuwa Lisa angekuwa mrembo kiasi hicho. Akikumbuka kuwa ni yeye ndiye aliyenunua nguo za ndani alizovaa chini, hisia zisizoelezeka zilijaa moyoni mwake.
"Ni bahati mbaya gani niliyopata katika maisha yangu ya mwisho kwamba nililazimika kukutana nawe katika maisha haya?" Sauti yake ya kiburi ilimfanya Lisa kuhisi hasira kali.
"Hilo ndilo ninalotamani pia kujua." Alvin aligundua kuwa mikunjo ya kifua cha Lisa bado inaweza kuonekana kwani fulana yake ilikuwa bado imeshikama na mwili.

Alivua shati lake badala yake na kumlazimisha alivae. Lisa aligoma. Ghafla Alvin alihisi kukasirika na kumsaidia kumvalisha kwa nguvu. Ulaini aliouhisi chini ya mkono wake ulikuwa kama unyoya unaoufurahisha moyo wake.
Sura ya: 335
"Alvin, kwa nini umekuja?" Wakati Sam, ambaye alikwenda kujaza sahani nyingine ya nyama, aliporudi, macho yake karibu yadondoke kutoka kwenye soketi zake alipoona tukio hilo. Alitazama huku na kule kwa pupa na kushusha pumzi baada ya kuona yupo Alvin tu. Hakutaka kugongana na Rodney, Sarah, na wengine. Kulikuwa na kejeli zisizoisha kila walipokutana.
“Si nyie mlikuwa mkienda clubhouse? Si unaandamana na Sarah?” Sama aliongeza aliongeza maswali mawili zaidi.
Hilo lilifanya uso wa Alvin kuwa mweusi. “Kwanini uniulize hivyo? Ina maana Lisa hajakwambia japo mmekuwa kwenye ‘hangout’ kwa muda mrefu tayari?” Akageuza kichwa kuelekea kwa Lisa na kuinua macho yake. “Cheti chako cha ndoa kiko wapi? Si huwa

unatembea nacho kila mahali ili kunitishia? Kitoe na uwaonyeshe."
Lisa kidogo akose la kusema. “Huoni hata aibu unaposema hivi kwa sauti? Huoni aibu kwa kutamba na kuringa na mwanamke mwingine wakati kumbe unajua bado kwenye ndoa! Mbaya zaidi unafanya kazi pamoja naye ili kuniangamiza mimi na kampuni yangu. Aibu kwako."
“Unajua wazi kwamba sina hisia na wewe. Ni wewe ndiye unayening'ang'ania. Ulijaribu hata kumuumiza Sarah. Unastahili hayo yote! " Alvin hakuonyesha kujali maneno yake hata kidogo.
Sam alikuwa amemzoea, lakini Joseph alishangaa kusikia maneno yake. "Sikujua kwamba maneno ya mtu tajiri zaidi wa Kenya, Bwana Kimaro ambaye kila mtu anamheshimu, yangekuwa ya ajabu kiasi hiki."
“Unafikiri wewe ni nani wa kuninyooshea kidole?” Midomo myembamba ya Alvin ilionyesha tabasamu la kejeli. "Au unampenda?"

Joseph alisema kwa upole, “Kwani kuna shida gani nikimpenda? Lisa ni mzuri na mrembo. Maadamu yuko tayari na yuko huru kuolewa nami, ninaweza kumkubali wakati wowote, tofauti na mtu fulani ambaye ni kama mbwa kwenye hori.”
Lisa alishangaa, lakini alielewa mara moja alipomwona Joseph akipepesa macho kwa siri. Moyo wake ukapata joto.
Alvin alikunja ngumi. Hasira yake ilimfanya Sam ashuku kwamba angemrukia mtu sekunde yoyote.
Sam ilikwenda kati ya watu hao wawili haraka. “Alvin, tulia. Joseph anatania tu.”
"Sikuwa na mzaha hata kidogo." Joseph alifoka.
Alvin, ambaye alikuwa akichokozwa tena, alipunguza macho yake. Alidhihaki, “Mimi sina shida naye, ila ni yeye ndiye hataki. Ni yeye ambaye sasa anakataa kuachwa.” Baada ya kuongea alimvuta Lisa kwake na kumtazama kwa ukali. “Sema mawazo yako. Uko tayari kunitaliki?”

Lisa alitabasamu. “Niko tayari!”
Uso wa Alvin ukawa mgumu ghafla. Macho yake makali yalionekana kana kwamba alitaka kumla akiwa hai. Alikuwa amekataa kabisa kutiasaini hati za talaka siku chache zilizopita. Hata hivyo, kwa kuwa sasa alikuwa na mwanamume mwingine, alitaka kumwacha mara moja.
“Lakini si sasa,” Lisa aliendelea kusema, “Wewe na Sarah mlinitesa na kuyafanya maisha yangu kuwa magumu. Nimeirudi baada ya miaka mitatu, lakini bado Sarah ananifanyia mambo mengi ya kijinga. Mwambie aendelee kuota ikiwa anafikiri nitasalimisha cheo cha Bi Kimaro kwa urahisi hivyo.”
Joseph mara moja akammiminia glasi ya mvinyo na kumpa kwa hisia ya upendo. “Nitakuunga mkono hata ufanye nini, nitakusubiri."
"Asante." Lisa alikuwa karibu kupokea glasi ya mvinyo. Hata hivyo, alishushwa kutoka kwenye kiti na Alvin kabla hata hajaigusa.

“Tunaondoka sasa hivi.” Alvin aliamuru.
“Hilo halitawezekana. Maisha ya usiku ndiyo kwanza yanaanza." Joseph akamshika mkono mwingine Lisa.
“Muachie twende. Ukinisumbua, bado ninaweza kusababisha madhara kwa Ruta Design hata kama siwezi kuiharibu. Haijalishi uko katika biashara tofauti,” Alvin alionya.
Macho ya watu hao wawili yaligongana. Lisa alimgeukia Joseph kinyonge na kusema kwa sauti nyororo, “Joseph samahani. Nitakuhudumia kwa chakula kingine wakati ujao.”
“Hauruhusiwi kula naye tena,” Alvin alitamka onyo lingine.
Joseph alicheka na kupuuza maneno ya Alvin. “Sawa, wakati ujao. Kuwa mwangalifu na unipigie ikiwa chochote kitatokea. Nitakuwa kando yako daima.”
“Asante—” Lisa alikuwa bado hajamaliza kuongea aliponyanyuliwa na kuwekwa kwenye mabega ya Alvin na kutoka nje.

Sam alimpa Joseph ishara ya dole gumba. “Unashangaza. Unathubutu kwenda kinyume na Alvin waziwazi. Huna hofu naye?”
“Niko kwenye biashara ya huduma na yeye yuko kwenye biashara za bidhaa. Hata kama anataka kuniangamiza, itachukua mipango fulani na muda mrefu. Haitakuwa rahisi hivyo.” Joseph aliinua mabega yake kwa utulivu.
"Ni mbaya sana kama utakuwa unamwigizia tu?" Sam alionyesha wasiwasi.
“Kwanini unasema naigiza? Sionekani kuwa serious kuhusu hilo?” Joseph aliinua nyusi zake kwa namna ya kutania.
Sam alishikwa na butwaa. “Hapana... Ina maana uko serious kabisa?”
"Wanaume siku zote hutamani wanawake warembo," Joseph alisema huku akitabasamu, "Ingawa najua kuwa siwezi kuwa naye, haibadilishi ukweli kwamba anaweza kuwa mpenzi wangu."
•••

Lisa alitupwa ndani ya gari na Alvin. Alipoanguka, ni kana kwamba viungo vyake vilikuwa karibu kuvunjika pia. Kiatu kimoja kwenye mguu wake kilianguka nje ya gari alipotupwa kama furushi.
“Kiatu changu...” Lisa alinyanyuka kukichukua lakini alimsikia tu Alvin akifunga mlango kwa nguvu. Mlango ulifungwa haraka, na hakuweza kuufungua hata alipojaribu kiasi gani.
Alvin akaketi kwenye kiti cha dereva. Akakanyaga moto na kuondoka kwa kasi.
“Alvin, simamisha gari. Kiatu changu kilianguka." Lisa alimsogelea na kumvuta.
“Usijaribu kunihadaa. Najua unataka tu kurudi kumtafuta Joseph, sivyo?” Alvin alikuwa na moto mkali ndani yake."Lisa Jones, kwanini wewe ni mtu mbaya hivi? Nilikuwa nikishangaa jinsi ulivyoweza kusaini ushirikiano na Kilimani Group na Ruta Design, na ikawa kwamba ulitegemea sura na mwili wako. Huna aibu?”
"Unasema nini?" Lisa alikodoa macho.

Alvin alidhihaki, “Unahitaji maelezo ya wazi kutoka kwangu? Kwa uwezo wako ninaoujua mimi, Kilimani Group ingeweza kufikiria hata Mawenzi Investments ikiwa hukuwa na maelewano yaliyo kinyume na maadili? Kweli una ujanja fulani juu ya mkono wako. Umemfanya Joseph akuangukie na hata hafikirii kuwa wewe ni mchafu.”
Lisa akashusha pumzi ndefu. Ingawa alijua kwamba hakuna maneno mazuri yanayoweza kutoka katika kinywa chake kibaya, alitaka kumpiga na kiatu chake hadi kufa kwa kumfikiria kwa mawazo hayo machafu.
Kwa kweli, alifanya hivyo. Haraka akavua kiatu kilichobaki kwenye mguu wake na kumpiga usoni bila kusita.
Alvin, ambaye hakufikiria kwamba Lisa angethubutu kufanya hivyo, aligongwa moja kwa moja usoni na soli ya kiatu chake. Gari hata lilitikisika kidogo kwa kukosa udhibiti kwa muda
"Lisa, nadhani lazima uwe umechoka kuishi." Alinyakua kiatu na kukitupa nje ya dirisha kwa

hasira. Ikiwa asingekuwa akiendesha gari wakati huo, bila shaka angemfundisha somo.
"Nani alikuambia uniambie maneno machafu kama hayo?" Lisa alijisikia kuridhika ajabu alipoona alama ya kiatu kwenye uso wake mzuri. “Alvin, umepoteza viatu vyangu. Lazima unifidie kwa jozi nyingine."
Alvin alidhihaki, “Kwanini? Unataka nikufidie pea ya viatu uvae mbele ya Sarah na kusema nimekununulia ili umuumize? Lisa, una mipango mzuri sana ya kuudhi."
"Ikiwa hutaki kumuumiza, unapaswa kuniacha niende na usisumbuane nami hapa katikati ya usiku." Lisa alitazama mbele, na haikuonekana kama ilikuwa njia ya kurudi nyumbani kwake.
"Alvin, unanipeleka wapi?"
"Wanawake wasiofaa kama wewe ni afadhali wafungiwe tu ili usiniaibishe na kunidanganya." Lisa alihisi baridi ikifika kwenye mifupa yake. “Unanifungia tena?”
"Umejitakia hili," Alvin alijibu.

TUKUTANE KURASA 336-340
ONYO: Ni marufuku kusambaza, kukopi wala kuuza kazi hii kwani endapo kama tutakubaini basi sheria itachukua mkondo wake (By: Official Dully)
 
LISA KITABU CHA SABA
SIMULIZI........................LISA KURASA......336 MPAKA 340
PRESENT: SIMULIZI ZA DULLY WHATSAPP: +255628924768

Sura ya: 336
Akikumbuka siku ambazo alikuwa amefungwa miaka mitatu iliyopita, Lisa alikimbia mbele na kushika usukani kana kwamba alikuwa mwendawazimu.
“Lisa, wewe ni kichaa! Achia usukani haraka...!” Alvin aliufungua mkono kumsukuma.
Lakini, Lisa wa sasa hakuweza kuzuiliwa kwa urahisi ikilinganishwa na miaka mitatu iliyopita. Usukani ulinyongwa bila mpangilio. Mmoja akinyonga kushoto na mwingine kulia. Hatimaye, Lisa aliuma sikio lake. Alvin aligeuza usukani ghafla na karibu kugonga kitalu cha maua kando ya barabara. Mguu wake ukaubana ili kukanyaga moto kwa nguvu.
"Lisa, acha haraka!" Alvin alishtuka baada ya kuona gari likipita juu ya vitalu vya maua, likielekea ukutani. Alvin, ambaye alikuwa amepagawa kwa maumivu baada ya kung’atwa, alishtuka. Haraka akakanyaga breki.

Lisa kwa siri alishika sehemu zake nyeti. Hilo lilimfanya Alvin alie kwa uchungu. “Alvin, sitaki tena kufungiwa na wewe. Wakati huu, tutakufa pamoja." Lisa alimtazama kwa macho ya kichaa na ya kizembe.
Alvin alishikwa na butwaa. Mshindo mkubwa ukasikika hatimaye! Kulikuwa na sauti kubwa ya mshtuko baada ya gari kugonga ukutani. Madirisha yalivunjwavunjwa. Mifuko ya hewa ya usalama ilitanuka na kubana pande zote mbili kwenye kiti cha dereva na abiria.
Alvin alihisi ubongo wake kupigwa na kusababisha mtikisiko. Alikuwa anahisi kizunguzungu. Wakati huo, aliona macho ya Lisa yenye kung'aa lakini meusi yakiwa yamejawa na furaha, kama fataki za rangi zikichanua kwenye anga la usiku lenye nyota. Alipotabasamu, mchiriziko wa damu ulitiririka kwenye paji la uso wake. Macho ya Alvin yalimtoka.
Kwa namna fulani, alihisi kama kitu kifuani kilikuwa karibu kupasuka kwa maumivu. Alihisi uchungu sana hadi hakuweza kupumua kawaida. Maumivu yalikuwa makali sana. Alihisi hata macho yake yakimsisimka kana

kwamba kulikuwa na majimaji yanayokaribia kutoka ndani yake. Ilionekana kama ... alitamani sana afe. Alikuwa amedhamiria sana kumfanya afe.
Alisikia watu wakipiga kelele kutoka nje ya gari.
"Ajali imetokea!"
“Pigia gari la wagonjwa!”
•••
“Beep, beep!” Sauti ya kidhibiti moyo ilisikika mfululizo. Alvin aliweza kusikia sauti ya kilio tu pembeni ya masikio yake.Alijitahidi kufumbua macho na kuuona uso wa Sarah uliokuwa na michirizi ya machozi.
"Alvinic, umeamka." Sarah akasimama mara moja.
Rodney na Chester waliingia kwa wakati mmoja.
Wakati akiwatazama, tukio la mwisho kabla hajapoteza fahamu lilimjia kichwani. Akafoka kwa silika, "Lisa yuko wapi?"

Uso wa Sarah wenye michirizi ya machozi ukakakamaa. Rodney alisema kwa hasira, “Bado una ujasiri wa kuuliza juu yake? Alvin, ulimdanganya Sarah eti una kikao lakini ulienda kumtafuta Lisa badala yake. Ulikuwa unajaribu kufanya nini? Polisi walikagua kamera za uchunguzi. Walisema nyinyi wawili mmegombana kwenye gari na ndio maana mlishindwa kulidhibiti gari, na kugonga ukuta. Ukweli kwamba alijaribu kukupokonya usukani ulipokuwa ukiendesha alimaanisha kwamba alitaka ufe. Polisi watamchunguza. Atahukumiwa atakapopata nafuu.”
Alvin alikuwa amebana midomo. Kwa namna fulani, tukio kabla ya kupoteza fahamu liliendelea kujirudia kichwani mwake. Macho ya Lisa yalikuwa yamechongwa sana akilini mwake.
"Alvinic," Sarah alimwita kwa sauti ya chini kwa koo kali.
Alirudi kwenye fahamu zake haraka. “Sarah, samahani...”

“Alvinic, kwanini ulinidanganya?” Machozi yalimtoka Sarah. “Alvinic, tumekuwa pamoja kwa zaidi ya miaka kumi. Ikiwa huwezi kumwacha Lisa, unapaswa... Unapaswa tu kurudi upande wake.”
"Sarah, unawezaje kusema hivyo?" Rodney alifoka. "Ukiniuliza mimi, nitasema wema wako unakuponza sana, Alvin. Je! unajua kwamba Sarah alikaribia kuzirai alipojua kwamba ulipata ajali? Amekuwa akikutunza bila kula wala kunywa. Amekungoja kwa muda mrefu sana. Ukimsaliti, nitakuwa mtu wa kwanza kuvunja urafiki na wewe.”
"Alvin, kwanini ulikwenda kumtafuta Lisa?" Chester alikuwa akimwangalia Alvin pia.
“Usimwulize maswali zaidi. Mwache apumzike vizuri,” Sarah alisema huku akimshika mkono Alvin. Macho yake yalijawa na dhiki.
Hatia ndani ya moyo wa Alvin ilizidi kuwa nzito. “Samahani, Sarah. Nitafikiria njia ya kupata talaka haraka iwezekanavyo. Hakika nitakuoa mwaka huu.”

“Sawa, nitakusubiri.” Sarah alishusha macho yake.
Alikuwa karibu kwenda wazimu kutokana na wivu. Kwanini Lisa aliendelea kumsumbua? Je, Lisa alilazimika kumlazimisha kufanya jambo la kutisha tena?
Kwa siku tatu zilizofuata, Sarah alimtunza Alvin bila kuondoka upande wake. Siku aliporuhusiwa, alimuona Lisa akishushwa na polisi wawili alipokuwa akishuka. Macho yao yakakutana.
Lisa alimkazia macho. "Alvin, unataka niende jela? Vibaya hivyo!"
Alvin alishikwa na butwaa. Sarah ambaye alirudi kutoka kuchukua dawa alifika na kusema huku akikunja uso, “Sio kwamba tunataka uende jela, lakini umevuka bahari safari hii. Alvinic karibu afe. Mbali na hilo, polisi wanafanya kazi zao kwa mujibu wa itifaki. Ulikiuka sheria kwa kumzuia dereva wakati akiendesha gari.”
"Hujui kwanini nilikuzuia?" Lisa alicheka. Macho yake mazuri yalikuwa tulivu na baridi.

Alvin alikunja uso, huku Sarah akiuzunguka mkono wake. “Alvinic, twende. Mpuuze.”
Kwa pembeni ya macho yake, Alvin alimuona Lisa akiingia kwenye gari la polisi. Alihisi kuudhika.
"Samahani. Lazima ufikiri kwamba mimi ni mbaya sana,” Sarah alisema kwa kujidharau, “ninaogopa sana. Tusipompa somo, ninaogopa kwamba atakuondoa wakati mwingine.”
“Usiongee ujinga.” Alvin akatikisa kichwa.
"Alvinic, kaa mbali naye. Siwezi kuvumilia maumivu ya kukupoteza,” Sarah alisema kwa huzuni.
"Hutanipoteza." Alvin alihema moyoni.
Baada ya dereva kumrudisha Sarah nyumbani, Alvin alienda kwenye kampuni. Alikuwa amechelewesha kazi nyingi sana siku alizolazwa. Alipoingia tu kwenye gari, alipokea simu kutoka kwa polisi. “Bwana Kimaro, samahani, lakini kuna mabadiliko katika kesi ya Bi. Lisa. Tafadhali njoo kituo cha polisi.”

Saa moja baadaye, Alvin alitokea kituo cha polisi. Kwenye kiti kilichokuwa nje ya kituo cha polisi, Lisa alikuwa tayari ameshamaliza duru yake ya mahojiano. Hakuwa na vipodozi vyovyote na alikuwa mtupu kabisa usoni. Nywele zake zilikuwa zimefungwa kwenye fundo moja, zikifunua uso wake mzuri na safi. Alionekana kama mwanafunzi wa chuo kikuu.
Hata hivyo, Alvin bado alikumbuka jinsi alivyoshika usukani na sehemu zake nyeti pia... F*ck, alikuwa na maumivu makali kwa siku chache.
“Habari! Tunakutana tena hivi karibuni." Lisa alimpungia mkono huku akitabasamu.
"Kuna nini?" Alvin alitembea kwa hatua kubwa.
Polisi walicheza rekodi. Sehemu ya mazungumzo yao kutoka walipoanza kurumbana ndani ya baa ya hoteli hadi kwenye gari ilichezwa.

Uso wa Alvin ukawa mkali. Mwanamke huyo alikuwa ameenda mbali na kurekodi wakati huo?
Polisi walisema, “Samahani, Bwana Kimaro. Ningependa tu kukuambia kwamba rekodi hii inajumuisha ushahidi kwamba ulikuwa unakusudia kumteka nyara na kumfunga Bi Jones. Ukweli kwamba Bi Jones alinyakua usukani unaweza kuhesabiwa kama jitihada za kujilinda na sio uhalifu.”
"Badala yake, ninaweza kukushtaki kwa kujaribu kuniteka nyara." Lisa alitabasamu, akionyesha meno yake meupe. "Oh, hata nilikuripoti kwa kutupa vitu nje ya dirisha wakati unaendesha gari."
"Nilitupa nini?" Alvin alishangaa. “Kiatu changu.” Lisa alimkumbusha. Sura ya: 337
Akili ya Alvin ilizunguka kwa muda. Muda mfupi baadaye, alirudi kwenye fahamu zake na kumtazama Lisa kwa hasira. Hata alitoa ripoti

juu ya jambo dogo kama hilo? Mwanamke mbaya kama nini!
Polisi alikohoa kidogo. "Aliripoti kwa polisi wa trafiki. Kulingana na sheria za trafiki, mmiliki wa gari atapata upungufu wa pointi mbili kwenye leseni yake na faini kwa kutupa vitu nje ya dirisha. Sawa, nyinyi watu tayari mnaweza kuondoka." Polisi walitaka tu Alvin na Lisa wapatane na kuondoka.
"Subiri, bado hajanifidia gharama zangu za matibabu." Kidole maridadi cha Lisa kilipita kwenye skrini ya simu yake na akaonyesha ujumbe kwa polisi. "Ada yangu ya kulazwa hospitalini na matibabu ilinigharimu shilingi milioni sita na laki nane."
Afisa wa polisi alihisi kuumwa na kichwa. “Kesi hii si rahisi kuhukumu. Iwapo nyote wawili bado mna mzozo, mnapaswa kuufikisha mahakamani. Hata hivyo, kuajiri wakili kutagharimu zaidi ya kiasi hicho cha fedha, kwa hiyo nashauri wote wawili msuluhishe suala hili nje ya mahakama.”
"Sawa, mradi tu Bwana Kimaro yuko tayari kunipa pesa." Lisa alimtazama Alvin huku

akitabasamu. Alionekana kama mbweha mjanja mbele ya Alvin. Aliufanya moyo wake kuwasha na kutamani kumpiga makofi machache kwenye uso wake.
"Pesa ni kitu kidogo tu kwangu, lakini kwanini nikupe?" Alvin aliuliza.
"Basi, naweza tu kupakia rekodi kwenye mtandao na kuwafanya wengine wasikie kwamba sio tu kwamba hatujaachana, lakini hata ulikuwa unapanga kuniteka nyara na kunifungia. Hilo lingependeza.”
Ilikuwa ni kama Lisa angeweza kukisia jibu lake kabla. Alvin alihisi kichwa chake ambacho kilikuwa kimepona, kinaanza kumuuma tena. "Lisa, kuna kitu kingine unachojua kufanya isipokuwa kunitisha?"
“Najua mambo mengine mengi. Unataka kujaribu?" Midomo ya Lisa ya rangi ya waridi yenye majimaji ilitabasamu na macho yake ya kuchecheza yakapepesa kwa namna isiyoeleweka. Alvin alichukizwa na mbwembwe na tabia yake ya kutaniana. Uso wake uligeuka kuwa mbaya.

Punde, gari jeusi lilikaribia. Joseph alishusha kioo cha gari na kumsalimia Alvin. Baada ya hapo, aliondoka na Lisa kwenye gari lake.
Alvin karibu kuwafuata kwa hasira, lakini alisimama alipokumbuka maneno ya Lisa.
“Alvin, bado umeniweka moyoni mwako...” Sauti ya mwanamke huyo ilisikika masikioni mwake. Akatoa sigara na kuiwasha kwa hasira. Ilikuwa haiwezekani. Alikuwa na Sara tu moyoni mwake.
10:00 Usiku.
Usiku ulikuwa kimya. Alvin alikuwa akiangalia ripoti ya maendeleo ya kampuni ya kipindi cha robo mwaka akiwa kwenye chumba chake cha maktaba. Sarah alikuwa amevalia kinguo laini cha kulalia chenye kutamanisha sana na kumkumbatia Alvin taratibu kwa nyuma. “Alvinic, umeshamaliza dawa. Hebu tujaribu.”
Mwili wa Alvin ulisisimka. Aligeuka na hakuweza kukataa alipomwona Saraha akimwangalia na kumsihi. “Sawa.”

Akiongea kimantiki, Alvin alikuwa na hisia kali kwa Lisa mara ya mwisho.
Hata hivyo, alipofika karibu na Sara, hakuna chochote alichohisi mwilini mwake zaidi ya baridi kali na mwili kupooza kabisa.
"Samahani, nadhani bado sijapona." Alvin alimsukuma kwa fujo. "Subiri kidogo tu."
“Ni ... ni sawa. Labda niilikuwa na haraka sana,” Sarah aliuma mdomo wake kwa kukerwa na kusema kwa sauti ya kutojiamini, “Ninaendelea kuhisi kukosa amani sana siku hizi tangu arudi Lisa. Nataka tu kwenda pamoja nawe ili moyo wangu uhisi raha.”
Alvin aliwasha sigara na kuivuta kwa kuchanganyikiwa. “Sarah, sielewi kwanini mimi pia niko hivi. Nikibaki hivi milele...”
“Hapana, hutafbaki hivi siku zote. Hata ukikaa hivi maisha yako yote, bado niko tayari kuwa nawe. Ninakupenda; mambo mengine si muhimu.” Japo aliongea maneno hayo ya kufariji, ubongo wa Sarah ulihisi kuchanganyikiwa. Mambo yasingeweza kuendelea kuwa hivyo yalivyo. Ilibidi atafute

haraka njia ya kuwa na mwanaume huyu peke yake.
"Samahani, Sarah." Alvin alijawa na hatia. Aliweza kuwa na hisia kali za
mapenzi alipokuwa na Lisa, lakini kwa nini hakuweza kuhisi hivyo alipokuwa na Sarah? Ingekuwa hiivyohivyo na kwa wanawake wengine pia au na ni Sarah tu ambaye hakuweza kumkubali?
Siku iliyofuata, akiwa njiani kuelekea kwenye kampuni, Alvin alimwambia Hans, "Niletee wanawake wachache na warembo hotelini leo usiku."
Miguu ya Hans karibu itetemeke, na akakanyaga breki. "Bwana Mkubwa, wewe-"
"Usiniulize chochote." Alvin alimkatisha.
Hapana, Hans alitaka kusema ni wanawake wangapi alitakiwa kumpelekea? Je, Alvin angeweza kumudu wanawake wengi hivyo?
8:00 usiku.
Hans alileta wanawake watatu ambao alikuwa amewachagua maalum.

Katika muda usiozidi dakika tano, wanawake hao watatu walifukuzwa nje kama mbwa. “Potelea mbali. Poteeeni nyote!” kishindo cha hasira cha Alvin kilisikika nje.
Hans aliwaondoa wanawake hao kwa haraka. Aliingia ndani na kumuona Alvin ameinama kichwa chini huku akiwa amekaa pembeni ya kitanda, mikono yake ikiwa hoi kwenye nywele zake. Alvin alikuwa akinung'unika, “Mbona iko hivi? Kwanini iko hivi...”
“Bwana Mkubwa, wewe... Uko sawa?” Hans aliuliza kwa wasiwasi.
Alvin alimpuuza na kumpita kwa hatua ndefu. Akaufunga mlango kwa nguvu na kutoka nje ya chumba cha hoteli.
Aliendesha gari kando ya barabara bila kujua alikuwa anaelekea wapi. Aliporudi kwenye fahamu zake, tayari alikuwa kwenye lango la jengo la nyumba ya Lisa, Karen Estate. Alisita kwa muda kabla ya kuegesha gari na kushuka.
Baada ya kuvuta sigara mbili, alimwona Lisa akitembea kutoka upande wake wa kulia. Alikuwa amevaa suruali nyeupe ya michezo na tisheti ya kawaida. Lilikuwa vazi la kawaida,

lakini liliangaza mitetemo ya vijana. Alikuwa ameshika mifuko miwili ya shopping mikononi mwake na amevaa earphone za Bluetooth. Labda kwa sababu alikuwa akisikiliza muziki mtamu kwenye simu ndo maana alikuwa akitabasamu kwa furaha. Lakini alichoongea hasa ndicho kilionekana kumfurahisha zaidi. Alvin aliweza kudaka maneno ya mwishomwisho kwa mbali;
“Mpenzi, pia nakukumbuka sana. Muah, ngoja nikubusu.”
Lisa alipomaliza kuzungumza, aliona kivuli kikimjia.
Alvin alikuwa akimwangalia kwa sura ngumu, na macho yake yalikuwa yakiwaka.
“Uko kwenye simu na nani? Joseph?” Alvin aliuliza kwa kuchanganyikiwa Hasa aliposikia akisema neno 'mpenzi' na akambusu mtu huyo upande wa pili wa simu. Alipofikiria kuhusu Lisa kuwa karibu sana na mwanamume mwingine, alikuwa na hamu ya kumnyonga.
Lisa alishtuka. Alikuwa akiongea na Suzie na Lucas. Asingeweza kamwe kuruhusu Alvin

kugundua kuwepo kwao. Angemsumbua mpaka mwisho wa dunia kama angejua uwepo wa watoto hao mapema vile.
“Ina uhusiano gani na wewe?” Lisa alitoa earphone kwa haraka na kutaka kukata simu. Hata hivyo, hakujua kwamba vitendo vyake vya kuhangaika vilimfanya Alvin ajisikie kuwa anajaribu kuficha kitu.
Alvin alimpokonya simu yake kwa hasira na kuweka simu kwenye spika.
“Joseph?”
“Alvin...” Moyo wa Lisa ulikuwa karibu kutoka kooni mwake.
Alitumaini kwamba Suzie na Lucas walikuwa na akili za haraka.
"Mjomba, Jotheph ni nani?" Sauti ya kitoto ilisikika kutoka kwenye simu.
Alvin alishikwa na butwaa. Hakutarajia kamwe kwamba ingekuwa sauti ya msichana mdogo. Zaidi ya hayo, sauti hiyo ilikuwa ikizungumza katika lafudhi ya kitoto. Inaweza kufanya mioyo ya watu kuwa laini.

Lakini, swali likamjia ghafla, kwanini Lisa alikuwa karibu sana na mtoto?
"Samahani toto. Wewe ni nani? Una uhusiano gani na Lisa?" Alvin alijaribu kupunguza sauti yake ili kuepusha kumuogopesha binti huyo.
Sura ya: 338
“Mjomba, mbona una mathwali meeengi kwani wewe polithi?” Suzie alisema bila furaha.
Alvin alikuna kichwa. Katika umri huo hakujua jinsi ya kuwasiliana na watoto hata kidogo.
“Alvin, nirudishie simu yangu.” Lisa alinyoosha mkono wake kumpokonya. Hapo hapo Alvin aliishika simu kwa mkono wake mwingine na kuinyanyua juu.
“Mjomba kwanini umeiba thimu ya Aunty Litha?” Suzie alisema kwa hasira.
"Shangazi?" Alvin alipigwa na butwaa. Kwa sababu fulani, ilionekana kana kwamba uzito fulani ulipunguzwa kutoka kifuani mwake. Alijisikia nafuu hadi rohoni. Alidhani Lisa tayari alikuwa ana mtoto na mwanaume mwingine.

"Hiyo ni thawa. Ulifikiri yeye ni mama yangu? Lakini yeye ni thawa na mama yangu pia." Suzie alianza kulia baada ya kusema hivyo.
Midomo ya Lisa ilitetemeka. Alishangaa sana hapo awali hata akasahau kwamba, ingawa Suzie alikuwa mvivu, alikuwa na akili ya haraka na malkia wa maigizo.
Alvin kwa kawaida alichukia sana watoto walipolia, lakini kwa namna fulani, alisikiliza kwa moyo mpole wakati msichana mdogo kwenye simu alilia. “Huna mama?”
“Thio hivyo. Mama yangu ni mkali thana kwangu. Yeye hunigombesha kila mara na hunikathirikia. Hanipi hata chokoleti. Shangadhi Litha ni tofauti. Yeye huninunulia chokoleti nyingi kila wakati. Nampenda thana. Lakini baada ya kwenda Afrika, hakuna mtu anayeninunulia chokoleti tena. Boo-hoo...”
“Mtoto mdogo, kula chokoleti nyingi ni mbaya kwa meno yako," Alvin alisema kwa upole.

Lisa alikosa la kusema. Je, Suzie alikuwa akimaanisha kwamba ampelekee chokoleti? Yule mtoto alikuwa na akili kweli.
“Meno yangu bado yapo vidhuri thana. Mjomba, una uhuthiano gani na Aunty Litha? Mbona unamthumbua?” Suzie aliuliza kwa hasira.
Alvin hakupata neno lolote la kumjibu. Ilionekana kana kwamba mazungumzo hayangeweza kuendelea tena.
“Mbona hujibu thwali langu?” Suzie alisema kitoto, "Yeye ni nani kwako?"
“Mtoto mdogo, nani kakufundisha maneno hayo? Wewe ni mdogo sana. Huelewi ulimwengu wa watu wazima.” Alvin alihisi kukereka na haraka akakata simu. Hii ilikuwa mara ya kwanza alihisi uchovu kwa kuzungumza na mtoto.
Lisa alichukua tena simu yake. Alvin aliuliza kwa hasira, “Ni mtoto wa nani huyo? Wazazi wake wanamlea vipi? Malezi yake ni mabovu sana.”

“Ndiyo, wazazi wake hawamfunzi kuhusu mambo haya.” Lisa alidanganya tabasamu na kusema, “Hasa baba yake. Ana mwanamke mwingine nje na mara nyingi hayupo nyumbani.”
"Baba yake si mwajibikaji kabisa." Alvin alimuonea huruma ajabu binti huyo.
“Ndiyo, kama wewe,” Lisa alisema, “Nilipokuwa ng’ambo, sikuweza kujizuia kukumbuka watoto tuliowapoteza kila nilipowaona watoto wa jirani yangu.”
Alvin alihisi kujaa ghadhabu. Alidhihaki, “Unajaribu tu kudokeza jambo fulani kunihusu. Kwanini tulifunga ndoa wakati huo? Ni wewe uliyekuwa umesisitiza kwa ujasiri kuolewa na mimi. Isingekuwa wewe kupanda kitandani kwangu, ningekupa nafasi ya kupata mimba?”
Lisa alitabasamu huku akimwangalia. “Niambie basi. Nilianzaje kupanda kitandani kwako?”
“Vipi bado unathubutu kunibishia? Hukunilazimisha kwa sababu uliongeza kitu kwenye kinywaji changu huko Dar es Salaam?” Alvin alimshutumu kwa ukali.

Lisa alitambua mara moja. Hali ya akili ya Sarah ilikuwa na nguvu sana hata kumbukumbu za Alvin ziliandikwa upya kiasi kwamba yeye mwenyewe hakuweza kuziona. “Kwa nini? Je, ulifikiri kwamba ningeisahau baada ya miaka mitatu?” Alvin alimdhihaki.
"Ndio, kumbukumbu yako ni nzuri sana. Nimechelewa, nataka kwenda kupumzika. Unataka kunifuata? Nani anajua, ninaweza kukuwekea kitu kwenye divai tena na kukulazimisha kupanda kitandani kwangu.” Lisa alitingisha mfuko wa plastiki alioushika. “Nimebeba mvinyo mwekundu humu ndani. Unataka kupata glasi pamoja na mimi?"
"Ni chafu." Alvin alimtazama kwa hasira. Kisha akageuka na kuondoka.
Lisa akatikisa kichwa bila kuongea. Alizunguka eneo lake kila siku wakati alikuwa na mwanamke nyumbani. Sarah lazima awe na wasiwasi.
Lakini, Lisa alipenda iwe hivyo. Kama sivyo, mpango wake usingewezaje kutekelezwa.

Baada ya Alvin kupanda gari, hakuwa na haraka ya kuwasha gari.
Alikumbuka sauti ya msichana mdogo kwenye simu. Ghafla alihisi hisia za kuumiza moyo.
Ikiwa watoto wao wawili wangekuwa bado hai, wangekuwa na sura gani? Hakika zingekuwa za kupendeza. Hata daktari alisema kwamba walikuwa mapacha. Katika miaka hiyo, hakuwahi kufikiria jambo hilo hapo awali. Hata hivyo, moyo wake ulikuwa na maumivu ghafla usiku huo.
•••
Akiwa kwenye jumba la kifahari la Alvin, Sarah alipokea picha chache kutoka kwa mpelelezi wake binafsi kwenye simu yake. Katika picha hizo, Alvin na Lisa walikuwa pamoja kwenye lango la jengo la makazi ya Lisa, kwenye eneo maarufu la Karen Estate.
Uso mzuri wa Sarah ulipinda kutokana na hasira na wivu. Asingeweza kuendelea hivyo. Ilibidi amshinde haraka Alvin.
Saa moja baadaye, Alvin alifika nyumbani kwa gari lake. Alipokuwa karibu kuoga, Sarah alimpelekea glasi ya maziwa juu ya ghorofa. "Alvinic, nimekutengenezea hii."

"Asante." Alvin alishusha yote ya maziwa tumboni mwake bila kufikiria tena. Hata hivyo, alipokuwa akioga, alihisi mwili wake ukizidi kukosa raha. Hata kuoga tena hakukuwa na maana.
Wakati huo, aligundua kinachoendelea. Mara moja alivaa na kutoka nje kwa kasi. Sarah akajitupa mikononi mwake. "Alvinic, nakupenda."
"Uliweka nini katika maziwa uliyonipa?" Alvin alimshika mkono huku macho yake yakiwa yamejaa hasira na kukata tamaa.
"Samahani, Alvinic. Sikutaka kufanya hivi.” Sarah akatikisa kichwa na kuanza kulia. “Lakini kwa kweli siwezi kukupoteza. Tangu Lisa aliporudi, unaendelea kurudi nyumbani usiku sana. Nataka tu kuwa na wewe. Ninaogopa sana kwamba atakuiba na kukuweka mbali nami. Alvinic, usiniache, nakuomba.”
Sarah alikuwa na taswira nzuri na ya kuvutia moyoni mwa Alvin muda wote. Huku akilia mbele yake, Alvin hakuweza kuelezea hisia aliyokuwa nayo ndani ya moyo wake.

Kulikuwa na hasira, ingawa. Huenda watu wengine hawakujua kuhusu hilo, lakini Sarah alikuwa anajua fika kwamba tukio hilo lilichukuliwa kuwa mwiko kabisa kwa Alvin, lakini, bado alifanya hivyo. Sababu kuu ikiwa hakumfanya ajisikie salama vya kutosha.
Alipokuwa akifikiria jambo hilo, ni kweli kwamba baada ya Lisa kurudi, Sarah alianza kumjali sana Alvin. Mbali na hilo, Sarah alikuwa amevumilia siku nyingi kwa sababu hakuweza kutosheleza hitaji lake la msingi. Kama binadamu, Alvin alisikitika, na moyo wake ukashuka. Hakuweza kujizuia kukataa ombi la unyenyekevu la Sara.
Alipoona kwamba alikuwa kimya, Sara alichukua hatua zaidi kuliko hapo awali. Japokuwa mwili wa Alvin ulikuwa unawaka moto, bado alihisi kuchukizwa na kuguswa na Sarah. Hakuweza kuvumilia tena na kumsukuma kwa nguvu. Sarah alianguka kwenye zulia kwa fujo.
“Sarah, samahani...” Alvin alipoona uso wake ukibadilika, alitikisa kichwa kwa kukosa raha. Aligeuka na kutoka nje ya chumba cha kusoma.

"Alvinic, subiri." Sarah alijitahidi kumfuata akiwa amevaa nguo zilizochafuka, lakini aliona tu mwonekano wa gari lake ukiondoka.
“Ah, Alvin, huna maana!” Sarah alikanyaga miguu yake kwa mshangao. Hakuweza kuamini. Tayari alikuwa katika hali hiyo isiyopendeza, lakini mwili wake bado haukuweza kumkubali. Kwanini? Ilikuweje akamfanya ahisi kuchukizwa hivyo? Hypnosis yake ilienda vibaya wapi?
Hata hivyo, mwili wake ukiwa katika hali hiyo, hangeweza kwenda nje kutafuta wanawake wengine, sivyo? Hapana, haiwezi kuwa. Hakuwa na uwezo wa kufanya ngono. Kutafuta wanawake wengine ingekuwa bure kwake pia.
Wimbi la wasiwasi lilimfunika. Hata hivyo... Vipi kama Alvin angeenda kumtafuta Lisa? Sarah alimpigia simu Rodney kwa haraka. Alimueleza kila kitu huku akilia.
Rodney alishtuka. "Nini? Alvin hawezi kufanya ngono?”

