LISA KITABU CHA NANE (8) SIMULIZI........................LISA KURASA..................361 - 365
PRESENT: SIMULIZI ZA DULLY
Sura ya: 361
Jua la mchana la uvivu liliangaza kutoka dirishani na kuangukia kwenye sura nzuri ya Lisa.
Akainama kutazama simu yake na kutabasamu kwa upole. Hata sauti yake ilikuwa laini. “Kwa hiyo mtashukia Dar es Salaam?”
"Ndiyo mpenzi, nimepata ndege ya moja kwa moja." Pamela alijibu upande wa pili wa simu. “Unaweza kutusubiri Nairobi. Sitakaa sana Dar, ni siku moja au mbili tu.”
“Hapana. Nitaenda kuwapokelea Dar, ni siku nyingi hata hivyo sijaenda kwenye jiji la nyumbani.” Lisa alinyamaza na kuinua kichwa chake, akionekana kuwa
katika hali nzuri. “Msafiri salama, utawapa hai hao malaika wangu.”
•••
Ndege kutoka Marekani ilitua kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere International Airport, majira ya saa tatu usiku. Lisa alisubiri kwa zaidi ya dakika kumi kabla ya kumuona Pamela akitoka akiwa na wapenzi wake wawili.
Lucas alikuwa amevaa shati la rangi ya bluu la mtindo wa Kiingereza. Ingawa mwili wake ulikuwa mdogo, sura yake ndogo iliyopendeza kupita kiasi iliwafanya watu waliokuwa wakipita hapo kumtazama.
Kwa upande wa Suzie alikuwa amekaa juu ya sanduku alilokuwa akiburuta Pamela. Mabutu yake mawili ya nywele kichwani yaliyumbayumba kwa
kupendeza. Watoto hao wawili walipomwona Lisa, walifurahi sana. Suzie aliruka chini mara moja kutoka kwenye sanduku na kumkimbilia kwa furaha.
“Mama, mama...”Suzie akaruka mikononi mwake mara moja, na kumganda mama yake kama luba.
Moyo mdogo wa Lisa ulilainika na machozi yalikaribia kumtoka. Tangu wazaliwe, hakuwahi kutenganishwa na watoto hao wawili kwa muda mrefu.
“Mama.” Lucas alijizuia zaidi, lakini macho yake pia yakawa na machozi.
"Sweetie, njoo hapa." Lisa alinyoosha mikono yake na kuwakumbatia.
"Jamani, ni bora kuwa na watoto wangu
wa kuzaa mwenyewe. Yaani mlipomwona mama yenu tu mimi tena basi,” Pamela alitania, “Mimi nawanunulia peremende kila siku lakini mnanisahau mara tu mnapomwona mama yenu.”
Suzie aliukunja mabega yake. “Godmother, fanya haraka na wewe uzae watoto tupate kaka na dada mdogo.”
“Asante kwa baraka.” Pamela alipiga kelele.
Lisa alisimama na kutabasamu. “Pole kwa safari na karibu tena nyumbani. Nimewaandalia chakula kitamu sana cha jioni. Nisingekuwa na watoto tungeanzia bar”
Pamela akacheka. "Hakika, twende."
Pamela alipokuwa anataka kuondoka ghafla sauti ya mshangao ikasikika nyuma yao.
“Pamela, ni wewe?” Ingawa ilikuwa imepita miaka mitatu, bado aliikumbuka vyema sauti hiyo.
Pamela aligeuka na kuwaona Patrick na Linda wakitoka nje ya geti.
Baada ya kutengana kwa miaka mitatu, Patrick alionekana mtu mzima zaidi na alionekana mpole kuliko hapo awali.
Kwa upande wa Linda, hakuwa amebadilika sana. Alikuwa amevaa tisheti nyeupe na sketi iliyofika magotini. Mikono yake miwili ilikuwa imeuzunguka mkono wa Patrick kiundani. Ilikuwa wazi kwamba walikuwa wapenzi.
Hata hivyo, Patrick alionekana
kumsahau Linda aliyekuwa pembeni yake na kumtazama tu Pamela bila kupepesa macho. Jeans yake ya rangi ya blue mpauko ilifafanua vyema miguu yake minene iliyonyooka, na mwili wake wa juu ulifunikwa na fulana nyepesi ya kijivu. Shati la drafti lilikuwa limefungwa kwenye fundo kwenye kiuno chake, likifunua kiuno chake kidogo.
Ngozi yake ilizidi kung’aa kwa weupe wa asili na nywele zake zilikusanywa nyuma ya kisogo na kufungwa kufichua mashavu yake yenye dimpozi. Macho yake yalikuwa makubwa na yenye kung’aa, yalimfanya aonekane mtu wa makabila mchanganyiko. Miaka mitatu ilikuwa imeacha alama kwenye uso wake, lakini ilimfanya kuwa kijana zaidi na mrembo.
Patrick alionekana kusahau mpaka
kupumua. Kando yake, Linda alisema kwa mshangao, “Pamela, ni wewe kweli. Umerudi? Tulikuwa na wasiwasi sana juu yako wakati huo tulipoona picha na video zako chafu mtandaoni. Uko salama?"
Patrick aliganda. Ndio, sasa alikumbuka. Miaka mitatu iliyopita, kulikuwa na habari kwamba Pamela alijirahisisha kwa Thomas Njau. Kisha Thomas alimfanyia mambo ya kisodoma na kurekodi video ambayo aliisambaza mtandaoni kwa watu kuona. Japo video hiyo haikuwa na uthibitisho wa kutosha kwamba aliyekuwa akifanyiwa kitendo hicho ni Pamela, teknolojia ilifanya kazi yake na kuuaminisha umma kuwa mwanamke huyo alikuwa ni Pamela. Habari chafu mara nyingi husambaa haraka, ndiyo maana tukio hilo la Pamela lilienea kwa kasi.
Muda mfupi baadaye, kulikuwa na habari kwamba alienda ng’ambo ili kukwepa aibu iliyomkuta. Macho ya Patrick ghafla yalijawa na karaha na tamaa.
Pamela kiasili hakuonyesha mabadiliko yoyote machoni mwake, akacheka tu na kusema. “Linda, unanipaka chumvi kwenye vidonda vyangu mara tu unaponiona, kwani hakuna habari nzuri za kuongelea hadi ukumbushie tukio baya kama hilo? Bado wewe ni wa ajabu tu kama zamani."
Sura ya Linda ilibadilika kidogo huku akijifanya ameziba mdomo kujionyesha kuwa amejawa na hatia. "Samahani-"
“Usiombe msamaha,” Patrick alisema kwa upole, “Kwa kuwa ulithubutu
kufanya mambo kama hayo, kwanini unachukia yakiongelewa na wengine?”