“Rodney, hayo tuyaweke pembeni. Haraka fikiria njia ya kumpata. Ninahofia kwamba kuna jambo litamtokea,” Sarah alisema kwa wasiwasi.
"Jambo ni kwamba, niko mbali na safari ya kikazi leo. Nitamwomba Chester amtafute haraka iwezekanavyo.”
“Haupo karibu?” Sarah karibu alitaka kutema damu. Huyo Rodney mjinga hakuwa na manufaa yoyote ilipofikia wakati muhimu.
Sura ya: 339
Usiku wa manane, gari lilitembea kwa kasi barabarani. Alvin alishusha madirisha yote. Upepo wa usiku wa baridi ulivuma, lakini haukutawanya joto katika mwili wake. Badala yake, alikuwa katika hatihati ya kuanguka. Hapana. Hii haikuwa nzuri. Uso wa Lisa uliangaza kwenye akili yake yenye giza. Alizidi kukanyaga moto.
Gari lilienda kwa kasi kuelekea Karen Estate. Akiwa ndani ya chumba chake cha kulala, Lisa hakujua kuwa kuna mtu alikuwa akimfikiria.

Alikuwa kwenye simu ya video na Suzie na Lucas. Kwa sababu ya tofauti ya wakati, bado ilikuwa mchana huko Marekani.
"Mama, kazi zako zimeendaje leo?" Suzie aliuliza kwa furaha, “Nilikusikia ukiita jina la Alvin, nikajua huyo ni baba yangu mchafu. Bila shaka, nisingemwambia mimi ni mwanao. Sitaki anirudishe na kumwacha mwanamke mbaya awe mama yangu wa kambo.”
“Koohkooohkoh...” Lisa nusura apaliwe na maji aliyokuwa akinywa. Binti yake alivyokuwa akiongea haikuwa kawaida. Ikiwa ni watoto wengine, wangekuwa na huzuni kwa nusu ya siku.
Hakuweza kujizuia kumkazia macho Lucas usoni mwake. "Mwanangu mpendwa, unaonaje?"
“Simpendi. Sitaki kuwa na baba asiyempenda mama yangu, usije ukamsamehe hata siku moja.” Lucas alifika moja kwa moja kwenye uhakika.
"... Pole, una hoja hapo." Lisa alishangazwa kwa siri na msamiati mpana wa mapacha hao.

“Mama, mimi pia simpendi. Hataniruhusu nile chokoleti,” Suzie alisema, “Tayari inatosha kuwa na mtu mmoja katika familia ambaye haniruhusu kula chokoleti. Ikiwa kuna mwingine, basi sitaweza kula chokoleti hata kidogo.
“... Ha, wewe ni mtoto mdogo mwenye akili sana.” Lisa alimsifia huku akihisi kuumwa na kichwa.
Wakati huo sauti ya mtu akigonga mlango ilisikika kutoka nje.
"Lisa, fungua mlango haraka." Alikuwa Alvin tena.
“Wanangu, kuna jambo la dharura limetokea. Tuzungumze kesho.”
"Mama, ni baba yangu mchafu alikuja kukutafuta tena?" Lucas alisema haraka,
“Hapana, byee...kesho!” Lisa akakata simu ya video. Aliuendea mlango lakini hakuwa na haraka ya kuufungua. “Alvin, unataka kufanya nini?”

“Acha kuropoka. Usipofungua mlango nitaupiga teke mpaka uvunjike.” Alvin alianza kuupiga mlango kwa mateke bila kukoma.
Lisa aliogopa kwamba angesumbua majirani saa za usiku sana, kwa hivyo alifungua mlango. Mara mlango ukafunguliwa, Alvin aliingia na kumfakamia. Midomo yake ilitua juu ya midomo ya Lisa kwa bidii.
Lisa alikuwa ametoka kuoga muda si mrefu uliopita na harufu hafifu mwilini mwake ikaingia puani mwake. Mawazo yaliyobaki ambayo Alvin alikuwa nayo yaliharibiwa kabisa. Wakati huo, Lisa alionekana kama kipande cha keki yenye ladha tamu kwake. Alikuwa anajaribu sana kujinasua lakini wapi.
“Alvin, unafanya nini?! Niache niende!” Lisa alishtuka sana. Aliweza tu kumsukuma mbali kidogo licha ya kutumia nguvu zake zote.
Uso wake mzuri ulikuwa umebadilika rangi na mwili wake ulikuwa joto kama mtu mwenye homa kali. Hakuhitaji maelezao. Aliwahi kujionea tukio kama hilo yeye mwenyewe na alikuwa akijua sana hali yake.

"Nakutaka." Alvin alimtazama kwa macho ya hamu.
“Umekuja mahali pasipofaa. Nenda kamtafute Sarah. Mimi—ah!”
Lisa alikuwa bado hajamaliza kusema wakati Alvin alimvamia kumbusu tena bila kumpa nafasi ya kuongea.
Usiku ukapita! Jua la asubuhi liliangaza kupitia madirisha. Lisa alifumbua macho kutokana na mwanga wa jua. Aligeuza kichwa na kumuona Alvin akiwa amelala fofofo. Alimwamsha kwa hasira.
Alvin ambaye alikuwa amelala fofofo, alikunja uso. Hata hivyo, hakufungua macho yake. Lisa alijitahidi kuinuka. Akaingia bafuni.
Alioga kwa maji ya moto kwa muda mrefu na akatoka baada ya nusu saa.
Alipofungua mlango wa bafuni, alimuona yule jamaa akiwa amekaa kitandani baada ya kuamka. Macho yao yakakutana. Alvin mara moja aliona michubuko kwenye shingo ya Lisa na sehemu ya kifua chake. Akashusha macho na kuona kitanda kikiwa kimevurugwa. Bado

aliweza kukumbuka kwa uwazi kilichotokea jana yake usiku.
Alikuwa amewekewa kitu na Sara kwenye mazima, kitu ambacho kililiamsha dude lake. Lakini alishindwa kabisa kumalizia mihemko yake kwa Sarah! Alikuwa mpenzi wake na mchumba wake. Ingawa alikuwa amefanya kosa, bado alimpenda na alikuwa tayari kumsamehe. Ni vile tu alihisi kichefuchefu kila alipomshika Sarah kwa nia ya kushiriki tendo.
Mwishowe alitoka nje na kuja kumtafuta Lisa bila kujizuia. OOh! Jamani, kwa nini imekuwa hivi? Sio tu kwamba alimkosea Sarah, bali hata alijirusha na Lisa?
Lisa aliutazama uso wake ambao ulionekana kuwa na maumivu kwa muda na kumuona akiuma meno muda uliofuata. Alimsonya kwa dharau na kumtupia taulo alilolishika mikononi mwake.
“Alvin, kwa hiyo haya ndiyo mapenzi uliyonayo kwa Sarah? Naweza kuhisi kinachoendelea.”
“Lisa acha kejeli zako.” Alvin alijibu. “Unafikiri nilitaka kufanya hivyo? niliwekwa dawa”

"Ha" Lisa alicheka. Kwa mara nyingine tena alidhihirisha upuuzi wake.
Yaani dawa awekewe na mwingine halafu zikapozwe na mwingine?
"Kwanini unacheka? Utakuwa ulifurahia sana janausiku, huh?” Alvin alikumbuka jinsi alivyokuwa akimpagawisha sana usiku wa jana. Alikuwaaa....aibu!
“Nimefurahi?” Lisa alikunuja mikono yake. Alionyesha alama za michubuko kwenye mikono yake iliyosababishwa na mtu huyo aliyemshika kwa nguvu nyingi. “Tafadhali, tazama hili. Nina michubuko mwili mzima. Ndugu, hujui hata kumpetipeti mwanamke kimahaba, yaani ulnachojua ni kuvamiana tu ngo’ombe? Pengine hata ngo’mbe ana nafuu. Usiku hukunitendea kama binadamu kwa kweli. Ninaweza kukushtaki kwa hili!”
Kuangalia michubuko hiyo, Alvin alibana midomo. Athari za kuomba msamaha zikamjaa.
“Una chuki gani na mimi hadi unifanyie hivi?” Lisa alizidi kulalamika. “Kwanini hukwenda

kumtafuta Sarah?” Lisa alijizuia kuonesha chuki machoni mwake.
Alvin alinyamaza kimya.
“Hauwezi... huna hamu na Sarah sasa?” Lisa akamsogelea hatua kwa hatua, akitabasamu. Baada ya jana yake usiku, alikuwa na alihisi hisia za ziada ya kuvutia kwake.
Utamu usiosahaulika wa usiku wa jana yake ulipita kichwani mwa Alvin. Hakuweza kusahau hisia hiyo hata wakati huo.
“Nimeelewa sawa?” Alipoona amenyamaza, tabasamu la Lisa likazidi kuongezeka.
"Unafikiria sana." Alvin alimpiga jicho kali ghafla. Maneno yake yalikuwa mabaya, kana kwamba yametiwa sumu. “Niliogopa kwamba ningepoteza akili jana usiku na kufanya jambo la kumuumiza Sarah. Anapaswa kutendewa vizuri na kutunzwa. Kwa upande wako, sijali unaumia kiasi gani."
"Ooh! Kumbe?" Tabasamu la Lisa taratibu likaganda.
Hakika huyu ndiye Alvin aliyekuwa anamfahamu. Siku zote alikuwa na njia ya

kugeuza uhalisia wa mambo ili tu kumfanya achukie.
“Wewe ni mke wangu wa jina tu. Kwa vile unakataa kuachia nafasi yako, basi inafaa utimize wajibu wako kama mke.” Baada ya Alvin kusema hivyo kana kwamba ni jambo la kawaida, alijisikia faraja. Hakuwa na chochote cha kuhisi hatia tena kwa Lisa.
“Unaweza kuthubutu kumwambia Sarah maneno haya?” Lisa aliuliza kwa kejeli.
Uso wa Alvin ulibadilika. Akamkazia macho. "Lisa, ikiwa utathubutu kufichua chochote kilichotokea jana usiku, nitakufanya ulipe."
"Alvin, katika hadithi ya 'Mkulima na Nyoka', wewe ni yule nyoka mwenye sumu." Lisa alijilaumu kwa kuwa mpole na kumhurumia Alvin jana yake usiku. Alipaswa kumfukuza na kumwacha ateseke na kufa.
Alvin alijiona kama amejidharaulisha, lakini hakuwa na jinsi. "Maadamu hausemi chochote, Sarah hatajua."

“Hakuna kinachoweza kubaki siri milele. Sarah atakaposikia kuhusu hili, mimi ndiye nitaonekana mbaya tena. Itakuwa kama mara ya mwisho uliponinunulia chupi. Sikusema neno lolote, lakini hukumwamini mwishowe?” Lisa alicheka na kuelekea mlangoni.
Alvin alishikwa na butwaa. Alikunja uso na kuuliza, “Bado unataka kukataa kuhusu hilo? Ikiwa hukusema lolote, Sarah alijuaje? Una maanisha Sarah alishirikiana pamoja na meneja huyo kunidanganya?”
“Nikisema ndiyo, utaniamini? Kati yangu na Sarah, hautawahi kuwa upande wangu.” Alisema hivyo bila kugeuka nyuma.
Sura ya: 340
Alvin alikuwa ametokwa na jasho jingi kwa shughuli aliyofanya usiku wa kuamkia jana yake, kwa hiyo alikuwa anajisikia vibaya mwili mzima sasa. Alitaka kuoga baada ya kuingia bafuni lakini hakuwa na taulo. Aliwaza na kuchukua taulo la Lisa tu.
Alikuwa kituko mbele zake mwenyewe. Hakuweza hata kuvumilia kutumia taulo la

Sarah kujifuta usoni. Hata hivyo, alipotumia taulo la Lisa, hakuhisi kuchukizwa hata kidogo. Kitambaa chake kilikuwa na harufu ya kupendeza, sawa na mwili wake.
Alipotoka bafuni, Lisa alikuwa amekaa kwenye sehemu ya kulia chakula, akiwa na pasta. Kulikuwa na yai la kukaanga pia kwenye pasta. Ilionekana kupendeza kwa kutazama mara moja tu.
Alvin, ambaye alikuwa amechoka jana yake usiku, mara moja alihisi njaa. “Kifungua kinywa changu kiko wapi?” Moja kwa moja akaketi kwenye kiti kilichokuwa kando yake na kuonekana kama alikuwa akisubiri mtu wa kumpatia kifungua kinywa.
Lisa alimtazama kwa uvivu. "Cha kwako? Ni nyumbani kwako hapa?" Hakuna mjakazi wa kukuhudumia kifungua kinywa hata ukisubiri milele hapa."
Matarajio usoni mwa Alvin yalionekana kupungua kwa kasi, badala ya hasira. “Lisa, nipo kwako sasa, sijali. Nina njaa, lazima unipikie kifungua kinywa sasa hivi.”

“Kwanini nikupikie? Unaweza kunishukuru ikiwa ningefanya hivyo? Sioni hata ukinishukuru kwa kukuokoa jana usiku.” Hasira ya ndani ya Lisa hatimaye ililipuka. "Unakula na kunywa vitu vyangu kila unapokuja hapa. Sio tu kwamba hulipii chochote, hata unaniingiza kwenye matatizo kila baada ya muda fulani. Potelea mbali!”
“Unathubutu kuniambia nipotee?” Mwale wa hasira ulitoka kwa Alvin.
“Nini tena? Unataka nikuambieje ili ujue namaanisha uondoke? Tatizo hujui hata lugha.”
Uso wa Alvin ulizidi kujawa na hasira. Kwanini hapo awali hakugundua kuwa Lisa alikuwa na mdomo mchafu? "Lisa, unatamani kifo?"
“Kwanini? Unataka kuniua? Niue basi. Nina maumivu mwili mzima hata hivyo.” Lisa akasimama. Macho yake mazuri, safi yalikuwa yakiangaza machozi. Alionekana mwenye huzuni.
Hasira kwa Alvin ilipungua ghafla. Hakuweza kustahimili kumuona akihuzunika namna hiyo.

Alikiri kuwa kweli alikuwa amevuka bahari jana yake usiku.
“Usilie. Si pesa tu...” Akatoa kadi ya benki kutoka mfukoni mwake na kumkabidhi. “Kanunue chochote unachotaka. Nataka tu nile sahani hii ya tambi."
“Sitaki. naumwa.” Lisa hakumtazama kabisa aliendelea kula pasta yake.
Alvin alitazama nyuma ya kichwa chake kwa muda. Alichukua uma kutoka jikoni na kula pasta pamoja naye.
"Alvin, huruhusiwi kula tambi zangu." Lisa alizuia uma wake. Macho yake mazuri yalikuwa yametoka kwa kung'aa. Midomo yake iliyovimba kidogo ilitiwa mafuta, lakini ilifanya tu midomo yake ionekane maridadi zaidi kama jeli.
Muonekano wake asubuhi hiyo uliufanya moyo wa Alvin kuwasha. Alijua kwanini midomo yake ilikuwa imevimba. Ni kwa sababu alikuwa ameibusu kwa vurugu jana usiku. Bado aliweza kukumbuka ladha ya midomo yake.

“'Nataka kula." Alvin alianza kumpokonya chakula.
Wale watu wazima wawili walikuwa kama watoto wanaopigana wao kwa wao. Yai liligawanyika nusu kwa nusu.
Wakati kulikuwa na ntambi chache zilizobaki, Lisa aliinamisha kichwa chake na kuzibugia zote. Baada ya kufaulu, aliinua kichwa chake kwa hasira, kana kwamba alikuwa mtoto aliyeshinda pambano.
Alvin alimtazama Lisa. Sura yake ya kitoto ilifanya moyo wake uende mbio. Aliguna na kusonga mbele bila fahamu, ambapo aliuma tambi iliyobaki ikining'inia mdomoni mwake. Alipoinama chini, midomo yake ikagusa midomo yake.
Macho ya Lisa yakamtoka. Kope zake nene zilipita kwenye ngozi ya mashavu yake, na macho yake safi yalikuwa yanawaka kama nyota angavu zaidi angani. Wakati huo, Alvin alihisi kitu kwenye ubongo wake.
Alitaka kushika nyuma ya kichwa cha Lisa na kumsogeza kupata ladha ya kile walichokuwa nacho jana yake usiku kwa mara nyingine tena.

Ghafla, kengele ya mlango ililia. Lisa alishtuka na kumsukuma Alvin pembeni. Uso wake ulitia haya kidogo huku akimkazia macho Alvin kabla ya kwenda kuufungua mlango.
Umbo la Chester refu na la kibabe lilisimama mlangoni. Mara macho yake makali yalipotua kwenye midomo ya Lisa, ghafla alihisi maumivu ya kichwa yakiongezeka. Baada ya yote, alikuwa na uzoefu pia.
“Ni kwa ajili yako. Tafadhali fanya haraka na uondoke. Sitaki kutuhumiwa kukutongoza tena.” Lisa aligeuza kichwa na kumwambia Alvin kwa madaha. Kisha, alichukua hatua hadi jikoni.
Alvin alipomwona Chester akiingia ndani, sura yake ikazama ghafla.
Hakuwahi kumuangalia Chester akiwa na macho kama hayo hapo awali. Ikiwa Chester asingegonga mlango muda huo, labda angekuwa kwenye sayari nyingine muda huo.
"Inaonekana nimekuja kuchelewa sana." Chester alikunja uso kidogo.

“Kwa nini uko hapa?” Alvin alishtuka ghafla. “Sarah...”
“Bado hajui. Twende zetu.” Chester akageuka na kutoka nje.
Alvin alimtazama Lisa aliyekuwa anaosha vyombo jikoni. Alitaka kusema kitu, lakini alipomfikiria Sarah, kichwa kilimuuma. Kwa hivyo, alitoka na Chester.
•••
Chini.
Alvin aliegemea ubavu wa gari huku Chester akimpa sigara. “Vema, kama Sarah asingelazimika kumpigia simu Rodney jana usiku, nisingejua kwamba hujawahi kumgusa Sarah kwa miaka mitatu iliyopita... Lakini hauonekani kama huwezi kufanya hivyo. ”
Alimzidisha ukubwa Alvin kwa sura ya ajabu machoni mwake, na Alvin akampiga jicho la onyo. “Unamaanisha nini siwezi? Naweza sana.”
"Basi, kwanini ulikuja kwa Lisa jana usiku? Humpendi Sarah?” Chester alishangazwa naye.

“Hata mimi sijui.” Alvin aliwasha sigara na kuivuta kwa muda mrefu. Alionekana mwenye huzuni kiasi fulani. “Ni ajabu. Kila ninapomgusa Sarah, ninahisi kukarahika moyoni. Ni sawa na wanawake wengine pia. Lisa pekee ndiye tofauti.”
“Inawezekanaje?” Chester aliinua kichwa chake na kuvuta pumzi ya moshi. “Najua una mysophobia. Unaogopa kwa sababu Sarah alikuwa...”
“Hapana, hapana.” Alvin alisema kwa kutatanisha, “Nimemwona daktari, na daktari amesema mimi ni mzima pia. Kwa kweli nilitaka kuwa na Sarah jana usiku. Nilijaribu, lakini sikuweza.”
Chester alirusha majivu ya sigara. “Hii ni mara yangu ya kwanza kusikia kitu kama hicho. Vipi kuhusu Sarah? Anakupenda sana. Ikiwa atagundua kuwa ulikuwa na Lisa jana usiku, atalia hadi kufa. Na wewe mbona hukukimbilia hospitali?”
Alvin alikuwa kimya. Kiukweli swali lile pia alilifikiria pindi akiwa ametulia, lakini kwa

wakati huo jambo lililokuwa akilini mwake lilikuwa ni Lisa. Hakufikiria hata hospitali.
"Inaweza kuwa hivyo ... haujamsahau Lisa?" Maneno ya Chester yaliufanya moyo wake kurukaruka.
“Haiwezekani. Ninayempenda ni Sarah."
“Unampenda Sarah, lakini huwezi kumgusa.” Chester aliuliza kwa mashaka. “Alvin huoni ajabu sana? Kabla ya ajali hiyo ya gari, ulionekana kuwa na wivu ulipowaona Lisa na Joseph Ruta wakiwa pamoja.”
"Mimi, wivu?" Alvin aliitikia kana kwamba nafsi yake imepondwa. “Mimi sina wivu. Sikutaka tu kudharauliwa.”
“Una uhakika kweli huna Lisa moyoni mwako? Ulikuwa unamfikiria nani ulipokuwa naye jana usiku?” Chester aliuliza kwa ukali.
Alvin alihisi kuridhika alipokumbuka kilichotokea jana usiku. Ilikuwa ni hisia ambayo hakuwahi kuwa nayo na Sarah. Alitamani hata kumbusu Lisa wakati anakula muda mfupi kabla.

"Chester, sijui nina shida gani." Alvin alikuwa na migogoro na huzuni.
Siku zote alikuwa wazi sana juu ya hisia zake. Alimpenda Sara, na alimchukia Lisa. Hata hivyo, sasa alikuwa amechanganyikiwa.
Kuona sura yake, Chester naye alikunja uso kwa wasiwasi. “Fikiria. Ingawa simpendi Lisa, hupaswi kuwaumiza wanawake wote wawili.”
TUKUTANE KURASA 341-345
ONYO: Ni marufuku kusambaza, kukopi wala kuuza kazi hii kwani endapo kama tutakubaini basi sheria itachukua mkondo wake (By: Official Dully)
 
LISA KITABU CHA SABA
SIMULIZI........................LISA KURASA......341 MPAKA 345
PRESENT: SIMULIZI ZA DULLY WHATSAPP: +255628924768

Sura ya: 341
Mara Rodney akapiga simu. “Chester, umempata Alvin? Ndege yangu ndo kwanza inatua Dar.”
Chester alitazama wakati. Ilikuwa saa 8:30 tu asubuhi “Rodney, inachukua saa saba hadi nane kuruka kutoka Paris. Je, ulikimbilia kurejea mara moja baada ya kupokea simu ya Sarah jana usiku?”
“Duh. Hukujibu simu zangu. Ikiwa nisingeharakisha kurudi, nini kingetokea kwa Sarah ikiwa Alvin alikuwa na mwanamke mwingine?”
"Nilikuwa kwenye upasuaji muhimu jana usiku." Chester akakohoa kwenye ngumi yake. "Hawezi kufanya hivyo hata hivyo, kwa hiyo huna chochote cha kuwa na wasiwasi kuhusu yeye. Atakuwa sawa baada ya dripu.”
Alvin ulitiwagiza huku akimwangalia Chester, ambaye alimpiga jicho na kumkonyeza.

Baada ya simu kukatika, Chester alishtuka akiwa hoi. “Unapaswa kufurahi kwamba Rodney si ndiye aliyekupata. Ikiwa Rodney ndiye angekukuta hapa, ungemweka Lisa katika matatizo makubwa.”
Wanaume hao wawili wakatazamana. Baada ya yote, wote wawili walijua hisia za Rodney kwa Sarah.
"Kuhusu Sarah ..."
"Hatajua lolote."Chester akafungua mlango wa gari, Alvin akaingia, gari ilipotoka tu jirani na hapo, Alvin akapokea simu kutoka kwa Sarah. “Alvin, uko wapi? Samahani. Sikukusudia kufanya hivyo jana usiku.” Sauti ya Sarah iliyokabwa ikatoka. “Ulienda wapi baadaye? Nilikuwa na wasiwasi sana hivi kwamba nilitumia usiku kucha kukutafuta.”
"Nilikuwa ... hospitalini nikitundikiwa dripu jana usiku." Hapo hapo Alvin aliingiwa na hatia aliposikia akilia.
“Kweli?” Sarah alinung'unika, "Nilikuwa na wasiwasi sana kwamba ungeenda kwa Lisa. Alvin, naogopa sana kukupoteza. Nakupenda."

"Najua, Sarah. Unapaswa kurudi na kupumzika. Bado nina kazi ya kufanya kwenye kampuni, lakini nitarudi nyumbani mapema alasiri.”
Bila kujua, Sarah alitoka nyuma ya lango la jirani huku akimbembeleza. Alipoona gari lake likiondoka, uso wake ulikunjamana kwa hasira. Baada ya kukata simu, alipiga kelele na kuvunja simu.
Alikuwa amekasirika kwa hasira. Ilimchukua juhudi nyingi kuongeza kitu katika maziwa ya Alvin, lakini baadaye ni Lisa Jones ndiye aliyefaidika mwishowe. Ilikuwa ngumu zaidi kwake kukubali kwamba Alvin alimdanganya tena. Kwanini alikuwa na hisia kwamba hakuwa na udhibiti tena?
•••
9:00 Asubuhi.
Lisa alikuwa amefungua mlango tu, tayari kwenda kazini, wakati Sarah mwenye nywele zilizochanganyikiwa alikimbia kama mwanamke mwendawazimu.
“Lisa Jones, wewe b*tch huna haya! Bibi wewe! Mshenzi wewe!” Alipiga kelele na kumpiga Lisa usoni, lakini, badala ya kumpiga

Lisa, aligonga mfuko wa taka uliokuwa mkononi mwa Lisa.
“Ni kwa ajili yako.” Lisa alimtupia lile begi la taka huku akitabasamu. Rundo la maganda ya matunda, mabaki ya karatasi, na mabaki ya chakula yalikuwa yametapakaa kila mahali mwilini mwa Sarah.
Sarah nusura atapike kwa harufu mbaya iliyotoka.
Aliondoa vitu hivyo kichwani mwake, lakini hatimaye, bado hakuweza kupinga kutapika kwa kuchukizwa na harufu kali.
“Mbona unatapika? Unaziona tishu zote hizo? Hizo ndizo mimi na Alvin tulitumia jana usiku.” Lisa alitabasamu huku akitoa kipigo baada ya kipigo.
Miaka mitatu iliyopita, Sara aligeuza maisha yake kuwa moto wa kuzimu.
Sara alikuwa amewaharibu marafiki na familia yake peke yake, lakini huyu hapa tena Lisa og. Mwanamke huyo alikuwa sasa, akiishi maisha ya utukufu.
Kila siku alipokuwa akiwaona Sarah na Alvin kwenye mitandao na vyombo vya habari,

hakutaka kitu zaidi ya kumsambaratisha Sarah.
Hivyo, hakuweza kueleza furaha aliyokuwa nayo kuona sura mbaya ya Sara ikidharirika.
Sababu pekee iliyomfanya ajilazimishe kumkubali Alvin jana yake usiku ilikuwa ni kumuona Sarah namna hii - akiwa na hasira na asiye na la kusema. Baada ya yote, aliona sura ya mwanmke huyo huyo mchafu ni chukizo tu mbele yake.
“Aah, wewe b*tch. Nitakuua!" Baada ya kukasirishwa, Sara alimkimbilia kama mwanamke mwendawazimu.
Hata hivyo, Lisa alimpiga teke tu hadi chini, na uso wa Sarah ukatua kwenye kitambaa.
Haikuwa na haja ya kusema jinsi tukio hilo lilivyompendeza. “Unadhani mimi bado ni mtu yule niliyekuwa miaka mitatu iliyopita? Sarah Njau sitasahau jinsi ulivyoniumiza miaka mitatu iliyopita.”
"Kwa hiyo? Anayempenda Alvin ni mimi!” Sarah alikuwa akijitahidi kuinuka. Alijua hafananishwi na Lisa na hakuthubutu tena

kutenda kwa pupa. “Lisa Jones, nitamwambia Alvin ulichonifanyia. Subiri tu uone atakushughulikiaje.”
“Hakika. Utamwambiaje?” Lisa alikuwa na tabasamu lisilo wazi usoni mwake. “Utamwambia kuwa mimi ndiye niliyekufuata na kukuambia kuwa alikuwa na mimi jana usiku na nilivua nguo zangu na kukuonyesha mikwaruzo ya mwili wangu? huo ndio mpango wako?"
Uso wa Sarah ulibadilika. Hakika huo ndiyo ulikuwa mpango wake.
Lisa alicheka. “Mbinu zitumike mara moja tu. Ulifikiri nisingeona baada ya kurudia mara nyingi?”
Kisha akatoa simu yake iliyokuwa kwenye rekodi, akaibonyeza na kumtumia Alvin. “Acha.” Sarah alijaribu kuinuka na kuikamata, lakini Lisa alikuwa ameshaiweka simu pembeni.
"Mbona unaogopa?" Lisa aliutazama uso wake wa rangi, na macho yake polepole yakageuka kuwa baridi. “Sarah, usifikiri kwamba sijui kwamba ulimlawiti Alvin kisaikolojia. Unaweza

kumdanganya ili akupende, lakini unapaswa kujua kabisa kwamba kila ulichonacho sasa kimeibiwa.”
Sura ya mshtuko ikaangaza machoni pa Sarah, lakini akatulia haraka.
“Sijui unazungumza nini. Mimi na Alvin ni wapenzi wa utotoni, na ananipenda kikweli.”
"Ndio hivyo? Unaweza kuendelea kujidanganya. Hypnosis inaweza kuharibu kumbukumbu na hisia za mtu, lakini sio milele. Lisa alitabasamu huku akinong'ona kwenye sikio la Sarah.
"Unamaanisha nini?" Matangazo ya wasiwasi katika moyo wa Sarah yalizidi kuwa na nguvu.
"Ina maana kwamba huenda alikupenda hapo awali, lakini vipi baada ya hapo? Unaweza kumdhibiti ili asibadili mawazo yake?” Lisa alitabasamu. “Ndio alikuwa na wewe moyoni japo ulikuwa umekufa, lakini bado nilimfanya anipende. Ninamjua na kuelewa ni aina gani ya mwanamke anayependa, na najua jinsi ya kufanya moyo wake upepee. Nina uhakika kwamba ninaweza kumfanya anipende tena.”

Uso wa Sarah ulibadilika mara moja. “Kwa hiyo huo ndo mpango wako. Acha nikuambie, unaweza kuendelea kuota!”
“Subiri tu uone. Angalau, alinipenda sana jana usiku.” Lisa alifungua kwa makusudi kitambaa cha hariri shingoni mwake, akifunua michubuko.
Wakati huo, Sarah alikuwa amekasirika sana hivi kwamba alikaribia kukohoa damu iliyojaa mdomoni. Hata macho yake yalikuwa mekundu kwa hasira. “Huna aibu. Ni mtu wangu!” Sarah alishindwa kujizuia tena na kumshika Lisa usoni. Alitaka kuiharibu sura yake mara moja.
Lisa alimkwepa kwa urahisi na kuziba pua yake. “Samahani, lakini ni mume wangu. Usiniguse. Unachekesha." Kisha, kwa sura ya kuchukia, akaingia kwenye lifti na kumwacha Sarah akipiga kelele peke yake kwenye korido.
Hata hivyo, muda si mrefu Sarah alichanganyikiwa, Alvin alipiga simu. "Sarah, ulienda kumtafuta Lisa?"

Sarah aliganda kwa muda kabla ya kuanza kulia. Mwitikio wake ulikuwa wa haraka sana. “Alvin, samahani. Kuna mtu nilimwomba anitafutie anwani ya nyumbani kwa Lisa, hivyo nikaenda kumtafuta lakini nilipofika nikakuona ukitoka kwake asubuhi ya leo. Siwezi kukubali kwamba ulinidanganya. Nahisi kupandisha kichaa!”
Moyo wa Alvin ulidunda kwa sauti ya yule mwanamke akilia. Kusema kweli, alipopokea rekodi kutoka kwa Lisa mapema, alishtuka. Hakutarajia Sara ambaye kwa kawaida alikuwa mpole na mwenye ufahamu angesema maneno hayo yasiyopendeza.
Ilimfanya ajiulize kama aliwahi kumlaani Lisa usoni kwa njia ile ile siku za nyuma. Hata hivyo, alipojua kwamba Sara alijua kuhusu uwongo wake asubuhi hiyo, aliaibika.
“Mbona hukuniambia moja kwa moja?” Aliuliza kwa shida sana.
“Sikutaka kwa sababu niliogopa kukupoteza...” Sarah alisema kwa uchungu. “Alvin, mimi ni mchafu na ninanuka sasa. Lisa alinitupia takataka zake zote na kunipiga mateke. Hata alisema atakuiba. Unaweza kuja kunichukua?”

“Sawa, nakuja.”
Alvin mara moja aliinuka kutoka kwenye kiti chake cha ofisi na kuelekea Karen Estate. Alipofika mlangoni, mara Sarah akaruka mikononi mwake huku akilia. Bado alikuwa amevaa nguo alizomwacha nazo jana yake usiku, lakini mwili wake ulikuwa umefunikwa na madoa ya mafuta na vimiminika vikali. Harufu ilikuwa ya kichefuchefu.
Alvin alikasirika. Lisa alikuwa amekwenda mbali sana.
“Uso wako... Nini kilitokea?”
“Alinipiga makofi mawili.” Sara alianguka mikononi mwake na kulia.
“Nitakupeleka hospitalini." Alvin alimpeleka haraka kwenye gari.
Sura ya: 342
Mawenzi Investiments. Saa 4:00 jioni
Lisa alipokea simu kutoka kwa Joel. “Lisa, siku hizi nimekuwa makini sana. Hatimaye

niligundua kuwa ni msaidizi wangu binafsi, Walter Maliga ambaye aliweka kitu kwenye chai yangu.” Joel alisema kwa upole, “Walter amekuwa nami kwa zaidi ya miaka kumi. Kwa kweli sikutarajia angehongwa na Nina.”
"Baba, pesa hufanya farasi kwenda. Hakuna kitu cha kushangaza kuhusu hilo.” Lisa alisema, “Nitakuja usiku wa leo na kutafuta mtu wa kumchukua Walter. Msifanye chochote kitakachowatahadharisha.”
“Sawa. Nitawaambia jikoni kuandaa
chakula zaidi usiku wa leo. Hujafika nyumbani hivi karibuni, na Baba anakukumbuka sana.”
"Nina shughuli nyingi hapa Baba." Baada ya Lisa kukata simu akapiga namba nyingine. "Nina kazi kwa ajili yako usiku wa leo."
Mtu wa upande wa pili alicheka mara moja. "Hatimaye sihitaji kumfuatilia huyo gaidi Hisan kila siku."
"Utapata siku ya kupumzika."

Saa 5:00 jioni, Lisa akiwa ameingia kwenye gari lake tayari kuondoka, ghafla palitokea vurugu nje. "Bwana Kimaro, huwezi kuingia."
Akiwa bado anashangaa, mlango wa ofisi ulipasuka ghafla, na Alvin akaingia ndani huku akiwa na jeuri na hasira. Walinzi kadhaa nyuma yake walisema kwa hofu, “samahani, Mwenyekiti Jones. Alilazimisha kuingia ndani. Hatukuweza kumzuia hata kidogo.”
“Ni sawa. Mnaweza tu kwenda nje.” Lisa alipunga mkono. Alijua Alvin alikuwa na uwezo gani. Sio watu wengi waliolingana na ustadi wake wa ajabu. Hata hivyo mara baada ya kusema hivyo, Alvin alimsogelea na kumshika kola. Kisha akamvuta kama kifaranga kidogo. Sauti na macho yake yalijaa hasira.
"Lisa Jones, una ujasiri mwingi sana sasa, huh? Unathubutu vipi kumpiga Sarah? Umesahau onyo nililokupa asubuhi ya leo? Kwanini unalazimika kumuumiza Sarah tena na tena na kuvuka mipaka?”
Lisa aliinamisha kichwa chake kwa utulivu. “Si nilikutumia rekodi? Yeye ndiye aliyekuja kwangu kwanza.”

“Lakini hukupaswa kumtupia takataka. Hata umempiga usoni.”
Alvin alitamani sana kumsababishia majeraha yale yale mara baada ya kuufikiria uso wa Sarah uliovimba. Hata hivyo, alipouona uso mzuri wa Lisa kwa mbali zaidi, kwa namna fulani hakuweza kujizuia kuchukua hatua.
“We unafikiri hapo nilimpiga?” Lisa akawaka kwa hasira. “Mbona nilimgusa tu! Ajichanganye tena siku nyingine kujiingiza kwenye anga zangu ndiyo atajua kuwa mimi ni msukuma niliyekulia uchagani!”
“Acha kujifanya jeuri.” Alvin alichukia kwa majigambo yake. “Sitaki kukupiga kwa sababu ninachukia watu wachafu, kwa hivyo utajipiga. Tumia nguvu nyingi kama ulivyotumia ulipompiga Sarah. Sitakuacha mpaka niridhike.” Alvin alionya.
Lisa alipunguza hasira yake na kukataa. "Sikumpiga usoni."
"Ikiwa haukumpiga, una maanisha alijipiga mwenyewe?" Alvin alicheka. "Nilikuwa naanza kukuona kwa namna tofauti jana usiku, lakini sikutarajia kuwa wewe ni katili kiasi hicho."

“Katili? Mimi?” Lisa alikosa la kusema. Hakuweza kuona mtu mwovu alikuwa nani hasa. Alikuwa kipofu kabisa. "Kwa kweli, mwanamume hatampenda mwanamke ikiwa sio mbaya." Lisa hakuweza kujizuia kuomboleza. “Hakuna mwanaume ambaye angependa mwanamke mkarimu na mwaminifu siku hizi.”
"Nini? Unajaribu kunibembeleza na kunifanya nikupende ili uchukue nafasi ya Sarah, sivyo?” Macho ya Alvin yalijaa dhihaka. “Sawa, ngoja nikuambie. Hutawahi kufananishwa na Sarah.”
Lisa ghafla akaachia kicheko cha uchungu na kutazama chini. “Sawa, nitafanya. Lakini unaweza kuniruhusu niende kwanza?"
Alvin aliachia kola yake. Macho yake yalitulia kidogo alipoona tabia yake ya utii. “Mradi tu ubadilishe tabia zako kuanzia sasa na usimletee matatizo Sara, naweza...”
“Unaweza kufanya nini?” Lisa alitazama juu, akionyesha macho yake yakiwa yamefunguliwa kwa matarajio na uso wake mzuri usio na dosari.

Alvin aliganda kwa sekunde kadhaa na kutazama pembeni kwa mashaka. “Naweza kukuchukia sana.”
“Kweli?”
Mwili wa Alvin ulisisimka baada ya kusikia sauti tete ya mwanamke huyo. Huku akiwa amechanganyikiwa kidogo, mwanamke aliyekuwa mbele yake ghafla alimrukia na kupiga magoti mahali alipokuwa hatarini zaidi. Mguno wa uchungu wa mtu huyo ulisikika pale ofisini.
Alvin aliinama huku sura yake ikiugulia maumivu. “Wewe...”
“Unafikiri ninajali ikiwa unanichukia?” Lisa alifoka baada ya kumuona Alvin akiwa na maumivu. “Unafikiri wewe ni nani? Wewe ndiye uliyenilazimisha jana usiku. Yaani wewe unipelekeshe usiku kucha kisha hawara yako naye anifuate mchana kunitukana, mnafikiri ninaweza kuwaacha tu mnionee hivihivi?”
Kadiri alivyozidi kusema ndivyo alivyozidi kupata hasira. Aliinyakua keki iliyoliwa nusu pembeni na kumponda nayo kichwani.

“Unakuja kusema kwamba nilimuumiza Sarah, lakini ni wewe ambaye huwezi kujizuia. Alvin Kimaro, nilimpendaje mwanaume kama wewe? Wewe huwa unasukuma lawama kwa mtu mwingine. Huoni aibu?”
Alvin alikuwa kwenye hatihati ya kulipuka kwa hasira. Hakuna mwanamke aliyewahi kumfedhehesha hivyo au kumpiga keki kichwani.
Alitaka kumuua mara moja, lakini mwanamke huyo alikuwa mkali sana. Mahali pake pa hatari zaidi paliumia vibaya sana hivi kwamba hakuweza kusimama.
“Jiangalie katika siku zijazo, na umtazame mwanamke wako pia. Acheni kuja kwangu, na kila kitu kitakuwa katika amani.” Lisa alimsukuma na kuondoka na begi lake.
"Lisa, simama hapo hapo."
Mlango ulipofunguliwa, walinzi waliokuwa nje ya mlango na idara ya mapokezi walimwona Alvin Kimaro na hadhi yake akitoka kwa maumivu. Kila mtu karibu aanguke kwa kicheko. Mwenyekiti wao Jones alikuwa hashindwi. Hasa ukweli kwamba Lisa

aliondoka bila kuangalia nyuma ilimfanya kila mtu atake kumwabudu.
Baada ya zaidi ya dakika kumi, Alvin alijikongoja kutoka kwenye lifti. Hans, ambaye alikuwa amengoja kwa muda mrefu, aliuona uso wake na akasema kwa sura ya ajabu machoni pake, “Bwana Mkubwa, wewe...”
Alvin aliuma meno na kusema. “Fanya haraka na uendeshe gari kunipeleka hospitali. Ninataka kwenda kwa idara ya andrology." Ikiwa kweli alimsababishia ulemavu, ange...Angemlipa.
Hans alikosa la kusema. Hakwenda kumfunza somo Lisa? Kwanini aliishia kuwa yeye aliyepigwa badala yake?
•••
5:00 jioni, Lisa aliegesha gari lake la kifahari nyuma ya jengo. Katika muda usiozidi dakika tano, kijana mmoja aliyeonekana na sifa za kihunihuni alijongea kuelekea kwake akiwa alimevalia koti jeusi. Alionekana kana kwamba alikuwa na umri wa miaka ishirini, akiwa amesokota dredi safi na hereni sikioni. Tabia zake zilimfanya aonekane kama jambazi.

"Boss, ni mambo gani mabaya unataka nifanye usiku wa leo?" Logan ilicheka vibaya.
“Kuna mtu anahitaji kupigwa kidogo.” Lisa alisema huku akipapasa goti lake.
"Ni nini kilitokea kwenye goti lako?"
Lisa alitazama miguu yake na kuinua kichwa chake. "Nilipiga kitu kichafu."
Akiwa mtu anayemfahamu vizuri, Logan alishtuka na kumuonea huruma mwanaume huyo aliyepigwa kwa siri.
“Bado hujapata njia ya kuingia ndani ya nyumba ya Sarah?” Lisa aliuliza.
“Bosi, yule gaidi Hisan amefanya maovu mengi nje ya nchi kwa miongo kadhaa na hajajulikana hadi sasa. Ni mzuri katika kuficha nyendo zake, na pia ni mwangalifu sana.” Mdomo wa Logan ulitetemeka. “Ilichukua zaidi ya mwaka mmoja kumpata. Sarah Njau alikaa na wahalifu hawa wa kimataifa kwa zaidi ya mwaka mmoja, kwa hivyo yeye pia ni mkatili na asiye na huruma.

Lisa akanyamaza kimya. Kwa kweli, sababu iliyomfanya kughushi kifo chake ni kumwacha Sarah ashushe ulinzi wake. Ni hivyo tu angeweza kwenda ng’ambo ili kujua historia mbaya ya Sarah katika miaka hiyo aliyokaa nje ya nchi. Ingawa Sarah alikuwa amewaondoa watu wengi wa zamani, Lisa alibahatika kupata alama fulani.
Sura ya: 343
Logan alilalamika. “Bosi, Sarah amekuwa na wanaume wengi sana. Sidhani kama ningeweza kustahimili ikiwa mimi ningekuwa mwanamume wake, kwa hivyo inashangaza sana kwamba Alvin Kimaro anaweza kumchukua. Lakini Sarah ni mjanja sana. Siku hizi muda wake mwingi anautumia kujivinjari na Hisan kwa upande mmoja na anajua pia kudili na Alvin kwa upande mwingine. Lazima atakuwa na akili nyingi sana."
“Sawa. Inatosha." Lisa alikunja uso.
“Usikasirike sana. Ni mpuuzi tu wa kuchukiza.” Logan alifikiri kwamba Lisa alikuwa amekasirika.

“Unawaza kupita kiasi. Ulichosema kilinifanya nichukie tangu yule fisadi aliponibusu jana usiku. Nenda uninunulie vidonge vya kuzuia mimba...”
Lisa akamtupia pesa taslimu mara moja. Logan akapepesa macho na kujiweka mbali naye.
"Unafanya nini?" Lisa aliuliza.
“Hapana... Bosi, nilisikia kwamba maisha ya faragha ya Hisan ni ya fujo sana. Ana wanawake wengi wagonjwa huko. Hisan analala na Sarah, Sarah analala na Alvin, na Alvin anafuatana nawe...” Logan alikuwa na mchanganyiko wa hisia. “Unapaswa kuwa makini.”
Lisa karibu akose nguvu. Ikiwa sio kwa sababu alikuwa na wasiwasi juu ya Joel kumngojea, angeenda hospitalini mara moja kuchunguzwa. “Utanipeleka hospitali nikachunguzwe baada ya kumaliza kazi yetu.”
Dakika arobaini baadaye, gari likafika kwenye jumba la kifahari la Ngosha. Lisa alipoingia, katibu wa Joel, Walter Maliga, alikuwa akiripoti hali ya kampuni kwa Joel.

"Sifa ya kampuni imekuwa ikishuka hivi karibuni, na Kampuni ya Campos imesitisha miradi mingi na Kampuni ya Ngosha. Wanahisa wana wasiwasi sana na wanasitasita ikiwa wamrejeshe Damien na binti yake kwenye kampuni.”
Joel alidhihaki. "Je, baba na binti huyo wanawezaje kujitokeza kwenye kampuni. Hawaogopi wengine kuwakosoa na kuwacheka?”
Walter alitabasamu vibaya. “Sifahamu kwa kweli. Mimi ni katibu tu.”
"Ndio hivyo? Sidhani kama wewe ni katibu tu.” Lisa aliingia huku akiwa na tabasamu la hasira na macho makali sana kiasi cha kuwafanya watu waogope. Hata Joel alishangaa kidogo. Ilikuwa ni siku chache tu tangu walipokutana mara ya mwisho, lakini binti yake sasa alikuwa na utisho wa hali ya juu zaidi.
"Binti mkubwa, sielewi unachosema." Walter alitabasamu huku akimtazama kijana aliyekuwa nyuma ya Lisa.

“Hellow!” Logan aliita na papo hapo akamzuia Walter kwa kumfunga kamba.
"Wewe ni nani? Niache.” Akiwa mwishoni mwa akili yake, Walter alijitahidi kwa nguvu zake zote. "Binti mkubwa, unafanya nini?"
Joel alikohoa kwenye ngumi yake na kusema kwa kukata tamaa, “Walter, ni jinsi gani ulivyo mkarimu? Umekuwa ukiniwekea sumu kwenye milo yangu kila siku. Na kwa miaka hii miwili iliyopita, umevujisha ratiba yangu yote ya kibinafsi, kwa hivyo haijalishi ni hospitali gani ninaenda kwa uchunguzi, umeweza kumlipa daktari mapema. Niambie, ni nani aliyekuhonga?”
“Bwana Ngosha, sijui unazungumzia nini.” Walter alijifanya mtulivu na kusema kwa uso wa uchungu, “Nimekuwa nawe kwa miaka kumi, na nimekuwa mwaminifu kwako kila wakati.”
"Hiyo ni sawa. Miaka kumi imepita.” Lisa aliitikia kwa kichwa.
"Ingawa mshahara wa katibu ni shilingi za Kenya elfu thelathini tu kwa mwezi, baba yangu huwa anakupa mara tatu zaidi pamoja

na milioni kama bonasi yako ya mwisho wa mwaka. Pia alikupa nyumba, gari, na kuwapeleka watoto wako wawili katika shule bora zaidi, lakini hivi ndivyo unavyomlipa? Walter, unaweza kukataa, lakini tunazo kumbukumbu za wewe kumpa baba sumu. Labda hujui, lakini tumeweka kamera zilizofichwa kila kona ya nyumba.”
Joel kisha akatoa kamera ndogo ya uchunguzi kutoka kwenye sanduku la kurekodia lililokuwa sebuleni. Uso wa Walter ulipauka mara moja kwa kukosa la kusema.
“Nitakupa nafasi nyingine. Nani alikuelekeza?” Macho mazuri ya Lisa yalikuwa makali.
“Hapana... hakuna aliyeniagiza. Nilifanya mwenyewe,” Walter aliguna na kutikisa kichwa. “Namchukia Mwenyekiti Ngosha. Mimi... nachukia kwamba yeye ni mbahili sana na mshahara wake ni mdogo.”
“Huna elimu yoyote, na ninakulipa mshahara sawa na mtu mwenye degree, na bado unasema ni kidogo sana?” Joel alikasirika sana hadi akakohoa huku akijishika kifua.

“Baba usihangaike naye.” Lisa alimtuliza baba yake. “Lazima uelewe kwamba watu wengine watakuwa na njaa zaidi kadri unavyowalisha. Ni kawaida tu kwamba mwanaume hawezi kuridhika kamwe.”
Lisa aligeuka na kumwambia Logan, “Mlete ndani. Nitamuacha mikononi mwako.”
“Wewe... utanifanya nini?” Walter alimtazama Logan aliyekuwa akimkaribia na kulalamika sana, lakini, Logan alimvutia tu chumbani, akimpuuza. Kwa muda mfupi, vilio vya huzuni na vya kikatili vilisikika.
Joel alitetemeka huku akisikiliza. “Lisa, wewe...”
“Baba, usipomfundisha somo, atakutumia vibaya kila wakati.” Kwa tabasamu, Lisa alimsaidia kuketi.
“Hapana, itabidi apelekwe kituo cha polisi baadaye, naogopa...”
“Usijali. Hakuna atakayejua kuhusu hilo,” Lisa alisema. "Nilimwambia Logan tu atumie mbinu rahisi lakini hatari. Atahisi kama amechomwa

na sindano elfu moja, na maumivu yake ni mabaya zaidi kuliko kifo, lakini hawezi kufa. Kadiri anavyohangaika ndivyo sindano zinavyopenya ndani zaidi, na ndivyo itakavyokuwa chungu zaidi.”
Joel alishindwa kujizuia kutetemeka. “Umejifunzia wapi ukatili wa aina hii? Na yule kijana...”
“Baba, hatimaye nimeelewa baada ya miaka hii yote. Tunaweza tu kujilinda ikiwa hatuna huruma.” Lisa alitabasamu na kumtazama. "Tunaweza kuwalipa watu mema kwa mema, lakini hakuna haja ya kuwa na huruma kwa watu wasio na shukrani."
“Uko sawa.” Joel alipoona jinsi alivyokuwa, alisikitika tena kwa jinsi alivyobadilika. Hata hivyo, hilo lilieleweka. Alikuwa ameteseka sana, na kama baba yake, alipaswa kuwa kama yeye pia.
Nusu saa baadaye, Logan alimkokota Walter aliyekuwa kachoka sana.
“Umefikiria vizuri na upo tayari kusema?” Lisa alimuuliza wakati akipitia kitu kwenye laptop ya

baba yake. “Nimeangalia akaunti yako ya benki. Tangu miaka miwili iliyopita, akaunti yako imekuwa ikiongezeka kwa milioni 10 za ziada kila mwaka. Si hivyo tu lakini kabla ya hapo, akaunti yako imekuwa na ziada ya elfu 100, na kisha elfu 200, na kisha elfu 300... Namba inazidi kuwa kubwa zaidi. Kama nipo sahihi, ningesema umekuwa ukifuja pesa, lakini kuna mtu aligundua na kukuamuru kumpa baba yangu sumu ili akufichie siri hii. Niko sahihi?” Lisa aliinama chini na kumshangaa.
"Y-ndiyo." Walter alimtazama kama shetani. "Ilikuwa Nina Mahewa. Hakutarajia Bwana Ngosha kama angenusurika kwenye ajali ya gari, hivyo aliniambia niweke sumu ya kumuua polepole kwenye milo yake. Maadamu Bwana Ngosha angekuwa amekufa, Bi... Bi. Ngosha angeweza kuchukua kampuni ya Ngosha kwa haki.”
“Huyo b*tch. Mwanamke mkatili huyo.” Mwili wa Joel ulitetemeka kwa hasira. “Nimeishi kwa miaka mingi na kuona watu wengi waovu, lakini sijawahi kuona mtu katili kama yeye.”

"Baba, wewe tulia." Lisa akatikisa kichwa kwa utulivu na kumtazama Walter, akisema, “Nina kazi kwa ajili yako. Kutana na Nina faragha na upate ushahidi kwamba alikuambia umtilie baba yangu sumu.”
Walter alinyauka mara moja.
“Najua Nina ana ushahidi wa ubadhirifu wako, lakini uliibia kampuni ya Ngosha. Ilimradi Mwenyekiti Ngosha hatafuatilia, ushahidi utakuwa hauna maana.”
Lisa akainama mbele yake. Ingawa sauti yake ilikuwa ya upole, ilikuwa ni ile ambayo inaweza kuwafanya watu waogope.
“Ikiwa hutashirikiana nasi, tutakushitaki moja kwa moja polisi na kukagua akaunti haramu za kampuni kwa miaka mingi. Kwa kuwa utashtakiwa kwa sumu na ubadhirifu, ninahofia hutaweza kutoka jela maisha yako yote. Fikiria mke wako na watoto wako wawili.”
Macho ya Walter yalitetemeka kidogo.
Lisa aliendelea kusukuma maneno magumu. “Ngoja nikukumbushe kuwa mkeo ana miaka

thelathini. Ikiwa utaenda gerezani kwa muda mrefu sana, anaweza kuchukua pesa zako na kuolewa tena. Kufikia wakati huo, watoto hawatakuwa wako tena. Huoni kwamba hiyo ni sawa na kupoteza maisha yako?”
Sura ya: 344
“Sawa, nitakusaidia kupata ushahidi,” Walter alisema huku akiwa amezidiwa na majuto.
"Kweli, lakini lazima ule kitu." Lisa akatoa kidonge. “Ni lazima tuwe waangalifu iwapo utatusaliti. Nitakupa dawa mara tu utakapomaliza kazi yako.”
Logan alizungumza, “Dawa hii ina sumu kali, na itakuua ikiwa hautapata dawa ya kuipindua ndani ya wiki moja. Bila shaka, daktari anaweza kutibu, lakini itachukua miezi. Hutadumu kwa muda mrefu hivyo.”
Walter aliitazama sura nzuri ya Lisa ambayo ilikuwa ya kutisha kwa wakati huo. “Sitakusaliti. Wiki moja inatosha kwangu kupata ushahidi.” Walter alikaza mishipa yake na kumeza dawa hiyo.

Baada ya zoezi hilo kuisha, Lisa aliongozana na Joel kwenye chakula cha jioni kana kwamba hakuna kilichotokea.
"Lisa, ulipata wapi dawa kama hiyo?" Joel aliuliza huku akiwa amechanganyikiwa. "Umepitia nini katika miaka yako nje ya nchi?" "Baba, nimekutana na marafiki wapya wachache tu na kujifunza ujuzi mpya." Lisa alicheza.
Alipoona binti yake hataki kumwambia, pia hakuuliza sana. “Lisa, unafanya kazi nzuri na Mawenzi. Ungependa kuchukua pia nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Ngosha? Nadhani uwezo unao.”
“Baba, wewe bado kijana. Una miaka hamsini tu. Ni bora ukiisimamia. Sitaki kusimamia makampuni mengi sana. Inachosha sana akili.” Lisa alikataa.
“Basi, kwanini usirudi nyumbani? Baba yuko... mpweke akiishi hapa peke yake.” Joel akahema.

“Ni mbali sana hapa, hivyo pia si rahisi. Kwanini usirudi kwenye makazi ya zamani na kuishi na Bibi na Babu? Lisa alimkumbusha. "Lazima wahisi kuchoka kwa kukaa katika nyumba kubwa kama hiyo pia."
"Hiyo ni kweli." Joel alishawishiwa.
Baada ya chakula cha jioni, Joel hakufurahi alipojua kwamba Lisa alikuwa karibu kuondoka. "Unakuja mara moja tu kwa wiki, na unaondoka mara tu baada ya chakula cha jioni. Hapana, ondoka kesho badala yake.”
“Baba, bado nina jambo la kufanya baadaye. Nitarudi kesho kukuweka sawa.”
Mara baada ya Lisa kuondoka kwa ngosha, Logan alimpeleka hospitalini. Baada ya kumuacha Lisa hospitali, Logan aliondoka kwenda kuendelea kumchunguza Hisan.
•••
8:30 Usiku.
Baada ya majeraha ya Alvin kuvishwa, alitoka nje ya idara ya andrology kwa wakati na kumuona Lisa akishuka kutoka kwenye escalator.

"Lisa Jones, simama hapo hapo." Hasira iliyokuwa ikimfukuta kwa muda mrefu ikampanda tena. Alvin alipuuza kabisa maumivu hayo huku akipiga hatua kwenda kumshika. “Umefika kwa wakati tu. Nilitaka kukufuata.”
Lisa akapigwa na butwaa. Mtu huyo aligeuka kuwa mzimu unaomsumbua? Alimwona kila mahali alipoenda. "Umekuja hapa kwa andrologist tena?"
"Nyamaza." Alvin alikasirika hadi akalaani. Hakukuwa tena na ule utulivu wake wa kawaida. Aligundua kuwa tangu Lisa arudi, alikuwa akipandwa na hasira kila siku. Alitilia shaka kama angeweza kuishi zaidi ya miaka arobaini.
"Umeniumiza sana mchana."
"Kwa hiyo?" Lisa alimtazama. "Nani angefikiria? Unaonekana mkubwa na mrefu. Sikutarajia kwamba eneo lako fulani lingekuwa dhaifu sana. Ni tabu tu.”
Alvin alikasirika. “Unataka nife bila mtoto?”

Lisa alikcheka kama mazuri. “Usijali. Iwapo utaishia kukosa mtoto, nitawajibika.”
Alvin alicheka kwa kejeli. “Unaonekana unalazimisha kuwa na majukumu kwangu, sivyo? Nikikaa na mwanamke mbaya kama wewe, nitakosa furaha tu."
Lisa alipepesa macho na kusema kwa uso usio na furaha wala huzuni, “Nadhani umenielewa vibaya. Niliposema nitawajibika, simaanishi kwamba nitatunza furaha yako ya maisha yote. Ninachomaanisha ni... Nitampatia Sarah mwanamume tajiri na wa kipekee wa kumfurahisha maisha yake yote. Nadhani ikiwa huwezi kupata watoto, mtu ambaye utamsumbua zaidi atakuwa yeye, sivyo?”
Alvin alishusha pumzi ndefu huku uso wake ukibadilika na kuwa mweusi kisha kwa hasira. Hans, ambaye alikuwa akisikiliza kando, karibu apige magoti mbele ya Lisa na kumsihi aache mara moja kumkasirisha bosi wake. Alikuwa amekaa na Alvin kwa muda mrefu, lakini ilikuwa ni mara ya kwanza kumuona Alvin akiwa na hasira kiasi kile.

"Kwani nimesema chochote kibaya?" Kuangalia sura yake ya hatari, Lisa kwa woga alipiga hatua mbili nyuma. “Oh, ni kweli, nilisahau. Hisia za Sarah kwako ni za kina kama bahari. Hata ukipungukiwa na nguvu, hatajali.”
"Funga mdomo wako," Alvin alimfokea. Hakuweza kujizuia tena.
Vurugu hizo ghafla zilivutia watu wengi kwenye hospitali yenye shughuli nyingi, ambapo watu walikuwa wakiingia na kutoka.
“Tunaondoka sasa hivi!” Alimshika na kuusukuma mlango mzito wa escalator kabla hawajaingia ndani.
“Unafanya nini? bado nasubiri majibu yangu hapa.” Lisa alimfokea.
“Majibu gani? Kwani wewe ni mgonjwa?” Hapo ndipo Alvin alipoona karatasi mikononi mwake. Aliinyakua na kuona maneno ya 'HIV Screening Test' juu yake, na masikio yake yakasisimka.
“Kwanini unaangalia HIV? Wewe... Je, umewahi kujihusisha na wagonjwa wa VVU?”

Ubongo wa Alvin ulikuwa karibu kulipuka. “Hii ilikuwa lini? Usiniambie ilikuwa kabla ya leo.”
"Ndio, ilikuwa kabla ya leo." Lisa alitikisa kichwa huku akitazama kwa hasira.
"Lisa Jones, unawezaje kuwa mchafu kiasi hiki?" Alvin aliutupa mkono wake kwa nguvu na kumfokea Hans nje. “Fanya haraka uniletee dawa ya kuua vijidudu.”
"Hakuna haja ya hilo," Lisa alisema kwa sura isiyo ya kawaida. “Mtu aliyenifanya nipime ni wewe. Ulifanya hivyo pamoja nami jana usiku, na nilipata wasiwasi. Niliogopa kuambukizwa kitu, kwa hivyo nilikuja hapa ili kuchunguzwa."
Vidole vya Alvin vilitetemeka, na kichwani kwake akahisi kupandisha mashetani. Alimtazama kwa macho yenye hasira kali na kumuuliza neno baada ya neno, “Unamaanisha... Unaogopa nitakuambukiza ugonjwa?”
"Najua ... kusema hii inaweza kukuumiza, lakini ... ni kwa amani yangu ya akili." Lisa alipiga hatua moja baada ya kuona kuwa hasira yake ilikuwa karibu kulipuka.

“Haha.” Alvin alicheka. Uso wake mzuri uligeuka kuwa kama shetani mbaya. "Lisa Jones, umenikera sana wakati huu." Kisha, akamtupa begani na kutoka nje ya hospitali. Hans akawatazama kimya kimya kisha akatazama dawa alizotumwa na Alvin mkononi mwake. Alimuombea Lisa kimyakimya.
“Alvin Kimaro, niache.” Lisa alimpiga kofi kali la mgongoni.
Hata hivyo, Alvin alijifanya kana kwamba hakumsikia. Akambeba hadi sehemu ya maegesho ya magari, akafungua mlango wa gari na kumtupa ndani.
“Alvin, unafanya nini?” Lisa aliinuka, lakini Alvin alimkandamiza begani kwa mkono mmoja na kumpasua shati lake kwa mkono mwingine.
Lisa alipigwa na butwaa. “Alvin, huna akili. Je, humpendi Sarah? Una uhakika unataka kumsaliti tena?"
Wakati huo Alvin alikuwa amekasirika sana na hakumsikiliza hata kidogo. “Si ulisema unanichukia kwa kuwa mchafu? Unahisi

nimekuambukiza maradhi, sivyo? Basi acha nikuambukize zaidi.”
Sura ya: 345
Saa tano usiku.
Gari jeusi lilisimama kwenye maegesho ya magari nje ya jengo kubwa la makazi kwenye eneo la maarufu la Karen Estate.
Alvin alitazama kiti cha nyuma. Lisa alikuwa amelala kuegemea kwenye dirisha, huku nywele zake zenye mawimbi zikiwa zimetanda kwenye mabega yake, mwanamke huyo alifinya macho yake pale Alvin alipowasha taa kwenye gari. Mwanga hafifu wa uso wake mdogo ulitoa haiba ambayo hakuna mwanaume angeweza kupinga.
Suti yake kubwa iliyofunika mwili wake mdogo ilimfanya aonekane kupendeza zaidi. Alvin aliegemeza kichwa chake kwenye usukani akiwaza kwa muda. Ikiwa dawa ziliathiri uamuzi wake wa kuja na kumwingia Lisa jana yake usiku, basi vipi usiku huo? Usiku huo alikuwa mzima kabisa. Mwanzoni, alikasirika na alitaka kumfundisha somo la kumtisha,

lakini kwa namna fulani alipoteza udhibiti wa hisia zake njiani na kujikuta akimwingilia tena.
Wakati wawili hao walipokutana, kitu mapenzi kilikuwa na mvuto wa kiasili sana hivi kwamba Alvin hakuweza kujizuia kujiingiza ndani yake. Hakujua kwanini ilikuwa hivyo.
Mchana, alishikwa hatia waziwazi na kuumia moyoni alipomwona Sarah akiwa amefunikwa na majeraha. Hata aliapa kukaa mbali na Lisa. Lakini, alihisi kama amepoteza busara yake mara tu baada ya kumuona tena Lisa. Ni kana kwamba aliwekewa dawa ya mapenzi na mwanamke huyu.
Akiwa amekasirika, alichukua sigara lakini akaiweka chini haraka alipofikiria kwamba kulikuwa na mwanamke nyuma yake. Baada ya kusubiri kwa dakika tano, bado mwanamke huyo hakuonyesha dalili za kuamka. Kwa hiyo, alishuka kwenye gari, akaenda siti ya nyuma na kumbeba Lisa kumtoa nje.
Hakuona wakati alipomnyanyua, lakini alipombemba aligundua kuwa alikuwa mwepesi sana. Midomo yake iliyovimba kidogo

ilikuwa imelegea, ikionekana laini na ya kuvutia. Alionekana kupendeza.
Kwa bahati mbaya, alipombeba juu, midomo ya Lisa ikagusa kwenye kifua chake na kusuguasugua kidogo juu yake. Wakati huo Alvin alihisi ghafla moyo wake umelainika kama mafuta. Hisia za msisimko zikaanza kufurika tena mwilini mwake.
Alvin akambeba Lisa juu juu na
kuchukua ufunguo kutoka kwenye begi lake ili kufungua mlango. Alipoingia ndani, akamweka taratibu kwenye kitanda kikubwa kilichokuwa chumbani humo. Mwanamke huyo mara moja alianza kujigeuzageuza juu ya kitanda. Alikumbatia mto na kurusha viatu vyake, akifunua miguu yake ya kupendeza. Rangi yangozi ya mapaja laini ya Lisa chini ya mng’aro wa taa ilikuwa inaroga.
Alvin nusura apate hamu ya kumbusu juu ya mapaja yake.
Lakini, wakati wazo hilo lilipopita, alishtuka. Jamani. Alikuwa anawaza nini? Alikuwa anafanya kama mpuuzi asiyejielewa. Mara aseme hamtaki, mara tena amtamani! Alvin akaamua kumfunika kwa blanketi kwa upole

kabla ya kufunga mlango nyuma yake na kuondoka.
Alvin alipotoka, aliwasha simu yake na kuona missed call kadhaa.
Akafungua WhatsApp. Nusu saa iliyopita, alikuwa ametuma ujumbe kwa Sarah. [Nina safari ya haraka ya kikazi jioni na sitarudi. Lala mapema.]
Alishika kichwa chake kwa maumivu na kumpigia Chester. “Umelala? Njoo tupate kinywaji.”
“Sina nafasi. Nilifanya zamu ya ziada jana usiku, na nimechoka sana.” Chester alikataa.
“Basi, nitakuja kwako,” Alvin alisema kwa huzuni.
Alipofika katika nyumba ya kifahari ya Chester, Chester alikuwa bado amelala huku akikoroma. Alvin alimvuta pale kitandani. “Amka tunywe.”
Chester akauma meno na kusema, “Una nini muda huu? Hukurudi nyumbani kwako jana

usiku, lakini uko hapa usiku wa leo pia. Huogopi Sarah atakuwa akikuwazia vibaya?... Subiri, ni harufu gani hiyo kwako?”
Chester alikosa la kusema. “Ni harufu ya mwanamke. Ni Lisa?”
“Umejuaje kuwa ni yake?” Macho ya Alvin yalimkazia.
“Nilisikia harufu yake alipofungua mlango asubuhi ya leo. Ilikuwa ni harufu nzuri, kwa hivyo nimeikumbuka."
"Umbea huo." Alvin alimpiga onyo kwa macho yake baridi mara Chester aliposema hivyo.
Chester hakujua la kusema. “Una mpango gani na hawa wanawake? Nilizungumza na wewe juu ya hii asubuhi tu. Kwa nini...”
“Vaa nguo.” Alvin akamtupia nguo zake na kutoka nje.
Chester alipanda juu kwa maumivu. Hata hivyo, alipotoka tu, alimuona Alvin akifungua chupa ya Lafite, mvinyo wa kifahari zaidi ambao Chester aliutunza kwa miaka kumi.

“Alvin, fungua pombe nyingine yoyote lakini hivyo iweke chini!”
Kilichomjibu ni sauti ya 'pop' ya kufunguka kwa chupa. “Kuna maana gani kuendelea kuuhifadhi? Mvinyo umekufa, lakini sisi tuko hai."
Moyo wa Chester ulikuwa karibu kupasuka. “Jamani, kwa nini hukuenda kwa Rodney badala yake?”
"Ikiwa nitamwambia Rodney kwamba nililala na Lisa siku mbili mfululizo, bila shaka tutagombana." Alvin akammiminia glasi ya mvinyo.
Chester akajipapasa paji la uso na kushusha midomo miwili ya mvinyo harakaharaka, Alvin asije akamaliza yote. “Kwa hiyo ulikuwa unafikiria nini? Kuishi na wanawake wote wawili?"
"Sijui." Alvin akatikisa kichwa. “Siku zote nilifikiri ninampenda Sarah, lakini ninapomwona Lisa tu natamani kumlaza kitandani. Unajua maana hisia hizo?"

Chester akamtazama. “Hilo si jambo geni. Ulikuwa na hisia kwa Lisa zamani.
"Ni lini nilipata hisia kwake?" Alvin alikosa la kusema.
"Kumbukumbu zako za miaka mitatu iliyopita zinazidi kuwa mbaya siku hadi siku. Pengine umesahau mambo mengi.” Chester hakuweza kujizuia kukumbuka mambo fulani ya zamani.
Akiwa mtazamaji, alikiri kwamba Alvin alimpenda zaidi Sarah, lakini Sarah alipokuwa hayupo, Lisa alikuwa na nafasi muhimu sana katika moyo wa Alvin. Hata hivyo, aligundua kuwa Alvin alikuwa amesahau baadhi ya mambo.
Alvin alipigwa na butwaa. “Nimesahau nini?” Chester akamtazama. "Unakumbuka kwenda Coco Beach na Lisa kipindi mnaishi Dar?"
"Nilienda Coco Beach?" Alvin alionekana kama amesikia mzaha. “Haiwezekani.”
Chester aliendelea, “Zamani, wakati Sarah hakuwepo, Lisa alikupeleka tukashangaa

unakula hadi miguu ya kuku ya kukaangwa uswahilini.”
Alvin alishangaa. Je, hilo lilitokea kweli?
Chester aliongeza, "Wakati mwingine, ulimuumiza Lisa na kumpeleka hospitali katikati ya usiku."
Alvin akapigwa na mshtuko tena. Ni kweli hapo awali alikuwa amefanya jambo kama hilo kwa Lisa? Ikiwa mtu mwingine angesema hivyo, bila shaka asingeamini, lakini Chester alikuwa kama ndugu ambaye alikuwa amepitia mazuri na mabaya pamoja naye. Maneno mengi aliyosema yanapaswa kuwa ya kweli.
“Chester, mimi ni mhuni? Nimekuwaje hivi?” Alvin alishika kichwa chake mikononi mwake. Mwenendo wake wa sasa ulimpa hisia zisizojulikana.
Chester alimtazama tu na kumwambia, “Mimi nimekuwa na uhusiano na wasichana wengi siku za nyuma, na watu wa nje wananijua kama mtu asiyetulia, malaya! Kila mara nilianzisha uhusiano mpya kabla ya kukatisha mwingine. Naweza kukusaidia”

"Nipe mawazo." Alvin siku zote alikuwa mtu wa maamuzi, kwa hiyo mara chache alikuwa na mkanganyiko kama huu.
Chester alimkumbusha, “Usifanye mambo kuwa magumu. Ninamfikiria Sarah kama dada mdogo na ninamtakia furaha. Lakini kusema ukweli, ukikataa kumgusa, hiyo ni shida pia kwa sababu huwezi kuishi nao wote wawili. Isitoshe, Sarah amekuwa na wewe kwa muda mrefu, na haujamgusa hadi sasa. Lisa ni rahisi kumwacha, Sarah ni ngumu."
Alvin alikunja uso. Mwishowe, alichukua glasi ya mvinyo na kuigonganisha na ya Chester tena. Maskini Chester aliongozana naye kunywa usiku kucha.
TUKUTANE KURASA 346-350
ONYO: Ni marufuku kusambaza, kukopi wala kuuza kazi hii kwani endapo kama tutakubaini basi sheria itachukua mkondo wake (By: Official Dully)
 
LISA KITABU CHA NANE (8) SIMULIZI........................LISA KURASA..................351 - 355
PRESENT: SIMULIZI ZA DULLY

Sura ya: 351
Baada ya Joel kujionea ‘live’ usaliti wa Nina, alishindwa kuvumilia na kupata mshtuko wa moyo. Lisa alimpeleka baba yake haraka hospitali kuingiziwa dripu ya IV. Ingawa kuona Nina akikamatwa kulimfanya Joel kupumua, afya yake ilidhoofika tena kwa sababu alikuwa amechanganyikiwa.
Haikuchukua muda Mzee Ngosha na Bibi Ngosha wakakimbilia hospitali. Mara baada ya Bibi Ngosha kuiona hali ya Joel, machozi yakaanza kumlenga lenga. "Nina hana akili. Tulimtendea vizuri sana kwa miaka mingi. Ajali uliyokutana nayo miaka mitatu iliyopita lazima inahusiana naye. Kwa bahati nzuri, mimi na baba yako tulimwomba Lisa akutunze. Vinginevyo...”

Maneno hayo yalipelekea mtetemo kwenye uti wa mgongo wa Mzee Ngosha. Sasa alipofikiria jambo hilo, alitoa shukrani zake za dhati kwa Lisa. "Tuna deni kubwa kwako, mjukuu wangu..."
Lisa alitabasamu na kukaa kimya kwa muda. “Usijali kuhusu hilo, babu. Sikuwahi kutarajia mengi kutoka kwa familia ya Ngosha, kwa hiyo sijavunjika moyo.”
“Wewe...” Mzee Ngosha aliona aibu ghafla.
Bibi Ngosha akamvuta. “Lisa yuko sahihi. Kwa kweli tabia yetu ilimkatisha tamaa tangu mwanzo. Ni kosa langu. Sikupaswa kumzuia Joel kumuoa mama yako. Samahani sana."

Mzee Ngosha alikunja ngumi na kukohoa kwa aibu. “Nakubaliana na bibi yako. Kuanzia sasa jisikie huru kabisa. Unakaribishwa nyumbani muda wowote utakao. Baada ya yote, hiyo ni nyumba yako."
Lisa alipigwa na butwaa kwa muda na kujawa na hisia mseto. Kwa kweli, alitamani kwamba babu na bibi yake wangemwambia hivyo alipofika Nairobi kwa mara ya kwanza. Hata hivyo, walimzingua pindi tu walipomuona. Siku zote alilazimika kupambana peke yake ndani ya jiji hilo, jambo ambalo lilimfanya ajisikie kama mgeni.
Wakati huo, kuna mtu aligonga mlango, ambapo Melanie aliingia akimsukuma Damien, ambaye alikuwa ameketi kwenye kiti cha magurudumu.

“Mnatafuta nini hapa?” Joeli alipowaona, alianza kupandwa na hasira na kukohoa kwa nguvu.
“Joel, usifadhaike. Ni mbaya kwa afya yako.” Mzee Ngosha kisha akawanyooshea kidole Damien na Melanie, na kusema, “Tokeni nje.”
“Babu tumekuja kukuomba msamaha. Kwa kweli sikujua kwamba Mama alifanya mambo hayo.” Melanie aliinua kichwa chake na kujibu kwa uchungu. Macho yake yalikuwa mekundu.
“Ulikuwa hujui kweli?” Lisa alidhihaki, “Wewe ndiye uliyempeleka Baba kwa uchunguzi wa kimatibabu kila mara. Wewe na Nina mlipanga njama hizi zote pamoja, lakini una bahati kwamba mama yako ndiye aliyebeba lawama zote.”

Baada ya ukimya wa muda, Lisa alihamishia macho yake kwa Damien. “Baba mdogo, ninazungumza na wewe hivi kwa sababu mimi ni mtu mstaarabu sana. Kama ningekuwa wewe, ningeona aibu kujitokeza hapa. Ikiwa baba yangu angekufa kwa sumu, Kampuni ya Ngosha ingeenda kwako na Melanie. Nyote wawili mngefaidika zaidi, na Nina aliyeenda gerezani kwa niaba yenu.”
Uso mzuri wa Damien ulilegea kabla ya kujibu, “Siku zote nimemchukulia kaka yangu kama baba yangu, kwa hiyo ningewezaje kujaribu kumuua kaka yangu? Kaka nitapiga magoti nakuomba msamaha sasa. Kwa miaka hii yote, nilipumbazwa na Nina na nimefanya mambo mengi mabaya dhidi yako, lakini sikupanga kukuua hata kidogo.”

Damien alipokuwa akizungumza, alijilazimisha kutoka kwenye kiti cha magurudumu na kupiga magoti sakafuni. Hata hivyo, miguu yake ilikuwa dhaifu sana kuweza kusimama. Mara miguu yake ikageuka kuwa mlenda, alianguka sakafuni vibaya.
“Baba.” Melanie alilia na kwenda kumshika kwa haraka.
“Melanie, nishike nipige magoti.” Damien aliendelea.
Kwa kuwa Damien alikuwa mwanae wa kumzaa, Bibi Ngosha alishindwa kuvumilia kumuona akipiga magoti. “Miguu yako imelemaa. Utapiga magoti vipi? Fanya haraka ukae kwenye kiti chako.”
"Ndio, miguu yangu imelemaa." Damien

aliinamisha kichwa chini na kububujikwa na machozi. “Tangu nilipozaliwa, watu wengi wamekuwa wakinidharau kwa sababu tu ya ulemavu wangu. Ninamshukuru Kaka, lakini wakati huo huo, ninamwonea wivu. Nampenda Nina, lakini hakuwa anavutiwa nami. Zaidi ya miaka ishirini iliyopita, sijawahi kumpenda mtu mwingine yeyote isipokuwa yeye. Nilimfanyia kila kitu bila kulalamika. Nilidhani angeniangukia hatimaye baada ya kupata Ngosha Corporation, lakini nilikosea. Ni sasa tu ndio nimeelewa utu wake. Baba, Mama, Kaka, ni kosa langu...”
Bibi Ngosha alikuwa kwenye hatihati ya kulia. Hakuweza kupinga kusema, “Yote ni makosa yangu. Sikupaswa kukuzaa na kukufanya uteseke sana na kujidharau.”

“Baba, Mama, mnaweza kunilaumu mimi. Ni sawa. Lakini natumaini hamtamchukia Melanie.” Damien aliinua kichwa chake na kuomba. "Melanie hana hatia. Sijawahi kuoa, na yeye ni binti yangu wa pekee. Yeye pia ni mjukuu wako wa damu.”
“Babu, Bibi, samahani. Nimekuwa mbali nanyi kwa muda mrefu, na imenisikitisha sana. Bado mnakumbuka jinsi mlivyokuwa mkinijali?" Melanie mara moja akapiga magoti karibu na Damien. Alitazama juu na kugeuza nywele zake kuelekea nyuma, akionyesha uso uliopigwa na kuvimba.
"Ni nini kilitokea kwenye uso wako?" Mzee Ngosha aliuliza kwa sauti nzito.
Melanie akasonga na kuuma mdomo. Kisha, Damien akasema kwa huzuni,

“Ni Jerome aliyempiga.”
"Ni mpuuzi sana huyo mwanamume." Mzee Ngosha alipandwa na hasira. "Familia ya Campos ina kiburi sana. Nitakutana na babu yake.
Familia yetu imewanyanyua sana mafukara wale wasio na shukrani, hawakuwa na kitu chochote!”
“Ni sawa, babu. Tayari wewe ni mzee. Hakuna haja ya kusimama kwa ajili yangu, na sitaki wewe kuwa upset kwa sababu yangu. Familia ya Campos sio sawa na ilivyokuwa hapo awali. Jerome alisema kwamba alinioa kwa sababu tu alifikiri nilikuwa...Binti wa Joel. Alichagua kuwa nami kwa sababu ya familia ya Ngosha.” Tabasamu la uchungu likapita usoni mwa Melanie.
“Ni dharau kiasi gani?” Damien alisema

kwa uchungu huku akimpapasa Melanie sehemu ya nyuma ya mkono wake. “Ni kosa langu, sio lako. Ananidharau kwa sababu mimi ni mlemavu na siwezi kumsaidia chochote”
“Inatosha!” Bibi Ngosha hakuweza kuvumilia tena kusikia hivyo. "Sasa kwa kuwa Nina yuko jela, acha yaliyopita yawe yamepita. Damien, bora usiishi peke yako huko nje. Rudi nyumbani. Uwe mtu mzuri na ulete sifa njema kwa familia ya Ngosha pamoja na kaka yako.”
“Naweza kweli kufanya hivyo?” Damien kwa tahadhari akahamishia macho yake kwa Joel aliyekuwa amejilaza kitandani. “Baba, ni sawa. Sitaki Kaka anielewe vibaya.”
Midomo ya Joel ilicheza, lakini kabla

hajazungumza, Melanie alisema, “Baba, msikilize babu. Mimi nakaa katika nyumba ya familia ya Campos. Nina wasiwasi kuhusu wewe kuwa peke yako katika hali yako. Je, ukianguka? Hata iweje, mtumishi wako si sehemu ya familia yetu kamwe.”
“Rudi tu.” Maneno ya Melanie yalimfanya Bibi Ngosha kukosa raha. "Hamia nyumbani leo."
Joel akafumba macho. Muda si mrefu, Mzee Ngosha na Bibi Ngosha waliondoka wakiwa na Damien na Melanie. Lisa alikuwa akitazama tukio zima kimyakimya. Hakuwahi kufikiria kwamba Damien na Melanie bado wangepokea hisani nzuri kwa wazee hao baada ya Nina kufungwa gerezani. Ukiachana na Melanie, Damien hakuwa na haya kama mwanaume.