Pamela aliinamisha kichwa chake. Huyu ndiye mwanaume ambaye hapo awali alikuwa akimpenda sana. Lakini, kwa sababu tu ya habari za uwongo, angeamini uwongo wa Thomas kuliko yeye.
Lisa hakuweza kujizuia. “Patrick Jackson, Pamela alikuwa nawe kwa muda mrefu lakini bado humfahamu vya kutosha?”
“Namfahamu vizuri sana.” Patrick alisema kwa dharau. “Nilipokuja kumtafuta mara ya kwanza huko Nairobi, alimbusu mwanaume mwingine hadharani tena mbele yangu. Ni wazi kwamba mtindo wake wa maisha umekuwa mchafu baada ya kufika
huko.”
"Patrick, usiseme hivyo." Linda akahema. "Pamela huenda alikuwa akijaribu kukukomoa wakati huo. Thomas Njau ni Mkurugenzi wa Kampuni kubwa tu, hata hivyo. Huenda alikuwa akijaribu kutafuta mtu aliye na hadhi ya juu ili akuonyeshe, lakini iliishia... kumrudisha nyuma. Hata hivyo, Pamela, nataka kukukumbusha. Wakati mwingine unapotafuta mwanamume, bado unapaswa kuzingatia tabia yake.”
Pamela alitumbua macho kwa kuchukia. “Uko sahihi. Sikuangalia tabia ya mtu wakati wa kupata mpenzi wangu wa kwanza. Wakati huo, nilisema kwamba rafiki yake wa utotoni ambaye aliendelea kumsumbua alivutiwa naye, lakini hakuniamini. Tazama sasa. Kwa
kweli waliishia kuwa wapenzi."
Uso wa Linda ulijawa na aibu, akamtazama Patrick ambaye naye alikosa cha kusema.
Pamela aliinama chini na kusema, “Nilimwambia mpenzi wangu huyo wa kwanza kuhusu hilo lakini alinilaumu na kusema hakuna kinachoendelea. Sasa nikifikiria juu yake, kwa kweli najilaumui sana. Nilipaswa kuondoka mapema. Badala yake, niliishia kuchelewesha uhusiano wa kimapenzi wa mtu fulani kwa miaka mingi sana. Mimi ni mjinga sana."
Rangi kwenye nyuso za Patrick na Linda zilibadilika mfululizo.
Linda aliuma mdomo wake na kusema kwa hatia, “Pamela, umeelewa vibaya. Amini usiamini, sikuwa na hisia zozote
na Patrick wakati huo, lakini baada ya wewe kuondoka, nilihisi kwamba alikuwa na huzuni sana. Baadaye, nilipokuwa nikimriwadha, sikuweza kujizuia kumpenda.”
“Huzuni?” Pamela alipigwa na butwaa.
“Ndiyo, nilikuwa na mfadhaiko sana.” Patrick alisema kwa sauti ya chuki. “Nilitapeliwa na mwanamke mnafiki kama wewe kwa miaka mingi sana,”
Pamela alishtuka sana hata ubongo wake ulikuwa umevurugika. "Pia nilikuwa kipofu kabisa kwa kupoteza miaka mingi ya maisha yangu na mtu wa kuchukiza kama wewe. Hapo zamani, nilifikirije kuwa wewe ni mpole na mwenye upendo? Nilikuwa kipofu kabisa.”
Pamela hakuweza kuwa na wasiwasi tena na akamshika mkono Lucas na kuondoka.
"Subiri, huyo ni mtoto wako?" Patrick akatazama kwa udadisi.
Pamela alitaka kukiri kwamba alikuwa mtoto wake, lakini Lucas alizungumza kabla yake, “Yeye ni aunty yangu.”
Linda alisema, “Sijawahi kusikia habari za Forrest kufunga ndoa. Je, ni mwanae wa haramu?”
Sura ya: 362
“Oh jamani, mmesahau? Mtindo wangu wa maisha ni mbaya sana, hivyo ni kawaida kwangu kupata mtoto mmoja au wawili wa haramu,” Pamela alitabasamu na kucheka.
Lakini, uso wa Patrick ulibadilika sana. “Ni kweli ni mwanao wa haramu?”
“Mjinga wewe,” Lucas alimdhihaki, “zaa na wewe wa kwako umwite mtoto haramu, mimi siyo mtoto haramu!”
“Unasemaje wewe mtoto? Nitakufinyaaa!” Patrick alikasirishwa na maneno ya yule mtoto na kukaribia kumshika.
"Jaribu tu kumwekea mkono wako uone." Pamela alishika mkono wake.
Patrick ambaye alikuwa mrefu kuliko yeye alishangazwa na maumivu ya mkono wake. Akamkazia macho Pamela, lakini alimtazama tu kwa dhihaka. Alipatwa na mshtuko kidogo alipokumbuka kwamba alikuwa akimwangalia kila mara kwa
kumwabudu. Moyo wake ulimuuma ghafla.
“Patrick Jackson, natumai kwamba tutakapokutana tena wakati ujao, usithubutu hata kunisalimia. Watu husema kwamba mapenzi ya kwanza ni mazuri, lakini mimi nakuona unachukiza kama nzi.” Pamela aliuachia mkono wake na kuondoka na Lisa.
Walipotoka, Patrick aliendelea kumtazama nyuma. Alimchukia waziwazi, lakini miaka yote hii, hakuwahi kufanikiwa kumfuta moyoni mwake.
“Patrick, uko sawa?” Linda kwa haraka akaja na kumshika mkono huku akimtazama kwa karibu.
"Si chochote." Patrick alikuwa hayupo.
Linda alipomuona hivyo alichukia kwa siri.
Ndani ya gari. Lisa alicheka akisema, "Patrick bado anakupenda sana. Bado aliendelea kukutazama tulipoondoka."
"Kwa hiyo?" Pamela alichungulia dirishani. “Baada ya tukio la Thomas, kila mtu alinisuta na kunisema sana. Huyu mpenzi wangu wa zamani pia alinitumia ujumbe akisema sijiheshimu.”
“Usijali Pamela. Sisi sote tumeteseka kwa kitu kimoja. Sote wawili tulikumbana na wahuni kwenye mapenzi yetu, wewe Linda na mimi ni Sarah” Lisa alilalamika.
“Hakika. Sitarudia tena makosa." Pamela alijipa moyo. Alikataa kuwa na
bahati mbaya hivyo tena.
"Sawa, natumai utakuwa bora kuliko mimi," Lisa alisema kwa dhati.
“Godmother, usijali. Ukishindwa kupata mwanaume mzuri, nikikuwa mkubwa nitakulinda,” Lucas alisema kwa uvivu.