“Unawaza nini baba?” Macho ya Lisa yakatua kwa baba yake. Ikiwa baba yake naye alifikiria sawa na babu na bibi yake, Lisa angejuta kujiingiza kwenye sakata hilo.
“Unafikiri kwamba mimi bado ni mjinga kama hapo awali? Baada ya kupitia mengi, nimeshajifunza somo langu.” Joel alilalamika. "Damien anatisha zaidi kuliko hata Nina. Anajua kabisa kwamba babu na bibi yako watamhurumia na kumbembeleza.”
“Najua." Lisa akahema. Babu na bibi yake walionekana kuwa wazee, lakini walikuwa na mali nyingi. Ingawa Mzee Ngosha alikuwa amestaafu kufanya kazi, bado alikuwa na nguvu katika Ngosha Corporation na ushawishi katika jiji la Nairobi. Mara baada ya Melanie na

Damien kupata kampuni ya Ngosha Corporation, wangemtumia tena.
Sura ya: 352
“Lisa, kwa kuwa niko hospitalini, nitakuomba unishughulikie mambo fulani kwa sasa.” Joel ghafla akampiga piga Lisa nyuma ya mkono wake. "Nitamwambia msaidizi wangu kuripoti kwako mambo yote ya kampuni kuanzia sasa."
Kichwa cha Lisa kilianza kumuuma. "Baba, unanilazimisha kijanja kusimamia Kampuni ya Ngosha?"
“Ninakulazimisha vipi?” Joel alimkazia macho. "Kama binti yangu na mrithi wa Ngosha Corporation, hutaitwa tena binti haramu. Unastahili kuwa na mwanmke

bora kabisa katika Kenya nzima. Hata Sarah pia hawezi kufananishwa na wewe.”
Nia ya Joel hatimaye ikamwingia Lisa. Hisia ya joto ikaenena ndani yake. Bila kusema, Joel lazima aligundua kuwa Alvin alikuwa akienda kufunga ndoa na Sarah, hivyo alitaka asihizunike. Kwa kuzingatia kwamba Lisa alikuwa mmiliki wa Mawenzi Investments, binti pekee na mrithi wa Ngosha Corporation, Sarah asingeweza kumshinda kwa heshima na hadhi. Haidhuru Sarah alikuwa na jeuri kiasi gani, yeye alikuwa mwanasaikolojia tu. New Era Advertisings, kampuni ya familia yao, ingekuwa imeanguka kwa muda mrefu bila usaidizi wa Alvin, na Thomas angekuwa jela kama si kukingiwa kifua na Alvin.

“Usijisumbue na mambo hayo mwanangu. Utaweza kupata mtu bora zaidi anayekustahili. Binti yangu ni mrembo sana, mwenye uwezo, na tajiri. Hakuna mtu yeyote katika Kenya anayeweza kukuzidi,” Joel alimtia moyo huku akitabasamu.
“Asante, Baba. Ninajiamini kila wakati. Kwa wale ambao hawakunichagua, ni hasara yao.”
"Safi sana." Joel alitabasamu.
Saa kumi jioni, Lisa alipanga foleni kwenye chumba cha pharmacy kilichokuwa chini ili kuchukua dawa. Alipomaliza, alirudi juu na kumuona Maya akitoka nje ya kitengo cha uzazi na magonjwa ya uzazi ya wanawake akiwa na Sarah.

Akiwa amevalia nguo nyeupe, Sarah alionekana kama malaika kiasi kwamba kila mtu hospitalini alimtazama mara mbili mbili. Kwa upande mwingine, Lisa alikuwa rafu kidogo kwani siku nzima tangu jana yake alikuwa akimuuguza Joel hospitalini. Hakuwa hata na chembe ya kipodozi usoni na nywele zake zilikuwa zimetimka kidogo, na alionekana amechoka.
Sarah alilinganisha sura yake ya nje na ya Lisa, akafurahi sana, na akapata nguvu ya kuongea mbele yake. "Hi, Lisa. Nini kinakuleta hapa? Nini tatizo? Hujisikii vizuri?”
Lisa akatoa macho yake na kuendelea kwenda mbele bila kumjali Sarah. Alihisi kuchoka sana baada ya kumtunza Joel kwa siku moja. Hakuwa na nguvu ya kupoteza kuongea upuuzi na

mwanamke yule.
“We mwanamke, mbona huna adabu hivyo?” Maya alipiga kelele, “Bi Njau alikuwa anakusemesha, ina maana hujamsikia?”
“Bi Njau ni nani na kwanini nijibu swali lake?” Lisa aliwageukia kwa jazba na kusimama kwenye korido. Aliwatupia macho wawili hao kwa hasira.
“Wewe...” Maya alikuwa amekasirika kwa hasira.
Sarah alimsimamisha Maya na kusema kwa upole, “Lisa, najua unanichukia, lakini nimejitayarisha kukukubali. Kwa kweli ninampenda Alvin sana, na wewe najua unampenda, kwa hivyo tunaweza tu kushea. Naweza kukubali hilo.”

Lisa alichukizwa. “Oh, asante. Lakini sina mpango wa kushea mume na mtu yeyote. Ninaogopa kuambukizwa maradhi.”
Sura ya Sarah ilibadilika kidogo, kisha akainamisha kichwa chake. “Unathubutuje kutoa maneno ya dharau hivyo? Unapolala naye kila siku haimaanishi kwamba unampenda?” Aligusa tumbo lake huku akisema, “Sawa, unaweza kukaa kando basi uniachie mume wangu. Nimepanga kuzaa watoto wengi kwa Alvinic. Nilikuja hospitalini leo kuangalia jinsi ya kupata mapacha au mapacha watatu kwa njia ya urutubishaji katika mfumo wa uzazi.”
Maya alitabasamu na kusema, “Ni Bw. Kimaro ambaye alipendekeza kufanya urutubishaji kwa vitro aliposikia kwamba Sarah alitaka kupata angalau watoto

wawili. Aliogopa kwamba angekuwa na wakati mgumu kuwa mjamzito mara mbili. Tayari amemuomba Dokta Choka kuajiri timu bora zaidi ya madaktari wa uzazi nchini kwa ajili yake.”
“Maya...” Sarah alimtazama kwa aibu na kudhihaki.
Macho ya Lisa yalitangatanga na kutua kwenye tumbo la Sarah kabla ya kucheka ghafla. "Ni bora kuwa mwanaume. Ni rahisi kwao kusema kwa vile wana kazi ya kutoa manii tu kwa ajili ya kuingizwa kwenye hiyo ‘artificial insemination’. Lakini wanawake wana kazi kubwa ya kupitia kila aina ya shida. Katika hatua za mwanzo, wanawake wanatakiwa kuchukua sindano na madawa. Nilisikia kwamba mchakato wa kuingizwa mbegu ni mchungu sana pia. Nakushangaa sana. Upendo wangu

kwa Alvin si kama wako.”
Uso wa Sarah ukabadilika ghafla. Kwa kweli, alijua kila kitu ambacho Lisa alikuwa ametaja. Yeye pia alikuwa hataki, lakini hakuwa na jinsi kwa sababu Alvin hakuweza kumgusa hata kidogo.
“Umemaliza? Una wivu tu.” Maya alimshutumu Lisa kwa hasira.
"Nina wivu?" Lisa aliinua mabega yake. “Nina wivu gani? Nimepata mimba ya mapacha hapo awali, kwa hivyo sihitaji kupitia shida hizi zote. Inaonekana nimeweka kiwango cha juu sana kwa Alvin kwamba mtoto mmoja hawezi kumtosha tena.”
“Umezidi sasa Lisa.” Sarah aliuma mdomo wake kwa huzuni, na machozi yakaanza kumlenga lenga.

Lisa alitazama pembeni, na hakika Alvin alikuwa akielekea kwao. Kulikuwa na viongozi wachache wa hospitali pamoja naye.
Alipofika juu na kumuona Sarah analia, alimwangalia Lisa mara moja. “Ulimfanya nini tena? Si tayari tumeachana, kwanini unaendelea kutusumbua?”
Lisa aliongea kwanza kabla Sarah hajafungua mdomo wake. "Nilikuwa nashangaa tu kusikia kwamba umemwambia Sarah akuzalie watoto kwa njia ya upandikizi wa bandia. Kwanini usimruhusu apate mimba kwa njia ya kawaida? Unajua kwamba ni lazima atumie sindano na dawa kila siku kabla ya kuingizwa mimba kwa njia ya bandia? Bi. Njau, sisemi uwongo, sivyo?”

Sarah, ambaye mwanzoni alitaka kulalamika huku akitokwa na machozi, alipigwa na butwaa. Lisa hapo awali alikuwa akimnanga Sarah, lakini sauti yake mbele ya Alvin ilimfanya aonekane kana kwamba alimwonea huruma Sarah. Sarah alipoona hali ya kutofurahi ya Alvin, alieleza upesi, “Alvinic ana wasiwasi kwamba nitakuwa nimechoka sana ikiwa nitaendelea kubeba mimba mara kwa mara.”
"Ikiwa una wasiwasi kuhusu kumchosha, basi inatosha tu hata kubeba mimba mara moja. Hakuna haja ya kuwachukulia wanawake kama mashine za kutengeneza watoto,” Lisa alisema huku akiachia tabasamu. “Kawaida wanandoa wanapoenda kwa ajili ya upandishaji mbegu kwa njia ya bandia, ni aidha hawana uwezo wa

kuzaa au hawawezi kufanya ngono. Lakini ninafahamu wazi kama una uwezo au la. Haiwezekani kuwa ni Bi. Njau ambaye hana uwezo wa kuzaa...” Aliziba mdomo kwa mshangao. “Nakumbuka sasa. Nyote wawili mmekuwa pamoja kwa muda mrefu, lakini bado hana ujauzito.”
Uso mdogo wa Sarah ulibadilika rangi kwa hasira. Kwa hakika angeweza kupata mimba, lakini Alvin ndiye ambaye hakutaka kumgusa. Lakini, hakuweza kusema hivyo waziwazi, kwa hivyo aliweza kukubali tu macho ya kushangaza kutoka kwa viongozi wa hospitali. Alifadhaika sana hadi machozi yakaanza kumdondoka.
"Lisa, nitakuchana mdomo ikiwa utaendelea kuongea upuuzi." Alvin alimvuta Sarah kwenye kumbatio lake.

Kisha, akasema kwa hasira kwa viongozi wa hospitali, “Mfukuzeni hapa. Sitaki kumuona.”
Akiwekwa katika hali ngumu, mkurugenzi wa hospitali alisema, “Bwana Kimaro, Lisa ni binti wa Bwana Ngosha. Bwana Ngosha kwa sasa amelazwa katika hospitali yetu...”
“Nataka familia ya Ngosha ihamie hospitali nyingine. Sitaki kumuona hapa,” Alvin alifoka na kuondoka huku akiwa amemkumbatia Sarah.
"Alvinic, yote ni makosa yangu. Nilikutia aibu.” Sarah alinung'unika mikononi mwake.
“Sio tatizo lako. Mimi ndiye nina makosa kukuacha uende kupandishwa mbegu kwa njia ya bandia.” Alvin

alichanganyikiwa pia. Maneno ya Lisa yaligusa udhaifu wake, na kumfanya ajisikie fedheha.
“Ni sawa. Ilimradi niweze kuzaa mtoto wako, niko tayari kufanya hivyo,” Sarah alisema kwa utulivu. Alvin akahema. Alijisikia vibaya kwa ajili ya unyonge wa Sarah.
Dakika 15 baadaye, Lisa alipokea taarifa kutoka hospitalini kuwaamuru wabadili hospitali. Joel alikuwa katikati ya matibabu yake, lakini alikasirika aliposikia kuhusu hilo. “Alvin ana kiburi sana. Kwani familia yetu ilikuwa na chuki dhidi yake katika maisha yetu ya zamani? Au, matibabu yangu yalimsumbua kwa namna yoyote?” “Baba si wewe uliyemsumbua, ni mimi.” Mapigo ya moyo wa Lisa yalikuwa chini. Angekumbuka kila kitu ambacho Alvin alikuwa amewafanyia.

“Lisa, usiwe na huzuni. Ni tatizo langu. Sikupaswa kuja katika hospitali ya familia ya Choka. Familia ya Choka na familia ya Kimaro zimetiwa lami kwa brashi sawa. Hebu tuondoke. Nitakumbuka ukatili huu wa leo. Sisi akina Ngosha tutarudisha walichotufanyia huko mbeleni,” Joel alisema huku akitulia.
“Ndiyo. Tutarudisha walichotufanyia.” Lisa aliitikia kwa kichwa.
Sura ya: 353
Siku iliyofuata baada ya Nina kuhukumiwa, Joel alitangaza hadharani kwamba amemfanya Lisa kikamilifu

kama mrithi wake na mrithi wa urithi wake. Zaidi ya hayo, Lisa angekuwa msimamizi wa kila jambo, liwe kubwa au dogo, alipokuwa amelazwa hospitalini.
Hapo ndipo watumiaji wa mtandao walipogundua kwamba utajiri wa Joel ulifikia kiasi cha dola za Marekani bilioni tatu. Pamoja na thamani ya soko la kampuni ya Mawenzi Investments, ilimaanisha kwamba Lisa angekuwa mwanamke tajiri zaidi nchini Kenya.
Si hivyo tu, lakini mitandao pia ilisheheni picha mbalimbali za urembo wake na sifa zake za elimu ya juu. Mamia ya maoni yalitiririka kufuatia habari hiyo kusambaa kama upepo mitamdaoni;
[Nimekuwa mmoja wa mashabiki wake. Ni mwanamume gani atastahili mwanamke tajiri, mrembo, na mwenye

kipaji kama yeye?]
[Hivi, hata anahitaji mwanaume kweli? Si bora kwake kuwa single? Anaweza hata kubadili kati ya wavulana wachache na wazuri wakati wowote anaotaka.]
[Ni ukumbusho tu kwamba yeye ndiye mke wa zamani wa Alvin Kimaro.]
[Hivi Alvin Kimaro ni kipofu? Lisa ni dhahiri kuwa ni bora kuliko Sarah kwa sura, thamani halisi na urembo.] Mashabiki wa Sarah ambao hawakuridhika walionekana kumtetea pia.
[Sarah ana shida gani? Yeye ni mwanasaikolojia maarufu. Ana kipaji na mzuri pia. Kando na hilo, yeye ndiye mmiliki wa New Era Advertisings.]

[Kwani ni nini ikiwa yeye ni mwanasaikolojia? Lisa pia ni miongozi mwa wabunifu bora wa Kilimani Group, na mkurugenzi mkuu wa ubunifu wa kampuni hiyo]
[Kilimani Group ni nini? Sijawahi kusikia.]
[Jibu mbele yangu. Ni sawa kama hujui, lakini tafadhali usifichue ujinga wako. Utaiona mara tu unapotafuta kwenye mtandao. Kilimani Group ni kampuni ya ujenzi maarufu na yenye mapato ya juu zaidi Afrika. Watu wengi wenye vipaji katika Kilimani Group ni wasanifu mashuhuri wa kimataifa ambao wamepokea tuzo nyingi, na mapato yao ya kila mwaka yanazidi makumi ya mabilioni kwa urahisi. Ili kuwa afisa mkuu wa kubuni wa Kilimani Group,

lazima awe mmoja wa wasanifu watano bora Afrika, angalau. Lisa alishinda tuzo kadhaa huko Tanzania na hapa Kenya kama vile Grand-Prix award ya Lexus Crowns]
[Hiyo haiwezekani. Lisa bado mdogo sana. Acha kukuza mambo.]
[Naweza kuthibitisha hilo. Siyo ya kujisemea tu. Baada ya kuhitimu kutoka chuo kikuu, nilipata fursa ya kufanya mafunzo yangu katika Kilimani Group mwaka jana. Nilitokea kukutana na Lisa, na wakati huo, hata Lorenzo alikuwa akimheshimu.]
[Lorenzo. Unazungumza juu ya mbunifu, Lorenzo, ambaye alichukua Tuzo la ‘AAK Duracoat Awards of Excellence in Architecture’ mwaka jana?]

[Ndiyo, huyo ni yeye.]
Huku kukiwa na mjadala mzito kwenye mtandao, Kilimani Group ilichapisha kimataifa picha ya Lisa: [Bi Lisa Jones, afisa mtendaji mkuu wa kampuni yetu, ambaye alichukua nafasi hiyo mwaka jana.]
Habari hizo zilishangaza Kenya nzima. Watu wengi walitoa maoni kwenye akaunti ya Facebook ya KIM International.
[Bwana Kimaro, hadhi ya mke wako wa zamani imekuwa juu sana. Unajuta?]
[Haha, Alvin Kimaro, asante kwa kumtaliki Lisa wetu. La sivyo, asingekuwa hapa alipo leo.]
[Bwana Kimaro, tafadhali usijute na uje

kumtafuta Lisa wetu siku zijazo.]
Kwa siku moja nzima, mratibu wa ukurasa wa Facebook wa KIM International alikuwa na kazi ya kufuta ujumbe mmoja baada ya mwingine, lakini maoni hayakuwa na mwisho, kadri alivyoyafuta ndivyo yalivyozidi kuingia. Jambo hilo lilimfanya aingiwe na wasiwasi kiasi cha kutokwa na jasho.
Wakati huo, mkutano wa ndani wa ngazi ya juu wa KIM International ulikuwa ukiendelea. Jack alikuwa akitazama chini kwenye simu yake wakati ghafla alifoka. Chumba cha mikutano, ambacho kilisikika sauti ya Alvin pekee, kilikuwa kimya sana. Kila mtu alitazama kuelekea Jack.
Umbo la Alvin la kifahari liliegemea nyuma, na kalamu iliyokuwa mikononi

mwake akaitupa mezani. Macho yake makali yalikuwa ya hasira kali. “Meneja Mkuu Kimaro unajishughulisha na nini? Kwanini haupo pamoja nasi kwenye mkutano?”
Jack aligusa pua yake. “Unataka kujua kweli?” Wasimamizi wakuu walishusha pumzi zao. Waliweza kuhisi hali ya hewa ikiwa imeanza kuchafuka. Wawili hao walipokaa pamoja haikupita hata dakika tano bila chumba kugeuka kama Urusi na Ukraine.
“Ninaangalia akaunti rasmi ya Facebook ya kampuni. Inakaribia kulipuka.” Jack alitabasamu bila kufafanua. "Inahusiana na wewe, Mkurugenzi Kimaro."
Meneja mmoja alicheka na kusema, “Lazima ni watu wanaompongeza Mkurugenzi Kimaro na Bi. Njau kwa harusi yao.”

"Hiyo ni sawa. Hivi majuzi, watu wengi walikuja kwenye kampuni kutoa baraka zao. Mkurugenzi Kimaro ndiye mtu tajiri zaidi wa Kenya.”
Alvin alibaki kutojali, lakini alikubaliana na kile wasimamizi wakuu walisema. Hata hivyo, hakupendezwa na mambo hayo hata kidogo. "Kwa hivyo ... hiyo ndiyo sababu umakini wako ulizunguka kwenye simu yako katika mkutano muhimu wa kampuni?"
“Hapana, umeelewa vibaya. Inahusu... mke wako wa zamani.” Jack aliinua mabega yake. "Huenda hujui kuhusu hilo bado, lakini Joel tayari amemfanya Lisa kuwa mrithi wake. Wanamtandao wanajadili thamani halisi ya Lisa, na kuna mtu hata akafichua madili yake yaliyofichwa. Kumbe yeye ni

mkurugenzi wa ubunifu wa Kilimani Group. Kilimani Group tayari imethibitisha hilo.”
"Kilimani Group?" Baadhi ya wasimamizi wakuu walishangaa. "Ni ukweli? Hiyo ndiyo kampuni ya juu zaidi ya ujenzi Afrika. Wanaofanya kazi huko wote ni magwiji katika uwanja wao. Ni lazima awe gwiji kwa kuwa na cheo kama hicho.”
“Sisemi uongo. Unaweza kujiangalia mwenyewe ikiwa huniamini.” Jack alimtazama Alvin kwa kuchekacheka. “Kaka, ulijua hilo? Hata hukuniambia.”
Alvin alikosa la kusema. Hakujua jambo lolote kati ya hayo. Haishangazi Kilimani Group ilikuwa ya kwanza kushirikiana na Lisa. Mwanamke huyo... alikuwa na uwezo mkubwa, jambo ambalo

hakulitarajia.
Tayari alishangazwa na kazi nzuri aliyoifanya kuwaondoa wanahisa wasiotii wa Mawenzi Investments mara ya mwisho, lakini, hakutarajia kwamba angemshangaza tena.
Alvin alikodoa macho. Hakuweza kujizuia kupendezwa na mwanamke huyo kwa mara nyingine tena. Akivunga hamu ya kuitoa simu yake na kutazama umbea, Alvin alisema kwa ukali, “Tuko katikati ya mkutano. Ondoka kama unataka kujadili mambo mengine."
Kila mtu katika chumba cha mkutano akanyamaza. Jack aliinamisha kichwa chake na hakuongea zaidi.
Mkutano ulipelekwa haraka haraka huku

mada zikipitiwa juujuu tu. Takriban dakika 10 baadaye, mkutano ulikuwa umekamilika. Kitu cha kwanza alichofanya Alvin ni kuitazama simu yake. Alipoona habari kuhusu Lisa, karibu apige namba yake, bila kujua lengo lake ni kumpongeza au kumdhihaki, lakini sekunde moja baadaye, akakumbuka kwamba alikuwa mwanamume aliyeoa.
Alijizuia na kuwasha sigara. Alipitia kila habari hadi mwishowe, macho yake yakatua kwenye picha nzuri ya Lisa. Alipigwa na butwaa kwa muda na hakuweza kupinga kuhifadhi picha hiyo. •••
Mawenzi Investments.
Wakati Lisa alipopita kuelekea ofisini kwake, nusura azime kwa kelele za pongezi kutoka kwa wafanyakazi wake.

"Mkurugenzi Jones, wewe ni wa kushangaza sana."
Kwa kustaajabishwa, Amba alikuwa akihaha kwa kugonga mikono na magoti yake. "Vyombo vya habari vingi vimepiga simu kuomba mahojiano ya kipekee na wewe asubuhi ya leo. Ulifanya nini hasa kubadilisha hali yako katika miaka mitatu?"
'Nilitegemea kitu pekee cha thamani alichonipa Mungu, akili, bila shaka.” Lisa alisema kwa utulivu. “Tafadhali kataa mahojiano yote ya kipekee. Niko busy,”
“Sawa, lakini umealikwa kuhudhuria Starlight Gala na Times Media kesho usiku. Bwana Ngosha awali alitakiwa kuhudhuria, lakini amelazwa, kwa hiyo mwaliko ulikuja kwako.”

Sura ya: 354
Lisa alipokea kadi ya mwaliko na kuichezea mikononi mwake. "Je, kuna maana yoyote kwa aina hii ya mialiko?"
"Watu mashuhuri kutoka kila tasnia watakuwepo. Nilisikia kwamba Cindy, mwimbaji mashuhuri wa kike unayemchukia zaidi, atatumbuiza pia.” Amba alimchombeza Lisa kwani aliogopa asingehudhuria mwaliko huo. “Ikiwa huna shughuli nyingi, unaweza kwenda kumpa wakati mgumu kidogo, si unakumbuka wakati ule alivyokuwa anachonga sana akiwa na Sarah?”
Sekunde chache baadaye, Lisa alicheka. “Wow, Msaidizi wa miye, unazidi kuwa mkorofi zaidi kama bosi wako. Cindy ni mpenzi wa Chester.

Huogopi kwamba nitaingia kwenye matatizo?”
Amba alisema huku akitabasamu, “Wewe ni mrithi wa kampuni ya Ngosha na mbunifu mkuu wa Kilimani Group sasa. Thamani ya kampuni ya Mawenzi Investments imepanda hata maradufu. Watu wengi sana wanajaribu kukufahamu. Ingawa familia ya Chokaina nguvu, wewe pia si haba. Ni lazima wajiulize mara mbili kwa sasa kabla ya kukufanyia ujinga wowote.”
“Una hoja hapo. Kwa bahati nzuri, nina jambo langu na Chester pia.” Lisa alifunga kadi ya mwaliko. Lisa alikuwa bado na kinyongo kwamba hospitali ya familia ya Choka ilimfukuza Joel mara ya mwisho.
•••
Usiku. Kwenye lango kuu la ukumbi wa

mikusanyiko, Ssafu na safu za magari ya kifahari yaliingia. Kwenye zulia jekundu refu, Lisa alishuka kutoka kwenye gari nyeusi aina ya Rolls-Royce Ghost. Alivalia mavazi ya nguva yenye matundu ya almasi, ambayo yalionyesha kikamilifu mikunjo yake yenye umbo la S. Iliyolingana na sifa zake maridadi na rangi ya korosho iliyokoza, alionekana kama binti wa kifalme moja kwa moja kutoka kwenye jumba la malikia. Alikuwa wa kisasa, wakifahari, mzuri, na asiye na mbwembwe. Angeweza kuelezewa kwa kila kivumishi cha sifa.
Wanawake wasomi na watu mashuhuri waliovalia mavazi ya kifahari usiku huo walipauka kwa kulinganisha na Lisa. Si nyuma ya Lisa, Cindy alishuka kutoka kwenye gari aina ya Bentley Bentayga. na kumshika mkono Chester. Hata

hivyo, Lisa alivutia macho sana hivi kwamba hakuna mtu aliyemwona Cindy pindi anaingia.
Cindy akasaga meno kwa chuki. Times Media ilikuwa moja ya makampuni makubwa ya Kenya, kwa hivyo hapo awali alikuwa amepanga kuwa bora usiku huo. Hata vazi alilovaa lilibuniwa na mbunifu wa hali ya juu, ambaye alikuwa ameombwa na Chester kwa muda mrefu. Kamwe hakutarajia kwamba Lisa angemwibia umaarufu tena. Hata alipata nafasi ya kusaini mkataba na Mawenzi Investments kama balozi wao, lakini Lisa aliuvunja.
Kwanini hakufa miaka mitatu iliyopita? Ikiwa angefanya hivyo, Cindy asingekuwa mtu wa kudharauliwa sana. Ilisikitisha zaidi kwamba Lisa alikuwa sasa mrithi wa Ngosha Corporation.

Hakuna kinachomkera mwanadamu zaidi ya mafanikio ya mwanadamu mwingine.
"Chester, sikuwahi kufikiria kwamba Lisa angezingatiwa sana. Ulikuwa unaangaziwa popote ulipoenda." Cindy alificha wivu wake na kumtania yule mtu mashuhuri kando yake.
Chester akarekebisha miwani yake yenye fremu ya dhahabu na kumtazama kwa mawazo. “Kwanini? Unamwonea wivu?”
Cindy alishangaa, lakini hakuthubutu kufsema ujinga wowote mbele ya Chester. “Hilo ni hakika. Ni nani hapa ambaye hatamuonea wivu? Ana bahati sana.”
“Una bahati pia. Unapaswa kujifunza

kuridhika na ulicho nacho.” Sauti ya Chester ilikuwa ya kubembeleza, lakini ilikuwa ya kutisha.
Cindy alitabasamu huku akisema, “Nimeridhika sana kukutana na wewe. Lakini... Alvin Kimaro na Sarah watakuwa hapa usiku wa leo pia. nina wasiwasi sana...”
“Hakuna haja ya kuwa na wasiwasi kuhusu watu wengine. Kila mtu yuko ndani ya jumuiya moja nchini Kenya na hatimaye tutagongana tu. Sarah lazima azoee.”
Baada ya Chester kusema kwa utulivu, Cindy aliweza tu kuinamisha kichwa chake na kunyamaza.
Lisa alipoingia kwenye jumba la karamu, aligundua kuwa kulikuwa na

watu wengi waliofahamiana naye usiku huo, kama vile Jerome na Melanie, Lea na Mason. Pia kulikuwa na Jack, Kelvin, Rodney...
Lisa akacheka. Hata damu katika mwili wake alihisi ikikimbia kwa kasi.
Usiku huo ulikuwa unaenda kuwa wa kuvutia. Baada ya miaka mitatu, watu waliofahamiana wote walikusanyika mahali pamoja.
Kelvin aliinua glasi yake kuelekea kwake kutoka mbali. Punde, alipokea ujumbe wa WhatsApp kutoka kwake: [Ninajua unalenga nini, kwa hivyo sikukukaribia. Lakini nitakuwa nikikutazama.] Moyo wa Lisa ukapata joto.
Jack, ambaye alivalia suti nyeupe, alimwendea kwa furaha na kumpa glasi

ya mvinyo. “Sikutaka kuhudhuria mara ya kwanza, lakini niliamua kuja mara moja niliposikia kwamba na wewe ungehudhuria. Usiku wa leo utapendeza sana.”
“Pamechangamka kweli kweli. Nimependa sana.” Lisa alikunywa mvinyo kabla ya mdomo wake kuinua tabasamu la kuvutia.
Mwangaza uliangaza machoni pa Jack. Ghafla akahema kwa majuto. “Usingeolewa na Alvin kwanza, hakika ningekuoa. Lakini nikikutongoza sasa hivi, wanafamilia wa Kimaro bila shaka watanisema vibaya. Hakuna mtu ambaye angeweza kukubali ndugu wawili kuoa mwanamke mmoja.”
“Kwa bahati nzuri, hukunitongoza. ningekubali.”

“Kwa nini?”
"Kwa sababu nina wachumba wengi sana." Lisa aliwatupia macho wanaume waliokuwa wakimtazama kwa pembeni. "Angalia, kuna watu wengi ambao wanajaribu kumrithi kaka yako."
“Ni kawaida. Sasa wewe ndiye mwanamke mrembo, mwenye kipaji, na mwenye thamani ya juu nchini Kenya.” Jack alinyoosha mkono wake kwake. "Unaweza kucheza na mimi? Ninataka kuwa mtu anayeonewa wivu sana usiku wa leo. Nipe furaha hii."
“Sawa.” Lisa aliweka mkono wake kwenye kiganja chake kikubwa, na wote wawili wakatembea kwenye uwanja wa muziki.

Walichukua nafasi kama wanandoa wakamilifu. Mara moja walivutia wivu na porojo za watu wengi, lakini wote wawili walipuuza yote na badala yake wakaanza mazungumzo.
“Sema, kwa nini umekuja leo? Kuharibu sherehe?" Jack aliuliza kwa utani.
Lisa akatumbua macho. "Ni tamasha la Times Media, kwanini niharibu? Nimekuja tu kucheza gitaa na kufurahi na kujumuika na marafiki.”
"Unajua kucheza gitaa?" Jack akakohoa. “Walimwalika Cindy kutumbuiza usiku wa leo. Yeye ni mtaalamu.”
“Ni vizuri. Nataka kutumbuiza baada yake.” Lisa alidhamiria. "Niliandika wimbo mpya, na nahisi watu

wataupenda sana. Unaweza kuusikiliza kidogo?”
Jack nusura apoteze stepbaada ya Lisa kumwimbia sikiono kipande cha wimbo huo. “Lisa, unataka kumchokoza Cindy? Huu wimbo ameuachia hivi karibuni na unafanya vizuri...”
“Ni wimbo wangu.” Lisa alimnong’oneza huku akitabasamu.
“Toka lini umekuwa mwanamuziki?"
“Huniamini?” Lisa alimkazia macho. “Mimi ndiye niliyeandika nyimbo maarufu za Cindy. Nilikuwa nikicheza gitaa na piano kabla hata Cindy hajajifunza kuimba. Ndoto yangu ya kwanza ilikuwa kuwa mwanamuziki lakini mazingira yalinibadilisha kuwa injinia. In fact ni kwamba Cindy alivutika

kuwa muimbaji kupitia mimi.”
Mshangao ulikuwa umeandikwa usoni mwa Jack. “Kwa hiyo huu wimbo mpya ni wewe pia uliuandika?”
“Sio huo tu, hata ule uliomtoa kwenye gemu niliuandika mimi. Ni vile tu kwamba amesahau kushukuru. Ni lazima nimfundishe hilo leo.” Lisa alilalamika.
"Una ujuzi gani mwingine ambao siujui?" Jack alikosa la kusema.
“Mimi ni hazina. Maisha yangu ya utotoni yalikuwa magumu sana hapo awali, na kipaji changu kilizuiwa na wengine. Sasa, ni wakati wangu wa kuangaza.” Lisa aliongea kwa kujiamini. Jack hakuweza kujizuia kuangua kicheko.

Sura ya: 355
Alvin na Sarah walipoingia, mara wakawaona Jack na Lisa wakiwa katikati ya ukumbi wa ngoma. Walikuwa wakicheza pamoja kama wanandoa waliokuwa na ‘chemistry’ nyingi. Mmoja alikuwa mrembo kama binti wa kifalme, wakati mwingine alikuwa amevaa suti nyeupe kama mtoto wa mfalme.
Chini ya mwanga, walizungumza na kucheka. Mara kwa mara, Lisa alikuwa akisema jambo ambalo lililomfanya Jack acheke kwa sauti. Pia alikuwa na tabasamu la kupendeza na tulivu usoni mwake. Tukio lile liliuumiza sana moyo wa Alvin. Wakati huo, alikuwa na hamu ya kukimbilia na kuwatenganisha wote wawili.
Kile Alvin alichohisi kilimfanya amkaze

kwa nguvu mkono Sarah. Sarah akashusha pumzi na kugugumia kwa sauti ya chini. "Alvinic, unaniumiza ..."
“Samahani.” Alvin aliachia mshiko wake kwa maneno ya kuomba msamaha, lakini macho yake hayakutoka katikati ya sakafu ya dansi.
Sarah alikunja ngumi kwa hasira.
Harusi yake na Alvin ilipaswa kuzungumziwa zaidi wakati huu, lakini Lisa alionekana kutawala kila mahali na kuiba umaarufu wake. Si hivyo tu, watu wengi walikuwa wakimlinganisha na Lisa kwenye mitandao. Ingawa alikuwa ameitangaza harusi yake hadi kwenye mabngo ya barabarani, bado alishindwa kabisa kupambana na Lisa.
Hatimaye alipata kuhudhuria hafla hiyo na Alvin, lakini Lisa alionekana kama

mzimu unaowasumbua. Kilichomfanya azidi kuchanganyikiwa ni kuona wivu machoni mwa Alvin. Ilikuwa ni aina ya wivu ambayo mwanaume angekuwa nayo kwa mwanaume mwingine.
“Alvinic, Aunty Lea yuko pale. Twende tukasalimie,” Sarah alisema kwa sauti nyororo ili kumpotezea mawazo ya Lisa.
“Sawa.” Walikuwa familia, baada ya yote, kwa hiyo walipaswa kutendeana vizuri hadharani.
Wote wawili walitembea kuelekea kwa Lea. Lea alikuwa akibadilishana maneno na rafiki wa zamani. Rafiki yake wa zamani alimtania, “Binti-mkwe wako na mwana wako wako hapa.”
“Habari yako, Aunty Lea,” Sarah aliwasalimia wale wanawake wawili.

"Ah, ana tabia nzuri sana." Rafiki wa zamani wa Lea alipoona kwamba familia ya Lea imeingia, alipata kisingizio na akaondoka kwenda kuzungumza na watu wengine.
Lea alimpa Sarah mtazamo wa chuki. Alimchukia sana Sarah, hasa pale kila Mzee Kimaro na Bibi Kimaro walipotaja kuharibika kwa mimba ya Lisa enzi hizo alipokuwa amebeba mapacha. Wanandoa hao wazee wangeizungumzia kila alipoenda kuwasalimia katika miaka hii michache. Kama si Sarah, Lisa asingepoteza ujauzito wake na angekuwa ni Bi. Kimaro zamani sana.
Ingawa Lea hakumpenda sana Lisa hapo awali, alifikiri kwamba Sarah alikuwa mkatili sana. Sarah aliweza hata kujihusisha na mwanaume ambaye

alikuwa ameoa na alikuwa akitarajia kupata watoto. Mwishowe, alisababisha mke halali apoteze mimba. Ilikuwa wazi kwamba Sara hakuwa na hisia zozote za maadili.
Sarah alionekana kuwa na huzuni baada ya kuona Lea anampuuza.
Alvin aliona ni vigumu sana kuvumilia na akasema, “Mama, salamu ya Sarah.”
“Najua. Mimi si kiziwi,” Lea alijibu bila kujali.
Sarah alilazimisha tabasamu na kusema, “Aunty Lea, nitakuletea chakula.” Hakutaka kujaribu kupata kibali cha Lea ili tu kukwepa asikutane na karipio kali.
Alipoona Sarah anaondoka kwa huzuni, Alvin alikasirika. “Inaonekana sikupaswa

kuja kukusalimia. Na kwanini hukumtupia jicho kali kama hilo Jack na kumwacha acheze na Lisa? Shemeji wa zamani na shemeji yake, ni aibu sana.”
Hapo awali Lea alifikiri kwamba haikuwa sawa pia, lakini kwa silika alienda kinyume na maneno ya Alvin aliposikia sauti yake. “Wewe na Lisa tayari mmeachana. Ni muziki tu wanacheza na sio mapenzi. Watu wengine hata hawasemi chochote. Ni wewe tu unayenyoosha vidole hapa. Unajiingiza sana katika mambo ya wengine.”
“Hata ikiwa watu wengine wanasema jambo fulani, hawatalisema mbele yako,” Alvin alijibu kwa ukali.
“Umekosea. Wanafikiria tu njia za kufahamiana na Lisa sasa. Yeye ndiye mrithi wa Ngosha Corporation na mkurugenzi mkuu wa muundo wa

Kilimani Group. Kwa utambulisho huu, hakuna mtu atakayetaka kupitisha nafasi hii ili kumjua. Kutakuwa na manufaa na hakuna hasara iwapo Jack atajenga uhusiano mzuri na Lisa.” Lea alisema kwa hisia ngumu, “Alvin, lazima uelewe kwamba Lisa si Lisa tena wa zamani. Ana uwezo wa kuongeza thamani ya soko la Mawenzi Investments kwa urahisi na kuifanya iingie kwenye orodha 100 bora za Kenya.
"Mbali na hilo, yeye ndiye binti pekee wa Joel Ngosha na mwanamke wa kweli wa familia ya Ngosha. Ingawa alikuwa ameolewa hapo awali, bado kuna wanaume wengi bora kutoka kwa familia tajiri ambao wanataka kumuoa na kufahamiana naye. Ikiwa huamini, jionee mwenyewe.”

Alvin alitazama tena ulingo wa muziki. Lisa alikuwa tayari amemaliza kucheza wimbo na Jack. Baada ya hapo, alialikwa kwa nyimbo nyingine na Erick Malugu mwenye uwezo na mwonekano mzuri, aliyekuwa mkurugenzi wa S.E Group. Alvin alikunja ngumi bila fahamu.
Lea akahema. "Wakati mwingine, huwezi kuwadharau wengine. Wewe unajiona ndiyo mwenye kujua kila kitu? Uvumi niliousikia zaidi leo haukuwa juu ya watu kumcheka Jack, lakini wanazungumza juu ya jinsi ulivyoachana na Lisa na kumuoa na Sarah! Atakuletea kitu gani kizuri? Kila mtu katika jamii ya juu anamuepuka Thomas Njau. Ikiwa sio wewe kuisaidia New Era Advertisings, hakuna mtu ambaye angekuwa tayari kushirikiana nao.”

“Imetosha, usiseme tena.” Alvin tayari alihisi kuudhika, na alizidi kukosa raha kusikiliza maneno ya Lea. “Nilipona kutokana na ugonjwa wangu kutokana na matibabu ya Sarah. Kama si kutiwa moyo na Sarah wakati huo katika hospitali ya magonjwa ya akili, ningekuwa tayari nimekufa.”
“Lisa aliwahi kukutia moyo pia. Ungeniua wakati ule isingekuwa yeye,” Lea alifoka.
Alvin alipigwa na butwaa, akahisi uvimbe kooni. "Je! kitu kama hicho kilitokea hapo awali?"
Lea alikosa la kusema. “Hivi ndivyo Sarah alivyoutibu ugonjwa wako? Umesahau kila kitu kizuri kuhusu Lisa."
Alvin alikuwa ameduwaa kutokana na maneno yake. Hata hivyo, alipojaribu

kutafakari kwa kina, ghafla kichwa kilianza kumuuma. Aliegemeza kichwa chake kwenye mikono yake.
Alvin alipoona kwamba Mason na Jerome walikuwa katika mazungumzo ya kina si mbali naye, alisema kwa upole, “Mtazame Mason. Alisema hakuwa na hatia, lakini bado ana uhusiano wa karibu na familia ya Campos. Bado unamwamini?”
Lea akatazama juu, na sura yake ikageuka kuwa mbaya mara moja. Aligeuka na kuelekea kwa Mason. "Mason, njoo hapa kwa sekunde."
Lakini, alingoja kwa dakika tatu kamili kabla ya Mason kumjia na tabasamu usoni mwake. “Lea, kuna nini?”
Lea akamtazama. Alihisi kwamba

alikuwa akizidi kumsoma vizuri. "Mason, si nilikuambia toka mwanzo kuweka umbali kati yako na familia ya Campos? Hasa Jerome—”
“Lea, jina langu la mwisho ni Campos. Pia ni familia ya wazazi wangu. Siwezi... kutowasiliana na familia ya Campos kwa sababu tu ya mpasuko kati ya familia ya Campos na familia ya Kimaro.” Mason alinyoosha mikono yake. "Mbali na hilo, maendeleo ya familia ya Campos miaka hii hayajazuia familia ya Kimaro kwa njia yoyote ile. Huoni kwamba familia hizo mbili zinaendelea kukua pamoja katika miaka ya hivi karibuni?”
Baada ya mshangao wa muda, Lea alisema kwa hasira, “Haijaizuiaje familia ya Kimaro? Baadhi ya kampuni tanzu za KIM International zilinyonywa faida

mara kwa mara na kampuni ya Campos. Si hivyo tu, kama isingekuwa msaada wa KIM International wakati huo, familia ya Campos—”
”Kwamba Familia ya Campos ingekuwa kama ilivyo leo? Nilijua ungesema hivyo tena,” Mason alimkatisha. "Familia ya Campos ipo kama ilivyo leo kupitia umoja wa wafanyikazi wote katika kampuni ya Campos. Isitoshe, kwani hatuendelei vizuri hata bila msaada wa KIM International miaka hii mitatu?”
"Kama nisingekupa makumi ya mabilioni hapo awali, unafikiri siku hii ingefika kwa Campos Corporation-"
“Sitaki kugombana na wewe, Lea.” Mason alimkatisha. “Siku zote ni sisi, familia ya Campos, ambao tunashutumiwa kwa kupanga njama na

kula njama kila tunapopambana kutoka kwenye dhiki. Ni kana kwamba familia ya Campos inapaswa kuwa na shukrani kwa familia ya Kimaro milele,” Mason alisema kwa kuudhika. Akageuka na kuondoka.
Lea alihisi ubaridi moyoni mwake. Mason hakuwa hivyo hapo zamani. Hata hivyo, alikuwa akizidi kukosa subira naye kadiri muda ulivyopita.
TUKUTANE KURASA 356-360
ONYO: Ni marufuku kusambaza, kukopi wala kuuza kazi hii kwani endapo kama tutakubaini basi sheria itachukua mkondo wake (By: Official Dully)
 
LISA KITABU CHA NANE (8) SIMULIZI........................LISA KURASA..................356 - 360
PRESENT: SIMULIZI ZA DULLY

Sura ya: 356
Baada ya Mason kuondoka, alienda moja kwa moja kwenye bustani iliyokuwa nje. Nyuma ya kitalu cha maua gizani, mwanamke alionekana na kushika mikono yake shingoni
mwake. "Kwanini ulitoka peke yako na kumwacha yule mwanamke mzee, Lea?"
“Kwa sababu nilikukumbuka. Hakika Lea ni mzee ukilinganisha na wewe." Mason alizunguka kiuno cha mwanamke huyo. Walianza kubusuana na kubadilishana joto.
“Mpenzi, hapa tutakutwa, ninapafahamu mahali ambapo pamejificha zaidi. Twende huko.” mwanamke alisema kwa utamu.

"Sweety babe, twende huko sasa.” Mason alitembea kuelekea nyuma huku akiwa amemkumbatia yule mwanamke. Walipeana peksi kadhaa huku wakitembea.
Hata hivyo, hawakutambua kwamba Lisa alikuwa ametoka nyuma ya mti wa kijani kibichi ili kuongea na wanaye kwa njia ya video. Aliwafumania wakati wanaondoka. Simu ambayo aliishika ilikuwa ikirekodi video. Alipotaka tu kuwafuata, mkono ukatoka nyuma na kumpokonya simu yake. Aligeuka nyuma kutazama. Alimuona Alvin akiwa ameshika simu yake na kuitazama ile video. Mara moja naye akaishiwa pozi.
"Huoni aibu kama mwanamke kwa kurekodi mambo haya?" Alvin alivunga. Baada ya muda, alimtazama Lisa kwa sura isiyo na furaha.

Lisa hakuwa na la kusema. Alifikiri kwamba Alvin hakuwa na furaha kwa sababu aliona tu video ya baba yake wa kambo akiwa na uhusiano wa kimapenzi na kibinti kidogo, lakini hakutarajia angezungumza naye.
“Kwanini nione aibu? Wewe ndo wa kuona aibu.” Lisa alitabasamu huku akisema. “Angalia jinsi baba yako wa kambo alivyo wa ajabu. Ana zaidi ya miaka 50 lakini bado anaweza kujihusisha kimapenzi na mwanamke huyo mdogo sawa na binti yake.”
"Futa video hiyo kutoka kwenye simu yako." Alvin alihisi kuudhika ajabu.
"Unafikiri mimi ni kompyuta ambapo unaweza kufuta chochote upendavyo?" Lisa akairudisha simu yake. Aligeuka,

akitaka kuondoka.
Alvin alimshika huku macho yake yakionekana kuwa makali. "Nitumie video hiyo."
Lisa alimnyooshea mkono. Chini ya mwanga wa mwezi, mikono yake midogo midogo ilionekana mizuri sana. Alivaa bangili ya almasi mkononi mwake. Ilikuwa rahisi, lakini ngozi yake nzuri ilifanya ionekane ya kifahari.
Moyo wa Alvin ulirukaruka. "Unataka nini?"
"Nilipe kwa uhamisho wa hakimiliki." Lisa alipepesa macho yake mazuri kana kwamba ni jambo la kawaida. "Video ya Mason itakuwa na thamani kubwa. Ni mkwe wa familia ya Kimaro na mtoto wa kiume mkubwa wa familia ya Campos.

Taarifa hizi lazima ziwe na thamani ya angalau milioni 80."
Alvin alimpiga jicho kali. “Milioni 80? Kwanini usiibe benki tu?”
“Alvin Kimaro, usinifikirie kuwa mimi ni mtu asiye na uzoefu na asiyeelewa soko. Paparazi yeyote anaweza kupata makumi ya mamilioni ya shilingi kwa urahisi kwa kashfa ya mtu Mashuhuri. Ikiwa hauko tayari kulipa, ninaweza tu kuuza video kwa vyombo vya habari. Lazima kuna watu watapigania kulipia, haswa familia ya Campos. Hata wataizika kwa mabilioni ya shilingi, nadhani.” Lisa aligeuka na kuondoka kwa utulivu.
Alvin alihisi anaumwa na tumbo kutokana na kumkasirikia Lisa. Alitakiwa kuhamisha video hiyo kwenye simu

yake wakati alikuwa amempokonya simu mapema. “Sawa, nitalipia. Nihamishie video hiyo.”
“Nipe pesa kwanza ndo nikuhamishie video. Wakati wa kufanya biashara, mimi huwa mwaminifu kwa wateja wakubwa na wadogo.” Lisa aliinua nyusi zake.
Mdomo wa Alvin ulitetemeka. Akatoa simu yake na kumhamishia pesa mara moja. Macho ya Lisa yalikuwa yamepinda huku akitabasamu alipoona kiasi hicho cha pesa. Tabasamu lile tamu liliujaza moyo wa Alvin hadi ukingoni.
Bado alikuwa na hasira kidogo mwanzoni, lakini ilikuwa ni kana kwamba hasira yake ilitulizwa kwa ghafula. Milioni 80 tu? Angeweza

kuirejesha kwa sekunde chache tu. Kwa thamani ya biashara zake kama mtu tajiri kabisa, alikuwa akiingiza angalau milioni 500 kwa saa, awe mamcho au amelala! Milioni 80 ilikuwa psa ndogo tu. Akiwa na huzuni, alipokea video hiyo kwenye simu yake.
“Kwaheri. Ilikuwa ni furaha kufanya biashara na wewe wakati huu." Lisa akageuka na kuondoka. Alikuwa ametoka nje kwa muda tu na kupata milioni 80. Jamani, alitaka kuhudhuria karamu nyingi zaidi kama hiyo.
“Subiri...” Alvin alifoka bila fahamu alipomuona akiondoka.
“Kuna kitu kingine chochote?” Lisa alitazama nyuma. Sehemu ya nywele zake ndefu za rangi ya korosho zilipeperushwa na upepo wa usiku,

ukifichua uso wake wenye kustaajabisha na shingo yake kama ya swala.
Koo la Alvin likamkauka. Hakuweza kujizuia kusema, “Usicheze na Jack tena kuanzia sasa. Inatia aibu.”
"Nicheze naye, nisicheze naye, hiyo haikuhusu. Wewe povu linakutoka la nini? Mwanamume hapendezi kuwa mbea"
Alvin alikunja uso. "Kwa hiyo mimi ni mmbea?"
“Kwa sababu unaendelea kujiingiza katika mambo ya watu wengine,” Lisa alijibu kwa kejeli.
Alvin alicheka. “Wewe ni mke wangu wa zamani. Jack ni kaka yangu. Je, watu watasema nini ikiwa nyinyi mtakuwa

pamoja? Nyinyi wawili hamna aibu, lakini mimi najali heshima yangu.”
“Unamchukulia Jack kama kaka yako? Ulimpiga upendavyo katika kampuni na kumfanya awe kicheko Nairobi nzima,” Lisa alimkaripia, “Sijawahi kuona mtu mbabe na mbinafsi kama wewe.”
"Kwa hivyo unajisikia vibaya kwa Jack sasa?" Alvin alikodoa macho. Hasira ilimtoka machoni pake.
“Aliokoa maisha yangu. Kwa hivyo ni lazima niwe upande wake?” Lisa alitabasamu aliposema, “Hata hivyo sisi sote tupo single. Kuna tatizo gani hata tukiamua kuwa wapenzi? Jack pia ni handsome kuzidi hata mtu fulani.”
“Thubutu!” Macho ya hasira ya Alvin yalionekana kana kwamba yanataka

kumrukia. "Familia ya Kimaro haitakubali hili."
“Haijalishi hata kama hukubaliani, kwa sababu Jack ametelekezwa katika Kampuni ya KIM. Anyway, hata mkimtimua kabisa, anaweza tu kufanya kazi katika kampuni yangu. Inaweza kutokea kwamba nina kampuni nyingi sana ambazo siwezi kuzisimamia zote. Nani anajua? Huenda utaniita 'shemeji' siku zijazo." Lisa alimtazama. "Hujui kwamba maisha yamejaa mshangao?"
Kifua cha Alvin kilidunda hadi kichwa kilimuuma. Aligundua kuwa asingeweza kufanya mazungumzo na Lisa. Kila mara alikuwa akikasirika sana hivi kwamba alihisi kama alikuwa karibu kupata mshtuko wa moyo.
"Lisa, ningependa kukuangamiza kuliko kukuacha wewe na Jack kuniingiza

katika aibu."
“Usijali, nilikuwa najisemea tu hata hivyo. Kuna watu wengi sana wanajaribu kunitongoza sasa. Jack ni chaguo moja wapo tu. Bado sijachagua mmoja.” Lisa aliondoka huku akionyesha dharau baada ya kusema hivyo.
Alvin aliupiga mti kwa hasira. Walikuwa wametalikiana, lakini kwa nini hisia zake bado zingeweza kutawaliwa na mwanamke huyo? Alitamani hata kumficha alipomwona akicheza na mwanaume mwingine.
Aliporudi kwenye jumba la karamu, Cindy alikuwa akicheza piano.
Sauti tamu na laini ya kuimba kucheza kwake ilisikika katika jumba la karamu. Wageni walifurahia onyesho hilo kwa

kuwa watu wengi katika familia za matawi ya juu walikuwa na mapenzi fulani na piano na muziki.
Watu walikuwa wakizungumza kumsifia;
"Cindy sio diva wa tasnia ya muziki bure. Anaweza kuimba noti za chini na za juu huku akicheza piano bila kuhitaji kuvuta pumzi.”
"Hiyo ni kweli. Uwezo wake sio wa maonyesho tu. Si ajabu Dokta Choka amekuwa akimsaidia miaka hii michache.”
"Sio tu kwamba anamuunga mkono, lakini pia anamdekeza sana. Chester humpa chochote anachotaka. Hata alimsaidia alipofanya mabadiliko kutoka kuwa mwimbaji hadi kuwa nyota wa filamu.”

"Ulienda wapi? Nilikutafuta kila mahali. Jack alikimbilia upande wa Lisa kwa haraka na kusema. “Unafuata baada ya Cindy...”
"Nimetoka tu kutafuta pesa kidogo." Lisa alimwonyesha milioni 80 ambazo alipata.
Jack alishtuka. "Ni nini, umepata wapi?"
"Ndugu yako." Lisa alimn”yooshea kidole Alvin ambaye aliingia kwa nyuma huku akionyesha giza totoro.
Jack alimpa dole gumba. “Nimevutiwa. Ninunulie dinner ya laki baadaye.”
“Siwezi. Bwana Malugu alisema atanirudisha nyumbani baadaye.” Lisa alipofikiria jinsi alivyokuwa amepata pesa hizo kupitia video ya baba yake,

hakuweza kujizuia kumuonea huruma Jack. Ilimsumbua kwa muda na kujikuta anashikwa na hatia. "Ili kufidia masikitiko yako ya kunikosa, nitahamisha milioni 40 kwako."
Jack alikuwa ameduwaa kutokana na mshtuko. "Wewe ... wewe ni mkarimu sana?"
“Sisi ni marafiki! Ni milioni 40 tu.” Lisa alimhamisha zile pesa bila mpangilio na kuondoka zake.
Sura ya: 357
Punde, Alvin alikuja upande wa Jack. Aliuliza kwa sura ya huzuni, "Lisa kakuambia nini?"

Jack alimulika simu yake kwa Alvin huku akitabasamu. "Hawezi kula chakula cha jioni na mimi kwa sababu anaenda kwenye miadi yake na
Bwana Malugu usiku wa leo, kwa hivyo amenihamishia milioni 40."
Wakati huo, Alvin alijionea huruma mwenyewe jinsi alivyokuwa amekasirika, kukasirika na kukasirika. Lisa alipata pesa hizo kutoka kwake na akamgawia Jack mara moja. Je, alimchukulia kuwa boya?
Subiri, alikuwa ana miadi na Erick Malugu baadaye? Alvin hakuweza kutulia tena.
Baada ya Cindy kumaliza wimbo wake, alisimama taratibu. Alitoka nyuma ya piano na kuinama. Kulikuwa na duru ya makofi ya radi katika ukumbi wa karamu. Wakati huo, Cindy alifurahi

sana. Alijua kuwa machoni pa watu hao kutoka jamii ya hali ya juu, alikuwa mtu mdogotu ambaye haonekani. Lakini, alijulikana kwa kila mtu kuwa alikuwa na kipaji adimu usiku huo.
Muda huohuo, alimuona Lisa akielekea kwake taratibu. Ni wawili tu ndio walikuwa wamesimama katika eneo ambalo vyombo vya muziki viliwekwa. Kwa wakati huo, kila mtu alikuwa amemtazama Lisa mrembo na mlimbwebde. Tabasamu la Cindy likalegea.
"Lisa, umekuja mahali pabaya? Hapa ni mahali pa kucheza piano." Cindy alilazimisha tabasamu na kusema kwa sauti ya upole.
“Sikjakosea hata kidogo. Wewe si umemaliza kucheza wimbo wako?

Nimezungumza na mratibu. Nataka kujaribu ujuzi wangu.” Nguo ya Lisa iliyojaa almasi ilifuata nyuma yake alipokuwa akiiendea piano na kuketi mbele yake.
Mwili mzima wa Cindy ukakakamaa. Aligeuka nyuma kwa haraka na kusema, “Lisa, watu ambao wako hapa leo si watu wa kawaida tu. Hata mwanamuziki maarufu, Nandy, yuko hapa pia. Si mahali ambapo unaweza kufanya mzaha wako. Ikiwa unataka kucheza piano... unaweza kucheza ukirudi nyumbani.”
“Unadhani nitajiaibisha?” Lisa alitabasamu bila kufafanua.
Cindy akabaki amebana midomo. Hiyo ilipaswa kuwa kinyume chake. Yeye pia alikuwa anamfahamu vizuri Lisa. Lisa

alikuwa na talanta ya kipekee katika muziki hapo awali. Walikuwa wamesoma piano na gitaa pamoja wakiwa shule ya sekondari. Wote walisoma kwenye shule ya ‘Dar es Salaam Independent Schools’ kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita. Lisa aliweza kujifunza kila kitu haraka na mara nyingi alisifiwa na walimu.
Lisa alikuwa akivutiwa sana na muziki kipindi hicho. Ni vile tu alitegemea kuwa mrithi wa kampuni ya familia yao Kibo Group, iliyojihusisha na mambo ya ujenzi, ndipo ilimlazimu kwenda kusomea Uinjinia wa mambo ya kubuni majengo, alipomaliza kidato cha sita. Vinginevyo angekuwa msanii mkubwa tu kwa kipaji chake. Na hata alitunga nyimbo na kumwandikia Cindy baada ya hapo. Lakini, Cindy hakuweza kupima ujuzi wake wa sasa.

Lakini Lisa asingeweza kufanya jambo lisilowezekana mbele ya umati ule wa watu maarufu. Cindy alihisi kutokuwa na utulivu moyoni mwake.
Wakati huo, wageni walianza kuzungumza juu yake pia. Macho yao yaliweka alama ya dhihaka huku wakimtazama Lisa.
Baada ya yote, Cindy alikuwa amemaliza kufunika kwa show kali. Ikiwa Lisa angeimba baada yake, bila shaka angeonekana mzaha.
Melanie alijifanya kana kwamba ana wasiwasi na kusema, “Dada, hii si karamu ya familia ya Ngosha ambapo unaweza kufanya chochote unachotaka. Isitoshe wewe ndiye mrithi aliyeteuliwa wa familia ya Ngosha sasa. Unapaswa kutunza heshima ya familia ya Ngosha.”

"Hiyo ni sawa." Joan Halua alichukua nafasi hiyo na kuunga mkono maneno ya Melanie.
Sarah alipoona kwamba kila mtu amezungumza, alisema kwa upole, “Hii ni kuhusu kucheza piano. Ni tofauti na kubuni majengo, baada ya yote. Una maoni gani, Alvinic?" Alimvuta mwanamume yule mrefu na mtanashati kando yake.
Alvin alikunja uso. Alikuwa amemsikia Lisa akiimba na kucheza gitaa hapo awali. Kwa kweli alikuwa mzuri sana. Angempoteza Cindy, na sauti yake ilisikika vizuri zaidi kuliko ya Cindy alipocheza gitaa. Lakini, hakuwa na uhakika kama ingekuwa hivyohivyo pia ikiwa Lisa angeimba huku akicheza piano. Baada ya yote, kwa kweli

hakuwa na uhakika na uwezo wa mapafu ya Lisa na uzoefu wake. Ikiwa mambo yangeenda ndivyosivyo, Lisa angejidhalilihsa kabisa.
"Sina uhakika." Alikaza midomo baada ya kusema hivyo. "Ni suala lake mwenyewe."
“Mwache ajiaibishe ikiwa anataka,” Rodney alisema kwa kejeli, “Nafikiri anajaribu tu kujionyesha baada ya kusifiwasifiwa na wengine kwa siku chache. Anadhani yeye ni mzuri kwa kila kitu.”
'”Namhurumia kweli. Anafikiri kwamba anaweza kumshinda Cindy? Cindy ndiye diva wa Afro-pop."
"Usijali. Mwache afanye kama anataka. Yeye ndiye mrithi wa Ngosha

Corporation, kwa hivyo umwacheni avurunde ili tupate sababu ya kumnanga hapo baadaye. Tutamsema hadi atamani kufa.”
Mbele ya maongezi ya umati, Lisa alitabasamu kwa unyonge na kukandamiza key ya piano, na kufanya jumba la karamu litulie.
Alirekebisha kipaza sauti na kusema kwa sauti ya kupendeza, “Huu ni wimbo mpya niliotunga. Leo itakuwa mara yangu ya kwanza kuucheza na kuumba, hivyo natumai kila mmoja atausikiliza.”
“Ana kichaa? Hata alitunga wimbo wake mwenyewe.”
"Labda anamuonea wivu Cindy na anataka kumshinda, lakini Cindy ni mwimbaji haswa."

"Siku hizi, kila mwanamke kijana kutoka kwa familia tajiri anataka kutengeneza nyimbo yake. Muziki umevamiwa kwa kweli.”
Kila mtu aliponong'ona masikioni mwa mwenzake, mlio wa muziki wa furaha ukiambatana na sauti ya key za piano ulisikika polepole.
"Nakuambia, 'simama hapo',
“Ndege inaruka juu ya anga ya buluu, "Ninakwenda safari,
"Ninakwenda safari ya mbali. "Machozi yananidondoka kifuani mwangu,
"Mahusiano haya hayataisha, "Tunafuatilia ndoto zetu za siku zijazo pamoja,
"Huu sio mwisho, ni mwanzo mpya."
Umati ulitulia taratibu na kusikiliza kwa

makini wimbo huo mpya. Wimbo huo wa furaha ulikuwa na kidokezo cha huzuni ambacho kilirejelea kuagana. Mara moja uliwakumbusha watu miaka yao ya chuo kikuu ambapo walilazimika kuwaaga wapendwa wao ili waweze kufuata ndoto zao wenyewe. Ilikuwa huzuni kidogo iliyochochea mioyo yao.
Alvin alimtazama yule mwanamke aliyekuwa anang'aa pale jukwaani huku akiwa haamini. Kichwa chake kilikuwa kimeinama chini, lakini mwili wake ulitoa mwanga ambao hakuna mtu angeweza kuuzuia.
Siku zote alikuwa hivi, akimshangaza mara kwa mara. Haishangazi alikuwa amepanda jukwaani akiwa na ujasiri kama huo. Ustadi wake wa piano na sauti vilikuwa bora zaidi kuliko za Cindy. Sarah aliyaona macho ya Alvin ya

kutamanika na nusura aingiwe na wazimu. Alifikiri kwamba Lisa angejifanya mjinga. Hii ilitokeaje? Miaka mitatu iliyopita, alikuwa amemponda Lisa kwa urahisi kama mchwa.
Miaka mitatu baadaye, wanaume wote nchini walikuwa wakimwona Lisa kwa sura mpya.
Cindy aliyekuwa amesimama pembeni ya Lisa alifedheheka sana hadi uso ukabadilika na kuwa mweupe. Hakuna aliyemjua Lisa kuliko yeye kwenye muziki. Ndio, hii ndiyo aina ambayo Lisa alikuwa amefanya vyema. Baadaye, wimbo uliisha kwa noti ya mwisho.
"Ajabu!" Msanii Nandy akiwa ameambatana na mumewe, alitangulia kupiga makofi. Wimbo huo uliimbwa vizuri, ulichezwa vyema, na hata kupangwa vizuri.

"Bi Jones, ni kweli ulitunga wimbo huu?" Bwana Lojas kutoka Times Media aliuliza kwa mshangao.
"Niliandika muziki na maneno mwenyewe." Lisa alisimama na kumuinamia Nandy. "Bi. Mfinanga, hongera, nimesikia mengi kuhusu wewe.”
”Nandy alijawa na sifa tele kwake. "Inasikitisha kwamba kipaji chako hakisikiki tena, Bi Jones. Tunaweza kurekodi nyimbo moja pamoja? Najuana na watu wengi katika tasnia ya muziki na wanaweza—”
“Asante kwa wema wako, Bi. Mfinanga, lakini muziki sio ndoto yangu. Ni hobby yangu tu,” Lisa alikataa kwa upole. "Kwa kawaida huwa na mambo mengi na nina

shughuli nyingi sana."
Bwana Lojas alicheka. "Bi. Nandy, hujui hili, lakini Miss Jones pia ni mbunifu maarufu wa majengo.”
“Hiyo ni ajabu." Nandy alifichua sura ya kupendeza.
Wakati huo, Joan ghafla alisema, “Bi Jones, ulinakili wimbo wa Cindy? Wimbo wako unafanana sana na 'Pepo Ya Ndoto’, wimbo maarufu wa Cindy."
Kila mtu alishtuka, na mtu mwingine akaongezea, "Ni kweli hata mimi nimekumbuka..."
“Bi Jones, haiwezekani kuwa umeiba, sivyo?” Jerome alidhihaki kwa nia mbaya.

Sura ya: 358
Mara tu kauli hiyo ilipotolewa, macho ya kila mtu yakatua kwa Lisa.
Cindy alionyesha uvumilivu na usemi wa ukarimu, akisema, "Kwa kweli, sio kweli. Ukisikiliza kwa makini, wimbo aliotunga Lisa una mahadhi mepesi kuliko wimbo wangu, 'Pepo Ya Ndoto'. Ina mtindo tofauti pia."
Lisa alimtazama Cindy. Kila mtu aliweza kusikia maana iliyojificha katika maneno ya Cindy. Ilikuwa ni kukiri kwa njia isiyo ya moja kwa moja kwamba Lisa alikuwa amenakili Cindy, lakini ni mtindo wa wimbo tu ndio ulikuwa tofauti. Kwa maneno aliyosema, alijionyesha kuwa mkarimu sana huku akimponda

chinichini.
Kwa hakika, wakati uliofuata, Joan alisema, “Bi Tambwe, unaweza kuwa mkarimu, lakini hupaswi kuendekeza wizi. Ukibadilisha na kupanga upya nyimbo chache za kigeni na kusema kuwa umeunda wimbo huo mwenyewe, si itakuwa dhuluma kwa waundaji asilia?”
Melanie naye alionyesha sura ya aibu. "Lisa, ingawa sisi sote ni washiriki wa familia ya Ngosha, huwezi kukosa akili." Kabla Sarah hajazungumza, tayari kila mtu alikuwa akimlenga Lisa. Moyo wake ulikuwa na furaha sana aliponong'ona masikioni mwa Alvin, "Alvin, ni kweli aliiba?"
Uso mzuri wa Alvin ulikuwa umepoa sana. Hakuna aliyeweza kukisia

alichokuwa akifikiria.
Rodney hakuweza kujizuia na kusema, “Haijaibiwa kabisa, lakini inafanana kwa angalau 60%. Ni kama nilivyosema. Hawezi kutunga. Mwishowe, bado alinakili kutoka kwa Cindy. Sijui ni nani aliyempa jeuri ya kupanda jukwaani na kujaribu kumwaibisha Cindy. Anamchukulia kila mtu hapa kama mjinga?"
Sara alifurahi aliposikia maoni hayo. Ingawa sura yake ilikuwa ya wasiwasi, moyo wake ulikuwa na furaha.
Mbele ya shutuma zote, Lisa alitabasamu na kucheza kwa starehe wimbo mwingine ambao hakuna mtu aliyewahi kuusikia hapo awali. Wimbo huu ulikuwa wa kutuliza zaidi. Lakini, sauti yake kama ya mbinguni ilisikika

kwa mtindo wa kitamaduni.
Wimbo ulipoisha, alicheza wimbo mwingine. Nyimbo hizi zilikuwa na mitindo tofauti na hakuna mtu aliyewahi kuzisikia hapo awali. Baada ya kucheza na kuimba nyimbo hizo, umati ulibadilisha tena mawazo yao na kuanza kumwangalia Lisa kwa jicho la kitofauti.
.
Cindy alihisi wasiwasi moyoni mwake ukizidi kuwa na nguvu.
Joan alifoka, “Kila mtu anazungumza kuhusu wizi wako. Mbona unacheza nyimbo tena? Haijalishi unacheza vizuri kiasi gani, haiwezi kuficha ukweli kwamba umeiba.”
Lisa alimpuuza na badala yake akamtazama Nandy. “Una maoni gani kuhusu nyimbo mbili za mwisho? Je,

zinafanana na nyimbo zozote huko nje?”
Nandy akatikisa kichwa. "Ni si msanii tu, bali mfuatiliaji mzuri wa muziki pia. Nyimbo hizi sijawahi kuzisikia popote. Ni nyimbo mpya kabisa."
“Bw. Campos, unaonaje?” Lisa aliwatazama wale watu waliozungumza kwa ukali zaidi hapo awali.
Jerome alisema kwa upole, “Tulikuwa tunazungumza kuhusu wimbo wako wa kwanza. Ingawa nyimbo zinazofuata hazijafahamika, ni nani anayeweza kuwa na uhakika kwamba hujanakili nyimbo za kigeni?”
“Ndiyo maana nilimuuliza Nandy kwanza. Unafikiri yeye asingeweza kuthibitisha hili kwa hadhi yake?” Lisa alirudi kwa utulivu.

Hadhi ya Nandy katika tasnia ya muziki iliheshimiwa. Haijalishi nafasi ya Jerome katika ulimwengu wa biashara ilikuwa ya juu kiasi gani, hakuthubutu kumkanusha waziwazi Bi. Nandy. Jerome akanyamaza kimya.
Lisa alisimama taratibu na kuyahamishia macho yake mazuri kwa Cindy. Alitabasamu ghafla, akauliza, "Unaonaje, Cindy?"
Cindy alishangazwa sana na swali la Lisa. “Unacheza vizuri sana. Endelea na kazi nzuri.”
Lisa akaachia mkoromo wa kicheko na kufinya macho huku akitabasamu. “Hata sasa hutaki kueleza kwanini wimbo wa kwanza ulifanana na wimbo wako, ‘Pepo Ya Ndoto’? Ni kwa sababu

nyimbo zote katika albamu ya 'Pepo Ya Ndoto', iwe mashairi au mahadhi yake, zote ziliandikwa na mimi."
Kwa tamko hilo, watu wote waliingia katika ghasia. Umati wa watu ulitupa macho yao kwa Chester bila kujua. Kila mtu alijua kwamba Cindy alikuwa mpenzi wa Chester. Alikuwa akimlinda kwenye duara miaka yote hii, akimdekeza kama yai kwenye kiganja cha mikono yake. Kwa Lisa kumwiaibisha Cindy sasa, hiyo ilikuwa ni sawa na kumpiga Chester usoni. Chester aliwasha sigara na kukunja uso sana.
Cindy alichanganyikiwa. "Unasema nini?"
Rodney alifoka mara moja, “Lisa Jones, nadhani umepandisha wazimu kweli! Nyimbo hizo ziliandikwa na Cindy, sio

wewe! Unawezaje kukosa aibu?"
“Ndio, unajua Cindy ana kipaji gani? Kwanini akuhitaji kumwandikia nyimbo?” Joan naye alipiga kelele.
Lisa alipuuza shutuma hizo na kusema, “Wimbo wa kwanza katika albamu ya 'Pepo Ya Ndoto', uliitwa 'Watatu Pamoja'. Ulihusu urafiki wangu na Cindy, na mtu mwingine wa tatu. Tulikuwa marafiki wazuri wakati huo. Mwaka huo, ndoto ya Cindy ilikuwa kuwa mwimbaji, kwa hiyo nilitoa nyimbo zangu nane bora nilizotunga mimi mwenyewe na kumpa Cindy bila mkataba. Kwanini nilicheza nyimbo mbili za mwisho mapema? Nyimbo hizo mbili ndizo nyimbo zangu za hivi punde zaidi. Nilitaka tu kuonyesha kila mtu uwezo wangu. Sikuwa na nia ya kumchafua Cindy hata kidogo.”

Uso wa Cindy ulikuwa umepauka, na alionekana kama anakaribia kulia. "Lisa, ni kwa sababu unataka kuwa mwimbaji? Ni sawa, ninaweza kukutambulisha kwa wanamuziki, lakini hutakiwi kukanyaga sifa yangu.”
Lisa alitabasamu na hata hakumtazama. “Hamkutakiwa kuwa na haraka ya kunishtaki. Kwa bahati nzuri, kitabu changu cha nyimbo bado kipo. Baadaye, nitapiga picha zake na kuziweka kwenye mtandao. Hata hivyo, kuna zaidi ya nyimbo nane katika kitabu changu cha nyimbo. Kuna nyimbo 18. Wale wanaojua muziki wanaweza kufurahia polepole. Unaweza pia kuja kwangu kununua hakimiliki ya nyimbo zangu zingine, lakini sitazitoa bure wakati huu, kwani...” Baada ya kunyamaza, alimkazia macho Cindy.

“...baadhi ya watu hawashukuru kwa vitu ambavyo wamepewa kwa nia njema. Kuna watu wengi wasio na shukrani duniani.”
Cindy karibu kuanguka. Alijua kabisa mtunzi wa nyimbo hizo ni nani.
Hata hivyo, hakuwahi kujali kuhusu hilo. Ilikuwa ni kwa sababu, wakati huo, Lisa hakuwa tishio kwake. Ilikuwa tu kitabu cha nyimbo, kwa hiyo kila mtu angefikiri kwamba Lisa alikuwa akimwonea wivu. Hata hivyo, kwa msimamo wa Lisa kulikuwa na haja ya kumuonea wivu Cindy? Lisa alikuwa binti wa kifalme wa familia ya Ngosha, familia iliyomiliki ardhi nyingi zaidi nchini Kenya. Sambamba na utukufu wake kama mbunifu mashuhuri wa kimataifa, bila shaka wengine wangeamini maneno yake zaidi.

Lisa alimaliza kuongea na kuinama. "Nilicheza tu piano kwa leo ili kufanya karamu iwe ya kupendeza zaidi kwa Times Media, lakini sikutarajia kusababisha usumbufu mwingi. Samahani zangu za dhati, Bwana Lojas.”
“Ni sawa, Miss. Jones. Ulicheza vizuri sana, haswa nyimbo mbili za mwisho. Mabosi wengi kutoka kwenye kampuni za muziki wapo usiku wa leo, kwa hivyo ninaamini kwamba wapo watakaojitokeza ili kununua hakimiliki ya nyimbo hizo hivi karibuni.” Lojas alikuwa mwerevu na alikuwa ameona mambo mengi ya aina hii kwenye tasnia hapo awali.
Hapo awali alimthamini Cindy, lakini alibadilishwa kabisa na maneno ya Lisa.Hata hivyo, bado alipaswa

kuzingatia sifa ya Chester. Alisema huku akitabasamu, “Kila mtu ajisevie chakula. Utapata nguvu ya kusikiliza hotuba yangu jukwaani ikiwa utakula vya kutosha.” Umati ulitawanyika taratibu.
Kulikuwa na watu wengi ambao walikuwa bado wanajadili kile kilichotokea.
“Oh, Bwana Cedo Kadenyi, wewe ni mtayarishaji wa muziki. Nini unadhani; unafikiria nini?"
"Kile Lisa Jones alisema kina uwezekano mkubwa kuwa kweli. Angalia tu nyimbo zake mbili. Ni nzuri sana. Akiachia moja anaweza ku pata tuzo ya muziki kwa urahisi."
Sura ya: 359

Chester akakaa kwenye sofa lililopo mkabala na Lisa. Kulikuwa na tabasamu angavu usoni mwake, lakini macho yake yalitoa mchomo mkali wa hasira. “Nipe kitabu asilia cha nyimbo.”
"Inaonekana Cindy alikuja kulalamika kwako." Lisa alitabasamu kwa utulivu. "Ni nini kizuri unakipata kwa mwanamke mnafiki kama huyo?"
"Ana mapungufu mengi, lakini bado ni mwanamke wangu," Chester alisema, "Lisa Jones, usiende kinyume nami. Familia yako ya Ngosha haiwezi kumudu matokeo ya kumkasirisha tajiri namba tatu wa nchi hii. Hujatosheka tu kwa kusharirisha nyuso za watu wengine usiku huu?”

Lisa alitabasamu kwa dhihaka. "Chester Choka, kama kijana tajiri namba tatu wa nchi, macho yako ni mabaya sana. Unapaswa kubadilisha miwani yako."
Macho ya Chester yaliangaza kwa ukali. "Uvumilivu wangu una mipaka yake, Lisa."
“Suala kati yangu na Cindy linaweza kuchukuliwa kuwa chuki ya zamani. Sikutaka kueleza yaliyopita, lakini... ni kosa lako kwa kuwa mkali sana, Dokta Choka.” Lisa alitabasamu kwa ujeuri. "Kwa neno moja tu, ulimfukuza baba yangu katika hospitali yako."
Chester aliganda na kukunja uso. "Sikujua kuhusu hilo."
“Hata ungejua, ungemruhusu Alvin

afanye hivyo. Inaeleweka kwamba nyinyi watatu ni ndege wa manyoya yanayofanana.” Lisa alisimama, macho yake mazuri yakionekana kuwaka kwa hasira. “Unataka nikupe kitabu cha nyimbo asilia? Dokta Choka, lazima uwe unaota. Unafikiri mimi ni mmoja wa wafanyakazi wako? Hakika, ikiwa unataka kuiondoa familia ya Ngosha, endelea. Sitajali hata kidogo. Sio kama sina pesa hata hivyo. Hata hivyo, ngoja nikukumbushe. Usiende kutafuta mchawi na kurudi nyumbani ukiwa umerogwa. Mtazame Alvin sasa.”
Chester, ambaye hakuwahi kamwe kushindwa waziwazi hapo awali, alikasirika sana hivi kwamba akavuta sigara mfululizo.
“Chester Choka, miaka mitatu iliyopita, nilishukuru sana kwamba ulipata daktari

wa kumuokoa baba yangu, lakini baada ya kugundua kuwa Charity aliruka baharini na kufa, nilipoteza kila sehemu ya shukrani niliyokuwa nayo kwa ajili yako. Ulimchukia mwanamke asiye na hatia na bado unamchukulia mwanamke kama Cindy kama hazina. Lazima kuna shimo kwenye ubongo wako." Baada ya Lisa kumaliza kuongea, alitoka bila kugeuka nyuma.
Nyuma yake, Chester alipiga mkono wake kwa hasira na glasi ya mvinyo ikaanguka chini. Uso wake ulikuwa umekakamaa kwa hasira.
Rodney akapigwa na butwaa. Kati ya hao watatu, ni Chester pekee ndiye angetabasamu na kuficha machungu yake moyoni mwake. Kwa kawaida hakuwahi kuonyesha kama alikuwa na furaha au hasira. "Hapana, Lisa alisema

nini kilichokukasirisha?" Rodney aliuliza swali lililoambulia ukimya tu.
Hata hivyo, Alvin alicheka na kutabasamu kidogo. “Angalau sasa unajua kwanini mimi hukasirishwa sana na huyo mwanamke.”
"Chester, usiwe na wazimu." Rodney alimfariji. "Kwa neno moja tu, sio shida kwako kuangusha familia ya Ngosha na Mawenzi Investments."
“Unadhani familia ya Ngosha ni kuku kwenye soko la mbogamboga? Hawawezi kuuawa kwa neno moja tu.” Chester alimtazama kwa ukali. “Si rahisi kihivyo. Lisa Jones wa sasa hana doa dhaifu.”
Alvin alipigwa na butwaa, Rodney akasema, “Hilo haliwezekani. Mtu anawezaje kutokuwa na doa dhaifu?"