"Lucas wangu ni mtu mtamu sana." Lisa alimkumbatia na kumpiga busu, na kufanya masikio yake kuwa mekundu.
"Mama, mama, na mimi nataka pia." Suzie alimkumbatia na yeye pia akataka busu.
“Kwanza kabla ya yote shosti nimezikumbuka kweli chipsi vumbi za uswazi na nyama za kuku, tuanweza kuzipata wapi sasa hivi?” Pamela aliuliza ghafla.
“Muda wowote unapata, lakini nyumbani nimewandalia chakula cha jioni kitamu sana...” Lisa alimwambia.
“Sawa, tupite uswazi basi nichukue hata vimiguu vya kuku tu kupoza hamu hamu.” Pamela alisisitiza.
Lisa akawapeleka sehemu moja huko Msasani. Hapo palipatikana kila aina ya chakula cha uswahilini, haswa chpisi, mishikaki, nyama za kuku, mihogo na vingine kama hivyo.
Wale watoto wawili walifurahia sana chipsi na nyama za kuku. Walikula na kujilamba hadi matumbo yao yakakosa nafasi kabisa.
Suzie aliinua mdomo wake mdogo mwekundu na uliojaa mafuta, na mkononi akiwa ameshikilia vipapatio
vya kuku vilivyokaangwa, akisema, “Hatimaye ninaelewa kwa nini Godmother huzungumza kila mara kuhusu chakula cha nyumbani, kumbe ni kitamu hivi?”
“Ni kitamu eeh?” Lisa aliuliza akitabasamu kwa bintiye.
“Ni kitamu sana. Sitaki kurudi Marekani tena. Nataka kubaki hapa na kula chipsi na kuku kila siku.” Suzie alisema huku akilazimisha kubugia vipande vya chipsi vilivyojazwa tomato sauce.
“Sawa mwanangu.” Lisa alihisi maumivu ya moyo.
"Sitaki kurudi pia," Lucas alisema kwa uso uliotulia,mdomoni akiwa amerundika minofu ya kuku wa kukaangwa. "Nataka nikae na wewe
nikulinde."
Sauti za watotowale zilimfanya Lisa acheke, lakini akasema kwa uzito, “Hamtaweza kukaa huku mkiwa bado wadogo. Baba yenu akiwajua atawaiba na kuwapeleka mbali na mimi, au nyie mnapenda kwenda kukaa na mama mbaya wa kambo?”
"Ndio," Pamela aliyekuwa busy muda mrefu akifakamia nyama za kuku wa uswazi alisema ghafla, "Mama yenu anawapenda sana, lakini baba yenu ni mhuni, hana huruma kabisa."
Watoto hao wawili waliinamisha vichwa vyao, wote wawili wakiwa kimya kwa muda.
Baada ya kumaliza kula, Lisa aliwapeleka Masaki, mtaa wa Buzwagi
ambako alinunua lile jumba la kifahari la Alvin siku za mwisho kabla hajaondoka kwenda Nairobi. Jumba lilikuwa kubwa na tulivu na muda wote lilikuwa likitunzwa na Jumbe, kijana wa kazi ambaye muda wote aliliweka jumba hilo katika mazingira nadhifu.
Siku inayofuata, Lisa aliamka mapema na kuandaa kifungua kinywa cha kupendeza kwa wapenzi wake wadogo.
"Wapenzi, mama atapumzika pamoja nanyi leo. Baadaye nitawapeleka beach kwenye uwanja wa michezo, sawa?" Lisa alisema kwa upole.
“Sawa.” Suzie akawa na furaha.
"Mama nataka uninunulie mpira." Lucas alisema aliokuwa akichungulia dirishani kwenye bustani kubwa iliyokuwa nje.
"Unavyotaka mwanangu."
Muda huohuo, Pamela alitoka nje ya chumba cha wageni akiwa amevalia nguo za kupendeza. Alijipaka vipodozi vyepesi usoni, na nywele zake ndefu zilishuka mabegani mwake. Alikuwa amevalia viatu vya visigino virefu."
"Watoto wangu, ninaonekana mrembo?" Pamela akasogea kwenye meza ya chakula
Suzie alipiga makofi. “Wewe ni mrembo sana. Wewe ni mzuri kama yule mwanamke anayeimba kwenye tv."
“Ooh! Msichana wangu wewe ni mzuri sana. Nitakuzawadia chokoleti." Pamela alitupa kipande cha chokoleti juu.
Lisa alimtazama Pamela kwa jicho la kumsifia pia na kuchombeza. “Kama usingesema kuwa unaenda kuhudhuria kongamano linalofanywa na SE Group, ningefikiria kuwa unaingia kwenye shindano la urembo.”
"Unajua nini? Nimesubiri wakati huu kwa muda mrefu sana. Tukio la leo ni muhimu sana kwangu kuanza zoezi langu la kulipiza kisasi kwa Rodney Shangwe wa Osher Corporation. Alinifukuza hapo awali, lakini hah! Siwezi kusubiri kuona macho yake ya huzuni na majuto sasa,” Pamela alisema huku kichwa chake kikiwa juu.
“Sawa, fanya haraka kula. Ondoka ukimaliza, usije ukaachwa na ndege.” Lisa alisema huku akizuia kicheko.
“Ni masaa mawili tu kutoka Dar hadi
Nairobi. Mkurugenzi wa SE Group ametuma ndege binafsi kuja kunichukua, sina presha. Kongamano halitakuwa na maana ikiwa mimi sitahudhuria.” Pamela alijigamba.
•••
Katika Jumba la kifahari la Rodney Shangwe.
Baada ya mpishi kutoa kifungua kinywa, msaidizi wa Rodney alimpa ratiba na kusema, “Bwana Shangwe, mwanakemia wa kimataifa wa vipodozi, Nicole, atakuwa akizungumza jukwaani kwa ajili ya kongamano la SE Group saa saba mchana wa leo. Ungependa kwenda? SE Group imetuma mwaliko.”
Rodney alikunja uso na kukoroma. "Huyu jamaa, Bwana Erick Malugu, ameweza kumwalika Nicole?"
“Ndiyo.” Msaidizi akapumua. "Lakini, Nicole ni wa kushangaza sana. Tumemwalika aje Kenya mara nyingi sana lakini amekuwa akikataa kila mara. Nilifikiri kwamba haipendi Kenya, lakini sikutarajia angekubali ghafla kuja wakati SE Group, mpinzani wetu kibiashara, alipomwalika. Osher ipo juu kuliko SE katika kiwango cha hadhi na brand. Watu wenye akili wangechagua kushirikiana nasi badala yake.”
Rodney alikitumbukiza kichwa chake katika mawazo mazito. "Je, Nicole amesaini mkataba wa ushirikiano na SE?"