"Labda mtu hatakuwa tena na maeneo dhaifu baada ya kupoteza kila kitu," Chester alisema kwa kufikiria.
Alvin alikunja uso. Moyo wake ghafla ukahisi kukosa raha. Aligeuka nyuma kwa umati wa watu na kumtafuta Lisa bila kujua, lakini alimuona tu akiondoka pamoja na bwana mdogo wa familia ya Malugu.
Kupitia madirisha ya sakafu hadi dari, aliweza kuwaona watu hao wawili wakizungumza na kucheka huku wakitoka pamoja. Alikaribia kuisaga kwa mikono glasi ya mvinyo mikononi mwake.
Dakika tano baadaye, hakuweza kukaa tena. Alimwambia Rodney amrudishe Sarah baada ya karamu na akatoa

udhuru wa kuondoka mapema. Alilifuata gari la Bwana Malugu mpaka waliposimama kwenye sehemu ya kuegesha magari mbele ya majumba ya Karen Estate. Hata hivyo, baada ya kusubiri kwa nusu saa, bado hakumuona Lisa akishuka kwenye gari.
Taa za gari zilikuwa zimewaka, lakini hakujua walikuwa wanafanya nini. Walikuwa na mazungumzo gani kwa muda mrefu hivyo? Inaweza kuwa...
Alvin alipofikiria kuwa Lisa na Erick Malugu wanaweza kuwa wanafanya jambo lile lile lililotokea kati yao siku kadhaa zilizopita kwenye gari, moyo wake ulianza kumuuma papo hapo. Alishindwa kuvumilia akatoa simu yake ili apige.
Hazikupita hata dakika kumi, polisi

mmoja aliendesha gari na kugonga kioo cha gari la Bwana Malugu.
“Kuna jambo?” Erick alishusha dirisha.
Ofisa huyo aliwatazama mwanamume na mwanamke waliokuwa ndani ya gari, akisema kwa mshangao, “Mtu fulani aliripoti kwamba mnafanya biashara isiyofaa kwenye gari.”
Ni aina gani ya biashara zisizofaa ambazo mwanamume na mwanamke pekee wanaweza kufanya ndani ya gari? Maneno ya Erick na Lisa yakawa mazito kutoka vinywani mwao.
Lisa aliuliza kwa mshangao. "Haya umeona kuna biashara gani inayoendelea hapa?"
"Samahani." Afisa huyo alimlaani mtu

aliyewaripoti. Mtu huyo lazima awe mwendawazimu.
Afisa huyo alipoondoka na Erick akijiandaa kuendelea na mazungumzo, gari la maji lilipita ghafla likimwaga maji kwa fujo. Kwa vile dirisha lilikuwa limeachwa wazi, Erick, aliyekuwa ameketi upande huo, alilowa maji. Alikasirika sana hata uso wake ukawa mbaya ghafla.
Lisa alizuia kicheko chake na kusema.“Samahani, naona bora urudi nyumbani ukaoge,”
"Ndio, labda kuegesha gari langu hapa kumemkwaza mtu." Erick alitabasamu kwa jazba. Alikuwa mtu mwerevu. Lisa alikuwa na wafuatiliaji wengi usiku huo, lakini ni yeye tu ndiye aliyepata nafasi ya kumpeleka nyumbani, kwa hivyo

lazima kulikuwa na wanaume wengi waliomwonea wivu.
“Hapana, lazima nimemkosea mtu. Huenda kuna mtu ambaye atakuja kunisababishia matatizo baadaye.” Lisa alimkabidhi kitambaa na kutoka kwenye gari kuelekea kwake.
Akiwa anakaribia kubonyeza lifti, ghafla mkono mkubwa uliibuka kutoka nyuma na kuzuia kitufe cha lifti. Kisha, harufu ya kupendeza ya mtu aliyemzoea ilimfunika kutoka nyuma.
Lisa hakutazama juu na akasema kwa kawaida, "Baada ya shida uliyotuletea, bado haujatosheka tu?"
“Nimewaletea shida gani?” Kicheko cha kejeli cha mtu huyo kilisikika juu yake. Ilionekana kana kwamba hakukubaliana

kabisa.
Lisa akageuka na kuinamisha kichwa chake. "Uliripoti polisi kwamba nilikuwa na 'biashara zisizofaa' kwenye gari na ukatuma mtu wa kummwagia maji Bwana Malugu. Usiseme kuwa si wewe.”
"Kwanini nifanye mambo ya kipumbavu hivyo?" Alvin alijifanya kama amesikia mzaha na kuvaa tabasamu la kejeli. Asingekubali kufanya jambo kama hilo hata kama angepigwa hadi kufa. Ingekuwa ni kujifedhehesha sana.
"Lazima kuna mtu aliwaona mmekaa kwenye gari muda mrefu na akaripoti kwa polisi kwa nia njema." Macho ya Alvin yalipita kwenye sehemu kubwa ya kifua chake iliyo wazi. “Jiangalie. Umevaa hivi na unakaa kwenye gari na

kijana mhuni kama Erick Malugu. Huogopi kwamba watu watakuita hujiheshimu?”
"Kwa hiyo ikiwa mimi sijiheshimu? Tayari tumeachana, kwa hivyo hayakuhusu, ndiyo maana ninakuita mmbea." Lisa aliunyosha mkono wake na kubonyeza kitufe cha lifti.
Alvin aliutazama mgongo wake mzuri na kuhisi moyo wake ukimuuma kwa chuki. “Unafikiri Bwana Malugu atafanya nini akijua kwamba tulilala kwenye gari langu siku chache zilizopita?”
“Labda atanionea huruma zaidi. Baada ya yote, wewe ndiye unakaribia kutulia na kuanzisha familia.” Uso wa Lisa ulikuwa umejaa dhihaka. “Alvin Kimaro, huoni kuwa wewe ni msumbufu? Tayari tumeachana, na ni wewe

uliyenilazimisha kusaini talaka. Sarah na wewe mnafanya taratibu za kupandikiza mimba, lakini bado unaendelea kunifuatilia. Usiniambie kwamba huwezi kuniacha niende, au labda...Unamtaka Sarah, lakini unanitaka na mimi pia.” Alimsogelea ghafla. Sauti yake ya kuroga ilikuwa kama sumaku.
Alvin alimsukumia mbali kwa nguvu na kumdhihaki, lakini umahiri wake wa kucheza piano na uimbaji wake wa ajabu usiku huo uliangaza akilini mwake ghafla—pamoja na kumwona akicheza na wanaume wengine na kumwona akiongea na kucheka na wanaume wengine...Ghafla aligundua kuwa alikuwa ametumia zaidi ya usiku huo kumwangalia.
Walikuwa wametia saini karatasi za talaka. Lisa alikuwa huru kabisa.

Angeweza kuwa na yeyote anayetaka kuwa naye. Hata hivyo, wakati Bwana Malugu na yeye walipokuwa ndani ya gari kwa muda wa nusu saa tu, alitaka kukwaruza moyo na mapafu yake na kuyatoa nje! Alijua kuwa hakutakiwa kuendelea kuwa hivyo. Ingemuumiza Sarah, na haikuwa haki kwake pia. Hata hivyo, Alvin hakuweza kujizuia.
Sura ya: 360
"Kwani kuna ubaya kuwa na nyie wote?" Alimshika Lisa mabegani na kumkandamiza ukutani, macho yake yakiwa yanawaka moto. “Lisa, lazima nikubali kwamba wewe ni mwanamke wa kuvutia sana. Ni mimi ambaye sikukufahamu vya kutosha hapo awali.”
Kisha, akalazimisha kumbusu Lisa

mdomoni, lakini, Lisa aligeuza kichwa chake na kukwepa. Midomo yake iliangukia kwenye shavu lake na harufu nzuri ya mwili wake ikamshika na kumfanya ashindwe kujiondoa.
“Alvin Kimaro, unakumbuka jinsi ulivyowaagiza kwa hasira walinzi wako kunikandamiza chini na kunilazimisha kutoa cheti cha ndoa wiki iliyopita? Unakumbuka jinsi ulivyonilazimisha kusaini karatasi za talaka? Bado unakumbuka jinsi ulivyokuwa jeuri wakati huo?"
Lisa alisema kwa upole huku akionyesha huzuni. “Kweli uliponibeba siku ile kutoka kwenye gari sikuwa nimelala. Nilihisi tu kama ni ndoto na sikuthubutu kuamka. Baada ya wewe kuondoka, nilifikiri juu ya mambo mengi na kuhisi kuwa labda bado kulikuwa na

nafasi kwa ajili yetu. Lakini siku iliyofuata, ulikuja kwangu kutoa talaka. Hukuniachia hata chembe ya heshima. Wewe...” Karibu na mwisho, sauti yake iligoma, lakini bado alijifanya kuwa na nguvu.
Mwili wa Alvin ulikuwa mgumu. Mwili wake ulionekana kuwa na kikomo, na kumfanya ashindwe kujisogeza.
Lisa alimsukumia mbali. "Baada ya hapo, nilikuona na Sarah ulipokwenda kufanya upandikizaji wa mimba hospitalini. Kwa vile umeamua kuwa naye, kwanini huwa unarudi kuniumiza? Kati yangu na Sarah, mimi ndiye jalala la hasira zako na tamaa zako za ngono. Ulisema unanitaka, lakini kati yetu sisi watatu, ni lazima nikubali tena na tena kwamba ni mimi pekee ndiye ninayeumia zaidi. Hakuna anayeweza

kujifanya kana kwamba hana wivu, sivyo? Lakini nikimuumiza Sarah, unanipiga na kunikaripia tena.”
Lisa alijiinamia na kulia ghafla bila kujizuia. Alvin alimtazama na ghafla akahisi uchungu ukimjaa kifuani. Kwa kweli, alijua pia kwamba alikuwa akimtendea kinyume na haki. Hata hivyo, alikuwa alishikilia sana msimamo wake na kudharau ushawishi wa mwanamke huyo kwake.
"Simama." Alvin alinyoosha mkono kumshika, lakini, Lisa alimsukumia mbali kana kwamba alikuwa na wazimu. “Ondoka. Sitaki kukuona. Niache na maisha yngu, sawa? Sitaki kujihusisha na wewe na mkeo tena.” Aliangua kilio cha uchungu tena na tena.
Mwili wa Alvin ulijhisi kuganda. “Sawa,

nitaenda.”
Aligeuka taratibu na kutoka nje ya mtaa huo hatua moja baada ya nyingine. Hapo awali, alikuwa akifikiri kwamba anachukizwa na Lisa. Hakuwahi kufikiria kwamba hata siku moja angeweza kuguswa naye.
Wakati mwingine, alimchukia sana hadi akakosa raha kabisa, lakini kwa sababu fulani, kamba za moyo wake zilipigwa kwa namna fulani. Ilikuwa ni huruma kwamba alikuwa amechelewa kukutana naye.
Alvin alikaa kwenye gari na kuwasha simu yake. Kwenye skrini kulikuwa na picha ya Lisa ambayo alikuwa ameihifadhi kutoka kwenye mtandao siku chache zilizopita. Aliificha mahali fulani kimya kimya.
Usiku kucha, Alvin alikaa kwenye

maegesho ya magari ya Karen Estate na kuvuta sigara. Hakujua kuwa wakati huo tasnia ya burudani ilikuwa imetikisika.
Saa saba usiku, menejimenti ya Cindy ilifanya mkutano wa dharura na hatimaye wakatoa tangazo rasmi kwa umma. [Bila kujua, imepita miaka mitano tangu niingie kwenye tasnia ya burudani. Mwaka huo, 'Pepo ya Ndoto' ilinifanya kuwa maarufu kote Afrika Mashariki. Kwa kweli, kwa miaka mingi, nimekuwa nikimshukuru kimya kimya mtu mmoja moyoni mwangu na huyo ni rafiki yangu mzuri, Lisa Jones. Yeye ndiye aliyeniandikia album nzima ya 'Pepo ya Ndoto'. Ninashukuru sana kukutana na rafiki kama yeye katika maisha yangu. Alikuwa akijiweka kimya na hakutaka kujionyesha, lakini kwa kuwa sasa anajulikana kwa umma,

sitaki kuficha kipaji chake tena. Ninataka kumpa zawadi ambayo nilitunukiwa wakati huo. Hii ni tuzo yake. Lisa, nakupenda.]
Baadaye, Cindy alichapisha tuzo kadhaa na picha aliyokuwa amepiga akiwa na Lisa shuleni. Katika picha, wawili hao walikuwa wakitabasamu sana na wakionekana kuwa na urafiki wa ajabu.
Wanamtandao walilipuka.
[Kwa hiyo Lisa na Cindy walikuwa marafiki wakubwa. Tizama toka wakiwa shuleni walikuwa warembo kweli!]
[Si hivyo tu. Aliandika hata nyimbo za Cindy. Ni zaidi ya urafiki!]
[Hakuna mtu atakayezungumza kuhusu

kipaji cha muziki cha Lisa? Hivi, kuna jambo lolote ambalo hawezi kufanya? Kwa kweli, Lisa shikamoo!]
[Cindy ni mkarimu sana. Amemkumbuka rafiki yake wa karibu na kuelezea alivyomsaidia?]
Lisa alipoamka asubuhi na kuona maoni ya wanamtandao, alitabasamu.
Kama alivyotarajia, Cindy angefanya kitu haraka ili kulinda hadhi yake ndogo iliyokuwa imebaki isije ikapotea yote. Alitoa simu yake bila haraka na kumpigia Sam. "Sam, umemaliza nilichokuomba ufanye?"
“Bila shaka. Unadhani mimi ni nani? Ninatawala Dar Es Salaam. Ni kazi ndogo sana kupata kitu chochote kutoka kwa Janet Kileo. Kwa jinsi familia ya Kileo ilivyo dhaifu sasa, Janet

ananitazama kama anamtazama babu yake—”
“Unaweza kunitumia sasa hivi?” Lisa alikatiza majigambo yake.
“Hakika. Una akili sana. Huenda Cindy alisahau kwamba aliacha mambo mengi mabaya alipokuwa akijaribu kuwalambalamba Lina na Janet huku Dar Es Salaam.” Sam alimtumia rekodi.
Lisa mara moja aliipachika chini ya chapisho la Cindy kwenye Facebook.
[Asante kwa kufunua ukweli, Cindy Tambwe, lakini nilikuwa mdogo
na mjinga nilipokuwa pamoja nanyi zamani. Sikujua jinsi ya kuwasoma watu wakati huo. Baada ya mambo mengi kutokea, sithubutu kukuchukulia kama rafiki tena.]

Wanamtandao walipakua na kusikiliza rekodi ambayo Lisa alichapisha kwa udadisi.
Kwenye rekodi hiyo ya simu, sauti ya Janet ilisikika ikisema, “Huogopi kwamba Lisa atagundua unakula chakula cha jioni na mimi? Sisi ni maadui wakubwa."
Sauti ya Cindy kisha ikajibu, “Kwa hiyo ikiwa atagundua? Kwa hali yake ya sasa, hatoki katika ulimwengu sawa na mimi.”
Janet akajibu, “Hiyo ni kweli. Nilisikia kutoka kwa Lina kwamba familia ya Jones ilimfukuza na hana hata mahali pa kukaa sasa. Alikuomba msaada?"
"Alinipigia simu, lakini sikuipokea."

"Haha, vizuri. Hivyo ndivyo inavyopaswa kuwa. Akikuomba kumkopesha pesa, usifanye hivyo.”
“Bila shaka, sitafanya hivyo. Lakini Pamela huyo mjinga hakika atafanya hivyo.”
Rekodi iliisha ghafla. Hata hivyo, ilitosha kwa wanamtandao kujua rangi halisi za Cindy.
[Hiyo ni sauti ya Cindy kweli?]
[Ni hakika. Ni sawa kabisa na uimbaji wake wa kawaida na sauti yake kwenye vipindi vya Runinga.]
[Kwa hivyo rekodi ilikuwa baada ya Cindy kuwa maarufu. Alimdharau Lisa na kukataa kupokea simu za Lisa au kumkopesha pesa wakati alihitaji

msaada zaidi? Ooh! My God, hata yeye ni binadamu? Alichapisha post yake na kusema kwamba Lisa na yeye walikuwa kama dada usiku wa manane. Huo ni unafiki mkubwa!]
[Bora na nyie watu mmegundua kuwa yeye ni mnafiki. Nimekuwa nikisema mara kadhaa hapo awali kwamba Cindy ana nyodo sana. Hana maana na anadharau watu, anajifanya kama yeye ni mungu wa kike.]
[Hata aliwaita wengine wajinga kwa kumkopesha Lisa pesa. Ana utu kweli? Ikiwa Lisa asingemwandikia nyimbo, angekuwa hapo alipo leo?]
TUKUTANE KURASA 361-365

ONYO: Ni marufuku kusambaza, kukopi wala kuuza kazi hii kwani endapo kama tutakubaini basi sheria itachukua mkondo
wake (By: Official Dully)
 
LISA KITABU CHA NANE (8) SIMULIZI........................LISA KURASA..................361 - 365
PRESENT: SIMULIZI ZA DULLY

Sura ya: 361
Jua la mchana la uvivu liliangaza kutoka dirishani na kuangukia kwenye sura nzuri ya Lisa.
Akainama kutazama simu yake na kutabasamu kwa upole. Hata sauti yake ilikuwa laini. “Kwa hiyo mtashukia Dar es Salaam?”
"Ndiyo mpenzi, nimepata ndege ya moja kwa moja." Pamela alijibu upande wa pili wa simu. “Unaweza kutusubiri Nairobi. Sitakaa sana Dar, ni siku moja au mbili tu.”
“Hapana. Nitaenda kuwapokelea Dar, ni siku nyingi hata hivyo sijaenda kwenye jiji la nyumbani.” Lisa alinyamaza na kuinua kichwa chake, akionekana kuwa

katika hali nzuri. “Msafiri salama, utawapa hai hao malaika wangu.”
•••
Ndege kutoka Marekani ilitua kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere International Airport, majira ya saa tatu usiku. Lisa alisubiri kwa zaidi ya dakika kumi kabla ya kumuona Pamela akitoka akiwa na wapenzi wake wawili.
Lucas alikuwa amevaa shati la rangi ya bluu la mtindo wa Kiingereza. Ingawa mwili wake ulikuwa mdogo, sura yake ndogo iliyopendeza kupita kiasi iliwafanya watu waliokuwa wakipita hapo kumtazama.
Kwa upande wa Suzie alikuwa amekaa juu ya sanduku alilokuwa akiburuta Pamela. Mabutu yake mawili ya nywele kichwani yaliyumbayumba kwa

kupendeza. Watoto hao wawili walipomwona Lisa, walifurahi sana. Suzie aliruka chini mara moja kutoka kwenye sanduku na kumkimbilia kwa furaha.
“Mama, mama...”Suzie akaruka mikononi mwake mara moja, na kumganda mama yake kama luba.
Moyo mdogo wa Lisa ulilainika na machozi yalikaribia kumtoka. Tangu wazaliwe, hakuwahi kutenganishwa na watoto hao wawili kwa muda mrefu.
“Mama.” Lucas alijizuia zaidi, lakini macho yake pia yakawa na machozi.
"Sweetie, njoo hapa." Lisa alinyoosha mikono yake na kuwakumbatia.
"Jamani, ni bora kuwa na watoto wangu

wa kuzaa mwenyewe. Yaani mlipomwona mama yenu tu mimi tena basi,” Pamela alitania, “Mimi nawanunulia peremende kila siku lakini mnanisahau mara tu mnapomwona mama yenu.”
Suzie aliukunja mabega yake. “Godmother, fanya haraka na wewe uzae watoto tupate kaka na dada mdogo.”
“Asante kwa baraka.” Pamela alipiga kelele.
Lisa alisimama na kutabasamu. “Pole kwa safari na karibu tena nyumbani. Nimewaandalia chakula kitamu sana cha jioni. Nisingekuwa na watoto tungeanzia bar”
Pamela akacheka. "Hakika, twende."

Pamela alipokuwa anataka kuondoka ghafla sauti ya mshangao ikasikika nyuma yao.
“Pamela, ni wewe?” Ingawa ilikuwa imepita miaka mitatu, bado aliikumbuka vyema sauti hiyo.
Pamela aligeuka na kuwaona Patrick na Linda wakitoka nje ya geti.
Baada ya kutengana kwa miaka mitatu, Patrick alionekana mtu mzima zaidi na alionekana mpole kuliko hapo awali.
Kwa upande wa Linda, hakuwa amebadilika sana. Alikuwa amevaa tisheti nyeupe na sketi iliyofika magotini. Mikono yake miwili ilikuwa imeuzunguka mkono wa Patrick kiundani. Ilikuwa wazi kwamba walikuwa wapenzi.
Hata hivyo, Patrick alionekana

kumsahau Linda aliyekuwa pembeni yake na kumtazama tu Pamela bila kupepesa macho. Jeans yake ya rangi ya blue mpauko ilifafanua vyema miguu yake minene iliyonyooka, na mwili wake wa juu ulifunikwa na fulana nyepesi ya kijivu. Shati la drafti lilikuwa limefungwa kwenye fundo kwenye kiuno chake, likifunua kiuno chake kidogo.
Ngozi yake ilizidi kung’aa kwa weupe wa asili na nywele zake zilikusanywa nyuma ya kisogo na kufungwa kufichua mashavu yake yenye dimpozi. Macho yake yalikuwa makubwa na yenye kung’aa, yalimfanya aonekane mtu wa makabila mchanganyiko. Miaka mitatu ilikuwa imeacha alama kwenye uso wake, lakini ilimfanya kuwa kijana zaidi na mrembo.
Patrick alionekana kusahau mpaka

kupumua. Kando yake, Linda alisema kwa mshangao, “Pamela, ni wewe kweli. Umerudi? Tulikuwa na wasiwasi sana juu yako wakati huo tulipoona picha na video zako chafu mtandaoni. Uko salama?"
Patrick aliganda. Ndio, sasa alikumbuka. Miaka mitatu iliyopita, kulikuwa na habari kwamba Pamela alijirahisisha kwa Thomas Njau. Kisha Thomas alimfanyia mambo ya kisodoma na kurekodi video ambayo aliisambaza mtandaoni kwa watu kuona. Japo video hiyo haikuwa na uthibitisho wa kutosha kwamba aliyekuwa akifanyiwa kitendo hicho ni Pamela, teknolojia ilifanya kazi yake na kuuaminisha umma kuwa mwanamke huyo alikuwa ni Pamela. Habari chafu mara nyingi husambaa haraka, ndiyo maana tukio hilo la Pamela lilienea kwa kasi.

Muda mfupi baadaye, kulikuwa na habari kwamba alienda ng’ambo ili kukwepa aibu iliyomkuta. Macho ya Patrick ghafla yalijawa na karaha na tamaa.
Pamela kiasili hakuonyesha mabadiliko yoyote machoni mwake, akacheka tu na kusema. “Linda, unanipaka chumvi kwenye vidonda vyangu mara tu unaponiona, kwani hakuna habari nzuri za kuongelea hadi ukumbushie tukio baya kama hilo? Bado wewe ni wa ajabu tu kama zamani."
Sura ya Linda ilibadilika kidogo huku akijifanya ameziba mdomo kujionyesha kuwa amejawa na hatia. "Samahani-"
“Usiombe msamaha,” Patrick alisema kwa upole, “Kwa kuwa ulithubutu

kufanya mambo kama hayo, kwanini unachukia yakiongelewa na wengine?”
Pamela aliinamisha kichwa chake. Huyu ndiye mwanaume ambaye hapo awali alikuwa akimpenda sana. Lakini, kwa sababu tu ya habari za uwongo, angeamini uwongo wa Thomas kuliko yeye.
Lisa hakuweza kujizuia. “Patrick Jackson, Pamela alikuwa nawe kwa muda mrefu lakini bado humfahamu vya kutosha?”
“Namfahamu vizuri sana.” Patrick alisema kwa dharau. “Nilipokuja kumtafuta mara ya kwanza huko Nairobi, alimbusu mwanaume mwingine hadharani tena mbele yangu. Ni wazi kwamba mtindo wake wa maisha umekuwa mchafu baada ya kufika

huko.”
"Patrick, usiseme hivyo." Linda akahema. "Pamela huenda alikuwa akijaribu kukukomoa wakati huo. Thomas Njau ni Mkurugenzi wa Kampuni kubwa tu, hata hivyo. Huenda alikuwa akijaribu kutafuta mtu aliye na hadhi ya juu ili akuonyeshe, lakini iliishia... kumrudisha nyuma. Hata hivyo, Pamela, nataka kukukumbusha. Wakati mwingine unapotafuta mwanamume, bado unapaswa kuzingatia tabia yake.”
Pamela alitumbua macho kwa kuchukia. “Uko sahihi. Sikuangalia tabia ya mtu wakati wa kupata mpenzi wangu wa kwanza. Wakati huo, nilisema kwamba rafiki yake wa utotoni ambaye aliendelea kumsumbua alivutiwa naye, lakini hakuniamini. Tazama sasa. Kwa

kweli waliishia kuwa wapenzi."
Uso wa Linda ulijawa na aibu, akamtazama Patrick ambaye naye alikosa cha kusema.
Pamela aliinama chini na kusema, “Nilimwambia mpenzi wangu huyo wa kwanza kuhusu hilo lakini alinilaumu na kusema hakuna kinachoendelea. Sasa nikifikiria juu yake, kwa kweli najilaumui sana. Nilipaswa kuondoka mapema. Badala yake, niliishia kuchelewesha uhusiano wa kimapenzi wa mtu fulani kwa miaka mingi sana. Mimi ni mjinga sana."
Rangi kwenye nyuso za Patrick na Linda zilibadilika mfululizo.
Linda aliuma mdomo wake na kusema kwa hatia, “Pamela, umeelewa vibaya. Amini usiamini, sikuwa na hisia zozote

na Patrick wakati huo, lakini baada ya wewe kuondoka, nilihisi kwamba alikuwa na huzuni sana. Baadaye, nilipokuwa nikimriwadha, sikuweza kujizuia kumpenda.”
“Huzuni?” Pamela alipigwa na butwaa.
“Ndiyo, nilikuwa na mfadhaiko sana.” Patrick alisema kwa sauti ya chuki. “Nilitapeliwa na mwanamke mnafiki kama wewe kwa miaka mingi sana,”
Pamela alishtuka sana hata ubongo wake ulikuwa umevurugika. "Pia nilikuwa kipofu kabisa kwa kupoteza miaka mingi ya maisha yangu na mtu wa kuchukiza kama wewe. Hapo zamani, nilifikirije kuwa wewe ni mpole na mwenye upendo? Nilikuwa kipofu kabisa.”

Pamela hakuweza kuwa na wasiwasi tena na akamshika mkono Lucas na kuondoka.
"Subiri, huyo ni mtoto wako?" Patrick akatazama kwa udadisi.
Pamela alitaka kukiri kwamba alikuwa mtoto wake, lakini Lucas alizungumza kabla yake, “Yeye ni aunty yangu.”
Linda alisema, “Sijawahi kusikia habari za Forrest kufunga ndoa. Je, ni mwanae wa haramu?”
Sura ya: 362
“Oh jamani, mmesahau? Mtindo wangu wa maisha ni mbaya sana, hivyo ni kawaida kwangu kupata mtoto mmoja au wawili wa haramu,” Pamela alitabasamu na kucheka.

Lakini, uso wa Patrick ulibadilika sana. “Ni kweli ni mwanao wa haramu?”
“Mjinga wewe,” Lucas alimdhihaki, “zaa na wewe wa kwako umwite mtoto haramu, mimi siyo mtoto haramu!”
“Unasemaje wewe mtoto? Nitakufinyaaa!” Patrick alikasirishwa na maneno ya yule mtoto na kukaribia kumshika.
"Jaribu tu kumwekea mkono wako uone." Pamela alishika mkono wake.
Patrick ambaye alikuwa mrefu kuliko yeye alishangazwa na maumivu ya mkono wake. Akamkazia macho Pamela, lakini alimtazama tu kwa dhihaka. Alipatwa na mshtuko kidogo alipokumbuka kwamba alikuwa akimwangalia kila mara kwa

kumwabudu. Moyo wake ulimuuma ghafla.
“Patrick Jackson, natumai kwamba tutakapokutana tena wakati ujao, usithubutu hata kunisalimia. Watu husema kwamba mapenzi ya kwanza ni mazuri, lakini mimi nakuona unachukiza kama nzi.” Pamela aliuachia mkono wake na kuondoka na Lisa.
Walipotoka, Patrick aliendelea kumtazama nyuma. Alimchukia waziwazi, lakini miaka yote hii, hakuwahi kufanikiwa kumfuta moyoni mwake.
“Patrick, uko sawa?” Linda kwa haraka akaja na kumshika mkono huku akimtazama kwa karibu.
"Si chochote." Patrick alikuwa hayupo.

Linda alipomuona hivyo alichukia kwa siri.
Ndani ya gari. Lisa alicheka akisema, "Patrick bado anakupenda sana. Bado aliendelea kukutazama tulipoondoka."
"Kwa hiyo?" Pamela alichungulia dirishani. “Baada ya tukio la Thomas, kila mtu alinisuta na kunisema sana. Huyu mpenzi wangu wa zamani pia alinitumia ujumbe akisema sijiheshimu.”
“Usijali Pamela. Sisi sote tumeteseka kwa kitu kimoja. Sote wawili tulikumbana na wahuni kwenye mapenzi yetu, wewe Linda na mimi ni Sarah” Lisa alilalamika.
“Hakika. Sitarudia tena makosa." Pamela alijipa moyo. Alikataa kuwa na

bahati mbaya hivyo tena.
"Sawa, natumai utakuwa bora kuliko mimi," Lisa alisema kwa dhati.
“Godmother, usijali. Ukishindwa kupata mwanaume mzuri, nikikuwa mkubwa nitakulinda,” Lucas alisema kwa uvivu.
"Lucas wangu ni mtu mtamu sana." Lisa alimkumbatia na kumpiga busu, na kufanya masikio yake kuwa mekundu.
"Mama, mama, na mimi nataka pia." Suzie alimkumbatia na yeye pia akataka busu.
“Kwanza kabla ya yote shosti nimezikumbuka kweli chipsi vumbi za uswazi na nyama za kuku, tuanweza kuzipata wapi sasa hivi?” Pamela aliuliza ghafla.

“Muda wowote unapata, lakini nyumbani nimewandalia chakula cha jioni kitamu sana...” Lisa alimwambia.
“Sawa, tupite uswazi basi nichukue hata vimiguu vya kuku tu kupoza hamu hamu.” Pamela alisisitiza.
Lisa akawapeleka sehemu moja huko Msasani. Hapo palipatikana kila aina ya chakula cha uswahilini, haswa chpisi, mishikaki, nyama za kuku, mihogo na vingine kama hivyo.
Wale watoto wawili walifurahia sana chipsi na nyama za kuku. Walikula na kujilamba hadi matumbo yao yakakosa nafasi kabisa.
Suzie aliinua mdomo wake mdogo mwekundu na uliojaa mafuta, na mkononi akiwa ameshikilia vipapatio

vya kuku vilivyokaangwa, akisema, “Hatimaye ninaelewa kwa nini Godmother huzungumza kila mara kuhusu chakula cha nyumbani, kumbe ni kitamu hivi?”
“Ni kitamu eeh?” Lisa aliuliza akitabasamu kwa bintiye.
“Ni kitamu sana. Sitaki kurudi Marekani tena. Nataka kubaki hapa na kula chipsi na kuku kila siku.” Suzie alisema huku akilazimisha kubugia vipande vya chipsi vilivyojazwa tomato sauce.
“Sawa mwanangu.” Lisa alihisi maumivu ya moyo.
"Sitaki kurudi pia," Lucas alisema kwa uso uliotulia,mdomoni akiwa amerundika minofu ya kuku wa kukaangwa. "Nataka nikae na wewe

nikulinde."
Sauti za watotowale zilimfanya Lisa acheke, lakini akasema kwa uzito, “Hamtaweza kukaa huku mkiwa bado wadogo. Baba yenu akiwajua atawaiba na kuwapeleka mbali na mimi, au nyie mnapenda kwenda kukaa na mama mbaya wa kambo?”
"Ndio," Pamela aliyekuwa busy muda mrefu akifakamia nyama za kuku wa uswazi alisema ghafla, "Mama yenu anawapenda sana, lakini baba yenu ni mhuni, hana huruma kabisa."
Watoto hao wawili waliinamisha vichwa vyao, wote wawili wakiwa kimya kwa muda.
Baada ya kumaliza kula, Lisa aliwapeleka Masaki, mtaa wa Buzwagi

ambako alinunua lile jumba la kifahari la Alvin siku za mwisho kabla hajaondoka kwenda Nairobi. Jumba lilikuwa kubwa na tulivu na muda wote lilikuwa likitunzwa na Jumbe, kijana wa kazi ambaye muda wote aliliweka jumba hilo katika mazingira nadhifu.
Siku inayofuata, Lisa aliamka mapema na kuandaa kifungua kinywa cha kupendeza kwa wapenzi wake wadogo.
"Wapenzi, mama atapumzika pamoja nanyi leo. Baadaye nitawapeleka beach kwenye uwanja wa michezo, sawa?" Lisa alisema kwa upole.
“Sawa.” Suzie akawa na furaha.
"Mama nataka uninunulie mpira." Lucas alisema aliokuwa akichungulia dirishani kwenye bustani kubwa iliyokuwa nje.

"Unavyotaka mwanangu."
Muda huohuo, Pamela alitoka nje ya chumba cha wageni akiwa amevalia nguo za kupendeza. Alijipaka vipodozi vyepesi usoni, na nywele zake ndefu zilishuka mabegani mwake. Alikuwa amevalia viatu vya visigino virefu."
"Watoto wangu, ninaonekana mrembo?" Pamela akasogea kwenye meza ya chakula
Suzie alipiga makofi. “Wewe ni mrembo sana. Wewe ni mzuri kama yule mwanamke anayeimba kwenye tv."
“Ooh! Msichana wangu wewe ni mzuri sana. Nitakuzawadia chokoleti." Pamela alitupa kipande cha chokoleti juu.

Lisa alimtazama Pamela kwa jicho la kumsifia pia na kuchombeza. “Kama usingesema kuwa unaenda kuhudhuria kongamano linalofanywa na SE Group, ningefikiria kuwa unaingia kwenye shindano la urembo.”
"Unajua nini? Nimesubiri wakati huu kwa muda mrefu sana. Tukio la leo ni muhimu sana kwangu kuanza zoezi langu la kulipiza kisasi kwa Rodney Shangwe wa Osher Corporation. Alinifukuza hapo awali, lakini hah! Siwezi kusubiri kuona macho yake ya huzuni na majuto sasa,” Pamela alisema huku kichwa chake kikiwa juu.
“Sawa, fanya haraka kula. Ondoka ukimaliza, usije ukaachwa na ndege.” Lisa alisema huku akizuia kicheko.
“Ni masaa mawili tu kutoka Dar hadi

Nairobi. Mkurugenzi wa SE Group ametuma ndege binafsi kuja kunichukua, sina presha. Kongamano halitakuwa na maana ikiwa mimi sitahudhuria.” Pamela alijigamba.
•••
Katika Jumba la kifahari la Rodney Shangwe.
Baada ya mpishi kutoa kifungua kinywa, msaidizi wa Rodney alimpa ratiba na kusema, “Bwana Shangwe, mwanakemia wa kimataifa wa vipodozi, Nicole, atakuwa akizungumza jukwaani kwa ajili ya kongamano la SE Group saa saba mchana wa leo. Ungependa kwenda? SE Group imetuma mwaliko.”
Rodney alikunja uso na kukoroma. "Huyu jamaa, Bwana Erick Malugu, ameweza kumwalika Nicole?"

“Ndiyo.” Msaidizi akapumua. "Lakini, Nicole ni wa kushangaza sana. Tumemwalika aje Kenya mara nyingi sana lakini amekuwa akikataa kila mara. Nilifikiri kwamba haipendi Kenya, lakini sikutarajia angekubali ghafla kuja wakati SE Group, mpinzani wetu kibiashara, alipomwalika. Osher ipo juu kuliko SE katika kiwango cha hadhi na brand. Watu wenye akili wangechagua kushirikiana nasi badala yake.”
Rodney alikitumbukiza kichwa chake katika mawazo mazito. "Je, Nicole amesaini mkataba wa ushirikiano na SE?"
"Hapana, lakini inasemekana kwamba Nicole anakuja Kenya wakati huu kutia saini mkataba na SE. Nilisikia kwamba ana fomula ya kipodozi cha kuzuia

kasoro za ngozi na kuimarisha ngozi mikononi mwake. Itakuwa shida ikiwa zitanunuliwa na SE. Baada ya yote, bidhaa zilivumbulia na Nicole miaka hii zimekuwa bidhaa maarufu ulimwenguni kote na hadi 80% ya watumiaji wanarudi kununua bidhaa hizo tena.”
Baada ya kuambiwa hayo, Rodney alihisi kuudhika. "Wataalamu wa vipodozi katika kampuni yetu wote hawana maana. Tunawekeza pesa nyingi sana kwao kila mwaka, lakini hawajawahi kufanya chochote cha kuridhisha.”
Msaidizi wake alikunja midomo yake na kusema, “Mkurugenzi wa Idara ya utafiti na maendeleo humsifia kila Pamela Masanja, mwanamke aliyewahi kufanya kazi Osher miaka minne iliyopita. Alikuwa na kipaji kikubwa, lakini inasikitisha kwamba—”

"Nyamaza." Rodney alimtazama msaidizi wake kwa ukali. “Pamela Masanja ni mwanamke asiyefaa. Hakuna kitu cha kusifia juu yake. Wataalamu wa vipodozi kama yeye wanaweza kupatikana kote nchini. Sitaki kumsikia!”
"Hiyo ni sawa. Pamela Masanja hakika hayuko kwenye kiwango sawa na Nicole.” Msaidizi alikubali kwa kichwa alipoona bosi wake akiwaka.
"Hata iweje, hatuwezi kuruhusu Nicole kushirikiana na SE Group." Rodney aliinuka ghafla. “Nipatie hiyo kadi ya mwaliko. Nitaenda kwenye kongamano la SE na kukutana na Nicole mimi mwenyewe. Nikienda kibinafsi, bila shaka atalazimika kunionyesha heshima fulani.”

Sura ya: 363
Katika hoteli ya nyota tano. Sankara Nairobi. Saa sita adhuhuri.
Baada ya Rodney kukabidhi kadi ya mwaliko na kuingia, Bwana Erick Malugu wa SE Group alimkaribisha kwa furaha. “Bwana Shangwe, karibu, karibu sana. Nilijua utakuja leo. Nilisikia kwamba Osher Corporation ilikuwa imemwalika Nicole mara kadhaa lakini siku zote ilikataliwa, kwa hivyo sikuwa na matarajio mengi nilipomwalika. Lakini ni nani aliyejua kwamba angekubali kwa urahisi?”
“Hongera sana, Bwana Malugu." Rodney alitabasamu vibaya. "Lakini

anakuja tu kuhudhuria kongamano, sio kushirikiana na wewe. Usisherehekee haraka sana, Bwana Malugu.”
“Hiyo ni kweli. Lakini Nicole pia amekubali mwaliko wangu usiku wa leo ambapo tutazungumza kuhusu fomula fulani ya kipodozi adimu.” Bwana Malugu alicheka. “Samahani, Bwana Shangwe. Ikiwa tutapata fomula hiyo, mauzo ya bidhaa zetu kwa nusu ijayo ya mwaka hakika yatapita yako."
Midomo ya Rodney ikatetemeka. Bwana Malugu akampigapiga begani. "Lakini Bwana Shangwe, hautajali, sivyo? Familia ya Shangwe ina viwanda vingi sana. Hata kama Osher Corporation itapotea, bado una kampuni nyingi katika tasnia zingine unaweza kuchukua. Tunaweza hata kuwa washirika wakati huo."

Rodney alikunja uso kwa ukali, uso wake mzuri ukasinyaa na kuwa mbaya ghafla. Ndiyo, familia ya Shangwe ilikuwa katika viwanda vingi, lakini wakati huo huo, familia ya Shangwe ilikuwa na watoto wengi na wajukuu. Osher Corporation pekee ndiyo ilikuwa mikononi mwake. Kama ingemfia, hakuwa na jeuri ya kudai kampuni nyingine kutoka kwenye familia yao. Ikiwa kampuni ingemfia mikononi mwake, angechekwa na familia zingine za Shangwe. Ilibidi ampate Nicole.
Kama mgeni muhimu wa kongamano la siku hiyo, Nicole angetokea tu wakati muhimu. Saa saba kamili mchana, mwenyeji alipiga makofi.
“Tumkaribishe mwanakemia mahiri wa vipodozi kutoka Marekani, Nicole. Nicole haitaji utangulizi. Akiwa na umri

wa miaka 25, alifundishwa na Mwalimu Simpson, mtu ambaye alianzisha tasnia ya urembo wa anasa. Leo, Nicole anafanya kazi na brand nyingi za juu za kimataifa. Mwaka jana, lipstick zake za mfululizo wa Sapphire alizobuni zilivunja rekodi kwa mauzo ya kimataifa."
Chini ya macho ya umati, mwanamke aliyevaa nguo ndefu ya kifahari alijongea kwenye jukwaa la ukumbi wa ‘The Kenyatta International Conference Centre’. Mwanamke huyo alikuwa na sifa maridadi, pua iliyonyooka, na macho yaliyoeleweka vizuri. Alionekana mzuri na mrembo kama waridi linalochanua.
Rodney aliminya kwa nguvu glasi ya maji iliyokuwa mkononi mwake, na kusababisha maji kumwagika na kulowesha mkono wake. Hata hivyo, hakutambua hilo. Hakutarajia kamwe

kuwa Nicole, mwanakemia maarufu wa vipodozi angekuwa... Pamela Masanja. Alikuwa ni mwanamke ambaye aliwahi kumdharau. Maneno ya kiburi aliyokuwa ameyasema asubuhi ya siku hiyo yalionekana kumpiga usoni.
Akiwa jukwaani, macho ya Pamela yalimtoka kabla ya kumwangukia kila mtu. Kwa tabasamu, alisema, “Halo watu wote. Mimi ni Nicole, ninayejulikana pia kama Pamela Masanja.”
Watazamaji walisimama, wakalikumbuka jina hilo la kawaida.
“Ndiyo, niliwahi kufanya kazi kama mkemia wa vipodozi katika kampuni ya Osher, lakini haikuchukua muda Osher kunishutumu kwa wizi na utovu wa nidhamu. Walinifungia kuajiriwa na

kampuni zote za vipodozi nchini. Kimsingi sikuweza kupata kazi nchini wakati huo.”
Pamela alitabasamu huku akiongelea maisha yake yaliyopita. Alimtazama Rodney ghafla. "Bwana Shangwe, baada ya miaka mitatu, najiuliza ikiwa bado unaamini kuwa kweli nilikuibia? Ikiwa ningefanya hivyo, ningekuwa na hadhi niliyo nayo leo?"
Kila mtu mara moja akamtazama Rodney. Kila mtu aliyekuwepo alikuwa aidha ni mkurugenzi wa kampuni fulani au mtendaji wa ngazi za juu. Wote walielewa kuwa huo ulikuwa mchezo wa kitoto kwa Bwana Rodney kumkandamiza mkemia mdogo wa vipodozi.
Isitoshe, ikiwa Pamela aliiba kweli,

angewezaje kuwa mwanakemia mkuu wa vipodozi na maarufu? Watu walitegemea nguvu ya kusema.
Akiwa ametazamana na umati wa watu, Rodney alikunja ngumi zake kwa siri zilizokuwa kwenye magoti yake. Uso wake mzuri ulikuwa karibu kugeuka majivu. “Sikuwa na habari nyingi kuhusu matukio ya mwaka huo. Labda... watu walio chini yangu walinipa taarifa potofu.”
Baada ya muda, Rodney aliweza tu kuweka uso wa ujasiri na kuelezea. 'Ndio hivyo?"
Pamela alitabasamu kwa utamu na kusema kwa sauti ya mzaha,
“Bwana Shangwe, uamuzi wako wa kunifukuza na kunifungia miaka minne iliyopita uliniumiza sana. Lakini sina budi kukushukuru. Ulikuwa kikwazo

kwenye njia yangu ya mafanikio. Kama si wewe, nisingekutana na Mwalimu Simpson baada ya kuondoka nchini.”
Kisha, Pamela akaachana na Rodney na kuingia kwenye kiini cha kongamano. Alizungumza kuhusu baadhi ya utaalamu wake juu ya bidhaa za vipodozi.
Hapo awali Rodney hakutaka chochote zaidi ya kumpiga teke, lakini kwa sababu fulani, kadiri alivyokuwa akisikiliza, ndivyo alivyokuwa akivutiwa zaidi. Ilibidi akubali kwamba Pamela Masanja alikuwa na uzoefu na ujuzi. Kwa kweli alikuwa bora zaidi kuliko wanakemia wa vipodozi katika kampuni yake.
Mwishoni mwa kongamano, mwandishi wa habari ghafla alisema, "Bi. Masanja,

nakukumbuka. Miaka mitatu iliyopita, tukio lako na Thomas Njau lilizua gumzo kubwa. Nilisikia kwamba ulijilahisisha kwa Thomas—”
Uso wa Bwana Malugu ulibadilika huku akimkodolea macho mwandishi huyo. "Unatoka wapi? Usizungumze ujinga.”
“Ninasema ukweli. Tukio hilo liliibua hisia wakati huo. Bi Masanja alinajisiwa na Thomas Njau na kupelekwa hospitalini,” mwanahabari alisisitiza kauli yake kwa nguvu.
Umati wa watu uliingiwa na kizaazaa, na macho yao walipomtazama Pamela nayo yakawa ya ajabu.
Tabasamu zuri usoni mwa Pamela likabaki. Alinyanyua miguu yake mirefu na kushuka kutoka jukwaani kwa

utulivu, akimsogelea mwandishi huyo hatua kwa hatua bila hata chembe ya woga machoni mwake.
“Mara zote mimi husema kwamba wanawake lazima wajitahidi kujitegemea. Wakati msimamo wako ni wa chini sana na hata kama hujawahi kufanya chochote kibaya, unapokutana na mtu anayetegemea mamlaka na watu wenye nguvu nyuma yake ... mkosaji ambaye huwadhalilisha na kuwadhulumu wanawake atakuwa mwathirika mwishowe."
“Bi. Masanja, unamaanisha kusema...” Kulikuwa pia na waandishi wengine ambao walisimama polepole na kuuliza.
Pamela alisema kwa upole, “Huu ndio ukweli nyuma ya kile kilichotokea wakati ule. Nilimkataa Bwana Njau mara nyingi

aliponinyemelea, kwa hiyo aliweka kinyongo na kunivamia ndani ya nyumba yangu. Alinipiga kwa nguvu kwa nia ya kunibaka. Kwa bahati nzuri, rafiki yangu alifika kwa wakati.
“Ingawa nilikuwa sawa, mimi na rafiki yangu tulijeruhiwa na kulazwa hospitalini. Kama mnavyojua, dada mdogo wa Thomas Njau anaungwa mkono na Mwenyekiti wa KIM International. Dada wa Thomas anakaribia kuolewa katika familia ya Kimaro hivi karibuni. Wakati huo, ningewezaje kushindana na familia ya Kimaro?”
Mwandishi alifoka, "Kwa maneno mengine, unajaribu kusema kuwa ni Bwana Kimaro aliyemuunga mkono Thomas Njau na kukuundia kashfa?"

Pamela alisema kwa unyonge, “Ikiwa huniamini, unaweza kuchambua mambo mengine yote ambayo Thomas Njau amekuwa akijihusisha nayo kwa miaka mingi. Miaka iliyopita, mwanafunzi wa chuo kikuu alilazimika kujiua baada ya kubakwa na Thomas. Mwishowe, Thomas alimtegemea dada yake mdogo na akaondoka mahakamani bila hatia.
"Miaka hii michache, pia alikuwa amelazimisha wanawake wengi kutoa mimba. Hadi sasa, hakuna mtu kutoka kwa familia yenye heshima ambaye yuko tayari kuolewa naye. Ningewezaje kupenda kipande cha takataka kama yeye?"
Kila mtu alivuta pumzi ya baridi. Wote walijua kuwa mdogo wa Thomas Njau alikuwa karibu kuolewa na Alvin Kimaro. Maneno ya Pamela yalikuwa ni sawa na

kumwita Alvin takataka.
Rodney hakuweza tena kujizuia. "Pamela Masanja, ninakusihi uangalie maneno yako. Usifikiri kwamba wewe ni mtu asiyeweza kuguswa kwa kuwa sasa unajulikana katika tasnia ya vipodozi.”
Sura ya: 364
“Ninasema tu ukweli kuhusu mwaka huo. Kuna uhusiano gani na mimi kutoguswa?" Pamela alijibu huku akicheka.
“Unathubutu kusema mbele ya kila mtu kwamba Thomas Njau ni muungwana, Bwana Shangwe? Sahau, neno 'muungwana' ni kubwa na tata sana. Wacha tutumie neno "heshima". Je, Thomas ana heshima hata hivyo?"

Rodney aliwekwa njia panda. Kila mtu aliifahamu tabia ya Thomas. Rodney angekuwa tayari kushusha hadhi yake na kusema kwamba Thomas Njau alikuwa na tabia nzuri? Kwa kweli asingeweza kusema, huvyo. Kwa kweli, hakuwahi kukutana na mtu mchafu kama huyo hapo awali. Ikiwa sio kwa ukweli kwamba alikuwa kaka yake Sara, angeweza hata kumkana kwamba hamjui.
Pamela alitabasamu na kucheka kwa furaha moyoni mwake. Alikuwa akifanya kazi kwa bidii katika miaka mitatu iliyopita ili kulipa fedheha zote
alizopitia wakati huo.
Lisa hakuwa peke yake aliyeshikilia chuki za nyuma; Pamela pia.
Ni wazi alikuwa mwathirika katika tukio

hilo la Thomas lakini kashfa zikamgeukia yeye kwa kuitwa majina machafu. Hakupenda. Popote alipoenda, alinyooshewa vidole. Hata watu wealiomuheshimu hapo awali aliokuwa akiwasiliana nao walianza kumtumia meseji katikati ya usiku, wakiuliza ingegharimu kiasi gani kulala naye kwa usiku mmoja.
Alipoondoka, alikuwa kama mbwa mnyonge aliyepotea, lakini sasa ulikuwa wakati wa yeye kurejesha tena hadhi yake katika jamii hatua kwa hatua.
Pamela kwa mara nyingine tena aligeukia kipaza sauti cha mwandishi na kusema, “Ni vizuri kwamba umegusia tukio la Thomas Njau. Ngoja nimtangazie Thomas kuwa nimerudi! Uliponitisha wakati huo, niliweza tu kumeza maneno yangu, lakini ukweli utafichuliwa mapema au baadaye.”

Kisha akageuka na kuondoka.
Rodney pia alionekana kupotea katika mawazo kwa muda. Alipochukua hatua kubwa kujaribu kumfuata, Bwana Malugu alimzuia. "Bwana Shangwe, tangu ulipomfukuza talanta kama Bi. Masanja miaka mitatu iliyopita, anakuchukia sana. Usimfuate tena. Nadhani hataki kukuona pia.”
“Ondoka njiani,” Rodney aliamuru huku akiwa na uso wa mkali.
"Fomula iliyo mikononi mwa Bi. Masanja itakuwa ya SE Group." Bwana Malugu alimtazama machoni bila kukata tamaa. Katika kura ya maegesho kwenye ghorofa ya kwanza ya basement ya hoteli.
Gari la michezo lilikuja.

Katika maegesho ya magari kwenye ghorofa ya kwanza ya basement ya hoteli.
Gari la kifahari likajongea. Pamela alifungua mlango wa gari na kukaa kwenye kiti cha abiria. Mara tu baada ya kufunga mkanda alipokea simu ya video kutoka kwa Lisa.
Hapo hapo Suzie alikandamiza midomo yake kwenye na kumbusu. “Godmother, wewe ni mzuri sana. Umeongea vizuri sana."
“Mmeona?” Pamela alishangaa kwa furaha.
"Kulikuwa na matangazo ya moja kwa moja." Lisa akajitokeza kwenye simu yake. "Ingawa si watu wengi walioitazama, habari zitaenea polepole."

"Hakika nitalipiza kisasi kwa kile kilichotokea mwaka huo." Pamela aliuma mdomo. “Simuogopi Thomas Njau. Ni kwamba Alvin Kimaro, ambaye yuko nyuma yake, anasumbua kidogo.”
“Usijali, chukua muda wako. Hebu tufanye kazi pamoja. Tayari nilimwambia Big V achapishe ulichosema. Sasa ngoja tuone.” Lisa alimwambia kwa furaha. “Rudi Dar mara moja, nimekuandalia chakula.”
Katika sofa walilokuwa wamekaa, Suzie aligeuka na kumnong’oneza Lucas, “Kaka, Alvin Kimaro ndiye baba yetu mchafu?”
“Ndiyo.” Lucas alikunja uso na kutikisa kichwa.

Suzie aliuma mdomo wake na kusema kwa hasira, “Kwanini baba yetu ni mchafu? Alimuumiza Mama, na alimuumiza pia Godmom. simpendi hata kidogo.”
“Hata mimi simpendi.” Lucas tayari alimtambulisha Alvin kama adui yake.
•••
Kile ambacho Pamela alisema kwenye kongamano hilo kilisukumwa polepole kwa vyombo vya habari na Big V, na kwa hivyo, habari za zamani za miaka mitatu iliyopita zilichimbwa tena.
[Namkumbuka huyu binti sasa. Miaka mitatu iliyopita, ilisemekana kwamba alimtongoza Thomas Njau, hivyo alikaripiwa na kila mtu.
Watu hata walimrushia mayai viza wakati anatembea.]

[Anashangaza. Yeye ni mwanakemia maarufu wa vipodozi sasa. Sijui ni kwanini, lakini kwa namna fulani naamini kwamba anasema ukweli. Labda ni kwa sababu yeye ni mrembo.]
[Kwa kweli nilitaka kusema hivi miaka mitatu iliyopita. Tabia ya Thomas Njau kweli si nzuri, lakini hakuna aliyeniamini.]
[Nina jamaa wa mbali ambaye alifanya kazi katika New Era Advertisings na mara kwa mara alitongozwa na Thomas. Mwishowe, alijiuzulu kwa sababu asingeweza kuvumilia tena.]
[Thomas Njau ni fisadi maarufu katika jiji hili. Nilikuwa na mwanafunzi mwenzangu wa chuo kikuu ambaye alivutia umakini wake, lakini alimkataa.

Mwishowe, alimlazimisha kwa nguvu akamsababisha hadi ajiue. Familia yake ilimshtaki, lakini haikufaa. Alitetewa na wakili bora kabisa.]
[Kila mtu anajua kwamba dada yake mdogo ni Sarah Njau.
Anafanya ushenzi tu kwa sababu anajua shemeji yake ni Alvin Kimaro.]
Mambo yalipoanza kuwa mbaya, Hans akaenda kuripoti kwa Alvin. Wakati huo Alvin alikuwa akiongozana na Sarah kujaribu mavazi yake ya harusi.
“Pamela Masanja?” Alvin bila ufahamu alimfikiria Lisa aliposikia jina hilo. Kipindi hicho alikuwa akijaribu kila awezalo kutofikiria juu yake. Hata hivyo, sasa jina la Pamela lilipotajwa, tukio la miaka mitatu iliyopita nalo lilijirudia tena akilini mwake.

"Ndio, inaonekana anataka kufichua ukweli kuhusu tukio la Thomas Njau miaka mitatu iliyopita." Hans Aliitikia na kusema, “Kwa kuwa sifa ya Thomas Njau imekuwa duni miaka hii, maoni yote mabaya ni dhidi yake. Sasa, watu kwenye mtandao... wanazungumza kuhusu Bi. Njau na wewe.”
“Wanasema nini?” Alvin aliuliza kwa uso wa hasira.
"Wanasema unatumia nafasi yako kuwadhulumu wengine."
Alipokuwa akijaribu mavazi ya harusi, sura nzuri ya Sarah ilibadilika aliposikia maneno hayo. Hakuwahi kufikiria kuwa Pamela angetokea tena. Si alikuwa tu mfanyakazi mdogo chini ya Rodney wakati huo? Aliwezaje kurudi tena kwa

nguvu kama Lisa?
Sarah aliuma meno lakini haraka akasema kwa hatia, “Samahani, Alvin. Sikutarajia tukio lile lingeweza kukuletea shida tena, lakini tayari nimeshawahi kumpa onyo kaka yangu kuhusiana na hili. Anajiheshimu sana sasa hivi.”
Hans hakuweza kujizuia kusema, “Lakini... niliona baadhi ya watu kwenye mtandao wakisema kwamba Bwana Njau... mara nyingi huwanyanyasa wafanyakazi warembo katika kampuni.”
Uso mzuri wa Alvin mara moja ukapoa. Sarah alimlaani Hans kwa siri, lakini uso wake ulionyesha huzuni tu. “Kwa kweli sikujua kuhusu hilo. Labda kuna mtu aliajiri watu kutoa maoni hayo... "
“Inatosha. Zuia jambo hilo kwanza.”

Alvin akageuka kumuamuru Hans. “Bila shaka.”
Baada ya Hans kuondoka, Sarah alimshika mkono Alvin. “Alvin, kuhusu suala hili, ni kaka yangu ndiye aliyemkosea Pamela. Vipi kuhusu mimi kumfidia dola milioni moja?”
"Ikiwa unafikiri kweli kwamba alikuwa na makosa, basi mwambie afunge mdomo wake." Alvin alikasirika bila kifani. "Yeye ndiye alikuwa na makosa lakini alikimbilia kwa waandishi na kusema kwamba Pamela alimtongoza. Ikiwa sivyo kwamba yeye ni kaka yako, ningemuua tayari.”
Mwaka huo, pia alikuwa Thomas Njau ambaye alimfanya kupoteza watoto wake kwa njia isiyo ya moja kwa moja.

Alvin alijawa na karaha kwa mwanaume huyo sasa.
Sarah alishtushwa na hasira iliyokuwa machoni mwake, na macho yake yakawa mekundu huku akiomba msamaha kwa haraka, “Samahani, ni kosa langu. Sikupaswa kuwa mbinafsi na kukuomba umwokoe kwanza.” “Sahau, si kosa lako. Hata hivyo, siku za usoni, sitajali iwapo ataishi au kufa tena,” Alvin alisema kwa kuudhika.
“Sawa.” Sarah alizuia machozi yake. "Alvin, je! vazi hili la harusi linanipendeza?"
Alvin alimtazama kwa kawaida na kutikisa kichwa. "Tutanunua hili." Kisha, akatoka nje. Kwa sababu fulani, alihisi kwamba ikiwa nguo hiyo ingevaliwa na Lisa badala yake,

ingekuwa nzuri zaidi.
Sarah alimtazama yule mtu wa nusu nusu na kukanyaga mguu wake kwa hasira.
Sura ya: 365
Wakati huo huo, Thomas alimpigia. "Sarah, yule b*tch Pamela Masanja amerudi. Wakati huu, hakika nitammaliza!”
Uso mrembo wa Sarah mara moja ukaangaza kwa mguso wa karaha. "Funga mdomo wako. Huu ni wakati mgumu kwani nitafunga ndoa na Alvin hivi karibuni. Usiniletee balaa.”
Thomas alishtushwa na karipio la ghafla. "Lakini haukuona alichosema

Pamela kwa waandishi wa habari"
“Alvin tayari ameweka mtu wa kuzima jambo hilo. Ikiwa una kinyongo, basi subiri baada ya harusi yangu.” Sara alisema neno baada ya neno, “ ikiwa kitu kitaenda vibaya, sitakusaidia."
“... Sawa.” Thomas alikata simu bila kupenda, lakini moyoni hakufikiri kwamba jambo lolote lingeharibika. Akageuka, akapiga simu. "Nenda utafute anapoishi huyo b*tch Pamela Masanja."
•••
Katika hoteli ya kifahari ya ‘The Concord Hotel & Suites.’
Mhudumu alimuongoza Pamela na kusimama kwenye mlango wa chumba cha faragha. "Hiki ndicho chumba

ambacho Bwana Malugu alipanga kwa ajili yako."
"Asante." Pamela aliusukuma mlango na kuingia ndani.
Rodney alikuwa ameketi mbele ya skrini ya kale. Alivaa shati la kahawia na vifungo viwili vya kwanza vilikuwa vimefunguliwa. Mikono ya shati ilikuwa imekunjwa, na macho yake yalikuwa makali kwenye uso wake mzuri, na kumpa mtazamo mbaya lakini wa mapenzi.
“Keti.” Akaelekeza kwenye kiti kilichokuwa kando yake.
Pamela hakuweza kuwa na wasiwasi naye na akageuka kuondoka, lakini alipojaribu kufungua mlango, aligundua kuwa umefungwa.

“Usiondoke. Kula. Chakula hakitakuwa na ladha kikiwa cha baridi.”
Rodney aliinuka na kumburuta hadi kwenye kiti. “Bi. Masanja lazima ulijisikia vizuri ulipokuwa ukizungumza kwenye kongamano leo. Nakubali, umenishangaa. Nilikosea juu yako hapo awali. Ninakupa toast hii kama msamaha, sawa? Una furaha sasa?"
Rodney alijimiminia glasi ya mvinyo mwekundu na kuinywa. Pamela aliitazama glasi ya mvinyo iliyokuwa mezani kwa muda kabla ya kwenda kumimina mvinyo ndani yake.
Rodney alifurahi, akifikiri kwamba alitaka kutoa toast, lakini bila kutarajia, aliinua mkono wake na kumwaga mvinyo wote kwenye uso wake mzuri.

"Pamela Masanja!" Uso wa Rodney ulibadilika sana. Alipokaribia kukasirika, Pamela alichukua chupa ya divai, akaifungua kola yake na kumimina vilivyomo ndani ya shati lake. Mvinyo ulikuwa baridi, na kusababisha Rodney kupiga kelele.
Aliruka pembeni na kuvua shati haraka, lakini suruali yake ilikuwa tayari imelowa. Suruali yake ilishikamana kwa nguvu kwenye mapaja yake, ikionyesha mistari ya kuvutia.
"Pamela Masanja, unataka kufa?" Rodney alikasirika. Hakuna mtu aliyewahi kuthubutu kumfanyia hivi. Mwanamke huyu alikuwa mwendawazimu! Anathubutu vipi kummwagia mvinyo?!
Alikuwa amepoa sana baada ya kuvua

nguo zake. Alitetemeka, na kwa macho yake, hakutaka chochote zaidi ya kumla akiwa hai.
Kwa upande mwingine, Pamela alikuwa akitabasamu kwa furaha. “Nilifikiri haujaamka kabisa, kwa hiyo nilikumiminia mvinyo. Rodney Shangwe, nadhani umezoea sana kutetemekewa kwa kuwa bwana mdogo tajiri sana. Hujawahi kunitendea haki hata kidogo. Wakati ule, ili kumsaidia Sarah Njau, ulitamka sentensi ya kawaida ambayo karibu kuharibu maisha ya juhudi zangu. Kama hukunipenda, ungenifukuza tu. Kwanini ulilazimika kunifungia kabisa kwenye tasnia?”
Kadiri alivyozidi kusema ndivyo alivyozidi kupata hasira. Aliivunja chupa, na kusababisha vipande vya chupa kusambaa kila mahali.

Rodney aliruka kwenye kiti kwa woga na nusura ateleze kwenye vipande vya chupa. Baada ya yote, hakuwa amevaa shati. "Pamela Masanja, usifikiri kwamba sitathubutu kukupiga!" Rodney alimfokea.
"Endelea. Hata usiponipiga nitakupiga.” Pamela alitumia uma kuokota kipande cha nyama ambavyo vilikuwa bado vya moto kutoka kwenye sahani na kumrushia Rodney.
Rodney aliitazama jinsi chumba kilivyokuwa kimechafuka kwa fujo za kila aina na kumtisha, "Pamela Masanja, nitaita polisi ikiwa utatupa kipande kingine."
"Endelea. Zaidi sana, nitaambiwa kulipa pesa. Naweza kumudu.” Pamela

alimtupia kila kitu mezani.
Rodney hakuweza kukwepa na aliweza tu kukimbilia kushika mikono ya Pamela. Mikono ya Pamela ilikuwa imezuiliwa, hivyo akageuza kichwa chake na kumng'ata kwa nguvu sikioni.
“Sawa!” Rodney alipiga kelele baada ya kuumwa na kuushika sehemu fulani ya mwili wake bila fahamu. Matokeo yake, alihisi kitu laini mikononi mwake. Alipogundua alichokuwa akikamata, tayari alikuwa amepigiwa goti katikati ya mapaja yake na Pamela. Macho yalimtoka kwa maumivu.
Ghafla, aliweza kuelewa maumivu ya Alvin siku nyingine. Haishangazi alikwenda hospitali kwa uchunguzi. Inaumiza sana.
"Tamu eeh?" Pamela alimtazama kwa

dhihaka. “Yako haina maana hata hivyo.”
"Yangu hayana maana?" Rodney alijikunja kwa maumivu na nusura apoteze pumzi.
“Umewahi kuitumia kwa nani?” Pamela alicheka. “Umejitolea kwa Sarah Njau, lakini ataolewa na Alvin Kimaro hata hivyo. Hatakuwa na nafasi katika maisha yako. Unapaswa kuwa towashi tu. Sijawahi kuona mwanaume mjinga kama wewe.”
"Pamela Masanja, thubutu kusema neno moja zaidi..." Macho meusi ya Rodney yalikuwa yamefunikwa na hasira.
“Nimesema kitu kibaya? Nilishakuambiaga muda mrefu. Wewe ni

mwanaume lakini bado una kelele kuliko mwanamke. Kuwa mwanamke katika maisha yako yajayo basi...”
Kabla Pamela hajamaliza, Rodney alimkimbilia na kumg’ata.
Macho yalimtoka Pamela na bila fahamu akajaribu kumpiga tena goti sehemu zake za siri. Wakati huu, Rodney alikuwa amejiandaa na kubana miguu yake haraka. Pamela alipoteza stepu na mwili wake ukaanguka moja kwa moja kwenye mikono ya Rodney. Wakati huo, sauti ya hasira ya Bwana Malugu ilisikika nje ya chumba akimfokea mhudumu. "Mara nyingi mimi huja kwenye hoteli hii. Siamini kuwa ulimleta mgeni wangu kwenye chumba cha mtu mwingine. Mgeni wangu akipata madhara yoyote, sitakusamehe...”

Ndani ya chumba, Pamela aliogopa na kujitahidi sana. "Rodney Shangwe, niachie!"
"Hapana." Rodney aliuma mdomo wake kwa ukaidi na hakumuachilia.
Pamela hakuwa na chaguo ila kuuma, na kwa sababu hiyo, wote wawili waliangukia kwenye sofa.
Kisha, mlango ukafunguliwa. Bwana Malugu na meneja wa hoteli waliingia ndani haraka. Waliona tukio la shauku ndani na walipigwa na butwaa mara moja.
Bwana Malugu alikasirika sana hadi uso wake ukakunjamana. Rodney alilegea, na Pamela akamsukuma kwa nguvu. Ingawa nguo zake zilikuwa safi, kulikuwa na alama za meno kwenye midomo yake na rangi ya lipstick yake

iliacha alama kwenye uso wa Rodney kwa uwazi sana.
“Bwana Malugu, uko kwa wakati. Yeye-”
"Nicole, ninaelewa. Alikutongoza, sivyo?”
Bwana Malugu alikatisha maneno yake. Alimkazia macho Rodney kwa ujeuri ambaye hakuwa amevaa shati na suruali yake ikiwa imelowa. "Bwana Shangwe, unaenda mbali sana. Kwa ajili ya kupata fomula tu, unawezaje kufanya kitu kama kuuza utu wako?"
Ingekuwa ni mtu mwingine, angekuwa na hasira kabisa. Lakini, Radney hakuwa na aibu. Alijipangusa kwa utulivu pembeni ya mdomo wake na

kutabasamu huku akiinua nyusi zake. "Bwana Malugu, unaweza pia kujaribu kuuza utu wako, lakini Bi. Masanja anaweza kufikiria kuwa wewe ni mzee sana."
Uso wa Bwana Malugu ulilegea. Pamela alichukua kitambaa na kujifuta pembeni ya mdomo wake kwa nguvu huku akimkazia macho Rodney. “Pole, Bwana Shangwe, lakini nadhani wewe ni mchafu sana. Mdomo wako huo ni kama choo cha umma. Nimechukizwa.”
TUKUTANE KURASA 366-370
ONYO: Ni marufuku kusambaza, kukopi wala kuuza kazi hii kwani endapo kama tutakubaini basi sheria itachukua mkondo wake (By: Official Dully)
 
LISA KITABU CHA NANE (8) SIMULIZI........................LISA KURASA.................366 - 370
PRESENT: SIMULIZI ZA DULLY

Sura ya: 366
"Ulibusu choo hiki cha umma kwa
furaha." Rodney akakonyeza macho.
“Na ulinivua nguo zangu na kunimwagia
divai. Nimependa michezo yako ya
kusisimua kama hii.”
Kwa maneno yake, meneja wa hoteli na
Bwana Malugu wote walimtazama
Pamela kwa njia isiyo ya kawaida.
Alionekana mrembo sana, lakini bila
kutarajia, alikuwa jasiri na asiyejizuia
kwa ndani.
“Bullsh*t!” Uso wa Pamela ukawa
mwekundu kwa hasira.
Rodney alihisi faraja kadiri alivyozidi
kumuona vile, na macho yake yalimtoka
kwa fujo. “Sahau, sitasema mengi
kuhusu mambo fulani. Baada ya yote,

mwonekano wangu wa sasa unaweza
kuthibitisha kila kitu.”
“Wewe una wazimu!” Pamela akampiga
kofi na kuondoka.
"Halo, vipi kuhusu formula?" Rodney
alifoka nyuma yake bila aibu.
"Endelea kuota!" Pamela aliondoka, na
Bwana Malugu akamfuata mara moja.
Mara tu walipotoweka, Rodney alipiga
chafya mara moja. Alianza kutetemeka
huku akimpigia kelele msaidizi wake
pale nje. "Herbert, vua koti lako na
unipe."
Damn it! alikuwa anaenda kuganda
hadi kufa kwa baridi la Nairobi.
Hakuwa amekula pia.
Herbert alimvulia Rodney koti lake

kimyakimya. "Bwana Shangwe,
mazungumzo ya fomula yaliendaje?"
“Ilikuwa sh*t. Hatukuwa hata tumeanza
kuongea kuhusu fomula na yule
mwanamke tayari ameshaanza
kugombana nami.” Rodney alimtazama
kwa ukali. “Mfuatilie Bwana Malugu.
Haijalishi ni njia gani unayotumia,
usiwaruhusu tu kusaini mkataba. Narudi
nyumbani kuoga.”
Baada ya kuoga kwenye jumba lake la
kifahari, Rodney alikasirika zaidi
alivyofikiria juu ya Pamela. Akampigia
Chester, akisema, “Uko wapi? Niko
katika hali mbaya. Njoo tunywe pamoja
nami.”
"Njoo mahali pa kawaida. Nipo na
Alvin.” Chester alimwambia.

Rodney alipofika aliwakuta Alvin na
Chester pekee yao. “Ni nyinyi wawili tu?
Wako wapi Cindy na Sarah?”
Uso wa Alvin ulikuwa umezama kwenye
giza la mawazo totoro. Hakuongea, na
haikuwezekana kukisia hali yake.
Chester alitazama juu na kutabasamu.
"Kwa hiyo tunatakiwa kuongozana na
wanawake kila mahali tunapokwenda?
Halo, nini kilitokea kwa mdomo wako?
Hiyo ni nadra. Umeumwa na
mwanamke?"
Kwa maneno hayo, Alvin naye
alimtazama kwa uvivu.
Rodney alisema kwa hasira, “Sio
mdomo wangu tu. Angalia sikio langu.
Iiling’atwa hadi likatoka damu. Pamela
Masanja, lazima alikuwa mbwa katika

maisha yake ya zamani. Kitu cha
kwanza alichofanya ni kunimiminia
chupa nzima ya divai mwilini. Nilikaribia
kuganda.” Kufikia hapo aligugumia
kidogo kabla hajasema kwa aibu, "kwa
hiyo, Chester, nisaidie kufanya
uchunguzi. Sehemu yangu ya chini
inauma kama nini baada ya Pamela
kunipigia kwa goti. Alvin, hatimaye
ninaelewa uchungu uliohisi.”
Chester alitoa macho kwa kuchukia.
“Potelea mbali. Mimi si daktari wa
andrology, lakini usijali. Alvin hakuweza
kutembea moja kwa moja alipokuwa
amepigwa nyeti zake na Lisa wakati huo, lakini alikuwa sawa mwishowe.
Sidhani kama kuna shida yoyote
itakutokea.”
“Sawa.” Rodney aliguna, “Pamela na Lisa kimsingi ni mtu na dadake. Hata

mienendo yao ni sawa. Je, walikuwa na
mshauri mmoja walipopotea katika
miaka michache iliyopita?”
"Labda." Chester alimtazama Alvin
kimaana.
Alvin aliwasha sigara. Alipokuwa
akisikiliza maneno ya Rodney, moyo
wake ulijikunja na kutabasamu.
"Alvin, unatabasamu nini?" Rodney
aliuliza.
“Hakuna kitu.” Alvin akainua midomo
yake. Hapo awali alitaka kutoka nje na
kupumzika kwa sababu alikuwa
amekasirika, lakini Rodney alipokuja na
kueleza mambo yake, moyo wake
ulipumua kidogo.
•••

Masaki. Dar es Salaam.
Lisa aliwarudisha nyumbani watoto
wake wawili baada ya kucheza siku
nzima.
"Mama, nataka kucheza kesho pia."
Suzie alimkumbatia Lisa na kukataa
kumuachia.
"Sawa, tutaenda kwenye aquarium
kesho."
Lisa alikuwa akijiandaa kwenda kuoga
wakati alipopokea ujumbe wa whatsapp
kwenye simu yake uliotumwa na
muuguzi wa hospitali kupitia simu ya
baba yake. [ Bi. Jones, tafadhali njoo
hospitalini sasa. Shinikizo la damu la
Bwana Ngosha lilipanda ghafla usiku
huu. Tulimpiga dripu lakini halijashuka.]

[Sawa, haraka mjulishe daktari kuhusu
hali yake. Nitakuwa hapo muda si
mrefu.]
Baada ya Lisa kukata simu, hakuwa na
namna zaidi ya kupanga safari ya
haraka kuelekea Nairobi. Alikata tiketi
kwenye mtandao ya ndege iliyokuwa
inaondoka muda wa karibu zaidi na
baada ya kuoga na kujiandaa haraka
haraka, aliwakusanya watoto wake na
kuelekea uwanja wa ndege. Masaa
manne baadaye alikuwa amefika
kwenye makazi yake huko Karen
Estate, Nairobi.
Ilikuwa ni usiku tayari, mida ya saa nne
hivi. Aliwaambia watoto wake wawili,
“Babu yenu hajisikii vizuri, kwa hiyo ni
lazima niende hospitali sasa hivi
kumuona. Mtabaki hapa nyumbani
mlale sawa? Godmother wenu atarudi

baada ya muda mfupi."
"Mama, tunaweza kwenda kumsalimia
babu pia?" Lucas aliuliza huku
amekunja uso.
“Sasa si wakati mzuri. Zaidi ya hayo,
babu ni dhaifu sana hawezi
kuzungumza na nyie. Tunaweza
kwenda kumtembelea wakati fulani
baadaye.” Lisa alijua wanawe
hawakuwa wasumbufu.
Aliwabembeleza hadi alipoona
wameanza kukole usingizi.
Baada ya kuwafariji watoto wake wawili
wapenzi, alikimbia hospitali akiwa hoi.
Akiwa njiani kwenda huko, alimpigia
simu Pamela, akimtaka arudi nyumbani
mapema.
Kumbe wale watoto wawili walikuwa

wamevunga tu kulala ili kumridhisha
mama yao. Baada ya Lisa kuondoka,
Suzie alikuwa wa kwanza kuamka.
Alikagua nyumba nzima kutafuta
vitafunwa. “Hehe. Nilijua mama
angeficha chokoleti hapa. Alidhani
nisingejua.”
Suzie akamtupia Lucas pakiti ya
chokolate. “Unaitaka?”
“Sili kitu alichotukataza mama, alisema
tutakuwa bubu.” Lucas alimjibu huku
akiifuata laptop ya mama yake iliyokuwa
mezani. Alipenda sana kuchezea
kompyuta tangu akiwa mdogo kabisa.
Suzie hakuelewa ni kwanini mama yao
aliwakataza kula chokoleti mara kwa
mara. Aliona aina hii ya chakula ni tamu
sana. Alihisi kwa kuwa mama yake
hakufurahia yeye kula chokoleti, baba

yake huenda angemruhusu. Hivyo
Suzie akatamani kumtafuta Alvin.
Lucas aliwasha laptop. Na kwa kuwa
eneo lile lilikuwa limeunganishwa na wi-
fi, laptop ilishika mtandao wa internet
mara moja. Lucas alikuwa anapenda
sana kutazama katuni kwenye mtandao
wa Youtube. Pamela alimfundisha jinsi
ya kuingia huko kupitia simu na
kompyuta na kwa sababu Lucas alikuwa
na akili nyepesi ya kitoto, alikariri
haraka.
Baada ya kufungua Youtube, mtandao
ulionyesha video ambazo Lisa alipenda
kutazama mara kwa mara. Kwa hivyo
video nyingi zilizomuonyesha Alvin na
Sarah zilionekana.
“Woooh! Lucas, ni baba yetu mchafu!”
Suzie aliruka kwa mshangao. Wote

waliifahamu vizuri sura ya baba yao
kwani walionyeshwa na mama yao
kwenye picha na video za simu.
“Bonyeza hiyo video tumuone baba...”
Suzie aliingiwa na shauku ya ajabu.
Muda mfupi baadaye, Lucas akabofya
video mojawapo na video ikaanza
kutembea. Suzie aliyekuwa anakula
chokoleti alimsogelea Lucas. "Wow, ni
mtu mzuri sana! Yeye ni mzuri zaidi
kuliko mjomba Kelvin. Lazima nipate
mchumba ambaye ni mzuri kama yeye
nikikuwa mkubwa."
“Baba yetu ni mchafu.” Lucas alimkazia
macho. "Mama labda alidanganywa kwa
sababu alikuwa na mawazo kama
yako."
“Woooh, baba anaongea, anasemaje

baba?” Suzie akatoa macho yake. Alvin
alikuwa akihojiwa na waandishi wa
habari kwenye video hiyo.
Lucas alijibu kwa sauti ya chini, “Mm.
Kulingana na habari, anaenda kuoa
mapema mwezi ujao. Mwanamke
ambaye atamuoa ni Sarah Langa, na
hivi ndivyo anavyoonekana.”
Suzie akaikazia macho sura ya Sarah
aliyeonekana pembeni mwa Alvin, kisha
akakunja midomo yake. “Ni mbaya
sana. Yeye siyo mrembo kama Mama.
Baba yetu mchafu ana mke mbaya
sana."
“Ndiyo.” Lucas alikodoa macho.
“Wamemuumiza mama. Ni lazima
tulipize kisasi kwa ajili ya mama.”
“Hakika, hakika. Kwa hivyo tutalipaje
kisasi?" Suzie alisisimka.

Wakati huo, ghafla sauti ya ajabu
ilisikika kutoka nje. Kulikuwa na watu
wanakuja!
Sura ya: 367
“Shhhh!” Lucas alimfanyia Suzie ishara
ya kunyamaza. Haraka akafunga laptop.
Kisha, akamvuta Suzie na kutafuta
mahala pa kujificha.
Akiwa na wazo, alimwaga nguo chache
kutoka kwenye sanduku kisha akamvuta
Suzie ndani ya lile sanduku na kuweka
nguo chache juu yao, halafu akalifunika
bila kufunga zipu. Wawili hao walikuwa
wamejikunja ndani kwa pamoja kama
sungura.
Suzie alipokuwa amejikunja huku
akishusha pumzi, alijisikia vibaya sana.

Aliuliza, “Unafanya nini Lucas? Lazima
ni Godmother anarudi—”
Kabla hajamalizia sentensi yake, Lucas
alimziba mdomo. "Nyamaza.
Godmother havuti sigara, we hujasikia
harufu ya sigara?” Lucas alijibu kwa
sauti ya kunong’ona. Alipomaliza tu
kuongea, mlango wa nje ukafunguliwa
kwa nguvu. Baadaye, sauti ya mtu wa
kushangaza ilisikika.
“Vega, sioni mtu yeyote hapa, lakini taa
zimewaka.”
"Anaweza kuwa kajificha. Nenda
ukaangalie pande zote."
Watu wachache walisikika wakiingia
chumbani. Walipekua kabati la nguo na
chini ya kitanda na kuonekana kukata
tamaa. "Hakuna mtu, bana, Vega."

“Umeangalia mpaka bafuni, stoo,
jikoni... ?” Mtu yule kwenye simu alizidi
kusisitiza. Wale jamaa mle ndani
wakasambaa kila kona kutafuta, lakini
hawakuona mtu.
Macho ya jamaa mmoja yakaangaza
kwenye chumba hicho. Akakazia macho
kwenye sanduku lililokuwa kwenye
kabati la nguo. Je, anaweza kuwa
kajificha humu? Aliponyoosha mkono
wake kulifungua, mtu aliyekuwa nyuma
yake alimpiga teke. “Una akili kweli
wewe! Unafikiri mtu mzima anaweza
kutoshea kwenye sanduku dogo kama
hilo?”
Alinyamaza kwa muda kabla ya
kuangaza huku na kule na kusema
kwenye simu, “Bwana Vega, hakuna
mtu humu.”