"Hapana, lakini inasemekana kwamba Nicole anakuja Kenya wakati huu kutia saini mkataba na SE. Nilisikia kwamba ana fomula ya kipodozi cha kuzuia
kasoro za ngozi na kuimarisha ngozi mikononi mwake. Itakuwa shida ikiwa zitanunuliwa na SE. Baada ya yote, bidhaa zilivumbulia na Nicole miaka hii zimekuwa bidhaa maarufu ulimwenguni kote na hadi 80% ya watumiaji wanarudi kununua bidhaa hizo tena.”
Baada ya kuambiwa hayo, Rodney alihisi kuudhika. "Wataalamu wa vipodozi katika kampuni yetu wote hawana maana. Tunawekeza pesa nyingi sana kwao kila mwaka, lakini hawajawahi kufanya chochote cha kuridhisha.”
Msaidizi wake alikunja midomo yake na kusema, “Mkurugenzi wa Idara ya utafiti na maendeleo humsifia kila Pamela Masanja, mwanamke aliyewahi kufanya kazi Osher miaka minne iliyopita. Alikuwa na kipaji kikubwa, lakini inasikitisha kwamba—”
"Nyamaza." Rodney alimtazama msaidizi wake kwa ukali. “Pamela Masanja ni mwanamke asiyefaa. Hakuna kitu cha kusifia juu yake. Wataalamu wa vipodozi kama yeye wanaweza kupatikana kote nchini. Sitaki kumsikia!”
"Hiyo ni sawa. Pamela Masanja hakika hayuko kwenye kiwango sawa na Nicole.” Msaidizi alikubali kwa kichwa alipoona bosi wake akiwaka.
"Hata iweje, hatuwezi kuruhusu Nicole kushirikiana na SE Group." Rodney aliinuka ghafla. “Nipatie hiyo kadi ya mwaliko. Nitaenda kwenye kongamano la SE na kukutana na Nicole mimi mwenyewe. Nikienda kibinafsi, bila shaka atalazimika kunionyesha heshima fulani.”
Sura ya: 363
Katika hoteli ya nyota tano. Sankara Nairobi. Saa sita adhuhuri.
Baada ya Rodney kukabidhi kadi ya mwaliko na kuingia, Bwana Erick Malugu wa SE Group alimkaribisha kwa furaha. “Bwana Shangwe, karibu, karibu sana. Nilijua utakuja leo. Nilisikia kwamba Osher Corporation ilikuwa imemwalika Nicole mara kadhaa lakini siku zote ilikataliwa, kwa hivyo sikuwa na matarajio mengi nilipomwalika. Lakini ni nani aliyejua kwamba angekubali kwa urahisi?”
“Hongera sana, Bwana Malugu." Rodney alitabasamu vibaya. "Lakini
anakuja tu kuhudhuria kongamano, sio kushirikiana na wewe. Usisherehekee haraka sana, Bwana Malugu.”
“Hiyo ni kweli. Lakini Nicole pia amekubali mwaliko wangu usiku wa leo ambapo tutazungumza kuhusu fomula fulani ya kipodozi adimu.” Bwana Malugu alicheka. “Samahani, Bwana Shangwe. Ikiwa tutapata fomula hiyo, mauzo ya bidhaa zetu kwa nusu ijayo ya mwaka hakika yatapita yako."
Midomo ya Rodney ikatetemeka. Bwana Malugu akampigapiga begani. "Lakini Bwana Shangwe, hautajali, sivyo? Familia ya Shangwe ina viwanda vingi sana. Hata kama Osher Corporation itapotea, bado una kampuni nyingi katika tasnia zingine unaweza kuchukua. Tunaweza hata kuwa washirika wakati huo."
Rodney alikunja uso kwa ukali, uso wake mzuri ukasinyaa na kuwa mbaya ghafla. Ndiyo, familia ya Shangwe ilikuwa katika viwanda vingi, lakini wakati huo huo, familia ya Shangwe ilikuwa na watoto wengi na wajukuu. Osher Corporation pekee ndiyo ilikuwa mikononi mwake. Kama ingemfia, hakuwa na jeuri ya kudai kampuni nyingine kutoka kwenye familia yao. Ikiwa kampuni ingemfia mikononi mwake, angechekwa na familia zingine za Shangwe. Ilibidi ampate Nicole.
Kama mgeni muhimu wa kongamano la siku hiyo, Nicole angetokea tu wakati muhimu. Saa saba kamili mchana, mwenyeji alipiga makofi.
“Tumkaribishe mwanakemia mahiri wa vipodozi kutoka Marekani, Nicole. Nicole haitaji utangulizi. Akiwa na umri
wa miaka 25, alifundishwa na Mwalimu Simpson, mtu ambaye alianzisha tasnia ya urembo wa anasa. Leo, Nicole anafanya kazi na brand nyingi za juu za kimataifa. Mwaka jana, lipstick zake za mfululizo wa Sapphire alizobuni zilivunja rekodi kwa mauzo ya kimataifa."
Chini ya macho ya umati, mwanamke aliyevaa nguo ndefu ya kifahari alijongea kwenye jukwaa la ukumbi wa ‘The Kenyatta International Conference Centre’. Mwanamke huyo alikuwa na sifa maridadi, pua iliyonyooka, na macho yaliyoeleweka vizuri. Alionekana mzuri na mrembo kama waridi linalochanua.
Rodney aliminya kwa nguvu glasi ya maji iliyokuwa mkononi mwake, na kusababisha maji kumwagika na kulowesha mkono wake. Hata hivyo, hakutambua hilo. Hakutarajia kamwe
kuwa Nicole, mwanakemia maarufu wa vipodozi angekuwa... Pamela Masanja. Alikuwa ni mwanamke ambaye aliwahi kumdharau. Maneno ya kiburi aliyokuwa ameyasema asubuhi ya siku hiyo yalionekana kumpiga usoni.
Akiwa jukwaani, macho ya Pamela yalimtoka kabla ya kumwangukia kila mtu. Kwa tabasamu, alisema, “Halo watu wote. Mimi ni Nicole, ninayejulikana pia kama Pamela Masanja.”
Watazamaji walisimama, wakalikumbuka jina hilo la kawaida.
“Ndiyo, niliwahi kufanya kazi kama mkemia wa vipodozi katika kampuni ya Osher, lakini haikuchukua muda Osher kunishutumu kwa wizi na utovu wa nidhamu. Walinifungia kuajiriwa na
kampuni zote za vipodozi nchini. Kimsingi sikuweza kupata kazi nchini wakati huo.”
Pamela alitabasamu huku akiongelea maisha yake yaliyopita. Alimtazama Rodney ghafla. "Bwana Shangwe, baada ya miaka mitatu, najiuliza ikiwa bado unaamini kuwa kweli nilikuibia? Ikiwa ningefanya hivyo, ningekuwa na hadhi niliyo nayo leo?"
Kila mtu mara moja akamtazama Rodney. Kila mtu aliyekuwepo alikuwa aidha ni mkurugenzi wa kampuni fulani au mtendaji wa ngazi za juu. Wote walielewa kuwa huo ulikuwa mchezo wa kitoto kwa Bwana Rodney kumkandamiza mkemia mdogo wa vipodozi.
Isitoshe, ikiwa Pamela aliiba kweli,
angewezaje kuwa mwanakemia mkuu wa vipodozi na maarufu? Watu walitegemea nguvu ya kusema.
Akiwa ametazamana na umati wa watu, Rodney alikunja ngumi zake kwa siri zilizokuwa kwenye magoti yake. Uso wake mzuri ulikuwa karibu kugeuka majivu. “Sikuwa na habari nyingi kuhusu matukio ya mwaka huo. Labda... watu walio chini yangu walinipa taarifa potofu.”
Baada ya muda, Rodney aliweza tu kuweka uso wa ujasiri na kuelezea. 'Ndio hivyo?"
Pamela alitabasamu kwa utamu na kusema kwa sauti ya mzaha,
“Bwana Shangwe, uamuzi wako wa kunifukuza na kunifungia miaka minne iliyopita uliniumiza sana. Lakini sina budi kukushukuru. Ulikuwa kikwazo
kwenye njia yangu ya mafanikio. Kama si wewe, nisingekutana na Mwalimu Simpson baada ya kuondoka nchini.”
Kisha, Pamela akaachana na Rodney na kuingia kwenye kiini cha kongamano. Alizungumza kuhusu baadhi ya utaalamu wake juu ya bidhaa za vipodozi.
Hapo awali Rodney hakutaka chochote zaidi ya kumpiga teke, lakini kwa sababu fulani, kadiri alivyokuwa akisikiliza, ndivyo alivyokuwa akivutiwa zaidi. Ilibidi akubali kwamba Pamela Masanja alikuwa na uzoefu na ujuzi. Kwa kweli alikuwa bora zaidi kuliko wanakemia wa vipodozi katika kampuni yake.
Mwishoni mwa kongamano, mwandishi wa habari ghafla alisema, "Bi. Masanja,
nakukumbuka. Miaka mitatu iliyopita, tukio lako na Thomas Njau lilizua gumzo kubwa. Nilisikia kwamba ulijilahisisha kwa Thomas—”
Uso wa Bwana Malugu ulibadilika huku akimkodolea macho mwandishi huyo. "Unatoka wapi? Usizungumze ujinga.”
“Ninasema ukweli. Tukio hilo liliibua hisia wakati huo. Bi Masanja alinajisiwa na Thomas Njau na kupelekwa hospitalini,” mwanahabari alisisitiza kauli yake kwa nguvu.
Umati wa watu uliingiwa na kizaazaa, na macho yao walipomtazama Pamela nayo yakawa ya ajabu.
Tabasamu zuri usoni mwa Pamela likabaki. Alinyanyua miguu yake mirefu na kushuka kutoka jukwaani kwa
utulivu, akimsogelea mwandishi huyo hatua kwa hatua bila hata chembe ya woga machoni mwake.
“Mara zote mimi husema kwamba wanawake lazima wajitahidi kujitegemea. Wakati msimamo wako ni wa chini sana na hata kama hujawahi kufanya chochote kibaya, unapokutana na mtu anayetegemea mamlaka na watu wenye nguvu nyuma yake ... mkosaji ambaye huwadhalilisha na kuwadhulumu wanawake atakuwa mwathirika mwishowe."
“Bi. Masanja, unamaanisha kusema...” Kulikuwa pia na waandishi wengine ambao walisimama polepole na kuuliza.
Pamela alisema kwa upole, “Huu ndio ukweli nyuma ya kile kilichotokea wakati ule. Nilimkataa Bwana Njau mara nyingi
aliponinyemelea, kwa hiyo aliweka kinyongo na kunivamia ndani ya nyumba yangu. Alinipiga kwa nguvu kwa nia ya kunibaka. Kwa bahati nzuri, rafiki yangu alifika kwa wakati.
“Ingawa nilikuwa sawa, mimi na rafiki yangu tulijeruhiwa na kulazwa hospitalini. Kama mnavyojua, dada mdogo wa Thomas Njau anaungwa mkono na Mwenyekiti wa KIM International. Dada wa Thomas anakaribia kuolewa katika familia ya Kimaro hivi karibuni. Wakati huo, ningewezaje kushindana na familia ya Kimaro?”
Mwandishi alifoka, "Kwa maneno mengine, unajaribu kusema kuwa ni Bwana Kimaro aliyemuunga mkono Thomas Njau na kukuundia kashfa?"
Pamela alisema kwa unyonge, “Ikiwa huniamini, unaweza kuchambua mambo mengine yote ambayo Thomas Njau amekuwa akijihusisha nayo kwa miaka mingi. Miaka iliyopita, mwanafunzi wa chuo kikuu alilazimika kujiua baada ya kubakwa na Thomas. Mwishowe, Thomas alimtegemea dada yake mdogo na akaondoka mahakamani bila hatia.
"Miaka hii michache, pia alikuwa amelazimisha wanawake wengi kutoa mimba. Hadi sasa, hakuna mtu kutoka kwa familia yenye heshima ambaye yuko tayari kuolewa naye. Ningewezaje kupenda kipande cha takataka kama yeye?"
Kila mtu alivuta pumzi ya baridi. Wote walijua kuwa mdogo wa Thomas Njau alikuwa karibu kuolewa na Alvin Kimaro. Maneno ya Pamela yalikuwa ni sawa na
kumwita Alvin takataka.
Rodney hakuweza tena kujizuia. "Pamela Masanja, ninakusihi uangalie maneno yako. Usifikiri kwamba wewe ni mtu asiyeweza kuguswa kwa kuwa sasa unajulikana katika tasnia ya vipodozi.”
Sura ya: 364
“Ninasema tu ukweli kuhusu mwaka huo. Kuna uhusiano gani na mimi kutoguswa?" Pamela alijibu huku akicheka.
“Unathubutu kusema mbele ya kila mtu kwamba Thomas Njau ni muungwana, Bwana Shangwe? Sahau, neno 'muungwana' ni kubwa na tata sana. Wacha tutumie neno "heshima". Je, Thomas ana heshima hata hivyo?"