“Sawa. Vunja kila kitu ndani ya
nyumba."
Kwa hayo, nyumba ya Lisa ikageuka
kuwa Ukraine. Vurugu ya vitu vikivunjwa
hovyohovyo ilisikika kwa kishindo.
Walivunja chupa za mvinyo, vioo vya
makabati na dressing table, madirisha,
vyombo vya jikoni, TV, pamoja na
kupora vitu vya thamani. Baada tu ya
kumaliza kuvuruga kila kitu ndipo
waliondoka wakiwa wameridhika.
Dakika kumi hivi baada ya wao
kuondoka, Lucas alifunua sanduku na
kutangulia kutoka kisha akamtoa pia
Suzie nje. Suzie alitoka akiwa na
mawenge ya woga, hivyo alihisi
kizunguzungu na kuanguka. Kwa bahati
mbaya aliangukia kipande kikubwa cha
chupa ya mvinyo ambacho kilimchoma

kichwani. Kichwa chake kilianza kuvuja
damu kwa wingi.
“Kaka, inauma sana...” Suzie
alimtazama kwa sura ya maumivu akiwa
na pakiti ya chokoleti mkononi mwake.
“Usiogope, Suzie. Nitakupeleka hospitali
sasa hivi.” Lucas alikuwa na wasiwasi
sana hivi kwamba machozi yalitiririka
kwenye uso wake ambao kawaida
ulikuwa mtulivu.
Muda mfupi baada ya Suzie kuumia,
Pamela akaingia, alishangaa kukuta
nyumba ikiwa kwenye vurugu kiasi kile
huku Lucas akiwa anahangaika na
Suzie. Hakukuwa hata na jirani
aliyejitokeza kusaidia.
Lucas alilia alipomuona Pamela,
“Godmother, Suzie ameumiaa.”

"Nini kimetokea?!" Pamela aliuliza kwa
mshtuko huku akimtumbulia macho
Suzie aliyekuwa akivuja damu kwa
wingi. Hapohapo akapiga simu kuita
ambulensi kishaakawabeba wale watoto
kushuka chini.
Wakiwa njiani kwenda hospitali, Pamela
alimpigia simu Lisa kumpa taarifa.
"Mungu wangu! Nimerudi tu na kukuta
nyumba yako kwenye fujo. Nimewaita
polisi. Suzie ameumia.”
“Nini kimetokea? Suzie kaumia? Hali
yake ikoje?” Lisa ambaye alikuwa
amewasili hospitalini, mara baada ya
kusikia maneno ya Pamela aliingiwa na
huzuni nyingi. “Alijijeruhi vipi? Je, ni
serious?”
“Lisa, hata mimi sijui kilichotokea.
Nitazungumza nawe baadaye. Suzie

amezimia. Nimepiga simu ambulensi na
sasa nampeleka hospitalini.” Pamela
alisikika akiwa amekabwa.
Wimbi la hofu lilimkumba Lisa, karibu
kumfanya apoteze akili yake.
Haraka akakimbia kwenda kwenye
hospitali nyingine. Alipofika alimuona
Lucas akiwa amesimama kinyonge
kwenye korido peke yake. Mikono na
uso wake ulikuwa umetapakaa damu.
Mara alipomuona Lisa, akajitupa
kwenye mikono yake huku akilia.
“Mama, Suzie ameumiaaa....”
“Usilie. Niambie kilichotokea.” Lisa
alifuta madoa ya damu usoni mwake
kwa uchungu.
“Muda mfupi baada ya wewe kuondoka,
watu wachache waliingia ndani ya
nyumba yetu, kwa hiyo nikaenda

kujificha kwenye sanduku la suti pamoja
na Suzie. Hawakutuona, lakini mwisho
walivunja kila kitu. Tulipotoka kwenye
sanduku, Suzie aliangukia chupa
ikamkata kichwani.”
Katikati ya maelezo yake, Lucas
alidondosha kilio. “Nilikuwa nimemziba
mdomo Suzie muda wote ili asipige
kelele.”
Lisa alitetemeka kwa hasira. Kamwe
katika ndoto zake za ajabu hakutarajia
kwamba kuna mtu angekuwa na ujasiri
wa kuvunja na kuingia ndani ya nyumba
yake. Aliogopa kufikiria nini kingetokea
kwa watoto hawa wawili ikiwa Lucas asingechukua hatua ya kijasiri kama
hiyo. Alikuwa amevunjika moyo na
mwenye hatia. Kama mama, alishindwa
kuwalinda watoto wake waliporudi hapa.

Muda mfupi baadaye Pamela alitoka
kwenye chumba cha daktari. Alikuwa
kampakata Suzie wakielekea kwenye
wodi kwa ajili ya mapumziko.
“Vipi hali ya Suzie?” Lisa aliuliza kwa
wasiwasi.
"Ametoka kwenye hatari."
Pamela alimkazia macho yake ya
huruma kwa Suzie ambaye alibaki
amepoteza fahamu. Kipaji cha uso cha
mtoto huyo mdogo kilikuwa kimefungwa
kwa kutumia bandeji, na mashavu yake
ya rangi ya waridi yalikuwa yamepauka.
"Hawa watu ni wakatili. Wanawezaje
kumdhuru mtoto?" Pamela alinyamaza
kwa muda kabla ya kuuliza bila kujali,
"Hii haimuhusu Thomas kweli?"
“Pengine.” Lisa aliitikia kwa kichwa bila

huruma. Alikuwa na maadui wengi
sana. Ikiwa Melanie na Damien
wangetaka kuchukua hatua dhidi yake,
wangefanya hivyo lakini wasingetumia
nguvu kiasi hicho.
"Yote ni makosa yangu," Pamela
alisema kwa hatia, "nilimchana makavu
Thomas hadharani wakati wa mkutano
wa waandishi wa habari leo. Lazima alichukia. Anajua nitakuwa nimefikia
kwako. Tayari alikuwa na ujasiri wa
kutosha kuingia nyumbani kwangu
miaka mitatu iliyopita, kwa hiyo sidhani
kama kuna jambo lolote anaogopa
kufanya.”
“Ndio. Alipokamatwa miaka mitatu
iliyopita, hata hakwenda jela. Ndiyo
maana sasa hana woga.” Sura ya
kusikitisha iliosha uso wa Lisa.

Pamela akainua midomo yake.
"Naogopa kwamba Alvin ... atamtetea."
Kifua cha Lisa kilihisi kubana. Aligeuza
kichwa chake na kumtazama Suzie.
Hasira kali ikamjia. Sarah Njauna
Thomas Njau! Ilimbidi kuwalipa
waliomuumiza bintiye!
Wakiwa kwenye wodi ya faragha, Lucas
alimwangalia Suzie na kusema kwa
huruma. “Mama, lilikuwa kosa langu.
Nilipaswa kuzima taa. Nilishindwa
kumtunza vizuri Dada!”
“Lucas, acha kujilaumu. Ulifanya kazi
nzuri. Ulikuwa sahihi kwa kuacha taa
ikiwaka.” Lisa alimkandamiza mabegani.
"Lazima watu hao walikuwa wakitazama
nyumba yetu kutokea chini. Walijua
kuwa taa zetu zinawaka, ungezima
ghafla, wangejua kuna mtu amejificha

ndani ya nyumba. Kwa hali hiyo,
wangegundua kuwa wewe na Suzie
mko kwenye sanduku. Mwishowe, nyote
wawili mngetekwa.”
"Mama, ni nani hao watu waovu?"
Lucas aliuliza huku akiwa amejilaza
mikononi mwake. "Nataka kulipiza kisasi
kwa niaba ya Suzie."
“Wewe ni mdogo sana kufikiria mambo
hayo. Suzie atakuwa sawa tu.” Lisa
alimtuliza mwanaye, lakini
asingewaruhusu wale waliomuumiza
Suzie kutoka kwenye ndoano.
Kwa wakati huo, daktari aliwatembelea
wodini. “Uchunguzi unaonyesha mtoto
amepoteza damu nyingi, lakini hatuna
damu ya kutosha aina ya AB hapa. Kwa
kuwa wewe ni mama yake, je, damu
yako ni AB pia?”

"Hapana." Uso wa Lisa uligeuka kuwa
mbaya.
Lucas alikunja mikono yake na kusema,
“Mama, yangu ni—”
"Hapana. Wewe ni mdogo sana kuweza
kutoa damu yako,” daktari akakatisha
sentensi yake. “Mgonjwa anahitaji
mililita 500 za damu.
Hata mtu mzima hawezi kuvumilia ikiwa
atatoa damu nyingi hivi. Mtoto hakika
ataanguka. Baba wa mtoto yuko wapi?"
“Baba?” Lisa alikunja ngumi. Ikiwa Alvin
angejua kuhusu hili, bila shaka
angemnyakua Suzie kutoka kwake.
Sura ya: 368

Kwa wakati huu, Lucas alivuta mkono
wa Lisa. “Mama, tunaweza kwenda
kumtafuta mjomba Jack.?” Jack Kimaro
ndiye pekee kutoka familia ya Kimaro
aliyefahamu uwepo wa watoto hao.
Alimsaidia Lisa kutoroka na mara kwa
mara alikwenda Marekani kumsalimia
hadi alipojifungua. Lucas na Suzie
walimfahamau vizuri.
Baada ya kupigwa na butwaa kwa
muda, Lisa mara moja akampigia Jack
simu.
Jack aliharakisha kifka hospitalini
pale ndani ya dakika kumi. “Vipi hali ya
Suzie? Mara tu nilipojua kuwa kuna
jambo limempata, nimepita taa nane
nyekundu kuwahi hapa.”
"Asante, Jack." Lisa alimshukuru sana.
“Suzie bado anaendelea na matibabu

ya dharura. Anahitaji mililita 500 za
damu.”
"Nina damu sawa na yeye. Fanya
haraka uchukue damu yangu.” Jack
alikunja mikono yake bila wasiwasi
zaidi.
“Subiri kidogo. Tunahitaji kuthibitisha
aina ya damu yako kwanza.”
Nesi alimshusha haraka haraka. Baada
ya kuthibitisha aina yake ya damu,
mililita 500 za damu yake zilitiwa
mishipani Suzie. Pamoja na hayo, hali
ya Suzie iliboreka taratibu.
"Jack, sijui jinsi ya kutoa shukrani zangu
kwako wakati huu." Lisa alihisi kwamba
alikuwa na deni kubwa la Jack.
"Hakuna wasiwasi. Baada ya yote,
Suzie ni mwanangu kiukoo.”

Kwa sura ya kuhuzunisha, Jack
alimaliza chupa ya maziwa. Alikuwa
mzima wa afya, lakini kutoa mililita 500
za damu bado kulimfanya ahisi
kizunguzungu kidogo. “Nenda
ukamwangalie Suzie. Nitapumzika hapa
kwa muda.”
•••
Kulipopambazuka, polisi walifika na
kumwambia Lisa, “Tumewatambua watu
waliovunja vitu vya nyumbani kwako.
Walikuwa wahuni kutoka jirani, na tayari
tumewakamata. Walikiri kwamba
walivunja nyumba yako kufanya wizi.
Tulipata vito na pesa taslimu. Angalia
na uhakikishe kama hivi ndivyo vitu
walivyoiba nyumbani kwako.”
“Ndiyo.” Lisa alivitazama vile vitu na
kuvipokea.
“Sawa. Kesi imefungwa."

Polisi walipokuwa tayari kuondoka,
Pamela alisema kwa kutoridhika, “Ni
wazi, haukuwa wizi. Kuna mtu aliwalipa
ili kulipiza kisasi kwetu.”
“Inatosha, Pamela. Polisi wamefanya
walichoweza.” Lisa alimsimamisha na
kuwaacha polisi waondoke.
"Nina uhakika Thomas amewahonga,"
Pamela alisema kwa hasira.
Lisa alicheka. “Bila shaka. Naam,
mazoea hujenga tabia. Kadri Thomas
anavyofanya matendo maovu zaidi,
ndivyo anavyozidi kuwa stadi. Kabla ya
hili, Alvin alilazimika kusafisha uchafu
wake. Sasa, anaweza kushughulikia
mambo peke yake vizuri hivi kwamba
hatahitaji hata msaada.”
"Kwa hiyo tutamwacha tu?" Pamela

aliuliza bila kuridhika.
"Tutaenda naye polepole. Lakini...
sitaweza kuishi vizuri hadi niwalipe.”
Lisa alimkabidhi Lucas kwa Pamela.
“Natoka nje mara moja, mtazame.”
“Mama, unaenda wapi?” Lucas aliuliza
kwa wasiwasi.
“Naenda kununua kifungua kinywa.
Nitarudi hivi karibuni. Mwangalie dada
yako kwa sasa.” Lisa alitoka hospitali
baada ya kumtuliza Lucas.
•••
8:00 asubuhi, katika jumba lake la
kifahari, baada ya Alvin kumaliza
kifungua kinywa, Sarah alitabasamu
kwa upole na kusema, “Kwa kuwa bado
ni mapema, unaweza kunisindikiza
hospitalini? Nahitaji kuchoma sindano."

Siku hizo, Sarah ilibidi atembelee
hospitali mara nyingi sana kuchoma
sindano ya kuchochea mwili ili aweze
kufanikiwa matibabu ya In vitro
Fertilization (IVF), au upandikizaji wa
mimba kwa njia ya matibabu.
Aliposikia ombi lake, Alvin aligeuka na
kumkazia macho yake magumu. “Kwa
kweli, hakuna haraka ya sisi kupata
mimba. Kwa kuwa bado ni
vijana, hatujachelewa kufanya hivyo
baada ya kufunga ndoa.”
“Alvinic, mimi si kijana tena. Ninataka
kuwa na watoto haraka iwezekanavyo
na kujenga familia na wewe. Siogopi
maumivu. Sijali kuteseka kwa ajili yako,”
Sarah alijibu kwa upole huku
akiizungusha mikono yake shingoni.
"Sawa, nitakupeleka huko." Alvin

aliinamisha macho chini kwa kuomba
msamaha. Ikiwa sio kwa sababu
hakuweza kufanya naye mapenzi,
asingelazimika kwenda kwenye shida
zote za kupitia IVF.
Lisa alikuwa sahihi kwa kusema
kwamba uzazi kwa njia ya IVF
kuliwaweka wanawake katika hali
mbaya.
Gari ilipowashwa tu na kuelekea nje ya
geti, ghafla gari aina ya SUV ilipita
kwenye geti la chuma na kuelekea
kwenye gari la Alvin.
Alvin aligeuza usukani kwa haraka ili
kulikwepa. SUV ilielekea kwenye maua
na kugonga kwenye dirisha la nyumba.
Baadaye, vioo vilivunjika na vipande
kutawanyika ardhini.
Lisa alifungua mlango kwa teke. Akiwa

amevaa jozi ya buti za Dk. Martens na
jeans, aliruka kutoka kwenye SUV kwa
macho ya kutisha.
Alvin alimkazia macho, huku Sarah
akiiweka mikono yake kiunoni huku
akitetemeka. Alionekana kuwa na hofu.
“Anapanga kufanya nini Alvinic? Hii
inatisha. Karibu atugonge.”
Alvin alifungua mlango kwa huzuni na
kutoka nje ya gari. Kuona fujo pale uani,
aliruka kwa hasira. "Lisa Jones,
unatamani kifo mapema asubuhi?
Nimetosha na vitimbi vyako sasa.”
“Mimi pi nimechoshwa na nyinyi wawili
pia.” Lisa akamsogelea taratibu huku
macho yake yakionyesha hasira.
“Kwanini sikufaulu kuwaua ninyi wenzi
wasio na aibu sasa hivi?”

“Wewe ni mgonjwa! Nenda ukachukue
dawa yako.” Alvin alimtazama Lisa kana
kwamba ni kichaa.
Sarah alishuka kwenye gari na
kumshauri Lisa kwa huzuni, “Tulia Lisa.
Najua habari za ndoa yangu na Alvin
labda zimekuchanganya, lakini
unachofanya sasa ni kinyume cha
sheria. Nimepiga simu polisi hivi punde.”
Alvin alishikwa na butwaa. Kisha, Sarah
akaeleza bila kujali, “Ameenda mbali
sana wakati huu. Umeona uharibu
kwenye ua wetu? Kwa bahati nzuri,
hakuna mtu aliyegongwa. Ikiwa
hatutamfundisha somo sasa hivi,
atafanya ujinga wa kiwango kikubwa
wakati ujao.”
Alvin alinyamaza kwa muda. Alijua
kwamba Lisa alikuwa bado anampenda,

lakini tabia yake ya ukichaa ilimtia hofu
sana. Aliona hitaji la kumfundisha somo
pia.
Akiwatazama wawili hao, Lisa
alidhihaki. “Acha kuwaza mambo kupita
kiasi. Nilikuja hapa sio kwa sababu nina
wivu na ndoa yako. Ninataka kukuonya
kwamba hasira yangu ina mipaka yake. Sarah Langa, bora uendelee kumkanya
Thomas. Watu wachache waliingia
ndani ya nyumba yangu na kuvunja vitu
vyangu jana usiku. Ni Thomas tu ndiye
aliyewatuma.”
“Kwanini umsingizie kaka yangu, una
ushahidi?” Sarah alichukia.
"Pamela alimuumbua Thomas mbele ya
vyombo vya habari wakati wa mchana
na tukio la uvamizi lilifanyika nyumbani
kwangu usiku huo huo. Inawezaje kuwa

bahati mbaya?” Lisa alifoka. “Ijapokuwa
wale watu ambao wamekamatwa kwa
kuingia ndani ya nyumba yangu ni
wahuni tu, aliyewaelekeza atakuwa ni
Thomas. Haiwezi kuwa mtu mwingine
yeyote.”
Uso wa Alvin ulibadilika kidogo. Hapo
ndipo alipoona sura ya Lisa iliyopauka
na macho yaliyovimba. Ilionekana kuwa
hakuwa amelala jana yake usiku.
"Ni Thomas ndiye amefanya?" Alvin
akageuza kichwa chake na kumtazama
Sarah kwa ukali.
“Hapana... Hapana.” Bila kujua lolote
kuhusu jambo hilo, Sarah alianza
kuingiwa na hofu. “Nilimpigia simu kaka
yangu jana. Alisema kuwa hatajali
maneno ya Pamela na hatamletea
shida. Lisa, nadhani umewaudhi watu

wengine. Huwezi kumlaumu ndugu
yangu kwa sababu tu unanichukia.”
“Sihitaji kukukumbusha jinsi Thomas
alivyo na jeuri ya kijinga, sivyo? Miaka
minne iliyopita, tayari alikuwa na ujasiri
wa kutosha kuingia ndani ya nyumba ya
Pamela na kutaka kumbaka. Licha ya
kujua kuwa nilikuwa mjamzito wakati
huo, alithubutu kunisukuma! Zaidi ya
hayo, dada yake ataolewa katika familia
ya Kimaro hivi karibuni. Angeogopa
kufanya nini?"
Lisa alimtazama Alvin kwa hasira.
"Endelea kumtetea Thomas milele. Kwa
sababu yake, sifa yako itaharibiwa
mapema au baadaye. Kila mtu
atachukizwa na jinsi unavyomsaidia na
kumsaidia.”
Sura ya: 369

Alvin alishtuka na kujikuta anakunja
ngumi bila kujijua. Aliongeza sauti yake
na kuuliza, “Thomas alikusukuma miaka
mitatu iliyopita?”
“Hata kama angefanya hivyo?
Ungejali? Pia alimpiga rafiki yangu na
kujaribu kumsumbua, lakini uliamua
kunitisha na baba yangu kwa ajili ya
mwanamke huyu. Baada ya miaka
mingi sana, hujisikii kuwa na hatia
kuhusu hilo, Alvin? Naam, sidhani kama
unafanya hivyo kwa sababu wewe si
tofauti na Thomas. Nyinyi wawili ni
mashetani katili tu.”
Ikiwa Alvin asingemsaidia Thomas tena
na tena, Thomas angekuwaje na ujasiri
wa kufanya jambo kama hilo sasa na
hatimaye kumuumiza Suzie? Alipofikiria
jinsi mtoto wake alivyokuwa na
uchungu, macho ya Lisa yalibadilika na

kuwa mekundu. Hakuweza kujizuia
kutetemeka pia.
“Wewe endelea tu kumtetea Thomas.
Jana aliharibu nyumba yangu, na mimi
leo nimeharibu mahali pako. Akimuua
rafiki yangu kesho, nitaondoa uhai
wako!” Macho ya Lisa yalijaa chuki.
Ndani ya moyo wake, Alvin alihisi hasira
sana bila sababu za msingi.
Hakupenda jinsi Lisa alivyomchukia.
Hata hakupenda sura yake ya machozi.
Punde, polisi walifika. "Bwana Kimaro,
ni yeye ndiye aliyeingia nyumbani
kwako na kufanya fujo?" Polisi
walitembea kuelekea kwa Lisa.
"Achana naye. Sitafuatilia suala hili,”
Alvin alijibu ghafla.

"Alvini." Sarah aliuma mdomo. "Yeye
karibu -"
"Nimesema kwamba sitafuatilia suala
hilo, basi!" Alvin aligeuka na kuingia
ndani ya gari bila kujishughulisha
kumtazama Sarah. Muda si mrefu
aliendesha gari na kuondoka.
"Alvini." Sara kadiri alivyozidi
kumkimbilia, ndivyo alivyozidi kuachwa
nyuma. Alvin alisahau kabisa kuhusu
ahadi yake ya kuongozana naye hadi
hospitali kwa ajili ya sindano.
“Unajisikiaje sasa kwamba
mwanamume wako mpendwa
anakuacha kama hakujui?” Sauti ya
Lisa isiyojali ilisikika masikioni mwa
Sarah.
Sarah aligeuka na kumtazama Lisa.
Jinsi alivyochukia alitamani kumpasua.

Sarah mara akajivuta. "Lisa Jones,
usiwe na majivuno. Alvin
amechanganyikiwa tu na vurugu zako.
Isitoshe, ulikuwa ukimshtaki tu Thomas
bila ushahidi wowote.”
Ikiwa Lisa angekuwa na ushahidi wa
kitendo cha Thomas, asingeenda pale
kuzua fujo. Badala yake, angemshataki
Thomas polisi moja kwa moja. Wakati
huo, Thomas hakuwa amemwomba
Sarah msaada. Ilimaanisha kwamba
alikuwa amejiandaa vya kutosha hata
Lisa asingeweza kumfanya chochote.
“Ndio, sina ushahidi, lakini hiyo
haimaanishi kwamba Alvin
hatalichunguza. Kwa vile ni kaka yako,
unadhani Alvin hatamshuku?
Sarah Langa, unaweza kumlaghai Alvin
ili akubaliane nawe, lakini huwezi

kubadilisha tabia yake kwa mbinu
potofu ya hypnosis. Yeye si mtu mbaya,
lakini kwa sababu yako, analazimika
kumvumilia Thomas tena na tena. Mara
moja au mbili ni sawa, lakini wakati
anaharibu zaidi na zaidi, watu wengi
huko nje wataanza kumkosoa Alvin kwa
kumsaidia na kumsaidia Thomas.
Unafikiri Alvin atafanya nini wakati
huo?” Lisa alipomaliza kuongea, uso wa
Sarah ukaanguka. "
Lisa alikunja midomo yake juu na
kuangaza huku na huko. “Pia, jumba hili
lilikuwa la Alvin na nyumbani kwangu.
Uliiba mahali pangu na hata unatumia
kitanda nilicholalia. Huoni aibu?”
Kwa hayo, Lisa moja kwa moja
alielekea kwenye gari lake bila
kuangalia sura mbaya ya Sarah.
Aligeuka na kuondoka.

Sara alikata tamaa kabisa. Muda
kidogo, akatoa simu yake na kumpigia
Thomas. "Ulituma watu waharibu
nyumba ya Lisa?"
"Hapana, niliwatuma kwa Pamela,"
Thomas alijibu kwa majivuno.
Sarah alipoteza utulivu wake. "Pamela
sasa anakaa kwa Lisa, kwa hivyo
uliharibu nyumba ya Lisa! Asubuhi ya
leo, Lisa alikuja hapa kuanzisha
ugomvi."
“Anathubutuje kuja huko?! Shemeji
atashughulika naye, sawa?" Thomas
aliongeza bila kujali, “Usijali. Mimi siwezi
kuingia matatizoni. Wale watu
nilowatuma kuchafua mahali hapo
wameshakamatwa kwa wizi. Polisi
watawachukulia tu kama wezi na
hawatanishuku. Zaidi ya hayo,

nimewapa pesa kimyakimya, kwa hivyo
watafanya siri.”
Sarah alishusha pumzi ndefu na
kuuliza, “Umewapaje pesa hizo za
kimyakimya?”
"Nilimwambia msaidizi wangu
kuihamisha pesa kwenye akaunti za
benki za familia zao."
Wakati huo, Sarah alikuwa akihema
kwa hasira. "Kumbe wewe ni boya?
Alvin anaweza kugundulika kwa urahisi
ikiwa atachunguza.”
"Shemeji atachunguzaje suala hili?"
Thomas alishangaa. “Unaweza
kuzungumza naye na kumshawishi.
Kama shemeji yake, mimi sio muhimu
kuliko Lisa?"

"Lisa alikuja hapa na kuongea mengi,
na zaidi ya hayo, Alvin bado ana hisia
kwake. Kama ndugu yangu, unaweza
kuacha kuwa mzigo kwangu? Siku zote
nimekuwa nikikuambia kuwa unaweza
kufanya chochote unachopenda baada
ya ndoa yangu kupita. Kwanini huwezi
kungoja?” Sarah alikazia macho baada
ya kukata simu.
Walisema wachezaji wasio na uwezo
wanaweza kuharibu timu.
Ijapokuwa Thomas alikuwa kaka yake
wa tumbo moja, angejikuta katika
matatizo makubwa mapema au
baadaye ikiwa angeendelea
kusababisha matatizo. Labda ulikuwa
wakati wa kuachana naye?
Baada ya kuondoka nyumbani, Alvin
alimpigia Hans. "Nenda ukaangalie ni
nini hasa kilitokea nyumbani kwa Lisa

jana usiku."
Kwa vile Hans alikuwa na mtu
anayefahamiana naye ambaye alifanya
kazi katika kituo cha polisi, alipata
habari hizo katika muda usiozidi dakika
kumi.
“Bwana Kimaro, wanaume wanne
walivamia nyumba ya Miss Jones
mwendo wa saa nne usiku wa jana.
Kwa bahati nzuri, Bi Jones alikuwa
hospitalini wakati huo kwani shinikizo la
damu la Joel lilikuwa limeongezeka.
Vinginevyo, angekutana na watu hao
wa kutisha... Nilisikia wanaume hao ni
wakatili ambao kila mara wanahusika
katika ujambazi na wizi.” Hans
alisimama ghafla katika hotuba yake.
Moyo wa Alvin ulishuka. Hata kama Lisa
angekuwa na ujuzi fulani wa kimsingi

wa kupigana, labda asingeweza
kuwashinda wanaume hao wanne
wakatili. Angekabiliwa na wanaume hao
wanne usiku, mwanamke mrembo
asingeweza kuwashinda. Anaweza hata
kubakwa!
Alvin bila fahamu akakaza mikono yake
kwenye usukani. "Kuna maeneo nyeti
katika kitongoji hicho. Ulinzi wa eneo
hilo ni mkali, kwa hiyo walithubutuje
kuingia ndani ya nyumba na kuiba vitu
saa nne usiku?"
"Ndio, hii ni kesi ya kwanza nzito
ambayo imetokea huko. Polisi
wamewakamata wahalifu hao wanne.
Wahalifu hao walidai kwamba walisikia
Miss Jones ndiye mrithi wa Ngosha
Corporation na walidhani yeye ni tajiri,
kwa hivyo walikwenda huko kutafuta
vitu vya thamani.

“Hata hivyo, ni mara yangu ya kwanza
kusikia wezi wakivunja kila kitu ndani ya
nyumba. Walivunja kila kitu
kilichoonekana hadi nyumba ikakosa
kutambulika. Haifai hata kwa binadamu
kukaa hapo sasa. Inaonekana walikuwa
wakilipiza kisasi.”
Alvin akasugua kichwa chake. Baada ya
muda, alisema kwa ukali, "Nenda
ukachunguze ikiwa tukio hili linahusiana
na Thomas."
Saa moja baadaye, Alvin alipokea
taarifa kutoka kwa Hans alipokuwa
ofisini. “Msaidizi wa 'Thomas'
alihamisha pesa kwa wanafamilia
wanne wa watuhumiwa waliokubali
kumlinda. Kila mmoja wao alipokea
shilingi milioni moja za Kenya.”
Alipomaliza tu sentensi hiyo, Alvin

aliyekuwa ameketi kwenye kiti cha ngozi
aligeuka na kurusha faili alilokuwa nalo.
“Hans, unafikiri... ninamdekeza Thomas sana eeh?” Uso mzuri wa Alvin uligeuka
kuwa mbaya, na mdomo wake ulipinda
na kuwa tabasamu la huzuni.
Hans alishindwa cha kusema. Sio tu
kwamba Alvin alikuwa akimtendea
Thomas kwa ukarimu sana, lakini pia
alikuwa ameenda hadi kuvuka msingi
wa maadili. Hata hivyo, Hans
alimkumbusha Alvin kwa tahadhari, "Ni
kwa sababu huwezi kuvumilia kuona Bi
Njau akiwa amekasirika, sivyo?"
Sura ya: 370
Sura ya huzuni ikaangaza machoni
mwa Alvin. Aliinamisha kichwa chini na

kufikiria. Hakika, alikuwa akifanya kila
kitu kwa ajili ya Sara. Miaka mitatu
iliyopita, hakutaka kumwokoa Thomas,
lakini alifanya hivyo dhidi ya dhamiri
yake kwa sababu ya Sarah. Hii ndiyo
sababu Lisa alikuwa amemwekea
kinyongo. Hatimaye, alipoteza watoto
wake, yote kwa sababu ya mipango
yake. Wakati fulani uliopita, Alvin hata
alipinga kesi dhidi ya dhamiri yake ili
kumuokoa Thomas aliyeharibu maisha
ya binti asiye na hatia. Lakini nini
matokeo yake? Badala ya Thomas
kubadili tabia yake, alizidi kuwa na
ujasiri na matendo yake maovu.
Alvin ghafla aliibuka kutoka kwenye lindi
la mawazo na kusema. "Peleka ushahidi
kwa polisi,"
Hans alipigwa na butwaa kwa muda.
"Lakini ikiwa Bi Njau atagundua-"

“Ikiwa atakuja kuniona kwa sababu ya
jambo hili, usimruhusu aingie. Alvin
aligeuka kwenye kiti chake cha ngozi na
kutazama nje ya dirisha.
“Sawa.” Hans aliitikia kwa kichwa na
hatimaye akahisi ahueni. Hatimaye,
dhamiri ya Bwana Mkubwa wake ilikuwa
inaamshwa polepole.
•••
Thomas alikuwa amemkumbatia
sekretari ofisini kwake tayari kumfanyia
jambo fulani. Mfanyakazi mmoja aliingia
ghafla kwa wasiwasi. “ Bwana Njau.
Msaidizi wako alichukuliwa na polisi
sasa hivi."
Thomas aliinuka mara moja, na
sekretari aliyefadhaika mikononi mwake
akaanguka chini. Kwa wakati huo,

hakuwa hata na wasiwasi juu yake.
Haraka akatoka nje na kupiga namba ya
Sarah. “Dada kuna tatizo.
Msaidizi wangu amechukuliwa na
polisi.”
“Kwanini unaogopa? Hukumkumbusha
Msaidizi wako yale niliyokuambia?"
“Nilifanya..."
“Usiwe na wasiwasi basi. Bila kujali ni
kiasi gani unamlipa, hakikisha tu
midomo yake imefungwa. Pia, afadhali
ujirekebishe kuanzia sasa au sitaweza
kukuokoa.” Sarah alichukia sana mara
baada ya kukata simu.
•••
Hospitalini, Lisa alipokuwa akimlisha
Suzie uji mikononi mwake, Pamela
alipokea simu.

Baada ya hapo, Pamela alisema, "Kuna
habari njema na mbaya. Habari njema
ni kwamba polisi walipiga simu na
kuniambia kuwa kuna
ushahidi unaoonyesha kuwa wezi hao
walikodiwa na mtu mwingine. Ni
msaidizi wa Thomas ambaye
alihamisha pesa kwa wanafamilia wao.”
Lisa aliinua kichwa chake na kusema,
"Kuhusu habari mbaya, msaidizi wa
Thomas amekiri kosa hilo?"
“Ndiyo! Ina maana kwamba Thomas
bado ametoroka kwenye kitanzi tena,”
Pamela alipumua. “Lakini unajua ni
nani aliyewasilisha ushahidi kwa polisi?
Ni Alvin! Ulimfanya nini asubuhi hii?”
“Nilimpaka dawa machoni. Nadhani
anaona vizuri sasa.” Ndani ya moyo

wake, Lisa alishusha pumzi.
Kwa kweli, alikuwa amecheza kamari
kwa kwenda huko asubuhi ya siku hiyo
ili kuanzisha fujo. Aliweka dau kwamba
Alvin bado alikuwa na hisia kwake na
asingeweza tena kuvumilia tabia ya
Thomas. Alikwenda kwake na
kumkumbusha kwamba Thomas
alihusika moja kwa moja kwa kupoteza
watoto wao miaka minne iliyopita. Kwa
bahati nzuri, alishinda Kamari yake!
"Wewe ni noma!" Pamela aliinua kidole
gumba.
“Godmother, mdomo wako uliumwa na
mbu? Umevimba.” Suzie ambaye
alikuwa akinywa uji huku akiwa
amejilaza kwenye mikono ya Lisa,
aliinamisha kichwa chake na
kumtazama Pamela kwa udadisi.

Pamela mara moja aliona aibu. "Mbwa
aliniuma."
"Lazima mbwa atakuwa mrefu kwani
anaweza kuuma mdomo wako," Suzie
alisema kwa tabasamu.
Pamela alimtazama Suzie kwa
mshangao huku mikono yake ikiwa
kiunoni. “Kwa kuwa unaweza
kunidhihaki, maana yake ni mzima.
Lakini ulikuwa unalia na kuomba
kukumbatiwa na peremende kwa mama
yako sasa hivi.”
Suzie alipiga kelele na kujipenyeza
kwenye mikono ya Lisa tena. "Mama,
inauma tena."
“Uliumia vibaya sana wakati huu
mwanangu. Acha nikubusu." Ni baada

tu ya Lisa kumkumbatia na kumbusu
kwenye shavu ndipo mtoto mdogo yule
alitabasamu kwa uchangamfu. Baada
ya yote, kichwa chake kilijeruhiwa
vibaya. Baada ya kunywa uji, Suzie
alihisi kusinzia.
Siku chache zilizofuata, Pamela alikuwa
na shughuli nyingi akimsaidia Lisa
kusafisha nyumba yake huku Lisa
akimhudumia Suzie hospitalini. Akiwa
na kazi nyingi sana, kwa kawaida
alifanya kazi huku akimtunza Suzie.
Lucas alikaa wodini kwa siku hizi tatu
bila kutoka nje. Alihisi ndiye
aliyesababisha majeraha ya Suzie.
Jack aliwatembelea tena usiku moja
usiku. Jack aliyabana mashavu ya
Suzie taratibu na kusema. “Suzie, ngoja
nikusindikize usiku huu, sawa? Mwache

mama naye akapumzike nyumbani.”
“Hakika, hakika. Ninakupenda zaidi,
Mjomba Jack. Suzie alimuonea huruma
mama yake pia. Mara moja akasema,
“Mama, unaweza kumpeleka kaka
nyumbani kwanza. Wacha nilale na
Uncle Jack.”
“Yeye ni mwanangu hata hivyo. Hakika
nitamtazama kwa makini.” Jack alimtoa
wasiwasi Lisa.
"Sawa." Lisa aliitikia kwa kichwa huku
akielewa nia ya bintiye. "Nitakuletea
chakula kizuri kesho."
Lisa alipoondoka na Lucas, alimuona
Jack akicheka na Suzie ambaye
alionekana kufurahihi. Hakuweza
kujizuia kukumbuka wakati Suzie
alipozaliwa tu. Siku zote Suzie alikuwa

akilia na hakupenda mtu mwingine
yeyote kumbeba isipokuwa Lisa. Hata
hivyo, Jack alipoenda kuwatembelea,
Suzie alikubali Jack kumbeba, na wala
hakulia. Pia Suzie alifurahia kuwa karibu
na Jack hasa. Ndiyo maana Lisa
alimuacha naye kwa moyo mweupe.
Pengine huu ulikuwa ni mfano wa
msemo 'damu ni nzito kuliko maji', au
pengine, ni kwa sababu Jack alikuwa na
mfanano wa kupita kiasi na Alvin. Mtoto
angeweza kuhisi.
Suzie alipokuwa mikononi mwa Jack
usiku, alimnong’oneza kwa ghafla,
“Anko Jack, baba yangu mchafu ana
upendo kama wewe anapokuwa na
watoto?”
Jack alipigwa na butwaa. Alipomwona
mtoto huyo mrembo ambaye uso wake
ulikuwa umepauka kwa sababu ya

majeraha yake, hakuweza kujizuia
kusema, “Kama yeye akimuona
mrembo kama wewe, hakika atakuwa
rafiki yako. Je! unatamani kuwa na ...
baba?"
"Sijui." Ghafla, Suzie alipiga kelele huku
macho yake yakiwa mekundu. "Watu
wale walipoingia usiku huo, niliogopa
sana. Nilikuwa nikifikiria... ingekuwa
vizuri kama nini ikiwa Baba alikuwa
karibu, lakini sikumwambia Mama
kuhusu hilo. Niliogopa angekasirika.”
"Wewe ni mtoto mzuri sana, Suzie."
Jack akashusha pumzi ndefu.
Alvin lazima awe amepigwa na laana.
Ikiwa Jack angekuwa na mtoto mzuri
kama huyo, bila shaka angemlea kama
binti wa kifalme. “Kama kuna chochote,
unaweza kunitafuta. Nichukulie tu kama
baba yako, sawa mtoto mzuri?”

“Sawa.” Suzie alilala taratibu huku
akimuegemea Jack.
Asubuhi iliyofuata, muuguzi
alimkumbusha Jack ampeleka Suzie
kwenye ghorofa ya nne kwa uchunguzi
wa ubongo wa CT ifikapo saa mbili
asubuhi.
Jack alimvalisha Suzie barakoa yake
vizuri kama alivyoagizwa na Lisa
walipokuwa wakitembea kwenda huko.
Lakini, Suzie alivua kinyago chake mara
tu alipoingia kwenye chumba cha CT.
Mara tu uchunguzi wa CT scan
ulipofanywa, Suzie alitoka akiwa
hajavaa barakoa yake. Mtu fulani
alimgonga Jack mgongoni kabla
hajamvisha Suzie barakoa.
Alipogeuka, Bibi Kimaro alikuwa

akimwangalia Suzie kwa mshangao.
"Jack, huyu ni mtoto wa nani?”
Akiwa amepigwa na bumbuwazi
moyoni, Jack aligugumia, “Bibi, kwanini
uko hapa?”
“Nakuuliza huyu ni mtoto wa nani.” Bibi
Kimaro alikuwa na wasiwasi sana hivi
kwamba alivuta sikio lake moja kwa
moja.
“Yeye... Ni mtoto wa rafiki yangu.” Mara
tu Jack alipomaliza kuzungumza, Bibi
Kimaro alimpiga kofi. “Unathubutu vipi
kunidanganya?! Unafikiri macho yangu
yamekufa, huh? Angalia jinsi
mnavyofanana. Je, ni binti yako wa
haramu?”
Jack alishtuka sana hivi kwamba sura

ya kutokuamini iliosha uso wake.
“Hapana, mimi...”
TUKUTANE KURASA 371-375
ONYO: Ni marufuku kusambaza, kukopi wala kuuza kazi hii kwani endapo kama tutakubaini basi sheria itachukua mkondo wake (By: Official Dully)
 
Mkuu tunashukuru kwa simulizi nzuri lakini hiki kipande cha mwisho ni kama umerudia
kukituma
 
Hii story hata kama ni fiction tu lakini inagusa uhalisia wa lifestyle ya jamii flani ktk ulimwengu huu.
 
Back
Top Bottom