Rodney aliwekwa njia panda. Kila mtu aliifahamu tabia ya Thomas. Rodney angekuwa tayari kushusha hadhi yake na kusema kwamba Thomas Njau alikuwa na tabia nzuri? Kwa kweli asingeweza kusema, huvyo. Kwa kweli, hakuwahi kukutana na mtu mchafu kama huyo hapo awali. Ikiwa sio kwa ukweli kwamba alikuwa kaka yake Sara, angeweza hata kumkana kwamba hamjui.
Pamela alitabasamu na kucheka kwa furaha moyoni mwake. Alikuwa akifanya kazi kwa bidii katika miaka mitatu iliyopita ili kulipa fedheha zote
alizopitia wakati huo.
Lisa hakuwa peke yake aliyeshikilia chuki za nyuma; Pamela pia.
Ni wazi alikuwa mwathirika katika tukio
hilo la Thomas lakini kashfa zikamgeukia yeye kwa kuitwa majina machafu. Hakupenda. Popote alipoenda, alinyooshewa vidole. Hata watu wealiomuheshimu hapo awali aliokuwa akiwasiliana nao walianza kumtumia meseji katikati ya usiku, wakiuliza ingegharimu kiasi gani kulala naye kwa usiku mmoja.
Alipoondoka, alikuwa kama mbwa mnyonge aliyepotea, lakini sasa ulikuwa wakati wa yeye kurejesha tena hadhi yake katika jamii hatua kwa hatua.
Pamela kwa mara nyingine tena aligeukia kipaza sauti cha mwandishi na kusema, “Ni vizuri kwamba umegusia tukio la Thomas Njau. Ngoja nimtangazie Thomas kuwa nimerudi! Uliponitisha wakati huo, niliweza tu kumeza maneno yangu, lakini ukweli utafichuliwa mapema au baadaye.”
Kisha akageuka na kuondoka.
Rodney pia alionekana kupotea katika mawazo kwa muda. Alipochukua hatua kubwa kujaribu kumfuata, Bwana Malugu alimzuia. "Bwana Shangwe, tangu ulipomfukuza talanta kama Bi. Masanja miaka mitatu iliyopita, anakuchukia sana. Usimfuate tena. Nadhani hataki kukuona pia.”
“Ondoka njiani,” Rodney aliamuru huku akiwa na uso wa mkali.
"Fomula iliyo mikononi mwa Bi. Masanja itakuwa ya SE Group." Bwana Malugu alimtazama machoni bila kukata tamaa. Katika kura ya maegesho kwenye ghorofa ya kwanza ya basement ya hoteli.
Gari la michezo lilikuja.
Katika maegesho ya magari kwenye ghorofa ya kwanza ya basement ya hoteli.
Gari la kifahari likajongea. Pamela alifungua mlango wa gari na kukaa kwenye kiti cha abiria. Mara tu baada ya kufunga mkanda alipokea simu ya video kutoka kwa Lisa.
Hapo hapo Suzie alikandamiza midomo yake kwenye na kumbusu. “Godmother, wewe ni mzuri sana. Umeongea vizuri sana."
“Mmeona?” Pamela alishangaa kwa furaha.
"Kulikuwa na matangazo ya moja kwa moja." Lisa akajitokeza kwenye simu yake. "Ingawa si watu wengi walioitazama, habari zitaenea polepole."
"Hakika nitalipiza kisasi kwa kile kilichotokea mwaka huo." Pamela aliuma mdomo. “Simuogopi Thomas Njau. Ni kwamba Alvin Kimaro, ambaye yuko nyuma yake, anasumbua kidogo.”
“Usijali, chukua muda wako. Hebu tufanye kazi pamoja. Tayari nilimwambia Big V achapishe ulichosema. Sasa ngoja tuone.” Lisa alimwambia kwa furaha. “Rudi Dar mara moja, nimekuandalia chakula.”
Katika sofa walilokuwa wamekaa, Suzie aligeuka na kumnong’oneza Lucas, “Kaka, Alvin Kimaro ndiye baba yetu mchafu?”
“Ndiyo.” Lucas alikunja uso na kutikisa kichwa.
Suzie aliuma mdomo wake na kusema kwa hasira, “Kwanini baba yetu ni mchafu? Alimuumiza Mama, na alimuumiza pia Godmom. simpendi hata kidogo.”
“Hata mimi simpendi.” Lucas tayari alimtambulisha Alvin kama adui yake.
•••
Kile ambacho Pamela alisema kwenye kongamano hilo kilisukumwa polepole kwa vyombo vya habari na Big V, na kwa hivyo, habari za zamani za miaka mitatu iliyopita zilichimbwa tena.
[Namkumbuka huyu binti sasa. Miaka mitatu iliyopita, ilisemekana kwamba alimtongoza Thomas Njau, hivyo alikaripiwa na kila mtu.
Watu hata walimrushia mayai viza wakati anatembea.]
[Anashangaza. Yeye ni mwanakemia maarufu wa vipodozi sasa. Sijui ni kwanini, lakini kwa namna fulani naamini kwamba anasema ukweli. Labda ni kwa sababu yeye ni mrembo.]
[Kwa kweli nilitaka kusema hivi miaka mitatu iliyopita. Tabia ya Thomas Njau kweli si nzuri, lakini hakuna aliyeniamini.]
[Nina jamaa wa mbali ambaye alifanya kazi katika New Era Advertisings na mara kwa mara alitongozwa na Thomas. Mwishowe, alijiuzulu kwa sababu asingeweza kuvumilia tena.]
[Thomas Njau ni fisadi maarufu katika jiji hili. Nilikuwa na mwanafunzi mwenzangu wa chuo kikuu ambaye alivutia umakini wake, lakini alimkataa.
Mwishowe, alimlazimisha kwa nguvu akamsababisha hadi ajiue. Familia yake ilimshtaki, lakini haikufaa. Alitetewa na wakili bora kabisa.]
[Kila mtu anajua kwamba dada yake mdogo ni Sarah Njau.
Anafanya ushenzi tu kwa sababu anajua shemeji yake ni Alvin Kimaro.]
Mambo yalipoanza kuwa mbaya, Hans akaenda kuripoti kwa Alvin. Wakati huo Alvin alikuwa akiongozana na Sarah kujaribu mavazi yake ya harusi.
“Pamela Masanja?” Alvin bila ufahamu alimfikiria Lisa aliposikia jina hilo. Kipindi hicho alikuwa akijaribu kila awezalo kutofikiria juu yake. Hata hivyo, sasa jina la Pamela lilipotajwa, tukio la miaka mitatu iliyopita nalo lilijirudia tena akilini mwake.
"Ndio, inaonekana anataka kufichua ukweli kuhusu tukio la Thomas Njau miaka mitatu iliyopita." Hans Aliitikia na kusema, “Kwa kuwa sifa ya Thomas Njau imekuwa duni miaka hii, maoni yote mabaya ni dhidi yake. Sasa, watu kwenye mtandao... wanazungumza kuhusu Bi. Njau na wewe.”
“Wanasema nini?” Alvin aliuliza kwa uso wa hasira.
"Wanasema unatumia nafasi yako kuwadhulumu wengine."
Alipokuwa akijaribu mavazi ya harusi, sura nzuri ya Sarah ilibadilika aliposikia maneno hayo. Hakuwahi kufikiria kuwa Pamela angetokea tena. Si alikuwa tu mfanyakazi mdogo chini ya Rodney wakati huo? Aliwezaje kurudi tena kwa
nguvu kama Lisa?
Sarah aliuma meno lakini haraka akasema kwa hatia, “Samahani, Alvin. Sikutarajia tukio lile lingeweza kukuletea shida tena, lakini tayari nimeshawahi kumpa onyo kaka yangu kuhusiana na hili. Anajiheshimu sana sasa hivi.”
Hans hakuweza kujizuia kusema, “Lakini... niliona baadhi ya watu kwenye mtandao wakisema kwamba Bwana Njau... mara nyingi huwanyanyasa wafanyakazi warembo katika kampuni.”
Uso mzuri wa Alvin mara moja ukapoa. Sarah alimlaani Hans kwa siri, lakini uso wake ulionyesha huzuni tu. “Kwa kweli sikujua kuhusu hilo. Labda kuna mtu aliajiri watu kutoa maoni hayo... "
“Inatosha. Zuia jambo hilo kwanza.”
Alvin akageuka kumuamuru Hans. “Bila shaka.”
Baada ya Hans kuondoka, Sarah alimshika mkono Alvin. “Alvin, kuhusu suala hili, ni kaka yangu ndiye aliyemkosea Pamela. Vipi kuhusu mimi kumfidia dola milioni moja?”
"Ikiwa unafikiri kweli kwamba alikuwa na makosa, basi mwambie afunge mdomo wake." Alvin alikasirika bila kifani. "Yeye ndiye alikuwa na makosa lakini alikimbilia kwa waandishi na kusema kwamba Pamela alimtongoza. Ikiwa sivyo kwamba yeye ni kaka yako, ningemuua tayari.”
Mwaka huo, pia alikuwa Thomas Njau ambaye alimfanya kupoteza watoto wake kwa njia isiyo ya moja kwa moja.
Alvin alijawa na karaha kwa mwanaume huyo sasa.
Sarah alishtushwa na hasira iliyokuwa machoni mwake, na macho yake yakawa mekundu huku akiomba msamaha kwa haraka, “Samahani, ni kosa langu. Sikupaswa kuwa mbinafsi na kukuomba umwokoe kwanza.” “Sahau, si kosa lako. Hata hivyo, siku za usoni, sitajali iwapo ataishi au kufa tena,” Alvin alisema kwa kuudhika.
“Sawa.” Sarah alizuia machozi yake. "Alvin, je! vazi hili la harusi linanipendeza?"
Alvin alimtazama kwa kawaida na kutikisa kichwa. "Tutanunua hili." Kisha, akatoka nje. Kwa sababu fulani, alihisi kwamba ikiwa nguo hiyo ingevaliwa na Lisa badala yake,
ingekuwa nzuri zaidi.
Sarah alimtazama yule mtu wa nusu nusu na kukanyaga mguu wake kwa hasira.
Sura ya: 365
Wakati huo huo, Thomas alimpigia. "Sarah, yule b*tch Pamela Masanja amerudi. Wakati huu, hakika nitammaliza!”
Uso mrembo wa Sarah mara moja ukaangaza kwa mguso wa karaha. "Funga mdomo wako. Huu ni wakati mgumu kwani nitafunga ndoa na Alvin hivi karibuni. Usiniletee balaa.”
Thomas alishtushwa na karipio la ghafla. "Lakini haukuona alichosema
Pamela kwa waandishi wa habari"
“Alvin tayari ameweka mtu wa kuzima jambo hilo. Ikiwa una kinyongo, basi subiri baada ya harusi yangu.” Sara alisema neno baada ya neno, “ ikiwa kitu kitaenda vibaya, sitakusaidia."
“... Sawa.” Thomas alikata simu bila kupenda, lakini moyoni hakufikiri kwamba jambo lolote lingeharibika. Akageuka, akapiga simu. "Nenda utafute anapoishi huyo b*tch Pamela Masanja."
•••
Katika hoteli ya kifahari ya ‘The Concord Hotel & Suites.’
Mhudumu alimuongoza Pamela na kusimama kwenye mlango wa chumba cha faragha. "Hiki ndicho chumba
ambacho Bwana Malugu alipanga kwa ajili yako."
"Asante." Pamela aliusukuma mlango na kuingia ndani.
Rodney alikuwa ameketi mbele ya skrini ya kale. Alivaa shati la kahawia na vifungo viwili vya kwanza vilikuwa vimefunguliwa. Mikono ya shati ilikuwa imekunjwa, na macho yake yalikuwa makali kwenye uso wake mzuri, na kumpa mtazamo mbaya lakini wa mapenzi.
“Keti.” Akaelekeza kwenye kiti kilichokuwa kando yake.
Pamela hakuweza kuwa na wasiwasi naye na akageuka kuondoka, lakini alipojaribu kufungua mlango, aligundua kuwa umefungwa.
“Usiondoke. Kula. Chakula hakitakuwa na ladha kikiwa cha baridi.”
Rodney aliinuka na kumburuta hadi kwenye kiti. “Bi. Masanja lazima ulijisikia vizuri ulipokuwa ukizungumza kwenye kongamano leo. Nakubali, umenishangaa. Nilikosea juu yako hapo awali. Ninakupa toast hii kama msamaha, sawa? Una furaha sasa?"
Rodney alijimiminia glasi ya mvinyo mwekundu na kuinywa. Pamela aliitazama glasi ya mvinyo iliyokuwa mezani kwa muda kabla ya kwenda kumimina mvinyo ndani yake.
Rodney alifurahi, akifikiri kwamba alitaka kutoa toast, lakini bila kutarajia, aliinua mkono wake na kumwaga mvinyo wote kwenye uso wake mzuri.
"Pamela Masanja!" Uso wa Rodney ulibadilika sana. Alipokaribia kukasirika, Pamela alichukua chupa ya divai, akaifungua kola yake na kumimina vilivyomo ndani ya shati lake. Mvinyo ulikuwa baridi, na kusababisha Rodney kupiga kelele.
Aliruka pembeni na kuvua shati haraka, lakini suruali yake ilikuwa tayari imelowa. Suruali yake ilishikamana kwa nguvu kwenye mapaja yake, ikionyesha mistari ya kuvutia.
"Pamela Masanja, unataka kufa?" Rodney alikasirika. Hakuna mtu aliyewahi kuthubutu kumfanyia hivi. Mwanamke huyu alikuwa mwendawazimu! Anathubutu vipi kummwagia mvinyo?!
Alikuwa amepoa sana baada ya kuvua
nguo zake. Alitetemeka, na kwa macho yake, hakutaka chochote zaidi ya kumla akiwa hai.
Kwa upande mwingine, Pamela alikuwa akitabasamu kwa furaha. “Nilifikiri haujaamka kabisa, kwa hiyo nilikumiminia mvinyo. Rodney Shangwe, nadhani umezoea sana kutetemekewa kwa kuwa bwana mdogo tajiri sana. Hujawahi kunitendea haki hata kidogo. Wakati ule, ili kumsaidia Sarah Njau, ulitamka sentensi ya kawaida ambayo karibu kuharibu maisha ya juhudi zangu. Kama hukunipenda, ungenifukuza tu. Kwanini ulilazimika kunifungia kabisa kwenye tasnia?”
Kadiri alivyozidi kusema ndivyo alivyozidi kupata hasira. Aliivunja chupa, na kusababisha vipande vya chupa kusambaa kila mahali.
Rodney aliruka kwenye kiti kwa woga na nusura ateleze kwenye vipande vya chupa. Baada ya yote, hakuwa amevaa shati. "Pamela Masanja, usifikiri kwamba sitathubutu kukupiga!" Rodney alimfokea.
"Endelea. Hata usiponipiga nitakupiga.” Pamela alitumia uma kuokota kipande cha nyama ambavyo vilikuwa bado vya moto kutoka kwenye sahani na kumrushia Rodney.
Rodney aliitazama jinsi chumba kilivyokuwa kimechafuka kwa fujo za kila aina na kumtisha, "Pamela Masanja, nitaita polisi ikiwa utatupa kipande kingine."
"Endelea. Zaidi sana, nitaambiwa kulipa pesa. Naweza kumudu.” Pamela
alimtupia kila kitu mezani.
Rodney hakuweza kukwepa na aliweza tu kukimbilia kushika mikono ya Pamela. Mikono ya Pamela ilikuwa imezuiliwa, hivyo akageuza kichwa chake na kumng'ata kwa nguvu sikioni.
“Sawa!” Rodney alipiga kelele baada ya kuumwa na kuushika sehemu fulani ya mwili wake bila fahamu. Matokeo yake, alihisi kitu laini mikononi mwake. Alipogundua alichokuwa akikamata, tayari alikuwa amepigiwa goti katikati ya mapaja yake na Pamela. Macho yalimtoka kwa maumivu.
Ghafla, aliweza kuelewa maumivu ya Alvin siku nyingine. Haishangazi alikwenda hospitali kwa uchunguzi. Inaumiza sana.
"Tamu eeh?" Pamela alimtazama kwa
dhihaka. “Yako haina maana hata hivyo.”
"Yangu hayana maana?" Rodney alijikunja kwa maumivu na nusura apoteze pumzi.
“Umewahi kuitumia kwa nani?” Pamela alicheka. “Umejitolea kwa Sarah Njau, lakini ataolewa na Alvin Kimaro hata hivyo. Hatakuwa na nafasi katika maisha yako. Unapaswa kuwa towashi tu. Sijawahi kuona mwanaume mjinga kama wewe.”
"Pamela Masanja, thubutu kusema neno moja zaidi..." Macho meusi ya Rodney yalikuwa yamefunikwa na hasira.
“Nimesema kitu kibaya? Nilishakuambiaga muda mrefu. Wewe ni
mwanaume lakini bado una kelele kuliko mwanamke. Kuwa mwanamke katika maisha yako yajayo basi...”
Kabla Pamela hajamaliza, Rodney alimkimbilia na kumg’ata.
Macho yalimtoka Pamela na bila fahamu akajaribu kumpiga tena goti sehemu zake za siri. Wakati huu, Rodney alikuwa amejiandaa na kubana miguu yake haraka. Pamela alipoteza stepu na mwili wake ukaanguka moja kwa moja kwenye mikono ya Rodney. Wakati huo, sauti ya hasira ya Bwana Malugu ilisikika nje ya chumba akimfokea mhudumu. "Mara nyingi mimi huja kwenye hoteli hii. Siamini kuwa ulimleta mgeni wangu kwenye chumba cha mtu mwingine. Mgeni wangu akipata madhara yoyote, sitakusamehe...”
Ndani ya chumba, Pamela aliogopa na kujitahidi sana. "Rodney Shangwe, niachie!"
"Hapana." Rodney aliuma mdomo wake kwa ukaidi na hakumuachilia.
Pamela hakuwa na chaguo ila kuuma, na kwa sababu hiyo, wote wawili waliangukia kwenye sofa.
Kisha, mlango ukafunguliwa. Bwana Malugu na meneja wa hoteli waliingia ndani haraka. Waliona tukio la shauku ndani na walipigwa na butwaa mara moja.
Bwana Malugu alikasirika sana hadi uso wake ukakunjamana. Rodney alilegea, na Pamela akamsukuma kwa nguvu. Ingawa nguo zake zilikuwa safi, kulikuwa na alama za meno kwenye midomo yake na rangi ya lipstick yake
iliacha alama kwenye uso wa Rodney kwa uwazi sana.
“Bwana Malugu, uko kwa wakati. Yeye-”
"Nicole, ninaelewa. Alikutongoza, sivyo?”
Bwana Malugu alikatisha maneno yake. Alimkazia macho Rodney kwa ujeuri ambaye hakuwa amevaa shati na suruali yake ikiwa imelowa. "Bwana Shangwe, unaenda mbali sana. Kwa ajili ya kupata fomula tu, unawezaje kufanya kitu kama kuuza utu wako?"
Ingekuwa ni mtu mwingine, angekuwa na hasira kabisa. Lakini, Radney hakuwa na aibu. Alijipangusa kwa utulivu pembeni ya mdomo wake na
kutabasamu huku akiinua nyusi zake. "Bwana Malugu, unaweza pia kujaribu kuuza utu wako, lakini Bi. Masanja anaweza kufikiria kuwa wewe ni mzee sana."
Uso wa Bwana Malugu ulilegea. Pamela alichukua kitambaa na kujifuta pembeni ya mdomo wake kwa nguvu huku akimkazia macho Rodney. “Pole, Bwana Shangwe, lakini nadhani wewe ni mchafu sana. Mdomo wako huo ni kama choo cha umma. Nimechukizwa.”
TUKUTANE KURASA 366-370
ONYO: Ni marufuku kusambaza, kukopi wala kuuza kazi hii kwani endapo kama tutakubaini basi sheria itachukua mkondo wake (By: Official Dully)